Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

MAMA USIFE ILI UNIGUZE

  

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

SIMULIZI; MAMA USIFE ILI UNIGUZE—SEHEMU YA KWANZA!


“Mimi siendi na Mama, hata kama ni siku yake ya kuzaliwa mimi siendi! Mama mwenyewe kila ukitoka naye anavaa hovyo hovyo kazi ni kulewa na kushikwa shikwa matako mimi sitaki! Kama vipi mimi nabaki nyumbani, kwanza nina homework za kufanya!” Nilikua nimesimama mlangoni kwenye chumba cha kusomea, Mwanangu Zack ambaye alikua na miaka 10 wakati huo akiwa darasa la tano alikua kakaa kwenye meza ya kujisomea, alikua yuko bize na madaftari yake, ni muda mrefu tulishamuambia kuwa ajiandae kwaajili ya kutoka.


JOIN US ON TELEGRAM

Ilikua ni sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa mke wangu, nilikua nimemuandalia mke wangu sherehe kwajaili ya familia tu lakini aligoma. Aliniambia kuwatayari alisha andaa sherehe yake yeye na marafiki zake hivyo niahirishe kwangu. Tulibishana kidogo kwani nilishaalika watu, nilishanunua vitu lakini mke wangu aligoma.


“Kwani ni wewe unazaliwa, hivi wewe mwanaume una akili kweli? Yaani unataka siku yangu ya kuzaliwa niende kukaa na Mama yako sijui na Dada zako kuongea ujinga ujinga wenu wa kilokole! Unaakili kweli, unaniandalia sherehe hakuna hata pombe kwenye siku yangu ya kuzaliwa, kwanini usingeniandalia misa kabisa!” Mke wangu alinijibu.


Nilitaka kubishana naye lakini watoto walikua sebuleni, nilimuona Zack akinyanyuka taratibu na kuelekea chumbani kwake. Alisikia maneno aliyoniambia Mama yake na nilioka kabisa yamemuumiza. Sikua na namna zaidi ya kukubaliana na mke wangu. Nilimuambia Binti wa kazi kuwaandaa watoto wengine wawili ambao ni wadogo kisha nikaenda chumbani kwa Zack na kumuambia ajiandae. Mwanzo aligoma lakini nilimlazimisha, nilirudi chumbani na kumuambia mke wangu kuwa alichokifanya si kizuri kutoa majibu yale mbele ya watoto.


“Wewe unaona ulichofanya ni sawa, unajua kabisa mimi simpendi Mama yako lakini unajitutumua kutuweka karibu! Mama yako hanitaki, tangu unataka kunioa alikua hanitaki, sasa ya nini mimi kujipendekeza?” Aliniuliza, ni kweli tangu siku ya kwanza namtambulisha mke wangu kwa Mama yangu alimkataa, aliniambia kabisa kuwa mke wangu si mtu sahihi kwangu lakini sikumuelewa, alinipa sababu kibao kubwa zikiwa ni tabia zake, namna alivyokua anaongea kwa dharau lakini mimi nilishampenda, Mama yangu hakulazimishia, aliniambia mimi ni mtu mzima na nina maamuzi yangu.


“Sawa lakini hukupaswa kuongea mbele ya watoto, unahisi wamejisikiaje kusikia Mama yao anaongea maneno kama yale?” Nilimuuliza, alikua bize kujiremba kwenye kioo alipoona nimembana alibadilisha mada.


“Hivi utaongea hapo mpaka saa ngapi? Mimi nishavaa tayari, nikimaliza kutengeneza nywele hapa kama hujamaliza nakuaha, siwezi kukaa kukusubiri wakati hata kuoga hujaopga.” Aliniambia, sikutaka kubishana naye, nilijua tu kuwa amenielewa kwani kwa kawaida yake mke wangu akikosea kitu si mtu wa kuomba msamaha, kwenye kitu ambacho hawezi ni kujishusha, hicho hakiwezi kabisa.


Kikubwa anachofanya akijiona kama kakosea ni kubadilsha mada au kunyamaza. Niliingia bafuni na kuoga, nilitoka bado yuko kwenye kioo, baada ya kumaliza kuoga na kujiandaa nilitoka kuwaangalia watoto kwani nilijua kuwa kama wasingekua wamejiandaa taayari basi kosa lingekua langu. Dada wa kazi alikua bize kuwavalisha wale wadogo. Nilienda chumbani kwa Zack sikumkuta ndipo niliamua kwenda kwenye chumba cha kusomea kwani nilijua kama usipomkuta chumbani basi anasoma.


Nilimkuta kakaa hana hata mpango na safari, nilipomuuliza ndipo alinipa majibu ambayo yalinichefua kabisa.


“Umesema nini? Nilimuuliza huku nikitembea taratibu kumfuata, kila hatua niliyokua napiga nilikua navimba, hasira zilikua zinanipanda, Zck hata hakujali, aliinama kuendelea kusoma vitavu vyake huku akining’unika maneno ambayo sikutasikia.


“Nimekuuliza umesema nini?” Nilimuuliza tena, sasa hivi nilikua nimesimama mbele yake, katikati tulikua tumetenganishwa na meza, yeye alikua kakaa, meza katikati na mimi nimesimama pembeni, kulikua na mwanga wa kutosha, alinyanyua uso wake na kuniona nilivyokua nimakasirika.


“Mimi nimesema siendi nina homework.” Alijibu kwa mkato, nafikiri alishatambua kosa lake hivyo hakurudia maneno aliyoyaongea mwanzo kuhusu Mama yake.


“Hapana, hapo nnyuma umesemaje kuhusu Mama yako! Nataka nikusikie vizuri, nilikua mbali sijasikia kityu…”


“Baba mimi sijasema kitu…” Aliniambia, lakini nilimkazia macho akabaki anatetemeka.


“Lakini Baba si ni kweli, Mama akila mkitoka naye anashikwaga shikwaga matako na wanaume….” Ssijui hasira zilitoka wapi sikifikiri mara mbili, niliikanyaga ile meza, ikasogea na kwenda kumbamiza ukutani, yeye na kiti hake walienda kugonga ukuta. Niliusindilia mguu kwa nguvu nikimbania kule.


“Baba nakufaa!” Alipiga kelele! Hata sikujali, niliisogeza meza pembeni, nikamrukia na kuanza kumpiga makofi.


“Huyo ni Mama yako, kwanini unaongea upumbau kama huo! Mtoto mshenzii kabisa! Mbwa kabisa, unajitia una kiburi, unajiona mwanaume sana, unaona kuwa ushakamilika!” nilitukana sana na kumpiga sana, alipiga kelele nyingi huku akiomba Baba nisamehe Baba nisamehe! Niliendelea kumpiga, nilikua na hasira, mpaka sasa sijui kama zilitoka wapi? sijui ni kwakua alimtukana Mama yake, sijui ni wivu kwakua labda mamboa liyokua anaongea yalikua ni kweli na sikua na uwezo wa kwenda kumuuliza mke wangu au ilikua ni nini lakini nilimpiga sana moto.


“Kwanini unataka kumuua mwanangu! Hivi unampiga hivi kwa kosa gani?” Mke wangu alisikia kelele, alikuja akikimbia na kunishika nisimpige. Niliacha na kwa hasira nilitoka kwenye kile chumba, mke wangu aliongea sana na kunitukana matusi mengi ya nguoni kwa kumpiga mtoto wake. Hakuuliza sababu na sikutaka kumuambia zaidi ya kusema mtoo kagoma kwenda kwenye sherehe yake.


“Umeona sasa wewe ndiyo unawafanya watoto kunichukia, kwani sherehe dioyo nini? Kama hataki kwenda si unamuacha, hivi unajua wewe ndiyo unafanya w3atoto wananiona mimi kama shetani, yaani unalazimishia mambo sana!” Mke wangu aliongea, ghafla alikua upande wa mtoto na kusema kuwa kama hataki kwenda abaki. Lakini mimi niligoma, nilimuambia ilikua ni sherehe ya Mama yake, akajiandae na wote tunaenda. Nilisimamia msimamo wangu, pamoja na maumivu yake lakini Zack alitoka na kwenda kujiandaa kwajaili ya sherehe ya Mama yake.


****


Ilikua ni sherehe ambayo mke wangu aliandaliwa na wafanyakazi wenzake, mke wangu alikua ni mtu mkubwa tu akifanya kazi katika shirika moja kubwa la kiserikali, alikua na kipato kizuri ingawa hakufikia hata nusu ya kipato changu kwani mimi niliajiriwa binafsi na nilikua na Biashara zangu nyingi tu. Tulifika tukiwa tumechelewa kidogo kwani mimi na watoto tulipata taarifa mwishoni kabisa.


“Si ulisema mume wako hatakuja?” rafiki yake mmoja alimuuliza, hii ilikua ni baada tu ya kuingia na kusalimiana nao. Mimi nilikua natafuta sehemua ya kukaa watoto, kwa namna walivyokua wameandaa kulikua na kiti cha mtu mmoja, ingawa hawakujua kama niliwasikia lakini walichokua wanaongea ni kama mke wangu aliwaambia kuwa atakuja mwenyewe.


“Ndugu yangu ukiolewa na watu ving’anganizi utafanya nini?” Hata mimi nilijua haji ndiyo hivyo kalazimishia.” Mke wangu alimjibu kisha akanisogelea. Hakujua kama nimesikia ingawa aliongea kwa nguvu, nilijifanya sijasikia, nikatabasamu na kumuuliza sehemu za kukaa.


“Mnaweza kukaa hata kule nyuma, mimi siti yangu ile pale, unaona madharaa ya kuchelewa kwenu?” Mke wangu aliniambia huku akinielekeza sehemu ya kukaa, ilikua ni nyuma kabisa, si sana kihivyo lakini kwa namna ile sehemu ilivyokua imepangwa kulikua na meza kuu, hiyo ilikua na siti nne ambapo tayari watu walishakaa kasoro siti moja.


Alikaa bosi wake, na rafiki zake wengine, kulikua na viti vingine vyenye meza zake zimepangwa kistaarabu kabisa. Hiyo sehemu ambayo alikua anataka nikae mimi na watoto ilikua ni nyuma kabisa, kama ushawahi kuhudhuria sherehe yoyote iliyopangwa kistaarabu basi kuna kule nyuma ambapo wazamiaji hukaa, wale amabo huletewa viti baadaye, wanawekewa bila kuwa na mezas. Ainiambia nikakae huko.


“Kule, kweli ni haki hii, unajua mimi ni mume wako, siku yako kubwa hii ningekaa mimi na watoto hapo mbele?” Nilimuuliza kama vile namuomba, tena kwa sauti kubwa.


“Acha utoto basi unaniaibisha ndugu yangu, yaani watu wazima tuanze kubishana kama vile watoto wadogo, kwani ukikaa kule utapungukiwa nini?” Alinaimbia kwa sauti flani kama ya kubembeleza.


“Shem njoo ukae hapa, mimi narudi kuile nyuma.” Rafiki yake mmoja, Mage, yeye nilikua namfahamu, ni rafiki yake wa karibu na alikaa mbele kabisa, alitaka kunipisha katika siti yake.


“Muache akakae na watoto, wewe kaa tu, hana tatizo, sherehe yenyewe fupi ni kwaajili ya wafanyakazi tu, mbona wamepitia hapa dakika tano tu wanaondoka, ngoja wakajigeshe kule nyuma, tukikata keki tu wanaondoka. Wanasherehe nyingine huko kwa Mama yao.” Mke wangu aliongea, sikutaka kumjibu, niliona kuwa ni kujiaibisha.


“Sem nimekuja tu kusalimia kidogo, mimi na watoto tunaondoka.”


Ingawa sikua na mpango wa kuondoka lakini sikua na namna, nililazimika kwenda na upoepo, kukubaliana na ukweli kuwa tunaondoka. Nilienda mpaka kule nyuma, tayari wahudumu walishatutafutia viti mimi wanangua na binti yetu wa kazi, Sakina. Zack alikua bado kanikasirikia na alionyesha kuchukizwa na sisi kukaa kule nyuma, watoto wengine walitulia ingawa walionekana kama wakiwa.


Mziki uliendelea na niliona wanaendelea na ratiba zao, walisema mambo ya zawadi, muziki a vitu vingine. Shughuli ikiwa inaendelea nilimuona mke wangu akimuita MC, waliongea kitu kisha MC akatangaza kuwa kwakua kuna watu walikua wanaondoka basi itaanza na kukata keki, kisha kufungua shampeni na ndipo mambo mengine yataendelea.


Mke wangu alinyanyuka na kuanza kukata keki, bila aibu alianza kwa kuwalisha marafiki zake, mabosi zake na kila mtu. Ilipofika zamu yetu hata hakutuita kule mbele, alikkatakata keki kwenye sahani na kuja nayo huko nyuma. Alikuja tulipokua tumekaa na kutulisha keki, kidogo nikatae lakini niliona nitajitia aibu, wakati katika kuwalisha watu wengine karibu wote walitambulishwa lakini sisi hakututambulisha, alitulisha tu kama waputa njia, yaani hata watoto wake hakuwatambulisha na huwezi amini wanangu ni kama walijua kuwa wametengwa hivyo walinyamaza kimya.


Tulikula keki hivyo hivyo, tukakaa na sherehe iliendelea, kama dakika tano mbeleni hivi mke wangu alikuja.


“Mnaoweza kuondoka, sasa hivi ni sherehe ya wafanyakazi, mtaborekea, mambo ya pombe hapa, bora uende kukaa na walojkole wenzako.” Mke wangu aliniambia.


“Lakini nilishawaambia kuwa sherehe imeahirishwa, nilijua tunakuja kusherehekea pamoja! Sasa kama ulikua hutaki nije na watoto kwanini ulilazimishia.” Nilimuuliza kwa hasira kidogo, pamoja na uvumilivu wangu lakini nilichoka, hasira zilinipanda na niliona kama nimedharauliwa.


“Unalalamika nini wakati ulikua hutaki kuja? Si umekata keki, shampeni zote ni za pombe, wewe unakunywa pombe, sherehe ishaisha na kama ni chakula basi nitawaletea, kwanza huu usiku unafikiri watotop watakaa mpaka saa ngapi hapa? Hii ni sherehe ya wafanyakazi, birthday ishaisha!”


Aliongea kwa namna ya kulazimishia, alipaza sauri baada ya kuona kama nakataa, watu waliokua karibu walisikia na kugauka, kwani mziki ni kama ulizimw2a paaap. Kuona hivyo nikaona isiwe shida, nikawachukua wanangu na kutoka nao, nilitoka mpaka mlangoni bila hata kuaga rafiki ake, bila kutambulishwa tena tukiwa na njaa zetu. Wakati nataoka nilipishana na Baba mmoja mtu mzima, ni mtu ambaye namfahamu kwani ni kiongozi mkubwa tu wa heshima ambaye nina uhakika yeye alikua hanijui, nilimsalimia na aliniitikia vizuri.


Lakini kabla sijatoka kabisa nilikumbuka kuwa tulikuja na gari yangu hivyo mke wangu asingepata mtu wa kumrudisha. Nilirudi kumuuliza kama nije kumchukua akimaliza kwani naondoka na gari nayeye hana usafiri.


“Sasa unataka kunikasirisha, inamaana hapa watu wote hawa nikose mtu wa kunirudisha, hembuo ondoka hhuko acha kuniaibisha.” Mke wangu alikua bado kasimama hajarudi kukaa kwenye siti yake, ni kama alikua anahakikisha kuwa tumeondoka ndiyo arudi kukaa, wakati huo yule Baba ndiyo alikua anaingia alikua nyuma yangu, kasimama kama anasubiri kitu.


Mke wangu alinisukuma ili nitoke, mpaka mlangoni kisha akarudi, ile natoka tu nnje nikamsikia Zack akimuambia Sakina.


“Huyo Baba nsimpendi, yaani ndiyo Mama anapenda kupanda kupanda gari yake na anapenda kumshika shika Mama matako ipo siku nitampiga hata ji…” Alinyamaza ghafla baada ya kuniona, hakutaka nisikie lakini nilisikia, hasira zilinipanda, nilihisi kitu, bila kujijua nilijikuta narudi kule ndani kuangalia kama yule Baba atamkumbatia mke wangu au la.


Nilichokiona sikuamini, niliwaona tayari wamekumbatiana, mke wangu kanipa mgongo na yule Baba kakumbatia mke wangu huku kweli mikono yake ikipapasa matako ya mke wangu. Mwili ulianza kutetemeka kwa hasira, mke wangu alikua ni kila kitu lakini sikuamini kama anaweza kufanya kitu kama kile tena mbele ya wafanyakazi wenzake, walikumbatia kwa muda kidogo, huku muziki bado ukipigwa, mikono ya yule mzee ambaye alikua ni mume wa mtu ilikua mgongoni mwa mke wangu na mke wangu alikua katulia tuli, nilishindwa kuvumili….


Katika mahusiano mtu wa kwanza kumpenda ni wewe, kaa hutaki kuumizwa sana basi hakikisha kuwa unampenda wewe kulijko mtu mwingine yoyote yule. Uwe ni mwanamke au mwanaume, kama furaha yako inamtegemea mwenza wako kwamba hata akijamba ni lazima unuse huwezi pepea mdomo au kutoka nnje basi wewe utakua ni mtu wa kuumia kila siku. Jifunze namna ya kujipenda.


SIMULIZI; MAMA USIFE ILI UNIGUZE—SEHEMU YA PILI!


(KWA WALE AMBAO HAMKUSOMA SEHEMU YA KWANZA; Zack anakataa kwenda kwenye shere ya Mama yake kwa madao kuwa huko anashikwa shikwa. Baba yake anampiga na kumlazimisha, wanaenda kweli, huo hawakai sana kwakua Mama hataki wakae anataka kufurahia na marafiki zake, wajati mume wake na wanae wanatoka basi Mama anakutana na mwanaume wake anaingia, wanakumbatiana na anashikwa shikwa mbele ya mume wake na watoto, basi endelea….)


Nilitaka kurudi kumfuata mke wangu na kuanza kuleta vurugu lakini ile naingia tu Zack yuko pembeni yangu.


“Si nilikuambia Mama anapenda kushikwa shikwa matako, uona, kuna yule baba mwingine ndiyo anamshika kwa nguvu muulize hata na….” Aliongea lakini nilimkatisha, sikutaka aendelee kumdhalilisha Mama yake, nilimshika masikio na kumvuta mpaka nnje, w3ote tukaelekea kwenye gari. Safari ya kuelekea nyumbani ilianza, kila mtu alikua kimya, hakuna aliyekua anaongea, gari zima lilikua limetulia mpaka mtu akipumua unamsikia.


Nilikasirika sana, haikua mara yangu kujua kuwa mke wangu anachepuka, nilijua mke wangu ana tabia za ajabu lakini sikudhani kama anaweza kufanya uchafu wake mbele za watoto. Iliniuma sana wanangu kuona yale mambo lakini sikua na namna. Tuliingia ndani, zaidi ya keki watoto walikua bado hawjaala, niliwauliza kama wanataka kula lakini kila mmoja alidai kushiba, nilijua wana njaa lakini hakuna mtu ambaye alikua kwenye mood ya kula.


Niliingia ndani na kupanda kitandani lakini sikupata usingizi, haikua mara ya kwanza mke wangu kuchelewa kurudi nyumbani lakini tukio la siku iole liliniumiza sana, yeye ndiyo alitaka sisi twende kwenye sharehe, nilishamuandalia sherehe na kuandaa kila kitu lakini aligoma kukaa na ndugu zangu kwa madai kuwa ni walokole akalazimishia mimi na watoto kwenda kwenye sherehe yake ya kazini, lakini tunafika watoto hata kula hawali wanaishia kula tu Keki kisha anatufukuza.


Bila kujali kama mimi nipo tena na watoto ananafanya ujinga wake, anakumbatiw ana wanaume mbele yangu. Jambo lile liliiniumiza sana, lakini sikua na namna zaidi ya kumsubiri, usiku ule nilikua na hasira sana. Mpaka saa kumi na moja za asubuhi simu ya mke wangu ilikua haipatikani, nilijaribu kumpigia rafiki yake lakini alikua hapokei simu zangu. Mpaka saa mbili asibuhi ndiyo mke wangu alirudi.


Moja kwa moja aliingia chumbani, mimi nilikua sebuleni nilikua nimekaa tu, sina hili wala lile, alinisalimia na kuingia chumbani moja kwa moja. Alionekana kama mtu aliyekasirika, hakuulizia chochote, hakusema chochote, hakuniambia ni kwanini alikua kachelewa, hakuniambia ni kwanini alizima simu. Nilimfuata chumbani na kukuta kashaingia bafuni kuoga, nilimsubiri mpaka alipotoka ili kumuuliza, lakini alipotoka tu alianza kulalamika.


“Hivi wewe ni mwanaume kweli?” Alianza kulalamika, nilibaki tu namshangaa kwani kama ni mtu wa kulalamika nilipaswa kuwa mimi.


“Mimi jana unaniacha kule, nikajua unapeleka watoto utakuja kunirudia lakini wala hukurudi, yaani unaniacha mimi na wale watu ulidhani nitarudije?” Nilishangaa kwani wakati naondoka nilimuambia kabisa kama naweza kwenda kumchukua lakini aligoma tena akinijibu kwa dharau.


“Lakini wewe si uliniambia kuwa una watu wa kukuleta?” Nilimuuliza, aliniangalia kwa dharau na macho yake ya ulevi, alionekana kuchoka sana, kama mtu ambaye alikunywa sana.


“Wanaume wengine ni wanaume tu kwakua mna mbo** hivi kweli unaweza kumuacha mke wako na wanaume wengine na kwenda kulala uapata usingizi!” Alijibu kwa hasira huku akijirusha kitandani, nilijaribu kumsemesha lakini hakunijibu, alionekana kuchona sana na kweli baada ya dakika kadhaa nilimsikia akikoroma, nilikaa kitandani nikimuangalia kwa uchungu, nilitamani kumuamsha lakini niliona itakua ni ugomvi mwingine.


Sikua na kitu cha kufanya siku ile, niliona kabisa kama nikikaa mule ndani ningeweza kumpiga au kufanya mambo mabaya. Nilitoka zangu na sikurudi mpaka jioni, sikwenda popote zaidi ya kuzunguka mjini, mwisho niliishia kwa Mama yangu, nilienda kumuona kwani yeye na dada yangu waliandaa sherehe ya siku ya kuzaliwa mke wangu. Mama hakua na maswali mengi sana lakini alionekana kuumizwa na ile hali ya sisi kuwadanganya kuwa tutakua na sherehe.


“David (sio jina lake halisi) uko sawa mwanangu, mbona naona kama hauko sawa kabisa.” Aliniuliza, mimi nilimjibu na kumuambia kuwa niko sawa, mimi na mke wangu hatuna shida yoyote.


“Lakini mwanangu kumbuka kuwa wewe ndiyo mwanaume, wakati mwingine ni lazima ufanye maamuzi ya kiume, ni vibaya sana kumsikiliza mke wako kwa kila kitu. Mimi ni mwanamke nakosea, wakati mwingine nakosea lakini Baba yako hanisikilizi kwa kila kitu.” Aliniambia, nilinyamaza bila kumjibu chochote nayeye alinyamaza, hakuongea tena, ahata wadogo zangu walipokuja na kuuliza alilazimika kudanganya.


“Wifi yenu alikua hajisikii vizuri, asingeweza kuja.” Roho iliniuma sana, nijisikia vibaya kwamba Mama yangu ambaye alikua ni mlokole, mtu wa kanisani alilazimika kudanganya kwaajili yangu. Nilishindwa kuvumilia, nikanyanyuka na kuondoka zangu. Nilizunguka mjini mpaka usiku, sikutaka kurudi nyumbani lakini kuna kitu kiliniambia rudi inawezekana watoto wapo wenyewe. Nikweli nilifika nyumbani na kukuta mke wangu katoka, niliuliza alikua kaenda wapi hakuna aliyekua anajua, kila mtu alikua kimya.


Watoto walionekana kama wanajua alipokua kaenda Mama yao lakini walinyamaza, kunai le unamuuliza mtu swali unaona kama ana jibu lakini anaogopa kusema, niliwabana lakini waligoma, mwisho nikiwa nimekata tamaa ya kuuliza Zck aliropoka.


“Yule Baba aliyekua anamshika matako jana alikuaj kumchukua!” Aliongea kwa hasira, alionekana kuwa na uchungu kuliko wengine. Niliumia sana kwamba mke wangu meruhusu yale kutokea, lakini nisingeruhusu wanangu kumdharau Mama yao.


“Nilikuambia nini kuhusu kumdharau Mama yako?” Nilimuuliza kwa hasira huku nikitaka kumpiga, nilijua kuwa atajitetea kutaka nisimpige lakini alisimama wima, alinyamaza kimya na kusubiri nimpige, nilinyanyua mkono lakini haukushuka, nilishindwa kumpiga mwanangu kwani alikua anaongea ukweli.


Siku ile mke wangu akijua kuwa watoto wanamuangalia, mimi nipo aliruhusu kushikwa shikwa na mwanaume mwingine mbele yangu. Niliumia sana, nilishindwa kumpiga Zack wala kuongea chochote, niliondoka kwa aibu mpaka chumbani kwangu. Nilichukua simu yangu na kuanza kumpigia mke wangu, nilijua hatapokea lakini alipokea. Niliweka simu sikioni na kusema haloo. Mtu wa upande wa pili hakuongea chochote, nilitaka kukata mpaka niliposikia sauti ya kiume ikisema.


“Halooo! Halooo wewe nani?”


Nilitaka kujibu, lakini kabla ya kujibu nilisikia sauti nyingine, ilikua ni sauti ya mke wangu.


“Usipokee huyo ni mume wangu.” Mke wangu alimuambia, walionekana kugombania simu kisha nikasikia.


“Kama ni mume wako mbona umemsave jina la kike, wewe utakua unatuchanganya na watu wengine, huyu si mume wako, utakua umerudiana na yule jamaa unanizuga, naomba unaimbie kuw ahuyu ni nani?  Mume wako mpuuzi hawezi kukupigia sasa hivi, na nilishakuambia ukiwa na mimi sitaki upigiwe na wanaume wako!” Alifoka sana, waligombana mpaka kupigana, yule mtu aligoma kabisa kumpa simu mke wangu alikua akimtukana na kumpiga.


Siku ilikaa hewani kwa dakika kama kumi hivi, nilisikia mke wangu akipigwa na mwanaume mwingine akimshutumu kuchepuka na kufanya umalaya, huyo mwanaume alionekana kuwa naye ni mume wa mti.


“Wewe ni Malaya sana, umeniharibia kw make wangu mpaka sasa hivi nyumbanio hawanielewi lakini bado unatuchanganya na yule mbwa, nakuambia, si anajifanya ni mheshimiwa, nitawachafua mpaka mtashangaa, na ukibidha nitamuambia na mume wako!” Alitukana sana mke wangua likua anaomba msamaha huku akipigwa, alionekana kupigwa sana, baada ya muda simu ilikata, niliipiga tena lakini haukupokelewa.


Binti wa kazi alikuja na kunigongea mlango, aliniambia chakula tayari lakini sikua tayari kwa kula. Nilikua na mawazo mengi, siku zote nilikua nahisi kuwa mke wangu anachepuka, kutokana na tabia zake na maneno yaw tau niliyokua nikiyasikia nilihisi kuwa anchepuka lakini hata siku moja nilikua sijawahi kupata ushahidi. Zaidi ya mapicha ya uchi ambayo anatumiwa wanaume na kudai ni marafiki zake tuligombana ananiahidi kuacha lakini haachi.


Nilipanda kitandani kutafuta usingizi lakini haukuja, sikula kabisa siku hiyo, mke wangua lirudi kwenye saa sita na nusu hivi usiku. Uso ulikua una maalama mengi, jicho liolikua limevujia damu, alionekana kuwa kwenye maumivu makali, nilimkaribisha ndani lakini sikusema chochote. Nilikua najua kila kitu hivyo sikuona sababu ya kumuuliza, alikua anatembea kwa kuchechemea, alinisalimia vizuri tena kistaarabu tofauti na kawaida yake, nilimuitikia na moja kwa moja aliingia mpaka chumbani.


Alivua nguo zake na kuingia bafuni uchi, mwanga wa taa ulipiga mapaja yake meupe ambayo yalikua na mistari mistari, alionekana kama mtu aliyechapwa na mkanda. Sikumuuliza chochote, aliingia bafuni kujimwagia maji, alifungulia bomba la maji na kuanza kuoga. Alikaa bafuni kwa muda mrefu, kwa zaidi ya lisaa limoja mke wangu alikua bafini, nilishtuka kwani pamoja na kuwaa anogaga muda mrefu lakini haikua kawaida yake.


Nilinyanyuka kitandani ili kwenda kumuangalia na kumuuliza tatizo ni nini? Ile nashuhsa tu mguu chini kwanza nikakutana na maji, nilishangaa, kuangalia chumba chote kilikua kimelowa, maji yalikua yamejaa chini. Nilishtuka, nilienda mpaka kwenye mlango wa bafuni na kuufungua, mke wangu alikua kalala chini, maji yamemzunguka, alikua kadondoka na kuziba lile shimo la kupitishia maji hivyo kufanya maji kujaa.


Nilimfuata na kujaribu kumnyanyua lakini alikua mzityo sana, alikua hajitambui, nilifunga maji na kumsogeza pembeni kidogo ili maji ambayo yalikua yamejaa pembeni kutoka, nilijitahidi kumnyanyua kwa shida mpaka chumbani ambako nako kulikua kumelowa. Nilimnyanyua mpaka kitandani, nikamfunika nguo, baada ya kumsitiri nilitoka mpaka nnje, nikamgongea jirani yangu mmoja ili anisaidie kumbeba kwani alikua mzito sana, mapigo yake ya moyo yalikua yanasikika kwa mbali hivyo nilijua bado yuipo hai.


Jirani yangu alikuja, tukambeba na kumpeleka hospitalini, kule waliniuliza kilichotokea nikawaambia ukweli kuwa kadondoka bafuni. Baada ya kumpokea na kumchunguza walianza kumhudumumia kwani alikua katika hali mbaya, niliulizwa mimi ni nani na kuwaambia ni mume wake. Ghafla walinzi wapale hospitalini waliniweka chuni ya ulinzi.


“Huyu mtu amepigwa, wewe ndiyo umempigwa mke wako, anaonekana kuumia sana, hatuwezi kumtibia bila RB lakini kwakua wewe ndiyo mtuhumiwa hatuwezi kukuruhusu kuondoka kwani akifa hapa utatoroka!”


Yule Daktari ambaye alikua mwanamke alionekana kuwa na hasira sana, alinilaumu sana kumpiga mke wangu, mke wangu alionekana kuumia sana. Nilimsihi kumhudumia alinijibu tu kwa dharau kuwa.


“Kama ungekua unampenda kweli usingempiga!” Niliwekwa chini ya ulinzi na walinzi wa ile hospitali na kama nusu saa baadyae hivi gari ya polisi ilikuja, walinichukua mpaka kituoni ambapo bila hata kuandikisha maelezo nilisukumwa ndani. Sikua nimefanya chochote hivyo sikua na wasiwasi wowote lakini mawazo yangu yalikua kwa mke wangu.


Wakati nambeba kumtoa bafuni mpaka chumbani kisha kumpandisha kitandani ndipo niligundua kuwa alikua kapigwa na kujmizwa sana, tumboni na kifuani kulikua na michubuko kama mtu aliyepigwa na kitu kizito, pia shingoni kulikua na mikwaruzo na kichwani nywele zilionekana kuvutwa sana kwani mbali ya kuvurugika lakini kuna baadhi ziling’oka. Nilikua namuwazia yeye na wanangu, sikuwaza kabisa kuhusu mimi mpaka alipoingia askari aliyeonekana kuwa ndiyo alikua mkubwa wao.


“Kafanya nini huyo? Namfahamu tunasali kanisa moja?” aliwauliza.


“Mshenzi tu, kampiga mke wake kisha kampeleka hospitalini baada ya kuona anataka kufa.” Mwenzake alimjibu.


“Mke wake namfahamu, mstaraabu sana yule Mama, kampiga sana.”


“Sio kumpiga, atakua kamuua maana hata kupumua hapumui, nahisi alitaka kwenda kumtupa hospitalini akimbie ndiyo walinzi wakamkamata, atakua alipanga kumuua.” Mmoja alielezea.


“Sio kama alipanga, amemuua, mimi nimemuona yule Mama haponi.” Hapo ndipo nilianza kuwaza kuhusu mimi kwani niliona kabisa kesi imenigeukia.


SIMULIZI; MAMA USIFE ILI UNIGUZE—SEHEMU YA  TATU!


Nilikaa mahabusu kwa siku tatu mfululizo, wakati wote huo mke wangu alikua hajazinduka hivyo pamoja na wanangu kusema kuwa sikumpiga Mama yao lakini hakuna aliyeniamini. Ndugu zake walinitukana sana na kuapa kuhakikisha kuwa naozea jela kwa kumpiga mtoto wao. Ndugu zangu walihangaika sana kunitoa lakini ilishindikana. Baada ya siku tatu mke wangu ndiyo alizinduka, aliulizwa kama anakumbuka kilichotokea akajifanya kusahau.


“Mimi nilirudi nyumbani nikiwa mzima, nilikua nimekunywa kidogo hivyo nikaingia bafuni kuoga na sikujitambua tena, ndiyo sasa hivi naamka niko hospitalini na nimeumia.”


Aliongea, aliulizwa kama anakumbuka kuwa nilimpiga alisema hakumbuki kitu, aligoma kabisa kusema ni nani alikua kampiga, hakusema ni mimi wala mchepuko wake. Kutokana na mazingira nilionekana ni mimi, lakini kwakua alishapata fahamu basi nilitolewa kwa dhamana, nilienda kumuona hospitalini na kujatibu kumkumbusha kilichotokea lakini aligoma kabisa kukumbuka, aliniambia kuwa inawezekana nilimpiga lakini yeye hakumbuki chochote.


Baada ya kama wiki moja hivi alitoka hospitalini, kwa madai ya usalama wake ndugu zake walimchukua, alienda kukaa huko kwa mwezi mmoja. Ulikua ni mwezi mgumu sana kukaa mbali na mke wangu, nilikua nishamzoea, kibaya zaidi nikuwa alikua hataaki kabisa kuongea na mimi, alijifanya kunikasirikia na kila siku alibadilika badilika, mara ya kwanza alisema kuwa hakumbuki kitu, lakini baada ya muda akasema kuwa anakumbuka aliporuidi kutoka kazini tuligombana nikimshurumu kuchepuka.


Aliongea maneno mengi mengi, kesi iliendelea, nikapelekwa mahakamani lakini mke wangu aligoma kutoa ushahidi, nilimuomba sana kufuta kesi ila hakufuta na mahakamani hakwenda. Baada ya muda polisi wenyewe aliachana na ile kesi kwakua walikua hawan aushahidi na mke wangui aligoma kutoa ushirikiano. Pamona na yote hayo lakini bado nilikua nampenda mke wangu na nilitamani kurudiana naye.


Nilimsihi sana kunirudia lakini hakutaka, aliniambia nimpe muda kuona kama anaweza kuishi na mwanaume kama mimi. Alidai bado hajakumbuka kilichotokea akikumbuka ndiyo ataamua kuwa aje kwangu au la. Nilimuomba sana kukumbuka kuhusu watoto lakini hakujali, aliniambia nimpe muda. Nilivumilia, miezi mitatu ilipita nikiwa naishi bila mke wangu, hali hiyo iliniumiza sana, niliwaonea sana huruma wanangu ingawa wao walionekana kuwa kawaida.


Walikua na furaha zaidi na katika kipindi chote hicho hakuna hata mmoja ambaye alimuulizia Mama yake. Siku moja nilitoka kazini, nilikua nimechelewa kurudi, baada ya mke wangu kuondoka nilikuia najitahidi sana kuwahi kurudi nyumbani ili kukaa na wanangu. Kwa kawiada ninaporudi nyumbani huwa nawasaidia kufanya homework kabla ya chakula, hivyo nilifanya hivyo.


“Hamjammiss Mama yenu?” Niliamua kuuliza, niliona kumekua kimya, hakikua kitu kizuri kwa watoto kumsusa Mama yao namna ile, nilikua nampenda sana Mama yangu, nilikua nataka wanangu nao kumpenda Mama yao kama mimi. Walikaa kimya, niliona kama kuna kitu wananificha, kitu ambacho hawtaaki kusema. Niliendelea kuwafundisha baada ya kuona ukimya, mood imebadilika niluliza tena.


“Naweza kuwapeleka kwa bibi yeni, anaishi kwa Bibi yenu…” Niliwaambia.


“Mbona Mama anakujaga kutuchukua shuleni, juzi alikuja na yule Mbaba wake wakatu….” Jane aliongea, lakini kabla ya kumalza kuongea Zack alimkatrisha, alimpiga kofi la uso na kumuambia.


“Nyamaza, nilikuambia usiongee! Si nilikuambia usimuambie Baba, unafikiri Baba akijua atafurahi!” Aliongea kwa hasira, Zack anakuaga na hasira za karibu, nilimshika na kumfinya.


“Kwanini unampiga mdogo wako muache aongee! Unataka afiche nini, nilishakuambia hizo hasira zako nitakujaga kukufumua kichwa!” Niliongea kwa hasira, Zack alinyanyuka na kuanza kuondoka, nilimshika ili arudi lakini hakurudi, alionekana kukasirika sana.


“Njoo uongee! Kuna nini na Mama yako?” Nilimuita lakini aligoma kabisa kugeuka. Nilimgeukia Jane kumuuliza ni nini kilikua kimetokea mpaka Kaka yake kuwa na hasira namna ile aligoma kuniambia. Alionekana kutaka kuniambia lakini alikua anamuogopa Kaka yake. Kila dakika aliniambia kuwa Kaka yake atampiga, alikua anamuogopa Zack kuliko alivyokua ananiogopa mimi. Nilipoona haongei chochote nilimuaacha, nilishidnwa kuendelea kuwafudnisha nikarudi chumbani kwagu.


Nilikaa huko mpaka muda wa chakula, tulikula kimya kimya, nilivumilia lakini nilishindwa, nilitaka kujua kilichotokea. Baada tu ya kula nilimuita Zack chumbani na kuanza kumhoji.


“Mama kila siku anakuja shuleni, anakiuja kutusalimia na wanaume zake, anasema kuwa ni wafanyakazi wenzake lakini mimi ni mtu mzima Baba, ni wanaume zake.” Aliongea, nilimsikiliza mpaka machozi yakaanza kunitoka, alionekana kuumizwa sana na tabia za Mama yake, hakuongea kwa hasira kama kawaida yake bali aliongea kama mtu mzima ambaye anaumia.


Nilijaribu kumtetea kumuambia kuwa hawakua ni wanaume wake bali walikua ni wafanyakazi wenzake.


“Nakujua Bba, ndiyo maana nilimuambia J, asikuambie, unamteteea Mama sana, sijui kwanini unamuogopa, hivi Baba mbona Mama akiwa hayupo tunaishi kwa amani, ni kwanini usimuache tu kama ni kufanya mambo yake afanye wmenyewe?” Aliniuliza swali ambalo kusema kweli sikua na jibu, nilishia kumuambia kuwa yeye ni mtoto akikua atajua.


Hakujibu chochote alitoka chumbani kwangu na kwenda zake kulala. Usiku sikualala kabisa, nilitamani kumpigia simu mke wangu na kumuambia ni kwanini anafanya yote hayo, nilitamani kumuambia arudi tutengeneze familia lakini nilisema hapana. Kama mpaka mtoto mdogo namna aile anaona kuwa Mama yake hayuko sawa sidhani kama naweza kusihi naye. nilityamani kumpigia nimuambie nimekuacha lakini nilishindwa, mwisho niliishia kumtumia meseji.


“Naona imefika mwisho, sidhani kama naweza kuishi na wewe, kesho naanza mchakato wa talaka.” Nilimtumia meseji. Tangu kuondoka alikua hajibu meseji zangu, ingawa alikua anaziona lakini hakua anazijibu, ila siku hiyo ghhafla niliona kajibu.


“Utakua umefanya jambo la maana sana maana naona kuwa unanichelewesha!” Alinijibu, ni jibu ambalo sikulitegemea, nilijua labda ataomba msamaha kutaka turudiane lakini hakufanya hivyo.  Nilituma meseji nyingine nyingi za kumbembeleza lakini hakuna hata moja ambayo ilijibiwa. Siku iliyofuata sikufanya chcohote, wiki iliisha sikufanya chochote, mke wangu alikua hapokei simu zangu. Baada ya wiki hicvi niliitwa kwa mtendaji wa Kata, mke wangu alienda kushitaki.


Alikua akidai talaka, akisema kuwa amekumbuka vizuri kuwa mimi ndiyo nilimpiga mpaka kufikia kulazwa hospitalini hivyo anataka kuachana na mimi. Pia alionyesha meseji kuwa nataka kumuacha hivyo kaamua kudai talaka yeye. Nilijaribu kumsihi lakini kila nilivyokua nikiongea kutokana na kupaniki basi nilionekana kuwa nina hasira, alianza kulia na kudai kuwa nimemfukuza nyumbani hivyo hana sehemu ya kuishi.


Tulibishana sana mwisho iliamuliwa kuwa wakati tukiendelee kutafuta suluhu kanisani basi mimi niondoke nimuachia nyumba ili yeye aishi na watoto kwani madai yake ilikua nimemnyang’anya watoto. Kusema kweli niliumia sana kwani nilikua nampenda sana mke wangu na mbaya zaidi nilijua kuwa hawezi kuishi na watoto. Mke wangu alikua amezaa lakini alikua si Mama, alikua na mambo mengi, nilijua anataka watoto ili kunikomoa, sikujua ni sababu gani wakati sijamfanyia kitu chochote kibaya lakini nilijua kabisa kuwa hakutaka watoto kwa wema.


Nilijaribu kumsihi hatakama anataka nyumba nimuachie na mimi kuondoka na watoto lakini alikataa, alilia na kunishutumu mambo mengi, alionyesha kuwa na uchungu akilalamika kuwa nimemnyang’anya watoto na sitaki awaone. Niliona hamna shida, nilikubali kumuachia watoto, nikaenda nyumbani na kuchukua vitu vyangu, kwa bahati nzuri wakati nafika na kuchukua vitu watoto hawakuepo nyumbani.


Nilichukua vitu vyangu na kuondoka, nilienda kupanga chumba kwani pamoja na kuwa na nyumba nyingine lakini zilikua na wapangaji, lakini pia nilijua kuwa ni ishu ya mpito hivyo sikutaka kukurupuka. Nilikaa kwa wiki moja tu, nilipigiwa simu na Mama mkwe wangu, alikua akilalamika kuwa tumempelekea watoto na kumtelekezea hata matumizi hatutoi. Nilishangaa sana kwani nilujua watoto wapo na mke wangu na si Mama yao.


Nilimpigia simu mke wangu akaniambia kuwa yeye kasafiri ndiyo maana akaamua kuwapeleka kwa Mama yake. Tuligombana sana mwisho akaishia kunikatia simu, nilikasirika sana, nilitamani kwenda kuwachukua wanangu lakini sikua na sehemu ya kuwaweka. Siku ileile nilitafuta nyumba, kwakua pesa haikua tatizo nilinunua baadhi ya vitu, moja kwa moja nilienda kwa mtendaji wa kata na kumuambia kilichotokea. Sikutaka kuwachukua watoto kienyeji, mke wangu alitafutwa kwenye simu lakini aligoma kupokea.


Nilikabidhiwa watoto na kurudi nao kwangu, sehemu ambayo nilikua nimepangisha ili kuishi na wanangu. Siku ya kwanza ilipita, lakini nilikuja kugundua kuwa watoto hawkaua na nguo, vitu vyao vingi waliacha nyumbani, nilimpigia simu mke wangu lakini alikua hapatikani. Nilimtumia meseji lakini hakuziona, simu ilikua imezimwa, kwakua nilikua na ufunguo wa nyumbani niliamua kwenda kuchukua nguo za wanangu na kurudi nikiamini kuwa labda mke wangu alikua amesafiri na alikua sehemu ambayo hakuna nework.


Nilimtafuta mtendaji wa Kata ambaye ndiyo alinikabidhi watoto na kumuambia, sikutaka kwenda kimya kimya ingawa ilikua ni nyumba yangu. Tulifika nyummbani na kufungua mlango wa geti, tukaingia mpaka ndani, lakini kufika malango wa sebuleni ulikua umeufunguliwa. Niligonga huku nikimuita mke wangu, niliita sana lakini hakufungua, kwakua nilikua na mtendaji nilifungua malango.


Nikaenda mpaka chumba cha watoto, nilianza kukusanya nguo za watoto taratibu, kama nusu saa baadaye ndipo mtu alitoka chumbani.


“Wewe nani na unafanya nini nyumbani kwangu?” Nilisikia sauti, ilikua ni sauti ya kiume, alikua akimuambia mtendaji, harakaharaka nilitoka kuangalia, Baba mtu mzima ambaye sikua nikimfahamu alikua kasimama amevaa Boxer tu, alionekana kutoka kulala.


“Nyumbani kwako? Wewe ni nani?” Nilimuuliza kwa hasira.


Tulijikuta tunaanza kubishanaa kila mmoja akimuuliza mwenzake ni nani na anafanya nini? Alikua ni Baba mtu mzima kliko mimi, tulijikuta ttunarusiana maneno mpaka mtendaji alipotuamua ndipo akatulia na mimi nikatulia.


Nilimuambia kuwa mimi pale ni kwangu ni nyumba nimejenga na kwa wakati huo alikua anaishi mke wangu amabye sijui yuko wapi? mwanzo nilidhani labda mke wangu kaamua kuuza nyumba au kupangisha bila kuniambia.


“Hapana, utakua umechanganya, hii nyumba ni yangu, huyu mwanamke alikua ni mchepuko wangu kwa miaka 10 sasa, nimemjengea hii nyumba alikua anaishi na Mama yake na sasa hivi nimekuja kuishi hapa kwakua nimeachana na mke wangu na yeye Mama yake kafariki hivyo anaishi mwenyewe.” Yule Baba aliniambia.


Kama unataka kuanzisha Biashara unatakiwa kufahamu kitu kimoja, sehemu ambayo Biashara yako ipo ni ya muhimu sana pengine kuliko kiasi cha mtaji ulichonacho, kuwa makini sana katika kuchagua sehemu, kile unachokiuza kiendane na mahitaji ya wateja wako na pia kiendane na mazingira, kiuzike eneo hilo.


SIMULIZI; MAMA USIFE ILI UNIGUZE—SEHEMU YA NNE


Nilimuelezea yule Baba kila kitu kuhusu mimi, nikamuambia kuwa mimi ni mume na ndiyo mwenye ile nyumba. Nilimuonyesha baadhai ya vitu vyangu ambavyo baada ya kuchunguza sana mke wangu alikua kavifungua stoo, nilimuambia kuwa nimeenda kuchukua vitu vya wanangu. Kwanza alishangaa kwani alikua hajui kama mke wangu ana mtoto.


“Mbona hajawahi kuzaa, ni kweli alishabeba mimba zangu lakini hakuzaa, kuna mimba moja iliharibika na miezi saba, nyingine alifanyiw aupasuaji kabisa mtoto akafia tumboni ikiwa na miezi nane, nakumbuka nilikua Uingereza na mimba ya tatu ilitoka akiwa na miezi saba ndiyo nikamuambia asizae tena.” Aliniambia, kwa kipindi ambacho aliniambia kuhusu hizo mimba ni kipindi ambacho mke wangu alikua na ujauzito wa wanangu.


Nilishindwa hata kuwa na hasira, nilishangaa huyu ni mwanamke wa aina gani? Nilijikuta naongea mambo mengi na yule Baba, ambapo aliniambia kuwa ameachana na mke wake baada ya kuwa mke wangu anamtukana kila mara na alimuambia kuwa ahcague kati ya yeye na mke wake hivyo akamaucha mke wake na wahsaanza mahcakato wa talaka mahakamani.


Nilimuuliza kuhusu mke wangu alipokua akaniambia kuwa katoka, wakati aliwaacha watoto kwa Mama yake kwa madai kuwa amesafiri. Wakati tukiwa pale kila mtu anamsahangaa mwenzake kwa kudanganywa gari ya mke wangu iliingia, lakini aliona gari yangu pale hivyo akajua kuwa nipo pale. Alikaa kwenye gari kwa muda wa kama dakika kumi hivi kisha akaingia, aliingia moja kwa moja na kuanza kutukana.


Alikua ananitukana mimi akiniambia kuwa ni kwanini nahangaika na maisha yake wakati hanitaki, nilijaribu kuongea sababu ya kuja pale lakini hakunisikiliza. Walianza kugombana na yule Baba ambaye alimshika kutaka kumpiga akimshutumu kwa kumharibia maisha yake. Mke wangu alijitetea huku akilia akiomba msamaha.


“Sikutaka kukuambia kwakua nilikua kwenye ndoa ya mateso, huyu mwanaume ananipiga, ananitesa, hanihudumii kwa chochote, juzi tu ndiyo nimetoka hospitalini, alinipiga mpaka nikalazwa wiki nzima sina fahamu. Huyu mtu ni mshenzi, nimejaribu kumuacha imeshindikana!


Muulize mtendaji, anajua kila kitu, nilikua na kesi polisi lakini kanitishia kuwa kama nikiendelea nayo akifungwa basi sitawaona watoto. Nina watoto kweli lakini si watoto wake, ni watoto wako, sikukuambia kwakua ananitishia mimi, unaona kaninyang’anya watoto wiki ya pili hii hataki hata niwaone, wewe ndiyo unanipa amani, kama huamini wewe ni mtu mkubwa, nedna kituo cha polisi ulizia kama si kuna kesi na yeye alinilazimisha niifute!”


Mke wangu aliongea sana kiasi cha yule Bba akuanza kumuamini, nilijua kuwa hatuwezi kuelewa, nilimuambia kuwa kilichokua kimenipeleka pale ni kuchukua vitu vya watoto tu. Sikutaka kusikia chochote kutoka kwa mke wangu, kweli nilichukua vitu vya watoto na kuondoka pale. Sikuwasiliana tena na mke wangu, sikumtafuta na wala yeye hakunitafuta, mpka baada ya wiki mbili hivi. Alinipigia simu akilia, sikutaka kumsikiliza lakini alikua akilia sana nikalazimika kumsikiliza.


Mama yake alikua anaumwa na yeye hakua na pesa, nilishangaa kwani asubuhi yake Mama yake alinipigia simu na kuongea na watoto. Nilimsikiliza akaongea sana lakini mwisho nilimkatia simu, alijaribu kunipigia simu na kunitumia meseji kuwa ana shida anahitaji kuongea na mimi lakini sikujali tena baada ya kile kitendo nilishafanya maamuzi ya kuachana na mke wangu, niliacha kumfuatilia na kaucha kuhangaika kabisa na mambo yake.


Alipoona nimempotezea alianza kuwadai watoto, alifanya hivyo kwa kwenda usatwi wa jamii. Nilienda na kuongea nao, baada ya mtendaji kuitwa na kuongea kilichotokea ilionekana kuwa mimi ndiyo natakiwa kuishi na watoto kwani hata watyoto hawkautaka kuishi na Mama yao. Kile kitendo kilimuumiza sana mke wangu, akawa mtu wa visirani, anawafuata watoto shule na kuwaambia maneno ya ajabu ajabu lakini sikutetereka.


Nilichokuja kugundua nikuwa, yule mwanaume ambaye nilimkuta kwangu alikua ndiyo mfadhili wake mkuu,. Baada ya mimi kumkuta alimuamini mke wangu na kumsamehe. Lakini baadaye aligundua kuwa mume wangu ana wanaume wengine hivyo akaamua kuachana na mke wangu na kurudi kwa mke wake, mke wangu alipoona vile ndiyyo alitaka kurudi kwangu. Sikukubali, miezi sita iliisha bila mawasiliano na mke wangu, alijaribu kuniomba msamaha, akatumia ndugu na kila kitu lakini sikukubali.


Baada ya mimi kuondoka na kumuacha mke wangu maisha yake ni kama yalibadilika, ni kama nilimfungulia milango ya mikosi kwani kazini alisimamishwa baada ya kugundulika kuwa kuna pesa alikua anaiba, alisimamishwa ili kupisha uchunguzi. Bosi wake ambaye naye alikua ni bwana wake alimgeuka kabisa na hakutaka kumsikia, wanaume wake wengio walimuacha, kutokana na aina ya maisha ambayo alizoea aliishia kuwa mtu wa kisirani tu na kugombana na kila mtu.


Mama yake ambaye ndiyo alikua kipendi chake waligombana sana, walikua wanatukanana kwani kila siku Mama yake alikua anamuambia kuwa alikosea kuachana na mimi kitu ambacho kilikua kinamkera mke wangu. Pamoja na yote hayo nilishindwa kabisa kuingia kwenye mahusiano mengine, sio kwamba nilikua sikutani na wanawake, hapana, nilikua nakutana nao lakini kila nikianzisha mahusiano naona kama nao wataniumiza kama mke wangu.


Nilikua naumia sana, kuna wakati nilikua Napata mtu, najua kabisa kuw ahuyu ni mtu sahihi lakini najikuta bila sababu ya msingi namuacha tu, nilikua sipo tayari kabisa kuingia kwenye mahusiano. Rafiki yangu mmoja alinishauri na kuniambia kuwa ili kuingia kwenye mahusiano siriasi ni lazima kuachana na mke wangu, kwakua waikiristo hatutoi talaka alinishauri kuanzisha mchakato wa talaka ya mahakamani.


Ilinichukua muda sana kukubali lakini mwisho wa siku nilikubali, nilitafuta mwanasharia ambaye aliniambia niende ustawi wa jamii, tukaitwa baraza la kata, mke wangu wakati huo alisharudishwa kazini baada ya kuhonga honga sana na alikua hanisumbui sana. Lakini baada ya kusikia nataka alaka aligoma akasema yeye hawezi kauchana na mimi. Tulisumbuana pale tukarudishwa kanisani, huko nako mambo yalishindikana, mke wangu aligoma kuachana na mimi niligoma kurudiana naye.


Kama unavyojua michakato ya talaka kanisani inakua migumu sana, walitushauri sana na kutuambia kuwa turudi tusihi pamoja ili kuona kama tunawezana. Mimi nilikataa lakini kwakua waligoma kutupa barua basi nililazimika kurudi kwa kipindi walichotuambia ili kuangalia kama tutaelewana na mke wangu. Kila mtu alirudi kivyake na kuwa na maisha yake, mke wangu yeye alianza kushi na mwanaume mwingine.


Hawakua wakiishi kama mke na mume kwani naye alikua ni mume a mtu lakini walikua wanatumia muda mwingi pamoja na kila mtu, majirani na mpaka watoto walikua wanajua kuwa Mama yao anaishi na mtu. Sikuweza kulizuia hilo kwani alikua akiwafuata shuleni akiwa na huyo mwanaume. Baada ya kama miaka miwili tangu kutengana na mke wangu nilikutana na mwanamke mwingine, wakati huo tulishamalizana na mambo ya kanisani na ishu ya talaka ilikua mahakamani.


Nilimuambia huyo dada kuwa mimi nimeoa lakini mke wangu tumehitilafiana na kesi yetu ipo mahakamani. Nilimuonyesha nyaraka zote na kumuambia kuwa nahitaji mtu wa kuingia naye kwenye ndoa si kumchezea. Nilimuambia kila kitu nilichopitia na kumuambia anipa muda na anivumilie mpaka talaka ikitoka basi ndiyo mimi nayeye tunaweza kwenda hatua nyingine.


Alinisikiliza na kunielewa kwani naye alikua ni mtu mzima, ingawa alikua hajaolewa na alikua hana mtoto lakini alipitia mahusiano ya mateso kidogo, aliishi na mwanaume kwa miaka saba bila kupata ujauzito, mwanaume hakumuoa hivyo alimuacha na kutafuta mwanamke mwingine kwa madai ya kutafuta mtoto. Kwakua mimi sikua na shida sana na mtoto, nilikua nikitaka tu mwenza nilimkubali na tukaanza mahusianao.


Alikua anafanya kazi, yeye alikua ni Nesi kaajiriw aserikalini, mahusiano yetu yalianza kama utani, taratibu lakini baada ya miezi sita hivi tulikua tunaishi pamoja na tayari alishabebe ujauzito wangu. Alikua anaishi na wanangu vizuri na kwakua kwa muda mrefu walikua hawajawa na Mama basi walifurahi, alikua anawapenda sana. Kitendo cha mimi kuishi na mtu kilimuumiza sana mke wangu, alinitumia meseji nyingi za vitisho, akaniambia kuwa hawezi kunipa talaka na hawezi kuruhusu mimi kuoa mwanamke mwingine.


Mimi nilimuambia kuwa huwezi, nilikomaa mahakamani, na kweli nilipata talaka ya mahakamani ambayo ilitolewa na mahakama ya mwanzo. Lakini baada tu ya kutoka talaka mke wangu alikata rufaa. Sikusherehekea ushindi kwa muda mrefu rifaa hata haikcuhukua miezi mitatu, mahakama ilitengua hukumu ya mwanzo, wakadai sijui kuna taratibu hazikufuatwa, kuja kuchunguza nikagundua kuwa mke wangu anatembe ana rafiki wa hakimu.


Walitoa hukumu kuwa kwakua kuna taratibu zilikosewa basi kesi irudi tena mahakama ya mwanzo na mimi nianze upya. Nilitaka kukata rufaa lakini shida ikawa ni kupata nakala ya hukumu, mara kuna hiki, mara kuna kile, mpaka ule muda wa kukata rufaa unaisha ndipo nagundua kuwa kumbe hata wakili wangu naye alikua ameshakula pesa ili kunihujumu. Niliumia sana kwani nilishaona kuwa nimejitoa kwenye mikono ya mke wangu.


Kibaya zaidi nikuwa, katika mahakama ya wilaya iliamuliwa kuwa watoto bado ni wadogo hivyo wabaki na Mama yao. Hapo ndipo nilichanganyikiwa kabisa, nilimbembeleza sana mke wangu ili mimi kubaki na watoto lakini aligoma. Alisema kuwa anawapenda watoto wake hivyo kamwe hawezi kukubali kuwa walelewe na mwanamke mwingine. Aliniambia kuwa kama kweli nawapenda watoto basi nirudi nyumbani ili tuishi pamoja.


Kusema kweli sikua tayari kabisa kwa hilo, lakini pia sikua na namna, mke wangu aliwachukua watoto, wakati anawachukua walilia mpaka nikawaonea huruma. Mke wangu wakati wote huo alikua akitukana akisema kuwa mimi nimewafanya watoto kumchukua yeye hivyo hawezi kuwaruhusu kuja tena kwangu, kama nataka kuwaona basi niende kuwaonea kwake. Hakutaka hata niongee nao kwenye simu, aliwafukuza wadada wa kazi watatu kwakua tu walinipa simu niongee na wanangu.


Nilianzisha mchakato mwingine wa talaka lakini nilizungushwa sana mpaka kukata tamaa, niliamua tu kuachana na ishi ya talaka na kukaa kimya. Lakini sikua na amani kwani huku nyumbani mwanamke niliyekua nikiishi naye alikua akilalamika na kunisumbua akiniambia kuwa kama siwezi kumaucha mke wangu basi nimuache yeye. Hali ilikua ngumu sana sikua na amani, nilikaa miezi miwili bila kuwaona wanangu, sikutaka kwenda nyumbani na shuleni aliongea na walimu niliua siruhusiwi, sijui alipata wapi amri ya mahakama lakini aliwoanyesha kuwa eti mimi nitawadhuru wanangu.


Pale nyumbani napo ilikua shida mimi kwenda kwani ni kama alikua anaishi na mwanaume mwingine, kila wakati mwanaume wake alikua hapo. Yaani pamoja na kulazimisha kuw anaataka turudiane lakini bado kulikua na mwanaume mwingine na mke wangu ni kama alikua anaishi naye. siku moja nilichelewa kutoka kazini, nilirudi nyumbani kwangu kwenye saa nne hivi, nilimgongea mke wangu mpya niliyekua nikiishi naye.


Wakati anafungua malango, nimeingiza gari kwenye geti basi ghafla nashangaa mwanangu Zack anaingia, alikua amekuja kwangu muda mrefu ananisubiria kutaka kuonana na mimi. Alikua bado kavaa nguo za shule, wakati huo alishakua mkubwa ana miaka 12. Nilimuuliza kuwa anafanya nini kwangu usiku wote ule na nguo za shule ila hakujibu, alianza kulia na kuniambia kuwa kama mimi siendi kuwachukua basi ni bora wafe wote.


“Baba ningekua mwenyewe ningekua nsihaondoka, lakini siwezi kuwaacha wadogo zangu na Mama bora nife, nimekuja kukuambia kuwa hatutaki kuishi na Mama, yule mwanaume wake anatupiga, anatufanyia mambo mabaya na Mama ukimuambia anatupiga zaidi anasema kuwa wewe ndiyo umetufundisha tuseme. Sasa Baba nakuambia nataka ukatuchukue, la sivyo mimi nitajua chakufanya!”


Aliongea kwa hasira kama kawaida yake lakini sasa hivi alikua analia, nilimuingia ndani, wakati tunatembea kuingia ndani alikua bado analalamika.


“Yaani nalazimika kulala na wadogo zangu watoto wakike, nikiwaacha atawabaka, mimi mwenyewe alikua anakuja usuiku eti ananishika matako anataka kunipaka mafura! Nikiamuambia Mama anasema kuwa nimepanga na wewe ili tuondoke, haniamini, Baba kama huji kutuchukua mimi nitaondoka na wadogo zangu na hutatuona tena!”


Aliongea wakati tunaingia ndani, alikua kanisubiri muda mrefu, lakini kabla hata yakufika ndani gari lilisimama nnje, mke wangu ndiyo alikua anataka kufunga geti wakati namuingiza mtoto ndani. Lilikua ni gari la polisi na walishuka mke wangu, huyo mwanaume wake na askari wa nne, wawili wakiw ana bunduki.


“Uko chini ya ulizi Baba, kwa kumtorosha mtoto na kumleta kwako kinyume na amri ya mahakama kuwa watoto wabaki kwa Mama yao.” Askari mmoja aliniambia huku akinionyesha karatasi yenye amri ya mahakama, nilipigwa pingu na kupandishwa kwenye gari.


Kilikua ni kitendo cha muda mfupi sana, wanaonekana walikua wananivizia mimi kurudi kwani baada tu ya mimi kuingia na mtoto kunifuata walijitokeza.


“Nilikuambia uachana ne huyo Malaya uje tulee watoto hukunisikiliza, unaona sas ayanayokutokea!” Mke wangu aliniambia kwa hasira wakati napandishwa kwenye gari. Hakujali wala kuona aibu kuwa pale alikuja na huyo mwanaume wake ambaye wanaishi wote, tena mume wa mtu usiku ule alikua kwake kaiacha familia yake.


Ndoa nyingi watu wanaonyanyasa hutumia vitu viwili, kipato na watoto, ingawa wanaume wengi ndiyo hutumia mbinu hizi kunyanyasa wake zao lakini kuna wanaume wengi pia ambao hunyanyasika katika ndoa zao. Kama upo kwenye ndoa au mahusiano ambayo yanakusumbua, soma kitabu cha “ndoa Yangu Furaha Yangu” labda kitakupa ahueni kidogo.


SIMULIZI; MAMA USIFE ILI UNIGUZE—SEHEMU YA TANO!


Nilichukuliwa mpaka kituoni, nililala kwa siku moja, siku iliyofuata mke wangu alikuja na kunitoa. Aliniomba sana msamaha huku akiniambia kuwa aliamua kufanya vile kwakua ananipenda na alikua anataka turudiane. Mimi sikua tayari kwa hilo lakini nilimuambia maneno ambayo Zack aliniambia.


“Nikweli, mimi mwenyewe nahisi kuwa kuna kitu yule Baba anawafanyia wanangu, lakini sijui namna ya kumuacha, nilifanya makosa mume wangu, kila nikijaribu kumuacha nashindwa, ananing’ang’ania, hata jana yeye ndiyo alilazimisha kuwa mimi nije kukukamata.


Baada ya Zack kuondoka nilijua tu kuwa lazima atakuja kwako, lakini wewe ni baba yake, sikua na shida mwanangu kuja kwako Baba yake, ila yeye alinilazimisha nije nikukamate na kukuvunjia heshima.” Aliniambia huku akilia, alikuja kunichukua mahabusu yeye na gari yake, alikua analia kama mtoto kiasi kwamba alishindwa kabisa kuongea. Kwa kumuangalia ni kama mtu aliyekua anaumia ndani kwa ndani, alishindwa mpaka kuendesha, kila wakati alikua ananiangalia.


“Paki pembeni.” Nilimuambia baada ya kuona kuwa anaweza kusababisha ajali, alipaki pembeni na mimi nikashika usukani kuanza kuendesha gari.


“Nakupenda sana mume wangu na wewe unajua. Kuna mambo mengi huwa nayafanya kwasababu ya utoto na ujinga, lakini baada ya kukaa na wewe mbali nimeona kuwa siwezi kusihi bila wewe. Najua nimekuumiza sana lakini nataka unsidie kubadilika.” Aliniambia, nilimuambia kabisa kuwa mimi siwezi kurudiana na yeye kwani nina mwanamke mwingine na nina familia mpya.


Aliniomba sana msamaha lakini sikukubali, nilimuambia kuwa bado nampenda na sitaacha kumpenda lakini kwa aliyonifanyia siwezi kurudi nyuma.


“Sikulaumu sana, una haki ya kuniacha na kunipa adhabu yoyote ile, najua nimekuumiza sana, ni ngumu sana kwenu nyie wanaume kusamehe. Lakini naomba kitu kimoja, watoto wetu wanateseka, mimi nataka kuachana na yule mwanaume, lakini kila nikimfukuza anakuja, ananitishia mpaka maisha, naomba unisaidie kuachana naye, naomba tu ujifanye tumerudiana ili aniache, nisaidie kwa hilo mume wangu, hata kama huwezi kufanya kwaajili yangu basi fanya kjwaajili ya wenetu.”


Aliniambia, kusema kweli nilikua na hasira na huyo mwanaume, nilitamani hata kumuua, kwa maneno aliyoniambia Zack nilikua sipo tayari kuona anaendelea kuishi na wanangu. Nilimuomba mke wangu kuwachukua wanangu lakini aligoma kabisa, madai yake ilikua anawapenda sana na kama nikiwachukua basi atachanganyikiwa kwa mawazo kwani asingweza kuishi bila wao. Niliendesha gari mpaka nyumbani kwangu, nilimkuta yule mwanaume kakaa pale kama kwake.


“Huyu kaja kufanya nini?” Aliuliza baada ya kuniona, nilimuangalia kwahasira lakini sikusema chochote. Niliongoza mpaka ndani, nikaingia mpaka chumbani kwangu, chumba ambacho nilikua nikilala mimi na mke wangu. Niliingia na kukusanya nguo zake ambaco zilikua mule ndani, nilizitoa na kumtupia, alitaka kuleta ubishi lakini nilimkata jicho na kumuambia kuwa, kama siku nyingine nikimuona katika nyumba yangu sitahangaika naye, nitaenda na kuikatakata mapanga familia yake yote kisha nitaenda polisi mwenyewe.


“Najua unadhani kuwa mimi ni mjinga kwakua nimekuacha ukae kwangu muda mrefu, lakini hapana, nilikua nakuangalia, najua kila kitu kuhusu wewe. Sina hasira na wewe nina hasira na mambo unayofanyia wanangu, siku nikisikia umekanyaga kwenye hii nyumba basi majibu yako utayapata kwenye mazishi ya mke wako na wanao watatu!” niliongea kwa hasira, alimuangalia mke wangu labda ataongea lolote lakini hakuongea, mke wangu alikua upande wangu, hata yeye hilo lilimshangaza.


Alichukua nguo zake, akabaa na kuingia kwneye gari yake na kuondoka, wanangu walikua wameenda shule, nilitoka ili kuondoka, mke wangu aliniomba sana nibaki lakini nilimuambia hapana, nina familia ya kuangalia. Niliondoka na kurudi kwangu.


Tangu siku hiyo mawasiliano na mke wangu yalikua mazuri, aliniruhusu kwenda kuwaona watoto ingawa niligoma kabisa kurudiana naye. Sikufuatilia tena kuhusu talaka na Mama Zana (mwanamke niliyakua nikiishi naye kama mke) alipokua ananiuliza tuliishia kugombana. Nilishapata naye mtoto mmoja wakike, kwasababu hiyo alikua na wasiwasi sana kuwa naweza kumuacha na kurudiana na mke wangu kwakua tulikua tunapatana.


“Inamaana hutaki niongea na watoto wangu, nimegombana na Mama yao lakini si wanangu!” Mara kwa mara nilikua namjibu kila mara alipokua ananisikia naongea na mke wangu. Maisha yaliendelea lakini nyumba ilikua haina amani, Mama zana kila siku alikua akilalamikia mawasiliano yangu na mke wangu. Nilijikuta nakua mtyu wa kukasirika, kisirani kila mara. nyumbani kwetu walikua wakimchukia sana mke wangu, ingawa sikua nikiwaambia kila ktu lakini walimuona mke wangu kuwa ni mshenzi na hawakutaka nirudiane naye kabisa.


Kila mara Mama Zana alipokua akiwapigia simu na kuwaambia jinsi nilivyokua nikiwasiliana na X wangu walikua wakikasirika, wananipigia simu na tunagombana. Nilikua sina amani kabisa ndani ya nyumba yangu. nikija nyumbani mke analalamika nikienda kwetu kwa Mama ni kelele, sheemu peke ambayo kulikua na amani ni kwa mke wangu. kule watoto walikua wanafurahi sana kuniona, naenda tunaongea, nakula vizuri na kweli nilimuona kama mke wangu kabadilika.


Mwanzo nilikua naenda mara moja moja, nakaa mpaka sa ambili naondoka, lakini jambo hilo lilikua linamuumiza Mama Zana, kila nikierudi tunakua tunagombana, namkuta kanuna, nyumba haina amanai, nikaanza kuchelewa, nikawa nikienda kwa mke wangu wakati mwingine nakaa mpaka saa sita usiku dnipo narudi nyumbani. Nikirudi mke kanuna, simuongelshi chcohote naoga napanda kitandani nalala. Hali hiyo iliendelea kwa mwaka mzima, sikua tayari kurudiana na mke wangu lakini pia sikutaka kumuacha Mama zana.


Alinichukua kipindi nimechanganyikiwa, nikiwa katika mawazo na alinisaidia mimi na wanangu mpaka kuwa sawa. Ingawa sikua nikimpenda kihivyo kama nilivyokua nikimpenda mke wangu lakini nilijua kuwa ananipenda sana na hawezi kumuacha, nilikua namuheshimu na kumuonea huruma kwani kwa wakati huo tulikua na mtoto mmoja na tayari alikua na ujauzito mwingine, nilikua naona kama ni dhambi kumuacha, pia sikua nimeanzisha mahusiano na mke wangu.


Ingawa karibu kila siku nilikua nikienda huko lakini tuliishia kuongea tu na kucheza na watoto, alinishawishi sana turudiane lakini sikuliruhusu hilo. Kichwani nilikua naamini kuwa nimeachana naye. Wakati Mama Zana akiwa na ujauzito wa miezi 8 mimba ilianza kumsumbua sana, mipango ilikua ni yeye kwenda wketu kujifungulia huko lakini kutokana na hali yake madaktari walimuambia kuwa asisafiri. Kwasababu hiyo Mama yangu mzazi alikuja kwaajili ya kumhudumia.


Hapo ndipo nyumba nilianza kuiona chungu, mbali na kelele za mke wangu nilikutana na Kelele za Mama yangu, ingawa nilijitahidi sana kubadilika lakini walikua hawanyamazi. Mama yangu ni mlokole, si mtu wa kuongea sana ila kwa mke wangu alivyokua anamchukia aliongea sana, kila nikichelewa kidogo waliongea, walikaa na mke wangu wakaungana kiasi kwamba suala la kurudi nyumbani lilikua gumu kwangu nikiwa njiani nafikiria mara mbili.


Kwa mara ya kwanza nilianza kulala kwa mke wangu, ilikua kama utani tu, nilimuambia kuwa naingia chumbani kwake kuoga. Nakumbuka ilikua ni siku ya jumatano, niliaga nyumbani kuwa naenda kuangalia mpira mechi za UEFA sikuwenda kuangalia mpira lakini sikutaka kelele. Nilienda moja kwa moja kwa mke wangu, baada ya kumaliza kufanya homework na watoto nilibaki na mke wangu sebuleni, tukaangalia mpira baada ya kuisha tulikaa sebuleni mpaka saa nane.


Nilimuomba kutumia bafu lake kuoga kwani nilijua kuwa nikirudi nyumbani kutakua na kelele nyingi, nilitaka kuoga ili nikirudi nyumbani nalala. Aliniruhusu ila nikiwa huko alinifuata bafuni, kwakua kule nyumbani tendo la ndoa lilikua la shida kwasabu ya ujauzito na kelele za mke wangu basi sikua na nambna, tulifanya yetu na huo ndiyo ukawa ni mwanzo wa kurudiana. Nilirudi nyumbani asubuhi, sikuongea chochote zaidi ya kuvaa nguo za kazini na kuondoka.


Jioni Mama aliniitisha kikao, nilimuambia tu kuwa mimi ni mtu mzima najua nianchokifanya hivyo sitaki kupangiwa maisha. Nilianza kuhamia kwa mke wangu, mpaka Mama Zana anajifungua mtoto wapili basi nilikua nimeshahamisha karibu kila kitu changu kwake. Mke wangu alikua na spiridi sana, baada ya kuona kuwa nimehamia kwake mazima, kule kwingine naenda kusalimia alizidisha mapenzi, kutwa kucha kunipost katrika mitandao ya kijamiki, alipenda kuongozana na mimi kila sehemu na kuonyesha kuwa mimi na yeye tupo pamoja na tuna furaha.


Katika maisha yangu yote tangu kumuoa mke wangu kwa mara ya kwanza nilijiona kama mwanaume, alinijali na kunihudumia kama malaika. Kiasi kwamba nilisahau kwamba nina mwanamke mwingine ambaye ana mtoto wangu mchanga, alikua ananisikiliza, ananitambulisha kwa marafiki zake kama mume wake tofauti na zamani ambapo alikua hataki hata niongozane naye. kila siku alikua ni mtu wa kuniomba msamaha, nilimpeleka kwa ndugu zangu alimuomba Mama yangu msamaha, kutokana na imani yake Mama alimsamehe.


Nilimuweka Mama katika mtrego, nilimuambia kuwa nimechoka kuzini na kwakua ndoa ya kanisani haivunjwi Mama hakua na namna zaidi ya kusamehe. Pamoja na yote hayo lakini sikuachana na Mama Zana, wala mke wangu hakunilazimisha moja kwa moja kufanya hivyo ingawa nilikua naweza kukaa hata miezi mitatu bila kwenda kuangalia watoto pamoja na wote kuwa dar.


Ilifikia kipindi nikawa situmi matumizi, hata kodi ya nyumba nilishindwa kulipa, majukumu ya nyumbani kwangu yalikua makubwa na mke wangu alikua ananibana sana tufanye mambo ya maendeleo kwaajili ya wenetu. Kuona hivyo Mama Zana aliondoka na watoto akaruidi kwao mwanza, ndugu zake walimfungulia biahsara na ikawa ndiyo nimeachana naye, sikutaka kuwasiliana naye, kila mwezi nilijitahidi kumtumia laki moja ya matumizi ya watoto.


Sikupiga hata simu kuulizia kama watoto wanaendeleaje, sijui kwanini lakini nilikau kama na chuki flani, kila nikifikiria kumpigia simu na kuongea naye nilihisi kama namsaliti mke wangu. Sikutaka kuharibu mambo, tayari nilishakua na amani na mke wangu niliona kabisa kuwa kabadilika. Akini amani haikudumu kwa muda mrefu, miezisita tu baada ya Mama Zana kuondoka mke wangu alipandishwa cheo kazini, majukumu yaliongezeka na msahara ulikua mkubwa.


Mwanzo mimi ndiyo nilikua na kipato kikubwa kuliko mke wangu, lakini baada ya kupandishwa chao pamoja na marupurupu yake kipato chake kilikua ni karibu ya mara mbili ya kipato changu. Mwanzo sikuona mabadiliko lakini taratibu alianza kufanya mambo yake bila kunishirikisha, alianza kuwa msiri, akaanza kuwa bize, akawa ni mtu wa kuchelewa kurudi nikimuuliza ananiambia yupo bize na kazi. Hali hiyo iliniumiza sana, nilianza kuona kama tunarudi kulekule tulipotoka.


Nilijikuta nakua na wivu wa ajabu, nakua na kisirani, kila siku nikulalamika na kukuambushia makosa ya nyuma, mke wangu alikua anakasirika, tunanuniana hata wiki hivyo nalazimika kumuomba msamaha. Baada ya kurudiana ile mara ya kwanza simu yake ilikua huru kwangu, nilikua nina uwezo wa kushika simu yake na kuangalia meseji zake, sikukuta chochote, lakini baada tu ya kupanda cheo alibadilika, simu akaweka password nikawa siruhusiwi kuigusa.


Nikimuuliza kwanini alikua akiniambia kuwa ana cheo kikubwa ni mambo ya siri siruhusiwi kujua. Siku moja usiku kwenye saa mbili hivi mke wangu alipigia simu, alitoka nnje kupokea, aliongea kama nusu saa hivi na kurudi ndani, nilimuuliza ni nini akaniambia kuwa ni mambo ya kazi. Aliingia ndani na kujiandaa kutoka, nilimkataza lakini hakukubali, alivaa na kuingia kwenye gari akaondoka bila kujali kuwa nasema nini.


Niliumia sana, hakurudi mpaka kesho yake asubuhi, aliniomba msamaha na kuniambia kuwa kazi zilikua nyingi. Sikuongea chochote nilivumilia, lakini haikuishia hapo, ilianza kuwa kama tabia yake, hazipiti siku tatu kabla ya yeye kutoka namna hiyo, nilikua naumia sana lakini sina chakufanya. Sikumoja akiwa nyumbani alipigiwa simu, ilikua ni usikuwa saa nne hivi, sikuuliza kwani nilijua lazima atatoka kama kawaida yake.


Alipotoka tu na mimi nilitoka, niliingia kwenye gari yangu na kuanza kumfuata nyuma. Wala hakua anaenda mbali sana, ni kama mitaa miwili tu alisimama na kuingia kwenye Baa moja kubwa tu, nilikaa kwenye gari akaingia kule alikaa kama masaa mawili hivi, hakutoka, nilichoka kusubiri na kuamua kuingia, lakini ile nashuka kwenye gari nikamuona nayeye anatoka, alikua amekumbatiwa na mwanaume mmoja, ni kijana zaidi yangu na walikua wameshikana kimahaba wanalambana lambana kimapenzi.


Nyuma yao walikua watu wengine wawili, mmoja nilimfahamu, nilshawahi kumuona anafanya kazi na mke wangu, si bosi wake lakini wanavyeo vilivyofanana sema idara tofauti. Mimi si mtu wa vurugu lakini siku hiyo hasira zilinipanda, niliwafuata bila kusema chochote nilienda na kumshika mkono mke wangu kumvuta ili tuondoke. Kwanza mke wangu alishangaa kuniona pale, pili aligpma kabisa kuondoka na mimi.


Pamoja na kumsihi sana lakini aligoma akiniambia kuwa sikwenda naye hivyo nisimpangie maisha. Ulizuka ugomvi mkubwwa, wale wanaume waliokua naye walianza kunisukuma sukuma kuniambia kuwa nimuache kama hataki lakini niliwaambia kuwa waniache kwani ni mke wangu. Mabaunsa wa ile baa walikuja, wakanisihi niondoke lakini niligoma na kuwaambia kuwa siwezi kuondoka mpaka niondoke na mke wangu.


Kuona hivyo wale watu aliokua nao waliingia kwenye gari yao wakiniacha mimi na mke wangu tukizozana. Mke wangu alikuja na gari yake lakini nilitaka aache gari yake na kupanda ya kwangu kwani nilihisi anaweza kuwafuata wale watu. Wakati tunabishana namshika kwa nguvu baunsa mmoja alikuja na kunishika, alinivuta na kunisukuma kwa nguvu. Nilipepesuka na kwa bahati mabya wakati ananisukuma gari ya wale watu aliokua nao mke wangu ilikua ndiyo inaondoka.


Ilikua inarudi nyuma na mimi nilirushwa ghafla, kwanza ilinipiga kwenye kiuno, ikanirusha nyuma,  nikiwa sijui hili wala lile bado ilikua inarudi nyuma ikanipitia kwenye miguu, tairi ikakanyaga kwenye mapaja na kuniruka.


“Nakufaaa!” Nilipiga kelele, watu walishtuka, dereva akasimamisha gari, nilikua chini ya gari, miguu na maummivu makali. Harakaharaka walinitoa lakini miguu yote miwili ilikua imevunjika mmoja ulikanyagwa kwenye mapaja na mwingine juu kidogo ya goti, nilikua katika maumivu makali. Nilianza kulia na kupiga kelele kama mtoto mdogo, walinichukua na kunipeleka hospitalini nikiwa sijitambui, njiani nilipoteza fahamu sikujua nini kinaendelea.


Dalili ya kwanza ya wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume ni umalaya. Wanapenda kuonekana kuwa wana wanawake wengi, sio tu kuwa wanachepuka bali wanataka kuonekana wanachepuka ili waonekane ni vidume. Ndani ya ndoa anajifanya hataki kufanya tendo la ndoa, akifanya basi ni dakika mbili tano, anaishia kusema hafurahii kufanya na mke wake anamkwepa sana.


Lakini mtu huyo huyo ana wanawake mia kidogo mpaka mkewe anahisi kuwa labda yeye ndiyo ana tatizo kwakua mume huko nnje anagombaniwa. Hii inatokana na ukweli kuwa wanaume hawa wanadhani wanadharaulika, wengine unakuta hata hawana matatizo ila kwakua wanaamini mwanaume unatakiwa kwenda raundi tatu na kukaa masaa mawili basi wanakua na vizirani vya bure.


SIMULIZI; MAMA USIFE ILI UNIGUZE—SEHEMU YA SITA!


Nilikaa hospitalini kwa miezi sita nikiwa sijitambui, nilikuja kuamka, mguu mmoja ulikua umepasukapasuka kwenye mshipa wa paja, waliuunga, niliwekewa vyuma, mguu mwingine ulivunjika kwenye goti, huu uliunga tu vizuri kwani ni kama ulikua umepastuka. Nilikua siwezi kunyanyuka wala kutembea. Baada ya kuzindika nilikaa hospitalini kwa mwezi mwingine mmoja kisha nikaanza kupata nafuu. Niliruhusiwa na kurudi nyumbani.


Wakati wote huo nikiwa sijitambui nilikua sijiui kilichokua kikiendelea, mke wangu alishagombana na ndugu zangu wote kuhusu kunihudumia. Yeye ndiyo alikua na kadi yangu ya mshaara na ndiyo alikua na kadi nyingine zenye akiba benki, alitakiwa kutoa pesa lakini alikua akigoma huku bila kuficha akiwamabia ndugu zangu kuwa kama nikifa basi ni yeye aabeba mzigo wa kuhudumia watoto hivyo alikua hawezi kutoa pesa kizembezembe.


Pamoja na kwamba nilikua na bima lakini kulikua na mahitaji mengi ambayo yalitumia pesa, ndutu zangu kila siku walikua wanachangishana, nilikua na viwanja vingi lakini mke wangu aligoma kabisa kuuza hata kiwanja kimoja ili tu mimi nipone. Ndugu zangu waliniambia mambo mengi sana lakini mwanzo sikuwaamini lakini baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini shida ilikua ni sehemu ya kukaa.


Ndugu zangu walitaka niende kwetu ili wakanihudumie, lakini mke wangu aligoma akawaambia kuwa yeye ndiyo mke halaii hivyo hawezi kuacha nihudumiwe na mtu mwingine. Alinihcukua mpaka nyumbani kwangu, kwakua nilikua bado sijajua mambo yake basi na mimi niikubali kurudi kwa mke wangu, kwa jinsi nilivyokua nampenda mke wangu nisingekubali kukaa mbali na yeye isitoshe yeye ndiyo mke, kwangu ilikua ni aibu kusafishwa na ndugu zangu.


Ingawa nilikua sijapooza lakini nilikua kama vile nimepooza, nilikua siwezi kusimama, siwezi kukaa na wala siwezi kufanya chochhote, hata mikono ilikua haina nguvu, ingawa haikuumia lakini waliniambia labda ni kwasababu ya kulala sana hivyo nahitaji mazoezi. Kwamaana hiyo nilikua ni mtu wa kufanyiw akila kitu, nikiwa hospitalini ni ndugu zangu walikua wananihudumia, lakini baada ya kugoma kwenda kwa Mama yangu, walikataa kuja kwa mke wangu hivyo nikabaki mimi, mke wangu, wanangu na binti wa kazi.


Siku ya kwanza mke wangu alinipeleka mpaka chumbani kwetu, tulilala pamoja, alionekana kunifurahia. Kwakua nilikua ni mzito sana aliajiri kijana kwaajili ya kunisaidia kuninyanyua na yeye ndiyo alikua akinisafisha pale nikijisaidia haja kubwa au ndogo. Lakini haikuchukau hata wiki, aligoma kunisaidia, kwanza kabisa alinihamishia chumba cha wageni, huku nikawa nalala na huyo kijana wa kazi. Madai yake nikuwa nalalamika sana maumivu usiku hivyo anakua hawezi kulala vizuri.


Sikua na namna zaidi ya kukubali, lakini hali ilizidi kuwa mbaya, mke wangu alibadilika sana, akawa ni mtu wa kuchelewa kurudi nyumbani na mara nyingi anarudi akiwa amelewa. Wakati huo Zack alikua sekondari, alishakua kijana mkubwa hivyo aliona mambo aliyokua anafanya Mama yake, kila siku walikua wanagombana kwani ni kama alinitelekeza. Katika utetezi wake kuhusu kunywa pombe mke wangu alikua akisema kuwa mimi nanuna sana hivyo hawezi kukaa na mimi bila kunywa.


Maisha yaliendelea, hali yangu ilizidi kuwa mbaya kwani nilikua sipati huduma kwa wakati. Kijana wa kazi ambaye aliajiriwa kwaajii ya kunihudumia mimi tu mke wangu alikua anamtumia kwa kazi zake nyingine, kwa maana hiyo wakati mwingine nilikua nakaa hata masaa sita nimeshajidaidia hakuna mtu wa kunisafisha kwani kijanaa anakua hayupo. Binti wa kazi alikua ni mdogo sana hivyo alikua hawezi hata kuninyanyua, walinitandikia mpira lakini ulikua hausaidii.


Pona yangu peke ilikua ni kwa wwanangu Zack kutoka shule, akasaidiana na binti wa kazi kuninyanyua na kunisafisha safisha kwa shida hivyo, mke wangu alikua hanigusi kwa chochote, ni mara chache sana alikua anaingia chumbani na akiingia hakai hata dakika mbili kwa madai kuwa kuna harufu mbaya ambayo alikua haipendi. Hali hiyo ilikua inaniumiza sana, pamoja na kumpenda sana mke wangu na kutamani kuishi kama familia lakini kuna wakati nilitamani kurudi kwa ndugu zangu.


Lakini niliona aibu kwani walishaniambia mambo mengi aliyokua anafanya mke wangu kipindi sina fahamu lakini niligoma kuwasikiliza. Baada ya muda hata yule kijana aliyekua ananisaidia mke wangu alikua hamlipi akaondoka. Hivyo watu pekee waliokua wananisafisha ni Zack na binti wa kazi akishirikiana na watoto wangu wengine. Kutokana na nilivyokua nimeumia ilikua ngumu sana kuninyanyua, mwili haukua umepooza kwa maana hiyo kama mtu akininyanyua vibaya basi ni kama ananitonisha vidonda.


Kwakua walikua ni wadogo na kunishika yao ni kama kunisukuma wanakua wananiviringisha upaande mmoja kusha wananisafisha na kunirudisha tena basi ilikua ngumu kwao kutoa uchafu wote, kulikua na uchafu mwini unabaki kiasi kwamba nakua natoa harufu nyingi, mimi nilishaizoea kwani sikua na namna, sikua na pakwenda. Nilikua naumia tu, ingawa Zack aliniletea TV chumbani lakini sikua na raha ya kuiangalia.


Kazini nilisimamishwa na baada ya kuona kuwa siwezi kunyanyuka tena mkataba wangu ulivunjwa hivyo nikawa sina kazi tena. Mke wangu alifuatilia mafao yangu na kudai kuwa nikwaajili ya kunihudumia lakini haikua hivyo, sikuona hata shilingi na nilipouliza ilikua ni matusi tu.


“Aisee mwanaume huna shukurani, hivi unakula bure, unalala bure, kilakitu unapata unafikiri pesa zinatoka wapi? watoto wanasoma shule bei ghali unafikiri nalipia nini?” mke wangu aliongea sana, huku akinitukana kutokana na kuugua. Wakati anaongea Zack aliingia, alikasirika na kuanza kumtukana Mama yake.


Zack huwa ana hasira na usipoangalia anaweza kupigana, alimuambia Mama yake ni mbinafsi na kama ishu ni shule basi si bora aache shule.


“Akina bibi walikuambia utoe pesa Baba apelekwe Nairobi lakini ukakataa! Sasa inawezekana kuwa labda angepona! Kama hutaki kumhudumia Baba kwanini humuachi akaondoka, ana ndugu zake wanaompenda sio wewe!” Nilitamani kuingilia na kumuambia asitukanane na Mama yake lakini nilishachoka, niliona kabisa kuwa alikua sawa kani nilikua nateseka sana.


Mke wangu alikasirika na kumkunja, alianza kumpiga makofi.


“Mshenzi wewe, najua hao mbwa washakujaza maneno lakini kwa taarifa yako Baba yako haondoki hapa! Hivi unafikiri kwanini wanamng’ang’ania, unafikiri wanampenda, wote wanaangalia mali, hivi unafikiri Baba yako akienda kwa hao mbuzi, si watamdanganya mali zote watachukua wao? Unafikiri akifa huyu nyie mtapata nini, wewe bado mtoto hujui kitu! Baba yako yuko hapa, hata akifa leo mali zenu ziko salama, lakini akiondoka watamdanganya na kuchukua kila kitu ksiha wataturishia kopo” Aliongea maneno ambayo yalinichom,a sana.


Pamoja na vituko vyote vya mke wangu lakini kuna kitu kilikua kinaniambia kuwa labda ananipenda, nilikua nadhani ni mapito. Usiku na mchana nilikua najiambia kama angekua hanitaki basi angenifukuza, angeacha ndugu zangu wanichukue, lakini ananing’ang’ania kwakua ndani ya moyo wake kuna kaupendo ambapko kamebaki. Maneneo yale tena mbele ya mwanangu yaliniumiza sana, Zack alimuangalia kwa hasira, Mama yake bado alikua amemshikilia huku akimtingisha tingisha kama vile anataka kumpiga.


“Wewe ni Mbwa na kama unafikiri Baba atatangulia kufa basi utatangulia wewe!” Zack alimuambia Mama yake, Mama yake alimsukuma kwa hasira na kumpiga kofi. Zack alisoge kama anaondoka lakini ghafla aliinama, chini kulikua na karai ambalo alikua analitumia kunisafishia, lilikua limejaa maji machafu yenye kinyesi na mkojo, alilinyanyua na kumwagia Mama yake usoni.


“Wewe sio Mama yangu Mbwa mkubwa wewe, ni heri ningezaliwa na nguruwe kuliko kuzaliwa na wewe! Malaya mkubwa wewe!”


Aliongea kwa hasira, nilikasirika, nilitamani kunyanyika kumfuata Zack lakini sikuweza, alikua kasimama anamuangalia Mama yake alivyokua ameduwaa. Ni kweli mara nyingi alikua anamkosea Mama yake heshima lakini si kwa kiwango kile, Mama yake alibaki kasimama, hata yeye hakuamini kama Zack anaweza kumuambia maneno kama yale. Nilimuambia Zack amuombe Mama yake msamaha kwani ni Mama yake hata kama ana mapungufu lakini aligoma.


“Baba nakuheshimu, lakini kama ni kuomba msamaha basi nenda kamuombe Mama yako ambaye alikusaidia miezi yote hiyo uko hospitalini lakini ukamuacha umekuja kuishi na kahaba! Hivi unajua kuwa wakati upo hospitalini Mama alikua analeta wanaume humu ndani wanamlala wakati sisi tunaona, hivi unajua kuwa Mama alichukua likizo mwezi mzima akaenda Dubai na mume wa mtu wakati wewe umelala kitandani hujitambui! Bibi kahangaika, ndugu zako wamehangika lakini bado ukaamua kuja kuishi na huyu mwanamke.


Huyu amenizaa lakini si Mama yangu, kama ni laana basi naikaribisha, na kuanzia leo Baba mimi naondoka, nishakua mkubwa naenda kwa Bibi, kama utaamua kuja sawa lakini kama hutataka basi baki tuone kama hutaoezea humu ndani! Nina uhakika nikiondoka na Dada naye ataondoka, sijui utaishi na nani, tuone kama huyu Malaya wako anaweza kukusafisha mavi!” yalikua ni maneno makali kwa mtoto kuongea kwa Mama yake, nilikua natetemeka kwa hasira.


Nilimbembeleza sana Zack kuomba msamaha lakini hakuomba, kilichoniumiza zaidi nikuwa hakua akiongea kama mtu aliyepaniki bali alikua anamaanisha, hakumuogopa Mama yake, hakujali kama Mama yake alikua analia. Pamoja na yote lakini nilijua kuwa bado ni Mama yake, Zack aligoma kuomba msamaha, mke wangu alikaa chini analia kama mtoto, anaona kama vile kadhalilishwa lakini Zack hakujali.


Zack alitoka na kuondoka, nilibaki mimi na mke wangu, mke wangu alianza kulalamika kuwa ndugu zangu ndiyo wanamjaza maneno mpaka kufikia kumtukana. Nilishachoka keleel zake hivyo sikumjibu kabisa, aliongea mwenyewe alipoona sijali tena basi aliondoka. Nilijua kama utani lakini Zack aliondoka, pale nyumbani nilibaki mimi, mke wangu na binti wa kazi, watoto wadoho walikua wanasoma Bweni, mwanzo alitaka kumpeleka na Zack lakini aligoma kabisa.


Baada ya Zack kuondoka hali ilikua mbaya zaidi, mke wangu alikua hanijali kwa chochote, alikua haingii hata chumbani kwangu kuniangalia. Binti wa kazi alikua hawezi kuninyanyua, alikau akijitahidi kusafisha chumba lakini nilikua naweza kukaa hata siku tatu na choo, hivyo kulazimika kuwaomba boaboda kuja kunisaidia, anawapa buku maisha yanaenda. Baada ya muda alichoka kwani neyeya kulipwa alikua halipwi tena, mke wangu alikua anaweza kukaa hata siku tatu harudi nyumbani.


“Baba mimi naondoka, siwezi kuendelea kukaa hapa, Mama hanilipi na chakula chenyewe haachi.” Aliniambia huku akilia, macho yake yalionyesha kabisa kunionea huruma lakini alikua hana namna alitamani kuondoka. Alinisihi sana kukubali kurudi kwa wazazi wangu, nikweli nilikua nataka kurudi lakini nilikua naona aibu. Nilimruhusu aende huku nikujua kuwa nitakuja kufia mule ndani kwani mpaka wakati huo mke wangu alikua hajarudi.


Alikusanya vitu vyake na kuja kuniaga tena, aliniomba tena nierudi kwa ndugu zangu nikamuambia hapana, hapa ni kwangu na siwezi kumumuacha mke wangu.


“Mama atabadiliaka, akijua kuwa nawewe umeondoka hataniacha nife, atakuja kunisaidia.” Nilimuambia, yule binti aliondoka huku akilia.


“Nimemuambia Bibi aje kukuchukua lakini hataki, amesema mpaka umuambie wewe, wewe ndiyo upige simu uombe msaada, omba Baba, hapa utakufa!”


Aliniambia tena, baada ya kutoka mara ya pili hakuridhika, hakua tayari kuniacha pale, alirudi akiwa kashikilia simu, alimpigia Mama yangu simu, akamuambia.


“Baba huyu anataka kuonge ana wewe.” Alichukua simu na kuniwekea sikioni, akaniambia ongea na Bibi, nilimsalimia Mama yangu, mwaka mzima ulikua umepita tangu kutoka hospitalini na kuonana na Mama yangu, walishanisusia na hakuna ndugu hata mmoja ambaye alikua tayari kuja kwangu wakati naendelea kuishi na mke wangu.


Nilimsalimia akaitika, hakuongea maneno mengine zaidi ya kuitikia salamu na kusema.


“Nakusikiliza mwanangu, unasemaje, nimeambiwa una ujumbe wanngu.” Mama aliongea kwa sauti ya huzuni, alionekana kama vile anatokwa na machozi.


“Hamna kitu Mama, nilikua nakusalimia, mimi na mke wangu tuko vizuri, nina furaha naendelea vizuri.” Nilimuambia Mama, kusikia vile binti wa kazi alichukua simu, alianza kumuelezea Mama ninavyoteseka na kumuambia kuwa waje kunichukua.


Lakini Mama alionyesha kukata simu na hakupokea tena alipompigia. Baada ya pale yule binti naye aliondoka, nilibaki mwenyewe ndani. Mke wangu siku ile hakurudi wala siku iliyofuata, nilikua nimechoka sana, njaa imenikaba, chumba kizima kilikua kinanuka kinyesi, nilikua nikijisogeza kidogo naona kabisa wadudu wamenizunguka. Nguvu ziliniishia, hata kufungua macho ikawa shida, harufu ilikua kali sana kuivumilia, pamoja na yote hayo lakini bado nilikua na imani kuwa mke wangu atarudi na akiona ninavyoteseka basi atanisaidia.


Watu wengi wanao teseka katika mahusiano wana kitu kimojaambacho kinawafanya kuendelea kuteseka kila siku, wanaamini kuwa kesho itakua bora zaidi, wanavumilai mambo mengi kiasi kwamba mioyo yao inakufa na kila wakati kusubiri mabadiliko ambayo hayaji. Wanakua wamejisahau wao na wanafikiri kuwa hawawezi kuwa na furaha mpaka wale watesaji wao waamue.


Wanakua kama mateka, kwamba pamoja na kufanyiwa vitendo vibaya hawawezi kutoka, wanajua kuwa hawapendwi, wanajua kuwa kesho ni mbaya zaidi kaini wanajipa moyo atabdilika. Anza kwa kujipenda wewe, anza kubadilika wewe, kama wewe mwenyewe hutaki kubadilika, hujipendi unafikiri huyo anayekunyanyasa atabadilika? Yeye anapata hasara gani kukunyanyasa mpaka abadilike.


SIMULIZI; MAMA USIFE ILI UNIGUZE—SEHEMU YA SABA!


Mke wangu alirudi na kukuta binti wa kazi alishaondoka, mwanzo alimtumia meseji na kumpigia simu lakini alikua haamini kuwa anaweza kuondoka na kuniacha katika hali ile. Aliporudi alifikiri kwamba nimekufa kwani nilikua nimepotze afahamu na sikujua kitu chochote, alinichukua na kunipeleka hospitalini, aliniachahuko kisha akawapigia simu ndugu zangu kuwa waje kunichukua.


Nilipata fahamu siku moja baadaye, Mama yangu alikua pembeni yangu, alikua analia, hakuna mtu ambaye alijua kuwa nitanyanyuka kutoka kitandani, kila mtu alijua kuwa nitakufa kwani nilikua katika hali mbaya sana. Ndugu zangu wengine  wala hawakuja, baada ya kuwakimbia wote walinitenga na kusema kuwa watakuja kuzika lakini si kunihudumia, mama alikua peke yake akinihudumia.


Nilikaa hospitalini kwa wiki mbili kisha nikaruhusiwa kurudi nyumbani. Nilirudi kwa Mama kwani katika kipindi chote hicho mke wangu hakuja hata kunisalimia au kujua kuwa ninaendeleaje. Lakini sikujali, nilikata tamaa na kuona kuwa maisha yangu yameisha, kila siku kwangu ilikua ni kilio. Nyumbani kwa mama alikuepo mdogo wangu ambaye alikua chuo, yeye alikua anamsaidia Mama mara kwa mara kunihudumia, Zack naye alikuepo na alikua ananihudumia kama kawaioda.


Hali ya maisha ilikua ngumu sana, Mama hakua na kazi, pesa za matumizi ambazo walikua w3anatoa ndugu zangu ndiyo kidogo zilikua zinasaidia ingawa walikua wanatoa kidogo kwaajili ya Mama lakini niliponea hapo. Mdogo wangu ambaye alimaliza chuo na kuondoka pale nyumbani, alipata kazi shinyanga, baada ya kuondoka hali ilizidi kuwa ngumu sana. Mke wangu alikuia ameshikilia kila kitu changu, nyaraka zote alikua kazishikilia na nyingi kabadilisha majinja kipindi naumwa.


Hakuniruusu kuwaona watoto wangu wadogo kwa madao kuwa nitakuja kuwabadilisha wakamchukia yeye. Zack naye hakutaka kuonana na Mama yake, alimaliza kidato cha nne na kufaulu vizuri, alipangiwa kwenda kusoma Iliboru Arusha, mwanzo aligoma kabisa kwenda kwa madai kuwa hawezi kuniacha mimi peke yangu. Nilimbembeleza sana na kumuambia ni bora nifre kuliko kumuacha aharibu elimu yake kwaajili yangu.


Aliondoka kishingo upande hivyo nikabaki mimi na Mama tu, hata binti wa kazi tulikua hatuna, kutokana na umri wake Mama alipata shida sana kunihudumia ikiangaliwa hakua na pesa. Mara nyingi alikua ni mtu wa kuwaomba majirani ili kumsaidia kuninyanyua na mambo mengine. Nilikua nimekata tamaa kabisa, nilitamani kufa, mara kibao nilijaribu kujiua hata kwa kujidondosha kitandai lakini sikuweza, mwili ulikua hauna nguvu na nilikua siwezi kufanya chochote.


Mama Zana, mwanamke ambaye niliichi naye kama mke kwa karibu miaka mitatu alisikia muda mrefu kuwa ninaumwa, lakini kama ndugu zangu wengine baada ya kukimbilia kwa mke wangu hakunitafuta. Alikua anawasiliana na Mama kila siku kuhusu hali yangu na kumuambia kuhusu wajukuu zake, nilikua nimezaa naye watoto wawili. Baada ya mimi kuhamia kwa Mama, Mama alimuomba sana kuja kunihudumia lakini alikataa.


Si kama alikua hanipendi tena au aligoma makusudi, hapana, alikua kwenye mahusiano mapya na kuna mwanaume alikua anataka kumuoa huko kwao mwanza. Habari hizo ziliniumiza sana kwani pamoja na yote yaliyotokea lakini niliamini kuwa nampenda na kuna wati nilitamani kurudiana naye. Mwanaume aliyekua anataka kumuoa alikua akiishi dar, kabla ya kufunga ndoa alihamia huku dar na kuanza kuishi na mchumba wake, watoto aliwaacha kwa Mama yake kwa muda.


Wakati akiwa huku Dar aliendelea kuwasiliana na Mama yangu, walikua wanawasiliana kila siku, na siku moja alimuomba Mama kuja kunisalimia kwani tangu kuanza kuumwa alikua hajawahi kuniona. Nakumbuka ilikua ni siku ya jumamosi jioni ambapo alikuja kuniona, nilikua katika hali mbaya sana, kwanza nimekondena, mwili wote umeisha, pamoja na kuhudumiwa vizuri lakini muda wote nilikua mtu wa mawazo sana hivyo nilikua nimekoda.


Kwa mtu ambaye alikua hajaniona muda mrefu, mtu ambaye aliniona kipindi nikiwa mzima basi angeshangaa sana kuniona katika hali ile. Alikuja nikawa namuomba msamaha kwa yote, alilia sana kuniona vile, alinionyesha picha za watoto ambao walishakua wakubwa, nilitamani sana kuwaona na nilijuta sana kwa kumpotezea muda wake na kumuacha. Alimsaidia Mama kazi nyingi za mule ndani na alipomaliza aliondoka.


Baada ya siku ile sasa akawa anakuja mara kwa mara kuniona, kwakua alikua hafanyi kazi na mchumba wake ni mtu ambaye yupo bize alitumia muda mwingi sana kunihudumia. Alinihudumia bila kinyongo mpaka ikafikia hatua anakuja katibu kila siku. Nilianza kupatwa na wasiwasi na kumuuliza ni kwanini anakuja kila siku wakati nayeye ana mtu wake, aliniambia mchumba wake ni mtu wa kusafiri sana hivyo mara nyingi anazokuja ni pale anapokua kasafiri.


Alifanya hivyo kwa wema tu, hatukuwa na mahusiano yoyote, lakini haikuchukua muda mpaka mchumba wake kujua, waligombana akamakataaza kabisa kuja kwangu wala kuongea na Mama yangu. alimuambia kama ni watoto wapo kwa Mama yake ni kwanini anaongea na mimi na Mama yangu wakati hatuhudumii chochote. Hicho kitu kilimshinda, pamoja na kukatazwa alikua anakuka mara moja moja na mwisho mchumba wake akagundua na kumuacha.


Aliachwa akiwa tayari kashatolewa mahari tena kwaajili yangu, baada ya kuachika hakurudi nyumbani kwao, alihamia kwa Mama yangu na kuchukua jukumu la kunihudumia. Niliumia sana yeye kuchika lakini kwakua nilikua nampenda nilishukuru Mungu kwa namna flani. Alinihudumia kwa miezi kama sita hivi,ndugu zake walimtenga, hawakutaka kunsiikia kwani nilimtelekeza bila kazi na wao ndiyo walimsaidia.


Waliumizwa sana kwa kitendo cha yeye kumauchamchumba wake, mwanaume aliyakua anampenda ambaye alikubali kumuoa na watoto wake wawili na kuja kwangu ambaye nilimtelekeza. Lakini kama unavyojua mapenzi ni upofu hakujali, tuliendelea na maisha, alinipa upendo wa jabu, tulipendana, wakati tunaishi pamoja kuna kiwanja alinunua, kilikua sehemu nzuri lakini kilikuja kupitiwa na barabara. Alilipwa milioni 70, baada ya kulipw akitu cha kwanza ilikua ni kunipeleka nnje kwa matibabu.


Mwanzo ilikua niende Nairobi lakini baada ya kupata pesa nilipelekwa India ambapo nilikaa kwa mwezi mzima nikarudi nikiwa naweza kusimama, kushika kitu. Nilifanya mazoezi mpaka nikaweza kusimama na kutembea kabisa. Ingawa nilikua siwezi kufanya kazi ngumu lakini hali yangu ilirudi taratibu, kila mtu alishangaa, hata ndugu zangu ambao walikua wamenitenga walianzakujileta na kuniona wamaana.


Sikua na kazi lakini baada ya kupona nilianza kufuatilia mali zangu, mke wangu alishangaa kuniona katika hali ile, alijua kuwa nitakufa hivyo nilitafuta wakili ambapo alinisaidia kupata haki zangu zote. Nyumba mke wangu alizibadilisha majina, lakini baada ya kwenda mahakamani kila kitu tuligawana na vingi nilibaki navyo mimi kwani mke wangu naye alikua akifanya kazi ila hakuweza kuwekeza.


Pia nilifanikiwa kupata talaka ya mahakamani na kuwa huru na mke wangu. Watoto wadogo walibaki na Mama yao na Zck alishakua mkubwa hivyo nilibaki naye mimi, hakutaka kumuona wala kumsikia Mama yake. Niliuza badhi ya viwanja, nikapata mtaji na kufungua Biashara, nilianza tena kuishi na Mama Zana kwa malengo ya kufunga ndoa. Niliwachukua watoto wangu ambao nilizaa naye na kuanza kuishi nao mimi.


Maisha yaliendelea na kweli yalikua mafupi, baada ya muda nilipata kazi nyingine ambayo ilikua ni nzuri tu, sikua nimefunga ndoa na Mama Zana, ingawa alikua anasisitiza sana lakini mimi sikuona umuhimu kwani tayari nilikua naishi naye. tulishi pamoja kwa miaka mitatu ndipo kero zikaanza, ishu kubwa ilikua kwenye mali, mimi nilikua nafanya kazi lakini kipato changu lkilikua vizuri lakini duka liiikua linaingiza pesa zaidi na yeye ndiyo alikua anasimamia.


Kwakua nilishaumizwa sana mwanzoni nilikua siwaamini kabis awanawaka, ingawa hakuwahi kunifanyia kitu kibaya lakini niliona kuwa wanawake wote wako sawa. Sikumshirikisha kwenye kitu chochote, dukani alikua ni kama muuzaji, pesa nakusanya na kama ni kuwekeza nawekeza na Mama yangu ambaye ndiyo mtui pekee nilikua namuiaminia, hata ndugu zangu sikuwa nawaamini.


Mwanzo hakusema chochote lakini baada ya muda alichoka kwani nilikua nambana sana, akawa analazimishia ndoa na mimi nilikua sitaki kwani nilijua tukifunga ndoa basitutagawana mali kama ikitokea tukiachana kama ilivyokua kwa mke wakwanza. Tuligombana sana, hakuninyanyasa wala kuzungumzia mambo ya nyuma lakini mimi mwenyewe nilisjishtukizia na kuhisi kuwa labda anataka nimshiriksihe kwenye mali zangu kwakua alinisaidia pesa ya matibabu.


Tuligombana sana, kitu kilichomuuma zaidi nikuwa, vitu vingi nilikua naandika majina ya wanangu hasa wale wakubwa ambao nilizaa na mke wangu wa zamani, alipoona alillamika kuwa simpendi yeye wala watoto wake, hapo na mimi nililalamika kuwa anawachukia watoto wangu ndiyo maana alikua hataki niwaandike mali. Tuligombana sana, nyumba ikawa haina amani kila siku ni ugomvi. Wakati huo huo mke wangu wa zamani alikua kabadilika sana, alikua ananiruhusu kuwaona watoto na nikikutana naye tunaongea vizuri tu kama marafiki.


Nikawa namuambia mambo yangu, namuambia jinsi ndoa ilivyokua inanisumbua, alikua akinisikiliza na kunipa moyo. Tukawa tunachat karibu kila siku, Mama Zana aligundua na kurishia kuondoka, kuseme kwali nilishamchoka kwani nilishachoka kelele zake, nilimuambia kama kaaamua kuondoka aondoke kwani hawezi kunipangia maisha mimi ni mwanaume.alijirudi na kuomba msamaha, lakini shid ailikuja kwa X wanmgu, alikua ni mtu wa kupiga simu kila siku, mtu wakunisumbua na wakati mwingine hata kumpigia simu Mama Zanba na kumuambia mambo ambayo tunaongea.


Siku moja nilikua nimetoka kazini, narudi nyumbani nakuta nyumba iko wazi, naangalia nguo za Mama zana na wanangu hazipo. Nikampigia simu akawa kaondoka, kumbe alishajikusanyia maji wake, alishanunua kiwanja chake na kujenga. Alipoona sieleweki alichukua vitu vyake na kuondoka, nilipompigia simu aliniambia, kama undahani kuwa nilikuja kwako kwaajili ya mali basi umekosea, naondoka na kuacha na mali zako.


Nilijua labda anatania lakini kumbe alikua kajipanga, aliondoka na kwenda kufungua duka lake la vifaa vya ujenzi mtaa wa pili tu na lilipokua duka ambalo nilimfungulia. Hakuiba kitu chochote lakini alichukua wateja wangu wote, miezi sita tu duka langu lilikufa, mbali na kupoteza wateja wangi lakini watu niliowaweka waliniibia. Nilibaki tu na kazi yangu, nilimtafuta Mama Zana kumuomba msamaha lakini aligoma.


Kule kwa X w3angu nako baada ya kujua kuwa nimeachwa alikatisha mawasiliano, nilikua nikimpigia simu ananikatia na mwisho akaniblock kabisa, ilikua ngumu sana kwangu kukubaliana na ukweli. Nikajikuta nimebaki mimi na Mama yangu tu, watoto hawanitaki, Zack mwenyewe alikua hanitaki, alikua ananichukia hasa baada ya kumuacha Mama Zana ambaye alikua anampenda kuliko Mama yake, X wangu hanitaki na mwanamke ambaye alijitolea kila kitu kwaajili yangu naye hanitaki.


Nilijikuta nahamia kwenye pombe, nilianza kunwa pombe kwasababu ya mawazo, nilikau nakunywa kila siku, nikawa nauza vitu vyangu taratibu ndani ya mwaka mmoja nilirudi kwa Mama yangu kukaa, sina kazi, sina nyumba na siwezi kukaa hata siku moja bila kulewa. Mama yangu aliumai sana, akawa ni mtu wakulia sana, siku moja nikiwa Bar niligombana na mtu akanisukuma kidogo nikadondoka na sikuamka tena, niliumia uti wa mgongo sehemu ileile ambayo uilikua inauma toka mwanzo.


Nikageuka na kuwa mlemavu, hapo ndiyo niliacha pombe na kuhamia kwa Mama yangu. Mama yangu ni mzee na maisha yake ni magumu kwakua ndugu zangu hawamsaidii sana, anafanya Biashara ya kuuza chakula na sasa hivi mimi ndiyo namsaidia kusukuma chapatti tunauza hapa na maisha yanaendelea. Namshukuru sana Mungu kwa kunipa Mama kama huyu ila naomba Mama usife ili uendelee kunihudumia kwani sijui maisha yangu bila wewe uatakuaje? Naishi kwa kubangaiza wanangu hawaruhusiwi hata kuja kuniona na ndugu zangu wamenitenga.


NB; Kama mnakumbuka kuna kipindi nilisimamisha hii stori, nikwakua Mama yake alifariki katika kipindi hicho. Msiba wa Mama yake ulimkutanisha na baadhai ya marafiki zake ambao walimsiadia kupata kazi. Sasa hivi anafanya kazi, bado ni mlemavu hawezi kusimama lakini angalau anakitu cha kumuigizia pesa ya kula na ulemavu wake anaumudu kwani mikono inafanya kazi.


MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG