Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

CHEZA NA MIMI LAKINI USICHEZE NA MUNGU WANGU

 

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO


ADAM; CHEZA NA MIMI LAKINI USICHEZE NA MUNGU WANGU!


Nilikua najua kuwa siwezi kumpata kwani huyu Dada alikua ni mtu wa imani sana, ilikua ngumu sana kwa mtu kama mimi kumtongoza. Mimi muumini wa dhehebu jingine lakini kwakua nilikua namhitaji sana huyu dada niliamua kwenda kanisani kwaajili yake. Hakuna mtu aliyekua akinifahamu kwani nilifika pale kwaajili ya kufanya Biashara tu.


Kanisa alilokua akisali lilikua ni dogo, haya makanisa yanayoanza hivyo nilijua ili kuteka akili za watu basi nilikua natoa sadaka sana, kwanza nilaihidi kununua mabati mia mbili kwaajili ya kupaulia. Sikua na mpango wala sikua na pesa ya kutoa hayo mabati.


Lakini nilikua najua kwamba, kama nikiahidi kununua mabati wakati kanisa ndiyo lilikua linaanza msingi, mpaka wanafikia hatua ya mimi kununua hayo mabati nitakua nimeshampata huyo binti na kuondoka zangu pale. Sikua na mpango wa kumuoa bali nia yangu ilikua ni kutembea naye siku moja.


Nilitenga kama milioni mbili ya sadaka amabyo nilijua kabisa kuwa itaniweka karibu na Mchungaji aniamini hivyo kumtumia yeye ili kuwa karibu na yule binti. Kweli nilifanya hivyo, nilikua natao laki laki kila jumapili, wakati mwingine natoa mpaka laki tano sema kwa malengo, kwa Kanisa kama lile kilikua ni kiwango kikubwa sana cha pesa mimi kutoa.


Kama nilivyotarajia mchungani aliniamini sana, alikua ni mchungaji wa kweli, ukiongea naye unajua kabisa ana malengo makubwa ya kuliendesha kanisa ingawa mimi nilihitaji tu kumtumia kwa mambo yamngu. Ndiyo ya mwezi mmoja tu nilikua nishatengeneza kauminiwa, hakuna aliyekua akinijua kuwa natokea wapi wala pele nimekuja kufanya nini ila hata sikujali.


Lengo langu lilikua ni kumuoa yule binti Aneth ambaye nilikua namhitaji kuliko kitu chochote kile katika maisha yangu kwa wakati huo.


“Baba Mchunaji, mimi Mungu kanibariki, nimejaaliwa mali lakini moyo wangu umpweke sana, sina fraha katika maisha yangu. Nimeshatoka kwenye ulimwengu wa kibinadamu nipo katika ulimwengu wa kiroho, lakini bado nimpweke kwakau Mungu bado hajanipa mwanza wangu, ni mwepe sana….”


Sikua na muda wa kupoteza, nilijua kuwa ni suala la muda tu pesa zitaniishia hivyo nitashindwa kutoa sadaka na maisha ya pale yatanishinda. Nilikua nahitaji kumuoa Aneth kabla mambo hayajaniwia magumu.”Kwanini unasema hivyo kwanini uwe mpweke?” Aliniuliza.


“Nimeshakua na wanawake wengi Baba mchungaji, lakini wote hao nilikua nao kipindi sijaokoka, sasa hivi nimeokoka na namjua Mungu, sipo tayari kabisa kurudi kwa wanawake wale. Tangu nianze kusali hapa nimekua nikifunga nikiamka usiku kumuomba Mungu, nahitaji kupata mchumba, tena wa hapahapa, nahisi Roho Mtakatifu sasa kanifungua, baada ya kusali sana kuna binti namhitaji, ningeweza kwanda mimi mwenyewe kuongea naye lakini nikasema hapana.


Unajua Baba mchungaji wewe umefunguliwa zaidi, Mungu anakutumia kwaajili yetu, kuna mambo mengi ambayo kwa macho ya kibinadamu hayawezekani lakini ki roho yanawezekana, kuna binti kila nikifunga macho na kusali naambiwa kuwa ndiyo mke wangu, hivyo naomba unisaidie kufunga na kusali, unisaidie kunifungua kujua kweli kama ndiyo ubavu wangu Mungu kaniandalia au la?


Nampenda tena sana lakini sitaki kamwe kuruhusu moyo wangu kunifanyia maamuzi!” nilishajiandaa, nilimpa mchungaji mistari abayo niliamini kabisa kwua hawezi kuchomoa. Aliniuliza ni binti gani nikamtajia, kwanza alishtuka lakini akatulia na kuniambia kuwa haiwezekani.


“Huyo binti amechumbiwa, mchumba wake ni muumini wa hapahapa, sidhani kama itawezekana….” Aliniambia, mimi sikushtuka kwani nilishachunguza kuwa huyo binti ni mchumba wa mtu na ndiyo sababu ya mimi kuamua kulitumia kanisa ili kumpata.


“Naomba unisaidie kusali ili kuona ni kwanini Mungu ananielekeza kwake kila siku wakati anajua kuwa ni mchumba wa mtu, nisaidie kabisa!” Nilimuambia mchunjaji lakinia lionekana kusitasita, ni kweli alikua ananiheshimu lakini toafauti na nilivyokua nimesikia kwa watu kuwa yule mchungaji ni feki anaangalia pesa tu hali haikua hivyo kabisa.


***


Kwangu mimi kumuoa Aneth kilikua ni kitu cha lazima sana, hakikua ni kitu cha kukatishwa tamaa na Mchungaji kisha kukubali kubali tu. Ilikua ni lazima kuoana naye hivyo nilipaswa kuhangaika na mchumba wake. Ningeweza kumfuata Aneth mwenyewe na labda kumshawishi ili kuachana na mchumba wake lakini nilijua kuwa hiyo ingechukua muda sana na sikutaka iwe hivyo.


Nilitaka Aneth kuniona kama malaika, kuona kama mimi ni mpango wa Mungu kwake, nilishasikia na kuonywa kuhusu imani yake kwa Mungu hivyo nilitaka Mchungaji kunisaidia kumtongoza. Niliamini kuwa, kama Mchungaji, Baba yake wa kiroho angemuambia kuwa kaoteshwa kuhusu mimi basi angenipenda sana na isingekua rahisi kwake kuniacha hivyo mipango yangu kutimia bila shida.


Nilienda kwa mtaalamu wangu kuzungumzia kuhusu Mchungaji lakini aliniambia kuwa haingiliki, kila mganga niliyekua nikienda kwake alikua akimuogopa mchungaji. Baada ya kuona imeshindikana kwa mchungaji nilipata wazo jingine la kuhangaika na mchumba wake. Nilijua kama nikiweza kumharibia na kumuaibisha mchumba wake basi Aneth atakua wangu, akili ilifanya kazi harakaharaka kwani ilikua ni lazima kumuoa Aneth ndani ya mwezi huo.


Pesa niliyokua nikitoa kanisani ilikua inakaribia kuisha na kwa kuangalia Biashara zangu zilikua kama zimekwama vile. Kwanza nilianza kujiweka karibu na mchumba wake, nikajua anafanya kazi gani na kujua ni namna gani yakumuingilia. Sikuhitaji nguvu kubwa, nilishohitaji kwake mimi ni salamu tu. Nilijua kama nikimsalimia na kushikana naye mkono tayari nitaweza kumchanganya akawa mtu mwingine tofauti kabisa.


Siku moja nilikua nimetoka kanisani, kwa kawaida huwa naenda jioni, si kwa lengo la kusali bali ni kujiweka karibu na Mchungaji ili kufanikisha mambo yake. Mchumba wake alikua ni mtu wa kanisani lakini si kama Aneth mwenyewe ambaye karibu kila sikua likua kanisani akiomba.


Nilishamjaribu mara nyingi kumuingilia kimiujiza lakini ilishindikana, kama mchungajio kila mganga niliyekua nikienda na kupeleka picha yake waliniambia ana nguvu kubwa hivyo niachane naye, lakini nisingeweza kumuacha, kwangu ilikua ni lazima kumuoa ili mambo yangu yaende vizuri. Nikiwa natoka kanisani kama bahati tu nilikutana na mchumba wake, alikua kasimamisha gari yake kwenye kibanda kimoja hivi akinywa soda, alionekana mwenye haraka kwani kila dakika alikua akiangalia saa yake.


Kwangu hii ilikua kama bahati kumuona, harajaharaka niliingiza mkono wangu mfukoni na kushika dawa.


“Bwana Yesu asifiwe….”Nilimuambia huku nikimpa mkono, ni kama alisita kidogo lakini aliuonyoosha na kunipa mkono wake. Hakuujibu salamu yangu, nilimuona kama kaganda flani, alikua kashikwa na butwaa flani hivi, bila kujali ni nani alikua ananiona nilichukua ile soda aliyokua anainywa, nikaitemea mate na kumrudishia. Kilikua ni kitendo cha haraka ila nilijua dawa imefanya kazi kwani baada ya kufanya hivyo aliichukua na kuinywa alipomaliza aliaga na kuondoka.


Niliondoka kwa furaha nikijua kuwa mpango wangu ushafanikiwa.Jumapili iliyofuata yule kijana sikumuona kanisani, lakini baada ya ibda nilimuona Aneth akielekewa kwa mchungaji, nilijua lazima mambo yashakua yamefanikiwa.nilimfuata kulekule na kujifanya na mimi nilikua na matatizo yangu. Nilisubiri mpaka akaingia ndani nikaa kwa mdua kidogo na mimi nikajifanya kugonga mlango huku nikiufungua, sikutaka kusubiri kuruhusiwa.


Aneth alikua amekaa kwenye kiti huku akilia.


“Bwana Yesu asifiwe, samahani Mchungaji, sikujua kama una mgeni, nitakuja wakati mwingine.”Nilimuambia huku nikitaka kutoka kuondoka, alinijibu na kuniambia nisubiri.


“Ulikua na shida gani Mwanange?” Aliniuliza.


“Hakuna tatizo Mchungaji,nilikuja tu kuna sadaka nilileta na nilihitaji kusali na wewe. Nimefunga siku tatu lakini kuna vitu Mungu ananionyersha, nimeona nahitaji msaada wako.” Nilimuambia, aliniangalia kama anataka kusema kitu lakini alisita kisha akaniambia.


“Basi njoo Baadaye, huyu binti ana matatizo,njoo baadaye, ngoja kwanza nimsikilize.” Aliniambia, nilimpa Pole Aneth kisha nikaondoka zangu huku nikicheka, nilijua mambo yanaenda kuwa mazuri karibuni. Sikwenda mbali, nilizunguka mjini kwenye mishemishe zangu. Kama nusu saa hivi Mchungaji alinipigia simu na kuniambia kuwa anataka kuniona.


Hataka hataka nilienda mpaka kanisani, sikumkuta Aneth, Mchungaji alinikaribisha ndani tukakaa.


“Niko tayari kufunga na wewe, naamini Mungu kuna kitu alitaka kunionyesha ila nikampuuzia.unakumbuka ulikuja kuniambia kuhusu huyu Binti lakini nikakukatalia na kukuambia kuwa ana mchumba wake?”Aliniuliza, niliitikia kwa kichwa huku nikijifanya kama nawaza, sikutaka kuenda kwa pupa kuonekana kama nina shida sana.


“Basi, kuna kitu kimetokea naamini ni hizi funga zetu, Mungu kamuumbua huyu kiumbe….” Alianza kunielezea akiniambia kuwa Aneth alienda pale kumlalamikia kuhusiana na mabadiliko ya ghafla ya mchumba wake. Alikua hataki ndoa tena kwani alikua na mwanamke mwingine.


“Hata kanisani hajaja, alikua anamdanganya binti yetu, yaani ni kama mtu aliyechanganyikikwa kwani akiambwia kuomba anakataa anasema yeye alikuja kanisani ili kumsawishi Aneth afanye naye mapenzi amuache, kwakua binti aligoma basi ameamua kumuacha, ana mwanamke mwingine na alipomuambia kuhusu kuja hapa kanisani basia litukana sana na kumuambia kuwa sisi ni wachawi, hataki kuja tena hapa!”


Alinielezea mambo mengi, mimi nilijifanya kushangazwa na hayo mambo, nikitaja jina la Mungu kila dakika. Mchungaji aliniomba kusali naye, tulipiga magoti na kuanza kusali, wakati nasali mimi nilikua nimeshikilia hizizi yangu, mfukoni. Nilifanya hivyo ili kushindana na nguvu ya mchungaji, lakini kila alipokua akitaja jina la Mungu ndipo na mimi nguvu zilianza kuniishia.


Nilisahonywa kuhusu huyo mchungaji, kila Mganga niliyekua nikienda ili aoteshwe mimi kumuoa Aneth alikua akinaimbia kuwa nifanye kila kitu lakini nisimuingilie huyo Mchungaji kwani ni mtumishi kweli waMungu. Lakini sikusikia, sikua tayari kuwa masikini kwa maisha yangu yote, ilikua ni lazima kumuoa Aneth na sikau na njia nyingine zaidi ya kulitumia kanisa.


Wakati mchungaji anasali, kanishika mkono Nguvu zinaniishia nilijikuta naanza kukabwa, kulikua na mtu kama kanishika shingoni ananikaba! Alikua kamka anaanitingisha, kichwa kilitingishika, nguvu zikawa zinaniishia, nikawa kama natingishwa ili kutapika kitu. Nilianza kupiga kelele lakini Mchungaji ndiyo kwanza alikua anaendelea na maombi, ni kama alihisi ananisaidia lakini kumbe alikua ananiua, nilikua natingishwa sana mwisho nguvu ziliniishia na kudondoka chini.


Adam anataka kumuoa Aneth, binti wa kiloloke ambaye ana imani sana ya dini. Ili kumpata anataka kumtumia Mchungaji amabye kutokana na imani yake basi haingiliki kirahisi. Ameshamharibu akili aliyekua mchumba wa Aneth kiasi cha kumuacha Aneth, unadhani nini kitaendelea? Kwanini Adam ana hamu sana ya kumuoa ANETH na si mwanamke mwingine, usikose simulizi hii ya kusisimua.


ADAM; CHEZA NA MIMI LAKINI USICHEZE NA MUNGU WANGU!–SEHEMU YA PILI


Nilijua nguvu ya Mungu inafanya kazi, nilijua kama sitakua makini basi nitaumbuka. Harakaharaka wakati na kamwa Mchungaji anaendelea kusali niliachia hirizi niliyokua nimeishikilia na kuutoa mkono wangu mfukoni harakaharaka.  Kila kitu kiliniachia, nikasimama na kutaka kuondoka lakini nguvu ziliniishia na kudondoka, Mchungaji alikua amemaliza kusali, aligeuka na kuniangalia.


“Kuna nini Mbona umedondoka?” Aliniuliza, kama dakika mbili hivi nilikua sijielewi elewi, lakini fahamu ziliporudi nilirudisha mkono mfukoni, nilijua kuwa tayari Mchungaji kashaacha kusali hivyo ninaweza kupata nguvu kubwa kutoka katika hirizi yangu.


“Nilikua naweweseka Baba, yaani nilikua nahisi kama nakufa!” Nilimuambia huku nikitoa machozi, hayakua machozi ya uongo, ni kweli nilikua na maumivu makali sana shingoni kiasi nilikua napungua kwa shida.


“Kuna nini? Inamaana ulikua unaona kile nilichokua nikikiona?” Aliniuliza, kidogo nilishtuka nikahisi labda Mchungaji alikua ananiona, nilisita kidogo kujibu mpaka pale alipoendelea kuongea.


“Kuna nguvu za ajabu nilikua nikizisikai, kila nilipokua nikijaribu kutaja jina lako na la yule binti kuna kitu nilikua nikikisikia si kizuri…” Aliniambia.


“Ohhoooh! Imekula kwangu, huyu Mungu mbona kaniumbua mapema namna hii!”Niliwaza lakini sikutaka kukubaliana na ukweli kuwa mimi na Aneth ilikua ndiyo mwisho, kusema kweli ilikua ni lazima kuwa naye, nilizidi kuibana Hirizi yangu nikikusanya nguvu za kuongea.


“Hata mimi Mchungaji, yaani kila nikitaka jina lake nilihisi kama kuna kitu kinanizuia. Haikuishia hapo, umeona nikiwa nimesimama, basi kuna mtua likua ananikaba, si shetani wala mapepo. Nilikua naona sura ya yule kijana, ananikaba, nimejaribu kupambana lakini nahisi kuwa sitaweza. Nahisi kama anatumia nguvu za giza!” Nilimuambia huku nikimuangalia kwa wasiwasi, hakua kwenye maombi ila bado nilikua namuogopa kwani maombi yake kidogo yaniue.


“Hata mimi nilihisi kitu kama hicho, kuna kitu yule kijana anakifanya kwa huyu Binti. Nadhani kuna nguvu inataka kuzuia binti wawatu asifanikiwe, nahisi amefungwa…” Niliongea, nilitaka kumchanganya Mchungaji ili aone kama kilichokua kikitokea si kwamba mimi nilikua na matatizo bali mchumba wake ndiyo alikua anafanya mambo kuhakikisha kuwa mimi na Aneth hatuoani. Mchungaji ni kama aliingia laini kwani aliniahidi kuwa kesho yake atanitambulisha kwa Anet, atataka tuonane naye.


Kwangu hiyo ilikua ni hatua kubwa, nilishakata tamaa ya kumshawishi Mchungaji, lengo langu lilikua ni kumuambia Mchungaji aseme kaoteshwa ili mimi na Aneth tuoane, lakini ilishindikana, kila nikimuangalia namuona kama ni mtu wa Mungu kweli hivyo hawezi kuingilika, kitendo cha kukubali kunikutanisha na Aneth kwangu niliona unatosha kumshawishi Aneth kuwa mimi ni mtu sahihi kwake.


“Omba sana! Sali sana! Najua unampenda yule biniti na kwa maombi yako ndiyo yalisababisha yule mchumba wake kuonyesha rangi yake, ila naona ana mpaka nguvu za giza.” Mchungaji aliniambia, nilikua najisikia vibaya kidogo kudondoka, alinipa moyo na nilijua kuwa nahitaji kuongeza Dozi ili niendelee kuaminika. Mtu pekee ambaye alikua ni mnyonge wangu alikua ni mchumba wa Aneth. Nilikua na namba yake na kwa vitu nilivyokua nimemfanyia alikua kama zezeta, nilijua kabisa kama nikitaka kuonana naye hachomoi.


Nilimpigia simu na kuomba kuonana naye, hakua na namba yangu na wala hakua akinijua kihivyo zaidi ya kusalimiana mara moja moja kanisani na siku ile niliyompaka dawa.


“Una haribu maisha yako, hivi kwanini umekua hivyo?” Nilimuuliza baada ya kuonana naye, tulikua tumekaa Bar ambapo nilimuita. Mimi nilikua nakunywa maji nayeye alikua ameagiza Konyagi.hatukua na mazoea kabisa lakini kwa vile nilikua nishamfanyia mambo alikua akinisikiliza kama rafiki.


“KIvipi Broo?” Aliniuliza, tayari nilishamuongezea dozi wakati tumekaa. Alikua hanywi pombe lakini baada ya kukutana na mimi na kumfanyia dawa alibadilika na kuwa mlevi kupindukia.


“Umeanza kunywa pombe kwaajili ya mwanamke…” Nilimuambia kimtego.


“Hapana, sijanywa kwaajili ya mwanamke, mimi napenda Pombe, mwanamke hawezi kunifanya kunywa pombe. Hivi unajua kuwa mimi ndiyo nilimuacha na tangu zamani sikua na mpango naye kabisa!”Aliongea huku akiendelea kunywa, ilikua ni Konyagi kavu lakini alikua anakunywa kama maji, mpaka mimi amabye nilimfanyia vile nilianza kumuonea huruma kwani nilijua namharibia maisha yake bila sababu yoyote.


“Haya mambo yanapaswa kuisha mapema, siwezi kuendelea kufanya hivi kwaajili ya mwanamke, pesa yenyewe inaniishia!” niliwaza huku nikichukua chupa na kumuambia kuwa hatakiwi kunywa tena. Mwanzo alibisha bisha lakini baadaye alinielewa akakubali kuacha.


“Aneth si mlokole kama unavyodhani, kuna vitu kakufanyia na mimi nataka kukusiadia, wewe ni mwanaume mwenzangu lakini kuna vitu naviona nashindwa hata nikuambie nini?”Niliopngea huku nikijifanya kusikitika, niliinama chini kama ninalia hivi, aliniangalia kwa mshangao.


“Broo vipi kwani kuna nini?” Aliniuliza,


“Sijui nikuambieje, kuna mambo yanatokea kanisani yananichanganya sana, yaani kuna wakati najuta kwanini nasali lile kanisa! Najuta sana!” Nilimuambia, alizidi kuniuliza lakini nilijifanya kama nakua mgumu kumuambia, kama sitaki kuongea chochote.


“Nahisi Mchungajia natembea na mchumba wako, wapo karibu sana na nahisi kuna vitu wanakufanyia vya kishirikina ndiyo maana umebadilika.”Nilimuambia huku nikifuta machozi, nililalamika sana namna ambavyo nimekua nikitoa sadaka katika lile kanisa lakini sioni kinachoendelea. Nilimuambia kuwa Mchungaji badala ya kujenga kanisa basi anatumia pesa zetu kuhonga wanawake. Haikua kazi kubwa kumshawishi kwani alikua tayari chini yangu.


“Nahisi hata mimi, nilikua nashangaa ukaribu wao, kila siku mtu unaenda kwenye maombi kufanya nini? Kanisani tunaenda wote lakini kila jioni anaenda kwenye maombi na mchungaji, lakinu kuna vitu vingine anavifanya vinanichanganya tena sana.amenunua kiwanja tena kikubwa anataka kujenga, kwa hela gani, mbona msahara wake mimi naujua, kama si kuhongwa ni nini? Nilifanya maamuzi sahihi kumuacha. Simtaki tena yule mwanamke, abaki na Mchungaji wake….” Aliongea kuonekana kuwa hataki tena kusikia kuhusui Aneth.


Hilo kwangu lisingsesaidia, nilitaka afanye kitu ambacho kitamtibua Mchungaji.


“Huwezi kuwa na amani kwa kumuacha tu, ni lazima ukaongee na Mchungaji kumuambia kuwa unaujua uwkeli. Wanafanya mambo ya kishirikina, wanakuloga, uchawi uko hivi, ukishamjua mchawi wako na ukamuambia kuwa unajua yeye ni mchawi basi hawezi kukufanya chochote. Ushauri wangu, nenda kwa mchungaji, wakiwa pamoja basi nenda waambie kuwa unajua kuwa wao ni wapendi na wanakuloga lakini hawatakuweza kwani nawe una kinga.


Kuna kitu nitakusaidia, chukua hiki, najua huamini mambo ya kishirikina kwani hata mimi siamini lakini kwa ninavyowafahamu wale watu najua hawatakua na amani mpaka wakufanye kichaa. Mungu anasema jilindeni na mimi nitawalinda, chukua hii weka mfukoni ili ukienda kule hata kama wana mambo yao mabaya basi yasikukute!” nilimuambia huku nikimpa hirizi kubwa, alishtuka lakini hakuikataa, aliichukua.


Nilimshawishi kwenda kuonega nao, nilijau muda sahihi ni uleule ambao Mchungaji atakua amepanga kuongea na mimi, nilipompa ile hirizi nilijua kabisa hachomoki kwa kile nitakachomuambia. Nilimuambia mimi nitaenda pale kama nahitaji maombi na wakati anaongea na Mchungaji basi nitaingia ili tumuumbue pamoja.


“Hakikisha unavizia, akiingia tu ofisini na mpenzi wako kufanya mapenzi basi nawewe unaingia na kuwapa ukweli wao. Hakikisha unapoingia mkono wako upo mfukoni, umeishikilia hii hirizi ikulinde, huu si uchawi bali ni kinga.” Nilimuambia huku nikimkabidhi ile hirizi. Kweli siku ya siku alienda kama tulivyokua tumepanga, mimi nilikua nikimfuatilia wka nyuma, baada ya kuona tu kaingia kwenye ofisi ya Mchungaji ambayo ilikua palepale mkanisani.


Kaliklua ni kanyumba kadogo, kama kachumba na sebule, kadogo sana ambako kalijengwa na mbao hivyo kila kitu kilisikika. Yule mchumba wake hakutaka kuwapa nafasi, alipoingia tu alianza kupiga keleel akiwatukana akiwaita wachawi na kuwaambia wanatembea pamoja. Alikua kapaniki, akamvamia mchungaji na kutaka kumpiga, hapo ndipo niliiingilia kati na kumshika.


|Unataka kufanya nini? Huoni hii ni nyumba ya Mungu?| nilimuuliza huku nikimshika na kumpapasa mwili wake, haikua shida kugundua sehemu aliyokua kaweka hurizi yake kwani alikua kaishikilia mfukoni kama nilivyomuagiza.


Sikutaka kupoteza muda, niliutoa ule mkono wake mfukoni kwa nguvu, ikatoka ile hirizi kubwa ambayo nilikua nimempa.


“Mungu wangu! Unataka kufanya nini? Hivi ni vitu vya kuja navyo kanisani?” mchugaji alimuuliza hukua kianza kukemea, kwakua nilijua mwenye matatizo ni mimi niliona kama Mchungaji anataka kuniharibia, nilimshika yule kijana na kumtoa nnje.


“Umekosea, mimi nilitaka uongee naye tu lakini unataka kumpiga Mchungaji?” Nilimuuliza, kwa nnje kulikua na watu ambao walisikia kelele hivyo walishaanza kujazana ingawa hawakua wengi.


Sikujua kama wamesikia kila kitu hivyo nililazimika kuongea kwa nguvu ili wasikie na kumltea aibu yule kijana.


“Mchugaji kaiona hirizo yako, atajua umekuja kumloga, kimbia, ondoka hama na kanisa hili. Kila mtu atakuona mchawi, ondoka, chukua hirizi yako na aondoka!” niliongea kwa nguvu zaidi, wakati namtoa hirizo mkononi ilidondoka chini, Mchungaji alipoanza kukemea basi mimi niliiokota hirizi yangu na kutoka nayo.


Nilipoona watu pale nnje niliona kama ni furasa ya kumuaibsiha hivyo niliiiitoa na kumkabidhi, hataa hakuikataa, kama ambavyo mtu akifumaniwa anakua kama zezeta ndivyo ambavyo yule kijana alikua. Alifanya kila kitu nilichomuambia, alichukua hirizi yake na kuiweka mfukoni. Nilimkimbiza mpaka kwenye gari yake na kumuambia aondoke. Baada ya yeye kuondoka mimi nilirudi ofisini kwa mchungaji, watu walikua wamemzunguka wakimuulizia nini kilikua kimetokea.


Mchungaji alitaka kuficha, hakutaka kuwaambia kila kitu, niliona hapana, itaniharibia, ili Aneth anikubali ni lazima aonekane kudhalilika. Nilipoona Mchungaji haongei kitu kuwaambia kilichotokea nilijifanya kumsiadia. Nilimfuata mchungaji huku nikimshika kama kumuingiza ndani nilianza kuwasihi wale watu waondoke.


“Jamani, mpeni nafasi ya kupumzika Mtumishi wa Mungu, kuna makumbwa yametoke, anahitaji kufanya maombi. Yule kijana kaja hapa akimshutumu Mchungaji kuwa anatembea na huyu binti, kisa tu kaachwa kutokana na tabia zake. Wote tunajua kuwa hawa walikua wachumba, lakini binti wa watu kaona kabisa hawawezani kamuacha, basi kaja hapa kumshutumu Mchungaji, alikua anataka kumpiga na kaja na hirizi, hivyo mpeni nafsasi ya kupumzika Mchungaji.”


Nilijifanya kama namsaidia lakini sikua na nia hiyo, nilimuingiza Mchungaji ndani kisha nikaondoka nikiwa nimeongozana na Aneth amabye alikuja na gari yake. Nilim, peleka mpaka nyumbani kwao kisha nikarudi zangu mjin nikiamini kuwa kila kitu kitakua kimekamilika kwani kwa namna alivyokua akijisikia Aneth niliamini likuja suala la ndoa na mimi basi angekubali tu ili kukwepa aibu.


****


Mipango yangu ilitimia, ingawa niliongea kuwa Mchungaji anasingiziwa lakini kashfa ile ilileta madahara. Kuna watu wengi walikua na chuki na Mchungaji na wengine walikua wakimchukia Aneth, wote walibadilisha maneno kuwa yeye ndiyo aliachwa na sababu kubwa ni kutembea na Mchungaji, kwangu hii ilikua ni fursa kubwa, nilikuja kama mkombozi nikamfuata Mchungaji na kumuambia kuhusu nia ya kumuoa Aneth.


“Najua ni haraka lakini ni lazima kulinda heshima ya Kanisa na heshima yako pia, huyu Binti nikimuoa hakuna atakayeamini tena huu ujinga unaosambazwa. Yule kijana ana pesa, kila mtu anamsikiliza yeye, kakugeuzia kila kitu. Naamini kabisa kuwa hii yote ilikua ni Mipango ya Mungu, kumuumbua yule shetani ili mimi nipate nafsi ya kumkomboa huyu binti.” Nilimuambia Mchungaji, ingawa alikua na mashaka lakini alikua kama kachanganyikiwa, hakua na namna, alionega na Aneth.


Kusema kweli hata Anetha hakuuliza kitu, alipowamabia wazazi wake walikubali bila hata kunichumnguza, walikua wakimuamini mchungaji, ukiangalia na sadaka nilizokua nikitoa, ahadi nilizotoa na ikarubu wangu na kanisa kila mtu aliniona makaika. Ndoa ilifungwa harakaharaka na Aneth akaja tukaanza kuishi pamoja kama mke na mume.


Usiku wa kwanza nikiwa kitandani na Aneth sikumgusa kabisa, kila nilipokua nikitaka kumuingilia uume wangu ulikua hausimami, nilikua napata maumivu makali kila nilipokua nataka kufanya naye mapenzi. Nilijifanya kuwa sijisikii vizuri kisha nikalala nikiamini kuwa nitaamka na kuweza kufanya. Kwangu ule ndiyo ulikua usiku muhimu sana, ilikua ni lazima kufanya naye mapenzi siku ya kwanza ya kuwa naye la sivyo kila kitu nilichokua nimekihangaikia kingekua ni kazi bure.


Saanane usiku nilishtuka kutoka usingizini, tumbo lilikua linaniuma sana, nilianza kupiga kelele huku nikimuita mke wangu ili anisaidie lakini hakunyanyuka wala kufanya chochotye. Nilijitahidi kunyanyuka nikawahsa taa, kumuangalia mke wangu kitandani alikua hayupo, kaungalia pembeni ya kitanda alikua kapiga magoti kainama anasali.


Hapo ndipo nilijua sababu ya mimi kuumwa na tumbo, nilimsogelea na kumshika lakinia kiwa kapiga magoti, kainama chini mikono yake kainyanyua kwa juu kashikilia bibilia kwa mikono miwili huku akisali ni kama aliisogeza mokono yake bila kujua na ile bibilia ikanigusa. Nilishagusana na bibilia sana, hata mimi nilikua namiliki Bibilia lakini ile ilikua tofauti kabisa, ilikua ni Bibilia ya moto.


Nikisema ya moto basi jua ninaamanisha ya moto, ile mkono wangu kugusa tu nilihisi kama nimepigwa shoti, mwili mzima damu ilichemoka, palepale nilibanwa na mkojo. Nilinyanyuka kwenda kukojoa lakini miguu ilikua hainyanyuki kabisa, bila kujua nilijikuta naanza kukojoa palepale kitandani.


Nilikojoa mkojo wa moto, ulikua unatoa moshi kabisa na ukifika chini unakua kama uanchemka, mara nikaanza kukojoa damu, ukiigusa ni ya moto kabisa. Nilipiga kelele sana lakini mke wangu hakunyanyuka, seehmu ya haja ndogo ilikua inauma ssana huku ikichemka kama vile inapikwa. Mke wangu yeye alikua tu nbado kainama chini, hanyanyuki na wala sisikii sauti, kama ni kusalia alikua akisali kimya kimya.


ADAM anaingia kwenye ndoa na mwanamke ambaye alikua anaamini kuwa anaweza kubadilisha maisha yake. Lakinin siku ya kwanza tu anaanza kuona maajabu. Je unadhani kuwa nguvu ya Adam itashinda maombi ya Aneth” basi nisikuchoshe, tukutane katika sehemu ya tatu.


ADAM; CHEZA NA MIMI LAKINI USICHEZE NA MUNGU WANGU!–SEHEMU YA TATU


“Hapa kuna kitu, nispokua makini nitakufa! Hapana lazima nifanye kiyu!” Niliongea kwa nguvu, nilaicha kukojoa na kujirusha kuelekea alipokua mke wangu. Ulikua ni upande wa pili wa kitanda.


“Puuuuu!” nilidondoka chini kichwa kikitangulia, nilipata maumivu makubwa kichwani kisha nikaamka. Kumbe nilikua ndotoni, nilikua nimelala, haraka haraka niliwasha taa, mke wangu alikua chini, ni kama nilimdondokea, hakua amelala kitandani.


“Unafanya nini hapa chini?” Nilimuuliza huku bado nikiwa na wenge la usingizi, bado nilikua sijakaa sawa nilikua sijui kama nipo ndotoni au la. Kabla ya kunijibu nilimsukuma pembeni na kwenda upende wa kitanda ambao nilikua nimeukojolea. Nilianza kuushika kuangalia kama ulikua na damu au majimaji, sikuona kitu chochote hivyo niliangalai na chini sikuona kitu.


“Unatafuta nini mume wangu mbona hivyo?” Mke wangua liniuliza, sikumjibu, nilingalia chumba kizima sikuona kitu chochote.


“Mbona hujalala, usiku wote huu ulikua unafanya nini? Kwanza ni saa ngapi? Hembu naimbie, ulikua unafanya nini macho? Unataka kuniua?” Nilimuuliza huku nikitembeatembea kama natafuta kitu. Mke wangu alikua akinishangaa hukua kiuliza maswali mengi kwani nilikua kama nimechanganyikiwa.


Nilikua najisikia vibaya hivyo nilitaka anyamaze, lakini hakunyamaza aliendelea kuuliza maswali yake amabayo niliyaona kama ya kijinga. Alipoona sijamjibu alienda kwenye kimeza kidogo ambacho kilikua pale chumbani na kuchukua Bibilia.


“Unataka kufanya nini?” Nilimuuliza huku nikimfuata na kumsgika mkono. Tulikua nyumbani kwangu, baada ya ndoa ambayo hata haikua kubwa tukisingizia aibu kumbe sikua na pesa nilimuambia mke wangu turudi nyumbani halafu honeymoon tutafanya baadaye. Alikubali kwani hakua na makuu, ilikua ni bibilia yangu amabyo kila siku naenda nayo kanisani lakini nilikua siajwahi kuisoma.


“Nilikua nimeamka kusali lakini ukanikatisha, sikujua kama kuna Bibilia humu na mimi ya kwangu nahisi niliisahau.” Aliniambia. Si kama aliishaau lakini mimi ndiyo niliificha, bibilia yangu ilikua ni tofauti na bibilia yake, labda niseme, lilikua ni ganda la bibilia lakini ndani lilikua limejaa vitu vyangu ambavyo vilikua vinanisaidia katika maisha yangu. Sikua nikisoma Bibilia na wala sikutaka ifunguliwe katika nyumba yangu.


“Kila siku huwa mimi naamka usiku kwaajili ya kusali sasa…: Alianza kuongea lakini sikumpa nafasi, nilimsukuma akadondoka chini. Sikumpa nafasi kunyanyuka, hasira zilianza kunipanda, kichwani nilikua nikiwaza maumivu ambayo niliyapata wakati wa ndoto. Ingawa ilikua ndoto lakini yalikua maumivu makali sana kiasi mpaka wakati huo nilikua nikiyasikia.


“Hapa kwangu hakuna kusali! Mshenzi mkubwa wewe, nimekuambia kuwa hakuna kusali!” niliongea huku nikimfuata pale chini na kuanza kumpiga. Nilimpiga sana kuanzia ngumi, mateke na kila kitu.


“Wewe ni malaya tu, ndiyo maana Bwana wako alikuacha, unajifanya kusali kumbe unatembea na Mchungaji, nakuambia nitakuua. Nitakuua! Na sitaki uende kanisani, sitaki uende kazini wala sitaki utoke nyumbani, nakuambia nitakuua.” Nilimpiga sana mpaka akataka kupoteza fahamu.


Akiwa chini nilimfuata na kumnyanyua mpaka kitandani, hakua na nguvu lakini bado alikua anafahamu. Ilikua ni lazima kufanya mapenzi hivyo nililazimisha kufanya naye mapenzi lakini kila nikijaribu kufanya naye mapenzi uume wangu uligoma kabisa kusimama.


“Hiki ni kitu gani? Huyu mtu atakua mchawi, hiki ni kitu gani?” Nilijiuliza, ilikua ni mara yangu ya kwanza kitu kama kile kunitokea, katika siku ile muhimu ilikua ni lazima kufanya mapenzi na yule binti la sivyo dawa zote nilizokua nimepewa, mahangaiko yote yangekua hayana maana tena.


Mwili wake ulikua umemvimba, sehemu nyingi za mwili wake zikiwa zimevilia damu. Alikua anaongea kwa suati ndigo huku akinisihi kuwa nimuache kwani kachoka sana lakini sikuweza. Nilijaribu kila kitu ikiwa ni pamoja na kumuambia anishikeshike labda atanisisimua lakini ilishindikana.


|Mungu wangu ile ndoto isije kuwa ya kweli!” Niliwaza, akili iligoma, nikachukua simu yangu na kumpigia mtaalamu wangu ambaye ndiyo alinipa dawa.


“Hakikisha unafanya naye mapenzi leo na anabeba mimba yako, la sivyo kitakachotokea mimi sijui!”Aliniambia.


“Lakini mimi siwezi chochote na hata kama nikiweza sijui kama yuko kwenye siku za hatari au la?”Nilimuuliza nilikua nimechanganyikiwa.


“Hakikisha!” Aliniambia na kukata simu, nilipojaribu kumpigia simu tena hakuipokea kabisa na baadaye simu ilikatwa. Nilikaa kitandani nikimuangalia mke wangu akiwa uuchi wa mnyaama bila kumfanya kitu chochote. Wakati jua linachomoza nilijihisi kama maisha yangu yameisha, siku ile ilikua siku Muhimu sana katika maisha yangu. Kulikua na maagano mengi sana katika maisha yangu ambayo ilikua ni lazima kuamuliwa na matukio ya siku ile.


****


Kwanini Aneth, kwanini wakati ule, kwanini ilikua ni lazima kumuoa? Kwanini si mwanamke mwingine na ni yule binti tena mchamungu na kwanini nadhani kuwa maisha yangu yameisha baada ya kushindwa kufanya tendo la ndoa na binti yule? Labda niwarudishe nyuma kidogo.


Nakumbuka baad aya kumaliza chuo nilikua sina kitu chochote. Nilimaliza hcuo nikiwa na malengo makubwa sana, nikiwa naamini kwua nitaajiriwa na kufanikiwa. Nilimaliza chuo nikiwa na mawazo ya siwezi kufanya kazi ya mshaara chini ya milioni moja. Kitaaluma mimi ni Daktari hivyo nilikua naujua mshara wa daktari na nilikua najua kuwa nikimaliza chuo tu basi soko langu lipo njenje.


Wakati niko Intern nilikua nalipwa Posho hivyo nilijua mambo mbona yatakua mazuri kama nikilipwa mshahara kabisa. Nilikua na mpenzi wangu ambaye tuliahidiana mambo mengi sana, nikipata kazi nitaenda kwao kujitambulisha na kumuoa. Salma, binti wa kiisalamu ambaye tulishapanga kufunga naye ndoa, yeye alikubali kubadilisha dini kwaajili yangu, tulianza chuo mwaka mmoja lakini kama mnavyojkua sisi madaktari huwa tunasoma miaka mitano na yeye alikua anasomea uhasibu miaka mitatu.


Hivyo wakati mimi naingia chuoni mwaka wa nne, Salma alikua kashamaliza na kwa bahati nzuri kwake na naweza ksuema mbaya kwangu alipata kazi, tena katika Benki kubwa tu. Nilifurahi kwani alikua akinipiga tafu sana, nikiwa chuo nikikwama alikua akinipa pesa na karibu kila kitu. Lakini mambo yalibadilika baada ya mimi kumaliza chuo.


Sikurudi nyumbani, Salma alikua kapangisha nyumba kubwa, nyumba nzima kabisa. Aliniambia kuwa alipangishiwa na Kampuni aliyokua akifanya kazi. Alishanununua Gari yake ambayo aliniambia kuwa alipata mkopo kwani kwa Benki kwao kupata mkopo ilikua ni rahisi.


Yaani ndani ya miaka miwili mpaka mimi namaliza chuo alikua akiishi maisha ya ndoto zake. Tulikua vizuri mpaka nilipotaka kwenda kuishi naye pale. Mwanzo nilikua nikienda kwake, nalala hata siku mbili wakati mwingine mpaka wiki ila nilipomalzia chuo na kumuambia kuwa nahitaji kuishi naye kwanza aligoma akiniambia kuwa siwezi kuishi naye kabla ya ndoa.


Hapo nilimuelewa lakini sikua na kazi, sikua nikitaka kuishi naye bali nilitaka kujiweka wkake tu kwa muda.


“Niko tayari kuja mpaka nyumbani kwenu kujitambulisha…” siku moja nilimuambia. Nilikua naishi kwa mshikaji wangu ambaye naye alikua hana kazi ila nilienda kwake kumsalimia.


“Kuhusu Dini, sidhani kama nyumbani watakubali…”Aliniuliza swali ambalo lilinishangaza.


“Unamaanisha nini, wewe si uliniambia Mama yako hana shida, hata yeye alikua muiikristo hivyo wewe kubadili haitakua shida.


“Baba!” Aliniuliza, nilizidi kumshangaa kwani Baba yakea lishafariki dunia, nilihisi kama ni mtu ananiwekea vikwazo, sikutaka kumuulizia sana kuonekana kama namlazimishia. Nilinyamazam tu kimya nikimuangalia kwa huzuni.


“Sisemi kama siwezi kubadilisha dini, lakini sisi bado wadogo, mimi ndiyo nimepeta kazi, wewehata kazi bado hujapata, sasa mambo ya ndoa ni ya nini sasa hivi?”Aliniuliza, swali lake lilikua la msingi, si kama nilikua nataka ndoa kwa wakati huo lakini nilikua na wasiwasi sana kwa yeye kukataa mimi kuishi kwake kwa muda.


Baada ya kuopna tunabishana sana niliamua kuondoka na kurudi kwa msela, sehemu ambayo nilikua nikiishi. Lakini nikiwa kule Mama yake alinipigia simu, nilikua na namba yake na alishanitambulisha kwake ingawa haikuwahi kuwa rasmi.


“Acha kumsumbua mwanangu, kama unataka nikuharibie maisha basi acha kumsumbua!” mama yake aliniambia, hakusubiri hata nimsalimie, alienda moja kwa moja kunionya kuhusu mwanae. Nilishangaa, ingawa sikua nimeagana vizuri na Salma lakini hatukugombana kitu cha kumfanya kumuambia Mama yake.


Nilisema hapana, hii haiwezi kuwa sawa, nilimpigia simu mpenzi wangu lakini hakupokea, nilipiga sana ila simu iliita tu bila kupokelewa mwisho ikazimwa. Nilijua ana hasira, nilihisi labda nimemkosea, nikaamua kwenda kwake kuomba msamaha. Ilikua ni usiku lakini nilisema hapana, ni lazima kwenda kwake kuomba msamaha kwani sikua tayari kumpoteza.


Alikaua kiishi nyumba nzima ambayo ilikua na geti, nilijaribu kugonga Geti lakini halikufunguliwa, nilikaa pale nnje usiku mzima nikisubiria, sijui ni kitu gani kiliniambia nikae pale nnje, kulivyopambazuka nilijaribu kuugonga geti lakini bado sikufunguliwa. Kwenye saa nne hivi bado nilikua pale, Salma alitoka akiwa na Gari yake, alishangaa kuniona pale nnje namsubiria.


“Unafanya nini sasa hivi, mbona hukunipigia kuwa unakuja.”Aliniuliza, alionekana kuwa na wasiwasi sana lakini mimi sikujali, nilimuambia jana yake nilipiga simu sana lakini hazikupokelewa mpaka ikazima.


“Ohhhh! Kumbe wewe ndiyo ulinimalizia chaji yangu! Yaani simu ilikua sebuleni, imeita mpaka ikakata. Ingia kwenye gari twende!” Aliniambia, niliingia kwneye gari, lakini nilishangaa hafungi Geti kwa nnje wakati alikua anaondoka.


“Unaacha geti wazi…” Nilimuambia huku nikishuka kutaka kufunga.


“Acha! Acha! Acha kufunga, hivi kwanini unahangaika na mambo ya watu wewe!” Aliongea kwa hsiara hukua kisimamisha gari, aliruka kwa haraka na kuja kunishika ili nisiingie ndani. Lakini alishachelewa, mlango wa Geti alikua kaurudishia tu, wakati nikiwa nimeushika nataka kuufunga nikaona mtu kwa ndani.


Nilishindwa kuvumilia niliufungua kabisa na kuangalia, kulikua na mbaba mtu mzima kavaa kaptula tu akanipungia mkono. Nilitaka kuingia lakini Salma alinishika na kunivuta kwa nyuma kisha akarudishia mlango.


“Unataka kufanya nini wewe? Mbona unaingilia mambo ya watu, unaingia nyumba ya wtau hujakaribishwa!” Aliniambia kwa hasira huku akinivuta mpaka kwenye mlango wa gari yake.


“Unamaanisha nini wewe, yule mwanaume ni nani? Inamaana ndiyo maana ulikua hupokei simu zangu, yaani ulilala na mwanaume mwingine tena mtu mzima, yule si makamo ya Baba yako!” Niliongea kwa hasira nikitaka kurudi lakini alinizuia.


“Una akili kweli wewe, hivi unajua kuwa yule ni nani? Aisee wanaume masikini mnakua na shida sana, yaani kila dakika unahisi kama unasalitiwa! Daa unahosha sana my dear! Iko hivi ule si mchepuko wangu wewe!” Aliniambia huku bado akinishika kunizuia nisiingie ndani.


“Ni nani? Kama si mwanaume wako mbona hutaki nikaongee naye? Niambie ni nani?” Nilimuuliza huku nikijivuta kutaka kuiingia.


“Baba yangu mdogo!?” Aliniambia kwa hasira;


“Kivipi” unamaanisha nini? Kwanini Baba yako yuko hapa usiku huu tena kavaa vile?”Nilimuuliza.


“Nyamaza, usipige kelele, hembu njoo huku kwanza, ingia kwenye gari, kwanini unataka kuniharibia maisha yangu. Hivi unafikiri haya maisha ninayoishi yanatokana na mshahara wangu” kuna mtu ananisaidia, hembu kuwa na akili kidogo!” Aliongea huku akifungua mlango wa gari, alinisukumiza ndani kama zuzu kisha akaniambia nikae nisishuke kwani ninaweza kumharibia,


“Yule ni kama Baba yangu mdogo, yaani ni Bwana wa Mama yangu na ninavyokuambia sas ahivi Mama yangu yuko ndani, au unafikiri kwanini nakukatalia wewe kuja kukaa hapa?” Aliniuliza, nilishangaa kwakweli sikumualewa kabisa.


“Bwana kivipi?”


“Mchepuko wa Mama yangu, ni mwanaume wake!” Aliniuliza, nilihisi kuchanganyikiwa kwani Mama yake alikua ni mke wa mtu. Baba yake Salma alifariki wakati akiwa mdogo, alkini Mama yake alikuja kuolewa na wmanaume mwingine ambaye ndiyo alimfanya kubadilisha dini. Kwa maana kuwa kabla ya kubadilisha Dini kwa Baba yake wa kwanza salma alikua ni muikristo.


Mama yake aliolewa tena yeye akiwa na miaka mitano na hapo ndipo alibadilisha Dini na kuitwa Salma. Mama yake aliolewa, alikua katika ndoa nzuri, inagwa nilikua sijatambulishwa kwa huyo Baba yake wa kambo lakini nilikua namjua, hakua mtu mzima sana lakini alikua ni mtu na maisha yake na kwa jinsi walivyokua wakiishi basi usingejua kirahisi kuwa Salma ni mtoto wa kambo.


“Unamaanisha nini? Mama yako anachepuka? Kwanini?” Nilimuuliza hayo maswali bila majubu, aliniangalia tu kama vile nayeye ananishangaa.


“Mimi sijui sababu zake lakini yule ni mwanaume wake na hii nyumba ndiyo kanipangia mimi.kwa maana hiyo huyu Baba anakuja hapa kuonana na Mama yangu na kuna wakati wanalala hapa wote, Mama yangu naye anamuaga Baba kuwa anakuja kunisalimia na kulala kwangu kumbe anakuja kukutana na mwanaume wake.


“Inamaana Mama yako yuko ndani?” Nilimuuliza, alikaa kimya kidogo kisha akanijibu.


“Hapan! Saa nne hii, ameshaondoka kwenda kwenye Biashara zake, huyo Baba haondoki kwakua amemuaga mke wake kuwa yuko safarini hivyo anaka ahapa hata siku mbili au wiki….”Aliniambia, kbla kumjibu chochote kioo cha mbele upande wake kiligongwa. Alikishusha, alikua ni yule Mbaba niliyemuona mule ndani.


“Huyu nani” mnaongelea nini hapa muda wote huu?” aliuliza. Ni kitu ambacho Salma hakukitegemea, alikua akitetemeka kama vile karushwa kwenye dimbwi la barafu, alitaka kujibu lakini alishindwa…”


Ni nini kulimbadilisha Adam, kutoka kuwa Daktari mpaka kuamini ushirikina, je huyo Baba ni nani? Vipi atatoka salama kweli? Nisikuchoshe…


ADAM; CHEZA NA MIMI LAKINI USICHEZE NA MUNGU WANGU!—SEHEMU YA NNE


Alikua ni Baba mtu mzima na bado alitoka nnje akiwa na kibukta chake, hakuonekana sana kujali.


“Huyu ni Kaka yangu, mtoto wa Baba, yule anayenilea, alikuja kumuangalia Mama huku!”Salma aliongea harakaharaka, huku akimkonyeza, ni kama alikua anamuambia kitu kingine tofauti na kile, yule Baba alinyamaza na kurudi dnani.


“Kwanini umemuambia kuwa mimi ni Kaka yako? Inamaana mimi ni Kaka yako?” nilimuuliza kwa hsaira huku nikimshika na kutaka kumpiga, nilihisi kuna mchezo nachezewa.


“Hivi una akili kweli, Mama yangu anamdanga huyu mwanaume, katuipangishia nyumba tunaishi, unataka nimuambie namimi naleta mwanaume wangu humu!? Nitaonekanaje, wewe mwenyewe huoni aibu kwamba uonekane unakuja kumuona mwanamke wako kwenye nyumba ambayo kapangishiwa na mwanaume mwingine?” Nilijikuta nanywea kwa majibu yake, nilijisikia vibaya mpaka kutaka kushuka kwenye Gari Lake, lakinia linisihi na kunibembeleza.


“Mimi naondoka, nina mambo yangu, sas akuhusu Mama, mbona alikua anaongea kama anatak tuachane?” Nilimuuliza.


“Achana naye, Mama nammudu, ila acha kasi yako ya kutaka kunioa wakati huna kazi, kama vipi tafuta kazi uwe na kitu cha maana ndiyo uje kwangu. La sivyo itakua shida, mimi sasa hivi nina mambo mengi, siwezi kukuhdumia tena!” aliniambia, sikua najibu la maana la kumpa, nilikua nampenda salma yeye ndiyo alikua kila kitu katika maisha yangu.


Tuliondoka mpaka mjini ambapo aliniacha, siku hiyo ilikua ngumu sana kwangu, nilikua na mawazo mengi. Ingawa niliambiwa kuwa yule mwanaume alikua ni mchepuko wa Mama yake lakini sikua na amani kabisa, nilikua nawaza kama Mama yake anaweza kufanya yale mambo meble yake vipi yeye, si anaweza kufanya zaidi.


Niliwaza sana kama chizi, nilikua nikitembea kama mtu aliyechanganyikiwa, yaani hata watu walioniona siku hiyo walikua wananishangaa.


“Mama nisamehe kwa jinsi nilivyomuongelea mwanao, lakini naumia sana, sijuii kama bado ananipenda?” Nilishindwa kuvumilia, mchana wakati nimekaa baharini sina hili wala lile nilijikuta nachukua simu yangu na kuanza kumpigia Mama salma. Ilikua ni lazima kuongea na mtu kwani nilikua nakaribia kudondoka kwa mawazo.


“Unamaanisha nini? Mbona kijana sikuelewi.” Safari hii Mama yake alikua akiongea kwa upole, alikua kama vile ananibembeleza tofauti na mwanzo.


“Naona kam akuna vitu vimebadilika Mama, yaani kawa watofauti kabisa, sijui kama ananipenda au la. Nimeenda kwake nimekuta kuna mwanaume anaishi naye, sasa nawaza kama ni mwanaume wake au la?” Nilimuuliza, ingawa nilishaambiwa kuwa ni mwanaume wa Mama yake lakini nililazimika kuuliza, nilijua si heshima kuongea na Mama mkwe yale mambo lakini sikua na namna, ilikua ni lazima kuongea.


“Yule ni Baba mkwe wako, huna haja ya kuwa na wasiwasi. Kama una wasiwasi njoo usiku, nitakuja nataka kuwatambulisha kwani naona kama hiki kitu kinaleta mzozo.” Aliniambia, yule Mama alinijulia, alikua akijua kubembeleza sana kiasi cha mimi kuingia laini, alitaka kwenda kunitambulisha kwa yule mwanaume ila nilikumbuka maneno ya Salma, hakutaka wote kuonekana kama tunamdanga yule mwanaume. Niliona kama si kitu kizuri hivyo niliamua kumuamini na kukubaliana naye.


Nilirudi kwa mshikaji nilipokua nimekaa, sikuweza kuongea kitu chochote ingawa nilikua na mawazo mengi sana. usiku nilijaribu kumpigia simu mchumba wangu ili kuona kama yuko na yule mwanaume. Nilijua kama yuko na mwanaume basi hatapokea simu zangu. Alipokea lakini wakati tunaongea nilisikia sauti ya kiume humo ndani, ni kama mtua likua anamsemesha.


“Nani huyo?” Nilimuuliza, alianza kwa kucheka huku akiniambia kuwa nina wivu sana.


“Si nimekuambia naishi na mchepuko wa Mama, kama huamini njoo umuone. Mama yupo wako huko chumbani,ndiyo katoka chumbani sijui walikua wanafanya nini, kama vipi na wewe njoo, ila sitaki mambo ya kuonana onana naye, mambo ya MKama yangu anafanya mapenzi chumba cha pili na mimi nafanya sitaki!”


Aliniambia kwa kujiamini, nilimkubalia kishongo upande lakini rafiki nyangu ambaye alikua pembeni anasikiliza aliniambia.


“Hakuna kitu kama hicho ndugu yangu, unaibiwa, huyo mwanamke ajnamdanga huyo Babu wa watu. Hakuna kitu kama hicho kwamba binti aishi na danga la Mama yake!” Aliniambia, alinichochea sana huku akinicheka.


“Huna pesa, binti ana kazi,ana gari wakati wewe huna kitu, unaibiwa, kama vipi nenda uone kinachoendelea humo, kama atakufungulia mlango basi si mtu wake, lakini kama akigoma basi jua kuwa hakuna cha Mama wala nini!”


Sikufikiria hata mara mbili, baada ya kuambiwa hivyo moja kwa moja nilinyanyuka, ilikua usiku lakini ilikua ni lazima kwanda. Nilikua na kama buku tano mfukoni, nikachukua Bodaboda mpaka alipokua akiishi Salma. Ilikua ni nyumba ya Geti, kufika mlangoni nilimpigia simu ili afungue mlango nataka kwenda kulala. Sikutegemea kama atafungua, nilijua kwakua yuko na mwanaume wake basi atakataa kufungua na hapo ndipo nitaamini kuwa nasalitiwa.


Lakini haikua hivyo kabisa, ile namuambia kuwa nipo nnje aliniitikia kwa furaha, alikuja kufungua geti, akanikumbatia na kuniambia niingie ndani. Nilishangaa kwa alivyokua amevaa, alikua amevaa nguo laini ya kulalalia, kilikua ni kikaptula tu na kitop ambacho ni chepesi sana maungo yake yote yalikua nnje, ni kama alikua uchi kwani kwandani ulikua unaona kila kitu.


“Ndiyon unavaa hivi ukiwa nyumbani wakati mwanaume wa Mama yako yupo?” nilimuuliza.


“Kwani kuna ubaya gani? Usiku unataka nivae nini tena, halafu nimekuja kukupokea wewe mpenzi wangu badala ya kufurahia kuwa ninakutega wewe unaanza kulalamika kuwa nimeavaa vipi, kwani nini cha ajabu hapa!” aliongea kwa kulalamika, alitembea harakaharaka kuingia ndani kama vile kakasirika, nilimfuata nyuma bado nilimuelezea madhara ya kuvaa vile.


“Hata kama unanifungulia mimi lakini sipendi, hivi huyo mwanaume akikuona katika hali hii hudhani kama atakutamani?” Nilimumbia lakini hakujali, aliondoka kama ananikwepa kuwa nina kisirani. Niliingia ndani moja kwa moja nikakutana na yule baba. Salma alikua kasimama anabishana naye.


“Kaka yako unamvalia hivi, si kama uko uchi kabisa!” Yule Baba alikua akilalamika. Alionekana kama mtu aliyekua kalala katoka chumbani.


“Nyew atgua cheni kunichanganya, hivi wanaume mna matatizo gani, kila dakika mnawaza ngono tu. Babu rudi chumbani kwako, Adam, kalisha matakoc hini, hamuwezi kunipangia namna ya kuishi, kama mmeniangalia na mnatamani mwili wangu basi uchukueni!”


Aliongea kwa hasira huku akimsukuma yule Baba mpaka chumbani, walikua bado wanabishana kama yule Baba alikua anataka maelezo lakini hakumruhusu. Nilikaa pale nikisubiri, walikaa ndani kama dakika ishirini hivi bila kutoka. Nilianza kupata wasiwasi, nikahisi labda kuna kitu wanakifanya, nilinyanyuka na kusogea mpaka mlangoni kutaka kusikiliza kama nitawasikie kelele wakifanya mapenzi au wakiongea lakini sikusikia kitu. Nikiwa pale mlangoni mlango ulifunguliwa.


“Unasikiliza kama nitapiga keleel za mapenzi?” Aliniuliza baada ya kuniona mlangoni. Nilinyamaza bila kusema kitu.


“Unataka kujua kama nafanya three4some na Mama yang?”Aliniuliza tena, sikumjibu chochote kwani sikua na chakuongea, alinishika mkono mpaka chumbani.


“Mbona leo tunalala huku?” nilimuuliza kwani tulikua tunalala chumba cha wageni, haikua mara yangu ya wkanza kulala kule siku zote nilikua nikilala katika chumba kikubwa lakini siku ile ilikua tofauti, nilikua nalala chumba cha wageni.


“Anayelipa kodi yupo, amelala na Mama yangu chumba cha pili, inamaana unataka tukalale huko?” Alinijibu kwa kejeli kidogo, nililazimika kunyamaza, kweli nilijiona mjinga. Tuliiingia ndani, kichwani nilikua najua kama amekesha na yule mwanaume basi hataweza kufanya mapenzi na mimi, lakini ilikua tofauti kabisa, Salma alikua na hamu sana ya kufanya mapenzi na mimi, ile kuingia tu alinivamia kaisi kwamba mimi kutokana na mwazo nilishindwa kufanya chochote.


“Huu sasa ni ujinga, kama ulijua umeenda kulala na wanawake zako huko kwanini ulikuja kwangu? Au umekuja kunionyesha kwua nawewe unaweza kuchepuka, unaweza kuwa na wanawake wengine?”Aliniuliza kwa hasira.


“Inamaana unachepuka, inamaana una mwanaume mwingine?”Nilimuuliza.


“Acha kuniona mjinga, najua huniamini, unadhani kama natembea na huyu Baba ndiyo maana umekuja usiku huu. Sasa kama umekuja basi kuwa mwanaume sio unakuja umelegea kama mlenda hapa halafu unajifanya kuona wivu!”aliongea kwa hasira kisha akageukia pembeni, hakutaka nimguse kabisa mpaka asubuhi yake.


****


Nilikua nikienda pale, siku nyingine nilikua nikikutana na yule ababa lakini sikunyingine sikumkuta. Ingawa niliambiwa kuwa ni mwanaume wa Mama yake na mara kadhaa nilikua namkuta Mama yake pale lakini nilikua sijawahi kukutana wakiwa pamoja, yaani kumuona Mama yake anaingia chumbani na yule mwanaume. Hali hiyo iliniumiza sana kwani nilikua nahisi naibiwa na mbaya zaidi nilikua sijui namna ya kumuuliza salma.


Nilikua nampenda sana, yeye ndiyo alikua mwanamke wa maisha yangu, sikutaka kumuudhi, nilijua nikimuuliza atakasirika na kuweza hata kuniacha.kuna wakati mambo yalikua magumu kwangu, rafiki yangu niliyekua nikikaa naye alipata mwanamke wakawa wanaishi naye, sogea tuishi, si ndoa lakini wanaishi tu. Kwakua alikua na chumba chake kimoja sikua na namna, nilienda kwa Salma kuishi naye, ingawa hakutaka lakini nililazimishia.


Nilikua najisikia vibaya sana kwani mara nyingi yule Baba akija anakua kakasirika, sijui kwanini ila alikua naye kama anamouogopa. Alikua akiingia tu akinikuta moja kwa moja anaenda chumbani kwake,a nakaa huko na kutuacha sebuleni, baada ya hapo mimi na Salma tunaingia chumbani kwetu na kufanya yetu. Sikuwahi kumuona Mama yake akija pale usiku, lakini kuna wakati Salma alikua akimka, nikimuuliza unaenda wapi ananiambia kuwa anaenda kumfungulia Mama.


“Kaa hapa, sitaki utoke, Mama akijua kua unalala hapa itakua shida!”Basi hutoka na kukaa kama dakika kumi au ishirini hivi kisha anarudi na kuendelea na mimi.siku moja alinyanyuka na kuniambia kua anaenda kumfungulia Mama yake, mara zote akiwa anaenda kumfungulia Mama yake simu yake huita na hapokei ila huniambia ni Mama hivyo anatoka na mimi nabaki kitandani sina wasiwasi.


Lakini siku hiyo alinyanyuka tu na kuniambia kuwa anaenda kumfungulia Mama yake. Alinyanyuka na kutoka, alipofika mlangoni ndipo nilishtuka kuwa, Mama yake hakupiga simu wala sikusikia geti likigongwa.


“Kuna kitu hapa! Yeye kajuaje kuwa Mama yake amekuja! Hapana kuna kitu!”Niliwaza huku nikitoka kuchungulia, taa ya sebuleni ilikua imewashwa, nilichungulia na kumuona anatoka kwenda nnje. Nikaenda kumfuata, niaksikia geti linafunguliwa ksiha likafungwa akarudi. Lakini cha kushangaza alirudi bila Mama yake.


Nilikua nimejibanza pembeni ya sofa namuangalia tu, aliporudis ebuleni alizima taa hivyo sikuona kama kaingia wapi. Basi nilirudi chumbani huku nikijipa moyo kuwa labda alihisi Mama yake kaja lakini haikua hivyo, Mama alikua hajafika. Niliingia chumbani lakini sikumkuta, chumba chetu ni selfu hivyo niliijngia mpaka chooni sikumkuta.


Nilikaa kama dakika tano hivi, nikasema hapana, lazima kuna kitu, nilinyanyuka mpaka sebuleni, nikasogea mpaka kwenye chumba cha yule Baba. Nilimsikia yule Baba akipiga kelele za mapenzi, hasira zilipanda nikaubamiza mlango lakini ulikua umefungwa. Nilianza kugonga kwa nguvu huku nikimuita, lakini mlango haukufunguliwa, yule mzee aliendelea kupiga kelele kama vile anafika kileleni mara ghafla nikaona kimya.


Nilikaa kama dakika mbili hivi nikigonga mlango, sikusikia chochote. Mara salma alitoka, alikua kavaa nguo zake za kulalia ambazo alizivaa wakati anaenda kumfungulia Mama yake mlango. Nilimvamia na kumshika kuanza kumpiga makofi huku nikimuuliza kwanini alikua ananisaliti.


Yeye alikua ananisukuma tu huku akijiteteea kuwa alikua hanisaliti.


“Nani akusaliti, mimi nilikuja kumfungulia Mama naingia ndani nasikia kelele huku chumbani ndiyo nikaja, sasa unaona Baba wa watu sijui amekufa,sijui kazimia, mimi sijui kitu!” Aliongea huku akikimbia na kuwasha taa. Niliangalia pale kitandani nilimkuta yule mzee kalala chali,huku kafunikwa shuka juu mpaka usoni.


“Umemuua Mzee wa watu?” Nilimuuuliza, alibaki kasimama ananiangalia, anaonekana kama ana wasiwasi.


“Mimi sijamgusa, nimeingia huku nimsaikia makelele nikasema anmsaidia sasa sijui alikua anafanya nini!” Aliniambia, nilijua kabisa kuwa ananidanganya.


“Unamaanisha nini wakati nimemsikia akipiga kelele za kufanya mapenzi, alikua anafanya mapenzi na nani wakati Mama yako nimekuona umeenda kufungua mlango Mama yako hayupo!” Nilimuuliza, alibaki kimya kwa muda, nilimfuata na kuanza kumdunda tena.


“Nataka uniambia huyu Baba ni nani? Kama ni mpenzi wako nakuhakikishia kuwa ankuacha kuanzia leo!” niliendelea kupiga kelele lakini hakunijibu.


“Nimekuambia mimi nilisikia kelele, Mama sijui yuko wapi, aliniambia anakuja niende kumfungulia lakini hakuepo. Niliporudi ndiyo nikakuta hiki kitu!”


“Kama ulisikia kelele kwanini ulifunga mlango, mimi najua mlichokua mkikifanya!”Nilipiga kelele nikianza tena kumpiga lakini alibadilisha mada.


“Bwanaeee! Hivi una wivu wa kijinga namna gani, hivi Baba wa wtau kalala amekufa wewe unapiga kelele kuwa umesaloitiwa!” Aliongea kwa hasira huku akinisukuma pembeni na kuenda kumuamsha yule Baba. Nilishtuka kidogo na kukumbuka yule baba alikua pale chini tunabishana hata hajitambui.


“Unafikiri watu wakija hapa wataonaje? Si wote tunafungwa!” Aliongea huku akizidi kumuamsha yule Baba loakini hakuamka.


“Nifungwe kwani mimi nimefanya nini?” Niliuliza kwa msahangao.


“Umefanya nini? Watu wanajua wewe ni mpenzi wangu, wakija hapa wakisema labda umekuja kunifumania, ukanikuta na huyu Baba halafu ukampiga mpaka kumuua?”Salma alionega kama utani lakini maneno yake yaliniingia, ni kama alikua kapanga kitu.


“Unamaanisha nini? Yaani mambo yako unataka kuniingiza mimi!”


“Sijakuingiza lakini wewe ndiyo hutumii akili, unaingia tu na kuanza kunipiga, hivi nikiamua kupiga kelele hapa si unaishia jela. Nikisema umenifumania ukamuua Baba wa watu na unanipiga unataka kuniua na mimi?”


Nilijikuta naishiwa nguvu hata ya kunyanyua mdomo. Kwa kumuangalia yule Baba nilijua kuwa amekufa tayari, maneno ya Salma yalimaanisha kuwa naenda kufungwa maisha.


“Tena wewe ndiyo utaonekana mgomvi maana umekuja nyumbani kwake, hii nyumba kapangisha yeye! Umekuja kufumania ukampiga na kumuua, haya si mauaji ya kukusudia!” Alizidi kuongea, alinyanyuka na kunifuata kisha akaniambia.


“Nipige, endelea kunipiga, wewe si mwanaume, huyu Baba akifa unafikiri itaonekanaje kama akifa huku umenipiga na kuniumiza!?”


Najua unataka kujua, msala utaishaje na Salma, vipi kuhusu Aneth, ilikuaje mpaka Adam kwenda kwake, je waliachana kwanza na Salma au kuna nini hapa? Usikose….


ITAENDELEA….


ADAM; CHEZA NA MIMI LAKINI USICHEZE NA MUNGU WANGU! —SEHEMU YA TANO


“Njoo huku, muache hapo kitandani!” Salma aliniambia kwa hasira huku akinivuta kutoka nnje. Nilikua kama zezeta, kitendo cha kuniambia kuwa anaweza kupiga kelele na mimi kukamatwa kiliniogopesha hivyo kunifanya kunywea na kukubaliana na kila anachokitaka. Alinivuta mpaka chumbani harakaharaka, kufika alinisukuma kitandani na kuvua nguo yake ya kulalia aliyokua ameivaa.


“Unataka kufanya nini?” Nilimuuliza lakini hakujibu, alinivamia kitandani na kunivua nguo.


“Una akili wewe, yaani Baba wa watu amelala kitandani sijui kafa au yuko hao wewe unataka kufanya mapenzi?” nilimuuliza huku nikijaribu kumsukuma, lakini hata nguvu nilikua nazo basi, alishanivamia, alinilazimishia mpaka nikajikuta nimefanya naye mapenzi.ingawa akili yangu haikua pale lakini sijui ni kitu gani kilitokea siku ile, nilijikuta nafanya mapenzi kuliko kawaida, mwisho nilijikuta nimelala usingizi bila kukumbuka hata kulikua na mtu kalala chumba cha jirani hajitambui.


Saa kumi na moja asubuhi nilishtuka kutoka usingizini. Haikua kawaida yangu kuamka wakati huo, lakini niliamshwa na Salma ambaye alinyanyuka kama ananyata kutaka kuondoka. Tayari kulishaanza kupambazuka ingawa kulikua na kigiza kidogho, niliwasha taa na kumshtua katika kutembea kwake.


“Unafanya nini? Mbona unaondoka kwa kunyata? Inamaana unataka kuniachia huu msala?” Nilimuuliza kwa hasira huku nikinyanyuka kumkimbilia. Alitaka kukimbia kutoka lakini nilimuwahi na kumrudisha.


Akili yangu ilikua ikiwaza kuwa labda alikua anataka kutoroka mule ndani na kuniacha na maiti ya yule Baba. Nilimrudisha na kumtupa kitandani kisha nikaanza kumfokea.


“Wanawake wkeli ni mashetani, yaani unataka kuniacha na mwanaume wako huku ndani, unataka kufanya nini? Huyu mwanaume kama nikumuua umemuua wewe, si mimi, lakini unataka kuondoka, ili nini? Unataka kwenda kuwpaigia simu Polisi kuwa nimeua? Niambie! Unataka kufanya nini?”Nilimfokera kwa nguvu.


“Hembu nyamaza basi, unapiga kelele wakati hujui kitu? Hakuna mtu wa kukukimbia, nyamaza atakusikia!” Aliniambia kwa ukkali kidogo lakini kwa sauti ya chini, ni kama kuna kitu alikua anakikwepa.


“Unamaanisha nini?” Nilimuuliza, aliniambia nikae chini anielezee, niligoma kukaa nikitaka aniambie vilevile nikiwa nimesimama.


“Yule Baba hajafa, alikua kalala, ndiyo kawaida yake…” Aliongea kwa uoga flani hivi.


“Kawaida yake kivipi?” Nilimuuliza. Usiku huwa anakunywa dawa za usingizi, akilala analala kama mtu aliyekufa, hivyo mimi huwa nina kawaida ya kwenda kumkagua. Namuivia pesa halafu narudi nazo, jana nilipoona umeingia nilichanganyikiwa!” Aliniambia, siriasi alizidi kunichanganya kwani haikua inaingia akilini.


“Kama ni hivyo mlango ulienda kufungua wanini?” Nilimuuliza, alikaa kimya kidogo kisha akanyanyuka na kutaka kutoka.


“Ulienda kumfungulia mlango wa nini? Halafu mbona ulijifungia ndani, kama unataka kumuibia mtu kunakua na haja gani ya kujifungia naye chumbani. Kwa uelew3a wangu nafahamu, kama unaenda kumuibia mtu basi unaacha mlango wazi ili labda akizinduka ndiyo unakimbia, sasa wewe unajifungia ndani.” Nilimuambia huku nikimshika, hakua na majibu, alinisukuma pembeni na kuondoka zake. Nilitoka huku nikitaka kumfuata, lakini aliubamiza mlango usoni kwangu, sijui alichukua funguo saa ngapi lakinia linifungia kwa ndani na kuondoka.


Nilipiga kelele kufunguliwa mlango lakini hakuufungua. Sikua na majibu ya maswali yangu na bado nilikua simuamini. Nilisukuma sana lakini hakufungua mlango, mwisho niliona ni ujinga, nikabaki kimya nikimsubiria.


Dakika kama kumi hivi mlango ulifunguliwa. Nilianza kufoka kabla hata ya kumuona aliyekua anafungua.


“Acha kelele katika nyumba yangu, ukiendelea hivi nitakufukuza, naaambiwa umelewa tangu jana unasumbua watu hawajalala!” Alikua ni yule Baba, pande la mtu limesimama mbele yangu. Alikua kavaa kikaptula tu, nilijikuta nanywea nanyamaza sijui hata nimjibu nini. Nilitaka kuchungulia kuona kama Salma alikua bado yupo ndani lakini hakuniruhusu, alikua kazimama katikati ya mlango.


“Wewe ni nani humu ndani? Unakuja kulala lala tui humu unatupigia kelele?” Aliniuliza, nilibaki kimya sina cha kujibu, aliniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akaondoka. Nilimfuatilia kwa macho, kulikua ndiyo kunapambazuka lakini niliweza kumuona, aliingia chumbani kwake na kufunga mlango. Sikutaka kuendelea kukaa tena mule ndani, nilivaa nguo zangu harakaharaka na kutoka, wakati natoka sebuleni nilisikia Salma akibishana na yule mwanaume.


“Nimekuambia kama ni kibwana chako nitakuua! Sitaki ujinga, tena nilishakuambia sitaki ndugu zako humu! Hata Mama yako anakuja huku kufanya nini?”


“Nimekuambia ni Kaka yangu, hana kazi mjini anakuja huku kushinda kwangu, anakunywa pombe sana kwakua ana stress, nimekuambia mara ngapi umtafutie kazi lakini hutaki. Mpe kazi, kama unanipenda mimi kwanini hutaki kusaidia ndugu zangu. Mimi naona kama tuiachane, mambo ya kutishiana kuuana sitaki!” Salma alilalamika.


Ingawa nilishahisi muda mrefu kuwa yule ni mpenzi wake lakini sikua na uhakika. Kuna kitu kilikua kiinaniambia kwua Salma hawezi kunisaliti, tumetoka mbali, ananipenda. Sikutaka kukubali kabisa kuwa anaweza kuwa na mwanaume mwingine. Kumsikia akisema vile kulinifanya nishindwa hata kuondoka, nilijikuta natembea mpaka kwenye Kochi, viatu vyangu mkononi nikakaa.


“Sijakutishia, nimekuambia kama unanisaliti nitakuua, mimi nakuhudumia kila kitu lakini bado uwe na mwanaume mwingine!?”Yule Baba aliendelea kulalamika.


“Wewe si una mke wako, kuna siku ulishasikia nalalamika, mimi si nakupigia simu usiku hupokei? Ni mara ngapi mke wako anakuja ofisini mimi nipo lakini nakaa kimya! Baba ni hivi, wewe una mke wako na mimi naweza kuwa na mwanaume yoyote yule nikitaka!”


“Unamaanisha nini, sasa? Unamaanisha kuwa huyu mlevi ni mwanaume wako!” Alimuuliza kwa hasira, nilihisi kama anamkaba kwani Salma alianza kupiga kelele.


“Niache, nimekuambia kua uniache! Huyu ni Kaka yangu ila nikitaka kuwa na mwanaume nakua naye na huna chakunifanya, kama hunitaki niache! Siwezi kuwa mtumwa wako, mimi ni mwanamke mzuri, rafiki zako wengi wananitaka, ukiniacha leo kesho napata Mwanaume mwingine, tena wamaana kuliko wewe!


Kila siku unajifanya unanipenda lakini hakuna cha maana unachonipa, au hiki kigari chako cha milioni kumi na mbili ndiyo unahisi kama utanitisha! Baba kuna watu wapo tayari kunipa hati ya nyumba si wewe umenipangishia kibanda hiki unaringa hata ndugu zangu hutaki kuwaona! Nimechoka, naondoka na baki na kinyumba chako hiki! Unanikaba unataka kuniua kisa nini!”


Aliongea kwa nguvu, ghafla nilimuona anatoka hukua kashikilia nguo zake za ofisini. Aliniona nikiwa nimekaa pale lakini hakujali, alikaa pembeni yangu na kuvaa vizuri kisha akaanza kulalamika.


“Hivi wanaume mnakuaje? Kutembea na mwanamke mara moja ndiyo unataka kumpangia maisha, mimi bado binti, hakuna mtu aliyenioa wala kunivalisha pete, hata kwetu hakuna mbuzi hata moja ambaye alishawahi kuja halafu mtu anataka kunipangia maisha!” Aliongea kana kwamba anaongea na shoga yake, nilimuangalia kwa hasira nikataka kumtandaika makofi lakini nilijizuia, nilikua na hasira sana nikajua kama nikianza kumpiga basi nitamuoa.


“Unaongea nini? Inamaana huyu Baba ni mwanaume wako?” Nilimuuliza huku nikimvuta bega kutaka aniangalie.


“Acha ujinga, mimi nikajua madaktari ndiyo wenye akili ya maisha kumbe wapi hakuna kitu. Yaani kweli uliamini kuwa huyu Baba ni mchepuko wa Mama? Kweli wanaume hamna akili kabisa. Inamaana kila siku usiku wakati natoika kwenda kufanya mapenzi nayeye huonagi?” Aliniuliza kama ni kitu cha kawaida, nilimshika na kumkaba koo lakini alifanikiwa kutoka, alichukua vitu vyake na kuanza kutoka nnje.


Yule Baba alitoka, alisikia kila kitu, badala ya kumkasirikiia yeye na kuniona kama mimi ni mhangaa lainvamia na kuanza kunipiga. Inagwa alikua na umri mkubwa lakini alikua na mwili mkubwa, alinivamia na kuniangukia kama Gogo la mti, alianza kunipiga, lakini name sikua mzembe kaisi hicho, nilijitahidi na kumuodnoa juu yangu. Tulianza kurushiana ngumu.


Nilipigana naye sana mwisho wote tulichoka.


“Ondoka nyumbani kwangu, sitaki kukuona tena wewe na malaya wako, unakuja kwangu na kujifanya kuwa ni ndugu yake kumbe ni mwanaume wake!”Aliongea sana na kunitukana kama mjinga flani, nilijisikia vibaya jinsi nilivyokua nikidhalilikana elimu yangu. Nilitoka pale kama yatima, niakchukua vinguo vyangu, yule Baba alihakikisha kuwa nadhalilika, alitoka mpaka nnje huku akinitukana, yaani watu waliokua nnje waliniona, nilijisikia vibaya sana.


Sikua na hata shilingi kumi mfukoni, hali yangu ilikua mbaya, nilianza kutembea taratibu nikiwa na mawazo mengi. Nilitembea kwa umbali kama wa mita mia hivi kisha ikaja na kusimama Bodaboda pembeni yangu. nilikua skama sijamuona wala kumsikia dereva wa ile bodaboda aliyekua akiniita.


“Broo, nakusalimia….” Alirudia baada ya kuona niko mbali, nilikua nahasira na nilimuona kama mchawi flani, mtu amabye anataka kuendelea kuniharibia siku yangu. lakini kwakua sikua na chakufanya, sikua na pakwenda basi niliamua kiumsikiliza.


“Nimekuona unatoka kwa yule sister, unafanya kazi pale au ni demu wako?” Aliniuliza, nilimuangalia kwa hasira nikamuona kama mmbea flani, basi niliachana naye na kuendelea kutembea.


“Brooo, nataka kukusaidia, tumkomeshe, nakuambia kuwa kama ni demu wako alivyokufanyia si sawa, anaingiza wanaume mule ndani kama nini? Nakuambia unawez akumkomesha!” Aliniambia lakini sikumjali, nilimuangalia kwa dharaau nikasema huyu vipi, atanisaidia nini? Hapana, atakua ni kibaka tu!”


Nilijisemea na kuendelea kutembea, alizidi kunifuata sasa ikaw akama ugomvi, nilijikuta namgeukia na kumshika kumkunja nakutaka kumpiga. Lakini alinizuia, ingawa alikua na mwili mdogo lakini alionekana kuwa na nguvu kuliko mimi.


“Nataka nikusaidie tu Broo, yule Baba alivyokua anakutukana si sawa, alazima ufanye kitu.” Aliniambia hukua kinitoa mikononi mwake, hapo nilihisi kutaka kuongea naye tu, aliponiambia kuhusu yule Baba nilihisi kama anataka kulipa kisasi. Nikaamua kumsikiliza.


“Unasemaje, ulikua unataka nini kutoka kwangu? Kama ni kukupa pesa ili ukempige siwezi, sina pesa…”“Hapana Kaka, Mimi sina shida kabisa ya pesa, nian shida na wewe. Siku nyingi nataka kukuzoea lakini nashindwa, kuna kazi nataka kufanya nawewe. Najua huna kazi, nataka nikupe kazi.”


Nilianza kucheka tu baada ya yeye kuongea, nilimuona kachoka, maisha magumu, nikaona kama vile ni tapeli.


“Wewe mwenyewe huna kazi halafu unataka kunipa kazi? Una akili kweli?”Nilimuuliza, aliniangalia kwa dharau kisha akacheka. Akaingiza mikono mfukoni na kutoa kibunda cha pesa, akanikabidhi. Mwanzo nilisita kupokea lakini akanisisitizia kuwa nichukue. Nilimuambia hapana lakini alilazimishia sana.


“Najua unashida, mimi si mgeni kwako, nakujua na nahitaji kukusiadia. Najua unashangaa ni kwanini naendesha Bodaboda halafui nina pesa hivi. Hapa mjini, unaonekana ni kijana mwenye akili sana, nakuambia, nakuhitaji tufanye kazi, si kazi haramu, hapana kila kitu halali lakini nahitaji mtu mwenye akili wa kufanya anye maisha. Chukua tu ondoka zako, najua ukishakaa sawa utanitafuta kwasasa hiyo pes aitakusaidia kwa mambo yako madogomdogo.”


Kabla hata sijaamua nataka kuzichukua au nini, nikiwa nimezishikilai mkononi aliwahs apikipiki yake na kuondoka.


“Sasa mbona unaondoka, nitakuapta wapi?” Nilimuuliza, nikama nilishafanya maamuzi ya kuzichukua zile pesa, alicheka kwa nguvu na kuniambia.


“Usiwe na shida, utanitafuta tu mwenyewe, wewe weka mambo yako sawa tu!” Aliondoka na sikumuona tena, kilikua ni kuibudna kikubwa cha pesa, nilihisi kuchanganyikiwa, tangu kumaliza Intern nilikua sijawahi kushika pesa nyingi namna ile. Nilianza kuzihesabu zilikua milioni mbili na laki nne. Zote zimefungwa sehemu moja, basi baada ya kuzichukua nilitulia kidogo.


Nilikua na mawazo sana namna ya kuzitumia hizo pesa sikua nikimjua huyo kijana, sikua nikijua pesa ni zanini. Kwanza niliondoka kabisa eneo lile, sikutaka kubaki pale nikiamini kuwa kama ni pesa za mazingaombwe au za madili ya ajabu za mtego nisikamatwe.


Niliwaza sana kuhusu kuzitumia zile hela lakini niliogopa, kwanza nilihisi ni za mambo ya madawa, akili nyingine ikaniambia ni mambo ya kishirikina. Niliwaza sana lakini mpaka jioni njaa ilianza kuniuma, yule kijana hajanitafuta mwisho nikasema hapana, ngoja nichukue elifu kumi nitafute chakula nile kidogo. Basi nilichomoa elfu kumi nikijua hata kama atakuja na kuihitaji ni rahisi kuipata.


Nilianza kula, lakini kabla ya kumaliza kula simu yangu iliita, namba ilikua ngeni, nilihisi ni yule kijana. Lakinis ikumpa namba yangu atakua kaipata wapi? Niliwaza sana sikua na majibu. Niliipokea ile simu kusema haloo ilikua ni sauti naifahamu, alikua ni rafiki yangu wa chuo ambaye tulikua tunatoka sehemu moja, kijiji kimoja.


“Nimemuona Mama yako kadondoka sokoni, ndiyo niko njiani naelekea hospitalini, hali yake mbaya sana, vipi huna mtu anaweza kuja….”


Aliniambia, nilishtuka kusikia hivyo, nilipotaka kumuuliza shida ni nini simu ilikata. Kabla sijafanya chochote simu yangu iliita, ilikua ni namba geni kabisa. Niliipokea, sikujua ni nani, nilisikia tu sauti inaniambia.


“Naona umeamua kutumia ile pesa, nitakutafuta baadaye tuongee. Usifanye kitu chochote bila mimi kukuambia.” Simu ilikatwa.


Hata mimi sijui, natamani kujua kitaendelea nini ila sina namna, ni kusubiri tu.


ADAM; CHEZA NA MIMI LAKINI USICHEZE NA MUNGU WANGU! —SEHEMU YA SITA


“Unamaanisha nini? Namba yangu umepata wapi?”Usijali Broo, namba yako kanipa Da salma, tunajuana vizuri, ni mtu wangu, nilikua nambeba sana kipindi hicho.” Aliongea, nilimuuliza alikua amejuaje kuwa nimeitumia ile pesa akasema alijua tu. Aliniambia kuwa hataki niende kumuona Mama yangu kwani atakua sawa, ila alitaka tu kunionyesha kuwa, kama nataka kufanikiwa ni lazima niwe tayari kwa lolote.


“Unamaanisha nini?” nilimuuliza.


“Wewe ni msomi na una mwanamke mzuri, nimekua nikikufuatilia sana lakini naona kama maisha yako hayalingani na elimu yako. Mimi usinione hivi, Digrii yangu ya pili nililimaliza miaka saba iliyopita, lakini nilihangaika kutafuta kazi pamoja na usomi wangu. Mwaka jana ndiyo mambo yangu yalianza kuwa vizuri, nataka ktuonane, tutengenezea maisha.”Aliniambia, moja kwa moja ilikua ni mambo ya kishirikina, katika maisha yangu kutokana na imani yangu niliapa hata mambo yakiwa magumu namna gani siwezi kuingia huko.


“Siwezi kumtoa Mama yangu kwaajili ya ujinga wa namna hiyo, mimi msomi, kama nipopopata kazi basi nitauza hata mchicha wa kutembeza lakini si kumuua Mama yangu kwaajili ya pesa!”Nilimuambia na kukta simu, kichwani nilihisi labda ni Salma kampa namba yangu, kama walikua wanajuana basi ni lazima yeye kutokana na tamaa zake za pesa aliamua kuniuza. Nilimpigia ili kuongea naye lakini simu yake ilikua haipatikani.


Wakati nikiwaza nini chakufanya simu yangu iliita tena, alikua ni yuleyule kijana.


“Si nilishakuambia sitaki ujinga wako, kama ni pesa zako njoo uchukue, sihitaji ujinga wako tena!” Nilimuambia lakini hakuonekana kupaniki, aliongea kiupole.


“Umeshatumia hiyo hela, umemtoa sadaka mtu uliyekua unampenda sana, kwa ulivyokua unang’ang’ania nilijua kuwa utamtoa Da Salma, lakini umemtoa Mama yako mzazi. Nipo hapa Mlimani City, unaweza kuamua, kuja kuongea na mimi nikusaidie au kubaki hukohuko na kiburi chako kesho ukaenda kumzika Mama yako!”


Aliongea kwa sauti ya chini lakini yenye msisitizo, alionyesha kabisa alikua anamaanisha kile alichokua akikiongea. Alikata simu na nilipojaribu kumpigia simu iliita bila kupokelewa, nilipiga na kupiga mwisho simu ilizimwa. Bado nilikua sijajua anamaanisha nini, niliamua kumpigia simu rafiki yangu kujua hali ya Mama yangu.


“Nisikudanganye Mama anuamwa, hawezi hata kufungua macho, kibaya zaidi nikuwa, anatoa harufu kama vile ameoza na mwili unakua unakakamaa huku majimaji yakitoka machoni na mdomoni.”


Kama daktari nilijua kuwa hakikua kitu cha kawaida, hali ya Mama kubadilika namna hiyo kulikua na shida ingawa nilikua siamini sana hayo mambo lakini sikua tayari kumpoteza Mama yangu kwa kipindi hicho. Alihangaika sana na mimi na roho ilikua inaniuma sana kuona kuwa, nimemaliza kusoma, hata kazi sina akafaidi matunda ya jasho lake basi anakufa. Hapana, nilijiambia hapana, nililazimika kuchukua Bodboda mpaka Mlimani City, Abdul, kijana ambaye ndiyo aliniita ni kama alikua ananisubiria.


Ile naingia tu aliniita,nilimfuata na kabla ya kuongea kitu chochote aliniambia subiri. Alipiga simu na kuongea na mtu, sijui aliongea lugha gani lakini yalikua ni maneno kama matatu hivi ambayo mpaka leo siyakumbuki.


“Umefanya maamuzi sahihi kuja….” Alianza kuniambia.


“Sikuja kukusikiliza, ninachotaka kujua ni kuhusu Mama yangu, vuipi utanisaidiaje.” Nilimuuliza kwa sauti ya juu kdito, kusema kweli nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa. Alinituliza kwa kuniambia Mama yangu hana tatizo lolote nisubiri tu simu ya rafiki yangu.


“Nilizidi kuchanganyikiwa zaidi kwani sikua nimemuambia kuwa aliyekua kanipa habari za Mama yangu alikua ni rafiki yangu. Lakini alionekana kujua kila kitu. Lakini kabla sijafanya chochote, wakati nikitafakari huyu mtu ni nani simu yangu iliita. Alikua ni rafiki yangu nilipokea lakini haikua sauti yake, ilikua ni sauti ya Mama.


“Nimeonana na rafiki yako hapa kanipa lift….”


Mama alikua anaongea kama mtu ambaye alikua njiani na kukutana na rafiki yangu. Hakuongea kama mgonjwa, ni kama alikua hakumbuki kitu chochote kile. Nilimuomba kuongea na rafiki yangu ili aniambie kilichotokea.


“Hata mimi sijui, Mama alikua na hali mbaya ghafla naona anatoka hospitalini yuko vizuri, yaani kama hakuna kitu kilichotokea, hii ni miujiza ya hali ya juu!” Aliniambia, nilimuangalia Abdul alikua anacheka tu, alikua anajua kila kilichokua kikiendelea.


“Unataka nini, kama ni pesa zako hizi hapa! Naiche na familia yanu!” Nilimumbia kwa hasira huku nikimmwagia pesa yake mezani, nilishatafuta elifu kumi yake niliyokua nimeitumia hivyo sikua na shida kabisa na pes ayake. Lakinia licheka, hakuonekana kuwa anataka pesa kabisa.


”Sina shjida ya pesa! Kama ungekataa ungekataa kipindi kilekile nakupa. Kwasasa huna namna!”Aliniambia.


“Unamaanisha nini? Unataka nini kwangu?” Nilimuuliza kwa hasira, aliniangalia kwa dharau flani kisha akaniambia.


“Sina shida na wewe, siajwahi kuwa na shida na wewe kabisa. Biashara zangu haziendi vizuri na najua kuwa ni wewe tu ndiyo utanisaidia!”


“Kivpi, unataka nimtoe sadaka Mama yangu, mimi si mshirikina, siwezi kufanya upuuzi huo, kama ulidhani kuwa unawez akunitishia hapa. Siwezi kuua mtu kwaajili ya pesa!” Nilitaka kunyanyuka huku nikiziacha zile pesa pale, hakuzigusa, watu wlaikua wanapita, wanatuangalia namna tunabishana lakini yeye hata hakujali.


“Acha ujinga, unajua utaruidi, sina shida ya Mama yako wala ndugu yako, na wala mimi si mtu wa kuua. Ninachotaka ni hivi, nataka urudi hapa ukae ili tuongee kama wanaume. Biashara zangu haziendi vizuri na wewe ndiyo mtu pekee wa kunisaidia, naomba unisidie, nitakulipa milioni kumi kama ukifanikisha hiki nianchotaka kukuambia.” Aliniambia hukua kinionyesha sehemu ya Kukaa, ingawa kweli nilikua na hasira lakini pia nilijua kuwa sikua na namna, ilikua ni lazima kumsikiliza kwani sikua tayari kuona akiidhuru familia yangu kwa mambo ya kishirikina.


“Unataka nini?” Nilimuuliza huku nikikaa, kusema kwlei nilikua namuogopa, nilikua natetemeka kama nimemwagiwa maji ya barafu. Aliniangalia na kucheka.


“wewe mwanaume ahca kuogopa, ni kitu kidopgo tu!” Aliongea huku akipepesa pepesa macho sehemu mablimbali, ni kama alikua anaangalia mtu, ni kama alikua anasubiri mtu.


“Namtaka salma, sina shida na wewe, nimemfuatilia sana huyu dada lakini nimeshindwa kumpata. Namtaka!” ni kitu ambacho sikukitegemea, nilikua nahisi labda atongea mambo ya kujiunga na Freemason lakini si kuniambia mambo ya kumtaka mpenzi wangu.


“Unamaanisha nini wewe?” Nilimuuliza, aliniangalia kwa tabasamu, alicheka.


“Namtaka Salma, si kama unavyodhani, simtaki kimapenzi, ninachotaka ni kuwa karibu naye. nataka kufanya naye Biashara.” Aliniambia, kusema kweli alizidi kunichanganya, mwanzo aliniambia kuwa kanijua vizuri kupitia Salma, sasa hivi ananiambia kuwa anataka kuwa karibu na mimi na anachotaka ni mimi kumsaidia.


“Biashara gani? Hembu niambie?” Nilimuuliza nikitegemea majibu, lakinia liniambia wazi kuwa hakuwa tayari kuniambia kila kiti.


“Ninachotaka ni wewe kuniunganisha naye, nataka umuambie kuwa mimi ni rafiki yake, aniamini na hapo tutakua tumemalizana!” Aliniambia, nilijaribu kulazimishia sana aniambia sababu ya kumtaka lakinia ligoma. Aliniambia katika maisha kuna vitu vingine si vyakujua, alichotaka ni mimi kumtambulisha tu kwa Salma.


“Lakini si mnajuan?” Nilimuuliza.


“Ndiyo lakini tunajuana kama mtu na Bodaboda wake si mtu na rafiki yake, nataka unitambulishe kama rafiki yako. Kama mtuw ako wa karibu, kama mtu unayemuamini. Baad aya hapo nakupa pesa yako na mimi sitaki tena kuhangaika na wewe, nitakua na maisha yangu na wewe utakua na yako!” Aliniambia.


“Vipi na Salma, ni kitu gani kitamtokea?” Nilimuuliza, alicheka na kuniambia kuwa hahitaji kumtumia ila naye anahitaji kutambulishwa kwa mtu mwingine.


“Kuna mtu natakaa nitambulishe kwake, kuna mtu nataka kufanya naye Biashara, lakini nahitaji kutambulishwa naye na si mtu mwingine.” Aliniambia, yaani sikumuelewa, aliniambia sina sababu ya kumuelewa zaidi ya kumtambulisha tu kwa Salma.


“Huyo anakuja, anomba unitambulishe kama rafiki yako. Tulisoma wote sekondari lakini mimi sikuendelea nilifeli sasa hivi nafanya Biashara ya bodaboda na pia ni ni Dereva mzuri wa magari makubwa. Muambie hivyo tu ukishamaliza pesa yako nakupatia jioni la siivyo usipofanya hivyo jioni unaenda kumzika Mama yako!”


Aliongea kwa kujiamini, alikua kajipanga, sijui alimuitaja Salma lakini alikua pale. Badi nilikua na hasira na salma, alikua kanisaliti, nilikua sijaongea naye chochote tangu liletukio litokee. Lakini nilijua kuwa kuna kazi nilikua natakiwa kuifanya. Ilikua ni lazima kujifanya mjinga ili kumtambulisha kwa yule jamaa.


“Nikishamtambulisha sitaki kusikia chochote, si huyu mbuzi wala mtu mwingine. Nakua na maisha yangu, hata pesa yake sitaki!” Niwaza kwa hasira, ndni ya siku mbili maisha yangu yalikua kama yamebadilika, nilikua sijielewi elewi. Basi salama alikuja, alikua anasita kunisalimia kwani alidhani bado nina hasira, lakini nilipomchangamkia basi naye alichangamka nikajifanya hakuna kitu kilichotokea.


“Kumbe unafahamiana na huyu Kaka, ni Bodaboda wangu.” Aliniambia baada ya kukaa, sikujau kafikafikaje pale wala sikutaka kujua, nilifanya kama nilivyoambiwa.


“Kumbe mnafahamiana, huyu ni rafiki yangu, nilisoma naye sekondari, ni Dereva mzuri wa Bodaboda na pia ni dereva wa Magari makubwa.” Nilimuambia, baada tu ya kumtambulisha Abduli alinyanyuka ka kumpa mkono. Ksiaha kaaga na kuondoka bila kusema kitu kingine chochote kile. Aliniacha mimi na Salma wote tukiwa tumekaa tunashanaga ni kwanini kaondoka ghafla namna ile.


Nilibaki na Salma huku tukiangaliana, nilikua nawaza ni kitu gani kitamtokea, kusema kweli pale nilisahau mambo yote aliyokua kanifanyia na kuwaza nimemuingiza kwenye majanga gani mpenzi wangu?


“Najua nimekuumiza, ukweli sikupanga kutembea na yule Baba, nakupenda sana, tena sana lakini tamaa zilinizidi, nisamehe dear, nakupenda na siwezi kuishi bila wewe!” alianza kujitetea, kichwa changu kilikua mbali sana, nilitamani kumtukana na kumkasirikia lakini nilikua naogopa sana nikidhani kama kuna kitu kibaya kitamtokea basi mimi ndiyo nitahusika.


“Unamfahamuje Abdul”Nilimuulzia kwanza alishangaa ni kwanini nilikua namuulizia kuhusiana na dereva bodaboda wakati nilikua nimemfumkania na mume wa mtu.


“Unamaanisha nini? Kwani yeye kakuambia nini? Mimi ni dereva boaboda tu wangu tena alinibeba kama mara mbili tu. Juzi ndiyo nilikutana naye kwangu pale nnje anapakigi, absi simu yangu iliibiwa yeye ndiyo alinisaidia kuipata, zaidi ya hapo hata simjui kwa chochote. Kwani kakuambia nini?”


Yeye alikau anajitetea, ni kama alidhani kuwa ninamhisi kuwa anchepuka lakini haikua hivyo.


“Kwahiyo humjui, huma mazoea naye na wala hakuna Biashara ambayo mshawahi kuifanya?” Nilimuuliza akanaimbia hapana.


“Basi kuwa makini sana naye, ni tapeli, nilisoma naye lakini ni tapeli, kuwa naye makini hata simu zake usipokee!” nilimuambia ingawa nilikua naogopa nini kitatokea lakini nilikua nampenda sana Salma, sikua tayari kuona kitu chochote kibaya kinamtokea.


Nilimtahadharisha huku nikisema liwalo na liwe, sijui alikuja pale kufanya nini lakini alitaka kuondoka. Nilimuomba sana kuondoka naye lakini hakutaka, sikau na nia ya kumrudia bali nilitaka tu kuondoka naye kwaajili ya usalama wake. Aliniambia kuna mtu alienda kuonana naye, basi sikua na namna zaidi ya kuondoka zangu. Lakini wakati natoka kuna Kaka alikuja na kusalimiana kama wapenzi, walikumbatiana na kupigana mabusu kabisa.


Nilijisikia vibaya nkwani nilikua kama hatua kumi tu pembeni yake, Salma alikua ananiona na hakujali kama namuona. Tofauti na yule wa kwanza, ingawa huyu naye alivaa pete ya ndoa kidoleani lakini alikau ni kijana tu kama mimi. Niliumia sana, nilitamani kwenda kumpiga makofi lakini niliogopa, ilikua ni sehemu ya wazo na ningeonekana kituko, niliogopa labda nikifanya kitu cha kijinga ndiyo nitakua nimempoteza.


Niliondoka nikiwa na mawazo sana, nilikua na hasira zilizochanganyika na huruma. Nilikua na pesa lakini sikuweza kuzifanyia kitu chochote, niliishia tu kuzunguka mpaka jioni bila kuwa na uelekeo. Usiku niliendelea kuzunguka kama chizi nikajikuta nipo nyumbani kwa Salma. Mlango ulikua umefungwa, nikaa nnje mpaka kwenye saa nane usiku. Gari yake ilikuja na kusimama kwa nnje, kuna mwanaume alimshusha, akamsimamia mpaka akafungua Geti ndipo akaondoka.


Alikua ni mwanaume mwingine kabisa, tofauti na yile wa mchana, walionekana kama wapenzi kwani waliagana kimapenzi kabisa. Salma hakulewa ile yule mwanaume alionekana kulewa, aliondoka na gari yake Salma aliingia ndani ila kabla ya kufunga Geti nililisukuma na kuingia.


“Unafanya nini wewe mbona unanifuatilia namna hiyo?” Aliniuliza kwa hasira, huku akitembea kuingia ndani, hakunga tena geti na wala hakujali kama niko pale.


“Una wanaume wangapi?” Nilimuuliza.


“Hivi una akili kweli, inamaana unataka nisiwe hata na marafiki, aisee una wivu wa kijinga jinga sana!”  Nilijikuta napatwa na hasira sana, nikamshika na kutaka kumpiga.


Mambo yanazidi kuchanganya, hatujui Abdul anataka nini kwa Salma? Kwanini amempa hiyo hela kwaajili ya kutambulishwa tu, kuna nini?


ADAM; CHEZA NA MIMI LAKINI USICHEZE NA MUNGU WANGU! —SEHEMU YA SABA


Salma alinisukuma na kuingia ndani. Dakika mbili mbele alinitumia meseji “Siwezi kuendelea kuwa na mwanaume kama wewe, pesa huna lakini una wivu wa bilionea, nikutunze na maisha unipangie! Ondoka kwangi na sikuhitaji tena!” nilijaribu kugonga mlango lakini haukufunguliwa, alizima mpaka taa za nnje, nilikaa pale nnje mpaka aubuhi lakini sikumuona akitoka, ni kama alijua kuwa nilikua namsubiria kwani mpaka saas ita mchana alikua bado hajatoka.


Niliumia sana kuchana na Salma, ingawa nilishaona dalili kuwa tunaachana muda mrefu lakini nilikua nikijiaminisha kuwa, kama Mungu akinijaalia nikapata kazi basi ingekua rahisi mimi kulirudisha penzi langu.


“Natakiwa kutafuta pesa kwa namna yoyote ile, mwanamke kama huyu siwezi kummiliki!”Niliongea mwenyewe huku nikiondoka, sikujua naenda wapi lakini nikiwa njiani nilikumbuka ile hela aliyonipa jamaa, nilikua bado sijaitumia.


“Poteli ya mbali, hata kama pesa ni za majini lakini nahitaji kuzitumia. Nitafute chumba cha kukaa kwanza sitakazobaki ndiyo nitafungua Biashara.” Niliwaza wakati nikichukua bodaboda kunizungusha kutafuta dalali wa chumba.


Nilipanga kukamilisha kila kitu siku hiyo hiyo, kweli nilipata chumba, nikalipia miezi sita kisha nikanunua godoro, nikatandika chini, nikanunua jiko dogo la gesi, nikanunua na vikorokoro vingine vya ndani kwani nilitaka kupika ili kupunguza gharama. Katika vitu vyote hivyo hivyo sikiutumia hata laki tano, nilitoka kidogo kupata kinywaji jioni, sikujua nilinunua bia ngapi lakini mpaka naamka aasubuhi nilikua sina hata shilingi kumi.


“Kuna nini kimetokea! Inamaana nimetumia hela zote, yaani milioni mbili imekata?” Niliwaza bila majibu, jana yake nilikua tajiri lakini ghafal naamka sina kitu. Niliwaza sana nilvyotumia pesa yangu lakini sikujua. Sikua na kitu zaidi ya chumba na vitu vidogo vya ndani. Nilihisi kcuhanganyikiwa, kama maisha ndiyo haya mbona nitakufa masikini. Nikiwa nawaza nini cha kufanya nilikumbuka milioni kumi zangu ambazo aliniahidi Abdul.


Sikua na uhakika kama atnipa lakini niliona ni vyema kama nikiongea naye. Isitoshe, sikua na kitu cha kupoteza. Kwa wakati huo nilikua siwazi kabisa mambo ya kishirikina.


“Hata kama ni uchawi ni wake, mimi ninachotaka ni pesa zake tu, sijali kazipataje!” niliwaza huku nikichukua simu yangu na kumpigia Abdul. Nilimuambia kuhusu pesa yangu, niliongea kishari nikidhani labda atakataa.


“Nilikua na kusubiria tu wewe, nikajua umeususa…” aliniambia, nilimuambia hapana, mimi siwezi kususa pesa. Nikamuuliza tukutane wapi akanimbia Mlimani City. Zilikua ni pesa nyingi, nilikua na akaunti Benki lakini kuwekewa pesa nyingi kwa pamoja wakati sina kazi niliona kama itakuja kunieltea shida.


“Kwanini tusikutane sehemu nyingine?” Nilimuuliza, lengo langu lilikua ni kukutanan sehemu ya wazo, nikiwa kwenye bobdaboda, ananikabidhi pesa yanu kisha naondoka. Hakua na shid,a tulipanga sehemu ya kuonana, nilimfika na kumkuta, alikua kashikilia kabego kadogo ka mgongoni. Alinikabidhi na kiuniambia niangalie kuhakikisha kama ziko sawa, lakini sikutaka kufanya hivyo, nilivyoona vibunda kumi vya noti za elfu kumikumi nilijua tu kuwa zimetimia milioni kumi.


Alinipa nakushikilia lile begi, nilichukua nakumuambia dereva wa bodaboda tuondoke.


“Una uhakika unazihitaji hizo pesa?” Aliniuliza, sikutaka hat akumjibu, nilikua nashida kila sehemu sikutaka kupoteza muda. Nilizichukua na kuondoka zangu mpaka nyumbani, kule sikukuamini kabisa, nilizitenga mafungu matano, nikaenda Banki, nilikua na akauntyi mbili Benki, nikaweka milioni mbilimbili kila moja. Niakenda na kufungua akaunti nyingine katika Benki mbili nyingine siku ileile nako nikaweka milioni mbilimbili. Mkononi nilibaki na milioni mbili ambazo niliamua kuzitumia kuanzisha Biashara wakati nikisikilizia upepo.


****


Nilianzisha Biashara ya Vitunguu, nilikua nikichukua mikoani na kuzungusha kwenye masako hapa Dar. Zile pesa nilizitumia vizuri, miezi sita tu Biashara yangu ilikua imesimama, nimenunua kiwanja na nilikua nishanunua Kirikuu nyangu amabyo nilikua nikiitumia pia kama gari ya kutembelea huku nikisambazia mzigo. Kwakifupi mambo yalianza kwenda vizuri niliona kama miujiza imetokea, nilisahau kabisa machungu ya kuachwa na mwanamke niliyekua nikimpenda.


Nilikua napesa na nilikua na uwezo wa kuchukua mwanamke mwingine yoyote yule niliyekua nikimtaka. Nilisahau kuhusu Salma, sikua nikimkumbuka tena na kusema kweli tangu kuahcana na Abdul siku ile nilikua sijawahi kuonana naye tena. Hivyo hivyo kwa salma, nilikua bize sana na maisha, sikumkumbuka na wala sikutaka kujua ni sababu gani Abdul alikua tayari kutoa milioni kumi ili tu mimi nimuunganishe kwa Salma.


Lakini siku moja nikiwa Mlimani City, sikua na kawaida ya kwenda huko ial siku hiyo nilijisikia tu kwenda, wakati natoka nikakutana na Salma yeye anaingia, alikua peke yake, aliponiona aliniangalia kama anaona aibu flani, ni kama alitaka kunikimbia nisimuone lakini kwa bahati macho yetu yaligongana. Sikufanya ajizi, nilimfuata na kumsalimia, aliitikia ikwa aibu hukua akiangalia chini.


“Vipi, muda mrefu hatujaonana? Naona umeingia kwenye ndoa tayari….” Nilimuuliza huku nikiangalia kidole chake cha pete. Alikua kavaa Pete ya ndoa, alikishika kidole chake cha pete na kuizungusha pete yake kwa aibu.


“Nikweli nimeamua kuoelwa….” Aliongea kama anababaika babaika, hakuonyesha furaha, niliona wakati anangalia pete yake alionekana kama ana maumivu, akma anajutia kitu flani.


“Mbona hivyo, inamaan huna furaha, unaongea kama untaka kulia?” Sikumkawisha nilimuuliza moja kwa moja kutaka kujua kwanini alikua vile.


“Hapana, hamana shida, niko vizuri… Naomba kuondoka, nafurahi kuonana na wewe, mume wangu anakuja na ana wivu sana!” Aliniambia huku akiondoka, nilicheka na kuondoka zangu, lakini wkaati natoka nnje nilikutana na Abdul, alikua amesimama anaongea an simu. Nilitaka kumpita kwani sikutaka kuonana naye lakini aliniona, aliniangalia na kunifuata kutaka kusalimiana na mimi.


“Nitakucheki baadaye, nimekutana na rafiki yangu hapa!” Alimuambia mtu aliyekua akiongea naye kwenye simu kisha akakata simu. Alikuja na kunisalimia vizuri tu, tuliongea machache lakini wakati naondoka aliniambia.


“Vipi, umekutana na mke wangu?” Aliniuliza, nililazimika kusimama na kumuangalia, kuna kitu kilipiga kwneye moyo wangu kama ganzi flani, nilikua kama nimepugwa na shoti ya umeme.


“Mke wako?” nilimuuliza.


“Mimi simfahamu, hujawahi kunitambulisha….” Ingawa nilishaanza kuhisi mtu aliyekua akimzungumzia lakini sikutaka kuonyesha kuwa nimehisi. Nilijifanya simjui hivyo kusubiri anitambulishe.


“Salma, naamini mlikutana, unajua nakushukuru sana ikwa wewe kunitambulisha kwake, la sivyo ingekua vigumu sana mimi kumuoa….” Nilihisi nitapata wivu, nilihisi nitachanganyikiwa kusikia Salama ameoa, nilihisi nitajisikia vibaya lakini kwa wakati ule kila kitu kilikua tofauti kabisa. Sikujisikia vibaya, nilijikuta nampongeza nakumuambia kuwa ilikua ni mipango ya Mungu.


“Dini ilitutenganisha, naamini mna furaha.” Nilimuambia huku nikimuaga, inawezekana ni kitu ambacho hakukitarajia, nadhani alidhani mimi nitapaniki na kutukana au kufanya vitu vibaya.


“Unamaanisha nini?” Aliniuliza wakati naondoka, alinishika mkono kwa nguvu na kunivuta kwa nguvu.


“Mbona unaongea kwa dharau namna hiyo dogo wakati mimi ndiyo njimekupa maisha, umepata pesa unaanza kunidharau, au hujui naweza kuzichukua dakika yoyote ile?” aliuliza kwa hasira, nilimuangalia kwa mshangao kwani sikuona kama nimeongea kitu kibaya kiasi cha kumkasirisha.


Yeye aliniambia kuhusu kumuoa X wangu, mwanamke niliyekua nikimpenda kuliko kitu chochote kile, mimi ndiyo nilipaswa kuumia, mimi ndiyo nilipaswa kulia, nilipaswa kukasirika lakini nilimuona kama yeye anaumia zaidi.


“Unamaanisha nini? Mbona mimi sina shida ndugu yangu, umemuoa X wangu nimekubali. Sina shdia naye tena, nina maisha yangu, wanawake wapo wengi kibao, sasa nakushangaa unapaniki nini?”Nilimuuliza huku nikimsukuma kwa nguvu kwania likua ameushikilia mkono wangu mmoja wakulia kwa mikono yake miwili.


“Una dharau sana, yaani uneonekana kama vile umeniachia huyu mwanamke, huna hasira naye!” Aliniambia, nilizidi kumshaa nikamsukuma kama katakataka flani na kuondoka zangu. Huku nyuma alikua akitukana, akinitishai mambo kibao lakini sikujali, nilikau simuogopi, ingawa huko nyuma alionyesha mambo mengi ya kishirikina lakini sikujali, niliondoka zangu huku nikiwa nimekasirika sana.


Siku yangu haikua nzuri, nilienda moja kwa moja Bar na kuanza kunywa, nilikunywa sana, usiku kwenye saa mbili hivi simu yangu iliita. Ilikua ni namba mpya, kwakua ni mfanyabiashara suala la kupigiwa na namba mpya lilikua ni jambo la kawaida sana.


“Umemfanya nini mume wangu? Mbona hali yake imekua hivi, yaani baada tu ya kuonana na wewe kila kitu kimebadilika?” Ilikua ni sauri ya Salma, alikua akiongea huku akilia, alikua akilia sana kama mtua liyetoka kupigwa.


“Kwani kuna nini kimetokea, vipi yule mshenzi kakupiga? Hembu ondoka hapo, nenda Polisi nakuja, kama kuna kitu kakuambia basi jua kuwa ni uongo!”


Nilimuambia huku nikinyanyuka kutaka kumfuata alipo, kichwani nilijua lazima Abdul kakasirika na kumpiga mke wake lakini haikua hivyo.


“Mume wanyu hajanipiga, lakini tangu kukutana na wewe hayuko sawa, tumetoka Mlimani hawezi hata kutembea vizuri, amevimba mwili mzima na hataki kwenda hospitalini, kila dakika anakutaja wewe tu. Niambie umamfanya nini mume wangu?”


Kusikia hivyo nilikata simu, nilihisi kama wanataka kuniharibia siku yangu. Salma aliendelea kupiga simu lakini mimisikupokea, nilichoka nikazima simu yangu ila ausbuhi niliopoamka na nilikuta meseji nyingi sana. Salama alikua anaomba kukutana na mimi, alikua anahitaji kuongea na mimi. Nilizisoma sana alikua akilalamika sana na kuniomba msamaha kwa makosa ambayoalikua kanikosea huko nyuma.


Sikua naogopa kitu chochote, nilimuambia kama ni kuonana na mimi basi tuonane ila mimi sina kitu cha kuongea naye kwani nilikua nishamalizana naye. Tulipanga na kukutana sehemu karibu na kwangu nilipokua nikiishi. Alikuja yeye, sikua na hisia zozote na Salma hivyo hata nilipomuona sikushtuka. Alianza kw3a kuniomba msamaha, kunaicha na kuoanana na Abdul.


“Uliondoka, nilijua nimekukosea sana huwezi kunisamehe, Abdul alinisiadia sana kwani kazi nilifukuzwa, baada ya kuahcana na Bosi wangu, alinifanyia figisu mpaka nikafukuzwa kazi, ndiyo nikakutana na Abdul basi akaniingiza katika Biashara zake na mpaka sas aniko naye, nampenda sana na sikuja hapa ili kurudiana na wewe….” Aliniambia kana kwamba mimi nilikua namhitaji, ukweli nikuwa, nilikua simhitaji kwa lolote lakini niliendelea kumsikiliza.


Aliongea mambo mengi kila dakika alimsifia mume wake mpaka ikaanza kuniboa, ni kama alitaka kunikasirisha lakini sikukereka niliboreka.


“Wakati nakukutanisha naye aliniambia kuwa anakuhitaji ili umtambulishe kwa mtu, alikua anataka umtambulishe kwa mtu gani?” NIlimuuliza makusudi ili kumkera, nilimuona kanyamaza kidogo, nilihisi labda alikua hajui kama mimi ndiyo nilimtambulisha kwake.


“Hakua akitaka kutambulishwa, alikua ananipenda muda mrefu, ameniambia kila kitu aliniambia alikupa milioni kumi ili tu umtambulishe kwangu. Mume wangu tunapendana, ananiambia kila kitu chake.” Aliniambia, niliona kama ananipotezea muda.


“Una shida gani? Sidhani kama umekuja hadi huku kuja kuniambia kuwa mume wako anakupenda, hukua na haja ya kuniambia hayo.” Nilimuambia, aliniangalia kwa wasiwasi kisha akaniambia.


“Nataka kurudiana na wewe, yule mwanaume mimi nimemchoka, simhitajin tena!” Sekunde mbili lakini alikua kabadilika kabisa, yaani hakua mtu yule niliyekua nikiongea naye hapo nyuma, alikua na tabasamu, akifurahia kama vile hakuna kitu kilichotokea.


“Unamaanisha nini?” Nilimuuliza kwa mshangao.


“Namaanisha kuwa, nakutaka, nataka kurudiana na wewe, nakupenda na wewe unajua, tumetoka mbali ila kama unavyojua, tamaa na pesa ndiyo vimeniponza!”


Aliniambia nilizidi kushangaa kwani aliongea kana kwamba ni kiotu ambacho alishakipanga muda mrefu.


“Unajua sikuelewi, wewe si una mume wewe?” Nilimuuliza. Alianza kwa kucheka kisha akaniambia.


“Mumer gani yule, yule mpuuzi alikuja kwangu kwakua aliambiwa na mganga wake sijui kuwa mimi nitampa utajiri, amenihangaikia muda mrefu yaani tangu muda kikmtu kinahangaika na mimi ila nimekuja kumpata hana hata maajabu. Mimi nakutaka wewe kwani una mwanamke?” aliniuliza.


“Sina mwanamke, lakini….”Nilijihisi kuchanganyikiwa flani, si kama alikua anaomba bali alikua kama analazimishia, ni kama alikua na uhakika kuwa atanipata.


“Basi kama huna mwanamke leo naenda kudai talaka yangu. Nimesubiri sana apate hizo pesa kwa mganga wake hakuna kitu. Vimganga vyenyewe anavyoenda ni vya kimasikini, aisee simtaki, mwanaume hana mvuto, hajui chochote. Angalau wewe unajielewa, mambo yako yanaenda vizuiri una akili sana.” Alinaimbia, nilijaribu kumuambia kuwa mimi siko tayari kuingia kwenye mahusiano lakini hakua tayari kwa hilo.


“Unadhani atakubali kukupa talaka, hata nikisema narudiana nawewe?” Nilimuuliza.


“Hilo niachie mimi, Jana ndiyo ilikua mwisho wake. Nilipokuona tu nilijua kuwa nahitaji mwanaume mwingine, shida yake nikuwa anapata pesa lakini mganga akimuambia kitu flani basi anafanya hivyo. Yaani nyumba yetu imejaa waganga, kila sikua anabdilisha, mara leo huyo mara kesho yule. Anataka kutembelea nyota yangu kufanikiwa lakini hakuna kitu.” Aliongea kwa ujasiri kiasi kwamba mimi niliogopa.


“Inamaana huogopi kuwa atakuloga kama ukimuacha?” Nilimuuliza, aliishia kucheka tu.


“Nilikua namuogopa, lakini jana alirudi nyumbani na kuniambia kuwa kaonanana na wewe. Alikua kabadilika, anatetemeka, anatoa harufu, mimi nikahisi kuwa kuna kitu kibaya umemfanyia. Basi akaniambia nimpigie simu mganga wake kwani yeye hafanyi kitu chochote bila kuongea na mganga wake. Mganga wake alipokuja na kumpa dawa akakaa sawa, wakati namsindikiza yule Baba alinitongoza.


Nilishtuka ndipo akaniambia kuwa mume wangu ashaisha alinioa ili kunitoa sadaka lakini imeshindikana hana jipya tena!” Aliniambia huku akitabasmau, nilimuangalia kwa uoga kidogo.


“Inamaana huogopi? Kama alikua anataka kukutoa sadaka ukimuacha si ndiyo atakuua!”


“Hawezi kuniua, nilishajua muda mrefu kuwa amenioa kwasababu ya kishirikina, nilikua namjua tangu huko nyuma, alihangaika sana kuwatumia marafiki zangu ili kuwa karibu na mimi. Alichotaka ni mimi kubeba mimba yake ilia toe sadaka kizazi changu. Hata siku ananioa nilikua najua malengo yake!”


“Ulijuaje? Kama ulijua kwanini ulikubali kuolewa naye?” Nilimuuliza, siku zote nilikua najihisi labda nilikua nimemharibia maisha yake lakini yeye hakuonyesha kama anajali.


“Nilimkubali kwakua nilijua kuwa ana pesa, ananipa pesa sana! Nimejenga nyumba zangu mbili na nina gari, ndoa haina hata mwaka lakimi mimba sijabeba na sadaka hanitoi.” Alizidi kunichanganya.


“Mimi ni mtu wa watu, tangu zamani wakati ananipa lift za bodaboda na kunipa vihela rafiki zake waliniambia kuwa huyu mtu anataka nini. Wakati nina watu wangu hata sikujali kuhusu yeye, lakini mambo yalivyokua magumu nilikubali kuingia kwenye ndoa naye lakini nilihakikisha kuwa hanigusi hivyo nilijua kabisa siwezi kupata mimba yake, kuniacha hawezi na pesa ndiyo itaisha.


Si ulishaona wale watu watoto wao wanakua mataahira, wangine wanaua, basi yeye alitaka nibebe mimba lakini nisizae ila nilimshtukia. Nimechoka sasa hivi nakuhitaji wewe nataka turudiane akinipa talaka!”


Unadhani Adam atakubali kurudiana na X wake, vipi mume wa Salma atakubali kumuacha kweli? Usikose….


ADAM; CHEZA NA MIMI LAKINI USICHEZE NA MUNGU WANGU! —SEHEMU YA NANE


Namna alivyokua anaongea ni kama alikua mtu mpya kabisa. Salma hakua mwanamke niliyekua nikimjua tangu awali, alionekana anayajua maisha, alionekana kama mtu anayetaka mafanikio kwa nguvu. Nilimsikiliza lakini nilishafanikiwa, nilikua na pesa zangu hivyo nilikua na kiburi.


“Unafikiri ile pesa aliyokupa ilikua pesa?” Aliniuliza, nilibaki kimya, namuangalia, namtolea macho nikitaka aendelee kuongea.


“Hivi unafikiri mafanikio yako yanatokana na nini? Unafikiri kuna mtu unaweza kukutana naye leo tu halafu akupe pesa kiasi hicho! baba kuwa na akili, mimi ndiyo nilikua nakulinda!”


Aliniambia huku akinisogelea na kutaka kunikumbatia, nilijisogeza pembeni kidogo kama namkwepa klakini alicheka, hakutaka kunikumbatia bali kuna kitu alikua ananionyesha. Alinisogelea na kushusha blauzi yak echini ili nione kifua chake. Nilihisi kama vile anataka kunilainisha kwa kunionyesha mwili wake.


“Siwezi kurudiana na wewe, sikutaki kabisa!” nilimuambia, alicheka kwa dharau kisha akasogeza kcihwa changu kifuani mwake ili tu niione tattoo yake. 


“Nikikutaka dakika yoyote ile nakupata, sikuonyeshi ili kukuchanganya, nakuonyesha ili ujue maisha yakoje. Unaona hiki hapa, hii si tatuu, hizi ni chale!” Aliniambia.


“Chale?” Nilimuuliza kwa mshangao huku nikinyanyua mkono wangu na kuzishiak, kifuani kwake kulikua na Tattoo ambayo alichora jina la Marehemu Baba yake, lakini kwa kuishika kulikua na chale nyingi nyingi, alikua kachanjwa sana.


“Ndiyo Baba, ndiyo maisha ya mjini siku hizi, hivi unafikiri watu waliofanikiwa mjini wamefanikiwa kwasbabau ya Mungu?” Aliniuliza, nilimuambia kabisa mimi siamini hayo mambo na kama nikufanikiwa nitafanikiwa Mungu akitaka.


“Mbona mimi nimefanikiwa, nina maisha mazuri lakini sijawahi kwenda kwa mganga na wala simjui mganga!” Alicheka sana baada ya mimi kusema vile, alicheka kiasi kwamba sas aikawa inaboa.


“Unamaanisha nini? Mbona unacheka hivyo tena kwa dharau?” nilimuuliza.


“Wewe ni kama wale wa Mama wa nyumbani ambao wameolewa na wanajeshi! Wanachojua wao ni kuomba pesa tu ya matumizi, wakinyimwa wanalalamika. Wanaume zao wakipata pesa na kujenga basi wao huishi kupoga picha na kufuarahia mafanikio, lakini hata siku moja hawajawahi kwenda vitani, hawajui bunduki inashikwa vioipi, hawajui kuna kupigwa risasdi, hawajui kuna kutandikwa makofi wala hawajui kwata ni nini? Unajiona umafanikiwa lakini hujui hayo mafanikio yako yametoka wapi?” Aliniambia huku akijisogeza pembeni.


“Ngoja Biashara zako ziyumbe ndiyo utakuja kwangu kuhangaika na mimi!” Aliongea na kunyanyuka, aliondoka bila kugauka nyuma, hata nilipomuita kutaka kujua alikua anamaanisha nini hakujali, aliondoka kwa kujiamini ni kama alijua kuwa ni lazima nitamtafuta.


Sikutaka kuhangaika naye mpaka baada ya kama wiki hivi, nilipoigiwa simu na mtu ambaye simfahamu na kuambiwa kuwa kuna maiti imeokotwa mteroni na namba yangu imeonekana.


Nilipouliza vizuri alikua ni Polisi na nilipoenda nikakuta ilikua ni maiti ya Abdul. Alikua kaokotwa mtaroni na kwa stori za watu nikuwa alikua amekunywa pombe, kalewa sana, usiku wake watu wlaimuona alivyokua anakunywa ambapo alidondoka mtaroni. Hapo pembeni na serhemu ambayo alikua kadondoka kulikutwa kuna matapishi, alitapika sana mpaka damu, na katika hayo matapishi kulikua na hirizi kubwa. Alikua katapika mpaka hirizi ndipo akafariki dunia.


Kusema kweli niliogopa, nilikua simfahamu sana huyo kijana lakini kukutana kwangu naye ndiko kulibaidilisha maisha yakel. Nilikua sijui kwao ni wapi, nilikua sijui kitu chochote kuhusu yeye na nilikua sijui ni kwanini bado namba yangu ilikua ipo kwenye simi yake na kanisave Kaka. Kiubinadamu niliamua kuhangaika, nikamtafuta Salma ambaye alinisaidia mpaka kwa ndugu zake. Alikua ni mke wake karibu mwaka mzima lakinia likua hajapelekwa ukweni, hajulikani kwa ndugu wala marafiki, yaani ilikua ni ndoa ya kimya kimya tu.


Tulifanikiwa kuwapata ndugu zake, ambao walimchukua na kuondoka naye. Sikutaka kuhangaika naye tena wala Salma naye hakutaka kuhangaika naye. Nilimuuliza nini kimetokea mpaka kufikia kunywa pombe kiasi kile.


“Mawazo, mambo yake yalikua hayaendi vizuri, alikua ananizunguka namimi nikamuonyesha kuwa sizungukwi!” Aliniambia tu hivyo, nilianza kumuogopa Salma, alikua anaongea kana kwamba n I yeye alihusika kumfanyia hivyo. Sikutaka kujua mengi, niliondoka na kurudi zangu kwangu.


****


Sikua nikiamini mambo ya kishirikina, lakini kwa niliyoyaona sikutaka kuwa karibu tena na Salma. Baada ya tukio la Abdul nilijua kuwa Salma si mtu mzuri, aliendelea kunitafuta lakini nilikua namkatia simu pamoja na kumblock kila mara. Alikaa kimya kwazaidi ya mwezi mmoja, nikajua kuwa kila kitu kimetulia, nikajua kuwa sasa ninaweza kuwa na amani. Lakini siku moja nikiwa kwenye baishara zangu, mambo yanaenda vizuri nilipigiwa simu na Mama yake na Salma. Bado nilikua na namba yake ya simu, ingawa nilikua siwasiliani naye lakini nilipokea na kumsalimia vizuri.


Aliitikia kwa huzuni, nilimuuliza hali akaniambia yuko vizuri, ni kama alikua anasita kuniambia kitu lakini name sikutaka kumuuliza.


“Njoo tu umuone, hali yake ni mbaya, alikua anakupenda.”Mama yake aliniambia, kuna kitu kilinipiga rohoni kama kisu hivi.


“Nimuone nani? Nani anahali mbaya?” Nilimuuliza, nilikua najua anamzungumzia nani lakini sikutaka kuonekana kama vile ninajua.


“Mchumba wako, anakupenda sana lakini hali yake ni mbaya!” Aliniambia tena, nilibaki kimya bila kutoa majibu, aliendelea kuongea lakini nilikua kama nimeshikwa na butwaa, nilisikia kama mtu anapiga piga kelele, sikumsikia vizuri, mara nikajikuta nakata simu.


Kusema kweli sikupanga kukata simu, lakini kuna kitu kilikua kama kinanilazimisha kufanya hivyo. Akili yangu haikua sawa kabisa, b aada tu ya kukata simu iliita tena. Alikua ni Mama Salma, niliipokea ila safari hii nilikua mimi ndiyo nina hamu ya kutaika kujua. Nilimuuliza kilichokua kimetokea ndipo aliniambia kuwa Salma anaumwa na hali yake ni mbaya.


Alikua anaishi na mwanaume, wakaw awanagombana kila siku huyo mwanaume akampiga akalazwa hospitalini kwa siku mbili. Alipona lakini baada ya kutoka hospitalini akawa kama mtu aliyechanganyikiwa, hataki kula, hataki kuoga wala kuvaa nguo. Hapo ndipo Mama yake alimchukua na kuanza kuishi naye kwania likua akiishi kwake kwenye nyumba yake.


“Hivi mwanangu anafanya kazi gani?” Aliniuliza wakati tunaongea, nilibaki kimya sina jibu kwani nilikua sui chochote kuhusu yeye, nilikua sijui kama bado anafanya kazi, sijui kama anahongwa na mwanaume au la?


“Sijui kwakweli, anaishi maisha mazuri lakini sijui kama anafanya kazi, hata kudanga hadangi kwani alikua akiishi na mwanaume hata pesa hana, niambie, mwanangu anafanya kazi gani?” Aliniuliza tena, lakini bado sikua na majibu.


“Anakutaja wewe kila saa, anakutaja kuwa wewe ndiyo wakumsaidia, naimbie, mwanangu anafanya kazi gani na kwanini anakutaja wewe tu!” Nilikua sina majibu kwakweli, Mama yake aliniomba sana ili niende kumuona. Basi sikua na namna, ingawa nilijua mambo yake ni ya kishirikina lakini nilikubali, nilienda kumuona. Kweli hali yake ilikua mbaya sana, alikua akama kachanganyikiwa, lakini baada ya kuniona akili yake ilikua kama imerudi.


Alinikimbilia na kunikumbatia, alikua kama anapata nafuu lakini tulipoingia ndani na kukaa hali yake ilizidi kuwa mbaya. Alikua anaongea vitu ambavyo havieleweki, mwisho aliomba tuingie chumbani kwake ili tuongee. Sijui ni kitu gani kilinifanya nikubali lakini niliingia chumbani kwake na sikujua kilichoendelea ila nilishtuka tu tupo kitandani tunafanya mapenzi.


Wakati nashtuka naye alijifanya kushtuka, alinisukumiza pembeni na kutaka kupiga magoti kama vile nilikua nambaka. Nilimrukia na kumziba mdomo huku nikimuomba asingoee chochote kwani angeniaibisha, kweli alinyamaza, nilivaa nguo na kuondoka.


Baada ya wiki mbili Salma alinipigia simu, alikua kachangamka, anaongea kama vile hana tatizo, alikua anaongea kwa furaha na kunishukuru sana.


“Nashukuru nina mimba yako, sasa mambo yangu yataanza kwenda vizuri…”Nilishangaa na kumuuliza imetokeaje lakini hakutaka majibu yangu. alikata simu na baadaye nilipomtafuta hakutaka kuongea na mimi, aliishia kunishukuru kwa mimba ila aliniambia kuwa hataki tujuane.


Sijui ni kitu gani kilitokea lakin I baaada ya siku ile nilianza kuhangaika na Salma, nilitaka kuonana naye, nilitaka kuwa karibu naye lakini hakutaka kabisa. Mambo ayangu yalianza kubadilika, kila sikua kili yangu ilikua inamuwaza yeye tu, sikuona tena tahmani ya maisha, ile hamu ya kutaka kumuoa ambayo nilikau nayo kabla ya kupata mali ilirudi. Yeye hakutaka chochote kuhusu mimi, alihama nyumbani kwao na kuishi katika nyumba moja kubwa.


Ghafla alianza kuuza nguo, alifungua duka kubwa la nguo Kariakoo, kila kitu kilienda bizuri, maisha yake yaliabdilika. Kwangu kila kitu kiliharibika, Biashara zilisimama, madeni yalikua mengi, ilifikia hatua nakosa hata pesa ya kula. Nikawa kila nikikwama basi naenda dukani wkake, ananipa alfu kumi naenda kula, nikimuambia turudiane anakataa na kuniambia kuwa yeye ana maisha yake na mimi si mtu wa hadhi yake tena.


Maneno yake yalikua yananiumiza sana, nilijikuta nakonda, nalia kila siku lakini hakujali. Alikua akinisaidia ila pewsa ya kula karibu kila siku lakini hakutaka nimguse wala kutaka kushirikiana na mimi kwenye tendo la ndoa. Mwaka mzima nilikua nahangaika, siku moja nimeenda dukani kwake sikumkuta, niliulizia kama chizi kutaka kujua yuko wapi ndipo niliambiwa kuwa ameenda kwenye harusi.


Mwanzo nilihisi ni harusi ya kawaida lakini baadaye nikaja kuambiwa kuwa alikua ameenda kuolewa. Nilihisi kama utani, nikajua ladba ni harusi kama ya mwanzo ambapo aliolewa na mwanaume kwasababu ya kutafuta mali au kumtumia kwenye mambo yake, lakini nilipotajiwa mtu aliyemuoa ndipo nilijua kuwa sina changu.


Alikua ni mtu mkubwa serikalini, mtu mwenye pesa zake, nilishindwa htaa kumtafuta kwenye simu na huo ndiyo ukawa mwisho wangu nayeye. Nilienda mara moja moja pale dukani kwake lakini sikuwahi kumuona, hakurudi tena, kwa nafasi aliyokua nayo hata yale maduka aliwaachia ndugu zake. Alibadilisha namba hata katika mitandao ya kijamii sikumuona tena. Nilikubaliana na ukweli na maisha yaliendelea.


****


Kuachwa na Salma kulinifanya kuwa na hasira sana, nilimkasirikia Mungu, nilijua kuwa kila kitu alichokua nacho Salma kilitokana na nguvu za Giza, nilimsshangaa sana Mungu kuwa pamoja na kumuabudu lakini alikua hawezi kunisaidia kitu chochote. Nilimuona Mungu mjinga na kumuona kama hana nguvu. Sikua na pesa, sikua na kitu, nilikua na elimu yangu lakini bado nilikua na hangaika mtaani.


“Kama Mungu ameshindwa kunipa hata kazi kuna haja gani ya kumaubudu, si ni bora kuhangaika na shetani!” Niliwaza, ingawa kuna wakati sura ya Abdul ilikua inanijia nakuaniambia achana na hayo mambo ila sikuacha. Nilianza kuhangaika kutafuta mganga kwaajili ya Biashara zangu, mambo yalikua magumu sana, kila mganga Dar niliona kama ni tapeli, masharti kibao lakini sikuona chochote.


Siku moja nikiwa katika mishemishe zangu ndipo nilielekezwa na rafiki yangu mmoja Mkoani Manyara. Kama kawaida nilienda, nilikutana na mtaalamu na kuanza kunitengenezea dawa, nikiwa huko nilijikuta naanzisdha mahusiano na Mama mmoja ambaye ni mke wa mtu. Huyo akawa ndiyo ananisaidia pesa kidogo kidogo, hakujua nimeenda pale kwaanili gani lakini baada ya kama wiki niliamua kubaki pale nikiamini kuwa kuna fursa nyingi.


Nilianza kuishi na yule Mama kwenye nyumba yake kama mpangaji, hakua na uwezo sana, yeye likua ni Mama wa nyumbani lakini mume wake alikua ni mfanya Biashara huko Mbulu Manyara. Nikawa naishi pale kama mpangaji wakati huohuo natembea na Mama mwenye nyumba, kwa mganga nako nilikua nikihangaika kupata dawa na hapo ndipo nilikutana na Aneth.


Aneth alikua akisali kanisa moja na yule Mama na Mama yake alikua ni rafiki mkubwa na Mama yake na Aneth, mara kwa amra alikua akija pale nyumbani ingawa sikua na mazoea naye, hata salamu tulikua hatupeani. Siku moja nikuwa kwa Mganga ndipo aliniambia kuwa, kama nahitaji kufanikiwa basi nihakikishe nazaa na huyo binti. Aliniambia tu kuna binti anamuona katika maisha yangu, nyota zetu zimeshibana, ili kufanikiwa basi napaswa kuoana naye kwani nyota yake ina nguvu sana.


Adam anaonyesha ni namna gani alikutana na Aneth na sababu zake za kutaka kumuoa. Tunarudi tena baada ya ndoa na kujaribu kufanya naye mapenzi, je atafanikiwa?


ADAM; CHEZA NA MIMI LAKINI USICHEZE NA MUNGU WANGU! —SEHEMU YA TISA


Mpaka asubuhi nilishindwa kufanya mapenzi na mke wangu, nilikua na hasira sana, akili yangu haikua inafanya kazi vizuri. Nilishapoteza pesa nyingi kumpata Aneth na nilitegemea kwa kumuoa basi pesa yangu ingerudi lakini haikua hivyo. Asubuhi nilikua nimechoka sana, nilishampiga mke wangu sana lakini sikuweza kufanya kitu chochote, uume wangu uligoma kabisa kusimama.


“Mbona unakua hivyo mume wangu, ni kitu gani nimekukosea?” Aneth aliniuliza, ilikua ni asubuhi kwenye saa nne hivi. Nilikua ndiyo narudi, ausbuhi baada ya kushindwa kufanya mapenzi naye kichwa changu kilikua hakifanyi kazi vizuri. Kutokana na matendo yangu pamoja na vipigo nilivyokua nampa mke wangu na ukweli kuwa pale ni kwao, ana ndugu wengi eneo lile kuliko mimi nilijua kabisa akiamka ataondoka.


Kwa maana hiyo nilipoamka kitu cha kwanza ilikua ni kimfinga mikono na miguu, nikamnyang’anya simu yake na kumfungia chumbani kisha nikaondoka zangu nikiwaza nini chakufanya?


“Unamaanisha nini? Inamaana hujui ulichonifanyia? Wewe ni mwanamke wa ajabu sana, yaani hujui umenifanyia nini? Inamaana hujui umeolewa kwaajili gani?” Nilimuuliza kwa hasira huku nikimfuata pale chini, alikua kaka chini bado nimemfunga Kamba lakini niliona kama ananidharau, nilihisi kama swali olake ni la kejeli. Nilimuinamia kama nataka kumpiga, alinyamaza bila kusema chochote.


“Inamana hujui kuwa ni haki yako kunipa tendo la ndoa,s asa mbona unaniangalia nahangaika, jana usiku mzima nilikua nahangaika lakini hunisaidiii!” nilimuambia, nilijua mimi ndiyo nimeharibu, nilijua kuwa mimi ndiyo nimeshindwa kufanya naye tendo la ndoa, lakini kama mwanaume sikutaka hicho kitu kijulikane, nilijua kama akijua kuwa tatizo ni mimi nimeshindwa kumshughulikia basi atanidharau sana na hata kuniacha.


“Lakini mume wangu…” Alianza kuongea lakini sikumpa nafasi, nilimtukana sana huku nikimuita mchawi, sitaki tena atoke ndani hata kanisani sitaki aende.


“Najua wewe ni mchawi, sijui ni kwanini nilikuoa lakini najua umchawi, ulimloga kijana wawatu akawa chizi sasa hivio unaniloga na mimi! Nakuambia nitakuua, ukijaribu kutoka humu ndani nitakuua!” Nilimpa vitisho vingi kisha nikamfungua kamba.


“Nina njaa, nataka unipikie chakula!” Nilimuambia, alinyanyuka na maumivu makali na kuanza kuniangalia, aliniuliza lilipokua jiko sikua na jiko wala kitu chochote cha kupika lakini nilitaka chakula.


“Wewe ni mwanamke, utajua mwenyewe namna ya kunipikia lakini sitaki utoke humu ndani!” Alibaki tu kasimama ananiangalia, hakua ananiaelewa, hata mimi kwa wakati huo nilikua sijielewi, nilikua najua kabisa kuwa sina jiko wala kitu cjha kupika lakini bado nilitaka chakula, lengo langu lilikua ni kumsumbua tu.


Wakati tumesimama tunaangaliana simu yake iliita, alikua ni Mama yake, lakini hata sikuamini kama ni Mama yake, niliipokea mimi na niliposikia sauti ya kike ndipo nilimkabishi, nikasogea pembeni ili kumsikia kama atamuambia Mama yake kitu chochote. Walisalimiana kumuulizia hali lakini hakuongea kitu, alikata simu na kumuambia Mama yake kuwa atamtafuta baadaye.


“Sitaki uwe unaongea na Mama yako kila siku, wa Mama kama Mama yako ndiyo wanavunja familia, mtu umeolewa hata hujamaliza siku mbili ashaanza kukupigia simu. Kuanzia sasa nitakua nakaa na Simu yako, nakuambia sitaki uwe unaongea sana na Mama yako” Nilimuambia,a liitikia kwa kichwa kitu ambcho kilinipa hasira, nilimfuata na kumsukuma tena kwa nguvu akadondokea kitandani.


“Ukiongea na mimi nakuambia hakikisha unatoa sauti, mimi ni mume wako, acha kunijibu kwa vichwa!” nilitamani kumvamia na kumpiga tena lakini kuna kitu kiliniambia.


“Adam, mbona unakua kama chizi, binti wa watu hajakufanya kitu chochote, hembu uache apumue utamuua!” Basi nilimuacha na kutoka kabisa pale nyumbani, nilitoka mpaka mjini, huko nilihangaika kumpigia simu Mganga wangu ili kujua ni kitu gani kitanendelea.


“Nimekuambia sikufanya kitu chochote, nimepoteza pesa nyingi sana kumpata huyu mwanamke, ninachotaka ni wewe kunipa dawa ili nifanikiwa. Nataka kuondoka hapa, nataka kumuacha huyu mwanamke hapa!” Kwa bahati Mganga alipokea simu, kichwa changu kilikua hakifanyi kazi vizuri, nilikua na hasira sana. Unapoingia kwenye mambo ya kishirikina inakua kama imani, ni kitu ambacho kinakuchanganya sana, kuna mambo unakua unayawazia kuwa, kama usipoyafanya basi maisha yako yataharibika.


“Mbona kama unaniamrisha, nilikupa msahariti lakini hukutimiza, sasa unataka kunipangia maisha. Unaniambia nini?” Mganga alinijibu kwa hasira, nilijikuta napoa ndani ya dakika moja na kuanza kuomba msamaha kama mtoto mdogo. Alionekana kunielewa lakinia linipa mtihani meingine ambao niliona kama siwezi kuumudu.


“Kama amekushinda basi mlete kwangu kesho jioni….” Aliniambia, nilijaribu kumuambia kuwa mke wangu ni mtu wa dini hawezi kukubali kwanda kwa Mganga lakinia liniambia kuwa hiyo ni shida yangu, kama nahitaji msaada wake basi nihakikishe kuwa nampeleka mke wangu kwake. Alikata simu na kuniacha nikiwa nawaza, ni kwanamna gani ninaweza kumtoa mke wangu nyumbani na kumpeleka kwa Mganga.


*****


“Siwezi kushinda hii vita kwa ubabe, kama nahitaji kushinda nilazima kujishusha!” Niliwaza wakati narudi nyumbani, nilijua kua kama nikiendelea kumpiga mke wangu basi hatanisikiliza kwa chochote.


“Ubabe ndiyo ulinifanya jana nikashindwa kufanya tendo la ndoa na mke wangu, sasa hivi nakua mume kwake!” nilijiambia huku nikinunua chakula mtaani, nyumbani sikua na jiko kwakua mimi sikua mtu wa  kupika wala sikua na malengo ya kukaa pale muda mrefu, hela niliyokua nayo ilikua inakaribia kuisha, nilishakopa washikaji wengi sana na ndugu zangu walishanichoka hata simu zangu walikua hawapokei.


“Mke wangu naomba unisamehe, sitaki hata kumsingizia shetani lakini mambo niliyokufanyiia jana sijui kama ilikua ni akili yangu au akili ya nani? Naomba unisamehe mke wangu!” Nilikua nimemnunulia Chips Kuku, nilipofungua mlango tu nilianza kwa kupiga magoti huku nikilia. Nililia sana nikimuomba mke wangu msahama, nilikau sina jiko lakini nilikua na Birika la umeme, nilichemsha maji na kuanza kumkanda mke wangu, nilimkanda mwili mzima huku nikimuomba msamaha.


“Sijui nini kimetokea mke wangu, kushindwa kufanya tendo la ndoa kulinifanya kuchanganyikiwa, naomba unisamehe….” Kila dakika nilikua naomba msamaha, sijui kama mke wangu aliniamini au aliona kama asipokubaliana na mimi labda nitampiga tena ila aliniambia kuwa kanisamehe. Sikutaka hat amsamaha wa kihivyo, nilichotaka tu ni mimi kuongea tu vizuri kwani bado nilikua sijajua ni kwanamna gani nitamshawishi mke wangu mpaka kukubali kwenda kwa Mganga.


Mpaka usiku nilikua vizuri, nilikua naongea kama mtu nikisubiria muda ufike ili niweze kwenda naye. usiku ulipoingia bado alikua amechoka, niliona fursa ya chakula cha usiku.


“Najua kuwa sina kitu humu ndani, sikupanga kuoa ghafla namna hii, lakini nitanunua kila kitu kesho. Kwa leo kuna Kaka yangu anataka kuonana na wewe, alishindwa kuhudhuria sherehe kwakau alikua anaumwa, ni kaka wa kufikia, nilipokuja hapa yeye ndiyo alinipokea….”


Nilijisemesha, alinisikiliza lakini ni kama alikua ananiogopa, alikubaliana na kila kitu nilichomuambia. Nilimuambia avae avazuri ili tutoke. Alivaa na kutaka kubeba pochi yake lakini nilimkatalia kwani ilikua na Bibiilai yake na mimi sikutaka abebe kitu chochote kinachohusiana na Mungu.


“Tunarudi sasa hivi, Pochi ya nini?” Nilimuambia, alinikubalia kishingo upande name sikujali. Tulienda mpaka kwa Mganga, haikua nyumba kama nyumba nyingine za wwanaganga, alikua ni mzee, ana nyumba yake nzuri tu, si Mzeee sana kamaMzee hapana, alikua na miaka kama hamsini hivi. Basi nilifika na kukaribishwa na mke wake, ambaye alikua ananifahamu na alikua akijua ujio wetu.


Alimchangamkia sna ana kukaribisha sebuleni, baada ya kama dakika kumi hivi Mganga alikuja, nilimtambulisha kama Kaka yangu. Mke wangua limsalimia kwa heshima na mpaka wakati huo kulikua hakuna kitu kibaya chochote kilichotokea. Nilikua na wasiwasi sana kwani nilikua najua nguvu za mke wangu, kama alinizuia mimi kufanya naye mapenzi vipi huyu mganga, vipi kama ana nguvu za kuziia dawa zake.


Niliwaza huku nikimuomba Mungu hilo lisitokee. Kusema kweli nilishachoka ile ndoa ingawa ilikua haina hata siku mbili, nilichotaka mimi ni kumtumia Aneth kama nilivyoambiwa kuwa ana nyota kali absi nifanikiwe niachane naye. Mganga alimsalimia kwa kumshika mkono, kisha akaja kunisalimia na mimi. Nilimuona kabisa akitetemeaka, nilijua ni Nguvu aliyokua nayo mke wangu hivyo nilizidi kuogopa.


Lakini mke wake ni kama alijua kuwa kile kitu kitatokea hivyo alijiandaa. Baada tu ya kumuona mume wake anasalimia na kuanza kutetemeaka moja wka moja bila kusubiri kuambiwa alileta chakula. Alikiweka mezani na kutupakulia wote, ni kama alijua kuwa Aneth ataomba hivyo baada tu ya kukiweka chakula mezani basi alipiga Magoti nakuanza kusali.


Alisali kwa sauti tu sala ya kawada, tgena ndefu alipomaliza alitukaribisha chakula hukua kitabasamu. Nilianza kula huku nikimuangalia mke wangu, kusema kweli sikujua kitu kilichowekwa kwenye chakula lakini nilipoanza kula nilipata nguvu ya ajabu kiasi kwamba chini ya suruali nilijihisi kama nasisimkwa.


Nilikula huku nikimuangalia mke wangu, kilikua ni chakula kizuri, wali mtamu na nyama ya kuku. Alikula vizuri tu mpaka akamaliza chakula alichotengewa. Baada ya hapo Mganga hakutaka akae, aliniambia niondoke na mke wangu ila tusirudi nyumbani niende naye sehemua mabyo hawezi kunidhibiti kwani hatujui ana nini kaja navyo nyumbani.


Nilifanya kama nilivyoagizwa, nilienda na kuchukua Gest, Aneth hakua kama awali, alikua kama kachangamka flani hivi. Hakuongea tena mambo ya kimungu mungu hivyo nilikua na amani kidogo. Kwelis iku hiyo niliweza kufanya naye mapenzi na kila mmoja wetu alifurahi. Siku iliyofuata tulirudi nyumbani, kwangu mimi nilikua nishakamilisha kila kitu hivyo ulikua ni wakati wangu wa kuondoka.


“Nina safari mke wangu, nataka kwenda nyumbani kumuona Mama. Kabla ya kwenda kukupeleka rasmi inabidi nikafanye maandalizi, kimila zetu mimi natakiwa kutangulia kabla ya wewe kuja.” Nilimuambia mke wangu, alishangaa kwani ndoa yetu ilikua bado changa, aliniuliza kwanini nafanya hivyo, sitaki kupata muda nayeyea ila nilijifanya kukasirika.


“Hivi wewe ni mwanamke wa namna gani? Yaani nakuonyesha mapenzi yote lakini unajifanya kuuliza uliza, kwanini hunisikilizi?


Kila kitu wewe ni kubisha! Kubisha! Kubisha!” Nilimuambia kwa hasira, nilimuiona ananyamaza na kunyong’onyea. Hapo nilijua nishamdhibiri, nilikusanya karibu kila kitu changu kama ni mtu amabye nahama, mule ndani sikua na vitu vingi, nilikua na vitu vichache tu kwani sikupanga kuishi pale muda mrefu. Nilimuacha na kitanda na godoro tu, aliniuliza kwanini nachukua kila kitu lakini sikumpa jibu la maana zaidi ya kumkasirikia.


Siku iliyofuata nilipanda Gari na kurudi Dar, nilikua bado sijampigia simu Mganga wangu, nilipanga nikishaondoka, nikaweka mambo yangu sawa ndiyo niwasiliane naye. Lakini nikiwa njiani alinipigia simu yeye na kuniuliza kama nilifanikiwa, nilimuambia kuwa nilifanikiwa na wakati huo nilikua njiani kuondoka.


“Hakuna shida, ila ukianza Biashara hakikisha kuwa unakuja kuchukua dawa, hii ilikua ni hatua ya kwanza tu. Kama ukifuata kila kitu kama nilivyokuambia nina uhakika kuwa kila kitu kitakua vizuri. Nilikubaliana naye, nikafika dar, kwangu nilipokua nimekaa, bado nilikua na nyumba moja ambayo nilikua sijaiuza. Niliichukulia mkopo Benki na ilishauzwa kwa mtu mwingine lakini nilifanya namna ikarudi kwangu, nikawa kama nimeinunua kwake hivyo nilikua na deni jingine.


Nilifikia kwangu na kuanza kufanyia kazi baadhi ya dawa nilizokua nimepewa. Ni dawa ambazo nilikua nimepewa muda mrefu lakini niliambiwa haziwezi kufanya kazi kama nisifanya mapenzi na Aneth. Wiki moja baadaye nilikau kwenye Biashara, kila kitu kilikua kinaenda vizuri. Sikua na mtaji lakini nilikua najuana na watu, mwanzo hakuna mtua liyekua akinaimini kunipa vvitu kwa mali kauli, lakini baada ya kurudi tu nilipigiwa simu na rafiki yangu mmoja.


Yeye alikua mwanza, alianza kuniuliza kama naweza kumpatia injini ya Scania, alikua anajua kuwa ninamiliki Magari, sikujua kama nawezakwani sikuwahi kuuza Injini lakini nilimkubalia, nilianza kuzunguka mjiini na haikua shida kumpatia. Aliniamini na pesa zake,a kanitumia nikamnunulia na kweli nilutengeneza milioni mbili siku hiyo.


Huo ndiyo ulikua mwanzo, nilisahau kabisa kuhusu Aneth, nikabadilisha na namba za simu, sikutaka kumjua kabisa. Niliwasiliana na Mganga na kwenda kuchukua Dawa nyingine ndipo aliniambia kuwa, ndugu zake walikua wananitafuta. Pale nilipokua nikiishi Kodi ilishaisha lakini Aneth ahakuondoka, alilipia ile kodi mwenyewe na kuendelea kukaa pale huku akinisubiri.


Lakini haikuchukua muda, miezi mitatu baada ya kuondoka kule nikamini kabis akwua mambo yangu yashanyooka na sitakua nikihangaika kabisa na mambo ya waganga nilipigiwa simu na namba mpya. Nilijua kuwa ni wateja wangu lakini hawakua wateja, mke wa Nganga, alijitambulisha huku akilia.


“Nilitaka tu nikuambie kuwa mume wangu amekufa, alikua anakuchukulia kama ndugu lakini amefariki kwa ajali ya gari…” Aliongea huku akilia, kusema kweli hata sikumsikiliza.


Nilijua kuwa Mganga hakua ndugu yangu wala rafiki yangu, nilishamlipa pesa yake na maisha yangu yalishaanza kwenda vizuri. Nilimpa pole nyingi na kujifanya kama nina haraka, nikakata simu, akapiga tena.


“Huyu Mama vipi, anataka pesa nini?” Niliwaza huku nikipokea simu, ni kama alinisikia kwani aliniambia.


“Sina shdia ya pesa lakini nahisi kuna tatizo. Wakati namuuguza mume wangu hospitalini kabla hajafairiki nilimuona mke wako. Ana mimba, alienda kiliniki, hii ni mbaya, ulipaswa kutembea naye, abebe mimba ya mizimu na si mimba ya mtoto!” Aliniambia, niliona kama ni ujinga tu.


“Sasa kama ana mimba kuna shida gani, mbona mume wako aliniambia nina hakikisha kuwa natembea naye ili abebe mimba, sas akuna nini tena?” Nilimuuliza kwa wasiwasi kidogo.


“Unatakiwa kutembea naye kweli, lakini hatakiwi kuzaa, kama akizaa basi jua kuwa na wewe ndiyo mwisho wako unarudi kulekule ulikotoka!” Aliniambia maneno abayo yalinitisha.


“Mwisho wangu kivipi? Nakufa au?” Nilimuuliza.


“Hapana, akizaa basi jua kuwa unabeba machungu yake yote!” Sikumuelewa kwakweli, nilimuomba kunielezea lakinia lionekana kama ana haraka, wakati tunaongea ni kama alikua kasahau kifo cha mume wake kidogo lakini nilipoendelea kumdodosa alianza kulia na ghafla akakata simu.


Nilijaribu kumpigia simu lakini hakupokea. Niliamua kumpuuzia, mambo yangu yalizidi kwenda vizuri, sikuona dalili yoyote ya Biashara zangu kuyumba, watu walizidi kuniamini hivyo sikuona sababu ya kuhangaika na mke wangu.


Nilikaa kimya bila kumtafuta Mganga tena, kusema kweli nilikua nishaanza kuachana na hayo mambo. Niliona kama ni kupotezeana muda, nilikua na kila kitu changu. Baada ya kupata pesa kwa njia ambayo si halali nilitaka kuwekeza na kutafuta pesa halali. Siku moja nikiwa sina hili wala lile mara nilianza kusikia tumbo linauma, lilikua linauma sana kiasi kwamba hata kunyanyuka huwezi.


Nilikua napata maumivu makali chini ya kitovu, nikikaa nahisi kama kuna vitu vinazunguka zunguka tumboni. Ghafla nilianza kutokwa na damu sehemu ya haja ndogo. Kusema kweli nilianza kuogopa, ghafla nikakumbuka ndoto ambayo nilikua nayo siku ya kwanza nilipomuoa Aneth, maumivu niliyokua nikisikia wakati ule ndiyo hay ohayo nilikua nikisikia. Kuna wakati nilitaka kujiaminisha kuwa nipo kwenye ndoto lakini haikua hivyo.


Nilisikia maumivu makali sijawahi kuyapata, nilipiga kelele nyingi lakini sikupata msaada wowote. Nilikua nyumbani kwangu peke yangu naugulia tu maumivu. Nilichukua simu ili kumpigia rafiki yangu kuja kunipeleka hospitalini kwani nilikua siwezi hata kunyanyuka lakini kila mtu niliyempigia simu yake ilikua eidha haipokelewi au haipatikani kabisa.


“Hiki ni nini jamani?” Niliwaza, nilihisi kuchanganyikiwa, nikiwa sina hili wala lile nilikumbuka mtu mmoja ambaye sikumpigia. Mke wa Mganga, niliamini labda anajua kitu kinaweza kunisaidia. Wakati huo ndiyo msaada pekee ambayo nilikua nakutegmea. Nilimpigia na bahati nzuri aliipokea simu. Ni kama alijua sababu ya mimi kumpigia kwani kabla hata ya kumuambia alianza kucheka huku akiniambia.


“Miezi tisa tayari, naona mnataka kujifungua!” Aliniambia huku akiongeza kicheko.


“Unamaanisha nini?” Nilimuuliza.


“Namaanisha kuwa, unanitafuta kwakua ushaaanza kupata maumivu ya uchungu. Ungekua umezaa basi ungejua ni kama uko leba, naona unamsaidia mke wako kuzaa! Hayo ndiyo maisha yako sasa!” Aliniambia, kila akimaliza kuongea alikua akicheka, ni kama alikua akinidhihaki bila kujua nilikua kwenye maumivu makali kiasi gani.


Nilitamani kumtukana na hata kumkatia simu lakini kwakua nilikua na shida basi sikua na namna. Nililazimika kuvumilia. Aliniambia sababu ya mimi kuumwa ni kwakua mke wangu ujauzito wake ulishafikisha miezi tisa na alikua anajifungua. Maumivu ninayopata nikwakua niliruhusu mpaka mke wangu kufikia kujifungua.


“Nilikuambia tangu mwanzo kuwa, sababu ya wewe kupewa yule mwanamke ilikua ni sababu ya Kizazi chake. Alipaswa kuwa mke wako lakini hakupaswa kuwa Mama wa watoto wako. Mlipaswa kuishi kwenye ndoa lakini hakupaswa kuzaa, sijui ni kwaninia libeba mim ba yako, sijui ni kwanini mimba haikuharibika ila sasa hivi kama unapata hayo maumivu basi yuko Leba anakaribia kujifungua.


Kama akifanikiwa kujifungua mtoto, awe hau au amekufa basi jua kuwa kila kitu chake kitakugeukia wewe. Huyo mwanamke alipaswa asizae. Mtoto alipaswa kuyeyuka tumboni na kutoka na kizazi chake kama Damu, baada ya hapo angeendelea kuingia hedhi kwa maisha yake yote.


Ili wewe kuendelea kupata pesa basi yeye ilikua ni lazima damu kumtuka kila siku. Lakini sasa hivi, kama akizaaa huyo mtoto basi jua kuwa damu ya hedhi itakua inakutoka kila siku katika maisha yako yote.


Nilijaribu kukuambia kipindi kile nilipomuona na mimba lakini hukunisikia. Kwasasa ni wewe kuharakisha uonane naye na uhakikishe kuwa hajifungui. Huyo mtoto hatakiwi kutoka kama mtoto b ali kutoka kama damu, anapaswa kutoka kama damu. Mizimu inataka sadaka ya damu na si sadaka ya nyama.”


Aliniambia kisha akakata simu, kwangu maumivu yalikua makali sana, nilihisi kuchanganyikiwa. Sikujua nini chakufanya, nilikua nimekaa chini najigeuzageuza, maumivu kama vile mtu ananichemsha. Yeye yuko Manyara na mimi nipo Dar, ni namna gani naweza kuwasiliana naye, ni namna gani naweza kujizuia ili asizae, sikua na jibu, nilihisi nguvu zinaniishia, nashindwa hata kuhema, akili ilisimama, haifanyi kazi tena.


Mambo ndiyo yanaanza, Adam alidhani kashafanikiwa na kuachana na mambo ya waganga lakini kumbe bado. Mambo ndiyo yanaanza kabisa. Unashani nini kitatokea, je Anetha tajifungua, naomba nisikuchoshe.


ADAM; CHEZA NA MIMI LAKINI USICHEZE NA MUNGU WANGU!—SEHEMU YA KUMI


Hali yangu ilikua inazidi kuwa mbaya siku hadi siku. Siku tatu mfululizo nilikua siwezi hata kunyanyuka, nilimpigia siamu rafiki yangu ambaye alinipeleka hospitalini ilia sikua na tatizo lolote lile. Nilipimwa kila kitu lakini hawkaugundua tatizo. Maumivu niliyokua nikiyapata yalikua hayaelezeki, nilikua naumia sana hapo ndipo niliamini kuwa uchawi upo.


“Nimemfunga ahwezi kujifungua, ataumwa uzazi weee lakini kujifungua hawezi. Unapasawa kuja huku, unapaswa kuja kuonana na mke wako. Yule mwanamke ana nguvu sana, kwasasa ana mimba tu, muda wake wakujifungua umefika anapata uchungu wa kawaida lakini sio ule uchungu wa kujifungua. Uchungu wa kujifungua unao wewe!” Siku ya tatu nikiwa sina hili wa alile mke wa Mganga alinipigia tena simu.


Aliniambia kuwa nitaumwa uchungu mpaka pale ambapo mke wangu atajifungua na huo ndiyo utakua mwisho wa Biashara zangu. Pamoja na maumivu niliyokua nayo lakini nilisafiri, nilimchukua rafiki yangu, tukapandan gari mpaka Manyara, sikujua naenda kuongea nini na mke wangu lakini nililazimika kufuata kila kitu alichokua akiniambia yule Mama.


Nilishukia kwake, yeye ni kama alikua akimfuatilia mke wangu kwani alikua akijua kila kitu kilichokua kikiendelea katika maisha yake baada tu ya kugundua kuwa ana mimba.


“Nilijua tu utarudi, mnajifanyaga watakatifu mkishasaidiwa!” aliniambia, nilikua katika maumivu makali, hata kumjibu niliona shida. Mume wake ndiyo alikua Mganga lakini alionekana kujua kila kitu, baada ya kufika kwake alianza kunitengeneza, aliniogesha yeye mwenyewe na kunipaka midawa mingi.


Kweli asubuhi nilikua vizuri, maumivu yalikwisha kabisa.


“Maumivu yamesharudi kwa binti wa watu, ni wakati wako sasa, nenda hakikisha kuwa hazai!” Aliniambia, nilimgeukia na kumuuliza ni kwa namna gani nitahakikisha kuwa hazai?


“Fanya naye mapenzi, hakikisha unafanya mapenzi na huyo mwanamke, kuna dawa nimekupa, ukifanya mapenzi naye mimba itatoka kama damu na huo ndiyo utakua mwisho wa matatizo yako.


“Nitampataje sasa?” Nilimuuliza, muda mrefu ulikua umepita, sijawasiliana na ndugu zake wala sihawasiliana na mke wangu. Alikua kwao, sehemu ambayo nilikua sijawahi kukanyaga tangu siku nilipokabidhiwa mke.


Nilikua nishaingia kabisa kuamini mambo ya kishirikina, udaktari wangu nilishauweka pembeni hivyo niliondoa aibu na kwenda nyumbani kwao. Tofauti na nilivytotegemea kumkuta katika hali mbaya, kutukanywa na kufukuzwa nilikaribishwa vizuri sana mpaka kuona aibu. Ilikua ni familia ya watu wa dini sana na waliamini katika ndoa. Hivyo nilivyofika nilipokelewa kama mume wake, yaani kama ndiyo nimetoka hapo jana yake.


Kusema kweli pamoja na kufurahia kupokelewa lakini nilijisikia vibaya kwani sikwenda pale kwaajili ya kuwasiadia bali kuzidi kumharibia Aneth maisha yake. Ilikua ni mchana, walinikaribisha vizuri na jioni ndipo niligundua kuwa Aneth kwa kukwepa aibu alikua hajawaambia wazazi wake kuwa nilikua nimemtelekeza na kuondoka zangu.


Alikua kawaambia tu kuwa nimepata kazi darn a kila siku tunawasiliana na malengo yetu ni yeye kubaki Manyara mpaka pale atakapojifungua. Kusema kweli nilishangaa, sana, nilipomuuliza ni kwanini aliamua kufanya hivyo aliniambia.


“Wewe ni mume wangu, niliapa kanisani mpaka kifo kitutenganishe, sasa nitakujaje kuwaambia wazazi wangu kuwa nimekuacha kabla ya kifo. Nilijua utarudi Yesu wangu aliniambia kuwa utarudi.” Aliniambia, kwakweli niliishiwa pozi nilishindwa hata kuongea, nilibaki kimya tu. Pamoja na yote hayo lakini kwangu ilikua ni rahisi sana kutimiza adhma yangu kwani usiku nilitaka kwenda kulala Gest lakini walinizuia, Aneth alisharudisha chumba changu nilichokua nimemuacha hivyo waliniambia nilale kwao.


Sikua nahiana kwani mwanzo nilikua nikizuga tu kuhusu kuondoka, niliandaliwa chumba na kwakua tulikua na ndoa ya kanisani basi tulilala chumba kimoja. Usiku nilikua na kazi ya kuomba msamaha, nilikua nikiongea huku nikijifanya kujutia, nilimuambia mambo mengi niliyoyafanya mjini.


‘Wakati nakuoa sikua na pesa, nilijua utanikataa, ndiyo maana kipindi kile nilikua na hasira sana, nilikua kama nimechanganyikiwa, nikaona kuliko kukuua kwa kipigo ni bora mimi kuondoka na kukuacha uendelee na maisha yako.”


Nilimuambia kuwa niliondoka ili kutafuta maisha nikirudi nina hela zangu.


“Nisingeweza kukaa na mwanamke ana kazi wakati mimi sina kazi yoyote, ilikua ni lazima kuondoka maana ningechanganyikiwa kama ningebaki hapa!” nilimuambia, kazi yake kubwa ilikua ni kunisikiliza na kuniambia kuwa ameshanisamehe. Aliniambia bado ananipenda na alishasali sana kuhusu mimi.


“Kila nilipokua najaribu kukuacha Mungu alikua ananiambia hapan! Aneth, huyo ni mume wako! Basi nilibaki nikijua kuwa ipo siku utarudi na kwa bahati nzuri leo umerudi!” Aliniambia, mimba ilikua kubwa, alikua nakaribia kujifungua, lakini bado ilikua ni lazima mimi kufranya mapenzi naye kwani nilikua nikiamini kuwa, kama nisipofanya naye mapenzi basi ndiyo utakua mwisho wangu.


Nilimuomba kufanya naye mapenzi, nilijifanya nimemmiss kwamba tangu kuondoka kwangu nilikua sijawahi kufanya mapenzi na mwanamke mwingine. Tofauti na nilivyodhani Aneth alikubali kufanya mapenzi na mimi. Nilifanya mara nyingi niwezavyo na siku hiyo hata sikupata shida kama siku za mwanzo. Niliamini kuwa labda ni dawa za yule Mama ndiyo zilikua zimefanya kazi. Tulichoka na kulala, lakini usiku wa manane Aneth aliniamsha, alikua anasikia maumibu makali.


“Nahisi nakaribia kujifungua, nisaidie…” Aliniambia.


“Chupa imepasuka mume wangu nisaidie….” Alizidi kuniambia hukua kijishika sehemu zake za siri. Niliwahsa taa kumuangalia kwa uoga nikiwaza kama atajifungua basi ndiyo mwisho wake. Lakini baada tu ya kuwahs ataa nilijikuta nafurahia mwenyewe, kitu alichokua kaniambia yule Mama ndiyo kilikua kimetokea.


Hayakua maji yamepasuka, hayakutoka maji ya uzazi bali zilikua zinatoka damu tena nzito nzito.


“Mbona ni damu, umefanya nini?” Niliongea kwa kuoaniki, alijiangalia na kweli aliona damu lakini cha kushangaza wala hakupaniki. Alikua abdo ananiambi nimsaidie ili ajifungue. Alikua katika maumivu makali hukua kipiga kelele akiomba msaada. Mama yake alikuja, kwakua mimi nilikua daktari hawakua na namna waliniacha nimzalishe, bila kujali kama mimi ni mkwe wake Mama yake naye alikuja kumsiadia binti yake.


Alikua anapiga kelele kama anajifungua lakini zilikua zikitoka dmau tu, baada ya kama dakika kumi hivi ziliacha kutoka damu na kuanza kutoka mabonge ya damu kama mikate midogo hivi, ilitoka kama mitano kisha kila kitu kikatika na Anetha kapoteza fahamu.


“Ni kitu gani kimetokea, mbona hivi?” Mam ayake aliuliza hukua kipiga kelele, mimi kichwani nilikua nafurahia.


“Mimba imetoka!” nilijaribu kumuelezea Mama mkwe lakini hakukubali maelezo yangu.


“Mimba ya miezi tis ainatokaje, inatokaje! Niambie wewe si daktari, ilitakiwa kutoka maiti kama mtoto amefia tumboni si uchafu huu!” Mama yake aliongea lakini mimi hata sikujali. Nilikua nishakamilisha kilichonipeleka pale nilianza kutafuta tu kitu cha kunifanya kuondoka na kuwaacha na mambo yao.


“Kazimia huyu tumpeleke hosputalini!” Nilimuambia Mama yake ambaye alikua kapaniki sana, ile kumuambia ndiyo kama nilimuamsha kutoka usingizini. Alinikubalia, akawaita tukamchukua mpaka kwenye gari, lakini kabla ya kuondoka aliamka na kusema kuwa yeye yuko vizuri hataki kwenda hospitalini anamhitaji Mchungaji. Nilimshi sana kama daktari lakini aligoma, nikaona ahaa kimbembe hiki, basi tukamrudisha ndani, lakini kutokana na chumba tulichokua tumekaa kilikua kimejaa damu wakampeleka chumbani kwa Mama yake.


Niliingic humbani huku nikijifanya kulia, nikaanza kusafisha kila kitu nikajifanya nafanya usafi lakini niliondoka na hivyo vitu, niliondoka kabla mchungaji wao hajaja kwani nilikua namuohopa flani. Nilivipeleka kwa Mama na kufanyiwa dawa.


“Sasa uko salama, unaweza kuondoka na usigeuke nyuma. Yule binti tushachukua kizazi chake, hatakuja kuzaa tena, damu zitamtoka mpaka anakufa!”Aliniambia, kusema kweli nilifurahi kwani niliona maisha yangu yanaenda kuwa mazuri.


Kila nikikumbuka maumivu niliyokua nikiyapata kipindi nimebeba mauivu ya uchungu wake nilipata amani sana, sikujali mambo yatakayo mkuta yeye na maisha yake. Nilitaka kuondoka siku iliyofuata lakini yule Mama Alinizuia, kuna dawa nililazimika kumalizia, nilijikuta nakaa pale wiki nzima. Sikurudi kwa mke wangu wala wao hawakunitafuta.


Jumamosi moja nilipanda gari na kuanza safari ya kurudi Dar. Nilikua na amani sana, niliamini kuwa kila kitu kishakua sawa, maisha yangu yatakua mazuri. Sikujuali kuhusu ndoa, sikujali kuhusu mwanamke ambaye alionyesha kunipenda. Nilikaa Dar siku mbili, usiku mmoja nilipokes imu kutoka kwa namba ngeni, nikijua ni wateja wangu ilikua ni sauti ya mke wangu.


“Hongera, umekua Baba, nimejifungua mtoto wakiume….”Mke wangu aliniambia, nakumbuka nilikua nimesimama nimeshikilia Soda mkononi, chupa ilidondoka na kupasuka wala sikuisikia.


“Unasema nini? Wewe si mimba ilitoka!?” Nilimuuliza kwa hasira, sikuonyesha kufurahishwa lakini yeye aliishia kucheka tu.


“Haikutaka mimba zilitoka damu, ulitoka uchawi, ilitoka mikosi!” Aliniambia, kwa namna alivyokua anaongea ni kama alikua anajua kila kitu.


“Umefanana naye mwanangu, yaani wewe mtupu…” Aliniambia, kusema kweli sikua na hata kitu cha kujibu, nilibaki najing’atang’ata, mdomo umekua mzito sana sijui hata nifanye nini! Nilimpa hongera, aliipokea huku akicheka, yaani ni kama alikua ananicheka, ni kama alikua anajua kinachoendelea.


“Mbona huna furaha?” Aliniuliza, nilijilazimisha kucheka lakini hakikusaidia, nilishindwa kuongea kisha nikakata simu. Simu iliita tena lakini sikupokea, nilikua kama naogopa, yaani nilikua natetemeka sana, mara meseji ikaingia kwenye simu yangu.


“Cheza na mimi lakini usicheze na Mungu wangu!” iliishia hapo, hapo ndipo nilijua kuwa mke wangu amejua kila kitu. Nilizima simu kabisa huku nikifuta ile meseji, ilikua ni meseji tu, tena ya simu, kwenye simu yangu lakini ilikua ikiniogopesha na kunitetemesha sijui kama nini! Sikuhiyo sikulala, nilimpigia tena yule Mama kutaka kumuambia kuhusu kilichotokea aliniambia.


“Huyo Dada Mganga wake simuwezi, tafuta Mganga mwingine lakini mimi sitaki kuhusishwa tena.”Alinikatia simu na hakuja kupatikana tena. Nilikaa kama miezi miwili hivi, siwezi hata kutoka ndani, nakua naogppa tu, yaani hakuna kitu lakini naogopa tu, nikawa hata siwezi kwenda kwenye Biashara zangu, kila kitu kilisimama tena. Ndani ya Muda mfupi nilirudi tena sifuri, nilikua sina kitu tena, yaani nikaanza tena kutafuta kazi, sina hata pes aya kula.


Niliamua kumtafuta Salma kuona kama anaweza kurudiana na mimi lakini aliposikia ni Mimi alinikatia simu. Siku moja nimekaa sina hili wala lile meseji ikaingia.


“Mume wangu kuna nafasi za kazi zimetoka, nimekufungia naamini utapata.” Ilikua ni meseji kutoka kwa mke wangu, alinitumia na Link za hizo nafasi, niliangalia walikua wanataka daktari kweli lakini uzoefu wake ni kama miaka mitano.


Mimi tangu kutoka Intern nilikua sijawahi kufanya kazi yoyote. Niliogopa kuomba nikaacha. Siku moja kabla ya deadline nilipokea meseji nyingine.


“Umeomba ile kazi?” sikuijibu ile meseji lakini nilikaa nikaandika Barua, nikajaza online nikatuma. Huwezi amini niliitwa kwenye usahili, sijui niliongea nini lakini niliipata ile kazi. Baada tu ya kuipata mtu wa kwanza kumpigia simu alikua ni mke wangu.


Hakuonyesha kushtuka, ni kama aliamini kuwa nitaipata ile kazi. Nilimshukuru sana na tangu siku hiyo sikutaka kuishi tena mbali na mke wangu. Niliomba sana msamaha lakini ni kama alishanisamehe. Ni kama alikua ananijua tangu mwanzo lakini alikubali kuolewa na mimi. Mke wangu hapendi kuongea haya mambo kabisa lakini ukiongea naye ni kama alikua anajua kila kitu nilichikua nakifanya.


Nashukuru sasa hivi naishi na mke wangu kwa amani. Nimejifunza mengi lakini kubwa nimejifunza kuwa imani inajenga. Ukimuamini Mungu kwa dhati basi mambo ya ulimwengu hayawezi kukusumbua. Kila nikiwaza ni kwanini mke wangu alikubali kunirudia pamoja na mambo yote hayo nashindwa kuamini, nina bahati, nimepata mwanamke ambaye hata si stahili. Ni kama Mungu alimleta ilikuja kuniokoa, nina furaha sasa na familia yangu.


MWISHO



0 comments:

Post a Comment

BLOG