Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

HATA UKIONA KIVULI CHANGU USIJARIBU KUKIGUSA!

  

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

AVID; HATA UKIONA KIVULI CHANGU USIJARIBU KUKIGUSA!


Ingawa tulisoma wote chuo kimoja lakini hatukuwahi kuwa marafiki, tulikuja kukutana wote miaka minne baada ya kumaliza chuo, wote tuliitwa katika usahili kwenye hoteli kubwa ya kifahari ambayo naomba nisiitaje. Ingawa wote tulisomea uhasibu lakini kutokana na tatizo la ajira tulienda kuomba nafasi ya kuwa wahudumu wa kawaida, wakati naomba sikujua ni uhudumu gani lakini nilikua na shida na ukiangalia mshahara wenyewe hata kama ingekua kusafisha vyoo basi ningefanya.


JOIN US ON TELEGRAM

Siku ya usahili tulisalimiana na kwakua ni sisi wawili tu ambao tulisoma darasa moja nilishangaa tunakua marafiki na kwa bahati nzuri wote tulipata kazi pale. Mimi nilipata kazi kama Waitress wakati yeye alipata kazi kama mhudumu wa stoo. Mishahara haikua mikubwa sana lakini kwa watu ambao tulishakaa nyumbani miaka minne kabla tulikua hatuna namna. Kufanya kazi sehemu moja ilitulazimisha kuwa marafiki, tulizoeana na kujikuta tunakua wapenzi.


Mimi kipindi hicho nilikua tayari nakaa kwangu, kabla ya hiyo kazi nilikua na vibiashara vyangu nikahama nyumbani na kupangisha, yeye bado alikua anaishi kwao kwani hakua na kazi nyingine yoyopte zaidi ya hiyo. Mapenzi yetu yalianza kwa kasi sana, kipindi hicho ndiyo nilitoka kuachana na X wangu, kwakua nilikua kwenye maumivu makali nilijikuta nampenda na kuchanganyikiwa sana juu yake kwani alikua ni mtu tofauti kabisa na X wangu.


Alikua ni mtu wa kujali sana hisia zangu, kwakua nilishamuambia kila kitu kuhusu X wangu, David (sio jina lake halisi) alifanya kila kitu ili kunifurahisha, alikua akininunulia  vizawadi vidogo vidogo, tukiwa kazini akinitumia meseji za mapenzi na kunipa pole, pamoja na kufanya kazi sehemu moja lakini alikua anaweza kunipigia simu hata mara tatu kwa siku kwakua tu hatukua tukionana mara kwa mara kwani tulikua vitengo tofauti.


Nilimshauri kuhama kwao, pamoja na mishahara yetu kuwa kama inalingana lakini mimi nilikua na kipato kikubwa kama mara tatu zaidi yake, hii ilitokana na kazi yangu, nilikua nahudumia wageni, wengi wazungu hivyo Tip zilikua nyingi, nilikua nikikusanya hela nyingi kwa siku na kwakua nilikua mchangamfu basi kila mtu alinipenda na chenchi chenchi nilizokua nikipata kila siku zilikua ni zaidi ya mshahara wangu.


Alikua bado hajajipanga, kwakua tulishakua wapenzi na tulikua tunapendana nilimuambia kuhamia kwangu, hakua na kipingamizi, alihamia kwangu na kuanza kuishi kama mke na mume. Baada ya kuanza kuishi pamoja ndipo nilianza kuona tabia zake, alianza kuwa mtu wa hasira, kuchat na watu wasioeleweka na hakutaka niguse simu yake kabisa. Tulianza kugombana kila siku bila sababu yoyote na kil,a mara nikiongea kitu maneno yake yalikua namnyanyasa kwakua yuko kwangu.


Mara nyingi alitishia kuondoka hivyo nikaishia kuomba msamaha tu na kujishusha kwani sikutaka kumpoteza. Baada ya kuishi pamoja kwa miezi kama sita hivi nilipata ujauzito, nilimuambia kuhusu mimi kuwa na mimba yake, alikasirika na kuniambia kuwa mimi nimzembe, alinisingizia kujitegeshea na kuongea maneno mengine kibao ya kashfa, aliniambia niitoe, mwanzo nilikataa lakini aliniambia kama sitaitoa hiyo mimba basi ni bora kuchana kila mtu abebe msalaba wake.


Alikataa katakata na kuniambia kuwa hakua tayari kuwa na mtoto kwa kipindi hicho kwani hata kazi alikua hajapata ya uhakika, nilimuelewa na kuamua kuitoa ile mimba. Baada ya hapo mambo yalirudi kama kawaida,a lifurahi kwa mimi kutoa mimba yake, akarudisha mapenzi ingawa alibadilika na kuanza kukojolea nnje. Lakini haikupita hata miezi miwili, baada nilijikuta nina mimba nyingine, nilipomuambia kama kawaida yake alikataa mtoto na kuniambia niitoe ile mimba.


Hapo niliogopa, ndiyo nilikua nimetoka kutoa mimba na sasa anataka nitoe mimba nyingine, nilimuambia hapana, alikasirika na kuchukua vitu vyake, aliondoka kabisa tukawa tunakutana kazini tu, hanisalimii wala nini. Lakini nilikua naogopa, pamoja na kutamani sana kuitoa ile mimba ili angalau turudiane kwani nilijiona kama mkosaji kwa kubeba mimba wakati yeye hataki lakini nilikua nahofia kufa au kupoteza kizazi kabisa. Kwakua nilikua na vihelahela vyangu niliamua kubeba mimba peke yangu huku kila siku nikimuomba Mungu abadilishe mawazo na kurudi kwangu.


Nilijua kabisa hatatoa msaada, si kwakua hataki mtoto bali kwaku ahata kipindi tunaishi pamoja mimi ndiyo nilikua namhudumia kwa kila kitu, pamoja na kuwa na kazi ambayo inamuingizia kipato lakini mimi ndiyo nilikua natoa kila kitu, kuanzia chakula, kodi ya nyumba, umeme na kila kitu. ikitokea nikamuomba pesa au kulalamika kidogo maneno yake yalikua “Kama hatujaoana unaninyanyasa hivi kwa vitu vidogo nikikuoa si unaweza hata kuninyima chakula!”


Maneno yake yalikua yakiniumiza sana hasa namna alivyokua akiyatamka na namna alivyokua akinuna na kunifanya nijione kama mkosaji. Nilijua kuwa nikijifungua nitahangaika mwenyewe, lakini kibaya zaidi nilijua nitapoteza kazi, pale nilikua kama kibarua, sikua na ajira ya kudumu hivyo suala la mimba ilikua ni kama kujifukuzisha kazi. Kweli mimba ilipoanza kuwa kubwa niliitwa na bosi wangu, aliniambia nafanya kazi vizuri ila kwa hali yangu basi nipumzike mpaka nikijifungua ndiyo nirudi kufanya tena kazi.


Nilipewa barua ya kusimamishwa nikarudi nyumbani, kipindi hicho nilikua na ujauzito wa miezi saba. Lakini sikushangaa sana nilikua nishajiandaa, nilirudi kwangu na kuanza Biashara ya genge palepale nyumbani, sikutaka kukaa na kuanza kutumia pesa yangu yote niliyokua nimejiwekea akiba kwani nilijua kuwa nikijifungua mambo yatakua magumu zaidi. wakati huo David alikua hawasiliani na mimi kabisa, alikua hapokei hata simu zangui ingawa alijua kuwa nimefukuzwa kazi.


***


Nilifanikiwa kujifungua salama, nilienda kwa Mama Morogoro, alinihudumia kwa mwezi mmoja, kwakua naye hali yake ilikua ngumu kwani kipindi hicho Baba yangu alikua anaumwa sukari, wadogo zangu walikua wanasoma na Mama hakua na kazi ya kueleweka zaidi ya vibarua vya kufuafua kwa watu niliamua kurudi Dar na mwanangu ili kuendelea kuuza genge na kumsaidia Mama kusomesha wadogo zangu.


Nilikaa kwa mwezi mmoja, siku moja nikiwa sina hili wala lile, David alikuja nyumbani, nilimkaribisha vizuri tu sikutaka kuonyesha kinyongo. Aliniambia kuwa kaja kumuona mtoto, aliniomba msamaha akiniambia kuwa alifanya makosa kunilaumu mimi kwa kubeba mimba yake wakati kitendo tulifanya wote, aliniambia yupo tayari kuhudumia mtoto na anataka turudiane na kuendelea kulea mtoto kama familia.


Ingawa nilifurahia moyoni lakini sikumuamini, nilimuambia kuwa kama anamaanisha basi anioe au hata kwenda kujitambulisha kwetu kwani tayari tuna mtoto wa kutuunganisha. Alikubali kunioa lakini aliniambia kwanza akajitambulishe na tukiweka mambo sawa basi atatuma watu kwetu. Nilifurahi sana kwani nilishakata tamaa ya maisha kumlea mwanangu, alienda kujitambulisha na nyumbani walimpopkea vizuri, aliporudi aliniambia kuwa hajapata sehemu ya kuishi, alikuja tukaanza kuishi pamoja.


Maisha yaliendelea lakini ghafala nilishangaa haendi kazini, alikua ni mtu wa kuchelewa kuamka, akiamka anatoka na kuzungukz zunguka kisha kurudi, mwanzo aliniambia kuwa yuko likizo lakini miezi miwili ilipita, kibaya nikuwa kila siku alikua hana pesa,a likua hahudumii kwa chochote na akirudi anataka chakula. Sikua na binti wa kazi hivyo kila kitu nilikua nikifanya peke yangu lakini alikua haisaidii kwa chochote, hata kuondoa kikombe kichafu mezani alikua anatuma.


Siku moja nilimuuliza kuhusu kazi akaniambia hayo ni mambo yake binafsi nisimuulize na kunitishia kuwa kama nimechoka kuishi naye nimuamhie, wanawake wapo wengi akitaka yeyote tu anachukua. Nilinmyamaza lakini niliamua kuchunguza, bado nilikua na mawasiliano na baadhi ya wafanyakazi wa ile hoteli, niliwauliza wakaniambia kuwa alishafukuzwa kazi muda mrefu, kuna wizi ulitokea nayeye alihusika, alifukuzwa kazi kipindi kile nimeenda kujifungua.


Baada ya kufukuzwa kuna mwanamke alikua anaishi naye lakini alimfukuza ndiyo akaja kwangu. Nilimuuliza akajishusha na kuniomba msamaha, nilikua nimekasirika na nahisi alijua kuwa nitamfukuza kwangu. Aliniomba tupambane kwa pamoja, akaniambia kashajifunza amejua maisha ni nini hivyo atanhangaika kutafuta kazi. Nilimkubalia, kwelia subuhi alikua anatoka na jioni anarudi lakini hakupata kazi na kila nilipomuambia kuhusu baishara aliniambia kuwa hakuna Biashara ya hadhi yake, anahitaji mtaji mkubwa ili afanikiwe kwa haraka.


Kwakua nilikua nikimuona kama familia niliumizwa sana na ile hali ya yeye kukaa tu, kuna mchezo nilikua nikicheza, lengo langu ilikua ni kufungua kaduka kadogo, nilikua nikicheza michezo miwili na pia nilikua na akiba kidogo. Nilijikusanya na kumpa milioni mbili, lengo likiwa yeye kufungua lile duka na mimi kubaki na genge, alikubali na kuzichukua. Laqkini hakufungua duka kama tulivyoongea, nilishangaa wiki mbili baadaye anakuja na Bodaboda,  nilipomuuliza aliniambia kuwa ameona biahsara ya duka si ya uhakika hivyo kaongezea na kanunua Bodaboda mpya.


Alinipigia mahesabu mengi namna itakavyozalisha mpaka nikamuelewa. Nikidhani kwamba atakua akiendesha yeye kwakua hana kazi niliona nataafuta dereva. Nilipomuuliza alinijibu kwa shara “Wewe mpumbavu kweli, hivi ulifikiria mimi na digrii yangu niende kuhangaika na vibodaboda, una akili kweli wewe! sijui hata kwanini niko na wewe, mwanamke hutumii akili, au unafikiri8 kiwakua wewe umekata tamaa unauza magenge kama mtu wa darasa la asaba unafikiri na mimi nitafanya hivyo!”


Alinitukana sana na kukulazimisha kuomba msamaha eti kwakua nimemdhalilisha kwa kumuambia kuwa aendesehe  Dodaboda. Ili kuepusha shari kwania litaka kunipiga nilimuomba msamaha, lakini hakunisamehe, aliondoka kwa wiki mbili bila kurudi nyumbani, baadaye alirudi na nilipomuuliza alikua wapi hakua na jibu zaidi ya kuniambia kuwa aliondoka ili kukwepa manyanyaso yangu kwania lijua kama akibaki kwangu anaweza kuniua.


Maqish ayaliendelea, pamoja na kumpa dereva boaboda lakini kila mara alikua anaitumia yeye, alikua anaweza kumpigia simu dereva na kumuambia ampe pikipiki, alikua anaunguka nayo kutwa nzima, kwa maana hiyo siku nyingi kulikua hakuna cha hesbau wala nini na mara nyingi hesabu ilikua ni elfu mbili mpaka tatu. Madereva wengi waliiacha mpaka ikaja ikapaki, alikua hawezi kuisimamia mpaka ikafikia hatua kuwa mafuta kwaajili ya pikipiki wkenye mizunguko yake nampa mimi.


Nilikua naumia sana kwania likua hahudumii chochote, niliamua kumuambia Mama amabye aliniambia kuwa nivumilie kwani wanaume wote wanachangamoto. Alinisema sana na kuniambia kuwa kama nataka kufanikiwa kwenye ndoa basi nihakikishe namtunzia siri mume wangu. Aliniambia kuwa mume wangu anapitia wakati mgumu kwakua hana kazi hivyo natakiwa kumsaidia ili akifanikiwa tusihi vizuri, nilikubali na kunyamaza huku nikiendelea kuomba Mungu abadilike.


Siku moja nikiwa katika Biashara zangu David alikuja na mwanamke mmoja, alikua ni binti mdogo wa kama miaka 16, alikuja naye mpaka kwangu na kuniambia kuwa ni mdogo wake. Nilishangaa kwani ingawa nilikua sijawahi kufika kwao lakini badhi ya ndugu zake nilikua nawafahamu. Nilimpokea lakini alionekana kuwa na mawazo sana na nikimuangalia alikua na mimba kubwa tu, David aliondoka na kumaucha pale. Niliamua kumuuliza yule binti na kumbana aniambie ukweli kuwa yeye ni nani na David ni nani kwake.


“Mimi nimefukuzwa ketu, nina mimba yake aliniambia ananipenda atanioa ila sasa hivi hataki kunioa, wazazi wamenifukuza ndiyo akanileta hapa niishi na Dada yake.” Alinijibu huku akilengwa lengwa na machozi.


“Dada yake? Dada yake gani?” Nilimuuliza kwa mshangao.


“Wewe kaniambia kuwa wewe ni dada yake utanihudumia mpaka nijifungue kwani yeye kapata kazi Mkoani…”


Mambo ndiyo kwanza yameanza, kama una rafiki yako hembu mtag na muambie kuwa simulizi hii ndiyo ipo sehemu ya kwanza asije kukosa.


ITAENDELEA…


DAVID; HATA UKIONA KIVULI CHANGU USIJARIBU KUKIGUSA—SEHEMU YA PILI


“Unaasemaaaaa?” Nilimuuliza kwa hasira, yule binti ambaye mwanzoni alikua anaongea kwa kujiamini alianza kutetemeka, kalikua ni katoto kaodgo, niliona namna kalivyokua kameogopa baada ya mimi kuonyesha kukasirika.


“Ameniambia nije hapa atanioa, mimi ni mwanafunzi nasoma kidato cha pili, aliniambia ananipenda ndiyo tukafanya akanipa mimba, nyumbani wamenifukuza!” Niliishiwa pozi kabisa, nilijua kuwa David ni kicheche lakini sikuwahi kufikiria kuwa anaweza kutembea na mtoto mdogo kama yule.


“Kwenu wapi?” Nilimuuliza.


“Mbezi mwisho….” Aliongea kwa kutetemeka kwani nilishabadilika, nilimuambia kuwa mimi ni mke wa David na hawezi kukaa pale, alishtuka lakini nilipomuambia kuondoka alianza kulia. Aliniambia kuwa yeye hana pakwenda na kama akiondoka basi Baba yake atamuua kwani alishamkataa na kamfukuza Mama yake kwakua tu yeye kapata ujauzito. Alilia san ampaka nikamuonea huruma, nilimuambia basia akae asubiri, lengo langu lilikua ni kumsubiri David.


Nilitaka aje na kusema hatimaya yule binti kwani sikua tayari kumlea na kuishi naye, tayari maisha yangu yalishakua magumu na sikutaka kuongeza mzigo mwingine. Muda ulikua unakimbia sana, cha ajabu nikuwa David hakuonekana, mwanzo nilikua nikimpigia simu hapokei lakini baadaye simu ilizimwa kabisa kwani ilikua haipatikani. Nilisubiroi mpaka usiku wa manane lakini hakutokea, mpaka subuhi ya siku inayofuata ndipo niliona meseji yake.


“Samahani Mage (sio jina lake halisi) Polisi wananitafuta, huyo ni mwanafunzi nitafungwa miaka 30, baba yake anasumbua sana. Nivumilia niweke mambo sawa nimtafutie huyo binti sehemu ya kukaa kisha nitakuja kumchukua.” Iliishia hapo, nilimpigia ili niongee naye lakini simu ilizimwa tena. Hakunitafuta ten ampaka jioni,a linipigia simu na kunisalimia, kabla ya kuongea chochote aliniuliza kama polisi walikua wamefika pale nyumbani.


“Hapana lakini inabidi tuongee, mimi siwezi kuishi na huyu binti, si unajua hali ilivyo….” Nilikuambia lakini sikujibiwa, aliposikia naongelea hayo mambo alikata simu kisha akatuma tena meseji.


“Kaa naye, usimpeleke popote, sitaki hata marafiki zangu kujua chochote! Kama unataka tuachane basi muondoe huyo mtoto hapo, ukimfukuza jua mimi na wewe ndiyo basi tena na usinishirikishe kwa chochote kile, hata mwanao akiumwa anahitaji damu usiniambie.”


Meseji iliishia hapo, hakupatikana tena na wala hakutuma tena meseji. Pamoja na yote aliyokua kanifanyia lakini bado nilikua nampenda, nilimuonea huruma hasa yule binti aliponitajia kuwa Baba yake ni nani? nilijua kabisa kama nikifanya chochote basi David atafungwa miaka 30 na mimi nitajilaumu sana. Ingawa nilitamani kumfukuza yule binti lakini kila nikiwaza maisha bila david nilijiona kama sijakamilika vile, nilimuambia kuwa ataka pale mpaka hapo David akija kumchukua baada ya kupata chumba cha kumuweka.


“Mimba yako ina miezi mingapi?” Nilimuuliza yule binti, alionekana kama haelewi chochote, alikua ananiangalia tu.


“Una kadi ya kiliniki?” Nilimuuliza lakini hakuonekana kuelewa chochote, alikua hajawahi kwenda hata hospitali kupima, hakujua kuwa mi mimba alipata lini.


“Mama ndiyo alisema nina mimba baaada ya tumbo kuwa kubwa nikafukuzwa nyumbani, mimi sijui chochote.” Tumbo lilikua kubwa ingawasi ile sana, nilimuuliza maswali mwnegi mengi kuona kama naweza kukadiria lakini wapi, ila kwa namna alivyoongea nilihisi kuwa inawezekana ana miezi saba.


“Inabidi twende hospitalini ukapimwe?” Nilimuambia lakini hakukubali, alikataa katakata akihofia kuwa atakutana na mtu anayemjua na itakua shida. Baba yake alikua amemfukuza nyumbani lakinia likua anamtafuta David. Baada ya kugundulika kuwa ana mimba alikataa katakata kumtaja, hicho ndiyo kilimkasirisha zaidi Baba yake, alimpigia simu David na kumuambia, mwanzo alikataa lakinia liposikia binti anataka kumuambia Baba yake kuhusu yeye basi ndiyo alikubali na kumchukua kimya kimya.


“Mmeongea nini? Kakuambia utaka ahapa mpaka lini?” Nilimuuliza kwa wasiwasi.


“Mimi kaniambia kuwa nikijifungua atamuacha mtoto kwa dada yake na mimi nitaudi shule…” Nilichoka kabisa na kuacha kuuliza, niliona kama nitachanganyikiwa bure kwani dada aliyekua akizungumziwa ni mimi. Niliamua kukaa na yule binti mpaka hapo David atakapokuja na kumchukua, sikutaka hata kushirikisha ndugu zangu kwani nilijua inaweza kumletea matatizo David.


****


Wiki mbili zilipita bila David kuonekana, hali ilikua mbaya sana, binti wa watu alikua akilia kila siku, alikua akilalamika kuwa kaachwa katelekezwa. Nilimuomba mawasiliano na hatra ndugu yake mmoja lakini hakunipa, kwanza alikua anaoghoopa lakini nilikuja kugundua kuwa nikua alikua akimlinda David, alionekana bado kumpenda na pamoja na kumuambia kuwa mimi ni mke wa David lakini aliamini mimi ni dada yake na ipo siku David atakuja kumuoa.


Siku moja nilikua kwenye genge langu, halikua mbali sana na nyumbani, nilisikia kelele. Kuna katoto ka jirani kalikuja kakipiga kelele. Kalikua kananiambia kuwa yule binti anazaa. Niliacha kila kitu na kwenda.


“Wewe ni nini?” niliuliza, chupa ilishapasuka na nguo imeloana, alikua kakaa kwenye kochi miguu kaipanua huku akipiga kelel za maumivu. Zilikua ni kelele za uchungu, sikua nimefikiria kuwa atajifungua mapema kiasi kile hivyo nilikua sijajiandaa kwa chochote. Nilimuambia yule mtoto akamuite Mama yake ambaye alikuja na kushauri tumpeleke hospitali.


Binti alikua anakataa, bado alikua anaogopa lakini hatukumsikiliza, tuliita Bajaji na kumbeba kisha tukampeleka kwenye zahanati moja ambayo ilikua jirani. Ilikua ni zahanati ndogo tu binafsi, hatukua na pesa lakini kwa hali yake walikuja kutuhudumia, tatizo lilikua ni mensi, alikua mmoja tu tena ambaye si mzoefu, mimi na yule Mama tulilazimika kuingia ili kumsaidia wakati wa kujifungua.


Alikua kashapata uchungu lakini tatizo lilikua ni njia, njia ilikua ndogo na kikubwa zaidi alikua hawezi kusukuma mtoto, hata alipoongezewa njia bado alishindwa. Alihangaika sana kusukuma mtoto bila mafanikio. Wakati wa kusukuma mtoto alikua akiishia kujamba tu na wakati mwingine kujisaidia wmenyewe.


“Pumbavu nyie kama mngejua kuwa anafi** kwanini msingeenda hospitali kubwa akapasuliwa!” Nesi alipiga keleel, mimi nilikua simuelewi ndiyo yule Mama akasema kuwa yule binti hawezi kusukuma mtoto kwani ahsaharibiwa nyuma.


“Tumpeleke hospitali kubwa…” Nesi mwingine ambaye alikuja baadaye kusaidia alisema.


“Atafia njiani, huoni kama nguvu zimemuishia!” Tayari tulishakaa kwa zaidi ya masaa mawili binti akisukuma mtoto, alikua kachoka sana hana nguvu, analia mpaka basi. Huku nyuma tulilazimika kumsukumizia matambala na kuyashikilia ili tu a[pate nguvu za kusukuma mtoto mbele. Daktari ambaye ndiyo alikua akimiliki ile zahanati alipigiwa simu, yeye alikua anafanya kazi katika hospitali nyingine lakini kwa wakati huo alikua na mgonjwa.


Tulihangaika sana na baada ya kama masaa manne alifanikiwa kujifungua. Lakini katoto hakakulia, tulihangaika sana ila mtoto alikua kashafariki dunia. Sijui nini kilisababisha, sijui ni ile hali ya kusukuma mtoto au alishakufa hata kabla ya kufika hospitalini kwani hakuwahi kwenda kiliniki lakini yule binti alipoteza mtoto wake wa kiume. Niliumia sana kwani alikua kapitia maumivu makubwa na mtoto kakosa.


Hatukumuambia kuwa kafiwa na mtoto wake mpaka baada ya kama masaa mawili hivi, tulimuambia lakini hakuonekana kuwa sawa.


“Mume wangu ataniua, sasa hawezi kunioa tena…” Alianza kulia, nilimshangaa kwania lichokua akililia si mtoto bali alikua akiogopa kumpoteza David. Nilimtuliza na kumuambia anatakiwa kuongea na ndugu yake yoyote, alikataakatakata, yule Mama alinisaidia kuwasiliana na baadhi ya watu wa hospitali kubwa amabo walisaidia kumhifadhi yule mtoto kwani alizaliwa akiwa kafariki tusingeweza kuondoka naye na wala hatukua na pakumpeleka.


Nililazimika kurudi naye nyumbani siku ile ile kwani hakukua na kulazwa katika ile hospitali, lakini pia hatukua na pesa kwani hata pesa za matibabu nilichukua katika mtaji wangu na sikujua naenda kula nini. Nashukuru Mungu pamoja na mikikimikiki yote lakini hali yake iliimarika, vidonda pekee alivyokua navyo ni vyakuongezewa njia lakini baada ya kama siku mbili alikua karudi kwenye afya yake vizuri. Hapo ndipo nilimuona kama akili zimerudi na kuanza kuulizia kuhusu mtoto wake.


Nilikua kama namhadithia upya na kumuambia kilichokua kimetoka, nilishindwa kumvumilia nikalazimika kumuuliza ilikuaje akapata ujauzito na alikutana wapi na David. Kumbe David alikua anatembea na rafiki yake ambaye ni mwanafunzi mwenzake, huyo mwanafunzi na ana kaka yake ambaye ni rafiki mkubwa wa David, sasa katika kusimuliana mambo wanayofanya ndiyo nayeye alitamani kufanya.


“Mimi nilikua naogopa mimba lakini aliniambia kuwa siwezi kupata mimba kwani wanafanya nyuma tu!” Aliniambia.


”Nani alikuambia?” Nilimuuliza.


“Rafiki yangu, aliniambia kuwa David anataka tufranye wote watatua, alimpa pesa Shilingi elfu kumi na kusema kuwa tukifanya wote itakua vizuri!” Aliongea kwa masikitiko, ilionyesha David alikua akifanya mapenzi na wasiachana wote wawili tena kwa wakati mmoja.


“Tulikua tunafanya nyuma tu lakini mimi alinipenda na kuniambia kuwa anataka kunioa hivyo tufanye na mbele kwani hata nikipata mimba atanioa, aliniambia atanipeleka katika shule nzuri na kunijengea nyumba yangu hivyo nisiogope. Aliniambia nisimuambie rafiki yangu kwani ana mdogo na hajui mambo mazuri. Kwakua nilikua nampenda nilikubali ndiyo tukafanya nikapata mimba. Mimi sikujua kama nina mimba, nilipojua na kufukuzwa nyumbani nilimfuata ndiyo akanileta huiku nikae wakati akitafuta nyumba kubwa ili anioe, sasa mtoto kafariki atanioa kweli, mimi sitaki kurudi kwa Baba ataniua…”


Kusema kweli niliumia sana, kwa namna yule binti alivyokua akiongea nilijua badoa nampenda David. Lakini kuna kitu nilihisi, kwa namna alivyokua akiongea, pamoja na mimi kumuambia sana kuwa David hawezi kumuoa na mimi ni mke wake bado alikuahaamini. Alikua anaongea kana kwamba ana uhakika kuwa mimi namdanganya na David alikua anaumuambia ukweli, nilihisi kitui na kumuuliza kama bado anawasiliana na David, alikataa lakini nilipombana na kumkagua nikagundua kuwa ana simu na kweli anawasiliana na David.


Niliangalia meseji zake, alikua akichat na David, lakini cha ajabu hakumuambia kuwa kajifungua na mtoto kafariki, alikua akimdanganya kuwa anaendelea vizuri na mimba inaendelea vizuri. Nilimuuliza kwanini kama anawasiliana naye hamuambii kuhusu mtoto kufariki alidai kuwa anaogopa kama akimuambia atamuacha. Nilishikwa na kumuambia sitaki kumuona kwangu, nilishachoka na ujinga wake, nilimuambia kuwa ameshajifungua hivyo nikamuambia kuwa sitaki kumuona kwangu.


“Mimi siondoki, hapa ni kwa mume wangu, David ndiyo kanileta hivyo kama umechoka ondoka wewe lakini mimi siondoki! Mimi ndiyo mke wake halali wewe ni dada tu!” Kale kabinti nilishangaa kananijibu tena kwa hasira.


Kama hukusoma sehemu ya kwanza basi hakisha unafollow ukursa wangu wa Instagram @iddimakengo na Facebook Iddi Makengo


ITAENDELEA….


DAVID; HATA UKIONA KIVULI CHANGU USIJARIBU KUKIGUSA—SEHEMU YA TATU


Nilimuangalia yule binti kwa hasira huku nikiwaza huyu hanijui, kashaniona mjinga sasa. Nilimuacha akabwabwaja mambo yake mengi. Wakati mwanzoni nilikua nikimuona kama mtoto na kumuonea huruma kwa aliyokua akifanyiwa na David nilianza kumuona kama mwanamke mwenzangu, nilianza kumuona kama mwanamke alinyeniibia mume. Hasira zilinipenda na nilianza kujisikia vibaya kwa kumsaidia.


“Ningemuacha filie mbali mshenzi mkubwa huyu!” Niliwaza, kwa hasira nilizokua nazo nilitamani kumtukia na kuanza kumtandika makofi, kalikua katoto tena kadogo lakini kanaongea kwa sharau ni kama alikua kafika. “Mtu mwenyewe alimnyang’anya mwanaume shoga yake, mshenzi kabisa huyu!” Niliwaza huku nikinyanyuka, tulikua tumekaa nnje, niliingia ndani na kumuacha pale nnje, nilikusanya vitu vyake na kutoka navyo kisha nikamrushia.


“Mshenzi mkubwa wewe! Nimekusaidia halafu unalete kibvuri, sasa ondoka tuone kama huyo mpumbavu mwenzako atakuja kukutetea!” Niliongea kwa hasira, alinyanyuika na kuanza kunitukana, aliongea maneno mengi kisha akachukua simu na kupiga namba flani, mimi nilikua nimesimama tu pembeni yake namuangalia anavyohangaika. Simu ilipokelewa na alikua anaongea na David, alianza kumuambia namna ninavyomfukuza na namna ninavyomuambia kuwa mimi ni mke na si dada.


Sikusikia alichokua anaongea david lakini nilihisi kama anamdanganya, namna binti alivyokua akiitikia ni kama alikua anaambiwa asiwe na wasiwasi hapo ni kwako. Kwa muda nilikua nikimpigia David hapatikani na wala hakujibu SMS zangu, nilikasirika kuwa yule binti alikua na namba ya simu ambayo inapatikana na walikua wakiongea mara kwa mara. Kusema kweli niliumia na niliona wivu kuwa pamoja na yote niliyomfanyia lakini bado alikua akimpenda yule mtoto kuliko mimi.


Nilipandwa na hasira, nikamfuata tyule binti, nikamnyang’anya simu, nilianza kutukana na kumuambia David kuwa sitaki kumuona tena nyumbani kwangu aje achukue mzigo wake. Nilimuambia kama alikua anaogopa polisi hakuna cha polisi tena kwani mwanamke wake alishajifungua na mtoto kafariki. Hapo niliongea kwa uchungu lakini uapende wa pili David ni kama alikua amefurahi, aliposikia nimetamka vile alianza kuniulizia kilichotokea, nilimuambia kwa kifupi.


“Sasa kama amekufa wewe unachopaniki ni nini? Cha muhimu huyo binti aondoke sisi tuendelee na maisha yetu.” Aliongea bila waswiasi wowote, pembeni binti alikua akilia kwanini nimemuambia, kiburi chote kiliisha alikua akilia huku akilalamika kuwa ataachwa. Nilimuonea huruma lakini sikutaka huruma zangu kuniponza, nilimuambia David simtaki, simtaki na sitaki hata kumsikia, arudi nyumbani nguo zake na takataka zake nyingine atazikuta nnje.


Nilikata simu na kurudi kucgunga mlango, nilimchukua mwanangu na kuondoka naye, nilimaucha yule binti akiwa kakaa chinia nalia na kuniomba nimsaidie. Sikutaka kumsikiliza, niliamua kuondoka na sikuwa na mpango wa kurudi tena siku ile. Nilitaka yule binti aondoke na kweli nilijua kama nikibaki pale basi nitamuonea huruma na kumrudisha ndani. Niliamua kwenda kwa rafiki yangu ambaye niliwahi kufanya naye kazi, nilimuomba kulala pale kwa siku hiyo.


Sikufika mbali, simu ilianza kuita, alikua ni David, sikutaka kuongea naye, niliizima kabisa kwani nilijua kuwa kama nikimsikiliza akianza maneno ayke basi ningeweza kumsamehe na kurudi kumsaidia yile binti. Niliondoka na kukaa kwa rafiki yangu siku mbili, kweli niliporudi sikumkuta yule binti wala vitu vyake, nilirudi ndani na kuendelea na maisha yangu nikiamini kuwa nitakua na amani.


Lakini sikua na amani, kichwa kilikua kinauma, pamoja na kuwasha simu lakini David hakunitafuta, pamoja na yote liyokua kanifanyia lakini bado nilikua nampenda, sikutaka kurudiana naye na kila wakati nilikua nikijiambia kuwa imefika mwisho nakua na maisha yangu. lakini huwezo amini, sijui ni upendo au ujinga ila ile hali ya yeye kutokunitafuta iliniumiza sana kichwa. Baada ya kukaa kama wiki bila kusikia chochote kutoka kwake niliamua mimi kumtafuta.


Sikutaka kumtafuta kumuomba msamaha kwani sikuona kosa langu, niliamua kujifanya bado nina hasira, nilianz akwa kumtumia meseji.


“Lini unakuja kuchukua haya matakataka yako, yananijazia chumba changu tu!” Niliandika meseji na kuituma, baada ya kuituma nilitamani kuifuta, nilitamani asiione na nilitamani kukaa kimya. Nilisubiri sana jibu lake lakini halikuja, nakumbuka niliituma hiyo meseji mchana lakini usiku sikuweza kulala, kichwa kilikua kama kinauma, nilijihisi kuchanganyikiwa.


Nilikua nawaza kuwa kaniacha na kwenda kumuoa yule binti, nilijiangalia kwenye kioo mara miamia kuona kama nina kasoro yoyote lakini sikuona. Asubuhi nilishindwa kuvumilia, nilimpigia simu na kwa bahati nzuri alipoke, nilimuambia kwa hasira kuhusu kuchukua vitu vyake, lakini yeye hakupaniki,a liniambia niviandae aakuja kuvichukua. Nilitaka aongee mambo mengine, nilitaka hata aniombe msamaha, hata aseme chochote lakini hakusema.


Baada ya kuniambia niandae vitu vyake basi alikata simu. Moyoni nilitaka aondoke lakini nilijihisi mpweke sana, inagwa alikua hanisaidii kwa chochote lakini nilikua kama vile namtegemea, niliona shida sana kuishi mwenyewe. Niliwaza sana na wakati mwingine nilihisi labda nimeharakisha kumfukuza, nilijihisi kama mimi ndiyo mwenye makosa lakini nilishindwa kupata majibu.


“Akija kuchukua vitu vyake nitamuomba msamaha, nitataka tuzungumze…” Nilijiambia huku nikiwaza, nilitaka kufungasha vitu vyake lakini nilishindwa, sikutaka David kuondoka, nilijua kama nikifungasha basi akija atajua kuwa nimemfukuza, nilichoamua kufanya ni kusubira aje kuchukua, wakati anapanga basi niongee naye labda atajirudi na kuniomba msamaha. Kusema kweli nilishajiandaa kumsamehe.


“Wanaume wote wako hivi, ahat nikimaucha huyu nitakutana na mwingine ambaye naye ana matatizo kama yeye nitalazimika kuishi naye hivyo hivyo!” nilijiambia wakati najiandaa, navaa vizuri, nilitaka aje na kunikuta nimependeza labda atanitamani na kutaka kubaki.


***


Nikiwa nimejiandaa kumpokea avid mlango uligongwa, nilitoka harakaharaka kutaka kujielezea, lakini hakua David, alikua ni kaka mwingine ambaye alinisalimia. Kwanza nilihisi ni mgeni wa jirani na kutaka kumuelekeza kwa jirani ili labda David akija asinione, lakini haikua hivyo, alikua ni Derava wa bajaji ambaye aliniambia kuwa katuimwa na david kuja kuchukua vitu vyake, havikua vitu vingi hivyo hata hakuvikuhitaji gari kubwa. Hasira zilinipenda, nilimjibu bvibaya kwa hasira lakin Kaka wa watu alikua mpole.


“Dada mimi nimetumwa tu hata sijui chochote…” Nilimuambia, lakini sikumsikiliza, nilimuambia aingie ndani na kuanza kutafuta mwenyewe nguo za David, alinishangaa kwani alikua hajui chochote.


“Dada kama hakuna mizigo basi niondoke…” Aliongea kwa hasira kidogo, nilishaanza kumboa, nililazimika kukusanya nguo zake mwenyewe na kumkabidhi, aliondoka na kunaicha, kichwani bado nilikua natukana, akili yangu ilimuona David na yule binti, nilihisi wahsaoana na wanaenda kuishi pamoja.


Niliiangalia simu yangu kwa hasira, nilitaka kumpigia na kumuuliza ni kwanini kaamua kunifanyia hivyo, lakini nilisita, niliifuta namba yake ila bado nilikua nayo kcihwani. Mchana siku yangu haikua nzuri kabisa, nilishinda tu ndani, ingawa sikua na pesa lakini sikutoka hata wkenda gengeni pamoja na watu wengi kuja kuulizia vitu. Nilikua na hasira hata kwa mwanangu mdogo nilimkasirikia bila sababu, nilijihisi vibaya sana siku ile.


Usiku nilishindwa kabisa kuvumilia, niliamua kumpigia simu David, simu iliita mara mbili bila kupokelewa. Nilipga tena lakini haikupokelewa, hasira zilinipanda zaidi, nilituma meseji nyingi za kumtukana na kumuambia namna alivyo mshenzi, nilimkumbusha mambo niliyomfanyia na namna alivyoniumiza. Hazikujibiwa lakini baada kama ya nusu saa simu iliita, nilipokea kwa haraka huku nikitamani nisingetuma meseji za kumtukana.


Lakini hakua David, nilikutana na sauti ya kike, alikua ni mwanamke mwingine, haikua ya yule binti alionekana ni mtu mzima, alianza kunitukana na kuniambia nikubali kuachika, alinitukana mambo mengi mpaka nikaamua kukata simu. Nililia usiku mzima lakini nilijua kabisa kuwa ashanaicha kwania subuhi nilikutana na picha nyingi za kula raha, alikua katika nyumba nzuri na huyo mwanamke, wkeli alikua ni mtu mzima, si sana lakini alikua kamzidi umri, nilinyamaza tu na kuumia kwani nilijua harudi tena.


Tayari alishapata mtu wa kumlea hivyo niliona kabisa kwangu ndiyo baibai. Sikua na namna, maisha ilikua ni lazima yaendelee, niliendelea na baishara yangu peke yangu, kutokana na upweke nilidhani kuwa kila mtu aliyekua ananizunguka alikua akijua kila kitu, niliona aibu hata kutembea hivyo nililazimika kuhama sehemu ile. Ingawa sikua na pesa lakini sikutaka mawasiliano na David na sikutaka kukutana na mtu yeyote aliyekua anamfahamu.


Nilihamia Sinza, nilipata nyumba ya kawaida lakini nzuri, nilichukua chumba kimoja, niliendelea na biashara ya Genge lakini niliongeza matunda. Wakati mmoja nikiwa mjini nilikutana na mtu akiuza matunda ya kukatakata, nilipata wazo la kufanya hivyo nikawana nauza na baadaye nilijitahidi nikanunua friji, nikawa nafunga barafu, icecream pamoja na kutengeneza juice. Kipato kilianza kuwa kizuri na niliana kuwa na furaha tena, nilijikusanya taratribu nikaanza kuwekeza kwaajili ya kiwanja, nilitaka sana kujenga na kuwa na maisha yangu mwenyewe.


Kweli nilifanikiwa kununua kiwanja, niliuziwa na Kaka mmoja ambaye alikua akienda Kenya kusoma Digrii yake ya pili, alikua ni mfanyakazi katika idara moja ya serikali na alitaka tu kukiuza kutokana na matatizo kidogo aliyokua ameyapata. Elias (sio jina lake halisi) alikua ni mchangamfu sana, nilijikuta namepdna tu, na yeye alinipenda kama rafiki, tulijikuta tunazoeana na hata alipoondoka kwenda Kenya tuliendelea kuchat kwa simu na kuongea mara kwa mara.


Yeye alikua bado hajaoa, ingawa naye alikua hajatulia sana lakini ghafala alijikuta ananipenda na mimi nilimpenda, sijjui tulianza lini mahusiano lakini tulijikuta tunapendana na kuwa wapenzi miezi mitatu baada ya kuniuzia kiwanja na sisi kujuana. Alikua akinijali, alikua akimjali mwanangu, alikua anajuana na watu. Alinishawishi kuanza kuomba kazi upya na kaucha kufanya bishara ambazo zilikua haziniingizii sana, nilimkubalia nikaaza kuomba ingawa kupata ilikua ishu.


Siku moja aliniuliza kama nikipata kazi nnje ya nchi basi nitafanya nilimuambia popote, aliniambia kuna sehemu anaweza kuniunganishia nipate kazi. Ilikua ni hoteli moja ambapo nilikua naenda kufanya kazi kama mhasibu, kweli aliniunganisha nikapata, mshahara ulikua mzuri na yeye ndiyo alikua amesimamia kila kitu mpaka mimi kwenda. Kutokana na ugeni wangu niliamua kumaucha mwanangu kwa Mama yangu ili mimi kutafuta pesa.


Nilifanya kazi kwa miezi mitatu na mambo yalikua mazuri, Elias bado alikua ananipenda, ingawa hatukuwahi kuongea mambo ya kuwa siriasi lakini alikua akinijali sana. Siku moja nikiwa naongea na Mama aliniambia kuwa David alikuja kumuona mtoto. Nilishaanza kumsahau na nilishaacha kuumia, lakini alipotaja jina lake tu nilijikuta nachanganyikiwa, kila kitu kilisimama kichwa changu na kumiwaza tu. Mama alikua hajui kama tumeachana, mara nyingi nilikua mtu wa kuficha matatizo yetu.


Alikua anajua hatuwasiliani lakini hakujua ni kwasababu gani, alidhani ni ugomvi tu wa kawaida.


“Anatia huruma, anaonekana kuchoka, anaongea na mtoto wanapendana, anasema sasa hivi hana kazi…” Mama aliendelea kunielezea, ingawa nilikua sitaki kusikiliza kwani nilikua naumia lakini nilijikuta namaucha Mama kuniambia kila kitu, aliniambia namna alivyochoka, namna alivyochanganyikiwa, na namna ambavyo analalamika maisha magumu.


“Kwanini usimtafutie kazi huko, hata kama mmegombana lakini ni mzazi mwenzako, yeye akipata na mwanao naye kapata.” Mama aliongea, hapo ndiyo nilijifanya kuaga, nilimuambia Mama kuwa nina kazi nitampigia baadaye. Lakini ukweli nikuwa nilikua nalia na si kutaka Mama kusikia sauti yangu, nilikua nawaza mambo aliyokua amenifanyia, kuna sehemu flani ya akili yangu ilifurahia na sehemu nyingine ilimuonea huruma.


Nikiwa sina hili wala lile Mama alinitumia smeeji. Ilikua ni namba ya simu mpya ya David na aliniambia kuwa nimtafute. Nilitamani kuifuta ile meseji lakini nilishindwa kabisa, nilikua na waza sana mpaka nikajikuta nampigia, kwanza alishangaa, aliniomba msamaha, aliongea maneno mengi na nilimuonea huruma kwani alianza kulia kama mtoto akiniambia namna ambavyo kuondoka kwangu kumemfanya kuwa kama chizi. Ulikua ni muda mfupi tu lakini alikua anaonekana kuchanganyikiwa sana.


Nilijikuta nalia, tuliongea kuhusu mtoto na mambo mengi, nilimsihi kutulia na kumlaumu kwa kunitelekeza, alizidi kuniomba smamaha huku akiongea kwa huzuni. Nikiwa katika hali ile nilishtuka nilipogeuka na kumkuta Elias kasimama mlangoni, sikujua alikuja muda gani lakini alionekana kuwa na wasiwasi.


“Unaongea na nani?” Aliniuliza hukua kinisogelea.


“Mona unalia ni nani huyo unaongea naye?” Aliuliza tena huku akinyoposha mkono kutaka nimpe simu yangu.


DAVID; HATA UKIONA KIVULI CHANGU USIJARIBU KUKIGUSA—-SEHEMU YA NNE


“Mtoto wa Shangazi yangu nilikua naongea naye.” Nilimjibu Elias, nilihisi kasikia nilichokua nikiongea hivyo nilikua naogopa nikalazimika kudanganya. Kumbe hakusikia chochote, ndiyo kwanza alikua anaingia, nilimdanganyadanganya kuhusu mtu niliyekua naongea naye mpaka akanialewa. Alitaka kulala kwangu lakini sikutaka, akili yangu haikua pale kabisa, nilikua bado nawaza kuhusu David, sijui kwanini lakini baada tu ya kusikia sauti ya David nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa.


Nilitafuta visababu sababu vya mimi kuwa mbali na Elias mpaka nikafanikiwa, haikua siku hiyo tu bali hata siku nyingine, nilianza kupokea simu zake, niliacha kumjali na kila wakati nilikua mtu wa hasira sana. Wakati huo huo bado nilikua nikiongea na David na sasa hivi ilikua ni ongea ya kila siku, pamoja na gharama kubwa za kuongea naye kwenye simu lakini nilijitahidi, nilimtenga Elias kabisa.


Lakini hatabyeye hakua mwanaume wa kubembeleza, haukupita mwezi alishaniacha na alikua na mwanamke mwingine, nilijifanya kuumia na kumlaumu yeye lakini wala hakujali, tulipotezeana na kila mtu kuendelea na maisha yake. Kuachana na Elias kulinipa nafasi ya kuwa na David kwa uhuru, nilianza kupambana kumtafutia kazi, nilijua kuwa itakua ngumu sana kwake kupata kazi Tanzania hivyo njia pekee ya kumsaidia ilikua ni kumtafutia kazi kwenye.


Nilihangaika sana mpaka nikampatia kazi palepale kwenye ile hotali, kwakua naye alisomea uhasibu basi alipata kazi, alikuja na kuanza. Tulianza kuishi pamoja kama mke na mume, mambo yalikua mazuri mwanzoni, lakini ghafla David alipandishwa cheo, pamoja na kufanya kazi kwa muda mfupi tu lakini alipandishwa cheo na kupandishwa mshahara, hakunizidi sana kikipato lakini kimajukumu alikua kanizidi sana.


Kwangu nilifurahia kwani nilimuona kama mume wangu, nilianza kumuambia kuhusiana na suala la kuoana lakini alikua akipiga tarehe, kila sikua likua na sababu mpya ambazo hata hazieleweki, lakini kwakua tulikua na furaha niliamua nisimtibue. Bado tulikua tukituma pesa nyumbani kwaajili ya mtoto, nilimuambia kwakua wote tuna kazi tumchukue mtoto na kuishi naye lakini alikatakatakata, aliniambia kuwa kwa wakati huo ni lazima tutengeneze pesa kwanza kabla ya kuwaza familia.


Mimi kichwa kilikua kinauma, nilikua nawaza sana kuhusu ndoa tu kuliko kitu kingine. Lakini ghafla David alianza kubadilika, alikua ni mtu wa kulala nnje na kunijibu hovyo, nikimuuliza alinigeuzia kibao na kunilalamikia mimi kuwa namsumbua, sina amani, sina raha hivyo namfanya asitamani kurudi nyumbani. Nilijaribu sana kujirekebisha lakini wapi, hakutaka kusikia chochote. Kuna kipindi akawa anakaa hata siku mbili bila kurudi nyumbani. Niliumia sana na kumpigia simu Mama, ingawa mwanzoni sikua mtu wa kusema matatizo yangu lakini yalinifika shingoni na kuamua kumuambia.


Mama hakusema chochote zaidi ya vumilia,, niliumia sana na nilikua katika wakati mgumu sana kwani sikujua hata nivumilie nini. Siku moja wakati nakagua vitu vyake nilikuta kuna laini ya simu, niliitoa na kuweka katika simu yangu, niliangalia na kukuta alikua anachat na wanawake wengi tu, kuna baadhi ya meseji za mapenzi ambazo nilizikuta, nilikasirika na aliporudi niliamua kumuuliza. Nilipomuuliza alikasirika na kuishia kunipiga. Aliniambia kabisa kuwa mimi nimemsaidia tu maisha lakini sijamnunua hivyo nikome kumfuatilia.


Mwisho wa siku mimi ndiyo niliishia kuomba msamaha lakini hakunisikia. Aliondoka kabisa nyumbani, hakuniambia kama tumeachana lakini alipangisha chumba chake na kuniambia kuwa kama nataka amani basi ni vyema tukaishi mbalimbali kwani anahisi kuwa atakuja kuniua. Aliondoka lakini baada ya kama ya siku mbili hivi nikiwa kazini nilidondoka na kupoteza fahamu, nilipelekwa hospitalini na kugundulika kuwa nina ujauzito wa miezi miwili.


Nilimuambia David lakini hakujali, aliniambia kuwa kama nampenda na nataka tuwe na maisha nitoe hiyo mimba. Nilikataakatakata lakini alisisitiza na kuniambia kuwa hataki mtoto na mimi hivyo ni lazima kuitoa. Aliniambia kama sitatoa ndiyo tutakua tumeachana, nilimshirikisha rafiki yangu mmoja akaniambia niitoe kwani kuwa na watoto wawili halafu nikiachwa itakua shida sana kwangu kupata mwanaume mwingine. Ingawa niliumia sana lakini niilazimika kuitoa.


Nilimuambia David nikitegemea kama atafurahia lakini ndiyo kwanza alikua kama kanawa mikono. Baada ya kumuambia kuwa sina tena mimba yake nimeitoa aliniambia nisimjue tena, hanitaki kwani nina tabia ya kumtegeshea mimba hivyo kwakua hataki mtoto na mimi basi hataki kugsana na mimi tena. Niliumia sana kwani nilifanya kila kitu kwa ajili yake, nilijisikia vibaya, nilishindwa hata kufanya kazi, yeye ndiyo alikua Bosi wangu hivyo karibu kila siku tulikua tunaonana.


Hali ile iliniwia ngumu sana mpaka kufikia kutaka kaucha kazi, lakini David alikua ameacha kuhudumia mtoto, alikua hatoi chochote na nikimuambia alikua akisema kuwa mimi nafanya kazi hivyo nisimsumbue na kama nataka ahudumia basi amchukue mtoto ampeleke kwa Mama yake yeye lakini hawezi kutoa pesa kwetu na kuilisha familia yetu. Sikua tayari kwa hilo kwani mwanangu alikua bado mdogo na tayari alishamzoea Mama, nilikataa na kukata shauri la kulea mwanangu mwenyewe.


Pamoja na kufanya kazi pamoja lakini nilijikuta namchoka, moyo ulikufa nikaanza kumuona kama mtu wa akwaida, niliamua kutokuumia na kuwekeza akili yangu kwa mwanangu na maisha yangu. nilimuona namna alivyokua akiabdilisha wanawake, namna alivyokua akifanya mambo ya ajabuajabu mbele yangu ili kuniumiza lakini sikuumia. Niliachja kumuomba mmatumizi, niliacha kumnyanyekee, ofisini tuliongea mambo ya kikazi tu, kwakifupi nilicha kuhangaika naye kwa chochote.


Rohoni nilikua naumia lakini sikua na namna, maisha ilikua ni lazima kuendelea. Lakini kumbe kutokujali kwangu kulimuumiza yeye, mwanzo alianza vituko kutaka kuniharibia kazi lakini alishindwa, nilikua makini sana na mabosi wangu walikua hawataki. Walikua kama hawamuamini flani, nilipokuja kuchunguza baadaye nikajua kuwa kumbe alikua akitembea na mtoto wa mmoja wa wamiliki wa ile hoteli na ndiyo ilikua hata sababu ya kupanishwa cheo ingawa walishaachana kwani huyo binti alikua na mchumba wake na alikuja kuolewa na huyo mchumba wake.


Alianza kuwa na hasira na alionyesha kabisa kazini, alijifanya kunichukia na kunifanyia vituko vingi, nilivumilia kwa miezi mitatu bila kuonyesha kuwa bado namtaka. Siku moja jioni alikuja nyumbani kwangu, aligonga mlango nikamfungulia, alinisalimia na kuniambia kuwa kaja ili turudiane. Kwanza nilinyamaza nikidhani kuwa ni utani, lakini alisisitiza kuwa mimi ni mwanamke wake na siwezi kumuacha. Nilimkumbusha kuwa yeye ndyo aliniacha ila alinilaumu kuwa mimi nina kiburi, sinyenyekei ndiyo maana alinaicha.


“Ulipoona nimeondoka wkanini hukunitafuta, kwanini hukuja kuniomba msamaha, mimi nakupenda tuna mtoto lakini nimekaa kimya kidogo unaksirika, umenifumania badala ya kuniuliza kwanini nimechepuka unakasirika, naondoka hunibembelezi!” Alinilaumu sana na kuongea manenop ya kashfa, nilishachoka nikamuambia kuwa nilijua hanitaki tena hivyo aniache na maisha yangu. alikataa katakata akiniambia kuwa hawezi kuniacha kwani mimi ni mwanamke wake na ananimiliki yeye.


Nilikua nimechoka na kazi nilitaka kupumzika, nilimuambia aondoke ili nipumzike lakini ni kama niliuwasha moto, alianza kunipiga, alinipiga sana na huku akinitukana kuwa nina kiburi, baad aya kunipiga alinilazimisha tukafanya mapenzi. Nilishindwa kujitoa kwake, alimaliza na kuondoka. Baada ya siku hiyo akawa kila siku jioni anakuja na tunafanya mapenzi, alijifanya kubadilika na kuomba rurudiane, mwanzo alikua kama ananibaka lakini baadaye niliamua kumkubali kwakua nina mtoto naye na nilikua bado nampenda.


Tulirudiana lakini bado alikua makini, aliniambia wazi kuwa hataki mtoto hivyo kama nikibeba mimba basi itakua ya kwangu. aliniambia nitumie vidonge vya uzazi wa mpango kweli nilitumia na yeye alikua akimwaga nnje. Tuliendelea na mahusiano ya namna hiyo, mara tunagombana mara hivi mara vile, nado alikua hahudumii mtoto na nilikua nikiongea mambo ya maendeleo au ndoa alikua akikasirika na kusema kuwa nina kasumba ka kumtibua na siridhiki na maisha yangu.


Niliamua kunyamaza. Siku moja nikiwa kazini kuna Mama mmoja aliniambia kuwa nina mimba, nilishangaa kwani sikua na mazoea naye lakini nilikua niemsimama najihisi kizunguzungu. Nilikataa kwani nilikua najua natumia dawa za uzazi wa mpango, ingawa nilikua na muda sijaona siku zangu lakini sikuwahi kusikia hali ya ujauzito, kutokuona siku zangu nilijua kuwa inatokana na mabadiliko ya kimwili hasa baaada ya kuanza kutumia vidonge vya uzazi wa mpango.


Lakini baada ya kuniambia nilianza kuwa na wasiwasi, niliona kuwa nipime tu na kweli nilikua na ujauzito wa miezi mitatu, nilishtuka sana na nilikua nikiogopa sana, kwanza nilikua nikiogopa kumpoteza David, nilijua kabisa kama nikimuambia kuwa nina mimba yake basi tananilazimisha kutoa au kuniacha, sikua tayari kutoa hivyo nilikaa na mimba yangu mpaka ilipofikisha miezi sita, nilikua naificha kwa kuvaaa manguo makubwa na David kila siku alikua ananiambia kua nimenenepa lakini hakujua kama nina mimba.


Nilikua naogopa sana kumuambia mpaka siku moja nilipoitwa ofisini kwa Bosi wetu, nilipewa barua ya kusimamishwa kazi kutokana na upotevu uliokua umetokea, sikua nikijua chochote mpaka nilipotoka pale.


“Unafikiri unaweza kubeba mimba mimi nisijue, sasa sikutaki, rudi Tanzania mimi uniache na maisha yangu.” Aliniambia kwa dharau, nilimuuliza kajua lini aliniambia muda tu alishajua nina mimba na alipanga kuniacha kwakua hanitaki tena, anahitaji kua mwanamke mwenye akili, mwanamke ambaye wanaweza kutengeneza maisha na si kama mimi wa kuzaazaa tu.


Niliumia sana lakini niliumia zaidi aliponiambia waziwazi kuwa suala la mimi kufukuzwa kazi ni mipango yake, alifanya hivyo baada ya kuona nataka kumharibia maisha yake hivyo hanitaki tena. Niliumia sana kwani alikua hanitaki na alishaniharibia kazi, nilimuomba msamaha lakinia likataa katakata alinikumbusha kuwa nafanya makusudi kwani nilimpa majukumu ya mtoto wa kwanza wakati yeye alikua hataki, aliniambia anataka kula maisha kwanza na nikizaa mtoto nitafute mwanaume wa kumpa.


Niliondoka Kenya nikiwa kama nimechanganyikiwa, nilirudi Tanzania, kila mtu alinichangaa, Mama na ndugu zangu wengine waliniambia kuwa nina mimba lakini nilikataa, nilikua naumia sana na nilikua nikimuwaza David, sikutaka kumuambia mtu kuwa nina mimba. Nilishukia nyumbani, kipindi hicho nilikua nawajengea wazazi wangu na nyumba ilikua ishakamilika. Ilibakia vitu vidogo tu, nilikua na chumba changu lakini sikutaka kukaa nyumbani, nilienda kwa rafiki yangu mmoja na kumuomba kukaa naye.


Sikumuambia chochote, sikumuambia kuhusu mimba au kuhusu kuachana na David, alijua nimekuja likizo na nilikuja kula bata hivyo alinipokea akiamini kuwa nina pesa nyingi za kutumia. Lakikini akili haikua pale kabisa, nilikua nawaza kuhusu mimba yangu, nilitamani kuitoa, kichwani kuna kitu kilikua kikiniambia kuwa kama nikiitoa na kurudia usichana basi David atanisamehe na atakubali kurudiana naye.


Nilijiambia hivyo, ingawa mtoto alishakua mkubwa lakini sikua tayari kuwa Mama tena. Nilienda katika hospitali moja binafsi, nikamuelezea daktarai hali yangu, nilitoa pesa kidogo kisha akanichoma sindano falni na kuniambia kuwa nirudi nyumbani kila kitu kitakua sawa. Nakumbuka ilikua ni siku ya jumatano, nilikaa kwa siku tatu bila kusikia chochote, lakini siku ya nne jumamosi usiku nikiwa nimelala nilianza kupatwa na uchungu.


Rafiki yangu yeye alikua katoka na mpenzi wake na hawakua na mpango wa kurudi, nilikua ndnai peke yangu, nilipata uchungu wa kujifungua kabisa, nilikua naumia na nikiwa sina hili wala lile mtoto alianza kutoka. Kwakua haikua mara yangu ya kwanza nilikua nikijua nini chakufanya, nilianza kumsukuma mtoto kwa nguvu, hakua mkubwa na kama dakika kumi hivi mtoto alitoka. Nikiamini kuwa tayari ashafia tumboni nilisikia sauti ya mtoto akilia.


Mwanzo nilidhani ni nnje lakini baada ya kusikiliza vizuri nilisikia sauti ikitokea katikati ya miguu yangu. hapo ndipo nilikua kama nimezindika, nilinyanyuka na kuangalia kile kiumbe. Alikua ni mtoto kabisa ana karibu kila kitu, ingawa kalikua kadogo kama kapaka flani hivi lakini alikua kama binadamu na abdo alikua analia. Nilijikuta nashikwa na ganzi mwili mzima, nilikichukua kile kchanga na kukipakata mikononi, bado nilikua sijakata kitovu, nilikua kama nimechanganyikiwa nakiangalia tu huku bado kikilia.


DAVID; HATA UKIONA KIVULI CHANGU USIJARIBU KUKIGUSA—-SEHEMU YA TANO


Nilijikuta napige kelele nyingi kuomba msaada, kwa bahati nzuri wakati huo rafiki yangu na mpenzi wake ndiyo walikua wanarudi, walinikuta nimekishikilia kitoto changu mikononi, sijakata hata kitovu, nilikua nikilia sana, rafiki yangu alinishika na kwakushirikiana na mpenzi wake walinisaidia kukata kitovu. Walikichukua kile kichanga na kukimbia nacho mpaka kwenye gari, waliniambia tupande na mpenzi wake alianza kuendesha gari kuelekea hospitalini.


Lakini hatukufika mbali, kichanga kiliacha kulia na kunyamaza kimya. Rafiki yangu alimuambia mpenzi wake kusimamisha gari. Alimuambia kuwa mtoto ameshafariki hivyo hakukua na haja ya kuelekea tena hospitalini. Alinigeukia na kuniuliza nini kilikua kimetokea, nililazimika kumuambia kila kitu, kwa wakati huo nilikua nikiongea tu kama chizi, nilikua sieleweki.


Waliogopa kunipeleka hospitalini kwakua nimetoa mimba, walinisaidia kukizika kile kitoto, lakini kabla ya kufanya hivyo rafiki yangu alichukua namba ya David na kumpigia simu, alimuambia kilichotokea lakini David hakujali. Alimuuliza sasa unaniambia mimi ili nifanye nini? Siwezi kumfufua huyo mtoto ila muambie kafanya uamuzi mzuri! Alikata simu, tukazika kitoto huku bado nikiwa siko wkenye hali nzuri kabisa.


Kwa kipindi cha miezi miwili nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa, nilikaa kwa yule rafiki yangu kwa muda, alipoona hali yangu inazidi kuwa mbaya aliamua kunirudisha nyumbani kwetu. Tayari nilishawajengea wazazi wangu hivyo walinipokea kwa uchungu kwani waliniona tu nakonda bila kujua sababu ya mimi kukonda. Nilikua mtu wa mawazo sana, nilijiona kama sina thamani, nilijihisi kama tatakata na kweli niliona kama maisha yangu yamesimama, kila siku nilikua nikiangalia simu yangu kuona kama David hata atanitafuta.


Bado nilikua nampenda, pamoja na yote aliyokua amenifanyia lakini ilikua ngumu sana kumchukia. Nilikua natmani anipigie simu, aniambie kuwa amebadilika na kila kitu kitakua sawa, nilitamani aniambie kuwa mimi ni mwanamke wa maisha yake, nilitamani aniambie kuwa ni shetani alimpitia ila yuko tayari kubadilika kwaajili yangu. lakini hakuniambia, hiyo simu haikupigwa na kila siku nilizidi kunyong’onyea.


Nikiwa katika ile hali ya upweke kuna rafiki yangu alikua akianzisha mgahawa, nilikua tu nyumbani sina kazi, alikuja na kuniomba nikae pale kumsaidia katika kupika. Hakua na mtaji mkubwa hivyo aliniambia kuwa atakua akinilipa Shilingi elfu tatu kwa siku. Kwangu ilikua ndogo sana lakini kwakua sikua na kazi na nilitaka tu kitu cha iunitoa nyumbani basi nilikubali kufanya ile kazi. Kweli ilinisaidia, kule kuwa bize na kazi kila mara kulinifanya kumsahau kidogo David.


Mchana nilikua bize sana na wateja, sikua na muda wa kupumzika na usiku nilikua nachoka hivyo kulazimika kulala mapema ili kujiandaa kwa kazi siku inayofuata. Hali yangu ilianza kurudi kuwa vizuri, nilianza kujihisi vizuri,. Afya ilirudi na nilianza kuwa na tabasamu tena. Watu walianza kuniona na kunitamani, wengi walinitongoza lakini sikua tayari kuingia katika mahusiano, nilikua na mipango yangu mingi na nilitaka kuelekeza akili yangu katika maisha hasa kumhdumia mwanangu.


Akili yangu ilikua inawaza Biashara tu, nilijikusanya sana mpaka nikapata mtaji wangu, nilikua na laki mbili na nilitaka kufungua sehemu ya kupika chips, nilijua kabisa kuwa nitauza kwani naweza kutengeneza pilipili nzuri na kachumbari tamu. Nilitafuta eneo ambalo nilikua nikilipia elfu mbili kwa siku, nilianza kupika chips na kweli nilianza kutengeneza pesa nzuri tu, mambo yalianza kubadilika taratibu, niliajiri mtu mwingine wakunisaidia na pia nilianza kuuza vinywaji, mwanzo ilikua ni vya rejareja.


Lakini kuna rafiki yangu amabye alikua anafanya kazi katioka kampuni moja ya maji, alipoona nina eneo zuri alinishauri kuwa nitafute stoo ili wawe wananiuzia maji kwa bei ya kiwandani na mimi niwe namtoa kidogo. Sikua na mtaji ndipo aliniambia kuwa anaweza kunifanyia mpango niwe nachukua maji kwa mkopo nalipa nikishauza. Lilikua ni dili zuri sana kwangu, nilikubali na kweli nilianza kuifanya hiyo kazi na nilianza kutengeneza pesa nzuri. Nilimaolizia vizuri nyumba ya wazazi wangu na kununua kiwanja kingine.


Katika miezi nane yote hiyo sikuwahi kuwasiliana na David na wala sikuwa na mahusiano mengine yoyote yale, nilikua na furaha na nilimchukua mwanangu na kuanza kuishi naye kwani kwa kipindi chote hicho alikua akiishi kwa Mama yangu. Mammbo yalianza kuninyookea, nilijikusanya na kununua gari Vitz kwaajili ya kutembelea kwani nilikua na mishemishe nyingi sana mjini. Siku moja nilipoke simu na namba mpya, baada ya kusalimiana niliikumbuka sauti, ilikua ni sauti ya Mama David.


Muda mrefu ulikua umepita nikiwa sijawasiliana nao, tangu kuachana na mtoto wao nilijiweka mabli nao, hata namba za simu nilibadilisha kwani kuna mdogo wake na David alikua na tabia ya kunipigiapigia sana kunisalimia. Hakua anajua kuwa nimeachana na Kaka yake, bado aliniita wifi. Mama David alinipigia huku akiwa analia, nilimuuliza kulilkua na nini akaniambia kuwa mdogo wake David ambaye alikua ndiyo anamfuatia alikua amefariki dunia na alikua anashangaa kwanini sijaenda.


Nilimuambia kuwa sikua na taarufa ndiyo aliniuliza kama mwenzangu hajaniambia.


“Mwenzangu nani?” Nilijikuta namuuliza kwa mshangao, kwa wakati huo hata sikufikiria kama anamzungumzia David.


“David,,,” Aliniambia, ndipo nilishtuka na kumuambia hapana.


“Yuko hapa njoo umuone…” Aliongea huku akimalizia na  maneno mengi ya kunisihi kuwa natakiwa kwena na kuonana na mwanae, aliniambia kuwa David alikua kaja kwenye msiba na mwanamke mwingine mkenya lakini yeye hamtaki.


“Wajaluo hapana, hawezi kuoa huko, hapana, anatakiwa kukuoa wewe, una mtoto naye na sisi tunakujua…” Aliongea maneno mengi sana akinipamba kuwa mimi ndiyo mwanamke pakee ambaye wananitambua, hawezi kuruhusu mwanae kuoa mwanamke mwingine.


“Tangu kuachana na wewe hata nyumbani katusahau, hatumi hata Shilingi kumi, kila kitu anamfanyia huyo mwanamke, hapana, njoo pigania ndoa yako, wewe ndiyo mkewe halali.”:


Mama aliongea sana, David alikua kaja na mwanamke kutoka kenye, tena Mama mtu mzima, ambaye alikua ameolewa na kuachika na ana watoto wawili. Alimtambulisha kama mkwe na ndugu zake walimkataa. Pamoja na kwamba nilipoachana na mtoto wao hata hawakujali, walikua upande wake lakini baada ya kumuona yule mwanamke mwingine walinikumbuka mimi. Walidhani labda dada wa watu ndiyo kambadilisha David ndiyo maana hatumi matumizi nyumbani lakini haikua kweli, ingawa huyo mwanamke mpya nilikua simfahamu kwani si yeye niliyemuacha naye Kenya lakini nilijua tabia za David.


Katika kipindi chote nikiwa naye alikua mbinafsi sana, alikua hahudumii kwao na ndugu zake mimi ndiyo nilikua nikiwasaidia. Mama yake akihitaji pesa alikua akiniambia mimi, akilalamika namtumia ili kulienda ndoa, nilichokiona nikuwa baada ya mimi kauchana ya mtoto wao hawakua na namna nyingine ya kupata pesa kwani walikua hawajamzoea huyo mwanamke. Mwanzo sikutaka kwenda kwani nilijua fika kuwa Mama yake alitaka kunitumia tu na hakukua na mapenzio, lakinia lisisitiza sana, akawa anaomba kumuona mjukuu mpaka nikaona sio ishu ngoja niende.


Wakati wote huo David hakuwahi kunitafuta, hakuwahi kuniambia chochote, ni Mama yake na ndugu zake wengine walikua wakinisumbua. Nilienda na kumuona, hata hakujali wala kufurahia kuniona, ni kama alijua mipango ya ndugu zake kwani alinichukua wakati wote nikiwa kule, hata wakati wa kutambulisha alinitambulisha kama mzazi mwenzake na kumtamulisha mwanamke wake kama mke wake. Nilijisikia vibaya sana na kujiona kama takataka. Lakini ile hali ya kumuona tu nilikua kama nimechanganyikiwa, kila kitu kiliamka upya, nilijikuta naanza kuumia kumuona yuko na mwanamke mwingine.


Nilikumbuka namna nilivyokua nimehangaika naye, nilikumbuka jinsi nilivyomtafutia kazi na machungu yote niliyovumilia. Nilijikuta nashindwa kuvumilia nikaanza kutokwa na machozi, nilikua katika hali mbaya sana, nilipoona mambo yamensihinda niliaga, nikamchukua mwanangu na kuingia kwenye gari nikaondoka zangu. Niliondoka nikiwa naumia sana, nilikua nikiwaza mambo mengi, niliendesha gari kama mwenda wazimu, sijui nilifikaje fikaje lakini mawazo hayakuisha.


Nilijitahidi sana kumsahau lakini wapi, sikuweza, niliumia kwa wiki mbili hivi ndipo nilipoke simu kutoka kwa David, alikua kasharudi Kenya na aliniambia kuwa amenitafutia kazi katika hoteli na kama vipi niende kuifanya. Kusema kweli nilichanganyikiwa, kwanza hakuomba msamaha, hakuongea kimapenzi na wala hakuonyesha hata kwamba ananitaka. Alionekana kujali tu kuhusu kazi na alipomaliza aliniambia nifikirie kehso yake nimpe jibu ili kama sitaki ampe kazi hiyo mtu mwingine.


Alikata simu na nilipompigia tena ili kupata maelezo mengine alikua hapatikani, usiku huo sikulala kabisa. Si kwamba nilikua nahitaji kazi hapana, nilikua na Biashara zangu na nilikua na kipato kizuri tu, lakini nilikua nikimkumbuka David na nilikua nahitaji mwanaume, nilikua mpweke sana na nilikua na maumivu makali kwenye moyo wangu. Niliwaza sana lakini sikupata majibu, David alikua anahitaji majibu haraka, kesho yake tu na mimi nilikua sijajipanga kwa chochote.


Niliwaza kuhusu Biashara yangu, mwanangu maisha yangu ya baadaye, kuna kitu kilikua kikiniambia kuwa labda kabadilika na kama nikienda basi tunaweza kuwa familia tena. Nilifikiria sana na kuamua kwenda. “kama hajabadilika nitarudi kuendelea na Biashara zangu!” Nilijiambia huku nikinyanyua simu na kumpigia dada yangu, alikua kaolewa na alikua hana kazi, nilimuambia nimepata kazi Nairobi na nilitaka kumuachia duka ili aliendeleze. Sikutaka kumuambia kuwa ni David kaniita kwani nilijua kua watapaniki na kunikataza.


Tayari walishajua alichonifanyia, ingawa walikua hawajui kila kitu lakini ile hali tu ya kunitelekezea mtoto iliwaumiza. Kwakua hakua na kazi na mara kwa mara alikua akija dukani kwangu basi alikubali kuja, nilimuomba kubaki na mwanangu ili niende kuweka mambo sawa kwanza kabla ya kurudi kumchukua, alikubali na nilimpigia simu David kumuambia kuwa nimekubali kwenda kuifanya hiyo kazi. Sikuulizia chochote kuhusu kazi, sikuulizia kuhusu malipo, sikuulizia kama ni wapi, akili yangu ilikua ikimuwaza David na nilijua aliniita kwakua bado ananipenda.


Siku mbili baadaye nilikua Nairobi, kwakua nilikua na kila kitu haikua shida kwangu kufika. Nilitegemea David atanipoke auwanja wandege lakini haikua hivyo, nilienda mwenyewe na hata nilipofika na kumtafuta aliniambia nichukue hoteli kwani yeye yuko bize. Hakunitafuta mpaka siku yapili, alinipeleka kwenda kusaini mkataba, alikua kanitafutia kazi katika hoteli nyingine ambayo ilikua mbali kidogo na alipokua akifanya yeye.


Baada ya kukamilisha kila kitu aliniambia kuwa nitakaa Hotalini mpaka pale ambapo nitapata chumba, nilishangaa kidogo na kumuuliza kwanini nisikae kwake.


“Kwangu, wewe vipi, mimi nimekutafutia kazi kukusaidia, unafikiri labda nakutaka, hivi una akili kweli, mimi nilishakuacha muda mrefu nina mwanamke wangu mzuri tu hivyo siwezi kuharibu mahusiano yangu kwaajili yako!” Aliongea kwa hasira kidogo huku akitoa simu yake na kunioneysha mwanamke wake, alikua ni mwingine tofauti kabisa na yule ambaye alimleta Tanzania.


DAVID; HATA UKIONA KIVULI CHANGU USIJARIBU KUKIGUSA—SEHEMU YA SITA


Nilihisi kama nimepigwa na kitu kizito kichwani kwangu, David kunitafutia kazi na kuniita Kenya kwangu ilikua ni kama kaniambia kuwa ananipenda na anataka turudiane, sikutaka kuamini kuwa aliniitia kwaajili ya kazi.


“Niliona unateseka nyumbani nikaona nikusaidie kupata kazi kama ulivyonisaidia, sitaki mapenzi na wewe, nimeshalipa deni langu la kunitafutia kazi, sitaki tena kuwa na mtu kama wewe!” aliniambia, kwake mapenzi niliona kama vile yameisha.


Nilijaribu kumbembeleza na kumkumbusha kuhusu mtoto, nikamkumbusha tulipotoka lakini hakujali.


“Kila siku unakumbusha trulipotoka, kwahiyo unataka niwe na wewe kwakua tu uliwashi kunisaidia, ni maisha gani hayo ya kipumbavu namna hiyo, mimi nishakuchoka, sikutaki, hizo habari zako za tulipotoka sitaki kuzisikia na ndiyo maana nimekutafutria kazi ili huu ujinga uishe kabisa!” aliongea, kwa namna nilivyomsikiliza alionyesha kuumizwa sana na mimi kumtafutia kazi.


Aliona kama mafanikio yake yote ya maisha yalitokana na mimi hivyo kwa yeye kunitafutia kazi ilikua ni kama kulipa deni. Nilitamani kurudi Tanzania kuendelea na maisha yangu, nilitamani kumuacha na kumuambia sihitaji msaada wake kwani shida yangu si pesa lakini nilijizuia. Kuna kitu kilikua kinaniambia “Vumilia, kama kakuleta huku inmaana kuna kitu katika moyo wake, bado anakupenda na kama ukirudi Tanzania basi ndiyo itakua mwisho wa mapenzi yentu.”


Nisauti ambayo ilikua haitoki kichwani kwangu, niliamua kuisikiliza na kuamua kubaki Kenya ili kuwa karibu na David nikiamini kabisa kuwa kama nikiendelea kuwa karibu basi upendo utarudi. Maisha yalianza, mara kwa mara nilikua nampigia simu kumjulia hali, alikua akipokea na kunijibu vizuri ingawa alikua ni mtu wa kunisimanga mara kwa mara pale ninapozidisha kumpigia simu. Nilijitahidi kujizuia lakini nilishindwa, nilikua natamani kuonana naye wkani hatukua tukikuutana mara kwa mara kwani alinipatia kazi katika hoteli nyingine kabisa mbali na alipokua akifanya yeye.


Siku moja nikiwa sina hili wala lile David alinipigia simu usiku, ilikua ni usiku sana na alinipigia Video Call, nilishangaa kwani alishanikaaza kumpigia simu usiku, niliipokea na kumuonakakaa kitandani uchi wa mnyama, nilikua nimezima taa, akaniambia niwashe taa, niliwasha akanikuta nimevaa nguo za kulalia.


“Vua hizo nguo nataka kuona mwili wako.” Aliniambia kama vile ananiamrisha, nilisita kidogo kwani ilikua ghafla na nilijua kuwa anaishi na mwanamke, lakini alilegeza sauti kidogo na kunibembeleza.


Ni muda mrefu sana ulikua umepita yangu kuongeleshwa vile na mwanaume.


:Kubali, ndiyo anarudi kwako.” Nilisikia sauti kichwani kwangu, nilijikuta naanza kuvua nguo, alinikatisha na kuniambia kuwa niwe navua taratibu kimahaba, aliniambia niwe naichezesha simu yangu na kujishika shika sehemu mablimbali za mwili wangu, nilikua nafanya hivyo kama alivyokua ananielekeza, nilimuona akiwa anachanganyikiwa, anajichua mpaka akakojoa. Baada ya yeye kufika kileleni alikata simubila hata  kuniaga, nilihisi ni network na kujaribu kumpigia lakini simua yake ilikua haipatikani tena, alishatoka online na hjata nilipojaribu kupiga kawaida ilikua haipatikani.


Niliumia sana kwani nilihisi kanitumia tu, lakini bado kuna kitu kilinipa moyo na kujiambia kuwa ni network inasumbua. Nilisubiri9 mpaka aubuhi nikampigia simu, kwa bahati alipoke ana kuongea vizuri, lakini hakuliongelea swala la jana yake, hakusema ni nini kilikua kimetokea mpaka kunikatia simu. Nilitamani kumuuliza lakini niliogopa kumuudhi, David ni mtu wa hasira za karibu na huwa hapendi maswali maswali mengi, nilijua kama nikimdodosa dodosa naweza kumkasirisha na kuiondoa amani ambayo ilishaanza kujitokeza.


Hakutaka kuongea sana aliniambia kuwa atanipigia simu usiku. Kweli usiku alipiga, alipiga Video call na kama jana yale alianza kuniamridha mambo mablimbali, kujishika sehemu mbalimbali za mwili wangu na kunilazimisha nijichue. Alikua akiongea maneno ya kimahaba na kusimimua, hata mimi nilisisimkwa ingawa niliishia kuumia kwani ni muda mrefu sana ulikua umepita tangu kukutana na mwaaume kimwili hivyo nilikua na hamu sana. Lakini kama jana yake aliishia kukojoa, alipomaliza alikata simu.


Hali hiyo iliendelea kwa wiki mbili hivi, kila siku usikua likua akinipigia simu na kuniambia nikae uchi, ananitumia mimi kujichua na kufika kileleni. Niliumia sana lakini kwakua nilikua bado namtaka niliamua kuvumilia, baada ya wiki mbili ilipokata ile hali nilipata wasiwasi sana, nilikua najihisi vibaya, nilidhani labda kuna sehemu nimekosea, labda kuna kitu nimekifanya ambacho kimemuudhi ndiyo maana akaamua kunipotezea, aliniblok kila sehemu na hata nilipo[piga simu zake niliambiwa yuko bize.


Nilinyamaza kimya nikiogopa kumfuata kazini kwake, lakini baada ya kama wiki mbili nyingine alinitafuta, hakuomba hata msamaha na tafuta tafuta yake ilikua ni usiku, alitaka nimfanyie vilevile kama mwanzo. Nilisita na kumuuliza kwanini ananifanyia hivyo na kwanini kama ni mapenzi hataki tuonane.


“Sitaki kuonana na wewe kwani nazijua akili zako, labda ukafunge kizazi kwanza kwani nikitembea na wewe unajibebesha mimba tu! Mimi sitaki watoto sasa hivi bado mdogo nakula maisha tu!” Aliongea kwa sharayu, maneno yake yaliniumiza na kunikumbusha machungu yote ya nyuma.


Nilijikuta natokwa na machozi bila hata kujijua, alipoona vile alikata simu, nilikaa kimya kwa kama dakika mbili hivi akapiga na kuniuliza kama  nataka kuendelea naye au naendelea kulialia, nilianza kumuelezea namna ninavyompenda na namna ninavyoumia lakini hakujali, aliniambia nivue nguo na kuanza kujitomasa kwani yeye ana hamu na mimi. Nilijikuta natii kile anachoniambia, nilivua nguo na kuanza kujitomasa mpaka pale yeye alipokojoa ndipo alikata simu nikalala. Mchezo huo uliendelea lakini baad aya wiki mbili tena aliniblock.


Ile hali ya kunitafuta wiki mbili na kuniblock kwa wiki mbili nyingine ilinifanya kuwa na wasiwasi sana, nialiamua kuchunguza ndipo nilipogudua kuwa kumbe mwanamke aliyekua akiishi naye alikua akifanya kazi sehemu mbili, Mombasa na Nairobi, alikua akisafiri sana, wiki mbili anakua Nairobi na mbili nyingine anakua Mombasa. Sasa kipindi akisafiri ndiyo hunitafuta na akirudi ili nisimharibie basi huniblock na kuendelea na maisha yake, niliumia sana kwania likua akinitumia kama chombacho chake cha starehe.


Pamoja na kujua ukweli, pamoja na kuumia sana lakini bado nilishindwa kumuacha. Nilikua nalia kila siku lakini kila siku nilikua najiambia kuwa David ni wangu. “Kama angekua hanipendi asingenitafuta, kuna wanawake wangapi angewapigia simu lakini kaamua kunipigia mimi ili kumridhisha, atakua ananipenda na yeye kashindwa kunisahau!” kila siku nilikua najiambia hivyo na kujipa matumaini kuwa nitakuja kuolewa na David.


Kitu kingine kilichokua kikinipa matumaini ni wazazi wake hasa Mama yake, alikua akinipigia simu mara kwa mara, alikua akiniita mkwe na kuniambia kuwa mwanae kaniita kwakua ananipenda na hata kama hatuishi pamoja lakini nipambane ili kuhakikisha anaachana na mkenya. Alinihakikishia kabisa kuwa mimi ndiyo natambulika na hataruhusu mwanamke mwingine yeyote ile kuolewa na mwanae labda yeye asiwe ndiyo kamzaa. “Hata nikifa kavuri langu litatikisika akioa mwanamke mwingine!” alikua akiniambia mara kwa mara.


***


Kwa miezi sita hali yangu haikua nzuri, David alikua akinichukulia kama takataka, hata ilipotokea nikaonana naye bado alikua ni mtu wa kunidharau, alipenda kuniongelea vibaya na kunifanya kila siku kujisikia kama takaaka. Niliendelea kuvumilia nikiamini kuwa ipo siku mambo yatabadilika. Alienda likizo Tanzania na katika kipindi hicho Mama yake alizidi kuniambia kuwa anaongea naye na mimi ndiyo nitakua mke wa mwanae, nilikua na matumaini kwani akiw atanzania alikua akinipigia simu na tulikua tunaongea vizuri tena hazikua ni zile simu za kunitumia kiingono na kunidhalilisha.


Siku moja aliened nyumbani kwetu, alimuambia dada yangu kuwa anahitaji gari langu na mimi ndiyo imemtuma. Dada alinipigia simu na kuniuliza, David hakuniomba gari lakini alikua analitaka. Nilimuambia ampe kwani ni kama mume wangu. dad ayangu hakua na namna alimpa ile gari, baada ya hapo ndipo nilimpigia na kumuuliza kwanini aliamua kwenda nyumbani kwetu kuchukua gari yangu bila kuniambia.


“Wewe si ndiyo kila siku unahangaika nikuoe, sasa kama utakua unaniuliza kwa vitu vidogo namna hii vikubwa itakuaje?” Aliongea kwa hasira, sikumuelewa alizidi kunishambulia.


“Mimi ndiyo mwanaume, mimi ndiyo natakiwa kuwa na nyumba, natakiwa kuwa na gari lakini si wewe, sasa kama hutaki nitumie gari yako basin iambie niirudishe, siwezi kuwa na mwanamke ambaye ananinyanyasia gari!” Nilijisikia vibaya kumuuliza vile, yeye ndiyo alikua mwanaume na sikutakiwa kufanya hivyo, nilimuomba msamaha na kumuambia sitarudia tena. Lakini nilipata faraja kwani alitaja neno ndoa, nilihisi maneno ya Mama yake yamemuingia na alikua tayari kufunga ndoa na mimi.


Alikaa Tanzania kwa wiki mbili na katika kipindi chote hicho hakuwahi kunitafuta tena, pamoja na kumpa gari yangu ili atumie lakini bado alionyesha dharau na hakutaka kuwasiliana na mimi tena. Siku moja kabla David hajarudi Kenya Mama yangu alinipigia simu, David alikua ameileta gari nyumbani kwetu na alionana na Mama yangu. mama alinipigia simyu hukua kilia,  nilimuuliza kwanini alisita kidogo kisha akaniuliza.


“Huyu mwanaume una mipango gani naye?” Nilijifanya sielewi.


“Mwanaume gani huyo?” nilimuuliza lakini alikasirika na kunaimbia hataki utani anataka majibu.


“Tutaoana, tunapendana sana mimi nampenda na yeye ananipenda.” Nilimjibu kwa kifupi, ingawa nilijua mambo si rahisi kihivyo lakini sikutaka kumuangusha Mama, nilimdanganya nikiamini labda ndityo jibu anataka kulisikia, lakini haikua hivyo Mama aliniambia kuwa sipaswi kabisa kuwa na David, nilimuuliza kwanini lakini alikataa, aliniambia kuwa hata kama nimezaa naye lakini David si mwanaume.


Nilimsihi sana Mama kuniambia mambo ambayo David kamfanyia lakini hakuniambia, alinisisitiza tu nihakikishe naachana naye kwani si mwanaume wa kuitwa mwanaume. Niliumia sana kwani ilikua ni mara ya kwanza kwa Mama yangu kuniambia vile, mara zote Mama ndiyo alikua mstari wa mbele kunisisitiza kuhusu kuoana na David, ni mara nyingi sana aliniambia nisirukeruke na kuoana naye ili wanangu wasiwe na mababa tofauti tofauti. Nilijaribu kumuuliza dada na ndugu wengine lakini hakuna aliyekua tayari kuniambia nini kilikua kimetokea mpaka kumfanya Mama kusema vile.


Nilisubiri mpaka David alipokuja Kenya, nilimtrafuta na kuomba kuonana naye, nikitegemea kuwa hatakubali nilishangaa kakubali kuja, ilimuuliza kuhusu Tanzania akaniambia kuwa mambo mazuri, nikamuambia kuhusu Mama alivyosema na kumuuliza kiichotokea jibu lake lilinichosha kabisa.


“Mama yako mshenzi kabisa, hivi unaishije na Mama kama yule, kamama kamekaa kapuuzi kapuuzi! Mimi nimekaambia ukweli lakini kanajifanya kutokuelewa!” Aliongea kwa shara, alionekana kufurahia kumdhalilisha Mama yangu, kabla hata sijajibu chochote aliendelea.


“Hata akili zako nadhani umechukua kwa Mama yako, umekaa kijinga jinga, unaongea sana lakini huna kitu kichwani! Ninakusaidia sana kuwa na wewe, mwanaume mwingine angekua kashakuacha zamani!” Aliniongelesha kwa dharau, David  alikua amekuja kwangu, nilitamani kumjibu lakini nilikua na hasira sana, nilitamani kumfukuza lakini nilishindwa, nilishaoze yeye kunitukana na kuniambia kuwa sina akili, nilsihazoea yeye kunipiga na kunifanyia kila kitu lakini kwa namna alivyomuongelee na kumdharau Mama yangu niliumia sana.


“Umepika nini? Nina njaa sana?” Aliniuliza hukua kinyanyuka, alienda kwenye jiko na kufungua sufuria kuangalia chakula nilichokua nimepika. Nikweli nilikua nimempikia Pilau la kuku, chakula ambcho nilijua kuwa anakipenda, baada ya kumpigia simu akakakubali kuwa anakuja kwangu nilikua kama vile nimechanganyikiwa, kumbuka kuwa  tangu kuniita Kenya alikua hajaja kwangu, alikua hataki kabis akuniona, hata nilipokua nikilzaimisha kuoanana naye mara nyingi ilikua ni kazini kwake na maeneo mengine ya wazi.


Nilijiandaa sana nikijua kuwa kama anakuja labd andiyo anakuja turudiane, nilijua kuwa maneno ya Mama tunaweza kuyamaliza bila kugombana, nilihisi ni kutokuelewana tu kwa kawaida na hakuna kitu kikubwa cha kuzuia penzi letu. Lakini kwa namna alivyokua amemuongelea Mama yangu stimu zote ziliisha, nilishindwa chakufanya, nilimuangalia wakati anapakua chakula mwenyewe na kujiongelesha namna alivyokua na njaa, alipakua na kula mpaka kumaliza bila kujali kama niko  vizuri  au la, baada ya kumaliza kula aliingia bafuni kwangu na kuoga.


Alipomaliza kuoga aliniita chumbani, bado nilikua nimekaa kwenye kochi nimeganda hata kula sijala, akili yangu ilikua haifanyi kazi vizuuri, kuniona vile alikuja na kukaa pembeni yangu. alianz akunishika shsika na kuniomba  msamaha kwa kunitukana hasa kumtukana Mama yangu.


“Mama ni Mama hata kama hajielewi lakini sikupaswa kumtukana, isamehe, najua nimekosea lakini mwenzako nakuhitaji…” Aliongea hukua kinishikashika, nilijitahidi kuonyesha ushirikiano lakini mwili ulikua hautaki, hakutaka kusubiri, alinishika na kunivua nguo, alifanya mapenzi na mimi kinguvu nguvu.


Unadhani ni nini kitatokea, je atamruhusu kuendelea, je huu  ndiyo miwhso wa mahusiano yao. Usiache kufuatilia katika ukurasa wetu wa Instagram @iddimakengo au Facebook Iddi Makengo


ITAENDELEA….


F1eb0ruar5y m2no0hr, t20e17c94  · 


DAVID; HATA UKIONA KIVULI CHANGU USIJARIBU KUKIGUSA!—SEHEMU YA SABA


Niliumia sana siku ile kwa kutukaniwa Mama yangu kiasi kwamba sikuweza kuonyesha ushirikiano, alipoenda raundi mbili bila ushirikiano wangu aliacha, alianza kunipiga huku akinitukana, aliniambia hanitaki tena, aliondoka na kusema ni bora akatafute Malaya mwingine lakini si mimi ambaye najifanya sitaki wakati nahangaika kila siku kumpata. Aliondoka siku ileile na hakunitafuta tena, nilikua naumia kwani nilikua nikipiga simu zangu zinapokelewa lakini haongei chochote na meseji zangu hata hazijibiwi.


Lakini kila nikiongea na Mama yake alikua akinipa moyo na kuniambia kuwa mimi ndiyo mwanamke ambaye wanamtambua na mimi ndiyo mke wa David. Nyumbani kwetu Mama alikua akipiga simu mara kwa mara kunikataza kuendelea na David lakini sikumsikiliza, bado nilikua natamani sana kurudiana naye na nilitamani kumtafuta na kumuomba msamaha ingawa bado nilikua hata sijui kosa langu ni lipi.


Hali yangu ilianza kuwa mbaya, nilikosa kaisa matumaini ya kuishi, nilikonda na kuwa kama mtu mwenye UKIMWI, kazini walikua wakinishangaa kwa namna nilivyokua, kila mtu alikua akinikwepa. Nilishindwa kuvumilia na siku moja niliamua kumfuata David ofisini kwake, nakumbuka ilikua ni siku ya Jumanne, nilikaa kazini mpaka saa tao nikashindwa kufanya chochyote, miezi mitatu ilikua imepita bila kuonana na David, kwangu ilikua kama mwaka kukaa bila kusikia sauti yake.


Alikua hanipigii tena, hata zile simu za usiku ambazo kwakawaid hunipigia ili kujichua alikua hanipigii, nilishajaribu kumpigia usiku nikiwa uchi na kumtuia picha zangu za uchi lakini wala alikua hafungui hata meseji zangu, kila ukiangalia Whatsapp unaona kabisa kuwa meseji hata hazijasomwa. Nilichoka na kuamua kumfuata kazini kwake, nilifika mapokezi na kumuulizia, baadhi ya watu walikua wakinifahamu kwani kuna kipindi niliendaga na alinipokea vizuri, lakini walinishangaa kutokana na nilivyokua, nilikua nimekonda kama mgonjwa ambaye alihitajika kurudi hospitalini.


Nilimuulizia nikaambiwa subiri, alipigiwa simu na kuambiwa kuwa ana mgani wake. Ofisi yake ilikua juu na ili kuonana na mtu yoyote pale ilikua ni lazima kuacha jina mapokezi, mhusika anapigiw asimu kuulizw akama mna miadi au ana muda wa kuonana na wewe na kama akikubali ndiyo unaruhusiwa kuingia kumuona. Alipigiw asimu na alipotajiwa jina langu niliiona sura ya dada wa mapokezi ikibadilika, ni kama alikua ananionea huruma, hata kabla ya kuniambia alichikua amejibiwa nilijua kabisa kuwa nimekataliwa.


Bila kujijua nilijikuta napiga kelele, nilikua nalazimishia kuonana naye na kujitambulisha kama mke wake.


“Mimi ni mke wake, tuna mtoito naye, ni lazima kuonana naye, angalia picha ya mtoto wetu, ni mume wangu nataka kumuona!” Niliaza kupiga kelele, kila mtu alinishangaa, nilitoa picha kumuonyesha yule dada, kwa busara kutokana na kuwa na wageni wengi, baada ya kuona kama naleta fujo alinisihi ninyamaze nitaonana naye. Alichukua simu tena na kupiga, alimuambia David kilichotokea na hapo ndipo aliniambia nisubiri David mwenyewe anakuja.


Kama dakika tatu hivi David alikuja, aliniona nilivyokua, mlinzi alikua kasimama pembeni yangu, baada ya kuona nataka kuleta fujo alitaka kunitoa pale.


“Unamfahamu huyu?” Mlinzi alimuuliza David ambaye alitingisha kichwa kukubali kuwa ananifahamu, alinishika mkono na kuniambia kuwa nitoke naye nnje, alinishika kwa nguvu akawa kama vile ananivuta, tulitoka mpaka kwenye sehemu yalipokua yamepaki magari, alisogea mpaka kwa nyuma hivi ya hoteli, sehemu ambayo hakukua na watu.


Kabla hata hajasema chochote alianza kunipiga makofi, alinipiga makofi na mateke huku akinitukana kwa kutokua na shukurani na kutaka kumaharibia akzi, alinipiga sana, nilipiga kelele wakaja wakaka wawili ambao ni walinzi. Walimuuliza nini kimetokea akawaambia ni mwizi ameleta fujo ndani na sasa anataka kuniibia, aliwaambia, kaka mmoja alinivamia na kuanza kunipiga lakini mwingine alimshika na kumuambia kuwa huyo ni mwanamke muacheni tumpeleke polisi.


Wakati huo nilikua napiga kelele kuomba msamaha, nilikua nikimuambia kuwa sitarudia, nilikua nikijaribu kuwaonyesha wale wakaka picha za David kuwa nafahamiana naye lakini hawakujali, walinichukua mpaka kwenye gari yao, wakaniingiza na kunipeleka polisi. Kule hata sikuandika maelezo, ilionekana wanajuana kwani walipiga simu wakati nikiwa kwneye gari na nilipofika tu niliweka ndani. David tulimuacha hotalini kazini kwake na aliniambia kuwa hanitaki tena na ameshachoka kwani kashanisaidia vyakutosha.


Kule mahabusu nilikaa kwa siku nne mfululizo, sikufunguliwa kesi yoyote na wala hakukua na mtu yeyote aliyekuja kuniangalia, kazini kwangu nilikua nimeondoka tu, sikuomba ruhusa na wala hakuna mtu aliyekua akijua nimeenda wapi. David hakuja hata kuniangalia na hakuna mtu wa ile hoteli yao ambaye aliifuatilia ile kesi. Sikuruhusiwa kupiga simu hata nilipoomba sana ilishindikana, nilikua ni kama nimetelekezwa pale. Siku ya nne ndiyo kuna dada mmoja alikuja pale, alikua na mikwaruzo mingi kama mtu aliyekua kapigana.


Alikua kaumia sehemu mbalimbali za mwili wake na kila mara alikua anaongea peke yake, askari walikua wakimtukana na kumuambia kuwa atafia jela. Sijui ilitokea nini lakini alianza kuwa rafiki yangu, ni kama mtu alikua na maumivu na alikua akitaka sehemu ya kuyatolea, alianza kunielezea kuhusu kilichomkuta, aliniambia kuwa amemchoma kisu mpenzi wake baada ya kumfuamnia na mdogo wake na mpaka wakati huo alikua hajui kama atapona au la.


Alinielezea mambo mengi, yeye alikua ni Mkenya lakini alikulia Tanzania na huyo mpenzi wake aliyemchoma kisu naye ni mtanzania. Aliniambia kuwa hajali na hata kama kafa atatoka tu kwani kwao wana pesa na Mama yeka anampenda. Aliniambia mambo mengi, ilibidi na mimi kufunguka na kumuambia mambo yangu. Ilikua ni asubuhi alfajiri ndipo yule dada aliletwa lakini kweli kama ambavyo alisema hawezi kukaa ndani muda mrefu, mchana tu Mama yake alikuja kumchukua. Mpenzi wake alikua hajafa  lakini alikua kaumia sana hivyo bado alikua ICU lakini walionekana wana pesa sana hivyo walihongahonga akatoka.


Ilikua ni kama miujiza tu kwani alipotoka haikuchukua hata nusu saa nilifunguliwa na kuambiwa kuondoka. Aliongea na wakili wa familia yao akaulizia kesi yangu na kukuta sikua na kesi kwani hakukua na hata jalada hivyo nikaruhusiwa kuondoka. Sikumuona tena yule dada kwani wakati natoka alishaondoka, nilirudi kwangu lakinii niliporudi kazini nilikua nimeshapoteza kazi yangu, kule kuondoka bila sbabau ilikua ni kigezo cha mimi kufukuzwa, hata nilipojaribu kujielezea haikusaidia, tayari alishatafutwa mtu mwingine.


Kupoteza kazi ilimaanisha kuwa nilitakiwa kurudi Tanzania, nilijipanga na kwakua kilichokua kimenipeleka pale haikua kazi bali David nilikubaliana na hali, nilijipanga kurudi. Niliwaambia nyumbani kuwa mkataba wangu umeisha, hata Mama yake David nilimuambia hivyo hivyo, sikutaka kumuambia kilicotokea kwani bado nilikua naamini kuwa ni shetani alimpitia. Wakati nakaribia kuondoka nilijaribu kumpigia simu David lakini alikua hapatikani, nililazimika kumtumia meseji na kumuambia kuwa mimi naondoka lakini nazo hazikujibiwa, nilijiandaa na kurudi Tanzania.


****


Nyumbani kila kitu kilikua kimeharibika, dada yangu ambaye nilimuachia duka na Biashara zangu alikua kafilisika, hakukua na kitu, ingawa mara zote alikua akinidanganya kuwa kila kitu kiko vizuri lakini sikukuta chochote. Nilifika na kuwa mtu wa kuanza upya, kutokana na hali yangu, mawazo na afya hata kufanya Biashara ilikua ngumu, mambo yalikua magumu sana. Nililazimika kurudi nyumbani kwa Mama, sikikuambia kitu kilichokua kimetokea lakini alijua.


“Yule si mwanaume ni shetani!” mama aliniambia, alitaka kumzungumzia David lakini nilisita, sikutaka kusikia alichokifanya lakini Mama alilazimishia.


“Kaja hapa kataukana, mambo aliyokua anaongea sidhani kama ni ya kiume, mwanangu unatakiwa kuachana na huyo mtu.” Aliniambia, mpaka wakati huo Mama alikua hajajua kama nimeachana na David, bado nilikua naficha na nilikua naona aibu kusema mambo aliyokua ananifanyia.


“Anaongea mbele yangu, mbele ya wadogo zako mambo mnayofanya kitandani!” Mama aliendelea kuniambia, David alipokuja nyumbani kipindi anachukua gari alinisema maneno mengi ya uongo. Aliwaambia wazazi wangu kuwa mimi ni Malaya, nina wanaume wengi, natembea na wazungu ndiyo wananipa pesa za kujengea. Alikua akiwasema na kuwaambia kuwa ameshanifumania mara nyingi nikifanyiwa mapenzi kinyume na maumbile, alinisingizia mambo mengi na kuwadhalilisha wazazi wangu huku akiwatukana kuwa wao ndiyo wamebifundisha.


Yalikua ni mambo mengi ya uongo, alinidhalilisha sana kwa wazazi wangu,  nniliishia kulia tu bila kusema chochote.


“Mwanangu, sikupangii mwanaume wakuishi naye lakini angalia sana, chunga sana yule sio mtu.” Mama aliniambia, mimi niliishia tu kumkubalia na kumuambia kuwa nitakua makini naye. Nililia sana lakini nilishindwa kumuambia Mama kila kitu nikiamini kuwa itamuumiza zaidi na kuona kama nitakua najidhalilisha kwa kusema mambo aliyoku akinifanyia.


Akilini nilishachanganyikiwa, maneno ya David, namna alivyokua akintitukana, kila wakati kuniambia kuwa mimi ni mbaya, kila wakati kusema kuwa sina akili, kusema kuwa siwezi kupata mwanaume mwingine zaidi yake yaliniingia sana. Kila sikua likua akiniambia kuwa mimi tayari nimeshazaa hivyo siwezi kuolewa, aliniambia kuwa uke wangu ushaanuka sana hata yeye haufurahii akifanya mapenzi na mimi ni lazima kufikiria mwanamke mwingine la sivyo hawezi kukojoa.


Huwezi amini aliwaambia wazazi wangu hivyo hivyo kuwa mimi nimeshachoka, uchi umepanuka hivyo hata akiniacha nitaishia kuwa Malaya na sitapata mwanaume mwingine. Niliumia sana kwani nilimuamini, niliogopa hata kutongozwa na kila nikikutana na mwanaume nilikua nikiangalia chini, nilikua naona aibu na kujiona kama vile wananiona na kuuona uchi wangu ulivyo. Nilikua naogopa na kila siku pamoja na yote nilikua nikiomba David arudishe moyop wake ili angalau anirudie niweze kuwa na mtu nisije kufa peke yangu.


Lakini David hakunitafuta, nilikaa nyumbani kwa mwezi mmoja. Nilikata mawasiliano na Mama yake kabisa, sikutaka kuendelea kuwasiliana naye, nilijilazimisha kukubaliana na ukweli kuwa hanitaki basi na ndugu zake hawanitaki. Lakini Mama yake baada ya kuona kimya alinitafuta, alikuja mpaka nyumbani na kuomba kuongea na mimi, aliniomba sana kurudiana na mwanae, nilimuambia ukweli kuwa mimi bado nampenda mtoto wake lakini kwakua hanitaki siwezi kumlazimishia. Nilimuambia kilichotokea mpaka mimi kufukuzwa kazi.


Alisikitika sana na kuniambia kuwa kuna watu wanamchezea mtoto wake na si akili zake, aliniambia tuhangaike naye, alinisihi sana na kuniomba niende kuishi kwake kwani itakua ni kama nimeilewa tayari. Aliishawishi sana na kwakua nilikua naamini kuwa David ndiyo mwanaume wangu wapekee nilikubali kwenda kuishi kwake, alifurahi, niliondoka peke yangu kwani mwanangu alikua anasoma, Mama alikataa nisimchukue, lakini kwakua hakuweza kunizuia niliondoka kwalazima.


Kule nilikaa vizuri, Mama yake alikua akimpigia simu kila siku na kumuambia kuwa mke wake yupo nyumbani hivyo arudi lakini hakutaka, alikua hataki hata kuongea na mimi, alimuambia Mama yake kuwa ashamalizana na mimi hivyo niachane naye kabisa na kama nikibaki kwao basi atamuoa yeye. Nilitaka kuondoka lakini Mama yake alikataa na kuniambia kama ni kazi atahangaika nipate hapo, sikujua kwa namna gani kwani nayeye hakua na uwezo hivyo kifedha lakini alisisitiza nibaki.


Nilikaa kwa miezi mitatu bila David kuja wala kutaka kuonana na mimi, nilichoka na kuaua kuondoka, nilimuaga Mama yake kuwa anenda kutafuta kazi, nilienda kwa rafiki yangu mmoja kujishikiza lakini siku mbili baadaye nilipokea simu kutoka kwa Mama yake, alikua na furaha sana na alikua akiniambia kuwa David karudi, anataka kuongea na mimi, anataka kuniomba msamaha kwani amejutia makosa yake na anataka kunioa.


Unadhani kwamba David atamuoa? Vipi kuhusu ndoa yao itakuaje? Lakini ni kitu gani kimemfanya  David kurudi na kutaka kuonana naye wakati alishamkataa na alikua hataki hata kuongea naye?


ITAENDELEA…..


DAVID; HATA UKIONA KIVULI CHANGU USIJARIBU KUKIGUSA—SEHEMU YA NANE


Sijui ni kitu gani kiliniingia, niliposikia jina lake na kusikia kuwa anataka kuniomba msamaha nilipata kanafuu flani hivi. Ingawa sikutaka kurudi lakini nilijikuta nashindwa kulala, nashindwa kufanya kitu chohote. Kichwani kulikua na mambo mawili yalitokua yakinisumbua, jambo la kwanza lilikua ni mapenzi juu yake, alishaniumiza sana, alishanifanyia kila baya na nilishachoka lakini bado nilikua nampenda na kwa namna flani nilikua nikiamini kuwa labda ndito ambaye Mungu  kanipangia.


Kuna wakati nilikua nikijiambia kuwa hata yeye ananipenda ila tu nishetani na kilichokua kikinichanganya zaidi ni Mama yake, yeye alikua akiongelea kuhusu uchawi, ingawa alikua hajui hata nusu ya mambo aliyokua akinifanyia mwanae lakini bado aliamini kuwa hazikua akili zake kunikataa mwanamke kama mimi na kwenda kuhangaika na wanawake wengine. Mama yake alikua akihangaika sana kwa waganga na nahisi walikua wakimdanganya kwani kila mara walikua wakimuambia kuwa wananiona mimi kama mkwe wake.


Jambo la pili lilikua ni mwanangu, tangu nikiwa mdogo nilikua na picha flani katika kichwa changu, nilikua naona mimi na mume wangu na wanangu wa nne. Nilikua natamani sana kuolewa na nilikua nikiamini katika Baba mmoja, kwa maana kuwa hakuna kitu amcbho nilikua nakichukia kama kuzaa watoto na Baba todfauti, nadhani hicho ndiyo kilinifanya kuwa kama chizi kila nilipokua nikisikia jina la david.


Pamoja na kumchoka sana, pamoja na kutaka kumuacha lakini kila nikifikiria kuachana naye na kuanza upya, kila nikifikiria kutafuyta mwanaume mwingine kwaajili ya kuzaa naye, kila nikifikiria kuwa naweza kumaucha David, nikatafuta mwanaume mwingine lakini baad aya muda nayeye akabadilika na kuwa kama david huku tayari nina mtoto naye basi watoto wangu wangekua ni wa mabakabaka, kwa maana ya kila mtoto na Baba yake kitu ambcho nilikua nakiona kama laana flani, kila nikifikiria hivyo nilitamani kumsamehe na kumrudia.


Kila nikimfikiria mwanangu na kuona kuwa analelewa na Baba ambaye si Baba yake niliwaza kurudi. Nilimuelezea rafiki yangu, kwa wakati huo niltaka kupata mtizamo wa mtu mwingine, nilimuambia baadhi ya vituko alivyonifanyia, ingawa sikumuambia vyote lakini niliona kuwa kasitasita, aliniambia kuwa anayeniombe msmaaha na kutaka niridi ni Mama yake, si David mwenyewe hivyo ni ngumu kujua kama kweli kabdilika, angalau angekua ananipigia na kuniomba msamaha yeye basi ningejua nini cha kufanya.


Baada ya rafiki yangu kuniambia vile nilimuelewa, nilimpigia Mama David simu na kumuambia kuwa mimi nimechoka, siwezi kurudi kwakua sijui kama David ananitaka au la, sijui kama  amejutia makos ayake au yeye ndiyo ananiambia huku David mwenyewe akiwa hajali. Lakini ni kama nilimtuma, siku inayofuata David alinipigia simu, aliniambia kuwa anataka tuonane, aliniambia ni kuhusu mtoto mambo ya malezi kwani alishakua mkubwa na anatakiwa kwenda shule, nilimsikiliza na kumuelewa, alitaka tuonane kwao nikakataa basi tukachagua sehemu ya wazi.


Baada ya kuniambia tu kuwa anataka tuonane nilichanganyikiwa zaidi, kwanza alionekana kuabdiliak, hakua David yule ambye alikua na madharau, hakua yule ambaye simu zake husihia kwa kunaimbia nalalamika sana, mimi mabya na ananisaidia kuwa na mimi. Alikua ni tofauti kabisa, alikua ni mtu aliyetulia,a naulizia hali yangu, hali ya mtoto, ananiambia mambo mazuri kiasi kwamba niluijukuta hata namsamehe kabla ya kusikia kama anataka kuniomba msamaha.


Moyoni nilikua nikijiambia poteli ya mbali, kama kabadilika namsamhe kwani hakuna mapenzi ambayo hayana changamoto. Nilijiandaa vizuri siku ya miadi, David alikua mpole siku hiyo, tuliongea sana na kutaniana, aliniomba msamaha sana lakinimpaka wmisho hakuniomba turudiane, alikua akizungumzia mtoto, aliniambia maisha yake ya kenye, aliniambia sababu za yeye kubadilika tabia kipindi akiwa kule, aliwalaumu marafiki, akalaumu vitu vingi isipokua yeye.


Nilimsikiliza sana na kweli alikua mtu ambaye kabadilika, niliondoka nikiwa na huzuni kidogo kuwa kakaa na mimi muda wote huo lakini hakuniomba msamaha, lakini nilipata kafuraha kidogo kuwa kabadilika na kuwa mstaarabu. Baada ya hapo nilipofika nyumbani tu alinipigia kuniulizia kama nimerudi salama, aliniulizia mtoto na mambo mengi, alikua akiongea vizuri na usikua linitumia meseji ya usiku mwema, kweli nilichanganyikiwa na kuona mwanaume kabadilika.


Siku iliyofuata linitumia laki moja, kisha ikafuata na meseji ikiseka matumizi ya mtoto. Nilishtuka kidogo kwani tangu mtoto kuzaliwa mpaka wakati ule anaanza shule alikua hajatoa hata Shilingi kumi yake, hata kipindi tukiwa  vizuri kila Shilingi mimi ndiyo nilikua nikitoa kuhusumia mtoto ingawa mara nyingi niliwadanganya wazazi wangu kuwa ni yeye katoa ili kumfichia aibu. Kitendo kila kilinifurahisha sana na nilihisi kweli huenda kabdilika ingawa sikuamuamini sana.


Alianza kuwa mtu wa kupiga simu kila siku, mtu wa kutaniana, mtu wa kunijali. Hali hiyo iliendelea kwa mwezi mmoja ndipo alikuja kuniomba turudiane, kusema kweli nilifurahia hilo wazo lake la kurudiana, nilijisikia vizuri lakini niliamua kujipa muda. Nilimuambia rafiki yangu, hata yeye alikua anaona mabadilika na alikua anafurahia, aliniona nilivyokua nimebadilika na nilianza biashara ikawa inaenda vziuri, aliniambia nimpe mdua kidogo kumchunguza ziadi na baadaye wote tuliona kama kabadilika.


Nilimkubalia krudiana naye lakini kwa shariti kuwa aende kuwaomba msmaaha wazazi wangu, nilimuambia namana livyokua kawakosea, nikamuambia namna walivyoingea na kumuambia kuwa bila kuwaomba smamaha hawawezi kupoke amahari yangu na hawawezi kunipa radhi zao kwani wamemia sana na hawmataki. Alikuabli na kuniambia nimpe muda ili akienda jkwetu anakua kamaliz akila kitu, kuanzia kuomba msamaha mpaka kunioa kwani hakutaka kupoteza muda, nilikubali nikiamini kuwa kila kitu kitaenda vizuri.


*****


David aliniambia kuwa karudi Tanzania kwaajili yangu mimi, kaona kuwa kule Kenya alikua akipoteza muda na hakukua na kitu cha maana alichokua akikifanya, aliniambia kuwa ameamua kurudi ili kutengeneza familia kwani ametangatanga sana. Wakatio huo hata mimi sikua na kazi, nilikua na vibiashara vidogo vidogo ambavyovilinitosha mimi na mwanangu tu. Nilikua nikiishi kwa rafiki yangu nimejibanza, ingawa nilishajenga lakini ninyumba ambayo niliwajengea wazazi wangu na gari niliwapa wao kulitumia.


Hawakunikataza kurudi nyumbani lakini sikua huru, nilikua nikiona aibu kuishi na wadogo zangu, mwanangu aliendelea kubaki kwa Mama lakini mimi niliamua kuondoka ili kutafuta. David alitaka twende kuishi kwao lakini nilikataa, nilimuambia kabisa kuwa kama tunaanza maisha ni lazima sisi wenyewe kujitegemea kwani kuna leo  na kesho, hatuwezi kuwategemea wazazi kila siku, alikubali, alikua na kaakiba kidogo, akatafuta vyumba viwili tukahamia, kw abahati nzuri mimi bado nilikua na vitu vyangu vya ndani hivyo hatukuhangaika sana.


Kwa namana livyoniambia nikuwa alikuja Tanzania ili kufanya bishara, nilikua nikiamini kuwa ana mtaji mkubwa na anaweza kufanya Biashara. Lakini muda ulivyokua unaenda kila siku zilikua ahadi tu na mipango, kwanza aliniambia kuwa anataka kununua bodaboda kama tano hivi na kuzisimamia, lakini iliishia juu juu, mwisho akaniambia kuwa anataka kufungua duka la jumla lakini nalo lilishia juju.


Sikujua kama ana pesa na sikuwahi kuziona ingawa kila siku alikua ni mtu wa mipango na ahadi kibao, alikua akisema kuwa ana mtaji mkubwa na mipango mingi,. Cha ajabu nikuwa kila mara nilipomuambia suala la kuhudumia familia aliniambia niwe na subira kwani pesa zake ni nyingi hivyo hatakikuzitumia kwa sasa. Nilimuamini na  upendo wkeli ulikuepo tofauti na zamani, mimi bdo nilikua na Biashara zangu hivyo nilikua nikiangalia zaidi amani kuliko pesa.


Siku moja aliniahidi kuwa anaenda mwanza, aliniambia kuwa kuna dili amelipata geita la mambo ya madini, aliniambia kuwa kuna rafiki yake anafanya Biashara hiyo na kwakua yeye ni mzoefu na anajuana na watu wengi sana Kenya basi atakua akifanya naye Biashara. Aliniambia niwazo zuri linahitaji pesa nyingi na yeye ana kama milioni theklathjini hivyo anaona kama vile hazitoshi, alinishauri nitafute kama milioni kumi kumuongezea lakini sikua nazo.


Alinitafutia mteja wa gari yangu ili niuze lakini nilimuambia hapana, aende na kuanza Biashara kwanza akifanikiwa basi nitajua chakufanya lakini siwezi kuuza gari. Nilimshauri kuhusu biahsara na kumuambia asipende kukurupuka na kuwekeza pesa nyingi kwa wakati mmoja, ingawa hakufurahi lakini alionekana kunielewa, alienda mwanza na kukaa mwezi mzima. Kila siku alikua akinipigia na kuniambia Biashara ilivyo ngumu, alikua akiniambia namna alivyoekeza pesa zake zote hana hata pesa ya kula, nililazimika kuwa na mtumia elfu tano kila siku kwani na mimi kipato changu kilikua kidogo.


Baada ya kama mwezi mmoja hivi alirudi, alikua kanong’onye na nilipomuuliza kwanini aliniambia kuwa yeye na huyo rafiki yake walikamatwa na polisi wakalazimika kuhonga ili kuachiwa na mzigo wote kwakua ulikua ni wa maendo basi umetaifishwa. Alikua kama mtu aliyechanganyikiwa, alikua na mawazo sana, alilalamika na kukonda kabisa, kusema kweli nilimuamini na nikawa namuonea huruma, nilimpa mopyo na kumuambia kuwa maisha ni lazima yaendelee na tutapambana mpaka kieleweke.


Alikaa nyumbani bila kazi akiwa ni mtu wa kula kulala, kila sikua anamka saa tano anakunywa chai na jioni anatoka zake kunyw abia akirudi kalewa, hakua na pesa na pesa zote nilikua nikimpa mimi. Nikiweka kapesa kidogo anachukua, nilishindwa kumuambia kwani nilihisi kuwa ataona kama namnyanyasa. Baada ya kuona hana muelekeo nilienda nyumbani, nikachukua gari yangu na kumkabidhi nikimuambia kuwa aisajili na itumike kam Uber. Mwnazo alikataa na kusema kuwa ni Biashara ambayo itamdhalilisha, nilimsihi sana mpaka akakubali.


Alichukua kweli gari na kujisajili, lakini pesa ilikua haionekani, si kwamba kulikua hakuna Biashara hapana, Biashara ilikuepo lakinia likua mzembe, kwanza alikua akiamka saa tano asubuhi, pili akiwa kalala anazima simu au akiwa nyumbani anazima simu, sasa nikimuuliza kwanini anafanya hivyo wakati baishara yenyewe inahitaji simu alikua akilalamika kuwa na mnyanyasa, mpaka kutaka kunisusia gari. Mwisho niliishia kumuomba msamaha nikishukuru Mungu sasa hivi hanipigi tena anaishia tu kununa si kama zamani.


Lakini kuna kitu kingine kilikua kinakirea, gari ilikua chafu sana, haoshi na inanuna, nilikuambia ananuna kama kawaida yake. Sikumona nilienda kusalimia kwao, nilikutana na mdogo wake ambaye alikua anasoma kidato cha nne, alikua ananipenda na alikua akiniita wifi, mara nyingi alikua akipenda kuniambia mambo yake na tulikua marafiki wakubwa. Aliponiona alikua hana raha kabisa, nilimuuliza kwanini akaniambia kuwa ananionea huruma kwani Kaka yek ni Malaya sana, nilishangaa, akaniambia kuwa kaka yake anawachukua marafiki zake na kwenda kufanyia nao mapenzi kwenye gari.


Aliniambia ni karibu kila siku na rafiki zake imefikia hatua wanamuita wifu na kumtania kuwa wataolewa na Kaka yake, wanasimulia na ni wengi tu wanatembea naye. Niliumia sana nikiwaza namna nilivyokua nikihangaika kumbe yeye anakula maisha na watoto wadogogo. Nilishindwa kuvumilia na siku hiyo niliamua kumuambia kuwa nimechoka kwakua namhudumia kila kitu lakini bado anaendeleaza umalaya wake, niliongea sana na kumuambia kila kitu nilichosikia.


Mwisho aliniomba msamaha na kuniambia hatarudia tena, lakini jioni yake nikiwa hata sijamuambia kuwa nimenasmaehe aliniomba kunitoa out, tulitoka tukaingia kwenye gari, lakini nilishangaa tunatoka mjini na kwenda maporini kabisa, alifika sehemu katikati ya kichaka akasimamisha gari, aliniambia nitoke kwenye gari, nikiwa sina hjli wala lile alitoa mkanda wake na kuanza kunipiga nao, alinipiga sana mikanda, mateke, ngumi na kila kitu huku akinitukana kuwa kanilea muda mrefu lakini nataka kumkalia kichwani.


ITAENDELEA…


DAVID; HATA UKIONA KIVULI CHANGU USIJARIBU KUKIGUSA—TISA


Alinipiga sana mpaka nikapoteza fahamu, sikujua kilichoendelea mpaka asubuhi yake, nilishtuka nikoc humbani kwangu nimefungwa kamba kitandani. Nilitaka kunyanyuka lakini nilishindwa, ilikua ni asubuhi na sikumuona David, kule ndani kulikua hakuna mtu mwingine yeyote. Nilikua nimefungwa miguu na mikono, sikuweza kunyanyuka, nilikaa vile mpaka mchana ndipo David alikuja, alikua kalewa sana.


Alikuja na kukaa pembeni yangu, alianza kulia kama mtoto, alilia sana huku akinilaumu mimi kwanini napenda kumsingizia mambo ya ajabu ajabu, kwanini nasikiliza maneno ya watu na siruhusu mapenzi yetu yakawa ya sisi wawili. Alikua akilia akilalamika kuwa mimi amnyanyasa kwakua nina pesa, alinilazumu kuwa mimi ndiyo nimesababbisha yeye kuwa masikini kwani ndiyo nilimsahawishi mpaka kufungua Biashara.


“Kila siku ulilikua unanilalamikia, ulikua hutaki kuniona nakaa nyumbani, umeona sasa nimepoteza kila kitu lakini bado hunipi amani!” Aliongea huku akilia, huku bado akiwa amenifunga kamba alinikumbatia pale kitandani na kushikwa na usingizi. Mwili wake mzito ulinilalia juu, kamba zilikua zinikiumiza mikono yangu huku nikivumilia harufu yake mbaya ya pombe, nilivumilia kwa muda mpaka nikajihisi napoteza pumzi.


Nilikua katika hali mbaya sana, nilijihisi kama nakufa, nilikua nikiumia sana na kwa wakati ule nilikua nikiapa kwa miungu yangu yote kuwa kamwe sitarudiana naye, nilijiandaa kuachana naye na nilijua kabisa ni mtu ambaye hawezi kuabdiliak, nilijua kuwa kamwe siwezi kuwa na furaha na David na siku ile ndiyo niliamua kuwa ni lazima kuachana naye kama nataka kuwa na furaha. Nilijikaza sana, nikakusnaya nguvu na kumsukuma pembeni, alisogea lakini hakunyanyuka, alikua kalewa sana na alilala fofofo.


Nilifunga macho ili kulala lakini sikuweza, nilikua katika maumivu makali sana, sehemu zangu nyingi za mwili zilikua zimevimbiana, macho yalikua yamevimba yanauma balaa, ukichanganya na harufu yake nilikua kama niko kifungoni,. Kama masaa mawili baadaye David alishtuka, pombe ilionekana kupungua, alishtuka kuniona katika hali ile, harakaharaka huku akiniomba msamaha alinifungua kamba, alionekana kujutia alinisihi sana nisimuambie mtu yeyote.


“Yote haya nafanya kwakua nakupenda, mimi siwezi  kuishi bila wewe, nakupenda sana lakini unaponiudhi nashindwa hata chakufanya,k najaribu kusahau lakini nashindwa, unanikwaza sana, hivi kwanini huwi kama wanawake wengine, ukaniheshimu na kunichukulia mwanaume. Wewe kila siku unanidharau, unanitangaza kwa watu kuwa unanilisha, unashirikiana na Mama yangu kunihujumu, kweli nakupenda lakini unanikwaza!”


Alilalamika, sikumuelewa alichokua akilalamikia kwani hakuna kitu hata kimoja ambacho kilikua na ukweli, nilimvumilia mengi lakini abdo hakuona kama ananifanyia mabaya, aliniona mimi kama ndiyo mbaya. Aliongea mambo mengi sana hukua kisisitiza nikae ndani nisitoke, aliniambia kuwa nikitoka watu wataniuliza nimefanya nini na wakiniona katioka hali ile watanishauri maujinga. “Ndoa ni uvumilivu, mimi nataka nikuoea lakini siwezi kukuoa kama hutabaidlika, nataka tutengeneze familia yetu, sasa kama hutabdilika unafikiri itakuaje?” Aliniambia.


Kwa wakati ule nilikua kimya tu, sikua na chakumjibu, nilikua katika maumivu makali na pia nilikua na hasira, nilitamani kumtukana lakini nilijua nitaishia kupigwa tu. Ili kumfurahisha nilikubaliana nayeye, nilimuomba msamaha kwa yote niliyomfanyia na nilimuahidi kuwa baada ya siku ile nitakua nimejifunda na sitafanya ujinga tena, nitamheshimu kama mwanaume na sitakua nikisikiliza maneno ya watu. Alionekana kuniamini na alifurahi sana, aliniambia kuwa kama nikiwa hivyo basi atanioa.


Kiukweli nilikua sihitaji ndoa kutoka kwake, nilitaka tu afurahi ili kuniondokea na mimi kuondoka kuanza maisha yangu. baada ya kumuambia vile alifurahi sana, alishangilia na kuniambia kuwa atabdilika, hatakua na hasira tena. Alinikumbatia na kutaka kufanya mapenzi na mimi, nilikua na njaa, nilikua nimechoka na nilikua katika maumivu makali, nilimkatalia na kumuambia kuwa nina umwa, nima maumivu makali lakini nilimuona kama anabdilika.


“Umeanza tena mambo yako, yaani tumekua na amani kidogo sas aunataka kunipangia!”


Alifoka kwanguvu, niliyaangalia macho yake na kuona kipigo, sikua na namna nilimruhusu kuniingilia, alifanya mapenzi na mimi kwa pupa bila hata kuniandaa, nilikua naumia, machozi yananitoka, natamani kupiga kelele lakini nilikua nikiogopa, cha kushangaza nikuwa yeye alikua anafurahia, aliona kama kituc ha kawaida kabisa, hakuona kama ananiumiza, alifanya mpaka liporidhika, alitoka na wkenda kuoga kisha akarudi.


“Sitaki utoke, nikuletee nini?” aliniiliza.


“Ngoja kwanza nitoke nikaoge…” NIlimuambia nikimaanisha aniruhusu kutoka nnje kuoga, nyumba tuliyokua tukiishi ilikua ni ya kupanga, chumba chetu hakikua na choo cha ndani.


“Hapana, utaoga usiku, humu ndani kuna wambea wengi, watakujaza ujinga wakikuona hivyo. Utaoga usiku wakisha lala, sasa hivi niambie nikuletee chakula gani?” Aliongea kwa sauti ya chini lakini ya msisitizo, alitaniatania na kulazimisha kujichekesha lakini nilijua kuwa hacheki, nilimuambia chips, sio kama nilikua na hamu ya kula lakini nilitaka aondoke tu ili nipumzike.


Lirudi na kunikumbatia kama vile mwanaume anamuaga mke wake mpendwa, alifunga mlango kwa nnje na kuondoka na funguo. Alikaa kama nusu saa hivi akarudi na mfuko wa chips kuku na soda, alinipa na kuniambia nile, sikua na hamu ya kula lakini nilijua kama nitakata akula basi anaweza kukasirika na kunipiga tena. Nilikula huku yeye akijiongelesha mambo mengi mengi, nilikua nikimsikia lakini sikumsikiliza, akili yangu ilikua mbali sana, nilishachoka na nilikua nikiwaza namna ya kuondoka na kumuacha.


****


Nilikaa ndani kwa muda wa siku tano, hakuruhusu nitoke mpaka nilipopona kabisa,a lichukua simu yangu hivyo sikuweza kuwasiliana na mtu yeyote, hata ndugu zangu sikuweza kuwasiliana nao. Nilishangaa ni kwanini rafiki na ndugu zangu hawaji hata nyumbani kunitafuta, sikujua amewaambia nini mpaka siku nilipotoka, alinirudishia simu yangu na mtu wa kwanza kumpigia simu alikua ni mama yangu, nilikua nimechoka na nilitaka kumuambia kila kitu.


“Hongera mwanangu, sijui kama kabadilika lakini ule msamaha wa juzi naamini atakua kajifunza…” Mama alianza kuongea, nilishtuka kwani sikujua kuwa anaanisha nini, nilimuuliza alikua anamanisha nini ndipo alinielezea. David alikua ameenda nyumbani kwetu, aliongoza an na mjomba wake pamoja na wazee wengine wawili, walienda kuomba msmaaha familia yangu kwa kuishi na mtoto wao bila mahari wala chochote.


Baad aya hapo pia alimuomba Mama yangu msamaha kuhusiana na tabia zake za awali, aliesma hazikua akili zake  ulikua utoto na sasa hivi baada ya kuishi na mimi ameona kuwa mimi ndiyo mwanamke wa maisha yake, alimuambia kuwa tumeongea na kukubaliana kuwa aende mwenyewe kuomba msamaha na si mimi kumpeleka wkani itakua na uzito ziadi. David alikua anataka kunioa na alikua tayari kupangiwa mahari yoyote ile na wakati wowote ule, aliwaambia kuwa mimi ndiyo nimeamua na nilikua nataka aombe msamaha yeye kwanza ndiyo mimi niende eti kwakua naogopa watakataa.


Mama aliongea mambo mengi sana ambayo yalinishangaza, nilijikuta nalia na kumuambia kuwa hakuna kitu kama hicho, nilienda kuoanana naye na kumuambia kuwa siwezi kukubali kuolewa na David, nilimuonyesha makovu na kumuambia kila kitu alichokua amenifanyia.


“Mama yule mwanaume ni mshenzi, atakuja kuniua, naomba unisiadie simtaki tena.” Nilimuambia Mama aliishia kulia tu kwani alichokiona na alichokua kaambiwa vilikua vitu viwili tofauti.


Mama aliniambia nibaki nyumbani kwanza na kuniambia kabisa kuwa siwezi kuolewa na mwanaume kama huyo. Kumbuka Baba yangu alikua ni mgonjwa wa sikuari, na alikua na presha kuna mambo mengi amabyo tuilikua hatumuambii kutokana na hali yake, lakini David alipokuja na kusema kuwa naatak kunioa aliongea na Baba, kwakua Baba alikua haelewi chochote kuhusu mimi na alikua akijua kuwa tuna mahusiano mazuri basi alikubali kuwa niolewe.


Wazazi wangu mwanzoni walikua wakiishi Dar, walikua na kanyumba kadogo, lakini baada ya Baba kustaafu na kuanza kuumwa walihamia Morogoro ambapo ndiyo nyumbani na ndipo tulipokulia, lakini nilipopata kazi niliwajengea nyumba kubwa katika kiwanja chao pembeni na ile nyumba ndogo na walirudi tena Dar, lengo lilikua ni baba kuwa karibu na matibabu, kipindi hicho nilikua na David hivyo hata wazazi wangu walikua wakijua kuwa David ndiyo ananisaidia kujenga.


Mama ndiyo baadaya alikuja kuujua ukweli baada ya David kumuambia mambo ya ajabu ajabu, kunitukana na kunidhalilisha akimshutumu Mama kuwa ndiyo kanilea vibaya. Baba alikua hajui chochote kwani pamoja na kuumwa lakini Baba yangu alikua mkali, alikua ni mwanajeshi hivyo alikua bado na yale mambo ya amri amri, hata David alikua anamuogopa kwani hakupenda ujinga ujinga.


Baba aliniona nimaerudi nyumbani, alifurahia kuniona na kunipongeza. Ni muda mrefu alikua akiulizia suala la mimi kufunga ndoa, kwa nilivyokua nikimfahamu mimi kuzalia nyumbani ingekua nikufukuzwa nyumbani, lakini kwakua alikua tayari kachoka, pesa yale yopte ya pensheni iliishia kwenye matibabu basi alinywea kwani alikua akinitegemea mimi kwa karibu kila kitu, hiyo ndiyo sababu pekee ambayo ilimfanya Baba yangu kunivumilia na kumkubali mwanangu aliyezaliwa nnje ya ndoa.


Pongezi zake ziliniumiza kwani nilijua kuwa nitamvunja moyo kama nikimuambia kuwa sitaki kulewa na David. Niliwaza sana namna ya kumuambia lakini nilishindwa, nilimuomba Mama kuongea naye lakini alionekana kuogopa.


“Baba yako anakupenda, ongea naye wewe atakuelewa mimi nikimuambia chochote atasema mimi ndiyo nakuharibu.” Mama aliongea kwa uoga flani hivi, kuna kitu nilikihisi nkwenye sauti ya Mama, alikua na hofu flani ambayo haielezeki, tangu nakua Mama na Baba waliklua ni mfano wa kuigwa, ni mara nyingi nilikua nikimuuliza Mungu ni kwanini hanipi mwanaume kama Baba yangu.


Sikujua kama kuna kitu mpaka wakati huo, namna Mama livyokua akiongea ni kama alikua anamuogopa Baba. Nilimuuliza Mama kama kuna kitu lakini alibishaa, aliniambia tu kuwa Baba anampenda David na hatakubali kirahisi namna hiyo.


“Ila wewe anakupenda, hawezi kuacha ukateseke, subiri akishameza dawa zake ndiyo umuambie.” Mama aliniambia, pamoja na ukali wa Baba lakini nilikua simuogope, hakuwahi kunipiga katika maisha yake yote, alikua ananipenda mimi na ndugu zake na ukali wake alikua anauonyesha mara moja moja.


Ingawa watu wa nnje walikua wakimuogopa na waodgo zangu kuna kipindi walikua wakimuogopa lakini mimi sikuwahi kumuogopa, kwangu nilimuona kama Baba tu na nilikua huru kumuambia chochote. Kitu pekee nilichokua nikiogopa na sababu ya kutokumuambia matatizo yangu ilikua ni ugonjwa wake, nilijua ananipenda sana na nilijua kuwa kumuambia matatizo yangu ilikua ni kama kumuongezea ugonjwa, lakini kwa hali ilivyokua imefikia ilikua haina namna zaidi ya kumuambia ukweli.


Usiku nilitafuta muda ambao Baba katulia, nilimuomba kuongea naye na alikubali, nilimuambia kuwa pamoja na David kuja kutaka kunioa lakini siwezi kuolewa naye, nilimuambia kuwa hajawa muaminifu kmwake, hanihudumii na mimi ndiyo namlisha na kumpa kila kitu, nilimuambia kuwa nimekua nikimfumania na wanawake mara kwa mara na pia amekua akinipiga na hata wakati anakuja kujitambulisha na kusema anataka kunioa alikua ametoka kunipiga na kunifungia ndani.


Sikumueleza kila kitu lakini nilimuambia mambo mengi ambayo niliamini kuwa yanaweza kumshawishi kukataa mimi kuolewa. Alinisikiliza kwa makini na kwelia lionekana kunialewa.


“Wewe ndiyo unayeolewa mwanangu, ndiyo unaenda kuishi na huyo mwanaume. Mimi siwezi kuingilia chochote, wewe ndiyo ulimleta hapa na kama ni kumkataa wewe ndiyo wa kumkataa.” Baba aliniambia kwa kifupi, hakuongea kitu chochote alinyanyuka na kuingia chumbani kwake. Wakati naongea naye Mama alikua chumbani, sisi tulikua tunaongelea sebuleni.


Binti wa kazi ambaye alikua akiwasaidaia Mama kwani wadogo zangu wengine walikua chuoni alikua kashaingia chumbani kwake na mwanangua likua kaenda kwa Kaka yangu. Mazungumzo hayakua marefu sana na tofauti na nilivyotegemea Baba alikua mulewa. Nilifurahi a na kuingia chumbani kwangu huku nikifikiria namna ya kuvichukua vitu vyangu na kuvileta nyumbani kwetu, ingawa chumba nilichokua nikiishi kilikua chakwangu lakini nilijua kuwa kwakuendelea kuishi pale David angeweza kuja na kuniletea vurugu.


Nikiwa chumbani kabla ya kupanda kitandai kulala nilisikia kelele, ilikua ni sauti ya Baba, alikua akitukana kwa nguvu.


“Mshenzi mkubwa wewe! umemuacha mtoto amekua Malaya, kazalia nyumbani sasa hivi mwanaume anakaribia kumuoa unamjaza ujinga ujinga wako! Kupigwa kitu gani, mwanamke kama hana adabu si anapigwa! Malaya mkubwa wewe nilisema sikupigi tena lakini sasa hivi nitakuua! Umuambia huyo mbwa wako labda kama mimi si Baba yake ataolewa, hawezi kunitia aibu kiasi hiki. Juzi watu wamekuja, wote tumeona nimeita ndugu zangu na kuwaambia leo eti niwaambie kuwa binti kakataa kuolewa!


Wataniona mwanaume wa aina gani! Yote haya ni wewe umemjaza ujinga!” Baba aliendelea kutukana, nilitoka harakaharaka mpaka nnje ya mlago wa chumba chao, Baba alikua aklimpiga Mama, nilisikia vibao, mateke na mekele mengine, Baba alikua akimpiga huku akimtukana, nilifungua mlango na kumkuta Mama kalala chini, Baba anampiga mateke na kashiklilia mkanda anamchapa kila sehemu ya mwili wake.


Alikua akimpiga sana huku akipiga kelele, kitu cha ajabu nikuwa Mama alikua halii, alikua kanyamaza kimya hapigi hata kelele, zaidi ya maneno nisamehe mume wangu! Nisamehe mume wangu hakuongea kitu kingine chochote kile! Kwa namna alivyokua ananipiga nilimuona David alivyokua akinpiga, hasira zilinipanda na niliumia namna Mama yangu alivyokua akipigwa. Bila kujijua nilimvamia Baba na kumsukuma pembeni kisha kumuinamia Mama ambaye alikua hoi pale chini.


ITAENDELEA


DAVID; HATA UKIONA KIVULI CHANGU USIJARIBU KUKIGUSA!—SEHEMU YA KUMI


Katika maisha yangu sikuwahi kufikiria kuwa Baba anampiga Mama, pamoja na ukali wake lakini alitupenda wanaae na alionyesha kuwa ni Baba bora, watu walimuona kama mtu mkali lakini sisi tulimuona kama Baba mwema na mwenye upendo. Mama pia alificha mengi, hakuna hata siku moja ambayo aliwahi kunielezea hata baya moja la Baba. Pamoja na kumuelezea matatizo mengi ya David lakini hakuwahi hata siku moja kuniambia kuwa hata Baba yako naye alikua ananinyanyasa.


Kitendo cha mimi kuingia chumbani na kumuona Baba akimpiga Mama ni kama kilimfedhehesha, ghafla niliona Baba kawa mpole, kanyamaza kanyanyuka na kukaa kitandani. Alikua kanyongonyea anatia huruma kabisa, nilimshika Mama na kutoka naye mpaka sebuleni, nilimuuliza kama ilikua ni kawaida ya Baba kumpiga, Mama alikataa na kusema kuwa imetokea tu mara moja. Lakini kwa mtu ambaye nilipitia manyanyaso na nilikua naficha nilijua kuwa Mama anamfichia Baba maovu yake.


“Sasa kwanini unamvumilia, mtu mwenyewe mgonjwa lakini bado anakupiga?” Nilimuuliza kwa hasira.


“Nyamaza huyo ni Baba yako, hutakiwai kuingilia kwa chochote kile!” Aliongea kwa hasira, nilijaribu kumshaauri kuondoka lakini hakunisikiliza. Wakati tumekaa pale Baba alitoka, alikua mpole na alionekana kama alikua nalia. Alikuja mbele yangu na kunishika mkono.


“Mwanangu ondoka kwa huyo mwanaume, ondoka, muache kabisa kwani atakuja kukuua.” Aliongea kwa huzuni, nilimuangalia Baba bila kummaliza, alionekana kuumia sana.


“Ondoka mwanangu, mimi nimemtesa sana Mama yako bila sababu, sijui kwanini na nitakufa na hiki kitu, sitaki uje kuwa kama Mama yako.” Aliniambia tena, hakukaa kwa muda mrefu Baba alirudi chumbani, alikua analia kweli, nadhani kitendo cha mimi kumuona akimpiga Mama kilimuumiza sana, kila siku alitaka kuonekana yeye mwema. Nilimuangalia Mama akaniambia msikilize Baba yako, kisha akarudi chumbani kwake, usiku ule sikulala lakini akili yangu ilikua inawaza kuondoka, niliamua kumaucha David na nilipanga kumuambia kesho yake.


Siku iliyofuata nilimpigia simu David nilimuambia kuwa nimeamua kumaucha, siwezi kuendelea kuwa na yeye, nilimuambia kabisa kuwa nimeamua kuwa na maisha yangu. Alikasirika sana na kunitukana, alinitukana sana huku akiniambia kuwa najidanganya siwezi kumaucha, nilimuambia kuwa nimeamua na nishawaambia wazazi wangu. Hakuamini, kila wakati aliniambia kuwa siwezi kuishi bila yeye, yeye ndiyo mwanaume wa pekee ambaye naweza kumpata na kamwe siwezi kupata mwanaume mwingine.


Nilimuambia sihitaji tena mwanaume ili kuwa na furaha na hata kama nikihitaji basi hatakua ni yeye. Alinitukana sana na kuniambia kuwa hanitaki, aliwapigia simu ndugu zangu Mama yangu na kuwatukana, akawaambia kuwa ni wachawi, wamemharibia maisha yake na hanitaki mimi pamoja na mwanangu. Alitukana sana lakini sikujali, nilishafanya maamuzi, alimpigia simu mama yake amabye naye alinipigia, aliniuliza kilichokua kimetokea nikamuambia, alinisihi sana nisimuache mwanae lakini nilikataa katakata.


Sikuendea kuchukua vitu vyangu kwani nilihisi kama atanifanyia vurugu, lakini yeye mwenyewe alikuja nyumbani kwetu, akanirudishia funguo zangu na kuniambia nisimtafute tena. Sikumtafuta kweli, nilienda kuchukua vitu vyangu na kuvileta nyumbani, niliamua kuishia nyumbani kwanza nikisubiri mambo yapoe. Lakini David hakukaa sana Tanzania, mwezi mmoja baadaye alirudi Kenya, aliniambia ili kuniringishia lakini sikujali, nilishaamua kumuacha na kumtoa kabisa moyoni.


Baada ya kuona kuwa David kaondoka nilianza kutafuta kazi, sikutaka kuondoka nyumbani bila kazi. Kwa bahati nzuri nilipata katika kakampuni kamoja kadogo tu, mshahara haukua mkubwa sana lakini uliniwezesha kuishi mimi na mwanangu, niliweza kupanga chumba changu na kuamua kumchukua mwanangu kuishi naye kwani alishaishi mbali na mimi kwa muda mrefu na nilihisi kama vile hanijui. Sikua na mawasiliano na David ingawa mara kwa mara alikua akinitafuta na kunitukana huku akiniambia kuwa hata nifanye nini yeye ndiyo mume wangu.


Sikua nikimjibu, mwaka jana mwanzoni alikuja nyumbani Tanzania, alikuja na kuniambia kuwa anataka kumhamisha mtoto kutoka kwenye shule ya kawaida aliyokua akisoma na kumpeleka kwenye shule ya binafsi International. Baada ya kaucha kuhudumia kwa mud amrefu ghalfa alitaka kuhusumia. Sikua na namna ingawa sikutaka lakini mwenyewe alienda na kulipia ada ya mtoto hivyo nikawa sina namna zaidi ya kumhamishia ile shule mtoto. Aliondoka na kurudi Kenya.


Lakini hakukaa sana, alikaa kama mwezi mmoja hivi, kwao kulikua na msiba, alienda kusalimia na alikuja nyumbani kumuangalia mtoto. Alipokuja sikua na namna zaidi ya kumkaribisha, alikuja na kumsalimia mtoto lakini kabla ya kuondoka wakati mtoto kalala ndani alinishika kwa nguvu aliniingiza chumbani na kunibaka. Nilishiddwa kupiga kelel kwa hofu kua mwanangu ambaye ashakua mkubwa angesikia na angejua kuwa mimi na Baba yake hatuko vizuri.


Baada ya lile tukio aliondoka kwa dharau huku akiniambia kuwa mimi ananimiliki na anaweza kunifanya chochote kile anachokitaka wakati wowote ule niliumia sana lakini sikua na namna zaidi ya kuvumilia na kuacha maisha yaende. Alirudi Kenya lakini baada ya miezi miwili tena aliudi na kunifanyia kitu kilekile, anakuja nyumbani wakati mwingine hata usiku na ananilazimisha kufanya mapenzi, nilianza kujiona kama mtumwa kwake, nilishindwa kutafuta msaada na kuna wakati nilianza kuhisi kama ni haki yake kunibaka.


Amenifanyia hivyo ziadi ya mara nne na zote nimekua nikivumilia, nilikua najihisi mnyonge naona aibu kumuambia mtu yeyote. Nimekua nikilia tu kwani baaad  ya kulipa ada hahudumii mtoto kwa kitu kingine chochote, shule aliyompeleka inahitaji vitu vingi, kuna usafiri kuna vyakula na vitu vingine vingi lakini nikimuomba pesa ya matumizi ananiambia kuwa hawezi kunipa nikajiuze nipate. Nilikua nimechanganyikiwa ndipo nilikutana na Kaka Iddi na kumuelezea kisa changu ndipo akanishauri.


USHAURI NILIOMA HUYU DADA;


Kwanza pole kabisa kwa yaliyokukuta, wakati nakusikiliza mara kadhaa nilikua napandwa na hasira, nilikuona mjinga na huna akili, nilikuona kama hujitambui na nilitamani kukutukana, lakini baada ya kumaliza kuongea na wewe nilijua kuwa wewe ni mhanga wa manyanyaso ya muda mrefu. Najua watu wengi watauliza ni kwanini umevumilia yote haya, wanachoshindwa kuelewa nikuwa wanawake wengi wanaovumilia manyanyaso ya namna hii hawajui ni kwanini wanavumilia.


Hawaju kwakua manyanyaso huanza kidogo kidogo, yanaanza kimasihara kama mwanaume kukuambia hujapendeza, kukuambia kuwa wewe ni mbaya, kuchepuka na rafiki zako, kukutukana na kuanz akukupiga makofi kidogo kidogo. Hapa kila mtu utakayeenda kumuomba ushauri atakuambia vumilia ndoa ndiyo zilivyo lakini baada unakuta kuwa umepoteza muda mwingi na mwanaume na kibaya zaidi unakua umejipoteza wewe mwenyewe kwani huioni thamani yako tena na unaanza kuamini kuwa huwezi kuishi bila huyo mwanaume.


Manyanyaso yanalivia, yanakufanya kuwa teja na unapokua teja ni ngumu sana kutoka katika uteja bila kupata msaada wa mtu wa jirani. Ubaya zaidi wa uteja ni kuzungukwa na mateja na wakawa ndiyo washauri wako wakubwa. Teja anayekula unga anapotaka kuacha kama ataenda kuomba ushauri kwa teja mwenzake basi ataishia kuambiwa kuwa anachojisikia ni kawaida na kupewa unga mwingine hivyo hataacha. Ili kuacha ni lazima kupata usaidizi kwa mtu ambaye si teja, mtu ambaye atamuambia kuwa hicho unchokifanya ni kibaya.


Wanawake wengi wanakua mateja wa mahusiano kwakua wamezungukwa na mateja wenzao, unaenda kumuomba ushauri Mama yako ambaye ana miaka 30kwenye ndoa na mpaka leo anapigwa, unamuomba shoga yako ambaye ndiyo katoka kumfumania bwana wake na katukanwa na kupigwa na bado anang’ang’ania. Hawa nui mateja wa manyanyaso na kamwe hawawezi kukuambia toka utakufa kwakua wao wenyewe wameshindwa kutoka na wanahitaji mtu wa kujadiliana naye mateso yao.


Sasa kuhusu mwanaume wako David, jua kuwa anakuogopa, wewe ni mwanamke mwenye nyota ya mafanikio na hicho ndiyo kinamfanya David kukunyanyasa. Pamoja na kusoma kwake lakini umemsaidia kupata kazi, kwanza ulikua unamlisha, pili ukampeleka nnje ya nchi, hii ikimaanisha kuwa mafanikio yoyote atakayoyapata huko basi ni wewe umempa kwani kwa akili zake asingeweza kufanikiwa, kwamba anajua kuwa yeye kwako ni kama takataka flani, hajiwezi kwakua hakuwezi.


Lakini anaumia kuwa una akili, kwamba wote mnafanya kazi ileile, ipato kilekile lakini wewe umeweza kuwajengea wazazi wako, unahudumia mtoto wako na gari umenunua wakati yeye hata kununua Boxer ni shida. Mwanaume wa namna hiyo anaumia sana ndnai yake, na ukweli nikuwa mwanaume wa namna hiyo hawezi kuwa na furaha akiwa karibu na wewe kwani mbele yako anajiona kama mwaamke tu analelewa, anajiona hana akili, anajiona falafala na anaona kama unajua kuwa yeye  ni  fala na anahisi unamdharau.


Iko hivi wanaume kiasilia tunaamini kuwa tuna akili kuliko wanawake, hivyo mwanaume ambaye hajiamini akikutana na mwanaume mwenye akili ilia ishi naye vizuri ni lazima kumnyanyasa, kumtukana na kumfanya yule mwanamke aishi au ajihisi kama takataka ili wawe sawa. Labda kam ahuelewi nikufafanulie kidogo, mwanaume asiyejiamini ni kama jalala, sasa jalala haliwezi kubeba chakula kisafi, ukiweka chakula kisafi jalalani basi jalala litatuma inzi ili kukichahfua ili wapiti njia wakipita wajue nacho kichafu.


David alikua anajua kuwa wewe ni jembe, hakuwezi hivyo ili kujisikia vizuri alilazimika kutuma inzi wakuchefue ili watu wengine wakuone kuwa unastahili kuwa na David jalala kwani hauna tofauti naye. Mambo yote aliyokua akikuambia ili ujisikie vibaya, ujione takataka jua kuwa ndiyo mambo ambayo yeye anaamini anayo, anataka mfanane. Ndiyo maana hataki kukuacha kwakua anajua kuwa kuna wengine wenye akili watakufuata, anataka kuendelea kukunyanyasa na kukuonyesha kuwa ana akili kuliko wewe na anawez akukufanya chochote.


Ushauri wangu kwanza acha kumtafuta, kumnyenyekea wala kuhangaika naye, kuhusu mwanao muambie kuhusu kuendelea na huduma nyingine, akikataa kutoa basi mrudishe mwanao wkenye shule ambayo una uwezo nayo, acha kujiua na maada ambayo huwezi kuyalipa. Mhudumie kwa namna unavyoweza na kama anataka hizo shule basia lipe kila kitu,a cha kujiua. Kuhusu David na hiyo kuja kukubaka, kwanza kabisa mtafute na muambie kuwa unajua ni kwanini anakufanyia hayo.


Muambie kabisa kuwa wewe ndiyo umemfanya yeye kuwa hivyo na anajaribu kukufanya ujihisi takataka ila kamwe hutakuja kuwa takataka kwani hta akifanikiwa vipi wewe ndiyo umempa mafanikio, alikua hana hata Pasport lakini ulimpa wewe na kumfungua macho wewe. Muambie kuwa siku ile aliyokubaka ndiyo ilikua mara yake ya mwisho kuugusa mwili wako. Muambie kuwa hatakanyaga tena kwako na kama ni mtoto mtapanga sehemu ya yeye kwenda kumchukua na kuonana na mwanae ila wewe hatakugusa tena hata kivuli chako atakionea kwa mbali.


Baad aya kumuambia basi achana naye, sasa hivi yuko Kenya lakini akirudi na kutaka kuja kwako basi iwe kakugusa au hajakugusa nenda Polisi, chukua RB na kama akija kufanya fujo basi mpeleke Polisi na fungua kesi ya jinai na si kwenda dawa ti la jinsia. Acha kumuogopa yeye si Mungu na hawezi kukufanya chochote kama ukiamua. Kama Polisi nhgazi flani hawatakusiadia panda ngazi ya juu, nenda sehemu nyingine watakusaidia lakini usikae kimya na wala usikubali tena unyanyasaji wake.


Maisha yako ni yako, wewe ndiyo mwenye uamuzi wa kesho yako, najua kuwa wakati mwingi mtu akinyanyaswa sana huogopa kuingia kwenye mahusiano na hata akiingia mara nyingi huangukia kwenye manyanyaso mengine. Amua kuwa hutakubali manyanyaso na ukiona dalili za manyanyaso kwenye mahusiano mapya jitoe mapema. Achana na ile kauli ya “Utaaacha wa ngapi!” hata ukiacha mia au ukibaki peke yako lakini kamwe usiruhusu David mwingine katika maisha yako, wewe ni watahamani na usiruhusu mtu yeyote kukuambia tofauti.


Je, unataka kujua mrejesho wa huyu Dada baada ya kuongea naye? Tukutane kesho kwani tayari kashanijibu!


ITAENDELEA


DAVID; HATA UKIONA KIVULI CHANGU USIJARIBU KUKIGUSA!—SEHEMU YA KUMI NA MOJA


Kaka…nakushukuru zaidi ya sana..comments ziliniumiza mwanzo lakini kadri navoendelea nazidi kuamini anaweza kuwa aliniroga or something..kuna comment moja tu ya mdada aliandika anahis nina nyota sana ya kufanya kila kitu kikafanikiwa na sichagui kazi ila shetani ameingilia kati hilo….hii imenipa nguvu sana na kunifanya nione mwanga wa kuanza upya..kifupi ni mwezi sasa tangu tulivyoongea nikamtumia hii msg kama ulivyoniambia nifanye.


Aliniblock nami nikafanya the same.kutokana na maneno yako nimeanza maisha mapya sitakaa nirudi kwenye ile kazi coz huwa inanikumbusha mateso yake.nimeamua kuanza biashara na kusahau yale maisha in total.nakuahidi ntaleta mrejesho hapa.Mungu aendelee kukutumia kaka…mateso yote niliyopitia hata mama mzazi hakuweza kuninasua.lakini kwa kuongea na wewe dakika chache nilifunguka..you are a blessing


****MWISHO


0 comments:

Post a Comment

BLOG