Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

MIMI, ANGEL, MAMA MKWE NA MUME WANGU KATIKATI!

  

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

IMULIZI; MIMI, ANGEL, MAMA MKWE NA MUME WANGU KATIKATI!


Nilishindwa kulala, tangu kupata habari kuwa Mama mkwe wangu alikua anakuja kichwa kilikua kinaniuma, nilikua kama mtu aliyepewa habari mbaya za msiba.


JOIN US ON TELEGRAM

“Umesema anakuja saa ngapi?” Nilimuuliza mume wangu, ndiyo kwanza alikua anajaribu kulala baada ya kumsumbua sumbua na maswali yangu hapo kabla.


“Wewe mwanamke una nini? Yaani tusilale, hembu lala huko…”


“Nilitaka tu kujua ili niweze kujiandaa, anakaa siku ngapi?” Mume wangu alinijibu kwa hasira, nilijitahidi kunyamaza lakini nilishindwa, bila kujua nilijikuta nauliza tena.


“Sasa mimi nitajuaje? Mama kaniambia kuwa anakuja, nitamuuliza kama anakaa siku ngapi? Mtu hata kabla hajafika nianze kumuuliza kuhusu siku za kukaa, ni akili kwelu hizo? Halafu ni Mama yangu unajua!” Hapa mume wangu aliongea kwa sauti ya juu kidogo, alionyesha kukasirika lakini hata sikujali, kichwa changu hakikua sawa kabisa.


Nilinyamaza kwa muda na kujaribu kutafuta usingizi, nilijua mume wangu hakua na majibu ya maswali yangu lakini ilikua nilazima niulize.


“Anakuja kufanya nini?” Sikua nimepanga kuliuliza hilo swali, kwangu ni kama nilikua naliwaza kichwani kwangu lakini kwa bahati mbaya likaniponyoka mdomoni na mume wangu akasikia. Hapa alinyanyuka kwa hasira zaidi, aliwasha taa, wote tulianza kufikicha macho kutokana na mwanga mkali wa ghafla.


“Hivi una nini wewe mwanamke? Hivi kama angekua anakuja Mama yako ungekua na maswali mengi kama hayo? Au mimi ndiyo Mama yako aje hapa nianze kukuulizia kuhusu anachokuja kukifanya ungenielewaje?”


Nilitulia kidogo, “Kweli nisingejisikia vizuri, lakini ile hiyo ni tofauti, Mama yako ni tofauti…” Nilijikuta naropoka tena bila hata kujijua, nikijua labda natengeneza mambo kumbe nilikua naharibu.


Mume wangu alikasirika zaidi. “Tofauti gani? Kwahiyo unamuona Mama yako ndiyo wa maana kuliko wangu? Au unamuona Mama yangu ana matatizo? Kweli nimeamini humpendi, kila siku ananiambia lakini simsikilizi ila leo nimeamini! Hapa nimekuambia anakuja tu, hata kufika hajafika hivi kama akija utaweza kuishi naye kweli?” Aliongea maneno ambayo yalinifanya kunyamaza kabisa bila kuongea chochote.


Kichwani nilijua kama nikiendelea kuongea nitazidi kuliharibu. Niligeuka upende wapili bila kusubiri taa kuzimwa nilifunga macho, mume wangu alikaa kimya kwa muda kisha akalala bila kusema chochote. Hata taa hakuzima alionekana kukasirika, kwa hasira namimi sikuzima taa, hivyo tukabaki hivyo hivyo. Asubuhi tuliamka vizuri, mume wangu si mtu wakuweka vitu kcihwani, alishasahau hivyo aliamka na kunichangamkia kama kawaida.


Mimi ndiyo bado nilikua na kisirani ingawa nilijaribu kukizuia. Siku hiyo nilikua siendi kazini, nilikua likizo hivyo nilibaki tu nyumbani. “Sijui kama nitapata muda leo, kuna kikao na Madiwani sijui kitaisha saa ngapi? Kama nitachelewa basi utaenda kumpokea Mama Ubungo.” Niliitikia kumkubalia, nililazimisha tabasamu, sikutaka aone kuwa bado siko sawa kuhusiana na Mama yake kuja nyumbani kututembelea.


***


Kwa kawaida mume wangu anapokua na vikao ofisini kwao huwa anachelewa sana kutoka, hivyo nilijiandaa kwenda kumchukua Mama kwani sikutaka kuchelewa. Tatizo nikuwa kila mara nilipokua nikimpigia ili kumuuliza wamefika wapi lakini wala hakupokea simu zangu, hata nilipomtumia meseji hakujibu, nilitamani kumpigia simu mume wangu kumuambia aongee na Mama yake lakini nilijua italeta ugomvi.


Sikua na namna niliamua kupanda gari ili kwenda Ubungo, nilijua kama akifika nilazima atampigia simu mume wangu hivyo mume wangu kunipigia simu mimi. Niliingia kwenye gari na kwenda Ubungo, asubuhi mume wangu aliongea na Mama yake hivyo nilijua anapanda gari gani, nilijua muda waliokua wanafika Ubungo. Nilifika na kuongea na watu wa booking wa lile gari wakaniambia bado hawajafika, waliniambia lilishapita Chalinze, nilitafuta sehemu na kukaa kuwasubiri.


Bado niliendelea kumtumia meseji Mama mkwe kumuulizia kafika wapi lakini hakunijibu, sikujali sana. Nikiwa nimekaa pale niliona Gari linaingia, nilimuona Mama mkwe wangu akishuka na mabegi yake, sikua na haraka nilitaka kumuangalia kama atanitafuta au la. Kama nilivyotarajia hakunitafuta, alimpigia simu mume wangu moja kwa moja na kumuambia kuwa alikua akinitafuta kwenye simu sipatikani.


Alilalamika sana kuwa kaachwa Ubungo peke yake. Mume wangu alinipigia nikamuambia niko Ubungo na gari nimeiona. “Ndiyo namfuata hapa namuona alikua anaongea nawewe…” Nilimuambia na kwenda kumsalimia Mama mkwe wangu. Aliniitikia vizuri tu na kujifanya kuwa simu yake ilikua na matatizo kila akipokea hanisikii, nilicheka tu kimoyomoyo na kutaka kumuambia “Kama ilikua na matatizo mwanao umeongea naye na nini?” Lakini haikua na maana, nilimpa pole na kumuambia tutamtafutia nyingine kisha nikamsadia kupandisha mabegi kwenye gari.


“Mbona unamucha mdogo wako? Angela, msalimie Dada yako.” Aliongea huku akimgeukia binti mmoja aliyekua amesimama mbele yetu. Alikua ni binti mrembo si mtoto hapana alikua mtu mzima hivi miaka kama 23 au 24 hivi. Alikua amevalia suruali ya jeans ya kubana, akivaa Crop top flani hivi ambayo kama asingefunga kisueta kiunoni basi angeacha kitovu wazi. Muda wote wakati sisi tunahangaika na mabegi yeye alikua bize na simu yake huku earphone zikiwa masikio.


Baada ya kuambiwa vile alitoa earphone masikioni na kunisalimia kwa kunishika mkono, alishuka chini kidogo kama anaonyesha heshima. Niliitikia ingawa kiuhalisia sikuona kama ana haja ya kunizalimisha, ni kama tulikua tumelingana flani, kweli nilimzidi lakini si kihivyo. Wakati huo ndiyo kwanza nilikua nimetimiza miaka thelahini. Lakini kwakua aliambiwa anisalimie basi sikutaka kubishana sana.


Nilimfungulia mlango wa mbele Mama ili akae, lakini alikataa akisema yeye hataki kukaa mbele. “Muache mdogo wako akae, alijue jiji, Angela (alimuita kwa lafudhi ya Kichaga) Hapa ndiyo Darisalama!” Alimuambia, binti aliingia kwenye gari, kabla hata sijamuambia kitu alifunga mlango wa gari, akafunga mkanda kisha kuendelea kuwa bize na simu yake. Mama mkwe aliingia na safari ikaanza.


Sikua na haraka sana ya kujua kama yule ni nani “Tunaenda nyumbani tu nitajua…” Nilijisemea kichwani kwangu. Tofauti na kawaida yake siku ile Mama mkwe wangu alikua amechangamka sana. Najua bado mnajiuliza nini kilitokea mpaka nilikua nawaza mara mbili mbili kumpokea Mama mkwe wangu. Labda nisema tu kuwa haikua hivyo nilipoolewa. Kipindi hicho nilikua mdogo, miaka 25 ndiyo nimemaliza chuo hata ajira bado nilikua sijapata.


Lakini kwakua nilikua napendana sana na mume wangu kipindi hicho akiwa mchumba basi tulioana, mambo yalikua mazuri nikapata kazi. Mambo yalikuja kubadilika baada ya mwaka kuishi bila mimi kupata mtoto. Alianza kumsisitizia mume wangu kuwa anataka mjukuu, mume wangu ni wakwanza kwao kuoa, ingawa si wakwanza kuzaliwa lakini Kaka zake wawili walikua bado hawajaoa kipindi hicho hivyo mjukuu pekee alitakiwa kutoka kwangu.


Mwanzo mimi na mume wangu hatukua na presha hivyo hatukuhangaika, lakini baada ya miaka miwili ya ndoa bila mtoto nilianza kuhangaika. Kwanza niliambiwa kizazi changu kiko mbali hivyo ili kupata ujauzito nilazima kivutwe, kilivutwa na kuvutwa lakini mwaka watatu ulipita bila mimba wala mtoto. Niakaambiwa mayai yangu hayapevuki vizuri, nikapewa Dawa lakini wapi, nilihangaika na kuhangaika lakini bado sikupata mtoto mpaka nafikisha miaka mitano ya ndoa sikua na mtoto.


Kaka zake walioa na kupata watoto, hata mdogo wao wamwisho wakiume naye alioa na kuapata watoto lakini si sisi. Mume wangu yeye hakua na shida, ni mkimya na kila mara Mama yake akilalamika husikiliza weee bila kujibu chochote, hata nikitukanwa nakuambiwa vipi hajibu baadaye huishia kuniambia “Kwani wanakupiga, si maneno tu, mimi si nakupenda unashida gani?


Yeye aliona kawaid tu lakini mimi nilikua naumia sana, maneno ya mawifi zangu, Mama mkwe wangu na kila mtu, hata majirani, nilikua siwezi kwenda Moshi hata kwenye msiba kwani kila nikienda ni manyanyaso tu na watu kunisema mimi na mume wangu. Yeye alikua hajali na mara kadhaa alikua akinishangaa kwanini naumizwa na maneno ya watu.


Mara nyingi Mama yake alishanitamkia kuwa hawanitaki na kusema mimi ndiyo namloga mwanae asipate mtoto na matusi mengi mengi. Ndiyo maana kila nikimuona Mama mkwe wangu nachanganyikiwa kwani naona amani inaelekea kupotea nyumbani kwangu. Nilikua naumia kwakua nilijua fika hanitaki na alishanifanyia vituko vingi, alishaniita mchawi na mara kadhaa alishaniwekea vitu vingi vya kishirikina ili niondoke lakini siku zote mume wangu aliniambia nisipaniki yeye ndiyo kanioa.


***


Nyumbani mume wangu alirudi usiku sana, nilishawakaaribisha wageni na kupika chakula cha usiku. Alisalimiana na Mama yake na kuongea vizuri tu, mpaka wakati huo Mama mkwe alikua bado hajaaanza kuonyesha mbwembwe zao, sikutaka kujisahau kwani namjua tabia zake. Baada ya chakula cha usiku wote tulienda kulala, nilitaka Angel kulala chumba cha wageni na Mama lakini Mama mkwe alikataa na kuniambia nyumba kubwa nimpe chumba chake.


Sikujali nilimuandalia chumba kingine, mpaka wakati huo bado nilikua sijatambulishwa ni nani na alikuja kufuata nini pale. Sasa nilikua na shauku ya kujua, nilitaka kumuuliza mume wangu lakini alikua kachoka sana, sikutaka tugombane hivyo nilipenda kitandani na kulala. Asubuhi kama kawaida yangu huwa naamka saa kumi na moja za alfajiri. Hata kama siendi kazini lakini nafanya hivyo ili kumuandalia mume wangu chai kwani kutokana na foleni saa hutakiwa kuondoka saa kumi na mbili kasoro ili kuwahi ofisini.


Niliamka na kukuta chai iko mezani tayari, nilishangaa kwani usiku niliondoa vyombo vyote. Nilienda mpaka jikoni na kumkuta yule binti. Alikua akipika chapati tena za kusukuma, alinisalimia, niliitikia kwa msahangao. “Unafanya nini asubuhi yote hii?” Nilimuuliza kwa hasira kidogo, alikua jikoni kwangu akipika bila idhini yangu hata haikuingia akilini. “Ohhh! Dada Mama aliniambia kuwa Baba anapenda Chapati za moto hivyo nikaamua niamke mapema kumpikia…”


Alijiongelesha, kusema kweli sikumuelewa. “Baba? Baba Gani?” Nilimuuliza kwa hasira zaidi, alikaa kimya bila kusema chochote, nilizidi kukasirika nikiona kabisa ilikua dharau. Kwanza kwa namna alivyokua amevaa ni kama alikua kashafika, alifunga khanga mbili, moja kifuani ya pili akaifunga kiunoni, lakini ilikua fupi kiasi kwamba akikaa au kutembea iliacha mapaja wazi, alizidi kunichefua.


“Wewe kwanza ni nani? Mbona mimi siwaelewi?” Nilimuuliza kwa hasira.


“Mimi natoka Kijijini, ndiyo nimemaliza chuo nikawa sina kazi, Bibi akaniambia nija huku mjini kufanya kazi za ndani?” Nilizidi kushikwa na hasira, nilitamani kumrukia kumpiga makofi, nilikua na maswali mengi lakini sikua na majibu.


“Chuo gani, natoka lini mwanafunzi wa chuo akafanya kazi za ndani?” Niliukiza kwa hasira, mimi nilipaniki lakini cha ajabu yeye alitulia tuli hakuonekana kupaniki kabisa.


“Nimesoma Uhasibu Arusha…” Alizidi kunichanganya sikujua hata anasema nini, sikutaka kuendelea kumsikiliza. Nilienda mpaka chumbani na kumuamsha mume wangu, kwa kawaida ni mzito kuamka asubuhi mpaka mimi nimuamshe lakini siku hiyo ni kama nilimnyanyua. Nilimshika mkono akiwa na usingizi wake uleule na kumvuruta mpaka jikoni. Yule binti alikua kakaa vilevile mbado anapika chapati, wala hakujali kupaniki kwangu, mume wangua lipokuja alimsalimia.


“Shikamoo Baba!” Nilimkata jicho mume wangu kiasi kwamba akashindwa hata kujibu.


“Baba! Baba! Gani, huyu ni nani na anafanya nini jikoni kwangu.” Niliuliza kishari shari.


“Mimi sijui, lakini juzi wakati naongea na Mama aliniamba ataniletea binti wa kazi, sasa sijui, nikajua alivyokuja mmetambulishana.” Mume wangu aliongea kwa utaratibu, moja ya vitu nilivyokua nikimchukia mume wangu nikua alikua si mtu wa kukasirika au kuchukulia mambo siriasi, kwake kila kitu alikua akikichukulia rahisi tu.


“Mfanyakazi! Hivi kweli ukimuangalia huyu ni mfanyakazi wa ndani, mtu kamaliza mpaka chuo kikuu unasema mfanyakazi!?” Niliuliza kwa hasira, mume wangu alijaribu kunituliza, alimgeukia yule binti na kumuuliza yeye ni nani ndipo alijitambulisha kama Angel na kweli alikua kaletwa pale ili kufanya kazi za ndani! “Umaona sasa ulikua unapaniki bure, huyu ni binti kaletwa kutusaidia kazi za ndani.” Mume wangu aliongea huku akitoka pale jikoni kuelekea chumbani.


ITAENDELEA…


SIMULIZI; MIMI, ANGEL, MAMA MKWE NA MUME WANGU KATIKATI—SEHEMU YA PILI


(ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA; Mama mkwe wangu ananiletea binti ambaye amemaliza chuo kikuu mzuri kuliko hata mimi. Naamka asubuhi namkuta yule binti anampikia mume wangu chapatti, namuamsha mume wangua naniamba atakua ni mfanyakazi wa ndani na haonyeshi hata kujali. ENDELEA… Kama hukusoma sehemu ya nwanza basi bonyeza hapa Iddi Makengo )


Nilikua namuangalia mume wangu kama atainywa ile chai, baada ya kuondoka na kuniacha jikoni aliingia chumbani kujiandaa. Nilimfuata huko huko na kuendelea kulalamika kuhusiana na yule binti.


“Kama ni mfanyakazi wa ndani mimi simtaki kabisa hapa!” Niliongea huku nikimchagulia nguo za kuvaa.


“Kwani kuna tatizo gani mbona wewe unapaniki sana?”


“Napaniki, hivi wewe hujamuona huyo binti kweli inaweza kuingia akilini kuwa ni binti wa kazi? Kwa shida gani aliyonayo?”


“Inawezekana lakini, si unajua siku hizi ajira ngumu. Isitoshe huna haja ya kuwa na wasiwasi, mimi naona tungesubiri Mama aongee aseme kama ni mfanyakazi au ni binti kaja naye tu! Kwani kuna kazi gani humu ndani za kuhitaji mfanyakazi?”


Aliongea kitu ambacho kilinipa matumaini kuwa hayupo ukurasa mmoja na Mama yake.


“Kwani wewe unahitaji msaidizi?”


“Hapana, msaidizi wa kazi gani? Mimi nyumba yangu naimudu…” Nilijibu kwa furaha.


“Ngoja tuone Mama atasemaje.” Aliongea huku akinibusu usoni, nilichukua begi lake mpaka kwenye gari. Hakunywa ile chai, Mama yake alishaamka hivyo alimsalimia, alimuambia kuhusu chai akasema atakunywa kazini kuna kazi nyingi hivyo anawahi. Nilifurahi kimoyo moyo kwani ni kama alikua kawakomesha.


Mama alimuangalia wakati anaondoka, aliniangalia na mimi na kurudi jikoni, yule binti alikua anasafisha jiko.


“Huyu si ndiyo mwanamke sasa…” Mama aliongea, nilijua anataka kuniudhi lakini sikutia neno. Nilitaka kumuonyesha mwisho wake.


“Umemka saa ngapi mwanangu?” Mama alimuuliza Angel.


“Saa kumi Mama, lakini hata sijachoka, mbona nishazoea kazi naiweza.” Aliongea kinafiki, nilijua wanataka niwaulize kitu lakini sikufanya hivyo. Sikutaka hata kujua kuwa yule ni nani, niliwaacha na kwenda zangu chumbani.


Dakika kama kumi hivi Mama mkwe wangu alikuja kunigongea mlango. “Mwanangu nina mzungumzo kidogo na wewe…” Aliongea baada ya mimi kutoka, sikuona kama ni heshima yeye kuingia katika chumba cha mwanae.


“Kuna mdogo wako hapa kuwasaidia, najua wote niwafanyakazi hivyo mnachoka hivyo huyu binti atakua anawasaidia kazi za ndani.” Aliongea kama vile ananipa taarifa, ilikua ni kama kitu kishaamuliwa.


Nilishtuka kidogo na kumuambia kuwa sisi hatuhitaji mfanyakazi, kazi zote ninazimudu hivyo kama alikuja kwaajili hiyo basi arudi alipotoka.


“Kama ungekua unazimudu mume wako asingekua analalamika kila siku. Yeye ndiyo kaniambia unahitaji mtu wa kukusiadia, sasa utaongea na mume wako lakini mimi siwezi kumrudisha binti wa watu kujijini wakati nishamleta huku!” Aliongea kwa kujiamini, kwa namna alivyokua akiongea nilijua fika hajaongea na mume wangu.


Lakini pia nilikua namfahamu mume wangu, nilikua nafahamu kuwa kama Mama yake akimsisitizia kitu basi atakubali bila hata kufikiria mata mbili. Mume wangu ni wale watu ambao hawawezi kusema hapana, anakubaliana na kila kitu. Mama yake anajua hilo hivyo alijua hata kama akimuambia basi atakubaliana naye. Tulibishana na Mama mwisho nikaona kama haitasaidia kitu, alishaamua hivyo mtu wa kumuwahi alikua ni mume wangu.


Sikutaka kusubiri mpaka jioni, niliamua kwenda kumfuata mume wangu ofisini, niliingia kwenye gari bila kuaga na kwenda ofisini kwake. Hakua na wageni wengi siku hiyo na kwakua nafahamika basi niliruhusiwa kuingia. Nilifika na kuanza kumuelezea maneno ambayo Mama aliyaongea, lakini ni kama alikua ananisubiria, ile naondoka tu Mama yake alimpigia simu na kumuambia kila kitu.


“Ndiyo nimetoka kuongea na Mama, alikua ananiambia mmekwaruzana! Hivi kwanini hamuwezi kuishi kwa amani, unajua nyie ndiyo wanawake wawili ambao nawapenda kuliko kitu chochote kile, sasa kama mtagombana unafikiri mnaniweka katika hali gani?” Alikua njiapanda kweli lakini nilijua kama mimi nitalegeza kamba basi yule binti atakaa pale na nina hakika mume wangu atachepuka naye na ndiyo utakua mwisho wa ndoa.


Nilimueleza wasiwasi wangu. “Tatizo wewe unachukulia kila kitu kirahisi, mimi sina mtoto na Mama anataka mjukuu hivyo yule kaletwa ni mke wako…”


“Hivi unaniona mimi mjinga kiasi hicho, unaona mimi ndiyo wakutembe ana yule mtoto, hata kama kaletwa kwajaili hiyo lakini haimaanishi kuwa nitatembea naye, au hiyo mimba atapata kwa kupika Chapati?” Nilijaribu kumuelewesha mume wangu lakini wapi, alishafanya maamuzi yake na kusema yule binti atakaa pale.


“Mama mwenyewe anaondoka kesho kutwa, kwanini huyu binti asikae hapa Mama akiondoka nitamtafutia kazi kwingine wote mtakua na amani sidhani kama huyo binti ni mjinga kiasi hicho kudhani kuwa nitakuja kutemeba naye, naamini ana maisha yake.” Niliona kabisa kashakubaliana na Mama yake, nilitoka kwa hasira na kumuacha bado akiongea, nilianza kutembea harakaharaka kwenda nnje kwa hasira nilizokua nazo sikutaka kuendelea kubaki pale.


“Mage… Magreth… mbona haraka hivyo!” Sauti ya kiume ilisikika nyuma yangu. Niligeuka na kuzidi kupata hasira, alikua ni Victor mmoja wa marafiki wa mume wangu, hakua rafiki yake kihivyo lakini walikua wakifanya kazi pamoja na nilikutana naye katika sherehe moja ya ofisini kwao. Kwa kumuangalia tu alionekana kuwa na tabia za ajabu ajabu, siku tuliyokutana alinitongoza tukiwa meza moja na mume wangu.


“Mimi shemeji yako Please niheshimu!” Nilimuambia kwa hasira huku nikigeuka na kuendelea na safari yangu. Hakusema neno aliniacha nikaondoka, niliingia kwenye gari na kuondoka maeneo yale. “Umependeza kama kawaida yako, nimefurahi kukuona, najua hutajibu hii SMS lakini unaonekana una hasira, ungeweza kunipigia na kunitukana tu nina uhakika hasira zako zingepungua, sura nzuri kama hiyo haitakiwi kukunjwa kabisa.”


Alinitumia meseji, niliisoma nakujikuta nacheka, kwa kawaida meseji zake ni za namna hiyo. Niliifuta na kuendelea na safari yangu. Nilirudi nyumbani na kumkuta yule binti akifua nguo tena za mume wangu. Sijui alipata wapi funguo kwani nilifunga mpango wakati anaondoka.


“Anafanya kazi eee!” Mama mkwe alijiongelesha baada ya kuniona, nilimuangalia nikitamani hata kumnasa makofi lakini nililazimisha tabasamu.


“Ndiyo lakini hapa kwangu hatakaa simhitaji, kama unahitaji mfanyakazi mchukue wewe!” Niliongea kwa hasira kisha nikaondoka bila hata kusubiri jibu lake, niliingia chumbani na kujilaza kitandani huku nikilia.


***


Kweli Mama aliondoka baada ya siku tatu tu, lakini alimuacha yule binti ambaye bado alikua akiigiza kama mfanyakazi wa ndani. Aina yake ya mavazi ilikua ikiniumiza sana kichwa ingawa mume wangu hakuonyesha kujali, alikua akifanya kazi zangu nyingi, asubuhi alikua akijilazimisha kuamka mapema kutuandalia chai na alikua akipika chakula cha usiku kwakifupi alifanya mambo mengi ya makusudi kama mke ili tu kunikera.


Kila nilipoongea alijishusha na kusema yeye ni binti tu wa kazi na hawezi kuondoka kwani aliletwa pale na Mama mkwe wangu hivyo kama nataka kumuondoa basi nimuambia mume wangu. Mume naye hakutaka kumuondoa, sijui kama alikua anamuogopa Mama yake au alikua anafurahia kile kitendo lakini hakuongea chochote. Mimi ndiyo nilikua muongeaji mkuu, ilifikia hatua nikaanza kuonekana kama mimi ndiyo nina kisirani.


Nilianza kuuona ukaribu wa mume wangu na Angel, walikua wakiongea na kucheka kuliko hata mimi, kwa kiasi kikubwa mazungumzo yangu na mume wangu yalikua ni kugombana tu hivyo mara nyingi mume wangu alikua karibu naye na kila nilipoongea alisema nina wivu wakijinga. Nilitaka kuondoka lakini baada ya kuongea na Mama yangu alinishauri kuvumilia.


Ingawa nilishachoka lakini aliniambia kama nikiondoka basi nitakua nimewafungulia milango ya wao kuwa pamoja kwani ndiyo kwanza nitakua nimewaachia nyumba wenyewe. Aliniambia hiyo ni mitihani hivyo mimi nivumilie ipo siku yatakwisha. Nilijivika joho la uvumilivu na kukubaliana na kila kitu walichokua wanakikifanya. Ingawa kila siku mume wangu alikua akiniambia hakuna kitu chochote kinachoendelea kati yao lakini nilikua nikiumia kama vile nimewaona wakifanya mapenzi mbele yangu.


Siku moja nilichelewa kurudi nyumbani, nilirudi na kukuta hakuna kitu, kwa kawaida tangu Angel kuja pale alikua akipika chakula cha usiku yeye, ingawa nilikua nikijitahidi kuwahi lakini yeye hakua na kazi nyingine zaidi ya kuharibu ndoa yangu hivyo alikua na mchana kutwa wa kumpikia na kumhudumia mume wangu. Mume wangu hakua nyumbani, nilijaribu kumpigia hakupatikana,. Lakini pia Angel naye hakua nyumbani, nilimpigia yeye alipokea.


“Baba aliniambia nimsindikize kwenye harusi.” Aliniambia baada tu ya kupokea simu, alikua akiongea kistaarabu kana kama vile hakikua kitu kibaya. Hapo ndipo nilikumbuka kuhusu harusi ya Mmoja wa marafiki zake, ni harusi ambayo tulishapanga kwenda kwani huyo binti aliyekua akiolewa alishakua rafiki yangu. Lakini kutokana na matatizo yangu ya kifamilia nilisahau kabisa kuwa kulikua na harusi.


Nilimuomba ili niongee na mume wangu lakini alinikatia simu. Niliingia ndani nikitaka kulala kwa hasira, sikua na hamu hata ya kula hivyo nilivua nguo ili kupanda kitandani. Lakini badala ya kupanda kitandani nilijikuta navaa nguo nyingine, nilikua navaa nguo kwaajili ya kwenda kwenye harusi. Si kitu ambacho nilikipanga, nilijikuta tu najiandaa, ndani ya nusu saa tayari nilikua kwenye gari nikielekea ukumbini.


Sikua nimepanga kufanya fujo lakini nilitaka tu kwenda. Ingawa sikua na kadi lakini nilitaka kwenda, nilitaka kuwaona, nilitaka mume wangu anione kwani najua aliniacha makusudi. Mpaka wakati huo nilishajua kuwa mume wangu anatembea na yule binti ingawa nilikua bado sijawafumania. Nilipaki gari, mlangoni niliitishwa kadi ambayo sikua nayo, nilisimama kidogo na kusitasita nikiwaza nini chakusema, mlinzi hakua akinifahamu hivyo ilikua ngumu kunielezea.


“Muache huyo aingie niko naye…” Nilisikia sauti ya kiume, haikua ngeni, ilikua ni sauti ya Victor, yule rafiki wa mume wangu ambaye alikua akinitongoza tongoza. Ingawa nilikasirika lakini sikua na namna, nilitaka kuingia hivyo nilikua tayari kukubaliana na msaada wa yeyote ili tu niingie ndani. Alikuja na kunishika mkono, niliudhika lakini kwake ilikua ni kama masihara flani.


“Nashukuru Mungu, kwangu kukushika mkono tu hata kama usiponikubali lakini ulivyomlaini namna hii ni kama vile nishatembea nawewe! Wakubwa wanafaidi!” Alianza kuongea maneno yake ya kuudhi, nilijitahidi kujikaza ili nisijiaibishe, Victor hakua ni mtu wa kuchelewa, alijua kabisa hawezi kuonana na mimi tena hivyo alitaka kuitumia ile nafasi vizuri.


“Shem unachotaka kukifanya si kizuri…” Alianza kuniongelesha, nilijua alichokua anazungumzia lakini nilinyamaza na kujifanya sijui chochote.


“Mumeo nimekaa naye sehemu moja, yuko na yule binti yenu wakazi, najua unajua lakini hembu kaa kidogo nikupe mbinu zakuingia. Huwezi kumkomesha kwa kitu ambacho unataka kukifanya, kikubwa utaharibu tu harusi ya rafiki yetu na kujidhalilisha!”


Kusema kweli mpaka wakati ule sikua najua nimeenda kufanya nini pale, nilikua nimeenda tu hivyo kwa namna flani nikama nilimuelewa lakini bado sikua tayari kuacha kuingia na kumsikiliza. Victor alikua mtu wa utani sana na kwa muda mchache niliokua namjua nilijua kuwa hajaoa lakini ni mtu wa wanawake sana. Kwa marafiki zake alionekana mtu wa masihara lakini kiuhalisia alikua ni kicheche hivyo sikutaka hata kuwa karibu naye kwani ingawa mimi najiamini lakini sikutaka watu waone kama kashanipitia.


“Kabla ya kuingia njoo ukae hapa, uniambie unenda kufanya nini kisha ndiyo nitakuruhusu uingie.” Aliongea huku akinivuta kw k kuelekea upande wa pili, katika lile jingo upande wa pili baada ya ukumbi kulikua kuna kasehemu kama kabaa flani hivi. Mziki wa taratibu ulikua ukipigwa, haukua ukisikika sana kwani ulifunikwa na mziki wa ukumbini. Ili kukwepa aibu ya kuonekana kama tunagombana nilijikuta namfuata kihiari kwani tayari alishaanza kunivuta na watu walikua wakituangalia.


“Shem unakunywa nini?” Aliulizia hukua kisogea Kaunta, sikutaka kunywa lakini kwakua tulishatoka pamoja na mume wangu kama mara mbili tatu alijua nakunywa nini. Aliniagizia Castle Light ya baridi akaifingua na kuweka mezani. Alianza kunihoji hoji maswali yake na kuongea mambo yake ya kijinga jinga lakini yakufurahisha, kwa namna flani nilijisikia vizuri kukaa pale kuliko kuingia ndani.


“Poteli ya mbali ni bora ninywe tu!” Niliwaza huku nikichukua ile bia, niiliinywa harakaharaka na kuimaliza ndani ya dakika tatu tu. Aliniagizia nyingine na nyingine, baada ya kuzinywa tatu za harakaharaka kichwa sasa kilikaa sawa. Nilitulia na kuanza kunywa taratibu.


“Kuna tatizo gani siku hizi, mbona wewe na jamaa kama hamko sawa kabisa! Unajua umechoka, unaonekana una mawazo sana?” Aliniuliza, lilikua swali la kunikera lakini ni kitu ambacho nilijua kabisa anajua majibu yake. Nilimuangalia tu kwa kumkodolea macho akawa kama amejua sitaki kuongea kwakua nafahamu anajua kila kitu.


“Lakini shemu wewe ndiyo unakosea, umempa nafasi yule binti. Kama ni mimi wewe wala nisingeshindana naye, ningemuacha afanye anayofanya kisha mimi najilia bata tu.” Alianza kumuongelesha lakini hata sikumuelewa.


“Kale kabinti kana akili, kanakuacha wewe uwe kisirani, jamaa kila siku anakulalamikia wewe, anasema wewe una mdomo, hamuwezi kuongea kitu chochote kabla hujalalamika, kila akiwaza kurudu nyumbani anawaza namna ya kujitete kwako. Lakini akiwa na yule binti basi anajisikia vizuri, anamfariji, halalamiki na wala hamuumizi kichwa, hata hanuni.”


Ingawa alikua anaingilia maisha yangu lakini alianza kuongea ukweli, kweli nilikua na kisirani, mara kadhaa mume wangu aliniambia nibadilike, aliniambia hamhitaji yule binti lakini mimi nayeye hatuwezi kukaa hata dakika tano bila kugombana ndiyo maana hataki hata kuongozana na mimi.


“Unajua Shem wanaume hata hatutaki makelele…” Nilishangaa kidogo kwani kwa mara ya kwanza aliniita Shemeji.


“Unapokua na mwanamke kila siku anarudia kitu kile kile ni kama anakusukuma na kumuambia fanya! Fanya! Fanya! Mimi namjua jamaa yako ana ufala flani hivi kwa wanawake, yule binti kashamsoma hivyo anakua karibu naye na kumfanya rafiki, akishakua rafiki tu nina uhakika atatembea naye!”


Aliongea maneno ambayo yalinishtua kidogo, alikua anazungumzia kuhusu kutembea naye, nilianza kumdodosa akaniambia mume wangu hawezi kutembea na yule binti ila nikiendelea na kisirani changu basi nijue kuwa atatembea naye.


“Unatakiwa kumuacha yule binti yeye ndiyo awe na kisirani, muache afanye hizo kazi kwani wewe unaumia nini akifua, si unajua lengo lake basi muache. Unajua huyo si kama mfanyakazi wa ndani ni mke mwenza, hivyo hembu muache yeye ndiyo awe na kisirani ili mume amchoka.”


Alinishauri mambo mengi ya busara, kwa kipindi kile nilianza kumuona wamaana. Nilijikuta navutiwa naye na ukichanganya na pombe nilianza kumshukuru na kumsifiasisfia. Harusi ilikua inakaribia kuisha hivyo alinishauri niende nyumbani kabla ya mume wangu na nikifika nikulala tu nijifanye hakuna chochote. Ingawa nilikataakataa lakini alinilazimisha, kwakua nilikua nimelewa alinichukua na gari yangu mpaka nyumbani.


Alinisaidia kufungua geti na kunipeleka mpaka ndani, nilimuambia akae lakini hakutaka, alikua na haraka na alihofia kuwa mume wangu anaweza kumkuta pale na haitaleta picha nzuri. Sijui ni, Pombe au nini lakini nilikasirishwa na yeye kutaka kuondoka, nilanza kumtukana na kumuambia kumbe yeye si mwanaume kweli, mbona anamuogopa mwanaume mwingine. Nilianza kulalamika labda ananiona si vutii na kama sivutii kwanini alikua ananitongoza.


Sijui ninini kiliniingia lakini nilimvamia na kumsukuma kwenye kochi, akiwa pale chini nilaianza kuvua nguo na kumkumbatia. Kuna mzuka flani ulinipanda na kutaka kufanya naye mapenzi, sikujali kama ilikua nyumbani kwangu lakini nilijihisi kama namhitaji. Nilimshika na kumkumbatia nayeye bila ajizi alinishika, alinikumbatia na kuninyanyua taratibu. Akili yangu haikuapale na nilikua tayari kufanya chochote, kichwani nilimuona mume wangu akifanya mapenzi na Angel hivyo nilijiaminisha kama nalipa kisasi.


ITAENDELEA


SIMULIZI; MIMI, ANGEL, MAMA MKWE NA MUME WANGU KATIKATI—SEHEMU YA TATU


(ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI; Mume wangu ananiacha nyumbani nakwenda harusini na Angel, kile kitu kinaniuma na kuamua kuwafuata. Kule nakutana na rafiki yake Victor ambaye ananituliza na kunirudisha nyumbani. Kwakua nilikua nimelewa najikuta nikimvamia na kutamani kufanya naye mapenzi, je nini kitatokea. ENDELEA… Kama hukusoma sehemu ya Pili Bonyeza hapa Iddi Makengo )


Victor alinyanyuka, nilikua nimemkumbatia bdo hivyo alinyanyuka na mimi. Alikua kama kanipakata hivyo na mimi nilionyesha ushirikiano kwa kuipitisha miguu yangu kiunoni kwake nikawa kama mtoto mdogo hivi. Nilimbana kwa miguu huku nikijiahidi kumpelekea mdomo.


“Shemu umelewa, hapana hatuwezi kufanya chochote…” Aliongea huku akijisogeza pembeni, nilijisikia vibaya yeye kukataa, lakini nilijua anazuga tu kwani ananitaka. Nilizidisha kumkumbatia lakini alikataa katakata, akainama na kunikalisha kwenye kochi.


“Umelewa Shem, ingawa nakutamani sana lakini hizi si akili zako. Mimi ni mwanaume kamili, siwezi kufanya hivi wakati najua umelewa.”


Hapo nilimuona yuko siriasi, nilijikuta naishiwa nguvu na kumuachia, sasa nilianza kupata aibu. Pombe zote ziliniishia na nilianza kujisikia vibaya kwa namna nilivyokua nikimlazimishia. Alitaka kuelezea na kuniomba msamaha, akiniambia siku nyingine nikiwa sawa lakini sasa sikutaka hata kuisikia sauti yake. Nilijisikia kichefuchefu kabisa, kila nilipomuangalia nilitamani kukiambia na kutoka mule ndani, alijua nilivyokua najisikia hivyo aliondoka bila kusema chochote.


Baada ya Victor kuondoka nilitaka kwenda kuoga, lakini nilikua napepeseka na nilichoka sana. Nilienda na kupanda kitandani, nilijitupa, sikushtuka tena mpaka asubuhi. Mume wangu alikua bado hajarudi, nilienda chumbani kwa Angel nikakuta naye bado hajarudi, niliingia bafuni na kujimwagia maji. Sikujisikia vizuri kupika niliennda kupata Supu. Bado kichwa kilikua hakiijakaa sawa hata lile suala la wao kuchelewa kurudi nilikua bado sijaliwaza.


Nilirudi nyumbani nikiwa sawa, hapo ndipo nilianza kupata akili, nilijua kama hawjarudi basi inawezekana kuwa walilala pamoja. Roho iliniuma sana na sasa nilijua kuwa ndiyo ndoa yangu inavunjika, lilikua ni suala la muda tu kabla hajapata ujauzito na mimi kufukuzwa. Nilikaa kitandani na kuanza kulia, akili yangu ilikua inawaza nifanye nini ili kukabiliana na ile hali. Kwa muda wote wa ndoa na mume wangu sikuwahi kumuona wala kuhisi kuwa anachepuka.


Lakini sasa nilikua naamini kuwa nilazima atakua anachepuka na kwa namna Angel alivyoletwa alikua ni mke na si mchepuko. Tena mke ambaye anapendwa mpaka na wakwe zangu. Nilijikuta nalia tu, nimekata tamaa, nikiwa katika hali ile simu yangu ilianza kuita. Ilikua ni namba ngeni, nilitamani nisipokee lakini nilihisi labda ni ofisini, kwnai bosi wangu ana kawaida ya kunipigia na namba tofauti tofauti.


Nilipokea, lakini haikua ni ofisini, nilikutana na sauti ambayo kwa wakati huo sikutaka kabisa kuisikia. Alikua ni Victor akinijulia hali, nilikua na hasira, nilitamani kukata simu lakini sikukata. Niliacha hewani huku nikikaa kimya bila kuongea chochote. Hakukata simu alianza kuongea, aliniomba msamaha kwa kitendo cha jana na kujielezea kidogo, lakini baada ya muda mwenyewe aliniambia tuyaache hayo. Nikama alijua kuwa mume wangu hakulala mule ndani, ingawa hakuongea moja kwa moja lakini alikua kama ananifariji.


“Acha kupambana, kama unataka mume wako achanganyikiwe acha kabisa kuuliza. Huyo binti si kaja kama mfanyakazi basi mfanyishe kazi mpaka akimbie mwenyewe, jifanye mjinga na kama umeichoka ndoa unataka kutoka toka kwani una kazi yako kwanini uteseke na mtu kama huyo!” Aliongea maneno mengi lakini kuna ambayo yaliniingia zaidi, aliposema binti kaja kama mfanyakazi nimfanyishe nilipata wazo, kusema kweli sikua tayari kuondoka, pamoja na kujua kuwa ndoa imesha lakini nilikua nampenda sana mume wangu.


Ilikua ni lazima nipambane, isitoshe nilikua bado natumia dawa hivyo nilijua kama nikiondoka bila kuhangaika kupata mtoto na kuanza maisha mapya itanichukua muda sana kupata mtu mwingine. Niliwaza hivi kama dawa zikifanya kazi kwa muda nitajuaje kama zinafanya kazi kama sina mwanaume wa kufanya naye mapenzi. “Siwezi kujitia mimba mwenyewe, nitabanana hapahapa! Hata kama nikifukuzwa lakini huyu binti ataisoma namba.”


Mwishoni nilimuaga Victor na kumshukuru kwa kunipigia. “Ya jana hayawezi kutokea tena, umepoteza nafasi yako sitaki tena usumbufu, sasa tuwe marafiki tu, wewe ndiyo nitakua nakupa umbea wangu maana unaonekana unajua kila kitu na mimi sina mtu mwingine wakuongea naye.” Alicheka na kukubali, alinitania tania kisha akakata simu. Kidogo nilikua na ahueni, niliamua kuwa hata kama nikiondoka lakini nitaondoka kwa kupambana, sikutaka kuondoka kirahisi rahisi hivyo!


Mume wangu na Angel walirudi mchana, Angel bado alikua akijifanya kumuita Baba na mimi kuniita Dada. Nilikua najichekea kichwani na kujifanya mjinga.


“Harusi ilichelewa kuisha tukaona kama tutakusumbua, tumelala kwa mfanyakazi mwenzetu…” Mume wangu alijiongelesha ongelesha bila hata kuulizwa. Nilimuitikia tu hamna shida kisha nikamgeukia Angel.


“Kuna mashuka ya kufua kule chumbani, angalia na vyombo sijiikii vizuri utapika na wali maharage, nimeshayachambua yapo jikoni.” Nilimuambia huku nikitoka, nilimuacha kaduwaa kwani ndiyo ilikua mara yangu ya kwanza kumpa kazi.


***


“Uwe una msaidia huyu binti wa kazi anachoka sana…” Siku moja mume wangu aliniambia. Ilikua ni asubuhi tumekaa mezani tunakunywa chai. Ilikua ni chai na chapati nilishamuambia hata mimi napenda chapati za moto. Tangu siku ile wanirudie mchana nilainza kumuona Angel kama mfanyakazi, nilijua fika anatembea na mume wangu lakini nilijifanya mjinga. Nilikua nampa kazi kama vile Punda, asubuhi aliamka nakufanya usafi, kupika chai, kutuandalia kila kitu.


Kwakifupi nilikua sifanyi chochote, wakati mwanzoni nilikua nashindana naye katika kufanya kazi sasa nilikua namuachia kila kitu. Nilimuona anachoka na kwakua alikua pale kunifanyia makusudi kuwa mimi nitachoka na kuondoka wala sikuchoka. Kwa nilivyokua namfahamu mume wangu asingeweza kunifukuza, alikua ni msaarabu sana ndiyo maana hata alimkubalia Mama yake ule ujinga bila kupenda na sasa alikua kwenye mapenzi na Angel.


“Anachoka na nini si kaja kufanya kazi?” Niliuliza kwa hasira kidogo.


“Ndiyo lakini?”


“Lakini nini? Kwani kuna kazi gani hapa, kabla ya yeye kuja hapa kila kitu si nilikua nafanya mimi, tena nikimaliza naenda kazini, yeye ni kukaa tu hapa nyumbani kutwa nzima! Ulishawahi kunisikia nikilalamika hata nahitaji mfanya kazi?” Niliuliza, mume wangu alibaki kimya.


“Au kuna nini kinaendelea, mbona unamuonea yeye huruma kuliko mimi? Vipi unampenda maana naona ghafla unataka nimsaidie, kama amechoka hawezi kufanya kazi si aondoke. Njia nyeupe lakini hawezi kuja kama mfanyakazi halafu mimi nimsaidie sasa nitakua namlipa pesa za nini kama hawezi aondoke nitafanya kazi mwenyewe.”


Mume wangu alinyamaza kimya bila kusema chochote. Kichwani nilikua najichekea kwani najua ashaanza kumpenda na anaumia namna ninavyomuendesha.


“Angel mdogo wangu eti unachoka na hizi kazi? Baba yako anasema eti huwezi kazi nakutumikisha nikweli?” Angel alijipitishana ki-khanga chake kimoja, lengo lake lilikua ni kuniudhi lakini sikuudhika.


“Hapana Dada, mbona mimi naweza kila kitu, chochote kikikushinda niambie tu. Mimi naweza vingi hata ambavyo huwezi kufanya!” Aliongea kwa kebehi huku akijichekesha kikahaba.


“Unaona mume wangu, mtoto anasema anaweza kila kitu ni sisi tu hamtumii vizuri! Mimi nataka nimtumie vizuri sijui wewe mwenzangu kama unamtumia?”


Mume wangu alikasirika na kuondoka kwa hasira, aliingia kwenye gari yake na kuondoka. Mule ndani nilibaki mimi na Angel, kwa kawaida huwa tukibaki wawili anajifanya kuwa na kiburi, ananijibu kwa dharau. Alienda na kukaa kwenye kochi kama kunionyesha kuwa hafanyi chochote.


“Amka Mama ufanye kazi zako za ndani sio kujipitisha pitisha na vikhanga hapa!” Niliongea kwa hasira huku nikitoka.


“Nisuala la muda tu nitakua mother house!” Alijiongelesha nikama alikua hanuiambii mimi lakini alitaka nisikie. Sikutaka malumbano hivyo sikumjibu, nilitoka zangu na kumuacha palepale akiota kuhamia pale.


***


Haikua rahisi kuishi na mwanamke ambaye najua fika anatembea na mume wangu. Ingawa mume wangu alikua akinifanya kama mjinga flani lakini yule binti alikua anajua, alikua akivaa vinguo nguo vya kunikasirisha tu, alikua anapenda kukaa karibu na mume wangu na kumsifia sifia. Mume wangu alikua akijifanya kukasirika lakini kwakua alihitaji mtoto niliona kabisa alikua karibu naye


Mama mkwe naye hakua kimya, kila siku alikua akipiga simu kunitukana na kuniambia kuwa nitaondoka tu. Ndugu wengine ambao walikua Dar walikua wakija kabisa na kumuita yule wifi, walinoionyesha dharau za hali ya juu na mara zote hawakutaka hata kuongea na mimi. Lakini hali ile haikunifanya kuwa mpweke, nilikua na rafiki yangu mpya, Victor. Alikua ni kijana kama mimi lakini kwa umri wa miaka 33 alikua bado hajaoa na wala hakufikiria kuoa.


Alikua ni muongeaji sana, pamoja na kwamba alikua akinitaka bado lakini aliheshimu nilipomuambia hapana. Ilifikia hatua akakata tamaa na kuacha kabisa kunifuatilia, tukawa marafiki, nikawa natumia muda wangu mwingi kuongea naye kwani alikua hependi kuchat. Tulikua tunaongea hata kwa masaa mawili, mume wangu anapokua hayupo au anapojifanya kuwa bize kwenye TV ili tu kuwa karibu na Angel nilitoka nnje na kua bize kuongea na mara chachechache kukiwa hakuna nafasi kuchat kwa simu.


Mara kadhaa Victor alikua akinitoa out kupunguza mawazo, alikua akinipa stori zake za wanawake na kweli alikua ni kicheche. Siku moja Victor alikua anaumwa, alikua na Malaria, alilazwa hospitalini kwa siku tatu mpaka kuruhusiwa. Pamoja na kwamba walikua na urafiki na mume wangu lakini si wakihivyo, hata suala la kuumwa mume wangu hakulijua lakini sikuweza kumtembelea hospitalini kwakua rafiki zake wangine wangeniona na kunishangaa.


Alipotoka Hospitalini niliamua kumtembelea nyumbani kwake, haikua mara ya kwanza kufika kwake, nilishaenda mara nyingi na mara zote tulikua tunaongea. Zaidi ya utani wake wa kila siku kuwa ananitaka hakuwahi kuniivunjia heshima kutaka kunilazimisha, siku zote alikua akiniambia kuwa “Nataka unipe mwenyewe ili unikatie hicho kiuno mpaka nichanganyikiwe!” Mimi nilikua naishia kucheka tu kwani kwa tabia zake nilishaapa kuwa siwezi kumpa mwili wangu kabisa, tutakua marafiki tu.


“Ukae vizuri, acha kunitega tega, unajua nina karibu wiki sijagonga shauri yako!” Alinitania wakati nampa supu ili anywe. Nilimnunulia Kuku sokoni na kwenda kumtengenezea supu. Sikua nimevaa kimitego kwakua ndiyo nilikua nimetoka kazini, nilivaa gauni flani hivi, si fupi sana lakini pana la kumwagika. Niliishia kucheka tu kwani  nilijua anatania, mara nyingi ni stori ambazo  hupenda kuzipiga kila tunapokua pamoja.


“Wewe fala kweli, yaani unaumwa lakini bado unawaza hayo mambo?” Niliongea kwa kumtania, niliyaangalia macho yake yalikua yakiangalia mapaja yangu. kwakua nilikua nimekaa na kulibania gauni katikati ya miguu ili lisipeperuke liliacha sehemu ya mapaja yangu wazi. Sikuona ajabu hivyo sikutaka hatakurekebisha.


“Sasa mwanaume utawaza nini zaidi ya hivyo, hivi kweli unataka niwaze mpira wakati nimekaa na mtoto mzuri kama wewe!”


“Kwanini usiwaze, hivi kweli na unavyoumwa uanweza kufanya chochote?”


“Kwanini nisiweze, hivi unaona naumwa kweli hapa? Hata kama ningekua na Drip mkononi lakini ningeweza kwani kinachoumwa ni nini? Tena hayo mambo yanasidia, halafu hata haya Malaria nina wasiwasi nayo, mimi si mtu wa kuumwa hivi.” Aliendeleza utani wake, tuliongea na kucheka, alikua akiniangalia kwa tamaa. Nilimuona kweli ananitamani na kuanza kucheka kwani kweli alikua anahangaika.


“Hivi kweli huwezi kukaa mwezi bila kufanya mapenzi?” Nilimuuliza sawli ambalo hata mimi nilijua jibu lake.


“Mwezi kwani mimi nina matatizo gani?” Alijibu kwa swali.


“Una kazi sana , mimi na mume wangu tunaweza kukaa hata miezi mitatu hatufanyi kitu!”


“Sema wewe si mume wako, si ana mchepuko wake, hata siku mbili hawakai!” Aliongea kiutani lakini niliudhika kidogo, aliona na kupotezea lile swala akaleta mada nyingine.


“Lakini kichwani ni kama nilitaka aongelee yale mambo, kweli nilikua na muda sijafanya mapenzi hivyo nilitaka kusikia habari hizo.” 


Nilimchokonoa kwakua namjua aliingia laini na kaunza kuongea. Alianza kuniambia namna ambavyo kidogo atembee na nesi mmoja, isingekua Mama yake ambaye alikua anampigia simu kila saa wangemalizana kwenye choo che wodini. Nilicheka sana na kuanza kumtania kama nikimpa wakati ule anaweza kufanya.


“Jaribu uone, tena utanisaidia hii Malaria ipone!” Aliongea huku akinisogelea, tulikua tumekaa kwenye kochi moja.


“Mimi hata ukinigusa tu na hivi vidude vyako namaliza kila kitu, hapa navuta picha ya bafuni kabisa.” Aliongea hukua kiniangalia kifuani, alikua akiyaangalia matiti yangu yaliyochomoza kwa usongo.


Nilijikuta nasisimkwa kwa namna alivyokua akiniangalia, nilitamani hata aniguse lakini hakufanya hivyo. Aliendelea kuongea mambo mengine ya kimahaba mpaka na mimi nilijihisi kuloana.


“Pumbavu wewe hivi unataka mpaka nikuanze! Mwanaume gani wewe!” Nilijikuta naropoka huku nikimvamia. Safari hii hakusita, alinivamia na kunipa shuguli pevu. Mpaka tunamaliza na ugonjwa wake uliisha. Alinionea aibu lakini nilimtoa wasiwasi na kumuambia nimefurahi na hakunifanyia kwalazima.


Nilirudi nyumbani nikiwa najisikia vizuri sana, baada ya kama miaka sita ya ndoa nilikua nimemsaliti mume wangu lakini tofauti na nilivyodhani hata sikujisikia vibaya, sana sana nilijisikia vizuri. Tangu siku ile kila kitu kilibadilika, karibu kila siku nikitoka kazini nilienda kwake, nilianza kuwa na furaha ingawa bado nilikua nampenda mume wangu lakini nilikua nasehemu ya kunipa faraja. Mume wangu kuniona nina furaha alianza kunitaka, nilikubali lakini niliona kama ananilazimisha.


Sikufurahia tena tendo la ndoa na mume wangu, nilijikuata namuambia kuwa siwezi kufanya tena mapenzi kama yule binti hataondoka. Hapo ndipo nilimkata stimu, alikasirika na kuniambia binti hawezi kuondoka kwani anafanya kazi vizuri. Tuliendelea kulumbana, lakini siku moja nilianza kujisikia vibaya wakati nikiwa kazini, niliishiwa nguvu na nilipopelekwa hospitalini nilikutwa nina ujauzito. Nilikua na mimba ya mwezi mmoja, sikuamini nilirudia vimipo zaidi ya mara tatu na majibu yalikua yaleyale,  zilikua ni habari nzuri sana kwangu.


Niliruhusiwa kutoka hospitalini, akili yangu ilikua inamuwaza mume wangu, nilijua dawa zimesaidia. Nilimuomba rafiki yangu kunipeleka nyumbani kwani sikutaka hata kuendesha gari. Niliingia ndani ili kuongea na mume wangu. Nilifika na kumkuta yuko kakaa sebuleni, Angel alikua amekaa pembeni yake. Walikua kama wamekumbatiana, waliponiona hata hawakushtuka, nilishtuka kwani nilishamuambia mume wangu amfukuze.


Kwakua nilijua kuwa mume wangu anataka mtoto na sasa nina ujzuzito nilipata kiburi. Nilianza kutukana na kumuambia simhitaji, hatakiwi aondoke mule ndani. Lakini mume wangu alimkingia kifua, alinyanyuka na kuniambia. “Mke wangu nakupenda sana lakini sasa hivi nilazima nifanye maamuzi, najua unafahamu kuwa nina mahusiano na huyu binti, nilikua natafuta mtoto sasa nimempata, Angel ana ujauzito wangu hivyo anakua mke wangu, si mfanyakazi tena.


Siku mbili tatu hizi umekua ukiniambia kuwa huwezi kuendelea kuishi na huyu binti hapa. Ukaniambia nimfukuze, najua tumetoka mbali lakini mimi nataka mtoto na hakuna kitu cha kumifanya nimtelekeze mwanangu. Angel hakutaki na yeye kabeba mimba yangu hivyo kusanya kilichochako uondoke…” Kidogo nidondoke, nilijikuta nashuka taratibu na kukaa chini. Ile furaha yote niliyokua nayo ilipotea ghafla.  Nilishindwa hata kunyanyua kichwa kuwaangalia.


ITAENDELEA…


SIMULIZI; MIMI, ANGEL, MAMA MKWE NA MUME WANGU KATIKATI—SEHEMU YA NNE


(ILIPOISHIA SEHEMU YA TATU; Niliammbiwa kuwa nimjamzito, baaada ya kuhangaika kutafuta mtoto kwa muda mrefu niliona kama ni kitu cha kumuambia mume wangu. Nilitaka kumuambia ili amfukuze Angel binti wa kazi aliyeletwa kwangu na Mama mkwe wangu. Lakini kabla ya kusema chochote mume wangu ananiambia niondoke kwani Angel tayari ana mimba na hanitaki. ENDELEA…. Kama hukusoma sehemu ya Tatu Bonyeza hapa Iddi Makengo )


Angel alianza kutukana, alikua ananiambia nitoke kwake kwani yeye ndiyo atamzalia mume wangu na ndiyo ana haki ya kuishi mule ndani. Mume wangu yeye alikua akiniangalia tu, kama kawaida yake hakusema chochote, pale chini nilikua kama nimeishiwa nguvu. Mume wangu alitaka kuninyanyua lakini Angel alimzuia, naye alijilaza kwenye kochi na kuanza kulalamika kuwa tumbo linamuuma, mtoto sijui anasumbua.


Nilishikwa na hasira, bado nilikua sijaamua kama nimuambie mume wangu kama nina ujauzito au la. Kusema kweli nilikua na waza mara mbili, ingawa nilitamani kumuambia lakini sikutaka mapenzi ya hivyo, sikutaka mume wangu kuishi na mimi kwakua tu nina mimba yake. “Nina thamani zaidi ya hiyo, kama hanipendi siwezi kulazimisha.” Nilijiongelesha huku nikikusanya nguvu za kunyanyuka, nilinyanyuka taratibu na kukaa, sikua na nguvu za kusimama.


“Kwahiyo ndiyo umeamua hivyo?” Nilimuuliza mume wangu, alikaa kimya bila kusema chochote, kuona hivyo Angel aliingilia.


“Ndiyo kaaamua hivi wewe Dada vipi, si ushaambiwa hutakiwi? Au unataka kukaa hapa ili uwe mfanyakazi wa ndani? Maana mimi siwezi kufanya chochote!” Aliongea kwa dharau kabla ya mume wangu kuingilia kati.


“Kua na adabu, hata kama una mimba yangu lakini huyu bado ni mke wangu wa ndoa hivyo unapaswa kumheshimu.” Mume wangu alijifanya kunitetea, nilimshangaa kwani mara kadhaa Angel alikua ananijibu hivyo lakini wala hakujali eti kisa anataka kunifukuza basi ndiyo anajifanya kunitetea.


Aliongea maneno mengi ya kujaribu kunituliza lakini nilishachefukwa.


“Kama huyu binti ana mimba siwezi kuwa na amani hapa ndani, huu ni muda wangu wa kuwa na furaha, siwezi kuendele a kugombania mume tena!” niliwaza, mume wangu bado alikua akinielezea mambo ambayo hata asikumuelewa.


“Kwahiyo inakuaje, unanipa Talaka au ni vipi, hembu fafanua, ninapoondoka hapa naondoka kama nani? Mtalaka wako au unanirudisha tu kwetu nikapumzike?” Nilimuuliza kwa kujiamini, hapo nilimuona mume wangu kama kanywea flani, hakufikiria kama nitamuuliza hilo swali.


“Hata mimi sijui, ninachotaka ni wewe tu uondoke, maana hatuwezi kuishi wote humu ndani!”


“Sikiliza wewe ni mume wangu tena wa ndoa lakini siwezi kulazimishia kushia na wewe. Nimekua mjinga kwa muda mrefu lakini naona sasa niwakati uamue wewe mwenyewe kama  unaniacha au la? Hapa ni kwangu, siwezi kuondoka tu kwakua wewe umejisikia, hata nikiondoka naondoka kwa msingi ipi, je nikifika huko naendelea na maisha yangu au mimi bado ni mke wa mtu, nilazima nijue kwasababu kuna leo na kesho, ya Mungu mengi naweza kutoka hapa nikakutana na mtu akanipenda, je nitapaswa kumkubali au nitamuambia mimi ni mke wa mtu?”


Mume wangu hakua na jibu, nilimuona kabisa akiumia, nilimuona akichanganyikiwa, ile hali ilimuumiza hara Angel, alidhani nitalialia, nitang’angania na kuomba msamaha au hata kama ni kuondoka nitaondoka kama Mbwa lakini haikua hivyo. Kusema kweli nilishachoka na kikubwa hasa kilichokua kinanifanya mimi kuvumilia ilikua ni kutafuta mtoto. Kwa umri wangu nilijua kama ningeachana na mume wangu kabla ya kupata mtoto basi ingeniwia vigumu sana kupata mwanaume mwingine wa kuzaa naye.


Kwa baraka ambazo Mungu alikua amenipa niliamini sitakiwi tena kubembeleze ndoa, kama mwanaume hanitaki hanitaki. Lakini pia nilikua na hofu, ile ndiyo ilikua mimba yangu ya kwanza, mawazo na stress za pale zingenichanganya na kufanya hata mimba iharibike. Nilinyanyuka na kuelekea chumbani, nikachukua mashuka na baadhi ya nguo nguo zangu na kwenda kwenye chumba kingine. Kwa nilivyokua nikijisikia sikutaka hata kumuambia tena mume wangu kua nina ujauzito, niliingia chumba kingine na kulala bila kusemeshana na mume wangu.


Siku iliyofuata sikua naenda kazini, baada ya kudondoka ofisini nilipewa ID ya siku tatu hivyo nilikua napumzika. Asubuhi asubuhi hata kabla sijaamka vizuri simu yangu iliita, ilikua ni namba ya Mama mkwe wangu. Nilimsalimia lakini hakuitika, alianza kunichamba kuhusu kukataa kuondoka na kuniringisha mimba ya Angel “Hizi ndiyo stress nilikua sizitaki.” Nilijisemea huku nikiweka simu pembeni, nilipunguza sauti kabisa kisha nikaiweka pembeni na kuendelea kulala zangu.


Sikutaka kumkatia simu wala kujibishana naye, nilishasema sitaki stress hivyo nilimuacha aongee mwenyewe na simu yake ili atoe sumu yake mwilini huku mimi nikifurahia usungizi. Aliongea mwenyewe kama nusu saa hivi kisha akakata simu, baadaye Victor alinipigia, alitaka kunijualia hali kwani nilimuambia kuhusu kuumwa, sikumuambia kuhusu ujauzito kwani nilikua naamini kua si wake.


Mara nyingi nilikua sikutani na Victor katika siku za hatari nilijaribu kujizuia hivyo, nilitaka miamba kutoka kwa mume wangu hivyo ingawa sikua makini kila siku lakini niliamini si yake. Tuliongea sana na kutaniana akitaka kuniona nikamuambia haitawezekana kwani niko nyumbani na siwezi kutoka. Baadaye tuliagana, niliamka na kujiandalia chai, Angel alishakua Mama mwenye nyumba hivyo hakutaka kufanya chochote na mimi sikujali.


***


Sula la kunacha moja kwa moja lilikua gumu sana kwa mume wangu, siku zilikua zinaenda na nilijua kuwa siwezi kuficha mimba kwa muda mrefu, nilijua kama nikiendelea kusubiri sana basi itajitokezea na anaweza kutaka kunirudia kwakua tu nina mimba kitu ambacho sikutaka kitokee. Mama mkwe naye alikua ni mtu wa kupiga simu kila siku, kwakua nilikua simsikilizi alikua akimpigia simu mume wangu na kumsumbua.


“Umekaa miaka mingapi hupati mtoto unang’ang’ania nini sasa hapa si uondoke!” Baada ya kukaa muda mrefu bila kuwa na uhakika kama nitaondoka au la Angel alianza kunisumbua.


“Nani kakuambia kuwa nina haraka, mimi niko kwangu labda wewe ndiyo unatakiwa kuondoka.” Nilimjibu kistaarabu, nilijua namuumiza zaidi nikiacha kupaniki kuliko ile hali ya kujibishana naye mara kwa mara.


“Watu wasio na vizazi wanashida! Wivu tu, tuache na mimba zetu!” Aliongea huku akiondoka, nilikua jikoni napika chakula cha mchana. Ingawa tulikua watatu mule ndani lakini mimi ni kama nilikua nimetengwa, walikua wakipika kivyao, Angel akimpikia mume wangu na mimi kupika kivyangu.


Nilimuangalia wakati anaondoka bila kusema chochote. Yeye alikua anapika jiko la pembeni yangu hivyo sijui hata aliondoka kufuata nini? Lakini aliporejea alianza kutukana, alianza kusema nataka kumuwekea sumu kwenye chakula, alilalamika kaniona nikikoroga chakula chake. Alikiacha pale pale jikoni bila hata kuzima jiko na kurudi chumbani akaanza kujiliza. Mimi nilibaki tu na cheka, nilijua anachotaka kufanya, ulikua ni wakati wa mume wangu kurejea kutoka kazini.


Alitaka nionekane mbaya ili kufukuzwa. Lakini wakati anaondoka kuna kitu kama kilinipiga kichwani. Hakikua kitu halisi lakini ni kama nilizindika flani. “Namimi ni mpumbavu, hivi nashidnana na mjinga, hawa watu hawana akili hivi wakiniwekea mimi sumu, au akinifanyia kitu cha kumdhuru mwanangu hata kiniloga nitamlaumu nani. Mungu kanipa mtoto lakini bado na mchezea na wapumbavu hapa!”


Niliwaza, kweli nilijiona mjinga, sikutaka kuendeleza na mchezo ule tena. Niliacha kupika na kuzima majiko yote, nilitoka na kwenda chumbani na kuanza kukusanya nguo zangu. Angel na mume wangu walikua wakilala chumba kimoja, katika chumba chetu cha zamani hivyo bado kulikua na vitu vyangu ambavyo nilitaka kuvichukua. Nilishaamua kuondoka hivyo sikutaka hata kulala mule ndani siku ile. Nilipanga kulala nyumba ya wageni mpaka nitakapopata nyumba yangu kwani pesa nilikua nayo.


Nilimgongea mlango wa chumbani lakini hakufungua, kwanza alidhani ni mume wangu hivyo akaanza kujiliza kijinga jinga. Alipojua ni mimi alitaka kuja kufuingua lakini niliusukuma.


“Acha kujishaua ushakua mtu mzima, mimi naondoka zangu kama shida ni ndoa Mama basi olewa wewe labda utakua na furaha…”


Nilimuambia mara tu baada ya kuingia chumbani, alianza kuongea maneno yake ya kashfa lakini sikujali, sikuonyesha hata kusikitika, nilikusnaga nguo zangu nilizokua nazihitaji na kutoka nnje.


Kila nilipokua nikitembea alikua ananifuata, ni kama alikua ananisuta, hata yeye hakutegemea kama nitandoka hivyo ni kama alikasirika flani. Alikua kama mtoto ambaye hulililia kitu kwa muda mrefu halafu ukimuachia anaona kama hakina maana.


“Utajiju Bibiiee! Najua una wivu kwakua nina mimba, ndiyo hivyo ondoka! Bwana kashakuja kwangu! Utajiju! Watu tunaringa na vizazi vyetu!”


Aliendelea kuongea maneno yake ya shombo, alinikasirisha sana kila saa kuzungumzia kizazi.


“Hata Mbwa mbona wana vizazi lakini hawasumbui, usijali wewe zalishwa tu! Atakuzalishawee lakini kumbuka hatakuja kukupenda kama naavyonipenda mimi!”


“Upendwe wapi? Angekupenda angekuacha!  Mwanaume kanasa kwangu na akitoka huyu namzalia mwingine na mwingine, kizazi si ninacho bibieee!” Aliendelea kutukana, nilichoka kelele zake hivyo niliamua kumtolea uvivu.


“Kwa taraifa yako nikitaka akuache anakuacha hata kesho, kizazi unachoringia hata mimi ninacho, Mungu kanibariki na mimi nina mimba na kwakua ananienda mimi najua hata nikimuambia leo utafukuzwa kama mbwa kurudishwa kijijini kwenu ila sitaki kuishia na mwanaume kisa tu mtoto!”


Niliamua kumuambia, nilijua fika kuwa hawezi kumuambia chochote mume wangu kwani ilimaanisha yeye kuachika. Alinibishia na kuntukana, aliniaambia nina wivu lakini nilimuambia.


“Mimba haifichiki, mimi naondoka lakini sihami mji, kazini kwangu unapajua na usingekua mchawi ningekuleta na ninapo hamia hivyo, subiri miezi miwili mitatu karibu kunitembelea tumbo litaonyesha, ila kwa sasa wewe endelea kubembelezea ndoa ila najua mume wangu akijua mimi ni mjamzito utafukuzwa kama Mbwa!”


Tayari nilishamaliza kupaki vitu vyangu, wakati huo mume wangu alikua asharudi, nilimuaga kisatarabu kabisa na kuondoka zangu. Mpaka naondoka Angel alikua haamini, zile mbwembwe zake zote ziliisha nadhani suala la kumuambia kua nina mimba lilimchanganya. Hakua na uhakika ila kwakua alikua anajua namna mume wangu anavyonipenda basi aliumiza kichwa. Niliondoka na kwenda kutafuta chumba kwenye Hoteli moja na kukaa nikijipanga kutafuta sehemu ya kuishi moja kwa moja.


***


Baada ya kuondoka nyumbani ndipo niliamua kuongea na Victor, nilimuambia kuhusu ujauzito wangu na wa Angel, alionekana kushtuka sana, ni kama alikua hataki mtoto. Ni kitu ambacho nilijua kitatokea kwani si mtu wa kubeba majukumu, nilikua namsikia mara kwa mara alivyokua anasumbuana na wanawake wengi aliozaa nao hivyo nilimhakikishia kuwa si yake ingawa bado hakuamini.


“Daa afahali maana na mimi nina bahati mbaya na wanawake, kila ninayetembea naye Mimba! Siwezi hata kuwalea!” Nilimuangalia bila kummaliza na kumhakikishia si yake.


“Mimi nina akili, kwani unafikiria sijui namna unavyohangaika nao, hivi kweli mimi ndiyo nizae na wewe. Kila siku za hatari nilikua nakupiga chenga, ni ya mume wangu nadhani ni Mungu tu alikuahajaamua kutubariki.” Nilimuambia, hata mimi sikua na amini hayo maneno kwa asilimia mia ila kwa tabia za Victor ilikua ni bora tu kuamini kwani mume wangu angekua Baba bora kuliko yeye.


Pamoja na kwamba niliendelea kumhitaji lakini baada ya kupata ujauzito Victor alijiweka mbali kabisa na mimi. Aliacha kupokea simu zangu, aliacha kuwasiliana na mimi na kwa muda tulipotezana, nilimmiss lakini hata mimi niliona ni bora tu iwe hivyo. Hakua akipenda watoto, suala la kukimbia mimba kwake ilikua kawaida, hivyo sikuona ajabu. Pia sikua nikimhitaji sana kwa wakati huo, akili yangu niliielekezea kwa mwanangu mtarajiwa tu, sikutaka kuumiza kichwa na watu ambao hawaeleweki.


Kwa upande wa mume wangu nilijaribu kumpotezea, hata yeye alfanya hivyo mwanzoni, lakini baada ya kama miezi miwili alianza kunitafuta. Alitaka tu kuongea na mimi, wakati huo tumbo lilishakua kubwa hivyo nilimkwepa, alitaka kuja kazini kwani hakua akifahamu ninapoishi lakini nilimkatalia na kumuambia siwezi kuwasiliana na yeye labda kama ni mambo ya Talaka. Kila nilipotaja neno talaka alikasirika na kunigeuzia kibao mimi.


“Inamaana ushanisahau, kwahiyo ushafikia kuwaza kuachana? Inamaana ushapata mwanaume mwingine, kumbuka wewe bado ni mke wangu na bado nakupenda!” Mara kwa mara aliniambia hivyo, nilishindwa kumuelewa kwani yeye tayari alikua akiishi na mwanamke mwingine tena alikua na mimba yake.


“Haya ni mamnbo ya kupita tu, kwani si kuna watu wanazaa na kulea watoto, mimi bado nakupenda na sitaki uwe na mtu mwingine.”


“Sina mpango wa kuwa na mtu mwingine kwa sasa lakini hata nikitaka huwezi kunizuia, ushanifukuza hivyo endelea na maisha yako.” Mara nyingi mazungumzo yetu yalikua yakiishia hivyo kwa mimi kumkatia simu.


Alizidisha kunipigia simu na kutaka kuniona kitu ambacho kilizidi kunipa wasiwasi, si kwamba nilikua namuogopa lakini sikutaka stress kwa wakati huo. Kila mara nilikua nasoma namna ambavyo wanawkae hupoteza watoto kwaajili ya mawazo hivyo sikutaka hilo linitokee. Kwa namna mume wangu alivyukua akiongea alionekana kua ana mawazo sana, Mama yake alikua akimchanganya kwani alishakuja kuishi naye.


Baada ya mimi kuondoka Mama yake aliamini kua ninaweza kurudi hivyo alitoka kijijini na kuja kwa mwanae ili kumsaidia ujauzito na kumsubiri mjukuu wake. Hali ile ilimchanganya mume wangu hakua na raha na kila mara alikua akiniambia mimi mambo yake mpaka nilipoona anazidi, nilimuacha apambane na hali yake. Nilijua zaidi kua hana raha kwakua mara kwa mara Angel alikua akinpigia simu na kunitukana akiniambia kua nikubali kuachika na nisihangaike na mume wake.


Alishaanza kumuita mume na alikua akiona meseji ambazo mume wangu alikua akinitumia kunijulia hali kitu ambacho kilimkera. Siku moja nikiwa ofisini, nakumbuka mimba ilikua na miezi mitano na ilishakua kubwa ya kuonekana, niliambiwa nina mgeni wangu na kuangalia alikua ni Angel nadhani alikuja kunisuta lakini baada ya kuona tumbo langu alishindwa hata kukaa.


“Kumbe kweli una mimba?” Aliniuliza kwa mshangao, nilimuona namna ambavyo kanywea, alikua mpole ghafla.


“Anajua?” Aliniuliza akimaanisha mume wangu, lakini mimi simkumjibu  nilimuacha aendelee kuhangaika.


“Umeshamuambia? Una mpango wa kurudiana naye? Ni yakweke au mwanaume mwingine? Mbona mlikaa muda mrefu hivyo bila kuzaa, atakua sio yeye!” Aliniuliza maswali mengi ambayo yalizidi kunichefua, yeye pia mimba yake ilishakua kubwa lakini alijua fika mimi ndiyo napendwa hivyo mume wangu akijua kua nina mimba basi atarudi kuwa Dada wa kazi.


Sikutaka kuongea naye, nlimshika na kumtoa nnje na kumuambia sina shida na matapishi kama hawana furaha ni wao hivyo aniondokee. Aliondoka kweli lakini alinichefua, kichwa kilikua kinauma kwa mawazo, nilitaka kuongea na mtu ambaye anafahamu maisha yangu. Ndugu zangu walijua nimetengana na mume wangu lakini hawakujua kila kitu, nilihitakji mtu mmoja ambaye anajua kila kitu hivyo sikua na namna zaidi ya kwenda kwa Victor.


Ingawa alishanitega flani lakini nilihitaji rafiki, nilimpigia simu kwa namba nyingine kwani mara nyingi hapokei simu zangu. Nilimuuliza yuko wapi akaniambia nyumbani, nikamuambia kama ana mwanamke amatoe kwani ninaenda kichwa kitapasuka nahitaji mtu wa kuongea naye.  Sikumpa chaguo, haukua ni mjadala nilitaka kwenda na nilienda kweli. Nilifika na kuanza kuongea, akili yangu ilikua imechanganyikiwa na nilihitaji mawazo yake.


Ninachompendea Victor nikua anajua kusikiliza na ukiwa na tatizo basi anajua ni kitu gani cha kukuambia na kama miujiza unaona tatizo lianisha. Kweli niliongea naye na alinisikiliza, akanifariji na nilisikia ahueni kidogo. Ilikua jioni jioni na kwakua nilikua naishi mwenyewe niliamua kupika pale ili nikiudi nyumbani nikulala. Victor anaishi nyumba nzima ni kwake kajenga hivyo nilienda jikoni na kuanza kufanya mambo.


Nikiwa huko nilisikia mlango unagongwa na Victor alikuja kunichukua, akidhani ni mmoja wa mwanamke zake aliniambia nikajifiche kwenye chumba cha wageni ambacho mwanamke asingeingia kwani hakutaka maneno. Kwa hali niliyokua nayo nilikubali kwani sikujua ni nani, nisingetaka itokee vurugu kama ni mwanamke wake. Niliingia harakaharaka na kujifungia kwa ndani, sikutaka shari kwa wakati huo, baada ya kuona kuko salama Victor alienda kufungua mlango.


Sikujua ni nani mpaka niliposikia sauti niliyokua nikiifahamu, ilikua ni sauti ya mwanamke.


“Leo nimemuona mke wake, ana mimba, najua ulisema kua hutaki mtoto lakini akijua kua mkewe ni mjamzito atanaicha, mimi sina kazi nikirudi kijijini na mimba wakati wazazi wangu wanajua niko chuo unafikiri itakuaje? Sitaki nitabidi unioe, siwezi kufukuzwa!”


Haikua sauti nyingine, Alikua ni Angel, kule ndani nilihisi kuchanganyikiwa, Angel alikua nyumbani kwa Victor akimluambia kuhusu mimi na mimba yangu huku akitaka kuolewa na Victor!


ITAENDELEA…


SIMULIZI; MIMI, ANGEL, MAMA MKWE NA MUME WANGU KATIKATI—SEHEMU YA TANO


(ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE; Baada ya kukorofishana na Angel niliamua kwenda kwa Victor ili kuongea naye, nilitaka tu kutuliza akili, lakini nikiwa pale mtu alikuja kugonga. Ghafla nasikia sauti ya Angel akizungumzia kuhusiana na Mimba yake ambayo alipewa na Victor. ENDELEA… Kama hukusoma Sehemu ya Nne hembu hakikisha una like ukurasa wangu Iddi Makengo usipitewa na chochote)


Kule ndani nilikua na hisia za namna mbili, kwanza nilikua nasherehekea kua ile mimba haikua ya mume wangu, kwa namna flani nilifurahi, lakini kabla furaha yenyewe haijakaa sawa nilikumbuka mimba yangu. “Hata hii inaweza kuwa ni ya Victor!” Hapo nilijikuta na nyong’onyea, pamoja na kukaa kwenye ndoa kwa muda mrefu bila mtoto lakini kila siku niliamini tatizo ni langu. Nilipoenda kupimwa mara moja na kuambiwa kizazi kiko mbali, nilipoanza kupewa dawa hakukua na haja ya mume wangu kupimwa tena.


Baada ya Angel kuja na kupata ujauzito nilijipa moyo kuwa kwakua mume wangu kaweza kumpa mimba Angel basi hata mimi mimba itakua yake. Ingawa tulishaachana lakini bado nilikua nampenda, sikua na mipango ya kurudiana naye lakini nilitaka sana mtoto wangu kua wake kwani moja kwa moja nilijua kua atahudumia. Mbali na kuhudumia nilijua atakua Baba bora, si kama Victor ambaye tabia zake alikua anazijua mwenyewe.


“Kaa utulie kwanza, huna haja ya kupaniki kwani kakuambia kua anamrudia mke wake?” Victor alijaribu kumtuliza.


“Hapana lakini akijua kua ana mimba yake basi atamrudia, mimi sitaki kusubiri kuachwa, mimi bado mdogo, nimeacha chuo kwakua Mama yake aliniahidi vitu vingi, sasa unafikiri nitarudije nyumbani wakati wanajua nishamaliza chuo na kuanza kazi?”


Angel aliongea kwa uchungu. Victor alinyamaza kimya kwa muda, kwa ninavyomjua alikua anatafuta uongo wa kumuambia.


“Saaa sasaaa…” Alishikwa na kigugumizi.


“Sasa nini, mimba hii yako, wote tunajua hilo, mimi sitaki chochote, kwanza wewe hujaoa, na yule ni mume wa mtu. Wewe si ulisema unanipenda, si kila siku ulikua unaniambia niachane naye ili nije kuishi na wewe! Mbona sasa unatetemeka.”


Kimya kidogo kilitawala, kidogo nilianza kumuonea huruma binti wa watu kwani nilijua kwa victor kagonga mwamba. Ingawa sikua na mpango wa kumuambia mume wangu chochote lakini nilijua ipo siku atasikia, atajua na atataka turudiane.


“Kwanini usitengeneze maisha yako? Usiwe na kitu chako mwenyewe!” Victor alishauri na nilijua kabisa ni uongo mwingine.


“Kitu gani, kivipi mbona sielewi?” Angel aliuliza kwa mashaka.


“Kitu kama biashara au urudi chuoni, ukamalize elimu yako…”


“Nitarudieje chuo wakati niliacha sikuahirisha hata mwaka. Isitoshe nina mimba unafikiri itakuaje?”


“Mimba si unatoa tu, mimi nafahamu Daktari mmoja hata kama mimba ni ya miezi nane unatoa tu!”


Pamoja na kumchukia yule binti lakini ushuri wa Victor ulinichefua kabisi, nilijua atamruka na kumkimbia lakini si kwa namna ile. Nilitamani kutoka pale na kumshauri yule binti lakini nilikumbuka pale si kwangu hivyo kuonekana pale mchezo wote ungejulikana. Nashukuru Angel hakukubaliana na lile wazo, alianza kutukana, wakapandishiana mpaka basi, alimuambia nilazima atalea mtoto na kama hataki watafikishana mbali.


“Lilikua ni wazo tu katika kutaka kukusaidia, lakini kama hutaki basi mimi nitalea mwanangu. Lakini sasa hivi hembu subiri mambo yatulie, jamaa yako ni kama bosi wangu pale ofisini hivyo kama akijua kua nimetembea na mke wake, mwanamke ambaye anampenda basi itakua shida. Nitafukuzwa kazi na kulea mtoto sitaweza….” Alianza kujitetea.


“”Hawezi kukufukuza kazi!”


“Wewe hujui tu anavyokupenda, hivi unajua tatizo ni yule mwanamke wake. Kila siku kazini analalamika kua anataka kumaucha lakini hawezi! Yule mwanamke si mtu, kashamtengeneza vyakutosha, hivi unafikiri ni mwanaume gani atakaa na mwanamke kwa muda owte huo hazai! Unafikiri Mama yake asingeingilia kati jamaa angepata mtoto alishatengenezwa yule.”


Bila aibu Victor alianza kuniponda, alijua niko ndani lakini niliona anamchota akili binti wa watu.


“Kivipi, hakuna uchawi anampenda sana mkewe, hivi unajua mara nyingi hata tukifanya mapenzi anamtaja!” Angel alimkatalia.


“Unaona, huko ndiyo kutenegenzwa ninako kuzungumzia, mimi namjua jamaa tangu zamani, alikua Malaya sana mimi cha mtoto ila baada ya kumpata huyo mwanamke ni kama alipata laana flani, mwanamke alikua mbinafsi na madawa yake ndiyo yalimfanya asizae. Hivi wewe hufikirii, umekuja tu mwanamke kapata mimba ni mambo ya dawa, mbona kila mtu ofisini anajua. Wewe ni kama umeharibu dawa zake, anakupenda lakini tatizo hawezi kusamahau yule mwanamke kwakua katengenezwa!”


Victor alimjaza maneno mpaka basi, kila kitu kiliangukia kwangu, alimuambia hakuna upendo na kama anataka ndoa basi akomae kwani yeye atamtafutia mtalaamu. Alimuambia asiwe na haraka kwani kama wakifanikiwa kutoa vitu nilivyomuewekea mume wangu upendo wote unarudi. Cha ajabu Angel alikubali nilimuona kabisa anaamini kwani mara kadhaa alikua akiongezea vitu, mara hata mimi nilimkuta anafanya hivi, nilikuta hiki, nikakuta kile. Victor alifanikiwa kumtuliuza mpaka akaondoka akiwa na mawazo ya kupambana na mimi kishirikina.


***


“Ulitaka nisemeje sasa si unaona ameondoka?” Ndiyo kitu cha kwanza alichoniambia Victor baada ya kutoka chumbani, nilimuangala bila kummaliza, hakuoesha wasiwasi wowote kwake ilikua ni kama kitu cha kawaida tu. Nilimuangalia kwa jicho la hasira bila kusema chochote.


“Wewe si ulikua unanibania, nilianzana naye hata kabla yako!” Alianza kunielezea, nilitamani kumuambia nyamaza, lakini moyo ulitaka kujua ni lini walikutana mpaka kufikia hatua ya kutuchanganya. Niliamua kunyamaza kimya na kumuacha aendelee kujielezea yeye mwenyewe.


“Mara ya kwanza ilikua ile siku ya harusi, tulikaa meza moja nikaona yuko karibu sana na mume wako. Nilijua kuna kitu kinaendelea kwani nilishasikia tetesi ofisini kua mnagombana na mume wako. Tulianziana hapo, nilijua kama ni kitu cha siku moja lakini aliniganda na kama unvayojua mwanamke mwenyewe hakua na gharama hivyo nisingeweza kumuacha!” Bado alizidi kunichanganya, kwa namna alivyokua anaongea ni kama walilala wote siku ile ile.


“Inamaana ulilala naye siku ile ile?” Niliuliza kwa mshangao, sasa sikua na hasira, nilitaka tu kujua Victor ni mwanaume wa namna gani, aliangalia chini kama anaona aibu, akatingisha kichwa kukubali.


“Wewe mshenzi kweli ilikuaje?”


“Unataka kujua kila kitu?”


“Ndiyo kila kitu, nataka nijue ushenzi wako!” Nilijibu kwa hasira nikijifanya kukasirika, lakini ukwekli nikua kwa wakati huo ni kama nilikua naangalia movie moja ya mapenzi na alikua anataka kuimalizia shemu nzuri.


“Tulikua tumekaa kama watu watano hivi kwenye meza moja, mimi nilikua nimeangaliana na Angel na mume wako alikua pembeni yake, walikua wamekaa kama wapenzi.” Alianza kuelezea.


“Kwakuangalia mume wako alikua naona aibu kukaa pale, unajua ofisini wanamuona kama mstarabu flani hivi na wanajua amekuoa, pamoja na kua kulikua na tetesi kua hamko vizuri lakini mumeo anajiheshimu. Hata siku ile hakupanga kutoka na Angel ni Mama yake alimpia simu, Angel aliona kadi za harusi na kwakua wanaongea kila kitu na Mama mkwe wako basi alimuambia ndipo akalazimishwa waende wote.” Hapo ndipo nilipata maelezo ni kwanini alindoka na kuniacha mimi wakati tulishapanga kwenda pamoja.


“Katika ile meza kulikua na watu watano, mumeo na Angel, rafiki yetu mwingine na mkewe pamoja na mimi, wote walikua na wake zao kasoro mimi. Kwakua kila mtu alikua anakujua wewe na mumeo walijua moja kwa moja Angel ni mgeni wangu kwani wanajua nabadilisha watu kila sherehe. Lakini Angel alianza kuonyesha manjonjo, katika sherehe alikua akichata na Mama mkwe wako hivyo alikua anamuambia aonyeshe mapenzi ili ofisini wajue kua umeachika.


Kweli alianza kummiminia vinywaji, kujifanya kalewa na kumlalia lalia na vitu vingine. Ile hali ilimkera mume wako, alinitumia meseji tutoke nnje, kule nnje aliniambia ukweli kuhusu ishu yenu na kuniambia watatoka kucheza na Angel na wakirudi tu nibadilishe siti ili mimi nikae karibu na Angel na yeye akae siti  yangu kwani ilikua mbali kidogo.


Sikuona shida kwani hata mimi nilishamtamani na nilikua naangalia nafsi tu ya kumtongoza. Tukafanya hivyo, mwanzo Angel alikasirika lakini kutokana na watu alishindwa kuongea. Nilianza kumchombeza chombeza na kumsifia sifia, kama unavyojua mdomo wangu. Tukawa tunakunywa bia na katika kucheza tena nilitoka naye na hapo ndipo nilimtongoza moja kwa moja, nilimuambia tukutane choo cha nnje. Ile sehemu ambayo tulika tumekaa alikuja na tukamaliza mchezo usiku ule ule.”


Hapo niliishiwa pozi kabisa, yaani anatomngozwa siku moja na kukubali.


“Inamaana wakati nakuja pale ulishafanya uzinzi wako? Au ndiyo maana hukutaka kulala na mimi?” Alinyamaza na kucheka nilielewa, kidogo nilijisikia kichefuchefu.


“Mwaname mchefu wewe! Kweli wewe ni shetani!”


Alizuga na kutaka kuipotezea ile stori lakini mimi bado nilikua sijaelewa kuhusu mimba kwani sherehe ilikua muda mrefu sana.


“Baada ya pole tuliendelea kuwasiliana, unajua Angel bado mtoto mdugo, hivyo kwa mumeo alikua anahitaji pesa tu na Mama mkwe wako alimuahidi pesa nyingi tu, alijua kuwa kama akiolewa yeye basi kila kitu cha mumeo angekipata. Lakini alikua haenjoy chochote kwani mumeo ana mambo ya kishamba kishamba, wewe si unamjua kwangu yule binti alifuata bata hivyo kwakua sihongagi alikua anakuja kuzitumia anazochuna kwa mumeo.


Baada ya pale alikua anakuja mara kwa mara kwangu, si unajua na mimi kazini siko bize kivile hivyo mchana wote nyie mkiwa kazini alikua anakuja hapa.


“Inamaana ulikua unamleta hapa? Mbona na mimi ulikua unanileta hapahapa!” Niliuliza kwa hasira, nilihisi kanikosea heshima lakini nilipofikiria mtu mwenyewe niliishia kucheka tu.


“Sasa hivi ana hahahaha kuhusu chuo, aliacha chuo kwa kudanganywa na Mama mkwe wako, alikua anaingia mwaka wa tatu Mama mkwe wako alimuambia anakuja kwa likizo tu akimaliza anaondoka. Lengo lilikua abebe mimba ya mume wako kisha arudi chuo lakini naona ilishindikana, alipotaka kuondoka Mama mkwe wako alimdanganya kwa vihela, akamuambia atamtafutia kazi kwa ujinga wake akaacha chuo.”


“Mungu wangu, kwahiyo na wewe ukamruhusu kuacha chuo?” “Hapana, mimi nilijua baadaye sana, baada ya kupata mimba alinifuata na kuniambia anajua mimba ni yakwangu. Nikamkwepa lakini ni kama alitaka nimuoe mimi, alidai kwamba ananipenda mimi nikamshauri atoe ndiyo alipoona sieleweki ikabidi akamuambie mumeo kua ni yakwake lakini alishaniambia mimi kua ni yangu. Hapo ndipo aliniambia kua kumbe aliacha chuo kwasababu ya mume wako.”


“Lakini hii mimba sio ya kwako, hii ni ya mume wangu najua kabisa, najua tarahe zangu sijawahi kutembea na wewe siku za hatari!” Nilijisemea kwa hasira, moyoni nilikua najua fika itakua ya Victor lakini kwa gharama yoyote sikutaka ajue kabisa kuwa ni yake.


“Najua sio yangu, mbona hata mimi nikimpa mwanamke mimba najua, huwezi kunisingizia!” Victor alinijibu kwa upole, nilijua fika ananipa moyo lakini sikua na namna. Nilikaa kama masaa mawili baadaye nikaamua kuondoka, sikuendelea kupika tena lakini sikutaka kuonekana nikitoka kwa Victor, nilisubiri mpaka kagiza kakanaingia ndiyo nikatoka.


Akili yangu ilikua inawaza mambo mengi, ingawa sikua namhofia mume wangu lakini sikutaka ajue kama ile mimba si yake. Alikua na hamu sana ya mtoto na kwa hali ilivyokua Angel ni kama alitaka mkumuacha hivyo angejua mimba ya Angel si yake na kuumia sana na angeumia zaidi kujua na mimi nina mimba ya mtu mwingine. Pamoja na aliyonifanyia bado nilimuonea huruma na nilikua nampenda.


Kwa bahati nzuri siku ile sikuenda na gari langu kwa Victor kwani Angel alikua analifahamu, angeliona angejua kua na mimi naenda pale. Nilitoka taratibu na kuvaa viatu vyangu ambavyo vilikua pale nnje. Sikutaka Victor anisindikize, ile natoka tu nilisikia sauti nyuma yangu, kuna mtu alikua kajibanza pembeni ya drisha.


“Nilijua tu huyu Malaya yuko na mwanamke, nilipoona viatu vya kike nikajua tu kuna mwingine, sikujua ni wewe! Makubwa! Mke mwenzangu kila sehemu! Nawewe huku ulileta mimba yako kwa Baba yake!” Ilikua ni sauti ya Angel, kumbe muda wote nikiwa ndani alikua nnje akitusikiliza!


ITAENDELEA..,.


SIMULIZI; MIMI, ANGEL, MAMA MKWE NA MUME WANGU KATIKATI—SEHEMU YA SITA


(ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO; Nikiwa pale ndani nilijua kua Angel aliacha chuo ili kuja kubeba mimba ya mume wangu. Nilikaa pale ndani kwa muda kisha kutoka, pale nnje wakati naondoka nikakutana na Angel ambaye alikua anasikiliza kila kitu nilichokua nikiongea na Victor akiwa dirishani. ENDELEA… Kama hukusoma sehemu ya Tano, Bonyeza hapa Iddi Makengo


Kusema kweli nilishtuka sana kumuona pale, alikua anaongea mfulilizo, kwanza yeye mwenyewe alionyesha kuwa na hofu kua najua kua ile mimba si ya mume wangu. Kila mara aliishia kusema “Ukisema na mimi nitasema!” nilimuacha akabwabwaja kwa muda mrefu kisha nikamuuliza kama kamaliza. Alinyamaza kimya bila kujibu chochote, ingawa nilikua na hofu flani lakini nilijua kama nikimnyenyekea na kuogopa atanipanda kichwani.


“Sikiliza mdogo wangu…” niliongea kwa utaratibu kabisa kama vile nambembeleza lakini kwa kumpa ushauri.


“Mimi sijali kama akijua mtoto si wake au la? Labda nikuulize, hivi kuna siku ushasikia nikisema mtoto ni wake? Au ushaniona hata siku moja nikisema nina mimba yake?” Nilimuuliza, hakujibu alibakiia kimya tu.


“Basi kama hujawahi kunisikia unatakiwa kujua, najua mwenyewe Baba wa mtoto na wala halimhusu huyo mwanaume wako au hao watu wengine unaowaabudu. Nina kazi yangu na naweza kumlea mwanangu hivyo kama ishu ni kumuambia wala mbona huna haja ya kuchelewa…”


Niliongea huku nikitoa simu mfukoni, nilipiga namba flani na ilipopokelewa nilimuambianilionge. “Mke wako kuna kitu anataka kuongea na wewe, nadhani kuna siri anataka kukuambia hembu msikilize..” Nilimaliza kisha nikampa simu Angel ili aongee na yule mtu. Alinywea, hakuipokea, nilichukua simu na kumuambia yule mtu “Naona anaogopa utamuuliza kama yuko wapi usiku huu na mimba yake.” Nilikata simu na kumuaga, kisha nikamuambia asipate shida siku akijisikia kumuambia mwanaume wake kua mimba si yake amuambie kwani mimi sijawahi kumuambia kua nina mimba.


Alinywea akimini kabisa kuwa mimi siogopi chochote, ingawa nilikua na hofu na sikutaka mume wangu kujua kua nina mimba lakini nilijua fika hawezi kuongea chochote. Hata namba niliyopiga ilikua ni ya rafiki yangu wa kike, sikua na mpango wa kumpa aongee naye ingawa nilijua hawezi kusema chochote. Niliondoka na kuwaacha nnje, Victor alikua kasimama tu anatuangalia hakusema chochote.


***


Sikutaka tena mawasiliano na mume wangu, nilimblock kabisa na kumuambia simtaki abaki na mke wake. Nilifanya hivyo kwani nilijua kua kama akinirudia basi Angel atakasirika na kuongea kila kitu, sikutaka hilo litokee, kwa wakati ule nilikua namuonea sana huruma mume wangu kwani niliamini moja kwa moka yeye ndiyo mwenye matatizo hivyo suala la kutokua na mtoto litamuumiza sana.


Hali ilitulia kidogo, mume wangu alikubaliana na hali halisi, lakini siku moja, wakati huo nikiwa na mimba ya miezi nane nilipigiwa simu na rafiki yangu mmoja. Ni rafiki wa muda mrefu ambaye tulisoma wote Mlimani, yeye alisomea mambo ya ardhi na alikua kaajiriwa Manispaa. Ilikua ni muda hatujawasiliana, si kama tumegombana lakini mambo ya ubize wa kazi, mara kadhaa tulikua tunasalimiana hasa tukikutana sehemu za kazi.


“Nini kimewakuta, najua sipaswi kuuliza lakini mbona mume wako anatoa nyumba kama zawadi?” Lilikua ni swali lake la kwanza mara tu baada ya kusalimiana. Nilishtuka kidogo na kumuuliza nyumba gani?


“Si pale kwenu, ile ya Kimara mnapoishi, mmeuza mnataka kukwepa kodi au nikweli mume wako anaitoa kama zawadi?” Aliniuliza swalia ambalo lilizidi kunichanganya.


“Sikuelewi kwanini mume wangu atoe zawadi bila kunishirikisha wakati nyumba tumejenga wote?” Nilimuuliza kwa mshangao.


“Hata mimi sijui lakini mume wako alikuja ofisini na kabinti kadogo kana mimba na kusema anataka kubadilisha umiliki kutoka kwake na kumpa yule binti, sasa nikawa na wasiwasi kwani ni binti mdogo asije akawa ni mchepuko na wewe unapigwa?”


Akili yangu moja kwa moja ilienda kwa Angel, aliponielezea nilijua tu ni yeye na kwakua nyumba ilikua na jina la mume wangu tu ingawa tulijenga wote basi mimi hata sikuhitajika kufika kusaini chochote. Kwakua yeye ndiyo alikua kila kitu pale ofisini nilimuomba awacheleweshe kidogo ili tuonane na nimuelezee mchakato mzima. Alikubali, lengo langu lilikua ni kufuatilia kwanza ili kujua nini kinaendelea.


Lakini kabla ya kufanya chochote rafiki yangu alinipigia simu tena, kuna shamba jingine na viwanja vingine vitatu ambavyo tulinunua na mume wangu tena vikiwa na majina yetu wote wawili mume wangu alikua anataka kumpa Angel.


“Mume wako naona kama kaingia mkenge kwani yule binti kuna kijana anakuja naye hapa. Baada ya wao kuja na kuona mchakato unachelewa yule binti alikuja na Kaka mmoja, wakanipa milioni moja na kuniambia kama naweza kuharakisha vitu vikaenda harakaharaka ndani ya mwezi mmoja.”


Nilishtuka na kujiuliza ni nani huyo anataka kuharakisha mambo na Angel. Nilimuuliza na aliponielezea namna alivyo haikunichukua hata sekunde tatu kujua kuwa alikua ni Victor. Ingawa mwanzoni sikutaka kuingila lakini nilijua mume wangu anaibiwa.


“Wanataka kupata kila kitu kabla mtoto hajazaliwa, wameshapanga kumuibia mume wangu!” Nilijikuta naropoka, rafiki yangu yule hakuelewa kitu ndipo nilimuomba tuonane nikamuelezea kila kitu.


“Pole sana Shogaa sasa utafanya nini kwani kila kitu pale mmechuma wawili na kama unvyosema ni kweli wakishapata vitu vyao basi mumeo anaachwa, nina uhakika atakuja kwako na wewe ndiyo utaubeba huo mzigo.”


Kusema kweli nilikua nimechanganyikiwa, nilimuomba anipe muda ili kuchunguza na kujua nini kimetokea mpaka Victor na Angel wanafanya kazi pamoja na nini kimetokea mpaka mume wangu anakubali kutoa vitu vyake kijinga kijinga. Moja kwa moja nilijua lazima Mama yeke anahusika kwani mume wangu kwa Mama yake alikua kama mtoto, hakua na maamuzi yoyote hivyo kabla ya kuongea naye ilikua ni lazima kujua nini kinaendelea.


***


Kaktika maisha kuna watu ni ndugu wa kuzaliwa na wengine ni ndugu kwa kukutana tu na kuishi pamoja vizuri. Mmoja wa watu ambao walikua ni kama ndugu yangu alikua ni Eliza au Mama Prisca, huyu alikua ni mke mwanzangu, kwa maana ya mke wa shemeji yangu, mume wake hakua akizaliwa tumbo moja na mume wangu lakini kwa namna tulivyokua tukiishi basi tulikua karibu sana.


Yeye alikua akiishi Moshi hivyo pamoja na kujua kua nimetengana na mume wangu kwa sababu ya mtoto lakini hakua akijua kua nina mimba. Niliamua kumtafuta kuongea naye, kwa bahati nzuri kwangu nikuwa yeye ni wale wanawake ambao wana taraifa zote. Hata baada ya kuachana na mume wangu yeye ndiyo alikua akiniletea umbea wote mpaka nilipomuambia kistaarabu tu kuwa naumia na sitaki kusikia mambo ya mume wangu.


Nilianza kumpotezea taratibu na yeye alijitenga flani, kama mnavyojua mmbea akitaka kukupa umbea ukamkata ulimi basi huchukia. Niliamua kumpigia ili tu kumsalimia, sikutaka kumuuliza moja kwa moja lakini nilijua tu maneno mawili matatu angesema.


“Vipi Mama mkwe wetu anaendeleaje?” Niliuliza kimitego.


“Si mko naye Dar inamaana hujui kinachoendelea au unanichota tu akili?”


“Shogaa nitajuaje, wewe uko Moshi lakini unajua mengi, mimi ile familia nina hamu nayo basi, hivi kwa waliyonifanyia naweza hata kuwaslimia njiani?” Nilijifanya kulalamika.


“Kweli Shogaa na wewe una moyo sana.”


“Si moyo sasa ningefanya nini, mwanaume nimekaa naye miaka, nimemvumilia katika umasikini lakini kaja kuniacha tushapata. Tumechuma vingapi, nyumba ngapi tumejenga, tumenunua viwanja lakini wala, kanifukuza kama Mbwa kisa sizai sasa huyo ni mtu wa kutaka kumjulia hali kweli…” NIlijisemesha huku nikitaka kulia, nilifanya hivyo makusudi nikijua atafunguka tu.


“Shogaa tena nikuambie, Mungu analipa hapahapa duniani. Huyo binti waliyempata sasa, anavyowaendeesha! Nakuambia hivi unajua Mama kwe wako ni kama alimdanganya, alimuachisha chuo ili kuja mjini kubeba mimba sasa binti kabeba, walidhani ni mjinga watamuendesha kama wewe, binti kagoma anasema mpaka apewe nyumba  ndiyo anzaa. Si wakadhani anatania siku ya siku Mama mkwe kakuta vidonge vya kutolea mimba mbona kahaha!


Shogaa walikudhulumu lakini mali zote zinachukuliwa na ninavyosikia sidhani hata kama ile mimba ni ya mume wako, mimi sijui chochote lakini shemeji zako washaanza kuwa na wasiwasi. Kaka yako kaambiwa lakini unavyojua hapumui na Mama mkwe ndiyo hivyo anataka mjukuu kwa gharama yoyote hivyo kila kitu anachotaka yule binti anapewa. Wewe kaa pembeni usubiri uone namna dunia inavyowafunza!


Aliniambia umbea mwingi ambao sikua na shida nao, sasa nilijua ni kwanini mume wangu yuko tayari kutoa kila kitu. Kwa namna ule mpango ulivyokua umepangwa nilijua fika kuwa Victor anahusika, nilijua Victor ni shetani lakini si kwa kiasi kile. Ilikua ni lazima nifanye kitu kabla mume wangu hajaumizwa, sikutaka kumuumiza kuhusu mtoto lakini nilijua kuwa nilazima tu ataumia kwani Angel akishajifungua na kupata mali zote atamuacha.


Lakini pia zile mali zilikua ni zangu, tulichuma wote nilimkuta akiwa na vitu vichache tu na vingine vyote tulichuma pamoja, nilijua kabisa kama nikiacha vikachukuliwa tungekosa wote. Ilikua ni lazima kufanya kitu hapo ilibidi akili ichanganye kwani sikutaka kuonana na mume wangu na wakati huo huo nilitaka ajue kua mtoto wa Angel si wake.


Kitu pekee ambacho ningekifanya ilikua ni kumfanya mume wangu awafumanie, pamoja na kujifanya mjanja lakini nilikua namjua vizuri Victor, anapotaka kitu kutoka kwa mwanamke basi humuweka karibu sana. Mara nyingi nilipokua naenda kwake nilikua siendi kwa Gari yangu ili kuepuka kuonekana, nilikua naenda kwa Bajaji, nilikua na dereva Bajaji wangu ambaye niizoeana naye, huyo ndiyo niliamua kumtumia, alinisaidia kuchunguza mpaka kujua siku ambazo Angel anakua nyumbani kwa Victor.


Pamoja na kwamba Mama mkwe alikua akiishi naye lakini mchana mara nyingi alikua anatoka na hakujali, mimba ilimfanya kuwa na kiburi na kufanya mambo bila kuulizwa, kwa hamu ya mjukuu Hata Mama mkwe alikua hana sauti juu yake. Kazi kubwa ilikua ni kumpeleka mume wangu nyumbani kwa Victor. Hiyo ilikua ngumu kidogo lakini baadaye nilikuja kugundua kuwa sihitaji kumpeleka mume wangu kule nahitaji kumpeleka Mama mkwe wangu ambaye yeye ilikua ni rahisi sana.


Yeye ndiyo alikua kama mfanyakazi mule ndani hivyo alikua akitumia Bajaji kwenda mjini, kwakua Bajaji niliyokua naitumia ilikua inapaki upande wa pili wa barabara lilikua ni suala la kusubiri wakati tu anatoka na kumpeleka.  Mama mkwe wangu alipopanda Dereva alianza kumpeleka, akashika njia nyingine kabisa na ya sokoni, Mama mkwe kuona vile aliuliza ndipo Dereva alimuambia.


“Mama ngoja kuna sehemu nakupeleka, kuna vitua mbavyo mwanao anafanyiwa na siwezi kuvukubali. Mimi ni dereva Bajaji na mwanao kanisaidia sana kwenye maisha hivyo siwezi kuona anataka kudhulumiwa nikanyamaza. Kuna mambo mengi nasikia lakini siwezi kukuambia yote nataka uone mwenyewe.” Dereva alimuambia, Mama mkwe wangu hakua na wasiwasi sana kwani yule Dereva alikua kama dereva wa familia, hata yeye likua anamfahamu.


Hakumuambia moja kwa moja kitu ambacho alitakiwa kuona, lakini kwakua alikua na uhakika Angel yuko kwa Victor na tayari Victor yuko nyumbani alitaka ajionee mwenyewe. Walifika na Dereva alimuambia agonge mlango, nyumba haikua na geti ilikua imezungushiwa tu uzio wa ukuta lakini geti lilikua bado halijawekwa. Mama mkwe aliingia mpaka ndani, kisha kwenda kugonga mlango bila kujua alikua anatakiwa kuona nini.


Walifika na Dereva alimuambia agonge mlango, nyumba haikua na geti ilikua imezungushiwa tu uzio wa ukuta lakini geti lilikua bado halijawekwa. Mama mkwe aliingia mpaka ndani, kisha kwenda kugonga mlango bila kujua alikua anatakiwa kuona nini. Aligonga kama mara mbili hivi na mlango kufunguliwa, hakua mwingine aliyefungua, alikua ni Angel akiwa ammevaa nguo ya kulalia.


Wakati huo alijitahidi kujifunga Khanga ili kujisitiri.  Ile kumuona tu Mama mkwe, Angel alishtuka, alikua kama mtu aliyepigwa sindano ya Ganzi, akaganda pale na kushindwa kuendelea na chochote. Kabla hata hajajielezea alikua anafanya nini Victor alitokea kava Bukta tu.


“Baby ni Nani huyo?”


Victor aliuliza huku akimshika Angel kiuno, alikua bado hajamuona mtu aliyekua kasimama mlangoni kwake.


ITAENDELEA…


SIMULIZI; MIMI, ANGEL, MAMA MKWE NA MUME WANGU KATIKATI—SEHEMU YA SABA


(ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA; Angel na Victor walikua wanataka kumdhulumu mume wangu Nyumba. Nikiwa najua kinachoendelea nilitengeneza mtego ili Angel kufumaniwa, alikutwa yuko nyumbani kwa Victor na nguo ya kulalia huku Victor akimkumbatia. ENDELEA… Kama hukusoma sehemu ya sita bonyeza hapa @iddi makeng


“Hiyo mimba ni ya mwanangu au ni ya huyo mwanaume wako?” Hilo ndiyo swali la pekee ambalo Mama mkwe wangu aliuliza, hakulalamika, hakuongea chochote, alinyamaza kimya, Angel bado alikua anatetemeka, alimsalimia Mama mkwe zaidi ya mara kumi lakini yeye alirudia swali lile lile. Victor baada ya kuona vile alirudi ndani harakaharaka ili kwenda kuvaa nguo. Angel alishindwa hata kuongea, aliona aibu, hakua na kitu cha kujitetea.


Mama mkwe alitoka nnje nakuingia kwenye Bajaji, aliondoka bila kusema maneno mengi kitu ambacho kilizidi kumchanganya Angel, kwake ni bora kama angetukana na kulalamika lakini aliondoka tu kwa hasira, hakujua cha kufanya. Matukio yote hayo nilikua nikifahamishwa na Dereva Bajaji, hata wakati wanaondoka tu alinitumia mseji kuniambia alichofanya Mama mkwe wangu.


Dakika kama kumi hivi baada ya Mama mkwe kuondoka simu yangu iliita, alikua ni Victor na alianza kunitukana, alikua akiniuliza kama najifanya mjanja, aliniambia kila kitu kitakuja kunirudia. Nilijifanya kushangaa na kumuuliza anamaanisha nini huku nikiongea mambo ya mtoto.


“Wewe si umeamua kunichomea kwa mume wako, sasa utajua mimi ni nani?” Aliongea kwa hasira.


“Unamaanisha nini, mbona mimi sijaongea chochote kwa mume wangu. Hivi nitamuambiaje mume wangu kua mtoto si wake wakati hata sijui kama ni wako, isitoshe mume wangu hata hajui kama nina mimba, hii ni mimba yangu nitalea mwenyewe wala sitaki mambo ya Baba!”


Nilijifanya kabisa sijui chochote, kwa mbali nilisikia sauti ya Angel akilia na kujilaumu kwa kuharibu maisha yake. Alikua akimlaumu Victor ambaye naye alikua na wasiwasi wake.


“Nyamaza kwani nilikulazimisha! Hivi unafikiri huyo hanithi wenu akijua kua ninatembea na wewe atanfanyaje! Mshaniharibia kazi washezi wakubwa nyinyi na nataka utoke hapa!” Victor aligomba, badala ya kuwaza kuhusu Angel na mimba yake kumbe alikua akiwazia kazi yake. Ingawa wote walikua wameajiriwa lakini mume wangu alikua ni Bosi wake.


Mbaya zaidi nikua mume wangu alikua ni mtu muhimu katika kampuni kuliko Victor hivyo alijua fika kama akijua na kuongea na mmiliki basi Victor angeondolewa ndani ya sekunde moja. Waliendelea kugombana kwenye simu kwa muda, sikutaka kukata simu niliamua kusikiliza kwa makini ili nijue namna ya kuwaendea kwani sikutaka kabisa niingizwe kwenye yale mambo.


Baada ya mud a wa kama nusu saa hivi walitulia, Victor akanigeukia ili tuongee kwenye simu, alishatulia kidogo na kuniambia kilichotokea.


“Inamaana hujui chochote, si wewe uliyeongea?” Aliniuliza kwa sauti ya chini, nilihisi kama anataka kuniomba kitu hivyo kuamua kujinyenyekeza.


“Hapana! Mimi sijui chochote, isitoshe mimi mwenyewe nina msala wangu, hivi unafikiri nikimchomea huyo binti mimi nitapona? Kumbuka nayeye alinifumania kwako sasa unafikiri nitapata nini kama nikianza kutangaza. Sijasema chochote na wala si mume wangu wala Mama mkwe anayejua kua nina mimba.”


“Sasa nani atakua kamuambia? Inavyoonekana ni kama vile alikuja kufumania, kama mtu aliyekua anajua kitu.”


“Ongea na huyo binti, muulize kama alikua makini. Yule Mama ni mdadisi sana, unajua wanajua mume wangu ni kama hajali hivyo anapenda kufuatilia, hata mimi zamani akija alikua anakagua mpaka simu zangu. Je Angel anapokuja kwako hupanda Bajaji ya moja kwa moja au anaunganisha?” Nilianza kumchota akili.


“Sijui kwani vipi?” Aliniuliza.


“Kama haunganishi Bajaji nina uhakika atakua kamfuatilia, unajua mimi wakati nakuja kwako nilikua makini. Kila nilipotoka nyumbani nilikua napanda Bajaji naenda mjini au nachukua Daladala kisha nikifika mjini nachukua Bajaji ya mjini ambapo hata hawanijui. Lakini kama alikua anachukua Bajaji pale nnje basi ndiyo wamepeleka umbea.”


Victor alinisikiliza kwa makini, kwa namna nilivyokua naongea nilijua fika lazima ataingia laini. Nilimpa muda wa kuongea na Angel na baada ya kama masaa mawili hivi alinipigia tena na kuniambia.


“Huyu mshenzi kaniharibia!”


“Mshenzi gani?” Niliuliza kana kwamba nilikua sijui chochote.


“Si huyu mtoto, kumbe alikua anachukua Bajaji za pale nnje kama ulivyosema na hata Bajaji iliyomleta Mama mkwe wako anaijua  anakuja nayo mara kibao. Sijui nifanyeje namjua Jamaa yako kazini hakutakalika halafu si unajua ni mshikaji.”


Alionyesha kupaniki lakini kichwani nilijua kuwa nishajitoa kwenye lawama.


“Kwani Mama anakufahamu? Anafahamu kua unafanya kazi na mwanae?”


“Hapana, sidhani, mimi nilshawahi kumuona Mara moja alikuja ofisini lakini sidhani kama alishawahi kuniona.”


“Kama ni hivyo basi hakuna shida, nadhani ni wewe kuongea vizuri na huyo mtoto. Kwa usalama wenu ni vyema akanyamaza na asikutaje, Mama anaweza kusema amemfumania na akafukuzwa kuwa mimba si yake lakini hawezi kutaja au kujua kuwa wewe unafahamiana na mume wangu. Cha muhimu nikua maji yashamwagika, yeye ajipange ajue nini chakufanya. Ninavyomfahamu yule Mama nikua huyo binti anafukuzwa sasa akifukuzwa na akifanya ujinga kukutaja basi na wewe kazi huna.”


Nilitaka kuonyesha kama nina wasaidia, kama nawajali na kuwafanya waamini kua wananihitaji mimi sana kufanikisha malengo yao ili na mimi mambo yasifumuke nikaaibika.


“Sasa nifanye nini maana kapaniki, hataki kuongea chochote, hataki kurudi wala nini?”


“Kwani mwanzo si mlipanga kuishi pamoja?” Nilimuuliza.


“Ndiyo lakini mimi siko tayari kuoa na huyu binti sidhani kama atakubali aondoke hapa.”


Nilitafakari kidogo kutafuta suluhu ya haraka, lengo langu ni ili ile ishu iishe harakaharaka.


“Hata mimi sishauri aondoke, chakufanya ni yeye kuishi hapo mpaka atakapojifungua ndiyo mtajua nini cha kufanya. Wote sasa hivi mmepaniki, hembu tulieni, kwa upande wangu nitaendelea kuwaangalia kule kama mambo yanaendeleaje, jamaa hatuwasiliani ila kwa hili nina uhakika atanitafuta na hicho ndiyo ninaogopa kwani atajua nina mimba na mimi sitaki.”


Victor alionekana kunielewa, Angel yeye alikua bado kapaniki hivyo nilimshauri kwanza kurudi nyumbani ili kama ni kufukuzwa afukuzwe kwanza. Hakutaka kuondoka akidhani Victor atamtoroka lakini nilimuambia anafahamu anapofanya kazi victor hivyo kama akimtoroka basi atamfuata kazini na kumharibia. Nilimshawishi sana mpaka akakubali, katika mchakato wote huo nilikua kama Dada mkubwa na wote walinisikiliza.


***


Mama mkwe alikasirika sana, kichwani alishaamini anapata mjukuu kutoka kwa mtoto wake wakwanza, njia nzima akiwa katika Bajaji alikua anatukana tu, alimuuliza Mudi (Dereva wangu wa Bajaji) kua alijuaje kama anachepuka na kwanini kaamua kumuambia. Mudi alimdanganya kuwa alisikia mipango yao ya kumdhulumu mume wangu nyumba hivyo kuamua kuongea na kwakua mume wangu alikua hapatikani sana ndiyo akaamua ampeleke yeye.


“Yule Dada nambebaga sana na juzi alikua anoangea kudhulumu nyumba, mwanao namfahamu ni mtu mzuri alishanisaidia sana. Hata hii Bajaji nilinunua kwa msaada wake, anaweza asinikumbuke lakini mimi niliijenga nyumba yake, nilikua kibarua.”


Mudi alimdanganya, nikweli alikua kibarua wakati nyumba yetu inajengwa lakini hakua akifahamiana na mume wangu, hakuwahi kumsaidia mimi ndiyo nilimsaidia kupata ile Bajaji lakini alijua sitakiwi kutajwa.


Ndani ya Bajaji Mama alimpigia simu mume wangu, alikua kapanikia na hakufikiria vizuri, alimuambia kila kitu kuhusu kumfumania Angel. Mume wangu naye alipaniki na kurudi nyumbani, ni kama alikua anamsubiri Angel kwani alipofika tu alimuambia akusanye vitu vyake. Hakutaka kujua chochote, hakuuliza hata kama ile mimba ni ya nani, ni kama alikua akitafuta sababu tu ya kumuacha, hata Angel alipomuambia mimba ni yake alikataa na kumuambia aende akajifungue na kama mtoto ni wake watapima DNA na yeye atamchukua ila hamtaki.


“Mama nawewe umeniharibia ndoa yangu, umeniharibia maisha yangu, umenifanya nikaachana na mke wangu! Sikulaumu kwakua mimi kama mwanaume ningetakiwa kusimama na kulinda ndoa yangu lakini sikufanya hivyo! Nakupenda sana na kwasababu hiyo sitaki nikukosee heshima, ukiendelea kukaa hapa tutagombana, hivyo kesho kama mlivyokuja na huyu binti utarudi huko huko nitakuja kukuona kijijini akili yangu ikitulia, kwa sasa sitaki kusikia chochote!”


Mume wangu alimfukuza pia Mama yake, siku iliyofuata alitafuta Dereva akawapakia Mama yake na Angel kwaajili ya kuwarudisha Moshi. Angel alianza kunitafuta, alikua akinilalamikia kutaka kujua afanyenini kwani asingweza kwenda nyumbani kwao na mimba. Alitaka kuondoka na kwenda kwa Victor kwani alijua kama akiondoka na kurudi Moshi basi Victor angeoa mwanamke mwingine. Nilimsihi na kumuambia kwakua walikuja mjini na Mama mkwe basi kurudi Moshi kisha ndiyo arudi Dar.


“Kwetu sio Moshi, mimi kwetu Mwanza, Moshi nilikua nasoma tu nikawa naishi na huyu Mama sasa anaponirudisha mimi nitafanya nini?” Alinitumia meseji, kweli hakua na chakufanya Moshi na asingeweza kwenda kwao Mwanza. Alianza kuniomba msamaha na kutaka kuja kwangu wakati akijifikiria nini chakufanya, sikua tayari kwa hilo lakini sikutaka kumuudi. Nilimjibu tu kistaarabu kuwa hawezi kuja kwani mimi mwenyewe ni mjamzito na karibuni nitaenda kwetu kujifungua hivyo kwakua nayeye ana mimba anahitaji mtu wa kuishi naye.


Nilimuambia kushuka kwenye gari, nikamtumia pesa ya Tax na kumuambia arudi kwa Victor. Nilimuambia akomae huko na kuhakikisha hatoki mpaka ajifungue kwani yule ndiyo kampa mimba. Alienda kweli na Victor alimpokea ingawa kwa shingo upande. Baada ya kuhakikisha kuwa wako pamoja sikutaka kuendelea kuishi Dar, Mume wangua likua peke yake hivyo angehakikisha kuwa ananitafuta mpaka kunipata. Angekuja mpaka ofisini ili kuongea na mimi na sikua tayari kwa hilo.


Niliomba ruhusa kazini, kwakua nilikua nimebakiza kama wiki tatu kujifungua nilirudisha nyuma na kuwaambia nimebakiza wiki moja na ninatakiwa kwenda kijijini kujifungua. Nilipewa likizo yangu ya uzazi na kuondoka. Mume wangu alijaribu kunitafuta kwa kutumia namba za watu tofauti, aliwatumia rafiki zangu lakini sikutaka kuwasiliana naye. Alienda mpaka ofisini kwetu na kuambiwa nimeenda nyumbani kujifungua.


Hapo alichanganyikiwa zaidi, kwanza aliwaza kuwa baada ya kuachana naye nilikua na mwanaume mwingine ndiyo maana nilikua sitaki hata kuoanana naye. Alianza kunitumia meseji, kutaka kuongea na mimi. Bado nilikataa na kumuambia kuwa mimi nishaendelea na maisha yangu nayeye aendelee na yake, nilijifanya kama vile nina mtu mwingine. Nilimzungusha mpaka nilipojifungua mtoto wakike ambaye nilifanana naye kila kitu. Ilikua ni ngumu sana kujua Baba alikua ni nani?


Sijui nini kilitokea lakini alifuatilia na kujua kuwa nimejifungua, siku moja wakati mtoto akiwa na wiki moja tu alikuja mpaka nyumbani kwetu. Ndugu zangu walijua kinachoendelea, walijua kua aliniacha wakati nina ujauzito hivyo walimchukia kwa hilo. Lakini mimi sikua na kinyongo, nilishamsamehe na kwa namna flani nilikua namuonea huruma, ilikua ndiyo mara yangu ya kwanza kuonana naye baada ya kuniacha, miezi kama nane hivi ilikua imepita.


Alikua kachoka sana, kakonda kabaki moja, kwa kumuangalia tu alikua na mawazo elfu kichwani. Nilimsalimia vizuri alikua bado na uoga, hakujua kama nitamruhusu kuingia ndani achilia mbali kumuona mtoto, lakini nilimkaribisha mpaka ndani. Ile kukaa tu mtoto ambaye ndiyo nilikua nimemlaza chumbani alianza kulia. Nilinyanyuka na kwenda kumchukua, aliniangalia akitetemeka na kutamani kuniomba ambebe mtoto, nilimuangalia kwa huruma huku mchozi yakinitoka nilimkabidhi mtoto, alimpokea, niliona mikoni kabisa ikitetemeka kwa uoga kama asingekua amekaa ungedhani anaweza kumdondosha.


“Nimepiga mehesabu, utakua uliondoka kwangu na mimba, miezi nane, huyu mtoto kazaliwa akiwa kakamilika, ulitoka kwangu na mimba…” Alianza kujiongelesha hukua kimuangalia mwanangu, ni kama alikua akimkagua kuona kama anafanana na nani.


“Najua utakasirika lakini ana pua ya Mama yangu, sura ni wewe mtupu lakini ana Pua ya Mama yangu…”


Aliendelea kuongea, nikweli pamoja na kua bado alikua mchanga lakini alikua ana pua kama ya Mama yake. Mara kadhaa nilimuangalia na kujisemea “Kweli mtu ukimchukia unazaa mtoto anayefanana naye…”


Mume wangu alikua na furaha ya ajabu, rohoni ingawa sikua na uhakika lakini nilijua kabisa mtoto si wake. Wazo kua mwanangu alikua mtoto wa Victor halikuondoka kichwani kwangu. Lakini kwa kumuangalia mume wangu alivyokua nafuraha nilijiapia kua siwezi kumuambia chochote.


“Anaitwa nani?” Aliniuliza, sidhani kama alikua anataka jina la mtoto, nikama alitaka kuhakikisha kuwa ni wake.


“Aneth…” Nilijibu kwa mkato, macho yalimtoka, aliniangalia kama alitaka nimalizie.


“Aneth Jacob Mushi” Nilimalizia, alipoumua kwa nguvu, alikua kama katua mzigo mkubwa aliokua kabeba kichwani kwake. Aliposikia nataja jina lake alipata nafuu.


Tuliongea nakucheka, aliongea na ndugu zangu, aliwaomba msamaha mara miamia na kwakua mimi nilishasamehe walikua hawana anmana zaidi ya kumsamehe. Alitaka tuongelee kuhusu kurudiana lakini sikua tayari kwa hilo, nilimuambia nahitaji kupumzika kwanza mengine tutayaongea baadaye. Hakujali, alikua na furaha ya ajabu, aliwamabia ndugu zake lakini hakutaka waje kunuiona, alijua sipatani nao kwa namna walivyo ninyanyasa kwasababu ya mtoto hivyo hakutaka mtu wakuniudhi.


Alikaa kijijini siku tatu kisha kurudi mjini, kila siku tulikua tunawasiliana na mapenzi yalirudi mara mbili yake. Kila mara alitaka niende Dar na mtoto lakini nilimuambia bado, nilikaa nyumbani kwa miezi miwili, nilipokua tayari alikuja kunichukua. Nilitaka kurudi nilikokua nimepanga akataa.


“Utarudi kwako, nitaelewa kama hunitaki, kama hutaki niwe mume wako lakini kila kitu ni chako, mimi nitaenda kupanga ila hii nyumba mtaishi wewe na mwanangu, hata nikifa leo najua kua nimeacha alama na kila kitu kitakua chako, mimi hata ukiniambia niondoke uchi bila nguo ili nyie muishi vizuri nitaondoka.”


Aliongea kwa hisia sana, nilijua fika anamaanisha, sikua na sababu ya kumbishia, nilimkubalia lakini kwa shariti kuwa hatutalala kitanda kimoja. Alikubali akiniambia hata nikitaka alale nnje atakubali. Kusema kweli nilishamsamhe na nilitaka kurudiana naye lakini nilikua makini, ilikua ni muda mrefu na nilitaka tupime afya zetu kabla ya chochote. Lakini pia sikutaka aone kama mimi ni mtu wa kupelekwa pelekwa, kwamba anaweza kuniacha na kunirudia tu kila akijisikia, alinikubalia na tukaanza kuishi pamoja lakini vyumba tofauti.


Mpaka wakati huo alikua hajui chochote kuhusu Angel na Victor, yeye alipoambiwa na Mama yake kuwa Angela anachepuka hakutaka hata kufuatilia alikua anachepuka na nani. Mimi bado nilikua nawasiliana naye, kama mimi Angel alijifungua mtoto wakike. Tatizo nikuwa Victor alikua anamnyanyasa sana, pombe zilikua nyingi, kubadilisha wanawake kila siku na kelele za hapa napale.


Kazini nako mkataba wake ulipoisha Victor hakuongezewa tena, ukiangalia na majukumu kwani baada ya wanawake wengine kuokua amezaa nao wakiamini atawaoa kuona anaishi na mtu walimletea watoto wake na kumtelekezea, aliletewa watoto watatu hivyo kuwa na watoto wanne, wengine pia walikua wakimsumbua matumizi. Hali ilikua ngumu mara kwa mara alikua akinipigia kuniomba msaada, hata Angel nilikua namsaidia kwani kuna wakati walikua wakikosa mpaka pesa ya chakula.


Lakini ile hali ilizidi, walianza kuniona kama Mama yao, kila siku kunililia shida, nilichoka na kubwa zaidi nilikua nikijua kama nisipokua makini mume wangu ambaye tulisharudiana na tulikua na furaha atajua na akijua ataumia sana, sikua tayari kumuumiza mume wangu. Nilijua kama nikiendeleza mawasiliano basi hata suala la mtoto litakuja kujulikana. Niliamua kuwaambia ukweli kuwa hali ngumu siwezi kuwasaidia tena hivyo wasinitafute, niliwablock wote na kuendelea na maisha yangu.


Walikaa kimya kwa mwezi mmoja, siku moja simu yangu iliita, ilikua ni namba ngeni na nilipopokea alikua ni Victor, kusikia sauti yake tu nilikuata simu. Ila nakata tu baada ya kama dakika tano hivi iliingia meseji. “Nilijua tu utakata simu, umeamua kunipotezea, kama hutaki mawasiliano na mimi na mimi sitaki ila kumbuka una damu yangu. Nataka kumchukua mwanangu, sitaki mwanangu kulelewa na mwanaume mwingine.” Kidogo nidondoke, nilichukua simu na kumpigia.


Nilimuambia yule mtoto si wake hivyo asinisumbue wala kunitisha, aliniambia yeye anajua mtoto ni wake kwani mume wangu hawezi kuzaa hivyo kama ninabisha basi tukapime DNA. Nilikataa katakata, aliniambia hata kama sitaki atamuambia mume wangu anachotaka ni mwanae. Nilijaribu kumtishia lakini hakutishika, alikua anamaanisha, alikata simu. Kichwani akili haikutulia, nilimpigia Angel ili aongee naye lakini naye alionekana kuwa upande wake.


“Wewe si umetutenga, tunataka mtoto wetu, unaona raha sana kuishi maisha ya raha sisi tunateseka. Ungekua unatusaidia haya yote ua singetokea.” Aliongea kwa nyodo na kukata simu, nilipojaribu kumpigia tena alikua hapatikani, ilionekana kama ni kitu wamekipanga na nilijua kuwa wananitisha ili niendelee kuwasaidia. Nilipanga kufanya hivyo ili wasinisumbue, lakini kabla ya kufanya hivyo, jioni wakati narudi nyumbani nikamkuta Victor nyumbani kwetu.


“Wewe ndiyo tulikua tunakusubiri, unamkumbuka Victor?” Mume wangu aliniuliza mara baada tu ya kusalimiana, nilikua natetemeka huku nikimuangalia Victor macho yakimsihi asiongee chochote kwa mume wangu.


“Amekuja anataka kuongea na wewe, kuna kitu anataka…” Mume wangu aliongea taratibu ni wazi alikua bado hajaambiwa chochote lakini nilijua Victor anaweza kuongea.


ITAENDELEA…


SIMULIZI; MIMI, ANGEL, MAMA MKWE NA MUME WANGU KATIKATI—SEHEMU YA NANE


(ILIPOISHIA SEHEMU YA SABA; Victor anaanza kunitafuta na kuniambia kua anataka kumchukua mtoto wake, ingawa sikua na uhakika kwa silimia mia kuwa ni mwanae lakini bado nilikua na wasiwasi. Narudi nyumbani namkuta Victor kakaa sebuleni na mume wangu, anasema kuna kitu anataka kuniambia, ni kitu gani hicho? ENDELEA… Kama hukusoma sehemu ya Saba Bonyeza hapa Iddi Makengo


“Nasikia kuna nafasi za kazi pale kazini kwenu, nilitaka uniunganishie niipate kwani kama unavyojua mkataba wangu kule uliisha…” Victor aliongea huku akiniangalia, mdomo ulikua unasema kitu kingine lakini macho ni kama alikua ananiambia. “Nakuvumilia tu ila ukileta ujinga namuambia mume wako!”


“Ni hicho tu?” Niliuliza huku nikipumua kwa nguvu, ni kama kulikua na mzigo mzito niliutua, mume wangu aliniona na kushtuka kidogo.


“Mbona hivyo kwani ulitegemea nini?” Mume wangu aliniuliza.


“Hapana! Hakuna kitu! Kwani nimesema kitu! Hapana nilijua tu ni habari mbaya!” Nilijibu kwa uoga huku nikitetemeka tetemeka, bado Victor alikua ananiangalia.


Ukimya ulitanda kidogo, wote tulikua tukiangaliana kuona nani ataanza kuongea.


“Umemsikia, kwahiyo? Hizo nafasi zipo au?” Mume wangu alivunja ukimya.


“Zipo… sijui kama zipo…labda niangalie…zitakuepo….” Nilipongea kwa kujichanganya, bado nilikua na kigugumizi gugumizi, kichwani nilikua nawaza mambo mawili, jambo la kwanza ni je Victor atamuambia mume wangu au anataka pesa na jambo la pili ni kama ni pesa ni kiasi gani na hiyo hali itaisha lini?


“Mbona hivyo, hizo kazi zipo au la? Kwani wewe huendi kazini ukajua kuwa kuna nafasi zimetangazwa?” Mume wangu aliniuliza kwa hasira kidogo baada ya kuniona nambwele mbwela.


“Zimetangazwa lakini bado hazijatangazwa…” Nilizidi kujikaganganya, kichwa changu bado kilikua hakijakaa sawa.


“Hawajaweka kwenye magazeti, mimi nilisikia tu ndiyo maana nikaja kwako Shemu kama unaweza kunisaidia kwani ajira siku hizi mpaka zinatangazwa ujue kashapatikana mtu. Victor aliingilia kati, wakati wote huo alikua akiniangalia kwa kunichora akijua najichanganya na kuchanganyikiwa mwenyewe. Mume wangu alimuelewa na kuniambia nifuatilie ili kama zipo basi nimuunganishe Victor.


Baada ya maongzi kidogo nilinyanyuka kuelekea chumbani lakini kabla sijafika kokote nilimsikia Victor akiaga.


“Sasa ndugu yangu ngoja mimi niende…”


“Hapana, shemjeji nyako ndiyo kaingia si usubiri hata msosi…” Mume wangu alitaka kumbakisha.


“Muache tu si amesema ana haraka…” Nilijikuta naropoka, mume wangu alinikata jicho la mshangao kwani hakuna wakati ambao Victor alisema ana haraka.


“Saangapi, inamaana hutaki mgeni?” Mume wangu aliniuliza.


“Sio hivyo, ninaharaka kweli, ngoja niwahi nyumbani. Kuna sehemu napitia nadhani nishachelewa unaona jioni inaingia.”


Aliongea na kuaga, lakini kabla ya kutoka nnje aligeuka na kumuuliza mume wangu.


“Mwenetu yuko wapi, sijamuona unajua sijapata nafasi ya kuja kukupa Hongera.” Kidogo nipasuke kwa uoga, nilikua ndiyo nimeshikilia mlango wa chumbani kutaka kuingia chumbani, nilishindwa hata kunyanyua mguu tena, niliganda palepale na kusubiri jibu la mume wangu.


“Kamelala, kana usingizi sana, siku nyingine uje rasmi kumuona mtoto, uoe sasa na wewe…” Mume wangu alimuambia hukua kimtoa, nilibaki pale mpaka wakatoka nnje, Victor hakua na Gari alishaiuza hivyo alitoka nnje na kwenda kwenye Bajaji. Mume wangu alimsindikiza na baada kama ya dakika tatu alirejea.


“Toka nnje, nimesimama upande wa pili, hapa kwenye Bajaji.” Meseji iliingia kwenye simu yangu, ilikua ni namba mpya lakini sikua na haja ya kuuliza kama alikua ni nani. Nilijua fika ni Victor na kusema kweli ni kitu ambacho nilikitegemea na nilikitaka kwani nilitaka kujua anataka nini hasa. Ili mume wangu sinifuatilia niliamua kumuamsha mtoto makusudi, alianza kulia, nilimnyanyua na kumpeleka kwa mume wangu.


Nilimpa ili ambebe na kumbembeleza kisha nikatoka nnje kama naenda kuchukua kitu, nilitoka mpaka upande wa pili wa barabara, haikua shida sana kumuona Victor alipokua amesimama. Nilimfuata harakaharaka kwani sikutaka mtu yeyote anione. Nilipofika hakukua na hata haja ya kusalimiana, alianza kuniambia moja kwa moja alichokua akikihitaji.


“Sina shida ya mtoto lakini kama unavyojua sina kazi hivyo nahitaji kufanya biashara, kama unaweza kunisaidia kama milioni kumi hivi kama mtaji basi sitakusumbua tena.”


Aliongea taratibu, ungeweza kufikiria ni mtu, nilimuangalia bila kummaliza nnilishindwa hata chakumjibu.


“Au kama hutaki basi mimi nianzea mchakato wa kumchukua mtoto, nina uhakika asilimia mia kuwa ni wakangu na wewe unajua hata kama si wangu mumeo akijua kuwa ulishatembea na mimi basi huna ndoa tena.” Aliongea huku akimalizia kwa kujichekesha chekesha.


“Mimi sina hiyo hela, na hata kama ningekua nayo nisingekupa, nitajuaje kama hata nikikuba itakua mwisho, nini kitakuzuia kutaka nyingine zaidi, nini kitakuzuia usitake kumi nyingine au hata hamsini.” Niliongea kwa wasiwasi, ukweli nikua nilikua tayari kumpa chochote ili tu asiniharibie ndoa yangu.


“Nilishakuambia shida yangu ni mtaji, najua wewe si tajiri ila milioni kumi unaweza kuipata najua unayo, sitaki kukuharibia lakini hata kwangu mambo yameharibika hivyo ni wewe mwenyewe, mume wako kujua au kunipa hiyo hela.”


Aliongea kwa sauti ya juu kidogo, kama kungeku ana mtu anapita karibu basi angesikia, nilimsihi kupunguza sauti.


“Kumbe unaogopa eee, sasa safari ijayo basi nitaongea mbele ya mume wako! Wewe unajua mimi si mtu wa watoto lakini nahitaji pesa nina madeni mengi na sipo tayari kufungwa wakati wewe ukila raha, nahitaji pesa.” Alimalizia na kuondoka, aliingia kwenye Bajaji na kuniacha nikiwa nimeloa jasho, kwa kumuangalia nilijua anamaanisha.


***


Ilikua ni wiki moja ngumu sana, karibu kila siku Victor alikua akimpigia simu mume wangu, hakuwahi kunipigia mimi, hapana alikua anampigia simu mume wangu kumuuliza nimkefikia wapi na mchakato wa kazi. Kusema kweli ilianza kuniudhi kwani ni kama alikua ananiambia “Naweza kumuambia wakati wowote nikitaka!” Sikua na milioni kumi kwa wakati huo, mume wangu alikua nazo lakini nisingeweza kumuomba kiasi kikubwa cha pesa namna ile kwani ni lazima angeniuliza ni zanini.


Nilitafuta sana, nilisumbuka, nilitaka kuuza kiwanja changu lakini sikupata mteja, nilitaka kukopa Benki kupitia mshahara wangu lakini nilihofia mume wangu akijua itakua shida sana. Nilijikusanya kwa ndugu na marafiki nikafanikiwa kupata milioni tano, ili kupunguza usumbufu nilimpelekea Victor na kumuomba anipe muda wa ziada. Bila aibu alinipa siku kumi na zilipoisha sijapata alianza tena kumsumbua mume wangu.


“Nasikia unauza kiwanja chako?” Siku moja Mudi aliniuliza, nilipanda Bajaji ili kwenda kwa Victor, mara nyingi nikienda kuonana naye situmii gari yangu ili kuepuka kuonekana.


Mudi ndiyo Bajaji ambaye napenda kumtumia kwani mbali nakua nimezoeana naye lakini anajua siri zangu nyingi hivyo ni kama kumuongezea siri nyingine tu.


“Ndiyo umesikia wapi? Kuna mteja umempata? Nina shida sana na pesa? Kama kuna mtu niambie!”  Nilijikuta natoa majibu mfululizo, nilionyesha dhahiri kuwa nilikua nimechanganyikiwa.


“Mimi tena kila kitu kinachoendelea mtaani najua, nilikua nataka kiwanja nikawa nafuatilia kuna Dalali akanipeleka katika kiwanja chako.”


Nikweli alikua akikifahamu kwani yeye ndiyo alinipeleka kwa mara ya kwanza na kusimamia kama shahidi wakati nakinunua.


“Unapesa ya kukinunua? Kama ni wewe basi hata tumkwepe Dalali nina shida sana.”


“Najua unashida… bado yule mtu anakusumbua…” Aliongea na kunishtua kidogo, nilimuuliza mtu gani,  bila hiyana alinijibu Victor.


“Umejuaje ananisumbua? Umesikia nini huko mtaani, kuna kitu uanjua unanificha?” Niliuliza maswali mfululizo nikidhani kama yeye anajua basi na watu wengine wanajua na nirahisi kwa mume wangu kujua pia.


“Siku anakuja pale kwako nilikuepo, nilishtuka ikabidi kusubiri wakati anatoka nilimuona mpaka akasimama na wewe kuja kumfuta, nilijua tu lazima kuna kitu hivyo nikawa nawasikiliza. Hata alipokua anaondoka alikuja kuchukua Bajaji yangu, mimi ndiyo nilimpeleka kwake, ingawa yeye hata hakunikumbuka lakini nilimsikia akiongea kwenye simu kuhusu mambo yenu.”


Nilimuuliza kama kuna mtu mwingine anajua akaniambia hapana, hapo nililazimika kumuambia kila kitu na kumuomba anisaidie milioni tano iliyobaki nitamlipa hata kama ni kwa kumuuzia kiwanja changu.


“Huhitaji milioni tano, una uhakika gani ukimpa hizo hatadai nyingine?”


“Sina uhakika lakini nitafanyaje, nisipompa atamuambia kila kitu mume wangu.”


“Hapana hawezi kumuambia, hata ukitaka ahame mji atahama, niruhusu nikusaidie…” Aliongea kwa suti ya utulivu kabisa, hakuonyesha kupaniki wala nini, alionyesha dhahiri kuwa anamaanisha kile anachokiongea.


“Sijakuelewa, unamaanisha nini?”


“Namaanisha kuwa watu kama hao wanaojifanya washenzi mimi nawajua, najua namna ya kudili nao, nina rafiki zangu wakimtembelea mara moja nina uhakika siku hata akikuona atakua anakimbia!” Aliongea kana kwamba wanataka kumfanyia kitu kibaya, nilianza kumuogopa Mudi na kumuambia kama ni kumpiga basi sitaki, nibora mume wangu ajue lakini si kumpa ulemavu au kumuua.


Alicheka na kunaimbia nisiogope, hawatamfanya kitu ila hatadai tena pesa wala mtoto.


“Wewe unachotakiwa kufanya nikuwa, leo ukifika kwake anza kumtukana, onyesha kupaniki kumuambia kuwa mume wako amejua kila kitu. Anza kumlaumu yeye kwa kumuambia mume wako na mtukane sana, muambie unaogopa na unamuogopa mume wako kwani unaona kakasirika sana halafu kesho nitakuletea pesa zako ulizompa na yeye hutakuja kumuona tena. Hatajua ni wewe uliyemfanyia hivyo atajua ni mume wako analipa kisasi kwa kutembea na mke wake.”


Niliogopa sana lakini sikua na namna, nilimuambia wasije kumuua, Mudi alisisitiza kuwa hatakumgusa hawatamgusa lakini ataondoka tu mjini na pesa zangu atanipa. Niliamua kufanya kama Mudi alivyoniambia, nilipofika nilianza kulia, nikamuambia amemuambia mume wangu, alibisha nakusmea hapana, nilimuambia mume wangu kakasirika ananitukana kama ni Malaya. Tuligombana sana, yeye alijua kua naigiza na kuzidi kuniambia nimpe pesa zake kama sitampa basi atamuambia kweli kwani bado hajamuambia. Niliondoka na kuingia kwenye Bajaji, Mudi aliniambia nimefanya vizuri sana nisubiri matokeo.


***


“Unaonekana wewe ni mwanaume sana?” Mudi alimuuliza Victor, ulikua ni muda mfupi tu baada ya kunileta nyumbani, Mudi aliwatafuta rafiki zake watatu na kwenda kugonga nyumbani kwa Victor. Walimkuta Victor na Angel, Angel alimkumbuka na kuanza kumshutumu kuwa yeye ndiyo alimchongea kwa Mama mkwe wake, alimuambia ndiyo na kumuambia atulie. Wale watu wengine watatu hawakua wanaongea, walitoa picha nyingi katika kabegi na kuziweka mezani.


Zilikua picha za kutisha sana, walitoa visu (sime) na kuziweka mezani kisha kumalazimisha Victor kuziangalia zile picha. Hawakumgusa lakini Victor baada ya kuona tu zile picha alianza kutetemeaka kwa uoga nusu ajikolojee.


“Hicho ndiyo kinatokea kwa watu ambao hutembea na wake za watu, mwanzoni tulikuacha uendelee kuishi kwakua ulikua unatembea na huyo Malaya, bosi wetu hakuwa nashida naye na alikushukuru kwa kazi yako. Lakini sasa umevuka mipaka, umempa mimba mke wake na umeshaanza kumtishia kwahiyo unataka kujionyesha kuwa wewe ndiyo mwanaume?”


“Hapana sio hivyo…” Victor alikua anatetemeka.


“Sio hivyo ni nini? Umemchukulia wanawake zake wote wawili na bado unataka kutangazia umma kuwa yeye ni hanithi, hiyo DNA unayotaka ni ili watu wajue kuwa yeye ni fala kasingiziwa watoto na wewe kuonekana kidume au? Au unafikiri yeye ni mjinga hajui mambo mnmayoongea kwenye simu na mke wake, unafikiri yeye ni mpumbavu haoni meseji za kijinga unazomtimia mke wake!”


Victor alikaa kimya, walimnyanyua Angel na kumuambia aangalie zile picha. Alingalia nayeye kuanza kulia, zilikua zinatisha kweli kweli. Zilikua ni picha za wanaume tofauti tofauti, mimi sikuziona lakini Mudi aliniambia kuwa wale vijana ambao alienda nao ilikua ndiyo kama kazi yao. Walikua wakidili na wanaume ambao hutembea na wake za watu wenye pesa, wanawaamua kuwafanyizia wale wanaume kwa kuwageuza wake na kuwapiga picha wakiwaingilia kinyume cha maumbile.


Ilikua ni kama kazi yao na walishafanya matukio kama matatu hivi ambayo yeye alikua akiyafahamu, mtu akijua mkewe anatembea na mtu flani basi huamua kumfanyizia yule mwanaume anayetembea na mkewe. Walimuonyesha Victor picha za wanaume wengine wakipigwa na kufanyiwa mapenzi kinyume na maumbile. Victor aliogopa kwani wala hawakauficha sura zao, walewale aliokua akiwoana katika picha ndiyo haohao walikua mbele yake.


“Una bahati aliyetutuma ni msatarabu la sivyo nasisi tungekufanyi hiki hiki na picha zote hizi tungeenda kumpelekea Mama yako mzazi ili kujua kuwa kazaa mtoto wa aina gani. Lakini kwakua hatukuambiwa hivyo mwenye mke kasema kuwa umuache mke wake, kwanza utampigia simu mke wake kumuomba msamaha kwa usumbufu, pili utarudisha Shilingi milioni tano zake, na tatu utawalipa hawa vijana ada yao ya usumbufu kwani hawakufanya kazi yao waliyokua wanataka. Kila mmoja utamlipa milioni moja moja hivyo mpaka kesho jioni unatakiwa uwe umeshapata hiyo hela.


Najua uanweza kujifanya unatoroka lakini ikifika jioni hujapata hiyo hela basi jua kuwa utaenda kumzika Mama yako na gharama utazifidia. Kitu kingine ukimpigia simu mke wake kumuomba msamaha, utampa pesa zake na utamuambia baada ya kufikiria sana umegundua mtoto si wako hivyo hutaki tena mambo ya DNA, utamrudishia pesa zake na kamwe hutataja kuwa tulikuja hapa, mkewe anatakiwa kujua tu kuwa yameisha kimyakimya, hatakiwi kujua kama mumewe alitutuma kwako” Walimuaga na kuondoka.


Siku iliyofuata nilipokea simu kutoka kwa Victor, aliniomba msamaha na kuniambia kuwa alikosea, aliangalia tarehe vizuri na mtoto si wake. Aliniomba akaunti yangu anitumie pesa zangu. Sijui hata alizipata wapi lakini alizipata na wale vijana aliwalipa. Baadaye kabisa ndipo nilijua kuwa aliweka rehani hati ya nyumba ya Mama yake ambayo baadaye ilikuja kuchukuliwa kwani hakuweza kulipa ile pesa.  Hakunisumbua tena na baada ya muda nilisikia kuwa Angel alitoroka akaondoka na kumuachia mtoto na kwenda zake kutafuta maisha. 


Ni miaka miwili sasa imepita tangu haya yote kutokea, sijawahi kumuona tena Victor, tetesi nikuwa kahamia Mwanza lakini sitaki kabisa kujua. Mimi na mume wangu bado tunaishi vizuri, hatujabahatika kupata mtoto mwingine na wala hatutafuti tena. Mume wangu anampenda mwanangu kupita kitu chochote na hakuna hata siku moja alishawahi kunyesha shaka kuwa si mtoto wake. Bado hayuko vizuri na Mama yake ingawa wanasalimiana na mimi kila siku namuambia amsamehe kwani Mama ni Mama.


***MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG