IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO
KIGAGULA; SITAKI AFE LAKINI SITAKI AWE MKE WAKE—- SEHEMU YA KWANZA.
Nilikua sijawahi kufika nyumbani kwake, kama meneje wa Benki alikua akiishi kazini, palepale lakini alikua na nyumba nyingine ambapo familia yake ilikua ikiishi. Ilikua ni nyumba kubwa, nzuri na ya kisasa na kwakweli kwa eneo lile ilikua ndiyo nyumba nzuri. Kama wafanyakazi wakujitolea ambao hatukua na kazini sisi ndiyo tulipelekwa kule kusaidia kazi za nyumbani.
JOIN US ON TELEGRAM
Meneje alikua nyumbani na familia yake. Nilimuona mke wake kwa mara ya kwanza, hakua mtu mzima sana, ni Mama tu wa miaka kama 38 mpaka 40. Ingaw3a mimi nilikua mdogo sana lakini nilimuonea wivu, alikua na shape yake nzuri, mwili umetaktiam vizuri yaani ukisikia namba nane ni namba nane. Alikua ndani ya Dera, analia ana huzuni lakini shape lake bado lilionekana, kiuno kimekatika vizuri, tako unaliona na kifua unakiona.
Uso uliokua unalia ulikua ni kama umetoka kupigwa makeup, kusema kweli alikua ni mzuri. Yaani nilipomuona tu moyo ulinipiga.
“Hivi kwanini wanaume wanahangaika, una mke mzuri namna hii lakini bado unataka kinyago kama mimi?” Nilijiuliza lakini sikupata majibu kabisa. Mwili ulikua kama umepigwa ganzi, ingawa wengine walikuja kwaajilia ya msiba lakini mimi sikuja kwasababu hiyo, nilienda pale kumuona mke mwenzangu, nilitaka kujishindanisha, nilishaanza kumpenda bosi wangu, nilishaanza kujiaminisha kuwa mimi hawezi kuniacha.
“Kashazoea kutembea na Malaya, mimi ni msomi, hawezi kunichezea na kuniacha!” Nilijiambia kila siku mara tu baada ya kuanza mahusiano na Bosi wangu. Watu walikua wanamsalimia Mke wake na kumpa pole za kufiwa na watoto wake wawili Mapacha ambao walifariki kwaajali ya Gari. Ilikua ni huzuni kubwa, alikua chumbani, mwanga ulikua haifu lakini niliweza kumuona vizuri, sisi tuliingia kama wafanyakazi kusaidia shughuli za ndani.
Alikua kakaa lakini wakati tunaingia alisimama, kuna Mama alikua anapita na kuna meza alikua anaitoa hivyo ilimlazimisha kusimama. Chumba kilikua kikubwa kama sebule za watu wengi, hakikua na vitu vingi vingi, kitanda kilikua kikubwa sana, cha kisasa, yaani kama vile vya kwenye TV. Kwa kukiangalia, kukiona nilianza kuona kama ni chumba changu.
“Hiki sijui ndiyo chumba chenyewe au ni chumba cha wageni, ninavyojua wasingeweza kuruhusu watu chumbani kwao, kama ni chumba cha wageni huko chumbani kwao kukoje? Yaani chumba kama cha hoteli!”
Niliwaza nikikishangaa kile chumba, akili yangu ilirudi mara ya kwanza kuingia katika hoteli ya nyota tano ambapo niliingia na Bosi wangu, yaani niliganda na kuchanganyikiwa, kwangu ilikua ni kama ndoto hivyo sikuweza hta kumkatalia Bosi wangu kunifanya kitu chochote, nilimuacha afanye yake bila hata kujijua.
“Haya ndiyo maisha ambayo natakiwa kuishi mimi si ule umasikini naishi kama nipo jalalani!” Niliwaza huku nikimsogelea yule Dada maana siwezi hata kumuita Mama ingwa alikua mkubwa sana kwangu. Alikua anataka kuakaa na mimi nilitaka kumgusa, sijui kwanini lakini nilitaka kuuangalia mwili wake.
“Usije kukuta nasifia shape kumbe kavaa vigodoro na matoto katia jeki bure, ngoja nimchunguze!” Kusema kweli nilikua na hasira na wivu. Mwanzo nilijua kua Bosi ni malaya kwakua mke wake ni mbaya, mchafumchafu ambaye hajielewi, hivyo nilijua kuwa itakua rahisi sana kwangu mimi kumteka kwani nilikua najiona mzuri, nina akili na bado kijana. Lakini baad aya kumuona nilichanganyikiwa.
Nilimfuata na kumkumbatia ili kumpa pole, nilijifanya kimpapasa papasa kama kumshikashika, nilianza na makalioni, nilimshika na kumkumbatia kwa mikono yote miwili, niliishusha mikono yangu kwenye makalio yake nikawa nammpinyaminya makalio kuangalia kama kavaa nini. Mwanzo hakushtuka lakini baada ya kuyashika makalio yuake nilikuta kavaa lile dera na Tight ya kawaida, haikua ya kuongeza makalio au mahips. Nilijikuta naganda pale, nimekumbatia, pole nyingi lakini kwa jinsi nilivyokua na mmonyaminya makalio alishtuka, aijisikia vibaya na kujitoa mikononi mwangu.
Matiti yake nilikua nayasikia kwenye kifua changu, sikuhisi yeye kuvaa sidiria achilia mbali kupiga jeki. Nilitamani kuyashika lakini rafiki yangu niliyekua naye pia alitaka kusalimia hivyo niliahca. Nilijisikia vibaya kuwa sijamchunguza vizuri, baada ya salamu tulitoka.
“Mke wake mzuri, hivi unadhani yale matoto ni yakwake au kaiga jeki?” Nilijikuta namuuliza mfanyakazi mwenangu. Aliniangalia kwa mshangao kisha akacheka kidogo.
“Una akili kweli wewe, yaani umekuja kwenye msiba unaulizia matiti, au mwenzetu unasagana?” Alinipa makavu ambayo yalinifanya kunyamaza lakini si kuacha kuwaza.
“Amenyonyesha watoto wanne, halafu uniambia matiti yasishuke, hapana, atakua anatumia dawa au nimemuangaia vibaya!” Niliendelea kuwaza, bado umbo la mke wake lilikua linanichanganya, nilijikuta napata hasira ambazo hazina msingi. Bosi alikuja kutusalimia, tukampa pole kwani tangu kufiwa na wanae jana yake tulikua bado hatujamuona, alitushukuru kwa kwenda kumsaidia kisha akaondoka, alionekana kuchoka, alionekana kama alilia sana siku hiyo lakini kwakua ni mwanaume alioneknaa kama alijikaza sana.
“Hivi unadhani kwanini Bosi ni malaya wakati ana mke mzuri namna ile?” nilimuuliza mfanyakazi mwingine.
“Wanaume wote wako hivyo, hawaridhiki, yaani anaweza kuwa na malaika ndani lakini akaenda kutafuta kinyago huko nnje. Sema wanaume utakuta anampenda mwanamke wake lakini kwakua tu ana nyege basi anachukua takataka huko mtaania anitumia na kuiacha. Si unasikia sifa zake, yaani nasikia harudii mwanamke, kila siku mpya, aisee huyu bosi sijui kamke kazuri lakini anahangaika na vinyangarakata huko mtaani havina nyuma wala mbele, kulia wala kushoto!”
Alinipa majibu ambayo yalinichefua, alikua ananiambia ukweli kwnai mimi nikilinganisha na mke wa bosi nilikua kama kinyago, si kama nilikua mbaya, hapana, nilikua na uzuri wangu lakini si kwa kunilinganisha na yule mwanamke. Hicho hakikuniumiza sana kwani nilipomuona mke wake nilijua kuwa mimi sina nafasi, kilichoniumiza ni ukweli kuwa, tangu kufanya mapenzi na bosiw angu ilikua imepita miezi mitatui sio kama tu hajataka kufanya mapenzi tena na mimi lakini hata salamu alikua hajawahi kunisalimia.
Nilimtumia meseji mara moja tu kumjulia hali akanijibu “SITAKI MAZOEA!” basi na baada ya hapo kila kitu kilisimama. Mkatab wangu tena wa muda kama kibarua tu ulikua unaisha na nilikua nahofia labda anaweza kunifukuza. Wakati natembea naye nilihisi labda ndiyo nitapata kazi lakini kazi zilitanangazwa, usahili ulifanyika lakini hakunisaidia hata kidogo, nilipotaka kuongea naye alinijibu kwa dharau kwa mkato “Mimi sio ninayeajiri!” baada ya hapo hakuongea na mimi kabisa mpaka siku ile tena alikua kuongea na sisi wote si na mimi.
Hata wakati wakuongea ingawa nilijitahidi kujionyesha ajue kuwa niko pale lakini macho yake yalikua ni kwa wale wengine wawili. Iliniuma sana kwani wakati mfanyakazi mwenzangu anaelezea kuhusu hao malaya, kutokurudia wanawkae nilijiona mimi. Mwanzo nilijihisi spesho kwakua alinitaka mimi, hatembei na wafanyakazi lakini mimi alitembea na mimi kitu ambacho niliona ni kama heshima. Niijua maisha yangu yatabadiika lakini baada ya kufanya mapenzi siku moja hakutaka hata kuniona tena, iliniuma sana.
****
Mama yangu ana sehemu ya chakula, sio kubwa sana lakini ndiyo inaendesha maisha yetu tangu nikiwa mdogo mpaka hii leo. Sisi kwetu tumezaliwa watatui, mimi nikiwa ndiyo mkubwa kwetu kuzaliwa, Baba yangu alifariki dunia wakati nipo kidato cha pili. Wakati huo Mama alikua ni Mama tu wa nyumbani, Baba alikua ni mfanyakazi katika kampuni moja binafsi, baada ya Kufariki na Mama kulipwa mafao ndipo alifungua huo mgahawa ambao ulisaidia kuendesha maisha yetu.
Kusema kweli hali ilikua ngumu sana, ingawa mgahawa ulikua mjini kabisa, lakini Biashara ilikua ngumu na mbaya zaidi tulikua tukiutegemea kwa kila kitu. Kuanzia chakula, kulipa kodi ya nyumba kwani wakati Baba anafariki alikua akijenga lakini nyumba ilikua haijakamilika, aliiacha ikiwa ndiyo imepigwa bati haina hata milango wala madirisha. Mbali na kodi pia lakini Biashara hiyo hiyo ndiyo ilipaswa kunisomesha mimi na wadogo zangu.
Mama yangu alikua anahangaika sana, nilikua namuonea huruma, alikua anahangaika tusome, alikua na madeni mengi, alichukua mikopo kila sehemu na kama unavyojua wale watu wa marejesho wakija kudai basi ilikua ni shida. Tulisoma hivyo kwa shida, nilimaliza kidato cha nne lakini sikufaulu vizuri, niliwaza kuhusu kwenda kidato cha sita lakini niliona kama nitapoteza muda sana, niliamua kubai nyumbani, nilitaka kumsiadia Mama kufanya Biashara lakini alikataa.
Mama alikua ananionea huruma, wakati mimi nilikua namuonea huruma kuwa anahangaika na ada kila siku yeye alikua anaona kuwa kama Baba asingekufa basi tungesoma hivyo alinilazimisha kurudi shule. Mwanzo alitaka nirudie mitihani ya kidoto cha nne lakini katika kuhangaikia kurudia nilikutana na Kaka mmoja ambaye alinishauri kusoma Certificate kwanza kisha niunganishe Diploma ndiyo itakua rahisi.
Aliniambia nikimaliza kidato cha sita kama sitachaguliwa chuo sitakua na tofauti na darasa la saba au Form Four tu, lakini kama nikijiunga na ngazi ya cheti, nikimaliza hata kama Mama yangu atashindwa kuniendeleza basi haitakua shida kwani angalau naweza kuomba kazi na cheti. Nilimuelewa na kuongea na Mama, alikubali hivyo nikaomba kusomea mambo ya uhasibu ngazi ya cheti.
Nilifanikiwa kumaliza kwa shidashida hivyo, Mama aliingia madeni mengi kwani wakati nasoma mdogo wangu anayenifuata wakiume alimaliza kiado cha nne nayeye alifeli kabisa hivyo akalazimika kurudia tena kwani Hakutaka tubaki nyumbani na mdogo wangu wa mwisho wa kike alimaliza darasa la saba hivyo alihitaji kwenda kidato cha kwanza. Ingawa alifaulu lakini Mama alitaka kumpeleka shule binafsi kwani shule aliyokua kachaguliwa ilikua mbovu sana.
Nilimuona kama Mama anachanganyikiwa, lakini kila wakati alisema kuwa yuko sawa na kamwe hakuonyesha kuwa anaumia au ana mawazo. Nilijitahidi kusoma mpaka nikamaliza Diploma, hapo nilisema siaendelei tena, nilitaka kutafuta kazi ili kumsaidia Mama yangu, niliona anaumia sana. Lakini pamoja na kusoma, kuwa tayari kufanya kazi bado ajira ilikua ni shida, nilihangaika sana katika kutafuta kazi, nilizunguka na CV mpaka basi.
Mwisho sikua na namna, nililazimika kurudi kwenye mgahawa wa Mama kumsaidia, ili kujitengenezea kipato changu mwenyewe niliamua kuuza matunda, haya ya kukatakata, kwakua sehemu ilikua imechangamka nilikua napata, kwa siku sikosei elfu tatu na wakati mwingine napata faida mpaka elfu tano. Kwangu ilikua kubwa sana kwani niliweza kujihudumia mahitaji yangu mwenyewe pamoja na kuwasaidia wadogo zangu vitu vidogo vidogo.
Wakati huo nilikua kwenye mahusiano na vijana waodgo tu kama mimi, yalikua ni mahusiano ya kudanganyana. Lakini pale mgahawani kwa Mama kuna Baba mmoja mtu mzima hivi, si sana kihivyo lakini alikua na miaka kati ya 45 na hamsini, alipenda sana kuja pale kwenye mgahawa wa Mama usiku wakati tunafunga funga, anasimamsiha gari yake anakunywa chai ya tangawizi kisha anaondoka.
Alizoeana sana na Mama lakini kutoka na umri wake mimi sikumshobokea kabisa, yeye alikua anafanya kazi Benki, alikua ni afisa Mikopo. Lakini pia alikua na Biashara zake nyingi nyingi hivyo kwa kipato alikua vizuri. Alikua ni mteja wa muda mrefu wa Mama, tangu kipindi naanza mgahawa unafunguliwa mpaka wakati huo namuona lakini niliishia tu kumsalimia na kumhudumia basi, sikua na mazoea naye na nilimheshimu kama Baba yangu kwani kwa umri wake angeamua angekua na mtoto mkubwa kama mimi, wakati huo mimi nilikua na miaka 23, hivyo nilimuona mkubwa sana ingawa muonekano wake ulikua ni wa kijana flani.
Yaani kuanzia mavazi, mazoezi na namna alivyokua anaongea, watu wlaiokua anaongozana nao alipenda kuonekana kujana ila kwa kumuangalia ulijua tu ni mtu mzima.
“Mbona nakuona kila siku hapa ushamaliza chuo?” Aliniuliza, nakumbuka ilikua ni usiku, baada ya kumhudumia, mara nyingi yeye ndiyo anakua mteja wa mwisho kwani sisi tunafunga kwenye saa mbili na nusu mpaka saa tatu. Huo ndiyo wakati yeye anatoka kazini, anakuja pale na kunywa Tangawizi yake kisha anaondoka.
“Ndiyo nishamaliza.” Nilimjibu nikiendelea na kupanga vyombo vizuri.
“Wewe Salma si umjibu vizuri huyu, si umuambie kuwa umemaliza chuo lakini huna kazi, muambie unasomea nini anaweza kukusiadia huko kazini kwao, wewe si ulisema umesoma mabo ya uhasibu, si ndiyo mambo ya Benki, inamaana hujui kama huyu ni mtu mkubwa huko Benki, ongea naye vizuri, simama acha kupanga ma vyombo huko.
Msomi badala ya kutafuta kazi unahangaika na mimi Mama yako hapa ambaye sijasoma! Muambie una Diploma ya nini, muambie umefaulu vizuri, muambie….”
Mama yangu alikua ni mshapu, alijifanya kunigombeza lakini ni kama alikua anampa yule Baba CV yangu.
“Ni kweli, ushamaliza chuo?” Yule Baba aliniuliza kana kwamba hakumsikia vizuri Mama yangu.
“Ndiyo, nimemaliza tangu mwaka jana lakini bado sijabahatika kupata kazi.” Nilimjibu huku nikiwa nimeskimama namuangalia, nilimuangalia usoni kwa adabu kwani Mama alikua pembeni kanisimamia kama vile hataki nikosee kitu.
“Basi kesho njooo na CV yako, nitaiangalia, kuna nafasi za kujitolea pale ofisini, wanatoa Posho ila naamini itakupa uzoefu na ni rahisi kuajiriwa.”
Aliongea huku akiondoka, alionekana kuwa na haraka zake.
“Umeona, unajificha ficha nini, mtu anakuuliza umemaliza chuo huongei kuwa huna kazi, hawa ni watu wakubwa, anaweza kukusaidia!” Mama alinifokea.
“Mama unafikiri ni kirahisi namna hiyo, huyu ameomba CV yangu kwakua umeongea, sanasana ataiangalia tu na kuitupa pembeni kama wengine…”
“Acha kuwa na maw3azo hasi namna hiyo!” Mama alinikatiza.
“Kwanini unajinenea mabaya, hembu tema mate chini, nakuambia, tema mate chini, acha kujinenea mambaya!” Mama linifokea hukua kinisisitiza kuwa kesho yake ni lazima kupeleka Cv kwa yule Baba na kweli nilifanya hivyo, nilimpa akaondoka nayo huku mimi nikijua kuwa hakuna ishu ya kazi wala nini ni mabo ya mtu unampa CV yako kisha anaenda kukaa nayo tu.
****
Sikua na imani kama atanitafutia kazi lakini baada ya siku mbili niliitwa kazini katika ile Benki aliyokua anafanya yule Baba. Haikua ni ajira ya kudumu bali niliajiriwa kama kibarua, ajira ya muda tulipewa mkataba wa miezi mitatu mitatu na tulikua tunalipwa laki na nusu pamoja na kula chakula cha mchana. Kwangu ilikua ni hatua kubwa sana, kutoka nyumbani na kufanya kitu kinachoendana na kile nilichokisomea kwanu ilikua ni Baraka kubwa sana.
Kazi ilikua nzuri na mwanzo hakukua na shida kabisa, nilikua nafurahia kila kitu kwani nilikua najifunza mambo mengi, nilikua ni mwepesi sana wa kujifunza na kubwa zaidi watu walinipenda kwani nilikua nafanya kazi vizuri sana. Nilifanya kazi kwa miezi mitatu, nikaongezewa mkataba mwingine wa miezi mitatu.
Siku moja nikiwa kazini niliitwa ofisini kwa meneja, sikujua sababu ya yeye kuniita lakini haikua kawaida yake. Niliingia ofisini kwake, ofisi ni ya vioo lakini baada ya kuingia mimi alishusha zile pazia za watu kutokuona ndani. Meneja alikua ni jkijana mtu mzima, alikua na miaka kama 45 hivi na alikua ana muonekano wa kijana sana. Pale ofisini alisifika kwa umalaya, akitembea na wanawake wengi tu ingawa si wa pale ofisini kwa maana ya wafanyakazi lakini ofisini walikua wanajua kuwa jmaa mtaani ni noma na mimi nilishamjua.
“Najua umeshaambiwa kuwa mimi ni Malaya, unajua kabisa huko mtaani wananisema…” Alianza kwa kuniambia baada tu ya kuingia ofisini kwake. Nilishangaa, nilishikwa na butwaa kwani hatukuzoana, katika kipindi cha kama miezi mitano nimekaa naye nilikua sijawahi kuongea naye neno lolote zaidi ya salamu. Nilishindwa kumjibu nikabaki natetemeka. Nilimuangalia kwa uoga akaniambia nikae lakini nilishindwa, miguu ni kama iliganda, mwili umekufa genzi, yaani nilihisi kuchanganyikiwa kwani sikujua ameniita mule ndani kufanya nini?
“Nasikia unafanya kazi sana, na mwezi ujao kuna nafasi zinatoka, tunahitaji kuajiri watu, sasa ajira ni ngumu naamini unajua ndiyo maana unajitolea hapa kama kibarua. Ni ngumu sana kupata tu kazi, hivyo, nataka ubaki hapa, nataka nikuajiri. Watu wananiongelea vibaya lakini si kweli, nataka nikupe nafasi ya kunijua, kesho kutwa nina safari ya kwenda Dar, nina semina na nataka kwenda na wewe, nimeshakukatia na tiketi ya ndege, ni safari ya kikazi na ni safari pia ya kujuana, tiketi hii hapa, kafikirie kama unaenda au la, wewe ni mtu maima, ushasikia kuwa mimi ni malaya na nimekuita hivi nadhani unajua nataka nini!”
Aliongea kwa kujiamini bila hata kunipa nafasi ya kuongea, katika dakika 20 ambazo nilikaa mule ndani kwenye ofisi yake, zaidi ya shikamooo mkuu wakati naingia nilikua sijaongea neno jingine lolote lile. Yaani nilimuacha akajiongelesha upuuzi wake kama mtoto na kisha akanipa hiyo tiketi na kuniambia nitoke, nilitoka kama zuzu, walioniona walinishangaa. Lakini kwakua hakua na tabia ya kutongoza wala kutaka wafanyakazi basi hakuna aliyenihisi vibaya, katika kazi alikua siriasi ila mtaani kila mtu alijua kuwa ni malaya.
Kusema kweli ni kama nilifurahi flani, sikuwaza kwamba yule ni mume wa mtu, sikuwaza kuwa ni bosi wangu lakini yeye kuniita, kutaka niende naye Dar kwenye semina, kunikatia tiketi ya ndege ilikua ni kunitongoza tosha. Ingawa hakuniambia moja kwa moja kuwa ananitaka lakini kwa mtu mzima nilijua tu kuwa ananitaka. Kweli ilikua hivyo, safari ilikua ni ya Dar lakini haikua ya kikazi, tuliposhuka uwanja wa ndege alinichukua moja kwa moja mpaka kwenye Hotali moja kuwa ya kifahari.
Alichukua chumba kimoja bila kuniuliza chochote na mimi nilijikuta namfuata mpaka chumbani.
“Au ulikua unataka nikuchukulia chumba chako.” Aliniuliza wakati tunaingia chumbani, kusema kweli nilishindwa hata kunyanyua mdomo, macho yangu yalikua yakiangalia kile chumba ambacho kilikua ni kikubwa, kitanda kikubwa, kimetandikwa vizuri yaani kila kitu kilikua kama ndoto. Nilikua naishi maisha ambayo nilikua nayaona tu kwenye TV.
Baada ya kuona nimezubaa tu alichukua begi langu na kuliweka kwenye meza, alinishika mkono na kuanza kunivua nguo taratibu. Hakua akiongea zaidi ya vitendo, dakika kama tatu hivi tulikua bafuni tunaoga. Ilikua ni jioni, baada ya kumaliza kuoga, tulifanya mapenzi ndipo akaagiza chakula mulemule ndani tukala. Hatukutoka mpaka kesho yake, baada ya kumaliza ndipo alianza kunitongoza na kuniambia kuwa anavuiwa na mimi, aliniambia atanisaidia kupata kazi na kuniahidi mambo mengi mengi sana. Nilijikuta nafurahia na kujiona spesho sana kwani nilipewa vitu ambavyo hata sijawahi kuviota.
Tulikaa pale siku tano, kisha tukarudi kwa ndege lakini baada ya hapo ndipo hakunitafuta, hata salamu hakunipa, meseji pekee aliyonitumia ni ile ya kuniambia hataki mazoea. Kuhusu kazi hakunisaidia, pamoja na yote hayo lakini bado niliendelea kumpenda na kujua kuwa ipo siku atakua wangu, alishanionjesha maisha matamu sikutaka kurudi katika umasikini. Sikuwahi kuwa naye karibu nnje ya maeneo ya kazi mpaka siku ile ya msiba.
Kumuona Bosi na mke wake kulinichanganya sana, watu walikau wakijiandaa na mazishi lakini mimi nilikua vize kuangalia ni namna gani nitapata nafasi ya kuongea na Bosi peke yake, nilitaka kumuona akiwa peke yake na kuongea naye kidogo. Nilikua na muwinda kutafuta upenyo wa mimi kuongea naye, nilikua na uhuru wa kuingia ndani, hivyo kila sehemu alipokua akiingia nilijipitisha na kwakua kila mtu alikua bize basi hakuna aliyehangaika na mimi.
Kwenye saa tano hivi wakati watu wakijiandaa na Misa nilimuona anaingia kwenye chumba kimoja hivi. Sijui ni nini kilinisukuma lakini nilijikuta naenda mpaka kwenye kile chumba, sikutaka kupoteza muda, kwakua nilijua mke wake hayuko pale na sikuona mtu mwingine nilitaka kuingia. Niligonga kwanza lakini sikuongea chochote, niligonga mara ya kwanza sikusikika, nikagonga ya pili ndiyo akauliza nani?
“Mimi, nifungulie?” Nilijibu lakini sikutaja jina langu nikijua kuwa akinisikia basi anaweza kugoma kufungua. Alifungua mlango kwa kuchungulia, juu alikua kifua wazi kuonyesha kuwa alikua anavua nguo. Kwangu mimi niliona hiyo kama fursa, nilijua kama anavua nguo na mke wake hayuko pale basi ni nafasi yangu mimi na yeye kuwa wawili, hiyo ilikua ni bahati ambayo sikutaka kuipoteza kwasababu yoyote ile.
Sijui nilipata wapi nguvu, nilisukuma mlango na kuingia nao, yeye alipepesuka kidogo kwani nilikua kama nimemgonga kwakua alikua kauegemea mlango wakati ananifungulia. Niliufunga mpango nakujikuta namuambia.
“Huwezi kunikataa tena, leo lazima uniambia kwanini umetemeba na mimi mara moja kisha ukanikimbia. Au na mimi umeniona kama hao malaya wako!?” Nilimuuliza kwa hasira huku nikivua nguo, yeye alikua ndiyo anaanza kuvua na alikua amebaki na suruali tu. Lakini wakati navua alinishika na kunizuia huku akiniambia.
“Una akili kweli, mke wangu yuko vafuni najiandaa na misa ya wanangu unataka tufanye mapenzo?”
Kigagula ni nani? Hivi unafikiri kwanini ameitwa kigagula, mimi sijui? Nadhani nitakua nimerudi, kwa wale wa vitabu karibuni, soon tunakuja na “Interview na Ajira” simulizi hii inatokana na stori ya kweli, usikose…
KIGAGULA; SITAKI AFE LAKINI SITAKI AWE MKE WAKE—- SEHEMU YA PILI!
Kusikia mke wake yuko Bafuni nilihisi kama kuchanganyikiwa, sijui ni ushetani, sijui ni nini lakini nilitamani kufumaniwa. Nilitamani mke wake kutoka mule ndani na kunikuta nimekumbatiana na mume wake.
“Atanifanya nini? Mume wake si ni malaya, nina uhakika ataondoka na nitachukua nafasi, mimi ni lazima nimchukue Ben!” Niliwaza, nilivua nguo harakaharaka na kubaki kama nilivyozaliwa, Bosi alikua akijaribu kunishika lakini kila akinigusa na muambia nitapiga kelele. Nilibaki uchi lakini hakuniangalia,m nguo zilikua chini na alikua anainama kuziokota na kunipa nivae lakini sikua tayari kuvaa.
Alikua kama kachanganyikiwa, nilimbana kwenye kona ambayo asingeweza kufanya kitu chochote kile. Nilijua hawezi kunipiga kwani nikipiga kelele mke wake akatokea au watu wa nnje wakasikia aibu ingekua kwake. Nilikua nampenda sana, nilimshika na kumkumbatia huku nikimlambalamba shiongo, ni kitu ambacho aliniambia kuwa anakipenda wakati tunafanya mapenzi na nilijua kwa wakati huo nitamsisimua lakini haikua hivyuo.
“Mbona unafanya mambo ya kitoto? Hivi kama ni mapenzi si titafanya sehemu nyingine, nimepoteza watoto wawili, mke wanmgu yuko bafuni, hata kuzika wanangu bado unanifanyia hivi?” Aliniuliza, lakini mimi sikujali, nilitamani sana kuvunja ndoa yake nikiamini kuwa nitaishi maisha yale.
“Wewe si ndiyo unanikwepa, unafikiri mimi ningekuona wapi, umetembea na mimi siku moja kama malaya wako ukaniacha halafu uantaak nikuonee huruma, mimi nakutana na siondoki hapa mpaka unihakikishie kuwa unanipenda na tukirudi tunaendelea na mausiano!”
“Sawa lakini vaa utoke, hivi unafikiri italeta picha gani nikikutwa na wewe hapa?” Sivai na sitoki mimi nakutaka na nina hamu leo, sijali chochote lakini nafanya mapenzi na wewe hapa, kama mke wako anataka basi aje kuangalia lakini mimi sitoki. Uinaona raha sana kucheza na hisia za watu, mimi nakupend,a umenichezea halafu unaicha!” Niliongea sasa hivi nilitoa sauti ili mke wake bafuni asikie. Lakini hakusikia, nilisikia tu sauti ya maji, aliniona niko siriasi nataka kufanya fujo.
Alianza kunishikashika maziwa, akinichezea mpaka nikalegea, nililala kitandani nikitaka tufanye mapenzi, alikuja na kunilalia kwa juu kisha akaniambia.
“Nitafute baad aya mazishi, njoo usiku, tutakua wawili na tutapata muda wa kufanya chochote.” Alikua anaongea sauti ya kimahaba, nilijikuta namkubalia,a lininyanyua harakaharaka na kunipa nguo zangu ili nivae. Hapo na mimi nilikua kama vile nimezinduka, nilishtuka nikoc humbani kwake, uchi, nilianza kuhisi aibu, nikachukua nguo zangu, lakini wakati navaa nguo ya ndani tu mlango wa bafuni ulisikika.
Kwa namna chumba chao kilivyo nikuwa bafu limezuiwa na kabati kubwa la nguo hivyo mtu anapotoka bafuni hakuoni moja kwa moja hapana, anatakiwa kutembea umbali kidogo kisha ndiyo akuone.
“Mume wangu njoo unisiadia…” Nilisikia sauri ikitoka bafuni, Bosi wangu alinisukumiza upande wa pili wa kitanda, akachukua shuka kubwa kam Duveti lakini si Duveti na kunifunika nalo, nilikua uchi nimevaa chupi tu hivyo nisingeweza kutoka nnje kwani ningekutana na watu waliojaa msibani.
Alimkimbilia mke wake na mimi kunniacha nipo ndani ya shuka.
“Kuna nini?” Aalimuuliza.
“Nimeshindwa kunyanyuka, nisaidie, nahisi presha imenipanda.” Mke wake alilalamika, ingawa niliambiw akutulia lakini nilitaka kuchungulia, nilitafuta ka upenyo na kuanza kuchungulia. Bosi alimshika mke wake akawa anamsaidia kutembea, mkewe alikua uchi wa mnyama, alionekana kuwa hata kuoga hakumaliza vizuri, ingawa alikua kakaa muda mrefu bafuni lakini nilimuona bado ana sabunisabuni. Moja kwa moja alimlaza kitandani, wakati ule ndipo nilimuona vizuri, niliona mwili wake, alikua mzuri, kila kitu kilikua vizuri, tumbo lake liliniumiza sana, yaani alikua kama mtu amabye hajazaa kabisa kumbe alikua na watoto, mimi ambaye nilikua hata sijabeba mimba ya bahati mbaya tumbo langu lilikua kubwa zaidi. kifua chake nacho kilikua ni mtihani, mpaka niliwaza hivi huyu Bosi alifuata nini kwangu.
Mimi nilikua binti lakini nilikua navaa sidiria nyonyo lishadondoka lakini yeye amezaa ila unaweza hisi ndiyo anavunja ungo. Alikau kalala, mume wake alimpepea na kumuambia apumzike, wakati wote huo alikua anamepepea mke wake hukua ananiangalia mimia kinisihi nisinyanyuke, aliniona namna nilivyokua nachungulia na alikua na wasiwasi kuwa labda nitanyanyuka na kumharibia.
Alimpepea kwa zaidi ya dakika 20, mkewe alipata kanafuu kidogo.
“Twende nikakumalizie kukuogesha, misha inaanza ni lazima twende sisi.” Alimuambia mke wake hukua kijaribu kumnyanyua.
“Navaa hivi hivi mume wangu, wanangu wanangu huko walipo nani anawaogesha… mume wangu….” Alianza kulia na mume wake akaanza kazi ya kumbembeleza, lakinia lifanya hivyoa hukua kimnyanyua, akamlazimisha mpaka wakaingia bafuni. Alimuacha huko kwa sekunde mbili kisha akaruidi na kunikuta hata sijishughulishi.
“Vaa uondoke, usinifanye nizine na mke leo. Ukinifanyia hivyo sitakuja kukusamehe na dunai utaiiona chungu!” Aliongea kwa hasira huku akinishika, ailinminyanyua kwa nguvu, alikua na hasira sana na isingekua hali ya pale basi angenipiga sana na kuniumiza. Basi sikua na namna, nilivaa na kuondoka,yeye alienda bafuni kumsaidia mke wake. Nilitoka nnje na kwakua kila mtu alikua bize na msiba hakuna mtu aliyenishtukizia.
****
Baada ya mazishi wafanyakazi wengi waliondoka, walibaki wachache tu hasa wal waajiriwa wakudumu. Mimi niliondoka lakini sikukaa sana nyumbani, nilimuambia Mama kutoka na msiba sisi wachache tumechaguliwa kwenda kukaa kule kwani sisi hatuna kazi nyingi. Mama hakua na neno, aliniruhusu, nilienda lakini sikujichanganya na wafanyakazi wenzangu, nilikaa na watu wa kawaida. Ilipofika kwenye saa tano usiku hivi nilianza kumtumia meseji Bosi wangu kuwa nipo pale hivyo anitafute kwani nataka kuonana naye.
Lakini hakunijibu, alinipuuza. Nilijipenyeza mpaka nikaingia ndani, nikawa karibu na mke wake. Wakati huo alishaingia chumbani kwake lakini alikua katika hali mbaya hivyo ndugu wawili waliingia kukaa naye, mimi pia nilipenyeza hivyo tukawa 3watatu. Nilipoona kuwa Bosi wangu ahjibu meseji zangu nilipiga picha nikiwa chumbani kwake bila wale kujua, nikamtumia na kumuambia, niko chumbani kwako na mke wako nimuonyeshe picha zetu za Dar?
Nilimtumia meseji nikijua lazima atapaniki, sikua na picha zozote za Dar lakini kwa hali aliyokua nayo mke wake nilijua kabisa kuwa kama anaamini nina picha za uchi, na k3wa tukio la mchana ataamini kuwa naweza kumuonyesha mke wake na kwa hali ile basi anaweza kufa kwa presha. Haikuisha dkaika tano alikua pale chumbani, alinisalimia na kujifanya kama ndiyo ananioana.
“Kumbe umekuja Binti, nashukuru sana. Anna huyu ni mfanyakazi wetu pale ofisini, naona mshajuana…” Alinitambulisha kwa shemeji yake, mdogo wake na mke wake, hata hawakumjibu.
“Njoo kwanza huku nnje, wafanyakazi wenzako wanakuhitaji.” Aliniambia nilijua kuwa amenielewa hivyo nilitoka zangu mpaka nnje. Aliniongoza mpaka kwenye chumba kimoja hivi kilikua kama stoo, ingawa kwa kukiangalia kilikua kizuri kuliko hata nyumbani kwetu lakini kwa namna kiivyokua kimepangwa na ukilinganisha vyumba vingine katika ile nyumba moja kwa moja kwa akili za kawaida ilionekana kama ni stoo.
Kilikua kikubwa kina kitanda lakini kulikua na mabegi mabegi machafu, makochi ambayo amewekwa kwa kupandiana na kilionekana hakijafunguliwa muda mrefu, hakikua na vumbi lakini kulikua na harufu ile ya kukaa muda mrefu vila kufunguliwa na uvundo wa nguo.
“Hivi una akili kweli wewe? Mbona unataka kuniharibia familia yangu, umeiona hali ya mke wangu lakini unataka kufanya ujinga? Kwanza nani kakuambia uje kwangu, si wenzako washaondoka?”
Aliongea kwa hasira hukua kinishika kama ananivuta, alinikaba na kutaka kunipiga.
“Walioondoka ni wageni, mimi hapa ni kwangu, si ulinitembea na mimi ushanivua chup** unafikiri nina tofauti na mke wako, mimi ni kama mke wako hivyo siondoke. Anachokupa mke wako ndiyo hicho hicho ninachokua mimi hivyo siondoki mpaka unitimizie haja zangu?” Nilimaumbia huku nikimsukuma, nilikua na ujasiri wa ajabu, nilijua ananishikashika tu lakini hawezi kunipiga kwania naogopa kelele.
“Haja gani unataka kutimiziwa, niambie kama ni pesa mimi nitakupa! Niambie mshenzi mkubwa wewe, niambie unataka shilingi ngapi!?” Alikua kakasirika kweli lakini mimi nilimuona kama fala tu.
“Una akili kweli, hivi unafikiri kwetu sisi masikini kiasi hicho, mimi sina shida ya pesa, nina shida yako. Ulitembea na mimi, wewe ni mpenzi wangu, mimi ni mwanamke, nahitaji kuguswa na mwaaume, kuna miezi mingapi tangu unifanye na mpaka leo sijaguswa….”
“Huna akili wewe, nakuona umechanganyikiwa!” Alinikatisha, nilimsukuma pembeni na kuanza kuvua nguo.
“Nidyo sina akili, wakati unatembea na mimi, unanidanganya kuwa nina akili jitapata kazi ulitegemea nini, nataka tufanye mapenzi na kama ukikataa napiga kelele hapa tuone nani ataaibika. Uzuri nina ushahidi, nina picha hivyo hata ukikataa mke wako akiona basi aibu ni kwako. Mimi sina cha kupoteza kama kazi sina, sina mume na wala sina mtu hata wakuniuliza chochote hivyo nakuambia tunafanya mapenzi!”
Alidhani ni utani lakini nilifua nguo, mwanzo hakutaka kabisa lakini nilimlazimisha kumshikashika aliposisimkwa mwenyewe alifunga mpango na tuilifanya mapenzi. Alikua na hasira bado hivyo alijitahidi kufanya kwa nguvu ili kunikomoa, lakini wkangu nilipata raha ya ajabu kuliko siku ya kwanza. Kwa zaidi ya masaa mawili tulikua wote chumbani, alionekana kuwa na hamu sana kwani kila akichoka anapumzika kidogo tunaendelea, tulifanya mpaka mimi mwenyewe ndiyo niakomba poo, nikamuambia inatosha.
Baada ya hapo alianza kutoka yeye, akaangalia usalama kisha akaniruhusu kuoka.
“Unatakiwa kurudi nyumbani kwenu?” Aliniambia baada tu ya kutoka nnje, ilikua ni kama saa saba hivi, nilimuambia kuwa siwezi kuondoka pale kwakua nyumbani nilishaaga kuwa nitalala naye aliniambia kuwa siwezi kukaa pale, aliniambia ni lazima kuondoka. Aliiniambia nitoke nikatafute gest ili nilale nirudi nyumbani kesho yake, nilijua ananifukuza na hakutaka nikutane na mke wake tena. Nilimuambia usiku huo siwezi kuondoka peke yangu, alitoka pale na kumfuata dereva flani wa tax, nilikua namjua, ni dereva wake ambaye alikua akimtumia sana kwa michepuko wake, nilishachunguza kila kitu.
Basi alimuambia anichukue na kunipeleka kulala gest, kwlei nilichukuliwa na kulala huko. Kufika hata sikuoga, nilikua nimechoka sana hivyo nililala tu. Asubuhi sikuhangaika hata kwenda kazini kwani nilijua kabisa kuwa kazi nishapoteza, nilijua bosi hatataka kuniona na kwa kitu nilichomfanyia nilijua kabisa hakuna mahusiano tena. Nilishakata tamaa kutokana na uzuri wa mke wake hivyo nilitaka tu kufanya mapenzi naye hata mara ya mwisho basi niridhike.
Nilirudi nyumbani na kumuambia Mama kuwa hatuendi kwakua tulilala msibani tuna ruhusa ya wiki mbili. Alishangaa lakini ilikua ni lazima anielewe, nilifanya hivyo kwakua sikutaka kumuambia Mama moja kwa moja kuwa nimefukuzwa kazi, nilitaka kujipa muda kwanza wa kuwaza nini cha kufanya, nilijua kuwa ishu ya kazi imeisha lakini sikutaka kukata tamaa, nilishapata uzoefu wa maisha ya ofisi na kuna watu nilishawajuajua hivyo isingekua ngumu kwangu kupata ya kujitolea sehemu.
Nilirudi nyumbani na kulala mpaka mchana, baada ya hapo nilienda kumsaidia Mama. Lakini ile nafika tu, wkenye saa saba hivi meseji iliingia. Ilikua inatoka kwa Bosi wangu. “Najua umechoka lakini nataka kukuona, jioni aga unakuja msibani, Kiko (Dereva wake wa Tax) atakuja kukuchukua”. Iliishia hapo nilituma kuuliza sababu za kuniita lakini hakujibu, nilimsaidia kazi Mama huku nikiwa na wasiwasi, ingawa nilimuambia kuwa jioni wataenda wengine msibani ila nilishaitwa, nilimuambia tumeitwa tena msibani hivyo nilazima kwenda, hakua na namna aliniruhusu.
Kweli Kiko alikuja kunichukua na kunipeleka kwenye Gest ileile, nilikaa mwenyewe mule nikisubiria Bosi kama atakuja au la. Nilikua na wasiwasi sana kwani sikujua anakuja kufanya nini, kwanza nilihisi labda ana hasira za mimi kwenda kwake na kulazimishia kufanya naye mapenzi.
“Akitaka kunipiga namtishia kuhusu picha!” lakini pia nilihisi labda nataka kuja kuchukua picha zake, lakini hauikua hivyo, akiwa na mawazo sana, analia akikumbuka wanae, yaani alikua kama mtu kachanganyikiwa.
“Nashindwa kukaa hata na mke wangu, kila nikikaa naye nalia tu, yaani sijui nifanye nini kichwa changu kukaa sawa. Walikua ndiyo wanangu pekee wakiume, uzazi ulikua wa shida, nilihangaika sana kupata watoto wakiume, kwanini Mungu amewachukua wale watoto, nachanganyikiwa, au ni sababu ya umalaya wangu, au nimefanya nini?” Alikua analia kama mtoto, nilimshika na kumkumbatia huku nikimfariji, kwangu hiyo ilikua ni fursa.
“Hivi kweli mke wangu atabeba mimba nyingine kweli, nikikumbuka jinsi tulivyosumbuka kuwapata hawa watoto nachanganyikiwa!” Aliongea mambo mengi na mimi nilimsikiliza, kwangu mimi ilikua ni kama fursa, yaani niliona kama vile Mungu kanitenda mijujiza.
“Kumbe na uzuri wote ule lakini kizazi cha shida! Basi mimi nitakuzalia mpenzi wangu, yaani kama ni kizazi ninacho na nitazaa watoto wakiume!” Niliwaza huku nikitabasamu, Bosi alikua kanilalaia kifuani, angefanikiwa kunyanyua kichwa chake na kuniona jinsi nilivyokua nafurahi wakati yeye analia sijui angefanya nini?
Nikweli niikua namuonea huruma, lakini mwisho wa siku si mimi niisababisha vifo vya wanae ila niliamua kutumia tu hiyo fursa kumuweka karibu yangu. Aliongea mambo mengi lakini mwisho wa siku tulijikuta tunafanya mapenzi. Alitoka kachangamka, akanipa laki mbili na kuniambia kuwa nipumzike kipindi hiki cha msiba lakini baadaye nirudi kazini, nilishangaa kwani nilijua kazi ndiyo nishapoteza.
Wakati nikijua kuwa anataka nipumzike kumbe yeye alitaka kunitumia, kila sikua likua ananiita tunaongea tunafanya mapenzi, wiki mbili za msiba wa wanae njdiyo ilikua kazi yangu.
“Unajua sijawahi kuwa na mahusiano ya namna hii kwa mwanamke mwingine zaidi ya mke wangu?” Siku moja aliniambia, ilikua ni jioni na siku hiyo hatukukutana kama kawaida yetu kufanya mapenzi bali tulikutana na kutoka out tu.
“Kwanini, mbona una wanawake wengi sana tu?” Nilimuuliza, swai lilimkera kidogo lakini alijibu.
“Ndiyo, lakini si kama wewe, wewe ni tofauti, wmanzo nilijua umkorofi lakini sasa hivi ndiyo nakuelewa, yaani nikiwa nawewe nakuwa tofauti kabisa, nakua huru, yaani nikfanya mapenzi na wewe najiona kama nilikua kifungoni na sasa nimekua huru.” Aliniambia, aiongea maneno mengi sana kunisifia lakini sikua sawa kabisa, nilimsikiliza tu ila sura ya mkewe, ule mwili wa mke wake akiwa uchi wa mnyama mbele yangu na nikijilinganisha na mimi nilijua kabisa hakuna kitu hawezi kunipenda namna hiyo.
****
Mahusiano ya mimi na Bosi wangu yalianza kwakasi, ikawa ninwatu wakutoka kila siku, kila siku ilikua ni lazima kuonana hata kama hatufanyi chochote basi alitaka tu kuniona. Mke wake alikua bado hajaanza kutoka, alikua hajamaliza 40 ya wanae. Pamoja na kuwa na mimi lakini bado alimjali mke wake, mara nyingi mke wake akipiga simu hupokea na kuongea naye mbele yangu bila kujali kuwa nilikua naumia. Kuna siku moja nakumbuka ndiyi tulikua tunajiandaa kufanya mapenzi, mke wake alipiga simu wakati tunajiandaa kufanya mapenzi, alipokea wakaongea sijui nini mara namuona anaaga kuondoka.
Niliumia sana na kuona kuwa, sasa hivi yuko karibu na mimi kwakua mke wake ana huzuni na ni mpweke, siku mke wake akitoka ndani na kuwa sawa basi mwanaume atanikimbia. Niliumia sana na sikujua nifanye nini, kwani nisingeweza kushindana na mke wake kwa chochote kile. Lakini siku moja wakati niko Instagram nikaona tangazao kwenye ukurasa mmoja wa Instagram, basi nikakutana na mtu anaongelea kuhusu kumfunga mwanaume.
Katika maisha yangu nilikua siajwahi kuenda kwa mganga wala kuwaza hayo mambo, lakini kwa wakati huo akili yangu ilikua haifanyi kazi, nilijikuta nachukua namba ya simu ya huyo mtu nakumpigia. Nilimuambia kisa changu na kumuuliza kama anaweza kunisaidia, aliniambia nijambo rahisi tu kama nina pesa.
“Una matatizo mawili, kwanza kumfunga mwanaume ilia sione mwanamke mwingine kwakua ni malaya kama ukimuacha aendelee na umalaya wake ipos iku atakutana na mwanamke mwenye nyota kali zaidi yako na atakuacha. Lakini pii ni kumfunga mke wake, anampenda mke wake sana na kwasasa hawezi kumuacha hivyo unachotekiwa ni kumfunga mke wake ili asitoke, tunampaka kinyesi ili amchukie asimtamani ila pia tunaweza kumpiga maradhi asivuke geti, kila akivuka Geri hata kwenda msibani anaoza hata utumbo ni wewe tu.”
Aliniambia mambo mengi ambayo anaweza kufanya lakini hata sikumuamini, niliona kama ni tapeli tu. Yeye alinihakikishia kila kitu kinaenda sawa na kuniambia tuanze kwa kumfunga mwanaume ili asichepuke tena na kumpaka kinyesi mike wake. Nilikubali lakini nilimuambia kabisa kuwa mimi sitaki mambo ya kuua na hao mambo ya kumpa maradhi mke wake mimi sitaki, ninachotaka ni mwanaume anipende na kunisikiliza.
Alikubali nilimtumia pesa na yeye alinitumia dawa na kuniambia nihakikishe tu inafika nyumbani kwa mwanaume. Wakati tunafanya mapenzi akiondoka tu niinyunyuzie kwenye nguo zake za ndani na mke wake akigusa tu nguo zake za ndani au nguo za mwanaume basi kila kitu kitakua kimekamilika. Kweli nilifanya hivyo, sikuona mabadiliko yoyote, niliona kama mambo ya kawaida tu, ananijali kama mwanzo na kila kitu kiko vilevile, nilijua nimetapeliwa kwani namba ya yule mganga ilikua haipatikani tena.
Kwakua sikutoa pesa nyingi hata sikuhangaika sana kumtafuta kila siku, baada ya kuona hapatukani tu niliamua kukaa kimya. Lakini siku moja usiku, nakumbuka ilikua ni siku mbili baada ya 40 ya watoto wao, Ben alinipigia simu, ilikua ni usiku, aliniambia kuwa anataka kuonana na mimi usiku huo. ilikua ni kama saa nane usiku hivi, wakati huo nilikua bado naishi na Mama yangu hivyo ilikua ngumu kutoka, nilimuambia lakini hakuonekana kuelewa, alikua kama mtua liyechanganyikiwa.
Nilitamani kutoka sana lakini ilikua ngumu, kwangu kumuambia Mama kuwa natoka usiku huo na kwa namna nyumba tuliyokua tunaishi ilikua nilikua na uhakika kuwa Mama angejua tu. Basi nilikataa na kuzima simu, hakuniambia sbabau lakini kesho yake kazini hakunisemesha mpaka mchana. Alinaimbia tutoke, alinipeleka sehemu kwenye nyumba mpya, nyumba nzima kabisa.
“Utakua unaishi hapa, siwezi kuwa nakutafuta usiku hupatikani, kachague fenicha mjini!” Aliniambia, nilimuuliza kwaninia nafanya hivyo.
“Yule mwanamke ananichosha, sina amani, yaani nikimuona nahisi kichefuchefu, natamani hata kumchoma visu, nahitaji mtu wa kupumzika naye, nahitaji nikikorofishana na yule MBuzi niwe na sehemu ya kuja, la sivyo nitakuja kumuua, sijui kwanini lakini namchukia, namchukia sana, nataka kupumzika, nahitaji kuwa na wewe kwa uhuru!” Aliniambia, nilijikuta natabasamu huko kichwani huku usoni nikionyesha kumsikitikia, dawa ilikua imefanya kazi ila shida nilikua nawaa vipi kuhusu Mama nitamuambiaje Mama yangu nahama nyumbani, naenda wapi? Kufanya nini, kazi yenyewe sina, hilo lilinichanganya?
Ndiyo kwanza tuko Sehemu ya Pili, mambo ndiyo yanaanza mwanzo kabisaa. Kwa wale ambao wanahitaji vitabu vyangu nimerudi, ushauri ni lazima uwe umenunua Kitabu changu na baada ya hapo ndipo unawea kunipigia tukaongea. Kuhusu kuongea nina watu wengi sana sana sana, hivyo naongea kwa Appointment. Appointment zote napanga siku ya Jumapili kuanzia saa Saba Mchana mpaka saa nane mchana, zingatia muda sana kwani napanga appointment za wiki nzima na zinajaa mapema.
Naamini muda huo ni sawa hata kwa wale wanaoenda Kanisani, watu ni wengi muda ni mchache hivyo nakua sina namna, anayewahi kupiga basi ndiyo anapata, zingatia muda saa saba mpaka nane mchana hakikisha kabla ya kunipigia ushanunua Kitabu changu kama ni ushauri wa mahusiano unanunua cha mahusiani na Biashara unanunua cha Biashara.
KIGAGULA; SITAKI AFE LAKINI SITAKI AWE MKE WAKE—- SEHEMU YA TATU
Nyumba ilikua kubwa na Ben alitaka mimi kuishi pale, hakutaka niwe naenda na kurudi, hapana, alitaka mimi niishi pale kama mke wake awe anakuja anavyojisikia. Niliwaza namna ya kumuambia Mama yangu lakini nilikosa jibu, nilimuambia nitafikiria kwani ni ngumu kumuambia Mama kuwa nahama nyumbani wakati sina kazi. Hata kama ningekua na kazi kwa nilivyokua namfahamu Mama nilijua lazima atakataa.
Sikumuambia mama kuhusu kuhama, nilichokua nikikifanya ni kuaga kuwa naenda safari za kikazi kisha naenda katika nyumba mpya nakaa hata wiki basi narudi nyumbani. Ben alinipenda, alinipa kila kitu, aliacha umalaya na muda mwingi aliutumia kwangu, siku moja usiku tulikua tumelala, simu yake iliita na alipopokea alikua ni binti wa kazi.
“Mama anaumwa, hali yake ni mbaya hawezi hata kunyanyuka.” Binti alimuambia, Ben alishtuka na kunyanyuka, mimi nilikua bado nina wenge la usingizi, lakini baada ya kumuona kanyanyuka niliamka.
“Unaenda wapi usiku huu?” Ilikua ni kama saa nane usiku, nilimuuliza kwa hasira ingawa nilisikia kila kitu alichokua anaongea na binti wake wa kazi kwani simu yake ilikua na sauti kubwa.
“Wife anaumwa, nimepigiwa simu….”
“Inamaana kama anaumwa unataka uondoke saa hizi? Unajua ni saa ngapi? Hivi unajua umekuja kulala kwangu lakini bado hatujafanya mapenzi?” Nilimuuliza kwa hasira.
“Lakini huu ndiyo muda wangu wa kuondoka, si unajua kuwa sijaaga nina safari ya kikazi, ni lazima nirudi nyumbani, unafikiri nitaelewekaje?” Aliuliza. Ni kweli, pamoja na kunifanya mchepuko wa kudumu lakini hakutaka mke wake kujua, mbele ya mkewe na ndugu zake alitaka kuonekana kama malaika, alikua akimfanyia mke wake vituko lakini hakumuonyesha kama anachepuko.
Ingawa muda mwingi alikua kwangu lakini nyumbani alikua anaaga ana safari za kikazi. Siku zote ambazo hakuaga kuwa anasafari alikua akija analala anaondoka usiku, wakati mwingine hata saa kumi za usiku lakini hakulala kwangu.
“Najau, tena nilitaka kukuambia, kama umeamua kuwa na mimi sitaki mambo ya kumuogopa mke wako, wewe ni mwanaume, hata usiporudi huna sababu ya kumuaga, au unampenda mke wako kuliko mimi?” Nilimuuliza nikijua kuwa ataniambia kuwa ananipenda mimi.
Lakini hakufanya hivyo, alivaa harakaharaka bila hata kuniaga aliondoka. Nilijisikia vibaya kwani niliona kama kanidharau, kamuona mke wake ni wamaana kuliko mimi.
“Huyu mbwa dawa itakua imeisha nguvu, ninatakiwa kufanya kitu kingine, la sivyo nitampoteza!” Niliwaza kwa hasira, usiku huo sikulala kabisa. Nilikua na mawazo mengi sana na kuhisi kama ninaachwa, ilikua ni miezi mitatu tu tangu kupangishiwa nyumba lakini mwanaume nilihisi kama anabadilika.
Nilishaonja maisha mazuri sikua tayari kurudi katika umasikini, alishaniahidi vitu vingi, alishabadilisha maisha yangu kwa kiasi kuwa nilikua natumia simu ya gharama, navaa nguo nzuri nikienda dar naenda kwa ndege si basi tena na nilikua nimekodiwa Tax yangu ya kunizungusha mjini kila siku nikitaka si mambo ya kuhangaika na bodaboda au bajaji tena, nilikua napata pesa, namsaidia Mama yangu kusomesha wadogo zangu na nilimuongezea Mama yangu mtaji na kila kitu kilishaanza kwenda vizuri.
Usiku ule ulikua mzito kwangu, nilishindwa kabisa kulala, nilimpigia simu mganga wangu usiku uleule lakini simu yake ilikua haipatikani. Alikua kanipa dawa ambayo kweli ilinisaidia lakini niliona kama imeisha nguvu, nilisubiri mpaka asubuhi ndipo nikampigia akapatikana.
“Tatizo lako wewe unataka tu matokeo, hujatoa chochote unataka mume, dawa ile ilikua ni ya kumvuta, kuvuta moyo wake na kumchafua mke wake, sasa hivi nunahitaji dawa ya kumshika awe wakwako. Unahitaji kuja huku, hakikisha unakuja mapema kwani sasa hivi mke wake anaumwa, kama ukiwahi basi hatapona kabisa!”
Aliniambia mambo mengi ambayo anaweza kunifanyia, mimi nlichokua nahitaji ni kuzidi kumtengeneza mwanaume ili aendelea kunipa pesa, kwa wakati huo sikua nawaza sana kuhusu ndoa kwani niliona kabisa ni kitu ambacho hakiwezekani. Kwanza nilimuona mtu mzima, mimi bado nilikua kijana, nilikua bado sitaki ndoa, nilihitaji mtoto sawa lakini si ndoa na kuwa na mtu wa kunibanabana. Pili nilikua najua ana ndoa ya kanisani hivyo ni ngumu kuvunjika, mimi nilihitaji tu kumchuna basi.
Asubuhi sikuhitaji kuaga nyumbani kwani tayari walijua nipo safarini, nilipanda gari na kuanza safari ya kwenda dar. Mwanaume sikumtafuta wala sikutaka kujua hali ya mke wake, nilikua na wasiwasi sana kuwa labda dawa yangu imeisha nguvu ndiyo maana ile ondoka yake ya usiku ilinichanganya. Huko nyuma alikua kama kachanganyikiwa juu yangu hivyo nilihisi kuna kitu.
Ilikua ni mara yangu ya kwanza kukutana na huyo mganga, kazi yangu ya kwanza ilikua ni kumtafuta, haikua ngumu sana kwani alikua akiishi mjini kabisa, si sana, alikua akiishi maeneo ya Tandika. Alinielekeza tu nikachukua Boaboda kisha akaja kunipokea. Tofauti na nilivyodhani kuwa atakua ni mzee, labda kavaa kihasarahasara hali ilikua tofauti.
Alikua ni mtu mzima lakini si sana, nyumba yake ilikua ni nzuri lakini kulikua kumejaa watu wengi, walionekana ni wagonjwa, wengi walikua ni mabinti wa dogo kama mimi na wamama watu wazima, hakukua na mwanaume hata mmoja niliyemuona pale. Alikuja kunipokea yeye mwenyewe kisha tukaingia moja kwa moja mpaka ndani. Wengine waliniangalia kwa dharau, nahisi walikasirika kuwa sikupanga fioleni.
Lakini mimi sikujali, niliingia ndani, sebule ilikua nzuri tu, ilikua ya kawaida, hakukua na watu sebuleni, aliniingiza mpaka kwenye chumba cha kawaida, hakikua na kitu chochote.
“Kaa hapo.” Aliniambia huku akinionyesha kuwa nilikua natakiwa kukaa chini, nilikaa kwa wasiwasi, hakukua na kitu, chumba kilikua cheupe, chini kulikua na zulia jeupe, ukuta na paa kila kitu kilikua cheupe kisafi, nilikaa kwa wasiwasi kwani niliona kuwa alikua tofauti na waganga wengine ambao ukifika unakutana na makorokocho mengi.
“Hatujawahi kuonana?” Aliniuliza.
“Ndiyuo, ndiyo mara yangu ya kwanza, nilikupigia tu simu ukanitumia dawa, imenisaida sana lakini juzi nilitishika kidogo ndiyo nikakupigia ukaniambia nije.” Nilimuambia.
“Vua nguo.” Aliniambia, nilianza kutetemeka kwani nilihisi kama vile na bakwa, nilikua na wasiwasi, aliniangalia kisha akacheka.
“Unaogopa, mdogo wangu, nikitaka kuwabaka nitabaka wangapi, unaowaona wote hapo nnje shida yao ni moja wanataka kuwatuliza wanaume, wote wanashida kama yako na ni wazuri. Sina muda wa kupoeza vua nguo baki kama ulivyozaliwa!” Aliniambia, hakua na maneno mengi, hakua na vitu vingi, aliongea kuwa anamaanisha.
Nilivua nguo na kubaki kama nilivyozaliwa, hakuongea kitu chochote, hakushtuka na hakiuonyesha hata kujali kwamba niko pale ni mwanamke niliyevua nguo niko uchi mbele yake. Baada ya kuvua niliona anatoa wembe kwenye mfuko wake, alinisogelea na kunilaza chali, alinipanua miguu, nilikua naogopa natetemeaka kuwa anaweza kunibaka lakini yeye hakujali, alikua na haraka zake alifanya kazi yake tu.
“Acha kujitingisha nitakukata na kidonda chake hakiponi!” Aliniambia, huku akinishika sehemu zangu za siri na kuanza kunichanja, sikusikia maumivu yoyote lakini niliona wembe na kuhisi wembe ukigusa mwili wangu, baada ya kuweka chele mkama hamisni hivi alichukua dawa flani kwenye kori lake na kunipaka. Wakiati huo nilikua na wasiwasi kuwa kaniachia alama, nilikua nikiwaza kuwa nikilala na mwanaume si atajua kuwa nina lama nimechanjwa.
Lakini ni kama alikua ananiosoma akili yangu, alinitoa wasiwasi aliniambia.
“Usiogope, ukifika nyumbani hata wewe hutajua kama uliwahi kuchanjwa.” Aliniambia, kisha akanishika mkono na kuninyanyua.
“Vaa nguo, kisha aondoka, malipo yangu utatuma ukifanikisha.” Aliniambia, nilivaa nguo bado nikiwa siamini kama hicho ndiyo kilinitoa Mwanza na kunileta mpaka Dar.
“Ndiyo dawa imeisha? Hakuna kitu kingine?” Nilimuuliza.
“Hapana, wewe nenda, ukirudi ongea naye, fanya naye mapenzi atakusikiliza kulikoa navyomsikiliza Mama yake mzazi.” Aliniambia, nilitoka na mtu mwingine akaingia, nilitembea taratibu mpaka nnje, wakati natoka nilisimama kuangalia Bajaji au Bodaboda ili kuondoka eneo lile kwani ilikua ni mjini kabisa kila ukitoka mtu anajua unatoka kwamganga na aina ya Mganga mwenyewe ilijulikana ni mambo ya mahusiano tu.
Nilisimama kama dakika kumi hivi vila kupata usafiri, nilitamani kutembea kwa miguu lakini nilikua kama naogopa hivi. Wakati nimesimama pale kuna gari moja ilikuja na kusimama pembeni yangu.
“Twende nikusogeze…” Ilisikika sauri ya kike, kuangalia ni yule dada ambaye nilipishana naye, wakati mimi natoka kwa mganga yeye alikua anaingia. Sikua nikimjua lakini kwa aibu ya macho ya watu niliingia kwenye gari.
Ukimya ulitawala kidogo kisha akaanzisha yeye mazungumzo.
“Ndoa hizi zinashida, mimi mume wangu kuna mtu kamshikilia, bila huyu Baba nisingeweza kumkomboa.” Alianza kuongea, nilinyamaza kimya kwani sikua na chakumjibu.
“Yeye kaja kwaajili ya mume wake mimi nimekuja kwaajili ya mume wa mtu!” Nilijisemea kichwani.
“Sasa hivi nimemdhibiti yaani hakurupuki, kawa kama zezeta, huyu Baba ni kiboko.” Aliendelea kuongea, alikua anaongea sana anaongea mambo yake, kwakifupi alikua ni mbea, mimi sikumuambia chochote, nilishindwa cha kumuambia.
“Wewe umekuja kumchukulia dawa nani? Unataka kumnasa nani? Ni mume wako au ni danga?” Aliniuliza, nilibabaika kujibu, lakini kabla ya kujibu aliendelea.
“Binti mdogo kama wewe ndoa ishaanza kuleta matatizo, wanaume bwana. Mdogo wangu, ukishamtuliza huyo mwanaume tafuta amani kwingine, mimi nimekuja hapa si kwaajili ya mume wangu, kuna mzee nataka amsahau mke wake, anapesa ni balaa, nitamchuna mpaka abaki na ngozi!” Nilipata kaamani kidogo kuwa na yeye ni mdangaji kama mimi.
Nilimuambia mimi ni mume wangu na ametekwa nyota ka Mama mtu mzima, alinipa pole na kuniambia kama nimefika kwa huyo Baba basi kila kitu kitakua sawa. Alikua anaongea sana kiasi cha kuniboa, tulipofika sehemu ambaopo naona kabisa naweza kupata usafiri nilimuambia nimefika. Wakati naondoka aliniomba namba yangu ya simu, alitaka tuwe marafiki, nilimpa lakini nilijua tu kuwa sitawezana naye, anaongea sana na mimi si mtu wa kihivyo, nilishuka na kuondoka zangu.
****
Mke wake alikua amedondoak bafuni nguvu zilikua zimemuishia, kwa miezi miwili ntyuma alikua akiumwa, alikua anapata siku zake kila siku, yaani kila siku alikua na heshi, damu zilikua zikimtoka ukeni hivyo kushidnwa kufanya mapenzi kabisa na mume wake, kwangu hiyo ilikua ni neema kwani mume wake alimchukia, hakutaka kuwa karibu na yeye na mara nyingi akichelewa kama mke akilalamika alikua anamuambia kuwa hana sababu ya kurudi nyumbani wakati kila siku alikua ni mtu wa pedi tu.
Aliingia chumbani saa 12 jioni, alikua amemaliza kupika chakula cha usiku na alimuambia binti wa kazi kuwa anaenda kuoga. Basi binti wa kazi alisubiri na kusubiri, mpaka saa nne usiku Mama alikua bado hajatoka, alihisi labda kalala na kwakua akilala hataki kusumbuliwa basi aliamua kumtengea chakula na kuendelea kumsubiri kama atatoka.
Binti wa kazi alikua anaangalia TV sebuleni na watoto walishalala, alipitiwa na usingizi na kuja kushtuka ilikua ni kwenye mida ya saa nane hivi. Aliangalia mezani na kukuta chakula bado hakijaguswa, hapo ndipo alishtuka na kutoka kwenda kumuangalia. Alimuangalia chumbani hakumkuta, lakinia lisikia maji yanamwagika bafuni, alienda na kugonga lakini hakusikia kitu , aliamua kufungua ndipo alimkuta Mama kalala sakafuni.
Alikua uchi wa mnyama, ameshikilia sabuni mkononi, maji yalikua yanamwagika yanaingia kwenye tundo la kupitishia maji, lakini si maji tu, uilionekana kuwa damu nazo zilikua zinamvuja, kulikua na damu nyingine zilikua zimeaganda kwa pembeni ikionyesha kuwa damu nyingi zilikua zinamtoka, lakini si hivyo tub ado damu kidogokidogo zilikua zimanmtoka mke wake sehemu za siri.
Kuona vile alichukua khanga na kumfunika, akachukua sumu ndipo alimpigia Ben ambaye alienda na kumkuta mke wake hana fahamu. Ben alimchukua mke wake na kumpeleka hospitalini, ambapo alipatiwa huduma ya kwanza ingawa hawakujua sababu ni nini? Alikuja kuzinduka asubuhi, damu zilikua hazitoki sana ingawa yalikua yanatoka matonematone.
Asubuhi baada ya kuona mke wake kazinduka Ben lainitafuta ili kuniomba msamaha kwakuondoka bila kusikilizana. Wakati huo nilikua kweneye gari na safari yangu ya kwenda Dar, alipoga simu lakini sikumpokelea, aliiga kama mara tatu hivi ila sikupokea. Baada ya hapo aliacha na hakunipigia tena mpaka nafika dar naenda kwa mganga natoka hajapiga. Kitu hicho kiliniumiza sana na kuzidi kunipa hasira kwani niliona kama kaniacha, niliona kama kanidharau kitu ambacho kilinipa moto wa kwenda kwa mganga.
Niliporudi nilienda kazini kama kawaida, yeye alikua anakuja kazini, tunaonana lakini haniambii chochote, alionekana kuwa bize na familia kwania likua anakuja anakaa kidogo anaondoka.
“Ana matatizo gani huyu?” Nilimuuliza Janeth,rafiki yangu ambaye alikua ni mbea sana pale kaszini anajua kila kitu.
“Mke wake anaumwa, yaani yule mwanamke tangu kufiwa na wanae hajakua sawa kabisa. Kila sikua naumwa, nimeambiwa kuwa anatokwa tu damu!” Aliniambia, wakati huo nilikua sijaongea naye kitu chochote, alinipa umbea kuhusu mke wa Bosi akiwa hajui kama mimi ndiyo sababu ya kila kitu, mwisho aliniboa kwani mambo mengi aliyokua akiniambia nilishaambiwa na mume wake tukiwa chumbani.
Siku mbili zilipita bila kunisamesha chochote, nilihisi kuchanganyikiwa, nilimpigia mganga na kumuelezea kila kitu.
“Hakikisha unafanya naye mapenzi, dawa haiwezi kufanya kazi bila kufanya naye mapenzi, kua makini, huyo mwanamke wake damu ikikatika basi jua na wewe unakatika!” Aliniambia na kukata simu bila kuniambia alikua anamaanisha nini kuhusu mimi kukatika.
Nilihisi kuchanganyikiwa kwakweli, nilipaniki nikijua kukatika alikokua anazungumzia ilikua ni kufa. Wakati naongea na Mganga wangu kwenye gari na bosi naye alikua anatoka. Aliingia kwenye gari yake, nilishindwa kujizuia na kumfuata, hakua kwenye gari ya kazini, alitumia gari binafsi, basi niliingia na kukaa siri ya mbele.
“Kwanini umenichunia, wewe ndiyuo umenikosea lakini umenichunia.” Nilimuuliza huku nikijifanya kujinunisha.
“Sitaki upumbavu wako, mke wangu anaumwa, hali yake ni mbaya, naweza kumpoteza mama wa watoto wangu halafu unaniletea ujinga hapa natakiwa kufanya mpango, anasafirishwa kwenda Muhimbili, shuka sitaki ujinga ujinga wako!” Aliniambia kwa hasira, nilijua mambo yameisha, alikua tofauti kabisa, sijui nini kilitokea lakini nilihisi kuwa nampoteza muda si mrefu.
Kuona vile nilianza kuvua nguo palepale wkenye gari, ilikua hata bado haijaondoka ipo kwenye parking za Benki.
“Nataka tufanye mapenzi, hapaha, narudi siti ya nyuma, gari yako ni Tinted, kama hatufanyi basi napiga kelele!” Nilimuambia, nilikua nimepagawa kabisa. Nilikua namuamini sana mganga na niliamini kama nikifanya naye mapenzi basi hawezi kuniacha lakini kama nilivyoambiwa nikiacha kufanya naye mapenzi mke wake atapona ndipo nimekatika sikua tayari kwa hilo.
“Acha ujinga, nitakutandika makofi na kukushusha hapa mshenzi mkubwa wewe, acha kunichanganya kabsia!” Aliniambia, niliendelea kuvua nguo na kubaki kama nilivyozaliwa, nilikua nimeka siti ya mbele, ingawa vioo vilikua ni Tinted lakini kioo cha mbele kilikua cha kawaida, mtu yoyote angeweza kuona.
Nilijua ataona aibu, alichukua nguo yangu akanifunika na kuniambia kuwa twenda nyumbani kwangu.
“Alikua na hasira, nilva tu nguo ya juu lakini chini sikuvaa kitu, mpaka tunaingia getini, niliingia hivyo hivyo, kufika ndani tu alinivamia na kuanza kufanya mapenzi na mimi. Alikua akifanya kwa hasira kama vile ananikomoa lakini mimi nilikua nafuraha kuwa dawa yangu inafanya kazi. Baada ya kumaliza nilimuona kapoa, hana hasira wala haraka tena kama mwanzoni.
Mara simu yake iliita, aliiipokea na kuanza kuongea.
“Mama shikamooo….” Alianza kwa kusalimia.
“Nakuja Mama, nipe muda kuna vitu namalizia kazini hapa nakuja.” Alikata simu ksiha kunigeukia, akaniambia kuwa alikua ni Mama yake anaongea naye.
“Mama yupo, nataka kumuona, nataka tuende wote.” Nilijikuta namuambia, sikua na nia ya kumuona Mama yake lakini nilitaka kupima kama dawa imeanza kufanya kazi au la, nilijua kuwa kwa akili zake asingeruhusu upuuzi kama huo lakini kwa dawa angekubali.
“Sawa lakini sasa hivi wameshajiandaa, tunaenda Dar na mke wangu, sasa huoni kama itakua shida. Tushakata tiketi za ndege, tunachelewa.
“Kwahiyo unataka kwenda Dar na kuniacha mimi hapa?” Nilimuuliza.
“ndiyo, nampeleka mke wang….”
“Sitaki, kama ni kuondoka tunaondoka wote na nataka kwenda kumuona Mama yako….” Nilimuambia kwa hasira, bado sikua na imani kama dawa imeingia vizuri hivyo niliona kama nikimuacha akaondoka mwenyewe mapenzi yangeweza kurudi kwa mke wake. Alitaka kunigomea lakini tulilumbana sana, mpaka anatoka nilitoka na kuingia kwenye gari kilazima.
Tulifika mpaka nyumbani kwake ambapo ile nashuka kwenye gari nataka kuingia tu nikakutana na Mama yake ambaye alikua anatoka nnje kuangalia kama Ben karudi au la.
“Huyu ni nani?” Mama yake aliuliza kabla hata ya salamu.
“Shikamoo Mama…” Nilimsalimia huku nikitaka kumpa mkono lakini aliukataa.
“Benard huyu ni nani na anafanya nini hapa?” Alimuuliza mwanae kwa hasira.
“NImfanyakazi mwenzangu nilitaka amsindikiza mke wangu….”
“Una akili kweli, hivi unafikiri nimezaliwa jana, huyu mwanamke si mtaki, simtaki kabisa, hivi mwanangu ndiyo washakutengeneza kiasi hicho! Huyu binti simtaki!”
“Lakini Mama hata humjui, ndiyo umemuona hapa hii leo!” Mama yake alinisogelea kwa karibu na kuniangalia machoni.
“Haya macho nilishayaona na si mazuri kabisa, mwanangu, simtaki kabisa huyu mwanamke hapa kwangu. Wakati sisi tunaangaliana Ben anatafuta kitu cha kuongea yule Mama aliingia ndani kwa kukimbia, alitoka baada ya sekunde chache lakini sasa alitoka na Pochi yake. Alinisogelea, akaingiza mkono kwenye pochi na kutoa chupa ndogo ya maji.
Alitoa maji na kumwagia kwenye mikono yake kisha akanimwagia.
“Hii sura niliiona jana wakati nasali usiku, mwanangu huyu si mtu, ndiyo maana nakuambia uwe unatembea na maji ya Baraka, mizigo kama hii usingebeba, binti ondoka, rudi ulipotoka hii nyumba inalindwa na Damu ya Yesu!” aliongea huku akiendelea kunimwagia yale maji.
Ushauri ni lazima uwe umenunua Kitabu changu na baada ya hapo ndipo unawea kunipigia tukaongea. Kuhusu kuongea nina watu wengi sana sana sana, hivyo naongea kwa Appointment. Appointment zote napanga siku ya Jumapili kuanzia saa Saba Mchana mpaka saa nane mchana, zingatia muda sana kwani napanga appointment za wiki nzima na zinajaa mapema.
Naamini muda huo ni sawa hata kwa wale wanaoenda Kanisani, watu ni wengi muda ni mchache hivyo nakua sina namna, anayewahi kupiga basi ndiyo anapata, zingatia muda saa saba mpaka nane mchana hakikisha kabla ya kunipigia ushanunua Kitabu changu kama ni ushauri wa mahusiano unanunua cha mahusiani na Biashara unanunua cha Biashara.
KIGAGULA; SITAKI AFE LAKINI SITAKI AWE MKE WAKE—- SEHEMU YA NNE.
Nilijua mambo yameharibika, baada ya yule Mama kuanza kufanya ulokole wake wakati kimi nina dawa mpya mwilini nilihisi nitaumbuka. Sikutaka kukaa pale, nilitoka nikikimbia kwenda nnje huku nikipiga kelele za kulalamika kuwa naitw mchawi, nilitoka mpaka nnje kabisa ya Geti nikisikilizia kama Ben atatoka na kuja kuungana na mimi, lakini hakutoka, nilimsikia anazozana na Mama yake.
“Umenitia aibu sana Mama, hivi unajau kuwa yule ni nani?” Alikua analalamika.
“Unamuita tu mchawi binti wa watu, hata humjui unaanza kumwagia mimajimaji yako tu!” Aliongea wka hasia.
“Kwahiyo unanifokea?” Mama yake alimuuliza.
“Ndiyo nakufokea, acha kuingilia maisha yangu, yaani kila kitu ninachokifanya unajifanya unajua. Kwanza nani kakuambia uje hapa, mke wangu anaumwa, nataka kumhudumia lakini unanibanabana, kila sehemu unataka tuwe wote! Nishakua mtu mzima Mama, sitaki kuongozana na wewe kila sehemu, siaki kupangiwa maisha na wewe!” Ben alimfokea Mama yake, alilalamika mambo mengu kuhusu Mama yake na namna anavyoingilia maisha yake.
Mimi kule nnje nilianza kucheka kwa fuaha nikijua kuwa dawa imeingia.
“Wewe ni mwanangu, nilikuzaa mimi na nitaendelea kuhakikisha unakua kwenye mstarai. Huyo binti simjui lakini nilishamuota mara nyingi, nilishamuona mara nyingi na mwisho wenu si mzuri! Mimi ni Mama siwezi kukaa kimya nikiona mwanangua naharibikiwa. Mke wako kalala hajitambui, badala ya kuja kuhangaika naye unahangaika na huyo mwanamke, umetoka kufanya nini huko, si ulienda kushughulikia usafiuiri, muda woe huo ulikua unafanya nini mpaka tunapigiwa simu kuwa hakuna kitu umefanya!
Nimesema mimi ni Mama yako, na kama unafikiri nitakuacha upotee kwakua sasa hivi umajiona umekua, una kazi nzuri na ndiyo unanihudumia basi sahau. Nitapambana na kila kitu, iwe nguvu ya kichawi au binadamu, ya kishetrani au kuzimu nitapambana kukulinda. Najua huna aimani, unaniona nimechanganyikiwa lakini….”
“Mama nimechoka na maneno maneno yako! Sisi tunaondoka na sitaki kukuona Dar kwa mke wangu, niachie familia yangu, kwanini unahangaika hangaika na mke wangu. Kila mke wangu akiumwa unakuja kwangu, unakuja kufanya nini? Ulikuja kuwachukua wanangu sijui mkakae kijijini huko, mimi nilikua sitaki lakini wanatoka kwako wanarudi wamepata ajali na sasa hivi hawapo tena! Sitaki uingilie maisha yangu….”
“Unasema nini mwanangu? Unataka kuniambia mimi ndiyo nimewaua wanao?” Mama yake alimkatisha na kumuuliza, sauti ilikua na msisitizo lakini alionyesha kwua na uchungu. Hata mimi nilijisikia vibaya kwani kwa alivyokua anaongea Ben ni kama alikua anamuambia Mama yake ndiyo anasababisha maatizo katika maisha yake.
“Hivyo hivyo ulivyosiokia, wanangu walikau salama nyumbani kwangu, lakini ukang’ang’aia unataka kuwaona wajukuu. Ile ilikua ajali gani watoto wadogo, unajifanya kuokoka kila sehemu na maji maji yako hayuo unayaita ya Baraka lakini hakuna lolote!
Tangu mke wako atoke kwako kijijini maisha yangu yameharibika, ametoka huko kapoteza watoto wawili, kila siku ni kuumwa, mke wangu ananuka kama maiti, sasa hivi anatyoa damu kial siku na uzee huo badala kuka akijijini kuhangaika umekuja hapa. Umekuja kufana nuni? Ukiulizwa umekuja kufanya nini kama si uchawi huo?” Nilitamani kuingia ndani na kumuambia Ben muache Mama yako.
Pamoja na kumtaka na usheani wangu mwingi lakini namna alivyokua anaongea na Mama yake iliniumiza sana, nilijisikia vibaya huku nikimuwaza Mama yangu, namna ailivyohangaika na mimi halafu mtu amuongeleshee maneno mabaya namna hiyo. Sijui nilipata wapi ujasiri, lakini niliingia na kumshika Ben.
“Bosi, hayo si maneno ya kuongea na Mama yako, hapana, kanikose alakini si maneno ya kuongea na Mama yako.” Nilimuambia huku nikimvuta kutaka kumtoa nnje.
“Acha unafiki, unajifanya kunitetea, huyu ni mwanangu, namjau, najua hizi si akili zake, kama unafikiri nitapumzika kwasababu ya mwanangu kuniita mchawi basi sahau. Narudia nakujua wewe binti, nimeshakuona mara nyingi, usijifanye mnafiki kunitetea kwakua mwanangu kanitukana, narudia namjua Benin a nakujua wewe! Toka nyumbani kwangu kabla sijakuharibuharibu an damu ya Yesu! Yule Mama aliongea, alionyesha ishara ya msalaba, akatoa kabibilia kadogo na kufungua, akaanza kukasoma, akachukua tena maji ya Baraka na kunimwagia.
Nilijihisi kutetemeka, nguvu zilianza kuniishia, nikajua nashindwa nguvu, nikatoka tena, lakini sikufika mbali, nilitembea kidogo nikadondoka. Sikua nimepoteza fahamu, Ben alikuja na kunisaidia kunyanyuka akaniingiz akwneye gari na kuondoka.
“Mam ayangu ni mchawi, huwezi kushindana naye, unaona anataka kumuua mke wangu, najua tu anataka kumuua mke wangu!” Ben aliniambia, nilikua sina namna, niliona yule Mama ni tishio hivy nililazimika kukubaliana naye.
“Hata mimi naona mpenzi, yaani alivyonisogelea nilihisi kama nabanwa pumzi, nilikua naona maruweruwe, naona picha ya mtu kashika kisu kikubwa anataka kunichoma nacho. Hapana aisee, nhimemuogopa sana Mama yako, mimi kama maisha yenyewe ndiyo haya bora tuachane, sitaki kufanywa kama mke wako, hivi mimi sina hata mtoto, nikianza heshi ya kila siku damu si nitachanganyikiwa?” Niliongea huku nikilazimisha machozi kutoka ingaw ailikua ngumu kwa machozi kutoka.
***
Wao walitangulia kwenda Dar, mimi nilienda siku inayofuata. Ben aliniambia anataka kuwa karibu na Mimi kwani alikaua nahisi kuwa akika ambali na mimi kuna kitu kibaya kinaweza kunitokea. Ingawa walishukia kwa Baba yake mdogo lakini nilipofika tu alikuja kwenye Hoteli niliyokuepo tukaendelea namambo yetu. Hali ya mke wake ilikua bado ni mbaya, alifanyiwa vipimo lakini haukuonekana ugonjwa wowote, kila kitu kilikua sawa hata madaktari walikua hawajui kuwa ni nini?
Tulikaa kama siku nne hivi, alitakiwa kurudi kazini na bado hali ya mke wake ilikua ni Mbaya.
“Mimi nadhani mngejaribu kuenjeji, najua huamini sana mambo hayo lakini sitaki umpoteze mke wako, ukifiwa na mke utachanganyikiwa, nilikuona kipindi unaomboleza vifo vya wanao, hapana, wale watoto nao ni wadogo, wanamhitaji sana Mama yao, jaribu kienjeji.” Nilimuambia, nilikua nataka kumteka akili, nilikua najua kilichotokea kwa mke wake hivyo nilitaka kujifanya kama vile namsaidia ili kuzidi kumuona mwema.
Kwa wakati huo alikua anaamini kuwa Mama yake ni mchawi na anahusika katika kuwaua watoto wake na pengine anataka kumuua mke wake. Mama yake alikua ananiona mimi mchawi na nilikua na uhakika kuwa ipo siku ataniumbua, niliona ni nafasi yangu kujisafisha.
“Hapana, hayo mambo sitaki kabisa yaingie akilini mwangu, ukishaanza umeanza.mambo ya kutoana sadaka ndiyo siyapendi, hapana, mimi naona tuhangaike hivihivi, maamini atapona.” Aliniambia, nilijua hofu yake ya kwenda kwa mganga ilikua ni mamboa ya kuambiwa labda mtoe mwanao au ndugu yako.
“Hakuna kitu kama hicho, mimi Shangazi yangu aliumwa, alihanagika sana hospitalini, wakamuambia kuwa maini yake yameoza, akahangaika sana lakini kuna Kaka mmoja akamsiadia, hakuna matunguli, hakuna kuloga na hakuna chochote. Naamini ni dawa za asili, kuna watu wamepewa karama ya kutibu, huna haja ya kuogopa kuna Kaka naongea naye uende ukamuone. Huna hata haja ya kummtoa mke wako hospitalini, hakuan haja ya ramli wala nini?
Niliongea naye kumshawishi, aliposikia hivyoa likubali, wakati huo tayari nilishaongea na Mganga wangu akaniandalia dawa. Niliondoka na kurudi kwake, tukafika na kuingia wote, Ben alishangaa kuona mazingira ya pale, hayakua mazingira ya Mganga. Tulifika katika chumba kilekile na kutuambia tukae, tulikaa. Ben akaanza kuelezea tatizo la mke wake kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
“Mimio sipigi ramli ila kuwa makini sana na Mama yako, anaweza asiwe mchawi lakini kuna watu wengine wana mikosi yao, kila wanachokigusa kinapotea. Shika hii dawa kampake mke wako tumboni na sehemu za siri, kesho ataamka na utamleta, njooni njie watatu.” Alimuambia, hatukukaa hata dakiak 10, hakutaka pesa alitoa tu dawa tena ya kupaka, wakati tunaondoka hata Ben alikua anadhangaa ni mganga gani wa namna ile, alihisi labda ni uongeo, mimi nilimuambia afanye kama alivyoambiwa ili kuona kama mke wake atapona au la.
Aliondoka na kwenda kufanya hivyo, baada ya kumpaka alirudi kwangu, sisituliendelea na mambo yetu. Asubuhi alipigiwa simu kuwa mke wake kaamka, hai yake ni nzuri hivy oanataka kuonana na mimi. Alirudka kitandani kwa furaha, alinikumbatia na kunishukuru, akanisifia sana.
“Wewe ni mwanamke wa kipekee, yaani nilidhani kuwa labda kwakua tuko pamoja utamchukia mke wangu kumbe wapi, nashukuru sana, wewe ni mwanamke wa kipekee na ajabu sana.” Alinikumbatia kwa nguvu mpaka nikaanza kukosa pumzi, nilimtoa kifuani kwangu na kumuambia tunatakiwa kwend a kumuona mke wake na kwenda naye kwa mganga ili dawa ifanye kazi vizuri.
Tulijiandaa na kuondoka, wakati tunafika alikua amesharuhusiwa kutoka alikua na baadhi ya ndugu. Ndugu waliponiona walikasirika, nilihisi labda walishaambiwa na Mama yake kuhusu mimi, lakini sikujali, mke wake aliponiona alinisalimia, akanikumbatia kwani alikua ananikumbuka.
“Sijakuona tena baada ya msiba?” Aliniuliza, siku ya msiba nilikua karibu naye sana nikijifanya kumsaidia kumbe nilikua namchunguza.
“Kazi tu dada yangu, pole kwa kuugua.” Nilizuga, walitaka kupandakwenye Gari la baba yake mdogo lakini Ben alikataa, alimuambia mkewe kuwa kuna sehemu anataka kumpeleka.
Ndugu walishangaa lakini alishaamua aliwaambia kuwa anahitaji kuwa na mke wake alichukua Tax na tukaingia watatu akiwaacha ndugu zake wakishangaa tu.
“Huyu Dada ndiyo kakusaidia, ungekufa!” Ben bila kuulizwa alianza kuelezea.
“Kivipi?” Mke wake ambaye alikua bado anashangaa na ile ondoka ondoka ya harakaharaka aliuliza.
“Utajua mbeleni, wewe mshukuru, sijui kwanini lakini wanataka kutumaliza.” Alimuambia, wakati huohuo simu ya Ben iliita, mke wake ndiyo alikua kaishikilia, kwani tulipoingia tu kwenye gari alitoa simu zake mfukoni, moja akawa anaitumia na nyingine akawa kashikilia mke wake.
“Mama!” Alimuambia huku akitaka kuipokea.
“Acha usipokee simu ya huyo wmanamke!” Aliongea kwa hasira huku akionyoosha mkono nakumuonyeshea ishara ili asipokee.
“Kwanini labda atakua anataka kujua kuwa naendeleaje…” Mke wake alimuambia hukua kitaka kuipokea. Utakufa wewe, kashajua umetoka hospitainiu anataka afanye uchawi wake, acha. Ben aliongea kwa hasira hukua kiipiga ile simu ili tu asiipokee. Mke wake alishanaga na kuuliza maswali mengi lakini hakupata majibu.
“Sitaki tu uongee na Mama, hayo mambo mengine utakuja kujua baadaye lakini sitaki!” Aliongea kwa hasira, tulifika mpaka kwa Mganga, tayari nilishampigia simu hivyo ingawa tulikuta foleni kubwa lakini alitufuata na kutuingiza ndani.
Tuliingia wote, alitukaribisha na kumuambia Mke wa Ben kuvua nguo, ya juu, Mbele ya beni nambele yangu, alisita kidogo lakini Ben alimuambia kfufanya hivyo. Basi baada ya kuvua alimchanja kidoho kifuani na tumboni, akampaka dawa kisha akawa kamaliza. Akaturuhusu kuondoka na kutuambia kuwa yeye kashamaliza kazi yake ya kutoa dawa kazi iliyokua imebaki ni ya Mungu ambayo ni kazi ya kutibu.
“Kua makini sana na Mama mkwe wako!” Alimuambia bile kusema sababu yoyote. Tuliondoka, mke wake alikua anajisikia vizuri, njia nzima waliongea, alimrudisha kwa Baba mdogo na siku ile alilala huko. Usiku mimi sikulala labida, nilikua na wasiwasi sijui ni dawa gani kapewa, tangu kuja pale alikua analala na mimi nhalafu ghafla anaenda kulala na mkewe, nilimpigia Mganga na kumuuliza akaniambia nisiwe na wasiwasi ndio wanaagana hivyo.
****
Ushoga ulianza na mke wake, aliniamini kuliko mtu mwingine yoyote, kila kitu tukaanza kufanya pamoja na mara nyingi nilikua kwake. Alikua hana kawaida ya kuja kazini kumuona mume wake lakini alianza kuja na akija ni lazima kuniita tnakaa ndani hata nusu saa. Kwa wakati huo mimi bado nilikua naendelea na mahusiano na mume wake, aliijua mpaka familia yangu, akawa rafiki na Mama yangu na mara nyingi nilikua nikienda kulala kwake.
Usiku mume wake alikua antoka tunalala wote bila yeye kujua. Alikua na duka kubwa, nilimuunganishia mdogo wangu ndiyo akawa anauza. Maisha yake niliyamiliki mimi, si hivyo tu, sikua naficha tena kuhusu kuhcepuka, nadhani mke wake ndiyo peke alikua hajui. Mke waka alikua anafanya kazi lakini alikuja tu kuacha bila sababu yoyote, duka alilokua anasimamia alimuachia mdogo wangu ambaye alikua anauza ila mimi ndiyo nilikua nasimamia kila kitu.
Mwanzume alininunulia Gari mbili za kutembelea, Harrier Moja na IST New Model moja. Mama yangu alijua kuwa nipo na yule mwanaume lakini kwakua nilikua nikisaidiwa pesa hakusema kitu chochote. Mwanzo alinisihi kuacha lakini mwisho alizoea tukawa kitu kimoja. Kazini nako mambo yalikua ni moto, mimi ndiyo nilikua kial kitu, bosi alikua akinisikiliza hata kwenye mambo ambayo hayanihusu.
Wafanyakazi wenzangu walikasirika, wakawa wananichukia lakini mimi sikujali. Nilichokua nikiangalia mimi nikuwa nilikua natengeneza pesa basi.
“Mwanangu, mimi ndiyuo nilikuleta hapa, nakuchukulia kama mwanangu, siwezi kuingilia maisha yako lakini hembu punguza kasi, unachofanya si sawa umeingilia ndoa ya watu na sasa umeingilia kazi, huyu hapa kaajiriwa, akiharibu tu ni dakika mbili wanamundoa.” Siku moja yule Baba ambaye alinitafutia kazi ya kujitolea pale aliniita ofisini kwake kuongea. Aliongea maneno mengi sana lakini hata sikujali, nilimsikiliza mpaka mwisho kisha nikamuambia.
“Kama unampenda Bosi mchukue, mbona na wenzako wengi tu wanaolewa, mwanaume mtu mzima unakua na kiherehere namna hiyo!” Nilimjibu kisha nikatoka zangu. Nilitoka nikiwa na hasira kwani nilihisi kama anaingilia maisha yangu. Jionio nilienda kumsalimai Mama kwani nilikua siishi naye tena, nilimkuta ana mawazo, nikamuuliza nini tatizo ndiopo aliniambia kuwa yule Baba aliyenitafutia kazi alikuja kumuona na kumuambia mambo mengi sana.
“Mwanangu kama unayuofanya ni kweli basi kuna sababu za kuacha, haya maisha pesa zinaafutwa, wewe bado binti mdopgo sana, acha kuharibu maisha yako kwasababu ya pesa.” Mama aliniambia, alikua anajua kuhusu mimi kutembea na Bosi wangu na ukaribu wangu kwake lakini hakujua kama nimeanza kuingilia na kazi, nimemteka bosi wangu hasikii chochote.
“Watu wanasema kuwa uanaenda kwa waganga na wewe mwenyewe ndiyo unatangaza!”
“Hivi unaju kuwa yule Baba aliw3ahi kunitongoza na kuna siku alitaka kunibaka kwenye gari yake?” Niliamua kudanganya baada ya kuona kuwa maneno ya yule Baba yanamuingia Mama yangu. Mama alinisikiliza lakini hakuonekana kuniamini, sikutaka kukaa pale niliona ananichanganya, niliaga na kuondoka zangu.
Kipindi hicho nilikua sina mganga mmoja, nilikua na waganga ziadi ya watatu kwani kila ukienda sehemu moja unakuta dawa inapungua nguvu ukiulizia unasikia kuna mtu flani ni kiboko basi unaenda. Niliamua kwenda kwa Mganga mwingine ambaye alikua kaibu palepale mwanza kuongea kuhusu yule Baba, nilimuambia kuwa ananisumbua an anaaka kuingilia maisha yangu.
Basi alinipa dawa flani na kumuambia kuwa nihakikishe kuwa hiyo dawa namuwekea ofisini kwake na anaikalia. Basi nilichukau ile dawa na kwenda ofisini kwake, nilivizia asubuhi kabisa na kuinyunyizia kwenye kiti chake. Nilikua namuangalia mpaka anaingia akaikalia kabisa, nikajua kuwa mambo yameisha, nimeshamuweza na nitamfunga mdomo mazima, sikujua ilikua inafanya nini lakini niliamini kuwa haitakua kwani mganga wangu tunafahaiana na nilishamuambia kuwa siwezi kuua.
Baada ya kama nusu saa hivi yule Baba aliniita ofisini kwake, alikau amekaa kwenye kiti kama zoba, ananiangalia tu, alikua hawezi kunyanyuka ana anapumau kwa shida. Aliniomba nimchukullie kabegi kake kadogo ambako kalikua pembeni tu ya meza lakini hakuweza kukachukua. Basi nilichukua, akaniambia nifungue nimtoelee flashi yake, nilifungua nakuingiza mkono kupapasa, nilipapasa mpaka niliposhika kitu kama flash.
Nikakitoa ili kumpa, lakini ila kuangalia haikua flash, uilikua ni hirizi, nilishtuka na kuiachia lakini haikudondoka. Nilihisi mwili kutetemeka kama kupigwa ganzi vile, nahisi kizunguzungu. Ghafla namuona yule Baba anasimama, yuko vizuri kabisa ananioangalia, nilikua siwezi hata kunyanyua kidole, alinishika nakunikalisha kwenye kiti hcake kisha akaniambia.
“Binti usidhani mpaka kufikia nafasi hii hapa kazini ni kazi ya Mungu, hapana, Mungu ana nafasi yake ila wengine tuna ulinzi binafsi, mimi huniwezi, huu unga uliomwaga hapa mimi nasongea ugali nyumbani kwangu!”
INTERVIEW NA AJIRA; Hiki ni Kitabu changu kipya ambacho kinazungumzia mambo ya AJIRA. Kina maelezo kuanzia namna ya kuandika Barua ya kuomba kazi, kuandika CV kujiandaa na usahili. Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kwenye Usahili na namna ya kuyajibu, namna ya kutengeneza Connection za kiajira na namna ya kutumia mitandao kupata ajira.
KIGAGULA; SITAKI AFE LAKINI SITAKI AWE MKE WAKE—- SEHEMU YA TANO.
Kichwa kilianza kuniuma, niliishiwa nguvu na kuegemea kwenye kile kitu.
“Baba umefanya nini?” Nilimuuliza huku nikijaribu kunyanyuka lakini nilishindwa, miguu ilikua haina nguvu kabisa na nilikua nikiongea kwa shida. Yule Baba hakunijibu, alitoka nnje na kuita mlinzi ambaye alikua anapita.
“Huyu binti atakua anaumwa, kaingia hapa kunisalimia naona kadondoka, hembu ita watu waje kumuangalia.” Alimuambia mlinzi ambaye alikimbia kuita watu kisha yeye akaudi na kunifuata kwenye kiti.
Aliniinamia na kuniangalia usoni, alinikodoela macho alichukua mkono wake wa kulia na kunishika kiunoni, alinifinya kwa nguvu sana, nilisikia Kaaaa! Kulikua nikama kitu kinavunjika.
“Nimekuona muda mrefu, unamfanyia Bosi wetu vituko na mambo yako nakuangalia. Lakini sasa hivi umevuka mipaka, umeingilia na kazi, sijawahi kufanya kazi na Bosi mpuuzi kama huyu! Kama utafanya ujinga akihamishwa au akifukuzwa basi tutashindwa kupiga madili yetu. Utaondoka na hutarudi tena hapa, nimeamua kukusamehe kwakua namheshimu sana Mama yako la sivyo usingevuka kisingiti cha mlango wa kuingia nyumbani kwenu leo!”
Aliongea kwa sauti ya chini lakini iliyojaa umakini na hasira.nilikua katika maumivu makali lakini nilishindwa kabisa kupiga kelele, sauti haikutoka kabisa. Aliniachia kwani watu walishakuja, ghafla nilianza kujisikia vizuri, kichwa kilikua chepesi tena, nilirudi kama kawaida,a kili zilinirudia. Nilitaka kunyanyuka kuondoka lakini nilikua siwezi, ile nanyanyuka tu kiuno kilianza kuuma. Nilisikia maumivu makali sana kiunoni, nilikua nahisi kama kiuno kimekatika kimelegea.
Nilijitahidi hivyo hivyo lakini nilishindwa, nilijikuta nadondoka mpaka chini, watu walinishika na kuninyanyua.
“Unaumwa wapi?” Waliniulza.
“Kiuno, kiuno kinauma sana!” Niliongea kwa hasira huku nikijaribu kunyanyuka tena, lakini nilishindwa, maumivu yalizidi mara mbili yake.
“Huyo mtoeni nnje atajisikia vizuri, nyie hamuoni kuwa humu ndani hakuna heawa! Mtoeani akapete hewa!” Yule Baba (Mzee Masumi) walininyanyua na kunitoa nnje, walinikalisha chini na kunilaza kwenye majani huku wakinipepea. Lakini ile nafika nnje tu nilianza kujisikia vizuri.
Mwili ulipata nguvu na nilipjaribu kunyanyuka niliweza, nilirudi katika hali yangu ya kawaida kabisa, huwezi amini yaani ni kama ile asubuhi wakati naingia kazini.
“Nilinyanyuka na kuanza kutembea, waliokua wamenibeba walishangaa kwani sekunde chache nyuma nilikua siwezi hata kusimama.
“Niko vizuri niacheni.” Niliongea kwa ukali kidogo kwani nilitaka kuingia ndani kurudi kuendelea na kazi wakati wao walikua wananiambia bado naumwa hivyo nipumzike kwanza sehemu yenye hewa.
“Si nimekuambia unaiche, mbona na wewe unakua na kiherehere namna hiyo!” Nilimuambia Kaka mmoja ambaye alijitahidi kunishika. Nilikua namuona kama kituko, wakati nakuja pale naanza kazi alinitongoza na nilikula vila vyake sana, nilikua bado sijamkubalia, nilikua na mpango huo na kwa wakati huo nilikua namuona wa maana. Kwangu ilikua ni kama fahari flani kutongozwa naye, lakini wiki hiyo hiyo kabla sijamalizana naye ndipo nikatongozwa na Bosi.
Ingawa yeye alikua ni kijana na labda ishu ya ndoa ingeweza kuja lakini nilizama haraka kwa bosi na yeye nilianza kumdharau. Pamoja na kuja kujua kuwa natembea na Bosi lakini bado alikua akijipendekeza kwangu, kuhangaika akiamini ipo siku nitakua wake. Kwangu mimi nilishamsahau akili yangu yote ilikua kwa bosi. Ile kunishika nilihisi kichefuchefu, nilimsukumia pembeni na kuingia kurudi ndani.
“Msikilize mwenzako, rudi kakae nnje na ukapumzike kwenu kabsia.” Mzee Masumi ambaye alikua kama ananifuatilia aliniambia, lakini sikumjali, nilimjua ni mchawi kanizidi dawa kwa siku hiyo lakini sikua namuogopa.
“Niko sawa wewe kaendelee kusonga ugali wako huko huko kwenu!” Nilimuambia, nilikua nakumbuaka maneno yake ya dharau ambayo alikua ananaimbia kipindi ameona dawa zangu, niliamini kinga nilizokua nazo zimenisaidia ndiyo maana nimesimama na kuushinda uchawi wake.
Niliingia mpaka ndani, lakini ile navuka mlango, sijapiga hatia hata mbili nilidondoka tena, kiuno tena kikaanza kuniuma nikashindwa hata kunyanyuka. Watu walikuja wakanibeba tena mpaka nnje, nilipofika nnje nikapata nafuu tena, nikataka kunyanyuka, lakini Mzee Masumi, alinifuata pale chini.
“Binti, wewe ni mtoto mdogo sana, najua una kinga, una hirizi kiunoni umeivaa na chupi, nishaivunja mwanangu. Nimekaumbia ningekumaliza lakini namheshimu sana Mama yako, ni Muisalamu safi kabisa, sasa nakuambia, ondoka, huwezi kuingia tena kwenye hii ofisi. Ujinga wako kafanyie huko huko na watu wengine, siwezi kufa masikini kwaajili yako, ukivuka tu ule mlango wa kuingilia ofisini wewe ni maumivu tu!”
Aliongea kisha akanyanyuka, alienda na kumuita Kaka mmoja ambaye alikua ni mfanyakazi pale.
“Wewe si unajua kuendesha?” Alimuuliza.
“Ndiyo.”
“Basi chukua Gari yangu mpeleke nyumbani, anahitaji kupumzika, kesho atarudi huyu leo kachoka.” Alimuambia, nilimtuma rafiki yangu kunichukulia pochi yangu, nikachukua lakini niligoma kupanda gari yake, nilikua niko sawa kabisa natembea mwenyewe. Mzee Masumi aliniangalia mpaka nikapotelea. Niliondoka nikiwa na hasira sana huku nikiwaza ni kitu gani kimeokea, niliangalia ile Benki kwa uchungu sana kwani niliona kama maisha yangu yanarudi kwenye umasikini.
****
Hakuna dhambi kubwa kama kukata tamaa, kwangu umasikini ilikua ni laana na sikua tayari kuurudia. Baada ya kutoka pale Benki nilianza kufanya mawasiliano. Unapokua mshirikina una mambo ya waganga ni ngumu sana kuwa na Mganga wa aina moja, unapaswa kuwa nao wengi kwani mganga ni kama ma daktari, kila mmoja ana utaalamu wake, kila mmoja ana sehemu amabyo amebobea.
Pamoja na kwamba madaktari wote wanatibu lakini ukimtafuta Daktaei wa meno na kumaumbia afanye oparesheni ya Kichwa utaua mgonjwa. Daktari Bingwa wa moyo hawezi ngoa jino, wa Macho hawezi tibu moyo, hivyo hivyo kwa waganga. Kuna ambao ni maalumu kwa mapenzi, ukienda kwake bwana ishi ya kumshika mwanaume au mwanamke ni dakika mbili, kuna ambao wapo kwenye kuua, kuna ambao wanaliga kulemaza watu, kuna ambao wataalamu wa kutoa mashetani.
Kuna wa aina nyingi, ukienda kwa mganga mara moja absi utawajua. Katika zile foleni za kusubiria kutibiwa kuna yale maongezi na wagonjwa flani, basi utasikia wanase, kuna mmoja uko sehemu flani, kama unataka kittu flani basi nenda sehemu flani yaani mnapeana connection huko huko hivyo ukiwa una shida basi unamtafuta. Baada ya lile tukio nilijua kabisa kuwa nipo kwenye vita, nilienda kwa Mganga mmoja nikamuambia amsome nyote yule mzee akaniambia kuwa hamuwezi.
Lakini sikukata tamaa, nilihangaika kutafuta dawa ya kupamba na naye kwa miezi mitatu bila mafanikio. Wakati wote huo bado nilikua naendeleza mahusiano na Ben, aliniambia kuhusu kazi nikamuambia sitaki kufanya kazi za kujitolea hivyo anipe mtaji ili nifungue Duka langu kwani nataka kujiajiri. Nilimuambia huku nikivuta muda nikiwaza namna ya kupambana na Mzee Masumi.
Nilitaka nimuache lakini nilijua kuwa ni lazima ataniharibia, alikua anajua mambo yengu mengi na nilikua na wasiwasi kuwa anaweza kuniharibia mapenzi, alishaniharibia kazini na nilimuona kama mtu mbaya, ili mimi kufanikiwa ilikua ni lazima kupambana naye kwanza. Basi nilihangaika kwenda kwa waganga, naelekezwa huyu naenda ila hakuna cha maana, mwisho nikamkumbuka shoga yangu Mama Patrick (sio jina lake halisi)
Kama mnakumbuke yule Mama muongeaji ambaye alinipa lifti siku ya kwanza natoka kwa mganga. Alishanipigia simu mara nyingi lakini kusema kweli nilikua sitaki mazoea naye kabisa, alikua anaongea sana, sikutaka anijue wala jue Mambo yangu. Lakini kwakua nilikua nimekwama sina namna ilinibidi kumtafuta. Nilimuambia shida yangu akaanza kucheka, mwanzo nilihisi ananicheka ila mwisho akaja kuniambia.
“Yaaani hicho ndiyo cha kukuhangaisha, nina mtu wangu ni dakika mbili tu anamaliza huyo Mzeee!” Aliniambia.
“Mimi sitaki kummaliza, sitaki kumuua, sitaki hiyo dhambi mimi ni Muisalamu, ninachotaka mimi ni kumkomesha, kumuondoa pale kazini.” Nilimuelewesha, alizidi kucheka kana kwamba ananishangaa.
“Nani kakuambia kuwa anaua, mimi mwenyewe kuu siwezi, nianchosema unamaliza unamfanyia kama mume wangu. Mimi mume wangu mwezi wa sita huu yuko kitandani, amelala kapooza upande mmoja kajilalia kama mzoga.” Alianza kunielezea.
“Mama maisha haya ni furaha yako, katika hangaika hangaika zangu nimfanikiwa kupata Mzungu shoga yangu, nimemshikiliza na kumshikilia. Bai Baba Patrick alivyoona simjali si ndiyo akaacha umalaya, akajua nina mtu akaanza kunichunguza, wakati huo Mzungu wangu penzi limekolea, huwezi amini shoga yangu yaani nakuambia, huyu mzungu sijampa chochopte lakini ananipenda kama nini, ananipa pesa nikikohoa tu pesa. Najenmga sasa hivi, kaninunulia gari na Biashara kanifungulia.
Basi mume wangu kelele nyingi anataka kumharibia basi nikasikua habari za mtu ambaye anaweza akumtuliza. Nimempiga jicho moja tu Mume wangu kadondoka, kapooza ni mwezi wa sita yuko nyumbani, Mama yake kaja kumuuguza mimi nakula maisha na Mzungu!” Alinielezea jinsi alivyomfanya mume wake akapooza, hawezi kunyanyuka wala kufanya chochote ili tu asimfuatilie na kumharibia kwa Mzungu wake.
“Kama umemchoka si ungemuacha, kulikua na haja gani ya kumfanyia hivyo?” Hata mimi nilimshangaa, alikua ni mume wake Baba wa watoto wake, nilishangaa ni kwanini asingemuacha kama anampenda sana huyo Mzungu.
“Nimuache ili iweje, Mzungu huyu mpitaji, huko kwao ana ndoa, na sina mpango wa kuishi ulaya mimi, anamaliza mkataba mwakani narudi kwa mume wangu tunaendeleza maisha. Nimuue mume wangu halafu Mzungu anaondoka sina hata mwanaume, na uzee huu nani atanioa, wanaume wote nilionao waume za watu, haya mambo ya kuhangaika kutafuta mume mwingine nani anataka. Mume wangu nampenda, nimempuuzisha tu kwa muda wakati natengeneza maisha!”
Kwa namna alivyokua anaongea ni kama kitu alichokua kakifanya ni kizuri, alikua anajivunia na kujiona wamaana kuwa hakumuua mume wake wala kumuach a bali alimpa ulemavu. Ingawa Mganga alimuambia kuwa akitaka kutegua mume wake atarudi kawaid lakini nilijiuliz a vipi mganga akifa, vipi kama ikishindikana? Sikupata majibu, lakini haikua kazi yangu, hata mimi nilikua na matatizo yangu hivyo nilihitaji msaada wake.
“Kun amtaalamu yuko Same, huko Upareni, sehemu moja inaitwa Makanya, Shoga yangu huyo ni kiboko. Yaani huna mambo ya kuweka dawa, sijui kuoga stend bali ni jicho lako tu. Ukamuangalia mbaya wako ukamkazia macho, unanuia tu unataka nini kimtokee basi kesho yake unasikia kimemtokea, namuaminia, yaani hana masharti kabisa na unalipa ukifanikiwa.” Aliniambia, kwangu umbali haikua tatizo kwani nilishaenda maeno mengi kwaajili ya waganga hivyo sikuona shida.
Nilimkatia tiketi ya ndege na mimi nikakata tukakutana Moshi, safari ya Same ilianza, kwakua yehye alikua ni mwenyeji ashaenda mara nyingi haikuwa shida sana. Ilikua ni sehemu ya ndani sana, kutoka hiyo Makanya yenyewe mpaka alipokua anaishi huyo Babu Bajaji ni elfu 15, ni ndani, yaani yuko sehemu kajitenga ni kama ana kamsiru kake. Ana vinyumba vyake vingi vya majani vimezunguka nyumba yake kubwa ambayo nayo ni ya majani ila ni kubwa.
Ukifika huko kwanza tu ile unaingia basi unapelekwa wkenye kanyumba kamooja, wote mnaambiwa kuvua nguo na kubaki uchi. Mnakalishwa chini, yaani mnaweza kukalishwa hata watu saaba, baada ya hapo watoto wa yule Baba ambaye ndiyo mganga wanakuja, watoto wawili wakiume wanakuja na kuanza kuwaogesha wote. Nawaita watoto kwani sihdani kama washafikisha hata miaka 20, wanawaogesha bila kujali kama ni mwanaume au mwanamke wote mnakaa sehemu moja kila mtu ana shida zake.
Lengo la huko kuogeshwa ni ili kila mtu kuacha mabalaa na kila kitu chake hapo. Kama umetupiwa kitu basi unaacha hapo na unapoenda kwa Mganga mwenyewe basi unakua mzima kabisa. Mkishamaliza hapo basi mnaenda kuotesha dawa, wao wanaita “Kuchimbia Dawa” hii sio kuchimba dawa kama tulivyozoea hapana, ni kuchimbaia. Basi mnachukuliwa kundi lilelile mnapelekwa mpaka kwenye kijumba kimoja wapo, kila kijumba kina maana yake na kina aina yake ya dawa.
Basi mkifika mnavua viatu, mnabaki peku, mnaingia mnaambiwa kila mmoja avue nguo tena na kujisaidia. Hiyo sehemu ukifika haina harufu lakini imejaa vinyesi, tena vingine unaona kabisa vibichi, yaani unafika hapo, unapanga mstari unaonyeshwa sehemu ya kujisaidia. Tena kw ampangilio, yaani sehemu uliyoonyeshwa ndiyo hiyo hiyo, vimejipanga kama matofali na unafanya hivyo wale watoto wakikuangalia.
Kila mtu anafanya na kila mtu ana shida zake hivyo hakuna anayejali, nilikua naona kinya a nataka kuacha lakini Mama Patrich alinipa moyo, yeye alishazoea na wala alikua hajali hakuhitaji maelezo.
“Mimi sijisikii haja kubwa…” Nilimuambia Mama Patrick kwa kumnong’onyeza.
“Hakuna shida, wewe chuchumaa utaona unashusha kichuguu kama si mlima!” Aliniambia huku akinisitiza kufanya haraka kwani kulikua na foleni ndefu. Basi nilivua nguo, niakchuchumaa kama nilivyoelekezwa, kweli haikuchukau sekunde tano nilishatoa mlima wa kinyesi, nikamaliza na kuondoka zangu.
Baada ya hapo sasa ilikua nifuleni ya kumuona Manga, kulikua na watu wengi, tulikaa pale kwa mganga siku tatu, tunasubiria zamu yetu. Katika kipindi chote hicho tulikua tunakual chakula kilichokua kinapikwa pale na hatukutoa hata shilingi kumi. Yeye hupokea pesa pale tu unapofanikiwa usipofanikiwa hutumi chochote ila ukifanikiwa basi utatoa zawadi kutokana na mafanikio yako.
Siku ya tatu ndipo tulifanikiwa kumuona Mganga, kama waganga wengine tu alikau sehemu chafu, kuna matunguli matunguli, nilimuelezea shida zangu akanipa kibuyu na kuniambia nitaje jina la yule Mzee mara tatu. Nililitaja lakini nilipomaliza tu nilimuona ananza kutetemea, anashika shingo kama vile anakabwa, alihanagika sana, anaweweseka. Akapandisha na amshetani, sasa wakaanza kuongea kilugha ambacho sikijuai, alikua kama anapigana, anakwepa ngumi, anatukana, yaani mambo kibao.
Aliendelea kupambana na hayo mambo mpaka unamuona anachoka, damu zinamtoka mdomoni na puani lakini haachi. Nilijikuta naogopa kwani kwa uzoefu wangu nilijua kabisa kuwa alikua anapambana na mashetani ya Mzee Masumi. Kile kibutu wakati ananipa alikua kakifungua, alinipa kwa mkono wa kulia huku mfuniko wake wa kitu kama gunzi hivi alikua kaushikilia kwa mkono wa kushoto basi katyika kupambana kule nilimuona anahangaika kukifunga kile kibuyo.
Yaani ni kama kuna mtu anashika mikono yake na kuanza kuivuta pembeni, anavuta mpaka basi, alihangaika mpaka akakifunga. Alipokifunga tu kila kitu kilisimama, aliacha kupiga kelele, damu zilikauka na akawa yuko vizuri kabisa.
“Mama, huyu mtu kweli alikuonea huruma, angeaka kukuoa kwa wewe ambaye huna kinga yoyote akikohoa tu anamaliza ukoo wenu mzima. Lakini tushamalizana naye, nimemfungia hapa na unaweza kumfanya chohote unachotaka, siku ukitaka kumfungua basi njoo.”
Aliniambia huku akinionyesha kile kibuyu kilichofungwa, baadaye alikichukua na kukieweka sehemu kama kwenyekabati hivi ambapo kulikua na vibuyu vingi vidogo vidogo kama kile. Baada ya kukifungia alimuita mke wake, ambaye alikuja.
“Nenda kawape dawa hawa, wapeleke namba 7” Alimuamia mke wake, tulinyanyuka tukaongozana na yule Mama mpaka kwenye kanyumba kengine. Hakkua na namba, alikafungua nah aka kalikua na harufu kali, ilikua ni mchana lakini kachumba kalikua na giza sana kiasi hatukuona ndani.
Mkononi alikua kashikilia Tochi kubwa zaile za solar, aliiwasha. Kalikua ni kachumba kama kale amba;po sisi tulienda kujisaidia utofauti wake ni kuwa, haka kalikua kamejaa sana, hakuna hata sehemu ya kuweka mguu. Kalikua kamejaa vinyesi ambavyo vimekauka sana.
“Okota kimoja.” Yule Mama aliniambia, nilimgeukua kwa mshanagao, nilitaka kumuuliza “Una akili kweli wewe Mama, yaani unataka niokote Mavi ya mtu mwingine!” Lakini Mama Paqtrick alinikata jicho huku akinifinya kana kwamba ananiambia kuwa sitakiwi kuongea chochopote. Sikua na namna, niliokota kama nilivyoamriwa, nikaokota kinyesi kimoja kilichokua kimekauka basi nikampa yule Mama.
Tukaongoza mpaka kwenye kanyumba kengine, akaanza kukitwanga mpaka kikawa unga kabisa, baada ya hapo alichanganya na dawa flani kisha akatupa na kuniambia niwe nakunywa kila sikua subuhi nachanganya kijiko komoja cha chai.
“Usichuje, weka kwenye kikombe na hakikisha unatafuna yale machicha kwa siku saba. Ukishamaliza basi mtafute mbaya wako, muangalie machoni kwa kumkazia jicho kisha nuia kitu ambacho unataka kimtokee. Hii dawa haiui, sisi hatuui bali tunatela ulemavu, ukitaka aktwe mkoni, awe taahira, awe kipofu basi ni wewe. Kama ukichoka na ukitaka kumsamehe bais ni lazima uudi ili kibuyu chake kivunjwe la sivyo atabaki hivyo milele!”
Aliongea huku akinikabidhi ile dawa, niliwaza kunywa kinyesi cha mtu mwingine ambaye hata simjui. Niliichukua lakini sikupanga kuinywa, wakati tunarudi Mama Patrick alikua ananisisitiza sana kuinywa.
“Ushakunywa dawa ngapi, hivi unafikiria hizo dawa zinatengenezwaje, unapewa tu unga unakunywa, mbona hii cha mtoto! Kuna sehemu nitakupeleka hapo ndiyo balaa. Hembu kunywa acha utoto, na kwa taarifa yako ukiacha mambo yanakugeukia!” aliniambia, nilijikuta natishika.
Nilirudi nyumbani nikiwa na mawazo sana, nilikua sijapaa muafaka kama ninywe ile dawa au la. Lakini siku ile narudi nilimpigia Ben kumuambia kuwa nimerudi kwani nilimuambia nimeenda kijijini kuna rafiki yangu kafiwa hivyo network ni ya shida. Lakini siku hakupokea yeye, alipokea mke wake, ilikua ni usiku kwenye saa mbili hivi.
“Una shida gani?” Aliniuliza. Kwanza nilishangaa kwani haikua kawaida yake, mke wake alikua akiniheshimu na kuniogopa, hata nikipiga simu kwa mume wake saa nane usiku alikua haongei kitu, alishakua kigagula changu sasa nashangaa ananijibu hivi.
“Naaka kuongea na mwenye simu.” Nilmjibu kwa utaratibu kabisa.
“Hataki kuongea na wewe ndiyo maana amenipa simu nikuambie kuwa acha kumsumbua, acha kabisa kumsumbua na unampigia ili nini, wewe si kazi umefukuzwa, sasa mambo ya kuhangaika na mume wangu kila siku ni nini? Au kwakua ulimpeleka kwa waganga wako ndiyo unaona kuwa unaweza kufanya chochote! Kaa mbali kabisa na mume wangu mshenzi mkubwa wewe!” Aliongea kwa hasira na kukata simu, nilishangaa nikahisi kuwa labda Ben alisahau simu nyumbani na mke wake kaichukua tu.
Niliamua kumpigia simu kwenye namba yake ambayo ilikua ni namba yetu, ni mimi pekee nilikua naijua, nilijua kuwa, kama hayuko nyumbani basi itaita na atapokea lakini kama yuko nyumbani haitaita kwani anaizimaga. Nilipgiga na iliita kweli, alipokea.
“Afadhali umepokea kwani nimepiga simu yako ile nyingine na mke wako kapokea, sijui kama umeisahau nyumbani?” Nilimuuliza kwabashasha.
“Wewe Kigagula, hembu ukiambiwa k0ma basi koma! Mume wangu hataki kuongea na wewe! Hakutaki!” Alikua ni mke wake tena, kabla sijajibu chochote.
“Huyu malaya wako haelewi, hembu ongea naye muambia asistusumbue….”
KIGAGULA; SITAKI AFE LAKINI SITAKI AWE MKE WAKE—- SEHEMU YA SITA.
Hasira zilinipenda, mwili mzima ulikua unatetemeka baada ya kumaliza kuongea na mke wake. Akili yangu yote ilihamia kwa mzee Masumi, nilijua tu kuwa yeye ndiyo sababu ya kila kitu. Nilitamani kwenda kwake siku ile na kumfanyia kitu kibaya lakini sikua na nguvu hizo. Bado nilikua sijanywa dawa na nikikumbuka namna ile dawa ilivyotengenezwa kusema kweli nilijihisi kuchanganyikiwa zaidi, kunywa kinyesi cha binadamu mwingine kwangu ilikua shida zaidi.
Nilikaa mpaka asubuhi bila kupata usingizi, akili nyangu ilikau inawaza kurudi katika umasikini ambao nilikua nimeshauacha kwa muda. Asubuhi ilifika nikiwa macho, niliamka nikiwa sina pawenda, asubuhi Mama Patrick alinipigia, alikua ananikumbusha kuhusu kunyw adawa huku akiniambia kama sitakunywa basi mambo yangu yataanza kuharibika taratibu, nilimuambia tayari yashaanza kuharibika na kumuambia kile kilichotokea.
“Sasa usipoangalia hata wewe utaanza kuumwa!” Alinitisha, sikumsikiliza sana, kwakua nilikua na dawa za waganga wengine nilaimua kuzitumia hizo kwanza. Sikua tayari kula mavi, kuna dawa moja ambayo nilipewa kwaajili ya Ben na nilikua bado sijaitumia kwani wakatyi huo mambo yalikua mazuri tu. Changamoto ilikua ni dawa ya kuweka kwenye chakula, hivyo nilitakiwa kumpata Ben.
Asubuhi nilisubiri mpaka wakati najua kuwa kashaenda kasini ndipo nilimpigia. Alipokea lakini si kama kawaida yake ambapo hupokea kimapenzi.
“Unasema nini?” Aliniuliza kwa hasira.
“Jamani, hata bila Salamu…” Nilimuambia kama natania lakini hata hakusubiri niongeze neno, alikata simu tena alikua hapokei. Nilimtumia meseji nyingi za kumuuliza tatizo ni nini lakini hakujibu hata moja, nilijipa moyo kuwa labda yuko bize sana hivyo akiwa free atanitafuta lakini haikua hivyo.
Siku hiyo ilipita, lakini kesho yake mchana alituma Dereva kuja kuchukua magari yake, nilizidi kuchanganyikiwa, alikua kanihonga magari lakini kadi alikua nazo yeye na zilikua na majina yake. Akanipigia simu na kuniambia kuwa, nifanye mpango wa kuhama. Kwangu ilikua kama ndoto flani, nilijua kabisa kuwa mambo yameumana an halikua kosa langu bali ilikua kazi ya Mzee Masumi.
Kwa hasira nilienda kuchemsah maji, nikapika chai kisha nikachanganya na ile dawa, niliinywa ile dawa kama nilivyoagizwa, siku nilipomaliza sikutaka kusubiri. Nilienda moja kwa Mzee Masumi. Nilienda asubuhi kabisa muda ambao najau kuwa ndiyo anatoka nyumbani kwenda kazini. Nilisimama nnje, niaksubviri ule wakati anatoka kuingia kwenye gari lake ndipo niligonga geti, nilikua nimekaa kwa nnje nchungulia kwenye mwanya wa geri ili kuona kilichokua kinaendelea ndani.
Nilipogonga alikuja mwenyew ekunifungulia.
“Nani?” Aliuliza huku akifungua geti, alipofungua tu macho yetu yaligongana, sikutaka kumpa mdua afanye mambo yake kwani nilijua nayeye ni mtalaamu.
“Kiharusi, nataka ashindwe kunyanyuka wala kuongea!” nilinuia huku nikimkazia jicho, wakati namuangalia nilimuona anaishiwa nguvu, alikua kashikilia mlango na mikono kuondoka, niliuona mdomo wake unapinda, alidondoka hini kama mgomba huku ananiangalia ananikodolea macho.
“Si ulikua unajifanya mshenzi kuwa uansongea ugali dawa zangu, basi kasongee na hii!” nilimuambia kisha nikaondoka zangu, sikutaka kuonekana pale tena.
Nilirudi nyumbani nikiwa bado siamini kama dawa yangu itafana kazi kwani nilimuona yule mzee kama vile ana nguvu kubwa kuliko mimi. Nilishasumbuka kwa waganga wengi lakini haikuweza kusaidia. Basi kurudi nyumbani nilikutana na watu, walikuja kufunga nyumba. Niliwaambia kuwa nyumba ni yangu na hawawezi kufanya chochote lakini pembeni kulikua na gari dogo, nililitambua kuwa ni gari la Ben, nilijua kuwa yupo mule ndani hivyo nilienda kwa hasira huku nikilia kwa kulalamika kuwa kwanini ananifanyia vile.
Lakini kabla ya kulifikia lile gari aliyekua ndani alishuka, alikua ni mke wake. Aliniangalia kwa hdarau bila kusema chochote.
“Unafanya nini nyumbani kwangu?” Nilimuuliza.
“”Nyumbani kwako? Hivi nyie malaya mbona mnakua hamna akili kweli? Unatembea na mume wangu, kaja kakuweka hapa kwenye nyumba yangu, nyumba ambayo tumejenga pamoja halafu anakudanganya kakupa nyumba, wakati nyumba ina majina ya wanngu, hivi una akili kweli? Umejifanya rafiki yangu kwa muda mrefu kumbe unanichukulia mume wangu, kwa taarifa yako mambo yako yote ninayo….” Alianza kuongea mambo mengi, nilimuangalia ka hasira, nikidhani bado nina nguvu nilimkodolea macho na kuanza kunuia adondoke lakini hakudondoka, alikua kasimama tu ananiangalia.
“Basi niacheni nichukue vitu vyangu!” Baada ya kushindwana na mke wake nilirudi na kutaka kuingia ndani, nilitaka kutoa vitu vyangu.
“Huna chochote humo mbwa wewe, kila kitu kilinunuliwa na mume wangu, hata chupi huondoki nayo!” Aliniambia, nilibaki nimesimama namjuangalia kwa hasira. Wakati nimesimama pale simu yake iliita, alikua ni Ben kwani baada ya kuiona tu namba aliniambia kwa dharau ngoja niongee na mume wangu. Lakini sauti yake ilibadilika ilionyesha kuwa alipokea habari mbaya.
“Yuko hospitali gani?” Aliuliza, sijui alijibiwa nini lakini baada ya kujibiwa aliondoka na kuingia kwneye gari. Alipoondoka niliongea na wale vijana kuniruhusu kuchukua nguo zangu, kama unavyojua wanaume kwa wanawake akili zao zinakua finyu hivyo waliniruhusu, sikua na shida sana na ngu bali kulikua na dawa zangu nyingi, mitego yangu mingi mule ndani ambayo nilijua kama wataiona wataniharibia.
Nilichukua kila kitu kilichochangu na kuondoka, njiani nilijaribu kumtafute Ben lakini hakupokea simu zangu. Nilipigia baadhi ya marafiki zangu kazini amabo wlainiambia kuwa yuko bize, Mzee Masumi kalawaza hospitalini na hali yake ni mbaya. Niliishia kujichekea tu nikijua kuwa watahangaika sana hospitalini, watapoteza pesa nyingi lakini hatapona kwani ugonjwa wake nilikua naujua. Nilirudi nyumbani, sikutaka kuongea na mtu, hata Mama aliponiuliza nini kilikua kimetokea sikumuambia kitu chochote. Nilikua na hasira na sikutaka kuongea na mtu yoyote.
****
Nilikua na duka lakini baada tu ya kuachika liliisha, nilishazoea matumizi makubwa hivyo nilishindwa kuliendesha, hali yangu ya maisha ilianza kuwa mbaya. Nilitaka kupumzika na mambo ya waganga lakini niliona hapana, ni lazima ni jaribu kwingine. Sikutaka kurudi same kwani nilisikia si mtaalamu sana wa mambo ya mapenzi. Nilianza kuhangaika kutafuta mtaalamu wa mambo ya mapenzi.
Siku moja nilikua naongea na Nesi flani, alikua ni arfiki yangu ingawa si sana, kuna kitu nilimsaidia kipindi flani. Basi aktika kuongea akazungumzia kuhusu mwanaume wake, hakua mwanaume mwenye hela, alikua ni mume wa mtu ila allikua anataka kumuoa.
“Atamuacha tu mke wake, kuna vitu nakamilisha nitaingia kwneye ndoa na huyo mwanamke ataachjwa!” aliniambia hukua kiongea kwa kujiamini, mimi nilijifanya mlokole kwani sikutaka kujulikana kuwa nina mambo hayo.
Kama unavyojua sisi wanawake, mtu anaokua na umbea wake basi ataongea mpaa kila mtu ajue.
“Kuna Baba mmoja, nakuambia huyo ni kiboko, yaani hata nikimtaka Raisi nampata, nikoboko!” Aliniambia, hapo alianza kunivuta, nikaaza kumdodosa kujua ni nani na anafanyafanyaje?
“Tena shoga yangu na uzuzi wako, una elimu yako lakini huna mume, nakuambia, ukikutana na huyo Baba mwanaume yoyote unayemtaka unampata! Sama tu masharti yake ndiyo shida!” Aliniambia, nilimuuliza ni masharti gani lakini hakutaka kuniambia, aliniambia kuwa kama nahitaji anipeleke niongee naye.
Kwa namna alivyokua anamsifia kwakweli sikua na namna, alinipeleka, alikua ni mganga wa mjini, yaani palepale mwanza mjini, hakua na mambo mengi kama yule Baba wa same. Tulienda mchana, akanipa dawa ya kunywa lakinia kaniambia nirudi usiku nikiwa peke yangu kwaajili ya kufanyiwa dawa. Basi, usiku nilirudi, aliiniingiza kwenye chumba kimoja hivi ambapo nilikutana na wenzangu, kulikua na watu kama kumi hivi kwenye kile chumba.
Wote walikua ni wanawake na wote walikua uchi, aliniambia nivue nguo na kubaki kama nilvyozaliwa, kusema kweli sikuona shida kwani nilishazoea mamboya waganga, kuvua nguo, kuogeshwa na kuchanjwa yalikua ni mambo ya kawaida sana. Basi nilivua, alitupaka dawa kila moja kisha akatuambia tutoke, tulitoka uchi tukawa tunatembea hakuna mtu anatuona, yaani tunapita barabarani na hakuna mt anatuona tunapishana tu na magari.
Akili zangu zilikua ziko sawa kabisa, kila mtu anaonekana yuko sawa, mganga anauelekeza njia. Tulienda mpaka Hospitali moja kubwa hivi, kufika pale alituambia kuwa, tunaenda kukusanya maiti za watoto ambao wamezaliwa kabla ya muda wao na wale wanawake aanaotoa mimba absi zilatakataka zinazotoka sisi tunakusanya. Kila mmoja alimpa mfuko wake, basi tukaingia kwenye wodi ya wazazi tunazunguka, mwanamke akijifungua tu mtoto akifia tumboni basi sisi tunamchukua na mwenye mtoto anaenda kuzika vivuli.
Lakini pia, kwenye mahosipitali mengi mara nyingi mtoto akifa kabla ya kuzaliwa huzikwa na hospitali basi sisi tunaenda kufukua makaburi na kuchukua maiti. Tulifanya zoezi hilo kwa usiku mzima na siku hiyo tulipata maiti tano. Tukarudi katika kile chumba, yeye akachukua zile maiti na mabaki ya miba kwaajili ya kutengenezea dawa, kila mmoja akavaa nguo na kuruhusiwa kuondoka kivyake.
Kesho yake ndipo nilienda kuchukua dawa, aliniambia kuwa, ili dawa ifanye kazi ni lazima kuhakikisha kuwa naonana na mhusika na kuongea naye na nihakikishe kuwa namgusa. Nilimuambia kuhusu mke wake ni mfanye nini akaniambia yeye hadhuru mtu, yeye dawa yake ni ya mapenzi tu, alinipa dawa mbili, moja ya mimi kunywa na nyingine ya kuhakikisha kuwa nampaka mwanaume wangu huku nikinuia ninataka nini kutoka kwake?
Nilirudi nikiwa na matumaini ya kufanikiwa, kuhusu kumpata na kuongea naye nilijua haina shida, nilikunywa dawa kama kawaida, ile ya kujipaka nikaweka kwenye pochio kisha nikaenda ofisini kwake. Nilijua kuwa nikimpigia simu hawezi kupokea wala kukubali kuonana na mimi, lakini kama nikienda ofisini kwake basi atakua hana namna. Anajiheshimu na ile ni Benki, ina wateja wengi wa maana hivyo akinijibu vibaya atajua nitafanya vurugu na kumharibia.
Nilienda kweli ofisini kwake, kila mtua likua ananijua na kila mtu aliniona kama mchawi, sikujua kama wanajua mambo yangu lakini nilihisi tu kwa macho yao namna walivyokua wananiangalia kwa hasira. Kusema kweli mimi sikujali kabisa, lengo langu lilikua ni kumpata Ben na nilijua nikimpata basi nitarudi pale kazini na kila mtu pale atakua chini yangu. niliingia mpaka ndani kama mteja mwingine, mlinzi alikua hajaniona kutokana na namna nilivyokua nimevaa.
Nilivaa hijabu, sikufunika uso wote lakini nilijitanda na miwani mnyeusi, nilikua na hisia tu kuwa hawanihitaji mule ndani na sikutaka kukatazwa kuingia, nilitaka kumuona kwanza. Kuna mfanyakazi alinitambua, alimshtua mlinzi ambaye alikuja.
“Da Salma habari?” Alinisalimia, tulikua tunajuana. Nilijua anataka kunaimbia nini hivyo nilimuwahi.
“Nzuri, nataka kumuona meneje, na kwa taarifa yako siondoki bila kumuona, najua haaki kuniona ila hii ni Benki, unaona wateja wote wale, hambu vuta picha nikianza kupiga kelele kuwa nina mimba ya Bosi wenu na kanitelekeza hivyo nahitaji kuonana naye?
Unajua aibu yake, vuta picha anavyoheshimika, unamuona yule Baba pale, anafanya kazi ofisi ya Mkuu wa Wilaya, vuta picha naharibu hali ya hewa hapa! Sasa badala ya kuja kunisalimia kinafiki, nishike mkono, nielekeze alipo Bosi wako, niongee naye kistaarabu au niharibu hali ya hewa. Mimi sina kazi, sina chochote, sina chakupoteza, sanasana utanishika hapa utanitoa nnje na kunishitaki huwezi!”
Nilimuona kabisa mlinzi anaishiwa pozi, aliniambia nisubiri pale nisiongee chochote. Alienda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi ya Ben, alikaa kama dakika mbili hivi kisha akarudi na kuniambia kuwa nimfuate, alinipeleka mpaka kwenye ofisi yake. Ben alikua na mgeni lakinia limuelekeza kwa mtu mwingine ili amsaidie kisha akanikaribisha mimi. Kwa kumuangalia niliona kabisa ana hasira, anatamani kunitukana ila alishindwa kwani alijua naweza kumharibia kazi.
Niliingi akaanza kuniongelesha kwa ukali, mimi sikua namsikiliza, niliingiza mokono wangu mfukoni na kushika ile dawa, nikaimwagia mikononi kisha nikamshika kama namkumbatia. Alinishika ili kunizuia, nikampa mkono, aliupokea, nikanuia nilichokua nikitaka kisha nikaakaa chini. Sikujua kama ile dawa itafanya kazi, basi nilikaa kumya kumuanglia. Nilimuona anakaa kiupole na kinyonge. Sikumuambia chochote, nilimuangalia tu huku nayeye akiniangalia.
“Nitakuja nyumbani jioni…” Aliniambia.
“Nyumbani nwapi? Kwa Mama yangu, wewe si ulinifukuza, si mke wako kaja wkangu na kunitoa kama mbwa!” Nilimuambia, nilianza kulalamika huku nikilia, alinionea huruma na kuja, akanikumbatia na kuniambia kuwa, yeye hakumtuma mke wake na kila kitu kitakua sawa.
Aliniambia kuwa sababu ya kubadilika kwake ni kuwa, Mama yake alikuja nyumbani wakaungana na mke wake wakamlazimisha kuniacha mimi. Nilijua tu ni mambo ya maombi, alipotaja jina la Mama yake nilitetemeka kwani nilikua namuogopa, alikua anatisha, alikua na nguvu flani ambayo kwangu ilikua inaniharibia mambo.
“Mimi naweza kurudiana nawewe, lakini kwa masharti, nataka kurudi kazini na sitaki tena kusikia kuhusu mke wako, nataka mambo yenu mmalizie huko huko!” Nilimuambia, nilimpa mmasharti mengi na yote aliyakubali.
Alinisindikiza mpaka nnje, kila mtu alishangaa kwani nilitoka ofisini kwake na tabasmau. Jioni alikuja nyumbani kabisa, alikuja kwa Mama yangu na hakujali kama Mama atamuona. Ni kitu ambcho kilinishangaza, alikaa nyumbani mpaka saa nne usiku hakuondoka, mke wake alipiga simu sana lakini hakupokea. Wakati namsindikiza aliniambia kuwa nitarudi katika nyumba yangu na kila kitu kitakua cha kwangu.
Kweli nilirudi, na nilifurahia kurudi, lakini bado nilikua sijaridhika, nilijua kuwa, kama bado mke wake ataendelea kuwepo basi ataniharibia. Ilikua ni lazima kufanya kitu ili yeye aachane na mke wake na hata kumuondoa mke wake kabisa. Nilipata habari za mtalaamu mwingine ambaye niliambiwa ni kiboko, anaweza kumpiga mtu Nuksi mpaka akasahaulika. Nilimtafuta alinipa dawa kwaajili ya mke wake, ambayo kweli ilisaidia.
Ben alikua anagombana na mke wake kila siku, alimfukuza mke wake na mimi nikaingia kwenye nyumba yake na kuanza kuishi, alimuacha mke wake na watoto wake. Mwanzo mke wake alirudi nyumbani kwakina Ben, kwa hasira nikijua kuwa atakua karibu na Mama mkwe wangu na mimi nitazidi kuchukiwa nilimuambia amfukuze, alimfukuza lakini Mama yake alikataa kwani alikua anaamini kuwa mimi ndiyo nimemloga mtoto wake.
Nilimuambia kama Mama yako hataki kumfukuza basi acha kutuma matumizi nyumbani, ukiacha mumpe pesa baski hataweza kumtumza. Kwakua yeye ndiyo alikua kila kitu katika familia yake, alikua na ndugu lakini hawakua wakisaidai sana basi mkewe alichoka na ile hali na kuondoka. Alirudi kwao, nilimkataza kuongea naye, mwanzoa lkua anatuma matumizi ya watoto lakini baadaye aliacha kabsia, kila kitu kiakwa kipo upande wetu.
Nilimjengea Mama yangu nyumba nyingine kubwa zaidi nikahamishia na wadogo zangu. Mama alimchukulia Ben kama mke wake, nilikua kama nimeolewa, shida ikaja katika kupata mtoto, nilihangaika sana kupata mtoto lakini muimba hazikutokea. Ben aliniambia twende hospitalini lakini nilikataa, nilijua si mambo ya hospitalini, baada ya kuhangaika sana na waganga kila kitu katika maisha yangu nilikua nikiamini ushirikina.
Nilianza kuhangaika mwenyewe kutafuta mtoto, kila nilikoenda nilipewa dawa lakini hazikusaidia.
“Shida ni Mama yako, Mama yako mzazi, Bila kumuondoa Mama yako mzazi huwezi kupata mtoto na huyo mwanaume!” Niliambiwa sehemu moja, kwanza nilijihisi kama vile nimesikia vibaya.
“Mama yangu au Mama mkwe wangu?” Nilimuuliza mganga.
“Hapana, si Mama mkwe wako, ni Mama yako, mambp yote haya ni Mama yako mzazi, ni lazima kumshughulikia Mama yako kama kweli unataka mtoto je uko tayari?”
Naomba nisiwachoshe, kama uko kwenye soko la ajira soma Kitabu changu cha “INTERVIEW na AJIRA”.
KIGAGULA; SITAKI AFE LAKINI SITAKI AWE MKE WAKE—- SEHEMU YA SABA.
“Mama yangu hawezi kuniloga, ananipenda sana, najua anachukia tabia zangu lakini nina uhakika kuwa hawezi kuniloga.” Nilimuambia Mganga kwa hasira, moja baada ya kuniambia kuhusu Mama yangu nilijua kuwa ni Tapeli hivyo nilitaka kuondoka.
“Sijasema anakuloga?” Aliniambia.
“Sasa unamaanisha nini unaposema kuwa, sababu ya mimi kushindwa kupata ujauzito ni Mama yangu?” Alitingisha vibuyu vyake na kuongea maneno ambayo mimi sikuyaelewa kisha akaniambia.
“Kila binadamu ana majini, Majini ni viumbe kama sisi tu, wanaishi ndani yetu, kuna majini wazuri na majini wabaya. Mama yako ana majini wazuri ambao hawakubaliani na vitendo vyako. Wewe ni mtu wa waganga, unatembea na mume wa mtu, unataka kuzaa na mume wa mtu, kwakua umebeba damu ya Mama yako basi Majini yake hayawezi kukuruhusu kufanya hivyo.” Alitongisha tingisha tena vibuyu vyake kisha akaniambia nifunge macho.
Nilifunga macho, alinishika usoni, akawa kanipaka dawa ambayo ilinifanya kama kupoteza fahamu hivi lakinibado nilikua nasikia kila kitu ila kichwa changu kilikua mbali kabisa. Ghalfa nilianza kuona vichwa vya vitoto vichanga, kulikua na vich3wa vingi vya vitoto vichanga ambavyo havina mwili, vilikua vikilia kimojakimoja kisha vinanyamaza, vilikua nvikihangaika kama mtu amabye anatapatapa akitafuta pumzi. Ghafla nilimuona Mama yangu, alikua amesimama pembeni yake hukua kichekelea.
Nikiwa bado katika hali ile nilijiona nimelala chini, chali, uchi wa mnyama, Mama yangu alionekana kama anachukua kitu sehemu za siri na kukirusha kwenye kundi la vile vichwa, basi kila Mama akirusha kitu basi kinageuka kuwa kichwa cha mtoto, kinatapatapa na baada ya muda kinanyamaza kama vile kimekufa. Mama alikua akifanya hivyo hukua ancheka, baada ya muda flani yule mganga alinipaka kitu kingine kisha nikazinduka na kuwa kawaida.
“Unakumbuka ulichokiona?” Aliniuliza, wakati huo nilikua natetemeka kwani kulikua na vichwa vingi sana vya watoto ambavyo vilitupwa chini, pia nilikua naogopa kumuona Mama yangu, akiwa pale na anachukua vitu kwnye sehemu zangu za uchi. Nilimuambia kila kitu nilichokiona kule ndipo akaniambia.
“Kila unapofanya mapenzi katika siku zako za hatari kutafuta mto basi hicho ndiyo hutokea, mbegu ya kiume ikikutana tu na mayai yako basi Majini ya Mama yako yanaua wale wwatoto kwakua ni watoto wa kichawi, una machaguo mawili, moja ni wewe ukubali tumshungulikie Mama yako, tuue majini yake, na chaguo la pili ni wewe kutafuta mwanaume mwingine, usitumie dawa yoyote ubebe mimba yake kisha umsingizie mwanaume wako.”
“Kumshughulikia kivipi? Unataka kumuua Mama yangu?” Nilimuuliza.
“Hapana, ni majini yake, Mama yako hatadhurika kabisa. Ni chaguo zuri, kwani kuzaa na mwanaume mwingine inaweza nayo isifane kazi, kwakua haya majini yake yanajua dini sana hayapendi uzinzi, hivyo yanaweza kuua wanao pia, yanapaswa kuondoka.” Aliniambia, nilikua na hamu sana na mtoto na nilimuambia nataka kuua majini ya Mama ili niwe na amani, alifanya mambo yake kisha akanipa dawa kuhakikisha kuwa namuwekea Mama kwenye chai, maji au soda kila siku kwa siku tano mfululizo.
Hilo kwangu halikua na shida kwani nilikua karibu sana na Mama yangu. niliweka kweli, na baada ya kama mwezi hivi nilibeba ujauzito, Mama yangu hakudhurika na chochote, alikua sawa, alifurahia mimi kupata ujauzito ingawa alikua na wasiwasi kuwa ninabeba mimba na mume wa mtu. Mimi nilimuambia kuwa yule si mume wa mtu, ni mwanaume wangu na mkewe hamtaki kashamtelekeza. Kwakua nilikua mtu mzima na nina kipato changu hakua na maamuzi yoyote juu ya maisha yangu.
Ben alizidi kunipenda, aliniatambulisha kwa ndugu zake wote kasoro Mama yake. Ndugu zake walinipenda ghafla na kila mmoja akamgeuka mke wake. Ilikua ni nguvu ya pesa, walikua wakijipendekeza kwakua yeye alikua na pesa na ni mtoaji. Kuhusu mke wake na wanae hakutaka kusikia chochote kabisa kutoka kwao, hata mimi nikimajia alikua anakasirika sana na kunaimbia tayari nina mimba hivyo nahitaji kutengeneza familia yangu na yeye.
Mimba ilikua vizuri, lakini ilipofikisha miezi mitatu hali ilianza kubadilika, nilikua silali, usiku nilikua nasumbuliwa na tumbo nusu kuchanganyikiwa, lakini ikifika asubuhi najikuta niko sawa tu. Lakini si hivyo tu, kule kwa Mama nako mambo yalikua mabaya, Mama alianz akuumwa, alianza na magonjwa madogo madogo, kichwa, miguu, mara ngozi ikaanza kuota maele. Kunaanza kipele kidiogo kisha kinakua jipu kubwa lakini halikauki.
Mwili mzima ulijaa majipu, alikua kwenye maumivu makali, lakini kitu kilichokua kinashangaza ni kuwa, yeye ia alikau akipata maumivui makali sana usiku ila ikifika asubuhi, bado anamajipu na vidonda lakini hasikii maumivu yoyote, hata ukivigusa basi unakuta viko sawa. Ali hiyo iliendelea mpaka nilipofikisha ujauzito wa miezi sita, kila siku ilikua ni kuumwa na hali ya Mama ilizidi kuwa mbaya.
Alikua hawezi htaa kutoka kutokana na vidonda, kila sehemu kwenye mwili wake ulikua na vidonda. Hospitalini walimpa dawa za kukausha lakini wapi, mimi maumivu nayo yalizidi kuwa makubwa. Baada ya kuona kua hospitalini mambo hayawi sawa basi niliamua kwenda kwa mganga, mganga aliyenipa dawa mara ya kwanza aliniambia vumilia, itaisha ni majini yanapambana.
Niliona ananiyeyusha nikatafuta mganga mwingine, akanipa dawa nikatumia kwa muda wa mwezi mmoja. Hali ile ilitulia, Dawa nilitumia mimi lakini Mama naye alianza kupona, mpaka nakaribia kujifungua Mama alipona na kuwa vizuri kabisa. Alikua kabaki tu na mabakabaka ya vidonda mwilini mwake. Siokujifungua kwa njia ya kawaida bali nilijifungua kwa oparesheni kwani mtoto alichelewa kutoka.
Nakumbuka nilifanyiwa oparesheni asubuhi, mtoto alitoke asalama lakini kila mtua lishangaa namna alivyokua katoka. Nilijifungua mtoto wa kiume, alilia vizuri kama watoto wengine lakini ngozi yake ilkua tofauti, kama Mama mwili wake ulikua umejaa makovu ya mapele, yaani ukimuangalia Mama kila sehemu ya mwili wake ambapo kulikua na kovu basi mwanangu naye ilikua hivyo.
Watu walishangaa sana lakini mimi nilihisi tu kuwa wakati Mama anaumwa anapata maumivu makali basi na mwanangu ilikua hivyo kwani wakati wa usiku kipindi naumwa tumbo nilisikia kama mtu anakanyaga, kama mtu ananichoma kwa ndani na kila akikanyaga basi napata maumivu makali nusu kuchanganyikiwa. Nilikubaliana na hilo, kwani nilijua kuwa atapona kwakua nilishapewa dawa na ndiyo imeonyesha matunda.
Lakini haikua hivyo, ulipofika usiku mwanangu alianza kuweweseka, mwili ulibadilika rangi na kuwa mwekundu. Ilipofika saa nane usiku alitulia, mimi nikajua kalala lakini kumbe ndiyo ilikua mwisho wake, mwanangu hakuamka tane. Alifariki dunia siku hiyo hiyo na siku hiyo hiyo lakini hali ya Mama baada tu ya mwanangu kufariki ilianza kuwa mbaya. Alikua hospitalini akinihudumia lakini ghafla nilimuona anashindwa kusimama, miguu inamlegea alidondoka chini na kuwa kama mtu aliyepooza lakini si ile ya kukakamaa mwili wake ulikua laini sana yaani ukimgusa na kijiti anatoboka. Alishindwa kunyanyanyuka na akawa ni mtu wa kuhudumiwa kwa kila kitu.
Pamoja na kwamba alikua ni mama yangu na nilijua kuwa hajahusika wka namna yoyote ile na kifo cha mwanangu lakini nilimlaumu yeye. Niliamini kuwa majini yake ndiyo yamemuua mwanangu na sikua tayari kumsamehe. Nilirudi nyumbani kwangu nilipokua nikiishi na Ben kama mke na mume. Ben aliniambia nisiwe na wasiwasi kama ni mtoto tutatafuta mwingine lakini sikua na amani kabisa, nilikua na hasira na niliamini kuwa, hata kama nikiendelea kuishi naye lakini kama ikitokea akifa basi mimi sina mrithi.
Ingawa wanae kawatelekeza lakini niliamini wana haki kuliko mimi, kwanza ni watoto wa ndoa ya kanisani, pili ni watoto wake, wanatambulika na kila mtu, vipi mimi? Lakini pia nilikua nikiamini kuwa uchawi hauingii kwa maiti hivyo kama akifa siwezi kumloga tena, siwezi kuloga ndugu zake wote wala siwezi kuloga mahakama ambayo itaamua mali ziwe za nani. Nilikua naumia sana, niliuguza kidonda changu kwa muda mrefu vila kupona hivyo hata suala la tendo la ndoa na mume wangu nalo lilikua la shida.
Alikua ananipenda sana, anajali familia yangu kuliko yake lakini mimi hayo sikuyaona kabisa, nilikua nawaza kupata moto nikiamini kuwa kama nikiwa na mtoto basi hawezi kuniacha.
“Mama yako analalamika kuwa hujaenda kumuona kwa muda mrefu, hali yak eni mbaya, kuongea ni kwa shida, sijui sababu ya kugombana kwenu lakini hembu nenda kamuone!” Siku moja Ben aliniambia, ilikua ni usiku, miezi sita ilikua imepita tangu mimi kujifungua mtoto akafariki na Mama kuanza kuumwa. Katika kipindi chote hicho nilikua mbali na Mama yangu na sikutaka hata kumuoa, hata simu zake nilikua sipokei, nilihisi kwua nikiwa karibu naye majini yake yataniulia wanangu.
Lakini bado nilikua sijapona kidonda, hospityalini walinisafisha mpaka kuchoka, walinipa dawa za kukikausha lakini haikukauka, kila siku kilikua kinatoa maji. Nilihangaika kwa waganga kimya kimya bila mafanikio. Nilikua nataka mtoto na Ben alikua hataki kufanya mapenzi na mimi, hali hioyo ilinishanganya sana, aijitahidi sana lakini alikua akihisi kama ananiumiza kwani kidonda haikua tu mboni tu, kilishuka mpaka karibu na sehemu zangu za siri, pembeni kidogo ya uchi wangu.
Nililazimishia sana lakini hakutaka, kitu cha ajabu nikuwa, kidonda hakikua na maumivui kabisa, nilikua na uwezo wa kukifunga, nikatoka na kutembea bila tatizo lolote. Hali nhiyo ilimshanagaza kila mtu, madaktari na kila mtu walishangaa kuwa kidonda cha oparesheni kinakaa muda wote huo bila kupona. Haikua hivyo tu, miezi sita baada ya kujifungua bado nilikua sijaanza kuona siku zangu. Yaani nilikua mkavu kabisa, hivyo hata nikifanya mapenzi nilikua sijui kama nitabeba mimba au la kwakua nilikua siwezi kuhesabu mzunguko wangu.
“Nimeshakuambia mara ngapi, mimi na Mama yangu tunajuana, wewe si unampa pesa, anataka anione ili nini, sina mpango wa kuonana naye kwasasa!” Nilimuambia Ban ambaye alikua ameshikilia simu yake mkononi akiichezea. Nilikua nikiamini kuwa matatizo yangu ya uzazi yanatokana na Mama yangu, hata kama hahusiki moja kwa moja lakini kama nikiendelea kujiweka karibu naye siwezi kupata mtoto.
“Sawa, lakini wewe ni mwanae, hivi uansema unaumwa lakini unasafiri kila siku kuona marafiki zako, unakaa siku ngapi huko?” Aliniuliza kwa haisra kidogo, ni kweli nilikua nasafariri, nafunga kidonda changu naisngizia misiba ya marafiki ili tu kwenda kwa wanganga, kwanza kumtengeneza Ben aili azidi kunipend ana pili kutafuta dawa.
“Kwahiyo unaona kama siumwi? Unasema eti nasem,a kana kwamba huniamini, hivi huoni hiki kidonda kweli? Nakuuliza kama hukioni au ni nini? Yaani nashindwa kabisa kuelewa…..” Nilianza kulalamika, lakini wakati huo kumbe alikua anapiga simu, alinipa simu na kuniambia.
“Ongea na Mama yako, kama unaweza kwanda Dar kumsalimia rafiki yako basi unaweza kuongea na Mama yako mzazi!” Aliniambia huku akinikabidhi simu, alikua kanishtukizia hivyo sikua na jibu la harakaharaka, nilishindwa kabisa kukataa nikajikuta napokea simu.
“Halooo!” Mama aliita, nilibaki kimya bila kusema chochote, sauti ya Mama ilinikumbusha kilio cha mwanangu hospitalini. Ghafla picha ya Mama akitoa vitu kwenye sehemu zangu za siri an kuvitupa chini kisha vichwa vya watoto wachanga vinatokea vikilia ilinijia. Nilishindwa kuongea, Mama aliita na kuita lakini nilishindwa, Ben alikua kakaa pembeni yangu ananiangalia.
“Ongea na Mama yako mbona unakaa kimya!” Aliniambia kwa hasira.
“Sasa unataka kusikia naongea nini na Mama yangu? mwanaume gani unakua mbea namna hiyo, toka niache niongee na Mama yangu!” Nilimuambia huku nikimsukuma, alitoka na kuniacha chumbani.
Sikuwa tayari kusikia sauti ya Mama yangu, harakaharaka nilikata ile simu, lakini nilijua kuwa lazima Ben atakua ananisikiliza hivyo ilikua ni lazima kuigiza kama vile naongea na Mama ili asijekulazimishia tena mimi kuongea.
“Mama mimi naumw2a, najua sijakutafuta ila hali yangu mbaya, sikuja kukuona kwakua sikuaka kukuumiza. Sitaki unione katika hali hii, lakini pia sitaki kukuona kwakua naumia nikikuona Mama yangu ulivyohangaika na mimi halafu uankua katika hali hiyo!” Nilijiongelesha.
Niliongea mambo mengi ili tu kama Ben anasikiliza basi aamini kuwa naongea na Mama yangu, lakini wakati najifanya kuongea nilikua nakagua simu ya Ben,, sina utaatibu wa kufanya hivyo lakini siku hiyo nilaimua kukagua. Katika kuangalia niliona kuna simu kapiga, ile namba nilikua naifahamu ni ya mke wake. Lakini kurudi kwenye M-Pesa niliona kuna pesa katuma kwa ile namba. Hazikua pesa nyingi,a lituma shilingi elfu saba tu lakini ziliniuma kama vile katuma milioni saba.
Kwangu niliona kama vile ni usaliti kwamba bado anawasiliana na mke wake wa zamani na anatuma pesa wakati tulishaamua kuwa tuwatelekeze. Niliumia sana lakini nilijituliza, aliporudi sikumuuliza kitu chochote, nilijifanya kama vile nimeumia kwa kutokuzungumza na Mama muda mrefu nikamshukuru kwa kuniunganisha na Mama yangu, lakini akili yangu ilikau mbali sana, nina mawazo mengi, mimi sina mtoto, yeye ana mke na watoto pamoja na dawa zangu bado anahangaika nao iliniuma sana.
****
Kwangu Ben kuendelea kuwasiliana na mke wake ilikua ni kunirudisha kaktika umasikini, mzunguko wangu ulikua haueleweki, hataki kufanya mapenzi na mimi na bado anawasiliana na mwanamke wake ambaye wana watoto naye. hapana, niliona kuwa itakua shida, siku iliyofuata nilimuaga Ben kuwa naenda kumkuona Mama na nitakaa huko siku mbili, alitaka kunipeleka lakini nilikataa, alikua na safari ya kikazi hivyo nilijua kuwa nitawahi kurudi.
Lakini si kwenda kwa Mama, sikutaka kumuona Mama yangu kabisa, kuna mganga ambaye niliwasiliana naye akaniambia anaweza kunisaidia kuhusiana na watoto wa Ben.
“Ukitaka kushinda acha kuwaweka wanae mbali na wewe, unahangaika na Mama yao lakini tishio ni wanae, hao ndiyo watakuja kurithi mali, hivyo unapaswa kuwachukua, wakishakua chini ya himaya yako unaweza kuwafanya chochote kile!” Mganga aliniambia, alinishauri mambo mengi kuhusiana na watoto wa Ban.
“Wafanye mandondocha amabyo hata wakipewa mali zinakua hazina maana kwao!” Alizidi kunishauri, alinipa dawa ambayo nitakua nikiwakwekea watoto wake kwenye chakula. Lakini aliniambia kuwa kazi ya kwanza itakua ni mumshawishi Ben kuwachukua watoto. Nilimuuliza kuhusu Mama yangu ni kwanini haponi na je nikienda kumuona itakua na shida kwangu kama yule mganga mwingine aliniambia kuwa Mama yangua na mashatani ambayo hayapatani na mimi kabisa.
Aliniambia kuwa sababu ya Mama yangu kuumwa ni kwakua mashetani yake yananguvu hivyo yanamtesa Mama yangu na mimi yataendelea kunitesa mpaka atakapoyamaliza. Alinipa dawa nyingina ya kumpa Mama ambayo ilikua ni dawa ya kunywa na ya kufukiza. Hakikisha Mama yako anafukiza hii dawa siku tatu mfululizo baada ya hapo mlete kwangu mimi nitamsaidia kwakua salama yenu wawili ni sisi kuyatoa kabisa hayo9 mashetani.
Aliniambia kuwa mganga wakwanza alikosea kwa kuniruhusu mimi kubeba ujauzito kabla ya kuyatoa mashetani yote kwa Mama. Nilimuelewa, nikaondoka mpaka kwa Mama, nilimpa dawa za kufukiza akagoma, nikamuomba kuhusu kwenda kwa mganga akaniambia kuwa ni bora kufa kuliko kwenda kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Alinihusia mambo mengi pamoja na jisi mitume walivyoteseka na maradhi lakini sikumuelewa.
Mwisho tuliishia kugombana, nilirudi nyumbani na kesho yake Bena lirudi. Aliniuliza kuhusu Mama nikamuambia kuwa nilienda lakini kuna dawa nimempa hataki kutumia, niliamua kumuambia ukweli kwani nilihisi nisiposema Mama atasema, sikumaumbia nimeenda kwa mganga nilimuambia ni dawa tu nimepewa na rafiki yangu za kufukiza. Hakuuliza maswali mengi sana, tuliongea mambo yetu ingawa alionekana hakua sawa kabisa.
Alionekana kuwa na mawazo sana, mimi pia nilikua na mawazo, nilikua nawaza ni jinsi gani nitamuambia kuhusu kuwachukua wanae ili nije kuishi nao mimi. Niliwaza kama nikianza kuongea mimi nikawachukua wakaanza kuumwa si nditaonekana mchawi, usiku nilikau na mawazo, nafikiria namna ya kuongea, lakini hata yeye alionekana kuwa na mwawazo, kuna kitu kilikua kinamchanganya.
“Mbona uko hivi, unaonekana una mawazo sana?” Nilimuuliza, nilitaka yey ekuongea kitu chake kabla yangu.
“Naomba unisamehe mke wangu….” Alianza kuongea huku akilia, kwa namna nilivyokua nimemtengeneza Ban alikua kama ananiogopa, ananipenda mpaka wakati mwingine inekera.
“Nikusamehe nini? Kwani umenifanyia nini?” Nilimuuliza huku nikimsogelea na kumkumbatia.
“Nikuhusu safari yangu, sikuenda kikazi, nilienda kuwaona wanangu, sikuenda kumuona mke wangu bali wanangu….”
Aliongea kwa kujihami, kama anajitetea kwa kufanya kosa kubwa, alianza kunielezea kuhusu hali za wanae, kawaona na anawaonea huruma, aliniambia kuwa hana mpango na mke wake wa zamani lakini hawezi kuwaacha watoto wateseke.
“Naomba tuwachukue watoto tuishi nao, ni wakubwa, hawatakusumbua….” Aliniambia, nilijikuta nacheka kimoomoyo, ni kama Mungu alikua anafanya kila kitu kwaajili yangu, bila mimi kumuambia alikua ananiletea wanae niwafanye ninachotaka!
Watoto ndiyo hao wanaletwa, unadhnai Salma atafanikiwa katika mipango yake….
KIGAGULA; SITAKI AFE LAKINI SITAKI AWE MKE WAKE—- SEHEMU YA NANE
Nilifurahia kuwa Ben anawaleta watoto wake yeye mwenyewe bila mimi kumuambia. Nilianza kwa kukatakataa ili nisionekane nawahitaji sana lakini baadaye nikakubali, nikamuambia kama kaamua hivyo basi nitawachukua na kuwalea kama wanangu. Alifurahi sana na kuniambia kuwa atahakikisha tunaishi vizuri. Kila kitu kilikamilika, siku ya kuja niliweka dawa zangu sawa kwani sikutaka kabisa kupoteza muda.
Siku walipokuja ndipo siku nilihisi kuchanganyikiwa, nakumbuka ilikua usiku kwenye saa nne hivi. Mume wangu alienda kuwachukua kijijini hivyo walichelewa kufika. Nilikua nimeandaa chakula kwaajili ya watoto, mimi nilishakula na nilikiweka dawa kabisa. Ile nafungua mlango nguvu ziliniishia, hakua mume wangu na watoto peke yao, bali alikua kaongozana na Mama yake.
“Nataka tuishi kwa amani, Mama yangu kaskukubali hivyo nimekuja mshikane mikono, amesema anakuja kukuomba msamaha!” Ben aliniambia baada ya kuniona namuangalia Mama yake kwa mshangao. Nilijikuta natetemeka, kwa hasira zilizochanganyika na uoga, sijui yule Mama alikua na nini lakini ile kumuona tu ilinipotezea ujasiri, yaani nilishindwa hata nifanye nini.
“Mwanangu nisamehe, nilikufikiria vibaya kipindi kile, lakini nimeamini kuwa wewe ndiyo utampa mwanangu furaha, kama mwanangu anakupenda basi nimekukubali kuwa mwanangu!” Kabla hata sijaongea chochote, Mama yake alipiga magoti kuniomba msamaha, alikaa chini kwa dakika kama tano hivi bila mimi kujitingisha wala kusema chochote. Ben alikua akiniangalia kama ananiambia “Muambie Mama anyanyuke yameisha!” lakini sikusema, allimshika Mama yake mkono na kumyanyua.
“Huna haja ya klupiga magoti Mama yangu, mke wangu amekuelewa na nina uhakika kakusamehe.” Aliongea huku akiniangalia, nilitingisha kichwa kukubaliana na alichosema lakini kusema kweli nilikua najisikia vibaya, nilikua nimechanganyikiwa na niliona kabisa kuwa mambo yangu yemeharibika kabisa. Waliingia ndani na moja kwa moja Mama alienda kwenye chakula, ni kama alijua kuwa kuna kitu nimeweka alisogelea chakula na kukiangalia kwa muda wa kama dakika mbili hivi bila kupepesa macho.
Baada ya hapo aliuondoka na kuwachukua wajukuu zake, akawashika mikono kishaa akanigeukia.
“Mwanangu tunalala wapi?” Aliuliza, nilikua bado natetemeka, sijielewi ikabidi mume wangu kuwaelekeza sehemu ya kulala. Waliingia na kutuacha sebuleni, baada tu ya Mama yake kutoka katika kile chumba akili zangu zilirudio, ndipo nilishtuka kuwa kumbe wamekuja na kuondoka bila kula chakula.
“Mbona watoto hawjaala chakula na wewe uliniambia kuwa niwaandalie chakula? Nilimuuliza Ben kwa hasira, nilijifanya kuumizwa na ukweli kuwa nimeandaa chakula lakini hawakula.
“Waache walele, wameshiba, wakati tunakuja Mama alisema anasikia njaa sana, alilazimisha tule, nilimuambia umepika lakini akasema tutachelewa kufika sana hivyo tule kwanza, tumeshiba, ila mimi naweza kula kidogo.” Aliniambia, niliondoka kwa hasira na kuchukua chakula kukitupa, sikutaka mume wangu ale kwani lengo la chakula kile ilikua ni kuwafanya watoto kuwa mataahira.
Nilikua nimekitenga chakula mezani lakini mume wangu nilimuandalia chakula chake chumbani, kile kilikua ni cha watoto. Mama mkwe wangu alikua kaharibu kila kitu, katibua mipango yangu. Nilipanda kitandani kulala kwa hasira nikiwaza maisha yangu yatakuaje na yule Mama. Alikua anasali sana na alikua na nguvu ya jabu ambayo ilinitisha, imani yake ilikua ni kubwa sana na kila siku alikua akisema mimi ni mchawi.
Kilichokua kinaniumiza zaidi na kunikoesesha usingizi ni ukweli kuwa ingekua ngumu kwangu kumfanya chochote kwani tangu kuanza kujihusisha na ile familia niligundua kuwa, anaota vitu kabvla havijatokea. Yaani akipiga magoti na kusali kama kuna jambo baya unataka kumfanyia basia ataota na ndoto zake mara nyingi zinakua kweli.
“Mama anaondoka lini?” Nilimuuliza ben, ilikua ni saa tisa usiku, nilikua sina usingizi, nilijua kwa vitu nilivyokua nimeweka katika ile nyumba nilisingeweza kukaa na yule Mama hata kwa siku moja.
“Abnaondoka kwenda wapi? Mbona ndiyo kafika, yaani Mama yangu kaja leo unataka aondoke?” Ben alinijibu kwa hasira.
“Sina maana hiyo, lakini wewe mwenyewe unajua kabisa kuwa mimi na Mama yako hatupatani, sasa ni kwa namna gani tunaweza kuishi ndani ya nyumba moja. Mimi siwezi kabsia, Mama hanipendi, Mama hanitaki….” Nililalamika sana lakini nikama nilimtibua Ben, alinyanyuka kitandani na kuwashataa.
“Hivi una akili kweli, unafikiri mimi sijui? Mama kanipigia sismu kuwa anataka kuja kukuomba msamaha, kaja kapiga na magoti, unamuangalia tu, lakini sasa hivi badala ya kuwaza ni namna gani utamaliza tofauti kati yako na Mama yangu unataka aondoke!”
Aliongea kwa hasira sana, nilijua tayari Mama yake alishaanza kumharibu, nilijua kabisa kuwa lengo la Mama yake kuja kwangu haikua kuja kupatana na mimi balia likua na kitu. Lakini sikua na chakufanya kwa wakati huo, nilipanga kuondoka asubuhi kwenda kutafuta dawa nyingine yenye nguvu zaidi ili kumkomesha Mama yake, nilijua hata kama ana imani namna gani lakini kama nikimpatia mganga mzuri basi naweza kummaliza kabisa, sikua na utani kwangu ilikua ni lazima Mama mkwe kuondoka.
****
Asubuhi ya siku hiyo niliamka mapema, si kama nililala hapana, nilikua nusu usingizi nusu macho, usingizi ulikua ni wa maruweruwe sana. Lakini siku hiyo ilikua tofauti kabisa, ile nafungua macho tu nikaanza kusikia maumivu makali tumboni. Najua nilikua na kidonda lakini hata siku moja nilikua sisikii maumivu yake, kilikua kinatoa maji lakini hakikua na maumivu. Ila siku hiyo nilisikia maumivu kiasi kwamb ahtaa kutembea ilikua shida. Nilijitahidi kunyanyuka kwani ilikua ni lazima kutoka mule chumbani.
Nilitaka kutoka ili hata kuongea na mghanga wangu kumuambia kila kitu kilichotokea. Nilitoka mpaka sebuleni, nikachukua simu yangu na kutaka kuongea, lakini kabla sijaongea kitu chochote nilimuona Mama mkwe wangu yuko nnje kashika jembe. Nilitoka harakaharaka kumuangalia, alikua anachimba na pembeni kulikua na hirizi pamoja na vitu vingine ambavyo nilikua nimechimbia katika ile nyumba. Alikua kazunguka nyumba nzima kavikusanya na kuviweka sehemu moja.
“Unachimbia uchawi, unachimbia uchawi!” Nilianza kupiga kelele, nilikimbia mpaka chumbani kumuamsha mume wangu na kumuambia kuwa nimemiona Mama yake anachimbia Hirizi, akili yangu ilikua inafanya kazi harakaharaka, nilijua kabisa kuwa kuna wakati walishamuambia Mama yake kuwa ni mchawi, nilijua kama mume wangu ataamka na kuambiwa ni mimi nilikua nikimloga basi ataniacha na mpaka wakati huo nilikua bado nsijaongea na mganga kumuambia kitu chochote.
Mume wangu alitoka na kukuta vile vitu, kulikua na hizizi 12, vichwa vya paka 10 na vitu vingine vingi, nywele, picha za mume wangu zimefungwa fungwa, picha za Mama mkwe wangu, picha za mke wake na vitu vingine vingi.
“Umeona, antaka kutumaliza, anataka kutumaliza!” Nilimuambia Ben huku nikimuonyesha. Mama yake wala hakua na wasiwasi, alikua kashikilia Bibilia yake mkononi na maji yake ya Baraka.
“Mwanangu hembu muulize kama nataka kuwamaliza si ningemm, Aliza nayeye, kuna picha nyingi hapa, zote ni za familia yatu, hakuna picha yake hata moja. Ningetaka kumliga yeye kwakua namchukia ningefukia na picha yake lakini mwanangu sijaingia chumbani kwenu, hembu twende huko mkaone mamboa mabyo kakufanyia!” Aliongea huku akitabasamu, nilitegemea Ben kukasirika lakinia linigeukia na kuniuliza nimefanya nini, nilimuambia sijafanya kitu labda kama ni yeye kafanya ananisingizia.
“Mwanangu twende uakone mambo ambayo mke wako kakufanyia!” Mama aliongea, nilitaka kuwazuia ili wasitoke lakini tumbo lilikua linauma, lilikua linauma kiasi kwamba nilishindwa hata kutembea, lakini ben alinishika, akanivuta hivyo hivyo mpaka chumbani. Nilishajua alichokua akikitafuta Mama mkwe wangu, katika sakafu ya chumba nilitoboa sehemu na kuwaka kibuyu flani hivi kimefungwa na kilikua na picha ya Ben. Alifika chumbani na mama yake moja kwa moja alienda mpaka sehemu niliyokua nimechimbia.
“Sogeza hilo kabati!” Alimuambia Bena na wote wakalishika na kulisogeza, kwa kuangalia tu kulikua na tile mpya katikati ya sehemu kabati lilipokua, ilikua imewekwa kwa kutegeshewa kwani nilitaka wakati nakuja kuongeza dawa nisipata ehisa kuibomoa. Mama mkwe aliisogeza na kutoa kile kibuyu, akakivunja na kuona picha ya mwanae imefungwafungwa!
Nilibaki nimenyamaza kimya, maumivu makali tumboani, sina chakusema, Ben akili zimemrudia alinifuata na kutaka kunivamia ili kunipiga lakini Mama yake alimshika.
“Acha kujifanya malaika, hata wewe ni mmshenzi kama huyu mwanamke, ungejali familia yako ukaacha kuchepuka haya yote yasingekukuta!” Mama yake alimuambia, maumivu yalikua makali nikashindwa hata kusimama, nguvu ziliniishia nikadondoka na kupoteza fahamu. Walinipeleka hospitalini ambapo kidonda kilikua kinaanza kuvimba.
Nilipatiwa huduma ya kwanza, nikakaa pale kwa wiki moja ndipo niliruhusiwa. Wakati wote nikiwa hospitalini mtu pekee aliyekua anakuja ni Mama mkwe wangu, alikua akiniletea chakula na kunihudumia kwa kila kitu kama mwanae. Ingawa sikutaka lakini sikua na namna, hata ndugu zangu hawakuja, nilijua ni kwasababu Mama alikua anaumwa au Mama likua hajui kuwa ninaumwa lakini nilipotoka hospitalini hali ilikua tofauti kabisa.
Nilimkuta Mama yangu mzazi kasimama, ni zima kabisa, nilimsalimia akaniitikia vizuri. Niliingia ndani lakini kila mtu alikua akiniangalia kwa jicho la hasira. Walijua kila kitu nilichokua nimekifanya. Baada ya kinga zangu zote kutolewa na Mama yakena Ben kila mmoja niliyemfanyia ubaya alipona na kurudi kama kawaida, wote niliokua nikiwashikilia kwa uchawi walifungulia. Mzee Masumi alipona, akanyanyuka lakini hakukaa sana, miezi miwili tu baada ya lile tukio alifariki dunia.
Hakuna aliyejua kuwa nimehusika kwa chochote, Ben aliniacha na hakutaka kujihusisha na mimi kwa chochote kile alirudiana na mke wake na kunisahau kabisa. Kuna vitu vingi nilikua nimechuma kwa Ben, magari na nyumba lakininvilipotea kwa mazingira ya kutatanisha. Gari mbili zilipata ajali kwa siku moja, zikaharibika zote, mbaya zaidi zilipata ajali siku moja tu baada ya Bima yangu kuisha, tena nilikua nimekatia Bima kubwa hivyo sikulipwa chochote.
Nilikua na maduka mawili, kwanza wateja walianza kupotea na baada ya muda nilishindwa kulipa hata kodi, nikachukulia mkopo nyumba moja ikachukuliwa na Benki na nyingine iliungua katika mazingira ya kutatanisha moto hata haujulikani umetoka wapi. hali ilikua mbaya , nyumbani wakawa hawanitaki, hawoangei lakini ni ile ukifika kama walikua wanaongea basi kila kitu kinasimama.
Maisha yangu yalikua ni ya upweke kiasi kwamba nikawa wakati mwingine natembea naongea kama chizi. Mambo yote hayo yalitokea kwa haraka, ndani ya miezi nane tu nilikua sitamaniki, nikawa kama chizi. Lakini bado sikukoma, nikawa nahangaika kwa waganga mpaka nikachoka, mwisho nilikutana na mganga mmoja akaniambia kuwa nyoteyangu ishakufa nisihangaike kama nina dini nimrudie Mungu tu kwani wataishia kula pesa zangu, lakini sikukubali, niliamini kuwa kama waganga waliweza kunipa mara ya kwanzwa watanipa tena.
Nilihangaika mpaka nikaingia kwenye mahusino mappya, haya yalikua ni ya kijana mwezangu, ilifikia hatua mpaka anakaribia kunioa, wakati kila kitu kishakamilika niliumwa sana, niliumwa tumbo la uzazi kama vile nina mimba ambayo imeharibikia tumboni. Lakini nilipofika hospitalini nikaambiwa haikua mimba bali ni kizazi changu kilikua kimeoza hivyo nilihitaji kusafishwa tu.
Sikuwalewa, lakini walinielewesha kuwa inaonekana kuna mimba iliharibikia tumboni zamani, nilitoa mimba au niliugua kizazi changu kikawa kinaoza taratibu. Nilisafishwa lakini mchumba wangua liposikianvile aliniacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine. Yaani hata hakukaa kusuibiri kunihudumia au kuseubiri nipone vizuri, michango ilaile, mapambo yaleyale na kila kitu kile kile pamoja na tarehe ya harusi ambayo ilikua nifunge ndoa naye alifunga ndoa na mtu mwingine.
Kusema kweli hali ilikua mbaya, nilikua naweza kukaa hata mwezi siogi, nanuka, nina mawazo mpakja ikafikia hatu Mama yangua linipeleka hospitali ya vichaa Milembe. Huko nilikaa kwa miezi miwili, walikua kama wamenitelekeza nilihangaika mpaka nikatoroka kwani hakukua na ndugu hata mmoja ambaye alikua anakuja kunitembelea, si Mama yangu mzazi wala si wadogo zangu, kila mmoja alinitenga.
Nilitoroka kwani sikujiona kichaa bali nilihisi nimeologwa, lakini baada ya kutoroka pale nilirrudi mtaani nikaanza kuombaomba, mwisho nilijiona kuwa mimi si mtu wa kuomba. Nilitafuta kazi kwa Mama lishe nikawa nalipwa elfu mbili. Nilifanya kwa muda mwisho nikaona hailipi nikaanza kuuza maandazi ni Biashara ambayo naifanya mpaka sasa inenipa kula. Lakini nimechoka, nina miaka 32 akini ukiniangalia ni kama kibibi kizee cha miamka 60, nimekua KIGAGULA.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment