Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

MUNGU KWANINI UMEUFUNGA MLANGO HUU!

  

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

MAMA MONICA; MUNGU KWANINI UMEUFUNGA MLANGO HUU!


“Unajua Ng’ombe kama hazai tunaita Tasa, hivi na binadamu naye tunaita hivyo hivyo, maana mke wangu ni mwaka wa kumi sasa anakula tu na kulala lakini hazai, ni kunijazia choo tu, heri Ng’ombe unajua mwisho wa siku utakuja kula nyama, lakini huyu naye nampeleka wapi?” Joseph aliongea kwa kejeli, alikua anamuambia mke wake Monica ambaye alikua kakaa pembeni akimlisha mtoto.


JOIN US ON TELEGRAM

“Usiseme hivyo Kaka!” Agness, mdogo wake wa mwisho alimuambia. Ndiyo kwanza alikua kidato cha sita na alikua akiishi na Kaka yake.


“Nisiseme kwani uongo?” Aliuliza huku akimuangalia Mama yake ambaye alikua anacheka kana kwamba kitu alichokua akikiongea mwanae kilikua ni kitu cha kuchekesha.


“Si umfukuze? Mimi unajua nakushangaa sana Kaka, una roho ya ajabu, yaani unakaa na mtu kama huyu hazai miaka yote hiyo, kama ni mimi nafukuzia mbali naendelea na maisha yangu! anakurudisha nyuma sana!” Dastan ambaye ndiyo alikua akimfuatia Joseph aliongea, yeye alishaoa na alikua na mtoto mmoja.


“Kaka yako ana roho nzuri sana, si kama wewe, unaona namna anavyomlea na kumhudumia huyu mwanaume, tatizo lijitu lenyewe hata halina shukurani, kutwa kucha kuhangaika kwa waganga, mtu kashaletewa watoto alee eti anataka kuzaa wakwake!” Mama yao aliongea, yalifuata maneno mengine mengi ya kashfa.


Kwa namna walivyokua wakiongea ni kama vile Monica alikua hayupo pale, pamoja na kuumia lakini alinyamaza kimya.


“Nina huruma lakini ananisaidia, msema ukweli ni mpenzi wa Mungu, hazai lakini anajua kuwa Mama, wewe unafikiri asingekuepo hawa watoto ningelea na nani? Labda Mungu kaamua kunipa mgumba ili wanangu walelewe vizuri.” Joseph au Baba Moreen aliongea, alikua akijichekesha chekesha, huku akimpiga piga mkewe mgongoni.


“Si unaona Moreen, kaliletwa kakiwa kadogo lakini sasa hivi kawa mkubwa na kalelewa vizuri, huyu  mwanamke muone hivi tu lakini anajua kulea, kwa hilo nampenda , angekua na kizazi tu basi angeweza kuwa mke mwema.” Baba Moreen aliendelea kujiongelesha na wote walicheka kasoro Agness ambaye baada ya mambo kuzidi alinyanyuka na kuondoka.


“Kana mpenda wifi yake, unajua kanaona kama tunakosea lakini ndiyo ukweli mtu kama hazai wanini sasa!” Mama yao aliongea huku akiwaangalia wengine, wote walicheka wakati Agness akitoka..


“Utoto tu, akikua atajua namna ambavyo mimi Kaka yake nateseka, unajua watu wanadhani mimi nafurahia lakini najikaza, ndoa miaka kumi bila mtoto unafikiri mimi naishije?” Monica alinyanyuka na mtoto na kutoka nnje, hakua akilia, alishalia sana kutokana na manyanyaso ya mume wake mpaka ikafikia hatua machozi hayatoki tena. Mara nyingi ndugu wa mume wake wakija na kuanza kujiongelesha maneno ya kumkera alikua akikaa kimya na yakimzidi basi huondoka.


Alitoka nnje kumbembeleza mtoto, alikua akilea mtoto wa miezi nane, huyo alikua ni mtoto wa nane yeye kuletewa na mume wake ili kumlea. Joseph na Monica walianza mahusiano yao tangu wakiwa chuo, walikutana kipindi Monica yuko chuo mwaka wa kwanza na Joseph yuko mwaka wa tatu. Pamoja na Joseph kutangulia kumaliza chuo lakini alisugua sana benchi akiwa hana kazi. Monica alimazlia chuo na kupata kazi katika shirika moja kubwa tu la kiserikali, akiwa na mshahara mzuri aliweza kumsaidia mpenzi wake.


Kwanza alikua akimhudumia yeye pamoja na ndugu zake mpaka alipopata kazi, tena yeye ndiyo alimuunganishia ile kazi. Mama yake ambaye kipindi hicho alikua ni mtu mkubwa serikalini alikua anajuana na watu wengi hivyo Monica alipomtambulisha rasmi kama mchumba wakena kuongea na Mama yake alimuunganisha na kupata kazi nzuri tu ambayo ilikua na mshahara mzuri pia.


Ndoa yao ilikua na amani mpaka ilipofika miaka miwili ya ndoa bila mtoto, mwanzo ilikua ni mipango ya Mungu lakini baadaye Joseph alichoka na kuchepuka, alimzaa binti yake wa kwanza Moreen, hakumuambia mke wake lakini alimuambia Mama yake ambaye kila siku alikua akimpigia kelele kua anataka mjukuu. Baada tu ya kuambiwa kuwa mtoto wake wakwanza wakiume ana mtoto basi alianza maneno, alianza kumlazimisha mwanae kumuoa Mama Moreen walishaanza na maandalizi lakini dakika za mwisho mwanamke alikiambia.


Alipata mzungu wake na kuondoka kwenda kuishi Marekani, kwakua alidanganya kua hana mtoto alilazimika kumuacha mtoto wake wa miezi mitatu kwa Joseph na kuondoka. Hata hakuga mpaka alipofika huko ndipo alipopiga simu na kumuambia kua yeye hawezi kuolewa na mwanaume ambaye anaendeshwa endeshwa na Mama yake. Kila kitu ni kama kilimuuma Joseph kwani baada ya hapo alianza kuwa mkali na alilazimika kumuambia mkewe, alimuomba msamaha kwa kuchepuka na ingawa Monica aliumia sana lakini hakua na namna.


Alishahangaika sana kutafuta mtoto bila mafanikio, alishafanyiwa mpaka upasuaji kuondoa uvimbe katika kizazi chake lakini hakuwahi kushika ujauzito. Aliambiwa kizazi kiko mbali akavutwa, akaambiwa homoni zake hazijakaa sawa akapewa dawa, aliambiwa mambo mengi sana lakini mwisho haikusaidia, alikata tamaa na kuamua kukubaliana na hali yake. Mwanzo mume wake alikua upande wake na walikua wakivumilia pamoja, alishangaa ghafla analetewa mtoto.


Alimchukua Moreen akiwa na miezi mitatu na kuanza kumlea kama mwanae, ingawa alijaribu kumficha na kumuambia kua yeye ndiyo Mama yake, lakini tangu Moreen akiwa mdgo hajitambui mpaka anajitambua na kuanza shule Baba yake alikua akimuambia kua yule si Mama yake.


“Mama yako yuko Marekani, huyu ni Mama wa kambo hivyo kama akikunyanyasa mimi ni Baba yako njoo niambie!” Mara kadhaa alikua anamuambia, Monica alishanga ni kwanini anafanya hivyo, alikua akimlalamikia lakini mumewe hakujali.


Alikua akimuambia yeye ni muikristo hawezi kumuambia mwanae uongo.


“Hata kama lakini huyu mtoto bado mdogo, akijua mimi si Mama yake anaweza kunichukia na kuacha kunisikilia.” Mkewe alimuambia.


“Heyyy! Kwahiyo uatakaje, unataka watu wajue kua una mtoto wakati unajua kua wewe ni mgumba, kwanini usikubaliane na hali yako tu!” Aliendelea kuongea kwa kejeli, Baada ya Moreen walifuata watoto wengine saba ambao wote alikua akimletea mke wake kulea tena wakiwa wadogo sana kwani pamoja na kuwa na kazi nzuri lakini alikua hahudumii chochote na kwa aina ya wanawake ambao hutoka nao basi anajikuta akichiwa watoto.


***


Mwanzo alikua akihangaika na mume wake katika kuzunguka kwenye mahospitali, lakini baada ya Joseph, kupata mtoto wannje aliacha kuhangaika kabisa, alijua tatizo ni la mkewe kwani wanae wote alikua anafanana nao kama vile kopi flani. Pamoja na manyanyaso yote hayo lakini Joseph hakua tayari kumuacha mke wake, Monica alikua na kazi nzuri na mara nyingi alikua akipata safari nyingi za kikazi hivyo alikua na pesa nyingi kumzidi.


Lakini pia alikua na akili sana, alikua bize kufanya mambo ya maendeleo wakati yeye pesa zake ziliishia kwenye pombe na wanawake, katika miaka kumi na mbili ya kufanya kazi alikua hana hata kiwanja alichokua kanunua na pesa zake. Kila kitu kilikua ni cha mke wake ingawa vyote vilikua na majina yake.


“Mimi ndiyo mwanaume humu ndani na kila kitu kitakua na jina langu kama hutaki ondoka!” Mara kadhaa alimuambia mkewe ambaye alikua akivumilia.


“Mume wangu naomba ujitahidi basi ada ya mtoto maana sasa hivi sina pesa kabisa.” Siku moja Monica alimuambia mume wake, yeye ndiyo alikua akiwalipia watoto wote ada, kazi ya mumewe ilikua ni kuzaa tu na kuwaleta pale.


“Mtoto gani? Wewe si ndiyo unajifanya Mama yake, sasa lipa ada, mimi sina pesa za mchezo, hivi kwanza wewe pesa zako umepeleka wapi?” Joseph alimuambia mkewe kwa hasira.


“Nimewalipia hawa wengine, hujui kuwa na Neema naye kaanza shule, imebidi nimpeleke chekechea, sina pesa kabisa na Mama yake naye hata hajali. Mama yangu naye anaumwa alikua Muhimbili juzi halafu hukwenda hata kumuona…”


Mama mkwe wake likua kalazwa muhimbili lakini Joseph alikua hajaenda kumuona, alikua na matatizo ya figo, ili kumfichia mume wake aibu Monica alilazimika kuwaambia ndugu zake kua mumewe alikua Mwanza kikazi pamoja na kwamba alikua akionekana mjini.


“Kwahiyo unanikomoa? Yaani kwakua sijaenda kumuona Mama yako ndiyo hutaki kuwalipia wanangu ada! Kwahiyo unaona kama Mama yako ni wamuhimu kuliko wanangu! Kama huwezi kuwapenda wanangu si unaweza kuniua wewe!” Alifoka kwa hasira.


“Hapana sio hivyo, Mama ana matatizo ya figo, zinahitajika pesa nyingi sasa na mimi nimeona nichangie kila siku nawaambia ndugu zangu kuwa sina pesa naona wamenichoka, yule ni Mama yangu kumbuka siwezi kumuacha kufa!”


“Uchangie kwenu si mnajifanya kuwa mna pesa! Sasa kama mnapesa kwanini mnashindwa kumtibu, kwanza wewe ni mtoto wakike, umeolewa ni kiherehere gani cha kuchukua mali za familia kwenda kumpa Mama yako! Hivi uliniomba ruhusa wewe, kuna siku ulikuja ukaniambia Mama yako anaumwa nikuruhusu kutoa pesa, au kwakua unafanya kazi ndiyo unataka kunipanda kichwani”


“Hapana lakini…”


“Lakini nini? Unamuona Mama yako ndiyo wa muhimu sana kuliko Mama yangu. Juzi Mama yangu kakuomba pesa, alikua aende kwenye harusi ya rafiki yake Mbeya ukasema kua huna pesa leo pesa za kumpa Mama yako ashazeeka mtu anakaribia kufa akatibiwe unazo! Hivi wewe mwanamke una akili kweli? Naona unataka kunipanda kichwani, hujafundishwa kwenu vizuri, hujui ndoa ni nini, mimi ndiyo mwanaume humu ndani sasa kama utanidharau na kuanza kutawanya mali za familia labda si mimi, siwezi kuruhusu upumbavu huo!”


Joseph aliongea hukua akimvamia mke wake na kuanza kumpiga, alifunga chumba na kutoa mkanda wake, alimtandika mke wake sana huku akimpiga mateke. Alainza kukagua mikoba yake kutafuta pesa za mkewe alikutana na Shilingi laki tano ambazo zilikua katika pochi ya mkewe na kuzichukua.


“Mume wangu hizo ni pesa za matibabu ya Mama, si zangu nimepewa na Kaka ili kununua dawa!” Monica alilalamika huku akimsihi kutokuzichukua zile pesa, alipiga magoti akilia lakini mume wake hakujali.


Hazikua pesa zake kweli, ni pesa ambazo alipewa asubuhi yake ili kwenda kumnunulia Mama yake dawa kwani Kaka yake alikua anasafiri kikazi hivyo asingeweza kununua. Mume wake alizichukua na kuondoka bila kujali kilio cha mkewe.


“Kwa taarifa yako hizi nachukua na hizo nyingine ulizochukua kumpa Mama yako ndiyo utalipia wanangu ada, huwezi kuchukua mali za familia na kwenda kuwapa ndugu zako, wewe ushaolewa yakwenu unaacha huko huko kwenu. Hivi huna akili hata kidogo ya kutambua kua mimi nakusaidia, mtu mwenyewe mgumba lakini unanisumbua namna hii, si bora nikuache tu nitafute wanawake wenye akili na vizazi vyao?” Aliongea hukua kimsukuma kwa teka na kuondoka na zile pesa.


ITAENDELEA…


MAMA MONICA; MUNGU KWANINI UMEUFUNGA MLANGO HUU—SEHEMU YA PILI


(ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA; Joseph anachepuka na kumletea mke wake watoto nane ili kuwalea, mke wake ambaye hamhudumii chochote yeye ndiyo kichwa cha familia, Joseph hahudumii chochote na anampiga sana mke wake. Mama yake Monica kalazwa Hospitalini lakini hajali, anampiga na kumnyang’anya pesa za kununulia dawa je nini kitatokea? ENDELEA…)


Kama kawaida yake Monica alificha mambo aliyokua anafanyiwa na mume wake, siku ile ile alihangaika kutafuta pesa kwaajili ya matibabu ya Mama yake na mpaka jioni alishaipata, alimnunulia dawa na kumpelekea. Bado hali ya Mama yake ilikua mbaya, ingawa alijikaza sana lakini hakukua na matumaini yoyote. Nyumbani pale alikua na binti mmoja tu wa kazi ambaye hata hivyo alikuahatoshi kwani kazi zilikua nyingi. Kuhudumia watoto nane tena wenye umri unaolingana lingana halikua jambo dogo.


Mtoto mkubwa Moreen alikua na miaka nane na mtoto mdogo kabisa alikua na miezi tisa, wote walitelekezwa na Mama zao, wanawake wengi aliozaa nao Joseph walikua ni wale wakujiuza, alikua akikutana nao katika mishe mishe zake mjini na wakibeba mimba zake wakidai matumizi kidogo anawaacha hivyo wakijifungua huja kumtelekezea watoto na alikua akimpa mke wake kuwalea.


Monica alikua hospitalini, mwanzo alimuambia wifi yake Agness kua atabaki hospitalini kwajaili ya Mama yake hivyo kwenda nyumbani kumsaidai Dada wa kazi kwani ingawa Agness alikua akiishi pale mara nyingi lakini siku hiyo alikua kwa Mama yake, lakini Agness alipomuambia Mama yake kua anaenda kumsiadia wifi yake kwakua yuko hospitalini Mama yake alimkataza, kwasababu hiyo Agness alimtumia wifi yake meseji kua hataweza kwenda kumsaidaia, lakini Monica hakuziona hali ya Mama yake ilikua mbaya sana hivyo alikua bize kumhudumia, hakusikia hata meseji zikiingia wala simu ikipigwa.


Alikaa hospitalini akijua kama wifi yake yuko nyumbani, lakini haikua hivyo, nyumbani alikua binti wa kazi peke yake. Kutokana na kazi nyingi alishindwa kufanya chochote zaidi ya kuwaangalia watoto ambao bado walikua wadogo sana. Joseph alirudi nyumbani akiwa amelewa, alipigiwa simu na Amina, mmoja wa wanawake ambao alizaa nao, huyu alikua kidogo anajielewa lakini walishindwana kwakua alikua hahudumii mtoto.


Mara kadhaa Amina alipenda kwenda nyumbani kwake kufanya fujo akidai mtoto wake lakini kila akipewa hukaa naye wiki mbili tatu na kumrudisha. Mtoto wake wakike alikua bado mdogo, alikua na mwaka mmoja na nusu. Alifika pale nyumbani na kumkuta mtoto wake kachafuka, analia na hakuna mtu wa kumbembeleza kwani msichana wakazi alikua bize na watoto wengine na alishindwa kuwamudu wote.


Kuona vile Amina alianza kutukana, alianza kudai mtoto wake na kusema kua atamchukua na Joseph hatamuona tena. Alimpigia simu na kumuambia anamchukua mtoto na siku inayofuata anampeleka Ustawi wa jamii. Joseph ambaye likua Baa akinywa alipaniki, aliingia kwenye gari na kurudi nyumbani, alimuulizia mke wake na kuambiwa kuwa alikua kaenda hospitalini kumuangalia Mama yake, alizidisha hasira, ingawa mkewe alimuagana akamruhusu lakini bado alikasirika, alimsihi Amina asimchukue mtoto kwa kujitapa kua anaweza kuhudumia watoto wake lakini Amina alikataa.


Kwa hasira aliingia kwenye gari na kwenda mpaka Hospitalini alipokua amelezwa Mama mkwe wake, alikua akijua wodi aliyokua amelazwa kwani mke wake alimuambia mwanzoni akitegemea kwamba atakuja kumsalimia hivyo alienda moja kwa moja kumuona. Wakati huo Monica alikua akijiandaa kuondoka ili kuwahi nyumbani kwani alikua akijua hekaheka za nyumbani kwake. Lakini kabla hajatoka alimuona mumewe, alifurahi akidhani kaenda kumuona Mama yake.


Ingawa haikua wakati wa kuwaona wagonjwa lakini Joseph aliwaambia walinzi kua kua kaenda pale kumchukua mkewe na si kuona mgonjwa, kwa namna alivyoongea ilikua kama mke wake anafanya kazi pale. Walimeruhusu kuingia lakini alipofika na kumuona tu alianza kumpiga makofi na kumtukana, hakujali watu waliokua wanaona, walinzi walikuja kumshika ndipo alimuambia hataki tena kumuona ana asirudi tena nyumbani kwake. Walinzi walimshika na kumtoa nnje mpaka kwenye gari lake na kumuambia aondoke.


Aliondoka lakini kwa kutukana, baada ya kuondoka akiwa kwenye gari alianza kutuma meseji za matusi, vitisho na kumuombea  Mama yake afie mbali. Kwake alikua akiumia na kukasirika kwanini mke wake aliacha wanae na kwenda kumhudumia Mama yake. 


“Tutaona sasa kama huyo Mama yako akifa utaenda kuishi wapi, sitaki kukuona nyumbani kwangu na takataka zako zitakufuata kwenu huko huko ukimaliza msiba wa Mama yako!” Aliandika, Monica alivumilia lakini alishindwa, mumewe alijua kua hakuna kitu kingine ambacho angeweza kumtukania nacho na kumuumiza zaidi ya Mama yake.


Alishamtukana sana kuhusu mgumba, alishampiga sana lakini bado alivumilia, Monica alishazoea lakini baada ya kutukaniwa Mama yake ukizingtia na hali ya Mama yake aliumia sana. Pamoja na yote hayo lakini bado Monica alirudi nyumbani, ilikua ni usiku alienda kugonga, alishangaa kukuta vitu vyake viko nnje ya geti na alipogonga tu mlango alitokea Amina. Alikua kajifunga Khanga moja.


“Mume wangu kasema uondoke, takataka zako hizo hapo!” Amina aliongea kwa dharau, mume wake alikua ndani na hakutaka hata kutoka. Monica alijaribu kuingia lakini alimzuia, 


“Moreen anaumwa kuna dawa zake natakiwa kumpa naomba basi nikamtolee.” Alimuambia huku bado akiomba kuingia ndani, Amina alikataa katakata. Ulizuka ugomvi mkubwa pale nnje, Monica akisisitiza ile ni nyumba yake na hakuna mtu wa kumzuia kuingia. Mume wake alitoka na kumuona pale, alimuomba msamaha na kumuambia kua anachohitaji ni kumtolea dawa mtoto na kuchukua baadhi ya vitu vyake.


Joseph kusikia suala la dawa alimruhusu kwani alikua anajua kuwa mtoto wake anaumwa tangu jana yake. Monica aliingia, watoto walikua bado sebuleni na alipoingia tu walimkimbilia kumkumbatia.


“Mama Monica! Mama Monica!” Walimuita na kumsalimia, ndivyo walikua wakimuita hivyo kwani mara kadhaa walipokua wakimuita Mama Baba yao alikua akiwakataza. Monica alienda mpaka sehemu alipoweka dawa alizitoa na kumpe mume wake.


“Mpe huyo ndiyo Maza house sasa hivi, nimeamua kuoa mtu mwenye kizazi chake, wewe huwezi kuwalea wanangu.” Mume wake aliongea kwa kejeli, Monica alionekana kuwa na mawazo mengi, hakutaka hata kumsikiliza.


“Niache mume wangu, Mama yangu yuko katika hali mbaya naomba uniache tu kwa leo hata nipumzike…” Aliongea lakini mumewe alilipuka.


“Mjinga kweli wewe! Mama yako ndiyo kitu gani, yule si ashakufa, tena yule mwanamke ndiyo anakupa kiburi na vimalimali vyake mpaka unaidharau ndoa yake, mnajifanya mnapesa lakini hamna lolote, sikutaki hata kama angekufa wala nisingejali.”


“Eeeeeh! Wakiwa na pesa wanajifanyaga watu wamaana sana na kutuidharau sisi wengine, kama anapesa sana muambie akununulie kizazi!” Amina aliingia kati, Monica alikua kakaa kitandani, mume wake alimshika na kumnyanyua, alimsukuma mpaka nnje, watoto waliona na kuanza kupiga kelele lakini Joseph hakujali, alimfukuza mke wake na kumuambia hamtaki tena.


Monica alilazimika kuondoka akiwa njiani mume wake alimpigia simu, alipokea na kabla ya kuongea chochote alianza kumtukana alimuambia ashamuacha na ameamua kumuoa Amina kwani ana kizazi hivyo anaweza kumlelea watoto wake vizuri.


“Nahitaji mtu ambaye anajua uchungu wa mtoto!” Alimuambia, Monica alijaribu kumbembeleza mume wake ili angalau ampe nafasi ya kumsikiliza na kumuambia kilichotokea lakini hakujali.  Monica alilazimika kwenda nyumbani kwao, lakini alipofika alikutana na vilio.


Mama yake ambaye alikua hana masaa mawili kumuona akiwa hai, kamuacha hospitali alikua tayari ashaaga dunia. Monica alidondoka na kuzimia zaidi ya mara tatu, alilala mpaka asubuhi ambapo alikumbuka kumtumia Mume wake meseji kumuambia kuwa Mama yake kafariki. Akitegemea labda hata atamuonea huruma 


“Kwahiyo hicho ndiyo umeona kitu cha umuhimu kabisa, hutaki hata kujua mume wako nimeamkaje. Unaniambia kuhusu Mama yako unataka nimfue au?”


ITAENDELEA…


MAMA MONICA; MUNGU KWANINI UMEUFUNGA MLANGO HUU—SEHEMU YA TATU


(ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI; Monica anachelewa Hospitaini, anarudi nyumbani na kukuta mume wake yuko na mwanamke mwingine na anafukuza. Wakati anaondoka anamtukana sana, anafika nyumbani anakuta Mama yake kashafariki, je nini kitaendela. Kama hukusoma sehemu zilizopita basi ingia Instagram na tafuta @iddimakengo @iddimakengo)


Baada ya majibu yake mabovu Monica alishidwa kuendelea kuwasiliana na mume wake. Alibaki kuendelea na msiba wa Mama yake, hakumuambia mtu yoyote kilichotokea, hakuna ndugu wa upande wa mwanaume walienda katika ule msiba kasoro Agness tu, kila mtu alishangaa kwani hata Mama mkwe wake hakuenda. Kitu kingine ambacho kilimuuma nikuwa, siku ileile kabla hata Mama yake hajazikwa mume wake alikodi gari na kukusanya vitu vyote vya Monica akawatuma watu kumpelekea.


Alimtumia meseji yeye pamoja na ndugu zake kuwa hamtaki na ameshamuacha yeye na ukoo wake wote. Monica aliumia sana kwani katika kipindi chote cha ndoa hakuwahi kuwaambia ndugu zake kuhusiana na matatizo ya ndoa yake, hata Mama yake mzazi alikua hamuambii, alikua akijisikia vibaya na kujiona kama yeye ndiyo husababisha mume wake kuwa vile kwakua tu hana mtoto.


“Wifi hivi kwanini bado upona Kaka yangu?” Wiki mbili zilishapita tangu mazishi ya Mama yake, mume wake alikua bado hajamtafuta, alikua bado akiishi na Amina lakini kutokana na wote kua walevi walianza kuwasambaza watoto wote kwa kuwarudisha kwa Mama zao kasoro Moreen tu ambaye Joseph alimpeleka kwa Mama yake mzazi. Amina alibaki na mtoto wake tu ambaye naye alikua akilelewa na binti wa kazi kwani muda mwingi walikua wametoka na wako Baa.


Agness baada ya kuona ile hali aliacha kuishi tena pale kwa kaka yake na muda mwingi alikua nyumbani kwa Mama yake. Siku hiyo alienda kumtembelea wifi yake na kumuulizia hali yake. Alishangaa kusikia wifi yake huyo akimuulizia Kaka yake ndipo alimuuliza kwa mshangao.


“Si mume wangu kwanini unauliza?” Monica alijifanya kushangaa.


“Hapana, hata kama ni ndoa lakini hapana, kwa yote anayokufanyia hata mimi ndugu yake siwezi kuvumilia.” Agness aliongea kwa kumponda Kaka yake na kumshangaa wifi yake kwanini alikua anavumilia ujinga kama ule.


“Mimi hata kama sina kazi mwanaume hawezi kunifanyia mambo yote hayo na bado nikanyamazia.” Aliendelea kuongea kwa hasira, wifi yake alisikiliza tu bila kuchangia chochote kuhusu hiyo mada, maneno yake yalionekana kumuingia kichwani.


“Moreen ananiulizia?” Alibadilisha mada ndipo alianza kumuelezea.


“Kila siku, anataka kumuona Mama Monica, kila mtu ni Mama Monica, hata hao wengine Mama anataka kuwachukua kwani watateseka, unajua Kaka ni kama mtoto na hao wanawake zake wote ni walevi, kila siku wanatukanana na mara nyingi watoto wanakutwa Baa, Mama amekasirika.


“Si angewapeleka kwa Dastan, mke wake si hana kazi ni Mama wa nyumbani?” Monicha aliuliza.


“Hivi unamjua yule mwanamke au unamsikia, yule ni Mchaga nadhani Kaka yangu akimfanyia ujinga kama unaofanyiwa wewe anaweza kumkatakata na kumtafuna mishikakia akashushia na damu yake kama kisusio. Hathubutu kabisa, kwanza siku hizi yeye na Mama hawaongei na kamuambia kua hataki kumuona Mama nyumbani kwake kwani yeye ndiyo kiherehere cha kuharibu ndoa. Nakuambia Mama kanywea hataki hata kumzungumzia.”


Agness aliongea kama vile anafurahia kile kitendo cha Mama yake kukatazwa kwenda kwa mwanae.


“Sio vizuri lakini yule ni Mama, Mama hakosei, hawezi kumkataza kumtembelea mtoto wake…” Monica aliongea, alionyesha dhahiri kuumizwa na kile kitu.


“Mama yangu kazidi, hata mimi nikiolewa sitaki akanyage kwangu kabsia, tutakutana huko huko kwake ila kwangu akija akikaa siku mbili namtimua, bora kuonekana mbaya lakini si kuwa na Mama kama yule, hapana.”


Agness aliongea, alionekana dhahiri kuchukia tabia za Mama yake, wifi yake alimsihi kuacha kumuongelea Mama yeke namna ile lakini hakujali, waliongea mambo mengi, Monica alionekana bado kumkumbuka mume wake na kuwaonea huruma watoto namna wanavyolelewa kwani alikua akiwafahamu tabia zao. Waliongea sana na mwisho waliagana, Agness alirudi kwao huku akimsisitiza wifi yake kuwa aanze maisha yake na kuchana na Kaka yake kwani ipo siku atamuua na hatapata faida yoyote. Monica aliishia tu kumuambia yeye bado mdogo hajajua maisha ni nini? Akikua atajua ni kwanini alikua anavumilia.


Nyumani kwao Monica walizaliwa watatu, yeye na Kaka zake wawili, Baada ya Mama yake kufariki alibaki na Kaka zake tu kwani Baba yake alishafariki tangu wakiwa waodogo, Mama yao aliwaachia mali nyingi tu lakini kutokana an uwezo wao mkubwa wa kifedha kaka zake hawakuhitaji chochote, walimuachia kila kitu na yeye aliendelea kukaa pale. Alikua akiishi  na baadhai ya ndugu zake, pamoja na kuwa na kila kitu lakini Monica alikua mpweke sana, mara kwa mara alikua ni mtu wa kujifungia chumbani na kulia tu bila sababu.


Kule nyumbani kwake nako hali haikua shwari sana, Joseph na Amina walikua wakishinda Baa hata mtoto wao ambaye alikua mdogo sana walikua hawajmali. Amina alikua ni mtu wa pombe tu na kupenda starehe, hakua na kazi yoyote zaidi ya kubadilisha wanaume mara leo huyu mara yule, alikua na watoto wengine wawili ambao walikua kwa Baba zao na alishakatazwa hata kuwaona.


Ingawa alikua ni mtu wa kelele sana lakini kukaa na mtoto kwake ilikua ngumu sana, alishindwa na kuondoka kwani Joseph nayeye hali yake ya kifedha iliyumba baada ya mke wake aliyekua akimtegemea kwa kila kitu kuondoka. Siku moja alikuja nyumbani kwa kina Monica, alikua kabeba mtoto, ulikua ni muda wa kazi na alijua kabisa kuwa hawezi kumkuta Monica, alikuta baadhi ya ndugu zake ambao walikua wakimfahamu, aliingia na kusalimia. Hawakua wakijua sana kuhusu tabia zake kwani Monica alikua hawaambii chochote, hata mume wake alipotuma meseji hamtaki na familia yake aliwaomba Kaka zake kumfichia siri.


Hakua mtu wa kutangaza matatizo yake, walimkaribisha vizuri na kama mtu muungwana alitoa pole ya msiba. Walimuitikia na kumletea kinywaji, lakini hakutaka kukaa, aliwaambia amekuja kumaucha mtoto pale kwani anasafiri.


“Tayari nimeshaongea na mke wangu akaniambia nimuache hapa.” Aliongea huku akienda harakaharaka na kuchukua mabegi ya nguo za mtoto kwenye gari yake, aliyashusha na kuondoka akimuacha mtoto kabla hata ya kujibiwa vizuri.


Joseph aliondoka bila hata kuaga, jioni Monica alipokuja alishanga akumuona mtoto pale, mtoto mwenyewe alifurahi kumuona kwani alishaanza kuongea na alikua akimuita Mama. Alimuona namna alivyochafuka kachoka, hakutaka kusema chochote, alimuogesha na kumbeba. Alijaribu kumtafuta mume wake lakini alikua hapokei simu zake, aliamua kutulia mpaka siku iliyofuata ndipo alienda nyumbani kwake.


Kumbuka tangu msiba wa Mama yake alikua hajarudi nyumbani kwake, mume wake alishamuambia kua hamtaki na kumpelekea nguo zake, kutokana na mawazo na mambo mengi aliyokua nayo alimaua kubaki nyumbani kwa Mama yake, hakutaka kuhangaika kwanza na mume wake. Alifika na kukuta geti liko wazi, kwakua ni kwake aliingia lakini alikutana na watu wageni kabisa, kulikua na watoto wanacheza nnje ambao walimsalimia. Alikutana na Mama mmoja mtu mzima hvi na kumsalimia, baada ya salamu alimuulizia mume wake.


Yule Mama alikua hamuelewi kabisa, alikua hajui jina la Joseph hata alipojaribu kueleweshwa.


“Mama mimi na mimi ni mgeni hapa, ngoja nikuitie wenyewe uongee nao.” Yule Mama mtu mzima ambaye alionekana kweli katoka kijijini kutokana na ongea yake na namna alivyokua kavaa. Alimkaribisha ndani lakini Monica alishtuka, hakutaka kuingia moja kwa moja kabla hajajua nini kinaendelea pale, aliendelea kubaki pale na kama dakika mbili hivi alitoka mdada kama kabinti flani hivi kadogodogo.


Alionekana wa kisasa, kabinti kadogo, kichwani alidhani kama ni mchepuko wa mume wake, alikaangalia kwa dharau kwani aliona kama mume wake kaoa mwanamke mwingine mbali na Amina.


“Mume wangu yuko wapi?” Monica aliuliza bila hata salamu.


“Mume wako? Dada mume wako humu ndani, mbona sikuelewi?” Yule dada aliuliza kwa mshangao, alikua akimuangalia angalia kama vile anamthaminisha.


“Ndiyo mume wangu, huyo alokuweka ndani! Umekuja kwenye nyumba za watu ushajimilikisha, nakuuliza wewe ni nani na mume wangu yuko wapi?”


Monica alionekana kupaniki kabisa lakini yule Dada hakupaniki, alikua  katulia na kumuomba kuongea taratibu, yule Mama aliingilia kati na kumsihi wakae waongee.


“Haya mambo ni ya kuongea mwanangu, huna haja ya kupaniki, hembu tuambie unamuulizia nani au umechanganya nyumba?” Mama wa watua liuliza lakini ni kama alitibua.


“Nimechanganya nyumba? Nyumba nijenge mwenyewe halafu mniambie nimchanganya, yaani nimeenda tu kumzika Mama yangu ndiyo mshaanza kujimilikisha kwa taarifa yako hii nyumba ni yangu na huyo mwanaume aliyekuleta hapa ni mume wangu tena tuna ndoa ya kanisani, kama alikudanganya hajaoa basi imekula kwako!”


Aliendelea kufoka, yule binti alizidi kuchanganyikiwa, pamoja na yote hayo lakini hakupaniki. Alichukua simu yake na kuanza kupiga namba flani.


“Kuna mwanamke wako kaja hapa anasema ni mke wako, hivi wewe mwanaume unanitaka nini? Yaani nimekuvumilia kote huko lakini bado uanifanyia haya, wewe si muisalamu wewe? Sasa haya mambo ya ndoa ya kanisani yanakuja wapi?” Yule Dada aliongea, naye alionekana kupaniki, ilionyesha alikua kadanganywa pia.


“Haya ni mambo ya kudhalilishana, kila siku hivi mpaka lini mume wangu? Una ndoa ngapi? Yaani umefunga na mimi ndoa ya msikitini kumbe kuna mwanamke mwingine umefunga naye ndoa huko ya kanisani, nimechoka na sasa hivi naondoka, nishakusamehe snaa mambo yako…” Yule dada aliongea lakini kabla ya kumalizia Monica alimnyang’anya simu.


“Nimechoka! Nimechoka! Hata watoto wako sitaki kuela tena, mimi ni mgumba kweli lakini sasa hivi najalia maisha yangu, sikutaki tena na mwanao kesho nakuletea, mimi nilirudi hata yaishe kumbe una ndoa nyingine.” Monica aliongea kwa hasira lakini kabla ya kukata simu alisikia mtu akiongea.


“Samahani Dada mbona mimi sikufahamu na mimi sijawahi funga ndoa nyingine, kuna haja gani ya kumdanganya mke wangu, sikujui lakini hata kama tulishakutana unatakiwa kuwa na heshima na familia za watu…”


“Wewe ni nani?” Monica alilazimika kuuliza, sauti aliyoku akiisikia kwenye simu ilikua ngeni kabisa, haikua sauti ya mume wake.


Walibishana bishana na kueleweshana ndipo huyo mwingine kwenye simu alijitambulisha kama Alli. Monica alikata simu na kumgeukia yule Dada.


“Mume wako ni nani?” Yule dada ambaye sasa alikua kashapaniki, hakumjibu alimuangalia tu kwa hasira uso kaukunja. Waliangaliana ikabidi Monica kuanza kujielezea kuwa yeye ni nani na pale alikua akimtafuta nani?


“Mimi ni mpangaji hapa, mimi na mume wangu tumehamia jana tu hapa.” Yule Dada alimuambia, Monica alishikwa na butwaa, mume wake alishawaondoa watoto wote na kwakua hakua na pesa ya matumizi kwani alishazoea vyakupewa aliipangisha nyumba yake na kwenda kuishi kwa Mama yake.


Kila mmoja alimuangalia mwenzeke kwa mshangao, walijikuta wanacheka tu kwani ilikua ni kama maigizo flani. Yule Dada alimkaribisha ndani lakini hakutaka kukaa, aliomba kumsindikiza akakubali, alimuaga yule Mama na kuondoka.


“Wanaume hawa ni shida, nyumba tuliyohama tuliondoka baada ya mume wangu kutembea na kumpa mimba mtoto wa mwenye nyumba wakati huo huo alikua anatemba na Mama mwenye nyumba, Baba mwenye nyumba alipogundua baada ya kumtoa mwanae mimba ikataka kumuua ndiyo ikabidi kuhama kwani yule Mzee ana hasira sana angemuua mume wangu.”


Yule Dada alianza kujiongelesha wakati wanatembea, alionekana binti mdogo lakini alikua na mengi, alikua mtu wakuongea sana na ingwa walikua hawajuamni lakini hakujali kumuambia siri zake.


“Wanaume hawa, yaani nilipokuona tu nikajua nawewe umedanganywa na ndoa kabisa, maana mume wangu ni shida, kila nyumba ninayoenda nilazima nikutane na mwanamke wake, nimechoka nimechoka, lakini ndiyo hivyo nitafanyaje, kila mtu ananiambia vumilia, kila mtu ananiambia vumilia, si unajua mwanaume akishakua na vipesa hata kama ni shatani Baba yako mzazi mwenyewe atakuambia vumilia.”


Walijikuta wanasimama na kuanza kuongea, waliongea kama nusu sasa hivi, ingawa Monica si mtu wa kutangaza matatizo yake lakini kwa yule binti ambaye ndiyo kwanza alikua na miaka 22 alijikuta anafunguka na kumuambia karibu kila kitu.


“Umefungwa shogaa! Umefungwa wewe, hakuna cha kizazi kushuka wala uvimbe, umefungwa, hao wanawake wote unafikiri wanafurahia wewe kuolewa, mwanaume mwenyewe anajua ukizaa wakwako wakwake hutalea, umefungwa shoga, haya mambo yapo, watu wanalogewa UKIMWI sembuse kupewa utasa, shogaa hiyo mbona dakika mbili tu unazaa!”


Binti aliku anaongea kama charahani, alimhakikishia kua anaweza kupata mtoto na kumrudisha mume wake.


“Mimi unaona hivi unafikiri mchezo, huyu kanikuta nina miaka 18, kanitoa uisichana kanipa mimba, mara oo namfumania na Mama mdogo wangu eti anataka kumuoa, nikasema thubutuu nani wakugeuzwa uwanja wa mazoezi mechi wachezee kwingine, nilimtengenweza hapuumui nakuambia shogaa nilianza kuhamishia chupi anashtuka nimehamia mzima ashanioa!”


Aliongea, Monica alikua akimsikiliza na kumshangaa, alikuaa kijiuliza kama kweli hayo mambo yake yanafanya kazi inakuaje mwanaume bado anachepuka lakini ni kama yule binti alimsoma na alikua najibu.


“Shoga tatizo mwanaume naye katengenezwa! Si huko kwao, hapana huyu mume wangu mwepesi lakini wanawake zake! Nakuambia kuna sehemu unafika unaambiwa huyu kashachimbiwa kaburini unamfukua unaondoka naye, mimi nimekaa na mwanaume ndani mwaka mzima haisimami haishtuki, lakini nimepambana, wakinifanyia hiki nafanya kile yaani mpaka kufikia hapa mwanaume katulia nimehangaika sana.”


Biti aliongea akimshawishi kuchukua namba ya mtalaamu wake, alimuambia suala la mtoto linawezekana na anaweza kuzaa na mume akamrudia. Monica bado alikua na wasiwasi lakini yule binti alimtoa wasiwasi, alichukua simu yake na kuandika namba ya mganga kisha kumkabidhi wakaagana. Ingawa Monica hakua akiamini sana hayo mambo lakini kile kitu kilimuingia kichwani, hakuwaza kitu kingine tena zaidi ya yule dada na mganga.


Usiku alikua akiwaza sana, alikua kalala kitandani, anawaza kama aisaliti imani yake kwa Mungu na kufungua ukurasa mwingine wa waganga. Alikua akiogopa na kutetemeka, alishika simu na kutaka kupiga ile namba lakini alisita. Aliiangalia mara mbili tatu na kuwaza kama apige au asipige. Alimkumbuka Mama yake, alikumbuka sala zake, alikumbuka namna walivyokua wakihangaika kwenye maombi, lakini baadaye alijikuta anapiga ile namba, lakini alikumbuka mateso anayopitia na kuona ni bora kupiga simu. Simu ilipokelewa lakini kabla hajasema chochote alisikia sauti ya upande wa pili, ilikua ni sauti ambayo anaifahamu, alishtuka kusikia ile sauti kidogo adondoshe simu.


MAMA MONICA; MUNGU KWANINI UMEUFUNGA MLANGO HUU—SEHEMU YA NNE


(ILIPOISHIA SEHEMU TATU; Monica anafiwa na Mama yake mzazi, mume wake anshindwa kuja kumuona pamoja na yeye mwenyewe kumuambia kua kafiwa. Baada ya msiba mumewe anamletea mtoto na kumaucha pale, Monica anaenda nyumbani kwake anakutana na mpangaji ambaye naampa namba ya simu ya mganga anaipiga na kusikia sauti anayoifahamu.)


Monica alisema Haloo, Haloo ila hakusikia majibu ya haloo yake, ndipo alipogundua kua simu ilikua haijapokelewa bado na sauti aliyokua akiisikia haikua ikitokea kwenye simu yake bali ilikua ikitokea sebuleni.


“Muambieni nimekuja kumuona, kama kalala basi subiri nimfuate huko huko chumbani.” Ilisema sauti ile, alishtuka na kunyanyuka, kwake ni kama alikua kaitoka ndoto, hasa aliposikia mambo ya chumbani.


“Anafanya nini hapa leo hii,  mbona hawa watu hawataki kunaicha nikawa na amani na maisha yangu?” Alijiuliza huku akikimbilia mlangoni, alikua kajifunga Khanga moja lakini hakujali. Alitoka mpaka sebuleni ili kumwahi mgeni wake.


“Kafunge nguo mimi ni Mama yako, unanijiaje nusu uchi, au huyo marehemu Mama yako hakukufundisha adabu!” Alikua ni Mama mkwe wake ambaye tangu kuolewa ilikua ni mara yake ya kwanza kumuona pale. Alishikwa na butwaa na kushindwa hata chakufanya, alibaki kasimama tu kama mtu aliyepotea njia.


“Nimekuja, nataka pesa za matumizi, watoto wote nishaletewa mimi, Mama zao hawataki kulea na kama unavyojua mwanangu ushamfanya zezeta hawezi kukaa na pesa hivyo nahitaji pesa za matumizi.” Mama mkwe wake aliongea huku akikaa chini, alinyanyua miguu yake na kuipandisha juu ya sofa akawa kama kajilaza flani hivi.


Kila mtu alishangaa kumuona vile, alikua ni mgeni lakini alikaa kama mwenyeji.


“Unataka bei gani?” Monica aliuliza, alionekana bado kama kapigwa na butwaa hajielewi flani.


Ndugu zake wengine ambao walikua pale walishangaa, alikua akiongea kana kwamba ni kitu walishapanga, walishangaa kumuona yule Mama akiongea vile na Monica akikubaliana na kila kitu.


“Nahitaji kama milioni mbili, si unajua familia kubwa.” Mama mkwe aliongea kwa kujiamini.


“Sawa kuna pesa za rambirambi zipo hapo hata hatujazigusa, nadhani nivyema nikakupa zikawasaidie watoto.” Monica aliongea hukua kinyanyuka.


Aliingia chumbani na baada ya kama dakika mbili hivi alitoka na bahasha ya kaki.


“Halafu mimi sitaweza kuwalea watoto wote, nadhani nitakuletea wewe, unajua kuwalea na wanakupenda sana au utakuja kurudi katika nyumba yako.” Mama mkwe aliongea huku akinyanyuka.


“Sawa Mama mimi napenda watoto sana.” Monica alijibu, alitoka na kumsindikiza Mama mkwe wake mpaka nnje. Aliporudi alikuta ndugu zake wanamuangalia na kumuuliza kwanini alifanya vile.


“Shangazi unajua niliogopa kukuuliza mbele ya yule Mama anatishatisha flani.” Mtoto wa Kaka yake alianza kuongea.


“Kwanini umempa pesa, kwani yeye ni nani hata hukufikiria mara mbili?” Alimuuliza lakini Monica alionekana kama haelewi kilichotokea.


“Pesa gani, unazungumzia nini wewe?” Aliuliza kama vile hakua akijua kitu, walimuelewesha lakini alishindwa kuwaelewa.


“Nyie mnanichanganya tu, kwani hata kama nimempa inawahusu nini?” aliongea kwa hasira na kuingia chumbani kwake. Alienda kukagua Droo ambayo anaweka pea hakukuta kitu.


Alipaniki kidogo, ni kama alikua hajui kilichokua kimetokea, alikaa kitandani na kurudia kushika simu yake, ndipo alikumbuka kuwa kuna mtu alitakiwa kumpigia. Alinyanyua simu na kupiga tena ile namba, ilipokelewa na sasa alisikia sauti ya kiume ikimuambia halooo! Alijaribu kuongea lakini mdomo haukunyanyuka, ghafla pale alipokua amekaa alishangaa kunaanza kuloa damu. Damu zilikua zinamtoka nzitonzito kama mtu ambaye alikua katika siku zake, alishangaa kwani ni siku nne tu zilikua zimepita tangu kumaliza siku zake.


Ingawa zilikua damu kama za mtu aliye katika siku zake lakini wingi wake ulimshangaza, zilikua nyingi kiasi kwamba zikalowanisha godoro. Alipaniki nakutaka kunyanyuka pale kitandani lakini wapi, hakuweza, mwili ulikua mzito sana. Alitaka kupiga kelele lakini hakuweza mdomo haukufunguka, mwisho alilindoka na kupoteza fahamu palepale kitandani.


***


“Nataka umrudie mke wako!” Mama Jose alimuambia mwanae, walikua wako nyumbani wanakukla chakula cha usiku, Joseph alikua ashahamia nyumbani kwao, pamoja na kuwa na kazi lakini alikua hana pesa ya kumuwezesha kupanga nyumba, pesa yote ya kodi ya nyumba aliyochukua iliishia kwa wanawake.


“Mimi simtaki yule mwanamke, nataka kuwa na furaha yangu!” Joseph alimjibu Mama yake kwa hasira, alijifanya kuacha kula kama vile anasusa.


“Nimekuambia utamrudia yule mwanamke anahitaji kurudi katika hii familia, si unaona mambo hayaendi, tangu umuache biashara zangu haziendi kabisa, nataka arudi na mrudi katika ile nyumba yenu!” Mama yake alifoka, lakini Joseph alionekana kutokutaka kabisa, walibishana  kwa muda. Wakati huo Agness alikua akiwaangalia tu.


“Hivi mnaongea hivyo kana kwamba huyo wifi mwenyewe anamtaka Kaka, hamtaki na kwa taarifa yenu anataka kupewa talaka!” Aggess aliingilia kati. Mama yake alimuangalia kwa hasira lakini hakumjibu, alimgeukia Joseph na kumuambia.


“Kama unataka kufa masikini basi muache yule mwanamke, nimeshakuambia nenda kamuombe msama, atakusamehe na rudiisha pesa za watu wafukuze wale watu katika ile nyumba, sitaki kuwaona pale. Hasa kale kabinti, si mtu mzuri, nimeenda pale kananiangalia kama vile nimekachukulia bwana sikataki!”


“Lakini Mama mimi pesa sina, nitarudisheje, pesa zao nishakula na sitaki kumrudia yule mgumba.


“Pumbavu, nimekuambia utamrudia, kama hutaki chukua takataka zako zote na ondoka kwangu, sijui utaenda wapi lakini siwezi kukulea hapa wakati sipati faida yoyote ile!”


“Wifi si mjinga kiasi hicho, hawezi kumrudia Kaka!” Agness aliendelea kuchomekea.


“Hivi una nini nawewe? Unajifanya kujua kila kitu, kwa taarifa yako nimeongea na huyo unayemuita wifi yako na anataka kurudi, hata leo nikimpigia simu anarudi, anataka kuja kuishi hapa lakini nimekataa, nimeshamuambia atarudi kwake na mume wake! Nawewe Mbwa nimekuambia kama ni pesa za kuwarudishia hao wapangaji wako mke wako atakupa, wana pesa nyingi sana wale, atauza hata nyumba ya urithi ili tu kuwa na wewe!”


Mama Jose aliongea kwa uhakika sana, alikua akijiamini kupita kiasi, Agness alikua anacheka tu, aliwaona kama vile vichaa kwani walikua wakipanga mambo ambayo hayawezekani. Baada ya kumaliza kile kikao alitoka na kwenda kumpigia simu wifi yake, alitaka kumuambia kila kitu kilichokua kikiendelea. Alimpigia lakini simu iliita bila kupokelewa, alirudia kupiga na kupiga lakini simu haikupokelewa. Alirudi ndani na kumkuta Mama yake kasimama mlangoni, ni kama alikua anamsubiria kumaliza.


“Hawezi kupokea, atakua yuko hospitalini kalazwa na kesho atakuja yeye mwenyewe kutaka kumrudia Kaka yako, wanapendana sana hivyo vidudu mtu kama wewe hamuwezi kuingilia chochote!” Aliongea kwa hasira, aliondoka huku akimsonya, Agness yeye alijikuta anacheka tu, alishindwa kuvumilia alianza kumtumia meseji wifi yake kumuambia kile kilichokua kikiendelea nyumbani kwao lakini hazikujibiwa, alikata tamaa na kuamua kuacha akipanga siku inayofuata kwenda kumuona.


***


Kila mtu alikua bize na mambo yake, baada ya kujifungia ndani walidhani kuwa kalala hivyo hawakutaka kumsumbua, mpaka usiku mlango ulikua haufunguliwi, walipata wasiwasi na kumuita kaka yeke Monica mkubwa, alijaribu kugonga mlango lakini haukufunguliwa, walilazimika kuvunja mlango, walimkuta Monica kalala kitandani kaloa damu. Harakaharaka walimchukua na kumpeleka hospitalini, alikua kapoteza damu nyingi sana lakini hakupungukiwa na damu kabisa, ilishangaza kwani ni kama alikua hajapoteza hata tone la damu.


Walimtundikia tu maji ili kupata nguvu na dakika kumi tu baada ya kufikishwa hospitalini Monica alizinduka.


“Mume wangu huko wapi? Baba Moreen! Baba Moreen!”” Aliongea kwa sauti ya juu, Kaka zake walikua wakimuangalia kwa mshangao, wifi zake na ndugu wengine walikua pale, aliendelea kumuita mume wake akiomba aende pale kumchukua.


“Nichukue mume wangu, wataniua! Wataniua! Wataniua!” Alipiga kelele kama mtu aliyechanganyikiwa, alikua akijirusharusha kama anataka kunyanyuka na kukimbia. Kaka zake walijaribu kumshika lakini ndiyo alizidisha kelele,


“Nimewaona! Mnataka kuniua! Mnataka kuniua kwa sababu ya mali za Mama! Mnataka kuniua! Sitaki mniguse wanafiki wakubwa, mnajifanya kuniachia kila kitu kumbe mnanizunguka mniue ili mchukue! Sitaki, sitaki mniguse namtaka mume wangu, ondokeni, ondokeni!” Monica alipiga kelele kama mtu aliyechanganyikiwa, ilibidi madaktari kuitwa, wakampiga sindano ya usingizi. Pamoja na kupigwa sindano lakini hakulala vizuri, alikua bado akijirusharusha na kuwa kama mtu anaweweseka, hakuna aliyeelewa kitu ila alikua katika hali mbaya.


Alikuja kuzinduka saa nane usiku, safari hii hakupiga kelele, aliomba simu zake na alipoletewa alichukua na kumpigia simu mume wake, simu iliita bila kupokelewa, alipiga sana lakini haikupokelewa. Alipoona haipokelewi alimpigia simu Mama mkwe wake, ambaye ni kama alikua anaisubiri hiyo simu kwani iliita mara moja tu na yeye akapokea.


“Mama njoo unichukue, mwanao nateseka ndugu zangu wanataka kuniua kwasababu ya mali, njoo unichukue Mama siwezi kukaa hapa wataniua! Wataniua!” Monicha alipiga kelele kwenye simu.


***


Ushauri nilazima uwe umenunua kitabu kama ni Mahusiano kitabu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” na kama ni biashara basi kitabu cha Biashara 50, bei yake ni shilingi elfu kumi kwa kila kitabu. Kupata Kitabu changu unalipia kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222 na ukishalipa Kitabu unatumiwa kwa Whatsapp, Email au Facebook. Ukishalipia kitabu Ndiyo unaweza kunipigia tukaongea Hakuna Kitabu cha karatasi ni mambo ya Digital tu bei yake ni Shilingi elfu kumi.


ITAENDELEA…


MAMA MONICA; MUNGU KWANINI UMEUFUNGA MLANGO HUU—SEHEMU YA TANO


(ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE; Mama mkwe wake anaenda nyumbani kwa kina Monica, anamuomba pesa na bila hiyana Monica anatoa, anaingia chumbani na kuanza kutokwa na Damu kisha anapelekwa hospitalini ambapo baada ya kupata fahamu anawaambia ndugu zake ni wachawi na kutaka kurudi kwa mume wake, je nini kitaendelea. Kama hukusoma sehemu zilizopita basi pitia ukurasa wangu wa Instagram; @iddimakengo )


Asubuhi alikua akiendele vizuri Mama mkwe wake limtuliza na kumuambia ataenda mwenyewe siku inayofuata kwenda kumchukua na kumuambia asiende popote atakuja mwenyewe. Ndugu zake walimuona kama mtu aliyechanganyikiwa, walishangaa ni kwanini alikua akiwaita wachawi, walihisi kama kuna kitu hakiko sawa, walimuacha mpaka asubuhi ambapo baada ya Daktari kupita alikua sawa kabisa na hakukua na sababu nyingine ya kuendelea kumuweka pale.


Aliruhusiwa alienda mpaka nyumbani kwao lakini hakukaa, alimtumia meseji Mama mkwe wake kuwa yuko nyumbani na anahitaji kumuona, alisubiri sana na kuona kama Mama mkwe anamchelewesha, kichwa kilikua kikimuuma sana kwa mawazo na hofu na hakutaka kuendelea kukaa ple nyumbani kwao. Pamoja na kwamba walikua wakimuangalia kwa karibu lakini alifanikiwa kuwatoroka na kwenda nyumbani kwake.


Huku nyuma Mama mkwe wake alikuja, alimuulizia akitaka kumchukua, hapo ndipo ndugu zake walijua kua kashaondoka kwani walipoenda kumuangalia chumbani kwake alipokua kajifungia hawakumkuta.


“Tangu jana alikua anasema anataka kurudi nyumbani kwake, atakua kaenda huko!” Binti wa kazi ambaye pia alikua naye hospitalini aliongea. Mama mkwe kusikia vile alipaniki sana, ni kama hakutaka aende kule, alijaribu kumpigia simu lakini haikuwa inapatikana, alipaniki na kumpigia mwanae Joseph simu.


“Nenda nyumbani kwako, hakikisha mke wako haingii kwenye ile nyumba nimekuambia nenda nyumbani!” Mama mkwe alifoka, mwanae hakuonekana kumuelewa kwani tayari alishalewa.


Alipanda Gari harakaharaka na kuelekea nyumbani kwa mwanae, alifika gati lilikua liemfungwa, alifika mlangoni na kuchungulia, hakuona kitu, nnje kulikua kumepooza. Alinza kugonga kwa nguvu ndipo Bibi mmoja alikuja kufungua mlango, walionekana kujuana kwani yule Bibi alimuangalia kwa dharau ni kama alikua hataki kumuona pale.


“Wako wapi hawa?” Aliuliza bila hata kusalimia.


“Hawa akikina nani? Ndiyo ulivyofundwa kuja kwa watu bila kusalimia!” Yule Bibi aliongea kwa hasira, lakini Mama mkwe hakujali, alimsukuma pembeni na kuingia ndani, alionekana kupaniki, alianza kumuita Monica bila mafanikio, aliingia na kuanza kukagua chumba hadi chumba lakini hakumuona.


“Unahangaika, wameshaondoka!” Aliongea, yule Bibi akimuangalia kwa dharau.


“Wameenda wapi? Niambie nataka kujua?” Mama mkwe aliuliza kwa hasira.


“Nitajua wapi mimi, huyo unayemuulizia kaja hapa na kaondoka na huyu sasa mimi nitayajulia wapi ya vijana.” Bibi alijibu, Mama mkwe alikasirika na kutoka zake, aliingia tena kwenye Bajaji na kuanza kuzunguka mjini kama anatafuta mtu, wakati wote huo alikua akimpigia simu Monica lakini haikua ikipatikana, aliishia kutukana tu na kupiga kelele kama vile kuna kitu amekikosa.


***


Asubuhi Monica alikua akijisikia vizuri, akili yake yote ilikua inamuambia anatakiwa kurudi nyumbani kwake kwani alihisi kama ndugu zake wanamloga hivyo hakutaka kuendelea kubaki pale, kichwa kilimchanganya na alitaka namna ya kutoka tu. Mara simu yake iliita, ilikua ni sauti ya yule mpangaji mpya, Leila, alimpigia kumjulia hali akitaka kujua ni kitu gani kilikua kinaendelea, alitaka kujua kama alimpigia yule mganga wake au la.


“Nimeshindwa, ndugu zangu ndiyo wanataka kuniua, mali za Mama ndiyo zinaniua. Nataka kuondoka lakini sijui nitawezaje kwani wananichunga…” Aliongea maneno mengi, alikua akiongea kama mtu aliyechanganyikiwa, Leila alimuelewa na kumuambia amuelekeze aondoke na kuja kwake kisha yeye atamsaidia. Alimuuliza kama anaweza kutoroka akamuambia hawezi kwani wanamuangalia.


Leila alimuelekeza kutoka nnje, kwakua anaumwa kuomba dawa za usingizi akiwaambia kua hawezi kulala na kichwa kinamuuma, alimuambia kama wakimpa dawa basi asizimeze anywe tu maji kisha kwenda kitandani, baada ya hapo basi hawatamuangalia sana kwani watajua kuwa kalala. Alifanya hivyo na kupanda kitandani, kweli waliendelea na shughuli zao akatoka kiurahisi tu. Alimpitia Leila nyumbani ambaye kumuona tu alimuambia ana tatizo na analijua hivyo kuna mtu wa kumsaidia.


Alimpigia simu mganga wake akimuambia kuwa anampeleke amteja, waliondoka na kwenda kwa huyo mganga. Kwa mambo ya kishirikina Leila alikua hajambo na kweli alikutana na mtaalamu kweli kweli. Baada ya kufanya mambo yake yule mganga alimuambia.


“Una mimba nyingi sana ambazo zilikua zinaingia zinatengenezwa lakini zinaishia tumboni, hivyo kama unataka mtoto nilazima kwanza kuzitoa kabla ya kubeba mimba nyingine.” Monica alikua kimya, ni kama alikua haamini amini, kwake yale yalikua ni mazingira mapya kwake.


Mganga alimpa dawa flani na kumuambia ainywe, aliinywa kama maji kwani mbali nakuwa na harufu mbaya lakini haikuwa na uchungu wowote. Baada ya kuinywa alimuambia asimame, alimuongoza mpaka kwenye chumba kimoja, akamuambia avue nguo kisha achuchumae kama anajisaidia katika beseni kubwa ambalo lilikukua pale. Mganga hakukaa wakati anavua nguo, alitoka na kumuacha Monica peke yake, alimuambia hicho ni kitu ambacho anatakiwa kukifanya mwenyewe. Hata Leila hakuruhusiwa kubaki pale, walitoka na kumuacha Monica peke yake.


Alivua nguo na kubakia kama alivyozaliwa, aliingia kwenye lile beseni kubwa na kuchuchumaa, ghafla alianza kusikia tumbo likimkata, lilikua linauma sana akawa anapiga kelele lakini hakuna mtu aliyetokea kumsaidia. Alianza kutoka damu sehemu za siri kama vile yuko kwenye siku zake, alitoka damu nyingi na zito. Zile damu zilikua na mabonge mabonge zilitoka zile damu kwa muda wa kama nusu saa hivi, kisha zikakata, mganga alikuja na kumuambia ajifunge Khanga katika hali ileile akiwa kajaa damu, alikuja na kuchukua lile beseni.


Alianza kuchambua zile damudamu na kutoa vitu vigumu, Monica alishindwa kuangalia, alitoa vitu vigumu kumi na mbili na kuviweka juu ya kitamba acheupe, vilikua kama vichwa vidogo vya watoto lakini vyaduara. Kisha akamuambia.


“Angalia, hawa ni watoto wako, hivi ni vichwa kumi na mbili vya mimba ambazo ulizipata lakini hazikuonekana, Mama mkwe wako alikua kashikilia, zindiko lake lilikua ni wewe kutokuzaa, wewe ndiyo unayoibeba ile familia ndiyo maana mume wako alikua hataki kukuacha, pamoja na umalaya wake lakini hata yeye alishatengenezwa na asingeweza kukuacha!”


Monica alikua akitetemeka kwa uoga, aliogopa lakini macho yalikua katika vile vitu ambavyo aliambiwa ni vichwa vya wanae. Aliogopa sana kiasi cha kuanza kutetemeka, alikua na hasira nyingi sana.


“Hawezi kukufanya chochote tena, lakini kuwa makini usirudi tena katika ile nyumba.” Alimaliza na kumpa dawa, alimuambia aende kuogea nayo, Mganga alitoka na kumuelekeza sehemu ya kuogea ile dawa. Monica aliingia kuoga na alipotoka alikua akijisikia vizuri, sana yalikua ni matukio ya kama lisaa limoja tu lakini alijisikia msichana kabisa.


***


Mama mkwe na Leila hawakua wakijuana kabla, lakini baada ya mume wa Leila kuhamia katika ile nyumba walikutana, siku moja Mama mkwe alienda kuangalia vitu vyake, kuna vitu alikua ameviweka hivyo aliposikia kuna watu wapya wameenda pale nayeye alienda kuviondoa. Alifika usiku na kuanza kufukua vitu alivyokua kamuwekea Monica. Lakini wakati akifanya hivyo Leila alikuja, alimuona na wote kuangaliana.


“Unafanya nini hapo? Unachofukua hapo ni nini?” Leila alimuuliza, Mama mkwe alishtuka na kujifanya hamna kitu, aliondoka harakaharaka na kuingia kwenye Gari yake bila kuchukua vitu vyake vyote. Leila alienda kuviangalia, wakati anaangalia Leila alikua akidhani kuwa yule Mama alikua anafukua vitu vyake, kumbe nayeye kuna vitu alifukia kwasababu ya mume wake, alikua anamdhibiti mume wake kwa mambo ya kishirikina.


Alichukua vile vitu vya yule Mama na kupeleka kwa mganga wake, siku Monica alipokuja na kuanza kuongea ndipo alijua kuwa aliyekua anafanyiwa uganga ni Monica ili kumkomoa Mama mkwe, aliamua kumsaidia Monica. Mama mkwe baada ya kufumaniwa akifanya mambo yake ndipo alianza kutaka wale wapangaji wapya waondoke pale kwani alijua watakua tishio kwake, lakini kabla hawajaondoka Leila alimuwahi na kumpeleka Monica kwa mganga wake.


Monica baada ya kutoka kwa mganga alirudi kwao, hakumuambia mtu yeyote kitu kilichotokea lakini aliwafuata Kaka zake na kuwaomba wamsaidie kutafuta talaka. Ni kitu ambacho Kaka zake walikua wakimuambia kila siku hivyo kusikia anataka talaka walianzisha mchakato harakaharaka, mume wake alijaribu kupinga lakini hakua na pesa kila kitu kiliendelea. Haikuchukua hata miezi sita walitengana na kugawana vitu walivyo chuma pamoja, nyumba ailiuzwa wakagawana.


Joseph na familia yake mambo yalizidi kuwa magumu, Mama yao alianza kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, alikua hapatani na mtu yeyote, alikua ni mtu wa kukaa tu ndani kama chizi. Agness alimaliza shule na kupata chuo lakini hakupata mkopo, ndugu zake hawakua tayari kumsomesha, Monica alijitolea kumsomesha. Baada ya miezi sita Monica aliingia kwenye mahusiano mengine na kubahatika kupata watoto mapacha wa wawili na sasa wanakaribia kufunga ndoa ya serikali na Baba watoto wake, Joseph maisha yake bado hayajabadilika sasa hivi anaishi na mwanamke mwingine ambaye naye hawajaoana ila kashamzalisha.


MWISHO***

0 comments:

Post a Comment

BLOG