IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO
SABRINA; KISIRANI CHA KUSHUKA!---SEHEMU YA KWANZA
“Nakuambieaje utaishia tu kulea lakini kupendwa tunapendwa sisi!” Mama Andrew (Sio jina lake halisi) aliongea.
“Kwa taarifa yako sisi ni wasomi, hakuna mtu wa kuja kushika mavi, unalilia kuolewa, hata mbwa wanaolewa lakini hawalishwio nyama na nakuambua tu siku nikisikia unamnyanyasa mwanangu nakuondoa hyapo, utajutaa kuolewa!” Aliendelea kubwabwaja, Sabrina alimuangalia tu bila kusema chochote, ilikua ni mchana na mume wake alikua kazini.
Alitoka na kuingia ndani, alichukua simu yake na kumpigia mume wake, alianza kulalamika kumuambia lile suala, palepale mume wake alimpigia simu Mama Andrew, waliongea kwa muda kidogo na Mama Andrew aliondoka lakini kwakutukana.
“Unafikiri nitaachwa kwakua umemuambia nimekuja kukutukana, hawezi kuniacha, mimi nimetoka naye mbali, sasa wewe jifanye kama unajua kuingilia mapenzi ya watu utaona, mimi ndiyo nilimkatakaa huyu mwanaume, nilimuachya mimi hivyo hawezi kuniacha mpaka niamue!”
Mama Andrew alionondoka, Sabrina ambaye kipindi hicho ndiyo alikua na ujauzito wa miezi sita alirudi ndani kuendelea na kazi zake. Hakua na binti wa kazi, kila mara alipolalamika mume wake alimuambia atamletea binti wa kazi lakini hakuleta. Alifanya kazi zake vizuri na kupika chakula cha mchana, aliingia ndani kulala. Jioni Andrtew ambaye alikua akisoma darasa la kwanza alirudi, alimsalimia, alimpa chakula vizuri lakini Andrew alikataa kula, hakumuuliza chochote kwani ilikua ni kama kawaida yake, alimuangalia tu na kumsubiri mume wake kurudi.
“Baba nina njaa!” Kilikua ni kitu cha kwanza Andrew kuongea, alikua kanyong’onyea kweli, Baba yake alienda jikoni kumpakulia chakula, ilikua ni kama mazoea, Andrew alikua hali mpaka kuwepo kwa Baba yake, kila siku alikua akilalamika kuwa Mama yake wa kambo anamnyima chakula kitu ambacho hakikua kweli.
Baada ya kumpa mwanae chakula Jackson (Sio jina lake halisi) alirudi chumbani, mkewe alikua kajilaza kitandani, hakumsemesha, alivua nguo na kuingia bafuni.
Sabrina alipomuona kaingia bafuni na kuanza kuoga alichukua simu yake, akaifungua na kuanza kusoma meseji. Kulikua na meseji nyingi nyingi kutoka kwa Mama Andrew, alikua akilalamika akisema anataka kumchukua mtoto wake kwakua anateseka kwa Baba yake. Jackson alikua akimbembeleza na kumuambia atulie kwani atadili na mke wake yeye mwenyewe.
“Nimeshakuambia tulia, Andrew ni mwanangu na huyu mwanamke nitamfundisha adabu mimi mwenyewe. Huwezi kumchukua mwanangu na kuishi na huyo mwanaume wako! Kama wewe anakunyanyasa namna hiyo unafikiri mwanangu atamfanya nini?”
Jackson alikua anamuuliza, Diana, Mama Andrew. Walichat sana na mara nyingi Jackson alikua akimuambia kuwa bado anampenda na kuwa kamsamehe lakini kwa sasa ana mke ambaye ni mjamzito hivyo hawezi kumuacha.
“Sawa lakini nataka muda wa ziada na wewe, mimi mume wangu yuko bize sana na kazi, nakosa mapenzi yako, anjua nilibugi mimi lakini ule ulikua ni utoto, haiwezekani mke wako kuchukua nafasi kubwa kiasi hiki, ananinyanyasia mwanangu lakini bado unamkiingia kifua, uneonekana unampenda yeye kuliko unavyonipenda mimi!” Diana alikua analalamika.
“Hapana si hivyo, ukisema hivyo utakua unakosea kabisa, wewe ndiyo uliniacha na huyu mwanamke nilimuoa tu kwakua sikua na namna! Nilishakuambia kuwa niko tayari kukuoa, uachane na huyo fala lakini hutaki, ulichagua pesa sasa hembu niache na mke wangu, najua hawezi kuwa kama wewe lakini angalau ananiheshimu na yeye si kama wewe!”
“Si kama mimi unamaanisha nini? Inamaana unataka kusema kuwa ni mzuri kuliko mimi?”
“Hapana, sijamaanisha hivyo, lakini wewe mpenzi wangu wakati wmingine ni mkorofi, hunisikilizi na unataka kunipanda juu kila wakati, ila mke wangu yeye ni mpole mtu wa kunisikiliza, ndiyo maana tunaendana, kuna changamoto za hapa na pale, najua haelewani na Andrew ila ajitahidi, nina uhakika nikwakua hajazaa, akizaa mtoto wake basi jua kuwa atakua Mama na atajua uchungu wa kuzaa atabadilika.”
“Naona unanichefua tu, wewe na wewe kuwa mwanaume, unawezaje kumsifia mwanamke mwingine mbele yangu! najua nina mapungufu kweli lakini umeniboa, kumsifia huyo mpumbavu wako kisa mpole unafikiri nafurahia, kwa heri lakini kumbuka tu kama hutaweza kumlea mwanangu vizuri nakuja kumchukua nampeleka kwa Mama yangu!” Diana aliandika, ilionekana kakasirika kwani baada ya hiyo meseji hakujibu tena meseji nyingine alizokua akitumiwa na Jackson.
Huko machozi yakimtoka Sabrina aliirudisha simu ya mume wake na kurudi kitandani, mumewe alitoka bafuni na kujichekesha chekesha, yeye alitulia tu na kujifanya kuwa anaumwa.
“Kwanini usipatane tu na mtoto, kwani unaona shida gani kumpa chakula?” jacksona alimuuliza mke wake, Sabrina alinyamaza bila kusema chochote. Alionekana kuwa na hasira sana na hakutaka kumjibu mume wake.
“Mbona unakua mchoyo namna hiyo, hivi unajua kuwa Andrew ni damu yangu na haendi popote?” Aliendelea kuongea lakini mkewe hakujibu, alikua kageuka kitandani, kalala analia.
“Unakalia kugombana tu na Mama yake, nimesema haya mambo nialzima yafikie mwisho!” alizidi kuongea lakini mkewe hakumjibu, aliendelea kulia bila kusema chochote. Wakiwa pale chumbani mlango uligongwa, Andrew alikua kwa nnje akimuita Baba yake. Baba yake alifungua, alimuona mwanae kanyong’onyea. Alimuuliza anataka nini akamjibu kuwa anataka kurudi kwa Mama yake, amechoka kukaa pale kwani mchana wake Mama yake wa Kambo alimpiga.
Jackson alimbembeleza na kumrudisha chumbani, ilikua jioni lakini alimuambia alale yeye ataenda kumaliza yale mambo mwenyewe. Alirudi chumbani na kumkuta mkewe bado kajilaza, bila kuuliza alimvamia pale pale kitandani na kuanza kumtandika na mikanda. Alikua akimchapa sehemu za miguu na mikono, alikwepa sana kumchapa tumboni.
“Sijakupiga muda mrefu, najua kwakua unadhani una mimba yangu siwezi kukupiga tena, niliapa sitakugusa ukiwa mjamzito lakini umenilazimisha nikupige!” Alilalamika hukua kimchapa mkewe, Sabrina alipiga kelele lakini hakua na mtu wa kumsaidia, alitandikwa sana na baada ya hapo mume wake aliondoka kabisa pale nyumbani.
****
Jackson alirudi usiku akiwa amelewa, alikua kaletwa na gari ya Diana ambaye alikuja mpaka pale nyumbani, aligonga mlango na kuingia mpaka ndani. Wakati huo Sabrina alikua jikoni akipika chakula. Diana aliingia ndani na kukaa sebulani, alimuita Andrew na kumkumbatia, alimuambia kuwa abaki pale na Baba yake lakini ipo siku atakuja kumchukua.
“Akikupiga tena muambie Baba yako, Mama wa kambo ni wabaya lakini usinyamaze mwanangu…” Alimuambia hukua kimkumbatia na kumbusu mara nyingi nyingi.
“Mama uliniambia niseme nataka kurudi kwako lakini mimi sitaki kukaa na yule Baba mwingine, nataka kukaa hapa…” Aliongea, lakini kabla ya kumalizia Mama yake alimkatisha, alimuangalia kwa jicho kali na kumziba mdomo, Baba yake alikua jirani lakini kutokana na pombe alikua hajamsikia vizuuri.
“Najua mwanangu uanteseka, sitakuchukua Baba yako atakulinda.” Aliongea huku akinyanyuka, hakuondoka moja kwa moja, safari yake isingekamilika kama asingeenda kumsumbua Sabrina,a lijua alikua jikoni hivyo alimfuata na kuanza kumtukana.
“Ni vitu gani hivyo unamlisha mwanangu?” Aliongea, Sabrina alikua kafunikia wali jikoni, alimuangalia tu bila kumjibu.
“Unaona upendo alionao mumeo kwa mwenetu, nakuambia utazaa mpaka yao la mwisho lakini hutakuja kupendwa kama ninavyopendwa mimi? Hivi unajisikiaje mwanaume yuko na wewe kitandani lakini hakojoi mpaka aniwaze mimi?” Aliendelea kubwabwaja lakini Sabrina hakumjibu chochote, alikaa kama mjinga na kumuachaa aendelee kuongea.
Akiwa bado anaongea Jackson aliingia, alimsikia na kuuliza nini kinaendelea, kuona vile Diana alimshika na kumkumbatia, akamuambia.
“Si huyu kidudumtu wako ananitukana, mimi na muambia asiwe anampiga mwanangu yeye ananijibu jauri, hivia najua sisi tumatoka wapi?” Diana alilalamika hukua kitaka kujiliza.
“Basi yaishe, wewe ondoka mimi najua namna ya kudili na mke wangu.” Jacksona aliongea kwa sauti ya kilevi, alimshika Diana kutaka kumtoa pale, lakini alikataa, Diana alimvamia na kumkumbatia,a lianza kumshikashika kimahaba.
Alimtomasa tomasa shingoni na kifuani hukua kiingiza mikono yake katika suruali ya Jackson, ingawa alikua akimsukumasukuma lakini Jackson alishindwa kabisa kujizuia, alionekana dhahiri kuchanganyikiwa kutokana na kile kitendo. Wakati huo Diana alikua akigeuka geuka kuangalia kama Sabrina anaangalia, hakua akiangalia alikua bize na kupika.
Alijiona mjinga na kuondoka zake, alimuacha Jackson akiwa hoi, ni kama alikua hajitambui kitu alichokua akikifanya. Baada ya Diana kuondoka Jackson likua kama kajitambua flani hivi, alijishauashaua kutaka kumuomba msamaha lakini Sabrina hakuonekana kujali, aliendelea na kupika zake.
“Wewe ndiyo unaniudhi, unajua ukishanitibua mimi nashindwa, najikuta namtafuta Mama yake ili kuongea mambo ya mtoto lakini sipendi kukupiga wala kukuonyesha haya yote.” Alijiongelesha lakini Sabrina hakuonekana kujali.
“Mbona nakuongelesha unakaa kimya, una kioburi ee, unajifanya kuwa una akili sana! Unajiona mjanja sana, kwanini huongei, unapanga nini juu yangu?” Jackson alifoka huku akimsogelea mke wake. Alimshika mkono kana kwamba anamvuta flani hivi lakini Sabrina aliuondoa, hapohapo Jackson alianza kumpiga, alikua akimtukana na kumuambia kama vile anataka kumpiga.
“Unataka kunipiga? Unampiga mwanangu na sasa unataka kunipiga na mimi?” Alifoka sana na kuanza kumpiga, bado alikua kalewa hivyo sasa hivi hakujali alipokua akimpiga, alimpiga sana kila sehemu.
Sabarina kuona vile alianza kujitetea, kwakua alikua kalewa Jacksona hakua na nguvu sana, Sabrina alifanikiwa kujitoa mikononi mwake, akamsukuma na kutoka nnje, lakini wakati anatoka Jackson alimshika kwa nyuma, alimvuta, gauni lake, Sabrina alifanikiwa tena kumsukuma, jacksona aliteleza na kudondoka chini, hapo ndipo Sabrina alifanikiwa kutoka nnje na kwenda kujifungia chumbani.
Alikaa chumbani kwa muda wa kama nusu saa hivi, alijua ni lazima mume wake atakuja kugonga mlango na kumtukana kutaka kumpuiga tena lakini kulikua kimya. Alipatwa na wasiwasi kwani mumewe alikua kalewa na wakati anatoka jikoni alidondoka, alifungua mlango na kutoka kwenda kumuangalia, alienda mpaka jikoni na kumkuta mumewe kalala chini alikua kalala kifudifudi, alijaribu kumgeuza na kukuta damu zinamtoka puani, kumuangalia aliona kama hapumui.
Akiwa bado hajaangalia na kujua nini kimetokea alisikia sauti ya Andrew ikitokea nyuma yake. “Umemuua Baba!”
Sabrina aligeuka na kumuangalia Andrew, alimtuma kwenda kumletea maji lakini hakuenda, alikua akipiga kelele tu kuwa akisema umemuua Baba umemuua Baba. Alinyanyuka mwenyewe na kwenda kuchukua maji na kumgwagia, Jackson alikua amezimia kutokana na pombe, pamoja na kuumia puani baada ya kujigonga alipodondoka lakini alikua mzima kabisa.
“Unataka kunifanya nini? Unataka kuniua eee!?” Alipiga kwelele huku akinyanyuka mwenyewe, alikua akipepesuka lakini alijitahidi mpaka akanyanyuka, alikua kaloana mwili mzima, alijishika uso na kugusa majimaji, mwanzo alidhani ni maji ya kawaida lakini baada ya kuangalia aligundua kuwa ni damu.
“Unataka kuniua!? Unataka kuniua!?” Alipiga kelele huku akimvamia Sabrina, alianza kumpiga kwa nguvu bila kujali alikua anampiga wapi, bado alikua hana nguvu hivyo Sabrina alifanikiwa kujitoa katika mikono yake na kuondoka. Alitoka nnje kabisa, hakutaka kwenda chumbani kwani alijua kuwa atamfuata na kuendelea kumpiga. Ingawa hakuwa na nauli lakini alipanda Bajaji kumpeleka nyumbani kwao, alifika na kumkuta Mama yake ambaye baada tu ya kumuuliza sababu ya yeye kwenda kule na kumuambia alimfukuza.
“Ondoka! Ondoka! Ondoka kabisa kabla Baba yako hajarudi, sitaki kabisa kuniletea matatizo, mume wako hajakufukuza, umempiga mwanaume sasa unatagemea nini? Rudi! Rudi kabisa usijekunisababishia na mimi kupigwa na Baba yako, mimi ndiyo nitaumia na kuonekana kama vile ndiyo nimekutuma ukampige mume wako!” Hakuwa na namna alirudi kwenye Bajaji ambayo ilikua inamsubiri nnje, alimuambia Dereva kumsubiri ili akachukue pesa kwa Mama yake kwani hakuwa na hata Shilingi wakati anaondoka nyumbani.
Haikuwa mara yake ya kwanza kugombana na mume wake na kurudi nyumbani kwao, kila mara alipoenda alirudishwa, Mume wake alikua ni mtu mwenye pesa, alikua akiheshimika hivyo hakuna mtu aliyekuwa akimuamini kuwa anaweza kupigwa. Mume wake alijua hilo hivyo aliiitumia hiyo njia kama vile kumuumiza. Alirudi nyumbani, hakumkuta mume wake na hakurudi mpaka asubuhi ya siku iliyofuatia, hakumuambia chochote, yeye alibaki na Andrew tu mule ndani kwani hawakuwa hata na mfanyakazi wa ndani.
***
“Unajua mke wangu mimi sitaki niwe nakupiga mara kwa mara, nakupenda na sijui ni kwanini tunakua tunagombana kila siku.” Jackson alimuambia mke wake. Siku tatu zilipita baada ya ule ugomvi na alijirudi, alimtoa mke wake out pamoja na mwanae.
“Inamaana wewe hujui au unataka niongee ili tuendelee kugombana?” Sabrina alimuuliza, Jackson alinyamaza kimya, alijua alichokua akimaanisha na alijua kuwa ni kweli.
“Lakini ni Mama wa mwanangu, siwezi kumzuia kwua karibu na mimi…” Alijisemesha baada ya ukimya wa kama dakika tano bila kusemeshana.
“Sawa najua lakini si kwa kutupangia kila kitu, nyie bado hamjaachana, sijui unataka nini kwake, kwanini bado unahangaika na mwanamke ambaye alikuacha na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine…” Sabrina aliongea lakini kabla ya kumalizia alinyamaza, alimuona mume wake, namna alivyokua amefura, suala la yeye kuachwa na Diana bado lilikua linamuumiza ni kitu ambcho alishindwa kukubaliana nacho.
“Nyamaza, naona ushaanza dhaaru zako, sitaki kusikia huo upuuzi, Diana ni Mama wa mwanangu na nampenda mwanangu, kama unaona huwezi kukubaliana na hilo basi ni bora uondoke wewe!”
Aliongea kwa hasira, Sabrina alinyamaza, alijua fika mume wake kakasirika na hakutaka kuiharibu ile siku. Alibadilisha mada harakaharaka ili kumfurahisha lakini kabla ya mumewe kujibu chochote simu yake iliita, alikua ni Diana, alikua akiongea kwa kulia, walikua kama hawasikilizani flani. Palepale Jackson alinyanyuka na kumuaga mke wake, alimuambia kuna mtu anaenda kumuona. Mkewe alijaribu kumuuliza ni nani lakini hakujibu, alijifanya ni rafiki yake.
“Najua atakua ni yeye, Mama Andrew ndiyo yeye pekee anaweza kukufanya uondoke kwa haraka namna hii, sijui hata kakupa nini? Mtu ana mume wake na anampenda lakini bado hutaki kumuacha, mimi nimechoka!” Alilalamika, mumewe alikua hajaenda mbali, kusikia vile aligauka na kumvamia mke wake, alimsukuma bila kujali idadi kubwa ya watu iliyokuwa pale, alimpiga mateke na tumbo lake, watu walinyanyuka na kuingilia kati, walimshika na kumuachanisha na mkewe, Jackson alijitoa kwenye kundi la watu akakimbilia mpaka kwenye gari lake akaondoka na kumuacha mke wake aligalagala pale chini.
Alienda mpaka nyumbani kwake, Diana alikua nyumbani kwake na wakatia nampigia simu alimuambia kuwa ameeenda nyumbani kumuona lakini hakumkuta ndipo alimuambia amsubiri.
“Nini tena?” Jackson alimuuliza mara tu baada ya kufika pale.
“Amenipiga tena, unaona alivyiniumiza, kampiga mpaka mtoto.” Diand ambaye alikua amembeba mtoto wake wapili mwenye miaka minne aliongea, alikua ameumizwa sana shingoni na usoni pembeni ya jicho. Jacksona limsogelea na kuanza kumuangalia, alikua akimkagua.
“Nilishakuambia uondoke, huyu mwanaume atakuja kukuua, sijui kwanini unamvumilia?” Jackson aliongea, alimshika na kumnyanyua ili waingie ndani.
“Hapana, katoka kidogo nikaona nije kwako kupumzika, nimechoka lakini kama akirudi nyumbania siponikuta basi ataniua.” Diana aliongea hukua kikataa kuingia ndani, Diana na mumewe walikua wakiishi mtaa tu wapili na mara nyingi kila akipigwa aliishia kwenda kwa Jackson kulalamika na kupata faraja.
Kwa unyongee Jackson alimuingiza kwenye gari, alimpeleka mpaka karibu na nyumbani kwake na kumuacha. Lakini kabla ya kuondoka alimuambia.
“Kama akikupiga tena nenda Polisi, atakuja kukuua, huyo si mwanaume!” Diana alimuangalia tu bila kusema chochote, alionekana kuwa na haraka na alionekana kabisa hakuwa tayari kufuata ushauri wa X wake. Alimbeba mwanae na kutembea harakaharaka kuelekea nyumbani kwake, Jackson alimuangalia mpaka anapotelea, alimuangalia kwa uchungu sana akuonekana kuumia sana kumuona vile. Baada ya Diana na mwanae kupotelea alipandwa na hasira, aliwasha gari na kuondoka kwenda kunywa pombe, hakujishughulisha hata kumfuata mke wake.
***
“Nataka ujue tu kuwa mimi ndiyo napendwa na nakuambia kuwa hutakua na raha na huyo mwanaume ni wakwangu tu, wewe kazi yako ni kulea tu!” Diana aliongea, ilikua ni siku ya Jumamosi, alienda kumchukua Andrew.
“Kwani tatizo lako ni nini? Kama unampenda si umchukue, kwanini kila siku kunikosesha amani, najua ndoa yako haina amani lakini kwanini kujaribu kuingilia ya kwangu!?”
“Wewe wewe! koma na ukome kabisa, mambo ya ndoa yangu yanakuhusu nini? Nani kakuambia sina amani, kwa taarifa yako napendwa kotekote, mimi ndiyo mwanamke bwana, na simmtaki huyo mwanaume wako ila ndiyo hivyo hakupendi! Hakupendi! Hakupendi! Bibie unang’ang’ania na kujibebesha mimba ukajibebesha, kwa taarifa yako hata ukizaa jua kuwa hutakuja kupendwa kama mimi!”
Diana alibwbwaja sana na kutukana, Andrew ambaye alikua chumbani akijiandaa alitoka, alimsikia Mama yake akitukana na kukimbia kutoka nnje, mara nyingi Mama yake akija pale alikua hataki kukaa kusikiliza wakitukanana kwani alikua akimfundisha mambo mengi mabaya.
“Njoo, kwanini unanikimbia, huyu ndiyo anakufundisha kuwa usiwe na adabu hata usimsalimie Mama yako?” Alimuita kwa suti ya chini.
“Mwanangu huyu si Mama yako, unatakiwa kunisikiliza mimi, nilishakuabia kama anakunyanyasa basi muambie Baba yako?” Aliongea huku akimshika shika mashavu, alikua kama anamlazimisha kusema mambo mabaya lakini Andrew alitingisha kichwa kukataa.
“Acha kumuingiza mtoto kwenye haya mambo, mimi sioni kama kuna haja ya mtoto kumjaza hico chuki zako!?” Sabrina alimuambia kwa upole lakini ni kama alichokoza moto.
“Kanisubiri nnje mwanangu…” Diana alimuambia mwanae huku akimsukuma nnje, ni kama alikua anataka shari. Sabrina alimuona na kuanza kuondoka kwenda chumbani.
“Unanitukana halafu unajifanya kukimbia? Unanitukana halagu unajifanya kukimbia? Huyu ni mwanangu, huwezi kunipangia namna ya kumlea, nimeshakuambia kuwa kama hujazaa hujui uchungu wa mwana, au kubeba hicho kimimba chako ndiyo ushajiona mzazi tayari!”
Alitukana sana lakini Sabrina hakumjibu, aliongeza mwendo kuelekea chumabni wkake, lakini kabla ya kuingia Diana alimfuata na kuanza kumvuta, ni kama alitaka kumpiga, Sabrina hakukubali, alimgeukia na yeye kumsukuma, walianza kusukumana, wkaati huo huo mume wake aliingia na kuwatenganisha. Diana alijifanya kuwa na hasira nyingi na kuendelea kumsuikuma mwenzake, alimvamia na kutaka kumpiga tena lakini mume wake alimshika, wakati wa kuvutana, Sabrina alidondoka chini, alidondokea tumbo kwenye meza ya kioo ambayo ilipasuka, baadhi ya vioo vilimkata usoni.
“Mama nakufaa!” Alipiga kelele, mume wake alimfuata pale chini, alionekana kuwa na maumivu makali hasa tumboni. Alianza kupiga kelele, damu zilikua zikimtoka usoni, kuona vile Diana alitoka harakaharaka akamchukua mwanae na kuondoka naye. Jackson alimsaidia mke wake kunyanyuka akamkalisha chini.
“Wapi kunauma sana?” Alimuuliza, uso bado ulikua unatoa damu, kilikua ni kidonda kikubwa tu. Sabrina hakumjibu, alinyanyuka kwa hasira, alichukua kitamba akikubwa pale mezani na kujifuta usoni, alitoka akaingia wkenye gari yeye mwenyewe na kwenda hospitalini.
Aliwaambia kadondoka wakamshona nyuzi nne usoni kisha akarudi. Alikua na hasira sana na hakutaka kuongea na mume wake, walinuniana kwa siku mbili, lakini alilazimika kumuomba mume wake msamaha kwakua hakua na pesa ya kula, mwanaume naye alinuna kana kwamba ndiyo kakosewa. Jackson limsamehe, wakati huo alikua na ujauzito wa miezi nane na wiki mbili, lakini siku tatu baadaye alishangaa kuona mtoto hachezi tumboni, alimuambia mume wake lakini alipuuzia.
Siku ya nne alikua bado hasikii chochote, hakua na maumivu sana lakini mtoto alikua hachezi. Bila mume wake Sabrina alijikong’oja mpaka hospitalini. Huko baada ya vipimo aliambiwa kuwa mtoto amefia tumboni, alikua kabakiza wiki mbili tu kuweza kujifungua. Nguvu zilimuishia nakudondoka chini, alipopata fahamu tena alimpigia simu mume wake ambaye alienda hospitalini kumuona.
“Kuna mtu yeyote umemuambia kilichotokea?” Mume wake alimuuliza.
“Hapana!”
“Mama yangu hujampigia simu?” Jackson alimuuliza kwa wasiwasi ni kama kuna kitu kilikua kikimsumbua.
“Hapana!”
“Basi usijemuambia kuwa ni Diana kakusukuma, anamchukia sana Mama Andrew, akijua kuwa ndiyo kakusababishia hivi basi atamchukia zaidi, usimuambie mtu yeyote kua ulisukumwa, ni mipango ya Mungu, sitaki Diana ajisikie vibaya na watu kumchukia!”
Sabrina alikua katika maumivu makali, maumivu ya kumpoteza mtoto wake wa kwanza ambaye alikua amebakiza muda kidogo tu ili kumpata. Mume wake alionekana kuwa na wasiwasi sana, alikua na mawazo mengi kupita kiasi.
“Ngoja nimpigie Mama Andrew, nimemuambia naenda hospitalini lakini hajajua kuwa kuna nini, simuambii kuwa umepoteza mtoto kwania tajisikia vibaya sana, unajua anakupenda, yule ana roho nzuri na mara nyingi anakusifia lakini wewe tu ndiyo hutaki kupatana naye.”
Aliendelea kuongea, Sabrina aligeukia pembeni, hakutaka kuendelea kumsikiliza mume wake kwani alizidi kumpa hasira. Mumewe kuona vile alitoka nnje ili kuongea na simu. Sabrina alikaa hospitalini kwa siku tano, walikua wakisubiri kujifungua kwa njia ya kawaida lakini ilishindikana, hali ilikua mbaya sana na alikua na maumivu makali sana tumbani, hawakua na namna walilazimika kumfanyia upasuaji na kiumbe kutolewa.
Alitoka hospitalini na kurudi nyumbani, Mama mkwe wake alienda kumhudumia mpaka alipopata nguvu, baada ya kama wiki mbili Mama mkwe alirudi kwake, katika kipindi chote hicho ambacho Mama mkwe wake alikua kwake angalau kulikua na amani, mume wake alikua bize kumsihi asimuambie mtu yeyote kitu kilichotokea hasa Mama yake kwani alikua anajua namna alivyokua akimchukia Diana. Alikua na wasiwasi kuwa Mama yake atakasirika zaidi.
Jackson na Diana walijuana tangu kipindi wapo chuo, baada ya kumaliza chuo Jackson alichelewa sana kupata kazi, Diana alipata kazi katika benki moja, pamoja na kutokua na kazi akijishughulisha katika vibarua vya hapa na pale, mara kufudnisha, mara kukaa dukani kwa Mama yake, mara kujitolea katika ofisi mbalimbali na vingine vingi abdo alibeba majukumu ya mwanaume. Kila siki alijitahidi kumpa mpenzi wake pesa ya saluni, Diana alikua na mshahara lakini hata siku moja Jackson hakuwahi kumuomba pesa.
Alikua akimuambia kuwa yeye ndiyo mwanaume hivyo anatakiwa kumsaidia na kumhudumia. Alika miaka miwili bila kazi, na katika kipindi hiki Diana ndiyo alibadilika, pamoja na kwamba walishatambulishana lakini alimsaliti, alianza kutembea na mfanyakazi mwenzake, walianzisha mahusiano na kuanza kuonyesha dharau za waziwadi, aliacha kupokea simu za Jackson, akabadilika na kuwa hataki Jackson aende kwao tena, kama alivyokuwa akifanya zamani.
Bila kumuambia Jackson Diana alitafuta nyumba na kupangisha, akawa anaishi na huyo mwanaume, alibeba mimba ya huyo mwanaume lakini mwisho alikuja kugundua kuwa alikua ni mume wa mtu. Alijua tu baada ya kubeba mimba, mwanaume alimuambia aitoe na alipokataa mwanaume alimuacha kabisa, kwa hofu alitoa lakini mke wa yule mwanaume alijua hivyo akaachwa. Wakati yote hayo yanatokea Jackson alikua akilia kila siku, alikua akiumia na kumuomba msamaha yeye.
Ndugu zake hasa Mama yake mzazi alikasirika sana na hapo ndipo alianza kumchukia Diana, lakini baada ya Diana kuachika kwa yule mfanyakazi mwenzake alirudi kwa Jackson aliomba msamaha na jacksona limsamehe, wakarudiana na katika kipindi hicho ndiyo alipata ujauzito wa Andrew, kishingo upande ndugu wa Jackson walimkubali baada ya kujifungua, alienda kujitambulisha na kila kitu kilikamilika, lakini kabla ya ndoa, Diana alipata nafasi ua kwenda kozi Ujerumani.
Alienda na kukaa miezi sita, aliporudi alirudi na mimba nyingine ya kaka mmoja ambaye walienda naye kwenye ile kozi. Walirudi kimya kimya na kufunga ndoa ya kiserikali, kabla Jackson hajashtuka mchumba wake alikua ametangaza ndoa ya kanisani. Waligombana sana, wakati huo Andrew alikua na mwaka mmoja, jacksona hakua na namna zaidi ya kuendelea na maisha yake, alikua mtu wa mawazo, alikua kama mtu aliyechanganyikiwa, alifanikiwa kupata kazi lakini haikusaidia, bado alikua anamkumbuka na kwa namna alivyoachwa aliumia zaidi.
Miaka mitatu baadaye ndipo alikutana na Sabrina, alishapita kwenye mahusiano mengi na yote yalikua yanaharibika kwakua alikua akiwachukia wanawake na mara kwa mara badoa likua akiwasiliana na Diana ingawa kimyakimya. Alipokutana na Sabrina ndugu zake walilazimisha sana aoe wakiamini kua itamsaidia kumsahau Diana ambaye walikua wakimchukia. Alimchumbia na kufunga ndoa ya kanisani wakaanza kuishi kama mke na mume, katika kipindi chote hicho bado Jackson alikua akiwasiliana na Diana.
Baada tu ya ndoa mume wa Diana alianza visa, kwanza alianza kusema kuwa hamtaki mtoto, alikua akisingizia kama mtoto wa Diana akiendelea kukaa pale basi hawatapata raha ya ndoa, alifanya visa na kumlazimisha Diana kumpeleka mtoto kwa Mama yake. Diana hakua na namna, ndoa ilikua changa na hakua tayari kuachika, alitaka kumpeleka mtoto kwa Mama yake lakini Jackson alikataa na kumchukua mtoto wake. Hapo ndipo mawasiliano yalianza rasmi tena waziwazi.
Kila mara Diana alipenda kupiga simu akisingizia kuwa anataka kujua hali ya mtoto wake, lakini aliishia kuongea mambo mengine hasa kumalalamikia kuhusu ndoa yake amabyo ilikua inasumbua sana. Jackson alianza kuwa kama mfariji wake, mara kadhaa hata kabla ya ndoa Diana aliwakuta wakiongea lakini alisingizia wanazungumzia mambo ya mtoto, aliomba msamaha lakini alirudia na kurudia mpaka ikafikia kuzoea. Walipoingia hali iliendelea kuwa ileile.
Jackson aliendelea kuwasiliana na X wake, mbaya zaidi ndoa ya Diana ilikua ni ya vilio kila siku hivyo alikua akitumia muda mwingi na Jackson ili kumfariji. Ndugu wa Jackson walikua wakimchukia sana ndiyo maana jacksona hakutaka Mama yake ajue kuwa Diana ndiyo alikua sababu ya yeye kumpoteza mjukuu wake. Bado alikua anampenda na alikua anamlinda kuliko alivyokua akimlinda mke wake. Hakujali maumivu ya mke wake, akili yake ilikua kwa Diana tu.
***
“Nimekuja kukupa pole ya msiba.” Diana alimuambia Sabrina ambaye alikua anatoka chumbani baada ya kusikia gari ya mume wake ikiingia, tangu kupata msiba wa mwanae Diana alikua hajaenda kwake kwakua Mama mkwe wake alikua pale na hakutaka kumuona. Sabrina alishtuka kumuona pale, kitu kilimkaba rohoni, hasira zilimpanda kidogo kutapika, alikua akitetemeka kwa hasira. Wakati huo mume wake bado alikua nnje akipaki gari vizuri.
“Nimekuja kumuona mwanangu nikaamua nikupe na pole, mimi ni mzazi najua unavyojisikia, inauma sana kupoteza mtoto?” Aliongea kwa sharau lakini alikifanya kama ana huduni.
“Ulishawahi kupoteza mtoto wewe?” Sabrina alimuuliza kwa hasira, alitembea harakaharaka kuelekea jikoni kwani hakutaka kukaa sehemu moja na yule mwanamke.
“Ndiyo, mume wako hajakuambia, kuna kipindi nilitoaga mimba, nakumbuka ilikua kubwa tu, ilinitesa sana, mpaka sasa inaniuma, najua hata wakwako hakua mtoto kabisa, lakini ukishakuwa Mama unajua, ukishaambiwa mimba unaiona kama mtoto!”
Aliongea hukua kikaa, wakati huo Jackson alikua ndiyo anaingia, aliwaona wakiongea, Diana alikua anajichekesha chekesha lakini Sabrina alikua kakasirika.
“Huyu anafanya nini hapa kwangu?” Alimuuliza mume wakwa kwa hasira.
“Kwako kwangu, umejenga nyumba hapa! Huwezi kunipangia maisha, nimeshakuambia huyu ni Mama wa mtoto wangu, huyu ana umuhimu kuliko wewe, kanipa mtoto, wewe umenipa nini?” Mume wake alijibu kwa hasira, ni jibu ambalo hakulitegemea kwani kwa yote waliyopitia alidhani labda mume wake atakua upande wake.
“Hata kama, lakini huyu ndiyo kasababisha kifo cha mwanangu halafu leo unamleta hapa, umekuja kuniumiza au unataka nini? Hata kama sijakupa mtoto lakini mimi ni binadamu naumia, hivi mbona hujali hisia zangu?”
“Kama nikuumia unajiumiza mwenyewe, mtoto ashafariki, huna haja ya kujilizaliza na kutaka watu wajisikie vibaya, hivi unachotaka hasa ni nini? Unataka huyu ajisikie vibaya, isitoshe kila kitu ni mipango ya Mungu, mimba imetoka kama nyingine zinavyotoka, ilipangwa hivyo! Acha kulialia, kwanza tuletee chakula, nina mambo mengi ya kunichanganya sitaki nawewe unichanganye?”
Sabrina alikasirika na kuondoka bila kuaga, hakuandaa chakula kama mume wake alivyomuagiza, Jackson alimpigia simu lakini hakupokea.
“Kuna binti wa kazi nataka aje kuka hapa, siwezi kumuacha huyu mwanamke na mtoto wangu anaweza kumuua!” Diana aliongea, aliingia jikoni mwenyewe na kuandaa chakula kama alikua kwake vile, wakati anapika Jackson alimfuata jikoni, alikua akimuangalia kwa furaha, ni kitu ambacho alikua akikitamani sana sik nyingi.
“Yasingekua mambo yako ungekua mke wangu!” Jacksona aliongea huku akimshika na kumkumbatia kwa nyuma.
“Niache, huoni kama napika, ninakuambia mambo ya maana wewe unaletaleta upuuzi wako!” Alifoka hukua kiiondoa mikono ya Jackson kiunoni kwake, aliacha kupika, akazima jiko kwa hasira na kurudi sebuleni. Jackson alimfuata kumbembeleza lakini hakutaka, kulikua na kitu kinamsumbua kichwani kwake.
“Nini mbona uko hivyo?” Jackson alimuuliza huku akimfuata kutaka kumshika.
“Niache nimekuambia, niache!”Alijibu kwa hasira zaidi, aliinama chini na kuanza kulia. Jacksona alishtuka na kujua kuwa kuna kitu zaidi ya kushikwa kiuno.
Alimbembeleza sana ili kuongea, Diana alikua anaringa ringa lakini mwishoni aliongea.
“Mume wangu kapandishwa cheo.” Aliongea kitu ambacho kilimchanganya Jackson, lilikua ni jambo la furaha yeye kwake alishangaa kuona kama ni kitu cha kulia.
“Kwahiyo ndiyo unalia, unamaana gani, hukutaka apande cheo?” Aliuliza lakini Diana alimkatisha kwa hdraau.
“Wewe nawewe kila kitu mpaka utafuniwe kama mtoto, hujielewi, amepandishwa cheo na kuhamishwa mkoa, kapelekwa Kigoma….” Aliongea na kushindwa kumaliza, alikua akilia kama mtoto. Hapo Jackson naye alinywea kwani alijua inamaanisha nini.
“Sasa sisi itakuaje? Inamaana nawewe unahama naye?” Alimuuliza.
“Sisi kitu gani, mimi namuwaza mwanangu wewe unawaza mapenzi kwa kipi hasa unachonipa mpaka nikuwaze wewe, namuwaza mwanangu na anwaza ni kwa namna gani ataishi na huyu shetani wako…”
“Lakini mimi si nipo?” Jackson alimkatisha.
“Wewe! hivi unaweza kumtetea mwanangu kweli wewe, hembu naiche mie nisije kukufuru! Yule mwanaume asingekua mshenzi ningemchukua mwanangu lakini kwa alivyo anaweza hata kumuua!”
Jackson alinyamaza, hakutaka kumjibu vibaya ingawa majibu yake yalikua yanakera sana, alijaribu kumtuliza na kumpa moyo kuwa kila kitu kitaenda sawa lakini Diana hakutaka kukubali. Alijua kabisa kuwa kama akiondoka basi mwanae nilazima atateseka alilalamika sana akimlalamikia Sabrina na kuanza kumshutumu mambo mengi akimuona kama tayari anamtesa mwanae.
“Au nimpeleke kwa Mama?” Jackson alimuuliza kwa wasiwasi, ni kamaalijua jibu baya alililokua linakuja hivyo kabla ya kujibiwa alijijibu mwenyewe.
“Lakini mama hapana, nitalea mwanangu mwenyewe, nitamsimamia na sidhani kama atamnyanyasa.”
Alijiongelesha lakini Diana hakumjali, nitakuletea binti wa kazi, tena sio binti, kuna mdogo wangu kamaliza chuo nataka aje akae hapa kipindi Andrew yuko likizo, lakini baada ya hapo mwanangu nataka aende bweni, ni kipindi cha mpito tu nitatafuta mfanyakazi ninayemuamini. Kwasasa namleta mdogo wangu, ni mtoto wa Shangazi yangu hivyo namuamini. Aliongea kama amri na kweli Jackson alikubali kila kitu alichoambiwa. Diana aliondoka hata kabla ya kumalizia kupika, mumewe alimpigia simu na alijua fika anaenda kula makofi kama akichelewa.
Baada ya kama wiki moja Diana aliondoka, alimleta mtoto wa Shangazi yake kuja kukaa pale kama binti wa kazi, alikua ni binti ambaye ndiyo kwanza alikua kamaliza chuo, ana miaka 23 na alikua akikaa kwa muda kipindi akitafuta kazi na wakati wakifanya mpango wa kumpeleka Andrew bweni. Sabrina hakua na kauli, yeye aliambiwa analetewa binti wa kazi tu na hakutia neno kwani alijua kuwa kama angeongea angeishia kipigo tu. Flora (sio jina lake halisi) alikuja pale si kufanya kazi bali kumuangalia mtoto wa dada yake asiteseke.
“Unafanya nini hapo?” Flora alimuuliza Andrew. Andrew alikua katoka shule, alikua ndiyo kamaliza kula chakula, Sabrina alienda nyumbani kwao kwani Mama yake alikua anaumwa hivyo alienda kumuuguza. Ilikua imepita wiki moja tu tangu Flora kuanza kuishi pale.
“Naangalia TV Mama mdogo…” Andrew alijibu huku akijigeuza geuza vizuri kwenye kochi.
“Pumbavu unaangalia TV, na vile vyombvo unataka umemuachia nani, yaani umatoka shule, nguo umevua umeweka kwenye besni, halafu unakalisha matako chini eti unaangalia TV, chakula umekula unataka na vyombo nikuoshee!” Flora alifoka, kabla Andrew hajajibu lolote alishangaa kushikwa sikio na kuanza kuvutwa mzimamzima.
Alipiga kelele za maumivu lakini Flora hakujali, alimsukumiza chini, lakini kabla ya kunyanyuka alimuinamia na kimshika mkono kwa nguvu, alimbana hukua kimfinya na kumuambia aondoe vyombo alivyotumia kula chakula na kuviosha.
“Mjinga mkubwa, unajifanya mtoto wa tajiri na huyo Mama yako alivyo mpumbavu eti analeta mtu wa kumuangalia! Anakudekeza kisa hivyo vipesa vyenu, mwenzako umri huo nafanya kila kitu sijui hata TV ni nini wewe unajikalisha kalisha tu na romoti!” Flora alianza kubwabwaja huku yeye ndiyo akikaa kuangalia TV.
“Lakini Mama mdogo mimi siwezi…” Andrew alijilalamisha lakini kabla ya kumaliza Flora alinyanyuka kwa hasira.
Mkononi alikua kashikilia Rimoti, kwa hasira aliirusha huku akitukana.
“Mshenzi mkubwa wewe pamoja na Mama yako! Mbwa kabisa! Huwezi! Huwezi! Nini!” Aliirusha ile Rimoti na kumpiga nayo Andrew kwenye jicho.
“Mamaaa Nakufa!” Alipiga kelele huku akishika jicho, damu zilianza kumtoka, Flora aliona lakini hakujali, alienda na kuokota Rimoti na kurudi kukaa mpaka kelele zilipozidi ndipo alinyanyuka kwenda kumuangalia.
Flora alimuangalia Andrew aliyekua kalala chini akilia, alionekana kuumia sana, hakujali, alimuacha kulia kwa muda kisha akanyanyua simu.
“Shemeji njoo nyumbani! Shemu njoo nyumbani Dada atatuua, naona kapaniki! Kaja kampiga mtoto anataka kunipiga na mimi, naogopa shemu naogopa!” Aliongea huku akilia, Kelele za Andrew zilikua zikisikika upande wa pili hivyo kumfanya Jackson naye kupaniki.
“Kuna nini kimetokea, mbona sikuelewi? Kuna nini ongea taratibu?”
“Mimi sijui, nilikua ndani nikasikia vitu vinavyonjwa vunjwa, nilipotoka ndipo nilimuona Dada analia, anapiga kelele anasema mmeniulia mwanangu mmeniulia mwanangu, analia na kuvunja vunja vitu! Alianza kumpiga Andrew na nilipojaribu kumtetea alinisukuma na kusema na mimi ataniua!”
Aliongea huku akilia, alionyesha kupaniki na uoga mkubwa. Jackson naye alipaniki kwani hakujua kilichokua kinaendelea.
“Mimi naona hata sio akili zake, anaonekana kachanganyikiwa kwani alitoka ausbuhi vizuri nashangaa sasa hivi karudi hivi, njoo haraka, mimi naondoka siwezi kuishi kwenye nyumba inavituko namna hii!” Alimalizia kuongea na kukata simu, baada tu ya kukata simu, alianza kuvuruga vitu pale sebuleni, alivunja vunja vitu, chupa za chai, meza ya Kioo na vingine vidogo vidogo.
Alimfuata Andrew ambaye alikua bado kaaka chini kashikilia jicho, lilikua linatoa damu sehemu ya juu kwenye nyusi ilionekana kupasuka ingaw asi sana, lilikua limevimba na alinekana kuwa katika maumivu makali sana.
“Umeona hivi vitu, Baba yako akija namuambia ni wewe umevivunja, sijui hata atakufanya nini?” Aliongea hukua kimshika na kumnyanyua, alimvuruta mpaka kwenye kochi na kumkalisha, alichukua kitambaa cha meza na kumfuta zile damu.
“Acha kudeka upumbavu wewe! nyamaza mimi si Mama yako au kile kibiriti ngoma mnachokichezea, hizi sheria mpya, nyamaza na nisikilize kwa makini!” Aliongea hukua kimtandika Andrew kofi ili akae vizuri, badala ya kulia Andrew alinyamaza kwa uoga kwania litishiwa kofi jingine.
“Baba yako akija nitamuambia umevunja vitu vyake, sasa una uamuzi, tuseme Mama yako wa kambo kaja hapa kakuvamia na kuvunja hivi vitu au tuseme ni wewe. uamuzi ni wako, chochote utaklachoamua mimi sitajali, lakini kwa ukinga wako kama ukinitaja! Ukinitaja!...” Aliongea huku akimnyanyua kusimama chini. Alimvua suruali na kumshika uume wake kisha akaanza kuuvuta kwa nguvu.
“Umesikia maumivu yake, sasa hapa nimevuta, hembu fikiria nikichukua kisu nikivikata hivi vidude vyako sijui utasemaje!” Andrew alimsikiliza akitingisha kichwa kukubaliana naye, alikua akipiga kelele nyingi za maumivu lakini Flora hata hakujali, aliendelea kumbinya uume wake bila kujali kelele.
“Hapo sasa nilikua nakufundisha kitu ambacho nitakufanyia kama ukiniaja hivyo kuwa makini sana na maneno yako! Najua unaongea na Mama yako, utamuambia nilivyokuambia la sivyo nitakata hicho kidudu chako na kumpelekea huko wakakalange wale ugali!” aliongea na kuondoka kwenda chumbani kwake, alikaa kwa dakika kumi, alikua akimsubiri shemeji yake, aliona gari linaingia, alitoka na kuanza kupiga kelele akilia, alienda kufungua mlango kwania liufunga kwa ndani.
“Kuna nini?” Jacksona alimuuliza.
“BNaogopa shem naogopa! Dada katoka lakini najua atarudi na atanipiga na mimi, amemuumiza sana mtoto, nimeogopa hata kutoka kwani anatishia kuniua, anasema eti nyie ndiyo mmemuua mtoto wake na nilazima alipe kisasi! Eti anasema kila kitu ni kaburi kwa kaburi!” Aliongea kwa kujiliza huku akijilaza kifuani kwa shemeji yake, alikua kama anaogopa lakini lengo lake ilikua ni shemeji yake kuugusa mwili wake, alikua kavaa Kanga moha na kitop chepes ambacho kilimuacha sehemu kubwa ya mwili wake wazi, kwa namna alivyokua akijirusharusha kwa kulia alikaa uchi mara nyingi.
“Muangalie mtoto, angalia,a litaka kumtoa jicho, Andrew mwanangu hembu muambie Baba nini kimetomkea.” Aliongea hukua kimnyanyua Andrew alimpakata na kuka akwenye kochi.
“Mama! Mama! Mama!....Mamaaaa!” Andrew alishindwa kuongea, wakati kampakata Flora alipitisha mkono wake nyuima na kuanza kumfinya matakoni, alishindwa kuongea nakuwa anapiga keleele tu.
“Shem tukachukue PF3, tumpeleke hospitali, huu ni uteseji!” Aliongea, jacksona bado alikua hajalewa nini kimetokea, alsihindwa kugfanya maamuazi.
“yuko wapi huyo mwanamke?” Aliuliza hukua kinyanyuka na kutembeatembea kuangalia vitu vilivyokua vimevurugwa vurugwa pale sabuleni.
“Mimi nitajuaje shemu! Nataka hiyo ni kazi ya Polisi kumtafuta, anasema mmemuulia wmanae, kwanini anasema hivyo?” Aliuliza maswali ambayo yalizidi kumchanganya Jackson na kumfanya kuamini alichokua akiambiwa.
“Hakuna kitu kachanganyikiwa tu!” Jackson alikua anajua kuwa hakuna mtu aliyekua anafahamu kilichotokea mpaka mke wake kupoteza ujauzito, alijua kuwa kama akimpeleka Polisi na kama kweli kachanganyikiwa basi anaweza kuongea chochote.
Hakua akijali kuhusu Polisi, alijua hawezi kufungwa kwakua hakuna ushahidi wowote, lakini aliogopa kuwa kama mkewe kachanganyikiwa kweli akimtibua atasema kila kitu na ndugu zake wakijua basi watazidi kumchukia Diana, bado akili yake ilikua kwa Diana na alikua anataka aendelee kuonekana mwema. Alikataa masuala ya Polisi na kumuambia Flora asimuambie mtu yeyeote kitu yeye atalishughulikia.
Alimtafguta mke wake kwenye simyu hakumpata mpaka jioni ambapo mkewe alimpigia simu akimuambia hali ya Mama yake ni mbaya hivyo atabaki kulekule. Mkewe alikua anaongea vizuri, hakua kapaniki, alimuuliza uliza maswali lakini hakuonekana kuchanganyikiwa kama alivyosema Flora. Alimuambia arudi nyumbani kuna tatizo, aliporudi tu kipigo kilianza akimtishia kuwa kama akimpiga tena mtoto wake basi atamuua kabla ya kumuambia mtu yeyote, mkewe aliishia kulia akiwa hajui hata ni kwanini anapigwa.
***
“Najua sio sehemu yangu kuuliza lakini hivi unaishije na mume wako?” Flora alimuuliza Sabrina. Ulikua ni mchana, siku mbili zilikua zimapita, Jackson alimkataza mkewe kutoka hata kwenda kumsalimia Mama yake ambaye alikua mgonjwa.
“Kwanini unasema hivyo, mbona tuko vizuri tu.” Sabrina alizuga kwani hakutaka kutangaza matatizo yake kwa kila mtu.
“Hapana, mimi ni mtu mzima, naona kila kitu mambo hayako sawa. Kwa mfano juzi Andrew kadondoka huko shuleni, karudi hapa nimempokea damu zinamtoka, lakini nashangaa anvaunja vunja vitu na muuliza anasema wewe ndiyo umempiga, tena anampigia Baba yake simu nawewe unapigwa? Kuna nini hapa hembu nieleze?”
Flora aliongea kama malaika, kwa kumsikiliza alionekana kama anajali sana kilichotokea na alikua ameumizwa.
“Hakuna kitu ni mambo ya kawaida tu…” Sabrina aliongea huku akitaka kunyanyuka, Flora alimshika mkono na kumrudisha chini.
“Najua huniamini, najua na mimi nimeletwa hapa kama kukuchunga, sio kwamba kuna kazi nafanya hapa, ila mimi ni mwanamke, namjua Dada yangu na namsikia, siwezi kuona unafanyiwa yote haya na bado na mimi nikashiriki kama vile hakuna kitu kilichotokea.
Najua unafahamu mimi si binti wa kazi, nina elimu yangu nasubiria tu ajira na kwa uzuri huu najua unafahamu kua nimeletwa ili kuharibu ndoa yako. Dada yangu nis hetani, ile familia yao naifahamu, wanajifanya wanajua kila kitu, ni binamu yangu hivyo hatuna ujkaribu sana ila wanadharau sana na wanapenda kukutumia wakiwa na shida. Mfano aliponiambia nije huku aliniambia anakuja kunitafutia kazi, nitakaa kwa muda kisha atanipeleka kuanza kazi, lakini baada ya kuja nilijua kuwa ni kudhalilishana tu…”
Flora aliongea mambo mengi sana kumponda Dada yake na kuonyesha kuwa yuko upande wa Sabrina lakini Sabrina aliishia kumuambia tu kuwa hajui chochote na hana shida na mume wake. Mwisho Sabrina aliondoka na kumuacha kakaa peke yake. Alijichekea na kusema ataingia laini tu na kunywea. Sabrina alikua hamuamini mtu yeyote hivyo hakutaka kuongea sana na Flora ingawa alikua ni mtu wa kujipendekeza kwake kila siku akijifanya mtu mwema kwa kila mtu.
Siku moja Jackson alienda safari, ilikua ni safari ya siku mbili ya kikazi, kabla ya kuondoka alimuita Flora na kumuaomba kuwa makini, kumuangalia Sabrina ili asifanye kitu kibaya.
“Shemu mimi naogopa, hakuna namna tukaenda kukaa sehemu nyingine, unajua namuogopa sana Dada, yaani ukiwa hupo sina amani kabisa.” Aliongea kwa kulalamika, uso ulikua wa majonzi na alikua akilwngwa lengwa na machozi.
“Hakuna ndiyo maana wewe uko hapa, mke wangu si mtu mbaya sana, anapitia katika kipindi kigumu, alipoteza mtoto na kwa kiasi kikubwa mimi ndiyo nilikua sababu, lakini sasa ana mimba nyingine najua akipata mtoto mwingine basi atabadilika.”
Jackson aliongea, kusikia vile Flora alishtuka sana, ni kama alikua kaambiwa habari mabya, alishtuka mpaka Jackson akaona na kumuuliza.
“Vipi nini kwani mbona kama umeshtuka?”
“Hapana shemu, umesema ni mjamzito, kwa hali yake anahitaji mtu wa karibu wa kumhudumia, mimi naona hata ungemepeleka kwa Mama ili akakae huko….”
Flora alijiongelesha lakini Jackson alimkatisha.
“Hapana huyu ni mke wangu na nampenda sana, najua nilifanya mjakosa lakini sasa hivi umri umeenda, nilazima niwe na familia, siwezi kurukaruka. Diana kashaolewa na yuko na mume wake, hawezi kunirudia tena bora ni baki na mke wangu nitengeneze familia yangu!” Jackson aliropoka kwa sauti.
“Diana? Kivipi? Kwani shemu bado uko na dada?” Flora aliiuliza kitu amabcho alikua na jibu.
“Hapana! Wewe vipi kwanini unapenda kuingilia ingilia mambo ya humu dnani! Wewe si umekuja kama mfanyakazi humu, au hutaki kazi?”
“Nataka shemu…”
“Sasa kama unataka maswali maswali yako ya kijinga jinga unamuuliza nani? Mimi nimekuambia ukae humu, mhudumie mke wangu na mwanangu, hakikisha mke wangu hafanyi kitu kibaya kumdhuru mtoto basi! Hayo mambo mengine ni ya kifamilia hayakuhusu, wewe ni mfanyakazi tu chukua nafasi yako!”
Jackson alifoka, alionekana kuwa na mawazo mengi, tangu Diana kuhama alikua amebaidlika sana na kuanza kumpenda mke wake, hawakua wakionana mara kwa mara kama zamani, simu yenyewe ilikua ni mpaka Diana ampigie kwani alikua akihofia akipiga mume wake angeweza kupokea. Muda pekee ambao walikua wanaweza kuongea kidogo kwa uhuru ilikua ni mchana, tena kwa shida kwani mara nyingi alikua bize na kazi na walikua wakiishia kuzozana.
Flora alikua akimpigia dada yake na kumuambia mambo mengi ya uongo kuhusiana na mateso ya mwanae, kwasababu hiyo kila dakika wakiongea Diana alikua akiishia kulalamika namna mtoto wake alivyokua analelewa kitu ambacho kilikua kinaboana kufanya wagombane kila siku. Mapenzi yalipungua na kujikuta taratibu anaanza kurudi kwa mke wake ambaye alikua akimpa faraja. Kitu pekee kilichokua kinamuumiza ni mahusiano ya mkewe na mwanae ambayo aliyaona kama mabaya.
Baada ya kufokewa flora alilazimika kukubalia kila kitu, muda aliokua anatakiwa kuishi pale ulikua unakaribia kuisha. Likizo ya Andrew ilikua inakaribia kuisha na walishaanza mchakato wa kumtafutia shule ya bweni hivyo alijua hatakua na kazi tena pale. Ilikua ni lazima afanye kitu, aliumia sana kusikia kuwa Sabrina ana mimba nyingine, hiyo kwake ilikua ni kama dharau sana, alikua akimtaka Jackson lakini pamoja na kumkalia uchi mara nyingi wala jacksona hakumuona kama mwanamke, alikua akimuangalia tu kama binti wa kazi.
Aliumia sana kwania lijiona mzuri tena sana, alijiona mzuri kuliko hata mke wa Jackson ana Diana, alijiona ana akili na msomi, tena binti mdogo mbichi lakini mwanaume aliyakua anamtaka alimuona kama binti wa kazi tu.
“Mama yako mdogo yuko wapi?” Alimuuliza Andrew, shemeji yake alishaondoka na walibaki watatu tu.
“Yuko ndani kalala.” Ilikua ni usiku, alikua jikoni akiandaa chakula cha usiku.
“Chukua hiki chakula ataka ule hapahapa, sitaki utoke na ukishakula basi jua kuwa hutakula tena mpaka kesho!” Aliongea kwa hasira.
“Sawa dada….” Andrew alikula kwa uoga mpaka kumaliza. Alipomaliza alianza kazi ya kuosha vyombo vyote, Flora aliingia chumbani, akajiandaa kwa kuvaa vizuri, alikua anatoka kwenda Club.
Baada ya kumaliza kula, alienda chumbani kwa Sabrina, aligonga na kumuambia kuwa yeye anatoka na boyfriend wake, chakula ameshapika kiko mezani. Sabrina alimjibu sawa, akatoka mpaka jikoni.
“Unajua kusoma saa?” Alimuuliza Andrew huku akimvuta sikio mpaka sebuleni akimuelekeza kwenye saa ya ukutani, Andreww alimuambia ndiyo kua anaweza.
“Sawa kama unaweza, nataka usimame hapa, ule mshale ukitembea na ukifika pale katikati kwenye 6 hakikisha unaenda chumbani kwa Mama yako mdogo kumuita kumuambia kuwa chakula tayari, usitoke chumbani kwake mpaka atakapotoka na kula chakula, sijui umenisikia?”
“Ndiyo nimekusikia…”
“Sasa ole wako uguswe hicho chakula nitakachokufanya hata Mama yako hatakutambua!” Aliongea kwa hasira hukua akimpiga kofi amablo lilimfanya kupepesuka pepesuka lakini hakulia kwani alijua kulia ilimaanisha kipigo kingine, Flora alitoka na kuondoka.
Andrew alisomama mpaka muda alioambiwa ukafika, akaenda chumbani kwa Mama yake wa kambo na kumuita chakula, hakuondoka kweli mpaka alipotoka, alikua anamuopgopa Flora kupita maelezo, kila wakati sauti yake ilikua masikioni kwake. Sabrina alishangaa kwanini alikua anamkazania vile kumuita lakinia linyanyuka, alimshika mkono na kwenda kukaa naye, alipakua chakula na kumpakulia, alimpa lakini alikataa akisema yeye ashakula na hawezi kula tena kashiba.
Alimsisitiza sana kula lakini hakula, Sabrina hakujali, alichukua chakula na kuanza kula taratibu, alimaliza kula na kuondoa vyombo, wakati akipeleka vyombo jikoni tumbo lilianza kumkata, alisikia maumivu makali zana tumboni na kuanza kupiga kelele, alianza kutapika, maumivu yalikua makali akadondoka chini hukua kipiga kelele. Andrew alikua kasimama pembeni yake, hajui hata nini chakufanya anamuangalia tu, Sabrina alikua akimpigia kelele atoke nnje akaite watu lakini hakutoka, aliendelea kubaki pale huku Sabrina akiishiwa nguvu na kushindwa hata kunyanyuka.
Sabrina alikua katika maumivu makali, lakini akili yake ilimuambia kitu, alihisi kala sumu.
“Umenilisha nini mwanangu?” Aliongea wakati akiwa pale chini, sauti yake nilitoka kwa shida.
“Mimi sijakupa kitu Mama mdogo!” Andrew aliongea kwa sauti. Hakutaka kubishana naye, alijikaza kwa kujvutavuta mpaka lilipokua friji, kwa bahati kulikua na maziwa, alinyanyuka wka shida, akalifungua akachukua galoni ya maziwa na kuinywa kama maji. Alikunywa bila kupumzika mpaka ilipofika nusu, hapo alijua hawezi kunywa tena, alijikongoja mpaka kwenye kochi na kujilaza.
Nguvu zilimuishia lakini bado alikua katika maumivu makali, alishioka tumbo lake na kuwaza “Mungu naomba ukilinde kiumbe hiki!” Aliongea na hapohapo alipata nguvu ya ajabu, alinyanyuka na kutoka mpaka nnje, alipiga kelele kuomba msaada, watu walikuja, aliwaambia anahitaji hospitali. Walimpeleka, Andrew alibaki tu nyumbani huku akitetemeka kwa uoga, hakujua nini kilikua kimetokea, lakinia liogopa kwania lijua kuwa ni kitu kibaya kilikua kimetokea.
Alifika hospitalini na kupatiwa huduma ya kwanza, mimba ilikua salama, akiwa pale simu yake iliita, alikua ni Flora, alimsalimia na kabla ya kumuambia chochote alimuuliza kama yuko wapi, alimuambia hospitalini.
“Hospitalini, kuna nini tena, wamekulisha sumu….najua tu ni yule mtoto katumwa na Mama yake, yaani nakuambia, ni yeye tu mimi chakula nilikiacha vizuri tu.” Hata kabla ya kuambiwa kitu alianza kubwabwaja, Sabrina alimsikiliza bila kusema chochote, alimuacha aongee yote kisha akamalizia.
“Haikua sumu, nilikua sijisikii tu vizuri, nilidondoka si unajua nina mimba nashani ni mambo ya ujauzito.” Aliamua kuficha kwania lishtuka kitu, mpaka wakati huo alikua hajamuambia mtu yeyote kuhusiana na sumu, hata majirani waliokua wamempeleka hospitalini alikua bado hajawaambia. Alika apale hospitalini wka siku moja tu, baada ya hapo alirejea nyumbani kwake, alirudi na kujifanya kama hakuna kitu kimetokea, hata mumewe aliporejea hakumuambia kuhusu ile ishu.
Flora alipaniki kwani alitegemea kama watagombana, lengo lake lilikua kuitoa ile mimba na kubwa zaidi kumfanya Sabrina kupaniki na hata kumpiga Andrew ili kumpa nafasi ya kuongea na Dada yake kuwa mtoto wake ananyanyaswa. Alipoona kimya alianza kujipendekeza. Sabrina alikua chumbani, Flora alikuja na uji ili kumpa, aligonga mlango na kabla ya kuambiwa ingia aliingia huku akijichekesha chekesha!
Sabrina alimuuliza kwa hasira.
“Hapana, Dada nilikulet…” Nimekuuliza nani kakuruhusu kuingia chumbani kwangu sijakuuliza umeniletea nini?” Alifoka huku akinyanyuka, Flora alikua kashikilia Bakuli la uji mkononi.
Huku akiwa anashangaa shangaa Sabrina alilipiga lile bakuli, uji wa moto kidogo ulimwagikia kifuani, alikua kafunga Khanga moja tu kama kawaid ayake.
“Mamaa!” Alipige kelele za maumivu kutokana na kuungua.
“Unaniumiza!” Alisema lakini Sabrina wala hakujali, alimvuta kile kikhanga na kumuacha uchi kabisa, ndani hakuwa na kitu.
“Wewe mpumbavu unanijia chumbani kwangu uchi kabisa, unamtaka mume wangu au unataka na mimi nikubake!” Alifoka hukua kifungua mlango. Aliitupa ile khanga ambayo bado ilikua mikononi mwake, kisha akamshika na kumvuta nnje, alimuacha na kurudi ndani, alipanda kitandani na kuendelea kulala.
Kule nnje, Flora alijinyanyuanyanyua kwa aibu, akachukua khnga yake na kujifunika, alikua hajaumia sana lakini alishangaa ni kwa nini Sabrina alikua vile, haikua kawaida yake, mchana Sabrina alitoka, aliingia jikoni na kujipikia chakula chake mwenyewe na kula bila kupika chakula cha mtu yeyote. Andrew alikua nyumani, hakumpikia wala kumpa chakula, Flora alipoona kama anapika basi alijua kuw aatpika chakula cha wote, lakini hakupika hata cha mume wake hakupika.
Alipoona vile Flora aliamua kuingia jikoni ili kupika chakula, alianza kupika wali, lakini akiwa ameshamaliza kaufunikia Sabrina alikuja.
“Nani anapika?” Alimuuliza.
“Ni mimi dada…” Alijibu kwa uoga kidogo, baada ya lile tukio la asubuhi alianza kumuogopa klwani alikua haeleweki.
“Nani kakuambia upike?” Alimuuliza kwa hasira, kamkazia jicho huku akitingisha tingisha mikono yake kama vile anataka kumpiga.
“Hapana, nimeona kuwa hakuna chakula nikaamua kupi…” Kabla ya kumaliza Sabrina alimzaba kofi.
“Pumbavu, mimi ndiyo Mama mwenye nyumba hapa, hakuna kupika! Umenunua kitu hapa mpaka utake kupika! Wewe umakuja hpa kama nani?” Alimuuliza kwa hasira.
“Kama Dada wa kazi.”
“Unafanya kazi za nani?”
“Za kwako…”
“Sasa nimekuambia upike mpaka unaanza kuchukua vitu huko stoo na kuvipika, wewe unajua thamani yake wewe, unajua bei yake?” Aliuliza kwa hasira, Flora alibaki kanyamaza, akiwa kasimama tu akidhani kama vile atapigwa alishanga akumuona Dada yake akienda kuchukua maji, akayamwagia katika jiko la chakula, likazima, akaumwagia na ule wali maji.
“Toka hapa jikoni, sitaki uguse kitu, na huyo mbwa mwenzako nikimuona anagusa hata maji ya bomba basi atanitambua!” Aliopngea kwa hasira na kuondoka, Flora alitoka ndani na kukimbilia chumbani kwake, alichukua simu yake na kuamua kumpigia Diana.
“Huyu mwanamke kashakua chizi, mimi naondoka atakuja kuniua, njoo umchukue mwanao…” Alimuambia mambo mengi,a limuambia namna alivyokua amebaidlika ghafla, hakumuambia kuhusu mimba, hakumuambia kama alijaribu kuitoa na kutaka kumsingizia mtoto wake.
Kuambiwa tu Diana alipaniki, alijaribu kumpigia simu Jackson lakini hakupatikana, aliamua kumpigia Saberina mwenyewe, kabla ya khata kusalimiana alianza kwa kutokana. Alimtukana sana akimuambia kuwa ataondoka, yeye ndiyo anapendwa na ndiyo kamzalia hivyo ataondoka na kama ni kuzaa mtoto hawezi asimnyanyasie mtoto wake, alitukana sana lakini Sabrina hakumjibu chochote, alinyamaza kama mjinga vile mpaka alipochoka na kukata simu.
Baada tu ya kukata simu, Sabrina alinyanyuka, alitoka na kuchukua Bajaji mpaka kwenye ofisi za mume wake, alimkuta mume wake ofisini, alianza kulia mbele ya wafanyakazi wengine, mumewe alipaniki, hakua akijua nini kimetokea, alimsihi kuingia ndani. Ile kuingia tualitoa simu yake na kubonyeza clip moja, kumbe alikua akimrekodi Diana wakatri anamtukana, alimsikilizisha mume wake mpaka mwisho ksiha akamuambia.
“Nilivumilia kipindi kile nikapoteza mtoto wangu wa kwanza, sikumuambia mtu kwakua nakupenda, lakini sasa hivi nitaenda barabarani kuwa ombaomba ila kamwe sitaruhusu huyu mwanamke kunipotezea mtoto mwingine. Mimi namsaidia kulea mwanae lakini wewe mwenyewe unajua alichinifanyia, sasa leo mwanae kanikuta jikoni napika, kachukua maji kamwagia jiko, mimi siwezi tena, nimekuja kukuambia kuwa naondoka, najua kwetu hawatanipoke alakini Mama yakoa nanipenda, sidhani kama atakubali mjukuu wake kuteseka, naenda na yeye akinikataa basi utanikuta mtaani!”
Aliongea kwa hasira, Sabrina alikua anajua fika kuwa mume wake anamuopgopa Mama yake hivyo kitendo cha yeye kutaka kwenda na kama angesikia yale mambo basi asingekikubali. Jackson kwelia liingia laini,a lismihi sana asiondoke lakini alikataa, alimuomba basia subihi hata mpaka jioni ili akamilishe mambo yake ndiyo aondoke. Sabrina alijifanya kukubali kwa shingo upane, hakutaka kuondoka na alilijua hilo, alirudi nyumban na kuingia chumbani kwake kulala.
Ile anaondoka tu Jackson alichukua simu yake, alimpigia Diana ambaye alipokea kwa pupa akitaka kumuambia mamboa liyoambiwa lakini alikutana na matusi ya ajabu. Hakumpa nafasi ya kuongea, baada ya yeye kumaliza kuongea alikata simu, alitoka na kuingia kwenye gari, alienda mpaka nyumbani na kukuta kweli chakula kimewekwa maji. Alimuita Andrew na kumtandika makofi, kwa mara ya kwanza katika maisha yake alimpiga na kumuambi anatakiwa kumheshimu Mama yake na kama hataweza basi ataondoka na kwenda kutafuta Mama mwingine.
Aliingia chumbani na kumuomba mke wake msamaha, alimuomba sana akimuahidi kuwa kitu kama kile hakiwezi kujirudia tena. Alitoka na kumfuata Flora, alimuambia kuwa pale kaja kama mfanyakazi na kama hawezi kuishi kama mfanyakazi basi aondoke, alimkanya tabia yake ya kukaa kaa uchi uchi, alimuambia kuwa hawezi kumvumilia na kama amechoka basi atarudi huko huko kwa Dada yake na akafilie mbeli, aliongea kwa hasira sana mpaka Flora akaogopa.
Alikubaliana na mke wake ilia siondoke na kwamba kila kitu kutabadilika, aliondoka na kurudi kazini. Flora kuona vile alikusanya kila kilicho chake na kuaga ili kuondoka.
“Hapa hapanifai, mimi siwezi kuendelea kukaa humu tena!” Aliwaza wakati akiwa chumbani akijiandaa kuondoka. Lakini kabla ya kuondoka Diana alimpigia simu, alimuuliza nini kinaendelea ndiyo akamuambia kuwa Shemeji kabdilika na Sabrina kawa kama kichaa haambiliki.
“Mimi nataka kuondoka, siwezi kuendelea kuishi ndani ya hii nyumba!” Alilalamika.
“Uondoke uende wapo? Mwanangu naye umuachie nini, hivi unafikiri nilikupeleka hapo kwa sababu gani? Kama kabadilika kawa hivyo unafikiri mwanangu atakuaje? Akimuua, ngoja kwanza niongee na Baba yake kujua hatima ya mwanangu lakini huwezi kuondoka!” Diana alimjibu kwa hasira kidono, alionekana moja kwa moja kupaniki kusikia mdogo wake anaondoka huku akiwa hajui hatima ya mtoto wake.
“Lakini Dada mimi siwezi, nishakusanya vitu vyangu, mimi msomi kuishi maisha haya…” Alijiongelesha jibu ambalo lilimkasirisha Diana.
“Pumbavu! Msomi kitu gani? Hivi unajielewa wkeli, huo usomi nani kakupa? Ni nani alikulipia ada kama sio mimi, vipi wadogo zako nani anawasomesha! Baba yakoa anumwa hajitambui nani analipia matibabu? Acha upumbavu kama unataka kuondoka ondoka lakini jua kuwa ukirudi nyumbani utakutana na maiti ya Baba yako, sitalipa chochote na nitamuacha afe lakini nitahakikisha hutaajiriwa popote, nadhani unanifahamu na unafahamu nina roho mbaya kiasi gani hivyo nijaribu uone!” Diana alionge kwa hasira na kukata simu.
Najua wakati mwingine inachelewa kutoka hivyo utamu kupotelea chini, nitalirekebisha hilo. Ila usikose sehemu ya sita ya simulizi hii, mambo ndiyo kwanza yanaanza kupamba moto!
Sabrina hakua ni mtu wa kuongea matatizo yake sana, lakini alikua na rafiki yake mmoja ambaye alikua anajua kila kitu chake, alikua akimuona namna anavyoteseka, namna alivyokua akinyanyaswa na mume wake na namna alivyokua akisumbuliwa na X wake. Sikua lipopoteza mtoto wake kwa mara ya kwanza rafiki yake alijua, rafiki yake ni mmoja wa wasomaji wa ukurasa wangu huu, alinipigia simu na kuniambia kuwa anahisi kuna kitu kimetokea, kwakua alikua akiishi mtaa mmoja na Diana na Diana alikua mtu wa kuongea alimsikia namna alivyokua akitamba.
Aliponiambia nilimuambia kabisa siwezi kumsaidia kama mwenyewe hawezi au hataki kujisaidia. “Nilazima rafiki yako kujua kuwa ana tatizo nakuhitaji msaada, kama hajui kama ana tatizo itakua ni kazi bure kwangu kutaka kumsaidia. Rafiki yake aliumia sana kwani alimuona namna alivyokua akiteseka, Sabrina alipojaribu kulishwa sumu alimpigia rafiki yake yule, ndiyo mtu pekee ambaye alimuambia kilichokua kimetokea, rafiki yake alinitafuta na kama kawaida nilimuambia anunue Kitabu.
Alimnunulia na kuniomba niongee naye, mimi nilimuuliza kama anataka nini? Je kamchoka mume wake anataka kumuacha, lakini je anaweza kumuacha, vipi akiondoka itakuaje? Je anaweza kujihudumia na mambo mengine mengi. Baada ya kumuuliza sana nilijua kuwa hawezi kuondoka kwa huyo mwanaume lakini kutokana na hali halisi ni dhahiri kuwa anaweza kuchwa wakati wowote.
Kitabia mume wake ni mtu wa kuendeshwa na wanawake, hana kauli kwa mwanamke, niliona kabisa kuwa mume wake alikua akimuogopa Mama yake na sababu pekee ambayo ilikua inamfanya mume wake kumnyenyekea Diana ilitokana na ukweli kuwa Diana alikua mkorofi, alikua anamuendesha na alikua haogopi kumuacha ndiyo maana alimuacha na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine.
“Kama ukiangalia Flora anahizo tabia, na usipokua makini basi jua atakuchukulia mume kwakua anaweza kumuendesha mume wako, ni lazima ubadilike, nilazima uamue kuwa unaacha kuwa mwanamke wa ndiyo mzee na kuwa mwanamke ambaye ndiyo atafanya maamuzi. Anza na kumdhibiti flora na dada yake, ukushaweza hilo basi mdhibiti mume wako. Acha kulialia, acha kuomba omba msiamaha isiyo na maana, lakini kuwa Mama wa kambo kwa muda flani lakini muda wote hakikisha unakua Mama.”
Kwa hatua aliyofikia Sabrina alikua kama mtu aliyechanganyikiwa, nyumbani kwao ni kama walikua hawamtaki kwani hawakua wakimsikiliza mara kwa mara akiwaambia kuhusu manyanyaso ya mume wake, lakini kwamume nako kila siku ilikua ni kelele, alishakata tamaa ya maisha hivyo alikua tayari kufanya chochote ili kujilinda.
“Kama ukiwachekea watakuua, nilazima kuonyesha kua wewe ni nani, sitaki umnyanyase mtoto kwani hajui kama ulivyo wewe naye ni mhanga wa Mama yake, lakinia napaswa kukuogopa na huyo mfanyakazi aliyemleta anapaswa kuogopa. Hata kama huna mpango wa kuwafanyia kitu kibaya lakini nilazima waamini kuwa walipokufikisha nikubaya na unaweza kufanya chochote kile hivyo wasikuchezee…” Nilimuambia Sabrina kwani hatima ya maisha yake ilikua mikonono mwake.
“Kwa ninavyoona mume wako hana tatizo, atakusikiliza tu kama utaamua kuwa na sauti, kama utaacha kulialia na kujiona mnyonge na kuamua kuwa dereva wa maisha yako.” Baada ya kutoka hospitali Sabrina alibadilika, nilikua na shaka kwani mabadiliko yake hayakutokana na ushauri wangu bali yalitokana na hali aliyokua kafikia. Alikua kakata tamaa, hakua akijua kuwa anaweza kuishi na mara nyingi alijiona kama vile kakwama maisha hayana thamani tena, alishachoka kuvumilia nikamuambia mbona hana hata haja ya kuvumilia, maisha ni yake na anaweza kuishi atakavyo bila kuvumilia.
Sikua liyopaniki na kumpiga Flora nilishtuka kidogo, nilishtuka zaidia lipomnyima chakula Andrew, nilimuambia hapana, anaweza kuwa mkali kwa Flora na hata wakati mwingine kumtandika makofi mawili matatu lakini si kwa Andrew. Nilimuambia;
“Kwa Andrew ni lazima uwe Mama na si Mama wa kambo, kuwa Mama ni pamoja na kuacha kuogopa kumuadhibu pale akikukose, kumkemea lakini kumpenda, muonyeshe mapenzi yote lakini usimdekeze kwakua tu unaona kuwa labda ukimkemea basi watu watakuona wewe ni Mama mbaya kwakua si wako. Lakini usimnyime kitu kwakua tu umegombana na Mama yake, pia jua kuwa huyo bado ni mtoto hivyo anakua kama bendera, kazi yake kubwa ni kufuata upepo, kwa maana hiyo kama Mama yake akimuambie chochote basi atafanya kwakua hajui kama ni kizuri au kibaya.
Ongea na mume wako, muambie kabisa kuwa utakua Mama kwa mwanae, lakini hutapangiwa namna ya kulea, muambie hutamnyanyasa lakini hutamdekeza ili tu uonekane mwena wakati ukimharibu mtoto. Muambie kabisa wewe ndiyo mke mule ndani, unajua kuwa alishaza kabla, alishapenda na alishataka kuoa lakini ilishindikana, muambie wewe ndiyo mke wake na X wake kashaolewa hivyo anawajibu wa kuwa mume wao.
Muambie utakua mke lakini kamwe na wala hutaruhusu tena Diana aingilie ndoa yenu. Muambie utafanya kazi na mimba yako na utakua na kipato chako kwani unajiandaa kuwa Mama. Muambie kazi ya kwanza ya kuwa Mama ni kumlinda mtoto wako na si kumsikiliza mwanaume tu! Muambie kuwa kama kazi ni kumlinda mtoto basi nilazima ujiandae na ukweli kuwa yeye kama Baba hatakuepo milele, inaweza kuwa ni kwakukuacha na kwenda kwa mwanamke mwingine au kwa mipango ya Mungu.
Muambie kuwa kama hataki ufanye kazi basi utaondoka, kama hatakuruhusu uwe mke wake basi utaondoka na Diana hatakua sehemu ya ile familia, muambie kuwa kama anataka kumuona mtoto wake utampelekea kwake lakini sikua kikanyaga mule ndani hata kama ni kuomba maji basi utaondoka na hutajali maneno ya watu. Nilazima uwe na msimamo kwani kwa uliyopitia bila kuwa hivyo, bila kutokumjali mume wako nina uhakika kuwa utakuja kufa kama si kwa kujiua bali hata kwa presha.”
Baada ya kuongea naye sana Sabrina alikubali, alinisikia na kunielewa na kwenda kuongea na mume wake. Kama kawaida mume wake alidhani kuwa antania lakini tofauti na zamani ambapo akiongea huishia kulalamika lalamika safari hii aliongea kama mtu mzima, hakuna chozi wala kulalamika, mumewe alishtuka kidogo. Lakini hakujali, aliona kama kawaida, lakini siku ailiyofauata aliporudi kutoka kazinia limkuta mke wake kashamfukuza kazi Flora bila kumuambia.
Kwa zamania singeweza na mume wake alipohojia limuambia “Flora alikua hapa kusaidia kazi za ndani, hizi ni kazi zangu, mimi simhitaji kwa sasa hivyo sidhani kama nilipaswa kukuambia, labda kama siku ukija ukakuta nguo zako hazijafuliwa nikalalamika basi ndiyo utaniuliza.” Alijibu kwa kigupi na hakuendelea na maelezo mengine, mumewe alishangaa. Usiku huo huo wakiwa pamoja Diana alipiga simu, alikua anataka kuongea na mume wake lakini Sabrina aliichukua ile simu na kumuambia.
“Huwezi kumpigia simu mume wa mtu usiku kama huu, kama unataka kujua hali ya mwanao itakua ni mchana na sikupiga kila siku, sasa hivi mimi na mume wangu tunalala isitusumbue!” Alimaliza kuongea na kukata simu, mumewe alibaki kaduwaa hakuamini kama mke wake kawa vile. Jackson hakua na namna ni kama kwa namna falania likubaliana na mabadiliko ya mke wake, ingawa mara kadhaa alikua akinuna nuna lakini Sabrina hakujali aliponuna bila sababu alinyamaza kimya bila hata kumuuliza kwanini kanuna.
Mwezi uliopita Sabrina alijifugua mtoto wa kike, Mama mkwe wake alienda kumhudumia na hakukua na kelele kelele tena. Andrew bado anaishi pale tena hasomi bweni kama zamani, hakuna mawasiliano ya kila siku na Mama yake, alishamuwekea kuwa kama akipiga nyimbani absi ataongea na mtoto wake mara tatu kwa wiki na kama hataki basi aje amchukue mtoto wake kwani ile ni nyumba yake hapangiwi. Sabrina anaishi vizuri na Andrew na anampenda kama mtoto wake na Andrew ana furaha kwani hakuna kudanganya danganya kwa Baba yake kuwa anapigwa au anateswa.
***MWISHO;
0 comments:
Post a Comment