Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

AKIKUUA TUTAKUJA KUCHUKUA MAITI YAKO

  

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

SIMULIZI; AKIKUUA TUTAKUJA KUCHUKUA MAITI YAKO!—SEHEMU YA KWANZA


Natamani kumtaja jina lake lakini ni mtu ambaye anafahamika sana hivyo kaka naomba tu watu wasome kisa changu. Nimeamua kuandika kisa changu baada ya kusoma kisa cha David, watu wengi walikua wakimshangaa sana yule dada kwanini alikua anavumilia mateso yote yale. Niliposoma niliwashangaa sana watu kwani mateso aliyokua akipitia yule dada ilikua ni kama nusu ya mateso ambayo mimi mpaka sasa napitia. Niliposoma Comment za watu ndipo nilikumbuka maneno ya Kaka yangu ambaye aliniambia “Si unajifanya unampenda mume wako basi endelea kukaa naye akikuua tutakuja kuchukua maiti yako!”


JOIN US ON TELEGRAM

Nilikutana na mume wangu miaka 10 iliyopita, wakati huo ndiyo nilikua nimemaliza chuo na tayari nilikua na ajira, yeye ni mfanyakazi wa shirika flani hivi na ana cheo kikubwa tu. Tulipendana na alikua ni mtu mzuri sana kwangu, mahusiano yetu yalidumu kwa miaka miwili ndipo alikuja kujitambulisha na kuleta posa. Hapo ndipo kila kitu kilibadilika, nakumbuka zilikua zimebaki wiki mbili tu kabla ya  harusi, alinipigia simu kuwa anataka kuniona, tulipanga kukutana sehemu ya wazi tu kwani nisingeweza kwenda kwake kutokana na wageni wengi ambao walikuja kwaajili ya harusi.


Ilikua ni siku ya jumamosi hivyo nilikua tu nyumbani na wageni wageni. Tulipanga kuonana saa nane za mchana, lakini kabla ya kuondoka nyumbani ambapo hakukua mbali sana na sehemu tuliyokua tumepanga kuonana, Bibi yangu mdogo alikuja nyumbani, alikua ametokea kijijini akiongozana na mjomba wangu. yeye ndiyo nilikua nimechukua jina lake, na kwakua alikuja kwaajili ya harusi yangu basi ile salimia salimia ilinifanya kuchelewa kama dakika kumi na tano hivi. Niliaga na kwenda kumuona mchumba wangu, nilikuta ameshafika kaagiza na kinywaji.


Lakini hali yake ilikua ni tofauti sana, alionekana kuwa na hasira sana, nilihisi labda huko alikotoka ndiyo walikua wamemuudhi, nilifika na kuvuta kiti, nikamsalimia lakini hakuitikia, alianza kuangalia saa yake huku akiniangalia kama mtu aliyetaka kusema “Ndiyo saa nane hii?” niliwaza atasema na kweli alisema.


“Ndiyo saa nane hii? Hivi wewe ndiyo mtu wa kuniweka dakika kumi na tano nzima?” Aliniuliza kwa hasira.


“Samahani, Bibi alikuja nika….” Nilijaribu kujitetea lakini kabla sijamalizia alivuta chupa iliyokua mezani na kuipiga chini, ilipasuka na vipande kunirukia.


“Pumbavu, kwahiyo bibi yako ana umuhimu zaidi kuliko mimi? Hivi ulijua kuwa nimekuitia nini? Kama ningekua na tatizo kubwa, mimi ni mchumba wako, keshokutwa nataka kukuoa, je kama ningekua nimeahirisha ungekaa na huyo Bibi yako? Kama unamuona Bibi yako ni wamaana sana kwanini usingeenda akakuoa yeye!” Alifoka sana mpaka watu wakaanza kusogea na kuulizia nini kilikua kimetokea, niliishia kuwaambia hakuna shida kwani hata mimi nilikua sijui ni kitu gani kilikua kinaendelea kwenye akili ya mchumba wangu.


Alikua ni mtu tofauti kabisa, katika kipindi chote cha mahusiano nilimuona kama mtu mstaarabu, anayejali na mara zote alikua ni mtu wa kunisikiliza. Mara nyingi kila tulipokua tunakosana hata kama kosa lilikua ni langu basi yeye aliishia kuniomba msmaaha.


“Kuna nini kwani mbona mambo haya ni ya kuongea na kuyamaliza?” Nilimuuliza huku nikijaribu kumsogelea na kumshika bega. Hapo ndiyo nilikua nimefanya kosa la karine, nilimtibua haswa kwani aiukamata mkono wangu na kuuviringisha kama vile aanauvunja, maumivu niliyoyapata niliikuta najikojolea mbele za watu.


Nikiwa nimeinama chini kichwa nimekijunja bado kashikilia mkono wangu anaubinya, alichukua chupa nyingine ya bia na kunipiga nayo kichwani, alikua akinipiga huku akinitukana na kuniita Malaya, sina akili najifanya mzuri lakini anaweza kuniacha wakati wowote. Kwa bahati nzuri watu waliingilia, kaka mmoja ambaye baadaye nilikuja kujua kuwa alikua ni mwanajeshi alimshika na kuanza kumtandika makofi, alimpiga sana akimuambia kama ana nguvu apigane na wanaume wenzake si kupiga wanawake. Baada ya hapo alimchukua na kumpeleka polisi kisha akaondoka na kumuacha hapo.


Mimi sikujua kama kapelekwa polisi kwani baada ya kuachiwa niliondoka huku nikilia, nilifika nyumbani mkono unauma huku kichwani nimepasuka damu zinanitoka, watu waliokuepo pale walinishangaa na waliponiuliza niliwadanganya kuwa nimepata ajali ya Bodaboda. Walitaka kunipeleka hospitali lakini nilikataa, nilimuomba Mama aje ili niongee naye. Nilimuambia kila kitu kilichotokea mpaka mchumba wangu kupigwa na yule Kaka ambaye baadaye tulikuja kujua kuwa ni mwanajeshi.


“Kwahiyo mchumba wako sasa yuko wapi?” Mama aliniuliza.


“Mimi sijui aliponiachia nilimuacha akigombana na yule Kak…” Nilimuambia lakini kabla ya kumalizia Mama alinikatisha.


“Unaakili kweli wewe? Yaani mwanaume anakuoa wiki mbili zijazo lakini unamuacha anapigwa bila kujua hata hali yake, hukusimama hata kumtetea! Hivi wakimuua ndiyo utakua umepata faida gani, tutakua wageni wa nani? kwa hiyo hata hujui kuwa yuko wapi?” Alinishutumu na kuniuliza tena, nilikua katika maumivu makali lakini Mama hakujali, mkono ulikua unauma na nilikua nahisi kama vile umevunjika.


“Mtu umechelewa mwenyewe ulitaka kaka wa watu afanye nini? Kwani huyo bibi yako usingemsalimia angekufa? Ndoa hujaianza uhsaanza kumletea Kaka wa watu visa!” Mama alifoka hukua kiongea maneno ya kunichoma, hakujali kuhusu maumivu yangu alichokua akiwaza ni kuhusu mchumba wangu na kunishutumu kwa kila kitu. nilikasirika na kutaka kutoka kumuacha akilalamika lakini alinishika.


“Hivi una akili kweli, unataka kutoka na hiyop hali yako utasema nini? Unataka Baba yako akuone hivyo, hivi unafikiri watu wakijua tabia zako italeta picha gani? Kalisha matako hapo mshenzi mkubwa wewe…”


Alinishika na kunisukuma chini, alitoka na kufunga mlango kwa nnje, nilikua katika maumivu makubwa lakini maneno ya Mama taratibu yaliniingia, nilianza kujihisi kama mimi ndiyo mkosaji, nilianza kujihisi kama vile kuchelewa kwangu ndiyo kulimlazimisha mchumba wangu kunipiga.


“Inawezekana kweli, haat sio mtu wa vurugu, lakini na mimi nimezidi, singenipiga vile ila nisingechelewa na kumuongelesha vile asigenipiga, inawezekana ni kosa langu….” Niliwaza huku nikitembeatembea chumbani, nilichukua simu yangu kumpigia lakini ilikua imezimwa, nilijua labda kanizimia hivyo nilizidi kujisikia vibaya.


Usiku ule ulikua ni mrefu sana kwangu, kila wakati nilikua nikiangalia saa yangu ili kukuche. Mchana mzima sikupata taarifa za mchumba wangu na hata usiku, baadhi ya ndugu zake niliowapigia simu walikua hawajui alipo, nilipata wasiwasi sana. Mama alizidi kunichanganya, kila baada ya dakika kadhaa alikuja chumbani kwangu kuniulizia kama nimewasiliana na mwenzangu, nilimuambia kuwa simu yake ilikua haipatikani, alondoka kwa hasira.


Kichwa sehemu niliyokua nimepigwa chupa bado ilikua inauma, mkono ulikua umevimba lakini sikuyajali maumivu, nilikua na mawazo sana kuwaza alipokua mpenzi wangu. mpaka asubuhi nilikua sijasikia chochote, kwenye saa nne hivi simu yangu iliita, ilikua ni namba ngeni, nilipokea na ilikua ni sauti ya kiume.


“Wewe ndiyo Hilda (sio jina lake halisi)?”


“Ndiyo, ndiyo mimi Kaka…” Nilijibu harakaharaka, sikujua imetoka wapi lakini nilihisi kabisa ilitoka kwa mchumba wangu.


“Kuna mtu wako yuko hapa, anasema wewe ni mchumba wake, anahitaji mtu wa kumuwekea dhamana…”


Iliongea ile sauti, alikua ni askari na mchumba wangu alikua kapelekwa Polisi, nilijiandaa harakaharaka kwenda kumuona, nilitoka bila kuaga mtu yeyote kwani sikutaka maswali mengi, bado mkono ulikua unauma lakini kusikia habari za mchumba wangu zilinipa nafuu kidogo. Nilienda kituoni kwaajili ya kumuwekea dhamana, baada ya kukamilisha kila kitu alitoka na kuambiwa arudi kesho yake, hakukua na faili lolote lililofunguliwa lakini ilionekana kama mtu aliyempeleka pale ni mkubwa na alitaka tu kumkomoa.


Tuliingia kwenye gari mimi nikiendesha, njia nzima hatukuongea, nilitamani kumuuliza kilichotokea lakini alionekana kuwa na hasira sana, alionekana kuwa na mawazo mengi, nilitaka kumpeleka kwake lakini alikataa, aliniambia nimpeleke sehemu nyingine kabisa, tulienda mpaka kwenye nyumba moja, akafika na kugonga kwenye chumba kimoja, alitoka mwanamke, mbele yangu alimkumbatia yule mwanamke na kuanzana kupigana denda huku nikiangalia. Alinigeukia na kunipungia mkono kunionyesha ishara kuwa naweza kwenda yeye ameshafika.


Lakini sikwenda, nilitamani kukanyaga mafuta lakini mguu haukusogea, nilikua nikitetemeaka kwa hasira na uoga, kuona vile alikuja kwenye gari na kufungua mlango.


“Unasubiri nini? Ondoka au unataka kushuhudia kila kitu?” Aliniuliza kwa sauti kama ya kunishtua hivi. Macho yangu hayakua kwake bali kwa yule mwanamke, nilimuangalia nikijaribu kuvuta picha kama nilimuona wapi, sura yake haikua ngeni sana kwangu lakini nilikua sikumbuki nilimuona wapi?


SIMULIZI; AKIKUUA TUTAKUJA KUCHUKUA MAITI YAKO!—SEHEMU YA PILI


Nilishindwa kuwasha gari nakubaki namuangalia yule dada nikiwaza nilikua nimemuona wapi? Mara akili ilinijia, kuna siku moja nilienda ofisini kwa mchumba wangu nikakutana naye, hakua mfanyakazi mwenzake bali naye alikuja pale kumuona na ilionekana kama walikua wanagombana flani hivi, nilijaribu kumuuliza mchumba wangu kuwa ni nani lakini aliniambia ni mambo ya kikazi walitofautiana hivyo sikutaka kudodosa zaidi. Hasira zilinipanda zaidi kwani nilikua na muamini sana mchumba wangu na hata siku moja sikuwahi kufikiria kama anaweza kuchepuka.


“Nimekukosea nini lakini mpapa unaamua kunifanyia yote haya?” Nilikuta namuuliza, aliniangalia kwa dharau kisha akanijibu.


“Inaama huoni ulichonifanyia? Jana mimi nakuita lakini ukawaona ndugu zako kama ndiyo wa maana zaidi, umechelewa nakupiga kidogo unanijibu hovyo? Wakati nadhalilishwa na yule mwanaume wako si ulikuepo, sasa kwanini hukunitetea. Wewe ni kama mke wangu, keshokutwa nakuoa sasa kwanini hukusimama ukasema kuwa huyu ni mume wangu ukaachwa mpaka nikakaa ndani?” Aliniuliza kwa hasira, nilishindwa kumuelewa kwani kama ni tukio la kuchelewa lilikua ni la jana yake lakini yeye alishaanza kuchepuka zamani.


“Na huyo mwanamke, inaana ndiyo umempata hiyo jana wakati umelala polisi?” Nilimuuliza, alinyamaza kidogo kisha akanijibu.


“Wewe kipindi kile nakuambia unizalie si ulijifanya kuwa hutaki kuzaa, sasa wenzako wenye vizazi wamenizalia…” Nilishindwa kuendelea kumsikiliza, hasira zilinipanda na kuwasha gari kuondoka. Akili ilishanichanganya na niliona kuwa ile ndoa siwezi kuiweza.


“Siwezi kuvumilia kupigwa na mwanaume, hapana! Anipige halafu aende kuzaa na mwanamke mwingine!?” Nilijiongelesha, njia nzima niliendesha gari huku nikiwa nalia, niliaka tu kufika nyumbani na kumuambia kila mtu kuwa harusi imeahirishwa.


Nilifika nyumbani na kupaki gari, lakini kabla sijashuka Mama alikuja, ni kama alikua ananisubiria, kama alikua anajua kuwa naenda. Aliingia kwenye gari harakaharaka na kuniambia niwashe tuondoke. Niliktaa na kutaka kumuelezea kwanza kilichokua kimetokea lakini hakunipa nafasi.


“ondoka! Ondoka! Unataka kuniaibisha, hivi watoto wa siku hizi mmekuaje? Baba wa watu anapiga simu hapa analia, kalala polisi lakini wewe hata huoni? Hata kuomba msamaha umeshindwa eti uansema kupigwa? Kupigwa kitu gani? Mshenzi wewe unataka kila mtu aninyooshee kidole, ndoa zanyewe za shida umepata mwanaume anakuheshimu eti unalalamika kupigwa…!”


Mama aliongea kwa hasira, alinilazimishia kuondoa gari, alitaka niondoke pale. Njiani ndipo aliniambia kuwa mchumba wangu alikua amempigia simu anamuambia kuwa mimi nina hasira, tulitofautiana kitu kidogo lakini mimi nimechukulia hasira hiovyo nataka kuvunja uchumba. Alivyomshenzi alikua akiongea kwa kulia na kumuomba Mama kumuombea msamaha kwani inawezekana alikosea. Alibadilisha kisa kabisa, alimuambia Mama kuwa jana yake kuna sehemu tulikua tumekaa.


Kuna  mwanaume mmoja akaja kunisalimia mimi kama vile tunajuana na yeye alihisi labda ni wapenzi, alipouliza basi yule mwanaume akapaniki na kuanza kumpiga, yeye akapigana na katika purukushani basi mimi nilipigwa chupa ya kichwa pamoja na kuniumiza mkono bahati mbaya kwani eti mimi nilikua namtetea huyo mwanaume. Baadaye polisi walikuja na kumchukua yeye kwakua huyo mwanaume ni askari mwenzao na mimi nikaondoka na huyo mwanaume. Mama alikua akiongea kwa hasira mpaka machozi yanamtoka.


Alishamuamini mchumba wangu, alishaamini kuwa aliyokua akiongea ni kweli kwakua kila mtu alikua akimuona mpole. Mchumba wangu alikua ni wale watu wakimya, haongei sana, mtu akiwa na tatizo humsaidia na huwezi kumkuta hata akibishana na mtu.


“Unakuja unalalamika umepigwa bila sbabau kumbe umefumaniwa? Kama una mwanaume wako na unafanya upuuzi wako kwanini uufanye mbele ya mchumba wako? Umeshindwa kumuambia huyo mwanaume kuwa wewe mchumba wa mtu akaheshimua hata uolewe! Haya Baba wa watu kafungwa umeenda huko umeleta vurugu unataka kuvunja uchumba unataka hao watu mimi niwaambie nini?”


Nilishindwa hata kitu cha kuongea, Mama alishaamini kila kitu, hata nilipomuambia kuhusiana na huyo mwanamke mwingine ambaye ana mtoto hakuamini, aliniambia ni maneno ambayo natunga kwakua nimemuona mwanaume wangu huko baaa hivyo nataka kumuacha mchumba wangu.


“Hata kama angekua na mwanamke mwingine nani wa kumzuia, huyo ni mwanaume, lazima awe na wanawake wengi, hivi unaona mimi na Baba yako tupo mpaka sas aunafikiri niko peke yangu. Nimevumilia mengi, ndiyo ndoa zilivyo, sasa unataka kumuacha mtu kwaajili ya mtoto, mbona una roho mbaya namna hiyo?”


Kabla hata sijamjibu Mama simu yangu iliita, alikua ni mchumba wangu, nikijua kuwa labda ataropoka kitu na kunitukana ili mama kumsikia, makusudi niliweka karibu na sikio la mama ilia sikilize.


“Mimi bado nakupenda, pamoja na yote uliyonifanyia lakini siwezi kuahirisha harusi kwasababu yoyote ile, naomba unisikilize, mimi ni mume wako hivyo nimekusamehe na nakupenda….” Hakuongelea kitu chochote kibaya alichokua kakifanya, aliongea maneno mengi ya kuonyesha kuwa mimi ndiyo mwenye tatizo simtaki hivyo anataka nafasi nyingine kwani hawezi kuniacha.


Nilijuta hata kumsikilizisha Mama yangu kwani ndiyo kwanza nilikua nimeupalia mkaa, alinitukana sana na kunionya, aliniambia kuwa kama nataka kumuacha mchumba wangu basi nijue kuwa yeye si Mama yangu. Alishuka kwenye gari na kuniambia kuwa uamuzi ni wangu, yeye kashaongea kamaliza hivyo hawezi kuongeza kitu kingine chochote kile. Mama alikua kapaniki sana, alitembea kwa mguu kama mtu aliyechanganyikiwa, ilinibidi kumfuata huku nikimuomba msamaha na kumuambia siwezi kumuaibisha.


Nilimuambia hivyo huku nikijipa moyo kwakuwaza kuwa labda kile kilikua ni kitu cha siku moja na mchumba wangu atajirekebisha. Nilijiongelesha mwenyewe maneno mengi sana kichwan, sikupata majibu ya maswali yangu yote lakini nilijipa moyo kuwa angalau labda akinioa hawezi kunipiga. Mama alipanda kwenye gari tukaondopka, njia nzima alikua akinihubiria kuhusu usiri, kufciha mambo yangu na nisiropoke ropoke kilichotokea hata kwa mashoga zangu, alinisihi sana na kuniabia kama nina tatizo basi nimuambie yeye na si kutangaza.


Nilimuahidi kumuambia, tukarudi nyumbani kama vile kulikua hakuna kitu klichotokea. Mchumba wangu alikuja nyumbani kuniona siku hiyo, alikua kawaida sana hakuonekana kujali, alinisalimia na kunichekea. Watu walipoondoka alinihakikishia kuwa hana mtoto bali alishawahi kuwa na mahusiano na yule dada lakini wakaachana na siku ile alinipeleka pale ili kuniumiza kama yeye alivyoumia eti kwa mimi kuacha kumtetea mbele za watu na kusema ni mpenzi wake, nilimsikiliza na kumkubalia ki shngo upande kwani nilijua kabisa ilikua ni uongo.


****


Mchumba wangu alibadilikanna kurudi kamja kawaida, kipindi chote cha sherehe alikua akiniomba msamaha na madai yake nikuwa nimekua nikimuudhi sana na kumfanyia dharau mara kwa mara ndiyo maana aliamua kunifanyia vile.


“Skupanga kukupiga, wewe mwenyewe unanifahamu nilivyo mpole lakini unajua kilichotokea, nilipandwa na hasira na wewe kama mwanamke ulitakiwa kujishusha.” Nilimsikiliza na kukubaliana na kila kitu alichokua anakisema, sikutaka kubishana naye kwani nilijua fika kama nikibishana naye basi anaweza kunipiga.


Kuhusu yule mwanamke aliapa kabisa kuwa hana mtoto naye na wala hana mahusiano naye. Bila mimi kumlazimisha alinipeleka mpaka kwa yule mwanamke na kumuuliza kama si wameshaachana, mwanamke alikubali na kusema kabisa kuwa hawana mtoto kwani yeye bado hajazaa. Niliridhika kidogo na kujipa moyo labda nikweli ila bado nilikua na wasiwasi kuhusiana na mabadiliko yake ya tabia. Hatusi iliendelea vizuri lakini niliumia sana kwani yule mwanamke alikuja na alikua akicheza makusudi kuniumiza.


Miezi mitano ya ndoa yetu ilikua ni mizuri sana, alikua ni mwanaume anayejali, mwanaume ambaye anapenda, mwanaume yule yule ambaye nilikutana naye kabla ya ndoa, yule ambaye alinitongoza na kunijali. Wakati huo nilikua nafanya kazi katika kampuni moja hivyo nilikua na kipato cha kutosha, tulikua tukishirikiana katika mambo mengi na uzuri nikuwa alikua najali, pesa yangu ilikua nadra sana kuitumia kwani yeye alikua akijitoa kwa kila kitu.


Baada ya miezi mitano ya ndoa nilipata ujauzito, nilipomuambia alifurahi sana, lakini hapo ndipo mambo yalianza kubadilika, alianza kuniambia nijiandae na kuacha kazi. Nilimuuliza ni kwa sababu gani akasema hataki mtoto wake kulelewa na mfanyakazi wa ndani hivyo mimba ikifikisha miezi sita nitaacha kazi kwani yeye ana kila kitu. Sikutaka kubishana naye sana, nilinyamaza lakini rohoni nilikua naumia, pamoja na yeye kuwa na kipato kikubwa mara tatu kuliko mimi lakini bado nilihitaji kufanya kazi.


Alikua ananihudumia kwa kila kitu sawa lakini kuna vitu vingi ambavyo nilikua nanunua mwenyewe na sikuhitaji kumuambia kuwa nataka kitu flani, kuna ndugu na marafiki ambao walikua wananiomba msaada na sikua na sababu ya kumuambia yeye. Maneno maneno yalianza, alianza kuchelewa kurudi nyumbani na lilipokuja suala la kufanya mapenzi alikua mkali.


“Wewe Malaya sana, yaani una mimba lakini bado unataka kutiw* tiw* ridhika unataka kuzaa mtoto wa nama gani?” Mara nyingi alinitukana tena bila sababu yoyote, niliishia kunyamaza na kujietea kuwa nilikua nafanya kwaajili yake.


Tabia yake ya kuchelewa kurudi nyumbani ilizidi, kuna wakati alikua akirudia subuhi na nikiongea naishia kupigwa, mwanzo ilikua ni makofi kawaida ila baada ya muda alianza kunipiga mateke bila kujali kama nimebeba mimba yake. Akishamaliza kunipiga basi akiniona nimekua mpweke hurudi na kuniomba msamaha.


“Unajua kuwa wewe ndiyo unanikasirisha, kwanini unapenda kuwa na kisirani namna hiyo? Mimi ni mume wako, ni mwanaume ni lazima uniheshimu, huna haja ya kunipigia pigia kelele kila siku, unanipangia maisha nikae na wewe na mimba yako hapa tufanye nini?” Aliniambia.


Nilinyamaza na kuomba msamaha, kila wakati nilijifanya kama mimi ndiyo mwenye makosa, sikua na mtu wa kumuambia, hakutaka niwe na marafiki akidai ndiyo huharibu ndoa za watu na kwa namna nilivyokua namfahamu Mama yangu niliogopa hata kumuambia kwani nilijua lazima atakua upande wake. Ujauzito ulipofikisha miezi sita alianza suala la mimi kuacha kazi, aliniambia mimi natakiwa kuandika barua ya kuacha kazi laini nilikataa na kumuomba asubiri mpaka nitakapojifungua.


“Unanipangioa? Unanipangia hivi hujui kama mimi ndiyo mwanaume humu ndani?” Aliniuliza, nilinyamaza bvila kumjibu lakini sikuacha kazi.


Niliendelea na kazi yangu lakini siku moja alikuja mpaka ofisini kwetu, akaingia kwa bosi wangu na kumuambia kuwa tumekubaliana kuwa mimi niache kazi, alileta barua ya mimi kujiuzulu akiwa kafoji saini yangi akamkabidhi  bosi. Kwa bahati nzuri bosi wangu alikua muelewa sana, aliniita mume wangu akiwepo na kuniuliza kama nikweli. Kwakuogopa nilikubaliana nayeye kwani nilijua kama nitakataa basi anaweza kunipiga tena nikirudi nyumbani kwa madai ya kumdhalilisha.


“Una uhakika Binti?” Aliniuliza bosi wangu, yeye alikua ni baba mtu mzima, kuna kitu alikiona kwa mume wangu na alihisi kuwa labda sijashirikishwa.


“Nikweli bosi, nimekubaliana an mume wangu na mimi ndiyo nilimuambia ailete hii barua.” Nilijibu kwa uoga, mume wangu alisimama na kumkabishi barua kisha akaniambia nikusnaye vitu vyangu ili tuondoke.


“Hapana kijana, si kwa haraka namna hiyo, ngoja kwanza niangalie barua na tujue imekaaje?” Bosi alimzuia, mume wangu alisimama pembeni yake mpaka akaisoma yote.


“Umemaliza, kuna chakuongeza?” Alimuuliza, bosi wangu amabye naye alikua kasimama alikaa chini na kumuambia mume wangu naye kukaa.


“Kijana, kila ofisi ina taratibu zake, huyu binti anafanya kazi nyteti sana hapa, hawezi kuondoka tu hivi hivi bila kutoa taarifa. Hilada kama ulisoma mkataba wako wa ajira basi kunja kipengele kinasema kama unahitaji kuondoka bais unatupa notisi ya mwezi mmoja, lengo ni ili kutupa nafasi sisi kutafuta mtu mwingine. Umefanya kazi nzuri sana na ningeomba utuelewe kuwa ukiondoka yutakwama, lakini ukitupa muda basi mwezi ujao unaondoka, naja hali yako ila naamini kuwa unaweza kuvumilia angalau kwa mwezi mmoja?”


Bosi aliongea kwa utaratibu sana, mume wangu alimsikiliza kwa makini, pamoja na ushari wake lakini mume angua limuelewa na kuniambia kuwa ananipa mwezi mmoja na hiyo barua iwe kama notisi.


“Hilda wewe uasemaje maana wewe ndiyo mhusika mkuu hapa yusikuamulie?” Aliniuliza, nilimuangalia  mume wangu kama vile naomba ruhusa ya kumjibu, kweli alikubali akaondoka na kuniacha kazini. Baada ya  mume wangu kuondoka bosi wangu aliniita, alianza kunidodosa kwanini naacha kazi, sikua na jibu.


“Anakulazimisha?” Aliniuliza, nilinyamaza lakini alielewa, aliniambia hawezi kuniruhusu kuacha kazi kijinga jinga namna hiyo.


“Wewe ni kama binti yangu, mwanaume yeyote akijaribu kucheza na binti yangu basi nitamuonyesha namna ya kuwa mwanaume, kama anakupiga niambie, kama anakufanyia chochote kibaya niambie. Sitafuti mtu mwingine, utaendelea kufanya kazi hapa mpaka utakapochoka mwenyewe!” Aliongea kwa hasira, nilijaribu kujitetea lakini alikataa kunisikiliza.


“Akili zenu wanawake naziofahamu, mnaendeshwa e4ndeshwa na hivi vijanaume ambavyo vimepata pesa wakati havijabalehe vizuri vinajiona miungu watu! Kazi hutaacha na mwanaume akikuletea shida nitadili naye mimi!”


Nilitoka ofisini kwa bozi nikiwa nimechanganyikiwa zaidi, nilijua mume wangu atakasirika zaidi kama akisikia bosi ananitetea namna ile. Siku zilikua zinakimbia na mwezi ulipoisha mume wangu alikumbushia, nilimuambia bado ofisini hawajapata mtu lakini hakunielewa, alivumilia kwa wiki mbili hivi kisha siku moja alikuja ofisini kunichukua, alimuambia bosi wangu kuwa mimi ni mke wake na hataki nifanye kazi hivyo ananichukua. Bosi alikataa na alipotaka kuleta vurugu aliwaambia walinzi kumkamata na kumtoa nnje, mume wangu alikua mpole.


“Nitaondoka mwenyewe lakini naomba nimuambie huyo mwanamke, kuchagua kati ya mimi na kazi yake. Nikitoka hapo getini tafadhali usinitafute tena, itakua ndiyo talaka yako, sikulazimishi ila kama umeamua kuchagua kazi basi.” Aliongea huku akiondoka, nilimuangalia bosi kwa uchungu, alikua akinisihi kuwa nisikubali kunyanyaswa namna ile ila nilishindwa, niliamua kuondoka na siku iliyofuata niliwaletea barua rasmi ya kuacha kazi. Kila mtu alishangaa kwani walikua wananipenda sana nanilikua mfanyakazi bora sana.


Mume wangu alifurahia mimi kuacha kazi, alibadilika kwa kama wiki mbili hivi. Siku moja mimba yangu ikiwa na miezi nane nilipigiwa simu, ilikua ni jioni, mimi nilikua chumbani na sikujua kuwa mume wangu kasharudi toka kazini kwani aliingia kimya kimya. Ilikua ni sibu ya bosi wangu, alikua ananiuliz akama nina mpango wa kurudi kazini.


“Leo tumelazimika kufanya usahili kwaajili ya nafasi yako, kuna vijana wengi wana uwezo ila bado sijakata tamaa na wewe nataka uniambie kama tuijaze hii nafasi ua la? Kama hutarudi tena niambie maana kesho bodi inataka majibu na sijui cha kuwaambia. Nimewasubirisha sana kuwa umjamzito na mimba inasumbua ila watu wahsajua, mambo aliyofanya mume wako hapa imekua ngumu sana mimi kukutetea…”


Aliniambia, kumbe mume wangua likua anasikiliza na aliingia wakati huohuo kabla hata sijatoa jibu, kwa uoga baada tu ya kumuona nilijikuta namjibu bosi wangu kwa hasira.


“Nimeshakuambia sitaki kurudi, weka mtu mwingine mimi niko kwenye ndoa yangu na nina furaha na mume wangu…” Nilikata sim,u harakaharaka na kunyanyuka kumpokea mume wangu, lakini hata sikumfikia, nilikutana na teke la tumbo ambalo lilinisukuma na kujikuta napiga kichwa kwenye mbao ya kitanda.


Mume wangu alinivamia na kuanza kunipiga huku akinitukana, kusema kweli nilisikia masauti kama makelele makelele kwani kishindo cha kugonga kichwa kwenye mbao kilinifanya kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa. Niliona marweruwe lakini nilisikia tu miguu yake na mikono yake ikinipiga, alinipiga mpaka nikapoteza fahjamu. Nilikuja kuzinduka saa tisa usiku, mwili umevimba nipo kwenye maumivu makali, nilijaribu kujinyanyua lakini nilishindwa, kila kitu kilikua kizito, tumbo lilikua linauma sana, nilijikuta nashindwa kufanya chochote na kulala palepale na maumivu yangu mpaka asubuhi.


Muda wote huo mume angua likua amelala kitandani, asubuhi aliamka na kuniamsha.


“Mwanamke mke wa mtu unalala mpaka sasa hivi unafikiri mimi kazini nitaendaje?” Aliongea kwa utani kama vile hakuna kitu chochote kilichokua kimetokea. Nilijitahdi kunyanyuka nikashindwa, alinishika mkono na kuninyanyua.


“Mke wangu na wewe kwa kujidekeza, kaugomvi kidogo tu unataka kusema huwezi kunyanyuka, sasa nani ataninyooshea? Leo chai ni kuywa ofisini tu…”


Alijiongelesha huku akiendelea kuchekacheka, kama kawaida yake baada ya kunipiga aliniomba msmaaha na kunilaumu, alikua akiniambia kuwa mimi ndiyo nimekkasirisha kwa kuongea na bosi wangu.


“Lakini nimependa jibu lako, mtu anaona tuna furaha anatraka kutuingilia, kwanini asimpe hiyo kazi mke wake…” Alijiongelesha, mimi sikumjibu, alitoa nguo zake na kuanza kuzinyoosha.


“Leo nakusiadia majukumu yako ila ukiendelea kudakadeka basi wenzako wapo wengi tu wa kukusaidia…” Aliendelea kuongea, mimi sikujali nilimuacha ajiongeleshe na kujijibu mwenyewe. Sikutaka kuingilia chochote kile mwili ulikua kwenye maumivu makubwa.


Maisha yaliendelea lakini siku mbili baadaye mtoto alikua ahchezi, nilienda kliniki kuwaambia, waliniuliza tangu lini nakumbuka ilikua ni mchana wa siku mume wangu aliponikpiga. Nilifanyiwa vipimo na kuambiwa niende hospitali kubwa. Kule nilipimwa na kuambiwa kuwa mtoto amefia tumboni.


SIMULIZI; AKIKUUA TUTAKUJA KUCHUKUA MAITI YAKO!—SEHEMU YA TATU


Hali yangu ilibadilika ghafla, ingawa mwanzoni walitaka nijifungue kawaida lakini ilionekana hali yangu ni mbaya, ili kuokoa maisha yangu walilazimika kunifanyia oparesheni na mtoto kutolewa. Alikua ni mtoto kamili kashakamilika kila kitu. Daktari ambaye alikua ni saktari wangu tangu mwanzo alishangaa ni kitu gani kilichokua kimetokea wakati mtoto alikua katika hali nzuri siku mbili kabla nilipoenda kiliniki. Nilishindwa kuongea nikimhofia mume wangu, mwanzo mume wangu aliniomba msamaha kwa kilichokua kimetokea akiniahidi kuwa hatanipiga tena.


Sikumuambia mtu yeyote kuhusu kupigwa na mume wangu, nilikaa kimya nikigulia kidonda changu na mume wangu kweli alibadilika kwa muda. Kutokana na kufanyiwa oparesheni niliambiwa kukaa angalau miezi mitatu kabla ya kufanya tena mapenzi. Baad aya kama mwezi mmoja tu hivi mume wangu alibadilika, alianza kuchelewa kurudi nyumbani na  kuwa mtu wa hasira sana, kila nilipokua nikimuuliza alikua mkali, hakunipiga lakini alikua akiongea maneno ya kejeli na kunitukana nikalazimika kunyamaza.


Siku moja alichelewa kurudi, alirudi nyumbani akiwa kalewa sana, akaingia moja kwa moja mpaka chumbani, nilikua nishamuandalia chakula lakini hakula. Alikaa chumbani kwa kama nusu saa hivi simu yake ikaanza kuita, alikua kalala fofofo, ilikua ni namba mpya haikuseviwa, nilimuamsha ili kuipokea lakini alikua kalewa sana hata hakunisikia. Baada ya kuona ile simu inasumbua sana niliamua kuipoke aili kumuambia mpigaji kuwa mwenyewe alikua kalala. Lakini ile napoke atu nilikutana na matusi kutoka kwenye sauti ya kike.


“Mshenzi mkubwa wewe, yaani unaniacha kwenye gari unaingia kwako! Nususaa mimi nakusubiri mbwa wewe! unataka nifie humu ndani! Unatomb** kwanza na mke wako ndiyo uje kwangu…” Ile sauti ilitukana sana, nilishtruka kwani mhusika alimaanisha alikua nnje, bila kumuamsha mume wangu nilitoka nnje, nilienda mpaka kwenye gari ya mume wangu na kukuta kuna dada, binti modgo tu ambaye alikua kavaa vinguo vya kimalaya Malaya alikua kasimama ameshikilia simu.


“Unafanya nini nyumbani kwangu?” Nilimuuliza, aliniangalia kwa dharau huku akikata simu.


“Kwako hapa? Wewe si kama mimi tu umeweka, umechangia tofali hap…” Alianza kuongea kwa dhara, nadhani zilikua ni hasira za mume wangu kunifanyia yote yale, nilijikuta namshika nyywele na kuanza kuzivuta, alipige kelele nyingi za maumivu huku akilia kuwa nimuachie. Nilivuta mpaka getrini, mlango mkubwa ulikua wazi kwani mume wangu alipoingia hakuufunga, ilionekana walishapanga kutoka tena na ndiyo maana yule dada alikua anmsubioria, nilimtoa nnje na kufunga geti langu.


Lakini ile narudi ndani mume wangu alikua kashatoka, alionekana ndiyo kwanza alikua kazinduka kutoka usingizini. Hakunisemesha chochote alitoka na kuingia kwentye gari, hakumuona yule Dada hivyo alikuja kwangu na kuniuliza nimefanya nini? Nilimuambia nilichofanya, bila kusema chochote alininyang’anya simu yake, alienda na kufungua geti akaingia kwenye gari na kutoka. Sikumuona tena mpaka siku iliyofuata, alirudi nyumbani saa tano asubuhi, alikua hajalewa yuko kawaida.


Ingawa nilikua na maswali mengi sana kichwani kwangu lakini sikumuuliza, nilijua kuwa haitasiadia kitu, alishaamua kuchepuka hivyo niliamua kumuacha na maisha yake.


“Mbona huniulizi chochote?” Aliniuliza baada ya kuingia ndani na kukaa kama nusu saa bila mimi kumuuliza kitu kilichotokea jana yake.


“Nikuulize kuhusu nini?” Nilimuuliza kwa mshangao, nilijua kabisa anataka kuleta gubu hivyo niliongea kwa sauri ya chini.


“Wewe utakua na wanaume wengine, haiwezekani mume wako anachepuka anakuja na mwanamke mpaka nyumbani lakini husemi chochote, hembu niambie, au unataka kuniua?”


Nilimuangalia kwa hasira nikitamani hata kumpiga na chupa ya chai ambayo ilikua mezani, mimi niliamua kunyamaza lakini kwake hilo nalo lilikua ni tatizo.


“Mume wangu unataka nini kwangu? hivi kweli unataka mimi niwe nakuchunga  kama mtoto, wewe ni mtu mzima, una akili zako, unataka nihangaike na wewe?”


“Inamaana hunionei wivu, kama hunionei wivu basi utakua hunipendi, wanawake wengine wangegombana lakini wewe umekaa tu, nahisi hunipendi, siwezi kuishi na mwanamke kama wewe, kama huwezi hatakunionea wivu mimi naona kabisa bora tuachane!”


Aliongea kwa suti ya chini kidogo huku akinisogelea na kutaka kunishika, hapa aliongea kama kautani kidogo lakini kwa kumaanisha. Nilijisogeza pembeni, sikutaka aniguse kabsia. Kitendo cha kujisogeza kilimuudhi, alianza kulalamika na kusema kuwa simtaki kimapendi ndiyo maana anamaua kuchepuka.


“Mume wangu mimi nina mshono unatraka nianze kufanya mapenzi? Kweli ni haki hiyo?” Nilimuuliza, alikasirika zaidi na kuniambia kuwa kuna wanawake wengi wanakua na miishono tena mikubwa kuliko wangu lakini wanafanya mapenzi na waume zao.


“Mimi nimchoka kuchepuka, nakutaka mke wangu na nataka kufanya mapenzi na wewe, kama huwezi basi ondoka nyumbani kwangu, kwani kinachofanya mpanzi ni tumbo au?” Nilinyamaza kimya bila  kumjibu, kitu ambacho kilimfanya kulalamika zaidi kuwa simpendio na nina kiburi. Alinichosha na kunipendisha hasira, bila hata kupanga nilijikuta nanyanyuka na kuondoka nikimuacha kakaa peke yake sebuleni, niliingi chumbani, sikua na kitu cha kufanya huko lakini niliingia ili tu kumkwepa mume wangu.


Hicho nacho kilimkasirisha mume wangu, alikuja kitandani na kunivamia, alinishikilia chini na kunilazimishia kufanya mapenzi, hakujali mshono, hakujali maumivu yangu na hakujali chochote kile. Nashukuru Mungu pamoja na kunifanyia kwa nguvu tena akifanya makusudi ili kuniumiza lakini sikuumia, hakunitonesha mshon, alifanya anavyotaka na kuanzia siku hiyo ilikua kama kazi, alikua akiniambia kuwa anataka mtoto na kwakua yule mwingine nimemuua makusudi basi hataki kusubiri.


Niliumizwa na vitendo vyake lakini niliumizwa zaidi na maneno yake, namna ambavyo alikua anaongea ni kana kwamba mimi ndiyo nilisababisha mimbayangu mtoto kufia tumboni.


“Tatizo lako unapenda kunikasirisha sana, ungekua na nidhamu sidhani kama mtoto angefia tumboni, wala nisingekupiga, sikudhamiria kukupiga!” Alikua akiniambia, kwa namna alivyoongea kuna wakati nilijihisi kabisa kuwa labda tatizo ni mimi, niliona kabisa kuwa mimi ndiyo nilimsababisha mume wangu ili kunipiga, kuna wakati nilipiga magoti na kumuomba Mungu msamaha kutokana na dhambi ya kuua.


***


Miezi mitatu baada ya mimba yaangu ya kwanza kuharibika nilikua na ujauzito mwingine, bado nilikua Mama wa nyumbani sina kazi, manyanyaso yalikua mengi lakini nashukuru Mungu niliweza kujifungua salama. Katika ujauzito huu mume wangu hakuninyanyasa, si kwasababu alikua anapenda, hapana nikwakua Mama yake alikua pale nyumbani. Mama yake alikua anaumwa hivyo alilazimika kuja kutibiwa, mume wangu ni wale watu wakupenda kujionyesha kuwa wanajali, wanapenda na kutaka kuonekana wema.


Kwa sababu hiyo Mama yake alikuja kipindi nina ujauzito wa miezi miwili, nilimhudumia mpaka nilipofikisha miezi sita alipona lakini alikataa kuondoka akinihudumia na mimi kwani alikua akiamini kuwa sababu ya mimi kumpoteza mtoto wangu wa kwanza ni kazi nyingi hivyo kwakua alikua nha hamu sana na mjukuu basi angekaa mpaka nijifungue. Kweli nilijifungua salama na mtoto alipofikisha miezi mitatu Mama mkwe aliondoka na kurudi kijijini kwao. Mume wangu ndiyo alimpeleka na ni kama alikua anasubiri Mama yake kuondoka ndipo aanze vituko vyake.


Ingawa alisema kuwa atakaa siku mbili lakini mume wangu alikaa siku sita, hakua kwao kwani Mama yake aliniambia kuwa ashaondoka. Alikua akinipigia simu kuniulizia kuhusu mtoto ila nilipomuuliza alipokuepo basi ilikua ni ugomvi kuwa nataka kumkalia kichwani yeye ni mwanaume na hapangiwi. Niliishia kunyamaza na aliporudi hata sikumuuliza. Maisha yaliendelea lakini mume wangu alianza kuwa mbahili, alikua hatoi pes aya matumizi, alimfukuza mfanyakazi wa ndani kwa madai kuwa mimi ni Mama wa nyumbani sina kazi ya kuhitaji mfanyakazi.


Alikua ni mtu wa kukaa mpaka siku tatu nne harudi nyumbani, haachi pesa ya chakula na nikiuliza tu ni matusi na vipigo. Nilitumia kila akiba niliyokua nayo mpaka ikaisha, mume wangu hakua anahudumia chochote, alinitelekeza na akirudi nyumbani alikua akihitaji chakula kama kawaida. Hali ilikua ngumu zaidi kwani mafao yangu ambayo nililipwa kazini aliyachukua kinguvu nikabaki sina kitu kabisa. Baada ya kuona hali inakua ngumu sana niliamua kutafuta kazi, nilizunguka sana kutafuta kazi kimya kimya bila mume wangu kujua lakini kazi nazo zilikua ngumu.


Nilizunguka sana bila mafanikio kwani kila sehemu nilipokua nikienda basi nilikua nikikataliwa kutokana na kuwa na mtoto mchanga. Baada ya kuzunguka sana kutafuta kazi za elimu yangu nilichoka na kuamua kutafuta kazi yoyote ile bora nipate hela ya kula kwani mume wangu alikua hajali, alikua anaweza kukaa hata wiki bila kurudi nyumbani, kujua nakula nini wala mwanae anakula nini. Nilipata kazi ya kufua, nilikua nikizunguka kwenye majumba ya watu, nawaomba kuwafulia na kufanya usafi wananilipa elfu kumi au siku nyingine tano na siku inaisha.


Siku moja nilikua nafua sehemu, wakati nafua kuna gari ilikuja na kusimama, ukiwa kwa ndani mlango mdogo wa geti ukiwa umefunguliwa basi unaona nnje, niliona lilikua na nembo ya gari la ofisi yangu ya zamani, sehemu niliyokua nikifanya kazi. Walishuka wakaka wawili, wote sikuwafahamu, waliingia katika vyumba vya jirani na yule mtu niliyekua nikimfulia, walikaa kama dakika kumi hivi ndipo aliingia mzee mmoja, huyu nilimkubuka kwani alikua ni dereva, tena dereva wangu kipindi nafanya kazi. Nilipomuona anaingia nilijigeuzia ukutani kwani sikutaka anione.


Alienda kwenye chumba cha wale wakaka na kuongea nao kitu kisha wakatoka, wakati anatoka alimuona mtoto wangu ambaye ndilikua nimemkalisha kwenye karai nimemuwekea na nguo kwani alikua bado hajaanza kukaa vizuri. Mtoto alipowaona alianza kulia tena sana, niliendelea kujibanza ili watoke nimchukue mtoto wangu lakini hawakutoka, walisimama na yule mzee alianza kumbembeleza mtoto, alimuangalia na alipombeba  mtoto alinyamaza kimya kama kashikiliwa na Baba yake.


“Wewe ndiyo Baba nini? Mbona kakupenda ghafla?” Wenzake walimtania, alicheka huku akinifuata kunipa mtotyo.


“Dada mwanao atakua na njaa ndiyo maana analia…” Aliniambia sikua na namna zaidi ya kugeuka, nilikua nimchoka sana ukilinganisha na mwanzoni. Mwanzo hakunigundua kwani hakudhani kuwa anaweza kunikuta maeneo kama yale,. Alinikabidhi mwanangu lakini kabla ya kutoka alikumbuka kitu na kugeuka.


“Dada samahani…” Alikua ni mzee mtu mzima lakinia liniita Dada, hakuniita hata mwanangu kwa namna nilivyokua nimchoka.


“Kuna Binti mmoja umefananana naye, anaweza kuwa mdogo wako au ndugu yako, mmefanana sana, mtu angeweza….” Hakumalizia, alinyamaza kidopgo kisha akaniangalia tena na kuniambia.


“Hapana, niwewe Bosi? Si Hilda wewe?” Nilitamani kumuambia kuwa amenifananisha lakini nilishindwa.


“Haya ni maisha tu kwanini nijionee aibu?” Niliwaza na kuamua kumuambia ukweli kuwa ndiyo mimi. Alikua na maswali mengi lakini aliitwa ikionekana kuwa mabosi wake wana haraka, aliondoka huku akiniachia noti ya Shilingi elfu kumi. Nilimshukuru sana kwani alikua kanisaidia sana.


Niliiangalia ile elfu kumi machozi yakanitoka, miaka miwili nyuma yeye ndiyo alikua anakuja kwangu kunililia matatizo ya familia yake na mimi kumpa elfu kumi sasa hivi yeye ndiyo alikua ananipa. Nilimshukuru sana Mungu kwa siku hiyo. Nilimalizia kufua na kurudi nyumbani, lakini jioni simu yangu iliita, ilikua ni namba ya Bosi wangu wa zamani, nilikua naijua kichwani, nilipokea baada ya salamu aliniambia kuwa kesho yake niende ofisini kumuona. Sikujua alipata wapi namba yangu kwani ilikua ni mpya lakini kesho yake nilikua ofisini kwake.


Tuliongea mengi, nikamuambia baadhi tu ya mambo ambayo yalinitokea katika maisha yangu namna nilivyopoteza mtoto na sasa hivio hali ni ngumu kwani mume ni kama kanitelekeza.


“Ile nafasi yako kwa sas ahaipo ila kuna nafasi za chini chini, unaweza kuanza huko huku tukikutafutia nafasi ya hadhi yako.” Nilisita kuchukua ile kazi nikiwaza kuhusu mume wangu lakinia liniondoa wasiwasi akiniambia kuwa mwanzo aloifanya makosa kuniacha niondoke ila si sasa.


“Huyo mume wako kama ni mwanaume kweli atapambana na mimi, niachie hiyo kazi hataongea chochote.” Aliongea kwa kujiamini, nilikubali ile kazi na kuanza, sikumuambia mume wangu kwani hakuepo nyumbani. Lakini sijui ni nani alimuambia kuwa nafanya kazi ila siku tano baadaye alikuja nyumbani na kunifukuza akisema kuwa natembea na Bosi wangu, nilimpuuzia na kumuambia kuwa sina mahusiano na Bosi wangu lakini hakuamini, aliniambia kuwa hanitaki. Kwakua nilikua na kazi sikujali sana, niliondoka na kwenda kulala Gest na mwanangu kwani nilikua naenda naye kazini.


Nilikua bado sijapata binti wa kazi hivyo kwakua hata bado nilikua sijapata kazi maalumu basi niliruhusiwa kumpeleka. Siku iliyofuata nilipanga kutafuta chumba ili nianze maisha upya kwani nilishachoka manyanyaso ya mume wangu. Lakini usiku nilipokea simu kutoka kwa mke wa Bosi wangu akiniambia niachane na mume wake. Mimi nilishangaa kwani sikua na mahusiano na Bosi wangu lakini yeye aliniambia kuwa anahabari kuwa nimemkimbia mume wangu kwaajili ya mumewe hivyo nikae mbali naye.


Alikata simu kabla ya hata mimi kujielezea. Usiku huo sikulala nilibaki na mawazo sana nikiwa sijui hatima yangu. asubuhi kama kawaida nilienda kazini, kwenye saa nne hivi niliitwa ofisini kwa Bosi na nilipofika nilimkuta mkewe kakaa kakasirika.


“Kwanini una mkingia kifua kama si hawara yako, anafanya nini hapa? Ni eidha mimi au huyo mwanamke wako, huwezi kumng’ang’ania mke wa mtu anakuhusu nini?” Wakati naingia mke wa bosi alikua akilalamika na bosi akimsikiliza.


SIMULIZI; AKIKUUA TUTAKUJA KUCHUKUA MAITI YAKO!—SEHEMU YA NNE


Mke wa bosi wangu alikua kafura, alikua kama mtu aliyechanganyikiwa akimshutumu bosi wangu kwa kutembea na mimi. Nilitaka kuongea kujielezea lakini Bosi wangu aliniambia kunyamaza.


“Sikukuita hapa ili ujielezee, hapana, mke wangu hahitaji maelezo yako ili kuniamini.” Aliongea na kutulia kidogo, mke wake aliniangalia kwa hasira. Bosi alinimuambia mke wake akae, alikataa lakini alimkazia macho mpaka akakaa.


“Naataka umuangalie huyo binti vizuri…” Aliongea, mke wake aliniangalia tena kwa dharau zaidi.


“Una miaka mingapi?” Aliniuliza, nilifikiri kidogo kisha nikamjibu.


“34, ndiyo nimefikisha juzi.”


“Mke wangu, Asha ana miaka mingapi?” Alimuuliza mke wake ambaye hakuonekana kama kumuelewa.


“Asha?”


“Ndiyo, Asha mtoto wetu.”


“Mhhh! Atakua na 27 au 28, mimi sikumbuki vizuri.” Mke wake alijibu huku bado akinikazia macho.


“Ana miaka 26 ila keshokutwa anaingia 27. Na suisi tumekaa kwenye ndoa yetu kwa miaka mingapui?” Alimuuliza na mke wake alimjibu miaka 35. Bosi alitabasamu kisha kuniambia kuwa niondpke, kabla sijaondoka mkewe alilalamika kuwa natakiwa kufukuzwa kazi ndipo Bosi alimuambia.


“Unanifahamu kwa zaidi ya miaka 40, tangu tunakutana kijijini mpaka nakuoa. Kama katika miaka yote hiyo basi unaweza kuamini maneno yam pita njia kuwa mimi naweza kufanya mapenzi na mwanamke sawa na binti yangu basi mke wangu hunijui vizuri na sidhani kama kuna maelezo yoyote ambayo naweza kukuambia yakawa na maana. Kama umekaa na mimi miaka 37 kwenye ndoa tunalala na kuamka pamoja lakini huwezi kuniamini unaamini simu moja ya mpumvavu mmoja basi nadhani sina haja ya kukuelezea sana, tukifika jioni nitachukua vitu vyangu nitaondoka kwani kama huniamini sidhani kama  mimi ni mtu sahihi kwako.”


 Bosi aliongea kwa uchungu sana mpaka mke wake akaanza kuona aibu na kuanza kujitetea.


“Lakini wanaume wanabadilika mume wangu…” Aliongea kama vile anabembeleza.


“Wanabadilika ila naamini unanijua vizuri sana mke wangu, kuna mambo unajua naweza kuyafanya na mambo ambayo unajua siwezi kuyafanya. Labda nakuhukumu bure, lakini naomba utoke na huyu binti kaongee naye kisha urudi hapa halafu uniambie hivi kweli kama kuna mwanaume angekua anamfanyia binti yetu mambo kama haya usingemsaidia huyu binti?” Bosi aliongea huku akituonyeshea ishara ili tutoke.


Nilitoka na mke wa Bosi mpaka ofisini kwangu, aliniambia nifunge mlango, mwanzo nilihisi kuchanganyikiwa nikidhani labda kuna kitu kibaya anataka kunifanyia lakini alinitoa hofu.


“Usiogope, namfahamu mume wangu, nilipaniki kidogo lakini namfahamu mume wangu, naomba uniambie kuna nini.” Nilifunga mlango na kukaa kisha nikaanza kumuelezea mke wa bosi mataizo yangu, nilimuambia kila kitu bila kuficha, namna mume wangu alivyokua akinipiga na kuninyanyasa, namna ambabyo mimba yangu ya kwanza mtoto alifia tumboni, nilimuonyesha makovu ya viboko mgongoni, nilimuonyesha mistari ya viboko kwenye mapaja na mateso mengine mengi.


Wakati wote huo alikua akilia, tulitoka pale mpaka kwa mume wake, alimuomba mume wake msamaha na kumuambia kuwa  nahitaji kuondoka kwa mume wangu, alimuambia wanaipe nyumba ili nikakae wakati nikijipanga lakini bosi alikataa.


“Huyu ni mtu mzima anapaswa kufanya maamuzi yake mwenyewe, kama anataka kuondoka basi hatupaswi kumpa nyumba, hapana atabweteka, anahitaji kuwa na kwake. Tutamlipia kodi ya miezi sita ksiha ataendelea mwenyewe na maisha yake kama wafanyakazi wengine.”


Alinipa muda wa kutafakari, kwakua nilishapanga kuondoka sikua hata na kitu cha kutafakari, baada muda nilimuambia nataka kuondoka, walinitafutia chumba na sebule wakaniambia nianze maisha sehemu amayo mimi nitakua na uwezo nayo kutokana na kipato changu. Niliondoka na kuhama bila kumuambia chochote mume wangu, alikua hayupo nyumbani kama kawaida yake. Baadaye alijaribu kunitafuta na kuniletea vurugu lakini Bosi alsihanipanga, nilienda Polisi na kwakua Bosi naye alikua akijulikana kama mume wangu walipambana na mume wangu akanywea na kuniacha niendelee na maisha yangu.


Maisha yalianza kuwa na amani nikiishi mimi na mwanangu, mume wangu alianza kuhangaika kwa ndugu na kutangaza kwa watu kuwa nimemkuimbia na kuiacha ndoa lakini sikujali, nilishaamua kuandelea na maisha yangu sikutaka kitu chochote kile kunisimamisha. Baada ya kuona kuwa sitetereki mume wangu alikata mawasiliano kabisa, alikua hahudumii mtoto chochote, hatoi matumizi wala hapigi simu kuulizia hali zake. Mimi pia sikujali na wala sikuulizia chochote, nilifanya kazi kwa bidii mpaka kupanda cheo na kuwa na cheo changu cha awali hivyo nikawa niko vizuri.


Baada ya kuona niko kimya naendelea na maisha yangu mume wangu alianza kunitafuta, alipitia kwa ndugu zangu, alianza kwa Mama yangu akimuomba kuongea na mimi. Alimuambia kuwa amejirudi na kuna mambo ambayo alikosea huko nyuma. Mama Alinitafuta, nilimuambia kilichotokea lakini hakujali.


“Mwanaume akikuomba msamaha unamsamehe, wewe ushakua mtu mzima, unafikikiri kuna mwanaume mwingine atakutaka kama ukiachika, vumilia mwanangu, mume wako ni msomi, ana kazi nzuri na anapesa sasa kwanini kuhangaika huko na vinyumba vyakupanga, kama mwanaume kakuomba msamaha basi msamehe.”


Mama aliniambia, kwangu ilikua ngumu sana kurudiana na mume wangu, Baba yangu hakua akijua kilichokua kikiendelea lakini aliniambia uamuzi ni wangu kwani mimi ndiyo nilikua naenda kuishi naye. Wadogo zangu na Kaka zangu sikuwaambia chochote, walijua tu tumegombana kawada. Mwanzo niligoma lakini baada ya mume wangu kutuma ndugu zake na kuapa kuwa hatarudia basi nilikubali kumsamehe. Aliniruhusu kuendelea na kazi na maisha yaliendelea. Mume wangu alibadilika kabisa, hakunipiga tena, alihudumia familia na kweli niliona kabisa kuwa ni mtu mpya.


Nilipata ujauzito wa pili na kujifungua salama, mtoto akiwa na miezi sita nilipata mimba nyingine, mume wangu alitaka nizae harakaharaka lakini mimi sikutaka, bado mwanangu wa pili alikua mdogo, nilitamani kuitoa mimba lakini baada ya kuongea na Mama aliniambia watoto ni baraka hivyo nizae tu. Baada ya kubeba ujauzito wa tatu mume wangu alianza kurudia hali yake ya zamani, alianza kuchelewa, alianza kuninyanyasa na maneno mengine ya kashfa kibao tu. Alitaka niache kazi lakini mimi sikua tayari kusha kazi, kisingizio chake kikubwa ilikua ni watoto wake, hakutaka wanae kulelewa na binti wa kazi.


Siku moja nilikua nimetoka kazini, nilikua nimchoka sana hivyo nilivyorudi nyumbani sikufanya chochote, moja kwa moja nilielekea mpaka chumbani kujilaza baada ya kumnyonyesha mtoto. Nikiwa nimepitiwa na usingizi niliamshwa na kelele za mtoto akilia. Mtoto wangu wa kwanza alikua kwa Bibi yake, hivyo nilikua na mtoto mchanga tu ambaye baada ya kumnyonyesha nilimlaza katika kitanda chake chumbani sebuleni kwani mchana tunakisogeza sebulani ili iwe rahisi dada wa kazi kumsikia.


Mtoto alikua analia sana kiasi cha kuniamsha mimi ambaye nilikua chumbani. Nilitoka na kumchukua, nilianza kumtafuta dada wa kazi ili kujua ni kwanini alikua anamsikia mtoto analia lakini hamhudumii. Nilizunguka sana ndani kote sikumuona, nilitoka mpaka nnje lakini sikumuona. Wakati nataka kurudi ndani niliona gari ya mume wangu ikiwa imepaki, nilishangaa kwani wakati naingia mume wangu alikua bado hajarudi, mlango wa nyuma ulikua umefunguliwa, nilijua mume wangu yupo hivyo nilienda kumuangalia na kumsalimia kwani nilihisi labda ndiyo anaingia nyumbani na huenda anavitu vya kubeba ndiyo maana kafungua mlango wa nyuma.


Nilitembea taratibu, ile nafika tu nasofeza mlango, nilimkuta mume wangu kainama, kashusha suruali mpaka chini kwenye magoti anafanya mapenzi na binti yangu wa kazi. Aliponiona hata hakushtuka, aliendelea kufanya binti wa kazi hakuniona kwani yeye alikua amelala chini. Nilitamani kupiga kelele lakini nilishindwa, nguvu ziliniishia nikadondoka chini nikiwa na mtoto mkononi. Sikupoteza fahamu hivyo nikiwa pale chini sina nguvu hata ya kunyanyuka nilimuona mume wangu akiendelea kufanya mapenzi na binti yangu wa kazi tena mbele yangu. ilikua ni jioni tu kigiza ndiyo kinakaribia kuzama hivyo kila nikifungua macho niliona kila kitu.


Alifanya mpaka akamaliza huku mtoto akiwa mikononi mwangu akilia, baada ya kumaliza alimchukua mtoto na kuingia naye ndani wakaniacha pale nikiwa chini. Baada ya kama nusu saa hivi nguvu zilinirudia, nilinyanyuka na kuingia ndani, nilimkuta binti wa kazi kajifunmgia chumbani analia, mume wangu kakaa sebuleni anmambembeelza mtoto. Kwanza nilimchukua mwanangu sikutaka ambemende, nilimpeleka chumbani na kumlaza kisha nikarudi mpaka kwenye chumba cha yule binti, nilianza kugonga mlango nikimuambia afungue, nilitukana na kutukana lakini hakufungua, mume wangua linifuata na kunipiga makofi.


“Wewe ndiyo umeyataka yote haya, mimi nilioa mke wa kunifulia na kunipigia, sasa kama huwezi makujumu yako kama mke kwanini wenzako wasikusaidie, kwanini unachagua kazi za kusaidiwa nazo na nyingine hutaki?” Aliniuliza kwa makofi, mume wangu alinipiga sana hakujali hata kama bado nimjamzito. Alinipiga sana na kuniambia kuwa hata nikimfukuza yule binti nikaleta mwingine naye atatemeba naye na kama nataka aache kutembea na mabinti wa kazi basi niache kazi na kumhudumia yeye kama mwanaume kwa kila kitu. Nililia sana lakini hakujali, aliniambia hawezi kuishi na mwanamke ambaye atembei naye.


Pamoja na yeye kuongea sana na kukataa nisimfukuze lakini asubuhi yake nilimfukuza yule binti nyumbani kwangu. Sikua na mpango wa kuacha kazi lakini nilikua na mtoto mdogo, nisingeweza kumpeleka kazini kwani mikiki mikiki ya kazini ilikua mingi. Nilimpeleka kwa wifi yangu wakati nikitafuta binti mwingine wakazi. Nilihangaika kutafuta binti wa kazi nilikosa ambaye angekua na vigezo vyangu, sikutaka kuacha kazi hivyo nilitaka kutafuta mwanamke mtu mzima ambaye mume wangu asingemtamani.


Baada ya kama miezi miwili ya kuhangaika nilipata, mume wangu alikasirika kwani alikua ni mama mtu mzima lakini sikujali, nilichotaka ni kulinda ndoa yangu na kuendelea kufanya kazi kwani nilijua kuwa kama nikiacha kazi manyanyaso ya kipindi kile yatarudi. Maisha yaliendelea, manyanyaso hayakupungua, mume wangua likua hampendi yule Mama hivyo hasira zake zote alinishushia mimi, alikua ni mtu wa kuchelewa kurudi, alikua ni mtu wa kunipga na kunitukana matusi ya nguoni kwa lengo la kunidhalilisha, vyote hivyo nilivumilia.


Siku moja mume wangu alikuja na kijana mmoja, alikua ni kijana mdogo tu labda wa miaka 22, aliniambia kuwa ni mdogo wa rafiki yaake, mimi nilimpokea na kumkaribisha vizuri tu. Alikaa pale nyumbani kama wiki mbili hivi, lakini kuna mambo ambayo nilikua siyaelewi elewi, yule kijana alikua na mambo ya kike kike, alikua na tabia za kingie chumbani kwengu na kuongea na mimi kama shoga yake, nilimuambia mume wangu akaniambia kuwa nimuache tu ni utoto.


Siku moja nilikua chumbani kwake, ni chumba cha wagani alichokua akilala, kuna vitu nilikua nachukua katika kabati nikakutana na nguo za yule kijana, kulikua na chupi nyingi za kike. Nilikasirika nikamuita na kumuuliza, mwanzo aliongea kwa kujiuma uma lakini baadaye aliniambia kuwa yeye ni shoga na mume wangu ndiyo kamleta pale akimuambia anakuja kufanya kazi lakini hajui kazi gani ila anamlipa. Nilimuuliza kama wana mahusiano na mume wangu alikataa katakata, tuligombana sana na siku ileile bila kumshirikisha mume wangu nilimfukuza.


Mume wangu alipokuja alikana kabisa kuwa alijua kama ni shoga bali ni mdogo wake na rafiki yake na alikasirika kwa mimi kumfukuza kwani nilimshalilisha. Mimi sikujali, lakini usiku uleule wakati nafanya mapenzi na mume wangu alijifanya kupotea njia, nilishtuka ndipo alinikandamizia na kuniambia kuwa mimi nina mimba hivyo hafurahii kufanya mapenzi na mimi sehemu za kawaida anataka kufanya kinyume na maumbile. Nilikasir8ika sana lakini sikua na nguvu, alinipiga sana siku hiyo, kila nilipojaribu kujitoa alikua ananipiga na alinifanyia mapenzi kinyume na maumbile mpaka alipochoka.


Asubuhi mume wangu aliamka akiwa analia, alilia sana na kuniomba msamaha, alikua akiniambia ni shetani kampitia na hajui kwanini alifanya hivyo, alilia na kuomba nisiondoke kwania tajirekebisha. Alionekana kujutia kuliko siku nyingine yeyote ile. Kwa kawaida mume wangu akifanya kosa si mtu wa kuomba msamaha na kama ukimuuliza uliza sana au ukijifanya kukasirika basi unsishia kupigwa na uumizwa, lakini siku hiyo aliomba msamaha huku akilia kama mtoto, nilishangaa sana na sikua na namna zaidi ya kumsamehe.


Maisha yaliendelea, alibadilika kwa siku tano hivi kisha akataka tenja ule mchezo, aliniambia kashaupenda hivyo nimruhusu, mimi nilikataa, kila nilipokua nikikataa alikua akinipiga, alikua akanipiga sana mpaka kufikia hatua ya kuzimia na asubuhi anaomba msamaha. Hayo ndiyo yalikua maisha yangu, baada ya kuwa namnyima kufanya mapenzi kinyume na maumbile alikataa kabis akufanya mapenzi na mimi na kuanza kubadilisha wanwake kama nguo, alikua akifanya hivyo huku akihakikisha kuwa najua na naumia, kama nikimfumania nisipoongea basi niliambulia kipigo.


Alikua akinipiga kuwa nitakua na mwanaume mwingine ndiyo maana simuonei wivu. Hali ile ilinichosha, niliona kama vile atakuja kuniua. Siku moja nakumbuka ilikua siku ya jumapili, niliamua kuondoka, nilimpigia simu mdogo wangu wa kiume amabye alikua kamaliza chuo na kumuambia kuwa anitafutie chumba kwani kuna rafiki yangu anahitaji chumba cha kupanga. Mdogo wangu alikua hafahamu sana matatizo, hivyo alipopata chumba alinipigia na aliponikosa kwenye simu alimoigia mume wangu na kumuambia kuwa aniambie kune chumba amepata sehemu.


Mume wangu hakujua kuwa nataka kuondoka, alikua safarini Morogoro lakinia liposikia hivyo alipanda gari na kurudi siku hiyo hiyo. Alifika nyumbani na kunikuta nipo tu nasubiria jibu la mdogo wangu, sikutegemea kama anaweza kupata chumba kwa hataka namna ile. Mume wangu alisubiri mpaka usiku ndipo aliniuliza kwanini natafuta chumba, sikumuelewa, nilijifanya sijui chochote, hapo ndipo alianza kunipiga na kuniambia kuwa anhtaaka kumdhalilisha tena kama awali.


“Mimi ni mwanaume, sina kasoro yoyote huwezi kabisa kuniacha, mimi siachwi bali ndiyo naacha!” Alifoka sana huiku akinipiga, alinipiga sana, hakuishia kunipiga kwa ngumi na mateke tu, alinipiga kwa kila kitu kilichokua mbele yake, nilipiga kelele yule Mama akaja kugonga mlango lakini alikua kafunga kwa ndani, aligonga sana lakini haikusiadia, pon a yangu ilikua pale alipoita watu wakaja kuvunja mlango, walinichukua mpaka hospitalini na mume wangu kukamatwa na Polisi. Nilikua nimeumizwa sana, ngeu kila sehemu, mwili umevimba, mimba ilishakua kubwa.


Nilikaa hospitalini kwa siku mbili nikaambiwa mtoto kafia tumboni tena kwa mara ya pili. Alitolewa kwa njia ya upasuaji lakini wakati wakinipasua niliambiwa kuwa kizazi changu kimeharibika sana hivyo kinahitaji kutolewa ili kuokoa maisha yangu. Nilikua katika maumivu makali, sikua na namna zaidi ya kukubaliana nao. Nilijikuta ndani ya siku moja napoteza mtotop pamoja na uwezo wa kupata mtoto mwingine. Nililia sana huku kila mtu akinipa moyo na kuniambia kuwa nishukuru Mungu angalau kashanijalia watoto wawili hivyo sina haja ya kusononeka sana.


Mume wake yuko Polisi, kashapoteza kizazi hivi unafikiri kama atarudi? Je mfano akirudi watakua na amani? Vipi mume wake atajifunza na kubadilika? Lakini vipi asiporudi unadhani maisha yake yatakuaje? Nisikuchoshe fuatilia ukurasa wangu wa


SIMULIZI; AKIKUUA TUTAKUJA KUCHUKUA MAITI YAKO!—SEHEMU YA TANO


“Hata kama amekupiga lakini huwezi kumfunga mume wako, ondoka lakini si kumfunga, ni mume wako wa ndoa na si hawala uliyemuokota okota huko mtaani, hao wanaokushauri kuwa usifute kesi wanakudnaganya, hivi unafikiri kama akifungwa na kuozea jela utapata faida gani?” Mama aliniambia, nilikaa hospitalini kwa wiki moja baada ya kutolewa kizazi, niliporuhusiwa sikurudi nyumbani kwangu, mume wangu alishatoka kwa dhamana lakini bado kesi ilikua inaendelea.


Kwa kuhofia hadhi yake, kwa kuhofia kufungwa kwani mashahidi walikua wengi mume wangu aliniomba sana msamaha, alituma ndugu zake, mshenga na viongozi wa diniili kuniomba msamaha. Walinishauri sana kuachana na kesi yangu kwani hata kama nikishinda sitapata faida yoyote.


“Huna kazi, huna chochote, mume wako akifungwa unafaidika nini? Unajua kuwa akifungwa anapoteza kazi, hivi hufikirii hata wanao kwakweli, unaona kama ni sawa tu kuwa watoto wako hawatasoma kwakua Baba yao kafungwa?”


Mama aliniambia, Baba alikua mkali sana kuhusu mimi kurudi kwa mume wangu na kumsamehe. Wadogo zangu walinisema sana lakini nilimuelewa zaidi Mama, baada ya kupona sikuona sababu ya kuendelea na ile kesi. Mume wangu alibadilika, alianza kunihudumia, alikua ananitumia matumizi, pamoja na kufanya kazi lakini bado alikua akinihudumia na kila siku alikua akiniomba msamaha akiniambia kuwa kajifunza kutokana na makosa hatarudia tena. Kwa miezi miwili alikua ni mtu wa kunipigia simu asubuhi, mchana na jioni, mtu wa kuomba msamaha, hakuwahi kunifokea nha hata nilipokua nikimjibu vibaya basi alikua akiniomba msamaha yeye.


Kuna upendo alikua akiuonyesha mpaka nilianza kumuamini, sikua na sababu tena ya kuendelea na ile kesi, niliifuta na baada ya kama miezi mitatu hivi tulirudiana. Mume wangu alibadilika sana, hakua akinipiga, aliniacha kufanya kazi kwa uhuru, aliahca kunionyesha wanawake zake, kila kitu kilikua kizuri sana. Kwa mwaka mzima niliishi na mume wangu bila kuwa na tatizo lolote, lakini mwaka wa pili baada ya kutolewa kizazi Mama mkwe alianza kuumwa, alikuja nyumbani kwaajili ya matibabu na mimi ndiyo nilikua nikimhudumia.


Sikujua kama ndugu wa mume wangu wana kisasi na mimi na wananichukia mpaka kipindi hiki. Alikuja na wifi yangu ambaye alikua kaolewa ndoa ikamshinda akaachika, alikuja kumuuguza Mama yake. Hapo ndipo maneno yalianza, kumbe bado walikua na hasira za mimi kumpeleka mtoto wao mahabusu, kitendo cha mume wangu kukamatwa na kulala ndani kiliwakera sana. Yalianza maneno ya chini chini, dharau za hapa na pale kila mara Mama mkwe akinitenga, kukataa chakula nilichopika mimi na mambo mengine madogo madogo.


Mimi nilivumilia kwani nilijua kuwa ni mambo ya kupita tu, sikutaka kuyapa kipaumbele hata kwa mume wangu sikulalamika. Lakini baada ya wao kuona kama mimi silalamiki wala sijali walianza kufanya mambo waziwazi. Wakijua kabisa kuwa mimi nimetolewa kizazi na siwezi kupata mtoto tena Mama mkwe alianza kulalamika kuwa anataka mjukuu mwingine, alianza kusema kuwa watoto wawili hawatoshi. Mwanzo alikua akiongea nasikia kwa majirani lakini alipoona sijali alianza kuongea waziwazi akimshurutisha mume wangu kuwa anahitaji mkujuu mwingine.


“Wewe ni Mwanaume unaweza kuoa mwanamke mwingine, huna haja ya kubaki na mtu ambaye hazai!” Siku moja tukiwa mezani Mama mkwe wangua liongea, mume wangu alimtuliza na kumuambia kuwa hayo mambo yashapita yeye hahitaji mtoto mwingine.


“Hata kama hutaki lakini mimi nataka mjukuu, huyu mke wako aliamua mwenyewe kutoa kizazi chake, angekataa unafikiri madaktari wangekitoa, kwanini hakukushirikisha, wakati anatoa kizazi eti wewe uko jela, walitaka kukufunga ili wabaki na mali lakini bado unaendelea kuishi na mwanamke wa namna hii!”


Mama mkwe aliongea, mume wangu alibaki kimya na kumuacha Mama yake kuongea meneno mengi ya kashfa, si Mama yake tu hata mdogo wake aliongea na mume wangu hakujibu chochote. Nilikasirika na kwenda chumbani, niliwaacha wakati wanakula na kwenda chumbani nikaanza kulia. Mume wangu alikaa huko mpaka usiku wa manene ndipo alirudi, alinikuta abdo niko macho nimekaa kitandani nalia, hakunisemesha alipanda kitandani na kulala, nilikaa macho mpaka kesho yake, sikua nikiumizwa na maneno ya Mama mkwe wangu kwani nilishajua kuwa ana hasira na mimi, nilumizwa kwa namna ambayo mume wangu alikaa kimya bila  kuniteta.


Hali ile iliendelea kwa wiki mbili hivi, mume wangu bado alibaki kimya, ni kama alikua anafurahia hiyo hali kwani aliwasikiliza na wakati mwingine kucheka bila kuchangia. Nilivumilia nikashindwa, siku moja usiku baada ya kuwaacha sebuleni wakila niliamua kuuliza.


“Hivi mbona unaacha Mama yako ananitukana namna hiyo?” Nilimuuliza, alijifanya kama hajalewa swali na kutaka kulipotezea lakini nilimbana tena ili aongeee.


“Kwahiyo unataka nini?  Unataka nimjibu Mama yangu na kumkosea heshima unataka niseme nini? Au unataka nimfukuze Mama yangu?” Aliniuliza kwa hasira.


“Hapana, lakini angalau….”


“Angalau nini, hivi unanitaka nini wewe mwanamke, nimekuvumilia mwaka mzima nimebadilika lakini naona hufuraghii, umeanza kisirani chako na nikikupiga kidogo uanenda kutoa mimba sijui na kutoa kizazi, sasa kizazi huna sijui sasa hivi utaenda kutoa utumbo!”


Niliumizwa sana na maneno yake kwani kwa namna alivyokua anaongea ni kama vile alikua ananishutumu mimi kwa kutoka kwa kizazi changu, alikua anaungana na Mama yake.


“Kwahiyo unakubaliana na Mama yako?” Nilimuuliza.


“Ndiyo, kwani Mama kaongea nini kibaya, mbona kila kitu kipo wazi tu, kizazi ulitoa ili ufanye umalaya wako bila kubeba mimba, wanawake wangapi wanapigwa na waume zao lakini hawatoi vizazi!” Mume wangu aliongea hukua kitoka nnje kwa hasira, hakurudi tena, alienda kulala chumba cha wageni, asubuhi aliamka kanuna, hakunisemesha aliingia chumbani akavaa nguo zake na kuondoka.


Nilikua kama mimi ndiyo nimemkosea, mum wangu alibadilika kabisa, hakutaka tena kuongea na mimi, alikua akiwaachia matumizi ndugu zake, akirudi anacheza na watoto lakini mimi hanisemeshi. Niliamua kumchunia kwa muda  lakini nilishindwa, hali ilizidi kuwa mbaya siku hadi siku, hata chakula nilichopika alikua hali. Baada ya kuona vile niliamua kujishusha, niliomba msamaha bila kujua kosa langu ndipo mume wangu aliamua kunisamehe na kurudi chumbani tukaanza kuishi kama zamani ingawa amani bado ilikua haipo kwakua Mama mkwe kila siku alikua akilalamika kuwa hataki kufa kabla ya kupata mjukuu mwingine.


***


Mama mkwe alipata nafuu na kuondoka kurudi kwake lakini mume wangu alibadilika sana, suala la mtoto lilichukua nafasi kubwa sana, alianza kuchepuka waziwazi na kila nilipokua nikiongea alisema kuwa watoto wawili hawatoshi hivyo kama sitaki achepuke basi niondoke na kumpa nafasi ya kuoa mwanamke mwingine. Nilikua katika kipindi kigumu sana katika maisha yangu, bado nilikua na umri mdogo hivyo kila nikiwaza kuondoka kichwa kilikua hakikubali, sio kwamba sikua na kazi au sikua na uwezo wa kuondoka na kuanza maisha yangu mwenyewe, hapana, nilikua na uwezo huo lakini nilikua naogopa.


Kila mara nikiwaza kuishi peke yangu niliogopa zaidi, tayar nilikua sina kizazi hivyo nilifahamu kuwa hakuna mwanaume ambaye angekubali kuishi na mimi halafu nisimpe mtoto. Niliamua kukubaliana na ile hali nikiamini kyuwa kama mume wangu akipata mtoto mwingine nnje basi atabadilika kwani atakua na amani, niliona kuwa kwangu ni bora kubaki na mume wangu ambaye tayari nina watoto wawili naye kuliko kuondoka kutafuta mwanaume mwingine  ambaye naye angetaka watoto na nisingweza kumpa.


Nilivumilia kila kitu mume wangu alichokua akinifanyia kwa imani kuwa anaweza kubadilika, sikua na mtu wa kumuambia matatizo yangu, ndugu zangu walishanichoka, Mama alikua akiniambia kuwa nimedekezwa sana ndiyo maana nalalamika kila siku sijui kuishi kwenye ndoa. Maisha yangu yalikua ya upweke sana, mume  alikua ni mtu wa kurudi asubuhi na akiwahi sana ni saa nane usiku, ukichelewa kufungua au kumpa chakula kilichopoa basi ni kipigo, nilipigwa sana mpaka nikazoea na kuona kama ni sheemu ya maisha ya ndoa.


Siku moja nilipigiwa simu na mwanamke ambaye nilikua simjui, ni binti mdogo tu ambaye ni mwanafunzi wa chuo, alikua akinitukana na kuniambia kuwa yeye ndiyo kaolewa na mume wangu kwania na kizazi na mimi kazi yangu ni kujaza choo tu. Kwakua nilishachoka hata sikumjibu, nilimkatia simu na alipotuma meseji zake wala sikuzisoma nilizifuta, sikumuambia  mume wangu wala kumuuliza chochote. Lakini siku mbili baadaye mume wangu aliwahi kurudi nyumbani, haikua kawaida yake, saa moja na nusu usiku alirudio, mimi ndiyo nilikua nimetoka kazini na kupumzika kidogo hivyo nilikua napika chakula cha usiku.


Alinikuta jikoni niko peke yangu tu, watoto walikua sebuleni. Ile kuingia tu alianza kutukana.


“Naona unanichokonoa, yaani kwakua wewe kizazi chako umetoa unataka kuniulia na wanangu, hutaki nipate mtoto mshenzi mkubwa wewe!” aliongea, mimi sikumuelewa, sikujua anazungumzia nini.


“Nimeshakuamba kuwa nataka kuzaa nnje ya ndoa, sasa nini kumpigia mwanamke wangu na kumuambia kuwa utafanya kila kitu kuhakikisha kuwa hazai! Nikuambie tu hiyo mimba ikitoka nakuua mimi mwenyewe mshenzi mkubwa na uchawi wako!”


Kusema kweli siku nikimuemewa, sikua nikijua anazungumzia nini, sikujua ni mwanamke gani nilimpigia na kumuambia maneno hayo, wala sikua nikijua kuwa kuna mwanamke ana mimba yake. Nilijaribu kumuuliza alikua anamanisha nini lakini ni kama nilimtibua.


“Unanidhihaki, unaniona mimi mjinga eee! Hivi unanichukulieje, yaani kwakua sijakufukuza kwaajili ya watoto ndiyo unataka kunikalia kichwani!” Aliongea huku akianza kunipiga, alinipiga sana huku akiokota kila kitu kilichokua mbele yake pale jikoni na kunipiga nacho, hakuchagua ni kitu gani, kila alichokiokota alikitumia kunipiga.


Alinipiga sana nilijaribu kujitoa kwake kwa kukimbia lakini alinikamata na kunipiga, alipoona sisikii bado napambana alichukua mchi, mtwangio mdogo niliokua nikitumia kutwangua vitunguu swaumu na kunipiga nao sehemu mbalimbali za mwili, nilipiga kelele kuomba smaada, nilikusanya nguvu na kumsukuma ili nitoke akapeepsuka kidogo. Wakati napambana ili kutoka jioni alichukua ule mchi akanirushia ukanipiga kichwani pembeni kidogo ya kisogo, nilidondoka chini na kupoteza fahamu.


SIMULIZI; AKIKUUA TUTAKUJA KUCHUKUA MAITI YAKO!—SEHEMU YA SITA


Nilikuja kushtuka saubuhi, nilikua katika kachumba kadogo hakuna helwa, nilinyanyuka taratibu kwa shida huku nikipapasa papasa mlango, ndani kulikua na giza nene. Nilijua kuwa niko stoo. Nilienda kugonga mlango, niligonga sana lakini sikufunguliwa.


“Nifungulie nakusikia unavyopumua hapo mlangoni.” Nilipiga kelele kwani nilikua nikisikia mtu akipumua mlangoni. Ukimya kidogo ulitanda, nilipiga tena kelele kumuomba anifungulie mlango huku nikitaja jina la binti yetu wa kazi ambaye mume wangu ndiyo alimleta.


“Dada Baba kasema nisikufungulie mpaka arudi anaogopa utaenda tena Polisi.” Aliongea, nilimsihi sana nikimuambia kuwa nipo kwenye maumivu makali na kamwe siwezi tena kwenda Polisi lakini hakujali, hakufungua mlango, nilisogea mmpaka Dirishani nikawa nagonga na kupiga kelele lakini watu hawakusikia, nyumba yetu ilikua ndani ya Geti hivyo hakuna mtu aliyesikia. Baada ya kuona napoteza nguvu niliamua kukaa ili kumsubiri mume wangu arudi na kunifungulia mlango.


Njaa ilikua kali, lakini kwakua ilikua stoo mwanga ulipoingia kidogo nilichukua maji na kunywa, nilikula Nyanya na vitu vingine ambvavyo vilibaki pale stoo. Kila baada ya kama nusu saa Binti wa kazi alikua akija na kuniira, ni kama alikua anataka kujua kama niko hai au la, nilihisi alikua anampelekea taarifa mume wangu ambaye alishaenda kazini. Niliamua kukaa kimya kwani nilijua kama akimuabia mume wangu kuwa siongei angekuja ghafla, kweli ilitokea hivyo, baada ya kutokumjibu kwa kama masaa mawili hivi mume wangu alikuja, alifungua mlango na kunikuta nimelala nimechopka.


Alinibeba mpaka kitandani, alianza kuniomba msamaha na kuniambia kuwa ni shetani alimpitia.


“Yule mwanamke alinichanganya sana, alisema wewe ni mchawi unataka kumuua mtoto wake ndiyo mimi nikapaniki, wewe si unajua mimi nilivyo, nina hasira za karibu, wewe ukanijibu kwa dharau mimi nikakasirika, sikupanga kukuumiza hivi mke wangu nisamehe…”  Aliendelea kulalamika, mimi sikumjibu, nilikua nimechoka na kichwani nilikua na maumivu makali, kuongea ilikua shida lakini nilijitahidi kumuamba.


“Naomba unipeleke hospitali mume wangu, nimeumia sana kichwa, kichwa chote nakiona kizito, nisaidie mume ….”


“Hapana, siwezi kukupeleka, hii ni mara ya pili nakupiga, kama nikikupeleka watadai PF3 kabla ya kukutibu na safari hii nitafungwa. Vumilia mke wangu, chukua dawa hizi, utapona, unaona ninavyokupenda, pamoja na yote hayo lakini bado nakuwaza wewe. nakupenda sana mke wangu lakini wakati mwingine shetani anakua ananitawala mpaka nashindwa kuzuia akili yangu. unaona kazini sikua na amani, nawaza hivi mke wangu akifa hawa watoto nitalea na nani, nimelia sana ofisini, sikua sawa kabsia, ona nimekueltea dawa kunywa mke wangu…”


Aliongea kama mtu vile, alinipa Panadol ili ninywe, sikua na namna zaidi ya kuzichukua, hakuruhusu nitoke na simu zangu alizichukua zote. Kila akitoka alikua akinifungia ndani, na alipoona Panadol hazisaidii alikua akinipa dawa za usingizi. Hivyo kila nikiamka nikilalamika maumivu alikua ananilazimisha kunywa dawa za usingizi nalala. Kwa wiki nzima hali ilikua hivyo, nilikunywa dawa zaa usingizi mpaka huwezi amini usingizi ulikata nikawa silali tena, niliamua tu kupona, pamoja na maumivu makali niliweza kuvumilia na kujifanya nishapona ili aniruhusu kwenda kazini.


Aliniruhusu lakini kwa misamaha mingi ambayo iliambatana na vitisho kama nikiongea.


“Najua uko karibu sana na yule mzee, safari hii ukienda kutangaza matatizo ya familia yetu kwa watu basi mimi nitadili na wewe, utaondoka hapa na hawa watoto hutawaona mpaka unaingia kaburini!” Alinitishia, nilimuahidi kuwa siwezi kuongea kitu chochote hivyo awe na amani kwani najua kuwa nikimuambia mtu nitamkera. Nilienda kazini na kukuta kuwa alishaniombea ruhusa kuwa nimefiwa na Mama yangu mdogo nipo kijijini, nilifika na kushangaa napewa pole nyingi za msiba ambao haukuepo.


Kama kawaida yake, mara nyingi mume wangu akishanipiga na kuniumiza sana basi hubadilika na kuwa mtu mzuri kwa muda kabla kisirani chake hakijajirudia na kuwa na hasira tena. Safari hii hakubadilika sana lakini angalau alikua hanjipigi tena, mwanake wake aliyekua amemuambia kuwa ana mimba yake alimdanganya kuwa imetoka hivyo aliendelea kuhisi labda mimi ndiyo nimemloga hivyo akazidisha kisirani kwangu. maisha yaliendelea, kichwa kilipona na niliendeklea kufanya kazi zangu vizuri tu. Mume wangu aliendelea kuchepuka wazi wazi kwa madai ya kutafuta mtoto lakini hakumpata.


Kila siku alikua akinilaumu mimi kuwa ndiyo namloga, Mama yake ndiyo alizidisha kelele kila siku kunipigia simu kunitukana. Sikua na chakusema, sikua na mtu wa kumuambia matatizo yangu zaidi ya mdogo wangu wa kiume ambaye mara nyingi alipenda kuniuliza. Kila mara alikua akiniambia ni kwanini naendelea kumvumilia mwanaume mshezi kama mume wangu. Sikua na jibu la maana kwani kama ni kazi nilikua nayo tena ya kipato kizuri tu, ningeweza kuondoka na kujitegemea, nikawa na maisha yangu ambayo hayamhusishi yeye kabisa lakini bado sikua na ujasiri wa kuondoka.


Nilikua mpweke sana, najua mtashangaa lakini pamoja na yote hayo bado nilikua nampenda mume wangu na kuna wakati nilikua sioni kabisa kuwa naweza kuwa na furaha nnje ya ndoa. Mume wangu alikua akiniaminisha kuwa mimi sina thamani, alikua akiniambia kila siku kuwa kama akiniacha basi siwezi kupata mwanaume mwingine wa kunivumilia kwani mimi ni mjeuri, sina akili, nina kiburi na sina kizazi hivyo kupata mwanaume mwingine basi itakua shida sana. Niliamini hivyo mpaka kufikia hatua ya kuwa nafanya kila kitu anachokitaka yeye na si ninachotaka mimi.


Pamoja na mume wangu kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha, pamoja  na kuwa na msmahara mkubwa kuliko mimi lakini baada tu ya mimi kuanza kazi na yeye kuona kama nina kipato basi alikua anahakikisha kuwa natumia pes ayangu yote. Yeye alikua akilipa ada ya mtoto, lakini chakula, umeme, maji na kila kitu ilikua mimi. Kila nikimuomba pesa alikua anahakikisha namuelezea namna nilivyontumia pesa zangu zote mpaka senti ya mwisho ndipo hutoa pesa zake. Katika kuwekeza kila kitu kilikua kwa jina lake, nakumbuka kuna kipindi nilikua najikusanya ili kununua Gari.


Nilitaka kununua gari ya milioni 12, nilikusanya mpaka kufikisha milioni 10, mume wangu aliniambia ataniongezea ili ninunue, akachukua pesa akaagiza gari lakini kuja lina jina lake akanikabidhi tu funguo. Sikuongea chochote, nililipokea na kukubali matokeo kwani nilijua kabisa kuwa kama nikiongea basi nitaishia kupigo tu na gari sitapewa. Nilijiona mfungwa na nilijua kuwa siwezi kuwa na furaha katika maisha yangu kama sitakua na mume wangu, hivyo mdogo wangu aliponiuliza niliishia kumuambia tu kuwa “Wewe ni mwanaume huwezi kujua, halafu hujaingia kwenye ndoa,s ubiri uoea ndiyo utajua.”


***


Sikumoja nilikua kazini, sikua nikiumwa wala kujisikia vibaya lakini wakati natembea nilijikuta nadondoka, nilianza kujirusharusha, kwa bahati nzuri kuna Mama mmoja alikuepo pale, akawaambia watu wanishike na kunipanua mdomo, waliangalia kitu cha kuniweka mmdomoni walikosa wakachukua kikatia kucha na kuniwekea. Nilikua nang’ata mdomo kwa nguvu, nilipelekwa hospitalini baada ya vipimo waliniambia kuwa nina Kifafa. Nilishtuka sana kwani katika maisha yangu na katika familia yangu hakukua na historia ya ugonjwa huo.


Waliniuliza maswali mengi ambayo sikua na majibu nayo lakini kwa namna walivyokua wanaongea nilijua tu kuwa tatizo linatokana na mimi kupigwa pigwa na mume wangu hasa kipindi kile aliponigigha kichwani. Niliruhusiwa kuondoka lakini kwa uangalizi maalum, baada ya hapo matukio ya kudondoka yalikua yanazidi, ilikua haipiti hata wiuki mbili kabla sijadondoka kifafa. Kazini kazi zilikua hazifanyiki, nililazimika kuomba likizo ya miezi mitatu kwaajili ya matibabu, lakini bado sikupona nikaomba likizo ya Bila malipo ya  miezi sita.


Mwanzoni mume wangu alikua Bega kwa bega na mimi wakati wa matibabu, lakini baadaye alikua kama kanisusa kwani maneno yalizidi kuwa najidekeza, nimelogwa na nina laana. Nikimuamba yeye ndiyo kasababisha kwa kunipiga alikua akiruka futi mia na vipigo huanza tena. Baada ya kuona hali inakua mbaya, siwezi kukaa na mtoto, siwezi kukaa  peke yangu kwani matukio ya kudondoka yalikua mengi mume wangu alinirudisha nyumbani kwetu ili nikatibiwa.


Nyumbani walijua sababu ya mimi kuwa vile, hapo dipo nilianza kuona kutengwa, kila mtu alikua akinilaumu mimi, akiniambia kuwa ni uzembe wangu na ujinga wa kumvumilia mwanaume kama yule. Mtu pekee ambaye alinifariji alikua ni mama yangu, najua alikua akijisikia vibaya kwani yeye ndiyo alikua chanzo cha mimi kluvumilia manyanyaso. Alinifariji na alikua bega kwa bega na mimi katika kutafuta matibabu, baada ya kuhangaika na dawa za hospitalini ikashindikana basi tulihamia kienyeji na kwenye maombi, mambo yalitulia kidogo lakini si sana.


Nikawa nadondoka lakini si ile mpaka ya kungata ulimu, nilikua nikidondoka nakuwa kama nimepoteza fahamu kidogo kiosha narudia katika hali ya kawaida baada kama ya nusu saa. Baada ya kuona nimepata nafuu kidogo nililazimika kurudi kwa mume wangu ili niweze kurudi kazini. Baadhi ya ndugu zangu walikua hawataki lakini nilishaanza kujiona mzigo, walikua wakiniambia nibaki lakini wakitoka ni manyanyaso, amsengenyo na kuniteta hivyo nikaona bora tu kuondoka.


Mume wangu alinipokea vizuri na kwa kumuangalia alikua anajisikia vibaya, ingawa alikua hakubali ukweli lakini alikua akijishtuia kila mara akiahidi kubadilika na kuniambia kuwa hjatanupiga tena.


“Hata ukiwa vipi mimi sitakuacha, nakupenda sana mke wangu, kuna wakati nakosea na kupendwa na hasira lakini hizo ni hasira tu, haimaanishi kama sikupendi.” Aliniambia maneno ya kunipa moyo, nilijipa moyo labda kabadilika lakini bado nilikua na wasiwasi. Hali ile ilipoa kidogo nikarudi kazini kuendelea na majukumu yangu baada ya likizo ya bila malipo kuisha.


Nilifanya kazi kwa muda wa kama miezi miwili tu hali ile ilianza kujirudia tena. Nilianza kudondoka na hospitalini waliniambia kuwa nipunguze kufanya kazi kwani nikichoka sana ndiyo hali inajirudia. Nilijitahidi kufanya kazi na kuficha lakini ilishindikana. Siku moja Bosi aliniita ofisini na kuniambia kuwa natakwa kupumzika, walinipa barua ya kusimamisha mkataba wangu kwani nilikua siwezi kutimiza majukumu yangu kutokana na hali yangu. Niliumia sana, sikua na chakulalamika kwani tayari walishanibeba snaa.


Nilichukua kilichochangu na kuondoka kurudi nyumbani, nilimuambia mume wangu kilichotokea, alilipokea vizuri na kuniahidi kuwa atanisaidia kunipa mtaji ili nifungue Biashara. Alinipa moyo  na kunifariji sana, maisha yaliendelea nikiwa sina kazi, nikawa mtu wa kukaa nyumbani tu, mawazo mengi nadondoka mara kwa mara kiasi kwamba siwezi tena kukaa mwenyewe, hata kukaa na binti wa kazi ilikua ni shida kwani nikidondoka anashindwa kunishika na kuniwekea kijiko mdomoni ili nising’ate ulimi.


Maisha yalibadilika sana, pamoja na mume wangu kujitahidi kunichangamsha, kujitahidi kunitoa out lakini sikua na furaha, nilikua na huzuni kila wakati nikawa mtu wa kulia tu. Siku moja mume wangu alichelewa kurudi nyumbani, alikuja usiku wa manane akalewa chakari, alishaanza kubadilika hivyo nilishangaa kumuona vile, lakini sikumuuliza kwani nilihofia kipigo. Alibadilika kidogo na kuwa na hasira, alianza kuongea maneno ambayo hayaeleweki, niliona kabisa alikua anatafuta ugomvi.


Nilijua kabisa kama nikimesemesha au kulalamikia chochote basi ningeishia kupigwa, kwasababu hiyo niliamua kunyamaza kimya bila kusema chochote. Lakini alishapanga mambo yake kichwani, aliniambia mwenyewe.


“Mimi nimechoka, hatuwezi kuishi maisha ya namna hii, naona bora uende nyumbani kwenu wakakuhudumie huko, mimi nitakua nikituma tu pesa, lakini siwezi kuendelea kuishi na wewe tena, nimechoka nataka uondoke, kesho kusnaya vitu vyako ondoka usije ukanifia hapa!” Mume wangu aliongea huku akinyanyuka na kutoka nnje, hakusubiri hata jibu langu aliondoka kabisa nyumbani na kuniacha pale nikiwa sielewi chakufanya.


Kuna watu wengi wakisoma hapa wanakua na hasira nas kumuona HiLdA kama vile hana akili kwanini avumilie haya? Nataka nikuulize swa wewe mara ya mwisho ulipopigwa ulifanya nini? Alipokuambia kuwa atabadilika na akakupiga tena ulifanya nini? Kabla ya kumtukana HiLdA basi tafakari hivi lile kofi lingekua ni kitu umepigwa 


SIMULIZI; AKIKUUA TUTAKUJA KUCHUKUA MAITI YAKO!—SEHEMU YA SABA


Mume wangu alikazania sana mimi kuondoka na kurudi nyumbani kwetu, nilimuambia kuhusu watoto akaniambia watoto ni wake na hawezi kunipa mimi watoto kwani ni mlemavu. Sikua na namna, ingawa sikupenda lakini nilirudi nyumbani, walinipokea vizuri kwani safari hii mume wangu ndiyo alimpigia Baba simu kumuambia kuwa kanirudisha nyumbani ili nikapumzike. Nilijua rasmi niemshachika, niliumia sana kwani mabli ya kuwa nilikua nimemzoea mume wangu lakini niliwamiss sana wanangu, niliumia zaidi kwakua sikua na pakukimbilia, sikua na kazi na kutokana na hali yangu nisingeajiriwa popote.


Nilikaa nyumbani kwa miezi sita bila kutoka ndani, nilikua mtu wa kushinda ndani, kulia, mume wangu hakutaka hata niwaone wanwangu akisema kuwa hawatakiwi kuniona katika hali ile4 wataogopa, aliwadanganya tu kuwa nimesafiri. Katika kipindi hicho ndipo ndugu zangu walijua kila kitu mume wangu alichokua ananifanyia, kila mtu alinishangaa ni kwanini nilikua namvumilia mwanaume wa namna ile. Mama aliishia kuniomba msamaha kwania lijilaumu kwa kila kitu, hakusita kuniambia kuwa yeye ndiyo alikua kasababisha kwani hakunisikiliza tangu mwanzo.


Pamoja na kuwa na hasira naye lakini sikua na namna, nililazimika kumsamehe kwani ni mama yangu, hakuna kitu ambacho angekifanya kingenifanya kumchukie, isitoshe kwa wakati huo sikua na namna kwani yeye pekee ndiyo alikua na muda wa kunihudumia. Niliendelea kuhudhuria kiliniki kila wiki kuangalia maendeleo gani, hakuna aliyejua hasa kifafa changu kilisababishwa na nini ingawa madaktari walisema inawezekana vipigo vya mara kwa mara vilisababisha kwani waliona nina mpasuko ambao ulishapona kwenye fuvu, Xray ilionyesha kuvujwa mbavu mbili ambazo zilishaunga hivyo walidhani hiyo ndiyo sababu.


Nilianza kupata nafuu, ingawa nilikua nikidondoka mara kwa mara lakini si kamja zamani, wakati huu nilikua nadondoka tu kawaida, sipotezi fahamu na wala sing’ati ulimi tena. Madaktari aliniambia inawezekana kuwa niemshapona lakini kutokana na msongo wa mawazo, kukaa peke yangu kila siku na kuwa mtu wa kuwaza wanangu basi labda ndiyo maana nadondoka. Walinishauri kuwa nawaona ona wanangu, nilimuomba mume wangu kuwaona lakini alikataa katakata, hali ilizidi kuwa mabya kwani nilikua napata msongo wa mawazo, nashituka na kudondoka mara kwa mara.


Ndugu zangu waliingilia kati, wakaenda ustawi wa jamii mume wangu akaitwa na kulazimishwa kuniruhusu kuona watoto. Kila wiki nilitakiwa kukaa nao siku mbili jumamosi na jumapili. Kweli ilinisaidia ingawa sikuacha kudondoka lakini nilikua amani na furaha zaidi. Baada ya kuona sipati nafuu kama walivyodhani  madaktari walinisihi sana kutoka ndani na kutafuta kitu cha kufanya. Kwakua nilikua siajiriki ndugu zangu walijichanga wakanipa mtaji na kunifungulia duka, nilikua nikikaa dukani pamoja na mfanyakazi, ingawa duka halikua kubwa lakini kutokana na hali yangu basi nilikua nahitaji mtu wa kuwa naye wakati wote ili nisijekudondoka na kujidhuru.


Biashara ilienda vizuri, kutoka kwangu nnje ilikua ni kama kitu kipya kwangu, nilikua kama vile ndiyo naanza kuona watu, mbali na kwenda hospitalini nilikua na zaidi ya miezi nane sijawahi kutoka nnje ya nyumbani. Hali ilianza kuwa nzuri, ile ongea ongea na watja ilikua inanipa nafuu mimi na nilianza kuzoea mazingira, nilitengeneza marafiki na watu walikua wanacheka na mimi bvila kujua nina matatizo nilifarijika sana na kusikia raha kuwa angalau nilikua nakutana na mtu hata mmoja ambaye hayafahamu matatizo yangu.


Nilifanya Biashara kwa miezi sita, ikawa inapanuka vizuri, nilikua ninaifanya kwa nia nzuri na nilikua najiona kabisa nafanikiwa, lengo langu lilikua ni mimi kujikusanga ili nihamie kwangu kwani nilikua na kiwanja nilitaka kujenga ili niwachukue wanangu. Lakini katika kipindi hiki nilipata tatizo jingine, mume wangu alipata ajali ya gari, alivunjika nyonga na kulazwa hospitalini kwa miezi minne. Mimi bado nilikua mke wake, pamoja na kwamba alinirudisha kwetu lakini alikua bado hajanipa talaka, alikua akiishi na mwanamke mwingine lakini baad aya kupata ajali aliondoka na kumuacha, kumbe alikua ni mke wa mtu na mume wake alikua mkoani.


Mume wangu alikua analijua hilo na hakujali, alipopata ajali mwanamke aliondoka hivyo ndugu zake walianza kunitafuta kuwa mimi ni mke wake natakiwa kumhudumia. ndugu zangu wengine walikataa kabisa na kuniambia nimuache apambane na hali yake, lakini Mama alikazania kuwa niende, Baba alikataa ila kwa nguvu aliyokua nayo Mama aliishia kuniambia kuwa nitaamua mwenyewe. Binafsi nilitaka sana kwenda kumhudumia mume wangu, nilikua bado nampenda na moyoni kuna kitu kilikua kinaniambia kuwa labda ajali itambadilisha na kumfanya kuwa mume mwema.


Pamoja na kwamba hata mimi nilikua naumwa lakini nilijiona nina nafuu, mume wangu alikua ni mtu wa kulala tu, kusogezwa, kunyanyuliwa, kuogeshwa, alikua ni wa kujikojolea na kusafishwa. Kazi zote hizo nilizifanya mimi kwa miezi minne, kutokana na kuwa bize na mume wangu baishara nayo ilisimama kwani msichana niliyemuacha aliniibia nakuondoka hivyo nikalazimika kufunga. Mdogo wangu wakiume ambaye alikua ananisaidia kusimamia alisusa na kuniambia hatakai kudili tena na mimi kwani nimeamua kurudi kwa mwanaume mshenzi, yeye aliona kuwa ile ajali ilikua ni malipo na mume wangu alistahili kufa kabisa.


Lakini mimi niliona ajali kama kitu cha kumabadilisha mume wangu, niliona labda ajali itamfanya kuwa mnyenyekevu na kama nikimhudumia vizuri basi atakumbuka wema wangu na kuniona kuwa mimi ni mwanamke sahihi kwake akanirudia. Kweli alinoomba smamaha, kila siku kitandani alikua akilia, alikua akijutia kwani katika miezi hiyo minne ndugu zake ni kama walimtelekeza. Dada zake walikua wakija mara moja moja, ldba Mama yake pekee ndiyo alikua akihangaika na mimi lakini ndugu wengine kila mmoja alikua na maisha yake, ziadi ya kuchanga changa pesa za matibabu hakuna aliyekua anamhudumia kihivyo.


Mama mkwe alijipendekeza kwangu, aliniomba msamaha karibu kila siku, mimi nilishamsamehe kwani nilikua na amani. Sikua nikidondoka tena mara kwa mara, katika miezi minne ya kumhudumia mume wangu nilidondoka mara mbili tu kitu ambcho kilinipa amani na kuhisi nimepona ingawa madaktari waliniamba bado na kuniambia kuwa niendelee hivyo hivyo kuacha kuwaza kwani msongo wa mawazo uanchangia kwa kiasi kikubwa mimi kudondoka. Mume wangu aliruidi nyumbani akiwa anatembea ingawa kwa shida si kama mwanzoni. Aliweza kurejea kazini na maisha yalianza kurudi kama zamani.


Nilipoona kapona nilirudi nyumbani, sikua nataka lakini sikutaka kujipendekeza. Nilitaka mume wangu kujiongeza, kwakua alikua kanifukuza yeye na kuniambia kuwa nirudi nilitaka aje kunichukua yeye. Kweli baada ya kurudi kwetu mume wangu alimuita mchungaji, alikuja na ndugu zake na badhi ya wazee, akaomba smamaha na kushika Bibilia kabisa kuwa hataninaynaysa, hatanipiga tutaishi kwa amani. Ndugu wengine bado waliniambia niachane naye nishikilie biashara yangu lakini Mama alishikilia msimamo kuwa nirudi, Mchungaji na wazee wengine walinisihi kurudi kwa mume wangu na mwisho wa siku nilirudi na kuanza kuishi kama zamani.


Maisha yaliendelea, yalikua na furaha mwanzoni kwani mume wangu alibadilika na kuwa mtu wa kuonyesha upendo. Lakini kadri siku zilivyokua zikienda mume wangu alianza kuwa mpole, mpweke na mtu wa hasira, kitandani alikua hataki nimguse, baada ya kupona tulikaa miezi saba bila kufanya mapenzi na kila nilipomuuliza alikasirika na kuniambia kuwa mimi ni Malaya, yeye abdo hajapona nataka nimuumize, nilivumilia lakini nilikasirishwa na namna alivyokua kaanza kuchepuka, nilianza kuona meseji za wanawake katika simu yake na nilipomuuliza aliishia kunitukana.


Niliumia sana na kutishia kuondoka lakini aliishia kuniomba msamaha ila kuhusu tendo la dnoa alishindwa kabisa. Mara kadhaa alijaribu kufanya mapenzi na mimi lakini uume ilikua hausimami kabisa, alikua ahasisimki, alikua anaweza kuniandaa na kunishika shika kila sehemu lakini hasisimkwi kabisa. Nilianza kupata wasiwasi na kumuuliza kama ana tatizo ila alinigeuzia kibao, alianza kunitukana akiniambia kuwa mimi ndiyo nina tatizo kwani akifanya mapenzi na wanawake wengine anakua sawa, aliongea bila kujali hisia zangu.


Ni kama alikua hajui kama kwa kuniambia hivyo ni kama kakiri kuwa anachepuka. Niliishia kuomba msamaha na kujisafisha mara kwa mara, nilijiona kama mimi sivutii, nikajiona labda kama ni mchafu na kujilaumu sana. Kwakua nilikua nikiona picha za wanawake wengine wakimtumia nilijua mimi ndiyo nina tatizo labda sivutii. Lakini siku moja wakati nakagua vitu vyake nilona dawa flani, nilishtuka nikidhani labda mume wangu kaathirika ni ARV, niliamua kuingia google kuziangalia, nilichokiona hakikunistua sana, zilikua ni dawa za kuongeza nguvu za kiume, nilianza kuwaza kama mimi ndiyo tatizo ni kwani anatumia hizo dawa.


Lakini pia niliwaza kama zinasaidia kwanini hafanyi mapenzi na mimi anafanya na wanawake wengine. Niliumia sana, nilitaka kuvumilia lakini nilishindwa, niliamua kumuuliza ni zile dawa ni za nini na kwanini hazitumii na mimi. Kwanza alishtuka lakini baadaye aliniambia ukweli kuwa baada ya ajali alipoteza nguvu za kiume na kahangaika sana ila hajapata suluhu, aliniambia kuwa anazitumia hizo dawa lakini hazifanyi kazi ndiyo maana hafanyi mapenzi na mimi, aliniomba sana kubaki na yeye na kuniomba nimlindie siri yake kwani watu wakijua haini tena sababu ya kuishi.


SIMULIZI; AKIKUUA TUTAKUJA KUCHUKUA MAITI YAKO!—SEHEMU YA NANE


Nilikua na amani kidogo aliponiambia kuwa ana tatizo la nguvu za kiume, sijui kwanini lakini nilidhani labda atatulia, hatakua akibadilisha wanawake na kwakua mimi najua ana tatizo basi atabadilika na kunipenda mimi peke yangu. lakini haikua hivyo, alizidi kuwa na hasira aliendelea kubadilisha wanawake na kunitukana mara kwa mara kuwa mimi ndiyo tatizo, mimi ndiyo ambaye simsimui kwani akiwa na wanawake wengine anakua kawaida na anakua anawafikisha kileleni.


Nilivumilia kwakua sikua na kazi, ndugu zangu waliokataa mimi kurudi kwa mume wangu walinitenga flani kasoro Mama yangu. mume wangu pamoja na kunifanyia madudu yote hayo, pamoja na kuwa na mahusiano na wanawake wengi wengi lakini bado alikua na wivu sana na mimi. Alikua hataki nitoke ndani, alikua hataki niwe na marafiki,  alikua hataki niwasiliane na ndugu zangu, kwakua tayari walishajua tabia zake hawakua wakimuona malaika kama zamani basia liwachukia na kila alipoona naongea na simu na ndugu zangu basi alikasirika, alitukana akisema kuwa wao ndiyo wananiharibu na wanafanya hivyo ili mimi nimuache.


Nilianza kuwasiliana na ndugu zangu kisirisiri, nilikua naishi kwake kama mfungwa, nikitoka ni lazima kuaga na nikifika huko ni yeye kupiga simu zaidi ya mara kumi. Siku moja nilipigiwa simu kuwa Mama anaumwa, alikua kadondoka chooni na alikua kalazwa hospitalini, ilikua ni saa nane mchana. Nilimpigia simu mume wangu kumuambia hali ya Mama yangu, aliniambia nisubiri anakuja nyumbani kunipeleka Hospitalini, nilisubiri saa nane, tisa, kumi mpaka saa nne usiku mume wangu alikua hajar8udi nyumbani.


Mwanzo alikua akiniambia kuwa yuko bize kazini lakini baadaye nikipiga simu nilikua nikisikia anapokea yuko Baa kwani kunakua na kelele nyingi, nilivumilia nikashindwa, Kaka yangu mmopja mtoto wa Mama mkubwa alinipigia simu na kuniambia kuwa hali ya Mama ni mbaya na kama sina usafri amtume mdogo wangu kuja kunichukua. Nilimuambia naenda lakini mpaka saa nane usiku mume wangu alikua hajarudi, alirudi saa tsa usiku tena akiwa kalewa chakari. Nilimuambia kuhusu Mama akaishia kunitukana na kuongea maneno ya kuudhi.


“Kwani wewe ni saktari, kama ni mtu wa kufa atakufa tu, hawezi kupona kwakua tu umeenda, kwanza Mama yako mwenyewe kashazeeka, unafikiri atapona kweli muacha afe kwa amani si kwenda kumlalamikia lalamikia!” Aliongea kwa dharau akiwa kalewa, kweli niliumia, nilichukua simu na kumpigia Kaka yangu, nilimuomba kuja kunichukua usiku uleule. Mume wangu kusikia kuwa nimewapigia simu ndugu zangu alikuja juu, alikasirika na kusema kuwa nimemdharau namuona yeye si mwanaume an kuongea maneno mengi mengi ya ajabu ajabu.


Lakini mimi nilishakasirika, nilikua naudhina na vimaneno maneno vyake vya kila saa, sikutaka kuendelea kumsikiliza kwani nilijua tutagombana, nilinyamaza tu kimya na kumuaacha abwabwaje mpaka achoke, alipoona simjibu alifunga mpango, akachukua funguo na kuniambia kuwa siondoki mule ndani hata kama ndugu zangu wakija. Tulianza kugombania funguo ndipo mume wangu alianza kunipiga, alinipiga sana nikawa napiga kelele, wakati huo kaka zangu walikua washafika, walikua nnje ya geti wakigonga. Baada ya kusikia kelele kwakua Geti lilikua limefungwa waliligonga na gari likafunguka, nilikua nikipiga kelele sana hasa baada ya kusikia Honi nnje nikajua ni ndugu zangu.


Kwakua walikua wanafahamu mambo ambayo mume wangu alinifanyia huko awali hawakutaka kusubiri. Walivunja geti la nnje na kuingie kisha wakaja na kuvunja mlango wa ndani. Aliingia, alikua Kaka yangu mkubwa wa Mama mkubwa, mdogo wangu wa kiume na Dada yangu wa Mama mdogo. Nilikua chini damu zinanitoka mume wangu  bado anaendelea kunipiga. Mdogo wangu wa kiume kuona vile alimvamia mume wangu na kuanza kumpige, yeye ana hasira sana, alimtandika sana mume wangu mpaka Kaka mkubwa alipomshika na kumuambia amuache.


Ulikua ugomvi mkubwa, hakutaka kumuacha alitaka kuendelea kumpiga na ndipo dada yangu alimuambia.


“Muache, acha kuendeleza haya mambo, Mama yako ndiyo amekufa na nyie mnaanza kugombana…”Dada aliongea huku akimsihi mdogo wangu kutulia. Kwa kauli yake ndipo niligundua kuwa kumbe Mama yangu alikua amekwisha kufa, niliuliza mara mbili, kumbwa walishajua muda lakini hawakutaka kuniambia, mume wangu kusikia vile ndipo alishtuka, pombe zikamuishia na kuanza kuaniomba mimi msamaha akidai alikua hajui chochote.


Hakuna mtu ambaye alimsikiliza, mdogo wangu alitaka tumpeleke polisi lakini Kaka yangu alisema haitasiadia, waliniambia niwachukue watoto tuondoke zetu. Tuliondoka usiku uleule mpaka nyumbani, Mama alifariki kwenye saa nane usiku, ikimaanisha kuwa kama ningewahi na kwenda kumuona ningemkuta Mama yangu akiwa hai. Niliumia sana kutokana na kifo cha Mama yangu, nililia sana, nilimlaumu mume wangu kwa kila kitu, aliniomba sana msamaha lakini sikua tayari kumsamehe, nilikua na hasira nyingi sana, hata kwenye mazishi nilishindwa klwani kila dakika nilikua ni mtu wa kuzimia.


Ndugu wa mume wangu walikuja, sikuweza hata kuonana nao kutokana na hasira nilizokua nazo juu yao, mume wangu naye bila aibu alikuja na alitaka kuonana na mimi lakini watu walimkataza. Baada ya mazishi niliendelea kubaki nyumbani, mume wangu alituma wazee kuja kuniomba msamaha lakini Baba yangu na ndugu zangu wengine walikataa katakata. Nilikataa na waliniambia sitakiwi kuendelea kuishi na mume wangu, aliondoka na kuendelea kunitumia meseji kila siku akisema kuwa kabadilika na kajifunza lakini sikumuamini.


Nilifunguliwa tena duka na ndugu zangu, nikawa nafanya Biashara nakaa nyumbani, mume wangu tulikua tukiwasiliana tu kuhusu watoto, mimi ndiyo nilikua naishi naye na alikua akihudumia tena vizuri sana. Alikua akituma pesa nyingi sana kuliko hata mahitaji yote hiyo kunionyesha kama amebadilika. Pale nyumbani wadogo zangu walikua chuo na wengine wana maisha yao, muda mwingi nilikua mwenyewe na wanangu pamoja  na Dada wa kazi, Baba alikua bize na mabo yake, alikua ni mtu wa kusafiri safari tu, pamoja na kupata kila kitu lakini nilikua mpweke sana.


Sikua na marafiki, sikua na mtu wa kuongea naye zaidi ya mume wangu ambaye mara kwa mara alikua ananipigia simu tunaongea hata masaa mawili. Yeye ndiyo alikua ananiondopelea upweke na kweli kila nikiongea naye nilimuona kama kabadilika, baada ya kukaa miezi kama nane hivi niliona nibora kumpa mume wangu nafasi nyingine. Nilimuona kabisa kuwa kabadilika, niliwaambia ndugu zangu kuwa narudiana na mume wangu lakini hawakutaka, walikataa ila niliona kuwa kila mtu ana maisha yake, niliona wao wanafuraha na mimi sina furaha na njia pekee ya kuwa na furaha ni kwakurudiana na mume wangu.


Nililazimisha kuondoka nikarudi kwa mume wangu ndipo siku moja mdogo wangu aliniambia “Nimaisha yako, rudi, umeamua hivyo lakini usije kutusumbua tena, siku akikuua sisi tutakuja kuchukua maiti yako!” Ndugu zangu wote walionekana kukerwa na maamuzi yangu, hakuna mtu hata mmoja ambaye aliniunga mkono, si Baba, Shangazi wala jirani. Niliumia sana na kumkumbuka sana Mama yangu kwani nilijua wakati kama huo yeye ndiyo anakua upande wangu. lakini nilijipa moto kuwa mume wangu atakua kabadilika, ataka kajifunza na hawezi kuninyanyasa tena.


Maisha yalikua mazuri kwa muda mfupi tu, lakini bado mume wangu alikua na tatizo la nguvu za kiume hivyo kisirani chake kilirudi palepale, kwakua alikua anajua sipatani na ndugu zangu hata simu zangu hawapokei absi alizidi kuninyanyasa,a liifunga tyena Biashara yangu nikawa mtu wa kikaa nyumbani tu. Nilikua nimekata tamaa kabisa ya maisha nikijiaminisha kuwa laba ipo sikua tabadilika. Lakini niliposoma kisa cha David hapa kwa Kaka idi ndipo niligundua kuwa mume wangu hatabadilika na naweza kuondoka hapa nikiwa mati.


Bado niko kwa mume wangu, sijui cha kufanya, manyanyaso ya kila siku yamezidi, hanipigi kwa sasa lakini kila siku ni matusi na kejeli, kubadilisha wanawake ni kama kawaid ain gawa sijui kama anafanya nini nao wakati kwangu hakuna kitu. natamani kutoka katika hii ndoa lakini sina uajsiri, nimesoma Post nyingi zako Kaka naomba unipe ujasiri, naomba unisaidie ni kitu gani chakufanya kwani ndugu wamenitenga hawataki kunisikia kwani hata nikisema naondoka hawaniamini tena. Napitia comment za watu najiona kama mjinga ila sijui nifanye nini kwani kwa sasa sina kazi na hakuna ndugu wakunisaidia tena, naomba nisaidie kaka nifanye nini naona kama maisha yangu yamesimama.


****MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG