Search This Blog

Wednesday, June 22, 2022

MANENO YA WATU, KAMA HUJAMFUMANIA MWENYEWE BASI HACHEPUKI

  


IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO


YAMENIKUTA; MANENO YA WATU, KAMA HUJAMFUMANIA MWENYEWE BASI HACHEPUKI

Nilikua nampenda sana huyu Kaka, nampenda na yeye ananipenda, alikua ananijali. Nilikua katika mahusiano ambayo kila rafiki yangu alikua anatamani kuwa na mtu kama mimi. Iddi (sio mimi ila ni jina lake halisi) alikua ananipenda, kikubwa nilichokua nikikipenda kwake alikua ni muwazi kwangu na mara nyingi akijihisi kuwa kakosea huniaomba msamaha bila hata mimi kuniambia.

Siku moja nilipigia simu na rafiki yangu, ni rafiki yangu wa karibu sana mabye alikua anajua kila kitu kuhusu mahusiano yetu.
“Wanaume ni mashetani, ungejua kitu ambacho Iddi anakufanyia halafu huyu mshenzi ndiyo anataka kukuoa, aisee….” Aliniambia mambo mengi sana, lakini hayakua maneno tu, mwisho alinitumia na picha ya mpenzi wangu kasimama na Dada mmoja, huyo Dada alikua kavaa kinguo kifupi na walikua kama wamekumbatiana.

Kulikua na watu wengine pembeni lakini nilitumiwa tena picha nyingine wakiwa wameshikana mikono. Kuna picha nyingine mchumba wangu alikua kasimama ila kamuinamia huyo Dada kwenye meza ni kama wanaongea flani, yaani kama wananong’onezana. Kusema kweli niliumia, nilipaniki, nilikasirika, nilivimba na kila kitu kilikua si sawa kwangu.

Mimi si mtu wa kuongea, mara nyingi huwa napenda kuchunguza sana mambo mpaka nikipata ushahidi. Nilibaki na zile picha kwenye simu yangu nikisubiri kama niyapata ushahidi mwingine. Nilianza kufuatilia simu yake, nilitafuta mtu akanifundisha namna ya kuhack nikawa nasoma meseji zake lakini sikuona kitu.

“Mama alikua akiniuliza mipango yetu vpi kwenu nataka kuja kujitambilisha…” siku moja Iddi aliniambia, nilimuangalia kwa hasira na kujikuta nanuna. Sikumjibu chochote, nilikua nimekaa nikaondoka kwa dharau.
“Wanaume ni washenzi, yaani juzi alikua na mwanamke mwingine eti leo ndiyi anajifanya kuja kwetu?” Hapana, nilimpigia simu rafiki yangu na kumuambia. Aliniambia nisikubali mpaka nijue huyo mwanamke ninani, aliniuliza kama nimemuuliza nikamuambia hapana, nakusanya kwanza ushahidi.

Sijui kwanini lakini kwa namna falani niliona kama rafiki yangu alihuzunika kidogo. Alianza kuniambia kuwa wanaume si watu wa kuwaamini, akaongea maneno mengi sana kuponda huku akiniambia.
“Kuwa na msimamo, kama ameanza umalaya sasa hivi kbla ya dnoa unafikiri akikuoa itakuaje.” Kweli nilimualewa na niliendelea kuchunguza.

Siku nyingine rafiki yangu alinitumia screenshot ya huyo dada katika Instagram, alikua kapost picha ya mpenzi wangu kaandika one in a milioni, siwezi kukusahau.” Kumbe alishamtafuta na kumpata, huyo dada alikua na picha nyingi sana katika ukurasa wake lakini alipost hiyo moja tu kuhusu mpenzi wangu. Nilizidi kuumia lakini sikusema chochote, mchumba wangu naye alikua kawaida ingawa kila siku alikua akiniuliza kama nina tatizo gani?

Sikumuambia kitu zaidi ya kusema kuwa nipo sawa, bado nilikua nafuatilia simu yake na sikuona kitu chochote. Siku moja nilikua napita sehemu, nikaiona Gari ya mpenzi wangu, niliamua kwenda kumuona lakini ile nafika tu niliona yule dada yuko kwenye siti ya mbele. Huyo dada aliniona lakini hakua akinifahamu, mchumba wangu alikua kwenye simu yake kama kuna kitu anaangalia hivyo hakuniona.

Niligeuka na kupanda bodaboda na kuondoka, hilo liliniuma sana. Nilijisikia vibaya na kuamua kuwa ndiyo ulikua mwisho wa mahusiano yetu. Nilimpigia simu rafiki yangu ambaye alikuja, tukaanza kuongea huku akiniambia nimuambie ukweli huyo mchumba wangu. Lakini mimi sikutaka nilianza kupunguza mawasiliano, nikabadilika, aliponiuliza ndipo nilimuambia kuwa nimeshagundua tabia yake hivyo hana haja ya kunidanganya.

Nilimtumia zile picha za yule dada na kumuambia nilishamuona sehemu na yule dada. Kwanza alicheka kisha akaniuliza “Inamaana unakasirika kwasababu ya huyu, hembu kuwa siriasi, mimi si wa kihivi…” Alimalizia kwa kucheka. Nilimuonyesha shoga yangu akaniambia kuwa wanaume wote ndiyo walivyo, mbona hakuambii kuwa ni nani?

Siku iliyofuata alinitafuta na kuniambia kuwa yule dada ni rafiki yake. Walikua wanafanya kazi sehemu moja na siku ambayo zile picha zilipigwa ilikua ni sherehe ya rafiki yao mwingine na alienda. Nilimuuliza kwanini hakuniambia kuwa kuna shereeh tukakubaliana anaenda peke yake alinijibu kuwa yeye ni mwanaume hawezi kuomba ruhusa kwangu.
“Nisamehe sikukuambia lakini sio kama kila kitu ninachofanya ni lazima kukuambia.” Nilimuuliza kuhusu hiyo siku nyingine kwanini ampakize mwanamke kwenye gari yake akaniambia yule dada alikua anatafuat chumba na yeye kama mwenyeji alimpa lift tu, tena sio kama walipanga bali alikutana naye akampa lift.

Nilimuambia sitaki kumuona tena na huyo dada aliniambia kwa upole.
“Nakupenda lakini mimi ni mwanaume, kama nitakuruhusu kunipangia mtu wa kuongea naye, huniamini kiasi kwmaba unaona naweza kuchepuka kwakua tu nimempa mtu lift basi hunijui vizuri, ni kama hauko tayari kuwa na mimi. Nakuamini na naamini kama utamaua kuchepuka utafanya kwamaamuzi yako hata nikikuchunga haitasaidia.”

Aliniambia tumalize hayo mambo kwani ananipenda na mimi nilikubali. Lakini nilipoenda kuongea na rafiki yangu aliniambia mambo mengi kiasi nikaogopa. Nilizidi kuchanganyikiwa, nikaacha kumtafuta, nikabadilika, mwisho nikajikuta na mimi nakua na ukaribu na Kaka mwingine ambaye alikua ni rafiki wa muda mrefu.

Sikua napenda urafiki naye lakini ni kama nilitaka mchumba wangu kuona na yeye kuumia. Siku moja nilim,post huyo Kaka na kuandika kitu kilekile ambacho yule dada aliandika. Nilijua mchumba wangu ataona, aliona kweli lakini hakuniuliza. Alibaki kimya kitu ambacho kilizidi kuniumiza, niliona kama hanipendi, kama hanijali tena.
“Angekua anakupenda angekasirika lakini ana mtu wake ndiyo maana hajali.” Rafiki yangu aliniambia, usiku wake nilijiokuta napata hasira, nikamtumia mchumba wangu meseji.
“Naona bora tupeane muda tu, kila mtu ajitathimini kama bado anamhitaji mwenzake." Nilimtumia hiyo meseji nikitegemea atanitafuta na kuniomba msamaha lakini alinijibu kwa kifupi tu “Poa”

Sikumtafuta tena na wala yeye ghakunitafuta. Kama mwezi hivi nilijikuta naingia kwenye mahusiano na yule Kaka mpya, sikua nampenda lakini nilikua mpeke nammiss mpenzi wangu nikiona kama ameniacha. Basi nikiwa kwenye mahusiano na yule kaka siku moja mchumba wangu alinitumia meseji.
“Tunachofanya ni utoto, unajua nakupenda, unajua siwezi kukusaliti, najua unanipenda na najua huwezi nisaliti. Hembu tuache huu utoto nakuja hapo kazini kukuchukua.”

Kabla ya kujibu hiyo meseji mchumba wangu alikua ofisini kwangu, aliniita mpaka kwenye gari. Kuingia tu nikamkuta yule dada.
“Aisee ongea na mke wangu kua wewe si mchepuko wangu, muambie…” Aliniambia, yule dada alianza kujielezea kuwa yeye ni rafiki tu walijuana na wanasiadiana.
“Muonyershe na picha.” Alimuambia, alinionyesha na picha nyingi za ile sherehe ambayo walipiga na watu wengi, wanaongea wana hug na kunionyesha mchumba wake katika lile kundi.

“Huyu ni mchumba wangu kanivalisha pete naye siku ile alikuepo na hapa akisalimiana na Iddi” Kusema kweli nilijisikia aibu kwani kila kitu kilikua wazi, ilikua ni sherehe ya washikaji wanaojuana na wadada karibu wote walivaa kizungu zungu. Nilijisikia vibaya kwani nilijiona kama vile sina akili, kama mshamba flani nakasirika na vitu vidogo vidogo.
“Huna haja ya kuomba msamaha wifi, hawa wanaume si wakuwaamini sana abiria chunga mzigo wako!”

Nilijisikia vibaya sana, nilitamani kulia, nilitamani kumuomba msamaha. Tuliingia kwenye gari na Iddi akaniambia kuwa kaniandalia surprise, sikujua ni nini lakini nilienda kishongo upande. Ilikua ni siku ya kazi, jioni hivi nilikua nimetoka kazini hivyo nilivaa kikazikazi. Iddi alinipeleka kwao kunitambulisha kwa ndugu zake.

Kalikua ni kama kasherehe falni hivi, ndugu zake wote walikuepo. Sikua nimejiandaa kwa chochote lakini ile nafika tu dada yake alinichukua mpaka chumbani kwake ambapo niliandaliwa nguo za kubadilisha, kusema kweli nilishangaa, kupe yule Dada alinitambulisha kwa mchumba wake ambaye naye alikuepo pale.

Kusema kweli nilifurahi sana, si kitu ambacho nilikua nakitegemea. Kwa namna alivyokua kanichunia nilijua kabisa atakua kaniacha. Tuliongea na kufurahi, baadhi ya ndugu zake walikua wakinifahamu, walifurahi na wale ambao walikua hawanijui ni kama walikua wananijua kwani anaonekana alinisema mazuri sana huko.

Nilisahau kula kitu kuhusu yaliyotokea, sikutaka kukumbuka nilitaka tu kufurahi. Usiku kwenye saa nne hivi alinirudisha kwangu, lakini wakati narudi ndiyo niliwasha simu yangu kwani niliizima makusudi. Ile nawasha tu merseji zikaanza kuingia, nyingi sana, mara simu ikaita, niliikara bila yeye kuona, ikaita tena, niliikata kwani alikua ni yule mchepuko wangu na meseji zote zilitoka kwake.
“Vipi hutaki kupokea? Kuna nini, pokea uongee naye…” Iddi aliniambia akionyesha kukerwa na kile kitendo cha simu kuita bila kupokewa.

Asma mambo yanaanza kwenda vizuri, lakini alishaharibu na kuchepuka je nini kitatokea? Haka ni kastori kafupi tu kataendelea, kama unataka kuwa wa kwanza kukasoma basi Bonyeza link hapo, kuna kitu kikubwa kinakuja.


“Achana naye nitamtafuta, kuna huyu Kaka kun apes ayake nilimuazima sasa naona kama ananisumbua tangu asubuhi.” Nilijikuta nadnaganya, Iddi aliniangalia kwa mashaka lakini kwa kawaida si muongeaji sana na ananiamini snaa.
“Kwanini humlipi? Ni bei gani uanakudai?” Aliniuliza, niliangalia chini kwa aibu huku nikitafakari cha kumuambia. Kusema ukweli sikua na kitu cha kumuambia kwani nilikua sidaiwi. Lakini ilikua ni lazima nimuambie, ilikua ni lazima kutaja pesa kubwa kwani kwa hali yangu ningetaja hela ndogondogo angeweza kunishtukuzia.

“Milioni moja na nusu”Nilimuambia huku nikimgeukia, kulikua na kagiza hivyo hatukuonana uso, lakini nilijua lazima ananiangalia na kujiuliza ni pesa za nini hizi hivyo nilijiongeza.
“Nilimuagiza simu, nilitaka kununua hizi iPhone mpya lakini ndiyo hivyo nikaahirisha. Sasa nilikua nimemuazima yeye pesa nikajikuta natumia kwenye mambo ambayo hata sio ya msingi. Yaani hata sijui kwanini nilipata hizo tamaa, pengine na stress, si unajua na mimi nikiwa na mawazo shopping ndiyo ugonjwa wangu na kipindi hicho sikua na pesa.”

Nilimuambia Iddi hakujibu kitu chochote, alibaki kimya, alinifikisha mpaka nyumbani tukaagana viziri. Niliingia ndani huku nikitetemeaka, sikutaka kuamini kama kweli mchumba wangu alikua kaniamini kwa nilivyokua nimemdanganya. Ile naingia tu ndani nilianza kumpigia simu, Lameck (Mwanaume niliyekua nikichepuka naye) nilitaka kumuambia kuwa simhitaji tena.

“Najau ni usiku lakini naomba unisikilize, nina matatizo, Mama yangu anaumwa sana, kapata ajali nataka kumpeleka Nairobi, samahani sikukaumbia lakini mchana ulikua bize sana, hapa sina akiba kabisa, nina shida ya milioni moja tu.” Aliniambia kabla hata sijamuambia kuwa nahitaji kuachana naye. nilijikuta naishia kumuambia pole, nilikua hata sijaajua nifanye nini kuhusu mahusiano yetu.

“Kuna kitu nilikua nataka kuongea na wewe, nahitaji kuonana na wewe ila sasa kama Mama yako anaumwa….” Niliongea lakini hakujali kuhusu hilo, alizidi kusisitizia kuhusu kumkopesha pesa. Nilimuambia sina lakini hakunielewa, alinisisitiza sana kumsaidia, mimi nilimuambia sina nikakata simu bila hata ya kumuambia kuwa nahitaji kuachana naye.

Wakati nakata simu meseji ya Mpesa iliingia, ilitoka kwa Iddi, alikua kanitumia shilingi milioni moja na laki sita.
“Mlipe huyo mtu, sitaki kabisa mke wangu kudaiwa na sitaki uchukua mikopo mingine.” Alinitumia meseji, nilimshukuru nikijijfanya naenda kulipa lakini sikua nikidaiwa kitu chochote.

Nilizima simu yangu na kulala, ausbuhi mtu wa kwanza kumtafuta alikua ni Shakila, shoga yangu ambaye nilikua namuambia kila kitu katika maisha yangu na yeye ndiyo alinitumia picha za mchumba wangu na yule mwanamke.
“Kama mnaoendana basi hamna shida, lakini angalia wanaume hawa siw atu wa kuwaamini.” Aliniambia, kwa sauti yake ni kama hakufurahia mimi kumsamehe mchumba wangu, lakini sikujali kabisa, nilikua nina firaha na sikutaka kuharibu tena mahusiano. Nilianzisha mahusiano ya kijinga na Lameck, kwanza sikua nikimpenda na pili hata kama ningempenda na kuamua kuwa siriasi naye basi ingekua ngumu sisi kuonana kwasababu ya Dini.
Siku mbili zilipita bila mimi kuongea na Lameck, alikua kama kaninunia flani baada ya mimi kumnyima pesa. Nilikua bado sijamuambia kuhusu kuachana naye, nilikaa kimya kusubiri amtibu Mama yake ndiyo niomngee naye. kwakua alikua anajua na Shakila na walikua na urafiki wa karibu kuliko mimi nilimua kumpoigia kumuulizia hali ya Mama yake.

“Mama gani huyo anaumwa? Mbona Mama yake alihsakufa muda mrefu?” Shakila aliniuliuliza kwa mshangao, hapo ndipo niligundua kuwa kumbea likua ananitapeli. Moja kwa moja nilimpigia simu na kumuambia sitaki tena mahusiano na yeye. Nilimuambia kuhusu Mama yake na nikatumia hicho kama kigezo kuwa sitaki mwanaume muongo hiv yo ninamuacha kwasabbau hiyo. Tofauti na nilivyotegemea labda ataomba samaha na kutaka kurudiana na mimi Lameck aliishi akunituakna na kuniambia kuwa tusijuane.

Kwangu ilikua ni kama kanipa ka ahueni flani, nilifurahia sana kuona kuwa amekubali kuachana na mimi bila maneno meneno. Nilifuta kila kitu chake kwangu, mahusiano yetu hayakua ni ya muda mrefu hivyo hatkua na mazoea sana, ingawa mara moja moja alikua akija kwangu lakini mara nyingi mimi ndiyo nilikua nikienda kwake hivyo hakukua na ushahidi mwingi sana kwangu.

Mahusiano na Idi yalikua mazuri, kila kutu kilirudi kama zamani na tulikua na furaha. Wiki mbili baada ya kurudiana na Iddi alisafiri kwenda nnje ya nchi kikazi. Ilikua ni safari ya wiki moja, niliumia kidogo kwani tangu kurudiana naye nilikua sijawahi kufanya kitu chochote na yeye. Nilikua nahamu naye lakini katika kipindi hicho alikua bizebize kiasi kwamba kila tukipanga kuonana kufanya mapenzi kazi zilikua zinambana.

Sikua na namna, nilikua najua kuwa ni wangu na kama ni suala la kufanya mapenzi tutafanya tu. Lakini baada tu ya kuondoka nilianza kujisikia vibaya, kizunguzungu, najisikia kuchoka, mara kutapika na vitu kama hivyo, mwanzo nilijishisi ni uchovu wa kawaida, lakinis iku moja nikiwa nimetoka na shoga yangu nilijisikia vibaya, kizunguzungu mpaka kushindwa kuendesha gari.

“Mara ya mwisho kuona siku zako ilikua ni lini?” sakila aliniuliza, nilikua kama nashtuka kwani nilikua nimepitisha siku kama kumi na tano hivi b ila kuona siku zangu. Sikutilia maanani mwanzoni kwakua mara nyingi nikiwa na stress huwa nakoa siku zangu lakini lile swali lilinichanganya.
“Haiwezi kuwa mbila unajua Iddi ndiyo tumerudiana na hatujawahi kufanya chochote! Hiyo mimba labda itoke kwa Roho mtakatifu…” nilijisema huku nikimaliziaa kwa kucheka.
“Lameck ulikutana naye lini mara ya mwisho?” Aliniuliza, nilishtuka kidogo lakini sikua na waiswasi sana.

“Hawezi kuwa yule mbwa, hivi unajua kila nikikutana anye natumiaga P2, najua sio nzuri lakini kama unavyojua kuwa ni lazima kujilinda, sikuwa tayari kuzaa!” nilimuambia lakini alionekana kuwa na wasiwasi, tulipitia duka la dawa na kununua vipomo, hata haikuchukua muda, nilikua na mimba, alinipa moyo labda kwenda kupima tutapata majibu tofauti lakini haikua hivyo. Nilikua ni mjamzito na ulikua wa mwezi mmoja.

Kusema kweli nilichanganyikiwa, nilikua sijawaza kkama hicho kabisa, yaani wakati ambao mambo yangu yamekua mazuri nabeba mimba ya mwanaume ambaye hata mpango na mimi. Niliwaza mambo mengi, niliwaza kuhusu kumsingizia Iddi, niliwaza kuhusu kumuambia ukweli lakini mwisho akili yangu na baada ya kushauriana sana na Shakila nilishia kuamua kutoa hiyo mimba.

Nilijua kuwa ni dhambi, nilijua kuwa kuna madhara mengi lakini sikua tayari kuachika kwa mchumba wangu kis ani ujauzito. Shakila hakupingana na mimi, yalikua nidyo maamuzi yake pia, alikubaliana na mimi moja kwa moja. Yeye alishawhai kutoa mimba, basi alinitafutia vidonge flani nikameza, nilimeza mara mbili nikiamini kuwa mimba itatoka lakini haikutoka.

Katika ile wiki nilihangaika sana, naingia Google, naingia kwenye mitandao kuangalia njia salama za kutioa mimba changa lakini haikutoka. Mpaka Iddi anarudi bado mimba ilikua imeng’ng’ania tumboni. Sikua na naman, huku nikiogopa kuwa anaweza kunishtukizia wakati wowote niliamua kumtetgeshea mimba. Wakati huo nilikua na ujauzito wa miezi miwili, nilifanya naye mapenzi na baada ya wiki mbili nilimuambia kuwa nina mimba yake.

Kwanza hakuamini, si kwamba alikua haniamini kuwa labda ni mimba ya mwanaume mwingine hapana, alikua na hamu sana ya mtoto hivyo nilivyomuambia kuwa nimebeba mimba alifurahi sana lakini hakuamini, kwake aliona kama ni miujiza.
“Sitaki mtoto wangu azaliwa nnje ya ndoa, nataka tufunge ndoa harakaharaka, mambo ya sherehe hembu achana nayo kwanza. Nataka kujitambulisha kwanu kabla mimba haiajwa kubwa, si unajua ukisema una mimba kidinin watatumbia mpaka ujifungue, mimi nataka nifunge na wewe ndoa sasa hivi na kama ni mambo ya mpaka kujifungua basi nitafunga ndoa nyingine ila nataka kuishi na wewe nilee mimba yangu!”

Aliniambia, kwangu ilikua ni Kama Baraka, sikua ni namna gani nitamdanganya huko mbeleni kwani nilikua na ujauzito wa miezi miwili lakini nilijua kua kama akinioa basi nitajua chakufanya mbeleni, nitakua nishaondokana na aibu. Basi nilikubali na maandalizi ya kuja kwetu yalikamilika. Niliwaambia nyumbani lakini nilipomuambia shakila kuwa Iddi anakuja kwangu anataka kunioa niliona kabisa kapaniki. Hakua sawa kabisa, alinishauri mambo mengi lakini sikumualewa.

Aliniambia nijipe muda, nitoe mimba kwanza, sijui niwe makini na mambo kibao lakini mimi sikumjali. Ingawa alijifanya kama anataka kunisaidia ila niliona kama anaona wivu. Nilimpotezea na kuenda nyumbani kumtambulisha mchumba wangu na kila kitu kilienda vizuri. Niliporudi Sakila alikasirika, yaani alionyesha chuki za waziwazi, alikua kaninunia na mimi sikujali.

Siku mbili kabla ya ndoa nilipigiwa simu na Lameck, aliniambia kuwa siwezi kuolewa nikiwa na mtoto wake tumboni. Kusema kweli nilijihisi kuchanganyikiwa, niliona kama nakufa. Nilimuambia kuwa sina mimba akaniambia kila kitu kuwa akaambiwa nina mimba yake na nataka kumsingizia mchumba wangu.

Alinipa vitisho vingi, nilijisiki vibaya sana, sikua na mtu wa kuongea naye. Nilimpigia Shakila kwani ndiyo mtu pekee aliyekua anajua kuwa nina mimba aliishia kunitukana na kuniambia kuwa umalaya wangu haunihudu. Kama nimeamua kumsingizi mwanaume mimba basi yeye hakusiki katika kunitangaza.

Nilishindwa kujua cha kufanya, nilikua mwenyewe ndani, siwezi kumuambia mtu yoyoite yule, kila nikifikiria kuongea na mchumba wangu nilijisikia vibaya, niliona kama nitamuumiza, nilijua jinsi nilivyokua nampenda, nilijua kuwa hawezi kunioa tena, nilijua nitaumia tena. Usiku wa ile siku ambayo nilitakiwa kwenda kufunga ndoa na mpenzi wangu mambo yalinishinda.

Nilikua na mawzo sana, nakumbuka nilitoka usiku kwenye saa nne hivi, nilienda kwenye duka la dawa ambalo nililizoea na kununua vidonge vya Malaria zaidi ya hamsini. Nilirudi ndani na kuandika Barua nikimuomba msamaha Iddi, nilimuambia ukweli kuwa nilimsaliti kipindi tumeachana na kubeba mimba ya mwanaume mwingine. Nilimuambia kuwa nimeamua kumsingizia lakini naona kuwa siwezi kuishi, nilivimeza vile vidonge.

Lakini kumbe wakati nanunua zile dawa yule dada wa dukani aliniona. Mimi nilikua sijazoeana naye na simfahamu vizuri lakini kumbe yeye alikua akifahamiana na Iddi, alikua akijuana na kaka yake na hata hiyo kazi ni yeye alimtafutia, baada ya kuniona katika hali ile alimpigai simu mchumba wangu na kumuambia kuwa kaniona nimenunua dawa na hajui kama niko kwenye hali nzuri.

Iddi hakutulia, alimpigia simu mdogo wangu wakiume na kumuambia aingie chumbani kwangu. Ulikua ni usiku, lakini kulikua na kasherehe kadogo basi watu walikua macho. Mdogo wangu aliingia na kunikuta nimelala, povu linamtoka, Iddi bado alikua kwenye simu, alimuambaia anipe maziwa, na kunipeleka hospitali yeye anakuja.

Walinichukua na kunipeleka hospitalini, hali yangu ilikua mbaya sana nililazwa kwa siku mbili, nilipoeruhusiwa mimba iliyokua tumboni iliharibika. Pale nyumbani mdogo wangu aliiona ile Barua, lakini hakuifungua alimpa mchumba wangu ambaye aliifungua lakini hakumuonyesha mtu yoyote yule. Nilifanikiwa kutoka hospitalini lakini suala la ndoa lilisitishwa kwa muda.

Watu wangu wa karibu tu ndiyo walijua kuwa nilijaribu kujiua. Nikiwa nimekata tamaa, sijui kama Iddia tanioa au la wiki moja baadaye alikuja kwetu na ndugu zake na kusema kuwa badoa nataka kunioa. Sikuamini, nilifunga naye ndoa kishongo upande kwani nilikua sijui kwanini ananioa wakati nilikua nimetembea na mwanaume mwingine.

‘Hata mimba nilijua kuwa si yangu lakini nilitaka kukuoa hivyo hivyo kwakua nilikua nakupenda. Rafiki yako aliniambia kuhusu mimba yako siku ya kwanza tu mlipoenda kupima na vipimo alinitumia. Niliporudi nilikubali kufanya nawewe mapenzi ili unisingizie hiyo mimba tuishi kwaamani kwani nakupenda.

Ningeweza kukuacha kuoa mwanamke mwingine lakini nisingekua na manani katika maisha yangu kwani nakupenda wewe. Hukuchepuka bali ulitetereke kipindi tuko kama tumeachana.” Aliniambia, kusema kweli mpaka leo siamini kuwa nimeolewa na huyu mwanaume, ambaye nimeshamzalia mtoto mmoja na ndoa yetu ina amani sana.

MWISHO


0 comments:

Post a Comment

BLOG