Search This Blog

Wednesday, June 22, 2022

KAKA UMEMUUA BABA SASA UNATUUA NA SISI!

  


IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

KAKA UMEMUUA BABA SASA UNATUUA NA SISI!


UNATUUA NA SISI!---SEHEMU YA KWANZA.


“Aliyekufa ni huyo Malaya wako, kwanini wewe unaumia, kwanini wewe unakasirika, yaani mwanamke alishakuacha, alikua anaenda kuolewa na mwanaume mwingine lakini leo umekaa unamlilia! Huyo mwanamke ni Malaya na amepata alichokua anakitaka!” Baba aliongea kwa hasira, nakumbuka ilikua ni siku ya jumapili, wiki mbili zilikua zimepita tyangu aliyekua mchumba wa Kaka yangu kufariki dunia.


Ni habari amabzo ziliniumiza kwani ni mtu ambaye tulikua tunamfahamu na kwa namna flani tulidhani labda ataolewa na Kaka, lakini haikua hivyo, kila siku walikua wanagombana kupigana kiasi kwamba ikaikia hatua ya kuachana. Baada ya kuchana na huyo mwanamke Kaka yeye alienda Kozi kusoma, Kaka yangu ni Mwanajeshi, lakini akiwa huko huyo mwanamke alipata mwanaume mwingine, walianzisha mahusiano, miezi minne tu baada ya kuachana na Kaka yangu huyo dada alimpeleka mwanaume mwingine nyumbani kwao kumtambulisha ili kuolewa.


Kozi aliyoenda Kaka ilikua ni miezi sita, akiwa kule hakuna mtu aliyemuambia kuhusu kuolewa kwa x wake kwani alikua anampenda sana na tulijua kama tukimuambia tutamchanganya. Lakini aliporudi alikuta ndiyo maandalizi ya harusi yanaanza, alikuja kuchunguza na kujua kuwa kumbe huyo mwanamke alikua na ujauzito tena mkubwa tu. Ilikua imepita kama miezi nane tu hivi, hivyo Baada ya Kaka kumuona na mimba kubwa alihisi kuwa ni mimba yake hivyo akaanza kumfuatilia kujua kama ni yake.


Lakini yule Dada alimkatalia, alimuambia kuwa mimba si yake na hana mpango na Kaka.

“Unajua nilimpa mimba akatoa?” Siku moja Kaka aliniuliza, ilikua ni asubuhi kwenye saa nne hivi, aliniambia nimsindikize sehemu, mimi nilikua likizo hivyo sikua na chakufanya, tuliingia kwenye gari yake, akaendesha mpaka kwenye hospitali moja hivi, mwanzo nilijua labda kaka anaumwa, lakini alipita sehemu ya hospitali na kuenda kupaki Gari kaqriobu na kiliniki moja hivi.


Alikua amepaki kwa kulificha huku tukichungulia kwenye kioo kuangalia watu waliokua wakiingia na kutoka. Mwanzo sikualewa mpaka nilipomuona X wake anaingia, alishushwa kwenye gari na Kijana mmoja ambaye nilimtambua, alikua ni mchumba wake. Nilikua namjua kwakua kipindi Kaka yuko na wifi nilishamuona mara kibao wakiwa pamoja, alikua ni radfiki wa X wake Kaka yangu, walisoma na Kaka yake hivyo walizoeana ingawa si kimahusiano.


“Nilimuambia anizalie lakini akakataa, yaani yule mbwa nilikua namuona kama Kaka ayke ndiyo kaenda kumjaza mimba mchumba wangu!” Kaka aliongea kwa hasira, nilimuona akitetemeka kwa hasira, jaso likimtoka.

“Lakini kaka wewe si ndiyo ulimuacha, nakumbuka wewe ndiyo ulimfukuza, ukasema humtaki, hata sisi mbona hatumtaki, kwanini unahangaika na huyo Malaya, yaani mtu anatembea na Kaka yake lakini bado unampenda, unamuona kama ni mwanamke!?” Nilimuuliza kwa hasira.

“Simtaki sawa lakini kwanini azae na mwanaume mwingine, sisi tumeachana yaani hata mwaka haujaisha kashapata mtu mwingine, hivi mimi ningetafuta mwingine angejisikiaje?”


Nilimshangaa Kaka kidogo kwani alikua na wanawake wengi sana, hata sababu ya kumpiga X wake kila siku ilitokana na kuwa na wanawake wengi. Kaka alikua amejenga, nyumba yake ilikua ni jirani tu na nyumbani kweu, kwakau muda mwingi alikua kazini, kambini basi mimi na ndugu zangu wengine tulipenda kwenda kushinda pale. Mara nyingi alikua anamleta huyo X wake, ndugu wanajua, mpaka Mama alikua anajua na kwakua alikua anatambulika basi tulimuona kama wifi yetu, alikua ni kama mke wake.


Pamoja na kuwa na mwanamke mmoja aliyekua anatambulika lakini kaka yangu alikua ni Malaya sana, alikua na wanawake wengi, alikua akiwabadilisha kama nguo na mara kwa mara X wake alikua anamfumania ila anaishia kupigwa. Nakumbuka kuna siku nilikua kwa Kaka, akaleta mwanamke wake ndani, sisi tulikuepo, wakati anafanya mapenzi huko wifi alikuja, aligonga mpango na kuingia mpaka sebuleni, akakaa, kaka akatoka zake huko na taulo, akaanza kumpiga ni kwanini alikua anakuja bila taarifa.


Wifi alimuambia kuwa yeye pale ni kwake kwania lishajitambulisha mpaka kwao na kutoa kishioka uchumba. Kaka alimpiga sana lakini wifi alikataa kuondoka, wakati anampiga sisi tulikua tukimtukana na kumuambia kuwa aondoke kwani mwanaume hapangiwi, Kaka alimsukuma mpaka nnje lakini wifi hakuondoka. Bila aibu Kaka alitoka na yule mwanamke, akampita wifi akiwa kakaa nnje, alimsindikiza yule mwanamke, akaondoka, aliporudi alimuambia kuwa ainmgie ndani, dada wa watu aliingia ndani ila alimpiga na kumfungia stoo, hapohapo Kaka alimpigia simu mwanamke mwingine, wakalala naye mpaka asubuhi, hapo ndipo alimfungulia wifi na kumuondoa asubuhi wakati yeye akiwa na mwanamke mwingine.


Kusema kweli ingawa ni Kaka yangu na nilikua ninamchukia wifi yangu lakini kama mwanamke kile kitendo kiliniumiza sana, nilishindwa kuvumilai na kuamua kumuuliza Kaka.

“Nimefanya makusudi, huyo mwanaume ni Malaya sana, ana wanaume wengi nilitaka tu kumuonyesha kuwa na mimi nawez akupata wanawake idadi yoyote ninayotaka hivyo asinisumbue!” Nilinyamaza kwakua nilikua namchukia huyo mwanamke lakini hali hiyo ilikua inaniuma.


Tulikaa pale kwa muda mrefu, wakaingia mpaka wakatoka Kaka yuko pale anaangalia tu, kulikua na ukimya sana, alikua anaonekana kuumia inngawa hakutaka kunionyesha.

“Bado uanmpenda?” Nililazimika kumuuliza.

“Hapana, mimi, nimpende yule Malaya, kwanza nashukuru Mungu tumeachana, alikua ananirudisha nyuma sana, huwezi amini baada ya kuachana naye mambo yangu sasa hivi yanaenda sana, nashukuru Mungu sana kwa hilo.”

“Sasa mbona unamfuatilia, si tondoke!”

“Namfuatilia kwakua ni mshenzi, mimi alitoa mimba zangu mbili, hakutaka kuzaa na mimi lakini huyu mbwa kamzalia, kinachoniuma nikuwa walikua wananizunguka, haiwezekani mtu tuachane siku mbili kashaapata mtu mwingine! Walikua wanajifanya marafiki kumbe ni wapenzi, nitawafanyia kitu kibaya hawatakuja kuamini, huyu mwanamke hanijui!”


“Lakini Kaka wewe ndiyo ulimpiga mpaka mimba zake zikatoka, tena ile ya pili kidogoa tolewe kizazi? “ Nilimuuliza, Kaka hakunijibu, aliniangalia kwa hasira bila majibu. Nakumbuka mimba ya kwanza sikuepo lakini wifi alikua analalamika kuwa Kaka kampiga mpaka mimba yake ya miezi minne ikatoka, alilalamika kwa Mama lakini kwakua Kaka alikua na pesa na ndiyo alikua anahudumia familia hakukua na mtu wa kumuongelesha chochote, kibao kilimgeukia wifi kila mtu akisema kuwa katoa kwa makusudi.


Hata mimi niliamini hivyo, ilikua ni rahisi kuamini kuwa alitoa yeye kulik0 kuamini kuwa Kaka yangu alikua ni mnyama kiasi hicho. Lakini mimba ya pili niliishuhudia mimi. Nakumbuka ilikua ni usiku, wifi alikuja nyumbani, pamoja na kwamba walikua hawaishi pamoja na Kaka lakini wifi alikua akitumia muda mwingi kwa Kaka, alikua anafanya kazi na alipangisha sehemu yake, lakini muda mwingi alikua kwetu kama mke wa Kaka.


Kaka alirudi usiku, alikua kalewa sana, wakati anaingia ndani alikua anaongea na mwanamke kwenye simu, wifi ndiyoa limfungulia, alipomuomba amkate simu Kaka limsukuma wifi, lakini kwakua alikua kalewa basi alidondoka yeye, alipepesuka akadondoka na kujigonga kwenye meza. Hapo ndiyo shida ilianza, Kaka alianza kumpiga akimuambia kuwa anataka kumuua,. Wakati huo wifi alikua na mimba ya miezi saba, alikua na tumbo kubwa tu, Kaka hakujali, alimpiga sana tena tumboani, mar azote wifi akipigwa tulikua tunabaki chumbani kujifanya kuwa hatujasikia.


Lakini siku hiyo ilikua tofauti, Kaka alikua anampiga sana, wifi alikua analia, alikua analalamika.

“Niue mimi lakini usimuue mtoto, acha kunipiga tumboni, nipige hata kichwani mume wangu!” Nilijikuta nanyanyuka na kwenda kumfuata Kaka, walikua sebuleni, taa inawake, wifi alikua kalala chini, kajikunja na kukumbatia tumbo lake, alikua anamzuia Kaka aliyekua anampiga mateke ya tumboni.

“Kaka unataka kumuua mtoto, hiyo mimbi ni ya kwako?” nilimuuliza huku nikimfuata na kumushika Kaka ilia muache wifi, lakini hakumuachia, aliendelea kumpiga huku akimshutumu kuwa ile mimba si yake hibvyo nimuachie amuue.


Lakini sikutaaka kumuachia, niliendelea kumshika, nilimvuta mpaka ndani chumbani kwake, nikamsukuma na kumfungia ndani, kurudi ili kumuangalia wifi alikua hapigi kelele tena, alikua kalala mkatulia.

“Kaka kaua…” Niliwaza, wakati nikihahahaha mdogo wangu wakiume alitoka, alimuangalia wifi na kukuta mapigo ya moyo yapo kidogo, aliniambia tumpeleke hospitalini, lakini kaka ndiyo alikua na funguo za gari, tulilazimika kumfungulia tukachukua funguo , lakini wakati tunatoka alilazimisha mpaka tukaingia naye kwenye gari, wakati huo ni kama pombe zimekata, alikua na wasiwasi sana kila dakika akiangalia mapigo ya moyo ya wifi, alikua anahisi kafa, kwa mara ya kwanza nilimuona Kak a yangu akiwa nauoga, alikua akitetemeka kabisa akijua kuwa kaua.


“Kadondoka wkenye ngazi, tukifika ndiyo itakua hivyo, siwezi kwenda polisi, nitafukuzwa kazi iikijuliakana.” Aliongea njia nzima, tulifika kwenye hospitali binafsi, ilikua ndogo na ni shemu ambayo Kaka alikua akijuana na Daktari, kwa maana hiyo tulibyosema sihu ya ngazi hawakuhitaji PF3 ingawa ilionekana moja kwa moja kuwa wifi kapigwa. Alitibiwa lakini hali ilikua mbaya, mimba ilikua imetoka na alihitajika kufanyiw3a upasuaji. Nakumbuka wakati nipo na mdogo wangu wakiume tunasubiria Kaka alikua anaongea na daktari.


“Mtoe kizazi ili umkomoe, huna haja ya kuhangaika, huyu kizazi kikitoka hataniacha, mimi nitazaa na wanawake wnegine lakini hataniacha kamwe!” Kaka laimuambia yule daktari ambaye ni rafiki yake, lakini alikataa katakata na kumuambia kuwa kimaadili ikijulikana atafungwa na kupoteza leseni yake. Walibishana sana lakini Doctor aligoma na kuondoka, alirudi ndani, Kaka alikuja na kukaa na sisi tukajifanya kama hatujasikia. Alituelezea hali yake na kutumbia kuwa hataki tumuambie mtu yoyote.


Mama alijua atachanganyukiwa, tutamuambia mimba ilitoka yenyewe. Tulikubaliana hivyo ndiyo maana nilishangaa ni kwanini Kaka alikua na hsira kuona kuwa X wake kapata mwanaume mwingine na wanakaribia kupata mtoto. Mimi nilidhani kuwa kashamuacha, hampendi ndiyo maana alikua anampiga na hata ilikua ndiyo sababu ya yeye kutaka kumtoa kizazi kwakua hakua na mpango naye.


Baada ya wale watu kuondoka Kaka aliwasha gari kuondoka, njia nzima alikua akiapa kuwa atamfanyia kitu kibaya na harusi haitafanyika.

“Usije kupiga, utafungwa!” Nilimuambia, kwa namana alivyokua na wasiwasi nlishindwa kuelewa ni kwanini alikua anafanya hivyo, nilishindwa kujua ni kitu gani anataka kwa mwanamke ambaye tayari alishamuacha. Sikujua atafanya nini lakini kwa nilibvyokua namfahamu Kaka yangu nilihisi kuwa atafanya kitu kibaya ingawa yeye alinihakikishia kuwa hatafanya kitu kibaya.


“Yule mwanamke ananipenda sana, najua kuwa yuko na huyo mwanaume kwakua mimi nimemuacha, nitaongea naye, nitamuambia kuwa nimebadilika na nina uhakika kuwa atanirudia!” Aliniambia.

“Kuhusu mimba, utakua tayari kulea mimba ya mwanaume mwenzako?” Nilimuuliza, alicheka na kuniambia kuwa mimba atatoa, watu wanatoa mimba za miezi nane sembuse ile ndogo namna ile.

“Hata asipotoa, akikubali nimuoe anaweza kuzaa mtoto amekufa tukazika basi maisha yakaendelea, simpendi ila kama mimi sijapata mke bado yeye hawezi kuoa, itakua ni aibu k3wangu, watu wataona kama vile mimi ndiyo nimeachwa, mimi ni mwanaume siwezi kuachwa, nitahakikisha kuwa nawaachanisha na yule mtoto hatazaliwa.


Kusema kweli nilikua nahofia kuhusu Kaka, nilijua atafanya kitu kibaya, nililazimika kumuambia Mama lakini hakujali, aliongea na Kaka kana kwamba ni kitu cha kawaida ila mwishoa limhakikishia kuwa akashamuacha wifi na hamtaki kabisa. Sikuzilienda, Kaka hakuzungumzia hicho kitu tena, harusi ilikua inakaribia na kila siku nikimuuliza atafanya nini alikua ananiambia kuwa nisubiri tu ila X wake hataolewa.


Kitchen Party ikafanyika, ilifanyika wiki moja kabla ya Send off, hapo ndiyo nilijua kuwa Kaka kashidwa, kashakubali ukweli,. Lakini nilimuona kama ana furaha, anaongea kuwa hawezi kuolewa labda kama yeye si mwanajeshi, nilimsikiliza lakini mwisho niliona kama ni maneno ya mkosaji, niliona kama vile anaongea tu ili kujifariji lakini hana uwezo wa kufanya kitu chochote.


Marafiki wa wifi ni walewale na marafiki wetu kwani walisoma na Kaka yangu hivyo walikua wanajuana na watu wa aina moja. Tulikua tunajau kila kitu kilichokua kinaendelea, mpaka siku ya Send off tulikua tunajua. Ingawa hatukualikwa lakini mimi nilikua nafuatilia sana, sijui kwanini lakini nilikua na wasiwasi sana nikihisi kuwa Kaka atafanya kitu kibaya. Kuna rafiki yangu mmoja alienda, alikua ananaijulisha kila kitu kilichokua kinaendelea.


Wakiwa ukumbini alinitumia picha ya kila kiti. Lakini kuna kitu kilikua hakiko sawa, kwa kawaida katika sherehe nyingi maharusi wanaingia ndiyo mambo ya kutambulishana, chakula au zawadi vinaanza na mambo mengine. Lakini mpaka kufika saa tatus usiku si bwana harusi wala Bibi harusi walikua washaingia, baadhi ya ndugu walikuepo lakini wazazi na ndugu wakaribu hawkauepo.


Wageni walianza kupewa chakula hata kabla maharusi hawajaingia, kusema kweli kila kitu kilikua ni tofauti, rafiki yangu alikua ananiambia mpaka nikawa na wasiwasi. Walikua hawajaambiwa chochote lakini kuna hisia mbaya zilijengeka, wapo waliosema Bini harusi kagoma kuolewa, wapo waliosema kuwa Bwana harusi kagoma kuoa na mambo kibao. Manenoyalikua mengi, niliamua kumtafuta Kaka yangu, alikua kambini na simu yake ilikua haipatikani.


Nilihangaika kumtafuta mpaka saa sita watu walikula na kuondoka lakinio maharusi hawkautokea na hawakuambiwa kitu, wageni wengi walikua washaondoka, hata rafiki yangu aliyekua akinipa matukio alitaka sana kuondoka lakini mimi ndiyo nilimzuia nikimuambia kuwa nataka kujua kilichokua kinaendelea. Ukimbi ulikua vurugu mecho, MC hana chakuongea, kila saa anawaambia watu maharusi wanakuja lakini hakua na taarifa yoyote.


Mpaka saa nane usiku kila mtua likua ashaondoka na hapo hapo ndiyo Kaka yangu alipatikana kwa whatsapp. Alikua kapost status ameandika “Alichokiunganisha Mungu shetani hawezi kukitengenisha.” Nilimpigia kwa whatsapp lakini hakupokea, kama nusu saa baadaye alinipigia simu, alikua amelewa na alikua ananiambia kuwa alisema kuwa ndoa haiwezi kufungwa sikumuamini. Aliongea maneni mengi sana ya kujisifia lakini mwisho wa sikua lisema kuwa X wake kaachwa na yeye hamtaki tena alitaka tu kumharibia.


Sikuelewa mpaka asubuhi, niliamka nakukutana meseji za yule rafiki yangu.

“Aisee kumbe jana Bibi harusi alishindwa kuingia ukumbini kwakua amefariki, aisee dada wa watu amekufa na tumbo lake!” Baada ya hapa meseji nyingi zilianza kuingia, watu waliokua wananifahamu walinipigia na kuniuliza ni nini, mimi nilikua sijui kilcihokua kinaendelea lakini kuna meseji ilisema kuwa Bibi harusi walikua amekunywa sumu na alipopelekwa hospitalini alikufa saa saba usiku na ndiyo sababu hakuna mtu alitokea ukumbini.”


Akili yangu ilihamia kwa Kaka, nilijua kuna kitu kafanya, nilijau kabisa kuwa anahusika kwani alishaahidi, pamoja na ukatili wa Kaka yangu lakini sikutaka kuamini kuwa anaweza kuua. Nilimpigia simu ikawa haipatikani, nikampigia mdogo wangu ambaye naye alikua anajua hizo taarifa.

“Unahdani Kaka anahusika? Jana alikua na raha sana ?” ndiyo kitu cha kwanza ambacho aliniambia baada tu ya kupokea simu, kusema kweli sikua najibu ingawa akili ilikua inaniambia kuwa ni kuwa ni kweli Kaka kamuua wifi yangu.


Kwa ushauri wa mija kwa moja hakikisha unanunua kitabu changu. Kwasasa nina vitabu vitatu, cha mahusiano ya kawaida hasa kwa wanawake, cha wanaume wenye changamoto ya kumfikisha mwanamke kileleni na cha Biashara, chagua kinachoendana na tatizo lako.


Bei ya kitabu kimoja ni shilingi elfu kumi. Kupata kitabu unalipia kwa M-pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222 Jina linakuja Iddi Makengo, sina namba nyingine zaidi ya hizo baada ya hapo kitabu utatumiwa kwa njia ya Whatsapp/Email/Facebook.


Siku ndiyo inaanza, bado mapema kabisa, unadhani kahusika kumuua X wake, unahdani alimpaje hiyo sumu kama ni sumu? Unadhani ni kitu gani kimetokea? Usikae mbeli, mtag rafiki, na rafiki yako na rafiki yake muambie mambo ndiyo yameanza.




Nilijaribu kuwapigia watu ili kujua nini kilikua kimetokea lakini sikupata majibu, nilimpigia Mama na kumuambia, alionekana kujua lakini aliongea kwa wasiwasi.

“Kaka yako yuko hapa lakini hayuko vizuri kabisa, kwani kuna nini?” Mama aliniambia, sikuaka kujibishana anaye, nilitoka nikachukua Bajaji nikaenda mpaka nyumbani. Kaka alishajua kuwa X wake amekufa.

“Umemfanya Nini dada wa watu?” Nilimuuliza baada tu ya kuingia.

“Wewe una akili kweli, kwanini unaanza kumshutumu Kaka yako na ujinga wako! Kwani ni yeye kamuua, si ameamua kujiua yeye mwenyewe, kwanini unataka kumshutumu Kaka yako!” Mama aliongea kwa hasira, Kaka alikua kanyamaza kimya lakini machozi yanamtoka, alionekana kulia sana huku akilalamika.


“Ni mimi ndiyo nimemuua, Mama hata unityetee vipi lakini mimi ndiyo nimemuua!” Kaka alipiga kelele, alionekana kujutia.

“Kwahiyo umempa suimu!?” Nilimuuliza kwa mshangao lakini kabla ya kujibu Baba aliingilia.

“Hakumuua, yule mwanamke alikua ni Mlaya, anatuma tuma picha za uchi, ni bora umezitoa mapema kwani huyo mwanaume angeweza kuziona na kuoa mikosi, umemsaidia mwanaume mwenzako!”


Baba aliongea, nilikaa chini na kuuliza kilichokua kimetokea kwani nilikua siwelewi.

“Wewe ulisema kuwa utafanya kitu ili kuhakikisha kuwa hawaoeni, ni kitu gani? Nilimuuliza Kaka, aliniangalia huku akilia, alifuta machozi na kuanza kuniambia.

“Kuna picha nilimtumia mchumba wake, nikawatumia na wazazi wake na wakwe zake, nilitaka kumuaibisha ili tu aachike nimuoe mimi lakini sikujua kama tajiua, niamini nikikuambia kuwa kama ningejua kuwa atajiua basi nisingezituma.” Aliniambia, nilimuuliza ni picha gani lakini hajkua tayari kuniambia, nilimuaomba kuziona ila akaniambia kuwa ameshazifuta.


“Huyo mwanamke alikua anapiga picha anatumia wanaume, sasa Kaka yako naye katumiwa na mwanaume wake mwingine, alitumiwa kipindi wapo pamopja, sas andiyo sijui waligombana akakasirika na kuziituma, si unajua kwenye mapenzi ukiumizwa wakati mwingine unakua na hasira. Muache Kaka yako apumzike, kaumia sana, muache ana mawazo ameumia sana!” Mama aliniambia, waliongea mamboa ambayo sikuyalewa, yaklikua hayaingii akilini, kwa nilivyokua namfahamu wifi, kwa namna Kaka alivyokua anamchunga niliamini kuwa kama ngekua anachepuka na kuona picha za uchi amabzo amepiga na mwanaume mwingine basi angemuua.


Nilijaribu kuulizia na kutaka kujua lakini Bbaa alinikataza, aliniambia niondoke kwani Kaka kaumizwa sana na msiba wa X wake hivyo nisimsumbue. Niliondoka lakini sikurudi nyumbani, nilimafuta rafiki yangu amabye alienda kwenye msiba, niliatka kuoanana naye lakini hakutaka kunioa, alisingizia yuko bize lakini sikukubalia, nilikua najua ofisini kwake hivyo nilijitahidi mpaka nikaenda huko.


Aliniona na hakua na namna, ilikua ni lazima kuongea na mimi, nilitaka kujua kuwa ni kiu gani kimetokea.

“Hivi Kaka yako ana akili wkeli?” Alianza kwa kuniuliza.

“Kwanini, mbona unanichanganya, kwani kafanya nini?” Nilimuuliza kama nalazimishia kwani niliona kama anazunguka zunguka sana, sikutaka kuendelea kuzungushwa.

“Kaka yako alikua anataka Dada wa watu aachane na mchumba wako ili warudiane, lakini Dada wa watu alikataa, kumbe Kaka yako alikua na picha za uchia mabzo alimpiga, sijui na mavideo wakkiifanya mapenzi, akamtishia kuwa atazisamabza lakini Dada aligoma kabiasa kurudiana naye, hapo ndipo alikasirika na kuanza kuzisambaza.


Alichukua namba za wazazi na ndugu wa karibu wa mwanaume nakuwatumia video na picha za ucni, akamtumia Baba wa bibi harusi na ndugu wengine, kisha akamtumia na mwanaume. Dada wa watu kuja kuona basi akapaniki, alipopigiwa simu kuwa kuna picha zake na sijui ni nani alimpigia basi akatumiwa naye hizo picha na ndugu yake, unaambiwa alichukua vidonge na kumeza.


Yaani huwezi amini Kaka yakoa livyomshenzi kazituma wakati dada wawatu anatoka kazini, sijui sasa walimpigia simu, sijui ilikuaje lakini ndiyo hivyo, amerudi nyumbani, kaingia kachanganay vizonge unaambiwa zaidi ya mia kanywa….” Aliongea maneno mengi lakini sikutaka kuamini kuwa kweli Kaka anaweza kufanya vitu kama hivyo, ni kweli Kaka yangu alikua ni smhenzi sana lakini si kwa kiwango hicho.

“Lakini huyo mwanamke si ndiyo alikua anasambaza mwenyewe video zake, mna uhakika gani kuwa ni Video za Kaka yangu, kama ni wanaume wengine wameamua kutuma, kwani Kaka alitumia namba yake?”


“Aisee mimi sijaziona lakini kwenye hizo video Kak ayako hata hajajificha, nasikia anaonekana na alipokua anatuma alijirekodi kabisa akimtukana mchumba wa marehemu kuwa hata kama anaoa asijekudhani kuwa anapendwa balia naoa Malaya. Sijui lakini ndiyo hivyo, kaka yako anahusika na kila mtu analia, ndiyo amaana sitaki hata kuonekana na wewe, nyie watu ni mashetani, kumbe mlikua manajua kuwa Kaka yenu anampiga na kumnyanyasa huyo mwanamke lakini mkakaa kimya, hapana, ondoka sitaki ushoga.”


Maneno yake yalinichoma lakini nilijiafnaya sijui chochote, nilimuambia mimi sijui kitu ndipo alinishushua.

“Kila mtu anajua, kila mtu anaijua familia yenu, huna haja ya kuigiza na kudanganya, unafikiri nani hajui kwua mlimtoa mimba mbili na mlitaka kumtoa kizazi. Yule Daktari ni rafiki wa familia, alisoma na Binamu wa marehemu, au ulikua hujui, na kipindi hicho yeye ndiyo alimuambia ilia aachane na Kaka yako kwani atakuja kumuua, kila kitu kiko wazi, jinsi Mama yako alivyuokua anamtetea Kaka yako.


Mtoto wa watu alikua anapigwa mnamfungia ndani na kumtishia asimuambie mtu, kila kitu kinajulikana, aisee toka hapa sitaki hata kuonekana na mtu kama wewe! Nyie ni mashetani aisee na Kaka yako kaua!” Aliniambia huku akinisukuma nitoke, kweli nilitoka kwa aibu kwani kila kitu alichokua akikiongea kilikua ni kweli. Nilitoka nnje na kumpiigia simu mdogo wangu, aliniambia kuwa yuko nyumbani na Kaka hali yake si nzuri kwani naye anatishia kujiua, anajisikia vibaya kwa kusababisha kifo cha X wake.


Kusema kweli nilijua kabisa kuwa Kaka anaigiza, sikutaka kuamini kuwa ana uchungu. Lakini siku ile alishindwa kwenda kazini, muda wote alikua ndani akijuita kitu alichopkua amekifanya. Roho ilikua inaniuma, kwa mara ya kwanza nilivaa viatu vya wifi na kumuona Kaka kama shetani, kusema kweli nilimchukia sana. Kila nikikumbuka namna yule dada alivyokua anapigwa nilihisi kutapoka.


Sikuenda nyumbani mpaka siku ya tatu, ilikua ni siku ya mazishi ya X wa Kaka yangu. Nilienda kwakua Mama alinipigia simu.

“Njoo uongee na Kaka yako, anataka kufanya kitu cha ajabu!” mama aliniambia, nilisangaa na kumuuliza ni kitu gani, akaniambia kuwa Kaka alikua anataka kwenda kwenye mazishi ya X wake. Kweli kilikua ni kitu cha ajabu, lakini Kaka alisisitiza, nilienda kumuona ili kuongea naye. lengio lilikua ni kumshawishi ili asiende lakini nilipofika hatkuata kabisa kuniona, alikua anataka wkenda na alishajiandaa.


“Nataka nikamuombe msamaha kabla hajazikwa, nataka watu wanione, kama nikuniua waniue, nimemfanyia makos amakubwa sana!” Kaka aliongea, alikua analia kama mtoto na kusisitiza ni lazima aende.

“Itabiodi uende naye, hawezi kwenda peke yake!” Baba aliniambia, nilimuangalia Baba kwa mshangao, niliona kama na yeye kachanganyikiwa, yaani baada ya yote hayo nipeleke sura yangu katika ile familia? Hapana, sikua tayari kwa huo ujinga, kwangu ilikua ni bora kufa kuliko kufanya hivyo.


“Unaniangalia nini? Nimekuambia unaenda na Kaka yako, yule alikua ni rafiki yako, wanakufahamu, Kaka yako hawezi kwenda peke yake, kwa hali yake hapani! Anaweza kufanya vurugu, muite na mdogo wako muende wote!” nilijaribu kupinga lakini haikusaidia, kaka alishaamua kwenda na wazazi wangu hawkaua tayari kumuacha aende peke yake. Kusema kweli nilijihisi kuchanganyikiwa, kwa mara ya kwanza niliichukia familia yangu, nilikua natamani ningezaliwa na wawazi wengine.


Sikujua ni kitu gani kingetokea lakini nilijiandaa kukimbia, nilivaa suruali ndani, raba nikavaa na gauni juu ili mambo yakibadilika basi nikimbie. Tuliiingia kwenye gari, mimi ndiyo niliendesha mpaka kwenye msiba. Ilikua ni mchaana kwenye saa anne hivi na wakati tunafika watu walikua wanapita kuaga. Kaka alitangulia na sisi wengine tukaw atuko nyuma, watu walituangalia, msiba ulikua na watu wengi sana kiasi hata kupita ilikua ni ngumu.


Watu walikua wanajua kuwa Bibi harusi kajiua kwasababu ya picha za uchi kusambaa, ingawa hawkaua wengi kihivyo lakini walikua wanajua ila walikua hawamjui aliyezisamabza. Kaka yangu hakua anajulikana sana kwa mwanamke, hata ndugu waliokua wanamjua walikua ni wachache wale wa karibu, kwa maana hiyo tuliweza kupenya tukapanga mstari kuaga huku mimi nikijificha kwa kujifunika.


Wapo watu ambao walimtambua Kaka yangu, lakini hawakufanya chochote kwani ni wachache wlaikua wanajua kuwa yeye ndiyo katuma hizo picha mpaka kupelekea Bibi harusi kujiua. Nilishukuru Mungu kwa hilo huku nikimihi kaka kujificha na kuhakikisha anaaga kimya kimya, nilimuomba asilie wkani ndugu wakaribu watajua kuwa amekuja na itakua shida. Lakini Akaka hakujali alikua anatembea kama vile hajafanya kitu chochote, alikua akilia kimya kimya kila dakika akifuta machozi.


Tulipokua tunakaribia jeneza macho yangu yaligongana na mdogo wa marehemu wakiume, alituona, akamuona Kaka, hakuongea kitu aliondoka alipokua amesimama pembeni kidogo ya jeneza lililokua na mwili wa dada yake. Baada ya kama dakika moja hivi walikuja watu wawili ambao sikuwafahamu, walimfuata Kaka na kumuomba aondoke pale lakini kaka alikataa.

“Nimekuja kumuaga mpenzi wangu, mpaka anakufa tunapendana, anapaswa kunisamehe hivyo siwezi kuondoka hapa mpaka anisamehe!” kaka aliropoka kwa nguvu, watu waliokua pale walishtuka na kuanza kumuangalia, baada ya kuona kuwa analzimishjia kukaa pale wale watu aliondoka. Walimuacha aendelee kuaga. Lakinia likuja mchumba wa marehemu, yule Kaka amabaye alikua amepanga kuoana na marehemu. Alinifuata mimi na kuniuliza.


“Mnafanya nini, hembu kuwanei hata na aibu, kwahiyo mkajikusanya familia nzima kuja kuhakikisha kuwa amekufa kweli? Muacheni mke wangu apumzike kwa amani!” Aliongea kwa sauti ya chini sana lakini iliyojaa majonzi, machozi yalikua yanamtoka akijizuia. Mimi nilinyamaza kimya nikishidnwa hata cha kujibu.

“Wewe ndiyo umemuua, usingemchukua mchumba wangu asingeniacha, wewe ndiyo umesababisha ajiue!” Kaka alimgeukia mchumba wa marehemu na kumuambia. Ni kama Kaka alitaka kuleta ugomvi, ila yule Kaka alikua mstaarabu hakujibu chochote.

“Nakuhakikishia utajuta kuzaliwa, hunijui vizuri, kitu ambcho nitakufanyia basi hutatamani kuishi, uatatamani ungekufa wewe na si mke wangu. Kwa taariffa yako mimba aliyokua nayo marehemu ni yangu!”


Kaka alikua anapandisha sauti, nilimshika kumsihi anyamaze lakini ndiyo kwanza nilikua nampandisha hasira. Kuona hivyo yule Kaka aliondoka harakaharaka ili kuepusha sahari. Kaka alitaka kumfuata kama ampige lakini nilimshika.

“Umekuja kuaga na kuomba smamaha, fanya hivyo.” Nilimuambia,a likubali tukatembea mpaka kwenye jeneza, kusema kweli mimi sikuweza kuangalia mwili wa marehemu, nilikua najisikia vibaya na kuona aibu. Lakini kaka alipofika alipiga magoti, alianza kulia kiama mtoto mdogo, kila mtu alimshangaa, kuna watu walitaka kumshika lakini ndugu wa marehemu waliwaambia wamuache. Dakika tano nzima Kaka alikua kapiga magoti, analia, anaomba msamaha na kuongea maneno mengi mengi, mwisho alikuja Mchungaji, akamshika na kumuombaa anyanyuke, alikubali akanyanyuka akatoka nnje na sisi tukamfuata.


Kila mtu alikua anamshangaa lakini hakuna mtu hata mmoja ambaye alimsemesha. Baadhi ya ndugu wamarehemu wa karibu walikua pale nnje, tuliwapita wakitushangaa, tukaondoka mpaka kwenye gari. Kaka aliingia kwenye gari na kutaka kuendesha yeye, nilitaka kumzuia lakini alilazimishia, nikaona isiwe shida, anaweza kuleta vurugu na kuharibu mambo kabisa. Aliendesha gari kwa kasi lakini hakurudi nyumbani, alienda mpaka baa na kuanza kunywa, hatukuweza kumuacha mpaka usiku alipokunywa akazidiwa mpaka akazima ndiyo tukambeba na kumuweka kwenye gari kisha kiumrudisha nyumbani.


***


Baada ya vituko alivyokua amevifanya siku ya msiba kila mtu alimjua Kaka, kila mtu alijua kitu alichokua kakifanya. Picha za uchi zilitumwa kwa ndugu wa karibu, kwa maana hiyo watu wengine walikua wanajua kuwa kuna dada kasambaziwa picha za uchi lakini hakuna ambaye aliwahi kuziona. Hata sisi hatukuziona na Kaka alitumbia kuwa ni picha ambazo nayeye aliumiwa na mwanaume mwingine ikionyesha kuwa marehemu ndiyo alikua anazisambaza kwakua ni Malaya.


Ingawa mimi sikuamini lakini wazazi wangu waliamini hivyo na walimuona Kaka kama malaika, waliona kama anahukumiwa bure.

“Umemsaidia mwanaume mwenzako, unafikiri usingemuonyesha akamuoa Malaya ingekuaje?” mara kwa mara Mama alikua anamuambia Kaka, alikua anamuambia kumpa moyo kwakua tangu mazishi Kaka alikua ni mtu wa kukaa ndani, akitoka anakunywa m,paka anarudishwa, hata kazini alikua haendi, simu zake hapokei. Ilibidi Baba kwenda kumuombea ruhusa kwani alikua akifahamiana na baadhi ya watu Jeshini.


Huwezi amini w3laianza kumuambia kuwa aoe, atafute mwanamke mwingine aoe kwani marehemu ni kama kamuachia gundu na bila kuoa anaweza asipate mwanamke mwingine tena. Kaka hakutaka, alikua na mawazo mengi na kila wakati alikua ni mtu wa kujilaumu tu. Pamoja na kujilaumu yeye lakini alikua pia anamlaumu mchumba wa X wake, mwanaume ambaye alitaka kumuoa, alimlaumu kwakua kabla alijua ni rafiki wa kawaida lakini aliumia kwakua anamuoa mchumba wake.


“Walikua wananidanganya, muda mrefu ananiambia ni rafiki yake, ni kama ndugu lakini kumbe wananigeuka?” Kaka akilewa alikua anaongea.

“Huwezi amini hata mimi tulishakuaga marafiki, yaani yule ni shateni, nilishawahi kumnunulia bia zangu kumbe anatembea na mke wangu!” Aliongea kw3a hasira, ingawa hakusema kitu chochote lakinia lionekana kama ni mtu mwenye kisasi, ni kama alipanga kumfanyia kitu yule mwanaume. Mimi nilikua namsihi kuwa aachane na hayo mambo lakini alijifanya kama hamna kitu ni wasiwasi wangu tu.


“Kwahiyo unaniona mimi mnyama, uandhani naweza kufanya kitu chochote kibaya?” Aliniuliza, nilimuambia hapana lakinia anapaswa kuwa makini.

“Wale watu wameumia, wanaomboleza, yule Kaka hana kosa, wewe ulishaachana na wifi hivyo alikua na haki….”

“Haki haki gani? Nyie wanawake ni Malaya sana, kwahiyo na wewe unaweza kufanya mambo kama aliyokua amefanya huyo marehemu, nimemsamehe lakini naumia sana, halafu anaenda kujiua kisa picha za uchi, mimi nilituma ili waachane lakini si kujiua…


Ningejua nisingetuma, yaani, naumia sana, kwanini ameamua kufanya hivi….” Alianza kulia tena, ni kama dakika mbilia anjilaumu yeye, dakika mbili anamlaumu mchumba wa X wake na dakika mbilia namlaumu X wake kisha anarudi kujilaumu. Kusema kweli ilikua inaboa, tulilazimika kuwa naye karibu kwani wazazi wangu walikua wanhdani anaweza kujidhuru. Kusema kweli niliona kama anaigiza kwa namna nilivbyokua namfahamu Kaka nilijua kuwa hajaumia kihivyo ila kwa jinsi wazazi wangu walivyokua wanauliza uliza kila saa, kuonekana kuwa labda yeye dniyo kaumizwa ilimfanya Kaka kudake kama mtoto.


“Hawa ndio wanamharibu! Huyu hajaumia chjochote, namfahamu!” mdogo wangu aliniambia, naye alishachoka tabia za Kaka lakini hakua na namna, yeye ndiyo alikua ndugu wapekee wakiume, alitakiwa kukaa naye ili tu asijidhuru.

‘Kaka ni mshenzi, linakua kama llitoto, unajau anamlaumu mchumba wa Marehemu eti ndiyo kasababisha, yaani ujicha mtupu, na Mama anamdekeza yaani kama yeye dniyo kafiwa.” Nilimuambia.

“Anaigiza mshenzi huyu, juzi kaenda kukuatana na mwanamke mwingine, jana kaondoka nyumbeni kaenda kwake, kalala na mwanaume na kampiga dada wa watu, namuuliza ananiambia kuwa bado ana hasira za huyo X wake, Kaka sio kabisa!”


Kila mtu alichoka na baada ya mdua tuliacha kukaa na Kaka, wiki mbili baadaye aliacha kujidekeza na akarudi kazini, maisha yaliendelea kama kawaida. Siku moja usiku tukiwa nyumbani kwa Kaka, mimi na mdogo wangu ndiyo pekee tulikua tukiishi pale kwani Kaka alikua kambini na hatukutaka kwenda nyumbani. Usiku kwenye saa mbili hivi kuna mtu alikuaj na kugonga mpango. Nilienda kufungua, ila nafungua tu na kutana uso kwa uso na aliyekua mchumba wa marehemu.


Alinisalimia wakati nashangaa na kuniomba kuingia ndani, kusema kweli nilishindwa ni jibu nini nilishikwa na butwaa lakini kabla hata sijamjibu kitu aliingia ndani na kufunga geti, gari yake aliiacha nnje.

“Haitachukua muda sana,” Aliniambia akiongozana kuingia ndani.

“Lakini Kaka hayupo kama ndiyo ulikua unmamtaka.” Nilimuambia, nilihisi labda kuna vitu anataka kuongea na Kaka.

“Hapana, si mhitaji yeye, najua hayupo, ameenda Iringa, kuna kazi katumwa na atarudi baada ya siku tatu, sikuja kumuona yeye bali ninataka kuonana na wewe na mdogo wako nyie pia si mlikua mnaishi na marehemu hapa?” Aliniuliza, nilimuitikia ndio ingawa sikujua sababu lakini nilidhani labda ana maswali kuhusu maisha ya marehemu.


Niliona labda alikua ameshindwa ku move on ndiyo maana kaamua kuja, niliwaza mambo mengi lakini yeye hata hakujalli kuwa mimi sikuwepo. Aliingia mpaka sebuleni, bila karibu alikaa chini, akaingiza mkono wake mfukoni na kutoa flash.

“Hii Tv yenu si inatumioa flash?” Aliongea hukua kitembea kuelekea kwenye TV kubwa pale sebuleni, aliiwasha na kuchomeka Flash, alifanya kama mwenyeji, ingawa sina kumbukumbu lakini ni kama alishawahi kuingia pale, alichomeka flash na kuniambia nikamuite mdogo wangu kwani kuna kitu anataka kutuonyesha.


Alirudi kwenye Sofa na Kukaa, nilitoak na mdogo wangu ambaye naye alishangaa kumuona pale, lakini yeye hakujali, alituambia tukae pembeni yake, ingawa alikua anaongea kawaid alakini ni kama alikua analazimishia flani, tulikubali na kukaa.

“najua mnaishi na Kaka yenu, mnajua tabia zake na mnawaza hivia kija kujua kama nimekuja nyumbani kwake atafanya nini? Msijali hatafanya chochote.” Aliongea na kunyamaza kidogo kisha akaendelea.

“Ninajua kuwa mnajua tabia zake, mnajua ushenzi wake lakini kuna kitu nataka muone, nataka mjue kuwa maisha yenu kuanzia siku ya leo yatabadilika sana, kuna vitu nitavifanya mpaka mtatamani hamkuwahi kuzaliwa ila wakati ninavifanya nataka mjue ni kwanini navifanya.”


Aliongea kwa sauri ya chini kabisa, lakini alionekana kumaanisha, ilijaa hasira sana na visasi. Flashi iliwaka, kwanza ilianza kuonyesha picha mbalimbali, zilikua ni picha zamarehemu za kawaida, kisha zikafuata picha za uchi, alionyesha picha nyingi za uchi za marehemu, akiwa amepigwa Kalala, nyingine amepigwa akiwa anajuakama vile kajiandaa kupigwa, picha akijichezea mwili wake na picha nyingine za ajabu ajabu.


Baada ya hapo zilifuata video, video ya Kwanza ilikua inemuonyesha Kaka yangu, yupo uchi wa mnyama anamlazimisha marehemu kukaa vizuri ili wafanye mapenzi na kuonekana kwenye kamera. Kusema kweli nilishindwa kaungalia nikajikuat naangalia pembeni.

“Hivi kwanini unatuonyesha, si uache haya mambo yapite, hapo unamdhalilisha Marehemu!” Nilimuambia, alinigeukia kwa hasira kisha akaniambia.

“Bado hujaanza kuona, nataka uone kila kitu, nataka ujue kitu alichokiafanya kaka yako!” Aliongea kwa hasira, alinilazimisha kuangalia, ile nageuza tu macho nilitamani kutapika kwa kitu alichokua anakifanya Kaka!”


NB; Kuna vitu katika maisha tunavifanya tukiviona vya kawaida ila mwisho wa siku vinaumiza wengine. Watu wanauliza hivi hii stori ni ya kweli? Mimi nawauliza, ni video ngapi za uchi ushawahi kuziona mitandaoni zimevujishwa na wanaume tena wengine watu tulikua tunawaona wamaana.


Je unafikiri hao mabinti wanakua katika hali gani wakidhalilishwa, naongea nao, kuna watu wshenzi, Binti, mwanaume akikuambia umtumia picha ya uchi muambie hapana, akinuna kwakua hujamtumia muambie kwaheri! Nasikia mengi sana naona mengi sana, and yes hiki kisa kinamhusu mtu!




Mambo aliyokua anayafanya Kaka yalikua yanatisha, alikua anamlazimisha X wake kufanya mpenzi kintyuma na maumbile huku akirikodi, katika sehemu hizo alikua anaficha sura. Alikua anampiga sana huku akimtishia kuwa kama akikataa basi atavujisha picha zake nyingine ambazo alikua ashamrekodi huko nyuma. Dada wa watu aliishia kulia na kukubaliana na kila kitu alichokua anafantyiwa, kusema kweli ilikua inasikitisha, nilitamani kuacha kuangalia lakini yule Kaka alilazimishia, hakua na silaha yoyote lakini alionekana mkali sana na alionekana kuwa hana utani.


“Mlikua mnaona yote haya, mlikua mnaona anvyonyanyaswa, nataka muangalie kila kitu ili mjue kuwa ndugu yenu ni mtu wa namna gani?” Aliongea, mimi nilianza kulia, yalikua ni mateso makubwa kusema kweli ilikua ngumu kuvumilia.

“Huamini? Hata mimi si amini, mwanzo mke wangu hakunaimbia haya, alikua ananiambia kuwa anapigwa basi, hakuniambia kama kulikua na unyama kama huu. Lakini Kaka yenu asibyo na adabu kaaamua kumdhalilisha, sasa hivia memuua mke wangu, lakini hakumuu tu mke wangu, kamuua na mwanangu, kanichukulia familia yangu!”


Aliongea kwa uchungu sana, alitaja mara nyingi mke wake na familia yake.

“Sina sababu ya kuendelea kuishi na maumivu ya namna hii, najua tunakatazwa kulipa kisasi lakini kwakua Kaka yenu amechukua familia yangu na mimi nitachukua familia yake, anajiona kuwa ana akili sana, anajiona kuwa ana nguivu, ana kazi nzuri, mshaara mzuri lakini bnakuhakikishia kuwa mpaka namalizana na nyie atakua hana kitu, atakua chizi na hatafanya chochote!” Alikua anaongea sauti ya kawaida, alikua anaongea kama vile anatania lakini alikua anaamanisha, nilianza kuogopa kwani alionekana mtu aliyeumia sana, alionekana kama mtu ambaye amaketa tamaa ya maisha na kama unavyojua watu waliokata tamaa wnaakua wabaya sana.


Alihakikisha tunaangalia kila kitu, vitu vyote, vipigo, picha za uchi na bideoa mabzo zilikua zinamuonyesha maehemu akifanyiw avitendo vya ajabu na Kaka. Baada ya hapo aliichukua ile flash na kuobondaboda, aliiharibu na kuweka mabaki yaake mfukoni kisha akanyanyuka na kusema.

“Nimeshafunga ukurasa wa mke wangu sasa nataka kufungua ukuufrasa wangu. Namba yangu hii, Kaka yenu akitudi muambieni nakuja kuchukua kopi ya picha zote na video zote za mke wangu, aniandalie na muambieni ahakikisha ananipa kila kitu!”


Alituambia wakati anaondoka, kusema kweli nilitamani iwe hivyo lakini nilihofia, kwa ninavyomjua Kaka nilijua kuwa hawezi kumpa kitu chochote na tukimuambia atakasirika, anaweza hata kumuua huyo Kaka wa watu. Niliogopa, niliamua kuongea na kumuonay kuhusu Kaka.

“Kaka yangu si mtu wa hivyo, mimi naona uniache niongee naye taratibu ili azifute, nikimuambia ulikuja hapa atakasirika na anaweza kukufanyia kitu kibaya.” Nilimuambia kwa uoga, nilikua najisikia vibaya kwakua niliona wifi yangu akinyanyasika na sikusema chochote, sikuaka hali hiyo itokee kwa Kaka wa watu ambaye alikua anaonekana mstaarabu sana. Niliamua kumuambia ili yasije kumkuta, lakini yeye hakuonyesha kujali, aliniangalia kwa dharau na kisha akajibu huku akicheka.


“Kaka yenu ni Choko tu, hawezi kunifanya chochote, ukiona mwanaume anapiga mwanamke huyo ni Choko atasumbua wanawake tu ila wanaume hawezi kuwezana nao. Mpeni taarifa kuwa ninakuja kuchukau nvitu vya mke wangu na akikleta ujinga nitamvalisha Pampas!” Alituacha na kuondoka, wote tulibaki na butwaa, nilishangaa ni kwanini alikua anajiamini namna ile wakati alikua anamjua vizuri Kaka yangu.


Baada ya kuondoka mimi na mdogo wangu tulikaa na kuwaza tufanye nini, ilikua ni kama vita na sijui ni nani angeshinda, tuliwaza kumuambia Kaka lakini wote tulikua tunamuogopa, tulijua atapaniki na anaweza kumfantyia Kaka wa watu kitu kibaya. Tuliwaza sana na mwisho ntukaamua kumuambia Baba kwani yeye pekee ndiyo anawezana na Bbaa, tuliamua kumuambia kila kitu kuhusiana na hizo picha, mwanzo hakuonekana kushtuka.


“Achaneni na hayo mambo, huyo mtu kachanganyikiwa, anachotaka ni huruma tu, kama ana ushahidi kuwa mwanangu kahusika basi aende Polisi, mbona mambo ni marahisi, mchumba wake ameshakufa, kajiua mwenyewe hivyo asimhusishe mwanangu!” aliongea kwa hasira na kutushutumu sisi kana kwamba ndiyo tunamuendekeza, alitutukana na kutumbia hataki kusikia hayo mambo.

“Lakinia masema kuwa Kaka akija tumuambie, anatakaa kuja kuchukua picha na kila kitu!”

“Nimewaambia sitaki kusikia tena huo upumbavyu, huo ujinga wenu siutaki kabisa. Aje kufanya nini? Picha picha gani, nawaambia sitaki muwasiliane naye, namba zake futeni, sitaki ujinga kabisa, kwanini mnakua hamna akili, mtu kafiwa na mke wake mtarajiwa, mwanamke wake alikua Malaya, ana hasira kwanini asipaniki!”


Baba aliongea sana, alitukataza kumtafuta huyo Kaka na kuchukau simu zetu, akafuta namba za hiyo Kaka huku akituambia tusiliongele tena hilo swala, tusimuambie Kaka wala mtu mwingine yoyote tena. Hata Mama tusimuambie kwani tutampa presha bure. Mkweli tulinyamaza, hatukuliongelea tena hilo jambo, hata Kaka aliporudi hakuna mtu hata mmoja ambaye aliongelea hicho kitu.


***

Mwezi mmoja ulikua umepita, yule Kaka hakutusumbua tena, lakini siku moja nikiwa mjini nilipigiwa simu na namba ngeni, nilipokea na alijitambulisha nikajua kuwa ni yule Kaka. Kusema kweli niliogopa kwani sikujua kama hata ana namba zangu.

“Namba zako nimepewa na Mama yako, nipo hapa nyumbani nasikia ujumbe wangu hukufikisha, hembu njoo mara moja kwani wewe peke yako ndiyo umekosekana.” Aliniambia kisha akakata simu, nilipaniki, nilikua kwenye gari nikashindwa kuendesha, nilikua naelekea kwa Kaka kuna mizigo alinituma kwaajili ya kuleta nyumbani wkani yeye alikua nyumbani. Nilimpigia kka ayangu ili kumuuliza yuko wapi lakini simu haikupokelewa, nikampigia Baba kumuuliza ila simu yake ilipokelewa na yule Kaka.


“Nimekuambia njoo nyumbani, kila mtu yuko hapa, hata Kaka yako yuko hapa, huna haja ya kuogopa njooo achana na hivyo vitu ulivyotumwa kwenda kuchukua utaenda nikiondoka!” Niliishiwa nguvu kabisa kwani kwa namna alivyokua anaongea ni mtu aliyekua akijiamini, nilishangaa ni namna gani anakuja nyumbani kwetu, Kaka yupo na jinsi ninavyomjua Kaka angekua ahsawaka mpaka basi, nilihofia kabisa kwamba inafikia hatua anapokea mapaka simu ya Baba.


Nilijitahidi na kuendesha gari mpaka nyumbani, nilifika na kuingia ndani, nilikuata wote wamekaa, nyumba ilikua kimya, Mama, mdogo wangunna Kaka walikaa kwenye kochi lililokua limeangaliana na yule Kaka ambaye alikaa peke yake, Baba naye alikaa kochi la peke yake, nilienda na kulaa alipokua kakaa Baba.

“Mnaniacha mgeni peke yangu, si vizuri….” Aliongea kama utani huku akicheka, lakini hakuna aliyecheka, wote walionekana kama vile wanamuogopa flani.


“Nisiwapotezee muda, kuna ujumbe nilikupa ili umpe Kaka yako, lakini naona kuwa hukumuambia ni kwa nini?” Aliuliza huku akisimama, alianza kutembeatembea akituangalia kama watoto wadogo. Nilimuangalia Baba lakini hakuonekana kama ana jibu, nikamuangalia Kaka alikua kimya sana, haikua kawaid ayake yaani kwa kumuangalia ni kama alikua anamuogopa, alikua kama anatetemeka falani, mpaka nilishangaa ni kwanamna gani Kaka siku ile alikua anaogopa.


“Huongeei kwanini hukumuambia Kaka ayako anikusanyie vitu vyote vya mke wangu na kwanini hukunipigia simu kuwa Kaka yako ameshakuja?” Aliuliza huku akinisogelea, niliwanagalia ndugu zangu lakini sikua na msaada wowote. Nilimuangalia Baba kisha nikasema.

“Mimi nilimuambia Baba lakini alisema tusumiambie Kaka na tuache kukusikiliza…” Niliongea kwa uoga, aligeuka na kumuangalia Baba kisha akamuambia.


“Kumbe wewe ndiyo unaharibu watoto, unajua kitu alichonifanyia mwanao?” Alimuuliza, Baba alinyamaza kimya, ujasiri wake wote ulimuishia, sijui yule Kaka alifanya nini wakati mimi sipo ila niliona kama vile wanamuogopa.

“Basi nitaanza na wewe, umeharibu familia yangu nitahakikisha na wewe huna familia. Wewe si ndiyo kila kitu, sasa muambie mwanao akaniletee ushahidi wote wa mke wangu, nataka kulinda familia yangu, sihitaji chochote kutoka kwenu lakini nahitaji kulinda familia yangu.”


Hapo aliongea kwa upole kidogo, Baba alimgeukia Kaka, alimuambia aende kuleta ushahidi, kaka alisema vitu haviko pale akamuambia aende kuvileta kwani yeye hana haraka. Yule Kaka aliniambia kuwa mimi niondoke nakuongozana na JKaka ili kuhakikisha kuwa anarudi na kuchukia kila kitu huku yeye akibaki pale. Kweli tuliondoka, mimi ndiyo nililazimika kuendesha gari kwani kaka alikua kama anatetemeka na sijui ni kwanini alikua vile.


Njiani tulikua kimya, mpaka tunafika Kaka hakuongea chochote, aliingia ndani na kuchukua flash, laptop yake na vitu vingine kisha akachukua Bastola yake.

“Kwanini uanchukua, unataka kwenda kufanya nini?” Nilimuuliza,a liniambia hakuna kitu anachukua kwaajili ya usalama.

“Kwani yule kaja na silaha, inamaana ndiyo kitu mlikua mnakiogopa, kawatishia.” Nilimuuliza maswali mfululizo.

“Hajaja na chochote ila sijui kwanini simuamini, nina wasiwasi ana silaha kwani anajiamini sana, nilitaka kummaliza ila nilikua sijajua kama ana silaha au la, anajiamini sana na sijui ni kwanini?”


Nilimsihi Kaka asichukue silaha lakini hakunisikiliza, alikua ahsaamua na kusema kuwa anachukua kwaajili ya tahadhari.

“Haya madude yake nataka nimpe, yaani hata mimi yananisumbua sana, unajua yanaweza kuvuja tena nikaambiwa ni mimi!” Aliongea huku tukiwa kwenye gari, ingawa alikua na silaha lakini alikua na wasiwasi kuliko kawaida. Nilimuuliza yule Kaka alikua kawafanyia nini lakini hakua na jibu.

“Aliingia tu na kusalimia,a kakaa chini na kutuita wote, mimi nilikua chumbani, nilipokuja nikakuyta kakaa, akanilazimisha kukaa chini, sijui nini kilitokea lakini sikua mbishi, nilijikuta nakaa chini na kumsikiliza kila alichokua anaongea. Sijui kama ana silaha lakini najaribu kumsoma ila siwezi, aani anajua mambo mengi sana kuhusu mimi, hata mambo ya ndani ya kazini kwangu anajua, mpaka naogopa, anaweza kuwa ana mtu ananifuatilia kazini ndiyo maanaa hata alijua kuwa leo nitakua nyumbani nashindwa hata chakufanya, nashindwa kumuelewa.


“Au na yeye ni Mwanajeshi, maana anajiamini?” Nilimuuliza Kaka wakati tunakaribia kuingia ndani.

“Hapana, namjua, nilikua namjua tangu zamani, anafanya tu Biashara zake, lakini sina uhakika, huyu si mwanajehi, sijui, labda usalama lakini hapana, ila anajuana na watu wengi kwani ananijua sana na hicho ndiyo kinaniogopesha.” Kaka alijibu, tulishuka na kuingia ndani, alikua amekaa anaongeaongea kama anatania anajichekesha mwenyewe. Baada ya sisi kuingia hakutaka kupoteza muda, alichukua vitu vyote pamoja na Laptop ya Kaka.


“Hiyo ina mambo yangu muhimu ya kazini, nimeileta ili uone nikifuta vitu!” Kaka alimuambia wakati anachukua, kwa hapo Kaka alipata ka ujasiri flani kwani ni kama alikua anamzuia asiichukue.

“Mambo gani ya kazini fala wewe, hivi unaniona mtoto, wewe huna cheo chochote ni mtu wa kutumwa, unaandika nini cha maana amabcho siruhusiwi kukiona, hembua chia huko.” Aliongea hukua kimsukuma Kaka aliiachia na kwenda kukaa.


“Unakumbuka siku ile nilikuambia kuwa Kaka yako ni Choko tu ataishia kupiga wanawake, sasa unaona, ameenda huko kachukua na Bastola eti kaja nayo, jamani mimi sina silaha yoyote, sihitaji silaha kwani sikuja kwa shari kabisa!” Sijui aliionaje kwani kwa sehemua aliyokua ameificha Kaka ilikua ni ngumu kuiona, alimuamrisha kaka kuitoa ile Bastola, kama zuzu Kaka aliitoa na kumkabidhi, aliiangalia na kuifungua kuona kama ina risadi, kweli ilikua nazo.


Aliifunga na kumkabidhi Baba.

“Kaa nayo, usimuache mwanao akakaa nayo kwani ipo siku unaweza kuja kusikia kajitundika risasi kichwani.”

Baba aliipokea huku akitetemeka, Kaka alikua kimya hakufanya chochote.

“Unajua kuitumia?” Alimuuliza Baba, Baba alitingisha kichwa kuonyesha kuwa hajui. Aliichukua tena ile Bastola akaanza kumuelekeza Baba.

“Ukitaka kuitumia kwanza sunafanya hivi…” alimuelekeza kisha akamalizia.

“Hata kama maisha yamekushinda na unataka kujiua, usinwye sumu kama mke wangu, inaumiza sana, mke wangu aliteseka sana, unaichukua unaweka mdomoni, unaingiza kabisa kiosha unavuta hapa, au unaweka chini ya kidevu ukipiga tu unakua umevuruga ubongo wote unakufa hapohapo hakuna maumivu tena.”


Aliongea, Baba alikua anatetemeka, alikua anakubaliana naye kila alipokua akiulizwa kama ameelewa au la?

“Ngoja tuangalie kama inafanya kazi…” Aliongea huku akiishika, aligeuzia Baba kisha akaacha na kumgeuzia Kaka. Mama kuona vile aliaqnza kupaniki, akaanza kupiga kelele kuomba smamaha, alianza kulia, Kaka mwenyewe alianza kumsihi kwua asifanye hasira, alikua anatetemeka mpaka akajikojolea, yule Kaka Alianza kucheka, yaani alikua anacheka kicheko cha mtu kama chizi flani, kama unaangalia movie za mazombi kuna wale ambao wanakua kama wajinga flani wanacheka kisha wanaua ndivyo alikua hivi yule Kaka.


“Inaumaeee! Mtoto anaume, hembu vuta picha mtu kakuuliza mke wako na watoto? Hivi mnavyolia hivi mnajua kitu ambcho mtoto wenu amenifanyia, mmenoan picha za mke wangu mwkeli, mnadhani alipenda kufa! Natamani niwaonyeshe ila ni kuendelea kumdhalilisha lakini huyu mtoto wenu hatakiwi kuendelea kuishi.” Aliendelea kuongea, kila alivyokua akizidi kuongea basi ndiyo ahasira zilikua zinampanda, alikua anazidi kumsogezea Kaka Bastola kichwani na mara tukasikia “Paaaaa!” mlio wa risasi!


Unataka kujua kuwa huyu mtu ni nani? Je amemuua Jamaa na ni nini kitafuata? Basi usikose kufuatilia.


(NB; Kisa hiki kime-base kwenye stori ya kweli ila baadhi ya vitu vimebadilishwa ili kuwalinda wa husika na familia zao)



“Haustahili kufa, unatakiwa kuishi kwa mateso mpaka ujutie siku ulipomuua mtoto wangu.” Yule Kaka alionge, ile risasi hakumlenga kaka yangu, aliipiga juu na baada ya kuipiga alichukua ile Bastoa na kumkabidhi Baba.

“Chukua kaihifadhi sehemu nzuri, nina uhakika kuna siku utaihitaji!” Aliondoka na kutuacha pale, kwa zaidi ya nusu saa tulikua tumesimama kila mmoja akimuangalia mwenzake, wote tulijawa na uoga hata Kaka ambaye alikua ni mwanajeshi, alikua anajiamini sana alikua anaogopa mpaka anatetemeka kabisa.


Baada ya yule Kaka kuondoka hakuna mtu aliongea kitu, kila mmoja alitoka kivyake, ni kama alikua ametuwekea dawa kwani hata Baba alifuata maelekezo yake na kwenda kuiweka ile Bastola hakumrudishia Kaka. Hali ya ukimya iliendelea katika familia yetu, tulianza kuishi kwa kuogopana, kila mmoja akimuona mwenzake kama adui, hakukua na maongezi tena. Nyumba haikua na amani tena, mimi niliondoka nyumbani na kwenda kuishi kwa rafiki yangu wa kiume, kusema kweli hali ya pale ilinitisha, sijui yule Kaka alitufanyia nini lakini mimi baada ya lile tukio nilijawa na hofu sana.


Usiku mmoja nilipigiwa simu, Baba alikua katika hali mbaya, nilishangaa kwani siku mbili kabla Baba alimpigia Mama simu kuwa anasafri, kuna rmzigo anaenda kuchukua Morogoro, alikaa kwa siku moja na kurudi. Lakini aliporudi nyumbani hali yake haikua sawa kabisa, alikua anatetemeka kama mtu mwenye baridi kali, alikua kama kachanganyikiwa, haongei kitu yaani ilikua ni hofu tu. Pamoja na yote yaliyotokea lakini nilikua nampenda sana Bba yangu, kama mtoto pekee wakike nyumbani wketu Baba yangu alikua ndiyo kila kitu. Niliongozana na mchumba wangu mpaka nyumbani, nilifika wakati wanajiandaa kumpeleka hopspitalini.


Lakini Baba alikua anagoma kupelekwa hospitalini, alikua haongei vitu vingine lakini likija suala la hospitalini absi anakataa aktakata, anaongea na hata kutaka kupigana. Kaka alipigiwa simu na kuja, alimuona vile na kuanza kumbembeleza Baba kukubali, baada ya kuongea naye alikubali, wakati huo tulikua sebuleni, akaomba kuingia ndani kubadilisha nguo ndiyo twende. Mama alitoka na kwenda jikoni, siju alikua anaangalia nini lakini haikupita hata dakika mbili, tulisikia mlio wa risasi “Paaaa!”


Kila mtu aliogiopa, Kaka alinyanyuka harakaharaka kuingia chumbani lakini alikuta Baba ameshafariki dunia. Baba alikua kachukua Bastola ya Kaka na kuiweka mdomoni kama alivyoelekezwa na yule Kaka na kujilipua, ubongo wopte ulikua chini, damu zilitapakaa chini kiasi kwamba hata kumuangalia ilikua ni shida. Mimi nilishindwa kuangalia, nilirudi sebuleni lakini kabla hata ya kukaa chini nilidondoka na kupotea fahamu.


Nilikuja kuzinduka masaa mawili baadaye nikiwa niko hospitalini, kumbe wakati nandondoka niliumia kichwa, kitu cha kwanza nilimuulizia Baba lakini watu waliniangalia tu, nilijua kuwa ameshakufa lakini nilitaka mtu kuniambia kuwa nilikua naota Bbaa alikua hai. Niliambiwa nikazimia tena, nikawa mtu wa kuzimia na kuzindika, nazimia nazinduka mpaka kesho yake ndiyo nilitolewa hospitalini.


Nilitoka hospitalini ambapo maandalizi ya mazishi ya Baba yalikua yanafantyika, hakuna mtu aliyekua anajua sabbau za Baba kujiua lakini akili yangu nilihisi kuwa kuna kitu ambcho yule kaka aalikifanya mpaka Bbaa kufikia hatua ya kujiua. Ilikua ni huzuni kubwa, kila mtu alikua anaumia kivyake kwani hakuna mtu aliyekua anaongea na mwenzake, Kaka ndiyo alikua kachanganyikiwa kabisa, kila wakati alijiona kuwa yeye ndiyo alikua ni sababu ya kifo cha Bbaa.


Maandalizi ya mazishi yalifanyika, siku ya mazishi yule Kaka alikuja kwenye mazishi ya Baba. Hakuishi kuja tu kanisani au makaburini bali alikuja mpaka kutusalmia na kutupa pole baada ya mazishi ya Baba. Yaani baada ya watu kutoka makaburini alikuja na kutusalimia sisi tena kwa kutushika mkono na kutupa pole. Nilikua na hasira sana lakini nilijikaza, alimfuata Kaka yangu na kumpa mkono, kaka alikataa kumshika mkono, alimshika Begani na kumuambia.


“Afadhali wewe umezika Baba ni mtu mzima kayachoka maisha mimi nimezika mke na mtoto kwa siku moja, inauma sana uchungu nilioupata hata nusu haujaupata.” Kaka alikasirika na kurusha kofi kutaka kumpiga lakini yule Kijana alilidaka lile kofi na kuurudisha mkono wake chini. Wakati hicho kitu kinatokea kuna Baba mmoja ambaye ni Bosi wake na Kaka yangu alikuja pale. Alimsihi kaka yangu kuacha vurugu na kisha kuanza kumuomb a msamaha yule kaka mwingine, akiomba msamaha kwa niaba ya Kaka tena kwa heshima, alimuomba waondoke akamuondoa pale.


Baada ya kama dakika kumi hivi yule Bosi wake na Kaka alimfuata Kaka na kumuuliza.

“Unamjua yule mtu uliyekua uantaka kumpiga?” Kaka alitingisha kich3wa kusema hamjui.

“Hata sijali, yule mbwa ndiyo kamuua Baba yangu!”

“Kivpi wakati unasema alijipiga risasi na wewe ulikuepo?” Bosi wake alimuuliza kwa mashaaka.

“Sijui lakini najua tu, hata kama hajampiga yeye ila ni yeye kasababisha, nina uhakika kuna kitu kamfanyia Baba yangu na nitajua tu undani wake!” Kaka aliongea kwa hasira.

“Basi nikuambie tu, hata kama ni kweli kakuumiza lakini achana na hayo mambo, yatakupotezea kazi, achana na huyo mtusi mtu mzuri usipambane naye! Hiyo ni amri na si ombi!”


Kaka alitaka kubisha alimuuliza huyo ni nani ndipo bosi wake alimuinamia na kumnong’oneza, hatukusikia chcochote lakini baada tu ya kuambiwa Kaka alinyong’onyea hakuongea kitu, alibaki kimya, mpaka Bosi wake anaondoka Kaka hakuongea kitu hata tulipomuuliza hakusema kitu. Maisha yaliendelea kila mtu akiwa kivyakae. Lakini haikuisha hata mwezi Kaka alisimamishwa kazi, akaanza kunyw apombea, akawa ni mtu wa vurugu kupiga watu mtaani mpaka akaja kugukuzwa kazi.


Mpaka wakati huo hakuna mtu aliyekua anajua sababu za Baba kujiua, hali ya Mama ilikua mbaya kwani alikua na presha na sukari lakini figo zake zilianza kufeli, maisha yalikua magumu, mimi nilikua nimemaliza chuo sina kazi, mdogo wangu anasoma chuo hana mkopo Kaka aliyekua anamlipia ada alishakua mlevi na hakua na kazi.


Ilifikia hatua hata chakula nyumbani ilikua ni shida, Kaka aliuza nyumba yake na pes ayote ikaishia kwenye pombe, Matibabu ya Mama yalikua ni ghali sana, huwezi amini niliamua kujiingiza kwenye Biashara ya kuuza mwili ili kuweza kumhudumia Mama kwani mdogo wangu wa kiume baada ya kusimamishwa chuo kutokana na ada aliondoka nyumbani akaw2a anaishi na mwanamke Mama mtu mzima ambaye alikua anamlea.


Nilihasngaika ili kuhakikisha angalau nyumbani wanakula, Kaka alitaka kuuza nyumba tuliyokua tunaishi lakini niligoma kwani hata nilikua nayo, ikawa ni ugomvi, kila sikua anrudi nyumbani, anataka chakula na akikosa ni kunipiga, alikua ananipiga sana, Mama alikua mdhaifu akiongea basi anamtukana matusi mpaka ya nguoni. Siku moja nilikua kwenye misha miehse zangu, nilikua na mwanaume ambaye alininunua.


Wakati natoka nataka kuingia kwenye gari na huyo mwanaume Kaka aliniona, alinifuata na kuanza kunipiga, alinipiga Mimisana na yule kaka alipoingilia alianza kumpiga, alimpiga sana mpaka watu wakaingilia, akakamatwa na kupelekwa polisi. Alikaa mahabusu kwa wiki mbili, hakukua na mtu wa kumuewekea dhamana, Mama alipojua aliniambia nimsamehe lakini sikua tayari kwa hilo. Lakini siku moja tu nilishangaa Kaka katoka, alirudi nyumbani na kujifanya kuomba msamaha kwani amejifunza.


Nilimuuliza ni nani kamuwekea dhamana akaniambia hajui ila kesi imefutwa, aliniambia huyo mwanaume niliyekua naye kaamua asinisitaki tena. Niliamua kumtafuta huyo mwanaume kwakua nilikua na namba zake, tukaonana nikamuuliza kwanini kafuta kesi basi alishangaa, akaniambia kuwa Kaka yangu mwingine alimfuata na kumpa milioni mbili ili asiendelee na kesi.

“Aliniambia nichukue milioni mbili nifute kesi au niache milioni mbili iende mahakamani akamazlizane na hakimu. Mimi nikaona kuwa Kaka yako hawezi kunilipa chochote, hata akifungwa basi hawezi siwezi kufaidika chochote. Nilichukua milioni mbili na kufuta kesi!”


Nilishangaa ni Kaka yangu gani ambaye anaweza kutoa milioni mbili, nilimuulizia aliponielezea ndipo niligundua kuwa alikua ni yule yule Kaka ambaye alikua ni mchumba wa wifi yangu. nilizidi kuchanganyikiwa kwani nilijua kuwa kama kamtoa Kaka absi ana malengo yake, kweli baada ya siku mbili alikuja nyumbani, akaja kutusalimia, alinikuta Mimi na Mama, Mama alikua kitandni hali yake mbaya, hata hakua anaweza kumtambua kwani kumbukumbu zake zilianza kupokea.


Alimuulizia Kaka yangu niakamuambia katoka, aliniangalia kwa dharau na kuniambia.

“Nashukuru, ndiyo nilichotaka….” Nilimuuliza anamaanisha nini.

“Kaka yako angefungwa angerudi ni mtu mzima, lakini sasa hivi na hizo pombe nina uhakika kama ambavyo mimi sina amani basi yeye hana amani na nyie hamna amani!” Aliongea kwa hasira, alionekana kuwa na chuko sana. Nilijikuta nakasirika na kumuuliza.

“Kwahiyo Bdo hujamsamehe Kaka yangu, unajua mke wako angekuepo angetaka umsamehe!”

“Najua, kwakua alikua ni mwanamke mzuri lakini Kaka yako na familia yenu mlimharibu, sasa hayupo kusamehe, nipo mimi na klazi yangu ni mpaka kuhakikisha kuwa mnaishi kwa mateso mpaka mtamani kufa!”


“Huoni kama na wewe unajitesa, kwanini usisamehe na kuwa na mania tu,”

“Najua najitesa lakini ndiyo hivyo, siwezi kusamehe, nataka Kaka yako ateseke mpaka siku moja atamani kujichoma kisu afe, tofauti na hapo nitaendelea kuhakikisha kuwa hawi na amani kwani mimi sina amani!” Aliongea huku analia, kusema kweli alikua na kisasi lakini alionekana yeye kuumia zaidi.

“Ulimfanya nini Baba yangu?” Niliamua kumuuliza, nilikua namuogopa lakini suala la kifo cha Baba liliniumiza sana, ni kitu amcbho nilishindwa kukisahau, kwa nilivyokua namfahamu Baba yangu nilijua kabisa asingeweza kujiua kizembe namna ile.


“Sikumfanya kitu, nilimuonyesha tu ushenzio wa mtoto wake ndipo akaamua kujiua…” Alianza kunielezea. Alipozichukua zile flash na memory za Kaka alitaka kuzichoma moto, lakini alibaki nazo, siku hiyo Baba anaaga anaenda Morogoro alikua hajaenda, alimchukua yeye mpaka nyumbani kwake, walikua wawili tu. Akamuonyesha Baba zile video zote, namna Kaka alivyokua anampaka mke mchumba wake, namna alivyokua anampiga na kumtukana.


Baada ya kumaliza kumuonyesha alimvua Baba nguo zote, kisha akamuambia.

“Unaona, mimi ni tofauti na mtoto wako, uko uchi mbele yangu, ningeweza kukuiga, kukubaka, kuwaita watu wakufanyie ushenzi na usingeweza kunifanya chochote lakini nimeamua kuacha kwakua mimi ni mwema. Sasa vaa nguo zako na ondoka, ninachotaka kukuambia kuwa mwanao hatakua na amani tena, alifanya makosa sana kuniulia mtoto wangu, alifanya makosa sana!”

“Inamaana hukumgusa Baba yangu?”

“Hapana, ningemgusa nisingekua na tofauti na Kaka yako, nilitaka kumuonyesha tu kuwa mimi ni mshenzi kama nikiamua kuwa mshenzi na mwanae ni chkoko tu kwangu.”

“Lakini ulijua kuwa atajiua?”

“Nijue kwani mimi ni Mungu!” Aliongea kwa hasira na kuondoka, aliniacha nikiwa nimeduwaaa.


Nilipata amani kidogo kujua kuwa Baba hakufanyiw akitu kibaya sana lakini niliumia kuwa ushenzi wa Kaka yangu ndiyo ulimuua Baba yangu. Hali ya Mama ilizidi kuwa mbaya, ilifikia hatua hata chakula kikawa ni cha shida mpaka mwaka jana mwishoni ndiyo Mama yangu alifariki dunia. Ingaw ani Mama yangu lakini nilishukuru Mungu kuwa angalau anaenda kupumzika, kusema kweli Mama yangu aliteseka sana. Kaka alilazimishai mpaka tukauza nyumba tukagawana kila mtu kibyake, kipindi hicho hocho ndiyo nilianza kukusoma Kaka Iddi.


Niliamua kuchukua pesa yangu nikanunua kitabu chako cha Biashara, nikafungua Biashara ya kuuza vyombo. Kaka yeye pes ayake iliishia Baa, alianza kuja dukani kwangu kunisumbua,a nataka pesa nikimnyima ananipiga, kuna siku alinipiga mpaka nikalazwa hospitalini, nikamuuliza amemuua Baba na sasa anayaka kuniua na mimi. Niliripoti Polisi na kufungua kesi lakini nahsii yule Kaka aliingilia kati Kaka ayangu katoka.


Ni Kaka yangu wa damu lakini natamani kumfunga, natamani asiwepo mtaani, yaani sina amani, nikiwa wkenye mahusiano atatafuta namna ya kuyavunja. Baada ya mambo kuwa magumu sana niliamua kumtafute yule Kaka na kumuomba msamaha, nilimuambia kama ni kujifunza tushajifunza atusamehe kwani familia yetu imeshasambaratika, aliniuliza unataka nifanye nini. Nilijikuta namjibu.

“Nataka sasa hivi nikim[peleka Kaka yangu Polisi umauche huko huko, muache aoende jela labda atajifunza.”


Yule Kaka aliniangalia kwa huruma na kuniambia.

“Sitaingilia tena mambo yenu, wewe mpeleke tu!” kusema kweli alikua anazungumzia mimi kumfunga Kaka yangu lakini jibu lake limenipa amani sana. Najua ni suala la mdua tu Kaka yangu ataharibu na mimi nitalazimika kumpeleka Polisi, ni ndugu yangu lakini nimechoka, Kaka yangu kamuua Baba, Mama na sasa anataka kutuuana sisi, hapana, na mimi nina msiha bora akaozee tu jela na sisi tupumue!


MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG