IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO
ANNA; MKE WANGU NAOMBA UNISAMEHE KWAKUKUOA—SEHEMU YA KWANZA
“Kwanini nisikupeleke Hospitalini, hivi unaona jinsi alivyokuumiza, aisee haya si mapenzi, nenda hospitalini ndugu yangu.” George alimuambia Anna, ilikua ni usiku, George ndiyo alikua anajiandaa kulala, Anna alimpigia simu huku akilia, alikua kaenda kumuona, Kelvin, mchumba wake ambaye ndiyo kwanza alikua katoka kujitambulisha kwao na kumtolea mahari. Wakati Anna anaendea kwa kelvin ilikua ni kwenye saa kumi na mbili hivi jioni. Walikua wako vizuri tu, alienda na kumsaidia mpenzi wake kufua, alifua mpaka kwenye saa mbili usiku hivi, baada ya hapo alifanya usafi wa nyumbani na kumpikia chakula.
JOIN US ON TELEGRAM
Baada ya kumaliza kupika hata kabla ya kula Kelvin alimuambia mpenzi wake aondoke.
“Nataka uondoke, mimi nataka kuamka mapema, hivyo ondoka nitakutafuta Kesho!” Kelvina aliongea kama anamkaripia mpenzi nwake, dakika mbili nyuma walikua vizuri, Anna ndiyo alikua anamalizia kupika na kutenga chakula mezani, lakini Kelvina lipokea simu ambayo ilimfanya kumfuata mchumba wake jikoni kwa haraka na kumuambia aondoke.
“Unamaanisha nini? Mbona uliniambia nakuja kulala, mimi nimekuja kulala, nitaondokaje?” Anna aliuliza kwa wasiwasi, alikua kashikilia Bakuli la wali mkononi, alishtuka kidogo kuliondosha kwani Kelvin alimtolea macho akionyesha kuwa anamaanisha.
“Nimebadilisha mawazo, kuna kazi natakiwa kufanya kesho asubuhi, bosi wangu kanipigia, naona ukikaa hapa utanifanya kuchelewa kuamka, hivyo ondoka! Ondoka! Ondoka!” Alishuka kidogo, akaongea kama anambembeleza lakini bado akionyesha ukali, alimshika kiuno na kumkumbatia, alichukua Bakuli alilokua kalishikilia mikononi na kuliweka juu ya meza, alianza kumsukuma akimuambia kuwa anataka aondoke.
“Sasa mbona haraka hivyo Baby, hata kama ni kuondoka si uache basi nioge, nitaondokaje nikiwa mchafu namna hii?” Anna alilalamika, alikua na wasiwasi lakini hakutaka kujibishana na mpenzi wake, alijua kuwa haiwezi kusaidia yeye kumkatalia.
“Utaoga kwako! Wewe vipi, kwanini wewe mwanamke si muelewa, nimekuambia nataka kazi zangu, ondoka.” Aliongea huku akimsukuma na kumvuruta mpaka chumbani, alimpa nguo zake ili kuzivaa, alimvua Khanga moja aliyokua kajifunika, kisha akaanza kumtupia nguo moja moja, alikua akifanya haraaka huku kila sekunde akiangalia ssimu yake, ni kama kuna kitu alikua anahofia, Anna alimuona na kuamua kuulizia.
“Mbona unaangalia angalia simu, kuna mtu unamsubiria?” Alikua anamalizia kuvaa suruali yake wakati anamuuliza.
“Huna kaili wewe, wewe ni mpumbavu mbwa mkubwa, nimetoa mahari tu kwenu lakini unataka kunipanda kichwani, hivi kwanini huwi muelewa, huna akili kabis,a yaani hapa sijakuoa hutaki kunisikiliza, hivi nikikuoa si napata hasara tu mimi! Nimekuambia nina kazi nataka kufanya wewe unawaza tu mapenzi na upumbavu wako! Nasema hivii, ondoka, ondoka! Nataka uondoke nifanye kazi zangu, maswali masawlai yako ya kipumbavu ndiyo yananifanya nashindwa kukaa na wewe!”
Aliongea kwa hasira sana, alimfuata na kumukuma hivyo hivyo mpaka sebuleni, Anna alikua kavaa suruali, tu, alikua kashikilia blauzi yake anataka kuivaa lakini mchumba wake hakumpoa hiyo nafasi, alisukumwa matiti yakiwa nnje mpaka sebulani, wakati huo alikua anahangaika kuvaa brazia yake, kuifunga lakini kutokana na kusukumwa alishinda.
“Inamaana hutaki hata nile chakula?” Alimuuliza kama utani hivi wakati anamalizia kuvaa Braa.
“Hivi una akili kweli, sikutaki, nataka uondoke unawaza kula, mimi Nawaza mambo ya maana, mambo ya kazi, mambo ya pesa wewe unaniletea upuuzi wako wa chakula. Haya si chakula unataka ngoja nikuonyezhe, ngoja nikupe hicho chakula.
Kelvin aqlimuacha Anna sebuleni, alienda jikoni, akachukua bakuli la mchuzi wa nyama, akaja nalo mpaka sebuleni, alichukua pochi ya mpenzi wake na kumiminia ule mchuzi wote, kisha akarudi,a kachukua sufuria la wali na kulileta sebuleni, alianza kuchota na kuuweka kwenye pochi ya mchumba wakeka.
“Basi bwana, sikumaanisha hivyo, acha nachukua, naondoka, nakuchia chakula chako, sitaki kula, acha tu…” Anna alikubaliana na matokeo, alimzuia kuendelea kuwaka chakula kwenye pochi yake ambayo ilikua na vitu vyake vingi, pesa, na kila kitu chake.
Walianza kunyang’anyana akiaka kuchukua huku Kelvin akilazimishia kuendelea kuweka chakula kwenye pochi yake, walivutana, kwakua Kelvin alikua kachuchumaa basi alikos abalansi, alidondoka, kaadondokea kwenye kiti ambacho alikua ameweka lile bakuli la mboga kidogo iliyokua imebaki. Hapo ndipo kimbembe kilianza, mboga zilimwagikia, akasimama na kuanza kutukana.
“Unataka kunipiga, yaani unataka kunipanda kichwani, nimekutolea mahari, nataka kukuoa lakini unataka kunipiga? Unajifanya wewe ndio mwanaume, sasa ngoja nitakuonyesha mwanaume ni nani?” Alimfuata mpenzi wake na kumvamia, alianza kumpiga, alimdondosha chini na kuanza kumpiga mateke, alimpiga mateke ya tumboni, mgongoni usoni na kila sehemu. Kila alivyokua anampiga alikua akimtukana, alikua anamuambia kuwa hamtaki na ana dharau.
“Una dharau sana, yaani una dharau, tangu nikutolee mahari umejiona kama nimekuoa, unataka kunipanda kichwani!” Alimpiga sana, Anna alikua akilia, hukua kijikunja kujizuia ili asiumizwe usoni, kwa ziadi ya dakika kumi alimpiga mpaka akahcoka, kisha akaanza kumvuta akitaka kumtoa nnje, alimvuta kwa kumburuza kama gunia, hakujali maumivu yake, lakini kabvla ya kumtoa nnje mlango uligongwa. Kelvin alipaniki sana, alianza kuzunguka zunguka, ni kama kuna mtu alikua anamsubiria, alkini alishindwa kuufungua mlango.
Alikua anatemba, nenda rudi, nenda rudi, huku akilaumu.
“Wewe mbwa nimekuambia uondoke hutaki, sasa unaona ulichonifanyia, nakuambia kuwa nitakuua! Yaani nikaichwa nitakuua! Nishakuambia kuwa sikutaki, kwanini unaning’ang’ania, mwanamke malaya, unakuja kwangu umelewa, nimekuambia sikutaki!” Aliongea kwa sauri ya juu kana kwamba alikua anataka huyo mtu wa nnje kusikia. Alizunguka zunguka, huko nnje naye alikua anagonga kwa nguvu.
“Najua upo ndani, gari yako iko hapa, kwanini hutaki kufungua?” Ilikua ni sauti laini ya kike, Kelvin alizidi kuchanganyikiwa, alijikaza na kumnyanyua Anna, alikua anamlazimishia kusimama lakini hakua na nguvu za kusimama. Akili yake ilifanya kazi harakaharaka, alienda kwenye friji, akatoa bia moja, akaifungua kwa meno, akaja na kumwagia Anna mwiliki, kisha akamsukumia pembeni na kwenda kufungua mlango.
“Naomba unisikilize, sitaki upaniki kwkaua nimechanganyikiwa, yaani nimechanganyiki3wa, hata mimi sielewei ni kitu gani kimetokea, huyu mwanamke nilichaachana naye miaka mitano iliyopita lakini kila siku alikua ananisumbua, unakumbuka kuwa kuna kipindi nilikua sipokei simu, badi ni huyu, sasa hivi kaja hapa, kalewa, sijui kapigwa huko, ndiyo kaja kwangu, mimi nahisi hata wamembaka, yaani sijui….” Kelvin aliongea maneno mengi sana, alifungua mlango na yule mwanamke ambaye alikua ni mrefu, kapanda juu anakuangalia Kelvin kwa chini.
Umbo lake lilikua namba nane, mweupe nywele ndefu kama za singa singa hivi, alikua na uzuri flani, hakua na manengo mengi, alimuangalia Kelvin kwa dharau flani, kisha akamuangalia na Anna pale chini.
“Kwahiyo kama kalewa kwanini usingemuacha huko nnje, kwanini umfungulie mlango, hivi unafikiri mimi sina ma X, kwamba hatwakai kuruidiana na mimi?” Aliuliza huku akiinama, alimshika anna na kumnyanyua, alikua ananuka pombe aliyokua amemwgiwa na Kelvin.
“Mbona anaonekana kama anajielewa, lakini kalewa hivi, dada ukiachwa kubali….” Alimuambia kwa dharau, alimsukuma chini kisha akaingia zake ndani.
“Utamaliazna na malaya wako mwenyewe, mimi nimechoka, na kama utedelea na huu ujinga wako, kila siku jipya mimi nitakuacha, sipendi mapenzi ya drama kabisa…”
“Dada mimi si malaya, huyu ni mchumba wangu na kujitambuli….” Anna alijaribu kujielezea lakini hakumalizia, Kelvin alimpiga teke la mdomoni, mdomo ukaanza kutoa damu, alimvamia pale cnini na kuanza kumpiga, alimpiga sana huku akimtukana, alimpiga ngumi mateke, aliokota na pochi yake na kuanza kumpiga nayo.
Yule mwanamke mwingine kuona vile alitoka nnje, alimuambia kuwa yeye hawezi kukaa hapo, kama ana matatizo na mtu wake badi wakamalizane kivyao. Wakati anatoka Klvin alimfuata kumbembeleza, alimumba asiondoke lakini hakukubali, alitoka nnje, akaingia kwenye gari yake na kuondoka. Kelvin alimkimbiza lakini hakumpata, alirudi ndani na kumkuta Anna anajitahidi kunyanyuka, alimshika na kumkokota mpaka nnje, alipomfikisha nnje alimsukuma na kumuacha chini, akaingia ndani na kufunga mlango, alichukua simu yake na kuanza klumpigia yule mwanamke aliyeondoka lakini hakupokea, alipiga simu sana lakini haikupokelewa.
Alianza kuzunguka zunguka ndani kwake, simu kashikilia mkononi, alizunguka kama dakika kumi kisha akatoka nnje, Anna alikua kakaa chini, hawezi kunyanyuka, alimsogeza pembeni, akafungua geti, akatoka na gari yake akaondoka na kumuacha pale nnje. Ile nyumba ilikua mbali kidogo na barabara, ni nyumba ambayo ilikua maeneo mapya hivyo hata kupata jirani nayo ilikua ni shida. Anna alikua hawezi hata kutembea na mvua ilianza kunyesha.
ANNA; MKE WANGU NAOMBA UNISAMEHE KWAKUKUOA—SEHEMU YA PILI
Matone ya mvua yalimpa nguvu Anna, aliweza kunyanyuka na kukaa lakini hakuweza kutembea, alikua kaumia sana, alichukua simu yake na kupiga namba moja. Alipiga mara ya kwanza ikaira bila kupokelewa, akapiga tena mara ya pili.
“Kwanini unanipigia usiku wote huu, mimi nimelalaa?” Sauti ya upande wa pili iliuliza.
“Njoo unichukue George, niko katika hali mbaya, nisaidie, niko kwa Kev, njoo, nitakuambia kila kitu nikija.” Aliongea kwa shida lakini kwa sauti ya kuamrisha kisha alikata simu. Hata simu ilipopigwa tena alishindwa kupokea, alikua katika maumivu makali.
Alikaa pale kama nusu saa hivi ndipo George alikuja na gari yake, alikua kaumia hawezi hata kuongea vizuri, George alimuuliza maswali mengi lakini hakumjibu.
“Nisidie tu kutoka hapa….” Alijibu kwa shida, George alimnyanyua na kumlaza siti ya nyuma, alikua kaumia sana hivyo alimpeleka mpaka hospitalini. Lakini walipofika Anna alikataa kushuka.
“Unanipeleka wapi?” Alimuumiza.
“Hospitalini, huoni ulivyoumia?” Alimjibu kwa swali, George alishashuka kwenye gari na kufungua mlango wa nyuma akitaka kumtoa ili kumuingiza hospitalini.
“Una akili kweli wewe?” Anna aliuliza kwa hasira.
“Unajua kabisa kuwa hospitalini hawawezi kunitibu bila PF3, watataka nimtaje mchumba wangu, watataka kujua kilichotokea, au ndiyo mipango yako ili Kev afungwe na wewe uwe na mimi. Nilikuita unipa msaada, unipeleke nyumbani si Hospitalini, muda mrefu unamchukia mume wangu lakini huwezi kututengenisha. Nipeleke kwangu, nitakua sawa, sitaki mambo ya hospitalini! Vitu vingine uwe unaulizaga, sio mambo ya kujiamulia tu!” Pamoja na kuwa kwenye maumivu makali lakini Anna aliongea kwa hasira, ni kama alikua akimtukana George mabaye alikua hajui kosa lake, aliongea mambo mengi mabayo hata hayahusiki.
“Nisamehe, mimi sikuwaza hivyo.” George alijibu kwa upole, alifunga mlango na kurudi kwenye usukkani, alimgeukia na kumuuliza.
“Kwahiyo nikupeleke wapi?” Aliuliza kama mtu aliyekata tamaa, lakini aliejawa na hasira, kwa kumuangalia tu George alikua anaumia sana, ni muda mrefu alikua anampenda Anna ingawa alikua hajawahi kumuambia kwa kuogopa kukataliwa lakini alikua anampenda sana, Anna alionyesha kuwa hampendi, alikua kafa kaoza kwa Kev, pamoja na kufanyiwa vituko vya kila siku lakini hakumuacha, aliendelea na Kelvin huku yeye akiishia kusimuliwa tu matukio. kila wakati akiwa na shida Anna alienda kwa George, alikua ni rafiki yake wa kumuambia kila kitu, kulia, kumuomba msaada, kila akiwa na shida alimfuata yeye na kwa bahati tu George alikuepo kumsaidia.
“Nipeleke nyumbani, nataka nikapumzike kesho kazini.” Alijibu kwa mkato, mbali na kuwa kwenye maumivu lakini Anna alikua na hasira, alimkasirikia George kwa kutaka kumpeleka hospitalini.
“Mahusiano yote yako hivi, kugombana ni kawaida, siwezi kumfunga mchumba wangu wka kitu kidogo kama hiki….” Alijiongelesha wakiwa njiani, George alinyamaza kimya, hakutaka kuingilia, alijisikia vibaya kwa namna ambavyo Anna alimsemesha pale hospitalini. Alienda naye mpaka nyumbani kwake, Anna alikua akiishi nyumba ya kupanga lakini walikua wakikaa wapangaji wawili, vilikua kama vikota flani hivi.
Alimfikisha na kumfungulia mlango ili atoke, George alikya kakasirika kidogo, alimuangalia tu kuona kama atashuka mwenyewe. Anna alijaribu kushuka lakini alishindwa, alimuomba George kumsaidia, kweli alifanya hivyo, alimshusha mpaka chini, akafunga mlango kisha akamsiadia kutembea mpaka mlangoni.
“Funguo?” George alimuuliza.
“Anna aliingiza mkono wake kwenye mfuko wa suruali ya jinisi aliyokua amevaa, alitoa funguo na kumpa, George alifungua mlango na kutaka kuingia naye.
“Hapana, ondoka, nitaweza kuingia mwenyewe.” Anna alimuambia kama anamuamrisha.
“Kwanini, huwezi kuingia, acha nikusaidie.” George alimuambia huiku akitaka kumbeba. Anna alikasirishwa na kile kitendo, alimsukuma George pembeni.
“Hivi una akili kweli, mbon aunakua mjinga mjinga namna hiyo? Wewe ni mwanaume wangu mpaka uingie nyumbani kwangu, una nini kwanini? Hivi kwa mfano Kelvin akija usiku huu na kutaka kuniomba msamaha itakuaje? Ondoka nenda kwako, umenisaidia, ushanifikisha kwangu hayo mengine hayakuhusu. Acha kuingilia mahusiano ya watu, unataka kuingia kwangu ili nini? Hivi ukinibaka hapa nitasemaje, wanaume wengine bwana!” Aliongea kwa hasira, kila mara alipkua akipandwa na hasira alipata nguvu kidogo, alimsukuma George na kuingia ndani, ingawa alitembea kwa shida lakini hakuhitaji tena msaada wa George, aliingia ndani, George alitaka kuingia ili kumsaidia kwani alikua anapepesukapepesuka lakini aliufunga mlango kwa nguvu kidogo umbamize.
Kuona hivyo alitoka na kuingia kwenye gari yake, aliondoa gari yake lakini hakwenda mbali, ni kama alihisi kuwa rafiki yake atashindwa kuvumilia, alipaki kama mita mia hivi pembeni kusubiria kama Anna atamtafuta. Alikaa pale nnje kwa zaidi ya masaa mawili, aliona hatafutwi, alimpigia simu Anana kuyaka kujua hali yake kabla hajaondoka lakini siku ilikua haipokelewi. Alihisi kitu kibaya, kwa hali aliyokua nayo alihisi labda anaweza kufia mule ndani, alishuka kwenye gari na kurudi kwa mguu. Ile nyumba ilikua na geti lakini si la kufunga, lilikua ni la kurudishia tu, alifungua na kwenda mpaka mlangoni, alisimama kuchungulia, alikuta taa zimezimwa.
Alisimama kama dakika 15 akiwaza agonge mlango kuulizia lakini alishindwa, mwisho alirudi kwenye gari, aliondoka na kurudi nyumbani kwake. Alifika nyumbani akiwa na wasiwasi sana, ilikua ni usiku wa maanane, kwenye saa tisa usiku hivi, alikua kachoka sana, kichwa kimejaa mawazo, alimuacha Anna katika hali mbaya na kwa namna flani alihisi labda nahitaji msaada wake. Wakati anapigiwa ismu mwanzoni alishaoga na kupanda kitandani kulala, pamoja na misukosuko ya kumsiadia Anna na kuchafuka lakini hakuoga tena, alikua kachoka, kichwa kina mawazo, alipanda kitandani kulala, lakini hakupata usingizi mpaka asubuhi, kwenye saa 11 hivi ndiyo alipitiwa na usingizi.
Alichelewa kuamka, aliamka kwenye saa mbili hivi za ausbuhil alichelewa kwenda kazini, alipoamka tu kitu cha kwanza ilikua ni kumtafuta Anna. Alimpigia simu sana lakini alikua hapokei, alihisi labda kuna kitu kibaya kimemtokea, alitamani kwenda kwake kumuona lakini alihofia kumuudhi, Anna alishamkatazaga kwenda kwake, mara nyingi hata akimpa lift alikua akimuacha mbali kabisa na nyumbani, alifanya hivyo kwakua Kelvin alikua na wivu sana, hakutaka kumuona akiwa na mwanaume mwingine yoyote, hata suala la kufanya kazi alishamuambia kuwa akimuoa ni lazima aache kazi.
Alifika kazini akitegemea kuwa atamuona Anna, lakini hakumuona, alimuulizia na kuuliza kama kuna mtu aliyempigia simua subuhi lakini hakukua na mtu. Alijua kilichotokea, alimpigia tena simu lakini simu haikupokelewa. Alijihisi vibaya, alihisi labda kuna kitu kilikua kimemtokea, alitamani kwenda lakini aliogopa, George alikiua anaogopa sana kumuudhi Anna, alikua anampenda sana hivyo alijua kuwa, kama akienda kwake bila tarifa basi anaweza kumnunia hata mwezi mzima kitu ambahco hakutaka kuona kinatokea. Alitamani kumuambia hata rafiki yake kwenda kumona lakini alisita.
Anna hakupenda mambo yake kujulikana na marafiki zake, ni mtu wa kujikweza, kupost furaha, kuweka status kuwa anapendwa. Alikua anampenda sana Kelvin na mara nyingi alipenda rafiki zake kujua kuwa anapendwa, mambo mengi aliyokua akijifanyia mwenyewe alikua akisingizia kuwa anafanyiw ana mchumba wake. Kwa rafiki zake mahusiano yake yalionekana kama ni watu wanapenda, hakuna rafiki yake hata mmoja aliyekua anajua kuwa Kelvin anampiga.
Rafiki zaoe wote walikua wanajua kuwa, nyumba aliyokua anaishi alipangishiwa na Kelvin, lakini ukweli nikuwa, kodi alikua analipa mwenywe na nyumba aliyokua anaishi Kelvin ni yeye alihsauri kununua kiwnaja, akamuongezea pesa Kelvin akanunua kiwanja lakini wakati wa kuandikishana yeye aliandikishwa kama shahidi wakati kiwanja kile alichangia pesa kubwa kuliko hata kelvin mwenyewe. Wakati ananunua kiwanja, Kelvin alitoa milioni mbili na Anna alitoa milioni tano, lakini kiwanja kikaandikwa jina la Kelvin.
Alipohoji aliishia vipigo na matusi, Kelvin alimuambia kama huniamini basi chukua makarasi ya viwanja lakini sitaki tujuane, uone kama hiyo nyumba ndiyo itakuoa. Wakati wa ujenzi alichukua mkopo kazini kwake, akachukua milioni 30, akampa Kelvin milioni 27 kumalizia nyumba kwa mashariti kuwa Kelvin aende kwao kujitambulisha na kuvalisha pete. Milioni tatu iliyobaki ndiyo alitumia kuandaa sherehe ya kubalishwa pete, kununua pete na marafiki zake walijua kuwa vitu vyote hivyo kafanyiwa na mchumba wake lakini ukweli nikuwa alijifanyia mwnyewe baada ya kuona kuwa wamekaa kwenye mahusiano kwa muda mrefu na hakuna dalili za ndoa.
Mtu pekee aliyekua anajua ukweli alikua ni George, yeye ndiyo alikua anamuambia kila kitu, alikua niz aidi ya shoga yake, alikua ndiyo bega leke la kulilia na hakuta mtu mwingine kujua kuwa anateseka katika mahusiano. Geogre alifikiri sana na kuona ni bora kwenda mwenywe, ingawa alihisi kuwa atamkasirisha lakini aliona kuwa ni bora kukasirika lakini kuokoa maisha yake, hasira zilimpanda kwani alimpenda sana na hakutaka kumpoteza, alitoka kazini, akawasha gari na kwenda mpaka nyumbani kwa Anna.
Alifika kutaka kugonga mlango, lakini kabla ya kugonga alikuta ufunguo kwa nnje, alikumbuka kuwa jana yake wakati anamfungulia mlango hawakuutoa ufunguo. Alishika mlango ulikua unafunguka, haukufungwa, aliingia huku akigonga, aliita lakini Anna hakuitikia, aliingia mpaka sebuleni,l hakufika mbali alimkuta Anna kalala sebuleni kwenye kochi, alikua katika hali ile miel ambayo alimuacha nayo jana yake. Asliangalia mapigo ya moyo na kukuta bado anapumua, alimshukuru Mungu kwa hilo, alimnyanyua na kumkalisha, lengo lake lilikua ni kumpeleka hospitalini, alishasema liwao naliwe.
“Bora anichukie lakini siwezi kumuacha afie hapa.” Aliwaza huku akimnyanyua, lakini wakati akifanya hivyo Anna alizinduka.
“George, umekuja, nilijua kuwa utakuja…” Aliongea kwa suati ya upole lakini ya kuchoka, hakuwa na hasira zile za jana yake.
“Nimejaribu kumpigia Kelvin lakinini hapokei simu zangu, sijui amepatwa na nini? Labda bado ana hasira na mimi?” Anna aliuliza.
“Atakua kachoka ausbuhi hii, atakutafuta tu.” George alikua anaumia sana, aliumia kuwa azubuhi ile alikua pale lakini mwanamke aliyekua anampenda alikua anazungumzia mwanaume mwingine.
“Hivi ana nini ambacho mimi sina, yaani mbona kimwanaume chenyewe ni kituko kabisa, yaani kanizidi nini?” aliwaza kwa hasira, alikua anaumia, anajitahidi kumliwaza Anna kwa kumuambia maneno mazuri. Alienda na kumchukulia maji, alimpa ili anywe, alienda jikoni, akamkorogea uji na kurudi, alimpooze ana kumnywesha. Tangu jana yake alikua hajala chochote, alikua kachoka hivyo alikua hana namna, hata hakuuliza kwanini George alikuja nyumbani kwake.
Baada ya kunyw auji alipata nguvu kidogo, lakini bado alikua na maumivu, hakuweza kunyanyuka wala kutembea, George alimbeba mpaka chumbani, mwili ulikua umevimbavimba, alimvua nguo na kubaki na nguo ya ndani tu, alikua kavimba sana, viungo vinauma, kila sehemu ya mwili wake ilikua inamuuma. Geogre alienda kuchemsha maji, alirudi na kuanza kumkanda mwili mzima, ingawa alikua anampenda lakini hakumkadna kwa matamanio, wakati anamkanda Anna alikua akipige kelele za maumivu, Geogre alijisikia vibaya, alikua anamunea huruma mpaka machozi ya kaanza kumtoka.
“Kwanini nisikupeleke Hospitalini, hivi unaona jinsi alivyokuumiza, aisee haya si mapenzi, nenda hospitalini ndugu yangu.” George uzalendo ulishinda na kuamua kumuuliza, Anna alikua katika maumivu makali, mwili ulivimbavimba, alikua na michubuko meingi sehemu za mapaja, hata hakujali Geogre alivyokua anamkanda, yeye alimchukulia George kama rafiki, kama shoga yake, kama mwanamke mwenzake, hakumchukulia kama mwanaume, ingawa alishaona dalili zote za kupenda, baadhi ya mjarafiki zake walishamuambia kuwa George anampenda lakini yeye hakujali, hakumuona hivyo, alimuona kama rafikitu.
“Hapana, najua ni shetani alimpitia, unajua kuwa Kelvin si mtu wa hasira kihivyo, jana ni mimi nilimuudhi, mimi ndiyo nilikataa kuondoka kwake, aliniambia niondoke lakini nil….” Alijaribu kumtetea lakini George uzaliendo ulimshinda, alishindwa kuvumilia, hasira zilimpanda mpaka akajikuta anaropoke.
“Wewe ni mpumbavu, hivi ni lini utajua kuwa huyo mwanaume hakupendi, hivi ni lini utaacha kujilazimishia hivyo kwa mtu ambaye hana mopanngo na wewe. Huyo mtu hakupendi, hakutaki ndiyo maana anakufanyia vituko namna hii, kila siku anakupiga hata hushtuki, ana wanawake kibao! Wewe kazi ni kumpa tu pes,a mwanamke gani huoni aibu unajinunulia pete mwenyewe, yaani unajilipia mahari mwenyewe halafu unajifanya unapendwa! Amka hupendwi, wewe ndio unajilazimishia….”
Aliongea kwa hasira lakini Anna hkumruhusu amalizie, alishapata nguvu kidogo, alinyanyuka, akachukua shuka na jikifunika.
“Naonaunavuka mipaka, yaani mimi kukukaribisha tu kwangu ndiyo unataka kunipenda na kichwani, unanipangia na maisha, wewe ni rafiki yangu lakini mambo yangu hayakuhusu! Ondoka kwangu, kwanza umekuja wkangu kufanya nini, unakuja unanishika shika mapaja hivi wewe ni mwanaume kweli au ni shoga tu! Ondoka kwangu, unajileta leta kwangu kila siku kujipendekeza kwangu ili iweje, hivi ulivyokuja hapa, unainga mpaka chumbani kwangu unafikiru Mume wangu akija kukuona ataelewaje, Baba ondoka, toka,s itaki msaada wako, naona mazoea yamezidi, mimi kukuelezea maisha yangu isiwe taabu, ondoka!”
Aliongea kwa hasira, alijifuunika kwa kuijificha kana kwamba ndiyo kwanza George alikua anaingia chumbani kwake na kumkuta uchi, kumbe yeye ndiyo alimvua nguo na muda wote alikua anamkanda.
“Nisamehe, sikumaanisha hivyo, sikutaka kukukose aheshima, ila nimeumia tu kwanini unemtetea mtu ambaye kakupiga namna hii….”
“Baba ondoka! Unang’ang’ania nini hapa?” Alimuambia kwa hasira! Alimsukuka kabisa kuondoka, George hakua na namna, alitoka na kumuacha Anna amabye alishapata nguvu kidogo. Alirudi mpaka kwenye gari lake, alikumbuka kuwa kuna fumu za ruhusa alikua kamletea, alirudi na kumgongea mlango.
“Unataka nini tena?” Anna alimuuliza kwa dharau.
“Nimekuletea fomu za ruhusa, nilijua kwa hali yako huwezi kuja kazini, wewe zijaze, saini hapo mimi nitekupelekea ili angalau upumzike siku mbili.” Kwa hasira Anna alichukua ile karatasi, alisaini na kumtupia George kisha akafunga mlango w3ake kwa nguvu. Geogre aliiokota, akaondoka zake na kurudi kwenye gari.
****
“Nimeahirisha kukuoa mpaka utakapokua na adabu, huwezi kunijia kwangu nakuambia uondoke hutaki.” Ni meseji ambayo Anna alitumiwa siku tatu baada ya lile tukio, hali yake ilishakua nzuri, alikua anaweza kurudi kazini lakini alikua na ruhusa ya siku nne. Meseji ile ilimchanganya kwani Kelvin alikua hapokei simu zake, alipiga sana simu zake lakini hakupetikana. Ingawa alikua amekatazwa kuwatafuta ndugu zake lakini kutokana na namna alivyokua kaumizwa basi aliamua kumpigia simu Mama yake na Kelvin.
Hawakua wakifahamiana, alikua hajatambulishwa kwao lakini alikua bado hajapelekwa ukweni. Yaani Keln alienda kutoa mahari kwa kina Anna kabla hajamtambulisha hata kwa ndugu zake, ni ndugu yake mmoja tu aliyekua akifahamu kuhusiana na mahusiano yao, hata siku ya kupeleka mahari hakutuima ndugu zake, alitafuta rafiki zake watu wazima ndiyo wakapeleka mahari amabye Anana aliitoa. Hata siku moja alikua hajawahi kumtambulisha kwa Mama yake hata kwa kuongea kwenye simu tu. Kila wakati alipokua akimuambia kuhusu kumtambulisha au kuongea na Mama yake alimuambia kuwa avute subira mpaka ampeleke.
“Sio heshima kuongea na Mama yangu kabla sijakuoa, utaongea naye ukishakua mke wangu.” Kelvin alimuambia, waliweza kuongea na Mama yake hata msaa mawili lakini hjakumpa simua ongee naye wala kumdokeza kuwa ana mwanamke ambaye anampango wa kumuoa. Anna aliiba namba ya simu ya Mama mkwe wake kwa Kelvin, alikua nayo muda mrefu lakini alikua hajwahi kumpigia, ni mara kibao alitamani kumpigia lakini alikua anasira, alikua anaogopa kumuuddhi ila aliendelea kubaki nayo.
Siku hiyo aliumia sana na aliona kuwa ni wakati sahihi wa kupiga simu. Alijikaza na kuamua kumpigia simu Mama mkwe wake ili kujitambulisha.
“Shikamoo Mama.” Alisalimia baada ya simu kupokelewa.
“Maahaba mwanangu, sijui za huko.” Mama yake alimjibu vizuri, kistaarabu kama vile mtu anayemjua, hiyo ilimpa matuimaini, kwa alivyokua anamuongelesha alitaka kujiaminisha kuwa labda atakua alimtambulisha, labda ashamuambia Mama yake kuhusu yeye.
“Mimi naitwa Anna, ni rafiki yake na Kelvin, sijui kama Kelvin mwanao alishawahi kukuambia kuhusu mimi?” Aliongea kwa wasiwasi, alijisikia vibaya yeye kujitambulisha kwa Mama mkwe wake badala ya kutambulishwa lakini hakua na namna. Kelvin alimuambia kuwa anamucha, alikua hapokei simu zake na alikua anaogopa kabisa kwenda kwake akihofia kipigo, katika kuchanganyikiwa kwake aliamini kuwa Mama yake anaweza kumuelewa kwani ni mwanamke mwenzake.
“Anna gani huyo, nielezee mwanangu, si unajua kuwa Kelvin naye ni msiri sana, uansema ni rafiki yake?” Mama Kelvin alimuuliza kwa upole, sauti yake ilimuambia Anna kuwa huyu ni mtu mzuri, unaweza kumuambia chochote, Anana alijikuta anamuamini na kufuinguka zaidi.
“Najua Mama, ni msiri sana, najua nimefanya vibaya kukupigia na yeye atakasirika akijua kuwa nimekupigia simu. Lakini mimi na mwanao tuko kwenye mahusiano muda mrefu, zaidi ya miaka mitano, ni mchumba wangu….” Hapo Mama alishtuka kidogo na kumkatisha.
“Mchumba wako, mchumba wako kivipi?” Aliuliza kwa asauti ya juu, ni kama alipata habari za mshituko.
“Ndiyo Mama, mimi na mwanao ni wachumba, ameshakuja kwetu kujitambulisha na kutoa mahari amenivalisha…”
“Unasema unaitwa Anna au nimekosea?”
“Ndiyo Mama, naitwa Anna.”
“Ngoja nikuulize, unamzungumzia Kelvin gani ambaye ni mwanangu?”
“Kelvin Samweli Marioga, ni mchumba wangu Mama na namba yako nimecukulia kwenye simu yake. Samahani kwa kukupigia kabla ya kutambulishwa lakini ukweli nikuwa nampenda mwanao na juzi tuligombana ameniambia anasirisha suala la ndoa lakini mimi bado nampenda, ameshakuja kwetu. Kuna mwanamke mwingine yuko naye, najua anamdanganya kwakua mimi kanitolea na mahari….”
Anna alijielezea, Mama Kelvin alimsikiliza kwa makini lakini alionekana kuwa hajamuelewa.
“Una uhakika hujakosea namba mwanangu?”
“Hapana, sijakose anamba, mimi nakufahamu Mama, wewe si unaishi Morogoro, Kihonda, nilsihakuja mpaka hapo jirani na nyumbani lakini Kelvin akaniambia siwezi kuja kuwaona mpaka anilete rasmi, sijakosea Mama.”
“Na umesema unaitwa Anna, mwanangu katoa mahari kwenu?” Mama Kelvin aliuliza kama mtu aliyekua anataka uhakika, aliyetaka kuthibitisha kuwa kile alichokua akikisikia ndiyo hicho alichopaswa kusikia.
“Ndiyo Mama, mimi ni mchumba wa Kelvin.”
“Nielewe mwanangu ninapouliza mara mbili mbili, mimi nahisi umekosea ingawa ni kweli nina mtoto anaitwa Kelvin na nipo Morogoro, kila kitu ni sawa lakini kwa ninavyojua kuwa mwanangu ana mchumba wake lakini haitwi Anna. Sio wewe kwakua mchumba wa mwanangu namjua, ashamleta hapa na wiki ijayo mwanangu anaoa, hhapa unaponipigia nimetoka kuongea na mkwe wangu kuhusiana namambo ya harusi…”
“Hapana Mama mimi ndiyo mchumba wangu, hawezi kuoa mtu mwingine!” Anna alijibu kwa hasira, alikua anatetemeka kabisa, ingawa alikua anajua kuwa mchumba wake ni malaya lakini hakudhani kuwa anaweza kuoa mwanamke mwingine zaidi yake.
“Basi utakua umekosea namba mwanaangu lakini Kelvin wangu anaoa wiki ijayo, pole labda umekosea namba.” Mama alijibu na kukata simu.
ANNA; MKE WANGU NAOMBA UNISAMEHE KWAKUKUOA—SEHEMU YA TATU
Anna alijaribu kupiga tena ile simu lakini aliambiwa ilikua inatumika, alipiga sana. Akili ilikua haifanyi kazi vizuri, alimpigia mchumba wake lakini naye simu yake ilikua inatumika, alihisi kuchanganyikiwa, aliangalie ile namba mara mbilimbili kuona kama kaikosea labda Mama Kelvin aliyempigia alikua ni Mama mwingine, hakuishia hapo, aliingia M-Pesa na kuangali, ilikua ni namba ya Mama mkwe wake.
Kabla hajajua ni kitu gani cha kufanya siku yake iliita, alikua ni ke,vin, alipokea kwa pupa.
“Nilipata wasiwasi, kuna mtu nimempigia ananiambia kuwa unaoa, ni kweli mpenzi? Tafadhali niambia kuwa niuongo, nimechanganya majina…..” Aliongea bila kuweka kituo, kabla ya kumaliza Kelvin alimkatisha.
“Wewe malaya nishakuambia sikutaki, unataka kumuua Mama yangu, kwanini ulimpigia Mama yangu! nani kakupa namba ya Mama yangu, unampigia Mama yangu simu unamuambia ujinga ujinga wako, unataka kumuua!” Kelvin hakumpa nafasi ya kuendelea kuongea.
Alianza kwa kumtukana, muda mchache tu baada ya Anna kukata simu Mama yake alimpigia Kelvin na kumuuliza kuhusu kuwa na mwanamke mwingine. Kelvin kwa Mama yake na ndugu zake wangune alikua ni kama malaika flani. Hakutaka familia yake imuone kama tapeli, alimtukana sana na kumuambia kuwa kamharibia maisha yake hivyo hamtaki tena na wameachana. Kelvin alikata simu na kumuacha Anna akilia peke yake.
Anna alikua katika wakati mgumu sana, aliumia sana kusikia kuwa mchumba wake alikua anaoa, alitamani sana kwenda kwa Kelvin ili kujua ni kitu gani kimetokea lakini alikua anaogopa, alijua kuwa akienda bila taarifa ataishia kupigwa. Alikua ndani peke yake, mawazo yalikua mengi, kuna wakati alitamani kwenda mpaka nyumbani kwa kina Kelvin Morogoro lakini aliogopa. Kichwa kilikua kinamuuma, alishalia sana mpaka machozi ya kamkauka.
Mtu pekee ambaye angeweza kumfariji kwa wakati huo alikua ni Geogre, alitamani sana kumpigia simu lakini kwa namna walivyomjibu kwa dharau wakati alikua anamsaidia alihisi kuwa hatapokea simu zake. Alibaki mwenyewe na mawazo yake tu, kwenye saa 11 hivi jioni simu yake iliita, alikua ni Geogre, aliipoke aharakaharaka kwani alihitaji mtu wa kuongea naye.
“Naomba unisamehe, nilikujibu vibaya, nisamehe, wewe ni rafiki yangu, naomba nisamahe…” Alianza kwa kuomba msamaha hata kabla ya kuambiwa sababu za kupigiwa. George kama kawaida yake alikua mpole, alimsikiliza mpaka mwisho kwani alikua akiongea huku akilia.
“Mambo ya kawaid atu, najua uliumizwa na mimi niliingilia uhuru wako, sikupaswa kuja kwako kama kwangu.” Alimjibu kisarabu lakini Anna hakukubali.
“Hapana, sikua sawa, najua nilikuumiza, nilipaswa kuwa mstaarabu….”
“Nimekuelewa, yaishe, nimekupigia kwakua nilitaka kujua kuwa unaendelea?” Aliamua kumkatisha na kumuuliza.
“Siko sawa kabisa, siko sawa kabisa, nina shida, nahitaji kuoanna ana wewe, nahitaji mtu wa kuongea naye, unaweza kuja kwangu, siwezi kulala peke yangu, nitachanganyikiwa….” Alimuomba sana George kwenda nyumbani kwake, alihitaji mtu wa kuongea naye.
Kwa namna alivyokua akilia na kulalamika George, alicha kila kitu alichokua akikifanya na kwenda kumuona. Alifika na kumkuta kajifunga khanga moja tu. Anna alipomuona alimfuatra na kumkumbatia, alimkumbatia kwa muda mrefu huku akilia.
“Kaniacha! Kaniacha! Kelvina naoa mwanamke mwingine, yaani kaniahca, nimemvumilia mengi sana.” Alianza kumuelezea huku bado kamkumbatia, aliku analia sana, George bila kutaka nayeye alimkumbatia, miiili yao iligusana.
Kwa George ilikua mtihani kidogo, mwili ulianza kumsisimika kiasi alikua hata hatamani kuachiwa. Lakini kwakua alikua akimheshimu Anna alimuondoa kifuani kwake ili asimkoesee heshima, alikua anampenda sana lakini hakutaka kumpata kwa namna ile. Alimuondoa na kumkalisha chini kisha akamuambia amueleezee tatizo lake, huku akilia Anna alimuambia kila kitu kilichotokea.
“Najua unampenda lakini unatakiwa na wewe kujipenda kidogo, huyo mtu anakuharibia maisha yako.” Alianza kwa kumuambia.
“Umeona, anataka kuoa mwanamke mwingine huko kwao, kila siku anakupiga, unampa pesa kila siku, yaani ukisema huna pesa anakupiga na kama mbwa, huyo si mwanaume ni shetani. Hivi kwanini unamng’ang’ania mtu ambaye hakupendi wakati kuna watu tupo tayari kufa kwaajili yako. Mimi nakupenda sana Anna, nakupenda kuliko maelezo, yaani hata ukitaka nikuoe kesho nakuoa, lakini naona kama unahangaika na huyo mtu, mshenzi kabisa….”
Kwa mara ya kwanza George alimuambia ukweli Anna, aliongea huku anatetemeka, ni kitu ambacho kilikua kinamuumiza kichwa muda mrefu. Topfauti na alivyotegemea kuwa labda atakasika Anna ni kama alifurahi, alimvammia na kumkumbatia,akwa kama anataka kufanya naye mapenzi.
“Hata mimi nakupenda, nakupenda sana lakini nilikua naona huniambii hivyo nikaona labda hunipendi.” Aliongea huku akilazimisha kufanya mapenzi, alifungua khanga mopja aliyokua kajifunga na kubaki kama alivyozaliwa.
George alichanganyikiwa na mwili wake lakini yeye hakutaka kufanya mapenzi, alitaka mahusiano. Kwa hali aliyokua nayo ya kuachwa alijua fika kuwa akili yake haifanyi vizuri kwa wkaati huo. alimzuia, akachukua kanga na kumfunika.
“Sio kama nataka kufanya mapenzi na wewe, nataka tuw ewa penzi, nataoa tuongee, nikuelezee hisia zangu, nataka….” Alijaribu kumuelewesha lakini mwenzake mzuka ulishapanda, hakuwa anataka kuongea, alichotaka yeye ilikua ni kufanya tendo la ndoa, alikua na hasira na kwake alikua ni kama analipa kisasi kwa Kelvin.
“Inamaana hutaki kufanya mapenzi na mimi? Inamaana na wew eunaniona mbaya, yaani umekuja kwangu, unaniambia kuwa unanipenda halafu nikitaka kufanya mapenzi na wewe hutaki?” Aliongea kwa hasira yhuku akinyanyuka, alienda mpaka mlangoni, hakujifunika khanga alikua kaishikilia, alifungua mlango na kumuambia kuwa kama hamtaki aondoke.
Anna alionekana kukasirika, aliotaka kumfukuza kweli lakini George aliomba msamaha, walijikuta wanakumbatiana na kufanya mapenzi usiku ule. Ingawa hakutaka itokee vile lakini alifiurahi, alijua kuwa kampata mwanamke wa maisha yake na aliamini kwua kwa yeye kuwa na Anna basi atakua kampunguzia maumivu mengi. Waliongea mengi usiku ulel walikumbatiana huku kila mmoja akimuambia mwenzake namna ambavyo alikua anampenda tangu zamani.
“Nimepoteza muda wangu mwingi sana na yule mshenzi, sijui ni kwanini hukuniambia tangu zamani kuwa unanipenda.” Anna alimuambia, George alifurahi kuwa nayeye anapenda, asubuhi wlaiamkia kwa Anna ili kwenda kazini, George hakua na nguo za kubadilisha hivyo baada ya kutoka pale alipitia kwake, akabaidlisha nguo kisha wakaenda wote kazini.
Kila mmoja aliingia ofisini kwake, wakati Anna alikua na mawazo mengi, kila wakati alikua akiangalia simu yake akisubiri kama Kelvin atapiga, ingawa alifurahia tendo la ndoa na George lakini maw3azo yake bado yalikua kwa mchumba wake, alikua anampenda na bado alikua haamini kama kamuacha. Kwa upande wa George kika wakati alikua anatabasamu, alikua ni mtu mwenye furaha, kila mtu ofisini alijua, alitamani kumuambia kila mtu lakini alishindwa.
Hakufurahia kufanya tendo la ndoa, hapana kwake hicho kilikua ni kitu cha kawaida sana, alifurahia kuwa, mwanamke aliyekua anampenda, mwanamke aliyemuumiza kichwa kwa muda mrefu alikua wakwake. Ilikua siku nzuri san akwake, mara kadhaa pamoja na kuwa ofisi moja lakini alimtyumia mjeseji kumshukurui, kumpa moyo na kumuambia kuwa anampenda.
Mchana kwenye saa saba hivi alimtumia Meseji kuwa anataka waende kula pamoja. Kwa kawaida pale ofisini kwao kuna letwa chakula, kuna Mama ambaye amepewa tenda ya kusambaza chakula ofisini kwao, kwa maana hiyo ule muda wa kula maa nyingi kila mtu anakua ofisini kwake. Lakini siku hiyo Geogre alitaka kumtoa mpenzi wake mpya.
“Nataka nikutoe out, ni Date yetu ya kwanza kama wapenzi, naomba ujiandae nakuja.” Alituma meseji akisubiria majibu, wakati meseji nyingine za mwanzo alizokua akimtumia zilikua zikijibiwa hii haikujibiwa, alijaribu kupiga simu lakini haikupokelewa na baada ya muda ilikua haipatikani.
George alitoka ofisini kwake na kwenda ofisi ya Anna, haikua mbali sana.
“Eti, Anna yuko wapi, nimemtumia meseji hajanijibu, lakini naona kama kazima simu kwani nilikua nampigia hapokei ila saasa hivi kila nikipiga naona simu haipatikani, kaondoka kaenda wapi?” Alimuuliza Sam, ambaye walikua wakikaa ofisi moja na Anna.
“Hata mimi sijui, alikua anaongea na simu, ilipokata nalikua kama analia hivi, ila alitoka hataka haraka, sijui kaenda wapi ila siku ya leo naona kama hakua swa, muda mwingi alikua analia, yaani sijui….” Sam alijaribu kumuelezea, George hata hakusubiri amalize kuongea, alihisi kitu, alitoka ofisini harakaharaka na kuingia kwenye gari.
Aliposikia tu kuwa Anna kaongea na simu alijua ni nani alikua kampigia, hasira zilimpanda, alijua kuwa lazima kuna kitu kaambiwa kikamuumiza.
“Ladbda kamtukana tena, kaona aende nyumbani, kwanini hakuniambia….” Allikua akiongea mwenyewe kwenye gari, alijisikia vibaya kwani ndiyo kwanza alikua amempata mwanamke wa maisha yake halafu anaona kuna mtu anataka kuingilia. Alijua kuwa labda Anna kapigiw aismu, katukan3wa kashindwa kukaa ofisini ndiyo maana akaondoka na kwnda nyumbani, aliondoka mpaka nyumbani kwa Anna ili kumuangalia.
****
Anna alikua anaumia sana, alijilazimisha sana kufurahia kuwa na geogre lakinia lishindwa, akili yake yote ilikua kwa Kelvin hasa kiwaza ni kwanini alikua akimuacha, akili yake ilikua haifanyi kazi kabisa. Alijua kuwa mchumba wake ni malaya lakini hakujua kuwa anaweza kumfanyia hivyo, kila siku aliamini kuwa, Kelvin atazunguka huko lakini mwisho wa siku atakuja kumuoa yeye kwani walishafanya mambo mengi ya maendeleo kama mke na mume.
Aliumia sana kusikia kuwa kuna mwanamke miwngine kamtambulisha.
“Nimemkose anini? Kwanini anifanyie hivyo?” Alikua akiwaza anajiinamia kwenye kiti chake na kuanza kulia.
“Mbona unalia, nini tatizo?” Dama mbaye walikua wanashea ofisi alimuuliza.
“Siko sawa, niache.” Alimjibu kwa mkato, hakutaka kuwaambia watu mambo yake, siku zote alitaka kuonekana kama vile ana furaha. Alitulia kidogo lakini baada ya mdua aliwaza tena na kuanza kulia tena.
“Kama bado unaumwa si urudi nyumbani, mbona kama hakuna kazi nyingi hapa?” Sam alishindwa kuvumilia na mumuuliza tena. Ingawa hawakua marafiki zana lakini walikua ni wtau wanaongea, hawakuwahi kukoseana heshima, ila siku hiyo Anna alikua na hasira, ni kama alikua anatafuta mtu wa kugombana naye mtu wa kumrudhia hasira zake.
“Hivi kwa nini wanaume wote siku hizi mmekua kama amshoga hivi? Hivi huwezi kukaa na kufanya mambo yako, yaani ni lazima kunifuatilia, nmimi nakuulizaga, nikilia machozi si yangu?” Aliongea kwa hasira, Sam hakuelewa ni kosa gani alikua kafanya mpaka kufikia kutukanwa namna ila lakini hakua na namna, alilazimika kunyamaza na kumuacha aendelee na mambo yake.
Wakati huo huo simu yake iliita, Anna aliiangalia, Likua ni Kelvin, alishikwa na mshtuko kidogo kwani kwa jinsi alivyomtukana jana yake hakutegemea kama atakuja kumpigia simu tena. Aliganda kwa muda simu ikaita mpaka ikakatika, alishidna kuipokea, iliita kama mara tayu hivi ndiyo akaamua kupokea. Alikua kama mtu ambaye kaganda, hajielewi hata chakufanya, alipoke aismu na kuiweka sikioni bila kusem achochote.
“Halooo… haloo…oo… unanisikia?” Kelvin alianza kuongea lakini ahkuitikia.
“Najua unanisikia, najua nimekukosea, nimekufanyia mengi lakini hukustahili. Wewe ni mwanamke wa maisha yangu, najua kuna wakati nakua kama chizi, kuna wakati nakufanyia vituko lakini baad aya jana nilishndwa hata kulala, nakupenda na sidhani kama naweza kuishi bila wewe. Nahitaji kuongea na wewe nahitaji kukuona.” Kelvin aliongea, sauti yake ilikua ni ya kumbembeleza ikoonyesha majuto, alionekana kama mtu anayelia.
Kwa Anna hiki kilikua ni kitu kipya kabisa, tangu kuanza mahusiano Kelvin alikua hajawhai kuomba msamaha kwa kitu chochote kile, kila mara akimkosea aliishia kumtukana, aliishia kununa mpaka kumlazimisha Anna kuomba msamaha. Kilikua ni kitu kipya ambcho kilimchanganya saana Anna. Ingawa alikua na hasira lakini ile kusikia kuombwa msamaha, jinsi Kelvin alivyokua anaongea ilimpa karaha flani mpaka akatamania endelee. Kweli kelvin aliendelea kuomba msamaha, kulalamika na kuomba nafasi nyingine.
“Uko wapi?” Anna alimuuliza.
“Niko nyumbani, nimeshindwa hata kwenda kazini kwaajili yako, yaani hata sijui nafanya nini? Najua nakukosea sana lakini wewe ni mvumilivu, wewe ni Mke.” Alimuambia, Anna hakuaka kusubiri, machozi yalimtoka lakini yalikua machozi ya furaha, alitoka mbio na kwenda kuchukua Bajaji kwenda kwa Kelvin,a litaka kumuona, alitaka kuombwa msamah auso kwa uso. Njiani meseji za Gorge ziliingia lakini hata hakuzisoma, aliziangalia tu na kurudisha simu yake kwenye Pochi, George alianza kupiga simu, aliona ni usumbufu akaizima kabisa.
Alifika kwa Kelvina na kukuta anamsubiri, walikumbatiana kwa mahaba, Kelvina alikua analia kabisa, alipiga magoti na kumuomba msamaha, alimuomba msamaha na kumtaka kumsamehe kwani alikua kamkosea sana.
“Huna haja ya kupiga magoti mume wangu, wewe ni biandamu, kama umeomba samaha naamini kuwa umejutia na utabadilika. Nimekusamehe nakupenda, wewe ni mume wangu, nakupenda. Walikumbatiana na kunyanyuana mpaka ndani, Pochi ya Anna ilidondoka lakini hata hakuiona, akili yake yote ilikua kwa Kelvin, walibebana mpaka kitandasni na kuanza kufanya mapenzi.
Kwa upande wa George alienda mapak nyumbani kwa Anna, hakumkuta ndipo akili ikakaa swa.
“Atakua kapigiw aismu na yule mshenzi, atakua kaenda kumuona.” Aliwaza hukua kigeua gari kwenda kwa Kelvin, hakujua ni kwanini anaenda lakini alienda. Alifika mpaka kwa Kelvina, akapaki gari mbali nkidogo ksihaakatembea kwa miguu, alifika mpaka getini kutaka kugonga. Alipofika moja kwa moja aliiona Pochi ya Anna ambayo asubuhi yake alikua kaibaba, ilikua imedondoka chini, mbele kidogo kulikua na viatu vyake. Kwa namna alivyokua anayafahamu mahusiano yao alihisi kuwa labda Kelvin alimpigia ismu kumtukana.
Anna kaakasirika na kwenda kuongea naye na alivyofika ndiyo kelvina kaanza kumpiga na kutupia vitu chini. Aliingia kwa hasira.
“Anna sasa hivi ni mpenzi wangu, hawezi kumpiga wakati nipo, ngoja nikamfundishe adabu.” Aliondoka maoja kwa moja na kuingia mpaka ndani, alifika na kukuta mlango uko wazi. Kabla ya kuingia akidhani labda Anna anapigwa alisikia sauti za watu wanagina, alisikia sauti za mapenzi, alimsikia Anna akilalamika akitoa sauri za mahaba. Alisogea karibu, akatafuta upenyo upande wa dirishani ndipo alimuona mwanamke amabye alishaamini kuwa ni mpenzi wake akifanya mapenzi na mwanaume mwingine.
Maumivu aliyoyapata kidogo adondoke, alikua anajua ni wapenzi,a likua anaelezea kila siku kuhusu mapenzi yao lakini hakuwahi kuumia hivyo. Nguvu zilimuishia kidogo adondoke, alitamani kuamini kuwa labda kalazimishwa lakini kwa namna walivyokua wakifanya, wanabadilisha saili alijua kuwa wamerudiana. Hakua na namna, alijihisi kuwa ni mtu mwenye mkosi wa jabu, aligeuza na kurudi kwenye gari, alikaa kwenye gari kwa zaidi ya nusu saa, nguvu zimemusihia, picha ya Anna akiwa amekunywa anafanya mapenzi na mwanaume mwingine iligoma kabisa kutoka kichwani kwake, alilia sana kwenye gari mwisho akaamua kuondoka.
Kule ndani Anna alikua anajisikia vizuri, baad aya kumaliza kufanya tendo la ndoa walilala kidogo, baadaye waliamka na kwenda kuoga pamoja kama wapenzi. Walipotoak bafuni ndiyo Kelvin Aliamza.
“Halafu unajau Mama kakasirika sana, yaani kakasirika sana jinsi jana ulivyoongea naye?” Alimuambia, Anna alishasahau kuhusu jana yake, alishasahau kuhusiana na mwanamke ambaye aliambiwa kuwa Kelvin anakaribia kuoa.
Alijaribu kumuuliza kama ni kweli lakini alikataa, alimuambia kuwa kuna mwanamjke ambaye ndugu zake wanataka amuoe lakini yeye hamtaki hivyo Mama yake alikasirika wewe kujitambulisha kama mchumba wangu.
“Mimi Mama yangu najua namna ya kuongea naye, hivi unafikiri ni wkanini sijakupeleka kwetu mpaka sasa, kuna mtu wanataka nimuoe lakini mimi si mtaki. Ila jana ulipoongea na mama umeyatibua, wanasema kuwa watamchukua huyo Binti na kumleta hapa, mimi sitaki, wewe ni mke wangu, hii nyumba tumejenga wote, siwezi kuruhusu mwanamke mwingine kuja hapa.” Kelvin aliongea ka uchungu snaa, machozi yalikua yanamlenga lenga.
”Sasa tufanyueje? Mimi sikujua, wewe hujawahi kuniambia chochote kuhusu familia yako, kila siku nikikuuliza unanizungusha. Mimi nilipaniki uliposema unaniacha, nisamehe mpenzi.” Annaa alijikuta anaishia kuomba msamaha yeye.
“Hakuna shida, ninachotaka ni wewe umpigie simu Mama yangu, umuambie kuwa wewe ni rafiki yangu tu. Tuliwahi kuwa kwenye mahusiano huko nyuma lakini mimi si mpenzi wako na sijawahi kujitambulisha kwenu.”
“Kwahiyo nidanganye?”
“Ndiyo, nataka udanganye ili Mama yangu atulie kwani ana presha, wewe muambie kuwa ni mwanamke tu unaning’ang’ania lakini….”
“Hapana mimi siwezi kufanya hivyo, wewe ni mchumba wangu unatakiwa kunitambulisha….”
Anna alijaribu kukataa lakini kabla ya kumaliza kuongea, alishtukia kapigwa kofi, Kelvin alianza kumpiga hukua kimtukana.
“Siwezi kuoa kinyago kama wewe, mimi nina mchumba wangu, nina mtu amabye nampenda, umeniharibia kwa Mama yangu, hivi unafikiri familia yangu itanielewaje…” Alianza kumpiga lakini wakati huo huo mwanamke mwingine aliingia, ni yuleyule dada ambaye alikuja kipindi kile. Aliingia hukua kilia, mkononi kashikilia simu yake, alikuja bila hata kuangalia kama Anna yuko pale, akamvaa Kelvin.
“Ni nini haiki nasikia kuwa unataka kuoa, hizi picha nimetumiwa umevalisha mtu pete na hizi ni kadi za mialiko zina majina yako na picha yako!” Aliongea kwa hasira huku akimuonyesha pcha kwenye simu yake.
ANNA; MKE WANGU NAOMBA UNISAMEHE KWAKUKUOA—SEHEMU YA SEHEMU YA NNE
Anana alishikwa na butwaa, mwanzo wakati anasikia kuhusu ndoa alijua kuwa ni yule mwanamke ndiyo anaolewa, lakini alishangaa kuona kuwa ni mwanamke mwingine anaolewa. Kelvin alibaki kimya, hakua na maelezo.
“Umenidanganya, yaani nimetoa pesa yangu nyingi, tumejenga nyumba, kwa taarifa yako hii nyumba huipati, yaani nahakikisha kuwa naiuza!” Yule dada mwingine alilalamika, kumbe nayeye alichangia katika ujenzi wa ile nyumba.
“Uuze ntumba kwani yako, nyumba nimejenga na mchumba wangu, huwezi kuiuza.” Ana alimkatisha.
“Nani umejenga naye, Mama, kila kitu kipo kwenye majina yangu, mimi mchaga, sijui wewe falafala wa wapi, hii nyumba document zina majina yangu, mimi ndiyo napendwa!” Yule Dada aliongea huku akimkunja Anna kwa hasira, Anna hakukubali, naye alimshika na wote wakaanza kupigana, kuona vile Kelvin alitoka nnje na kufunga mpango, akwafungia mlango, akaingia kwenye gari lake na kuondoka akiwaacha pale.
Wakati anaondoka aliondoka na simu ya Anna, alienda mpaka ofisini kwao, alichukua ile simu, akamtafuta dada mmoja na kumuomba aongee na Mama yake.
“Kuna malaya nilikua anye, kampigia mama kuwa ni mchumba wangu sasa Mama kapaniki, yaani kakasirika sana, nataka uchukue hii simu, mpigie simu Mama yangu na muambie kuwa wewe si mchumba wangu, uliongea hivyo kwa hasira kwakua unanipenda na tuliwahi kuwa kwenye mahusiano miaka ya nyuma ila ukanisaliti hivyo mimi nikakuacha, baad aya mimi kukuacha ukawa unaniomba msamaha sana sikukubali, ndiyo uliposikia kuwa naoa basi ukaamua kuniharibia kwa hasira.” Kelvina alimpa mapelezo yule dada.
Pamoja na umalaya wake lakini kelvina likua anamuogopa sana Mama yake, alikua anamheshimu na alipnekana kama malaika. Baad aya Mama yake kusikia suala la kutoa mahari ilimuumiza sana mpaka kufikia hatua ya kutaka kuahirisha ndoa, lakini Kelvin hakua tayari kwa hilo. Mwanamke aliyekua akimuoa alikua ni rafiki wa Mama yake, mabli na urafiki tu lakini yeye alimpendea kutokana na pesa za familia yake.
Mchumba wake alikua ni mtoto wa pekee kwa Mama yake, Baba yake alishafariki dunia muda mrefu na kuwaachia mali nyingi. Mama yake aliziendeleza na kutengeneza utajiri mkubwa hivyo alijua kuwa akimuoa huyo binti basi mamboyake yataenda sawa. Hata hakua akimpenda, walikaa kwenye mahusiano kwa mwaka mmoja tu na Kelvin ndiyo alikua analazimisha kumuoa.
“Unanipa shilingi ngapi?” Mfanyakazi mwenzake alimuuliza, alijua kuwa Kelvina anashida hivyo ni lazima atatoa pesa.
“Kwahiyo unataka nikulipe kwa kumdanganya Mama yako?”
Sasa, hivi kuna kitu cha bure hapa, wewe nakujua, mpaka unakua hivyo kuna kitu umepata, kama hutaki mtafute mtu mwingine umuambie, lakini kama unavyojua, kuna wambea wnegi, angalau mimi unaniamini.”
“Nakuamini wapi, kwani wew ehuwezi kutangaza?” Kelvin aliuliza huku akiingiza mkono wake mfukoni na kutoa noti mbili za elifu kumi kumi.
“Nitangaze ili nini, yaani huniamini kweli, mimi tumetembea wote lakini mademu zako wote wakija hapa najifanya wifi, hakuna mtu hata mmoja ambaye anajua kuwa ulishanilala ndiyo nije kusema hiki…” Aliongea huku akipokea zile noti, alimuangaiia kama anataka hela ya ziada lakini kelvin alionyesha kutokutaka kutoa tena.
“Hivi huyo mwanamke anaolewa na wewe ana akili kweli, mwanaume mbahili namna hii, yaani ni kuelelwa tu?” Alilalamika, kwa namna alivyokua anamfahamu Kelvin alijua fika kuwa hawezi kutoa pesa nyingine.
Alichukua simu, akapiga namba ya mama yake Kelvin na kuanza kuongea, alikua anaongea kwa kulia kabis ahukua kiomba msamaha.
“Nisamehe Mama, najua nimekuumiza, Kelvin ni mtu wa Mungul nilimuumiza mwanzo na nilikua siamini kuwa anawez akuniacha, lakini nimefikiria nikaona kuwa hakuna haja ya kuvunja ndoa ya kanisani, nisamehe, najua nimekukwaza, una mtoto mwema sana, mimi ndiyo nilimsaliti na rafiki yake ndiyo naana mpaka sas anina hasira kwani huyo rafiki yake kaniacha na mimba, yaani nimechanganyikiwa sijui hata naishije, alkini mwanao hajawahi kuja kwetu, hajawahi kunidanganya.”
Kwa namna alivyoongea ilikua ni lazima Mama wa watu kuamini, alikua anaigiza vizuri na aliweza, aliongeza hata vitu vingine ambavyo hakuambiwa.
“Nimekuelewa mwanangu, ndoa inapangwa mmbonguni, kama haikupangwa uolewe na mwanangu basi jua kuwa Mungu kakupangia mume wako sehemu nyingine, cha muhimu ni kufanya toba. Nenda kaungame, kamuambie Mungu madhaifu yako kwani yeye anasmahe….”
Alipewa wosia wakutosha, mwisho waliagana na kukata simu. Hazikupita hata dakika tano, simu nya Kelvin iliita, alikua ni Mama yake, alimuelezea kila kitu.
“Nisamehe mwanangu, sikukuamini uliponiambia kuwa huyo mwanamke si mwanamke wako, nisamehe Mwanangu, nilichanganyikiwa, mimi siajalea mtoto wa namna hiyo, nadhani binti kajifunza….” Mama yake aliongea kwa uchungu sana alionekana kuumia kwani mwanzoni aliamini kuwa mwanae anaweza kwenda kujitambulisha kwa mwanamke mwingine bila kushirikisha familia yake.
“Mama huna haja ya kuomba msamaha, hata kama ni mimi ningemuamini yule binti, nashukuru Mungu yameisha, ila Mama acha kusikiliza hawa mabinti wa mjini, shid anikuwa nina marafiki wengi ambao nawasaidia, lakini wengi wanachukulia vibaya, hivyo acha kusikilia maneno yao, mimi si mtu wa namna hiyo, unanijua mwanao.” Waliagana na Mama yake, bila kujali kama kule nyumbani alikua ameacha watu alimchukua yule dada mfanyakazi mwenzake wakaenda kwa yule dada wakaongea ongea mwisho wakajikuta wanafnaya mapenzi.
****
Wakati Kelvin anandoka, Anna na yule mwanamke mwingine walikua wanapigana, walikunjana, lakinibaada ya muda walijiona wajinga, mtu waliyekua wanampigania alikua kaondoka kawafungia ndani. Baada ya kama dakika kumi hivi waliachana, walipojaribu kufungua mlango walishindwa, kufungua na kulazimika kukaa, mwanzo walikaa wamenuniana, lakini baada ya muda walichoka na kujikuta wanaongea.
“Wewe una muda gani uko na Kelvin?” Anna alimuuliza yule Dada.
“Kelvin? Kelvin ndiyo nani?” Yule dada alishangaa kusikia lile jina, ni kama ndiyo ilikua mara yake ya kwanza kulisikia.
“Si huyu mwanaume tunayemgombania, inamaana hujui hata jina lake, au na wewe ni wale wanawake zake wa siku mmoja moja.” Anna aliuliza kwa dharau kidogo alipoona yule dada anashanaga alijisikia vizuri kidogo kuwa kumbe yule mwanamke alikua ni malaya tu na hakua mchumba kama yeye.
Kua na adabu, mimi si malaya, hivi ukiniangalia mimi naweza kuwa malaya, labda wewe uliyedanganywa jina, mimi niko na Saidi mwaka wa nne sasa!” Yule dada naye alimjibu kwa dharau huku akimpanisha na kumshisha.
“Saidi? Saidi ndiyo nani?” Anna aliuliza.
“Inamaana hujui hata jina lake, yaani wanawake wengine mnachekesha, huyu ni mchumba wangu, kanivalisha mpaka Pete, jina lake ni Saidi, hilo la Kelvin mimi silijui.
“Hakuna kitu kama hicho, Kelvin ni Muikristo na kanisani anaenda, ninaenda naye mbona kila mara.”
“Uikristo autoe wapi, Kelvin ni muislamu, au unafikiri hizo kaznu zilizojaa humu ndani anamvalia nani? Yaani ni muislamu mpaka unaboa, hivi unajua mimi alikua ananikaaza mpaka kuvaaa suruali, yaani?”
Walionekana kuchanganyana, kila mmoja alikua analilai kuwa Kelvin ni wa dini yake. Yule msichana mwingine ambaye baadaye alijitambulisha kuwa anaitwa Salma, alikua kwenye mahusiano na Kelvin kwa miaka minne, alikua akimtambua kama Saida. Anana hakuamini kuwa Kelvina anaweza kuwa ni muisalamu, Salma alitaka kumuonmyesha, waliingia chumbani wkake, wakaanza kukagua, wlaivurumusha kila kitu, wakafungua mabegi ndipo akaja kukuta kuna begi maalumu limewekwa uvunguni ambao lina kanzu na vitu vingine vya kislamu.
Hakuamini macho yake, wlaifanikiwa kuona vyeti vyake, hapo ndipo aligundua kuwa Kelvin jina lake si Saidi ni Kelvin, kwa maana kuwa kwa miaka minne alikua akidanganywa, alikua akimuamini na alishanga anajuamambo mengi ya kiislamu kuliko yeye. Katika kupekua pekua ndipo waliona Kopi ya hati ya kiwanaja, wakati Salma alikua na mkataba wa mauziano ambao ulionyesha kuwa kiwanja kina jina lake, yaani lake peke yake, huku Anna yeye akiwa hana chochote lakini aliamini kuwa kiwanja kina jin ala Kelvin mchumba wake waliona kuwa kile kiwanja kina hati na ina jina la Mama yake na Kelvin, waliona kopi tu, walihangaika kutafuta Origional yake lakini hawkauiona.
Walijikuta wanchoka na kukaa huku wakiangaliana. Wote walichoka na kila mmoja alitamani tu kuotoka mule ndani, lakini walishindwa kwakua Kelvin alikua kafunga mpango kwa nnje. Anna aliabnza kutafuta simu yake, akajua kuwa hakua nayo ndipo alikumbuka kuwa kuna wakati Kelvin alikaua meioshika kipindi tunagombana.
“Nilimpigia simu Mama yake kumuambia kuwa mimi ni mchumba wake na kashakuja kwetu kujitambulisha nahisi ndiyo maana alinitafuta ili kuongea na Mama yake.” Anna alilalamika.
“Mimi mbona kahsanipeleka kwa Mama yake Singida.” Salma aliongea.
“Mama yake gani yupo singida, singida ndipo aliposoma Sekondari lakini hakuna Mama yake kule, Mama yake yupo Morogoro na unfika ungejua tu kuwa ni muikristo kwani ni mtu wa dini sana.”
“Mhhh, sasa singida kwa huyo Mama aliyenipeleka ni nani? Wewe umemuona Mama yake.”
“Nilishamuona lakini hanifahamu, nilimuona kanisani, baada ya kuona kuwa hataki kunipelaka kuna kipindi nilikua Morogoro kikazi, nikaenda kanisani makanikamuona, nilishasalimiana naye kama mtu mwingine wa kanisa lakini hajui kabisa kuwa ni mimi.” Anna aliongea kwa hisia sana, alikua anaumia kwani alikua anampenda sana Kelvin, alikua ni kila kitu kwake, pamopja na vipigo, kumfumania mara kwa mara, kudhalilishwa lakini bado alikua anampenda na alikua akiamini kuwa iopo siku atabadilika, atamuoa na watakua familia.
“Aisee, saidi ni shetani, yaani mimi kanipeleka mpaka Singida akanionyesha mwanamke ambaye akaniambia ni Mama yake, yaani huyo mwanamke kila mara nampigia somu, tunaongea, namtumia mpaka pesa.”
“Anakuomba pesa?”
“Ndiyo, ananiambia kuwa anshida, mara sijui kakwama wapi, mara hiki mara kile?”
“Mama yake si mtu wa kuomba pesa, kwao mbona wana uwezo mzuri, Mama anafanya kazi nzuri tu, ni Mhasibu, sasa kwanini aombe pesa.”
“Yaani kuna wakati ananiomba mpaka nimtumie vocha, sas ahuyo atakua ni nani? Hembu muangalie, mimi mpaka nikahisi wamefanana, yaani…” Salma aliongea huku akitoa simu yake, alifungua upande wa picha na kumuonyesha Anna picha za mwanake ambaye yeye alikua akiamini kuwa ni Mama mkwe wake.
“Angalia hizi nilipiga naye kipindi anaenda kunitambulisha na….”
“Phuuuu…. Pguuuuu… phuuuu…! huyu ndiyo Mama yake?” Anna alimkatisha baada tu ya kuona zile picha, alianza na kucheka.
“Kwanini unacheka.”
“Huyo mwanam,ke namfahamu, ni Mama malaya tu, ni mwanamke wake tangu anasoma sekondari! Huyo Mama alikua ni Mwalimu wake na wametembea pamoja muda mrefu,k nishamfumania sana, hata hapa aalishawhai kuja.” Anna aliongea kwa hasira hukua kichekacheka kumshangaa kwa kudanganywa kiasi kile.
“Hapana, hawezio kutembea na Mama mtu mzima namna hiyo? Hawezi, yaani ningekua na simu yangua liyochukau ningekuonyesha, nina picha zake nyingi za uchi ambazo nishazikamata kwenye simu ya Kelvin. Tena huyo mwanamke anakuja mara nyingi hapa, nishawafumania wakifanya mapenzi hapahapa sebulani, si kuambiwa.”
“Kuja najua anakuja, na akija ananiambia, anasmea nije kumsalimia Mama, nishakuja mara nyingi kumpikia nikijua ni Mama mkwe wangu.” Salma alijibu kwa mshanagao, kwa salma kila kitu kilikua ni mshangao, yeye alionekana kudanganywa kikubwa.
“Ngoja nikuulize, kama unajua mwanuame ni malaya namna hii mbona uko naye, hivi unajua kuwa mimi sijawhai kumfumania, toafuti na kipindi mile nimekuja na kukukuta hapa, tena akaniambia kua wewe ni X wake mimi siajwahi kumfumania, tena kama ni kuja nakuja nikijisikia lakini sijawahi kukuta mwanamke mwingine humu ndani. Sasa kama unamfumania kwanini bado uko naye.” Salma alimuuliza kwa mshanagao, alimuangalia kama kituko.
”Kweli hujawhai kumfumania?”
“Hapana, hata siku moja. Hivi kweli nimfumanie mwanaume nimlete kweli, na nakuja mara kibao nalala. Nakusangaa wewe kama unajua ujinga wote huo kwanini uko naye?”
“Hata mimi sijui, labda nikakuwa ndiyo mwanaume wangu wa kwanza kumpenda, nilishawahi kuwa na wanaume wengine lakini si kama huyu, nimejaribu snaa kumuacha lakini nimeshindwa, nampenda sana, amenifanyia vituko vingi lakini kila wakati naamini kuwa atabadilika, yaani sijui hata chakufanya.
Nilishamfumania mara nynyingi, tena si kumfumania tu, kuna wakati nilikua nafanya naye mapenzi, mwanamke wake akaja kugonga, yaani huyo mwanamke alikuja bila taarifa. Akanitoa chumbani tulikkua tunafanya mapenzi na kunifungia chumba cha wageni, akaingiza mwanamke wake, wakapika na kula niko chumbani kisha akamuingiza chumbani kulala ndiyo akanitoa na kuniambia niende kwangu.” Anna aliongea huku akilia.
“Yaani mwanaume kakufanyia yote hayo na bado uko naye, hivi una akili kweli?” Salma alimuuliza.
“Tatizo nampenda.”
“Hata kama, lakini siwezi kufanya ujinga kama huo. m,imi nilimfumania mara moja nawewe na nilitaka kumuacha, ningekua nimemfumania kama wew eningemuua kabisa. Sasa hivi nimekubali kumuacha, nilikua hapa kumuambia kuwa atanirudishia kila kitu changu na kamwe siwezi kurudiana naye, na nina uhakika atanirudishia.
“Kivipi wakati nyumba kaandika majina ya Mama yake?” Anna aliuliza kwa wasiwasi.
“Hunijuli na wala huyo mwanaume wako hanijui, hata kama angeandika majina ya malaika ila nina uhakika mali zangu nitapata. Mimi ni mtoto wa mjini, nimetoka familia ya kimasikini sana, yaani mimi pekee ndiyo nimetoka, nimekuja mjini kutafuta, unaponjona hapa niliacha shule nikiwa kidato cha pili, nimekuja mjini nimetafuta mpaka nimejisomesha nina digrii moja na sasa hivi natafuta yapili, nina Biashara zangu, nilikua najenga naye najua kuwa ni vitu vya familia lakini kama niliivyomuambia, hii nyumba naichukua na nitaiuza kwani sihitaji kumbukumbu, na nilitaka tugawane ila kwa ushenzi alionifanyia hachukui hata shilingi.”
Salma aliongea kwa kujiamini, wakati mwenzake alikua akilia yaye aliongea huku akimsikitikia.
“Utafanya nini sasa, mwenzako atafuta kisheria!”
“Ulishawahi kubakwa?” Salma alimuuliza.
“Hapana, kwanini wewe ulishawahi?”
“Ndiyo, wakati naingia tu mjini, kipindi hicho nilikua mjinga mjinga, nilikua nauza matunda kariakoo, kuna Baba mmoja akanipenda na kuniambia kuwa atanipa mtaji. Basi, kwakua nilikua namfahamu nilikubali, ni Baba mtu mzima, alinichukua kwake kama anaenda kunisaidia, alitaka nikafanye kazi za nyumbani.
Nikamuambia hapana, mimi siwezi kufanya kazi za nyumbani, sikutoroka kijijini ili kuja kufanya kazi za nyumbani, basi akaniambia atanipa mtaji. Lakini nilipofika kwake, usiku alikuja chumbani kwangu, akaniingilia kimapenzi kwa nguvu, hakuishia kuniingilia kawaida, aliniingilia mpaka kinyume na maumbile. Alinitishia kama nikiongea ataniua, basi mke wake asubuhi alijua kwani alikuja na kuniambia nikaoge nijisafishe, nilimuambia alichokua kanifanyia mime wake lakini hakujali, alinijibu wewe malaya umekuja kujitega kwa mume wangu unasema umebakwa.
Niliumia sana nikaondoka bila kupewa hata shilingi kumi, lakini wakati naondoka binti wa kazi amabye alikua pale aliniambia ni kawaida, hata wao wanafanyiwa hivyo. Unajua nini kilichotokea?”
“Sijui, ulienda Polisi?” Anna aliuliza, alishaacha kulia alikua akimsikiliza Salma, kwa namana alivyokua anaonekana hakuonekana kabisa kama amepitia maisha magumu, alionekana kama mtoto wa kishua lakini ukweli nikuwa alihangaika sana katika maisha yake na alisaiodia mpaka ndugu zake wakatooka kimaisha, alipokuatana na Kelvin ndiyo kwanza alikua kamaliza kusaidia ndugu akawa anajichangachanga kwaajili ya kutengeneza familia.
Alikua ana duka la nguo, hakua akipata pesa sana ila alijichanga kusidia ndugu na nyingine aliwekeza na Kelvin.
“Polisi kufanya nini? Kwa ushahidi gani wakati kabla ya kuondoka mke wake lihakikisha kama ninaoga, yule Mama alikua anajua kila kitu. Kilichotokea ni kuwa, yule Baba baada ya wiki moja alijirusha kutoka Ghorofani akafa haophapo.” Anna aliongea huku akifunga macho, alikua kama anakumbukia lile tukio, alitabasamua kidogo kama vile alikua anavuta hisia kisha anapata raha flani.
“Wewe ndiyo ulimsukuma?” Anna aliuliza huku akimuangalia kwa uoga, namna alivyokua anafurahia kifo ilimtisha.
“Hapana, sikumsukuma, lakini unajua kwa mwanamke kuingiliwa kinyume na maumbile inauma, lakini kwa mwanaume lazima uchanganyikiwa. Yeye alinibaka, akanilazimisha na kuniona mimi mtoto, lakini kumbuka kipindi hciho nimekuja mjini, sina pakulala, nalala barabarani. Niliondoka kwake sina hata shilingi kumi, hata mtaji wangu ulikufa, nilirudi mtaani kule ambapo kuna wanaume.
Nakumbuka nilitafuta vijana wawili, wakamvizia na kumfanyia kilekile alichonifanyia. Unaua niliwalipa nini ha0 vijana?”
“Sijui” Anna alikua anajibu kwa uoga, wakati anaielezea ile stori Salma alifanya hivyo kwa hisia kazi sana.
“Nilitembea na mmoja wao kama malipo ili tu wakamfanyie vile yule Baba na nilishuhudia, nilitaka aone kuwa mimi si kama wale mabinti wa kazi aliokua wanawafanyia ujinga. Kipindi hicho nilikua binti mdogo, sina kazi sina pesa, sas ahivi ni mtu mzima, nina uhakika, kabla hajafunga ndoa na huyo mwanamke wake hii nyumba itakua ya kwangu.”
“Sasa na mimi, unajua na mimi nimechangia, sasa kama akikuachia yote itakuaje?” Anna alihisi wamekua mashoga, alitoa pesa zake nyingi kwenye ile nyumba na alishaona kama anaweza klupata msaada kutoka kwa Salma.
“Dada mimi sio shoga yako, tumeshea Bwana na naongea na wewe kwakua tumefungiwa ndani lakini hata tukitoka hapa sitaki kujuana. Wewe ni mpumbavu, kama unafanyiwa ujinga wote huo na bado unavumilai basi wewe ni mpuuzi na mimi katika maisha yangu sitakagi ushoga na wapuuzi, kama ni kudai chako hakikisha utadai kivyako ial hii nyumba huyu mwanaume haoi kabla ya kunipa.”
Ukimya ulitanda, walijaribu kumpigia simu Kelvin lakini ilikua haipatikani, kuona vile Slma alimpigia mtu mwingine.
“Njoo kule saiti kwangu, nimefungiwa ndani njoo uangalie namkna gani utavunja kitasa.” Alikata simu na kukaa katulia, hakuongea neno jingine, kama nusu saa hivi alikuja kijana mmoja, akafika kwenye kitasa na kuanza kukichokonoa mpaka mlango ukafunguka. Salma aliondoka na kumuacha Anna pale alishangaa shangaa, pamoja na mlango kufunguliwa lakini bado hakutaka kuondoka.
Salma alienda lakini baada ya kama dakika mbili hivia ligundua kuwa kuan vitu vyake alisahau, alirudi na kushangaa anamkuta Anna pale.
“Vipi wewe huondoki? Inamaana unamsubiri huyo mbwa mpaka arudi?”
“Ndiyo sasa nitaondokaje wakati mlango haujafungwa, mimi sina funguo yake na hata kama ningekua nayo kitasa kimevunjwa, naweza kuondoka huku numa akaibiwa.” Anna aliongea kwa kuajali, Salma alimuangalia kwa dharau kisha akatema mate chini.
“Kweli wewe ni Taahira, yaani mwanaume kakudhulumu mali zako na ujinga wote huo lakini bado unawaza yeye kuibiwa, aisee kwa heri baki na utaahira wako.” Aliongea akaondoka na kumuacha Anna pale.
Sitaki kukuchosha na mambo mingi, kama unajiona wewe ni king’ang’anizi kama Anna, wewe ndiyo wale ambao unamfumania mpenzi wako akinuna tu unamuomba msamaha basi soma sehemu ya Nne ya Kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” kwani usipojipenda hata kidogo tu basi utakua zaidi ya Anna.
ANNA; MKE WANGU NAOMBA UNISAMEHE KWAKUKUOA—SEHEMU YA TANO!
Mpaka saa nne usiku Kelvina likua bado hajarudi nyumbani, usili ulishaingia lakini Anna hakutaka kuondoka, alihofia kuiacha nyumba wazi.
“Hata kama ameniumiza sana lakini hivi vitu tumenunua wote, vikiibiwa ni kama mimi nimeibiwa.” Aliwaza, alikua kachoka sana, mishemishe za mchana zilimchosha, na kila wakati alikua anapitiwa na usingizi, kwa kutumia simu yake ndogo alijaribu kumpigia Kelvin lakini simu haikupokelewa. Alikaa mpaka saa nane usiku ndipo Kelvin alirudi, alirudi akiwa kalewa sana, hata gari hakurudi nayo, ni Dereva wa Bajaji ambay elimleta na kumuacha pale nnje.
Alikua kalewa sana kiasi kwamba alikua hata hakumbuki chochote.
“Mke wangu, naona umekuja, samahani nimechelewa, nakupenda sana…” Aliongea kwa sauti ya ulevi, Kelvina likua hajitambui, mara kwa mara alimkumbatia, kumpiga mabusu na kumuambia kuwa anampenda.
“Niache bwana, wewe si unaenda kuoa mwanamke mwingine halafu unajifanya kunipenda, niache!!” Anna alilalamika huku akimsukiuma. Pamoja na kwamba alikua amechoka, analia kutokana na kuumizwa lakini shikashika ile ilimpa hamasa, alijisikia vizuri.
“Unanioiita mke wakati unaenda kuoa mwanamke mwingine?” Alimuuliza huku akimkokota mpaka kitandani.
“Wewe ndiyo nakupenda, hujui tu, mimi ni malaya wkeli lakini kila siku narudi kwako, mimi siwezo kukuacha, hata wakinilazimisha kuoa siwezi kukaucha, sitaoa, nitakua na wewe… nakupenda… nakuependaaa mpenzi wanguu, wewe ndiyo maisha yangu….” Aliongea kwa sui yake ya kilevi huku akiimba, Anna alimfikisha kitandani, alimvua nguo na kumlaza, alitaka kuondoka lakini Kelvin hakutaka, alimvunta mpaka kitandani na kumkumbatia.
“Usiniache, usiniache, nitakufa, usiniache!” Alimuambia huku akimkumbatia kwa nguvu zaka, Anna hakua na namna alilala pembeni yake.
“Wewe kila siku unanifanyi vituko halafu unasem aunanipenda, kuna upendo kweli kati yetu?” Aimuumiza, lakini kugeuka Kelvin alishalala manakoroma usingizi, alikua kazima, alimlaza vizuri lakini ile anamuweka kitandani tu alishtuka, na kumuuliza.
“Unaenda wapi mke wangu?” Alikua anataka kama kunyanyuka lakini alishidnwa.
“Naondoka, mimi naudi nyumbani, nilikuja kwakua uliniambia unanihitaji, lakini nimegundua hukuwa unanihitaji, ulitaka tu niongee na Mama yako ili nisikuharibie ndoa yako, nimekubali kuwa wewe si wangu, hunipendi na wala hujawahi kunipenda, nimekubali kuwa huwezi kuwa wangu wewe endelea na….” Aliongea kama analalamika lakini Kelvin alikua ameshalala, alitoka kitandani na kurudi sebuleni, hakuaka kulala mule ndani, usiku ulishaingia hivyo alitamani kuondoka.
Lakini aliopofika mlangoni alikumbuka kuwa mlango ulikua umevunjwa hivyo ilihitajika fundi kuutengeneza, kwa hali aliyokua nayo Kelvin alijua kuwa hawezi kuamka na kufunga mpango kama yee akiondoka. Alifunga mlango kwa ndani kwa kutumia vitasa vya ndani, kisha akaenda kulala chumba cha wageni, hakutaka kwenda kulala pamioja na kelvin kwani angeweza kumlazimishia kufanya mapenzi wakati yeye hakuwa tayari kwa hilo.
Alilala mpaka asubuhi, yeye ndiyo alikua wa kwanza kuamka, baada ya kuamka alienda kumuamsha Kelvin ili kumuaga kuwa anaodnoka. Alimuamsha, lakini ile kumshika tu Kelvin alishtuka, ni kama alikua kaona mzimu flani.
“Unafanya nini hapa nyumbani kwangu? Wewe si umeniharibia kwa Mama yangu, si unataka kuharibu maisha yangu unafanya nini?” Alioongea kwa hasira huku akimsukuma.
“Hakluna nimekuja kukuaga, jana uliniita lakini ukatufung….” Alijariubu kumuelezea lakini Kelvin hakumpa nafasi, haakaharaka alinyanyuka na kumshika mkono, alikua uchi wa mnyama, hajavaa nguo lakini alimshika Anna na kumvuta mpaka mlangoni, 0ndoka, sikutaki hapa, umeshaniharibia kila kitu.
“sawa naondoka, nilibaki tu kwakua mlango ulivunjwa?” Anna alijiteea huku akitoka.
“Mlango ulivunjwa? Ulivunjwa na nani?” Aliuliza, alionekana kama vile hakumbuki chochote.
“Mwanamke wako, tena kuwa makini na yule mwanamke, kuna kitua anweza kukufanyia, sijui unamjuaje lakini mimi jana nimeongea naye, yule dada ni mshenzi, yaani mimi mwenyewe kama namuogopa, kuwa makini anaweza kukufanyia kitu kibaya.” Kelvina likua bado akshikwa na butwaa, alisimama kwa muda hukua kiangalia juu, alikua anawaza ni kitu gani kimetoke ajana yake, alishika shika mlango sehemu iliyovunjwa ndipo alianza kukumbuka.
“Anasema kuwa umemdhulumu, mimi umenidhulumu lakini nakupenda, kuna kitu kibaya anataka kukufanyia kabla ya harusi yako, kuwa makini, nakushauri usionane naye…” Alijaribu kumuelezea kuhusiana na Salma lakini Kelvin alikua haelewi.
“Unamaanisha nini? Mbona sikuelewi, ananifabnyia nini, kwani unajua nini kuhusu yeye.”
“Simujui sanalakini jana wakati umetufungia ndani aliniambia mambo mengi, aliniambia kuwa kuna Baba aliwahi kumbaka akajiua kwaajili yake, sijui walimbaka na yeye huyo Baba muhindi, kuwa makini, wanaweza kukufanyia mambo mabaya, anaonekana kujua na na wahuni, hivi unajua kuwa alikua analala mtaani, alikua ombaomba….”
“Hujui unachoongea, utakua umechanganyikiwa, hembo ondoka nyumbani kwangu, sitaki kukuona tena. Nishamalizana na wewe, sikutaki, naoa wiki mbili zijazo, naondoka kesho kutwa kwa maandalizi ya harusi, sikutakii, sikutaki, kama ukipata mwanaume mwingine olewa, sina muda na wewe!” Kelvina liongea kwa dhara, Anna ni kama alikua anasikia maneno yake kwa mara ya kwanza.
“Lakini jana ulisema unanipenda kule umelazimishwa kuoa?” Aliongea huku akilia na kumsogelea Kelvin, aliinama kama kumkumbatia, Kelvin alimsukuma na kurudishia mlango kwa nguvu. Anna alipepesuka kidogo adondoke lakini alijitahidi na kunyanyuka, alitoka nnje akatembea mpaka karibu na barabara, akakutana ana bajaji akapanda na kuondoka, ilitakiwa kwenda kazini lakini hakufanya hivyo, aliondoka zake na kurudi nyumbani ambapo aliishia kulia tu.
***
Baada ya Anna kuondoka Kelvina lipigiwa simu kuwa anahitajika kazini, aliingia bafuni kuoga kisha akaenda kazini. Alikutana na Bosi wake ambaye alimuambia kuwa likizo yake imtacheleweshwa kwakua kutakau na wakaguzi, alitaka kuchukua likizo kwakua Mama yake alimuita, alitaka awepo wakati wa maandalizi, lakini yeye kama yeye hakutaka kwenda nyumbani, hasa baad aya lile tukio, alitaka kuendelea kubaki dar na kula maisha, alimpigia simu Mama yake na kumuambia, Mama hakua na namna ziadi ya kukubali.
Hakukaa sana kazini, alikua bado ana uchivu, alitoka na kwenda kunywa supu.
“Nisamehe kwa mlango wako lakini sikua na namna mpenzi, jana ulinikwaza san.” Meseji iliingia, alikua ni Salma kamtumia, aliiangalia na kucheka mwenywe.
“Nilijua tu kuwa hawezi kuniacha, hasira zote zile za jana leo katulia anaomba msamaha, sasa nitakavyomsumbua hataamini. Alichukua simu yake na kumpigia, alianza kwa kumfokea kwa hatua yake ya kumvunjia mlangop, aliongea kwa nyodo sana.
Pamoja na kwamba alikua amaezaea kumnyanyasa Anna lakini alikua ahjawahi hata mara moja kumtukana wala kujibu vibaya Salma, yeye alikua ni mtu wa kukasirika kasirika na kila mara akifanyiw akitu kibaya alikua anaongea, tena si kwa kubembeleza bali kwa hasira na kumuambia kama hawezi kumuongelesha vizuri kama mtu mzima basi amuache, kwa namna flani ni kama alikua anamuogopa hivyo siku ile alivyoona anaomba msamaha na kwakua alikua anatafuta sababu ya kumuacha alimkasirikia, akamtukana sana.
Wakati anatukana Salma alikua anaomba msamaha, alikua anamuambia kuwa ampe nafasi nyingine lakini Kelvin hakua tayari.
“Naomba tuonane, nisiadie, nataka kuonana na wewe, kumbuka hata kama nimekukosea lakini tulikua wapenzi, najua unaoenda kuoa lakini nipe nafasi nikuambie yakwangu ya moyoni, nipe nafasi nikuombe msamaha.” Aliongea huku analia, Kelvin alimuambia kuwa hayuko nyumbani bali aje jioni, Salma alishukuru sana, alimuambia atakuja na hataleta kama mwanzo.
Baad aya kukata simu Kelvina alishangilia na kujiona mshindi, alirudi nyumbani Kulala, jioni kama walivyoahidiana Salma alikuja nyumbani, alikuta Kelvina bado kalala, alimgongea akamfungulia mlango. Alikuja kiunyenyekevu, Kelvin alimkaribisha, alipomuona jinsi alivyokua mpole alipata nguvu na kuanza kumkoromea.
“Mimi nimekuacha kwakua ulikua unajifanya mbabe, nilikua nakupenda na….” Aliongea lakini Salma hakumpa nafasi.
“Baba, sikuja hapa kufokewa, huna uanaume huo wa kunipigie kelele mimi. Kilichonileta nikwakau, nataka uchukua hizo Fomu, ni za wakili, ni za huhamisha umiliki wa kiwanaja na hii nyumba kuja kwangu. Najua hati ya hii nyumba umeandika jina la Mama yako, sasa najua wkenye hati huwezi kufoji, hivyo Mama yako alisaini. Sijui utamuambieje lakini nataka uchukue umepelekee Mama yako, asaidi weke na dole gumba lake kuwa kaniuzia hiki kiwanja na nyumba na kila kitu humu, una siku mbili za kufanya hivyo, nataka uende kwenu Morogoro umpelekee Mama yako?”
Kelvina laishangaa kusikia hivyo vitu, Salma alikua na kila kitu, alikua na kopi ya hati ya kiwanja ambayo aliichukua jana yake, alishaanda amkataba wa mauziano wa ile nyumba, akaandika majina ya Mama yake na Kelvin kuwa yeye ndiyo atatakiwa kumkabidhi, yaani alikua kajiandaa.
“Unaakili kweli, kwanini nifanye huo ujinga, hivi unafikiri mimi sina akili, yaani kwanza haya mambo umejuaje, kwahiyo jana wewe na huyo mjinga mwenzako ndiyo mliambiana hivyo? Hivi una akili kweli, yaani unadhani kama niliweza kukudhuklumu, kuwadanganya nyie wote mkanijengea nyumba unafikiri ni kitu gani utafanya mpaka nikuogope!”
Ingawa alijitahidi kuongea kwa kujiamini lakini alikua anaogopa, hakujua ni namna gani Salma alikua amejua vitu vyake lakini hakutaka kujionyesha mnyonge.
“Baba nadhani hunijui, mimi si dhulumiwi, labda nikuambie kuhusu mimi…” Salma alianza kumuelezea hisotoria ya maisha yake, alimuambia kila kitu mpaka kuhusu huyo mwanaume ambaye alimbaka na kumuingilia kinyume na maumbile.
“Acha kuniambai ujinga wako, kwahiyo unaniambia ili niogope au?”
“Hapana sina sababu ya kukutisha, siwezi kukufanyia hivyo kwakua kuna wakati nilikua nakupenda, hukunibaka na ni ujinga wangu kumuamini mwanaume. Lakini uanchotakiwa kujua ni kuwa, nimetoka katika familia ya kimasikini, nimeteseka sana.
Mwanaume wangu wa kwanza alinibaka, akaniingilia kinyume na maumbile, niliumia sana, mwanaume wangu wa pili ni mwanaume ambaye nilimlipa pendi ili akanisaidia kulipa kisasi. Wakati sijui nilikua na miaka 17, ndiyo nilikua mdogo, lakini jinsi nilivyo na kisasi cha ajabu, nilitafuta wanaume wawili, nikatembea nao kama ujira, ili waende kufanya mapenzi na yule baba, wampige picha kama kulipa kisasi. Sijui hata hizo akili nilizitoa wpai lakini niliridhika sana baad aya yule baba kubakwa kama mimi.
Lakini niliumia sana kusikia amejiua, si kwasababu nilitaka aishi bali nilitaka ateseke kuwa kila sikua kitaka kubaka binti mwingine akumbuke nina picha zake. Sasa hembua ngalia hizi picha, na angalia hili gazeti ambalo liliandika mfanyabiashara Kariakoo ajiua kwa kujirusha kwenye Ghorofa, hii ilikua ni kazi yangu, sijui hata kwanini naziweka mpaka sasa, lakini iswezi kuzifuta. Unakumbuka kipindi kile, aisee mimi ni shida, kipindi kile kulikua hakuna hata kamera za simu, lakini mimi nikatafuta na mpiga picha kabisa ili mzee, aone, vuta picha sasa hivi nachukua na video kabisa.”
Alikua anaongea taratibu sana, yaani kama mtu anaongea na mtototo anataka kumuelewesha ili baadaye kusijekuwa na maswali mengi. Kelvin aliziangalia zile picha kwa hofu, alimuangalia mwanamke aliyekua kaaka ambele yake kama vile ndiyo anamuona kwa mara ya kwanza, alikua anajua kuwa Salma si mtu wa mchezo mchezo hapendi ujinga lakini si kwa kiwango hicho.
“Kwahiyo unanitishia, unataka kunitumia watu?”
“Hapana, sikutishii, ningekua nakutisha ningekuja na watu, lakini nakuambia tu kuwa mimi sidhulumiwi, nilikua nakupenda sitaki siku moja ujiue kwasababu ya aibu. Hivi fikiria siku ya harusi yako Mama yaako anatumiwa video mtoto wake anashikwashikwa makalio, anafanyiwa mapenzi mkitume na maumbile, hivi usipojia wewe si atajiua Mama yako, sitaki tufike huko, natumaini una akili hivyo utafanya maamuzi sahihi.
Lakini najua wanaume hawaamini mpaka waonyeshwe vitendo ndiyo maana nimeamua ili usinipotezee mdua basi nikuonyeshe kuwa mimi nimekulia uswahilini.” Salma aliongea huku akinyanyua simu, aliBeep namba flani kisha mlango ukagongwa, alinyanyuka na kwenda kuufungua, waliingia vijana wawili tu wa kawaida. Hapo Kelvin alianza kutetemeka.
“Ndiyo huyu?” Walimuuliza, alijibu kwa kichwa kukubaliana nao.
“Unataka kunifanya nini? Mnataka kunifanya nini? Wewe ni msheniz, mnanifanya nini?” Kelvin aliuliza akitaka kukimbia lakini walimkamata. Mmoja alimshika Kelvin na kumkaba shingoni na meingine akaanza kumvua nguo, akabaki uchi wa mnyama kama vile alivyozaliwa, uoga ulimzidi, akawa naatetemaeka mpaka akajikojolea. Alitamani kupiga kelele lakini hakutaka watu waje, pia nyumba yake ilikua mabli asingweza kupata mtu wa kuja.
Walimvua nguo tu na kubaki kama alivyozaliwa, Kelvina alipambana sana, alijirusha huku akitukana lakini Salma hakujali.
“Nina kisasi cha ajabu sana, yaani nina kisasi cha jabu, sikufanyii hivi kwakua hukunioa, hapana, ndoa zipo tu, mbona watu wanaachana kila siku. Au unafikiri wewe ni wakwanza kuniacha, lakini nikikumbuka nilivyopata shida kutafuta hizi pesa nitakua mjinga kama nikikuachia kila kitu. Najua nikiondoka bila kufanya chochote hutakua siriasi, utadhani natania, ngoja nikuonyeshe kidogo tu kuwa na mimi ni mshenzi.” Aliongea hukua kimsogelea Kelvin ambaye alikua kashikwa na kukabwa vizuri na wale vijana uchi wa mnyama. Hakikisha unabonyeza;
ANNA; MKE WANGU NAOMBA UNISAMEHE KWAKUKUOA—SEHEMU YA SITA
(ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO; Kelvin amewadanganya Anna na Salma kuwa anawapenda lakini anaenda kuoa mwanamke mwingine. Wote wanaenda kwake lakini anawafungia ndani, wanagundua hati ya nyumba ina majina ya Mama yake. Salma anaondoka lakini Anna anabaki, Salma ametoka mtaani, alishawahi kubakwa na kulipa kisasi kwa mbakaji.
Anaahidi kuchukua nyumba, anatafuta vijana wawili, wanakuja nyumbani kwa Kevin, anamuonyesha picha za mwanaume ambaye alimbaka akiwa mdogo na kulipa kisasi, anamuambia kuwa anataka nyumbaibadilishwe majina la sivyo atamfanyia kitu kibaya, kumrekodi na kusambaza picha kwenye harusi yake. Wanamvua nguo na Kelvin anaetemeka kwa uoga hajui nini nikafuata…ENDELEA…)
Salma alikua hacheki kabisa siku hiyo, alimsogelea Kelvina litekua anatetemema kwa uoga, kumbukumbu za picha za uchi za yule mzee, akifanyiwamapenzi kinyume na maumbile zilimjia kichwani.
“Hapana, usinifanyie hivyo mimi ni mpenzi wako, ni shetani tu alinipitia!” Alianza kupiga kelele hukua kiomba msamaha. Salma alimsogelea karibu, akamuinamia usoni, akaanza kumshikashika makalio, akampiga vimakofi viwili kenye makalio kisha akamuambia.
“Nadhani umeona kuwa nipo siriasi, kama wameweza kukuvua nguo basi jua kuwa siku nyingine watakufanyia wanavyotaka ksiha siku ya harusi yako itakua ni zawadi ya Mama, nitahakikisha inaonyeshwa siku ya harusi yako wakati wa kupiga wimbo wa kumtunza Mama. Ulkua hunijui, basi jua kuwa mimi ni mshenzi, hii nyumba nilitoa nusu lakini nachukua yote. Nakupa tu kesho, kwenda kumsainisha Mama yako kesho kutwa nakuja kuchukua hati zangu na wewe uondoke.
Nakumbuka kuwa mimi ni mtu wa kisasi sana, unaweza usine shida Mama yako akikuona ukifi** kakini nadhani utachanganyikiwa siku ukiona Baba yako yuko kwenye miandao, Mama yako akibakwa na wanaume kumi, wadogo zako maisha yakiharibika! Umenipotezea maisha yangu mshenzi wewe lakini mimi ni mnyama. Nina uhakika una akili, nina uhakika unaipenda familia yako, nina uhakika utafanya maamuzi ya maana!” Alimaliza kuongea na kuondoka, aliwaambia vijana wake kumuachaia wote wakaondoka.
Kelvin ni kama alikua amelala na kuota ndoto ya kutisha, alikua anaogopa sana kwani alihsi anabakwa. Hakusubiri mpaka hiyo kesho ifike, alichukua zile karatasi alizopewa, akaenda kuvaa nguo zake na kuanza safari ya kwenda Morogoro. Kwa muonekano wa Salma alikua hatanii, alienda usiku ule mpaka nyumbani kwao, alifika asubuhi na kukuta wazazi wake wamelala. Aligonga, mama yake alishangaa kumuona pale wakati mchana wake alimuambia kuwa kakosa ruhusa.
Alikua kachoka sana alitaka kulala kwanza, alilala mpaka saa nane mchana ndipo aliamka. Alijua namna ya kufoji sahihi ya Mama yake lakini alijitaji mpaka dole gumba la Mama yake. Kichwa kilikua kinamuuma, aliwaza ni namna gani ataongea na mama yake na kumuambia kilichokua kimetokea.
“Kuna kitu nimefanya, yaani nahisi kuchanganyikiwa kwakua sio mimi. Yaani sijui nikuambieje Mama ila naona kama mimi nimkosaji, wakati nataka kuingia kwenye ndoatakatiofu inabiddi kwanza nitubu Mama.”
Alianza kumuambia Mama yake, walikua wamekaa wawili tu sebuleni, wengine waliklua wametoka.
“Kitu gani mwanangu, hembu niambie?” Mama yake alimuuliza.
“Unakumbuka kipindi kile nimekuambia kuwa kuna kiwanja nimenunua nataka kujenga, nikaja na kukusainisha mpaka hati na kukuambia nimekununulia wewe kama zawadi?” Alimuuliza.
“Ndiyo, na si uliniambia kuwa umeshaanza kujenga ndiyo nyumba unaishi?” Mama yake alimuuliza.
“Hapana, sikujenga, ile nyumba ninayoishi nimepangisha, nilikuambia vile kwakua nilitegemea kuwa mpaka naoa nitakua nimemaliza. Lakini Mama nyumba si tatizo, nitajenga, pesa ninayo, kinachoniume ni dhambi niliyoifanta….” Alimuambia,a likua akiongea kwa kutetemeka, anaongea maneno mawili analia, mawili analia.
Mama yake alimuonea huruma, alimsogelea na kumkumbatia.
“Mimi ni Mama yako, unaweza kuniambia kitu chochote, hata kama umefanya nini mwanangu mimi ni Mama yako, tutaongea, tutaomba, tutafunga hakuna ambalo limshindalo Mungu. Mwanangu umesahau imeandikwa kwua Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Sasa kwanini unakua na hofu mwanangu, niambie, kuna tatizo gani?
Maneno ya Mama yake ambaye alikua ni mtu wa dini yalizidi kumuumiza. Mama yake alikua anatumia Kitabu cha Mungu kumfariji wakati yeye alikua akijiandaa kumdanganya.
“Mama, kile kiwanja wakati nakinunua kilikua na Mgogoro, mimi mwanzo sikujua kama ni mkubwa kiasi hicho, kilikua kiwanja cha urithi, aliyeniuzia alikua ni Mama, kumbe alikua si mke wa marehemu bali alikua ni mcheuko tu. Kuja kugundua baadaye nikakuta kuwa, kiwanja hakikua chake, kilikua ni mali ya watoto wa marehemu, tena si Baba yao ambaye alinunua, hapana, alinunua Marehemu Mama yao, baad aya Mama yao kufariki basi ndipo Baba akapata mwanamke mwingine akamrubuni na kumpa kila kitu.
Nimekuja kujua hilo juzi, imeniuma sana na nafsi yangu imeshindwa kuvumilia. Mama mimi ni Mkristo, umenilea katika imani, naenda kuingia wkenye ndoa takatifu, Mungu akinibariki Waototo sitataka wakangu kudhumuliwa, Mungu kanibariki pesa nina uwezo wa kununua kingine. Nitakununulia kiwanja kingine Mamaila sitabeba hiyo laana….” Alishindwa kumalizia akaanza kulia, hakulizwa kwa uchungu wa stori yake bali alikua akilia kwasababu ya kumdanganya Mama yake.
Mama yake limkumbatia kwa nguvu na kumuambia.
“Nashukuru Mungu kwa kunipa mtoto kama wewe, nashukuru sana, Mwanangu nilifurahi uliponinunulia kiwanja kama zawadi lakini sasa hivi nimefurahi kwakua una moyop wa namna hiyo, tupihge magoti tu Sali kumshukuru Mungu.” Kelvin hakua na namna alipiga magoti na Mama yake, walisali na kuomba sana. Mama yake alimshukuru Mungu kwa kumpa mtoto wa namna ile, baad aya hapo alimpa zile fomu akasaiini. Wakatoka na kwnda kutafuta wino steshenari,a kawake na dole gumba lake. Hati halisi za kile kiwanja alimpa Mama yake na zilikua Moprogoro.
Mama yake alimkabidhi huku akilia, akimshukuru Mungu, hakukumbuka hata kumuulizia kuhusiana na simu alizopigiwa na mwanamke mwingine. Kelvin naye hakutaka kukaa, jioni ya siku ile aliingia kwenye gari, akarudi Morogoro. Alipofika, usiku uleule alimpigia simu Slma, akamuambia ashakamilisha kila kitu, Salma alienda na kuchukau hati na kila kitu, alimuambia kuwa hataki kumuona nyumbani kwake.
Atazipeleka zile hati kwa mwanasheria wake ili kuhakikiwa ila kesho yake anataka achukue takataka zake kwani hataki kabisa kumuona. Hakutaka kuombwa msamaha na wala hakutaka kuongea chochote, alichukua nyaraka zake, akachukua mkataba akapeleka kwa mwanasheria na kuanza kufuarilia kubailisha jina la hati ya ile nyumba.
****
Siku iliyofuata Kelvin alihangaika sana kutafuta nyumba, aliipata na kuhamia, la,kini hakurudi tena kazini, aliomba ruhusa na kuondoka kabisa kurudi Morogoro. Hakutaka kuendelea kuishi Dar, alikua anaogopa sana kuwa labda Salma na watu wake wenaweza kumfanyia kitu kibaya. Alienda na kufunga ndoa na mwanamke mwingine kwasababu tu ya mali, siku ya harusi yake alikua na wasiwasi sana, nalikua anahisi labda kitu kibaya kitaotokea, mpaka harusi inamalizika alishukuru Mungu kuwa imeisha salama
Kwa upande wa Anna alikua haamini kama Kelvina tamuoa mwanamke mwingine zaidi yake, hakutaka kuamini kuwa Kelvin aataoa mpaka alipoona picha za harusi katika mitandao ya kijamii. Aliumia sana na kwa kipindi hicho alikua katika wakati mgumu sana kwnai picha zilisambaa, kila mtu alikua anamuonea huruma. Marafiki zake ambao walidhani kuwa yupo kwenye mahusiano yenye furaha walimcheka, walijiofanya kumuonea huruma lakini mwisho waliishia kumcheka tena wengine waziwazi.
Hai hiyo ilimuumiza sana, alishindwa kufanya kazi mpaka akalazimika kuchukua likizo. Lakini hali ilikua mbaya zaidi kwani hakua na mtu wa kuongea naye, George ambaye alikua ni rafiki yake, mtu wa kumuambia kila kitu walikua hawaongei, tangu alipomuona akifanya mapenzi na mwanaume mwingine alikua amejiweka pembeni kabisa nayeye, alikua hataki hata kumuona, mara nyingi kazini walikua wanapishana tu hata salamu kulikua hamna.
Ingaw ahata yeye aliumia lakini alijua kuwa, hawezi kumlazimisha kumpenda, angalau mwanzo alikua bado hajamuambia kama anampenda au la, hata klama alikua anamuona anaenda na kukubali manyanyaso ya Kelvin lakini angalau alikua hajui kama anampenda, aliumia kuwa alimuambia anampenda lakini bado akaenda kulala na mwanaume mwingine.
Likizo hiyo alishindwa kukaa mjini, akaenda kukaa kijiji kwa Mama yake. Alikaa mpaka likizo ilipoisha, pamoja na maumivu aliyokua nayo lakini ilikua ni lazima kurudi kazini kwani alikua akitegemewa na ndugu zake. Lakini wakati anaondoka Mama yake alimuuliza swalia ambalo lilimchanganya.
“Umeshamuambia kaama una mimba yake?”
“Mimba! Mimba gani?” Anna aliuliza kwa mshanagao, hakuwa akujua kuwa ana ujauzito, lakini Mama yake alimuangalia na kumuambia kuwa ana mimba.
“Kwani wewe siku zako umeziona lini?” Alimuuliza, Anna hakua na jibu, alikaa kwa muda hivi akifikiria ndipo aligundua kuwa ana zaidi ya miezi miwili hajaona siku zake.
“Nina zaidi ya miezi miwili, lakini mimi nilihisi kuwa ni kwasababu ya mawazo, sidhani kama nina mimba…”
Alimjibu Mama yake kwa wasiwasi, Mama yake alimuambia kuwa ana mimba hivyo kama hajajua basi ajue na amuambie mwanaume wake kuwa ana mimba yake. Wakati huo ndiyo alikua anaingia kwenye gari, kichwa kilikua kinamuuma, alihihisi kuchanganyikiwa, alijihisi kama chizi, akifikiria kuwa ana mimba hakuamini. Safari nzima mpaka kufika alikua analia tu,a biria wenzake walimuuliza sababu lakini hakutaka kuongelea mambop yake, basia lipofika alikua kachoka,a liingia bafuni na kuoga.
Alipanda kitandani bila hata kula kitu chochote lakini kutokana na kcuhoka alipata usingizi. Asubuhi alimka mpema na kitu cha kwanza ilikua ni kwenda kupima kama ni mjamzito au la. Alienda kupima na majibu nikuwa alikua na ujauzito wa wiki sita. Hakuamini, alienda kupima tena na tena na tena, majibu yalikua ni yaleyale. Shida ilikua ni kumjua Baba, katika kipindi alichoambiwa alikua ametembea na wanaume wawili, wote katika kipindi kimoja, alitamani sana mtoto kuwa ni wa Kelvin lakini kila akifikiria kuwa alikua kaoa, kamuacha kama takataka aliona ni kama kumtesa mtoto wake.
Chaguo pekee lilikua ni George, ingawa walikua hawaongei lakini hakujua sababu. Yeye alikua anahisiu kuwa George alimkasirikia kwakua baad aya kufanya mapenzi alimkimbia ofisini, alihisi kuwa George alinuna kwajaili hiyo. Hakujua kama alimfuatilia na kumkuta akifanya mapenzi na Kelvin, George naye hakumuambia, aliamua kujieka tu mbali, alijisikia vibaya lakini hakumuambia. Kwasbabau hioyoa lijua kuwa, kwa jinsi alivyokua anampenda basi ni lazima akimuambia kuwa ana mimba yake atakubali.
Aliwaza kuhusu kutoa mimba lakini akili iligoma, wakati akiwa chuo kuna rafiki yake mmoja alitoa mimba, kwa bahari mbaya alifariki na hicho kitu kilimfanya kaupa kuwa, hata kama hatakua na mwanaume kamwe hawezi kuthubutu kutoa mimba. Lakini yeye ni mtu wa dini, hivyo hakutaka kuzaa bila mwanaume na mtu pekee ambaye alikua kabakia alikua ni George, ingawa hakua na uhakika na hilo lakini hakua na namna, mtoto wake ilikua ni lazima kupata Baba na hakukua na mtu mwingine zaidi yaGeorge.
Hakutaka hata kumpigia simu, alimtumia meseji tu “Njoo nyumbani, kuna kitu nataka kuongea na wewe.” Ilikua ni meseji ya kwanza kwa George kutumiwa baada ya tangu siku ile, walikua wamenuniana. Alitamani kuipuuzia lakinia kili yame ilisimama, kila kitu kilisimama, alikua kazini, alishind3wa kuendelea kufanya kazi. Picha ya mwanamke wake akifanya mapenzi na mwanaume mwingine haikuondoka kichwani kwake, lakini pia hamu ya kumuona na kujua anaitiwa nini ilizidi.
Aliiangalia simu yake kwa karibu dakika 20 hivi bila kusema chochote, mwisho akaamua kupiga.
“Mimi sina muda, kama vipi niambie kwenye simu.” Alimuambia kwa mkato.
“Si kitu cha kuongea kwenye simu, nataka kuonana na wewe.”
“Hapana, kuonana na wewe nsihamaliza, wewe ulinikimbia, ulionionyesha kuwa….” Slianza kulalamika lakini Anna alimkatisha.
“Bwanaee, nina mawazo yangu kibao, sikuikupigia simu ili unilalamikie na kunipigia kelele, sina muda huo, nina mimba yako, sas akama unataka kujua nnjoo, kama hutaki kujua usije ukanilaumu kwa maamuzi nitakayoyachukua!” Anna aliongea kwa hasia na kukata simu, alimuacha George katika mshangao.
George hakumuelewa, hakuta akuelewa kuhusu mimba, alijua kuwa alifanya mapenzi naye na kufanya mapenzi siku moja tu kunaweza kumpa mwanamke ujauzito, lakini pia alijua kuwa kesho yake alilala na Kelvin.
“Amejuaje ni yangu?” Alijiuliza hilo swali mara nyingi lakini hakupata jibu kabisa, alijihisi kuchanganyikiwa, kichwa kilikua kizito. Kauli yake ya mwisho kuwa usije kunilaumu ilimuumiza kichwa zaidi, alihisi kuwa anaweza kwenda kuitoa ile mimba. Alishakua kwenye mahusiano kwa muda mrefu na hakuwahi kumpa mwanamke ujauzito.
“Hivi kama ni yangu na akaitoa, nitamuambia nini Mungu kama huyu ndiyo mtoto wangu pekee?” Alijiuliza bila kupata majibu, bila hata kujielewa alijikuta yuko nyumbani kwa Anna.
“Una uhakika kama ni yangu, wakati nikiwa na wewe ulikua na Kelvin?” Alimuuliza, Anna alimuangalia kwa mshangaona kumjibu kwa ukali.
“Hivi unaniona mimi malaya sana, unahdani mimi sijielewi nimebeba mimba nisijue mtoto ni wanani? Nimekaa na Kelvin miaka mingapi, sijawahi kubeba mimba yake, au unafikiri nilikua sifanyi mapenzi, unafikiri nilikua sina kizazi, hii mimba ni yako, nin auhakika asilimia mia kwakua nikiwa na Kelvin nilikua najilinda, sikuwahi kufanya naye mapenzi bila kutumia kinga huvyo najua kabisa mimba ni yako kwani wewe pekee ndiyo sikutumia kinga.”
Aliongea sana mpaka George akamuelewa, ingawa alikua na wasiwasi lakini alishindwa kukataa, hakumuuliza kuhusu kufanya mapenzi siku ile, alibaki kimya.
“Hakuna shida, mimi nipo tayari kuhudumia na mtoto akizaliwa tutajua.
“Hakuna cha mtotoa kizaliwa, kama hutaki mimba naimbie nitoe, mimi ni ukubali mimba na unioe, kama hunioi basi niambie kesho nitoe mimba, siwezi kubeba mimba nikiwa sijui kama nitaolewa au la, nataka ndoa kama hutaki niambie nitoe” Anna aliongea kwa hasira, hakua na mpango wa kutoa mimba lakini alishapaniki, alikaa kwenye mahusiano na mwanaume kwa muda mrefu, mwanaume ameoa, kila mtu anamcheka halafu mimba bila ndoa.
“Hata kama si mpendi nitampendea huko huko mbeleni!” Aliwaza hukua kimuangalia George aliyekau kachanganyikiwa hajui ni cha kujibu. Hakua na muda hata wa kuwaza, alilazimishiwa na mwisho akakubali kumuoa. Alikua anampenda sana, ingawa alikua hajajipanga lakini alikua hana namna. Alimuambie abebe mimba atamuoa.
“Basi tutafanya maandalizi, kesho tukatafute pete, nataka univishetufanye sherehe iliw atu wajue na mimi naolewa, kila mtu anajua nimeachwa ananionea huruma, nataka kila mtu ajue kuwa na mimi nilikua na mtu wangu sio kama nimeachwa.”
“Kesho? Mbona harahka hivyo, miomi sijajipanga?” George alilalamika.
“Hujajipanga kivpi? Huna hela ya Pete?”
“Ninayo.”
“Huna mpango wa kunioa?”
“Ninao.”
“Sasa kama una mipango ya kunioa kwanini tusubiri, mimi nakupenda na wew eunanipend,a nina mimba yako, nataka kuolewa mwezi huu. Sijali cha mafundisho wala nini lakini nataka kuolewa, ksho tunaenda kuchagua pete kesho kutwa unanivalisha kisha tunaenda kwetu. Kama hutaki natoa hii mimba na wala tusijuane.”
Aliongea kwa hasira na kumuambia George aondoke kufikiria, aliondoka kwa unyonge, njia nzima alikua anawaza, alikua anampenda sana lakini kulazimishwa kuoa kwake ilikua ngumu kidogo. Ila kila alipowaza kuhusu mtoto, labda atakua wake basi aliamua kukubali. Siku iliyofuata walienda kutafuta pete ya uchumba, walipopata walitangza, akamavalisha pete na ndani ya wiki moja alishajitambulisha.
Anna alifurahi kuvalishwa pete, alipost kila sheemu, ingawa hakumtag lakini alijua ni lazima kelvin ataona, atamuumiza. Hakupost kwakua alikua na furaha bali alikua kama anamkomoa Kelvin. Kweli kama alivyodhani Kelvin aliiona hiyo picha. Alimpigia simu na yeye alikubali, alimpa hongera na kuomba kuonana naye. Mwanzo Anna alikataa, lakini Kelvin alikua kaudhiwa, walipanga kuonana naye, Kelvin akamkaribisha nyumbani kwake.
“Na mke wako?” Anna alimuulzia.
“Mke wangu bado yuko Morogoro, anafanya kazi kule hivyo hajahamia mazima huku, nahitaji kuonana na wewe, kuna mambo mengi hatujaongea, isitoshe wewe ni mchumba wa mtu na mimi ni mume wa mtu, nahitaji kuoana na wewe.” Alimbembeleza na Anna wala hakuchukua muda, alijiandaa na kwenda nyumbani kwa Kelvin. Ilikua imepita tu siku mbili baada ya kuvalishwa pete na mapenzi yake na George yaklikua ni Bam, bam, walikua wanapendana na kupostiana kila mahali.
“Kwahiyo wakati uko na mimi ulikua na huyo mwanaume wako?” Kelvin alimuuliza baada tu ya kufika, tofauti na alivyodhani kuwa wanaenda kuongea alimkuta Kelvina nakunywa pombe na ana hasira.
“Ulikua unanisaliti, si ndiyo, unanichanganya na mwanaume mwingine. Halafu si nilishakuuliza kuhusu huyo mwanaume wako, ukanaimbia ni rafiki tu, na mimi nilivyomjinga nikakuamini!?” Alizidi kuongea kwa hasira, akimshutumu kuwa alimsaliri, kuwa haiwezekani mwanaume akamlalisha pete muda mfupi tu baada ya kuachana lazima kuna kitu.
“Unanislaiti mimi? Unanisaliti Mimi, sasa kwa taarufa yako nitakuonyesha, nitahakikisha kuwa hata mkioana ndoa yenu haina amani.”
“Nisamehe, naomba usinipige, niasmehe naumwa.” Anna aliongea hukua kipiga magoti.” Kelvin baada ya kunyang’anywa nyumba alienda kupangisha nyumba nzima kwaajili yake na mkewe. Ile nyumba haikau na wapangaji, alikua peke yake hivyo allijua kuwa hata akipiga kelele hakuna mtu atakayemsikia.
“Hata sikupigi, najua ushazoea kupigwa hivyo haitasaidia.”
Aliongea huku akimfuata na kumkamata, alimshika kwa nguvu na kumvua nguo zote, alimbnia chini na kumlazimisha kufanya mapenzi. Kelvin alikua najua kuwa Anna ni mtu wa dini, kwamba moja ya vitu ambavyo hawezi kuvifanya ni kufanya mapenzi kinyume na maumbile, aliamua kumkomesha, alimbania chini na kumuingilia kinyume na maumbile. Alifanya hivyo makusudi kumuumiza. Alikua akifanya kwa nguvu, anafanya hukua kimtukana, alikua anafanya huku anampiga, Anna alijaribu kupiga kelele lakini hasikuzikika, hakuna mtu ambaye alikuja, alizidiwa nguvu na mwisho akaamua kumuacha aendelee kufanya mwenyewe.
Tuone sasa kama huyo mwanaume wakoa takuoa, wewe ndiyo wakunisaliti mimi, yaani mimi nilikua nakupenda, nakupa kila kitu lakini unanisaliti. Halafu unanidanganya unanipenda. Mpakanga na yule malaya mwenzako kunifanyia unyama, mimi ni mtoto wa mjini, najua kila kitu, nitakukomia na nitahakikisha kuwa huolewi na mwanaume yoyote yule, nitakuonyesha kuwa mimi ni nani!”
Aliongea kwa hasira, wakati wote huo alikua anafanya mapenzi huku Anna kamuacha tu, alikua kama kapigwa na ganzi, mwili kama umepooza anamuacha kufanya kila anachotaka. Hali hiyo pia ilimkera Kelvin, kuona hakuna kupigana, hakuna kuvitavuta alihisi kama vile Anna alishazoea huo mchezo na haumii chochote.
“Wewe ni malaya, nilijua nakukomoa kumbe wapi, sasa ngoja nimpigie simu huyo mwanaume wako, tena nampigia simu video caa aone kabisa kua tunafanya nini ili tuone kama hiyo ndoa ityakuepo!” Aliongea huku akichukua simu ya Anna, akatafuta namba ya mchumba wake, akaingia Whatsapp na kuanza kumpigia Video call, huku akifanya mapenzi na Anna”
ANNA; MKE WANGU NAOMBA UNISAMEHE KWAKUKUOA—SEHEMU YA SABA
Anna alikua kama kaishiwa nguvu, alimuacha Kelvin kufanya anachotaka. Lakini wakati ameshika simu anahangika kutafuta namba na kupiga Video Call alipata nguvu kidogo, alinyanyuka kwa nguvu na kumsukuma. Kwakua alikua kavua suruali ipo magotini alikosa balansi na kudondoka chini. Kabla ya kufanya chochote, Anna aliokota ile simu ambayo ilidondoka pembeni na kuichukua, aliokota nguo zake na kabla Kelvin kunyanyuka alifanikiwa kuzichukua na kutoka akikimbia.
Bado alikua uchi na katika maumivu makali lakini hakua na namna. Alikimbia mpaka nnje, akaanza kuvaa nguo zaake, hakuchukua hata viatu, alitoka na kupanda bodaboda mpaka kwake ndipo alipochukua pesa na kumlipa dereva. Aliingia ndnai na kuanza kulia upya, alisikia maumivu makali sana katika sehemu za haja kubwa, alilia san asiku hiyo huku akimlaumu Mungu ni kwanini aliruhusu yoite hayo.
Aliingia bafuni kuoga na kujifanya kama vile hakuna kitu kilichotokea, alirudi ndani na kulala. Kesho yake aliamka asubuhi mapema, hakuenda kazini, alikua hajisikii vizuri, kila kitu kilikua kama kimeharibika. Kwa kitendo alichofanyiwa alijua kabisa kuwa Kelvin hampendi na hana mpango naye.
“Sasa kwanini ananitafuta? Inamaana alitaka tu kunikomoa, ana mke lakini kwanini ananitafuta? Aliwaza asna lakini hakupata majibu ya hilo swali, George alimpigia lakini hakutaka kuongea naye, alijifanya kukasirika huku akimimbia kuwa kama hamuoi basi anatoa ile mimba.
Kwa upande wa George ni kwali alipanga kumuoa, lakini baada ya kuwaambia ndugu zake kuhusu kumuoa huyo mwanamke walikataa. Walimuambia kuw ahawamfahamu, hawaijui familia yake hivyo kama anataka kumuoa basi wajauane na hawawezi kufanya harusi ya harakaharaka namna hiyo. Ni kitu ambcho hakukiwaza, hata yeye ingaw3 alikua anampenda sana Anna lakini alikua hana uhakika wa kumuoa.
Bado alikua haamini kuwa mtoto ni wake na alikua hayuko tayari kuoa mwanamke ambaye ana mimba ya mwanaume mwingine.
“Sio kama wamekataa nisikuoe, lakini wanahitaji muda, ndoa si kitu cha siku moja?” George alimuambia Anna baad aya kuoanana.
“Kwani mimi naolewa na wewe au ndugu zako?” Anna alimuuliza kwa hasira tena wka dharau, alikua na mambo mengi kichwani, alikaua nahisi kuchanganyikiwa. Pamoja na kujiona kama yuko sawa, kujaribu kuishi maisha yake, kujiambia kuwa hakubakwa bali yalikua ni mapenzi lakini kitendo cha kuingiliwa kinyume na maumbile na kuolewa na mwanaume ambaye alikua anampenda kilimuumiza sana.
“Ni mimi lakini ndoa si ya mtu mmoja, ndoa ni ya familia pia mimi nataka ujifungue kwanza, mtoito akikua ndiyo tufunge ndoa…”
“Nyanyuka!” Walikua wamekaa wanaongea, Anna alinyanyuka na kufungua mlango, kisha akarudi na kumshika George akimuambia kuwa ananyuke.
“Nini mbona kama ugomvi?” George aliuliza, hakutana kunyanyuka lakini Anna alimnyanyua kwa nguvu. Akamvuta mpaka mlangoni kisha akamukuma nnje.
“Kwanza sitaki hata unioe, nahitaji mwanaume na mtu ambaye hawezi kufanya maamuzi yake, kama kunioa unaambuliwa na Mama yako hivi tukiiingia kwenye ndoa si ndiyo Mama yako atafanya kila kitu. Sikutaki, ondoka, waambie ndugu zako nimekukataa, nibora kubaki mwenyewe kuliko kuwa na mwanaume ambaye hata hajielewi. Hapana, ondoka! Ondoka!”
Aalimsukumiza na kufunga mlango, ingawa George alimsihi sana kumfungulia mlango lakini hakua tayari kwa hilo. Alikataa katakata kumfungulia na kumuambia kuwa hamhitaji katika maisha yake. Mwisho George aliondoka, ilikua ni jioni, Anna alikua hata hajala kitu, bado alikua na maumivu ya jana yake ya kuingiliwa kinyume na maumbile, alikua na upweke wa ajabu, kila wakati akiwaza kuhusu maisha yake.
Aliingia kwenye ukurasa wa Instagaram wa Kelvin, alikua kamblock lakini alikua akitumia akaunti feki kumuangalia. Mwanzo Kelvin alikua si mtu wa mitandao ya kijamii, alikua hapost picha na wala hataki kupostiwa, lakini baada ya kuoa alibadilika. Kila wakati kumpost mke wake, kumtakia maisha mema, kumuambia kuwa anampenda na vitu kibao. Ilikua ni mpaka kero, kila mtu anasifia kuwa wanapendana, yaani kila kitu kilikua sawa, aliwaonea wivu,a lijikuta analia.
Alipanda kitandani, alakini hakulala, siku iliyofuata hakwenda tena kazini, alibaki nyumbani. George alimtafuta lakini alikua hapokei simu zake wala kujibu meseji zake. Siku nyingine hivyo hivyo, alibaki nyumbani bila taarifa, hali hiyo ilimchanganya sana George, kila alipojaribu kumpigia simu alikua hapokei na meseji hajibu. Alienda kwaake na kujaribu kugonga lakini hakumfungulia mlango, hakutaka kusikia chochote kutoka kwa mtuu yoyote. Alikua na mawazo mengi kuhusu Kelvin na vitu alivyomfanyia, pamoja na yote hayo lakini bado alikua tayari kumsamehe na kuendelea naye.
Hakutaka kuwa na mwanaume mwingine, alibaki kimya, alibaki ndani tu akidhani labda Kelvin atampigia simu hata kumuomba msamaha. Lakini hakufanya hivyo, aliendelea kubaki nyumbani, kuona hivyo George alihisi kumpoteza, alijua kama asipokua makini atampoteza mwanamke amabye alikua anampenda na alikua na mimba yake. Ingawa hakua na uhakika sana lakinia liamini inaweza kuwa yake kweli.
“Nadhani ni yangu, amekaa kwenye mahusiano kwa muda gani? Mbona hakubeba mimba ya yule mwanaume, mimi nimefanya naye mapenzi mara moja tu ana mimba, hii ni yangu.”
Aliwaza, hakutaka kumpoteza, baada ya kuona kuwa hajibu meseji zake aliamua kwenda nyumbani kwao. Alitafuta wazee wawili na kuongozana nao, alifioka na Barua ya poesa kabisa. Kila mtu alishanagaa, ndugu zake walikua wanamfahamu Kelvin lakini walishangaa kuona mwanaume mwingine anakuja kulete Barua ya posa. Dada yake alikua akifahamu kilichokua kikiendelea, alikua akijua kuwa Anna na George ni marafiki lakini hakua akijua kuwa ni wapenzi, lakini alikua akijua pia kuwa Mdogo wake ameachwa na Kelvin kaenda kuoa mwanamke mwingine. Walimpokea lakini kabla ya kuikubali Barua ya posa walimpigia simu yeye kwanza.
Dada yake alipompigia simu kumuambia kuhusu Posa alipata nafuu kidogo. Hakua akitaka kuolewa, lakini alitaka kulipa kisasi.
“Yeye si anajifanya kuoa sasa na mimi naolewa, ataumia tu!” Alijiambia, hakua anampenda George lakini alikua ni mjamzito na hakutaka Kelvin kumuona mpweke, alikubali, wakaanza mchakato wa harusi. Mwanzo alitaka harusi ndogo, lakini baada ya kuona kuwa, kitendo cha yeye kuwa na mwanaume mwingine kinamuumiza sana Kelvin aliamua kufanya harusi kubwa.
Hakutaka ajifungue kwanza lakini watu walichangishwa na akiwa na ujauzito wa miezi Nane alifunga ndoa na George. Kwa George alishaamua kusamehe kila kitu, aliondoa mawazo juu ya yeye kuwa baba wa mtoto, aliapa kutokuulizia hicho kitu kabisa na kusema kuwa, hata kama mtoto hatafanana na yeye basi hatahangaika kuulizia kuhusu Baba na atamlea mtoto kama wake. Alikua anampenda na alitaka kuwa na ndoa ya amani, kweke ilikua ni kama ndoto kuwa na Anna.
Kwa upande wa Anna hali ilikua tofauti kabsia, aliingia kwneye ndoa na kulazimishia harusi kubwa akiamini kuwa labda hicho kitu kitamuuma Kelvin hali haikua hivyo. Kila siku Kelvin alikua anampost mke wake, yaani ni kama alikua anafanya makusudi, mke wake alishahamia Dar na walikua wanaishi pamoja. Kila wakati akipost picha mpya yuko na mke wake Anna alikua anakasirika,a najisikia vibaya na kuona kama andiyoa ansalitiwa upya.
“Lakini hawana mtoto, mimi nitamzalia Kelvin ndiyo atajua kuwa kapoteza nini, lazima aumie kuwa mtoto wake analelewa na mwanaume mwingine.” Aliwaza, alikua ni mjamzito, alikua kaolewa na kuna uwezekano mimba ilikua ni ya mume wake lakini hakutaka hivyo. Alitaka kuzaa mtoto aliyeanana na X wake ili tu kumkomoa. Alikua anaomba sana mimba iwe ni ya X wake, alihitaji sana mtoto na Kelvin. Lakini hali ilikua tofauti, alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume.
Kwa kumuona mtoto haikua na haja ya kuuliza Baba alikua ni nani? Yaani tangu mtoto akiwa mchanga, sura ndiyo inatokezea, alitoka kopi ya Mume wake. Kw3a George ilikua ni furaha sana, kila mtu akija kumuona mtoto na kumuambia kuwa mwanae kafanana naye basi alihisi kuchanganyikiwa, alipata furaha ya ajabu. Kwake kila kitu kilikua kizuri, kwake aliona kama vile maisha yamekamilika, alisahau kila kitu, alizidisha upendo kwa mke wake, alimpenda na kumpa kila kitu.
****
“Hivi wewe una akili kweli? Una akili nakuuliza?” Anna alimpigia simu mume wak4e, ilikua ni mcchana, wakati huo mtoto alikua na miezi miwili kama na nusu hivi, abdo alikua anaendelea na likizo ya uzazi. Alikua hajarudi kazini, aliingalia kwenye status ya mume wake na kuona kuwa kamuweka mtoto wake, hakuishia hapo, aliingia kwneye Instagram ya mume wake pia, akakuta kuwa ameweka picha ya mtoto wake.
“Kivipi sikuelewi, mbona unanipigia simu na kunitukana, mimi ni mume wako niheshimu?” George ambaye hakujua kosa lakae aliuliza, alipandisha sauti kidogo, alikua na mshanagao kwani wakati anaondoka ausbuhi walikua sawa kabisa.
“Mume kitu gani, hata mbuzi anaweza kuwa na mume! Kama ni mwanaume lakini umjinga kwanini usitukane! Hivi ni kwanini unamtangaza mtoto wangu, yaani unana raha gani kupost picha za mwanangu, mtoto bado mdogo unampost, unataka nini!?”
Anna alikua anaongea kwa hasira, mumewe alishangaa kwani kilikua ni kitu kidogo sana, ilikua ni picha tu kapost na kama angekua hapendi angemuambia kisaarabu.
“Kuna kingine, mbona unanitukana namna hiyo, si suala tu la kuniambia kuwa mume wangu ondoa picha za mtoto kwenye mitandao mimi sipendi. Lakini huyo ni mwanangu, ni damu yangu na mimi nina uhuru naye, naweza kuamua kumposta u kutouamua.” Mume wake aliongea kwa upoel, tangu kuingia kwenye ndoa mke wake alikua na kisirani cha namna hiyo, kila siku walikua wanagombana na yeye kujishusha akiamini kuwa ni kwasabbau ya mimba akijifungua hali itakua tofauti.
Tangu kufunga ndoa walikua hawajawhai kufanya mapenzi, kwa kifupi aliwahi kufanyaa mapenzi na mke wake mara moja tu, kipindi kile mwanzoni, ile ya bahti mbaya, kipindi bado hawajaoana. Lakini baad atu ya kuingia kwenye ndoa, kila akitaka kumgus abasi mke wake anakasirika, anamuambia kuwa hayuko tayari na mimba yake haimtaki. Kama mwanaume alikua anaumia lakini ili asimuudhi mke wake alivumilia. Baada ya kujifungua alijua kuwa anatakiwa kuimpa muda, lakinia litegemea kuwa kisirani kitamuishia, matusi yatapungua lakini haikua hivyo.
“Mke wangu unatakiw akuniheshimu, mimi ni mume wako, acha kunikosea heshima, nilikuvumilia kwasababu ya mimba lakini na mimi nachoka, nimechoka kila siku kutukanwa. Yaani nimekua sina amani kabisa, kila siku nikirudi nimenuniwa, hembu naimbie kosa langu ni lipi, yaani nyumbani wkangu naishia kuongea na binti tu wa kazi wakati nina mke” George aliongea kwa sauti ya chini, ni kama alikua anambembeleza mke wake na kumtaka kubadilika.
“Ohoooooh kwahiyo umenichoka, unaniona mimi nina kisirani, si umenichoka, unaona kuw aqbinti wa kazi ni wamuhimu. Basi muoe, si unaona kabisa kuwa mimi nina matatizo naiche na matatizo yangu….” Anna alimbadilishia kibao mume wake, alianza kulalamika akisema kuwa mume wake anamjali binti wa kazi.
“Nakuona unavyomuangalia, si unampend yeye, basi mpende, mimi si sina thamani, basi kila kitu utakua unaongea naye!” Aliongea kwa hasira na kukata simu, mume wake hakujua sababu lakini kila alipojaribu kumpigia simua likua hapokei, alipiga sana mwisho mwanaume alimblock. George aliona kuwa hakuan shida, aliamua kufuta zile picha ili kumridhisha mke wake. Jioni kama kawai alairudi nyumbani, lakini alikuta mke wake hataki kuongea na yeye, amenuna, hamesemeshi, hata karibu kulikua hamna.
George alijua ni kisirani cha muda cha kawaida cha mke wake na mambo yakitulia basi kitaisha, lakini mwezi ulipita mke wahe hataki kuongea naye walikua wanalala kitanda kimoja lakini walikua hawaongei, kila mtu akimka anajiandaa kivake, wanaingia kwenye gari, wanaenda mpaka kazini hakuna kuonge. Mwanamke akihitaji matumizi anamuambia binti wa kazi, yaani kila kitu kilikua ni binti wa kazi. Mara muulize baba anataka kula nini? Muambie mboga hakuna, yaani ikaw h ivyo, kama akijaribu kumuongelesha na kumuuliza tatizo ni ni basi ataambulia matusi.
“Inamaana hujui tatizo ni nini? Kuwa mwanaume basi, yaani hujiongezi kuwa wewe ndiyo tatizo!” Alipenda kumuambia, hali hiyo ilimuumiza sana George lakini alishindw akufanya chochote. Hakutaka kuongea mambo yake kwa ndugu wala marafiki, alikua anaqona aibu kuwa ndoa yao ilikua inakaribia mwaka lakinia likua hajawahi kufanya mapenzi na mke wake. Mtoto alipofikisha Mwana, Mama yake mdogo na Anna alikuja, alikua amekuja Muhimbili hivyo wakawa wanakaa pamoja, hapo ndipo alianza kuongea na mke wake, mpaka Mama mdogo anaondoka walikau vizuri, waliongea vizuri.
Siku moja tu baada ya kuondoka, George alitaka kufanya mapenzi na mke wake, alikua na hamu sana, alishachoka kumalziia haja zake bafuni hivyo kwakau mke wake alikua kwenye mood nzuri alitaka kufanya mapenzi nayeye.
“Unaonaje kama leo tukijaribu, si unajua tuna muda sana hatujafanya kitu.” Walikua kitandani, alimgeukia mke wake na kumshika kiunoni, Anna naye alikua na hamu muda mrefu alikua hajafanya tendo la ndoa, hakumjibu kitu lakini alimruhusu, walianza kushikana, lakini wakati George ashasisimke, anataka kufanya mapenzi na mke wake Anna alimsukumua pembeni.
“Unanuka jasho, mi mi hamu imeniishia!” Alimuambia, lakini George hakumsikiliza, kichwa kilikua kishapoteza akili, akili pekee iliyokua imebaki ilikua ni ya tendo la ndoa. Aliendelea kufanya lakini akawa kama analazimishia, Anna alilala tu bila kujishuhulisha kwa chochote, alilala kama gogo. Mwisho George alishindwa kuendelea na tendo la ndoa na kuacha, walilala wamenuniana. Kwakua amani ilishaanza kurudi George hakutaka kuipoteza, alijua ugumu wake hivyo kesho yake aliamka akiwa swa kabisa, alimchangamkia mke wake na kumuomba msamaha kwa kila kitu kilichotokea jana yake.
Mkewe alimuambia sawa, alikubali kana kwamba niyeye kakosewa. Walifika kazini na kila mtu akaenda sehemu yake. Lakini kule kushikwa kwake usiku kulimchanganya sana Anna, alianza kuwa na hamu sana ya kufanya mapenzi, alijisikia vibaya jinsi alivyomfanyia mume wake jana yake, aliamua kubaidlika na kujisemea kuwa siku hiyo atafanya mapenzi vizuri na mume wake. Kweli usiku huo alibadikika kabisa, wakawa wanafanya mapenzi na mume wake na alifurahi. Mambo yaliendelea vizuri, walikua wana amani lakini kuna kitu kilikua hakiko sawa, wakati akifanya mapenzi na mume wake kuna raha ambayo alikua haipati kabisa.
Alijihisi kama vile anajilazimisha, akawa anafanya kumridhisha, baada ya muda alijikuta anaingia kwenye mahusiano na Kaka mmoja amabye walikua wanafanya kazi shemeu moja. Huyo Kaka alikua ni mume wa mtu na walianza mahusiano yao kama utani lakini baada ya muda alijikuta anampenda na kufurahia kufanya tendo la ndoa na huyo Kaka kuliko hata mume wake.
Alikua anampenda sana huyo Kaka lakini tatizo lilikua ni moja tu, huyo Kaka pamoja na kuwa na msahara mkubwa kuliko yeye kwani yeye bado alikua na mkopo. Alikua hajamaliza deni la mkopo aliochukua kujenga kipindi akiwa na Kelvi, huyo Kaka alikua anapenda pesa sana, alikua anapenda mtelezo, kuhongwa na alikua hamhudumii kwa chochote. Yeye ndiyo alikua analipa mpaka pesa ya Gest. Pamoja na yote hayo lakini alimpenda na alikua na amani sana wakati akiwa naye.
Hali hii ilimfanya kubadilika ziadi, alikua na furaha sana tofauti na mwanzo lakini hakua vizuri na mume wake, muda mwingi walikua ni watu wa kugombana na mume wake alihisi kuwa labda anachepuka. Ingawa yeye alikataa lakini alihisi kuwa anachepuka. Siku moja akiwa na huyo Kaka aliona mesjei ya mwanamke mwingine, hakua mke wake, basi Anna alikasiika kuwa yule Kaka alikua anamsaliti, alichukua ile namba ya kumpigia yule mwanamkea kimtukana na kumuambia aachane na mwanaume wake.
Akamtumia meseji nyingi sana za matusi, lakini hakujua kuwa yule mwanamke aliyekua akimtukana alikua anamjua, anajua kuwa akolewa, hivyo alivyoanza kutukana na kumpa vitisho basi yule Dada mwingine alienda polisi. Alionyesha meseji za matusi, vitisho kuwa atamfanyia kitu kibaya na vitu vingine vingi, aliwapa na voice note. Jioni wakati wanaktoak kazini, yupo kwenye gari na mume wake, walisimamishwa na askari, Anna alichukuliwa mpaka kituo cha polisi huku mume wake akimfuara kwa nyuma.
Kwa wanaohitaji vitabu vyangu nina Vitabu vitatu, cha Mahusiano na namna ya kujipa furaha, cha tatizo la nguvu za kiume na maumbile madogo, namna ya kuishi na hiyo changamoto au kuishi na mtu mwenye hiyo changamoto na kitabu cha Biashara 50, namna ya kuanzisha na kuendesha Biashara.
ANNA; MKE WANGU NAOMBA UNISAMEHE KWAKUKUOA—SEHEMU YA NANE
Alifikishwa Polisi akitetemeka, George laikua anamfuatilia nyuma, walipofika walikutana na mwanamke ambaye wotew alikua wanagahamiana. Alikua ni dada ambaye alikua anawaletea chakula pale ofisini. Alipomuona G4eorge tu alichanganyikiwa, hakujua kama George atakua pale kwani ni moja kati ya watu aliokua akiheshimiana nao sana. George alikua ni kama Kaka yake, si kwa undugu bali kwa mazoea, alianza kuleta chakula katika ofisi yao kama mhudumu tu wa kawaida.
Lakini ilifikia kipindi Bosi wao alikua na mikopo mingi, hivyo akashindwa kuleta chakula. Akawa hana kazi, siku moja akiwa hana hata shilingu 10 alimfuata George na kumuomba mtaji wa elifu kumi ili awe ananunua Boxer na kuzizungusha. Alimfuata George kwania likua ni mtu rahisi kuzoeleka, mara nyingi alikua anamheshimu, wakati anakusa alikua akimuachia hcenji mara nyingi. Pia kuna kipindi mwanae alikua anaumwa basi George alimsiadia kumtibu mpaka akapona.
Basi alipomfuata na kumuomba mtaji, George limuuliza ni kwanini auze Boxer wakati alikua anapika chakula kizuri na bado wateja wapo. Ndipo alimuambia kuwa Bosi wao kafilisika yeye na wasichana wengine wamelazimika kuacha kazi.
“Lakini nyie mna kila kitu, mna nguvu, si mnajua kupika?” George alimuuliza.
“Ndiyo tunajua.”
“Sasa kwanini msipike, mkapikia nyumbani kama kawaida na mkaleta chakula nyie kama nyie, watafute wenzako, njooni, mimi nitawapa mtaji wa kuanzia, kununulia vifaa. Mishaanza mtanirudishia taratibu.” Kweli aliwanunulia vifaa vyote vyakupikia, akawapa na kianzio. Aliwasimamia mpaka walipokusanya pesa ya kumlipa, aliwapa kama laki atu. Walipompelekea ile pesa akawaambia kuwa wafungue akaunti yao ya pamoja, wasajili kikundi na wawe wanafanya kazi kikampuni atawasimamia.
Aliwasimamia mpaka wakasimama na kupata tenda maeneo mengine, yule dada akwa Bosi hivyo akawa haji haji tena pale ofisini lakini alikua anatuma wasichana wake. Alikua anafahamu George, alikua anajua kuwa ameoa lakini alikua hamjui mke wake, pia alikua anamfahamu Anna, na wakati anamchokoza alijua kabisa kuwa ni mke wa mtu lakinia likua hafahamu mwanaume aliyemuoa. Alisikia tu kaachika kwa mwanaume wake na kisha kaolewa na mwanaume mwingine.
Walisalimiana na George, mwanzo hakujuaa kama George kaja pale kwasababu ya mke wake, alijua kuwa kaja kumsindikiza kama mfanyakazi na rafiki yake kwani alikua anajua ni marafiki tangu kitambo.
“Huyu ndiyo kafungua kesi, umemtukana na kumtishia maisha kwasababu anatembea na Mwanaume wako….” Aliambiwa wakati huo Anna alijihisi kuchanganyikiwa, mume wake alikua pembeni lakini alikau anashitakiwa kwa kumgombania mwanaume mwingine.
George alikua mpole, ingawa alikasikirika baad aya kusikia kitu alichokamatiwa mke wake lakini hakutaka kupaniki, alijua mke wake kamkosea lakini alijua kuwa, mwanaume ukimfumania mke wako hutakiwi kupiga kelele sana, unatakiwa kutulia kwani kuongea sana ni kujidhalilisha.
“Samahani naweza kuongea na huyu Dada pembeni, huyu aliyefungua kesi.” Aliongea na askari amabye alikua anamsimamia mke wake kuvua viatu na kukabidhi vitu kabla ya kuingizwa Mahabusu.
“Hakuna shida, ongea naye, yeye ndiyo mlalamikaji, ongea naye tu.” Askari alimruhusu, kwa muonekano wake George alikua kapenda juu, ana muonekano mzuri, Handsome, hivyo alipoongea tu yule Askari wa kike ni kama alichanganyikiwa, alijikuta anamruhusu huku akimuangalia kwa tabasamu, alikua anamkodolea macho kama mchaga kaona pesa.
“Naomba ufute hii kesi, haya mambo ni ya kudhalilishana tu, hutapata chochote kumdhalilisha.” Aliongea kwa sauti ya kubembeleza, ingawa angeweza kumuamrisha na kumuambia nataka ufute hii kesi lakini hakutaka, alikua mnyenyekevu kama kawaida yake na alitaka yule dada kuona kuwa anaheshimiwa na si kama analazimishwa.
“Broo nakuheshimu sana lakini huyu Dada ni malaya sana, ni mara nyingi naona vitu vyake. Najua ni rafiki yako lakini huyu si mwanaume wangu wa kwaqnza ananinyang’anya, nilikua namuangalia tu namsubiria ajichanganye. Kuna mkaka mwingine alikua ananipenda lakini huyu dada kamchanganya na pesa zake, yaani amemhonga mpaka kaniacha, sasa nataka nimkomeshe, mwanaume mwenyewe si wake, ni mume wa mtu, sasa mimi kwanini anitukane, mwenye mume yupo katulia, hana ngebe lakini yeye ana kiherehere. Nakuheshimu Kaka lakini nataka nimtie aibu, hata alale mahabusu siku moja atashika adabu.”
George alikua kasimama, nguvu zilimuishia akashindwa kuendelea kusimama, kwani alijua kuwa mbali na kugombania mume wa mtu lakini alikua na mwanaume mwingine tena anmhonga. Hili lilikua ni jipya kwake, alijitahidi kutembea mpaka kwneye benchi kisha akakaa. Alikaa kama dakika mbili hivi, akapata nguvu na kusimama tena, alimsogelea yule Dada nakumuambia. Najua kakuudhi lakini siwezi kumuacha alale ndani, tuna mtoto mdogo, siwezi….” Alianza kuomba tena, hapo ndipo yule Dada alijua kuwa kumbe alikua ni mke wkae.
“Inmaana Kaka huyu Malaya ni….” Yule Dada aliongea lakini hakuweza kumalizia, hasira zilimpanda, kusikia mke wake anaitwa Malaya George alimrushia kofi lakini kwa bahati nzuri halikumpata kwani mwenyewe alikua anapepesukapepesuka, anasikia kizunguzungu kidogo kudondoka.
“Unataka kumpiga mtu katika kituo cha polisi, yaani unafanya vurugu kituo cha polisi. Mkamateni huyo mpeleke ndani, ajue kuwa hakuna kupiga mwanamke.” Askari mmoja mwanamke ambaye alikua pembeni aliona kile kitendo, alikua ni msaiodizi wa kituo cha polisi, aliwaamrisha askari wengine ambao walimfuata George na kumkamata.
“Hapana, sio hivyo Dada, hajanipiga, huyu ni Kaka yangu, ni Kaka yangu kabisa, mimi ndiyo nina makosa, naomba mnisamehe.” Yule Dada alipoona kuwa George anakamatwa kwa kuaka kumpiga alianza kumtetea.
“Hapana , nimeona, alikua anakupioga, atalala ndnai, haya si maamuzi yako ni yangu. kuna wanawake wengi kama wewe wanateswa na wanaume lakini wanaishia kuwatetea sasa ili ajifunze lazima kulala ndani!” Yule Mama alionekana kuwa na hasira zake, pamoja na kuombwa msamaha, George kumsihi sana kumuomba kuwa ilikua ni hasira lakini alikataa, George aliambiwa kuvua viatu, mkanda,a kaandikisha vitu vyake na kuingizwa ndani.
Wakati anaingia alimuangalia yule Dada na kumuambia anaomba afurte hiyo kesi ili mke wake aende kuangalia watoto kwani nyumba ina binti wa kazi ambaye ni kama mtoto tu na mtoto wao mdogo. Yule dada hakua na namna, inagwa alikua na hasira sana lakini alifuta ile kesi na Anna aliachiwa. Alichukua gari ya mume wake na kurudi nyumbani, alikua na hasira sana, alijihisi kudhalilishwa kwa kushitakiwa, njia nzima alikuaa najiongelesha akiapa kulipia kisasi, hakuwaza kuhusu mume wake alijiwazia yeye tu.
****
“Mama mimi nataka kuondoka si mtaki huyu mwanaume, nimechoka vituko vyake. Yaani sasa hivi yuko mahabusu, yeye na ahwara yake wlaipanga njama ili kuniweka ndani, wanisingizie kesi ili nifungwe waniharibie maisha. Lakini Mungu alivyomkubwa wamefika huko wameanza kupigana yeye ndiyo yuko ndani, mimi nimesema kuwa siendi kumuona, sifanyi chochote, sihangaiki kabisa na huyu mwanaume. Nina maisha yangu, sitaki, sitaki Mama, nimevumilai mengi, mtoto wenue ypo mahabusu hivyo muamue wenyewe kama mtaenda kumtoa au la?”
Kuwekwa ndani kwa mume wake kulimpa nafasi ya kuamua cha kuongea, alijua watu watajua tu lakini hakutaka yeye kuonekana malaya, basi alichofanya baada ya kufika nyumbani ni kumpigia simu kila mtu aliyekua akimjua na kumuambia kuwa anataka kuachana na mume wake kwakua alikua anataka kumsingizia kesi ya matusi yeye na hawara wake. Alianza kw akumpigia Mama mkwe wake, akalalamika na kusema kuwa anaondoka, akafuatia kumpigia Mama yake kisha ndugu na wafanyakazi wengine.
Ni kama alikua amekasiorika kweli kwani siku iliyoafuata wakati ndugu wanaenda kumuangalia Mume wake yeye alienda kazini kama kawaida na huko kazini alitangaza kuwa mume wake kamsaliti na muuza chakula na wlaitaka kumsingizia kesi. Kila mtu alishanmgaa kwani George alikua hana tabia hizo, watu wengi walikua wanamheshimu.
“Watu wakimya achana nayo, hivi wewe unaweza kufikiri kuwa mume wangu anaweza kuchepuka. Kila siku kwenye ndoa mimi ndiyo naonekana kama ndioyo mbaya lakini leo yememkuta.” Alilalamika wakati anamuelezea rafiki yake mmoja kuhusiana na mume wake.
“Sema kwa mume wako mimi nilijua tu lazima yuko naye, hivi si unakumbuka kuwa huyu Dada alikua ni mfanyakazi tu,a nazungusha chakula, kakini mume wako ndiyo alimpa mtaji, tena nakumbuka kipindi kile ndiyo mmefunga ndoa tu akampa huyu mwanamke mtaji. Kamfungulia Biashara na nasikia sasa hivi ni bosi,a na mgahawa mkubwa, anasambaza maofisi kibao.” Rafiki yake aliongea, yaani ni kama alikua anmamfahamu, yeye kuuza chakula kwneye ofisi nyingine kwao walichukulia kama ana lihoteli.
Walijazana ujinga mpaka basi, kila mtua likua anamuonea huruma Anna akimuambia kuwa wanaume wapole ndiyo walivyo. Anna hakudfanya chochote, hakufuatilia kuhusu kutoka kwa mume wake, hata ndugu zake mwenyewe walipompiigia simu kumuuliza aligoma kuongea chochote akidai kuwa anchotaka ni talaka na kuendelea na maisha yake.
Kwa upende wa yule dada yeye alijisikia vibaya, alikau akimheshimu sana George hivyo kwanza aliona aibu kuwa anajihusisha na mume wa mtu. Alikua anatabia zake mbaya tu na alikuahajali waume za watu, lakini kitendo cha kuonekana na mtu aliyekua anamheshimu kilimuumiza. Asubuhi na mapema alienda pale kituoni, hakulala siku hiyo, aliacha kazi zake na kwenda kujaribu kuomba ili atoke kwnia lijiona kama yeye ndiyo alisababisha. Akiwa kule alikutana na Mama yek mdogo na George ambaye naye alienda kumuangalia na kuangalai kuhusu dhambana.
Waliambiwa tu kuwa hana kesi wanasubiri bosi wao aliyesema awekwe ndani aje watamruhusu. Basi walikaa pale mpaka wkenye saa tano hivi ndiyo alitoka, alienda moja kwa moja mpaka nyumbani. Yule dada alimuomba msamaha, akamuambia kuwa kafuta kesi na hatahangaika tena na mke wake kisha akaondoka. Mamja yake mdogoa limrudisha George nyumbani.
“Umuombe msamaha mke wako, kitu ulichomfanyia si kitu kizuri, haikubaliki kabisa, mimi ni mwanamke, nimeolelwa hivyo nina uchungu.” Mama yake mdogoa limuambia, George alikubali kuwa atamuomba msamaha.
Hakujua Mama yake anamaanisha nini, bado alikua hajajua maneno ambayo mke wake aliku akiyasambaza lakini hakutaka kumuambia chochote. Alimauchaa baki na alichokua akikiamini, hakutaka kumtangaza mke wake kama malaya kwani angeadhirika yeye. Mama yake mdogo aliondoka, George alikua kachoka sana hivyo moja kwa moja alioga, akala chakula cha mchasha akaingia chumbani kulala. Mke wake aliprudi alikua bado kalala, hakumuamsha, aliendelea na mambo yake mpaka alipoamka mwenyewe.
“Umerudi saa ngapi?” Alimuuliza mke wake ambaye alikua Akaka sebuleni anachezea simu yake.
“Nimaswali gani sasa hayo unaniuliza, kwani hujui kazini huwa natoka saa ngapi?” Alimjibu kwa hasira, hakutaka hata kumgeukia wala kumsalimia mume wake, ghafla ile kumuona mume wake basi alianza kununa. Alikunja uso kana kwamba yeye ndiyo alikuakafumaniwa. George hakutaka shari, alienda kukaa pembeni yake, walikaa kimya kama dakika 15 hivi ndipo George aliendelea tena.
“Najua kuna makosa umefanya, lakini inabidi tuongee…” Alianza hukua kimshika mke wake mabegeni ili amuangalie, baada ya yeye kukaa pele karibu yake mke wake aliangalia pembeni kabisa, akiwa bize na simu na simu yake, kusikia hivyo alimgeukia mume wake kwa hasira.
“Sikiliza Baba, mimi sina cha kuongea, umesikia ulichosikia, ukiamini ni kweli sawa, hukuamini mimi sijali. Kama unataka kuomwba msamaha Baba sina muda huo, kama unataka kuniacha basi niache, mimi sina shida, wewe si pumzi kama ukiniacha nitakufa!” Aliongea kwa hasira hukua kinyanyuka na kuondoka, aliingia chumbani, hata mume wake alipomuita ili waongee hakujali, alimuambia yeye ni mwanaunaume afanye anachotaka.
***
Hali ya mule ndani ilikua mbaya mambo ya kununa ndiyo yakazidi, kupitia stori za mtaani Anna alijua kuwa, siku mume wake anatoka Polisi yule dada naye alikuepo. Kwakua lishatangaza kuwa walipanga njama kumsingizia kesi basi aliendeleza kuwa wakati yeye mke wake yipo kazini hawara alikua anamtoa mume Polisi. Ingawa alijua kuwa ni uongo lakini ilimuuma sana, kutokana na tabia zake mbaye kuna wakati alijisikia vibaya kufanya mambo yake, alikua anataka sbabau ya maana ya kumnunia mume wake lakini mara nyingi alikua haipati hivyo kununa bila sababu.
Lakini baada ya lile tukio alikua hana namna, alianza kulazimishia kuwa mume wake anachepuka na huyo mwanamke ndiyo maana alifuta kesi.
“Unajifanya umenisaidia kumbe uluikua unakimbia kuumbuka?” Ilikua ni usiku wa manane, ilishapita miezi miwili tyangu lile tukio kutokea. Anna alikua kamnunia mume wake, mwanzo mume wake alikua anabembeleza sana lakini baada ya muda aliacha kabisa, akawa anaingia na kutoka, akihitaji kitu anamuambia Dada wa kazi. Mume wake alimsikia lakini alijifanya kunyamaza, hakutaka maneno na mke wake, alishasikia maneno kuwa yeye dniyo alifumaniwa, alishasikia fitina zote za mke wake lakini hakuongea kitu chochote.
“Unajufanya mpole, oohhh sijui futa kesi, sijui watoto kumbe hakuna kitu. Nimemtukana mwanamke wako mnapanga mnipeleke polisi, Baba najua kila kitu. Ulimfungulia Biashara, ukampa mtaji, umemtafutia maofisi mengine, unafikiri mimi sijui, unaniona mjinga eti mnataka kusema mmenifumania…..” Aliendelea kuongea mpaka mume wake hasira zikampanda, kaamka na kukaa.
“Hivi unaongea nini wewe mwanamke, hivi una akili kweli, kwahiyo mimi nitembee na kile kitoto kweli? Umefanya umalaya wako huko, umefanya mambo yako huko, mmetukanana nimejaribu kukusaidia lakini huna shukurani? Unaraka nikufanyie nini wewe mwanamke, unagombana na watu wako huko, mimi nahusikaje?”
“Unahusikaje? Wewe ndiyo kila kitu Baba, hivi unafikiri kwanini nilimtukana, unafikiri kwanini niligombana. Kwa akili yako ilivyofinyu unafikiri nimemtukana kwasababu ya mchepuko, aisee, mimi nigombanie mwanaume mwingine tena mnaambiana mume wa mtu, nigombanie mume wa mtu wakati mimi nina mume wangu. Zile mesjei nilimtukana kwakua nilisikia anatembea na wewe mpaka ukamfungulia Biashara na sasa hivi unamjenge. Hivi unafikiri mimi ni mwanamke wa namna gani, kila siku unasema huna pesa, familai nahudumia mwenyewe kumbe unenda kuhonga, unamjengea mwanamke mpaka nyumba!”
Anna alimgeuzia kibao mume wake, alikubali kwua kweli alimtukana yule Dada lakini si kwakua anachepuka bali kwakua aligundua kuwa huyo dada anatembea na mume wake.
“Muogope Mungu mke wangu, hivi ni lini uloomba kitu ukakosa, unafanya kazi kweli lakini ni lini nilikuambia ununue hata chumvi. Wewe umeme ukiisha nanunua mimi, maji, chakula kila kitu, hivi kweli unasema kuwa sihudumii familia?” Mke wake aliona aibu na kunyamaza kidogo lakini mwisho aliendela.
“Simtaki yule dada, sitaki awe analeta chakula kazini!” Anna aliongea.
“Unamaanisha nini, kama humtaki si ndiyo unaacha kununua chakula chake kwani umelazimishwa, mimi siwezi kumuondoa kwani si mimi niliyemuweka.”
“Unaweza ukitaka unaweza, wewe ndiyo ulimuambia aje, ukampa mtaji basi ndiyo utamuondoa, sijui uamuondoaje lakini kama zikipita siku mbili hajaondoka naondoka mimi, ndoa sitaki tena.” George alikua kachoka kumsikiliza, bila kuongea chochote alijifunika na kulala zake. Walilala mpaka subuhi, kazini hawakusemeshana. George alijua kuwa ni utani, hakuhangaika hata kusema wafanyakazi wa yule Dada waije pele, lakini baada ya siku mbili alirudi nyumbani na kukuta mke wake kaondoka na mtoto.
Kabla hajakaa sawa alipigiwa simu na Mama yake mdogo, alimuambia kuwwa kuna kikao. Alienda kwa Mama yake mdogo ambapo hapakua mbali sana, alipodfika alimkuta mke wake, amekaa anaonekana kama alikua analia. Alikaribishwa na kutakiwa kuongea, hakikua kikao kikubwa bali alikua ni Mama yake mdogo na mume wake pamoja na mkewe.
“Mke wako kashatuambia upande wako, sasa kila mtu aseme chakwake hapa ili tuyamalize haya mambo. Mama ongea, tuambie ulichotuambia, ongea mbele ya mume wako na mume wako naye ataongea.
Anana aliongea uongo wake, alimuambi Mama mdogo kuwa mume wake anamsaliti na huyo mwanamke na walipanga kumsingizia kesi na kumfunga ili waoane. Kwa George ulikua ni kama mshangao, alikua anamjua huyo mwanamke lakini hakuwahi kuwa na mahusiano naye.
“Kweli nilimtukana, lakini nilimtukana kwakua nimesikia anatembea na mume wangu. Niliamua kumuuliza tu kistaarabu lakini hakunijibu vizuri, akanitukana, Mume anaume Mama mimi nikamjibu basi ndiyo wakapanga na mume wangu eti nionekane kama nilikua namtukana kwasababu ya mume wa mtu.”
Alikua anaongea huku analia, alidanganya bila kupepsa macho. Kwa upende wa George hakusema mabaya ya mke wake alikubali tu kumsidia huyo mwanamke lakini akasema kuwa hajawahi kutembea naye.
“Nilishawahi kumsaidia, kama rafiki, lakini hajawahi kuwa mwanamke wangu.” Alisema, kibao klilishamgeukia, mke wake alianza kulalamika yeye hivyo watu walikua wanamuamini yeye zaidi.
“Rafiki ndiyo umfungulie Biashara, kwanini kila akifanya kitu anakuambia, na nina meseji zenu, au unafikiri mimi ni mjinga. Eti mnajifanya kuitana kaka wakati mnakulana, hapana!”
Aliongea huku akitoa simu yake, alikua anajua kuwa mume wake anamsidia yule mwanamke kama rafiki, alikua anajua wana mawasiliano hivyo baada ya kuanza kutengneza uongo wake alichukua simu ya mume wake. Akaingia kwenye meseji akaona meseji walizokua wanatumiana. Kwakua alimsaidia na alikua anamsimamia basi mara nyingi yule Dada alikua anamtumia meseji, anamtumia picha za chakula, anamuomba ushauri, akaziscreenshot na mumuonyesha Mam mdogo.
“Kama haamini anaona mimi ni muongo muambie afungue simu yake. Nina uhyakika hajafuta hizo meseji, muambie akuonyeshe!” George hakua na kitu cha kuficha, alitoa simu yake na kumpa Mama yake mdogo, zile meseji zilikuepo. Alijaribu kujielezea lakini mke wake alijifanya kukasirika, akauambia kuwa ampe muda, anaondoka. Walijaribu kumsihi lakini hakukubali, aliondoka na kumuambia kuwa anamuacha mume wake.
Mama mdogo alimsihi sana, kwanza alishangaa kwani wkaati anakuja alijua ni ugomvi mdogo tu wa kusuluhisha, lakini ghafla Anna akawa anataka kuondoka, anadai talaka na kusema kuwa hataki kuendelea kuishi na mume wake.
“Basi kama ni hivyo ngoja mimi niondoke, wewe ni mwanamke, siwezi kukuacha uzurure na mtoto sehemu nyingine. Mimi nitaonmdoka na kukuachia nyumba.” George alimuambia mke wake, alakini Anna hakutaka.
“Huo ujinga ni nani afanye, nyumba ni yako, mimi sitaki, nahitaji uhuru wangu. Naondoka na kama shida ni mtoto basi mchukue, huyu ni mwanao, utamtafutia Mama miwngine si una mwanamke tayari, mchukue mpelekee. Si hutaki nizurure na mwanao, mchukue mimi simtaki!”
“Lakini nakuachia nyumba mke wangu?” George alibembeleza, aliomba msamaha sana lakini mke wake alikataa, alimuambia anaondoka na mtoto haondoki naye. Aliondoka kweli, hakuwaambia kuwa anaenda wapi lakini alimuacha mtoto na kuondoka.
***
“Uliniambia utamuacha mke wako uje tuishi na wewe, sasa mbona kial siku unaenda kwake, mimi nimemuacha mume wangu, nimeacha na nina mimba yako lakini bado upo na mke wako, nataka umuache mke wako, kama humuachi mimi nampigia simu kumuambia kuwa tuko wawili!” Ilikua ni usiku, Anna na Hamisi walikua wamekaa wanakula chakula cha kusiku. Glasi ya maziwa ilikua mkononi, walikua wamekaa huku wanaangaliana.
Hamisi alimuangalia Anna kwa hasira, uso wake ulibadilika, alichukua ile Glasi ya maziwa na kuirusha, ilimpiga Anna kichwani katikati ya utoso. Anna aipiga kelele z amaumivu, ilimpasukia na damu kuanza kutoka.
“Wewe kum* unataka kunipanda kichwani, mazoea zoea na mke wangu sitaki. Kama umezoea kumchezea huyo mbuzi wako sio mimi! Umpigie mke wangu, tena nikijua hata una namba ya mke wangu kwenye simu yako nakuua! Nipe hiyo simu! Nipe hiyo simu malaya mkubwa wewe! Mbwa kabisa! Nhipe hiyo simu!” Hamisi aliongea kwa hasira hukua kinyanyuka, hakujali kelele za maumivu za Anna.
Alifuata simu yake na kuifungua, aliangalia majina kuona kama kuna jina la mke wake hakuona.
“Una bahati ningekuua kabisa mbwa wewe! Unajua mke wangu nimetoka naye wapi? umekuja tu na vichupi chupi vyako hapa unataka kuniharibia ndoa yangu! yaani umuambie mko wawili, wawili na nani? Wewe si malaya tu nimekcuhukua, uandhani una hadhi ya kuwa mke wangu, yaaani nikuoe wewe, mtu mwenyewe umekimbia mume mimi nije nikuoe, halafu ngoja…”
Alishtuka, badala ya kuangalia majina aliandika namba ya mke wake kwenye simu ya Anna na kupipiga, alishangaa kuonanamba ya mke wake imeseviwa jina la dada wa Anna. Alihakikisha mara mbili na kukuta kweli ni namba ya mke wake lakini imeandikwa jina la Anna.
“Nilijua tu, yaani nimekutomb* miezi miezi mitatu tu unataka kuniharibia ndoa yangu, aisee hunijui!” Alichukua simu ya Anna na kuipiga chini, aliivunja na kuikanjagia, alichukua ana simu nyingine na kuifanya hivyo hivyo,. Akatoa laini na kuzitafuyunatafuna mbele yake.
“Sitaki uwe na simu, mimi ni mwanaume wako, nikitaka kuwasiliana na wew enitakuja nyumbani! Sitaki uongee na mtu na kama ni mambo ya ofisini ni ya ofisini, sitaki mtu akupigie simu, sitaki utoke.
Kama nikutoka hata kama usikie Mama yako karfa ni lazima nikuruhusu mimi. Wewe ni malaya, nikikupa uhuru utakuja kuniacha, sitaki chochote, nimemuambia sitaki! Kama ukiwa na tabia nzuri basi nitakununulia simu, lakini kwa tabia hizi hapana. Kama hutaki kukubaliana na mashariti yangu absi ondoka, siwezi kukupangishia nyumba halafu ukafanya unavyotaka, au kwakua una kielimu vbidigrii viwili ndiyo unajifanya kuwa una akili ziadi yangu. mimi nina akili kuloko wewe na wewe ni mwanamke tu, huwezi kunipanda kichwani.
NB; Wanawake wengi wanaonyenyaswa wanafikia hatua wanakua mateja, wanajichukia na kutokutambua thamani yao. Hata ukiwapend avipi hawauoni upendo huo kwakua wao wenyewe wanajichukia. Dada jifunze kujipenda mwenyewe kabla ya kuwa teja wa manyanyaso.
ANNA; MKE WANGU NAOMBA UNISAMEHE KWAKUKUOA—SEHEMU YA TISA
(ILIPOISHIA SEHEMU YA NANE; Anna anapona kuingia ndani, anatoka huku akimgeuzia mume wake kibao kuwa yeye ndiyo alikua anachepuka. Anajifanya kutokutaka kuendelea na ndoa kwamadai kuwa kaumizwa. Anamuacha mtoto na kuondoka, anaonekana kukutana na mwanaume mwingine hamisi, ambaye alimdanganya kuwa atamucha mke wake, lakini anaanza kwa kumpiga baada ya kutaka kumpigia simu mke wa hamisi. Je hamisi ni nani? Walikutana wapi na nini nitaendelea…. ENDELEA….)
“Shika namba yangu, kama mtu yoyote akikusumbua nitafute mimi. Hizi ni kesi za kijinga sana na kwa uzoefu wangu inawezekana hata mume wako anatembea na huyo mwanamke, chunguza sana, mimi ni askari, najua haya mambo yanatokea.” Hamisi alimuambia Anna, ilikua ndiyo marayao ya kwanza kukutana, ilikua ni kituoni, siku ambayo Anna alikua amekamatwa. Baada ya yule Dada kumuombea msamaha na kukubali kufuta kesi aliondoka na gari ya mume wake, lakini kabla hajatoka kituoni kabisa Hamisi alimsimamisha.
Kwanza alidhani labda anaaka kurudishwa tena lakinia lipewa kikaratasi ambacho kina namba ya Hamisi. Hamisi alikua ni askari tu wa kawaida, hakua na cheo chochote lakini alikua na muonekano wa kibabe flani.
“Nashukuru Kaka.” Anna alipokea huku akitetemeka, alikua ameponea chupuchupu kuingia mahabusi na alikua kwelia anogopa.
“Hakikisha aunanipigia, nipigie ukifika nyumbani ili nihakikishe kama uko salama, polisi wana kawaida ya kumkamata mtu baada ya kumuachia, hakikisha unanipigia.” Hamisia lisisiriza, Anna aliondoka lakinia lipogika nyumbani kitu cha kwanza kilikua ni kumpigia Hamisi, waliogea kidogo lakini baada ya hapo, Hamisi alikua na namba yake na kila mara alikua anampigia simu kumjulia hali.
Alikua akimuulizia kuhusu ndoa yake, kujua anaendeleaje na kila kitu. Alikua kama rafiki kwake, alikua ni mtu wake wa kuppootezea muda na baada ya muda alikua hawezi kulala bila kuongea naye. Katika kipindi chte wanaongea Hamisi hakuwahi kumtongoza, kumuambia kuwa anampenda zaidi ya kumjali na kumsikiliza. Hata hakutaka kuonana naye, kila wakati Anna alipotaka kumuona allitafuta sababu ya kuwa bize, alikua kama vile anamkwepa.
Hali hiyo ilimuumzia sana, hali ya kuonyesha kana kwamba hatakiwi, yaani mwahaume kutokua anamtaka, kutokumnyenyekea ilimchanganya sana, alianza kumkumbuka Kelvin, namna ilivyokua ngumuo kuonana naye, namna ambavyo alikua hajali, namna ambabvyo alikua akijilazimishia kwake. Siku moja alishidnwa kuvumilia,a limpigia Hamisi simu kumuomba aje nyumbani kwake.
“Kuna matatizo, naomba uje, nahitaji kuongea na wewe na siwezi kutoka hapa.” Ilikua ni mchana, siku ya kazi, mume wake alikua kazini lakini yeye siku hiyo aliyondoka mapema, hakuaga wala kuomba ruhus, hata hakumuambia mume wake kuwa anatoka. Aliondoka akitaka kuonana na Hamisi, alikua na hamu sana ya kumuona, lakini alijua kama watapanga kuonana kwa kutoka out basi atamzungusha na hatakuja.
Alishafanya hivyo mara nyingi, aliamua kusingizia kuwa ana matatizo ilia je nyumbani kwake.
“Ni nini?” Hamisi alimuuliza, alishtuka kidogo kwani hiyo aliongea kama vile anaumwa, kama amepigwa, kama ana matatizo kibao.
“Njoo,s iwezi kukuambia kwenye simu, naomba uje nyumbani haraka, njoo haraka.” Alimuambia.
“Mume wako kakupiga, niambie, nije na RB kabisa.”
“Njoo utaona mwenyewe… nhoo….” Alikata siku bila kumuambia sabbau na alipopigiwa simu hakupokea. Binti wa kazia likua jikoni na mtoto, lakini hakujali alitamani kumuona Hamisi, hakupanga kufanya chochote zaidi ya kumuona tu.
Kweli Hamisi alikuja, alifika mpaka getini na kugonga mlango, alimfungulia na kumuambia aingie. Alishangaa kumuona yuko vizuri lakini yeye hakujali, alimuambia aingie. Alipofika ndani tu alishindwa kujizuia, alimrukia na kumkumbatia kisha akaanza kulalamika.
“Mbona hutaki kuniona, mbona hunitaki, au hujui kuwa nakupenda.” Alimuambia.
“Nimekuambia kuwa mimi nina mke, ninakuheshimu sana, hatuwezi kwua wapenzi.” Aliongea lakini wakati huo nguo zilikua zishavuliwa, bado walikua sebuleni,a likumbatiwa, midomo ya Anna ilikua ikizungukazunguka kwenye mwili wake.
Hamisi hakua tayari kufanya hivy, palepale alimsuikuma na kumzaba kofi.
“Wewe dada vipi, jiheshimu!” Alimsukuma pembeni na kutaka kutoka, lakini ASnna hakumruhusu, ni kama alikua kachanganyikiwa, alipiga magoti na kumshika miguu huku akimvuta kuwa asiondoke. Kimuonekano mume wake alikua na muonekano mzuri kuliko Hamisi, alikua na pesa, anajali na kila kitu ambacho mwanamke angehitaki kwa mwanaume alikau ancho. Lakini hakua na kitu kimoja ambacho kilkua kinamchanganya. Mume wake alikaua najali sana, akikose yeye mume anaomba msamaha, akimtukana hampigi, mwanaume alikua anajali sana, alikua kachanganyiiwa juu yake, alikua akibembelezwa kama mtoto lakini yeye alikua hataki hicho kitu, alikua ashazoea mapenzi ya purukuishani.
Alimvutavuta mwisho Hamisi ualendo ulimshinda, alikubali yaishe, wakaingia chumbani, wakawa wameshikana shikana, tayari hamisi alishasisimkwa na alikua tayari kufanya mapenzi walivua nguo na kupanda kitandani, wakati huo uume wake ulikua umesimama, lakinii ile anapanda kitandani tu, anataka kuingia basi akajikuta anakojoa, anafika kileleni na kumkojolea mapajani, hata hakuingia ndani. Baad aya hapo uume ulilala kabisa, Anna alijitahidi sana kumshtua lakini hakuna kitu, alimshika na kumshika lakini hakukua na kitu.
“Sijisikii vizuri, umenilazimishia ndiyo maana sijisikii vizuri, sikujiandaa, siku nyingine tutafanya vizuri, usijali.” Hamisia lijiteteea kwa aibu, mwanamke mzuri alikaua melala mbeel yake uchi kitandani, lakini uume wake ulimuangusha, mpira uliisha hata kabla hajaingia uwanjani.
“Nisamehe, najuua ni uoga kwakua umekuja kwangu, mimi nadhani tupange siku tuonane, nahitaji kuwa nawe karibu, tunahitaji muda mrefu wa maandalizi.” Alimuambia, huku akivaa nguo zake kwa aibu Hamisi alikubaliana nayeye, alimuambia kuwa atajipnanga wakatu mwingine na atafanya vizuri zaidi, alivaa nguo zake na kuondoka, aliondoka kabla mume wake hajaja.
****
Hamisi alipenda kuonega lakini hakupenda vitendo, muda mrefu alikwepa kumuona kwakua alijua kuwa ana matatizo, alikau mzuri sana mdomoni, alikua anachepuka kwa mdomo, anachat naye, anamuomba picha za maungo yake na maneno mengine matamu, alimpagawisha Anna hata kabla ya kuonana, akamuambia vitu vingi ambavyo alikua anapenda na kuweza kuvifanya lakini hakufanya hata kimoja, siku walipokutana alikua ni tofauto kabisa.
Baada ya ile siku Anna alikua na hamu sana ya kumuona, alikua anampigia simu kila wakati, wanapanga kuonana lakini anamzuga hawanonani. Wakati mmoja alilazimishia, mume wake alikua anaumwa hivyoa lijua hawezi kutoka. Alipanga kuonana na Hamisi mchana kwani Hamisi alishamuambia kuwa ameoa na hawezi kullala nnje ya nyumbani kwake kwani anamheshimu mke wake. Anna alilipia Hoteli jna kila kitu, ingawa alijua kuwa siku hiyo Hamisi anaweza asifike lakini alikua hana namna, alilazimishia.
Walipanga kuonana, kwakua alijua tatizo lake siku hiyo Hamisi alimeza kidogo, alimeza Viagra, alijua itamsaidia, alikua na wasiwasi sana. Walifika na kuanza kuongea, dawa ilianz akufanya kazi mwilini, wakati anashikwa alisisimkwa na alitaka kufanya harakaharaka, lakini Anna alihitaji maandalizi, alihitaji kushikwa shikwa kwanza kwani alikua mkavu sana. Hapo ndipo walishindwa kabisa kuelewana, wakati wmenzeke alikua tayari kufanya, Anna hakua tayari kufanya, alijibana na kulazimishia kuandaliwa kwanza.
“Paaaaaa!” Hamisi alimtandika kofi, ule msuguano wakati wa kutaka kufanya mapenzi ulimchanganya, alishajiandaa na aliona kama anacheleweshwa.
“Wewe mpumbavu sana, yaani umeniita hapa ili tufanye mapenzi halafu uananibania miguu! Mjinga kabisa! Kama hutaki uansema, Malaya mkubwa wewe, mtu nimekutana nawe kwasababu ya umalaya halafu unajifanya hutaki!” Allimuambia kwa hasira huku akiendelea kumpiga, alimpiga sana, baadaye alitaka kufanya mapenzi nayeye, lakini hakufika popote, uume wake ulilala na kubaki mpole.
“Sijui ni nini kimetokea? Nismaehe, nisamehe, ni hasira tu lakini mimi simpigaji, sipigi wanawake, nisamehe, naomba unisamehe, nisamehe!” Baada ya uume wake kulala na kushindwa kufanya tendo la ndoa alianza kuona aibu. Uanaume wote ulimuishia, zile nguvu za kupiga ziliyeyuka, alibaki kamanyong’onye akama kifaranga cha kuku kilichonyeshewa na mvua.
“Usijali mpenzi, mimi ndiyo mwenye makosa, mimi ndiyo nilikukatalia kuingia.” Anna alijifanya kumuelewa, kwa muonekanao wa nnje wa Hamisi alionekana kama mwanaume barubaru, mtu ambaye anaweza kwenda raundi hata kumi lakini akzi yake ilikua ni hafifu sana.
Pamoja na yote hayo lakini bado Anna alimpenda, siku hiyo waliongea tu kidogo kisha kwa aibu Hamisi aliondoka akisingizia kuitwa kazini. Anna aliendelea kumtafuta lakini Hamisi alikua anamkwepa, kwenye simu walikua wanaongea, kutumiana Video za uchi, kupigiana video call yaani mpaka usiku wa manene. Wakati huo Anna alikua haongei na mume wake, alikua kajifanya kumnunia, hivyo mara nyingi alikua chumba cha wageni akiongea au kuchart na Hamisi.
“Hivi wakati unaongea na mimi mke wako anakua wapi?” Siku moja Anna alimuuliza.
“Tumetenaga vyumba, mke wangu na mimi tunagombana kila siku, mke wangu mimi ni malaya, simuamini, nahisi ana wanaume wengi hivyo nimeamua kuishi naye kwasababu ya watot.” Alimuambia, ni kweliw alitengana vyumba, si kwasababu mke wake alikua malaya au kweli hamuamini ila Hamisi alikua akimkwepa mke wake. Tangu mke wake kujifungua mtoto wa pilia likua hana hamu kabisa ya kufanya mapenzi, ingawa mwanzoni alikua na matatizo kidogo lakini mke wake alipojifungua alishindwa kabisa kufanay tendo la ndoa, alikua akifanya kidogoa nashindwa.
Mwanzo aliweza kudili na tatizo lake kwa kumuambia mke wake kuwa hwezi kufanya mpenzi kwakua mtoto ni mdogo lakini hata baada ya mtoto kukua alikua anamkwepa. Kwasbabu hiyo, kila wakati ambapo mke wake alikua anaomba tendo la ndoa alikua anatafuta sbaabu ya kugombana, kukasirika na kumhama kitanda. Mchana walikua wanaongea vizuri, anamjali, anamhudumia kwa kila kitu, anapenda watoto, anamheshimu na kila kitu, lakini iifika usiku, wakipenda kitandandani ikitokea mke wake akamgusa basi atakasirika na kuhama kitanda.
Alikua akimtumia mtoto kama ngao, alilazimishia kulala na mtoto ili mke akiomba mecho basi yeye husema kuwa hawezi kufanya mapenzi mbele ya mtoto. Mke alimhamisha mtoto lakini bado hali ilikua hivyo hivyo. Kufanya tendo la ndoa kwao ilikua ni mara moja moja tu, tena akimeza dawa na wakati mwingine hata akimeza uume wake ulikua bado hausimami hivyo kuishia kugombana na mke wake bila sababu yoyote na kumhama kitanda.
“Natamani ningekua mke wake, hivi mwanauem kama wewe anakusalitije, kweli nimeamini kuwa sisi wanawake ni mashetani!” Anna alimuambia, kwa namana flani alimuamini Hamisi na kuamini kuwa mke wake ndiyo mwenye matatizo.
“Natamani sasa hivi ningekua na wewe, niwe mke wako mimi, nikutunze na nikuonyeshe maana ya mapenzi. Lakini wewe ni mwanaume, hivi kwanini humuachi, mimi ningekua mwanaume huyu mbuzi wangu ningeshamuacha, lakini sina namna, yaani, sijui nikuambie nini, huyu mwanaume nilikubali kuolewa naye kwasababu ya hasira tu, nilikua nimeumia kwa kuiachwa na X wangu, la sivyo nisingemuoa.” Alilalamika.
“Mimi kinachoniweka ni watoto, alkini nikipata mtu wa kunilelea wanangu huyu mwanamke namuacha.” Allimuambia, waliendelea kuongea usiku wote. Wakitumiana video na video call. Ulikua ndiyo kama mchezo wao, Anna alitaka sana kuonana naye lakini yeye alimkwepa. Siku moja Hamisi alimuambia kuwa anataka kuonana naye, ilikua ni usiku, akamuambia anapenda kufanya mapenzi usiku. Anana alikua nyumbania napika chakula cha usiku, Hamisi alimuelekeza sehemua lipokua na kumuambia aende. Hakumalizia hata kupika, alimuambia binti wa kazi amalizie, yeye aliingia ndani na kuvaa nguo kisha akatoka.
Wakati natoka sebuleni alikutana na mume wake anammbeleza mtoto alale.
“Unaenda wapi usiku huu?” mume wake alimuuliza. Anna alimuangalia kwa hasira na dharau kisha akamuambia.
“Naenda kutomb**” unataka kuja, anatuweza wote wawili!” Mume wake hakujibu chochote, aliishia kumziba masikio mtoto, akamuacha akatoka. Alifika na kumkuta Hamisi kashajiandaa kwa ajili yake, walifika na bila kufanya maandalizi yoyote, baada ya kushikana shikana Hamisi aliingia. Safari hii aliweza kuingia lakini hakukaa muda sana, alikaa kama dakika mbili akamaliza.
“Umeridhika?” Alimuuliza hukua kichekacheka kwa aibu.
“Leo umefurahieee.” Alimuuliza tena hata kabla ya kujibiwa, kwa mikwaju ambayo Anna alikau ameizoea hasa kwa mume wake pale alijiona kama vile hajaguswa, alikua kama vile kashikwashikwa na kuachw, hakuhisi cchochote, lakini akikumbuke kipigo cha siku ya kwanza alilaizmika kukubali.
“Nimeridhika, leo nimefurahi sana…” Aliongea kwa kulazimishia sauti iwe na furaha na mshawawasha lakini hakikua hivyo.
“Sasa kama umefurahi mbona sikusikia Gaaa! Gaaaa! Gaaaa!” Alimuuliza.
“Gaaa! Gaaa! Ndiyo nini?” Allijifanya kutokujua.
“Kupige kelele mwanamke akifika kileleni, unajifanya hujui?
“Inamaana wewe hujawhai kufikishwa kileleni hujawahi kusema Gaaa!” Alimuuliza, Anna alimuangalia na kuona kama hasira zake zinataka kupanda.
“Nilishawhai, hata wewe umenifikisha lakini shida nikuwa mimi si mtu wa sauti, nafika kimyakimya.” Alimuambia, hapo hasira kidogo zilipungua.
“Njoo ukae hapa….” Alimuambia, alimvuta upande wake, wakawa wamekaa, wanakumbatiana.
“Najua hujaidhika sana, lakini mimi siko hivi, nadhani nikwakua sijazoea kutembea na mke wa mtu. Mimi nikiwa na mke wangu naenda hara raundi kumi, yaani ni yeye mwenyewe anachoka, sijui nini kimemnitokea kwako, wewe ndiyo mwanamke wangu wa kwanza kuchepuka, ndiyo maana nilikua naogopa kuonana na wewe, ila naamini kuwa ukimuacha mume wako, nikakupangishia chumba tukawa tunaishi pamoja utafurahi.” Alimuambia.
“Kuishi pamoja kivipi? Wewe si una mke, mimi sitaki kuolewa mke wa pili, siwezi kubadilisha dini kuwa muisalamu, hapana, mambo ya wake wawili sitaki!” Anna aliongea huku akimuangalia, kuna kitu kilikua kinamvuta kwa Hamisi ingawa alikua hajui kuwa ni kitu gani.
“Najua nina mke lakini nataka kumuacha mke wangu nataka kuwa na wewe, nataka kuwa huru na wewe, nikiwa na uhuru na wewe bila kuwaza kuwa wewe ni mke wa mtu nina uhakika nitakua nafanya vizuri.” Alimuambia kwa upole, Anna alikataa lakini baada ya kuondoka pelw na kurudi kwa mume wake, alianza kubadilika.
Alizidi kumchukia mume wake, kila akimpigia simu Hamisi kutaka kuonana naye alimuambia kuwa hawezi kwenda kuonana naye kama hajaachana na mume wake. Alikua anamsumbua, akimuambia yupo tayari hata kumlea mtoto wake. Siku moja Hamisi alienda kumuonyesha nyumba, alimuambia kampangishia nyumba ili wawe wanakaa. Baada ya hapo Anna alihisi kuchanganyikiwa, kuna kitu kilikua kama kinamuiwasha, aliamani kuondoka na kwenda kuishi na Hamisi.
Mwisho aliamua kumchukua mtoto wake na kwenda kwenye nyumba ambayo alionyeshwa. Alimpigia simu Hamisi kumuambia, lakinia lipokuja na kumkuta na mtoto alimuambia amrudishe kwanza mtoto mpaka wazoeane.
“Nikiwa namuona mwanao sitafanya mapenzi vizuri, subiri tuzoeane kwanza ndiyo utakuja kumchukua.” Hamisi hakutaka mtoto kwakua alidhamiria kuishi naye, alipokataliwa kuishi na mtoto ndiyo akaenda kwa Mama yeke mdogo na Mume wake na kujifanya hataki ndoa, lengo lilikua ni yeye kumuacha mtoto pale na kweli alimuacha na kwenda kuishi na Hamisi kama mke na mume.
Najua unajiulzia hivi kweli kuna wanawake wa namna hii? Yes wapo wengi tu tena wananisoma, mateso ni kama dawa za kulevia, ukishaanza kutumia ni ngumu kuacha. Yaani hata ukipewa amani kuna wakati unakua teja, yaani Tena wa madawa, ukimpa chakula bila dawa anaweza kutoroka kufuata dawa, ndiyo hivyo hivyo mateso yalivyo.
ANNA; MKE WANGU NAOMBA UNISAMEHE KWAKUKUOA—SEHEMU YA KUMI
Hali ya Anna ilikua inabadilika siku hadi siku, kila siku alikua ni mtu wa kulialia tu. Hamisi alikua anamnyanyasa, anampiga mara kwa mara, kila akipata pesa alikua anamlazimisha kumpa, ingawa alimuambia kuwa atamuacha mke wake lakini hakufanya hivyo, hakua tayai kabisa kumuacha mke wake. Katika kipindi chote hicho George hakuwahi kuwa na mwanamke mwingine, kila siku walikua wanakutana kazini, alijitahidi kuwa karibu naye loakini Anna hakumkubalia, alikua anamkwepa.
“Unatakiwa kurudi nyumbani, pamoja na yote hayo lakini wewe ni mke wangu, ni Mama wa watoto wangu, sipendi kukuona ukiteseka, najua unaishi na mwanaume na najua kuwa anakutesa sana!” George alimuambia, walikua ofisini, ulikua ni muda wa chakula na ofisini kwake Anna hakukua na mtu mwingine, alimfuata muda huo kwakua alitaka kuongea nayeye, alijua kuwa hakuna muda mwingine ambao angeongea naye wakaelewana ziadi ya huo.
“Maisha yangu hayakuhusu, niwe naishi na mwanaume au naishi peke yangu lakini maisha yangu hayakuhusu! Fata mambo yako, wewe ni mwanaume, tafuta mwanamke mwingine, mimi nina furaha na maisha yangu!” Anna alimjibu kwa hasira, hakutaka kuongea naye kabisa.
“Nina furaha na maisha yangu, sikutaki, nina maisha yangu, nina mwanaume wangu, ananipenda na sina mpango wa kurudiana na wewe!” Aliendelea kuongea, George alimsohele,a kisha akatoa simu yake na kumuonyesha.
“Hii ndiyo furtaha unayozungumzia?” Alimuuliza huku akimuonyesha video aliyokua katumiwa.
Ilikua ni video ikimuonyesha Anna akiwa uchi wa mnyama, alikua akicheza kumkatikia mwanaume ambaye hakuonekana, lakini hakufanya hivyo kwa mapenzi, alikua anacheza hukua kipigwa na kulazimishwa kukatika viuno huku akibadilisha staili mbalimbali.
“Hii ndiyo unaita furaha, kwanini uanjidhalilisha hivyo mke wangu, umekosa nini kwangu?” Alimuuliza.
“Umeipata wapi?” Anna alimuuliza hukua kitetemeka kwa uoga, alimuangalia mume wake kwa aibu kwani si kitu ambacho alitegemea kuwa kitamtokea.
Hamisi alikua anampenda sana kumdhalilisha, alikua anamuomba pesa na akikataa anampiga, siku moja alimlazimisha kucheza akiwa uchi kisha akamuambia kuwa akmaa sipomchukulia mkopo kazini kwo basia tazisambaza hizo picha kwa kila mtu ofisini kwao. Anna alikua na mawazo sana alianza mchakato wa kujaza fomu kuchukua mkopo lakini kabla ya kutoka Hamisi aliona kama anacheleweshwa hivyo akamtumia picha na video mume wake huku akimtukana.
“Ishu sio nimeipata wapi, ishu ni kwanini unaendelea kuishi na mtu kama huyu, kwanini bado unajidhalilisha namna hii?” Alimuuliza, Anna hakua na jibu zaidi ya kulia, alimuambia kila kitu kuwa anachotaka huyo mwanaume ni milioni 16 na kamuambia achukue mkopo ilia mpe.
“Hakuna haja ya kuchukua mkopo, hatasambaza picha zako, mimi ni mtu wa mwisho kunitumia hizi picha?” George alimuambia.
“Utafanya nin? Mimi nataka tu nimpe hiyo pes aili tuachane, sitaki kudhalilishwa, kama kakutumia wewe unafikiri anashidnwa kutumai watu wengine!?” Alimuuliza.
“Najua anaweza, lakini naomba uniruhusu nikusaidie, yule mwanaume ni Askari, najua namna ya kudili naye, ninachotaka ni wewe kubadilika, nataka kukusaidia kwakua bado nakupenda na wewe ni Mama wa mtoto wangu, hivyo siwezi kuona unadhalilika nikakuacha, mtoto wetu akikua na kuona hizi picha itamuathiri sana.”
Anna alikua na uoga sana, Hamisi alikua akimtishia mara kwa mara kuwa akimuacha atamfanyia kitu kibaya, ingawa alishachoka kupigwa na kudhalilishwa lakini hakuwa na ujasiri wa kumuacha, alihofia kudhalilishwa. George alimuambia kuwa hatamfanya kitu chochote, anachiotaka ni kujua kuwa kama anahitaji msaada wake au la. Alimuambia anahitaji msaada wake, hapohapo Georga alichukua simu yake na kupiga namba flani.
“Tayari, mnaeweza kuendelea.” Aliongea kisha akarudi ofisini kwake, alimuomba Anna kurudi naye nyumbani lakini hakua tayari, bado alitaka kujua kuwa ni kitu gani kitatoke kwa Hamisi, badoa likua anamuogopa. Alirudi jioni hakumkuta, alimppigia simu lakini simu yake haikupatikana. Alimpigia simu rafiki yake ndipo alimuambia kuwa Hamisi alikua mahabusu, alikua amekamatwa kwa kosa la kupokea rushwa ya shilingi Miliioni mbili.
Jioni hiyo hiyo kuna watu walikuja nyumbani na kukagua kila kitu, waliangalia kama Hamisi kuna vitu aliacha nyumbani, hawkaukuta chochote lakini baadaye George alimpigia simu na kumuambia kuwa, wamefika nyumbani kwake na kukuta flash disc ambayo alikua na picha nyingi za uchi za wanawake pamoja na yeye, wakakuta kwneye laptop ambapo alikua aanamrekodi mpaka mke wake.
“Hiyo kesi itamsumbua sana kwani si kesi ya kutungwa, ni kweli alikua anataka kupokea rushwa, ni kawaida yake na hakuna mtu wa kumsaidia.
“Akitoka hata kazi atakua hana.” Alimuambia akidhani kuwa labda atafurahhia, lakini kwa upande wa Anna ni kama kuna kitu kilimchoma, alijisikia vibaya na kukata simu, hata mume wake alipompigia hakupokea. Kesho yake hakwenda kazini na mumewe alipompigia simua liishia kumkatia. Alienda Polisi kufuatilia kuhusu Hamisi, pamoja na yote hayo lakini bado alikua anampenda, huko alikutana na mke wake, walikua wanajuana, waliangaliana kwa hasira lakini hawakusemeshana, hakuruhusiwa kumuona.
Aliondoka akiwa na hasira na kwenda kazini, alimfuata George na kumuambia.
“Nilichokua nataka mimi ni kuchukua picha zangu za uchi tu lakini si kumfunga. Nataka umuachie, nataka umuachie, hiyo kesi ni ya kutengenezwa.” Aliongea kwa hasira, George alikua hajali.
“Nilikuuliza kama unataka msaada wangu ukasema ndiyo, imeshatokea mimi siwezi kukusaidia tena.” Alijibu kwa hasira kidogo kwani alishachoka kumvumilia.
“Isitoshe, haya ni maisha yako, nimekuvumilia sana mpaka najiona mjinga, sikutaki tena, kama umeamua kuwa malaya, kuhangaika na wanaume wanaokkunyanyasa basi mimi nimeamua kuchagua maisha yangu. sitaki tena kusikia chochote kuhusu wewe, nitalea mwanangu na sikuhitaji tena!”
Aliongea kwa hasira lakini Anna hakujali, waliishia kutukanana, lakini George hakurudi nyuma. Siku iliyofuata alienda ustwawi wa jamii ili kutafuta Barua ya kumruhusu kwenda mahakamani kuchukua talaka. Tangu mwanzo Anna alidai talaka lakini yey ndiyo alikua anazuia. Anna aliitwa na kuambiwa kuwa mume wake kakubali kumpa talaka, kwa hasira naye alikubali, hakutaka usumbufu wa kanisani, wopte walikubaliana kuachana hivyo wakapewa Barua na kwenda kufungua kesi mahakamani.
Mwanzo Anna aliona kama kawaida, hakujali sana, lakini hata kabla kesi haijaanza aligundua kuwa alikua na ujauzito, kwa vyovyote vile alijua kwua mimba itakua ni ya Hamisi. Alizidi kuchanganyikiwa, alijaribu kuitoa lakini ilishindikana, kasbla hata hajakaa vizuri alisimamishwa kazi. Iligundulika kuwa kuna pesa nyingia likua anaiba, wakati anaishi na Hamisi alikua akimhudumia kwa kila kitu, hakua na pesa hivyo alikua akiiba kazini, alisimamishwa kazi kwajaili ya uchunguzi.
Baada ya kuona hivyo alinywe ana kuanza kuomba msamaha, George hakua tayari kumsamehe mpaka siku moja alipopigiwa simu kuwa mke wake alikua amekunywa sumu ili kujiua. Aikua kalazwa hospitalini, aliamua kufita kesi ya talaka, akamchukua mke wake na kuanza kuishi naye. Lakini ukweli nikuwa, Anna hakunywa sumu, alikunywa vidonge ili kutoa mimba lakini vilimzidi kwakua alikua na matatizo na mume wake basi kila mtu alidhani kuwa kanywa sumu. Walianza kuishi tena kama mke na mume.
George alimsaidia kulea ile mimba mpaka akajifungua. Mtoto alifanana na hamisai, bila sababu Anna alimchukia sana yule mtoto, hata kumnyonyesha alikataa, ilifikia kipindi hata akiamka usiku na kulia alikua hafanyi chochote zaidi ya George kuamka na kumbembeleza mtoto mpaka akalala. Kesi ya Hamisi iliisha juu juu lakinioa lihama kabisa na hakujua hata kama Anna aliwahi kuwa na mimba yake, aliondoka na familia yake.
Anna alifukuzwa kazi na sasa hivi ni Mama wa nyumbani kwani kila Biashara anayojaribu kufanya inashindikana. George alimsamehe na anamlea mtoto wa Hamisi kama wake, yeye ndiyoa namhudumia na kumjali kwakua Anna hampendi, hataki hata kuwa karibu naye. Kelvin alifanikiwa kupata mtoto mmoja na aliwahi kumtafuta Anna kumuomba msamaha, mpaka sasa wanaongea ingawa George hafahamu chochote.
MWISHO
ANNA; MKE WANGU NAOMBA UNISAMEHE KWAKUKUOA—SEHEMU YA KUMI NA MOJA
Najua hakuna aliyeamini kuhusiana na kisa cha Anna, yaani namna kilivyoisha kila mtu alidhani kuwa Anna yatamkuta. Nilikua napitia Comment nacheka kwani hata mimi wakati naanza kusikiliza nilikua nishamuambia huko kichwani kwangu huyu ni mwanamke wa kuacha kabisa apambane na hali yake.
Huu mrejesho nilipanga nikae nao kwa muda lakini na mimi nimewashwaaa, nimeona niandike leo. Ngoja nianze kuwaambia kitu kilichotokea, mtu wa kwanza kunitrafuta alikua ni Mama yake mdogo na George. Mnakumbuka yule ambaye alitaka kuwasuluhisha, basi ni msomaji wangu, ni Mama mtu mzima tu lakini ananisoma.
Alinitafuta kwakua yeye alielezewa na mwanae ambaye alimuona kama anachanganyikiwa. Yaani baada ya George kurudiana na mke wake kila mtu alikasirika, lakini huyu Mama alinitafuta, kanunua Kitabu changu na kuniambia niongee na mwanae ili awe sawa kwani alikua kama amechanganyikiwa. Basi nikamtafuta George akanielezea kila kitu, mwisho aliniambia bdo anampenda mke wake, naatamani kumuacha lakini hatakua amemtendea haki mwanae.
“Nataka umsaidie mke wangu, huyu si mke wangu tu ni Mama wa mwanangu, hivi anavyojidhalilisha hivi, nikifa leo mwanangu akaenda kulelewa na aina ya wanaume ambao aanao si wanaweza kuniharibia wanangu.” Haki ya nani hata mimi nilishangaa kwani hata mimi huo moyo sina, yaani nilimuambia kabisa kuwa ingekua mimi nishamuacha lakini nikamuelewa, lengo si kuachana, niliongea na George na kumuweka sawa, nikamuambia namna ya kuishi na mwanamke kama huyo.
Tatizo la Anna nikuwa ni teja, yaani alishanyanyaswa mpaka imefikia hatua kuishi maisha ya kawaida hawezi. Huwezi amini, wako wengi ambao ni kama Anna au wanaelekea kuwa Anna. Ngoja nikuulize wewe uliyetoa povu kwenye Comment, hivi si ulipigwa na mume wako, ulimfumania wewe na bado akakudunda. Unadhani kwanini hukuondoka, yes hukuonoka kuwa ushaanza kuwa teja.
Shida ni kuwa. Uksihazoea mateso ni kama vile mtu aliyezoea kula pilipili, basi anaizoea na kuona kawaida, wengine wanaweza kuiona chungu lakini kwakua yeye kaizoea basi anaona kama kawaida na maisha yanaenda. Baada ya kumaliza kuongea na George nilimtafuta Anna, kwanza hakutaka kuongea na mimi, lakini nilimuambia kuwa hana namna, mimi ndiyo nimeshikilia ndoa yake.
“Najua uanjua kua George hawezi kukuacha, lakini niamini nikikuambia kuwa, George hawezi kukuacha si kwakua anakupenda sana bali kwakua naye ni teja wa penzi lako. Nilimuambia kuwa, nikiongea na George na kuanza kumfundisha namna ya kuacha uteja wake basi atamuacha, na kumuambia kuwa, wanaume kama George wakiacha wanaacha mpaka vivuli, yaani hata ukoo wenu, majina ya huko kwenu wanaacha na kukinahi kabisa.
Hunijui, labd nhujawhai kunsiikia, lamini nakupa wiki moja, nisome, soma post zangu, soma ninachoandika, na nina uhakika mume wakoa kinisoma naweza kumfundisha namna ya kuachana na mwanamke kama wewe.” Hakuamini ila alinitafuta baada ya wiki moja, akanielezea matatizo yake, katika kuongea alikua anamlaumu George, anaongea kana kwamba George ndiyo mwenye mataizo.
Tuliongea sana, akanieleze akila kitu, zaidi ya masaa mawili tuliongea. Nilipomaliza nilimuambia hivi, acha kuwasiliana na Kelvin kwakua ni mshenzi, mwanaume mshenzi hajui kupenda, nilimuambia amuombe mume wake msamaha, halafu amrudie Mungu wake. Nilimuambia kwakua mume wake ananisoma atabaidlika, kuna vitua atacha kuvifanya, na kwakua mume wake kaniomba ushauri nina uhakika atafuata ushauri wangu.
Nikamuambia kuwa, kama mume wako akifuata ushauri wangu, na wewe usifuate uishauri wangu basi jua lazima atakuacha lakini kama wote mkifuata ushauri wangu absi hakuna kuachana.
“Wanaume kama George ni matoleo ya zamani, yaani kama zile simu za zamani ambazo zinakaa na chaji muda mrefu, siku hizi haziotoki, ni chache sana, mimi mwenyewe ninayeshauri nit oleo jipya, yaani smartphone lazima utembee na chaji la sivyo inakuumbua.”
Tuliongea sana na nina uhakika kuwa alikasirika, kwa watu ambao mshaongea na mimi andhani mnajua kuwa kwanini alikasirika, kwa maana alishanichosha, yaani hata mimi uvumilivu ulinishinda. Basi nikamuambia ahcague kunyoa au kusuka. Alikaa baada ya wiki mbilia kanipigia simu na kuniambia kwua Kelvin kamuambia kaachana na mke wake, nilimuambia hata akiachana naye hawezi kuwa mume wake, basi tukaongea tena akaniambia atabadilika lakini nilijua habadiliki.
Nilimtafuta George, nikamuambia kama anampenda huyo mwanamke badi abadilike, apunguze matumizi ya kijinag, aache kumuomba msamaha na vitu vingine vingi kweli George alibaidlika, baada ya mwezi alinitafuta, alikua hashiki simu ya mume wake anamdharau lakini akwa anahangaika naye, akihisi anachepuka, nilimuambia hachepuki ila kaamua kufuaraushauri wangu.
“Na kama unakumbuka nilikuambia kuwa mume wako akifuata ushauri wangu ni suala la mdua tu uanaachwa na ukiachwa basi jua imekula kwako, hakuna cha Kelvin, Hamisi wala nani aakutaka?” basi hakunitafuta tena, mpaka juzi aliponitafuta, yes alibadikila, wanaishi vizuri, George kamsamehe wana amani. Sasa hivi ana ujauzito wa mume wake, na anakaribia kujifungua, wanafuraha.
Najua kuna watu mmenuna, lakini niwakumbushe kitu, hivi kwanini mwanaume anaposamehe vitu kama hivi anaonekana mjinga wakati mwanamke akisamehe anaonekana ana akili, anatetea ndoa na vitu vingi. Mfano, ukisoma Comment za watu waliokasirika Anna kusamehewa nyingi ni wanawake, lakini kwa mambo ninayoandika hapa wanawake wanafanyiwa wakirudi kwa waume zao wanaonekana mashujaa.
Kuna wanaume wanapenda, shida nikuwa, mwanamke ukimpenda sana na aklijua kua huwezi ishi bila yeye, huwezi kumuacha basi anakuona kama fala flani. Kuna wanawake wanapenda na wavumilia makubwa kuliko haya, ushauri wangu, ukipenda mtu penda kwa kiwango, acha kumpenda silimaia mia, kumi baki nzo, jipende na wewe, isifikia hatua unasema siwezi kuishi bila wewe.
Anna hana mawasiliano tena na Kelvin, hiki kisa ni cha mwaka jana tu na nimeamua kukiandika baada ya mrejesho na wahusika kuniruhusu. Majina hayana ukweli hana maeneo. Nishamaliza, naamini mmenielewa, hii sio stori ya kubuni hivyo siwezi kuimaliza ninavyotaka mimi. Nisisahau, kama unajijua hujipendi usisahau kununua Kitabu changul, cha furaha yangu, soma sehemu ya Nne itakuinua kwa namna flani, nishamaliza.
MWISHO WA MWISHO WA MREJESHO!
0 comments:
Post a Comment