Search This Blog

Wednesday, June 22, 2022

MWAKA MMOJA WA NDOA YANGU

  


IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO


HALIMA; MWAKA MMOJA WA NDOA YANGU ----SEHEMU YA KWANZA!

Ndoa yangu ilikua mwaka jana mwezi wa pili (2021), ilikua ndoa kubwa sana kwani mume wangu ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kifedha. Wakati nafunga naye ndoa nilijua ni mfanyabiashara tu wa kawaida, lakini wiki mbili tu baada ya ndoa, mume wangu alininunulia Gari ya aina ya Prado ya milioni 150.

Hapo ndiyo nadhani kila kitu kilibadilika, baada ya ndugu zangu kuona gari nililonunuliwa wakaanza kufuatilia kuhusu kipato cha mume wangu. Mama alikua anananipa maswali ya kumuuliza mume wangu ili tu kujua kipato chake.

Mume wangu hakua akinificha kitu, alikua akinishirikisha kwa kila kitu na mara nyingi alitaka nijue namna anavyofanya Biashara zake. Yeye ni mfanyakazi wa serikali, lakini anasimamia Biashara za Marehemu Baba yake kwani ndiyo mkubwa kwao na hizo ndiyo ambazo humpa pesa nyingi.

Ana wadogo zake wa nne, ambao wanaishi kama familia moja, ingawa haishi nao lakini yeye ndiyo kama Baba yao, Mama yake anamuamini sana hata baada ya mimi kuolewa aliniona kama mwanafamilia, akaniamini.

Ni zile familia ambazo mali si kitu, yaani kwao ni upendo, ingawa nililingana kiumri na mdogo wake wakike lakini kwakua niliolewa na Kaka yake aliniheshimu na nilionekana mkubwa pale. Baada ya kununuliwa Gari nyumbani kwetu niliitishwa kikao.

Kilikua kikao cha watu wa nne, mimi, Mama, Baba na Dada yangu ambaye naye alikau ameolewa. Walianza kuniuliza kuhusiana na familia ya mume wangu, wako wangapi, wanaishije na mali zimeandikwa majina ya nani? Mimi sikua najua kitu chochote, niliwaambia nimekuta tu wanaishi vizuri na kila kitu wanafanya pamoja.

“Unatakiwa ujue, hivi unafikiri huyo mwanaume akifa hapo watakuthamnini? Leo mume wako akifa utaondoka na nini zaidi ya hicho kigari chako amabcho hata kununua mafuta huwezi!?” Babam alinifokea, nilishangaa kukiita kigari wakati ukoo wetu mzima tajiri alikua ni Baba yangu mdogo ambaye alikua akimiliki pikipiki tena ya Serikali ambayo alipewa kwakua tu ni Bwana Shamba.

“Mume wako anapata mshaara kiasi gani?” Dada yangua liniuliza.
“Sasa mimi nitajuaje wakati ndiyo kwanza ndoa ina wiki tatu, hivi mnajua hata mshaara haujaingia tangu nifunge naye ndoa….” Niliongea kama utani lakini wenzangu walikua siriasi, tena siriasi sana. kweli mshaara hata ulikua bado haujaingia tulifunga ndoa mwaka

Mama alinikata jicho kama ananiambia “Hivi wewe mshenzi una akili kweli? Unatakiwa kujua kila kitu mjinga wewe!” nilijikuta naacha kucheka na kuweka uso siriasi hata kabla Mama hajasema chochote kwani nilijua kama nikiendele kujichekesha anaweza kunikata kibao.

“Mwanangu, si kama tunakupangia namna ya kuishi kwenye ndoa yako, hapana, lakini hii dunia imeharibika, wewe ndiyo umeolewa, unaona kila kitu nikizuri, ukipata mimba hapo huyo mwanaume akafa unafikiri huyo mtoto utalea na nani?

Utakuja hapa na sisi nidyo tutateseka na wewe, au unafikiri mtotoa takula gari? Hivi mwanaume anakupa Gari ya milioni mia sijui na hamsini, hujifikirii? Huna hata kiwanaja unachukua tu! Nakuambia utakuja kujuta…”

Mama aliongea kwa uchungu sana, mpaka nilishtuka labda nimefanya kitu kibaya, mpaka nilianza kuhisi labda mimi ni mjinga, “Kwanini nachukua gari wakati sina Nyumba?” niliwaza huku bado nikimsikiliza Mama ambaye hakuacha kuongea.

“Kabla ya kubeba mimba kwanza hakikisha kuwa mali ni za nani, una ndoa ya kiislamu, huyo mwanaume anaweza kuoa wake wawili, watqtu na hata wanne. Ni lazima kwanza ujue mali za mume wako, zenye majina yake na si majina ya ndugu zake, ujue mshahara wake na ujue mnautumiaje! Usikae kijingajkinga, akununulie kiwanja au akupe nyumba moja ndiyo mambo mengine yafuate!”
Dada aliniambia.

“Lakini dada, mbona bado mapema, nitamuulizaje kuhusu mambo ya mali wakati ndoa haina hata mwezi, si atajua kama ninataka kumdhulumu…” Niliongea kwa ukali kidogo kwani niliyekua namjibu alikua ni Dada yangu sikua nikimehshimu kihivyo, na wala sikutaka aingilie ndoa yangu kwani yuake ni kama ilishakufa muda mrefu, lakini kabla sijamalizia kuongea kuna kitu kizito kilidondokea usoni kwangu.

“Paaa! Paaa!” Baba alinitandika makofi mawili ya nguvu nusu kudondoka. Nilipepesuka na kudondosha glasi ya maji ambayo ndiyo nilikua nataka kuiokota ili kunywa maji.

*****

Ulikua ni wakati wa chakula, usiku, siku hiyo Mama alimpigia simu mume wangu kunuiomba niende nyumbani kwani kulikua na kakikao kidogo. Ingawa mume wangu alishangaa kwani ilikua mapema sana mimi kuanza kwenda kulala nyumbani kwetu lakini hakua na namna, alihisi kuna matatizo makubwa hivyo aliniruhusu bila kuuliza maswali mengi sana.

Kwakua bado nilikua sijajua kuendesha gari alinileta yeye mwenyewe, akanaimbia atakuja kunichukua kesho yake.

Sikujua sababu ya wao kuniiita, usiku wakati tumekaa kwenye meza ya chakula, nilishangaa Mama anawaambia wadogo zangu wengine kwenda kulia chakula nyumbani. Kwakua walikua na hamu sana na mimi walikua kama wanagomagoma ila Baba livyoongea ndipo walijua kuwa siriasi wanatakiwa kuondoka na kurudi ndani.

Waliingia ndani, pale sebuleni kwenye meza ya chakula, nikabaki mimi, Dada, Baba na Mama. Dada yangu alikua ameolewa lakini ndoanyake ilikua kama haijasimama, mara nyingi alikua ni mtu wa kuja nyumbani na kulala nyumbani akilalamikia kuchoshwa na tabia za mume wake.

Hata siku hiyo yeye hakuitwa kwaajili ya kikao, alikua pale nyumbani tangu kipindi cha ndoa yangu, ilionekana walikorofishana na mume wake, kila siku ilikua ni sababu mpya, mara mwanaume kuchelewa kurudi, mara hahudumii familia, mara sijui dada kafumaniwa, mara mwanaume kashika simu yake na mambo mengine kama hayo.

Makofi mawili ya Baba yalikua ni makali sana, ilikua ndiyo mara ya kwanza kwa Baba kunipiga, Baba yangu si mpigaji, sio kama ni mpole hapana, mara nyingi likija suala la kupiga alikua anapewa Mama, utasikia anamuambia.

“Ongea na huyu mwanao, nitakuja kumuua!” Hapo moja kwa moja ndiyo unajua kuwa Baba kakasirika na Mama anatakiwa kutoa dhaabu ya kipigo, kwa siku ile kunipiga makofi nilijua kuwa kakasirika tena sana.

“Hivi una akili kweli, Mama Hamida, hivi kweli huyu mtoto mlimfunda, huko kwenye Kitchen Party mlienda kula wali tu na kurudi, kuna kitu mlimfudnisha kweli huyu kuhusu ndoa!” Aliongea huku ananyanyuka, alinishika mkono na kunivuta kuelekea chumbani.

“Au unataka mimi Baba yako nikakufundishe namna ya kuishi na mwanaume! Unataka mimi ndiyo nikakufundishe namna ya kumkatikia mwanaume mpaka anakuambia kila kitu! Njooo! Njooo! Si Mama yako hajakufunda wewe! Nakuambia, si Mama yako hajakufunda! Una akili kweli wewe!”

Baba alikua kakasirikan sana, alinivuta mpaka chumbani kwao, akanisukuma mkitandani, wakati huo Mama na Dada walikua wanatufuata nyuma, wanaangalia bila kufanya chochote, taa ilikua inawaka, nikawa mimi niko kitandani nimekaa, Baba kasimama anaongea huku akirusharusha mikono, Mama na Dada wanaangalia hawataki kuingilia.

Kwa alivyokua ni kama alikua anajiaandaa kufanya mapenzi na mimi, nilimuangalia Baba nakuona kama vile kachanganyikiwa, kwanini anataka kufanya kitu kama hiki, mbona Baba si mtu wa namna hii, kwa namna nilivyokua namjua Baba yangu sikuwahi kudhani kama anaweza kufanya kitu kama kile/

“Hapana, Baba sio hivyo nilikua namaanisha….” Nilitaka kujitetea kwani Baba likua anakuja kitandani kwangu kama vile anataka kunibaka.

“Unamaanisha nini? Kwamba mimi sijakufunda namna ya kuishi kwenye ndoa, kwamba mimi sio Mama mzuri, unaona mpaka unataka kuniaibisha mbele ya Baba yako, Baba yako ndiyo aje kukufundisha kumteka mwanaume!

Akili zote hizo unashindwa kumuuliza mwanaume kuhusu mshara wake!? Ni mume wako, narudia ni mume wako nilazima kujua kila kitu chake. Unaona umeolewa, umenunuliwa gari? Sisi kama wazazi wako tumepata nini? Hivi mwanaume mweney pesa namna hiyo, siku ya harusi badala ya kutupa kitu cha maama nimi Mama yako amenipa nini?

Pochi, yaani Pochi ya elfu hamsini ndiyo anakuja kunipa mimi? Ana akili kweli, eti Baba yako anampa kitambaa cha suti! Nani kamuambia kuwa sisi hatuna nguo!” Mama aliongea sana huku akilia, kusema kweli nilishangaa sana kwani mimi na mume wangu hatukua na shdia yoyote.

“Haya mambo yameanza lini, mbona kipindi cha uchumba Mama ndiyo alikua ananiambia nisipende kuombaomba pesa hata kama mwanaume ana pesa basi ni heshima kama nikisubiri akanipa mwenyewe, iweje sasa hivi anakuja na mambo ya kuniambia nimchune mume wangu!”

Wakati wanaongea mimi nilikua nawaza mambo yangu, hata sikuwasikia walikua wanaomngea nini, niliona wanatingisha vichwa na kila wakiniangalia na mimi nilitingisha kuonyesha kuwa nakubaliana nao ingawa sikua najua chochote kilichokua kikiendelea pale.

“Nyanyuka, ila yashike yote tuliyokuambia, hakikisha unajua mali za mume wako, sitaki mambo ya wajukuu ambayo hayana kichwa wala miguu!” Baba liniambia huku akinishika mkono na kuninyanyua. Alikua mtu mpya kabisa, hapo ndipo walianza kuniuliza habari zafamilia, walichangamka na kutaka kujua ndoa yangu ikoje, kama naifurahia au kuna manyanyaso yoyote!

Niliwajibu kwa wasiwasi kwani sikujua walikua wanataka nini. Nilitaka tu ile siku ipite nirudi kwa mume wangu maisha mengine yaendelee. Asuibuhi nilimpigia simu mume wangu aje kunichukua, aliniambia atakuja baada ya kutoka kazini lakini nilimuambia hapana.

“Kuna nini, mbona umekua hivyo ghafla, sauti yako siielewi?” Mume wangua liniuliza, hapo ndipo niligundua kuwa nilikua nimebadilika kidogo.
“Sijisikii vizuri kabisa, nahisi nina homa, njoo unicheki nikapime Malaria.” Nilimuambia mume wangu, kweli hakuchelewa kwani saa mbili na nusu alikua nyumbani. Hakuwaambia kuwa alinipigia simu, alidanganya kuna kasehemu tulipanga kwenda ndio maana alikuja kunichukua mapema.

“Kuna nini? Mbona kama hutaki kuaa kwenu?” Mume wangu aliniuliza kama anatania, lakini sijui ni nini, nilijikuta napadwa na hasira, na kupaniki.

“Kwanini nisitake kukaa kwetu? Unadharau nyumbani kwetu? Kwahiyo unatuona sisi masikikni, au kwakua umenipeleka kwenye nyumba znuri ndiyo unafikiri nimesahau kwetu!

Kwanza nyumba yenyewe sijui hata ni ya nani lakini unaninyanyasa nayo! Hapana aisee kwetu hata kama kubaya namna gani ndiyo nilipokulia….”

Nilijikuta napaniki mpaka mume wangu akaanza kuomba mismahaa ambayo haiishi. Jinsi alivyokua ananiomba msamaha ndiyo jinsi nilivyozidi kupaniki, nilizidi kulalamika na kuongea maneno mabaya.

Mume wangu aliamua kukaa kimya mpaka tulipofika nyumbani, hakuongea kitu chochote, mimi ndiyo sasa nikawa nawaza yale mambo niliyokua namuambia, ghafla ninajikuta nashika na kizunguzungu nadondoka.

Mume wangu alinikimbilia na kunishika, alininyanyua na kunikalisha kwenye kochi, lakini bado hali yangu haikua nzuri, ghafla nilihisi kama miguu yangu kuloana.

“Naona kama nimekalia maji?” Nilimuuliza mume wangu kabla hataa hajanijibu nilijua kuwa sio kukalia kwani nilihisi kuna vitu vinataoka sehemu zangu za siri. Zilikua ni damu.

“Damu, una maumivu au umaingia kwenye siku zako?” Mume angu aliniuliza, hata mimi nilishangaa kwani sikua katika siku za hatari, lakini kwakua nilikua niemshapitiliza nikahisi labda ndiyo nimeingia.

Ila ilikua tofauti, nikaanza kuhisi maumivu makali tumboni chini ya kitovu. Maumivu yalikua makali kiasi kwamba hata kunyanyuka ilikua shisa.
“Mume wangu nakufa?” Nilimuambia mume wangu ambaye naye alikua kapaniki hajui nini cha kufanya. Alininyanyua kunitoa nnje ila sasa damu zilikua nyingi, yaani kama zinachuruzika, hapo ndipo nilijua kama si damu za hedhi bali kulikua na kitu kingine.

“Kuna nini mbona hivi mke wangu?” Mume wangu aliniuliza, kabala hatujafika nnje simu yaangu iliita. Ilikua kwenye kochi, tuliipuuza ila baadaye tunafika kwenye gari mume wangu alirudi na kuichukua kwani ilikua inakata ainaanza kuita tena.

“Mama yako, ngoja nimuambie unaumwa…” Mume wangu aliniambia, sijui kwanini lakini nikajikuta namnyang’anya simu ili kuongea naye. nilipokea nikasikia sauti ya Mama inaniambia.
“Ni damu za kawaida tu, zikianza kutoka nenda tu kasafishwe hakuna shida!” Nilishtuka maumivu yakasimama kwa muda mpaka mume wangu naye akashtuka!”

Kuna nini mbona umeshtuka Mama anasemaje, nimesikia kama anasema Damu? Ni damu gani anazungumzia kajuaje?” Aliniuliza huku akiwa amegadna, ananikodolea macho!



(ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA; Halima kaingia kwenye ndoa, wiki mbili tu mume wake kamnunulia Gari ya milioni 150. Ndugu zake wanapaniki na kumuita kikao baada ya kujua ana mali nyingi kiasi hicho.

Wanamtaka kuacha kuzaa kwanza na kuhangaikia mali. Anaondoka kwao, ghafla damu zinaanza kumtoka sehemu za siri na Mama yake anampigia simu kumuambia asiwe na wasiwasi kasafishwe tu mume wake anashtuka na kumuuliza Mama yake kajuaje kuhusu Damu ENDELEA…)

Nilimuangalia mume wangu na kuona kama mtu aliyekasirika, ni kama alihisi kuna mchezo kati yangu na Mama yangu kwani tangu nianze kutokwa na damu nilikua sijampigia simu Mama kumuambia chochote, hata mimi sikujua alijuaje ila nilipaswa kudanganya ili kuiokoa ndoa yangu.

“Kwani kuna shida gani Mama kunipigia simu, inamaana hata ndugu zangu hutaki wajue mambo yangu?” Nilimuuliza huku nikipiga kelele za maumivu, ishu haikua maumivu ila nilitaka apotezee!

“Sio hivyo lakini wewe huoni ajabu Mama yako kukupigia simu kutaja mambo ya damu wakati hujamuambia?” Alinikazia macho kaisi cha kushindwa hata kunyanyua mdomo, binafsi nilishahisi kitu kibaya, ila sikua na ujasiri wa kumuambia.

“Lakini si nilikua na Mama, si nilikuambia najisikia vibaya, jana usiku vilitoka vidamu vidogo, nikamuambia Mama ila akaniambia hakuna shida, asubuhi ndiyo nikaamua kukupigia simu, unakuja unaanza kunidhihaki na mambo yako!

Mimi nilitaka uje unipeleke hospitalini wewe unakuja na mambo yako sijui ya sitaki kukaa kwetu! Hivi na hali hii ningekaa nyumbani ingekuaje, umenioa lakini ni kama hunijali, au kwakua umeninunulia gari ndiyo unaona ushafanya kila kitu!”

Sijui majibu yalikujaje lakini ulikua uongo mzuri, mume wangu alibaki kimya, akaniingiza vizuri kwenye gari, akafunga mlango tukaondoka. Njiani nilikua naugulia maumivu, yeye kikubwa alichokua akikifanya ni kuniambia pole na kuniomba msamaha.

“Hata sikufikiria mata mbili, kumbe ndiyo maana ulikua na hasira namna ile….” Aliendelea kuongea ila mimi nilibaki kimya napiga kelele zangu, sikutaka kumjibu kabisa. Hospitalini nilipimwa na kuambiwa kuwa mimba imetoka, kwangu ilikua msahangao kwani nilikua sijui kama nina ujauzito.

“Unaonekana ulikua una mimba changa ila kwa hizi damu zilizotoka sijui ni kwanini, ni kama mtu aliyetoa ujauzito wa miezi minne.” Daktari aliniambia, wakati huo mume wangu alikua nnje, nilishasafishwa Daktari alikua ananihoji tu.

Sikujua kajma nina mimba na damu zilizonitoka nilipata mashaka, nilikua kwenye mawazo makali, sikujua kuwa huku nnje kutokana na wasiwasi mume wangu alishampigia simu kila mtu ili kuja kuniona.

Wakwanza kuja kuniona alikua ni Mama mkwe wangu, alikua na wasiwasi sana, kila dakika kuniuliza naendeleaje, baadaye alikuja na wifi yangu ambaye alinihudumia kama mtoto. Jinoni ndipo Mama yangu alikuja, wakati huo mume wangu alikua ashaondoka nilikua nimebaki na wifi tu.

“Mhhh! hii ni Hospitali au Hoteli?” hicho ndiyo kilikua kitu cha kwanza kwa Mama kuuliza. Sikuwa nimechanganywa na wagonjwa wengine, mume wangua linichukulia chumba changu mimi mwenyewe ‘Private’ kila kitu kilikua ni VIP pale, hata Nesi nilipewa wakwangu ambaye muda wote alikua anapatikana.

“Shikamoo Mama…” Khadija, wifi yangu alimsalimia Mama yangu kwa mchangamfu hukua kimshika mkono.
“Marahaba mwanangu.” Mama aliupoke amkono wake kisha akaanza kumuangalia kama anamkagua. Nilikua nimelala kitandani lakini kwa kukaa, nikiwa nimeegemea mito kichwa nimekipandisha kwa juu kidogo hivyo niliwenza kumuona Mama namna alivyokua anamuangalia wifi ,anakagua mavazi yake hukua kimfinyafinya ngozi yake.

“Umekomaa hivi halafu unakuja kunishika mkono! Unapofanya kazi sehemu zenye pes aunatakaiwa kujiweka kama wao, unaona sasa chumba kizuri kama hoteli lakini mtu akiingia anakuona umevaa vibauyavibaya namna hiyyo! Hembu ondoka hapa marafiki zangu wakija usijekuniabisha!”

Mama aliendelea kuongea, nilitamani kumrukia na kumziba mdomo. Wifi yeye alikua anatabasamua tu, hakuongea kitu, aliangalia chini kwa aibu.

“Toka hapa nataka kuongea na mwanangu!” alimsukuma pembeni kama takataka kisha kuja kwangu.

“Nlishakuambia mwanangu hii sio familia, hawana upendo na wewe kabisa. Yaani umepata shida kama hii, badala kuja Mama mkwe wako, au wifi yako kukuhudumia wanakuacha na huyu mfanyakazi wa ndani.

Hapa bado mume wako yuko hai, hivi mume wako akifa leo si wanakufukuza. Haya ndiyo nilikua nakuambia jana…” Mama aliongea huku akinisogelea na kukaa pembenai yangu kitandani, nilijaribu kumshika mkono kama namkonyeza ili anyamaze lakini hakuona.

“Mamamaam!” Nilimuita kwa sauti kama vile namuonya, kama mtu anasema “Shhhh!” Nyamaza wewe mjinga mbona unaniharibia.

Alishtuka kidogo, akageuka nyuma na kuona wifi alikua bado kasimama.
“Ondoka, si nimeshakuambia utoke! Mwanangu, huyu mfanyakazi ni wakuondoa, ashakua mnafiki anasikiliza mambo ambayo hayamhusu!” Alimfokea wifi ambaye hakutaka kubishana naye alitoka na kutuacha mimi na Mama.

“Haya niambie, mimba imetoka, imekuaje, wanasemaje? Mume wako kachanganyikiwa au amekuaje?” Nilimuangalia Mama bila kummaliza, sikujua nimuweke katika fungu gani?
“Hivi huyu ni Mama yangu kweli?” niliwaza bila majibu, nilitamani kuongea lakini niliona kama nitapoteza muda wangu ila asingenielea.

“Mwanangu hii ndiyo nafasi yako ya kutamba, hapa ndiyo unaweza kumuomba mume wako kitu chochotena atakupa! Usije kupona kijinga jinga, ni lazima uumwe mpaka mume wako kuchanganyikiwe! Huu ndiyo muda wa kupiga pesa ya mume wako! wanaume wenye pesa wanapenda watoto, ni lazima ajue umeumia kwa mimba yako kutoka!”

Alionega hukua kitabasmau, ni kama alikua na mpango flani kuhusiana na tatizo langu, bado nilikua na maswali mengi kichwani, kwamba alijuaje kuwa nina ujauzito kiasi cha kunipigia simu kuwa natakiwa kusafishwa.

Nilitamani kuacha kumuuliza lakini nilishindwa, nikaamua kumuuliza.
“Sikua najua kitu chochote lakini ulipokuja jana nikahisi tu una mimba, niliona matiti yako yalivyokua, na macho nikajua tu una mimba….” Aliniambia, ila bado haikujibu swali kuhusu yeye kujua kuwa ujauzito wangu uemetoka, nilimuuliza tena.

“Hukuondoka viziru, nilihisi tu kuwa kuna kitu, tangu unaondoka nilihisi! Mimin ni Mama, wamama tunajua vitu sana… haya hebu niambie, mmeshaamua nini na mume wako.

Mshapanga mtu wa kukuhudumia, najua wana makazi yao wako bize. Mimi na Baba yako tumejadiliana na kukubaliana kuwa nije kuishi kwako mpaka utakapokua sawa.” Aliniambia, walishapanga kila kitu kuhusu mimi bila kuniuliza mimi wala mume wangu.

******
“Mbona sasa kamekomaa hivyo, mimi nilijua mfanyakazi wa ndani?” Mama aliongea kwa dharau baada ya kumuambia kuwa, Khadija alikua ni wifi yangu na si mfanyakazi wa ndani kama alivyodhania. Hakuonyesha kabisa kujali hata aliporudi ndani aliendelea kumtuma kama vile ni mfanyakazi.

Khadija yeye alikua kimya, mnyenyekevu, hakuonyesha kumjali Mama.
“Achana na hayo mambo wifi, wamama nawajua, ukitaka kuingilia mambo yao utachanganyikiwa.” Baada ya Mama yangu kutoka nnje nilijaribu kumuomba msamaha na kutaka amchukulie Mama yangu kama kichaa flani.
“Hapana, kwa namana livyokuongelesha sio sawa.”

“Kwani wifi kuwa mfanyakazi wa ndani ni kitu kibaya, mbona nao ni binadamu kama sisi. Lakini anaongelea mwili wangu, mimi ni mwembamba kweli lakini hicho hakinpunguzii chochote, hakiniondolei ubinadamu wangu.” Aliniambia hukua kinituliza na kuniambia nilale, alinisishi sana niache kuwaza kwani ndiyo kwanza nimetoka kunpoteza mtoto.

Nilikaa hospitalini mpaka kesho yake ndipo niliruhusiwa, Mama mkwe wangu alitaka kunichukua lakini mume wangu alikataa, aliwamabia kuwa anataka kuniuguza kwake. Kwangu niliona bora kwenda ukweni kwani nilijua kama nikienda kwangu basi Mama atakua anakuja kuja mara kwa mara.

Lakini mume wangu aligoma kabisa, hivyo Mama mkwe wangu akamuambia wifi yangu kuja kunihudumia nyumbani. Alikua kazini lakini alilazimika kuwahisha kuchukua likizo yake ya mwaka ili tu kuja kunihudumia.

Kitu ambacho sikujua ni kuwa, si kama mume wangu alipenda mimi kurudi nyumbani, hapana, Mama alishamfuata na kumuomba kuja kunihudumia nyumbani kwangu. Ingawa yeye na Mama yake walishaongea kabla kuwa nitaenda ukweni lakini Mama alilazimishia na mume wangu hakua na namna zaidi ya kukubali.

“Nimekuja kukufunda vizuri namna ya kuishi na mume, unaonekana hujui majuku yako!” Mama aliniambia, ilikua ni asubuhi, mume wangu alishaenda kazini na Mama alikua chumbani kwangu.
“Mama nahitaji kwenda chumba cha wageni kwanza, si heshima wewe kuingia chumba ambqcho ninalala na mkwe wako…..” Nilimuambia lakini ni kama hakunisikia, aliniangalia na kucheka kisha akapanda kitandani.

“Kuna watu wanaishi, maisha mazuri kama haya mwanangu halafu unaruhusu sisi kuishi kwenye kijumba kama kile, hiki chumba tu mwanangu si unajenga ile nyumba yetu!” Mama laianza kunliaumi mimi nilivyokua mbinafsi, siwajali na mambo kibao.

“Mama hivi unajua ndoa ina wiki tatu tu, unataka nianze kuwajengea naitoa wapi hiyo pesa?” Nilimuuliza Mama kwa ukali.
“Unasubiri nini? Usipotujengea sasa hivi na mume wako akifa sisi tutakua tumepata nini?” Mama aliniulzia, swali lake lilinikera kwani liliongelea mambo ya mume wangu kufa tu. Tukiwa mule ndani tunaongea wifi yangua ligonga mlango.

“Wifi naweza kuingia?” Aliuliza, nilimruhusu kuingia ila alipoingia tu Mama alimuwahi.
“Hivi wewe umefunzwa kweli? Narudia umefunzwa kweli? Unawezaje kuingia kwanye chumba cha Kaka yako ambacho analala na mke wake. Utakua na mahusiano na Kaka yako, halafu unafanya nini, wewe si rika la mwanangu, huna mume wako, huna maisha yako! Huna kazi badala asya kuka ahuko unakuja kuharibu ndoa ya Kaka yako.

Mwanangu kuwa makini na hawa mawifi, anajifanya yuko karibu na wewe halafu anakuja kukuharibu nyumba yako! Hata hii mimba nadhani ndiyo kakutoa!” Mama aliongea kwa hasira, maneno yake yalinsihinda kuvumilia mpaka nikalazimika kunyanyuka na kuanza kugombana naye.

“Umevuka mipaka Mama, huyu ni wifi yangu na kaja kunsiaidia!”
“Kukusaidia au kukuloga, hivi mwanangu huoni, kwanini unamini watu kama hawa! Vijitu kama hivi ni vichawi, mtu kaoa lakinia mafuatafuata, mambo ya kujifanya ndugu hatutaki! Aondoka kweko, mfukuze, hapa uchague kati yangu mimi na huyu shetani ambaye katumwa kuja kukuchunguza!”

Mama liniambia hukua kitoka kwa hasira. Nilishikwa na butwaaa, aibu imenijaa, nakuangalia wifi yangu nashindwa nimuambie nini?
“Mama na amatatizo gani mbona anaongea maneno makali hivi? Kuna kitu nimefanya wifi cha kukukwaza?” Aliniuliza, wakati huo nilikua nalia kama mtoto ananibembeleza kwani nilikau naona aibu sijui nafanyaje kuhusu Mama yangu.

“Nilikuaj kukusaidia, sikujua kama Mama yakoa takuja, nilichukua likizo kwajili yako, lakini kamautakua sawa, kama Mama yuko sina haja ya mimi kukaa hapa!” wifi aliniambia.
“Hapana wifi, utakaa hapa ni kwa Kaka yako, Mama anaondoka, ana matatizo na Baba hivyo kila mtua nayemuona anamuona kama adui, havina uhusiano kabisa na wewe! Ni mambo ya kifamilia lakini naona nikuambie!

Baba amempiga Mama na ndiyo sababu ya kuja hapa, Shangazi zangu dniyo sababu ya maugomvi yao hivyoa nachukia mawifi kama nini,a anadhani labda na wewe utanifanyia kama alichofanyiw ana wifi zake!” nililazimika kudanganya kwani niliona mma akiendele ahivia anaweza kunivunjia ndoa.

Familia ya mume wangu ilikua familia iliyoshikana sana sikutaka kuivuriuga. Wifi alinielewa na kunituliza. Lakini kabla ahata hajatoka simu yangu iliita.
“Khadija yupo hapo?”
“Ndiyo, niko naye chumbani….”
“Nipe niongee naye!”

Alikua ni mume wangu, aliongea wka ukali, sana, nilipokea simu, hata bila salamu alianza kumuulizia Dada yake. Waliongea kama dakika mbili hivi kisha wifi yangua kanaikabdihi simu.
“Kwani unahitaji watu wawili wa kukuhudumia?” mume wangu aliniuliza kabla hata sijamjibu aliendelea.
“Hata kama unahitaji nitachukua mtu dukani kumleta akusaidie, nataka mdogo wangu aondoke hapo! Atamtukanaje Mama! Halafu na wewe kwanini hukuniambia kilichotokea jana Hospitalini?”

Mume wangu aliniuliza, nilibaki na mshangao sijui anamaanisha nini, sikujua Mama kamuambia nini?
“Kwanini hukuniambia au ulidhani kuwa sitajua!” Alizidi kuongwa kwa hasira.
“Niliona ni mambo madogo ambayo ni ya kawaida sana, sikutaka kukuambia kwakua…”

Ya kawaida, hivi mtu kumtukana Mama yako ni jambo la kawaida, au na wewe unamdhaarau Mama yako. Mtu kaacha shughuli zake kuja kukusaidia, lakini katukanwa unakaa kimya!” Alifoka sana.
“Mama mtu mzima ananipigia simua nalia, hivi una akili kweli wewe?”

“Hivi nyie wanawake mna nini, mnagombana kwa mambo ya kijinga, kama ni kuolewa si ataolewa tu kwnaini kutaka kukuumiza wewe!” mume wangu aliongea, kusema kweli sikumuelewa, alikata simu huku akisisitiza mdogo wangu kuondoka.

“Kuna nini? Mbona Kaka yako ana hasira namana hii?” Nilimuuliza wifi yangu amabye sasa alikua analia.
“Wifi kuna kitu kibaya nimekufanyia?” Aliniuliza, nilimuambia hapana, nilizidi kumuuliza kuna tatizo gani lakini hakuniambia.
“Naomba niondoke ila kama ku a kitu kibaya nilikufanyia au unahisi nimekufanyia nisamehe! Nilipenda sana uwe na mtoto, nilikua na hamu sana na kucheza na katoto ka Kaka yangu, sikujua kama una mimba na wala sikuwa na mpango wowote wa kukufanyia kitu kibaya, nisamehe sana kama nimekukosea!”

Bado nilikua sijajua wifi yangu kaambiwa nini na Kaka yake, nilikuasielewi chochote, huku aklilia wifi yangu alichukua vitu vyake na kuondoka, nilijaribu kumsihi kusubiri lakini wapi, hakukubali kusubiri wala hakuniambia kitu chochote.

Baada tu ya kuondoka Mama aliingia chumbani kwangu, nyumba tulibaki wawili kwani bado nilikua sijapata mfanyakazi wa ndani, ingawa nyumba ilikua kubwa lakini wala nilikua simhitaji mfanya kazi kihivyo kwani nilitaka kufurahia ndoa yangu mimi na mume wangu.

“Afadhali yule shetani ameondoka, sasa hivi nina amani, unajua niliogopa, nilipomuambia Dada yako ndiyo akaniambia nihakikishe ninamuondoa!”
“Mama kwani kuna tatizo gani, umemuambia nini mume wangu ambacho kimemkasirisha namana hiyo?”

Mama aliingia chumbani kwangu na kuanza kujiongelesha kama vile hakuna kitu kilichotokea, sitaka kumsikiliza nilimuuliza maswali mfululizo ili kujua shida ni nini?

Mwanangu, mume wako sasa hivi ana maumivu, kitu chochote utakachomuambia lazima atakusikiliza. Hatumii akili, simu moja tu kashamfukuza mdogo wake, kama unataka mali hazipatikani shambani, unamtenga kwanza mume wako na ndugu zake, akishabaki peke yake basi atakusikiliza kwa kila kitu!




Mume wangu alirudi na kunikuta niko kwenye lindi la mawazo, mambo aliyoyafanya Mama yaliniogopesha.
“Mbona una mawazo namna hiyo, bado unawaza kuhusu wifi yako?” mume wangu aliniuliza, alikua akilazimishia tabasamu lakini nilijua kuwa anaumia, kuna kitu alitaka kusema ila alikua na hofu ya kiniumiza.

“Sitaki kukugombanisha na ndugu zako, mimi niko sawa, naona kama Mama aondoke mana animeshapona, sioni sababy ya yeye kukaa hapa!” Nilimuambia mume wangu kwa sauti ya upole, lakini nilishangaa kabadilika.

“Unamaanisha nini? kwanini aondoke, kwasababu ya Dad ayangu?” aliniuliza kwa hasira.
“Hapana, lakini naona tu sihitaji msaada wake….” Nilimuambia lakini alinikatisha kabla hata ya kumaliza.
“Hivi mimi ni nani kwako?” mume wangu aliniulzia kwa ukali.
“Ni mume wangu kwanini unauliza hivyo?”
“Nataka kujua unanichukulia mimi kama nani? Maana naona kama vile sijui unaiogppa au unaogopa familia yangu, hivi kwanini mambo yanatokea lakini huniambii?”

Aliniuliza sikua na jibu, nilimuuliza mambo gani lakini hakunijibu, alitoa simu yake na kufungua sehemu ya meseji kisha akanionyesha.
“Kwanza hukuniambia kuwa una mimba, lakini uakenda kuonga na dad ayangu, haitoshi hapo dad ayangu kakutukana hujaniambia kitu chochote. Mambo yote haya nakuja kusikia kutoka kwa Mama yako!”

Nilishangaa alikua anaongea ini lakini baada ya kuichukua ile simu nilikuta meseji nyingi amabzo mume wangu katumiwa na Mama. Lakini hazikuonyesha kama zinatoka kwa Mama bali zinatoka kwa wifi yangu.
“Hivi unafikiri hiyo mimba ni ya Kaka, yaani umeolewa juzi sas ahivi una mimba, hapana, na tutapima DNA!”

“Nakuambia hivii, nyie maiskini mna shida gani? Yaani umeingia kwneye dnoa na kuzaa, kizazi chakoc ah karibu peleka hukohuko!”
“Nitahakkiisha kuwa huzai, wewe si unajifanya mjanja, huyo mtoto usipozaa ng’gwebasi mimi sio Khadija!”

Kulikua na mesjei nyingi zikionyesha wifi yangua kinitukana. Nilikua nazishangaa kwani kwangu zilikua ndiyo naziona kwa mara ya kwanza.
“Juzi nilikuulzia kwanini unaenda nyumbani ukaniambia kua wamakutia kuna kikao. Hukuniambia sbabau za kikao, kumbe umetukanwa na Mdogo wangu, ukamtumia hizi meseji Mama yako badala ya kunionyesha mimi, kwanza simu yako iko wapi?”

Alimniuliza hukua kininyang’anya simu yangu, aliichukua na kuanza kuangalia,a liangalia mesjei za wifi yangu ashakukuta kitu. Kishakaangalia meseji za mama yangu, kulikua na meseji moja tu ambayom mimi ndiyo nilionekana kama nilimtumia Mama yangu.

“Mama futa zile meseji nilizokutumia juzi, mume wangu amegombana na Dada yake, nakuomba sana futa!”
“Nimeseji gani ulikua unamuambia mama yako kufuta?” mume wangu aliniuliza lakini sikua najibu, hata hiyo meseji sikuituma mimi. Nikakumbuka kuna wkatai Mama alikua na simu yangu, nikajua ulikua ni mchezo wake.

Mume wangu alinibana sana lakini niligoma kabsia kumuambia, alinikasirikia akiamini namlinda dad ayake ila ukweli sikutaka kusshiriki kwenye ushetani wa mume wangu.
“Hakuna kitu, wifi hajawahi kunifanyia kitu kibaya, ananipenda, sijui hizo meseji umezipata wapi lakini hakuna ukweli wowote!” Nilimuambia.

“Hivi unapata faida gani kuongea uongo, hivi unaona kama tumempotez amtoto, kama dada yangu anahusika unafikiri nina sababu ya kumuita ndugu! Mama yako dniyo kanitumia hizi meseji na wewe ndiyo ulimmtumia, au unataka kuniambia Mama yako ni muongo?”

Aliniuliza, nilibaki kimya, bila hata kubadilisha nguo mume wangu alitoka kwa hasira, na kuniaha mule ndani nikiwa sna mawazo. Baada tu ya mume wangu kutoka Mama liingia huku akicheka sana, alianza kuongea mambo ya kumkomesha wifi yangu lakini mimi hata sikumsikiliza, nilikua nahasira na sijui ni kwa namna gani ningeweza kumuelezea mume wangu akaniamini kuwa Mama yangu ndiyo shetani.

*****

Kila nikitaka kunyanyuka Mama alikua hataki, alitaka niendelee kubaki kitandani, mimi nilishapona hivyo nilitaka kunyanyuka na kuendelea na mambo yangu. wiki ilikua imekatika na sikuona dalili za Mama kuondoka. Siku moja nilinyanyuka kitandani na kumuambia Mama aondoke kwani niko sawa kabisa.

“Una akili kweli? Hivi unafikiri tuliitoa hiyo mimba ili nije na kuondoka dakika mbili?” mama alijikuta anaropoka, nilimkodolea macho kama kumsuta lakini wala hakujali alirudia.
“Mimi ndiyo nilikutoa hiyo mimba na mimi ndiyo nitaamua kuwa unapona lini, Baba yako alikua sawa kuwa huna akili, unaumwa lakini hutaki kumtumia mwanaume wako!” alinifokea kwa hasira.

Nilimuambia kuwa mimi sitaki mali zozote za mume wangu, nina furaha na ndoa yangu.
“Najua wewe ni mbinafsi, sisi tumekuhangaikia kwa maombi na funga mpaka kuoelwa sasa hivi unataka kutusahau ni lazima mume wako kutusiadia, maisha ni kusaidiana!” aliniambia lakini mimi bado nilishika msimamo wa kuwa yeye ni lazima kuondoka.

Alinikubalia kwa shingo upande. Nilimuahidi kama ni kumsaidia nitamsaidia akiwa kwake lakini si yeye kuendelea kubaki kwangu. Alikubali kabisa mpaka nikashangaa, ingawa nilihisi labda kuna kitu,a na mpango wake lakinis ikujua ni kitu gani.

Mama alishawafanya ndugu wa mume wangu kupunguza kuja kwangu. Tangu wifi yangu kufukuza nilihisi mabadiliko, mtu pekee aliyekua anakuja kuniona alikua ni Mama mkwe pekee, wadogo zake na mume wangu hawakuja, nilihisi wameshaambiana ila hawakuamuambia Mama yao au aliambiwa lakini kwakua ni mtu mzima alishindwa kunichunia.

Mume wangu alikua ni mtu wa mawazo sana, muda mwingi akirudi nyumbani alikua ni mtu wa kujifungia chumbani, anafanya kazi zake haongei na mtu. Hata kuongea kwenye simu na ndugu zake ilikua ni mara chachechache sana.

“Baba mimi naomba niondoke….” Mama alimuambia mume wangu.
“Naona mkeo anaendelea vizuri, sioni kama msaada wangu unahitajika tena hapa.” Mama liongea kwa upole sana usiku wakati wa chakula. Nilimuona mume wangu akiitikia huku akimshukuru sana, ni kama naye alifurahia kwani hakumuambia baki hata ile ya kinafiki.

Asubuhi Mama ndiyo alikua mtu wa kwanza kuamka, alifanya kazi zote za ndani kisha kuja kutugongea chumbani ili kutuaga. Ilikua ni kama saa kumi na mbili za usiku, aligonga lakini sikumsikia, nilikua nimelala fofofo, mume wangu aliamka na kunishika ili kuniamsha.

Nilikua namsikia lakini sikuamka, kichwa kilikua kizito sana, kilikua kinauma kinagonga kama nini, jinsi alivyokua akinishika kuniamsha ndivyo nilikua nikisikia maumivu makali sana kichwani. Nilijikuta napiga kelele sana kutokana na maumivu.

“Niache! Naiche! Utaniua niache!” Nilipiga kelele kwa nguvu huku nikimsukuma mume wangu. Maumivu yalikua ni makali na niliyasikia yakismabaa mwili mzima kutoka kichwani mpaka kwenye unyayo wa miguu.

“Mama nakufaa! Mamama nakufaaa!” mama aliingia chumbani bila kujali kama mume wangu yupo, alipdna kitandani na kunishika kichwa, alianza kuongea manenoa mabyo hayeleweki ya kiatabu kama vile ananisome. Aliongea maneno mengi sana ambayo hayeleweki. Nilijua kuwa si kiarabu kwani Mama yangu hakusoma dini ya aina yoyote ile.

Wakati anafanya hivyo mimi hali ilizidi kuwa mbaya, nilianza kutetemeka mwili mzima huku maumivu yakizidi.
“Mtamuua mwanangu, kama ni mali mbona sisi hatuna shida na mali!” mama alimgeukia mume wangu.
“Unamaanisha nini Mama? Mbona sikuelewi!” Mumewangu aliongea kwa mshaao sana, ingawa nilikua katika maumivu makali lakini niliisikia sauti yake ya wasiwasi.
“Inamaana hujui mambo wanayofanya ndugu zako, wameniuliza mjukuu wangu na sasa wanataka kuniulia na Mwanangu….”

Kwa kumsikia ungedhani kuwa ni mtu mwenye uchungu lakini haikua hivyo. Nilijau tu kuna kitu Mama kanifanyia lakini nisingeweza kuongea mbele ya mume wangu.
“Mama tumpeleke hospitalini….”
“Ili ukamuue, hivi hujishtukii au kwakua ni ndugu zako, nilikutumia meseji ambazo mdogo wako alimtumia mke wako, sas ahivi unayaona haya! Mimi naondoka, sitaki kuingilia ndoa yako lakini sitaki uniletee maiti ya mwanangu, kama kifa utazika mwenyewe ni mke wako.”

Mama alinyanyuka na kuondoka, aliniacha pale chini nikiugulia maumivu. Mume wangu alinishika na kuninyanyua mpaka kweney gari huku nikipiga kelele, Mama alishaondoka zake, alitoka nnje na kuchukua Bajaji akaondoka bila kujali kitakachonitokea.

Mbali na maumivu makali lakini mwili likua unakua mwekundu, unatoa mapuneypunye ya kuvilia damu. Kilikua ni kitu cha haraharaka, yalikua ni mabadiliko ambayo sikuyategemea. Alinifikisha hospitalini nikiwa katika hali mbaya, sijitambui, yaani naona kama mapichapicha tu.

Nilikuja kuzinduka masaa nane baadaye, nilikusisikii maumivu lakini mwili bado ulikua unawake moto, tena sana. mume wangu alikua pembeni yangu akiniangalia.
“Kuna nini mke wangu mbona tunapitia mitihani mingi namna hii wakati dnoa yetu abdo changa?” aliniuliza lakini sikua na majibu, bado akili yangu ilikua haijakaa sawa tana.

“Mama amkeuja anasema si kitu cha hospitalini ni mambo ya kuhangaika kwamashehe lakini mimi samini. Mambo ya kishirikina siamini kabisa. Nikijua ni Mama yake nilimuambia amsikilize kwani kwa uhalisia nilijua kabisa kuwa kuna jkitu Mma ayangu kanifanyia hivyo kama nikisomewa vizuri basi nitakua sawa.

“Unaona kama kuna kitu mke wangu? Hata wewe unayaamini haya mambo?” Aliniuliza baada ya kuona nakubaliana na mawazo ya Mama.
“Nilikua siamini lakini baada ya kumpoteza mwanangu, na maumivu niliyopitia saubuhi namaini kuwa si kawaida, nahisi kuna kitu hivyo niko tayari kwa Dua.”

Nilimuambia huku nikamini kuwa, kama Mama yake kaona hiki kitu kwakua yeye ni mtu wa kusali na kuomba, anafunga mara kwa mara nilikua naimani kuwa ni lazima kuna kitu.lengolangu lilikua ni kumkomesha Mama yangu mzazi. Sikutaka aingilie maisha yangu tena.

Nilitokla hopspitalini loakini hatukurudi nyumbani, asubuhi kabsia mume wangu alinipeleka sehemu ambayo alielekezwa na Mama. Ni nyumba ya mtu, tena nzuri, tukakutanana ustadhi mmoja ambaye alianza kutusomea. Ikawa ndiyo kazi ya kila siku, mume wangu kabla ya kwenda kazinia likua akinipeleka pale ananiachanasomewa na mchana anakuja kunichukua.

Ingawa maumivu yaliisha lakini sikupata nafuu, nilianza kuwa kama zezeta flani hivi, yaani sijielwielewi. Nasomeawa lakini hali haibaidiliki. Mpaka siku moja nikamuambia mume wangu kama ni maombi basi tubadilishe mtu wa kunisomea dua.

“Mama alisema huyu mtu anamuamini, hivyo uwe na subira.” Aliniambia, nilijikuta nakuwa na wasiwasi sana kwani kwa kipindi cha wiki mbili nasomewa Mama mke wangua likua akinpigia simu tunaongea lakini hata siku moja alikuahajawhai kuniulizia kama naendeleaje.

Nilianza kuwa na wasiwasi kama anajau naumwa mpaka kunitafutia Ustadhi wa kunisomea kwanini hataki hata kuja kuniona au kuniulizia hali yangu.
“Kama anajali hivyombona hata simu hapigi, mbona naona kama vile hajali?” Nilijikuta namuuliza mume wangu. Mume wangu alishangaa kwani katibu kila siku Mama yangu alikua ananipigia simu kuongea naye.
“Mbona unaongea na Mama kila siku, asubuhi si nilikuambia kuwa kuna pesa nimemtumia….” Mume wangua liniambia, kusema kweli nilijihisi kutapika. Dawa zote na vizomo vyote nilitamani vitoke mwilini mwangu.

“Inamaana yule mchawi ndiyo amekuambia unilete huku!” nilimuambia mume wangu kwa hasira baada ya kusikia kuwa suala la kusomewa lilikua ni wazo la Mama yangu.
“Unamaanisha nini kumuita Mama yako mchawi!” Mume wangu aliniuliza kwa hasiea.
“Nmaanisha kuwa Mama yangu ni mchawi na kila kitu kinachotokea kwenye maisha yangu ni makosa yake. Mama ndiyo kanifanyia hivi vitu vyote, hata mimba yangu kutoka ni Mama!”

Njilimuambia, nilishachoka mambo ya Mama yangu, nikaona mbwai iwe mbwai! Sikutaka kuendelea kuteseka na madawa kusomewa wakati anjua mchawi ni nani? Mume wangu aliniangaliwa kwa hasira kisha akamaliza kwa kucheka!
“Acha ujinga, Mama yakoa kuologe wewe ilia pate nini? Naona bado hauko sawa!” aliniambia, nilijaribu kumueelewesha lakinia ligoma kunisikia. Mwisho nilaimua kumuambia kila kitu kuhusu Mama yangu.

“Walikua hawajui kama kwenu mna pesa, uliponiinunulia gari kila kitu kilibadilika, sasa hivi Mama yangu anachotaka ni kujua kila kitu katika maisha yako. Anataka kujua kama mali ni za nani, kama zina majina ya nani, mshara wako na vitu kama hivyo. Hata kuhusu dada yako zile meseji zote ni za kutungwa.

Alikutumia yeye na si dada yako, lengo ni wewe kuichukia familia yako, anaamjini kamaukiwa mbali na familia yako basi ndiyo ataweza kukucontrol. Niamini nikikuambia kuwa Mama yangu ni shetani….” Niliongea huku nikitetemeka kwa hasira.

HALIMA anaamua kumuambia mume wake ukweli, je unahisi mume wake atamuelewa, vipi atakata mawasiliano na Mama yake, usikose sehemu ya Nne. @aziranimagazine



(ILIPOISHIA SEHEMU TA TATU; Baada ya kuona vituko vya Mama yake vimezidi, ameanza kumpeleka mpaka kwa waganga, Halima anaamaua kumuambia mume wake ukweli. Anamuambia kila, kitu kuanzia namana alivyotengeneza meseji za kumshutumu wifi yake mpaka kuhusu yeye kupoteza mtoto.

Je, mume wake atamsikia na kumuelewa au naye ndiyo dawa zioshakolea, basi nisikuchoshe, ENDELEA….)

“Mama yako anaweza kukufanyia kitu kama hiki kweli?” Mume wangu aliniuliza, alikua kama anachekacheka, kama vile haniamini.
“Kwani pesa ni kitu gani, mbona ananiomba pesa nampaga, kuna shida yoyote, kama kuna kitu anahitaji si angeniambia, vitu kama hivi haviingii akilini kabisa.” Aliniambia, nilijaribu kumuelewesha sana kumuonyesha tofauti ya sisi na wao.

Yeye alitoka katika familia ya kitajiri, mambo ya pesa kwao haikua shida kabisa, kugombana kwasababu ya mali kilikua kitu cha ajabu kwao sembuse kufikia hatua ya kutaka hata kumuua binti yako kwasababu ya mali.

“Una roho nzuri sana mume wangu, lakini ulimwengu hauko hivyo kabisa. Mimi nilianza kumuogopa Mama yangu kipindi Dada yangu anaolewa, Mama hakutaka kabsia Dada yangu asiolewe kwakua tu mwanaume hakua na pesa, ndiyo maana wakati nikiwa kwenye mahusiano na wewe sikutaka kabisa wao kujua hali yako ya kimaisha.

Kosa nililofanya ni kupokea Gari yako, iliwauma sana ni kwanini mimi naishi maisha mazuri wakati wao wanateseka…” Mume wangu alinisikia, aliniambia niachane na hayo mambo tena. Ashaujua ukweli hivyo hataki kuyazungumzia.
“Kwahiyo unamaanisha kuwa Dada yangu hana shida yoyote, shida kubwa ni kwakua wazazi wako wanataka mali zangu?” Aliniuliza, nilimuhakikishia kuwa wifi ni mtu mzuri na hana shida.

“Nimeona nikuambie, kama utaamua kuniacha kwakua tu familia yangu iko hivyo basi niache, lakini siwezi kukubali hali hiyo kuendelea. Unatoka katika familia nzuri, wewe ni mtu mzuri, tena sana, siwezi kuharibu maisha ya familia yako kwakua tu familia yangu ni masikini, sitakua na raha kamwe kama nikikufanyia hivyo.”

Nilimuambia, alinihakikishia kabisa kuwa hawezi kuniacha kwani ananipenda, uliachana kabisa na mambo ya kusomewa.

Sikutaka kuendelea tena kuharibu ndao yangu, nilimpigia simu Mama na kumaumbia kuwa niemshamuambia ukweli kuhusu kila kitu alichonifanyia, sitaki kabisa kumuona kwenye maisha yangu.
“Ukweli gani mwanangu ambao unauzungumzia, mbona mimi sijafanya kitu chochote!” Mama aliongea kwa sauti ya mshangao, ungemsikiliza ungedhani ni mtu tofauti kabisa, alijua sana kuigiza.

“Hata kama hujafanya kitu lakini sikutaki katika maisha yangu! Utabaki kuwa Mama yangu lakini mambo ya mali na kunipangia namna ya kuishi na mume wangu sitaki kuyasikia!” Alinisikiliza kwa makini na kunijibu tu neno moja “Sawa kama ndiyo umeamua hivyo.”

Kisha alikata simu, kidogo nilikua na amani, ingawa sikua na uhakika kama Mama yangu ataendelea kutusumbua lakini angalau nilikua na amaani kuwa mume wangu anaujua ukweli na hawezi kugombana na ndugu zake, akaichukia familia yake kwasababu ya uongo wa Mama yangu.

Wiki ilipita bila kumsikia Mama wala kuongea na ndugu zangu wowote.
“Mama anaendeleaje, si kawaida yake kukaa kimya, sijampigia kwani bado nina hasira naye, lakini sitaki ugombane na ndugu zako kwaajili yangu?” Ingawa mwanzo nilikua sijui lakini kumbe Mama yangu tangu kujua kuwa mume wangu ana pesa, kila siku alikua anampigia simu, kumsalimia na mwisho kulalamika.

Mama yangu ni wale wanawake ambao hawezi kukuomba pesa moja kwa moja lakini kama ni mtu mwenye akili basi utajua kuwa anaomba. Anaweza kukupigia simu mkaongea vizuri ila mwisho akamalizia “Haya mwanangu, kifurushi nacho kimesiha na gesi ndiyo naona haitafika usiku, Baba yako ameenda kuhangaika hangaika sijui kama atapata!”

Hajakuomba lakini unajikuta unamtumia pesa, alikua akifanya hivyo kwangu na kumbe hata mume wangu alikua naye akimpigia.
“Sitaki kujua mambo yao, nataka kuwa na amani…” Nilimjibu mume wangu, naye hakusema chochote. Hali yangu kiafya ilianza kuimarika, tangu kuachana na mambo ya kusomewa na kuhudumiwa na Mama kila kitu kilianza kuwa vizuri kwangu, hiyo pia ilimuaminisha mume wangu maneno yangu kuhusu Mama yangu.

Kuondoka kwa Mama yangu kulinifanya kuwa karibu tena na ndugu wa mume wangu. Nilimuomba msamaha wifi yangu naye alikubali, Mama mkwe alikua hajui chochote lakini kipindi Mama anaishi kwangu ni kama alihisi kitu kwani mtoto wake alibadilika kidogo, ila baada ya kila kitu kuwa sawa nikaanza tena kuwa karibu na Mama mkwe wangu.

Wiki mbili baada ya mimi kumuambia mume wangu ukweli nilikua nipo WhatsApp, naangalia status za watu. Mara nikaona picha ya Mama yangu kwenye status za wifi yangu.
“Nashukuru Mama nyangu, unafiki kwako mwisho!” Wifi yangu aliandika kwenye status yake. Kusema kweli nilihisi kama nimepigwa huna kitu kizito kichwani, nilishangaa sana ni kwa namna gani wifi yangu anakua na ukaribu na Mama yangu, mtu ambaye hata walikua hawajuani, mtu ambaye siku ya kwanza kuonana naye alimtukana kiasi kile!

Nilijaribu kuvumilia lakini nilishindwa, jana yake tu nilikua naongea na wifi yangu na tulikua vizuri leo kwanini ampost Mama yangu? Sikua na majibu, niliamua kumpigia simu ili kumuuliza kwanini amempost Mama yangu. Nilipiga simu zadi ya mara kumi lakini haikupokelewa.

Sijui kwanini lakini nilipagawa, nilipaniki nikawa napiga kama chizi kutaka kujua nini kinaendelea lakini simu haikupekelewa, nilirudi WhatsApp ili kumtumie meseji ila nikakuta kapost picha nyingine, hii ndiyo iliniumiza zaidi, alikua nyumbani kwetu, sebuleni yuko na Mama yangu, wamekaa wanakula.

“Umefanya nini Mama, kwanini huniachi na maisha yangu?:” Nilimpigia simu Mama ambaye aliipokea na kuniongelesha kama vile hakuna kitu kilichotokea.
“Unamaanisha nini Mwanangu?” Mama aliniuliza kwa sauti yake ya upole.
“Namaanisha umemshindwa mume wangu sasa unahamia kwa ndugu zake, hivi una nini Mama?”
“Mimi hata sikuelewi, uliniambia niachane na ndoa yako, nisikanyage nyumbani kwako, na hata mume wako nisimpigie simu yote nilikubali, au umesahau na meseji ulizonitumia kuniita mchawi niachane na ndoa yako?”

Nikweli nilimuita mchawi, nilimtumia meseji nyingi lakini zilikua za hasira.
“Nimeachana na ndoa yako, sasa unanitakia nini tena? Mimi si sio Mama yako?” Aliniuliza, nilibaki tu kimya.
“Basi niache, kama hutaki kuongea na mimi, kama hunioni mimi kama Mama yako basi jua kuna watu wananipenda na kuniona kama Mqma yao, hivyo kaa mbali na mimi!”

Aliongea kwa ukali na kukata simu. Nilishindwa kuvumilia, nilimpigia simu mume wangu ili angalau kuongea naye kwani nilihisi kama vile kuchanganyikiwa. Kwa bahati mbaya mume wangu naye hakupokea simu, nikajikuta nampigia simu tena wifi yangu, safari hii alipokea.

“Nakusikiliza ulikua uansemaje wifi?” Aliniuliza baada ya kuona niko kimya sana, ni kweli nilikua hata sijui ni kitu gani cha kumuambia.
“Nimekuona umempost Mama yangu, naona pia ulikua nyumbani kwetu?” Nilijikuta namuuliza. Baada ya yale maneno kunitoka mdomoni ndipo niligundua kuwa lilikua ni swali la kipumbavu.
“Ndiyo nimempost, nilikua kwenu pia, Mama ndiyo alinialika, au kuna shida wifi? Au ulikua hutaki niende nyumbani kwenu?”

Nilijiona mjinga zaidi nikabaki kimya.
“Hakuna, sikujua kama Mama yangu mna ukaribu wa namna hiyo, baada ya ile siku nilihisi labda hamtaongea tena….” Nilijisemesha.
“Kwahiyo ulitaka nisiongee na Mama yako?”
“Hapana, sikumaanisha hivyo?”
“Ulimaanisha nini? Ulimaanisha kuwa kuna vitu umevifanya labda hutaki niwe karibu na Mama yako, nitavijua au nitajua kuhusu wewe au ulikua unamaanisha nini?” Aliniuliza maswali ambayo yalikaa kimtego, kwa namna alivyokua anaongea nilihisi lazima Mama yangu ashaanza kumteka akili.

Sikujua ni kitu gani Mama yangua alifanya mpaka wifi yangu kumuamini tena na kuwa karibu naye namna ile ila nilijua kuwa hakikua kizuri.
“Mbona kimya wifi? Kuna kitu nimekosea kuwa karibu na Mama yako, kama nakumbuka vizuri ni wewe uliniambia kuwa Mama yako ni mtu mzima, kuna wakati akili zake haziko nzuri nimsamehe, nimeamua kumsamehe amekua kama Mama yangu au hilo nalo lina shida…”

Ingawa mimi ndiyo nilikua nimepiga lakini nilijikuta nakata simu kwa hasira, niliona kama Mama ameshinda, sikujua mama alikua anataka nini kwa wifi yangu kwani hakua na hela kihivyo. Wifi yangu alikua anafanya kazi nzuri kweli ila kipato chake kilikua kidogo akitegemea msharahara.

Pesa zake nyingine zilikua ni mali za familia ambazo alikua akisimamia mume wangu. Hakua ni mtu wa matumizi na hakua anajua kitu chochote kuhusu biashara, yeye akwia na shida ya pesa alimuambia mume wangu.

Labda anataka kubadilisha Gari, anataka kutoka na marafiki zake hana pesa alikua akimuambia mume wangu, silikua ni pesa za kawaida, sikujua kabisa Mama anataka nini kwa wifi yangu ila nilikua nauhakika kuwa si kitu kizuri, na kingekuja kunigeuka kuniharibia ndoa yangu.

*****

“Sasa mimi nifanye nini kama kaamua kumsamehe?” Mume wangu aliniambia kila mara nilipokua namuambia aongee na mdogo wake kuhusu Mama yangu. Ingawa mambo yalikua yamepooza, nilishapata nafuu karibia kupona lakini sikua na amani kabisa, nilijua Mama yangu kuna kitu anataka kukifanya.

Ukaribu wake na wifi yangu ulionifanya kutokua na amani, kisirani kila siku kugombana na mume wangu, hata ndoa nilianza kuiona chungu. Ndiyo kwanza ilikua na miezi minne lakini kulikua na matukio mengi kama ndoa ya miaka kumi.

Nikiwa sina hili wala lile siku moja nilipigiwa simu na Mama mkwe wangu.
“Mkwe kuna wageni wanakuja Jumamosi, sijui kama wifi yako kashakuambia lakini kama Mama nimeona nikuambie mimi mwenyewe, nilimuambia mume wako asikuambie mpaka niongee na wewe.” Mama aliniambia.
“Wageni gani Mama? Bado wifi hajaniambia bado, hatujaongea siku mbili hizi…” Niliuliza kwa shauku.

“Wifi yako amepata nusura, kuna mwanaume anataka kumuoa, sasa jumamosi anakuja kujitambulisha. Sio kutoa mahari, hapana, anataka kuja kumtambulisha ili tumfahamu, ni kashughuli kadogo lakini nimeona nikuambie kwani wewe nawe ni mwana familia.” Mama aliniambia.

Nilitamani kujua ni nani alikua anakuja kujitambulisha lakini nisingeweza kumuuliza Mama mkwe wangu. Nilimuitikia kuwa nimesikia na nitaenda siku hiyo. Muda ulikua umepita bila mimi kuonana na wifi yangu, tukiongea kwenye simu ilikua ni kulumbana, ishu ile kwangu ilikua ni kama sababu ya sisi kuonana.

Pia nilifurahi kama akiwa na mwanaume basi atakua bize na maisha yake na kuachana na Mama yangu. Mume wangu hakuniambia kitu chochote mpaka nilipomuuliza.
“Mama aliniambia atakuambia yeye mwenyewe, si unajua mambo ya wanawake…” aliniambia na nilimuelewa.
“Ila sio lazima ni kitu kidogo, hata sioni umuhimu wake, wala sio hata ishu ya mahari, ni mwanaume anakuja tu, hata sijui kama mimi nitaenda…” Mume wangu aliongea.

Kuna kitu nilihisi, aliongea kana kwamba hataki niende, nilishangaa kwani ilikua si kawaida yake.
“Kuna nini, kwanini nisiende, Mama mwenyewe kanialika?” Nilimuuliza.
“Sijamaanisha vibaya, nimekuambia tu, kuwa unaweza usiende, mimi sijui kama nitaenda ila uamuzi ni wako. Kwani mwenyewe kakuambia au ni Mama?” Aliniuliza swali ambalo lilinionyesha kuwa inawezekana wifi yangu hakutaka niende, lakini kwakua nilitaka kwenda kuonana naye na sikutaka kumuudhi Mama mkwe nilimuambia nitaenda kwasababu ya Mama.

Siku ya shuguli nilienda mapema kabisa, tofauti na ambavyo mume wangu aliniambia kuwa anaweza asiende tulienda wote na alionekana kuipania. Kalikua ni kashughuli kadogo lakini kakisasa, nyumba ilipambwa na ndugu wa damu tu ndiyo walikuepo, Mume wangu, wadgogo zake na Mama yake, hakukua na ndugu mwingine yoyote yule.

Hakukua na kuipika, walikodi mpishi hivyo sisi tulienda kusubiria tu. Wifi yangu siku hiyo ni kama alikua ananikwepa, alivaa vizuri, akapambwa na kupambika. Sijui kwanini lakini roho yangu ilikua inandunda sana, yaani ni kama nilihisi kuna kitu kibaya kinaenda kutokea ingawa sikujua ni nini?

Wageni walipokuja ndipo nilijua ni kwanini nilikua na wasiwawasi namna ile. Walikua wakaka wawili, mmoja nilikua simfahamu kabisa, sijawahi kuonana naye katika maisha yangu na mwingine alikua ni X wangu Elibariki (sio jina lake halisi). Mwanaume ambaye kabla ya kukutana na mume wangu nilikaa naye kwenye mahusiano kwa muda wa kama mwaka mmoja hivi.

Nilishamtambulisha mpaka nyumbani lakini tulikuja kuachana kwasababu ya dini. Mama alipojua kuwa ni muikristo alikataa hata kumuona, wakati huo mimi nilikua tayari kabisa kubadilisha dini kwaajili yake. Lakini tukiwa katika hiyo misuguano niliona kama kabadilika, akawa hajali tena, nikimpigia simu zangu hapokei na mambo kibao.

Mwisho nikaamua kuachana naye, baaada ya mimi kuachana naye sasa ndipo niliona anaanza mazoea na Mama yangu, wanapigiana simu, Mama anakua ananiulizia kuhusu huyo mwanaume na hata kuna wakati mwingine alikua ananiambia nikubali tu kuolewa nibaidlishe na dini lakini mimi sikutaka.

Kwanza alishaanza mambo ya Pombe, kuongea na mimi kwa dharau, alikua analewa mpaka kufikia kusimamsihwa kazi, nikimuuliza ananiambia ni kwakua nimemkataa, Mama naye alikua akiniiambia anamuonea huruma hivyo nibadilishe dini kwaajili yake kwani wanaume ni wachache.

Nilishangaa kumuona pale kwani kabla kuolewa naye alifunga ndoa tena ya Kanisani na mwanamke mwingine ila hawakudumu sana kwani mwanamke alimkimbia. Tuliwakaribisha vizuri, sikutaka kujifanya kama namjua, ingawa nilikua na wasiwasi sana lakini nilihisi kamsindikiza tu yule mwingine ambaye niliku simjui.

Haikua hivyo, wakati wa kutambulisha wifi yangu alimtambulisha kama mchumba wake, tena hakumtambulisha kwa jina niliokuja nikimfahamu. Alimtambulisha kama Abubakari. Hapo ndipo niliishiwa pozi kabisa, sikujua wamekutana lini, ni lini alibadilisha dini, ni lini alimpa talaka mke wake lakini kitu ambacho nilikua na uhakika nacho nikuwa Mama yangu alikua anahusika kuwaunganisha.

Ilikua ngumu kuamini kuwa, siku zote naongea na wifi yangu ananiambia hana mtu, analaalamika kuhusiana na mahusinao, namana ambavyo hana bahati na wanaume, ghafla anakutana na mwanaume tena X wangu na mbaya zaidi baada ya kuanza kuwa na urafiki na Mama yangu, hapana nilijua lazima kuna kitu hakiko sawa.

Nilinymaza kimya mpaka shughuli ilipoisha, Elibariki alinichunia kabisa, alijifanya hanijui nami pia nilijifanya simjui, sikuongea kitu chochote mpaka walipoondoka. Nilijua lazima kuna mchezo wifi yangu anachezewa na sikutaka iwe hivo, nilijua lazima Mama yangu anahusika.

Baada ya wageni kuondoka nilitamani sana kuongea na wifi yangu lakini hakunipa nafasi, nilimtumkia mpaka meseji kuwa nataka kuongea naye kuna kitu nataka kumuambia lakini hakunijibu.

“Wifi kamjua lini yule Kaka?” nilimuuliza mume wangu baada ya kumaliza sherehe wakati tunarudi nyumbani.
“Hata sijui aisee, mimi hata nilikua sifahamu kama ana mahusiano, ndiyo kwanza nimemuona hii leo.
“Kwanini huchunguzi sasa, wewe ni Kaka yake, unamfahamu vizuri huyo mwanaume, kama anamdanganya? Kama anataka kumharibia maisha yake?”
“Kivipi anamdanganya mbona sikuelewi?” Aliniuliza, nilibaki kimya nikifikiria kitu cha kumuambia lakini sikua na jibu la maanaa.

“Sijui lakini anaonekana kama si mkweli, ungecghunguza kujua Dada yako anaenda kwenye familia ya namna gani?” Nilimuambia lakini hakuonyesha kujali, alijaribu kubadilisha stori lakini mimi nilirudi palepale, mpaka mume wangu akakasirika.

“Una nini na Dada yangu? Au hutaki aolewe, mbona naona unachukia yeye kupata mwanaume, mwanaume umemjua leo ushaanza kutoa kasoro!”
“Sio hivyo, nataka tu uchunguze dada yako asijekuingia mkenge, si unajau ana pesa isije kuwa amepenende mali zake!”
Mume wangu alikasirika kiasi cha kusimamisha gari!
“Haya niambie, amefuata mali gani? Yaani kweli unataka kuniambia unamchuikia wifi yako namna hiyo mpaka huamini kuwa anaweza kupata mwanaume akampenda bila kujali mali zake?”

“Sio hivyo mume wangu, lakini….” Lakini nini? Au kuna kitu unanificha! Unajua nilikua najiuliza ni kwanini Dada yangu hataki uje lakini sikua na majibu? Hivi mwanaume umemuona tu kwa macho unaanza habari za mali!

Unafikiri kila mtu anawaza mali tu, au hata Mama yako alikua mkweli umeona yamekushinda ndiyo ukaanza kumuita Mchawi!?” Nilijua nimebugi, nikamuomba mume wangu msamaha, hakunijibu alibaki kimya mpaka tunafika nyumbani.

Khadija anataka kuolewana X wa wifi yake, unadhani ndoa itafungwa, je Mama Halima anataka nini, nini kilitokea, usikose ndiyo kwanza bado asubuhiii!



(ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE; Khadija anaenda kumtambulisha mchumba wake, wifi yake anagundua kuwa ni X wake, anaamua kumuambia mume wake amchunguze vizurin lakini kibao kinamgeukia, uandhani ni nini kitatokea? ENDELEA…)

Mume wangua likasitika sana, kwa mara ya wkanza mume wangu aliniongelea maneno mambaya. Kusema kweli nilimuelewa, ingawa nilijisikia vibaya kwani ni mume wangu alipaswa kuwa upande wangu ila kwa upande mwingine nilimuelewa.

Dada yake alikua hajawahi kuwa na bahati kwenye mahusiano, wanaume wengi walikua ni wa kumuumiza, ingawa hakua mtu wa kuongea kwa Kaka yake ila mimi nilikua najua na nahisi mume wangu alijua.

“Naomba unisamehe, sijui nawaza nini lakini suala la Mama kuwa karibu na wifi baada ya mambo yote yale mpaka leo linanichanganya.” Nilimuambia mume wangu, kwa bahati nzuri alinielewa.
“Sitaki tena hiyo Mada, nakuambia sitaki, dad ayangu ana furaha, muache na maisha yake, kama mwanaume kampendea pesa ni yeye, hayatuhusu!” Aliniambia huku akiinikumbatia.
“Nimekuelewa mume wangu nitaachana na haya mambo, hata ishu za Mama sitaki kuzisikia tena.” Nilimkumbatia mume wangu na kila kitu kiliicha wakati uleule.

Mume wangu ni ile aina ya watu abao akiikuambia kitu kimeisha basi kimeisha, nilijua wazi siwezi kumuuliza tena kuhusu Mahusiano ya dada yake lakini moyoni sikua na amani. Nilijua ni mpango tu wa Mama yangu, nilijua kama nisipofanya kitu basi Mama taniharibia ndoa yangu.

Nilikaa kama siku mbili hivi bado nikiwaza kitu cha kufanya, pamoja na kuambiwa niache mambo ya watu lakini sikua na amaani. Niliamua kumpigia mdogo wangu simu ili kumuuliza mambo nyumbani yanaendeleaje.
“Tuko sawa, hakuna shdia yoyote.’ Alinijibu, hakunipa nilichokua nikikitaka, ni kama alikua ananikwepa. Nilihangaika sana kupata taarifa lakini ilishindikana, wakati nawaza ndipo nilikumbuka kitu kimoja.

Wakati Elibariki yuko kwenye ndoa na mke wake alikua akinisumbua sana, aliniambia kila siku kuwa ananipenda na yuko tayari kauchana na mke wake kwaajili yangu. Hiyo ilikua ni moja ya sababu ya yeye kukimbiwa na mke wake, ndoa yao ilikua hina amanai, mke wake alishanitafuta kwenye simu mara nyingi kunilalamikia kuhusu mume wake.

Akinionya niachane na mume wake, nikakumbuka kuwa nina namba yake kwani namba nasave Google. Ingawa nilikua najua kuwa wameshaachana lakini sikua na uhakika kama wamepeana talaka ya mkahakamani au la. Nilimtafuta Kaka mmoja ambaye ni dereva Bodaboda na kumuomba anisajilie namba mpya.

Niliichukua ile laini na kufungua Whatsapp kisha nikamtafuta yule dada, nilichokifanya ni kumtumia pciha za wifi yangu na mchumba wake. Picha za kutambulishana, ingawa hazikua picha za mapenzi lakini kuna miako unaona kabisa huyu mwanaume kaja kutambulishwa.

Nilimtumia nikiamini kuwa, kama bado wana ndoa basi yule Dada atapaniki na kutaka kujua nini kinaendelea. Hata haikuchukua muda, alinitumia meseji kuniuliza mimi ni nani na kwanini namtumia picha za X wake.
“Kumbe mshaachana, basi nilijua kama bado mpo kwenye ndoa kwani naiskia katangaza ndoa sehemu nyingine.”

Alitaka sana kujua jina langu lakini nilimuambia hapana, nilimuambia tu ni msamaria mwema, kama wameshaachana basi. Nilaicha kuchart naye na kuikaa kimya nikisubiri kciwha kipate moto.

“Nimeachana naye lakini hatujapeana talaka, ninamtoto naye, hamhudumii mtoto, mimi ndiyo nahangaika na mtoto kila siku. Haitoshi nina ujauzito wake, yaani ameniacha lakini kila akija kusalimia mtoto analazimisha kuwa ili anipe matumizi lazima tulale naye….” Dada alianza kufunguka magazeti, nikaanza kumdadisi zaidi kwani ndiyo kitu nilichokua nakitaka.

“Anataka kuoa, kumbe ndiyo maana juzi kanitafuta anataka kunipa pesa ili nitoe hii mimba yake, itakua huyo mwanamke hajui kitu chochote kuhusiana na mimi! Sidhani kama hata anajua kama aliwahi kuoa!” Alinimbia.
“Mwnamake Muisalamu, anabadilisha dini kwajaili yake, sidhani kama dada wa watu anajua. Pigania ndoa yako, unaenda kujifungua mtoto wa pili, hivi mwanaume anakuambia utoe mimba ina miezi nane unafikiria nini?

Nenda kuongea naye, usikubali huo ujinga aisee, nimekuambia mapema, hata ukitaka namba za huyo mwanamke mimi nitakupa, lakini anza kuongea na Eli kwanza.” Nilimuambia yule dada, baada ya kuoona kanielewa nilijitoa whatsapp, nikafuta kila kitu cha ile namba na kuka akimya nikisubiria majibu.

****
Wiki mbili zilipita bila kusikia kitu chochote, nilitamani kumuuliza mume wangu ila nilikua naogopa kwani alishanikataza kuingilia mambo ya wtau. Siku moja nikiwa nyumbani mume wangu alinipigia simu.
Aliniambia kuwa atachelea kurudi nyumbani kwakua Dada yake akapata ajali na kaumia kichwani. Niliogopa sana, wifi alikua hospitalini, lakini hakukaa sana, alishocnwa nuzi 21 na kuruhusiwa.

“Sina uhakika kama ni ajali, anasema alipanda bodboda, tangu lini Khadija na bodaboda!” mume wangu alilalamika baada ya kurudi nyumbani.
“Kuna nini? Kwanini adanganye sasa?” Nilimuuliza.
“Hata mimi sijali ila nahisi kama vile hayuko sawa, kabisa, kunakitu kinamsumbua ila sijajua ni nini? Nahisi kama kapigana, sijui ila nahisi kuna mtu kamppiga, ule mpasuka si wa ajali kabisa.”

Sikuwaza chochote mpaka Mama aliponipigia simu kunisalimia. Tuliongea kidogo,a liongea na mimi kama vile ananichimbachimba kujua mambo katika familia yangu yanaendeleaje lakini sikumuambia kitu chochote.
“Mume wako anasemaje? Mbona hutaki kuongea kitu chochote, wifi yako kamuambia kitu!?” Mama aliongea kwa wasiwasi, nilishangaa kwani Mama alikua si mtu wa kujinyenyekeza kiasi kile.

“Umanaaanisha nini, kamkuambia kitu gani?” Nilimuuliza, yeye alikua anaamini kuwa ninajua.
“Unajua kila kitu na ulishawahi kuulizia, wifi yako kapigana na Mama Prisca (Mke wa Elibariki) walikua wametoka kamtafuta dada wa watu, kampiga kamvunjia chupa usoni!” mama aliongea, nilimuuliza yeye kajuaje hayo mambo ila hakuniambia, nilimkazia.

“Kama huwezi kuniambia basi na mimi siwezi kukuambia.” Nilimuambia kisha nikakata simu, mwili ulikua unanitetemeka, nilimuambia Mama Prisca ili kuja kuharibu lakini sikujua kama atakuja kumdhuru wifi yangu. Baada ya kama dakika mbili hivi kabla hata sijafanya kitu chochote mama alipiga simu.

“Mimi ndiyo nilimuunganishia wifi yako kwa yule mwanaume, ni rafiki yangu, alikua hana kazi maisha yememshinda nikaona niwaunganishie, kija wa watu kabaidlisha na dini ili kumuoa wifi yako….” Mama aliamua kuniambia ukweli.
“Nilijua tu unahusika, hivi mama utaachana lini na ndoa yangu, si nilishakuambia kuwa achana na mimi!?”
“Wewe nilishachana nawe, nimemtafuta wifi yako kwakua ana pes aila hana mwanaume, sasa kuna ubaya gani hapo mimi kumsaidia!?”

Mama aliongea kama vile ni kitu cha kawaida sana, hakujua kua alichokua anakifanya ni ushetani. Nilimsema sana lakini yeye alichotaka kujua ni kama mume wangu kajua kuwa yule kijana ana mke na Dada yake kapigwa.
“Hapana, sidhani kama kamuambia, ila mimi nitamuambia, ni mume wangu, anatakiwa kujua ukweli.” Mama alinisihi sana nisimuambie mume wangu lakini nilisema hapana, Khadija hawezi kujisimamia, na kama wakiendelea na mpango wao basi atakuja kuumia huko mbeleni.

Nilimkatia simu Mama ila baada ya kama dakika kumi hivia lipiga tena simu.
“Shetani mkubwa wewe, unajifanya hujui kitu chochote kumbe ulikua unanichora! Yaani wewe ndiyo wa kumtafuta mke wa X wako ili kuja kumpiga wifi yako!” Mama aliongea kwa hasira, alinitukana sana kisha akakata simu.

Alikata simu lakini hakua na amani, alinitumia mesjei nyingi zana za vitisho. Mara simu yangu ikaita, ilikua ni namba ngeni, nilipokea na sauti ilikua ni ya Eli, tulisalimiana vizuri, tofauti na nilivyodhani kuwa labda atanitukana aliongea kwa upole.
“Naomba kuonana na wewe, naomba uje kunisikiliza ili ujue ni kitu gani kinaendelea, najua ulimtafuta mke wangu lakini huyo mwanamke kuna sababu niliachana naye.”

Aliongea kama binadamu, alinisihi sana kufanya mpango wa kuonana naye siku hiyohiyo.
“Hali ya Khadina ni mbaya, ananiona kama tapeli, najua hata wewe unaniona kama tapeli kwasababu ya Mama yako. Nikweli nilikutana naye kwasababu ya Mama yako, najua pia sababu za Mam ayako kutaka mimi nimuoe, lakini mimi siko hivyo, umenifudnisha mambo mengi sana.

Baada ya kcuhana ana wewe maisha yangu hayajaswahi kuwa sawa, naomba uje unisikilize.”

Aliniambia kwa kunisihi sana, nilimuambia mjume wangu kuwa naenda nyumbani kuonana na Mama kwani hayuko vizuri na kanipigia simu kutaka niende. Mume wangu alikua hayuko sawa, ana mawazo mengi hivyo alinikubalia. Niliondoka mpaka sehemu niliyopanga kukutana naye.

Nilimkuata akiwa amepoa kabisa, alinikaribisha kunywa soda, niliagiza, nikiwa niko pale hata kabla hatujaongea kitu chochote, Mama Prisca alikuja, hapo nikashtuka kidogo, nilihisi kama vile ni mtego flani, nikanyanyuka na kutaka kuondoka lakini alinizuia.

“Usiondoke, huu sio mtego, kuna kitu nataka usikie kutoka wka huyu mwanamke ili uweze kuniamini, nimekuita hapa ili uisikie mwenyewe.” Aliniambia, nilitulia na kukaa, nilitaka tuongee harakaharaka ili nirudi nyumbani lakini mazungumzo hayakuanza, ilikua ni jioni na haikau kawiada yangu mimi kutoka mpaka wakati ule.

“Tunasubiri nini? Mbona mnaangalia kamavile kuna mtu mnamsubiria?” Nilimuuliza Eli lakini hakutaka kuongea, aliniambia nisubiri tu, kama nusu saa hivi gari ilizimama. Ilikua ni gari ya wifi nyangu, mwanzo nilijipa moyo kuwa labda ni gari ya mwtu mwingine lakini fumba na kufumbua wifi yangu huyu hapa, anashuka kwneye gari na mabandeji yake kichwani.

“Nimekuja harakaharaka, uniambie unanitakia nini maana nimechoka mambo yako, nyumbani hawjaui hata kama nimetoka!?” Aliongewa kwa hasira, nilijua kabisa kama mimi hata yeye hakytaka kuwpo pale, alionekana kuvurugwa sana kiasi kwamba hata hakuniona nilipokua nimekaa.

“Usiwe na haraka, kaa na salimiana na wifi yako….” Eli alimuambia, alimuoneysha sehemu ya kukaa, hapo ndipo wifia liniona na kushangaa nilikua nafanya nini pale.
“Huyu anafanya nini hapa? Wewe si uliniambia nisishirikishe ndugu zangu? Ukaniambia nakuja kukutana na mwanamke wako sijui kuna kitu anataka kuniambia, sijui anataka kuniomba msamaha, sasa mambo ya kumleta wifi yangu yanatoka wapi?”

Aliuliza kwa hasira, kwekweli hata mimi nilitaka kujua maana sikuambiw kitu chochote kuhusu kuwepo kwa wale wanawake wawili pale.
“Tulia, huyu ni lazima kuwepo, yeye ndiyo chanzo cha mambo yote haya, yeye ndiyo mzizi mpaka kupelekea wewe kupigwa, sasa ni lazima huu ukweli uongelewe.” Eli aliongea.

“Chanzo gani, mimi nahusika nini na mambo yenu?” Niliuliza kwa mshangao huku nikinyanyuka kutaka kuondoka, lakini Eli alinishika na kuniambia kuwa nikiondoka atampigai simu na mume wangu ili ajue ukweli wote.

“Nakuambia hivii, siwezi kukubali ndoa yangu kufa kwaajili yako, ulsihainharibia mahusiano yangu ya kwanza sas ahivi huwezi kuniharibia tena…”

Aliniambia huku akianza kulia, nilishangaa “Nimahusiano gani tena haya nimeharibu?” Nilijiulzia bila jibu, bila kutaka nililazimika kukaa ili kumsikiliza.
“Halima ni rafiki yangu, nimejuana naye kwa zaidi ya miaka kumisa mimi tangu mwanzo nilikua namchukulia kama rafiki yangu, sikujua kuwa mwenzangu ananipenda, basi kutokana na ukaribu wangu kwake, alinipeleka kwao, nilimjua Mama yake na ndugu zake wengine.

Mama yake alinipoke avizuri sana, yule Mama ni mtu mzuri sana….” Alitulia kidogo na kujifanya kama anafuta machozi.
“Unaongea nini wewe mpumbavu, mbona unakua hivi…” nilijua kabisa anataka kudanganya sikutaka kumpa nafasi ya kunichafua, nilipaniki na kuanza kutukana huku nikinyanyuka ili kuondoka. Lakini hakuniacha,a linishika na kunikandamizia chini.

“Ghafla niliona Mama yaka anaanza kunichukia, mara sijui ahataki niende kwao tena, ikafikia hatua mpaka Baba yake anataka kuniua. Mimi hapo sijui sababu, ila baadaye ndiyo Mama yake ananishutumu kuwa nataka kumbadilisha dini mtoto wake, mimi nikashangaa sana kwani katika mkaisha yangu mimi nilikau sijawaza hicho kitu.

Kumbe kaende kunitambulsiha kwao kuwa mimi ni mchumba wake na anataka kunibaidlisha dini. Kumbuka hapo mimi namchukulia kama rafiuki tu….” Niliishia hata nguvu ya kubisha, Eli alikua anaongea kwa uchungu huku akitokwa na machozi, nilijua kuwa anaigiza lakini kila nikitaka kuongea alinizuia.

Haikuishia hapo, wakati huo mimi nilikua na mchumba wangu, ambaye ndiyo huyu hapa, tulishatambulishana kwetu na mipango ya harusi kuanza. Basi baada ya kusikia akaanza kumtafuta, akamtukana sana na kumuambia kuwa ahta kama nikimuoa kamwe hataruhusu tuwe na amaani, tukawa tunagombana kila siku.

Basi wka hasira nilimuambia tuanza kuishi pamoja, tukaishi pamoja bila ndoa, nikawaambia watu nimemuoa yote hiyo ni ili wifi yako kuniacha kwa amani, lakini haikua hivyo.” Aliendelea kuongea kambla ya kumalizia Mama Prisca aliingilia kati na kuendelea.

“Nikachoka kushindana na mwanammke mwingine, nikaondoka nikiwa na ujauzito wa Eli na kuanza maisha yangu. Sisi tulishaachana lakini hata baada ya kuolewa alikua bado ananisumbua akiamini kuwa Eli ni wake. Nilishamshaau nina maisha yangu na sasa hivi kuna mwanaume ninaishi naye, basi ndiyo akanitafuta.

Angalia meseji ananitumia, sijui ni nini kilinipata Dada kwakua mimi si mtu wavurugu lakinia linipigia simu na kuniambia mambo mengi kuhusu wewe, jinsi mnavyinitukana mwisho nikaamua kuja kufanya vurugu.”

Wifi yangua likua akisikiliza huku analia, alikua haamini kama naweza kufanya mambo kama yale, walimuonyesha meseji na picha, na vitu vyotye nilivyokua namuambia.
“Alivyo na akili hata hajatumia namba yake, katumia namba ya mwanaume mwingine, huyu mwanaume mimi namjua, tangu ananiambia ananitaka alikua naya, sasa mimi nikashangaa, mbona ananiharibia kwangu wakati ana mwanaume mwingine!

Hembu angalia, hizi picha zimepigwa nyumbani, unadhani ni nani angesambaza, siku ile ilikua ni familia yako tu!? Yote haya ni kwakua tu hataki kuniacha niwe na amani…” Eli aliongea huku akitokwa na machozi!



(ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO; Ili kumsaidia wifi yake, Halima anamtafuta mke wa Elibariki, ambaye anamfuata wifi yake na kumpiga. Ghafla anaitwa kuonana na Elibariki, anakutana na wifi yake pamoja na mke wa Elibariki, wote wanamgeuka na kumshutumu kuwa yeye ndiyo alikua anamharibia Mahusiano yake, wifi yake anatumiwa meseji alizokua anamtumia mke wa Elibariki pamoja na pichA. ENDELEA...)

Nilitamani kujitetea lakini kila kitu kilikua mbele yangu, nilijua hata nikiongea nini wifi yangu haezi kunisikiliza. Nilimuangalia macho yake na kugundua alishaamini yale maneno.
“Mimi naondoka, sitaki tena kujihusisha na hii familia, siku ile nilivyojua kuwa ni wifi yako nilitamani kaucha na wewe kwakua nilijua hawezi kutuacha kuwa na amani!” Aliongea huku akilia.

“Najua ni mipango ya Mama, ndiyo Mama yangu ndiyo kafanya yote haya, ndiyo kakuunganisha na huyu mwanaume!” Nilijitetea kwa hasira, tayari nilishapaniki sikutaka kufa na tai shingoni!
“Kila kitu wewe ni mama yako, najua mambo mengi uliyonifanyia lakini niliamua kukaa akimya kwakua wewe ni wifi yangu, wewe ni mnafiki na leo kila kitu kimejionyesha.

Umaingia kwenye ndoa na Kaka yangu, tukakupokea vziuri, lakini Mama yako anakuja hospitalini unamuambia kuwa mimi ni binti wa kazi! Yaani Mama wa watu unamuambia kuwa mimi nimfanyakazi na nakunyanyasa!

Unafikiri sijui kwanini Mama alinikasitikia sana siku ile? Wewe si ulimuambia kuwa mimi ni mfanyakazi wako na nataka kutembea na mume wako! Sio wewe ulisema, Mama wa watu anaingia anaanza kutukana halafu unajifanya kumuombea msmahaa!”

Alilalamika, hapo ndiyo nilijua kitu Mama yangua limuambia wifi mpaka kunigeuka na wao kuwa mashoga. Nilikua nakuheshimu kwakua ni mke wa Kaka yangu na sitaki maneno, unamuambia Kaka yangu awajengee kwenu, kashakununulia na kwianja, vituvyote hiovyo najua Mam ayako mpaka anashangaa leo unamtaja tena!”

Sikua najua hata nyumbani kwetu tunajenga, wifi yangu alinishutumu mambo mengi, alinionyesha mpaka meseji ambazo Mama yangu alimtumia na kudai kuwa alimtukana kwakua alitumiwa hizo meseji, kwamba mimi namtukana hawezi kupata mwanaume kwakua ana roho mbaya.

“Ondoka, sikutaki tena katika maisha yangu, najua kuwa bado utakua ni mke wa Kaka yangu na Kaka yangu anakupenda lakini sitaki hata uhudhurie kwenye ndoa yangu. Nyumbani wanajua nimepata aajali, ukilogwa na kuwaambia kuwa nimepigwa absi nitawaambia kila kitu na sahau kabisa kuhusu hii ndoa!”

Walininyanyua na kunifukuza pale, nilitoka kama takataka na kurudi nyumbani. Mume wangu aliniuliza nini kilikua kimetokea kwa Mama lakini sikumjibu, nilipanda zangu kitandani kulala huku nikiwa na mwazo mengi sana. Nilijaribu kusaidia lakini ilishindikana, nikaapa sitahangaika tena na maisha ya watu.

“Kama anaenda kutapeliwa basi akatapeliwa sitahangaika tena, Mama kashinda!”

*****
Mambo yalibadilika, mimi na mume wangu tulikua vizuri lakini alikua hanishirikishi tena kwenye mambo yake kama zamani, muda mwingi alikua kwa ndugu zake mpaka kuna wakati nilikua najisikia vibaya, hakutaka niende kwao wala kuongea na Mama yake.

Sijui kwanini, Mama mkwe ambaye alikua ananipenda sana aligeuka na kuwa kama shetani, hata nikimpigia simu anakua na majibu ya mkato.
“Kuna nini mume wangu, mbona umekua hivi?” nilimuuliza siku moja, hakunijibu zaidi ya kuendelea kuchezea simu yake, niliona kama amenidharau hivyo nikaanza kulalamika nhuku nikilia.

“Kama mambo yenyewe ndiyo haya si bora nirudi kwetu….” Niliongea kwa kutania nikiamini kama nikimtishia kuondoka basi atanibembeleza.
“Shetani mkubwa wewe!” Nilisikia sauti ya hasira ya mume wangu ambayo iliambatana na Kodi kubwa. Alinivamia na kuanza kunipiga huku aklilalamika, mume wangu alikua na hasira sana, katika kulaamika ndipo niligundua kuwa ndugu zake wameanza kudai mali zao.

“Umekuja katika familia yetu umeharibui kila kitu, si nilishakuambia uachane na mambo ya Dada yangu, sasa maisha yake hayako sawa, wanaume anataka kumaucha kisa wedwe!” mambo yalikua yamebadilika Eli alimpa msaharti wifi yangu kuwa kama anataka amuoe basia achane na Kaka yake, kwamba adai mali zake ambazo ni za urithi.

Alimuambia Mama yake lakini alikataa, ila bila kujali mtu yoyote wifi alienda mahakamani kudai mirathi yake, tayari alishakua mtu mzima hivyo alikua anataka kuendesha mambo mwenyewe. Haikuishia hapo tu, waodgo zake wakubwa nao walitaka mali zao, Mama yake alipojua sababu ni mimi ndiyo alimkasirikia.

Mume wangu alinipiga sana kisha akaniambia kama ni kuondoka basi niondoke, kusema ukweli nilitamani kuondoka lakini sikua na pakwenda. Nyumbani nilishatibua na sikua na kzai, nilijua kama nikirudi nyumbani wasingenipoke kwani mipango yote ilikua ni ya mama yangu.

Sikujua malengo ya Mama yangu lakini alishaniharibia ndoa yangu. Niliomba msamaha sana ila mume wangu hakunisikliliza, jinsi nilivyokua naomba msamah andivyo ambayo mume wangua likaua nakasirika. Mwisho hata hakuniuliza kama nataka kuondoka au la bali alinipakiza kwenye Gari, usiku uleule akanipeleka mpaka Kibaha nyumbani kwetu.

Alimuambia Baba yangu kuwa amenipeleka ili kunipumzisha nikijifunza adabu basi atakuja kunichukua. Tofauti na nilivyotegemea Mama alinipokea vizuri, aliniambia nisiwe na wasiwasi hata kama tumegombana mimi ni mtoto wake, nilishangaa kwani nilijua bado ana hasira na mimi.

“Umeona sasa hivi umerudi nyumbani, si ulikua unadhani mwanaume hawezi kukuacha! Sasa unaona kinachotokea, kachagua ndugu zake, unaona alivyokupiga?” Mama aliniuluza, bado nilikua na hasira naye, akili yangu ilikua hijakubalaina na ukweli kwua ndoa yangu ilikua imeharibika kwakua tu niligoma kukubali kumchuna mume wangu.

Siku iliyofuata ilikua nzuri, nyumbani wlainichukulia kawaida mume wangu hakupiga hata simu kuniulizia kama naendeleaje na mimi sikumtafuta. Lakini kama jioni hivi wifi yangu alinipigia simu, alinitukana sana na kuniaminia nimemharibia maisha yake, mimi sikujua sababu kwani kama ni yale ya kumtafuta X wa Eli yalishapita!

Mama alirudi na kuniuliza ni kitu gani kimetokea, sikutaka kumuambia lakini mambo yalishaharibika, niliamua kumuambia ukweli kuhusu simu ya wifi yangu, hakushangaa bali alicheka.

“Mambo yameshaharibika huko, kile kiwifi chako kimeshaachwa, nakuambia mwanaume hamtaki tena, kaona hakuna pesa yoyote kaamua kumuacha!” mama aliniambia, nilimuuliza nini kimetoka na yeye alijuaje lakini hakua tayari kuniambia. Ilionekana kuna kitua meongea na Eli, kuna mipango yao walikua wanafanya.

“Achana na hayo mambo, nilichotaka ni kuhakikisha kuwa ukirudi kwa mume wako basi kila kitu kinakua chako si cha hao ndugu zake! Hivi unafikiri ningeruhusu mtu baki kwenda kuchukua mali zote zile wakati mtoto wangu yupo?” Aliniulzia.
“Umefanya nini Mama, na huyo Eli una mahusiano gani naye, mbonakama anakusikiliza wewe kila kitu!?” Nilimuuliza lakini hakunijibu.
“Achana naye mjinga yule, mtu mwenyewe teja ukimpa elfu kumi tu anakufanyia chochote, achana naye, tuongee mambo ya maana!” Mama aliniambia, mimi nilimuambia sina cha kiuongea nasubiria kama mume wangu atakuja kuniomba msmahaa.

“Una akili kweli wewe, msamaha huo akuombee wapi! una nini cha kuombwa msamaha, ni lazima ukaombe wewe, na sas ahivi tafanya ninachotaka mimi, lazima nikutengeneze kwanza kabla ya kwanda kwa huyo mwanaume wako, ni lazima arudiane na wewe!”

Alinaimbia hukua kinyanyuka na kutoka, alienda hcumbani kwane na kuchukua daw aflani, aliniamrisha kuvua nguo, nikabaki uchi wa mnyama, Mama alianza kunipaka dawa sehemu za siri, nilisikia muwasho wa ajabu, aliniambie niende chooni kukojoa.

Sikua na mkojo alinilazimisha, naingia tu chooni nimekaa ili kukojoa mara vitu vyeusi vinaanza kutoka sehemu zangu za siri, aise ni kama damu lakini iliyokaa muda mrefu mpaka kuwa nyusi, ilitoka nyingi kama maji ningikinga inaweza kujaza hata ndoo.

Sikusikia maumivu yoyote, baada ya kumaliza, natoka chooni Mama akampigia simu mume wangu, alianza kulalamika kuwa anataka kuonana naye, akamuomba sana waonane, aje nyumbani. Mume wangu hakubisha, alikuja nyumbani, ingawa alikua hataki kuongea na mimi ila baada ya Mama kumbembeleza sana alikubali kuongea na mimi, aliniambia kanisamehe lakini niake nyumbani kwa muda kwanza.

Mama hakubisha, alimtengea chakula cha usiku na kula, baad aya hapo Mume wangu alikua kama hajisikii vizuri.
“Mpeleke chumbani mwenzako akapumzike, sidhani kama anawez akuendesha gari mwenyewe.” Mama aliniambia, wakati wote huo wadogo zangu walikuepo, ni kama nao walijua kilichokua kinaendelea kwani hakuna hata mmoja ambaye aliongea kitu.

Basi nilimchukua mume wangu mpaka chumbani kwangu, alikua kama kalewa flani mpaka nikahisi Mama kamchanganyia poimbe kwenye chakula.
“Unataka kwenda wapi? njoo huku tulele wewe ni mke nwangu…” Mume wangu aliongea wka sauti ya kilevi wakati namuacha kitandani nataka kuondoka, nilisita kwani pale palikua nyumbani kwetu wazazi wangu wapo niliona aibu kufanay mapenzi na mume wangu.

Alakini yeye hakujali, alinishika na kunivutia ktandani, akalazimisha kufanya mapenzi na mimi na mwisho tukalala mpaka asubuhi. Asubuhi mume wangu alikua ni mtu wa tofauti kabisa, kwanza hakuamka kuswali kama kawaida yake, alichelewa kuamka kama saa nne hivi, nilipomuuliza kuhusu kazi alidi kuwa ile ni siku yetu anataka kuondoka na mimi hivyo hatenda kazini.

Sikutaka kubishana naye, nilikubaliana na kila kitu kwani ndiyo nilikua naomba msamaha. Siku hiyo mume wangu alishinda kwetu lakini tangu siku hiyo mume wangu hakua mume wangu tena. Ni kama alikua mume wa Mama yangu wkani kiola kitu alichokua anafanya ilikua ni lazima kuomba ushauti wka Mama yangu kabla ya kukifanya.

Kama Mama akisema sitaki basi hicho kitu kisingefanyika, alianza kutiujengea nyumba harakaharaka lakini wakati huo ndugu zake hawakukaa kimya, Mama yake aliongana na wanae kwenda mahakamani ili kuzuia yeye kutumia maliza familia.

Ni kama walijua kuwa sisi ndiyo tunamuendesha, nilikua nabeba ujauzito mimba zinatoka, nikimuuliza Mama ananiambia muda wa kuzaa bado, nikienda hospitalini naambiwahakuna tatizo. Kwanza alikuja Mama yangu, kama anataka kuja kunihudumia kutokana na mimba yangu kutoka, lakini ghafla na wadogo zangu mwiasho ndugu zangu wote wakahamia nyumbani kwangu.

Kusema kweli nilichukia lakini mume wangu hakua na kauli, aliungana na ndugu znagu hata kunichukia mimi akisema nina roho mbaya, yaani kila kitu kiliparanganyika, kule nako ndugu zake wamekumalia, mume wangu akawa hana pesa yoyote!

Mama mkwe wangu alikua hajishughulishi chochote na Biashara za familia, yeye baada ya mume wake kufariki alimuachia mume wangu. Lakinia likua ni Mama mwenye akili sana, baada ya kuona mume wangu kaanza kubadilika alimuita na kuongea sana, lakini hakusikilizwa, hapo ndipo aliaza kuchukua hatua.

Alifungua kasi mahakamani na kabla ya kusikilizwa kwa ile kesi waliomba zuio la Mahakama ili mume wangu aisendelee kusimamia zile mali na akaunti zote zikafungiwa mume wangu kuzigusa. Ilikua kama utani lakini kilifanyika tena harakaharaka kwani Mama alikuaa najuana na watu wengi.

Kukosa pesa kulimfanya mume wangu kuwa kama zezeta, hakua na mali za maana ambayozo zilikua na majina yake, vitu vingi alikua anafanya kwa majina ya kampuni hivyo hata magaria liyokua akitumia yalikua ni ya kampunj. Gari pekee ambayo ilikua si ya kampuni ilikua ni gari yangu ambayo alininunulia kwa jina langu.

Kutokana na hali kuwa ngumu alishindwa hata kuliendesha, hakua na pesa ya mafuta. Alikua mtu wa mawazo, kazini haendi mpaka wakamsimamisha kazi.
“Mama kuna haja gani ya kufanya yote haya, kwanini usimuache tu mume wako akaendelea na maisha yake….” Siku moja nilimuuliza Mama, kila mtu alikua kimya, ndani kulikua hakuna amani, Mama alidhani kwa kumteka akili mume wangu atakua amechukua mali zake lakini haikua hivyo.

“Unamaaisha nin?” Aliniuliza, nilishindwa kumaumbia kuwa wewe ndiyo mchawi hivyo nikaamua tu kubaki kimya.
“Kama ni kuondoka aondoke akuache wewe, si amekuoa, basi aondoke yeye ubaki kwneye hii nyumba.” Mama aliniambia akiamini kuwa ile nyumba ilikua ni ya mume wangu. Hata mimi wkatai huo nilikua nikiamini kuwa nyumba ni ya mume wangu Mama alinisikuma sana kudai talaka na wkeli nilifanya hivyo, nilidai talaka, mume wnagua ligoma kabisa kunipa, baada ya kuona imeshindikanakwa mume wangu kunipa niliamua kwenda BAKWATA kudai talaka, sijui mama yangu alifanya nini huko lakini walinipa talaka.

Baada ya kupewa talaka nilikaa eda huku mume wangu bado akiomba kurudiana na mimi, alishakua kama chizi, ndugu zake hawtakai kumsikia, akija kwetu ni manyanyaso ya kila dakika. Mahakanai nilidai talaka na kugawana mali za mume wangu huku nikitaja nyumba ambayo tulikua tunaishi kuwa ni ya kwetu.

Ndugu zake waliposikia wakawa kama wamefurahi, walikuja na kuwa upande wa mtoto wao, basi wakaonyesha document za nyumba kumbe bado zilikua chini ya majina ya Baba yao. Mahakamani Mama yangu alijua ukishaolewa na mwanaume basi mnagawana kila kitu chake.

Kumbe haikua hivyo, kugawana ni mali ambazo uemchuma na mhusika kipindi cha ndoa, ndoa ilikua haina hata mwaka na katika kipindi chote hicho mimi na mume wangu hatukuchuma chochote.

Mahakamani tulitoka kapa, mimi nilibaki na gari tu ambayo mume wangu alininunulia. Baada ya mimi kupewa talaka, walimchukua mume wangu na kuondoka naye pale nyumbani tulikuja kufukuzwa na Baba yake mdogo, mimi na ndugu zangu wote tuliondoka.

Walinaichia gari ambalo nililiuza kwa milioni 60, nililazimika kufanya hivyo kwakua baada ya kuchana na mume wangu nilainza kuumwa, niliumwa sana mpaka kulazwa hospitalini sijitambui, kupimwa nilikua na ujauzito ambao ulitunga nnje ya kizazi na mpaka napelekwa hospitalini kizazi kilishaoza.

Madawa aliyokua akinipa Mama yangu akiniwekea sehgemu za siri ili kumpumbaza mume wangu ndiyo yalisababisha yote hayo, nilitolewa kizazi na sasa hivi siwezi kuwa na mtoto tena. Milioni sitini nilinunua kiwanja na nyingine nikamalizia nyumba ambayo Mama mume wangu alikua anmejengea Mama yangu.

Kama milioni 15 hivi ndiyo nimefungua Biashara nafanya mpaka sasa hivi. Si Biashara kubwa lakini nashukuru Mungu maisha yanaendelea. Ndugu zangu hawataki kuhangaika na mimi, wananilaumu nimechezea maisha, sina chakufanya kwani sijui hata ni kitu gani kilinitokea mpaka kuwa hivi.

Mume wangu naye namuona tu, kasharudishwa kazini na maisha yao yamerudi kawaida. Kuhusu wifi yangu sijui chochote kama yuko kwenye mahusaino au la, kwa Elibariki mke kamkimbia tena kwani kama Mama alivyosema ksahakua teja, unga umemuathiri.

Baada ya Mama kumjaza ujinga wifi nyangu ndipo alimuunganisha na Elibariki, akahakikisha kuwa wanapendana na kutaka waoane. Lengo lake halikua ndoa bali alitaka kumtengenisha mume wangu na ndugu zake, alitaka ndugu zake kuncihukia ili niwe tayari kufanya chochote kurudisha ndoa yangu.

Amefanikiwa ila maisha yangu ndiyo yameharibika. Kibaya zaidi nikuwa karibu kila mtu anajua, majirani wanaonge, ndugu wanaongea, Mama yangu ni kama ameivunja ndoa ya dad ayangu na sasa hivi akivunja yangu.

Baba yeye yupo tu, anafuata chochote kile ambacho Mama anaongea. Kusema kwlei sijui ni Mama wa namna gani kwani dada yangu kaolewa, ingawa ila anamtafutia wanaume wenye pesa ili awadange, huyo ndiyo Mama yangu, sina namna maisha lazima yaendelee.

MWISHO


0 comments:

Post a Comment

BLOG