IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO
MINA; NITAJIUA SIKU YANGU YA KUZALIWA IKIFIKA ILI WASHEREHEKEE VIZURI
“Kaka najua utaratibu wako ni mpaka ununue Kitabu, ila mimi kama ni hiyo elifu kumi nitakupa, lakini naomba uongee na huyu mtu maana simjui ila nahisi kuna kitu kibaya, naomba uongee naye, nimemuambia wewe ni saktari nahisi kuna kitu kibaya anataka kukifanya, amekuja kununua dawa nimemuambia wewe utamsaidia namna ya kuzitumia, nakata ila nakupigia nikiwa naye uongee naye.”
JOIN US ON TELEGRAM
Alinipigia simu Dada mmoja ambaye alikua akiongea kwa kunong’ona. Nilishtuka kidogo aliponiambia kuwa anataka kununua dawa. Mara nyingi kuna watu wananipigia bila kununia vitabu vyangu na kudai kuwa wana maumivu makubwa, ila ukiwasikiliza unakuta kaiba mume wa rafiki yake na hamhudumii amekasirika. Lakini huyu nilihisi kuna kitu, nilimuambia hakuna haja ya kulipia anipigie akiwa naye.
“Ongea naye huyu hapa.” Aliniambia huyo Dada wa duka la dawa ambaye mpaka sasa hivi hata sijui kuwa ni nani?
“Haloo Doctor” nilisikia sauti laini ambayo kwa akili ya kawaida nilijua ni ya binti wa miaka 22 kama sio 23. Alinisalimia na kukaa kimya, ikawa kazi kwangu kumuuliza kama ana tatizo gani. Kabla hata yakunijibu alianza kulia. Hapo nilijua kazi imeanza kwakua naogopa sana machozi, najikuta nakua na huruma na mara nyingi mteja akilia nashindwa kuongea naye vizuri maana badala ya kumuambia ukweli basi najikuta naogopa naanza kazi ya kumtia moyo.
“Natamani kufa Doctor….” Alianza kuniambia huku akilia, hatukua tukiongelea tena kuhusu dawa bali alianza kunipoa stori yake.
“Kaka nina mika 32, nimetoka kuachana na mpenzi wangu, ameniambia tu hanitaki, ameniambia akibaki na mimi atanitesa, kaka nitakua ni mtu wa kuachwa mpaka lini, nimechoka, nahisi tu kufa….” Aliendelea kuniambia.
“Mlikua kwenye mahusiano kwa muda gani?” Nilimuuliza, alinyamaza na kusira kidogo kama vile anahesabu, nilidhani ni mtu aliyekaa naye kwenye mahusiano kwa muda mrefu mpaka anaona kama kapotezewa muda lakini haikua hivyo.
“Kaka nina kama miezi miwili sasa, tulishapanga mambo mengi Kaka….” Natamani kushangaa kuwa miezi miwilianataka kujiua kwaajili ya mwanaume ila nimeshaohna mengi. Naamua kunyamaza na kuendelea kusikiliza.
Nikidhani laba natamzungumzia huyu mwanaume labda kuna kitu kamfanyia lakini hapana, stori inakua nyingine kabisa. “Kaka, mimi ni Binti wa pili katika familia yetu, kwetu tuko wa tano, wakwanza ni Dada yangu ambaye kaolewa, anafuatia Kaka yangu, Mimi, halafu kuna wadogo zangu wawili, wote ni wakike, mmoja ana miaka 28, na ameolewa na mwingine ana miaka 35 ndoa yeke ni mwezi wa sita mwaka huu.
Ashatolewa mahari na kila kjitu kimekamilika. Kaka najihisi kama vile nina mkosi, sijawahi kuwa kwenye mahusiano ya maana hata siku moja. Kwanza siwezi kusema kama nimeshawahi kuwa kwenye mahusiano, labda nianzie nikiwa chuo Kaka ili uone jinsi nilivyo na bahati mbaya. Niliingia chuo nikiwa na miaka 19, nilikua mdogo na nimekuja kumaliza chuo na miaka 22 kasoro.
Katika kipindi chote cha miaka mitano chuoni sikuwahi kutyongozwa na mwanaume yoyote. Kaka najihisi nina gundu, mimi ni mzuri, si ile sana ila hata ukiniona unaweza kunitamani, naona marafiki zangu wengine nimewazidi uzuri lakini walikua na mahusiano na wana furaha. Mimi haikua hivyo, sikuwahi kutongozwa na mwanaume yoyote, nilikua na marafiki wakiume lakini hakuna hata mmoja aliwahi kunitongoza.
Nakumbuka nikiwa chuo mwaka wa tatu kulikua na Kaka mmoja ambaye alionekana kunipenda. Hakua na muonekanao mzuri lakini kwakua sikua na mpenzi na mimi nilitamani sana kuwa kwenye mahusiano kupata ile raha ya kuwa na Boyfriend basi nilijikuta nakua naye karibu, nilipenda kuonenana naye karibu na mara nyingi kwakua mimi nilikua napata Boom na pia ndugu zangu wananipa hela basi nilikua na pesa.
Nilipenda kumtoa out, kuongozana naye na kutengeneza mazingira ambayo kila mtu akiniona naye alidhani kuwa ni mpenzi wangu. Rafiki zangu walianza kuniuliza kuhusu huyo Kaka, sikuwaambia kama ndiyo mpenzi wangu lakini nilijichekesha chekesha ili wajue kuwa ni mtu wangu. Basi walikua wananiambia tunaendana, wananisifiasifia, nilijua ni sifa za kinafiki lakini huwezi amini kaka nilikua nikijisikia raha kuona kama na mimi nilikua na mtu.
Sio kama nilikua sijawhai kufanya tendo la ndoa, au labda tendo la ndoa nilikua nalitamani kihivyo, hapana, nilishawahi kufanya nikiwa kidato cha nne lakini ilikua ni ile ya kitotototo. Tangu kujitambua vizuri kama mwanamke nilikua sijawahi. Lakini kwangu kikubwa halikua ni tendo la ndoa bali ilikua ni ile kuonekana nina mtu, ile hali ya kuwa na mtu wa kuchart naye, kuongea naye, kula naye pamoja ilikua inaniumiza.
Huyu Kaka nilimuona kama mkombozi wangu, alipoanza kuwa karibu yangu basi niliona hata wanaume wengine nao walikua wakija kwangu, kuniongelesha kama mwanamke na hata kunitongoza. Nilikua naye karibu sana lakini hakunitongoza, alikua ananijali kama mpenzi wake lakini hakuna hata siku moja aliniambia kuwa ananipenda au anataka kuwa kwenye mahusiano na mimi.
Nilijisikia raha, nilijiona kama mwanamke kuwa naye karibu. Nakumbuka siku moja ilikua ni siku yangu ya kuzaliwa, nilitaka iwe spesho kuliko siku nyingine, kwa kawaida nilikua nikiiona rafiki zangu wanafanyiwa visherehe, surprise hata kama ndi ndogo lakini wanafanyiwa na wapenzi wao. Hata mimi nilitamani kitu kama hicho, lakini ningefanyaje, sikua na mpenzi wa kunifanyia.
Niliwaza kuhusu yule Kaka, ingawa alikua hajawahi kunitongoza lakini si alikua anajifanya kama mpenzi wangu. Hakua akijua kama ni siku yangu ya kuzaliwa, lakini kwakua muda mwingi tulikua pamoja tukisoma pamoja basi nilijiongelesha mpaka nikajua.
“Nataka siku yangu ya kuzaliwa iwe tofauti, sijui nitafanya kitu gani, hembu niambie kama ni wewe ungefanya kitu gani special?” Nilimuuliza kama swali lakini ndiyo nilikua nampa taarifa kuwa ni siku yangu ya kuzaliwa hivyo anifanyie chochote.
Tofauti na nilivyotegemea niliona kama yeye kafurahia, aliniuliza ni siku ganio nikamuambia.
“Fanya kitu kidogo, fanya na marafiki zako wachache, kama una hela watoe sehemu, kwenye kahotali, kunywa na vitu kama hivyo….” Aliniambia huku akinipa plan nzima, alijua pesa ninazo hivyo alichagua sehemu nzuri. Mimi nilijifanya kama sijui chochote kuhusu sherehe, nikamuomba nimpe pesa ili yeye ndiyo asimamie kila kitu.
Kweli alikubali, aliniambia kwakua ni siku yangu ya kuzaliwa basi nisihangaike yeye atafanya kila kitu kuandaa sherehe na kualika watu mimi atanisuprise tu. Aisee hakuna raha ambayo nilisikia kama siku hiyo, kwa namna aliv yoongea na alivyokua kajiandaa kunisaidia katika hiyo sherehe nilihisi kupendwa. Ingawa wazo la sherehe nilitoa mimi, pesa nilitoa mimi lakini nilijipa moyo nikiamini kuwa, yeye kuamua kuifanya ni kwa mapenzi.
Nilimpa pesa na kumuacha afanye kila kitu, sikumuuliza kitu chochote, hata marafiki zangu sikuwaambia kitu mpaka siku ya sherehe, kama inavyokua kwa wengine nilijifanya sijui kitu. Rafiki yangu akaniambia tutoke wakanisuprize na kweli ilitokea hivyo. Nilijisikia sana kuwa na mimi nilifanyiwa sherehe na mpenzi wangu, nilijiongeza na kujiona nina bahati.
Baada ya sherehe tulirudi chumbani, nilikua nimepanga nnje ya chuo nikiishi na rafiki yangu ambaye alishakua kama Dada yangu. yeye alikua na mpenzi wake ambaye si mwanafunzi, baada tu ya kunifikisha aliniambia kuwa mpenzi wake kampigia simu na kumuambia kuwa anatakiwa kuonana naye.
Tulikua tumechukua Tax hivyo kw auoga yule Kaka ambaye nilimuona kama mpenzi wangu aliniambia kuwa amsindikize kwakua ni usiku. Kusema kweli nilijisikia vibaya kwani siku hiyo niliamini kuwa yule Kaka atanitongoza, hata kama tusingelala naye lakini atanitongoza, kwajinsi alivyokua ameandaa siku yangu ya kuzaliwa niliona kabisa kuwa ananipenda na kuna kitu ataniambia.
Ilikua ni usiku na nilitegemea baada ya kutufikisha basi angeniita pembeni na kuniambia kitu ila haikua hivyo, alikua anamsindikiza rafiki yangu. Waliondoka na kuniacha peke yangu, usiku huo sikulala, ilipofika saa saba hivi za usiku bado nilikua macho. Simu yangu iliita, alikua ni yule Kaka, niliipokea harakaharaka nikiamini kuwa naye alikua kashindwa kulala kwakunikumbuka hivyo tunaenda kuwa pamoja.
Niliipokea harakaharaka, aliniuliza kama nilikua nimelala nikamuambia hapana, aliniomba kuonana naye usiku uleule kwani kuna kitu cha muhimu alikua nataaka kuniambia. Nilijifanya kukataa kataa nikisingizia usiku lakini alilazimishia sana, kwakua ndiyo kitu nilikua nikikitaka basi nilikubali nikatoka nnje na alikuja kunichukua.
Hata yeye alikua kapangisha chumba off campus, jirani kidogo na kwetu. Tuliongozana mpaka chumbani kwake, alikua akiishi na rafiki yake, nilijua kuwa kama iluivyokawaida kuwa mwanaume akiwa na mwanamke wake basi humuambia rafiki yaka kumpisha nilijua kabisa kuwa siku hiyo rafiki yake hatakuepo. Nilishangaa kukuta rafiki yake yuko ndani, nilijisikia vibaya sana kwani niliona kama vile hatutaweza kufanya kitu chochote.
Lakini sikua na namna, niliingia nikakaa huku nikiamini kuwa rafiki yake atatoka tu. Lakini baada ya kukaa tu yule Kaka ambaye mimi ndiyo nilikua nampenda alitoka kama anaenda kuchukau kitu nnje lakini hakurudi. Dakika kama kumi hivi nikaona kimya ndipo nilianza kushtuka, nikasema kuna kitu haopa, huyo rafiki yake aliyekua akiishi naye chumba kimoja nilikua namfahamu tunaonana lakini hatkua marafiki.
Naye alinyanyuka na kwenda kufunga mpango, nilihisi kuna kitu kibaya, kengele ya hatari ililia, nikasema hapana, hapa lazima kuna kitu, kwanini afunge mpango. Nilinyanyuka na kutaka kuondoka lakini alinishika na kunikalisha chini.
“Mbona unataka kuondoka?” Aliuliza kwa dharau flani, nilimjibbu vizuri kuwa ni usiku nataka kurudi chumbani kwangu lakini alinizuia.
“Chumbani kwako ukafanye nini wakati Amani (Yule Kaka niliyekua nampenda ila si jina lake halisi) yulo na Scholar kule (Rafiki yangu, si jina lake halisi).”
“Unamaanisha nini?” Nilimuuliza huku nikinyanyuka tena na kulazimishia kuondoka.
“Namaanisha kuwa rafiki yako alikua hapa, walikua wanataka niwaachie chumba wafanye mapenzi, lakini nikawaambia kuwa mimi sina mtu siwezi kutoka. Ndipo scholar akasema kuwa anaweza kuniunganisha kwako kwakua wewe huna mwanaume huwezi kukataa….” Aliniambia huku akinishika na kutaka kiunikuambatia, nilimsukuma pembeni kwa hasira.
“Unamaanisha nini?” Nilimuuliza, alionekana kuwa mkali sana, alinusukumiza na kunibana chini kisha akaniambia kwa dharau.
“Mbona unaringa wakati mimi nakusaidia, rafiki yako ameniambia hujawhai kuto*** wanaume wanakukimbia, acha kupiga kelele umejileta mwenyewe!” Aliongea maneno mengi, namna ambav yo rafiki zangu wlaikua wakinitangaza kuwa mimi nina gundu, sijawahi kuwa na mwanaume na wanahisi kuwa mimi nina laana au ugonjwa flani.
Kwajinsi alivyokua anaongea ilionekana Scholar alikua kanichafua sana. Nilijisikia vibaya, nikajikuta napandwa na hasira, yeye bado alikua ananilazimishia kufanya mapenzi na mimi ila mimi sikukataa.
“Piga kelele kila mtu aje, useme nimekubaka wakati umekuja mwenyewe chumbani kwangu. Halafu ulivyombaya namna hiyo nani atakuamini kuwa umebakwa na mkaka kama mimi. Ninawanawake wengi, wazuri mara mia kuliko wewe unafikiri kuna mtu ataamini kuwa mimi naweza kubaka Kinyago kama wewe!”
Hapo ni kama alikua kashanidhibiti, si kwa kutumia nguvu bali kwa kutumia maneno yake tu, nilijiona sina nguvu, nikajiona kama takataka flani, nikajikuta namuachia afanye anachokitaka. Kweli alilazimishia na kufanya mapenzi na mimi usiku huo. Sikusikia raha yoyote ile alifanye yeye mpaka akamaliza. Nilitaka kuondoka usiku uleule lakini alinikatalia kwa madai kuwa Amani atakasirika kwakua “Alinipa wewe kama zawadi ili yeye akatembee na rafiki yako halafu uende kuwaharibia!”
Sikutaka kukasirika, sikutaka kumuamini, kweli niamini kuwa Amani anaweza kunifanyia kitu kama hicho. Hapana,ni lazima huyu mbuzi atakua ananidanganya. Niliwaza huku nikitoka kurudi chumbani kwangu. Chumba nilichokua nikiishi na rafiki yangu kilikua ni chumba cha nnje. Kwa maana kuwa, kulikua na nyumba kubwa halafu na vyomba vya uani ambavyo wengi waliokua wamapangisha ni wanafunzi.
Ilikua ni usiku lakini si kila mtu alikua amelala, kuna watu bado walikua wanasoma kwani niliona taa nyingi zikiwa zimewashwa. Nilienda mpaka chumbani kwangu na kugonga, mlango haukufunguliwa, ulikua umefungwa, nilikua na funguo na ilikua ni kawaida yetu mtu akiingia anatoa funguo ili mwenzake kama katoka labda kwenda kusoma akirudi asimsumbue. Niliingiza ufunguo kujaribu na kweli usiku huo Scholar alitoa ufungu.
Nilifungua mlango na kuingia ndani, kulikua kimya mpaka nikahisi hakuna mtu. Niliwasha taa ndipo walishtuka, rafiki yangu alikua amelala uchi wa mnyama na mwanaume niliyekua nampenda. Walinyanyuka huku wakiwa bado na wenge la usingizi. Walishangaa kuniona pale, nilitamani kutoka kukimbia lakini minguu haikunyanyuka, nilijisikia kama vile nimepigiliwa misumari kwenye miguu.
“Vipi umerudi, Jamaa hajakupenda?” Amani aliniuliza, swali lake moja kwa moja liliniambia kila kitu nilichokua nimesikia kutoka kwa rafiki yake. Walikua wamepanga kunitoa mimi sadaka.
“Vipi shoga yangu,mbona kimya au hujampenda, si ulikua unalalamika mwanaume, nimekupa yule mbona umerudi….” Scholar aliniuliza, hakuhangaika hata kujifunika, yeye na Amani waliendelea kubaki uchi huku akiniongelesha kwa kejeli.
Kwa namna walivyokua wanaongea ni kama watu waliokua wananisaidia, walijiona kama wamefanya kitu kizuri.
“Sasa utalala wapi, sisi bado hatujamaliza.” Amani aliniambia huku akimshika rafiki yangu na kukumbatiana, walianza kufanya mapenzi mbele yangu.
AMINA; NITAJIUA SIKU YANGU YA KUZALIWA IKIFIKA ILI WASHEREHEKEE VIZURI—SEHEMU YA PILI
Maumivu niliyoyasikia miguu ilinyanyuka na kutoka nnje. Nilimuaha rafiki yangu akifanya mapenzi na mwanaume niliyekua nikimpenda na ambaye niliamini ataniondolea aibu ya kutokuwa na mwanaume tena. Nilijisikia vibaya sana huku nikiwaza, hivi scholar kakosa nini? Mbona ana wanaume wengi sana wanampenda, inamaana kashindwa kuniachia hata huyu mmoja?
Nilishindwa kwenda mbali, nilibaki pembeni kidogo ya nyuma niikakalia msingi mpaka subuhi, Amani alitoka na kunikuta pale nnje. Hakusema kitu aliondoka, nilirudi chumbani na kumkuta Scholar kalala, nilijiandaa, nikaingia bafuni kuoga kisha nikatoka na kumkuta ndiyo anaamka.
“Vipi jana ulienda wapi tena? Niambie shoga yangu, nilikutafutia mwanaume yule Kaka ni malaya lakini ndiyo mambo ya chuo, niambie kila kitu, ilikuaje? Mlifanya, Amani kanitumia meseji anasema jamaa anakusifia, ni kweli….” Aliongea kishakunaku, kama mtu anayetaka kujua, kama vile ulimuaga rafiki yako kuwa unaenda kuonana na mpenzi wako kwa mara ya kwanza hivyo anakua anataka majibu, anataka kujua mambo yalikuaje.
Nilikua najisikia vibaya, aibu, nasikia kichefu chefu lakini sikua na namna, sikutaka kuongea sana. Sijui ni kwanini lakini sikutaka kuonekana mjinga, sikutaka kuonekana kama nimebakwa au nililazimishwa.
“Ilikua poa…” Nilimuambia kisha nikatoka zangu, sikujua naenda wapi lakini nilihisi kuchanganyukiwa. Kwa mara ya kwanza nilijiona kama nina mikosi na nilitamani sana kujiua.
Niliingia darasani nikiwa na wasiwasi sana, nilikua na mawazo ni kitu gani kitatokea, mwanaume niliyekua nikimpenda alikua hanioni kama mpenzi wake.
“Nina shida ya elifu kumi….” Amani aliniambia, ilikua ni siku ya pili baada ya lile tukio, tulipoonana alionekana kutokujali, wakati mimi nilikua na maumivu makali yeye alionekana kama hajafanya kitu chochote. Yeye na rafiki yake walikua wakiongea na mimi kama vile hakuna kitu kilichotokea, yaani kwao ilikua ni ikama utani.
”Mimi sina pesa na hata kama ningekua nazo nisingeweza kukupa!” Nilimjibu kwa hasira, mimi nilikua nimetangulia yeye ananifuata kwa nyuma, alisimama kidogo kwa hasira na kutaka kugeuka kuondoka, kuna kitu kiliniambia hapana, huwezi kumuacha hivi hivi, yaani mtu kakudhalilisha namna hiyo halafu umuache, hapana!”
Niliwaza, bila kujijua nilijikuta nageuka, nilimfuata na kuanza kumshika kama vile nataka kumpiga.
“Hivi wewe njdiyo wa kunifanyia hivyo, mimi nilijua kuwa wewe ni rafiki yangu kumbe unaenda kuniuza kwa rafiki yako….” Niliongwa wka hasira lakini nilishindwa kumalizia, machozi yalianza kunitoka, hnikajikuta natetemeaka kama nimemwagiwa maji ya baridi.
“Una nini wewe mjinga, ulitaka nini? Mimi nilikua karibu yako ili kumpata rafiki yako, hivi unafikiri nilikua nakupenda! Nimekuona muda mrefu unajiletaleta kwangu, tena shukuru sana rafiki yangu amekugonga, unafikiri ni mwanaune gani angekupenda! Niache, unanishika hivyo wewe kama nani? Hivi unanionaje, unafikiri naweza kutembea na kinyago kama wewe! Mjinga kabisa, ondoka hapa!”
Amani alinisukuma kwa nguvu, alizidi kunitukana mpaka watu wakaingilia, niliondoka pale nikiwa naa ibu sana, nilishaharibu mambo. Wakati naondoka nilimsikia akiwalezea watu, kila mtu aliyekua anakuja kumuuliza kwanini tulikua tunagombana alikua akimuelezea, nilijisikia vibaya, nikakimbilia mpaka chumbani kwangu na kujifungia.
Siku iliyofuata kila mtu alikua anajua, ilikua nin habari ambayo ilisambaa haraka. Ukiniangalia mimi kua sikuwahi kuwa na mwanaume nilionekana kama vile ni kituko. Sikuwahi kuwa na mahusiano tena mpaka nilipomaliza chuo, maisha yangu ya chuo yalikua ni ya shida, nililazimika kuendelea kukaa chumba kimoja na rafiki yangu ambaye alinichukulia mwanaume.
Si kama sikua na uwezo wa kuhama, hapana, nilikua na uwezo wa kuhama na hata kuishi peke yangu. lakini nililazimika kubaki naye kwani kila mtu alinitenga, hakukua na mtu hata mmoja ambaye alikua tayari kuishi na mimi. Nilijitahidi sana kufanya vizuri darasani ili watu wanipenda lakini hakukua na mtu ahta mmoja alinipenda kwa dharai.
Wengi waliokua wanakuja kwangu walitaka niwasaidie kitu flani, iwe ni pesa au darasani kimasmomo. Nilimaliza chuo kwa ufaulu wa juu kuliko mwanafunzi yoyote lakini sikua na amani, sikua na furaha kwani nilikua najiona kama takataka. Tofauti na wenzangu ambao wakimaliza vyuo inakua shid asana kupata kazi lakini mimi nilifanikiwa kuapata kazi hata bila cheti.
Tena serikalini, nilipata kazi katika taasisi moja kubwa tu kwa kutumia Transcpt. Niliingia kazini nikiwa na matumaini makubwa, nikiamini huko labda mambo yatakua toafuti, labda kwakua nitakutana na watu wazima basi watanichukulia vizuri.
Kweli mambo yalikua mazuri kidogo. Nilikutana na Kaka mmoja, yeye alikua ni injinia, nilipofika tu hata sijamaliza wiki alitaka kuwa karibu na mimi. Kwangu hicho kilikua ni kitu kipya kabisa kwani sikuwahi kutongozwa na mwanaume hasa ikizingatia kuwa, pale ofisini kulikua na wadada wengi tena wazuri kuliko mimi pia kuna ambao niliajiri8wa nao, wao pia walikua ni wazuri.
Sikuamini kabisa kama ananipenda, nilihisi kama utani flani, lakini mwezi mmoja baadaya tulikua kwenye mahusiano. Erick alikua ni kijana mtanashati, ana maisha yake, alikua kazini muda mrefu hivyo alikua na pesa. Miezi mitatu ya kwanza tulikua bado hatujaingiziwa mshaghara, yeye ndiyo alikua akinihudumia kwa kila kitu, huwezi amini hata kodi ya nyumba alinilipia yeye tena ye miezi sita.
Hapa ndipo niliona mwanaume ndiyo huyu, tangu kuzaliwa kwangu nilikua sijawahi kula pesa ya mwanaume lakini yake nilikula tena si ya kuomba bali pes aya kupewa. Nilijisikia vizuri, mbali na kuwa kwenye mahusiano lakini niliona hata wanawake wenzangu nao wanakua karibu yangu, natengeneza marafiki, ni kama kutembea na Erick kulifungua mlango wa upendo kutoka kwa watu wengine.
Erick alionyesha kunipenda, mara nyingi alikua anazungumzia mambo ya ndoa, alikua ananiambia kuwa anatak kunioa, anataka kuwa siriasi na mimi na hataki kunichezea. Alikua akinishirikisha katika kila kitu chake, alikua akiniambia mambo yake. Wakati nakutana naye ndiyo alikua ametoka kununua gari na kiwanja, aliniambia kuwa anataka kujenga harakaharaka ndipo aoe.
Alikua ni mjanja, hakuwahi kuniambia moja kwa moja kuwa atanioa lakini aliongea kana wkamba anataka tutengeneze maisha pamoja. Kwa mfano, badala ya kusema nataka nimaliza kujenga ndiyo nikuoe, alikua anasema kabla ya kuoana inabidi tuwe na nyumba yetu, sitaki mke wangu kuja kuishi kwenye nyumba ya kupanga, sitaki hiki sitaki kile.
Nilifurahia mahusiano, nakumbuka mshaar wangu ulipoanza kuingia lainiambia kuhusu suala la kuchukua mkopo, alikua anataka kuanza ujenzi. Aliniambia kwakua yeye alishachukua mkopo wkaajili ya gari itakua ngumu sana kupata mkopo mwingine. Lakini alinishauri mimi kuchukua mkopo ili tumalize nyumba yetu haraka na kuhamia.
Kwangu ilikua ngumu kidogo kwani ndiyo nilikua nimeajiriwa, hata mwaka nilikua bado sijamaliza, nilikua sijaile pesa yangu vizuri. Nilimuambia kuhusu kusubiri kumaliza mwaka kwanza ili kupata mkopo kama kanuni za utumishi zinavyosema lakini alikataa.
“Sio lazima kumaliza mwaka, mimi nafahamiana na afisa utumishi, ni rahisi mbona? Au ni kwamba hutaku tuchukue mkopo, kama hauko siriasi na mimi niambie, mimi nataka kutengeneza maisha na wewe lakini unaonekana kama una mambo yako? Kama hunitaki, una mtu mwingine, niambie, mimi sitaki kupotezewa muda…”
“Hapana, si hivyo, lakini naona kama ni haraka…” Nilimuambia huku nikimbembeleza,a linikubalia kwa kichwa na kuniambia nitajua mwenyewe.
“Ni pesa zako, siwezi kukupangia, kama unaona kuwa huwezi kufanya kitu na mimi basi sawa…” Aliniambia, siku hiyo alikua kwangu, nilikua nishampikia chakula cha jioni lakini hakula, alijifanya kuchoka na kuniambia kuwa atanitafuta kesho yake.
Ilikua ni ijumaa hivyo kesho yake haikua siku ya kazi, hakunitafuta mpaka siku ya jumatatu tulipokutana kazini. Kusema kweli nilichanganyikiwa, nilijihisi kama nimefanya kitu kibaya, kama nimemkosea. Nikiwaza kuwa alikua ananijali, ananihudumia kwa kila kitu kipindi sina kazi, halafu sasa hivi ananipa miapngo yake ya maana mimi namkatalia nilijisikia vibaya sana.
Nakumbuka nilipofika kazini alinisalimia kama kawaida ingawa hakua na uchangamfu kama kawaida yake. Nilimuomba kuongea naye lakinia aliniambia yuko bize. Nilirudi ofisini kwangu nikiwa na mawazo mengi sana, bila kujijua nilijikuta namtumia meseji.
“Najua nimekukosea, unawaza kuhusu familia lakini nimekuangusha, mimi nakupenda nipo tayari tuchukue mkopo ila sijui pakuanzia.”
Nilijifanya kuwa nuilikua nataka kumchukulia mkopo na kujenga naye ila sikua najuan taratibu. Hakuijibu ile mesjei yangu mpaka jioni, wakati wa kutoka kazini alinifuata na kunipakizan kwenye gari yake.
“Una uhakika unataka tutengeneze maisha?” Aliniuliza, nilimjibu kwa kichwa kuwa nina hakika, ingawa nilikua na wasiwasi labda anaweza kuniacha lakini alinisisitizia kuwa suala la kuniacha halipo.
“Una akili sana, ni mwanamke pekee ambaye nimeweza kudumu naye kwenye mahusiano kwa muda mrefu hivi, mimi sinaga kawaid aya kuchukua wanawake wa kazini, vijanamke vya hapa vinakia na kisirani, hamuwezi kutenteneza maisha pamoja, ila wewe naona uko tofauti.”
Aliniambia, nilijisikia vizuri sana kwangu kusifiwa na mwanaume tena kwa kulinganishwa na wanawake wengine ambao nawaona kama wamenizidi kila kitu kilikua kitu kigeni nilikubali, nikaenda kuongea na afisa utumishi, alinisaidia mpaka nikakubaliwa kuchukua mkopo kazini wakati hata mwaka nilikua bado sijafikisha.
Wiki moja kabla ya mkopo wangu kutoka nilipigiwa simu na dada mmoja. Sikua nikimjua lakinia linitukana sana, aliniambia anataka niachane na mume wake kama nisipofanya hivyo atanifanyia kitu kibaya. Nakumbuka nilikua ofisini, hakuniambia mume wake ni nani lakini kwa alivyokua anaongea ni kama alikua anamuongelea Erick.
Sikutaka kusubiri, nilimtafuta mpenzi wangu na kumuambia kuhusu huyo Dada. Tofauti na nilivyotetemea, labda atshtuka na kukasirika lakini hakikua hivyo.
“Nilijua tu kuwa yule mjinga atakutafuta, namba yake si inaishia na 49?” Aliniuliza.
“Ndiyo!” nilimjibu kwa hasira, nilikua nimepaniki kwani nilisha process mkopo halafu naambiwa mambo ya mwanamke mwingine.
“Ninani nhuyo dada na kwanini anitafute na kuniambia niachane na mume wake, kwani wewe umeoa?” nilimuuliza, alinishika mkono mpaka wkenye gari yake, huku akicheka aliniambia nisimuwaze huyo mwanamke kabisa.
“Ni X wangu, niliachana naye baada ya kukutana na wewe. Kama nilivyokuambia huko nyuma, siajwahi kukaa sana na mwanamke, si kama nilikua malaya, hapana, lakini mimi anchagua sana, nahitaji mwanamke wa kutengeneza naye maisha si mwanamke wa starehe. Diana, alikua anapenda sana starehe, tulishapanga mambo mengi, nilikua nampenda lakini nikaona hatutawezana.
Mimi nakunywa pombe lakini najielewa na nakaribia kaucha. Lakini yeye ni mlevi kabisa, si hivyo tu, ni yule mtu ambaye anataka kila weekend kutoka, hamfanyi mambo ya maendeleo. Wakati nanunua gari mimi nayeye tulipanga kuchukua mkopo wote, mimi ninunue geri kutokana na kazi zangu za site mara nyingi napata shida na hiyo hela nyingine ninunie kiwanja ila yeye achukue mkopo tujenge lakini haikua hivyo.
Alichukua mkopo kweli lakini sikuona hata shilingi kumi yake, mimi nikafanya mambo ya maana, nikanunua gari na kiwanaja na kama ulivyoona nimeanza ujenzi ndiyo hela yangu ikaisha. Lakini yeye sasa, alichukua mkopo ila kila ukimuambia kuhusu kufanya kitu cha maana, kujenga yeye hataki, ulipoisha ana alipoona nimekutana na wewe una akili ndiyo akaanza kunitafuta. Hembu angalie meseji zake anavyolaumu…”
Aliongea kwa uchungu sana, kwa kumuangalia ungehdani alikua anataka kulia. Alinioneysha meseji ambazo yeye hakujibu, mwanamke alikua analalamika kamuacha, kamdanganya kuchukua mkopo sasa kapata mwanamke mwingine na mambo kibao.
“Unaona, kachukua mkpo kweli lakini hajanipa hata shilingi kumi, nikimuambia kuhusu kitu cha maana hataki ananiambia ni pesa zake. Mwanamike wa namna hiyo mimi siwezi, maisha yenyewe magumu, uoe mtu ambaye kachukua mkopo kamalizia pes ayake baa wakati wewe unafanya mambo ya maendeleo kweli ni haki hiyo?” Aliniuliza, nilimuambia hapana, si haki, nilimuonea huruma na kujisikia vibaya hata kwa kumuuliza.
“Uamuzi ni wako, mkopo wako unakaribia kutoka, sitaki kukupangia maisha, unaweza kutumia pesa unavyotaka au kuzipeleka wkenye ujenzi. Mimi sitaki kushika pesa yako, ni yako ni jasho lako. Nataka kama ni kujenga unaenda kununua vitu wewe na kuvipeleka site, nataka usimamie wewe, unanonekana una akili ukisimamia kila kitu kitaenda vizuri.”
Nilimuelewa na kumuambia hakuna haja, mimi namuamini hivyo hakuna haja ya sisi wote kusimamia. Kweli mkopo ulipotoka nilimkabidhi lakini nilihakikisha ameutumia vizuri nyumba ilikamilika mpaka kupaua na kila kitu kilikua kinaenda vizuri tu.
Mambo mengi alikua akisimamia yeye, mimi nilikua napita pita tu kuangalia na mara zote ingawa site hakukua mbali lakini alitaka twende wote, hakutaka kabisa mimi kwenda peke yangu. Nilimuelewa kwani alikua akinishirikisha kila kitu. Nilimuona kama mume wangu kwani mbali na ukweli kuwa muda mwingi alikua akiutumia kwangu lakini nilikua huru kwenda kwake kama mke wake, kila kitu nilikua namfanyia, naenda kumfulia na wakati mwingine kumpikia.
Nakumbuka ilikua ni likizo ya mwezi wa kumi na mbili. Aliniambia kuwa hataki niende kwake kwani dada yake anakuja kwake na watoto wak na kutokana na mila zao kwakua bado sijatambulishwa basi isingekua vizuri mimi kwenda kuonana naye. aliniambia hataki ndugu zake kuanza kuniongelea vibaya kabla ya ndoa.
“Nawajua ndugu zangu, kuna mwanamke nilikua naishi naye, basi bila sababu walimchukia kwakua tu walidhani si mtu wa maadili. Nyumbani kwetu ni watu wa dini sana, wanaangalia dini kama nini, ingawa umekubali kubadilisha dini lakini nina uhakika wakijua wewe ni muisalamu kabla hatujaweka mambo sawa ataanza kuleta chokochoko, subiri nikishakutamb ulisha ndiyo niwaambie kuwa nakuoa na dini utabadilisha.”
Aliniambia, kwa namna alivyokua anaongea nilijujua kabisa ananipenda, alikua anajali, nilikubali kuwa sitaenda kwake mpaka Dada yake kuondoka kwake. Akawa anakuja kwangu na usiku nampigia simu tunaongea vizuri, katika kipindi hicho ambacho dada yake alikua kwake muda mwingi alikua akiutumia kwangu.
Mchana aolikua kwangu na siku nyingi za kazi alikua analala kwangu. Ni kama alikua kahamia kabisa, aliniambia hapendi kukaa na dada yake hivyo ni bora kukaa na mimi. Nilifurahi na kuzidi kumuamini kwani nilijua kama ingekua ni uongo basi asingehamia kwangu. Dada yake alikaa kwa mwezi mzima, aliniletea watoto wake wawili, wote alifanana nao, nikawaona ingawa hakutaka niwe karibu yao sana.
“Ukiwazoea watamuambia Mama yao kuwa nina mwanamke.” Aliniambia na nilimuelewa. Lakini siku moja usiku alikuja nyumbani, alionekana kuwa na mwazo sana, sikumuelewa ila alionekana kama kuna kitu kinamsumbua. Nilijaribu kumuuliza lakini hakunipa jibu, alikua na mwazo ni kama analia.
Kila nilipomuuliza alikua ananiambia tuyaache hayo mambo lakini kusema uwkeli nilishindwa kabisa kuyaacha, nilitamani sana kuongea naye. usiku nililazimishia mpaka kuongea.
“Dada yangu kasimamishwa kazi na ana matatizo na mume wake, alikua ananiomba kuja kuishi kwangu, lakini nilimuambia mimi siwezi. Ameniambia kuwakwakua mimi nina nyumba basi nimpangishie, atanilipa kodi ili afanye Biashara kwani ana familia kama akipanga chumba kimoja itakua shida.
Nimemuambia kuwa mimi nakaribia kuoa nitakua na familia yangu lakini amenaimbia hamna shida, akipokea pesa yake ya NSSf ataondoka na kwenda kuishi wkake. Najua nyumba tumejenga wote, siwezi kufanya maamuzi bila wewe lakini ni dada yangu na sijui chakufanya?” Nilijikuta napandwa na hasira kwani nilitetgemea nyumba ikiisha basi tutahamia wote, lakini haikua hivyo, nyumba yetu mpya alikua anataka kuanza kuishi na dada yake.
Lakini nikifikiria mambo aliyonifanyia, jinsi alibyokua akinijali mpaka kunifanya kujihisi mwanamke tena niliona labda ninakasitika bure. Isitoshe mimi nilikua na kwangu, bado hatujaoana, hata kama imekamilika nisingeanza kuishi naye kabola ya ndoa. Nilijifikiria sana mwisho niliamua kukubaliana naye, nilikubali akaniuliza mara nyingi kama niko sawa, labda sijakasirika nilimuambia hapana.
Nilikubaliana naye, akaondoka na siku iliyofuata aliniambia kuwa niko huru kwenda kwake kwani dada yake alishahama. Nilifurahia kidogo kuwa naenda kwake, nilifika lakini nilishangaa chumba kikiwa kitupu, alikua kaondoa kila kitu chake, nilimuuliza shida ni nini akaniambia kuwa ameamua kumpa dada yake vitu vyake vya kuanzia maisha na yeye atakuja kuishi kwangu.
“Sasa unaishije bila ndoa, hata kwetu hawakutambui?” Nilimuuliza, aliniambia hakuna shida, atakuja kwetu kujitambulisha kisha atanipeleka kwao. Kusikia mwanaume anakuja kujitambulisha nilihisi kuchanganyikiwa zaidi kwa furaha, kwangu kilikua ni kitu cha ajabu kwani kila siku tangu kuanza kazi nilikua naulizwa naolewa lini?
Alikuje kwetu kujitambulisha, suala la dini nyumbani kwetu walikua wakali lakini cha ajabu aliwaambia wazazi wangu kua yeye yuko tayari kubadilisha dini kwani ananipenda. Nilishangaa sana kwani haikua mipango yetu, wazai wangu walimuelewa na sikuongea kitu chochote, baada ya kuondoka kwetu nilimuuliza mbona kasema atabadilisha dini akaniambia wazazi wangu wanaonekana watu wa dini sana hivyo hakutaka wamkatae.
Nilikua sina namna zaidi ya kukubali nikiamini kuwa kwa kukubali kubadilisha dini alikua ananipenda sana. Tulienda kwake kuchukua vitu vichache vilivyobaki ili kuja kwangu, lakini wakati nakagua vitu nakusanya nilikutana na Bahasha ambayo ilikua kama imechanika hivi, ni yazamani, nikaamua kutoa vitu ili kuviweka vizuri ndipo nilikutana na cheti cha ndoa tena ya kanisani.
Kilikua na jina lake na jina jingine ni la yule mwanamke ambeye aliniambia ni Dad ayake, niliangalia nikakuta na picha za harusi na nyingine wakiwa wamepakata watoto wawili tena kwa furaha, watoto niliwakumbuka ni wale ambao aliniambia kuwa ni wa Dada yake. Nilijikuta naishiwa nguvu, nilitamani kunyanyuka na kumfuata lakini nilishindwa, miguu ililegea nikawa hata kuongea siwezi.
AMINA; NITAJIUA SIKU YANGU YA KUZALIWA IKIFIKA ILI WASHEREHEKEE VIZURI—SEHEMU YA TATU
“Kwanini umenifanyia hivi?” Nilimuuliza Erick, baad aya kuona kile cheti cha ndoa na picha za yeye na mke wake. Aliniangalia kwa dharau kisha akatema mate chini.
“Inamaana uliamini kweli nitakuoa? Hembu jiangalie na kisha uniangalie na mimi, hivi wanawake wote wazuri pale ofisini halafu nije kuoa kituko kama wewe, hivi una akili kweli?”
Aliniuliza, nilikua nimeumia sana, hata kunyanyua mdomo kumjibu sikuweza. Aliniambia kuwa alikua na mimi kunisaidia kwani anaona kama vile siwezi kupata mwanaume bila yeye.
“Mimi ni star, unaona tangu niwe na wewe wanaume wanakutongoza, wanakutaka, ukiniacha hata mtu wa kukusalimia hutapata!” Aliendelea kuongea maneno mengi ya dharau ambayo yalinichoma sana. Nilijikuta nakasirika, nikaacha vitu vyake pala, nikapanda bajaji na kuondoka kurudi kwangu
Nikidhani labda atanitafuta na kuniomba msamaha lakini haikua hivyo, hakunitafuta na wala hakuja kwangu. Nikajua sasa mapenzi yameisha, lakini mimi nitaishije, pale kazini nitafanya nini, kila mtu alikua anajua kuwa natembea na Erick, mapenzi yetu hayakua ya kuficha, hata baadhi ya ngugu zangu walikua wanamfgahamu.
Pamoja na yote aliyokua amenifanyia lakini abdo nilitamani kuongea naye, nilitaka ajue ni kwanini amenifanyia hivi, kwanini hakuniambia kama ameoa, akanidanganya mpaka kumchukulia mkopo. Niliwaza sna aiskupata jibu, niliwaza ni namna gani alikua na mke wakati muda mwingi alikua akiutumia kwangu, nilikua nalala naye karibu kila siku lakini hata siku moja sikuwahi kusikia mke wake akimpigia, ni mke wa namna gani ambaye alikua kimya namna hiyo, kusema kweli sikujua mpaka pale nilipokuja kugundua kuwa kumbe alikua ns imu mbili, moja ilikua ikikaa kwenye gari na hakua akiitoa. Kila mara alipokua akiingia ndani tukiwa naye alimpigia simu kwanza mke wake na kumuambia kachoka na akzi hivyo analala.
Anazimka simu na subihi wakati wa kuamka humpigia na kisha kuingia nayo ofisini ambapo soko naye. Nilienda kazini kwa aibu nikijua labda atakua kamuambia kila mtu kuhusu mimi na kuachana kwetu. Lakini haikua hivyo, kazini alinisalimia kawaida na kuniomba tusiwaambia watu kwani hataki mambo yake kujulikana.
Nilijisikia furaha kidogo na amani kwani niliona kama kanijali, sitapata tena aibu. Siku iliyofuata alikuja kwangu, alikua na ufunguo hivyo nikiwa ndani nilishangaa mtu kaingia tu.
“Najua nimekuumzia sana lakini naomba unisikilie, siku ile nilikujibu kwa hasira kwakua uliniuliza kwa hasira, ulianza kwa kunishurumu badala ya kuuliza….”
Alianza kuongea baada tu ya kuingia ndani kwangu, nilikua na hasira lakini sikua na budi kumsikiliza. Kwanza bado nilikua nampenda lakini alichukua vitu vyangu vingi, mbali na mkopo wa kazini ambao nilimpa akajengea lakini kuna pesa ambayo nilimdhamini kwa ndugu yangu. nilimkopea milioni 4 kwa kaka yangu ili kumalizia nyumba. Hizo aliniambia kuwa atalipa yeye na alishaanza kurejesha laki nne hivyo bado nilikua namdai milioni tatu na laki sita.
Kuachana na kumnunia ilimaanisha nakosa kila kitu.
“Mimi nakupenda, wewe ni mwanamke mwenye akili sana, lakini najuta kwani nilikuona baad aya mimi kuoa. Nina uhakika ningekujua kabla ya kumuoa mke wangu basi ningekuoa wewe, lakini nilikuona nikakupenda nikiwa mume wa mtu…”
Kwa namna alivyokua anaongea nilihisi kumuonea huruma, nilianza kumuamini na kuhisi labda kweli ananipenda mimi na mke wake ni kamabahati mbaya.
“Kwa kipindi ambacho nimekuona umenibadilisha maisha yangu, mimi sikua hivi, nilikua mlevi, mtu wa wanawake lakini sasa hivi nimekua na wewe miezi hii michache, ona nina nyumba, nina kila kitu, hivi unafikiri mimi naweza kukuacha, ninachohitaji kwako ni kwa wewe kunipa muda, nimuache mke wangu taratibu.”
Aliniambia hukua kinibembeleza, nilikua namsikiliza najua kabisa ni uongo, naamini kabisa hawezi kumuacha mke wake lakini kuna kitu kinaniambia mkubali, “Amina ushapotza kila kitu unafikiri una nini tena cha kupoteza? Hembu kwanza jiangalie, una nini? Maisha yako hatyana maana, nani atakuoa, hivi kuna mwanaume mwingine atakupenda kuliko huyu?” Sauti ilisikika masikioni mwangu.
Ni kama aliniona nalegea, ni kama alijua nitamsamehe ila nilikua nahitaji kusukumwa kidogo. Alinisogelea na kunikuambatia, alinshika sehemu mablimbali za mwili wangu nikajikuta naingia laini na siku hiyo tukafanya mapenzi. Kwa namna alivyofanya mapenzi na mimi ilikua ni kama mwanaume mpya, kama mtu ambaye sijawhai kumuona kabla.
Ilikua ni mechi nzuri hivyo nikaamini ananipenda na kuamini msamaha wake. Hakuna namna mwanaume angeweza kufanya mapenzi namna ile halafu asinipende. Hapo hapo tulirudiana, nilimuuliza kuhusu mke wake akaniambia nisihangaike naye.
“Una nyota bya mafanikio, tangu kumuoa yule mwanamke hakuna kitu cha maana ambacho nilishawahi kukifanya nikafanikiwa. Lakini nimekua na wewe muda mchache nafanikiwa, hakuna aisee, nitamuacha nipe muda, kwa sasa hajanikosea kitu chochote hivyo sina sababu ya kumuacha, nipe mdua nitampiga matukio ataondoka mwenyewe.”
Niliamini kabisa kuwa atamuacha mke wake, niliamini hawapendani na labda ni kwasababu alishafunga naye ndoa na wana watoto, nikaamua kukubali ukweli kuwa mimi ndiyo mpenzi wake na mke wake ni mpita njia tu. Nilitaka tu kuwa na furaha kwa wakati huo hivyo nilisahau hata kama alishawahi kunitukana na kuniambia kuwa mimi si wa hadhi yake.
****
Mambo yalirudi kama mwanzo lakini sasa hivia likua huru kuongea na mke wake. Mara nyingi alikua akiaga kwa mke wake kuwa anasafiri kikazi hivyo anakuja kwangu anakaa kama wiki ndiyo anarudi, alikua kama mume wangu na nilijisikia vizuri, aliniomba kuja kwetu kujitambulisha ili nimuamini zaidi.
“Nataka nikimuacha mke wangu nakuoa hapohapo, watu wanasema kama ukimuacha mwanamke halafu ukachelewa kukuoa anaweza kukuloga halafu usioe tena. Aliniambia, nilikubali kumpeleka kwetu, akaja na kutoa kishika uchumba, sikuwaambia nyumbani kuwa ana mke na wana ndoa ya Kanisani. Alishakuja mwanzoni kama kujitambulisha tu, lakini sasa hivi alikuja rasmi kwa mara ya pili, akatoa kishika uchumba, kwakua alishaoa aisngweza kuwaambia kwao kuja kutoa mahari kwetu.
Alitafuta watu tu huko mtaani, wakaja na kupangiwa mahari, akaahidi kuja kuyalipa. Alinivalisha na pete ya uchumba, ingawa aliniambia nisipost lakini nilitamani kufanya hivyo, nilitamani kila mtu kujua kama na mimi naolewa, nilikua natamani watu waone, kwangu niliona kama vile bado hayuko siriasi na mimi kama sitapost.
Wakati huo Facebook ndiyo ilikua inapamba moto, nilipost katika ukurasa wangu bila kujali kama ataona au la. Alikasirika sana na kuniambia nifute. Kwakua baadhi ya watu niliowalenga walikua wameshaona sikuona shida, nilifuta. Lakini usiku wake nilipokea simu kutoka kwa mtu ambaye si mfahamu.
“Unamjua huyo Kaka vizuri, kwanini unampost mchumba wangu?” Nilitumiwa meseji na namba ngeni, kabla hata sijaijibu ile namba ilipiga, nilipokea, alikua ni mwanamke, alianza kwa kunitukana, kuniambia niache umalaya, akatukana sana na kuniambia kwa taarifa yangu yeye ndiyo mchumba wa Erick na ameshampeleka mpaka kwao.
Aliniambia mambo mengi kuhusu mchumba wangu kuonyesha kuwa anamjua na anajua anachokionega, niliishia kushangaa kwani huyo alikua ni mwanamke mwingine toafuti na mke wake na tofauti na yule ambaye alinitafuta huko nyuma. Nilitafuta jina lake kwenye M-Pesa kisha nikaingia kumtafuta, hapo ndipo nilishangaa, alikua na picha nyingi sana za Erick tena nyingine akiwa na mtoto.
Nilijikuta napaniki kwani wlaikua ni kama rfamilia, nilisubiri Erick akaja kwangu nikamuuliza kuhusu huyo mwanamke, alinipa jibu ambalo sikulitegemea, hakuomba msamaha wala kujielezea labda aknidanganya, hapana, aliniambia “Nilikuambia usopost, umepata ulichokua unakitaka usiniaumbus!”
Aliongea hukua kielekea chumbani, alivua nguo akaingia bafuni na alipotoka alidai chakula. Hakutaka kabisa kuongelea hilo jambo, usiku alitaka kufanya mapenzi na mimi lakini sikua tayari kwenye mood, niligoma lakinia lilazimishia. Baada ya kumaliza aliondoka na kuniambia kuwa nifuate maisha yangu kwani hapendi kisirani yeye si mtu wa kuendeshwa endeshwa na wanawake.
Nilijaribu kumuomba msamaha lakini aliniambia tupeane muda afikirie kama ananihitaji au la.
“Mwanzo nilijua una akili, unawaza pesa na kutafuta maisha, lakini sasa hivi naona kabisa kuwa huna tofauti na mke wangu au malaya wengine, yaani hutumii akili kabisa, unaniuliza mambo ya kijinga jinga, mara nina mtoto sijui nina wanawake wengine. Hivi hata kama ni kweli mimi si ni mwanaume, mimi sitaki kuwa na mwanamke ambaye ananichunga, kama nafanya umalaya wangu nataka nifaney kwa uhuru!”
Aliniambia nakuondoka, nahisi huo ndiyo kama ulikua mwisho wetu kwani baada ya hapo hakurudi tena kwangu. Kazini tulikua tunapishana kama magari, hakuna salamu wala hakuna kuongea. Alikua kama kanisusia, yaani kila nikimuambia kitu hata kama ni cha kikazi atanijibu vibaya. Haikuishia hapo, alianza kuwaambia marafiki zake kuwa kaamua kuachana na mimi kwakua nilikua namloga.
“Nilishaanza kusahau familia yangu, yaani sijui huyu mwanamke alinipa nini!” Siku moja nilimsikia akiongea, ni kama aliongea makusudi ili nimsikie na kuniumiza. Haikuishia hapo, alianza kumleta mke wake kazini na watoto wake ili tu kuniumiza, alitaka tu nione na kweli niliumia kwani nilikua nampenda sana.
Nilikua katika msongo wa mawazo kwa kipindi cha kama miezi miwili, pale kazini karibu kila mtu alinitenga, aliniona mchawi na kuonekana kama niliingilia ndoa ya mtu mwingine. Hakuna mtu aliyekua upande wangu, wasichana ndiyo walizidi kunitukana, kwamba nilikua naringa sana lakini wanashukuru kuwa nimekomeshwa.
Nilikonda sana, sikuweza kuacha kazi kwakua ndiyo ilikua kila kitu kwangu, kwetu walikua na uwezo kidogo lakini wasingenielewa kama nikiacha kazi. Haikuishia hapo, baada ya miezi miwili tu niligundua kuwa nina ujauzito wa yule Kaka. Hapo ndipo nilizidi kuchangantikiwa.
Nilitamani kuitoa mimba, nilitamani hata iyeyuke kwani mbali na kuwa nilikua nampenda X wangu na sikutaka kumbukumbu yake yoyote katika maisha yangu lakini piasikua na pesa, nilikua na madeni mengi, mshahara wangu wote ulikua ukiishia kulipia madeni niliyokopa kwaajili ya Erick nilijua kabisa kuwa siwezi kuhudumia mtoto.
Niliwaza sana mwisho nikaamua kumuambia kuwa nina mimba yake ili yeye kaumua cha kufanya, nilimuambia kwa kumtumia meseji kwani hakua akipokea simu zangu na pale kazini kila nilipokua nataka kuongea naye alikua hataki kabisa.
“Najua tushaachana lakini nimeenda kupima na nina mimba yako, unajua hali yangu, nilishakuchukulia mikopo hivyo siwezi kumtunza huyu mtoto naomba tuonane ili tuongee.” Nilimtumia ile meseji, hakujibu kitu chochote kwa siku mbili, hata kazini sikumuona, niliambiwa kasafiri kikazi lakini sikua na uhakika.
Siku ya tatu ndipo alinipigia simu kwa namba ngeni, aliniambia kuwa aliona meseji yangu ila anataka tuongee na hataki kuja kwangu. Nilifarijika kidogo akanialekeeza sehemu ya kukutana naye, aliniambia ni kwa rafiki yake ambaye mimi hata nilikua simjui. Kwakua mimi ndiyo nilikua na shida sikua na namna, nilienda kama aliyonielekeza mpaka nikafika. Alinifungulia yeye lakini ile nyumba kwa kuingalia tu nilijua lazima itakua ni ya mwanamke.
Kuna picha ukutani niliiona ya mwanamke amabye naye nilishawhai kumuona kabla ila sikumbuki ni wapi. kuangalia kwenye makochi kulikua na midoli mingi pamoja na vitu vingi vya kike. Aliniambia nikae lakini kabla sijakaa chini alitokea binti wa makamo na kuanza kutukana.
“Wewe ndiyo unasema una mimba ya mume wangu, sasa kwa taarifa yako hiyo mimba itatoka leo!” Alinaimbia, kabla hata sijajielewa vizuri Erick alinishika na kuanza kunipiga, alinipiga sana hukua kinishurumu kwua nataka kumharibia maisha yake yey hataki mtoto na mimi. Alinipiga sana kisha akanishika na yule dada alinibana mdomoni, akaninywesha dawa flani za mitishamba, niligoma kabisa kunywa lakini walinilazimishia.
Wakati wote huo walikua wanatukana huko huyo dada akimuita mume na Erick akisema kuwa nimejibebesha mimba ili kumharibia yeye na huyo dada wasioone. Nilikunywa dawa nyingi sana, baada ya hapo walinichukua mpaka kwanye gari, ilikua ni usiku tayari, walinifikisha mpaka ndani na kuniacha kisha wakaondoka. Alinipa vitisho vingi kuwa kama nikimuambia mtu yoyote au kwenda Polisi basi watanifanya kitu kibaya.
Ni ngumu sana kwa wanawake wengi kutoka katiak mahusiano ya mateso. Hii ni kwasababu wengi wao wanakua tayari wameshakua mateja hivyo kila wakijaribu kutoka wanajikuta wanarudi na kuna wakati wanamiss mateso. Wwengi wao wanakua wanajidhaaru, wanajiona kama si lolote kitu hivyo kuishi na watesi wao kama njia ya kujikinga.
AMINA; NITAJIUA SIKU YANGU YA KUZALIWA IKIFIKA ILI WASHEREHEKEE VIZURI—SEHEMU YA NNE
Nilikua katika maumivu makali sana kiasi kwamba hata siku iliyofuata sikuweza kwenda kazini. Tumbo lilikua linaniuma, mara damu zikaanza kutoka sehemu za siri. Nilitamani kutoka na kwenda kazini lakini nilikua naumwa sana, sikua na marafiki wa kihivyo wa kuwaambia mambo yangu hivyo niliendelea kubaki ndani nikitegemea kuwa nitapona lakini haikua hivyo.
Siku ya tatu nililazimika kwenda Hospitalini, mimba ilishatoka hivyo nilisafishwa na kwa bahati nzuri haikuathiri kizazi changu. Nilirudi kazini nikijiambia kuwa sitahangaika kabisa na Erick, nilishakubali kupoteza kila kitu na kuangalia maisha yangu, nikiamini kuwa kama nikimuacha, nikiacha kumtafuta na kukubali kumuachia kila kitu basi hatanisumbua na ataniacha na amani.
Lakini haikua hivyo, wakati nikitegemea nitakua na amani Erick alikua akinitangaza vibaya. Nafika kazini nakutana na habari analalamika kwa watu kuwa nimetoa mimba yake na kumlia pesa zake nyingi kwasababu ya umalaya. Aliwaambia watu sikua naumwa bali nilitoa mimba yake, nilifika ofisini kila mtu akiniangalia kama mnyama, yaani kila kitu kilinigeukia mimi, sikua na marafiki, nilikuja kugundua kuwa hata wale wanawake wenzangu ambao nilikua nawoana kama marafiki kwanza walikua wananionea wivu na pili walijiweka karibu na mimi ili kujua mambo ya Erick.
Hali hiyo iliendelea mpaka nikaja kuizoea, nikajikuta ni mtu wa kukaa peke yangu, sina marafiki ni kazi tu. Majungu hayakuisha, kila kitu nilichokua nikikifanya kilileta maneno, pamoja na yote hayo lakini sikukata tamaa ya kuishi. Kutokana na upweke, sina kitu cha kufanya niliamua kufungua Biashara. Kipindi kile bodaboda ndiyo zilikua zinmapamba moto na kulikua na maduka machache sana ya vifa avya bodaboda.
Kwangu hiyo ilikua ni kama fursa, nilikua na akiba yangu kidogo nikatafuta fremu na kufungua duka la vifaa vya bodaboda, nilianza kama urtani, sehemu ambayo nikiwa sina kazi au nikitoka kazini ile saa tisa na nusu naenda kukaa. Nilitafuta mafundi wawili ambao walikaa pale na vijana wao, ghafla kila kitu kikabadilika. Biashara ikaanza kuwa nzuri nikaanza kushika pesa.
Nilitopup mkopo wangu nikachukua hela yote niliyopata na kuiweka dukani, hapo ndipo nilianza kuona faida yenyewe. Kila kitu kilikua kizuri lakini bado nilikua sina furaha. Biashara yangu ilikua kubwa, nilianza na mtaji wa milioni tano lakini ilipanda mpaka nikafikisha mtaji wa milioni thabini ndani ya miaka miwili na bado ilikua inakua.
Sikiua na matumizi makubwa kwani hata nyumbani kwetu hawakua wakinitegemea sana, nilinunua kiwanja na kuanza kujenga, pamoja na yote hayo lakini bado nilikua sina furaha. Sikua na mwanaume, sikua na mtu wa kuongea naye usiku, sikua na marafiki hivyo muda mwingi nikiwa nyumbani peke yangu niliishia kulia tu. Nilitamani sana kutoka lakini sikua na mtu wa kutoka naye, sehemu niliyoklua nikiishi kamji kalikua kaodgo hivyo hata kukutana na watu wapya ilikua ngumu sana kwangu.
Katika kazi zangu za kuuza spea nilifahamiana na maderava wengi wa bodboda, kuna kaka mmmoja nilizoeana naye sana na nilikua nampenda. Hakuwahi kunitongoza na kusema kweli sikua najua kitu chochote kuhusu yeye lkaini nilitamani kuwa nayeye.
“Wanaume wasomi nawasumbia, ni heri nichukua mtu ambaye hajasoma, ambaye hana kazi ya maana niwe naye labda atanihehimu.” Hayo hayakua ni mawazo yangu, nakumbuka yalikua ni mawazo ya Facebook, nilikua kwenye group flani la wanawake tu ambapo kila siku walikua wakizungumzia na kupost matatizo ya ndoa.
Kila nikiangalia wanaume wengi wenye pesa ndiyo walikua wakisumbua hivyo kuna watu walikua wakisema kama unataka kuwa na furaha basi kama una pesa zako basi tafuta mwanaume ambaye hana pesa, mchukue ishi naye hatakusumbua. Niliona kama ni kitu kizuri kwangu, niliona kama nikifanya hivyo kwa yule Kaka labda nitakua na amani kwani nilishachoka kuteseka.
Nilianzisha mazoe ana yule Kaka, naye alikua mshapu kwani nilipoanza kujipeleka kwake alijiongzea na kunitongoza. Mwanzo nilitaka kumsoma kwanza, kujua tabia zake, tayari nilishaumizwa hivyo sikutaka kukurupuka. Nilimuona yuko tofauti kabisa, mbali na kujua kuwa nina pesa lakinia likua anabeba majukumu yake kama mwanaume. Yeye alikua kaajiriwa, anaendesha Bodaboda ya mtu, lakini kila kidogo alichokua anakipata alikua ananisaidia.
Alipenda tutoke wote, alipenda kuninunulia zawadi na hakuwahi kuniomba pesa. Niliona haya ndiyo mahusiano, basi nikajikuta naingia mazima, sikutaka aendelee kuendesha Bodaboda za watu, nilijichanga na kumnunulia Bajaji, sikumpa moja kwa moja nilimuambia kuwa ni ya kwetu na atakua analeta hesabu kama watu wengine.
Tulifanya hivyo kwa miezi sita ila niliona kama ana akili sana, alikua ananishauri mambo mengi kuhusu Biashara, akaniunganisha na watu wengi nikaona kabisa kuwa huyu tunaweza kutengeneza maisha. Nilimuabia aache ishu ya bodaboda na kuhamia kwenye duka langu.
Kweli alifanya hivyo, yeye ndiyo akawa msimamizi, akwa kama mume wangu. Nilikua nishamaliza kujenga nyumba yangu hivyo tulihamia na kuanza kuishi pamoja. Mambo yalienda vizuri, biahsara zilienda vizuri, nilimuamini sana Abdul (sio jina lake halisi) na kumuona kama mume wangu. Kwakua alikua hajasoma na alikua hajiamini nilijitahidi sana kumpa vitu ili aendane na hashi yangu, nilimbadilisha kila kitu, kuanzia mavazi na nilikua nikimpa magari yangu kuyatumia.
Alikua na nidhamu sana hivyo nilimuamini kwa kila kitu. Nilipanda cheo kazini hivyo muda mwingi nilikua bize kazini na kila kitu nilimuachia yeye, alikua ni kama mume wangu. Mambo yalikua mazuri hivyo nilitaka ndoa, hapo ndipo niliana kuona mabadiliko kidogo. Nilimuambia aje kwetu kujitambulisha akaniambia hapana hawezi kwani kwao kwani kwao hali ni ngumu, anaona aibu kunipeoleka hivyo ni lazima kwanza awajengee wazazi wake kabla ya mambo yote.
Kusema ikweli nilimualewa, kwajinsi nilivyokua naijua familia yangu nilijua ni lazima watanikatalia kuolewa na huyo mwanaume kama wakijua kuwa ni masikini. Nilimsaidia kujenga, kwao, sikua nikipafahamu na hakutaka kunipeleka lakini kila sikua likua akinipigia picha za kunionyesha maendeleo ya nyumba yao.
Lakini ghafla kila kitu kilibadilika, aliacha kunionyesha picha na kila nilipokua nikimuuliza alinuna.
“Mbona unanijengea kwa masimango hivyo…” Aliniambia hivyo nilikua sina namna zaidi ya kunyamaza. Tabia zake nazo zilibadilika, mara zote kila nikitoka kazini nilikua napitia dukani, duka lilishakua kubwa, hatukufungua duka jingina lakini tulikua na stoo tatu ambapo mbali na kuuza spea za rejareja lakini tulikua tunasambaza na za jumla.
Kila nikitaka kwenda dukani alikua akiniambia kuwa simuamini ndiyo maana namfuatilia, mara alikua anasema hataki mimi niwe nakaa dukani kwani kule kuna marafiki zake wengi ambo nimalaya hivyowa tanitongoza. Kusema kweli nilishangaa kwani alinikuta na Biashara yangu na sikutongozwa. Tulianza kugombana kila siku, akiniambia kitu nikikataa basi hulalamika kuwa namdhaarau kwakua kila kitu ni changu.
Nilijitahidi sana kumridhisha, kufanya kila kitu anachotaka yeye lakini hatukua na furaha. Kila kitu kilibadilika, Abdul alikua ni mtu mpya kabisa, alianza kunidharau na ikuniongelesha vibaya. Kila wakati alikua ananikosoa, niklifanya kitu kidogo utasikia, wewe huna akili hivi mwanamke gani uko hivyo acha nitafanya mimi.
Dukani alidhibiti kila kitu, yeye ndiyo alikua anaenda kununua mzigo, anaongea na wateja na wafanyakazi anafukuza yeye akitaka. Kila nikiongea alikua akinikasirikia huku akiniambia kama siwezi kumuacha asimamia basi ni bora tuachane na kila mtu kuishi kivyake. Niliishi kwa kuvumiliakwani sikutaka kuahcana naye, mbali na kuona aibu ya kuwa mtu wa kuachika kila siku lakini pia nilikua nampenda.
Abdul alishakua sehemu ya maisha yangu, alikua ananisaidia mambo mengi hasa katika Biashara. Kwa miaka miwili ambayo nilikua naye nilishashaau mambo ya TRA, kwenda kununua Mzigo, alikua anaenda mpaka China kununua mzigo ana sikua nikijua kitu chochote tena. Ilikua ni lazima kumnyenyekea kwani nilijua kama nikimuacha basi na Biashara zangu zitasimama.
Mwanzo nilikua na uhuru wa simu yake, nilikua nikishika nakufanyia chochote lakini nilishangaa amebadilisha password, hakutaka nishike na nikiuliza yalikua ni maneno. Siku moja nilikua nimetoka kazini, ilikua ni kama saa mbili usiku hivi. Siku hiyo kulikua na wakaguzi hivyo nilichalewa na kwakua nilikua na wakaguzi nilishindwa hata kumjulisha kuwa nitachelewa.
Kwa kawaida yeye hufunga maduka kwenye saa nne, akipiga mahesabu mpaka kumaliza anarudi nyumbani kwenye sa atano hivi. Lakini siku hiyo sijui ni kitu gani kilitokea, nilirudi nyumbani saa mbili na kumkuta Abdul ameshafika, alikua amekaa sebuleni ameshikilia mkanda wake, alionekana kuwa na hasira, niliingia ndani na kumsalimia lakini hakuniitukia, nilimuulizia mambo vipi mbona siku hiyo kachelewa inamaana ameshafunga na duka lakini hakunijibu.
Kuona hivyo kwakua nilikua nimechoka sikutaka kubishana naye, niliondoka kuingia chumbani lakini sikupiga hata hatua mbili. Alinishika nywele zangu kwa bahati nzuri nilikua nimevaa wigi hivyo lilitoka tu, kabla sijafanya kitu alianza kunipiga na mikanda.
“Mshenzi wewe, ulikua umefanya nini mpaka mwanaume nawahi kurudi nyumbani kwangu! Una dharau sana kwakua umesoma, kwakua una pesa, mimi ndiyo mwanaume humu ndani. Kila siku nahangaika huko kumbe ndiyo kawaida yako kuchelewa kurudi. Unatoka kazini saa tisa na nusu, mpaka saa hivi saa mbili ulikua unafanya nini huko?”
Aliongea huku akinipiga, alinishika na kunivuta kunizungusha sebuleni, alinipiga sana kisha akanifungia chumbani na kuondoka. Hakurudi mpaka asubuhi ambapo nililazimika kumpigia simu ilia je kunifungulia kwani nilitakiwa kwenda kazini na nilikua na wakaguzi, kulikua na hoja nyingi za kujibu.
Alipokea simu lakini badala ya kuja aliishia kunitukana.
“Si unaona hiyo kazi ni muhimu, basi tuone ukiipoteza utafanya nini?” Aliniambia, nilimbembeleza sana lakinia aligoma kuja kunifungulia, nililazimika kumpigia simu Bosi wangu kuwa ninaumwa siwezi kuja, nashukuru kwa bahati nzuri wakaguzi nao hawkauja siku hiyo, walikua na kikao chao hivyo wakaomba udhuru kuwa watakuja siku inayofuata.
Mpaka saa saba mchana ndiyo alikuja kunifungulia. Alifungua huku analia, ananiomba msamaha kwa kunifanyia vile.
“Nakupenda sana lakini nahisi unanidharau, mimi sina pesa lakini ndiyo mwanaume, unaporudi usiku bila kuniambia uko wapi huwa napata wasiwasi. Nashindwa nini chakufanya, usiwe unanipandisha hasira namna hiyo….”]
Nilishachoka na kupanga kumuacha siku hiyo, lakini kwa namna alivyoomba msamaha nilijuua kuwa labda kajutia na hatafanya tena hayo mambo. Lakini haikua hivyo, baada ya kumsamehe suala la kupigwa lilikua kama kawaida, matusi tena ya nguoni yalikua mambo ya kawaida.
“Mwanamke gani hujui hata kuoga, hivi umesoma nini lakini unanuka uch*” Alipenda kuniambia, alipenda kunidhalilisha mbele za watu, nikiongea kidogo ananiambia kuwa sina akili hivyo ninyamaze. Lakini tukirudi nyumbani basi anabadilika, anakua mkimya anaomba msmaaha.
“Unanikwaza ndiyo maana nakua hivyo, mimi nakupenda lakini sitaki uwe unanijibu mbele za watu!” Ananiambia, alikua anaongea kwa namna ambayo hata akinipiga naishia kuomba msamaha mimi kwani najiona kama mkosaji. Alikua hajiamini hivyo hataki nitoke, hataki niwena marafiiki, hataki niongee na wafanyakazi wenzangu. Kila nikitoka kazini basi simu zangu anazichukua yeye, hata kama ikitokea ni mfanyakazi mwenzangu kanipigia simu basi atapokea yeye kwanza ndipo akijua ni mambo ya kikazi hunipa mimi.
Alikua ananichunga sana kiasi kwamba hata likitokea tatizo nyumbani kwetu hataki niende. Nikitoka kazini basi ni kubaki nyumbani, hakutaka niingie katika mitandao ya kijamii, kwa kifupi nilikua kama mfungwa wake, sifanyi kitu bila yeye kuniruhusu. Pamoja na kunibana kote huko lakini sikua na uhuru na simu yake, alikua ni msiri sana, simu yake anaishikilia kila sehemu. Hata akienda chooni huishikilia, hakutaka niiguse na kila wakati nikiwa naye basi huilaza chini ili hata meseji ikiingia au simku ikipigwa nisijue ni nani amepiga au kutuma meseji.
Hali hiyo iliniumiza sana lakini sikuwahi kumuuliza kwanini anafanya hivyo kwani kila wakati alikua anatishia kuniacha au kunipiga. Nilianza kuongelea suala la ndoa tena lakinia linijibu kwa dharau.
“Siwezi kukuoa mpaka uwe na adabu, utambue tahamni yangu na kujua kuwa mimi ndiyo mwanaume humu ndani. Kama huwezi kuniheshimu siwezi kukuoa. Alipenda kuniambia, kusema kweli nilikua naumia sana kwani nilijitoa sana kwake, nilimheshimu kuliko maelezo. Nilimpa kila kitu changu, yeye ndiyo akawa anasimamia, nikamfanya akawa mwanaume lakini bado alikua anaona kama sifai kuwa mke wake.
Sikua nikijua chochote kilichokua kikiendelea kwenye Biashara zangu, alinikataza hata kuongea na wafanyakazi wangu, kila mfanyakazi aliyekua anaongea na mimi alimfukuza kwa madai kuwa natembea naye. Siku moja akiwa kasafiri nilienda dukani, ingawa alishanikataza lakini niliona kama duka ni langu hivyo ni lazima kwenda. Nilikaa kutwa nzima pale dukani nikaona mauzo yake yalivyo.
Wafanyakazi hakuna akiyetaka kuongea na mimi, walikua hawataki kuniambia kitu chochote. Jioni kuna dada mmoja aalikuja, alikuja kama mteja lakini ghafla niliona anaingia sehemu ya kuuzia na kuanza kukagua droo ya pesa.
“Dada unaenda wapi?”Nilimuuliza huku nikimshika mkono kumzuia asichukue pesa. Alinigeukia kwa dharau na kutaka kunizaba Kofi lakini nilimkwepa na kumsukuma pembeni. Wafanyakazi wlainishika kwani nilishapandwa na hasira kutaka kumpiga.
“Madame, wewe ondoka tu, Bosi akija ndiyo utachukua pesa….” Mfanyakazi mmoja ambaye mwanzo nilimuajiri mimi alimshika yule dada na kutaka kumuondoa pale lakini hakukubali.
“Kwanini niondoke dukani kwangu, siondoki na nimekuja makusaudi, nilijua kabisa kwakua mume wangtu hayupo huyu Mmama atakuja hapa, nakuambia siondoki!” aliongea huku akinyanyuka, alinivamia na kutaka kunipiga lakini sikumruhusu.
Nilishahisi mwanaume wangu ana mtu mwingine, sikuwa nikimjua ila nilidhani ni vimalayamalaya vyake tu, sikudhani kama anaweza kuingia kwenye duka langu. Tulianza kushikana na kupigana, kutukanana, watu w3akitushika tunahangaika kujitoa kisha tunarudiana, hatukupigana sana lakini watu walijaa. Nikaona najiaibisha nikatoka na kuondoka zangu.
Nilirudi nyumbani nikiwa na hasira sana, nilikua najua mwanaume wangu ni malaya lakini si kwa kiwango cha kumruhusu mwanamke kuingia dukani kwangu. Nilijiapiza kumuacha lakini kabla sijafanya chochote mlango uligongwa, walikua ni Polisi wakiongozana na yule dada, alikua na RB yangu kwa madai kuwa nimeenda kumvamia dukani kwake, nimemfanyia vurugu na nimemuibia pesa zote za mauzo ya siku hiyo milioni 12.
Kwanza nilishangaa kama kuna mauzo ya namna hiyo, kila siku Abdul alikua analalamika kuwa hakuna Biashara sasa nilishangaa ni kwa namna gani kuuza kiasi kile?
“Duka ni la kwangu huyu ni malaya tu anatembea na mume wangu!” Niliwaambia askari kwa dharau wkani nilikua na uhakika kuwa duka ni langu wala si la mwanaume. Hakukua na kitu chake pale.
“Kwa taarifa yako huyo mjinga mwenzako akirudi wote mnaondoka dukani kwangu!” nilizidi kuongea kwa kujiamini.
“Dada una uthibitisho wowote kuwa duka ni lako, maana huyu naye anasema ni duka lake na wewe ulienda kumfanyia vurugu?” Askari mmoja aliniuliza. Sikutaka kumjibu kwa maneno, niliingia ndani na kutoa Tin namba yangu na mikataba ya kulipia kodi ya nyumba ya il sehemu.
“Mbona nyaraka za zamani hivyo?” Aliniuliza, nilimuambia vitu vingine vipo dukani, tuliongozana mpaka dukani. Kufika yule dada alichomoa TIN namba ukutani na kuwaonyesha, ilikua si TIN namba binafsi bali ilikua ni ya kampuni.
Sikujua kuwa kumbe mwanaume wangu alishabadilisha kila kitu, alifungua kampuni ambayo yeye na huyo dada walikua wakimiliki asilimia thelathini kwa thelathini na nyingine arubaini ziligawanywa kwa watoto wawili.
Kusema kweli nilihisi kuchanganyikiwa kwani sikuwa najua hicho kitu, alionyesha usajili wa Brela na yeye alikua kama mkurugenzi mimi hakua na jina langu popote. Sikuamini kwanza kama yule mwanaume anaweza kunifanyia hivyo lakini pia sikuamini kama anaweza kuwaza hata mambo ya kampuni.
Nilimchukua akiwa hana kitu, hajui kitu chochote kuhusu Biashara, ameishia Darasa la saba nikajua kuwa nitaweza kumdhibiti lakini kanigeuka.
“Hili ni duka langu, huyu mwanamke alikua anatembea na mchumba wangu huko nyuma, amesikia naolewa anajifanya kutaka kuja kunisumbua. Amekaa na mwanaume miaka minne hata kumzalia kakataa mimi nimemzalia na kwao wananijua, amekuja kunipiga dukani kwangu na kutuibia milioni kumi na mbili!”
Aliongea kwa hasira, ni kama nilipigwa shoti kwani kila kitu kilikua ni kigeni kwangu. Kwanza nilijua kuwa mchumba wangu situ ana mwanamke mwingine lakini pia wamezaa watoto wawili. Lakini pia alishaninyang’anya Biashara, historia ilikua inajirudia, nilikua namuamini kwakua hajasoma hatanisumbua lakini ndiyo hivyo, ana mwanamke mwingine na karibu kila mtua likua anajua ila hawakuniambia. Nilikamatwa na kupelekwa Polisi ambapo nilifunguliwa kesi ya kinai kwa kumpiga pamoja na wizi wa pesa.
AMINA; NITAJIUA SIKU YANGU YA KUZALIWA IKIFIKA ILI WASHEREHEKEE VIZURI—SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE; Amina anaamua kumtafuta kijana ambaye hana elimu na kazi ya kueleweka akiamini huyo ataweza kumkontrol na kuishi naye vizuri. Lakini anambadilikia, anabadilisha majina ya Biashara zake na anagundua kuwa ana mwanamke mwingine wamezaa watoto wawili, anakamatwa baada ya kwenda dukani kwake na kutuhumiwa kuiba milioni saba…
NIKUKUMBUSHE; Kuna matapeli wengi wanatumia majina yangu Instagram wamebadilisha herufi tu. Unapomuelekeza mtu katika ukurasa wangu kumbuka nina aakaunti moja tu ya Instagram ya @iddimakengo na akaunti ya kampuni @aziranigroup sina nyingine.
Pia nina namba mbili tu ambazo ukilipia jina linakuja Iddi Makengo, M-Pesa 0742-381-155 na Tigo Pesa 0657-552-222 nyingine zote ni Matapeli namba yangu ya Whatsapp ni moja tu 0742-381-155. Siunganishi watu uchumba na wala siombi kutumiwa picha kwaajili ya kuunganisha watu uchumba…. ENDELEA…
Nilimuona mjinga, nilimuona kwakua hajasoma, hana uwezo basi atakua wakwangu tu. Niliamiani kuwa kwakua alikua hana kitu basi hawezi kuniacha. Lakini haikua hivyo, nilijikuta nalala mahabusu kwaajili yake. Nisingekua najuana na baadhi aya watu waliokua wanajua kila kitu wangenifungulia kesi ya wizi na Abdul asingehangaika kabisa na mimi.
Siku ya pili nilitoka mahabusu ndipo niligundua kuwa, mchumba wangu hakua kasafiri, alipanga njama na mwanamke wake akijua kabisa kuwa nitaenda pale lengo lilikua ni kunipa kesi na kunifunga. Walifoji vitu vingi lakini katika maisha kuna wakati ukijuana na watu inasaidia. Kuna Mama mmoja ambaye alikua ni mwenye nyumba wangu wa kwanza, sikujua ana cheo gani ila aliposikia kuwa kuna kitu kama hicho aliniita nikamuambia kila kitu.
“Unataka nini?” Aliniuliza, nilimuambia kuwa ninachotaka mimi ni vitu vyangu kwani nimewekeza sana kwa huyo mwanaume na kanidhulumu Biashara zangu.
“Narudia, unachotaka ni nini kwani mabinti wa siku hizi hamueleweki, unaweza kuwa una hasira hapa kumbe umekasirika kwakua umenyang’anywa mume, nataka nijue nakusaidia nini?” Aliniuliza tena, nilimhakikishia kuwa simhitaji huyo mwanaume, ingawa nilikua bado nampenda, nilikua naumia kwa kupotezewa muda lakini nilikua tayari kabisa kumpoteza angalau nibaki na biashara zangu.
Katika zile Biashara kila kitu nilikua nimesajili kwa majina yangu, mwanzoni kabisa mimi ndiyo nilikua na mikataba na mwenye nyumba na nilikua nikilipa TRA. Nilikua na leseni ya Biashara na TIN Namba ilikua ni yakwangu. Mikataba na mwenye nyummba nilikua nikipeleka TRA nalipia na ile asilimia ya mwenye nyumba. Mama aliniomba vielelezo mpaka mwisho wa mimi kulipia TRA. Kuna miaka miwili ambayo nilikua sijalipia, hiyo ndiyo miaka ambayo nilimuachia Abdul kila kitu.
Alichoniambia yile Mama ni hivi, “Wanaweza kuwa wamefungua kampuni, wanamiliki kampuni lakini haimaanishi kua wanamiliki kila kitu. Kampuni ni jina, unapeleka TRA unapewa TIN namba lakini ofisi inaweza kuwa popote. Wao wana kampuni, lakini wewe unamiliki duka, na katika hilo duka ulilipia kodi ya miaka minne. Haijaisha, najua walikuzunguka na kwenda kusalini mataba mwingine na mwenye nyumba.
Ila mkataba wako ulikua haujaisha hivyo kama mwenye nyumba alitaka kukuondoa basi angekupa notsi na kuvunja mkataba, hawakufanya hivyo kwa maana hiyo walichosaini ni batili, hakuna mkataba juu ya mkataba.”
Nilikua namuona yule Mama kama mtu mjinga, si Mama yaani niseme ni Mbibi ambaye alikua ni mtu mkubwa sana huko nyuma na alikua anajua mambo mengi. Kwanza alinaimbia niende TRA, nikakadiriwe kodi ambayo nilikua sijalipa kwa miaka miwili, akaniambia nilipe na faini kisha nilipie na ile kodi ya mwenye nyumba anayopaswa kulipa, nikitoka hapo nichukue Polisi na kuwatoa dukani kwangu.
Wao kubandika jina la kampuni, kuweka ujinga wao wa BRELA haimaanishi wabnamiliki kitu, kama huyo mwanaume atasema vitu ni vyake basi itabidi kuonyesha kuwa alivipata wapi. Ni kwa namna gania litoka kwenye bodaboda mpaka kumiliki Biashara kubwa kiasi hicho. wewe ni mfanya kazi, ulishachukua mikopo mingi hivyo una uwezo kudhibitisha.
Yule Mama ainisaidia kila kitu, kweli nilifanikiwa, Abdul na mke wake hawakua na chakuongea, ilionekana ni kama walichukua makabrasha yao na kuja kutundika dukani kwangu. Nilimfukuza na kuchukua kila kitu changu, kitu pekee amabcho nilishindwa kuchukua ilikua ni nyumba ambayo alijenga Kijijini kwao.
Nilimshukuru sana yule Mama, Biashara zangu zilibaki, ingawa niliyumba sana lakini angalau nilikua na kitu. Sikumuona tena Abdul, ni kama walikimbia mji kwani sikuwasikia tena, hata mimi nilichoka kuishi pale, niliona kama nina gundu na kuamua kutafuta uhamisho, nikahamia Iringa na kila kitu changu ili kuanza maisha upya nikiamini kila kitu kitakua sawa.
****
Umri ulikua unaenda lakini sikua na hamu tena na wanaume. Nilishakata tamaa kabisa na wanaume, niliamua kuchagua vitu viwili, kwanza ni kumtumikia Mungu wangu na pili ni kutafuta pesa na kusaidia ndugu zangu. Nilisahau kabisa masuala ya wanaume nikaamua na kusema kuwa sihitaji tena mwanaume, ingawa nilikua na hamu sana ya kupata mtoto lakini kwa mambo niliyopitia sikua nikihitaji kuolewa.
Biashara zilikua zinaenda vizuri, nilikua nafanikiwa, nasaidia ndugu zangu, nawasomesha wadogo zangu, nilikua na furaha, sikutaka kuwaza kabisa kuhusu wanaume. Lakini siku moja Mama yangu alinipigia simu, aliniambia kuwa hali yake si nzuri hivyo anataka kuniona. Binafsi nilikua najiona kama mtoto anayependwa sana nyumbani kwa wakati huo kwani mimi ndiyo nilikua na kipato kikubwa kuliko hata Kaka zangu na katika matatizo mengi nilikua nikiambiwa mimi.
Mama yangu alikua ndiyo kila kitu kwangu, mtu anayenipa furaha na kila wakati nikihisi kuchanganyikiwa kidogo nilikua nikiongea naye nakua vizuri kabisa. Ingawa sikuwahi kumuambia kuhusu matatizo yangu na mambo ninayopitia lakini kama nikikwazika nampigia simu naongea naye, ananiuliza kwanini nalia, namuelezea mambo mengine labda matatizo kazini, basi ananipa pole ananifariji basi najisikia vizuri.
Niliposikia kama anaumwa basi nilijisikia vibaya sana, sikua na kitu kingine katika maisha yangu zaidi yake hivyo niliwahsa gari na kuanza safari. Njiani nilinunua kila aina ya zawadi ili tu kumfurahisha Mama yangu lakini haikua hivyo. Kwanza nilifika na kumkuta mzima, alikua zake shambani, mpaka nilishangaa, nikaanza kumshikashika kumuona kama anatatizo lakini naye ni kama alinishangaa.
“Mbona uko sawa Mama?” Nilimuuliza kwa sauti ya juu kidogo kwani alinipanikisha bure.
“UNa gari zuri, badala ya kutafuta mwanaume uolewe unaenda kununua magari, hivi unafikiri ni mwanaume gani atakuoa kama kila siku nikujipitisha na magari kujifanya kama una pesa….”
Mama yangu hata hakuhangaika kujibu swali langu, moja kwa moja alizungumzia mada ambayo inanikera. Haikua mara ya kwanza kwa Mama yangu kuniambia suala la mtoto hivyo nilijifanya kupuuzia.
“Mama nawewe, hutaki hata nikapumzika ushaana mambo yako ya ndoa….” Niliongea huku nikijichekesha, nilijua kuwa yuko siriasi lakini sikutaka kugombana na Mama yangu kwasababu hiyo, nilikua na maumivu yangu ya kuachwa na wanaume sasa kwanini kuhangaika naye.
Baba yeye aliniangalia na kushangaa kwanini nilikua nimeenda, hakuongelea suala la ndoa na kila siku yeye alikua akiniambia.
“Mwanangu siku Mungu akiamua uolewwe atafungua milango yako na Bwana harusia takuja. Hakuna kuwahi wala kuchelewa katika ndoa. Kuna wanaowahi kuoelwa wanaishi ndoa za mateso, wanawahi kuingia kwenye ndoa lakini wanahangaika kupata watoto miaka nenda miaka rudi ila kuna wanaochelewa lakini wanaishia kuwa na furaha. Hivyo najua Mama yako kila siku anakuambia kuwa anataka wajukuu, ila asichojua kuwa ndoa haileti wajukuu ila Mungu ndiyo huleta.”
Alikua akiniambia kwa kunipa moyo, ingawa nilikua naona kabisa kwenye macho yake kuwa anatamani niolewe, niwe na familia yangu lakini hakunisukuma na mara nyingi alikua akigombana na Mama, ndugu zangu, majirani na watu wengine pale anaposikia kuwa wananiambia habari za ndoa.
“Ni salama mwanangu?” Baba aliniuliza, sikumuambia kuwa naenda nyumbani, Mama aliponipigia nilijisahau hata kumuambia.
“Salama Baba, nimekuja tu kuwaona…” nilimdanganya, sikutaka kumuambia kuwa ni Mama aliniita kwani nilishahisi kuna kitu na sikutaka kuwagomabisha.
“Sawa” Aliniambia, Baba yangu si muongeaji sana hivyo hayo maneno yalitosha. Usiku nikiwa chumbani kwangu Mama alikuja, nilikua nishahisi alichokua ameniitia lakini sikutaka kupaniki, niliamua kumsikiliza.
“Hivi unafikiri nafurahia mambo unayonifanyia?” Mama alianza kwa kuniambia.
“Mambo gani Mama, mbona nimefanya nini?” Nilimuuliza kana kwamba nilikua sijui kama tatizo ni nini ila nilitaka tu kurefusha mazungumzo.
“Unajifanya hujui, una kila kitu lakini huna mwanaume, hivi unajua kuwa ni kama una laana?” Mama aliniambia maneno ambayo nilihisi kama vile mtu kanichimbia kaburi na kunifunikia nikiwa ndani. Sikuweza hata kumjibu. Kuna wakati nilijihisi kama nina laana lakini kwa Mama yangu mwanamke aliyenizaa kusema kuwa nina laana nilijihisi kuchanganyikiwa.
Nilibaki kimya bila kumjibu chochote, ingawa nilijikaza sana lakini nilishindwa mazozi yalitoka ka amaji.
“Mdogo wako anataka kuolewa, aliniambia tangu mwaka jana, lakini kwakua niliona wewe bado nikiamini kuwa utaleta mchumba nikamuambia asubiri ila naona kama wewe si wakuolewa, hivi ulishawahi kuwa na mwanaume kweli wewe?” hapo Mama aliongea kama kwa dharau flani hivi, nilijisikia vibaya, nilishazoea maneno kama hayo kutoka kwa mashoga zangu lakini kutoka kwa Mama yangu mzazi iliniuma sana.
“Mama kwanini unasema hivyo unajua wewe ni Mama yangu?” nililazimika kumuuliza, nilipandisha sauati juu kidogo.
“Sijui una matatizo gani lakini naona mikosi yako inataka kumuathiri mdogo wako, nilimuambia subiri ila naona kama anataka kugombana na mchumba wake na yote ni kwasababu yako…” Mama Aliniambia, nilitaka kumjibu kujielezea lakini hakunipa nafasi.
“Wewe ulishaleta mwanaume hapa lakini akaja akakuacha, sasa mdogo wako naye alileta mwanaume lakini naona anafuata nyayo zako. Wewe si wakuolewa, naona hata utafute mwanaume uzae naye mwanangu uondoe nuks ila mdogo wako ataolewa utake usitake!” Mamka alikua akiongea kwa hasira kana kwamba nilikua nimekataa kwa mdogo wangu kuolewa. Kwanza sikua hata nimesikia kitu kama hicho, mdogo wangu mimi ndiyo nilikua nimemsomesha mpaka kumaliza chuo, alikaa kwangu kwa muda na alikua anajua baadhi ya matatizo yangu, mimi ndiyo nilimtafutia kazi.
Kama ni ishu ya kupata mwanaume mpaka kuolewa basi angeniambia, mimi nisingekua na shida yeye kuolewa kabla yangu. lakini alikua hajaniambia kuhusu kupata mwanaume, ingawa tunaongea mambo mengi lakini hakuniambia kitu hicho, kama Dada yake niliumia kwakua nilimuona kama mdogo wangu anapaswa kuniambia kila kitu.
“Mbona mimi hajaniambia kitu chochote kuhusu kupata mchumba, lakini hata kama angekua naye, kwanini kusubiri, kwani mimi nimemuambia nataka kusubiriwa, nataka aolewe….” Mama hakusubiri hata niongee, alinikatisha na kuanza kunisema.
“Unataka akuambie kama nani? Wewe ni dada yake kweli lakini mwanaume yuko wpai? Si utamuonea wivu, alitaka kukuambia lakini nilimkataza kabisa kuonega na wewe kwani nawewe una shdia zako!”
“Inamaana Mama unadhani naweza kuwa na chuki na mdogo wangu?” Nilimuuliza Mama yangu kwa mshangao kwani ingawa nilitamani kuoelwa lakini hakuna hata siku moja niliwahi kumuomba Mungu kuolewa kabla ya wadogo zangu.
Mama aliongea kana kwamba mimi nilikua namuonea wivu mdogo wangu kuolewa. Kusema kweli sikuwahi kufikiria kama wananichukia kiasi kile, suala la mwanaume kuja kwetu kujitambulisha na kisha kuniacha lilifanya nionekane kama nina mikosi.
“Hivi wangejua niliyokutana nayo wangefanya nini?” nilijiuliza huku nikilia, kila niliopokua nikiwaza namna Mama alivyokua anaongea ni kama alikua anaongea na mtoto wajirani, ule upendo wote niliokua nikiuona usoni kwa Mama yangu ulipotea, alikua akiniangalia kwa chuki kana kwamba nina kitu kibaya nimepanga kumfanyia mdogo wangu.
“Sijaongea na baba yako haya mambo lakini najua kua anakupenda na atataka wageni wakija kujitambulisha kwaajili ya mdogo wako na wewe uwepo…” Alitulia kidogo kama anawaza kitu kisha kwa msisitizao aliniambia.
“Sitraki uje nakupenda lakini sitaki uje, hata mdogo wako hataki uje usije kumharibia, utatafuta kitu cha kumuambia Baba yako. Kuna mambo ya kazi muambie, ndiyo maana nimekuita leo hapa kwani wageni wanakuja wiki ijayo ili ukimuambia Baba yako kuwa huwezi kuja wkakua umekosa ruhusa kazini akuelewe.”
Mama aliniambia, kwa wakati huo nilikua kama sisikii kitu. Nilimkubalia Mama kila kitu huku nikiumia, nilikua nawaza mambo mengi sana, nikihisi labda kuna kitu kikubwa nimekifanya mpaka kufikia kudharaulika kiasi kile.
“Hivi lakini haya maisha yana maana gani, yaani pamoja na kuhangaika na familia yangu namna hii lakini bado hakuna mtu anyenithamini kisa mwanaume?” Niliwaza bila majibu, wakati huo wote Mama alikua akiongea, kikubwa ni alikua ananiambia nisimlaumu mdogo wangu.
“Wewe ni dada yake hawezi kukuambia lakini mimi ni Mama, najua kuwa una mikosi, inaniuma kusema hivi lakini unahitaji kuangalia nyendo zako una waodgo zako wawili. Dad ayakoa liolewa na kutuletea heshima, wewe unatuaibisha kila siku, mdogo wako asipoolewa basi jua ni wewe hivyo baki huko huko utakuja siku ya harusi kama wageni wengine!” Mama aliniambia, niliitikia kwa kichwa huku bado nikilia, Mama hakujali hata machozi yangu, aliondoka huku akisisitiza nisimuambia baba kuhusu sababu ya yeye kuniita.
*****
Nilijua kuwa Mama anaumwa hivyo kazini niliomba ruhusa ya wiki moja na niliipata. Nilijua nitakaa kwa muda mrefu kumuuguza Mama na nilipanga kama nitakuta hali yake ni mbaya basi nitaomba na likizo moja kwa moja kwani nilikua bado sijachukua likizo. Lakini kwa maneno ya Mama nilishindwa kabisa kuendelea kubaki pale, asubuhi nilimbia Baba kuwa kuna dharura, nimeitwa kazini nataka kuondoka.
Baba alishangaa sana lakini Mama ni kama alikua anataka niondoke, ndahani alikua hatakiw atu wajue nimekuja nyumbani au alidhani kama nikikaa muda mrefu basi nitamuambia Baba maneno yake. Baba yangu si muongeaji sana, ingawa alihisi kama kuna kitu lakinia liponiuliza nikamuambia hakuna kitua likubali na kuniruhusu kuondoka. Mama alinifauta kwneye gari hukua kinisisitiza kuwa nisimuambia mtu hata mdogo wangu akiniomba kuja basi nikatae.
“Mwanangu tafuta hata mtu wa kuzaa naye, kama vijana wenzako hakuna tafuta hata mume wa mtu zaa naye basi, umri unaenda, ushafikisha miaka 30, sasa unadhani ni nania takuoa, tafuta mwanaume zaa….” Mama aliniambia, nilimuitikia kwa kichwa na kupanda zangu kwenye gari, sikutaka kuongea chochote. Ingawa nilikua na hamu sana ya kuolewa na kuwa na mwanaume wangu lakini sikujiona kama ni mkubwa sana mpaka Mama yangua lipotaja umri wangu.
Miaka 30 kwake ilikua ni mingi sana na aliona kama nimechelewa, alishanikatia tamaa akiamini kuwa sitapata kijana wakinioa, yaani Mama yangu mzazi ananiwazia hivyo. Niliwaza sana lakini sikupata jibu, niliingia kwenye gari na kuondoka. Wiki nzima ile sikua vizuri kabisa, baada ya kama wiki mbili hivi nakumbuka siku ya Jumamosi asubuhi Baba yangu alinipigia simu.
“Inamaana umeshindwa kabisa kuja kwenye shughuli ya mdogo wako?” Baba aliuliza, kwa namna alivyokua anauliza ni kama alikua anahsnagaa, alikua haamini, yaani ni kama alikua ananisuta flani. Yaani ni kama alikua ananiambia hata kama wewe hujabahatika kuolewa lakini hukupaswa kumsusia mdogo wako shughuli. Kusema kweli sikua najua kilichokua kinaendelea, ni kweli Mama aliniambia kuwa mdogo wangu ataletewa mahari lakini hakuwahi kuniambia kama ni siku gani.
Nilikua naongeana Mama kila siku lakini hakuwahi kuniambia, nilikua naongea na Baba kila siku lakini hakuwahi kuniambia. Dada yangu pamoja na mdogo wangu aliyekua akiolewa naye hakuniambia ingawa nilikua naongea naye kila siku na wiki moja kabla aliniomba nimkopeshe laki tano, hakuniambia ni za nini lakini kwakua Mama alishaniambia kitu kama chicho kuhusu kuolewa nilimpa bila kuuliza kitu.
“Mama yako aliniambia umekasirika lakini sikudhani kama ni kwa kiasi hiki. Mwanangu, chuki inafunga milango mingi. Una miaka 30, wewe bado ni mdogo, kila siku nakuambia kuwa siku yako itakuja kufika lakini kama unataka kufanikiwa basi furahia mafanikio ya watu wengine….” Baba aliniambia, kusema kweli sikumuelewa mpaka alipoendelea.
“Ulimuambia Mama yako utakuja, mdogo wako alijua utakuja, ndugu wote wapo hapa kasoro wewe tu, hivi utaleta picha gani kama huji. Nilitaka nikuambie lakini Mama yako aliniambia una hasira unajisikia vibaya ataongea na wewe. Lakini kwa majibu uliyompa Mama yako na leo nakupigia simu unasema umebanwa na kazi huwezi kupata ruhusa kweli binti yangu…”
Baba alizidi kuongea, niliwaza kumuelewesha na kumuambia kilichotokea lakini niliona haitasaidia. Ingezidi kuleta ugomvi kwa kumgombanisha yeye na Mama. Kumbuka hawakuniambia kitu chochote, Baba aliongea maneno mengi ya kuonyesha kukatishwa tamaa na jinsi nilivyosusia sherehe ya Mahari ya mdogo wangu, mimi nilibaki kimya tu mpaka alipokata simu. Nusu saa baadaye nikiwa sijui nini chakufanya simu yangu iliita, alikua ni mdogo wangu aliyekua anaolewa.
“Dada naomba niolewe kabla yako….” Aliniambia, nilijisikia vibaya kwani kwa namana livyokua anaongea ni kama alikua na chuki na mimi. Nilishangaa ni kwa namna gani ningeweza kukasirika kwajaili ya kitu kama kile.
“Olewa mtu mdogo wangu mbona hakuna shida yoyote!” Nilionega kwa sauti ya juu kidogo, kusema kweli nilikua siwaelewi.
“Nashukuru Dada leo naletea mahari, nataka siku yangu iwe nzuri, naomba usiniharibie Dada.”
Kabla hata ya kumuuliza ni namna gani nitamharibia, kabla hata ya kumuambia hongera alikata simu. Nilijaribu kumpigia simu lakini hakupokea, nilimpigai Dada yangu naye hakupokea, Mama naye hakupokea, nikampigia simu Kaka yangu ambaye tulikua hatujaongea muda mrefu, alipokea, naye alikua nyumbani, nilimsalimia lakini hakuongea sana, alijifanya yuko bize kisha akakata simu.
Kusema kweli nilijihisi kuchanganyikiwa, niliwaza hivi suala la mimi kuolewa ni kubwa namna hii? Nyumbani kulikua na sherehe na ukiangalia ni pesa yangu kwa kiasi kikubwa ndiyo iliandaa hiyo sherehe. Ingawa sikujua inafanyika lini, Mama alinificha lakinia laikuia akiniomba pesa ya vitu vingine vya ajabu ajabu nampa nikijua kuwa ni kwaajilia ya mdogo wangu lakini hawakutaka niende.
Niliwaza sana, nilijisikia vibaya, niliona kama dunia imenitanga, hivi kweli kukosa mwanaume ndiyo kunawafanya ndugu zangu kunitesa namna hii? Nikiwa nawaza nini chakufanya nilipigiwa simu na Mtoto wa Shangazi yangu, ni binamu yangua mabye ni kama Dada yangu, tumekua pamoja na tumeshibana.
“Shogaa ndiyo nini kumsusia mdogo wako shughuli… nipo na Mama hapa anatamani hata kulaia anatamani ungekuepo…” kusema kwlei nilizidi kuumia, yaani Binamu yangu anaalikwa kwakua tu ameoelwa wakati mimi Dada mtu sijaalikwa na kila mtu ananilaumu?
Alimalizia kwa kunipa moyo, hukua kiniasa nisiwe na hasira kwani na mimi ipo siku nitapata mtu wangu. Siku mjibu kitu kwani nilishachanganyikiwa, hata simu sikujua kama nimekata. Niliingia jikoni na kuchukuua kisu kisha nikarudi nacho sebuleni. Nilikua sijielewi na nilikua sioni njia.
Amina anaonekana kuchanganyikiwa, kachukua kisu, anahisi kila mtu kamtenga hana rafiki na hata wazazi wake wamemtenga, unafikiri atafanya nini? Basi usikose pia usaisahau kumkumbusha rafiki yako kuwa, kuna matapeli wengi wanatumia Jina la Iddi Makengo hivyo awe makini, siunganishi watu uchumba, siombi picha za kukuunganishia kwa mwanaume.mwanamke na ukilipia jina lisipokuja Iddi Makengo basi huyo ni tapeli, instagram nina akaunti moja tu @iddimakengo.
AMINA; NITAJIUA SIKU YANGU YA KUZALIWA IKIFIKA ILI WASHEREHEKEE VIZURI
Nilichukua kile kisu nikiwa sijui nifanye nini? Nilijihisi maisha yangu yameisha hivyo niliona kama nina wajibu wa kufanya kitu.
“Bora kufa sasa vitu vyote hivi vina maana, gani, kama ndugu zangu mpaka Mama yangu mzazi ananichukia, Baba yangu ambaye alikua akinipa moyo kila siku ananichukia kuna haja gani ya kuishi? Miaka 30 nimekua ni mtu wa kuachwa tu, hapana lazima kufa!”
Niliwaza huku nikinyanyua kisu mna kutaka kujichoma tumboni, lakini mikono iligoma, nilikua natetemeaka kama nimemwagiwa maji ya baridi. Nilijikuta nazidi kupandwa na hasira kwa kushindwa kujiua, nilichukua kile kisu na kukirusha kwenye TV, nikaanza kuvunjavunja vitu mule ndani, nilivunja karibu kila kitu huki nikiwaza, vina faida gani hivi kama nimeshindwa kupata mwanaume?
Baada ya kumaliza kuvivunja nilitoka ndani, kwa kawaida mimi ni mtu wa kukaa ndani tu, huwa sina mambo mengi, usiku nilikua natoka na mpenzi wangu na kama hayupo nakaa ndani. Nilitoka na kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilikunywa pombe. Nilifanya hivyo ili kujiondolea mawazo, nilikunywa bia mbili lakini sikusikia chochote,ingawa ilikua ni mara yangu ya kwanza na niliamini labda nitalewa sana lakini hata sikusikia kitu chochote.
Asubuhi niliamka kawaida kabisa lakini cha ajabu nilikua najisikia vizuri, nilikua naona kama vile maisha yangu yamebadilika na sihitaji tena wanaume. Kuna kafuraha nilikua nako mpaka nikahisi kuwa mimi ni mtu mpya kabisa.
“Labda Pombe ndiyo dawa, hakuna haja tena ya mwanaume, ni Pombe tu!”
Kwakua ndiyo nilikua naanza kunywa pomnbe sikutaka watu kuniona, mtaani nilikua na kaheshima flani hivyo nisingepata uhuru, basi niliwasha gari yangu na kuanza safari ya kwenda Doddoma. Ni muda mrefu nilikua nikisikia kuhusu Bata za club, wakati nasoma chuo nilikua nikiwaona rafiki zangu wakitoka lakini mimi sikuwahi kufanya hivyo.
“Huu ndiyo wakati wangu, sitaki tena wanaume, nataka kula maisha!” Nilijiambia, njia nzima nilikua nawaza kuwa na furaha, nilifika Dodoma na kushikia katika hotali nzuri, lakini wakati nikijiandaa ili kutoka simu yangu iliita. Alikua ni Baba yangu, nilitaka nisipokee lakini nilijikuta napokea.
“Nisamehe mwanangu kwa maneno yangu ya jana, hukufanya sawa lakini sikupaswa kukuambia hivyo, sijui unayopitia hasa mambo ya kazi….” Baba aliniambia, alikua akiongea kwa upole sana, ni kama kuna kitu kilikua kinamuumiza.
“Vipi Baba mbona unaongea hivyo?” Nilimuuliza, yeye alizidi kuniomba tu msamaha ingawa niliumia sana kutokana na Maneno yake lakini sikutaka kumuonyesha. Nilijifanya kama ni kitu cha kawaida, sikutaka kumuumiza Baba yangu.
“Baba mbona hakuna shida….” Nilimjibu huku nikibubujikwa na machozi, nilijaribu sana kuzuia sauri yangu isiwe ya huzuni lakini haikua hivyo, Baba alinisikia.
“Najua upo katika wakati mgumu sana, jana nilikua naongea na Mama yako. Mwanangu kuolewa ni mipango ya Mungu. Acha kumsikiliza sana Mama yako, unajua nyie wanawake mnapaniki sana, yaani mambo mdogo yanawaumiza sana. ngoja nikuambie kitu kuhusu Mama yako, baada ya kumuoa Mama yako alichelwa kupata mtoto, mimi sikuona tatizo, ilikua ni miaka miwili tu lakini Mama yakoa lichanganyikiwa. Alikua akiwaza maneno ya watu zaidi, alikua akiwaza kuhusu wazazi wangu, mimi nilikua nampenda, nilimuambia hakuna haja ya yeye kuumia lakini Mama yako hakunisikia.
Najua anakupa wakati mgumu kuhusu kuolewa, lakini wewe bado ni binti mdogo sana, kwanza mzuri, una akili ya kichwani na ya maisha, una kila kitu ambacho mwanaume anakiitaka, mwanangu, ni wakati wako bado tu haujafika.” Baba aliniambia, tuliongea sana na Baba siku hiyo, ingawa hakuniambia lakini nilihisi lazima kuna kitu tu Mama kaongea ndiyo Baba akagundua kwua mimi sikufanya makusudi kutokuenda kwenye shughuli ya mdogo wangi, kila wakati alikua akinisisitiza kuwa nisimsikilize Mama ndivyo alivyo.
Alinielezea jinsi shughuli ilivyokua, mwanaume ambaye mdogo wangu alimpata na kuniambia mambo yote waliyokua wamepanga. Nilipojua kuwa Baba ameongea na Mama na Mama alikua akiniongelea mambo mabaya hataki nihudhurie shughuli ya mdogo wangu ni pale Baba aliponiambia.
“Mimi ni Baba yako, hii ni nyumba yangu, hapa ni kwangu, hata kama hawataki lakini utashiriki kila kitu mwanangu, hakuna wa kukutenga….” Baba hakupanga kunaimbia maneno hayo lakini alionekana kukasirika sana hivyo kujikuta anaongea.
“Achana na Mama yako mwanangu, naamini ipo siku atameza maneno yake, musimsikilize kitu chochote!” aliniambia, tuliongea sana kisha akakata simu. Baada ya kuongea na Baba kila kitu kilibdilika, ile furaha niliyokua nayo ya kuwa huru ilipotea kabsia. Ingawa Baba aliongea kwa nia ya kuniponya lakini nilihisi kuwa nahitaji kulinda heshima yangu, ni kama Baba alinipa mzigo mwingine wa kuhakikisha kwua najilinda na kuwa mke mwema.
Nguvu za kutoka ziliniishia, nilijikuta naagiza chakula palepale chumbani, nikalala mpaka asubuhi nikarudi zangu Iringa. Maisha yalirudi kama zamani, mawazo ya ndoa yalikua mara mbili zaidi yake, mdogo wangu alikua anaolewa wakati mimi sina hata mwanaume. Mipango ya ndoa iliendelea, mimi sikushirikishwa kwa kitu chochote zaidi ya kutuma pesa tu, walikau wakihitaji pesa zangu lakini hawkautaka hata niwepo kwenye kamati.
Kila nikisema sina Mama alikua akilalamika, hata hakuficha, alikua akiniambia kuwa nina chuki kwakua mdogo wangu anaolewa.
“Chuki haijengi, kama hutafungua moyo wako mdogo wako ataolewa lakini utaendelea kuumia. Acha chuki mwanangu!” mama aliniambia, nililazimika kusimamisha baadhi ya Biashara zangu ili tu kugharamia shughuli ya mdogo wangu kwani sikutaka kuonekana kama ninachukia yeye kuolewa kabla yangu.
****
Ilikua harusi kwa mdogo wangu, ilikua sendoff lakini kwangu ulikua kama msiba. Kila mtu alikuepo kama dada wa bibi harusi nilipaswa kwua karibu naye lakini haikua hivyo.
“Utakaa huko jikoni na wengine, hapa chumbani atakaa dada yako!” Mama aliniambia mapema kabisa, alikua anaamini kama nikikaa karibu na mdogo wangu nitamtia mikosi.
Kusema kweli nilishamzoea Mama hivyo sikua na sbabau ya kubidhana naye, nilimkubalia na kurudi zangu jikoni.
“Tunasubiri yakwako sasa, mdogo wako kashakufungulia njia.” Shangazi yangu aliniambia ile tu naingia jikoni.
“Ila mwanangu ndoa ni ibada, si kila mtu anabahatika kupata hiyo nafsi, umri umeenda kama unaona hakuna njia tafuta mtu na zaa naye tu!” Aliongea kama kashanikatia tamaa, si yeye peke yake, karibu kila mtu katike ile harusi aliniuliza kuhusu kuolewa kwangu.
Hata wale niliokua nikifahamu kuwa ndoa zao ni za tia maji tia maji nao wlaininanga, sikua na amani, kila mtu utaolewa lini. Nilijiona mkubwa sana, nilijiona kama mtu aliyeyakosea maisha, nashukuru Mungu harusi iliisha salama. Sasa nyumbani kwetu kukaw akumebaki mabinti wawili, mimi na mdogo wangu wa mwisho wakiike ambaye yeye bado alikua chuo ndiyo anamalizia hivyo kila mtu alikua akiniangalia mimi.
Simu za kila siku za Mama kuniuliza kuhusu mtoto zilizidi, hakua akiniuliza tena kuhusu ndoa, alishanikatia tamaa hivyo alikua akiniambia wazi nitafute hata mume wa mtu nizae naye maisha yaishie hapo.
Ndugu wengine nao nilikua sitamani hata kuongea nao, tofauti na Baba na Kaka yangu hakuna ndugu mwingine ambaye ningeweza kumpigia simu ili kuongea mambo ya kawaida tu asiniulize kuhusu ndoa. Niliboreka zaidi na mdogo wangu, ni kama alikua ananiwekea status kwani kila nikiingia ni kumpost mume wake na kusifia ndoa yake, yaani nilijihisi kuchanganyikiwa.
Ukimpigia simu unataka kuongea naye mambo ya kifamilia au unataka kumsalimia utasikia mume wangu hiki mume wangu kile. Yaani mume wangu inakua mume wangu mpaka unatamani kukata simu ila unavumilia ili tu usionekane kama una chuki.
Maneno ya Mama yaliningia kichwani, nilishajikatia tamaa, kila mtua likua ananikatisha tamaa. Kazini ni kama nilitengwa hivi, wasichana wadogo ambao walikua hawajaolewa walikua wananiona kama mzee, wananiona siwezi kuongea kitu nao na wale wa umri wangu kwanzw alikua wakiniogopa. Mazungumzo yetu na urafiki wetu ulikua ni wa kazini tu, walikua hawawezi kunikaribisha makwao kwakua tu wana ndoa na mimi sina hivyo walihisi labda nitawachukulia waume zao.
Yaani yalikua ni manyanyaso mwanzo mwisho, hata katika group la kazini la Whatsapp kulikua na Group la wote na jingine la kwao ambalo wamejitenga flani mimi siruhusiwi kuinganishwa. Kitu cha pili ni kuninanga, kila tukikaa wananiambia naiche kuchagua mwanaume ni mwanaume. Yaani niliwaza na kuwazua, hivi hawa ni kwamba hawaoni namna ilivyoshida kupata mwanaume wanaongea mambo ya kuchagua, tangu lini nilichagua, hivi wenzangu walifanya nini mpaka kuolewa ambacho mimi nakosea, nikiangalia uzuri wengi wao niliwashinda lakini nashangaa mimi nipo tu hata mtu wa kuniambia umependeza hakuna.
Hali hiyo iliniumiza sana, nilikua mpweke, nikaweka shauri kuwa nitazaa, sijali kama ni mume wa mtu, sijali tena kitu chochote ninachotaka ni kuwa na mtoto basi angalau na mimi niheshimike. Si kama nilikua sitongozwi, nilikua natongozwa na mara nyingi ilikua ni waume za watu, nilikua nikiwakata kwani mwanzo nilikua na matumaini kuwa na mimi nitapata wangu, lakini baada ya kuona hakuna namna ya mimi kupata wangu niliamua kumkubali yoyote.
Nilibadilisha vigezo, nikaacha kuwaza kuhusu mwanaume ambaye anaweza kunioa na kuamua kutafuta mwanaume yoyote yule ambaye anamvuto bila kujali tabia zake, kujali kama ameoa, nikajiambia tu nataka mbegu nzuri. Nilijiambia hivyo kila siku mpaka nikaona kama ni kitu cha kawaida, katika kuhangaika hangaika nikakutana na Kaka mmoja.
Nilikutana naye kwneye mtandao wa Facebook, mimi si mtumiaji sana wa mtandao huo hivyo nilikua natumiwa meseji nyingi huko lakini sizioni, baada ya kuwaza kuhusu kuolewa ndipo niliamua kuingia Facebook kutafuta mwanaume wa kuzaa naye.
Alinivutia hivyo nilimjivu vizuri, madai yake nikuwa alikua kao lakini yeye na mke wake wametengana, si kwa kutengana kuachana hapana, walikua wametengana chumba kwakua alishamfumania meke wake zaidi ya mara tano hivyo amebaki kwaajili ya watoto. Alinipa stori nyingi lakini kwakua mimi nilikua najali kuhusu mtoto sikujali kitu, alikua na muonekano mzuri tena sana hivyo niliona kama atanifaa. Hakuniambia kuhusu kazi yake, alikua kama anajificha ficha, kama mtu anayefanya kazi nyeti, alikua ananiaminisha kuwa labda ni mwanajeshi au usalama wa taifa.
Kila nikiongea naye kidogo utasikia hembu nitakutafuta kuna msafara wa kiongozi, mara nyingine utasikia nipo kwenye oparesheni maalun sitapatikana kwa wiki nzima. Hakuambii anafanya kazi gani lakini wewe mwenyewe unajiongeza kuwa huyu mtu ni mtu muhimu na yuko wkenye mfumo, basi unakaa kimya. Kwakua akipatikana anakua mchangamfu, mnaharit mpaka usiku na katika kukuaminisha kuwa yeye na mke wake hawako vizuri alikua anaweza kukupigia video call hata saa nane usiku.
Kusema kwlei mimi nilikua sihitraji kuaminishwa, nilishakata tamaa lakini yeye alikua analazimishia kama vile ananipenda mimi sana hivyo anatak kujua kama namsaliti au la. Kwakua sikua na kitu cha kuficha nilikua naamka, napokea video call zake kisha nalala, anafurahi na maisha yanaendelea. Alikua anapenda sana kutumiwa picha za uchi, kwakua nilikua sijamjua nilimuambia mpaka tujuane kwanza, hakukasirika, alikua ni mtu poa sana.
Yeye alikua anaishi dar lakini alikua ni mtu wa safari safari sana, mara atakutumia picha yuko Dodoma, mara Mwanza, mara Arusha yaani kwa kifupi alikua hatulii. Tukiwa tuna mwezo mmoja tangu kujuana aliniambia anasafari ya kikazi Iringa, hakuniambia ni safari gani kwani hata hakuniambia kama anafanya kazi gani lakini aliniambia kuwa anataka kuja niwe mwenyeji wake.
Sikutaka ashukie kwangu naye hakulazimishia, alikuja tukaonana, kwelia likua ni kijana mzuri, ana miaka 35, ameoa na ananiambia wana mtoto mmoja ila ndoa yao haina amani, ananiambia kutokana na kazi zake za kusafiri basi mke wake anaingiza wanaume mpaka ndani lakini hawezi kumuacha kwani wana mtoto na anampenda sana hivyo wametengana vyumba.
Siku ya kwanza tulikutana hotalini, na nilichokipenda kwake zaidi ni kujali, alikua akijali afya yake akaniambia tupime kwanza, nilifurahi kwani wote tulikua salama. Baada ya hapo kila mmoja akwa huru kivyake, alikaa hotlini kwa siku tatu, lakini kuna siku nilienda kumsalimia hotelini kwake. Nilimkuta anagombana na wahudumu kuwa kuna begi lake aliacha humbani halioni na lilikua na vitu vya muhimu.
Alikua anaongea sana, wanagombana, wanatukanana, wahudumu wanamuambia hawajaona kitu ila yeyeansisitiza alikuja na begi na lilikua na vitu muhimu. Nilimsihi sana hasa nikimuambia kuhusu kwenda polisi lakini aligoma.
“baby, kuna nyaraka nyingi sana za siri, kama ikijulikana nimepoteza utakua ni uzembe mkubwa na kazi nitakua sina, yaani nahisi kuchanganyikiwa….”
Aliniambia, alionekana kweli kama ni mtu mwenye mawazo sana, kama mtu aliyechanganyikiwa kutokana na hayo mambo, nilimsihi sana kumsaidia lakinia ligoma. Alianza kuwapigia washikaji zake simu kuazima pesa kwani kadi zake za Benki zilikua zimepotea, nilimuomba kuja kukaa kwangu kwa muda ila aligoma kabisa, kumbuak katika kipindi chote hicho hakuwahi kuniomba pesa wala hakutaka kuja kwangu, mara zote alikua akionyesha kwua anajiweza na hata pesa ndogo ndogo alikua ananipa.
Nilimbembeleza sana kuja kwangu, akakubali ki shingo uapende, alishangaa naishi kwangu na nina nyumba nzuri namna ile, ingawa nilimuambia kuhusu kufanya kazi na Biashara lakini hakujua kuwa nilikua na pesa kiasi kile. Tuliishi pamoja kwa wiki moja kisha akaondoka na kuniambia anaenda mbeya, kweli alienda akakaa wiki moja na baadaye akarudi akaniambia atakua iringa kwa mwezi mmoja hivyo anataka kuhamia hotelini kwakua hayaki kua mzigo kwangu.
Nilikua na malengo yangu kwake, nilitaka mtoto na kwasiku alizokaa kwangu nilijua kabisa ina ujauzito kwakua sikua katika siku zangu za hatari. Richard (sio jina lake halisi) alitaka kuondoka ila nilimuomba kukaa kwangu, nilimuomba nikiamini kuwa nikishabeba mimba yake basi ninamfukuza. Lakini haikua hivyo nilijikuta naanza kumzoea, mwezi uliisha lakini hakuondoka, aliniambia kaongezewa kazi hivyo atabaki Iringa na mimi kwakua nilikua bado sijabeba ujauzito basi nilizidi kufurahia.
Kuna wakati nilihisi labda Mungu anajibu maombi yangu kwania likua anaongezewa muda wa kukaa Iringa na mwezi wa tatu akiwa hapa ndipo nilibeba mimba yake. Mwanzo nilipanga kubeba mimba kimya kimya nisimuambia nihudumie tu mtoto lakini kadri siku zilivyokua zinaenda niliona matumaini ya ndoa, kila siku walikua wanaongea na mke wake wanatukanana, anaomba matumizi wanatukanana nikawa nafurahi labda wataachana na mimi kuolewa.
Nilimuambia kuhusu kuwa na mimba yake na alifurahi, aliongelea kuhusu kuja kwetu kujitambulisha.
“Lakini una ndoa ya kanisani, vipi kuhusu mke wako?” Nilimuuliza, hakuonekana kujali kabisa.
“Nilikua naishi na yule mwanamke kwasababu ya mtoto wangu, lakini kwakua nimepata mwanamke ana akili kama wewe, mzuri basi nahisi nitakua na wewe, nataka nianze mchakato wa Talaka ili nikuoe, haitachukua mdua si unajau mimi najuana na watu wengi.”
Mpaka wakati huo bado alikua hajaniambia anafanya kazi gani ila mara nyingi nikitoka abusuhi natoka naye namuacha mjini na nikirudi namkuta nyumbani, hakunaimbia na mimi sikuchunguza. Mambo yalibadilika baada ya ujauzito miwili. Alikuja na kuniambia kuwa amesimamishwa kazi kwakua muda mwingi alikua anatumia na mimi kuliko kazi.
Kwanza nilishangaa kwani aliniambia kuwa amepangiw akikazi Iringa sasa mimi nahusikaje. Alinilaumu san akuwa nimemharibia maisha yake kisha akaniambia kuwa anataka nimkopeshe shilingi milioni tano afungue biashara. Kwakua nilishajifunza huko nyuma nilimuambia hapana, alikasirika sana ana kuniambia kuwa anondoka, nahisi alidhani kama ananikomoa lakini kwakua nilikua na shidaya mtoto tu basi nilimuambia njia nyeupe ondoka.
Alipoona sijali kuhusu yeye kuniacha alianza kunipiga huku akiniambia kuwa kama anaondoka basi nihakikishe natoa mimba yake. Alinipiga sana hasa sehemu za tumbo huku akiniambia kuwa hataki kuacha mbegu yake nyuma kwani kama akiniacha na mimba yake nitamloga. Alirudisha vitu vyake na kuniambia kuwa hawezi kuniacha mpaka nijifungue achukua mtoto wake au nitoe mimba yake ndiyo aondoke.
AMINA; NITAJIUA SIKU YANGU YA KUZALIWA IKIFIKA ILI WASHEREHEKEE VIZURI—SEHEMU YA SABA
Nilikua na hamu sana ya kupata mtoto hivyo ili kulinda mimba yangu nilikubaliana naye, nikamuambia anaweza kuishi kwangu na kuwa kama mume wangu. Lengo langu ilikua ni aishi kwangu mpaka pale nitakapojifungua basi sitakua na sababu tena ya kuendelea kuishi naye. Niliishi naye kwa mwezi mmoja lakini ni kama niliishi naye kwa miaka kumi.
Mambo yalibadilika, katika kipindi hicho alikua anaongea na wanawake wengi katika mitandao tena mbele yangu. Ilikua ndiyo kazi yake, hakua na kazi yoyote zaidi ya kutongoza wanawake na kuangalia kama wana pesa, alikua anahangaika na wanawake watu wazima ambao anaona wana hamu sana ya ndoa.
Baada ya kama mwezi hivi aliondoka, aliniambia anasafiri kikazi ila mimi nilijua kuwa anaenda kwa mwanamke mwingine. Sikuomuona tena yule Kaka mpaka leo, hata kwenye mitandao ya kijamii sikumuona tena na namba za simu alibadilisha. Kwangu nilishukuru kwani sikua nikihitaji tena mwanaume, nilikua na mimba hivyo kupata mtoto ilikua kama faraja.
Mpaka nafikisha miezi nane nilikua sijamuambia ndugu yangu yoyote kuhusu mimba yangu. Nilikua naona aibu, nilijua watanicheka hivyo sikutaka kujitia stress, nilitaka kufanya kila kitu kimya kimya waje kushtukia nina mtoto. Lakini sijui umbea ulifikaje nyumbani kwetu, siku moja Mama alinipigia simu, baada ya salamu nilishangaa ananiambia.
“Mdogo wako bado hajaolewa ndiyo anamaliza chuo usije kumharibia, kama ukizaa basi zalia huko huko nitakuja kumuona mjukuu ila sitaki majirani wajue kuwa umezalia nyumbani!” mama hata hakuniuliza chochote, hakuuliza kuhusu Baba wa mtoto, hakuuliza kuhusu ninaendeleaje, hakuniambia kitu, niliwaza huyu si ndiyo alikua ananiambia kuwa nitefute hata mjukuu sasa mbona kabadilika?
Aliniambia kuwa hataki hata nimuambia Baba yangu au mtu mwingine yoyote hivyo nikikaribia kiujifungua nimuambie aenda kunihudumia. Kusema kweli niliumia lakini sikua na namna, kama Mama yangu mzazi mtu ambaye kila siku alikua akiniambia nizae kama sijapata mtu wa kunioa ananiambia hivyo ni nani mwingine atanisikiliza na kunielewa?
Wiki moja kabla ya kujifungua mama alikuja, alijifanya kufurahia mimi kuwa na mtoto, alinipongeza na kuniambia nimefanya maamuzi ya maana kwani umri wangu umeenda na angalau ataona mjukuu wake. Nilijilazimisha kufurahi lakini kusema ukweli ilikua ni wiki ngumu sana kwangu, kuna wakati nilitamani hata kumuambia Mama aondoke nibaki mwenyewe.
Bado nilikua nangaika kutafuta binti wa kazi kwani niliyekua naye aliondoka mwezi mmoja kabla alipata mwanaume ambaye alimuoa.
“Umeona hata mfanyakazi wako kaolewa wewe umezalia tu nyumbani?” Nakumbuka baadan tu ya Mma akufika aliniuliza, alijua kua kaolewa kwani yeye ndiyo alinitafutia mfanyakazi, wakati namtafuta sikumuambia kama natafuta binti wa kazi kwaajili yangu bali kwaajili ya rafiki yangu, sikumuambia kwakua sikutaka ajue mambo yangu, naamini hata ni yeye alimuambia kuhusu mimba yangu.
“Ameolewa na injinia kabisa, binti hajasoma lakini kaoelwa, wewe na elimu yako umepewa mimba na mwanaume ambaye hata humjuisijui ni mume wa mtu ndiyo maana unagoma kumtaja?” Mama aliendelea kunichokonoa, ni kama alitaka kujua kuhusu Baba wa mtoto wangu lakini name sikutaka kumuambia, nilijisemea kuwa, kama kweli anataka kujua kitu chochote basi aniulize mimi kama mimi na si kuongea mafumbo.
Kila sikua alikua akiongea kwenye simu na waodgo zangu, hawaambii kama nina mimba nakaribia kujifungua lakini alikua anaongea sana mambo ya ndoa, nilijua kabisa kuwa ananichoma roho.
“Raha ya kuzaa mwanangu ni kwenye ndoa, mtoto awe na Baba sio unazaa zaa tu mtoto hana mbele wala nyuma unazaa kama mbuzi!” nilikua chumbani, Mama yuko sebuleni nikamsikia anaongea tena kwa sauti na mdogo wangu.
Alikua anamuulizia mdogo wangu kuhusiana na mtoto wake, kila siku ndiyo zilikua stori, niliumia sana nikajikuta ni mtu wa kulia tu, kujifungia ndani lakini Mama hata hakujali. Alikuja kunihudumia mimi lakini ukweli ni kama mimi ndiyo nilikua namhudumia yeye, hakua akifanya kitu chochote zaidi ya kukaa na kutuma.
Mimba yangu ilikua kubwa sana kiasi kwamba hata kuinama ilikua shida, lakini nilikua napika, nafua na kufanya kila kazi ya ndani, Mama alikua kama kanisusia. Kusema kweli asingekua ni Mama yangu mzazi basi ningefukuza lakini sikua na namna, alikua ni Mama yangu na alikuja kunisaidia. Kwa bahati nzuri mimba yangi ilikua haisumbui hivyo niliweza kufanya kila kitu peke yangu.
Hata isku ya kujifungua nilienda hospitalini mwenyewe, Mama alikuja baadaye na hiyo ndiyo siku pekee Mama alinipikia uji. Niliambiwa kuwa nitajifungua kwa njia ya kawaida, hata nilipofika na kupimwa njia ilikua vizuri sana lakini ulipofika wakati wa kujifungua ile nasukuma mtoto alishindikana kabisa kutoka, walihangaika sana kwa masaa kama saba hivi ndipo ilishauriwa nijifungue kwa njia ya upasuaji.
Kweli nilifanyiwaparesheni na mtoto kutoka, mwanangu alitoka akiwa hai kabisa lakini sekunde chache baada tu ya kujifungu ahali yake ilibadilika, alikua halii, walifanya kila kitu ili alie na kuweza kupumua kwa njia ya kawaida lakini haikuwezekana, dakika kama tatu hivi mtoto wangu ambaye alizaliwa mzima kabisa alifariki dunia.
Ilikua ni siku ngumu sana katika maisha yangu, kwanza sikutaka ikuamini, nilibaki na mwanangu kwa masaa manne nikiamini kuwa atanyanyuka. Mwanangu, binti yangu ambaye nilishamnunulia na nguo, nilishamuandalia na chumba chake, nilishamfanyia kila kitu lakini alikua hayuko na mimi. Walijaribu kumuondoa mikononi mwangu lakini niligoma, nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa, sikujali kuhusu mshono wangu wala kujali kitu kingine nilichokua ninataka ni mwanangu.
Wakati wote huo Mama alikua pembeni yangu,a likua akiniangalia anaongea na simu zake lakini hakumiambia mtu yoyote yule kuwa nimejifungua mtoto amekufa. Alikua anaingia na kutoka ananiangalia, ananisihi niwaache manesi kumchukua mtoto. Mwisho nilikubali, nilimuambia Mama nataka kumzika mwanangu kwani alikua kazaliwa hai hivyo ni kama watoto wengine lakini jibu aliponipa ni Mungu tu anajua, katika kipindi kile kigumu Mama alizidi kuongea mambo ya kuniumiza.
“Un akaili kweli wewe, hicho kinyago ndiyo tukifanyie mazishi, tena ukome, shukuru hata Mungu huyo mtoto kafa ungetuletea laana kwenye familia yetu, mdogo wako hata hajaolewa unataka kumharibia naye awe kama wewe. Watamzika humuhumu kama wengine na sitaki kusikia kama ulibeba mimba na kuzaa, kama ni kulia ulilia hukuhuku ila usijekutuletea laana zako!
Hili la kuolewa hujalimaliza unataka kutiletea tena na la watoto, hivi unajua watu wakijua kuwa tunazaa maiti mdogo wako hatapata mume!” mama aliongea maneno mengi ya kiniikatisha tamaa, siku ile nilitamani kufa, niliona kama maiaisha yangu yameisha, nikahisi kuchanganyikiwa, Mama hata hakukaa, hakujali, aliondoka baada ya siku mbili akinaimbia hawezi kukaa kuhudumia mshono wakati hata kuzaa siwezi.
“Umeshindwa kuolewa na kuzaa nako umeshindwa!” mama aliniambia hivyo, Kaka niliumia sana kiasi kwamba sikukanyaga nyumbani kwetu tena, hata wakati mdogo wangu wa mwisho anaolewa nilidanganya kuwa nimesafiri nnje ya nchi kikazi ili tu nisiende nyumbani.
Niliambiwa mapema kwani mdogo wangu wa mwisho alikua ni kama shoga yangu, yeye alikua haamini kwenye mambo ya laana na kila siku alikua ananipa moyo akiniambia “Dada ndoa inapangwa na Mungu….” Yeye alikua ni kama Baba nilichangia kila kitu na kila mtua lijua nitaenda lakini si kwenda, niliwaambia nimepata safari ya nnje ya nchi kikazi nikajifungia nzangu ndani na kuzima simu.
Mdogo wangu alinilaumu sana lakini sikua na namna, sikutaka kwenda kabisa nyumbani kwetu. Miezi miwili iliyopita ndipo nilikutana na huyu Kaka, yeye alikua tofauti kabisa na wanaume wengine. Kwanza aliniambia kuhusu yeye kuwa alishawhai kuumizwa sana na wanawake hivyo hataki mpenzi kabisa, aliklua kama mimi, alikua anaingia kwenye mahusiano anaachwa wanaenda kuolewa na watu wengine.
Nilijikuta namuamini kwani nilimuona kama ni mwenzangu, nilimuona kuwa ni mnyonge mwenzangu hivyo kama tukioana basi tutaelewana, nikamuambia stori yangu naye akanipenda, kwakua naye umri ulikua umeenda aliniambia kuwa hakuna haja ya kupiteza muda, alinipeleka kwao na kuniambia kuwa anataka kunoa.
Basi nilifurahi, nikawaambia nyumbani kila kitu kikapangwa, ilikua aje kwetu wiki ijayo lakini jana amenipigia simu an kuniambia tuahirishe nimemuuliza sababu hataki kuniambia, ananiambia shida ni yeye sio mimi. Nilimbana sana lakini hakuniambia nikwanini alikua anataka kuniacha ila hakuniambia kitu chochote. Leo ndiyo rafiki yake akaniambia ukweli.
Aliniambia kuwa huyo mchumba wangu alikua na mwanamke wake waliachana akaenda kwa mwanaume mwingine lakini leo karudi hivyo wamerudiana. Ila alikua ananilalamikia kuwa mimi nimeshazaa na nina mshono hivyo akiwa na mimi hajisikii vizuri, hayo ndiyo maneno yaliniuma Kaka, natamani kufa, sitaki tena kuishi.
Hivi unafikiri nitaenda kuwaambia nini nyumbani kwetu kuwa mwananuem niliyepanga kumuoa kaniacha kwakua nimezaa na nina mshono, kama huyu kaniacha ni nani mwingine wa kuwa na mimi? Kaka niache, nina mambo mengi ni bora kufa kuliko kuendelea kuteseka!”
Amina aliniambia stori yake, nilimsikiliza kwa muda mrefu na kila alipokua akiongea ni kama nilikua nasikiliza sauti za wanawake wengi, kitu alichokua akikipitia ni wanawakwe wengi walikua wanapitia. Kutengwa na jamii kunawafanya wanawake wengi kuona ndoa kama ni mafanikio kuliko kitu kingine chochote kile.
“Umesema una miaka mingapi?” Nilimuuliza, sauti yangu ilijaa matumaini kwani sikuona kama ana matatizo.
“Nina miaka 32 Kaka…” Aliniambia.
“Leo sitakushauri kitu chochote, leo nataka tuongee tu mimi na wewe, kwakua naona kama umechanganyikiwa unaona kama maisha yako yameisha ila mimi kwa uzoefu wangu nikuwa huna tatizo bali unachukua matatizo ya watu na kuishi nayo.
Ngoja nikupe mifano miwili naomba uchague mmoja. Kulikua na vijana wawili, John na Jackson, walisoma pamoja lakini walipomaliza chuo waliomba kazi sehemu moja lakini John ndiyoa liipata Jackson hakufanikiwa kuipata ile kazi Jackson aliumia sana kwani ile kazi ilikua na marupurupu mengi na kulikua na madili mengi, John akanunua Gari na kujenga nyumba mbili za kifahari, maisha yake yalikua ni mazuri sana, ndani ya miaka mitano John alifanikiwa kumiliki biashara kubwa wakati huo Jackson alikua bado hajafanikiwa kupata kazi.
Wote wakiwa na miaka 30, John akiwa kafanikiwa sana alisimamishwa kazi, alikamatwa na kiuwekwa ndani kwa kesi ya uhujumu uchumi, akiwa na miaka 31 John alifungwa kifungo cha miaka 15 jela. Wakati huohuo Jackson alifanikiwa kupata kazi katika shirika moja la Umoja wa Mataifa. Alikua analipwa msahara mkubwa ndani ya mwaka mmoja akafanikiwa kujenga na kununua nyumba kubwa akaoa na sasa anaishi na mke wake.
Miaka 7 Jackson aliteseka katika kupata kazi, Mungua limnyima kazi nzuri akampa rafiki yake Jackson ila baadaye Mungu akampa kazi nzuri na John akaingia kwenye mtego sasa hivi anatumikia miaka 15 jela, je unafikiri kati ya John na Jackson ni yupi ambaye Mungu kambariki sana na je, ingekua ni wewe kuchagua ungechagua maisha ya nani? John au Jackson?” Nilimuuliza, hakufikiria hata mara mbili alinijibu kwa kuniambia.
“Jackson ndiyo amebarikiwa hata mimi ningeomba maisha yake, aliteseka sana lakini ni kama Mungu alikua anamuepushia matatizo.” Aliniambia.
“Sasa ni kwanini unataka kujiua, unaamini katika Mungu?”
“Ndiyo naamini.”
“Unaamini kuwa Mungu anayajua yote na anakupa kile unachostahili?”
“Ndiyo naamini lakini Kaka kwanini hanipi Mume kwanini mimi inakua hivi….”
“Hilo swali jibu lake litakuja kesho, kwaleo itoshe nikuambie tu kuwa, inawezekana ukaona Mungu hakupendi lakini ukweli nikuwa inawezekana Mungu amekuondolea hao wanaume wote kwakua tu anataka kukukinga na kitu flani. Labda alijua kuwa watakuja kukutesa ndiyo maana hajakupa hao wanaume.
Kikubwa kinachokusumbua wewe ni kuhangaika na maisha ya watu ambao wanatamani maisha yako. Nikianza kuchambua ndugu zako wanakusumbua kwa kila siku kuuliza unaolewa nini ndoa zao ni za moto. Hembu sasa hivi mrudishie huyo dada aliyekupa namba zangu hizo dawa, muambie kweli ulikua unataka kujiua lakini umeahirisha, kesho tutaongea tena na usipopona nitamuambia akupe dawa Bure ukajiue ila kesho njoo tuongee….”
AMINA; NITAJIUA SIKU YANGU YA KUZALIWA IKIFIKA ILI WASHEREHEKEE VIZURI—SEHEMU YA NANE NA TISA
“Swali lako la jana lilikua ni kwanini Mungu hanipi Mume?” Nilimuuliza siku ya pili Amina aliponipigia simu.
“Ndiyo Kaka, kwanini amewapa waodgo zangu waume lakini mimi hajanipa? Nimemkosea nini, mimi tangu nikiwa mdogo, tangu niko chuo sijawahi kupendwa, kwanini mimi, najihisi kama nina laana? Hembu niambie kama unadhani mume anatoka kwa Mungu na wakati wa Mungu ndiyo sahihi kwanini mimi hanipi mwanaume?
“Una Miguu miwili?”
“Ndiyo.”
“Mikono?”
“Ndiyo.”
“Macho?”
“Ndiyo.”
“sasa kwanini hujiulizi hili swali, mbona Mungu akakupa wewe mikono, miguu, macho na kila kitu lakini kuna ambao wamezaliwa hawaoni, hawana miguu na wala mikono, kwanini Mungu akupe hivyo vitu inamaana kuna kitu labda ulikifanya au hao ambao hawana hivyo vitu wana laana?”
Alibaki kimya, nilimuambia.
“Mungu anatoa kwa wakati wake na kwa matakwa yake, anajua kila kitu na anajua ni kwanini flani nimpe hiki na fglani ni mpe kile. Lakini tuachane na mambo ya Mungu kwani siwezi kumjibia, siwezi kujua sababu za kuchelewa kukupa mume. Ila kuna swali umeniuliza, unasema hivi kwanini wewe hupendwi kwanini tangu uko chuo hujawahi kupendwa? Si ndiyo hivyo?”
“Ndiyo Kaka, kusema kweli nataka kujua kwanini mimi kila siku ni mtu wa kulialia tu, yaani naumizwa umizwa na wanaume kila siku?”
“Hilo mdogo wangu nina jibu lake, ila kabla ya kukujibu hembu naomba nikuulize swali na naomba unijibu jibu la ukweli kabisa.”
“Sawa Kaka uliza…”
“Umetoka nyumbani, umeenda kwenye Mgahawa, umefika umeagiza chakula, baada ya kuletewa chakula kabla ya kuanza kula kile chakula ukamsikia mhudumu analalamika. Kula tu hiki chakula ni kibaya sana, yaani kila mtu anakikwepa, angalia mchele wake ni ulivunda, uliingia mikojo ndiyo tukapikia, hembu kula tuone kama hutaumwa. Hivi utakula kile chakula au utakiacha. Tena si kama una njaa au huna pesa, hapana, unapesa zako nyingi tu na kuna migahawa kibao, utakula hapo au hutakula.”
“Kusema ukweli sitakula Kaka nitakiacha…”
“Ngoja nikupe mfano mwingine, umeenda kwenye Mgahawa, umeagiza chakula, mhudumu anakuja anakuambia sahani ni laki moja unamuambia sina, anakupunguzia mpaka anakuambia anakupa bure, hamu ya kula ni kama imesha, anakuambia chukua nitakupa na pesa hii ili uchukue hiki chakula ila sikitaki, wewe chukua tu. Vipi utachukua amekupa na pesa?”
“Nitachukua chakula na kuondoka nacho ili nichukue na pesa lakini sitakula kile chakula…”
“Kwanini usile wakati umepewa chakula cha bure kabisa tena na pesa juu.”
“Kaka pesa naipenda lakini mtu anakupa chakula tena na pesa juu, kinaweza kuwa kina simu, hapana, nitachukua tu pesa na kama akiniambia nile ndiyo anipe pesa nitamuambia baki na pesa zako ila chakula cha namna hiyo sili.”
Sasa dada yangu, hupati mwanaume wa kukupenda kwakua, mwanamke ni kama mpishi, na uzuri wake ni kama chakula. Hata mpishi apike chakula kizuri namna gani kama hakipendi chakula chake, anakipondea kila dakika basi hakuna mtu atakuja kula. Katika mfano wa kwanza, ulipokua chuo ulikua hupati wanaume kwakua ulikua unajichukia, ulikua unajinenea mabaua hivyo una huzuni.
Suala la mwanamke kutongozwa mkiwa chuo haihusiani kabisa na uzuri bali namna unavyojiweka, kuna wadada wazuri sana ambao kila mwanaume anatamani kuwatongoza lakini namna wanavyojiweka wanaogopeka. Lakini namna wanavyojitangaza wanajiharibia majina na kuonekana kama hawatongozeki, ni wagumu kumbe hakuna kitu.
Ngoja nikupe mfano, nikiwa chuo kuna dada nilikua nampenda sana nlakini nilikua naona kabisa kuwa si saizi yangu, pia washikaji wengi walikua wanamgwaya sana, lakini nilipofika mwaka wa tatu chuoni naongea naye ndiyo nikajua wakati sisi tulikua tunamuona mzuri anatembea na watu wenye pesa zako kumbe yeye alikua hana hata mwanaume, yaani hata kutongozwa hajatongozwa, so wakati tunaongea namuambia kuwa liakua crush wangu wa muda mrefu anacheka haamini wakati yeye ni mpweke mimi nilikua namuona ni bonge la mtu simuwezi.
Sasa shida inakuja hivi, ulipokua chuoni hukutongozwa kwakua labda watu walikua wanakuogopa, labda mtu anakuona uko siriasi sana anaona utamkataa, wanaume wengi wanaogopa kutongoza hasa mwaka wa kwanza chuoni kwakua wanaogopa kukataliwa. Ulipozoea chuo badala ya wewe kuona kawaida basi ukaanza kuwa mpweke, ukaanza kujihisi kuwa una matatizo, kwanza ukaanza kujinenea mbona wenzangu wanatongozwa sana mimi si mzuri, mimi nina shida, mimi niko hivi mimi ni ko vile.
Hapo ni kama mpishia anakisema chakula chake kibaya, haikuishia hapo ukaanza na kutangza, ukiongea na rafiki zako unalalamika hujawhai kutongozwa, unalalamika unatamani kuwa na mwanaume, unawaonea na kawivu. Hapo ulijilevo mwenyewe kuwa wewe ni mbaya hupati mwanaume, yaani hata kama unegkua huwapati kweli ulipaswa kusema hujaamua kwa wakati huo na si kwakua hutongozwi.
Ndiyo maana rafiki zako wakawa wanakulazimishia kwa mtu yoyote kwakua ulishajitangaza kuwa wewe hupati mtu. Lakini turudi kwa mpishi kwenye mfano wa pili, alipokuja mwanaume wa kwanza, badala wew ekuwa kama chakula yeye ndiyo aje kukuhangaikia basi ukaanza kujilazimishia kwa mwanaume, wewe ndiyo unamhonga mwanaume, unahangaika kupiga simu mara nyingi.
Hii moja kwa moja ni kama unasema kuwa mimi sina thamani nichukue. Ukatoka kugonga mwanaume wa kwanza ukafuata wapili, watatu na wannne wote unawapa pesa. Ukipika chakula kizuri unaweza kuwapa watu bure wakala lakini ukiwapa na pesa ili wale chakula chako basi jua kuwa watakudharau na watachukua pesa na kukuacha.
Wanaume waliokua wanakuacha nikwakua hukutaka kuwa mwanamke kwao, unaingia kwenye mahusiano unaanza kumpa mwanaume pesa. Kwanza ananza kuringa na kuhisi unampenda sana, pili anaanza kuhisi una kasoro ndiyo maana unamnunua na tatu anaona kama huna pakwenda hivyo atakunyanyasa atakavyo, na nne kama ulivyosema mwenyewe, ukipewa chakula halafu mtu akalazimishia kukulia ili ule basi utachukua pesa na kuacha chakula ndivyo walichukua pesa kwako na kukuacha wewe.”
“Daaah! Kaka kwahiyo mimi sitakuja kuolewa?”
“Hapana, mimi si Mungu kusema hivyo, lakini furaha yako haipaswi kuamuliwa na matumaini ya ndoa. Kama unataka kuolewa kwanza anza kujipenda, kujithamni na mwanaume anapokuja kwako uamini kuwa kaja kwako kwakua umzuri, umtamu na unavutia na si kwakua una pesa. Kwa maana hiyo, mwanaume akija kukutongoza hata kama hana pesa kama wewe, hata kama anaishi maisha duni, ishi maisha yake.
Acha kale kakiherehere kakusema nataka kumsaidia ili awe hadhi yangu, muangalie, tena chagua, angalia kama kakuvutia na ishi maisha yake. Kama kutakau na haja ya kumsaidia iwe ile ya kumsiadia kama mshikaji ka kwama na si kutaka kumpa pesa ilia kupende. Jifunze kujipenda mwenywe utaona kila mtu atakupenda na wanaume watakuja tu lakini hata kama wasipokuja unajipenda tauari.”
“Vipi Kaka kuhusu ndugu zangu, nitafanya nini?”
“Ndugu zako kivipi, wanahusika nini na furaha yako?”
“Sijui lakini wananiambia kila siku kuhusu ndoa ni kama wamenitenga…”
“Kuna ndugu yako hata mmoja ambaye anafanya kazi ya kugawa Oxygena kusema kwamba akikununia hutaishi?”
“Hapana Kaka.”
“Basi hawakuhusu. Tena ngoja nikufundishe kitu kimoja kuhusu ndugu.
Kuna kanuni oja ya maisha ambayo inasema, ukiona mtu anahangaika na maisha ya watu kuwa yakwake yamemshinda. Hakuna mtu mwneye raha kwenye ndoa yake anaweza kukununia kwakua tu hujaolewa, narudia hakuna mtu mwenye raha katika ndoa yake anahangaika kuuliza maswali ya kinafiki kama utaolewa lini, tunasubiri ya kwako, si utafute mtoto. Ukichunguza wote wanaokupigia kelele ndoa zao zimekufa au ni tia maji tiamaji, hama huamini tuanze na ndugu zako.
Tena hata Mama yako, Mama kuuliza si mbaya, ni haki yake na wengi huuliza kwa upendo, lakini kwa namna Mama yako anavyouliza ni kwa chuki, ni kama anakuchukia, ni kama anataka kulipa kisasi flani na hiyo inaweza kutokana na vitu viwili. Kwanza labda Baba yako alimtesa sana huko nyuma au Mama mkwe wake alimtesa sana kwenye ndoa yake hivyo ana visirani vyake.
Lakini utajiuliza mbona kwenus ijui mko wa tano hahangaiki na hao watoto wengine. Huna haja ya kuniambia, jibu ni rahisi, hahangaiki nao kwakua kwenye familia yenu wewe kama sio mwenye akili basi umefanikiwa kipesa kuliko wengine. Ni kama Mama yako anakuonea wivu kwamba anakuchukia kwakua anahisi una kitu ambacho yeye hakukipata. Narudia Mama yako anakuonea wivu kwa kitu flani, unaonekana kuna kitu ambacho unacho watoto wengine hawana ndiyo kinamchoma na anajaribu kukuumiza kwa kitu ambacho huna…”
“Daaahhh wewe Kaka ni Mchawi au?”
“Kwanini?”
“Mmaa yangu wakati anaolewa na Baba yangu alikua anaomea Udaktari lakini Baba aimuachisha chuo mwaka wa pili, basi akawa ni Mama wa nyumbani. Baba hakuwahi kumnyanyasa lakini Bibi alikua hampendi kwakua tu si kabila moja na Baba. Alikua anamtukana mpaka sisi tunakua hatuendi kwa Bibi. Alikua ananyanyaswa na Shangazi wanakuja nyumbani, na kila siku Mama alikua anatumbia kuwa tusome kwani elimu ni kila kitu, anatuambia kuwa kamwe usiache kazi kwaajili ya mwanaume.
Kuhusu kwetu ndiyo, mimi ndiyo mwenye akili na mafanikio, tangu sekondari nilipata divisheni one, pia kwenye kazi mimi ndiyo nahudumia kila kitu nyumbani, hata Kaka yangu ni mkubwa lakini hanifikii kipato, nawasomesha watoto wa dada yangu lakini naye ananitukana hivyo hivyo.”
“Unataka nianze kukuchambulia ndugu zako mmoja mmoja na ndoa zao, hasa huyo mdogo wako anayekufuata, yule ambaye hata hakutaka uende kwenye harusi yake, unataka nikuambei matatizo yake maana nina uhakika ndoa yake ilikufa hata kabla ya kuanza. Kwa namna ulivyomsaidia na namna alivyokufanyia hakuolewa kwa upendo bali aliolewa kama vile anataka kukukomoa, mdogo wako ni wale wenye wivu anaona kama kila kitu umefanikiwa kasoro ndoa ndiyo maana hakukualika ili uumie.”
Sikua najua chochote lakini kwa namna mdogo wake alivyokua akishirikiana na Mama ayeka nilikua na uhakika kuna shida.
“Mwanzo kila mtua lifichwa lakini baadaye ndipo tukajua kuwa mume wake alishaoa mwanamke mwingine na wakatengana yeye ni kama mke wa pili kwani huyo mwingine hakumpa talaka. Mdogo wangu alikua anajau na Mama naye alikua anajua, hata harusi ndugu waliokuja si ndugu zake halisi, ni marafiki tu kwani wazazi wake waligoma asioe mke wa pili.
Mpaka sasa hivi mwanaume bado yuko na mke wa kwanza ila mdogo wangu hawezi kuondoka kwani kashamuachisha kazi, ni Mama wa nyumbani anametegemea kwa kila kitu…”
“Nilikuambia watu wenye chuki kwao furaha hakuna, hivyo vitu havikai nyumba moja, sasa swali linakuja mbona unaumizwa kichwa na watu walioshindwa. Watu wanaokuonea wivu, hivi unajua kuwa mdogo wako anatamani angekua wewe, asingeingia kwenye ndoa kwa kukurupuka akabaki angalau awe na maisha kama wewe?”
“Sijui Kaka, maisha yangu naona kama yameishak nikiona marafiki wanapost ndoa zao nahisi kuchanganyikiwa, nikiangalia umri wangu na nina mshono hivi wanaume watanipenda kweli?”
“Dada wanaolewa wenye watotop sembuse wewe mshono, tulia kuwa na fuaraha utavuta wanaume wenye furaha.
Maisha ni kama Mzinga na Jalala, unachagua mwenyewe, kama unataka kuwa na furaha, chagua kuwa Mzinga utavuita nyuki utengeneze Asali, lakini kama huwezi chagua kuwa na huzuni, utakua kama Jalala, utavuta Inzi utengeneze Kipindupindu, uamuzi ni wako. amua kua na furaha yako na kama ukiingia kwenye Mahusiano basi zingatia mambo haya.
Kwanza kabisa achana na historia yako, acha kuelezea maumivu yako, achana na mambo ya nimeumizwa sana na kusema sijui nataka mtu siriasi. Ukishaanza hivyo jua kuwa utakayempata atakukimbia, hakuna mtu anapenda mtu ambaye kaumizwa sana kaachwa achwa, ingia kama mtu mpya na akikuuliza kuhusu mahusiano ya zamani muambia tulishindwana kila mtu alikua bize na mambo yake imeisha hivyo.
Kitu cha pili mkubali kwakua kakuvutia si kwa yale aliyokuahidi. Sio kwakua kakuahidi ndoa bai uchanganyikiwe, ahadi za ndoa kabla ya kujuana na kufanya chochote nyingi ni za uongo hivyo akuvutie, anza mahusiano kisha kama ikijja ndoa basi itakuja tu yenyewe na si kwakua alikuahidi. Akuvutie ili hata akikuacha ujue ulivutiwa naye na si kumchukua kwaajili ya watu.
Acha kuhonga, unakutana na mwanaume leo ashajua mali zako na ushaanza kumpa kusimamia, hapana muwe na mahusiano kwanza, asiguse maliz ako kusimamia na kama ni shdia muwe mnsaidaiana sio kama unampa tu kila siku kama unamhonga wewe, tenganisha mahusiano na Biashara zako.
Mwisho hata kama hayatafanikiwa kuwa na amani ukijua kuwa wakati wa Mungu ndiyo wakati sahihi, acha kupaniki na kuangalia watu sana. watu wataongea, usipoolewa wataongea, ukiolewa wataongea na chochote kile kuongea kwao ni kawaida hivyo achana na maneno ya watu, wana maumibu yao subiri wakati wa Mungu.”
MREJESHO; Nilinunuliwa Kitabu chako na Dada mmoja, akanipa namba yako hata sikuujua, nashukuru ulinisikiliza kwani nilitamani hata kufa kutokana na manyanyaso ya ndugu zangu. Nimekua nikiongea na wewe kwa muda na sikua kwenye mahusiano kwa zaidi ya mwaka ila sasa hivi nina miaka 33.
Nipo kwenye mahusoano mwezi wa pili sasa, sijui yatafika wapi naomba Mungu yawe vizuri lakini nina furaha, nimemzidi mwanaume kipato lakini sina shobo kama za zamani, sijachanganyikiwa na wala sina mchcheto. Natamani ndoa kweli lakini kwa mara ya kwanza nafurahia mahusiano yang.
Nina furaha kama ni ndoa kuja ije kwa mipango ya Mungu ila kwasasa nina furaha. Nilianza kwa kujipa furaha yangu mwenywe yaani najiona mwanamke tena, sina ile mambo ya kuhudumia tena, nashukuru sana kwa ushauri wako.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment