IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO
Baada ya kuachishwa kazi kutokana na vyeti feki nilikuasina pakwenda. Kila kitu kilisimama, nilikua ni mjamzio na ndiyo kwanza nilikua nimetoka kuachana na mpenzi wangu wa muda mrefu, aliniacha na kwenda kumuoa mwanamke mwingine ambaye alichaguliwa huko nyumbani kwao. Nilikua sina akiba yoyote kwani mshahara wangu wote ndiyo nilikua nikiutumia kusomesha wadogo zangu.
Kodi ilikua imeisha, sikua na pakwenda. Rachel (sio jina lake halizi) rafiki yangu ambaye tulikua kama ndugu, nilisoma naye na kwa bahati nzuri tulikua tunafanya kazi pamoja alinichukua kuishi naye pamoja. Yeye ndiyo kwanza alikua kaolwa, ndoa yake ilikua na kama miezi mwaka mmoja na miezi mitatu. Aliongea na mume wake ambaye ni mkimya, sana na kumuambia kuhusu mimi, kweli alikubali.
Wakanichukua nikawa naishi nao, wakati huo nilikua na ujauzito wa miezi sita, nilika apale nikisaidia kazi za nyumbani mpaka ulipofika wakati wa kujifungua, kwakua sikua hawakua na mfanyakazi wa ndani na yeye pamoja na mume wake wanafanya kazi huko Rachel akiwa ni mtu wa kusafiri sana basi tulipanga mimi kwenda kijijini kujifungua ili kupata mtu wa kunihudumia.
Lakini haikua hivyo, nilipata uchungu mapema, mtoto akalazimika kuwekwa kwenye mashine ili kutimiza miezi tisa. Kwasababu hiyo nililazimika kubaki pale. Sam (Sio jina lake halisi) mume wake na Rachel alimuomba Mama yake kuja kunisiadia kunihudumia. Mama yake ambaye alikua ni nesi, ndiyo alitoka kustaafu, alikua akiishi Tanga, hivyo alifunga safari mpaka Dar kuja kunihudumia.
Familia yao ni familia ya upendo sana, Mama yake alikuja na kunihudumia kama mwanae, lakini katika kuja kwake niligundu akitu kimoja. Yule Mama alikua hampendi sana rafiki yangu, ingawa alikua anaigiza mbele ya mwanae na kujifanya anampenda lakini kuna vitu vidogo vidigo vingi alikua anavifanya kuonyesha kuwa hampendi. Tatizo kubwa nililoligundua ilikua ni kabila, Sam wao ni watu wa kanda ya ziwa, wasukuma huku Rachel akiwa ni Mpare.
Mimi pia ni Msukuma, alinipenda sana, na kila mara alikua ananiambia anatamani mimi ndiyo ningekua mke wa mwanae. Nilijisikia vibaya kwani nilikua niko kw3a rafiki yangu, alinipenda, akawa anamhudumia mwanangu na kuwa karibu na mimi. Baada ya kumaliza uzazi na mimi kuwa sawa alirudi Tanga alipokua akiishi, lakini hali ya hewa mule ndnai ilibadilika, kila mata alikua anapiga simu kulalamika kuwa anataka mjukuu.
Alikua anamlalaimikia mtoto wake, yakazuka maneno kuwa aliondoka kwakua rafiki yangu alikua anamnyanyasa kitu mabacho mimi sikukiona. Mtoto wangua lipofikisha miezi 6 bado nilikua pale, nilianza kutafuta kazi, nilihangaika sana lakini sikupata. Nilikua katika mawazo sana, akili haifanya kazi. Nilianaza kujikuta nakua na hasira, nakua na wivu nikimuona rafiki yangu jinsi ambavyo anapendwa, anahudumiwa, mume wake ni mpole, anamjali, wana kazi nzutio yaani wana kila kitu nilijikuta nakua na hasira sana.
Nikajikuta bila kujua naanza kumchukia, kwanza hakua mzuri kama mimi, lakini darasani hata hakunizidi chochote. Nilisoma naye chuo hivyo namjua, mimi sikufoji hivyeti kwakua sikua na akili, hapana, nilikua na ufaulu mzuri tu darasani lakini wakati wa mtihani niliumwa sana, nikashindwa kufanya mtihani, lakini pia sikujisajili na kuna mambo yalitokea mpaka nikahitajika kurudia darasa.
Nilikua nasoma shule binafsi ambayo nilikua nalipiwa na ndugu kwani wazazi wangu hawakua na pesa, basi nikashindwa kupata mtu wa kunisomesha tena, nilikaa nyumbani miaka miwili, ndipo nikapata cheti cha mtu, nikakitumia kuingia chuo cheti na kisha niakendelea mwenywe. Nilikua naumia sana kwani mimi nilikua na akili kuliko yeye, kazini nilikua napendwa, nilikua namzidi kila kitu lakini yeye alikua na maisha mazuri ila mimi naishi kwake tena kama mgeni.
Katika kumchukia na kwakua nilikua nabaki na mume wake mara nyingi kwani yeye anakua bize na kazi na mara nyingi anakua ni mtu wa kusafiri basi nilijitegeshea kwa shemeji yangu, tukajikuta tunaingia kwenye mahusiano. Mwanzo ilikua kama kawaida tu, kama utani utani lakini jinsi shemeji yangu alivyokua nanihudumia, ananijali nilijihisi kumpenda, nilimpa kila kitu ambacho najua mke wake hampi mpaka nikamchanganya. Alibadilika na kuanza kumchukia mke wake, kwakua walikua bado hawana mtoto basi wakawa wanagombana.
Kila siku mama anapiga simu anataka mjukuu, mume analalamika kuwa mwanamke yuko bize na kazi ndiyo maana ahazai yaani ni kugombana, shoga yangu akija ananiambia analalamika, analia namfariji lakini mwisho wa siku naishia kucheka tu kwani nilidhamiria kumchukua mume wake. Mahusiano yetu yalipamba moto na kwakua nilikua naongea sana na Mama yake tulishakua mashoga basi nilimuambia kuwa niko na mwanae.
Alifurahi sana na akaanza kulazimisha kuwa nilolewe kama mke wa pili. Kisukuma suala la kuoa mke wapili ni jambo la kawaid, hata kama mtu una ndoa ya kanisani lakini ukienda kutolewa mahari kimila basi unakua mke tu. Alifanya hivyo akanitolea mahari kimya kimya sasa nikawa naishi kwake kama mke. Mama mkwe aliniambia nisiondoke kwani huyo mwanamkie mwingina hajazaa hivyo nihakikishe nambebea muimba mwanae.
Maisha yaliendelea, rafiki yangu alihisi mume wake anchepuka, akawa ananihadithia, akanaiambia kuwa anatafuta tu ushahidi ili akadai talaka na kuond0. Baada ya kuona hivyo niliona kam ni fursa kwangu, sikutaka ajue kuwa mimi ndiyo natembea na mume wake, nilitaka ajue wakati nimeshabeba mimba na kujihakikishia kuwa mimi ndiyo mmiili wa mwanaume.
Nilienda na kusajili laini ya simu kwa kutumia kitambulisho cha mtu mwingine, nilibaki na ile laini, basi nikawa namtumia mwanaume picha za uchi, nampigai usiku, nabadilisha sauri naongea naye, nilikua namtumia rafiki yangu meseji za matusi, namtukana na kuweka status picha za mume wake, ilikua ni laini kwaajili yake hivyo sikujali sana. Kila nikifanya kituko wlaikua wanagombana na yeye alikua anakuja kuniambia mimi, mwanzo niliona kama itakua n rahisi, kwamba ataona picha za uchi tu na kukasirika akaondoka.
Lakini hakuondoka, yaani aliona picha zangu za uchi, akaona mesjei, nikamtukana, nikawa napiga usiku wamelala namsumbua lakini alivumilia. Hali hiyo ilinikera sana, nikawa nahangaika kubeba ujauzito lakini sikufanikiwa. Nilijua kuwa mimba pekee ndiyo itanifanya kubaki kwenye ile familai, Mama mkwe naye alikua ananisumbua kwanini simletei mjukuu.
Kuna kipindi mpaka nilihisi kama shoga yangu ananiloga kwani mimi nilikua na kizazi lakini sikuweza kuzaa. Wakati huo ndoa yao ilikua na kama miaka mitatu na nusu na walikua hawana mtoto, kila siku wanagombana na mimi mahusiano yetu yalikua na zaidi ya mwaka ila sijabeba mimba yake. Nilikua sina kazi na sikua natafuta, rafiki yangu alishanitafutia kazi mbili, lakini niliangalai maslahi yake na kwakua nilishajihidi mke basi sikutaka kuondoka.
Kila kazi aliyonitafutia nilitafuta sababu ya kuiacha ili kuendelea kubaki kwake. Alikua ananipenda sana na kwakua mimi ndioyo nilikua msahauri wake mkubwa basi alinisikiliza sana, hakua na marafiki wengi, ndoa yake ilikua na shida, wakwe zake wlaikua hawampendi, basi kila akiumizwa anakujakwangu, tunaongea anakua sawa hivyo hakuona hata sbabau za kunifukuza. Pia alipenda watoto na alimpenda mwanangu. Kla akisaifi ilikua ni laizma kumletea zawadi, alimpenda kama mtoto wake na mwanangu pia alimpenda.
Kuna wakati hata nilikua namuonea wivu sitaki awe karibu na mw3anangu kwani walikua wanapendana sana kana kwamba yeye ndiyo Mama yake. Kuna sikua likuja na kuniambia habari nzuri kwake nambaya kwangu, aliniambia kuwa amepima na ana ujauzito.
“Nimepima mara zaidi ya kumi, tangu mwezi uliopita napima lakini sikua na uhakika, nilitaka kuhakikiha ila sasa hivi nina uhakika kuwa nina mimba ya miezi miwili.” Aliniambia, nilionyesha kufurahi lakini kwangu ilikua ni kama mtu kanichoma na kisu kwneye moyo, nilijikuta naishiwa nguvu, napata kizunguzungu yaani, nililazimisha kucheka lakini kicheko hakikutoka.
“VIpi mbona hivyo?” Aliniuliza kwani alihisi kama sijafurajia, nilijikaza na kutabasamu.
“Tangu jana siko vizuri, najikaza lakini tumbo linauma.” Nilimdanganya.
“Ohhh! Pole, umekunywa dawa au nikupeleke hospitalini?” Aliniuliza, nilimjibu kuna dawa nimekunwa ili tu anyamaze.
“Shem anasemaje?” Nilimuuliza ili kujau kama ashamuambia au la, aliniambia bado hajamuambia, nilimuambia basia jipe muda kumuambia asubiri mpaka mimba ifikishe miezi minne. Sijui kwanini nilisema hivyo lakini nilikua sijajipanga, nilihisi kama akimuambia mume wake kuwa ana mimba basi anaweza niacha kwania likua na hamu sana ya mtoto.
“Kwanini nisimuambie, ni mume wangu anatakiwa kujua?” Aliniuliza kwa wasiwadi.
“Najua lakini hembu fikiria, ukimuambia lazima atamuambia Mam ayake, yule Mama hakupendi, na nafikiri hata sababu ya kuchelea kupata mimba ni wao wamekufunga. Kiketu hivyo vitu vipo, nilikua sijakuambia tu lakini nilihisi kuna hciho kitu, ukimuambia kuwa una mimba kabla haijafikisha miezi mitatu ni rahisi kuifunga usizae, lakini kimila zetu mimba ikishavuka meizi mitatu hakuna wakuifunga.
Usimuambie, jifanye hata kama ulikua hujui, ukifikisha miezi mine ndio utamuambia, nakuambia kwasababu najua sisi wasukuma tulivyo.” Nilimuambia maneno mengi ya kumjaza hofu mpaka akakubali, alikubali kutokumuambia Mume wake kuwa ana mimba. Kusema kweli kwa wakati huo nilikua sijui kama nitafanya nini lakini kitu pekee nilichokua na uhakika nacho nikuwa sitaruhusu wawe na furaha na mimi kuondoka kwenye ile nyumba.
Kichwa kilikua kinaniuma, nilijua kabisa kuwa kama rafiki yanguakisema kuwa anamimba basi nitaondolewa pala, pia nilijua kuwa, Mama mkwe pamoja na kumchukia rafiki yangu lakini alikua anataka mjukuu hivyo akisikia kuwa ana mimba angenichukia mimi kwani ni muda mrefu nilikua nataka mtoto bila kufanikiwa. Ilikua nilazima kumharibia rafiki yangu, kwakua alikua ananisikiliza sana niliamua kumtegeshea mwanaume.
Nilitaka mume wake kumfumania ili hata kama akisema kuwa ana mimba yake basi awe na mashaka kuwa mimba si yake hivyo kunipa mimi nafasi ya kuweza kubaki pale na kumbebea mimba mume wake. Siku moja nilikua na mtoko, nilimuambia rafiki yangu kunisindikiza kwani kuna mwanaume nilikua naenda kuonana naye, nilimuambia sijaingia kwenye mahusiano kwa muda mrefu na nilikua siamini wanaume sana, nilimuambia kuwa nahitaji yeye kuongozana na mimi ili nisijekufanya kosa la kuondoka na huyo mwanaume.
Kwakua ilikua ni mchana alikubali, nilikua na rafiki yangu wa kiume ambaye niliongea naye, lengo lilikua ni mimi kwenda na shoga yangu, kuonana naye kisha wapige picha pamoja na mimi kumpa namba ya mume wake amtumie zile picha. Alikubali kwani kulikua hakuna shida yoyote. Nilitoka na rafiki yangu mpaka sehemu tuliyopanga kuonana, mwanzo nilimuambia kuwa ni hotelini, lakini baadaye huyo mwanaume niliyepanga naye akanipigia simu na kuniambia kuwa anataka tuonane kwake.
Nilijifanya kwa rafiki yangu kuwa nina wasiwasi kwenda kwa mwanaume, nikajifanya kuhirisha, lakini yeye alinisisitiza twenda pamoja kwa madi kuwa, tukiwa wawili hawezi kunifanya chochote, niligoma sana lakinia linilazimishia kwani alikua akinionea huruma mimi kuwa peke yangu. nikajifanya kukubali kwa shingo upanda, basi tukaenda kwa yule mwanaume, akatukaribisha ndani kama kawaida, tukakaa na kuongea tu kama marafiki.
Wakati niko pale nilikua najisogeza sogeza, nilikua najifanya kusimama, kuangalia nvitu nakua huru flani huku nikichezea simu yangu. lego langu lilikua ni kupata picha ya pamoja kati ya rafiki yangu na yule mwanaume ili zikitumwa aonekane kama aliwahi kuwa pale. Kwakua mwanaume alikua anajua kilichokua kinaendelea alijisogeza sogeza, akijifanya labda anampa kitu, labda anaokota kitu ilimradi tu wawe karibu na mimi nikapata picha.
Baad aya kupata picha nilimuambia kuwa nataka kuondoka, lakini yeye alisisitiza kuwa tubaki, nilimuambia rafiki yangu tuondoke, lakini katika kunyanyuka ilikua shida, alikua hajisikii vizuri na baada ya muda alipatwa na usingizi. Nilimuuliza kamfanyia nini ndipo aliniambia kuwa, ili aaminike ni lazima wafanye wkeli, amtumie mume wake picha za uchi kabisa, hivyo alikua kamuweke dawa ili alale kabisa na kupoteza fahamu.
Aliniambia nimsaidie kumbeba mpaka chumbani, nilikataa lakinia liniambia kuwa kama hataki basi rafiki yangu akiamka anamuambia kila kitu. Sikua na namna nilikubali, tulimpeleka mpaka chumbani, akamvua nguo zote na kumpiga picha nyingi za uchi akiwa kitandani. Aliniambia kuwa nitoke kwani kuna kitu anataka kufanya, sikukubali kwani nilihisi kuwa anataka kumbaka, aliniambia kuwa hata kama sitaki basi yeye atafanya.
KISA HIKI nitakimalizia jioni, saa 11 chote kabisa, muendelezo wa Anna ni Kesho Mungu akipenda usikose, na ukitaka kisa kizima basi bonyeza hapa na follow huo ukurasa.
(ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA; Ninapoteza kazi, rafiki yangu ambaye anaishi na mume wake ndoa yake bado changa ananichukua kunisaidia, basi nakaa pale mpaka najifungua, naanza kumuonea wivu, naanisha mahusiano na mume wake.
Anapata ujauzito, ananiambia, nahisi kuwa mumewe akijua ataniacha, namuambia asimuambie mumewe kwanza, napanga na mwanaume ili wapige picha nimuonyeshe mume wake akiambiwa ajua mtoto si wake. Lakini mwanaume niliyepanga naye ananigauka, anamuingiza chumbani na kumvua nguo ananiambia nitoke nisione…” ENDELEA….)
Kweli alimuingilia kimwili rafikli yangu tena nikiwa palepale, rafiki yangu alikua hajielewi kabisa, alikua ampoteza fahamu, kuna wakati hata nilidhani kuwa amefariki. Nilishindwa kuvumilia nikatoka, alimbaka na baada ya kumaliza alimsafisha vizuri na kwa pamoja tukamlalisha nguo kama vile hakuna kitu kilichotokea. Lakini bado alikua hajapata fahamu, kwa wakati huo nilikua kama nimechanganyikiwa, yule Kaka liniambia tumpeleke hospitalini na kuwaambia kuwa amedondoka, na kwakua ni mjamzito basi kuzimia lilikua ni jambo la kawaida.
Kweli tulifanya hivyo, tukampeleka hospitalini ambapo tuliwaambia kwua ana mimba na alikua na kizunguzungu akadondoka na kupoteza fahamu. Lakini kabla hata hawajampa huduma ya kwanza alizinduka akiwa hospitalini, alianza kulalamika maumivu sehemu za siri lakini mimi nilisisitizia kuwa amedondoka kwakua ni mimba, walimpima na kukuta mtoto yuko salama.
Alibaki pale kwa uangalizi ndipo aliniambia kuwa hawezi kuficha tena, aliniambia anataka kumuambia mume wake. Nilimuambia kwa taarifa kama hizo basi asubiri mpaka atoke hospitalini ili waongee uso kwa uso. Alikubali, lengo langu lilikua ni kumuwahi kabla ya kuongea, nilitaka kuomngea na mume wake na kumuambia ukweli. Nilimuacha hositalini na kumpigia simu yule Kaka, nilimuambia amtumie picha mume wake, kweli alimtumia na kumuambia kuwa anatembea na mke wake na ana mimba yake.
Akamtukana sana akimuambia kuwa yeye hawezi kumap wmanamke unauzito na anataka waachane iliw ao waoane. Nilimuambia atume picha za kawaida lakini alituma mpaka picha za kitandani wakati anafanya mapenzi na mke wake. Baad aya kupata zile taarifa mume wake alinipigia simu, alitaka kuonana na mimi, tulikutana akaniuliza, mwanza nilijifanya kukataa lakini mwisho nilimuambia kuwa ni kweli ana mahusiano mengine kwakua aliona yeye hampi ujauzito ndipo maana akaenda kutafuta kwingine ujauzito unakaribia miezi mitatu lakini alikua hataki kumuambia kwania litaka kumucha kwanza.
Mwanaume alia kama mtoto, alilalamika, alionekana kumpenda sna make wake, alipaniki na kutaka kumfuata hospitalini lakini nilimuambia atulie kwanza. Asubiri mpaka mwanamke akitaka kumdanganya kuwa ana mimba yake ndipo amuambie na kumuonyesha hizo picha. Pamoja na kuumia sana lakini alikua ananisikiliza, alikubali na kuamua kukaa kimya bila kumuambia mke wake chochote.
Rafiki yangu alitoka hospitalini usiku, pamoja na kuwa vizuri laklini alikua analalamika maumivu sehemu za siri, kw3akua nilijua kabakwa nilimuambia hakuna kitu, ni sababu ya mimba na alidondoka, sikutaka kumuambia ukweli. Usiku ule ulipita, kesho yake ndipo aliamua kumuambia mume wake uikweli, alimuiambia kuwa ana mimba. Lakini mwanaume kusikia vile alianza kumpiga akimtukana na kumuambia kuwa yeye si mjinga kuweza kumsingizia mimba yake.
Rafiki yangu alikua haelewi chochote, alijaribu kujielezea kuwa yeye hajawahi kuchepuka ndipo mume wake alimuonyesha picha zake za uchi. Alimuonyesha akiwa kwenye ile nyumba na mwanaume mwingine, moja kwa moja alijua kuwa ni mimi kwani alikumbuka sebule. Alijaribu kujielezea na kunilaumu mimi lakini mume wake hakumsikiliza. Mume zilikua ni picha mbaya sana mabzo mtu yoyote asingeweza kumuamini.
Mwanaume alimuambia hamtaki, alimuambia kuhusu mimba lakini akamuonyesha mesjei kuwa ile mimba si yake. Alimpiga sana siku hiyo. Alimlazimisha kuondoka, pamoja na kujua kuwa mimi ndiyo nimemfanyia hivyo lakini Rachel hakuniambia kitu chochote. Alichukua nguo zake na kuondoka, hakuchukua kitu kingine chochote zaidi ya nguo tu, walichumba vitu vingi lakini hakuchukua, aliondoka.
Alipoondoka mume wake alimpigia simu mama yake, alimuambia kila kitu, Mama yake alikasirika na kumuambia kuwa ahakikishe kuwa anachukua talaka na kulienda mali wkani huyo mwanamke anaweza kumfilizi, alimuambia mambo mengi. Walikubaliana kubadilisha nyumba na kuandika majina ya Mama yake, wakati huo mimi nilikua naangalia tu, nisingeweza kuongea kitu chochote.
Rachel alirudi kwao, alijaribu kusuluhisha mambo lakini alipoona kuwa mume wake niko naye na nina mahusaiano naye alaicha. Vikao viliitwa lakini havikufikia muafaka, mwisho wa siku mwanaume alienda mahakamani kudai talaka. katika kipindi chote hicho Rachel hakuwahi kunitafuta, hakuwahi kuwaambia kitu chochote, hali hiyo iliniumiza kwani nilihisi kama anataka kunifanyia kitu kibaya.
Kwa upande wa mume wangu hatukua na shida, ingawa kila siku alikua akimzungumzia Rache, namna alivyomuumiza, jinsi alivyokua anampenda lakini sikuwaza sana, nilijua ni kipindi cha mpito tu na baada ya muda atakua sawa.
Sikumoja nikiwa nyumbani alinipigia simu Rafiki yetu mmoja, hakua anajua kilichotokea, alikua anajia naishi na Rachel lakini alikua hajui sababu za Rachel kuachana na mume wake, wala alikua hajui kama mimi bado naishi pale baada ya yeye kuondoka. Alinipigia simu tukaongea sana, ndipo aliniuliza kuwa niko wapi? nilimuambia kuwa nipo nyumbani, sikumuambia nyumbani wapi, sikutaka watu wajue mambo yangu.
“HIvi ni kweli shoga yetu kaathirika, maana nasikia mume wake kamuacha sababu hiyo, eti ana mimba ya mwanaume mwingine na ana UKIMWI wameima yeye anao ila mume hana kamtimua.” Aliniukuza kutaka umbea kwakua alijua mimi naishi naye alihisi najua kila kitu. Ingawa nilikua najua sababu ya kuondoka kwa mume wake lakini sikutaka kumuambia, sikutaka kuonekana namsaliti rafiki yangu kwani kila mtu alikua anajua namna alivyonisaliti. Nilimuambia si kweli kisha nikakata simu.
Lakini kusikia suala la ukimwi nilipata wasiwasi, nilipata wasiwasi kwakua mimi nilikua natembea na mume wake hivyo kama anao basi na mimi ninao. Jioni niliamua kuongea na mume wangu, na kumuuliza kuhusu kupima, nilimuambia kuwa kwkaua Rachel alikua anamsaliti ni muhimu tukapima na kujua afya zetu, hakubisha, siku iliyofuata tulipima sehemu kama tatu hivi tukakutwa sala,a hapo niikua na amani, lakini sikutulia, nilitaka kujua ukweli kuhusu Rache, nilitaka kujua je kama ana UKIMWI kweli au ni watu wanasambaza.
Nilikua namjua rafiki yangu kuwa si malaya hivyo nilijua kama kweli kaathirika basi itatoka kwa yule Kaka, nilikumbuka kuwa siku ile wakati anafanya naye mapenzi hakutumia kinga. Nilimtafuta yule kaka na kumuumiza, bila aibu alinijibu kuwa yeye ni muathirika mud amrefu na hatumii vidonge kwani anataka kaumbukiza watu kama yeye alivyoambukizwa. Nguvu ziliniishia, nilijihisi kuchoka, nilijihisi kuchanganyikiwa, ingawa nilikua namtaka mume wake, namuonea wivu lakini sikua tayari kumuua.
Nilitamani kumtafuta, kumuopmba msamaha na kumuambia kuwa ni shetani lakini niliogopa. Niliamua kumfuatilia, kwakau alikua mjamzito ilikua rahisi juua pakumpata, nilifuatilia hospitaini kweli nikagundua kuwa anaenda kliniki na nilifuatilia kwa manesi tu ambao hata hawakua marafiki zangu lakini nilitengeneza ushoga na kutoa vihela nikaambiwa kweli kuwa alikua ni muathirika.
Niliumia sana kwani Rachel hakunifanyia kitu chochote kibaya, nilianza kujutia mambo yote mabyo nilimfanyia, lakini wakati huo sikua na namna. Ilikua ni lazima kuendelea na maisha yangu, nilijitahidi sana kutafuta ujauzito lakini sikuupata. Wakati nachunguza kumbe sikua peke yangu, mume wake naye alichunguza na kama mimi akajua kuwa Rachel ameathirika, alianza mchakato wa talaka, hata watu walipotaka kuwasuluhisha aligoma kabisa.
Mchakato wa talaka haukuchukua muda mrefu, walikubaliana ili kuepusha kudhalilishwa kwakua mume wake alikua na picha zake za uchi alikubali kutoa talaka. Tofauti na ndoa nyingine za kikristo ambazo talaka huweza kuchukua miaka kwao ilichukua miezi mitatu tu. Katika kuachana Rachel alimuachia kila kitu mume wake, ingaw awlaijenga nyumba pamoja an walikua na miradi mingine lakini mume wake hakumuachia kitu chochote.
Si kama hakutaka, ingawa walijenga pamoja lakini mume wake alimtishia kuwa kama akidai mali mahakamani basi atasambaza picha zake za uchi, alikua na hasira sana kwa kudanganywa. Basi alikubali kumuachia mume wake kila kitu, baada tu ya talaka hakukaa muda akajifungua mtoto wa kiume. Lakini wakati anajifungua kwa bahati mbaya alifariki, alijifungua kwa uapsuaji na damu zilimtoka nyingi, Rachel alifariki hata kabla ya kumuona mtoto wake.
Mume wake alipigiwa simu na kuambiwa kuhusu mkewe, alijifanya kutokujali, akawaambia kuwa alishamuacha na hata mtoto si mtoto wake. Hakujali chochote, mimi nilitamani sana kwenda kwenye msiba lakini nilihofia macho ya ndugu zake, nilijua kuwa wanajua kila kitu, nilishindwa kwenda msibani. Nilizima simu zangu kabisa kwani sikutaka mtu kujua kama nina taarifa lakini sikuweza kwenda.
Maisha yaliendelea, nilikua mke kamili na kwa muda mimi na mume wangu tulisahau kuhusu Rachel, Mungu alibariki nikapata ujauzito, yaani mambo hapo yalikua mazuiuri, mapenzi yalizidi, wakati ujauzito wangu ukiwa na miezi saba, mwaka mmoja hivi baad aya Rachel kujifungua na kufariki dunia nikiwa mjini nazunguka na mume wangu tumeongozana na mimba yangu nilikuatana na Dada na Mama yake Rachel.
Walikua wananifahamu wote kwani hata kwao nilishawahi kuishi kwa muda. Waliponiona wakati mimi naona aibu wao walinichangamkia, wakanisalimia vizuri, lakini waliana kwa kunipa pole.
“Rafiki yako amefariki, najua mlikua mnapendana sana lakini hatukua na namna ya kukupata, sijui kama ulikua unajua…” Mama yake aliniambia huki akinikumbatia, alikua ananipa pole kana kwmaba ni mimi nimefiwa, aliniomba smamaha kwa kushidnwa kuniambia lakini waliniambia kuwa wlaipaniki hata hawkaukumbuka.
Nilijikuta naanza kulia, nilikua nalia si kwasababu ya msiba lakini kwasababu ya upendo, sikuamini kuwa Rachel kwa yote niliyomfanyia hakumuambia Mama yake au Dad ayake ambaye alikua anamuambia kila kitu. Wakati nakutana nao, nasalimiana nao mume wangu alikua akipaki gari vizuri, hawkaumuona, ila baadaye akuja kuungana na mimi, ndipo walimuona, walishangaa kumuona pale, wala hawkaujua kama tuko pamoja.
Alipokuja ingawa kwa kupoteza uchangamfu walimsalimia, mume wangu alishikwa na butwaa, alishidnwa hata kuitikia kwani mabli na kwamba hakuenda kwenye msiba wa mke wake lakini alikua hajwahai kuwasiliana na ile familia, yaani hata hakuwahi kumuonna mtoto ambaye alikua anaamini si wake. Lakini wakati tumesimama mdogo wake na Rachel wakiume alikuja, alikua amembeba mtoto, ambaye kwa kumuangalia tu usineguliza alikua ni mtoto wa naani.
Alikua ni mtoto wa Rachel na kwa kumuangalia alikua ni kopi kabisa ya baba yake, yaani walifanana kila kitu. Kitu cha kushangaza zaidi, alikua akabebwa na mjomba wake lakini baada tu ya kufika pale,a lilazimisha kushiuka, akamkimbilia Baba yake, akamshika miguu, akamkumbatia kwa nguvu, dakika tano nzima alikua kamkumbatia miguu, kamganda kamshika kama sumaku hamuachii.
Kila mmoja alibaki kimya haongei chochote wanamuangalia yule mtoto, mume wangu hakua na namna alimchukua na kumbeba, mtoto alimuangalia usoni baba yake, alimuangalia kama mtu anayesoma ramani. Mume wangu alsihidwa kuvumilai na kuanza kulia, alilia sana, alishindwa kitu cha kusema.
Bibi wa mtoto alitaka kuja kumchukua mtoto lakini haikua hivyo, mtoto aligoma, walipotaka kumchukua aligoma na kumkumbatia. Tulikaa pale zaidi ya nusu saa tunaangaliana, ndipo walilazimishia na kumchukua mtoto. Waliondoka na kutuacha pale, mume wangua likua analia kiasi cha kushindwa kuingia kununua vitu, alirudi kwenye gari na kuanza kulia kwenye usukani. Niliingia kumbembeleza lakini alibailika ghafla, aliniangalia usoni na kuniambia.
“Niambie ukweli, hivi kweli Rachel alinisaliti?” Aliniuliza, si wawlai ambalo nililitegemea, nilimuangalia usoni na kumdanganya na kumuambia ni kweli alikusaliti.
“Lakini kama alijua ana mimba yangu alikua na haja gani ya kupiga picha, alikua na haja gani, si angebeba tu…” Aliuliza maswali mengi bila majibu, alinigeukia tena na kuniambia nimuambie ukwlei, alilazimishia sana mwisho nikashindwa, alikua na maswali magumu, mwisho nilimuambia kuwa hakumsaliti nililazikika kumuambia ukweli nilijua kwakua rachel alishafariki basi hawezi fanya chochote.
Sikumuambia ukweli wote, nilimuambia kuwa racel hakumsaliti lakini mwanaume aliyempiga picha alikua ni rafiki yake wa kawaida ambye alikua anamtaka. Hakuelewa hiyo stori, alilazimishia kujua ukweli kwani wakati wanaachana aklimuambia kuwa ni mimi nilihusika na kumuambia jinsi nilivyomdanganya.
Sikua na namna zaidi ya kukubali, nilimuomba msamaha sana na kumuambia kuwa nilifanya yote hayo kwakua nampenda na sikutaka kumpoteza. Aliniambia kufunga mkanda na tuondoke, hakusema kitu, inagwa nilijaribu kumuomba samaha lakinia liniambia kuwa nimuache kwani ana hasira sana. Aliendesha gari kwa kasi, tulifika sehemu kwa makusudi akaenda kuligongesha gari kwenye nguzo, wakati anagongesha niliona kabisa kuwa analenga upande wangu, lakini haikua hivyo, ilimshinda na ikagonga zaidi upande wake.
Mume wangu alifia palepale, mimi niliumia sana, lakini wka bahari nzuri nilipona, kwa bahati mabya mimba ilitoka. Ndugu wa mume wangu alipoona mtoto wao kafariki, mimba imetoka walinifukuza hivyo nikalazimika kurudi kijijini. Sasa hivi nipo tu nyumbani, kila ninachogusa hakifanikiwi, ninaumia sana kwani najua nilikosea, kila wakati najaribu kumlaumu shetani lakini hapana, hakua shetania liyyenipitia bali wivu ndiyo umenifikisha hapa, sijui kama nitakuja kusamehewa ila naamini siku moja nitakutana na Rachel na atanisamehe.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment