IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO
Kuna wale madada wa kazi (mkiniita House Girl inakua na ladha zaidi kwani ni kizungu) ambao tuna hamahama, sina uhakika kwanini mnatuhamisha sana lakini mnatufanya tunakua kama Kiraka, kuziba pale ambapo kuna tundu. Basi mimi naweza kusema nilikua binti wa kazi Kiraka. Nilianza kufanya kazi kwa Mama mwenyewe, sijui hapa tumuite Bibi, lakini mtoto wake alipojifungua na kukosa binti wa kazi nilipelekwa huko.
Nilikaa mpaka alipopata mfanyakazi nikarudi kwa Mama lakini nako huko sikukaa, Binti mwingine alikua anasafiri kwenda ukweni, kwakua alitaka kumuacha binti yake wa kazi na watoto wengine na alikua na mtoto mdogo basi niliambiwa niende naye kijijini, huko ukweni. Nilikua nahamahama kila mara, hakukua na posho yoyote wala kuongezewa mshahara lakini sikua na namna, niliazimika kuvumilia kila kitu.
Mwisho nilipata makazi ya kudumu, Mama alikua anaumwa hivyo alitakiwa kuishi na mtu, waliamua aishi kwa mtoto wake wa kiume mkubwa. Hii stori inamhusu, hapa nilifurahi kwakua yeye ndiyo ‘Big Boss’ hela kwake zipo, nyumba nzuri, hakuna mambo ya magengeni magengeni ni mambo ya shopping na kama mnavyojua kwa matajiri kunakua na wasaidizi wengi wengi, kulikua na wakata fensi, wasafishaji uwanja ambao huja mara kwa mara na kufua ilikua ni mashine.
Binti wa kazi niliyechukua nafasi yake aliondoka kwa kuolewa, Mama huyo ndiyo Bosi wangu mpya alimlea kama mwanae hivyo send off, yenyewe ilishinda harusi ya huko kwa bwana harusi. Baada ya kufika pale nilikua naomba sana nibaki pale milele na milele. Nilikua naomba huyu Bibi asife lakini basi asipone na kurudi kwake. Najua mnaweza kudhani ni mbea natoa siri za ndani lakini hakuna kiapo cha ma house girl hivyo hamuwezi kunishitaki.
Sisemi kwasababu ni mbea ila nasema kwakua inaweza kukutokea hata wewe. Nakumbuka siku ya kwanza kuijua vizuri hii familia ilikua ni siku ya Jumanne. Mama na Baba, hawa ni mabosi wangu nitakua nawaita hivyo walikua kazini, pale nyumbani alikua Bibi, Shangazi wawili, na Baba mdogo mmoja. Si ndugu zangu lakini ni waite hivyo, nilikua nafanya usafi na wao wanaongea.
“Mama inabidi tubadili mbinu, huyu mwanamke ana akili. Kaka akimuacha au akifa sisi hatupati chochote! Wakigawana hapa wanagawa mali nusu kwa nusu!” Baba mdogo ambaye ndiyo msomi msomi aliongea.
“Na akifa!” Nilishtuka, ni Shangazi mkubwa alikua anaulizia.
“Kaka akifa ndiyo hatuambulii chochote, kama hajaacha wosia mali zote zinaenda kwa wanae na msimamizi ni huyu mwanamke! Huyu sijui ni mwanasheria au nani lakini aliwaelekeza Dada zake na wao walikua wanatingisha vichwa, walikua wakipanga mikakati ya namna ya kuishi na mke wa Kaka yao.
Niliwaangalia na kushindwa kuwaelewa, wote walikua na maisha mazuri, Kaka yao pamoja na kuwa na pesa zaidi lakini alikua ni mtu wa watu, mnyenyekevu na alikua akiwajali. Ni mara nyingi sana nilishuhudia akiwapa pesa nyingi tu kila wakimuomba. Kama mfanyakazi wa ndani sikua na chakufanya zaidi ya kuangalia tu, kwanza na mimi nilikua na matatizo yangu, ndiyo ilikua mara yangu ya kwanza kufanya kazi kwenye ile nyumba hivyo sikutaka kuharibu kabisa.
Shangazi walikua wanakuja pale mara kwa mara kumuangalia Mama yao, kila walipokuja ndiyo waligeuka kama mabosi wa ile nyumba.
“Unafanya nini?” Siku moja, Shangazi mkubwa Mama Abdul (si jina lake halisi) aliniuliza. Yeye alikua akiishi mtaa wapili tu kutoka pale hivyo mara nyingi kwakua alikua akifanya biashara alikuja pale nyumbani kumsalimia Mama yake.
“Namuandalia Mama chakula, hajisikii vizuri ameniambia nimpelekee chakula chumbani.” Nilimuambia, nilikua kwenye meza nikipakua chakula. Mama alikua ametoka kazini mapema, kichwa kilikua kinamuuma na alikua kalala ndani.
Wakati wa chakula ulipofika nilienda kumuit aakaniambia nimpakulie kidogo tu na kumpelekea chumbani kwani hajisikii vizuri. Ilikua ni mchana na kwakua mara nyingi hakuna watu wengi nyumbani chakula kikiwekwa mezani kila mmoja hujipakulia mwenyewe na kulia sehemu ambayo anaona inafaa.
“Hivi wewe hapa Bosi wakoni nani?” Aliniuliza huku akininyang’anya sahani, alikirudishia chakula kwenye hotpot na kulifunika. Nilinyamaza kwani nilishindwa kujibu, niliajiriwa kweli na Bibi lakini sasa nilikua katika ile nyumba niliamini mimi ni mfanyakazi wa wote.
“Mbona hunijibu nani kakuajiri?” Aliuliza tena baada ya kuniona nimeduwaa tu pale.
“Ni Bibi, yeye ndiyo aliniajiri.”
“Hapa umekuja kwa sababau gani?” Aliuliza tena.
“Bibi anaumwa hivyo nimekuja kumuuguza hapa.”
“Sasa huyo unayemtengea chakula na kumpelekea huko chumbani ni Bibi yako au ni nani?” Aliuliza kwa hasira zaidi, alionekana kukasirika kama vile ni kitu kikubwa. Nilimuambia nimeshamtengea chakula Bibi anakula.
“Acha kujibu ujinga! Tunakulipa ili umhudumie Mama yetu, na si vikaragosi vingine! Kama kazi imekushinda sema! Mama anakula wewe uko mezani huku unahangaika na watu wazima! Hivi huyo mpumbavu anashindwa nini kuja na kuchota chakula chake hapa! Ondoka nenda kamuangalie Mama yangu, hivi unataka hata kama chumvi haijakolea aanze kupiga kelele kuita!”
Aliongea kwa hasira hukua kinisukuma kuniondoa pale, nilitaka kwenda chumbani kumuambia Mama ili aje achote chakula chake mwenyewe lakini alinivuta na kutaka hata kunipiga, sikujua hasira zake zimetoka wapi kwani wote tulikua na amani na dakika kama kumi nyuma wakati anaingia tulikua tunaongea na kucheka. Pamoja na kwamba mimi ni Dada wa kazi tu lakini walinichukulia kama mtoto wao, walikua wakinipenda kwakua niliwasidia kulea watoto wao na watoto walikua wananipenda.
Niliondoka na kutoka nnje, Bibi alikua kakaa nnje kwenye kochi lake akila.
“Una nini?” Aliniuliza baada ya kuniona siko sawa.
“Hakuna kitu niko sawa.” Nilidanganya, sikutaka kumuingiza kwenye maugomvi ambayo kwangu hayakua na maana. Nilikaa huku nikiwa na wasiwasi, nilijua kabisa Mama ataniona kama vile nimemdharau kwa kushindwa kumpelekea chakula. Nilijikuta nashindwa kufanya chochote nikiwaza, ndiyo kwanza nilikua nimeingia kwenye ile nyumba na nilikua natafuta kua mfanyakazi wa kudumu sasa naanza kwa kukata kumfanyia bosi wangu kitu kidogo kama kile.
***
Siku ile ilipita, Mama hakutoka ndani hivyo mchana hakula kabisa, roho ilinaniuma sana, nilitamani kumuambia kilichotokea lakini nilihisi labda hawezi kuniamini, lakini pia nilihofia kumgombanisha na wakwe zake. Ingawa hakulizungumzia hilo swala lakini nilijua kabisa kakwazika kwani hakunichangamkia tena kama awali. Nilijisikia vibaya sana na kuna wakati nilijiona kama vile nimefukuzwa kazi tayari.
Kesho yake ilikua ni siku ya Jumamosi, Baba hua anaenda kazini lakini Mama anabaki nyumbani, wana watoto wanne, wawili wakike na wawili wakiume. Jumamosi nao huwa nyumbani, Shangazi nao walikuja asubuhi kabisa. Mama Abdul ndiyo alianza kuja kisha alifuatiwa na Mama Aziza, mimi nilikua nafua na Mama alikua jikoni akiandaa chakula cha mchana, watoto walikua wakicheza huko nnje.
Walifika na kuingia chumbani kwa Mama yao, walikaa huko mpaka ulipofika wakati wa chakula cha mchana. Mama alikitenga chakula mezani na kuwakaribisha, walikuja wote na kukaa mezani, mara nyingi siku za Jumamosi kwakua watu wengi wanakua nyumbani tunakaa mezani na kula pamoja. Walikuja na kukaa ili kula, kabla ya kuanza kula, alikuja mdogo wao wa kiume, Karim (sio jina lake halisi), aliwasalimia kwa mbwembwe na Mama alimkaribisha chakula.
Kwa uchangamfu alichukua sahani na kutaka kupakua chakula lakini dada yake alimzuia.
“Usiwe unakula kula tu vitu vya watu!” Mama Aziza (Sio jina lake halisi) alimuambia huku akimnyang’anya kijiko cha kuchotea na kumpa Mama.
“Wifi shika uchote chakula kwanza.” Aliogea kwa kebehi huku akijichekesha chekesha. Mama yeye hakujali, ni kama alielewa alichokua anakifanya. Alichukua kile kijiko na kujichotea chakula, akaonja kidogo ksihaa kawaambia.
“Karibuni.”
Waliangaliana na bila aibu Mama Abdul alimuambia.
“Sasa unaweza kula, ukifika kwa watu sio unajiliajilia tu, hujui nani kapika, kama kuna sumu vipi, unataka utufie tukupoteze mdogo wetu. Kaka yako tushampopteza unataka tukupoteze na wewe? Tunakupenda mdogo wetu, kafamilia kenyewe kadogo haka…”
Aliongea kama vile utani lakini alikua anamaanisha, nilijisikia vibaya kwani kile chakula alikipika Mama na alikua akiongea mbele ya watoto wake, tena watoto wakubwa kuweza kutambua nini kilikua kinaendelea. Nilimuangalia Mohamed-Mod(si jina lake halisi) mtoto mkubwa ambaye alikua darasa la tano akiwaangalia Shangazi zake kwa hasira. Mama alijifanya kucheka, hakutaka wanae kuona kama ni kitu kikubwa sana lakini Mod alikasirika.
Walikua wameitawala ile nyumba, wakati wa kula walikua wakiongea na kucheka, hawakujali kama mezani kulikua na watu wengine. Watoto walimaliza kula na walipotaka kuondoka shangazi waliaambia wakae ili kusubiri wao wamalize.
“Hivi unajua wifi unatuharibia watoto? Mama Abdul alianza.
“Mitoto haina adabu kabisa sijui hata unaifundisha nini, yaani hata kuwaambia tu kua hawatakiwi kunyanyuka na kutoka mezani wakiwaacha watu wazima wanakula umeshindwa? “
Aliongea kwa dharau na kejeli, nilishangaa kwani hakukua na kitu cha ajabu chochote. Kilichonishangaza zaidi nikuwa Mama alinyamaza, hakumjibu chochote zaidi ya kuwaambia wanae.
“Rudini mkae hamuoni wakubwa wanakula.” Watoto walirudi na kukaa, chakula kiliendelea wao wakiongea na kucheka, ilikua ni kama hakuna kitu kilichotokea na kwa namna walivyokua wakicheka ni kama ile nyumba ilikua yao, kuna wakati nilidhani labda wao ndiyo wamiliki wa kila kitu kwani walikua wakimuendesha Mama kama mtoto mdogo vile.
Baaada ya chakula nilinyanyuka ili kuondoa vyombo lakini Shangazi alinizuia.
“Wewe hivi hujui kazi zako, wewe ni mfanyakazi wa Mama, hembu acha kufanya kazi za hawa mbuzi. Wewe kwani huwezi kunyanyuka na kuosha vyombo!” Mama Abdul aliongea kwa hasira, alikua kakaa pembeni ya Aziza, ambaye alikua mdogo kwa ile familia, alikua na miaka minne alimshika sikio na kumfinya huku akimnyanyua juu kwa kumvuta.
“Muache mwangau, huwezi kumpiga mwanangu mbele yangu wakati hajafanya chochote kibaya!” Hapo Mama alinyanyuka na kuingilia kati, alionekana kukasirishwa, walinyamaza bila kusemja kitu. Mama lianza kuondoa vyombo mimi nikiwa nimekaa, kwakweli nilijisikia vibaya.
Nilishafanya kazi sehemu zote na pale ndipo nilikua napataka, ndiyo sehemu pekee nilijua naweza kutengeneza maisha sasa anataka kunigombanisha na Bosi wangu. Nilitaka kunyanyuka na kusaidia kuosha vyombo lakini nilikumbuka kua pamoja na kuwa wale ndiyo wana pesa lakini aliyekua kanileta pale ni Bibi na wao wana nguvu kubwa sana kwake.
“Watoto wake, alikuja na watoto hapa! Yaani Kaka amepata hasara, mtu anaharibu watoto kiasi hiki!” Walianza kuongea, walijadili tabia mbaya za watoto tena wote wakiwa pale, hawakujali kama wanamvunjia heshima Mama, waliongea bila kujali.
Mimi sikutaka kuendelea kukaa pale kwani nilikua naona aibu, nilitoka nnje kwenda kufanya shughuli zangu, nilikua nafua nguo za Bibi, baada ya mdua ano walitoka na kujikalisha huku wakiagiza vitu kama kwao. Tukiwa pale Baba alikuja, walijifanya kuchangamka, alishuka kwenye gari, watoto wake walimkimbilia kumsalimia kwa kumkumbatia. Aliwapa zawadi kama kawaida yake, wakatia nawapa zawazi Mama Abdul naya alichukua pochi yake na kutopa Biscuit kisha kuwaita.
“Shangazi zangu njooni, nilikuja na zawadi zenu na kusahau kuwapa, njooni mchukue.” Aliongea hukua kijichekesha, alipanua mikono kama vile anataka kuwakumbatia walisita kwenda mpaka Baba yao alipowaambia.
“Mnaona Shangazi zenu wanavyowapenda? Nendeni mkapokee zawadi sema msisahau kupiga mswaki mkimaliza!” Aliongea hukua kwiaacha waende, watoto walienda kwa shingo upande na kumkumbatia huku wamenuna, yeye alikua akijichekesha chekesha na kuwasifia sifia.
Kwa namna walivyokua wakijichekesha kwa Kaka yao ungedhani kua ni familia inayopendana, walikua wakiwabeba watoto wake na kuwadekeza kama Malaika. Mama Aziza alienda mezani na kumtengea Kaka yake chakula, ni kitu ambacho kilinishangaza kwani mke wake alikuepo lakini alijifanya kimbelembele.
“Wifi wewe pumzika, najua umechoka, ngoja sisi leo tupo tukusaidie, kazi za humu ndani zinachosha na Mama yupo hapa ndiyo tenaa hata hupumziki…” Alijisemesha wakati anampakulia Kaka yake chakula.
Nilimuangalia bila kummaliza, baada ya chakula Karim alikuja, yeye muda wote alikua chumbani kwa Bibi. Bibi alikua mgonjwa hivyo mara nyingi pamoja na kua hakuzidiwa sana lakini alikua akipenda kukaa ndani hasa watoto wake wakiwepo. Sijui walikua wanaongea nini lakini wangeweza kukaa huko kwa hata masaa matano bila kutoka, hata kama ni usiku, ni kama walikua wakijitenga flani.
“Mama anakuita…” Alimuambia Kaka yake baada ya kumsalimia, Baba alishamaliza kula hivyo alinyanyuka kwenda kumsikiliza Mama yake. Kiumbea tu nilinyanyuka na mimi kwenda chumbani kwa Bibi, niliingia katika choo cha ndani na kujifanya nafanya usafi.
“Dada yako ana shida lakinia anogopa kukuambia.” Baada ya kusalimiana Bibi alianza kuongea.
“Yupi tena, shida gani?” Baba aliuliza.
“Mama Abdul, kumbe mume wake alichukua mkopo na nyumba inataka kuuzwa, sasa ile nyumba ikiuzwa wajomba zako unafikiri wataishi wapi. Amehanagika na kupambana lakini hana kitu, wenzako wamemchangia changia lakini hamna. Najua hatafurahi kwamba nimekuambia,a anajisikia vibaya kuona kama ulimsaidia kujenga lakini mwanaume kamuangusha…”
Bibi alinza kulalamika, alikua akiongea kana kwamba hakutumwa.
“Nilishamuambia kuachana na yule mwanaume hataki, sijui anampendea nini mwanaume hana kazi ya kueleweka, hahudumii familia, hivi unajua hata kusomesha watoto ni Dada yako ahangaike, kabiashara kenyewe unakaona! Nashindwa kuelewa wanangu, sijui nikifa itakuaje, nina waiswasi sana, yaani napata presha, wajukuu zangu wataishi wapi?” Aliendelea kulalamika, Baba alikua kimya akimsikiliza, nilitamani kutoka mule ndani kuona uso wake.
“Anahitaji Shilingi ngapi?” Baba alimuuliza.
“Hata sijui, labda umuite mwenyewe aje akuambie, mimi haya mambo siyaelewi kabisa, hakutaka nikuambie lakini nyie wote ni watoto wangu unafikiri nisipowaangalia nani atawaangalia. Mary! Maryyy!” Bibi aliniita, nilitoka kule chooni akaniambia nimuite Shangazi. Nilienda na kumuita, alipokuja Bibi alimuambia ataje ni kiasi gania anadaiwa. Alijifanya kukataa na kumuambia Mama yake kua atapambana mwenyewe, alikataa katakata kutaja.
“Unataka wajukuu zangu walale nnje, hivi kwanini wewe unakua hivyo, huyu ni Kaka yako anaweza kukusaidia! Hivi lakini kwanini mnanifanyia hivi? Kama niko hai hamuwezi kusaidiana, huwezi kumuambia Kaka yako kitu nikifa si ndiyo mtakau hamuongei kabisa?” Bibi aliongea kwa hisia, alikua analia kabisa, Baba alimbembeleza na shangazi alijifanya kumuelewa.
“Alichukua mkopo wa milioni thelathini na marejesho anatakiwa milioni moja na laki mbili kwa mwezi ila mpaka sasa hajarudisha kitu huu ni mwezi wa pili wanataka kuuza nyumba, nimechanganyikiwa Kaka, wewe si unajua kale kanyumba nilivyokajenga kwa shida.”
“Kwahiyo unatakiwa kama Shilingi ngapi?”
“Milioni mbili, nimejikusanya kusanya pale dukani nimepata laki nne, hizo nyingine ndiyo najaribu kukopa kopa kwa watu, Karim nayeye biashara haziendi na Mama Aziza naye unajua anasomesha ndiyo katoka kujifungua hana kitu kabisa. Sikutaka kukuambia kwakua umenisaidia sana mpaka naona aibu.”
Baba alinyamaza kimya, aliwaza sana, nilikua nimekaa kitandani namuangalia tu, mara nyingi washanizoea na wananiona kama mtoto wao hivyo hawajali kama nasikiliza mambo yao au la.
“Sasa hivi hali ni ngumu kidogo, ila ngoja niongee na Mama Mod, kuna kamkopo alichukua kazini ili tumalizie ile nyumba yetu nadhani tunaweza kukusaidia.” Aliongea kwa uchungu, alionyesha dhahiri kuguswa na matatizo ya Dada yake.
“Mhhhh! Mhhh!” Bibi aliguna.
“Nini?” Baba alimuuliza.
“Ushamtaja huyo mke wako unafikiri kuna kitakachopatikana tena, kwanini usiwe na maamuzi yako mpaka umshirikishe mke wako, wewe ndiyo mwanaume!” Bibi aliongea kwa hasira, Baba alijaribu kumuelewesha kua wao ni familia nna wanapaswa kufanya mambo kwa pamoja lakini hakumuelewa.
“Yeye akisaidia ndugu zake hua anakushirikisha?” Bibi alimuuliza, wakati huo Shangazi yeye alinyamaza kimya.
“Tunashirikishana kwa kila kitu Mama.” Baba alijibu kistaarabu, hakutaka kumkosea adabu Mama yake.
“Haya! Ila mwanangu katafute tu namna nyingine, yule mwanamke akaimbiwa basi hakuna kitakachopatikana, mimi namfahamu, mtu ambaye anaweza kukunyimia chakula unafikiri anaweza kukupa pesa yote hiyo!” Bibi alijiongelesha.
“Kukunyimia chakula? Kivipi? Mbona mke wangu hana tabia hizo?” Baba aliwaka kidogo, alishangaa hata mimi mwenyewe nilishangaa.
“Mama nyamaza, si kila kitu lazima useme, utaharibu ndoa za watu, inawezekana ndiyo utaratibu wao!” Mama Abdul alijiongelesha.
“Utaratibu gani? Mbona siwaelewi, kwani kuna nini, mke wangu kafanya nini tena?” Baba aliuliza, Mama Abdul alijifanya kujizuia kusema. Sijui walipanga saa ngapi lakini kwa namna walivyokua wanaongea mtu yeyote angeweza kuwaamini.
“Mke wako hatutaki hapa, hivi unajua anakasirika tunavyokuja, chakula unajua ni chakupima, yaani anamuambia huyu binti wa kazi kupima chakula cha watu wachache kwakua wageni wamekua wengi. Sisi ndiyo wa kunyanyasiwa chakula, hivi hajui hawa wanakuja kwakua mimi niko hapa? Unafikiri kwa roho yake wasingekua wanakuja kumuona Mama yao wangekuja kukusalimia?”
Bibi aliongea hukua kijiliza, nilishtuka kua na mimi nimetajwa katika hiyo mada wakati nilikua sihusiki, sijawahi kuambiwa kupima chakula na hata Mama akipika mwenyewe hupika chakula kingi cha kubaki.
“Muulize huyo binti maelezo aliyopewa!” Shangazi alidakia hukua kiniangalia, alinikonyeza kama vile ananiambia nikubaliane na ninachoambiwa.
“Umepewa maelezo gani?” Baba aliniuliza, nilibaki mdomo wazi, nilitamani kukataa lakini nilijua nikikataa nitawaumbua wao na wale ni ndugu, watasemeheana lakini mimi nitafukuzwa kazi. Niliwaza kukubaliana nao lakini nilijihisi dhambi kwani hakukua na kitu kama kile.
“Muache binti wa watu, unataka akujibu nini wakati yeye hapa kaajiriwa? Mimi ni Mama yako nimekuambia kwakua mimi ndiyo niemsababisha yote haya, nisingekua naumwa nikaja kwako yasingetokea yote haya, lakini nitafanya nini, hawa dada zako wananiambia niende kwao kila siku lakini hawa ni watoto wakike, wameolewa wana miji yao, sasa unafikiri nikienda huko….” Bibi aliongea, Baba alimkatisha kwa hasira.
“Hakuna wa kukuondoa hapa, wewe ni Mama yangu, kama mtu hakutaki ataondoka yeye na si wewe! Dada yangu hiyo hela utapata, mimi ndiyo mwanaume humu ndani na nyinyi ni ndugu zangu, mtakuja hapa na mtakula mnachotaka, hata kama mkitaka kulala kila siku laleni!” Aliongea kwa hasira na kuondoka, nilijua lazima anaenda kugombana na Mama.
Alipotoka na mimi nilitaka kutoka lakini Shangazi alinizuia.
“Ndiyo nini kunyamaza vile unapoulizwa maswali? Ulitaka kutuumbua?” Alinishika kwa hasira.
“Sasa Anti ulitaka mimi nijibu nini wakati mmenishtukiza, kitu kama kile mlitakiwa kuniambia mapema.” Nilijitetea, sikutaka kuwaambia kua nilikua sipendi tabia zao.
“Uwe na akili wewe! Ndiyo maana utakufa masikini, kichwa chako kinatakiwa kufanya kazi harakaharaka, mambo kama yale unatuunga mkono. Kwanza hembu tuambie wewe uko upande gani?” Aliniuliza swali, ingawa nilimualewa lakini nilizuga.
“Upandwa gani kivipi?” Nilijifanya kuuliza, nilimuona dhahiri kakasirika.
“Tatizo lako ndiyo hilo, unafanya kazi lakini akili ya kufikiria huna, huna kabisaa! Hujui hata ni upande gani? Nakuuliza upo kwetu au kwa yule Mbuzi unayemuita Mama!?”
Sikua na namna zaidi ya kumkubalia na kumuambia kua niko upande wao, aliniambia niwe makini kwani wao ndiyo wameniajiri, nisijisikie nimefika kwakua tu niko pale.
“Hapa uko kwa hisani ya Mama, hivyo Mama ndiyo wa kumhudumia, hao wengine si mabosi wako.” Alinisisitizia, nilimuambia namuelewa, sikutaka ubishi naye kwani nilijua siwezi shinda. Isitoshe kwangu muhimu ilikua ni kazi ndiyo kilikua kimenipeleka pale, mambo mengine ya familia yao yalikua hayanihusu.
***
“Mume wangu unajua bado tunaishi nyumba ya kupanga?” Tulikua kwenye gari, mimi na Mama tulikua tumetoka Site, kuna nyumba waliyokua wanajenga na ndiyo sehemu walitaka kuhamia, Baba alitupitia wakati anatoka kazini.
“Najua si ndiyo maana tunajenga.” Baba alijibu kwa kifupi.
“Lakini ujenzi ni kama umesimama, kila siku unasema huna pesa, nimechoka maisha ya kuishi kwenye nyumba za watu!”
“Kwani unalipa kodi wewe, si nyumba tunalipiwa kila kitu na kampuni, sasa wewe tatizo lako nini? Kuna siku hata moja umeambiwa kulipia kitu?”
“Hapana lakini jua hizi ni kazi tu, hivi leo na kesho unasimamishwa kazi si tunafukuzwa na kwenda kuishi mitaani. Ndugu zako wote wana nyumba, Karim hata kazi ya maana hana lakini kashajenga, sisi bado tu tunaishi nyumba ya kupanga!”
Mama ni kama alimchokoza, mjadala uliabdilika kutoka kujenga mpaka kuwa unawahcukia ndugu zangu.
“Kwahiyo ndugu zangu kuwa na maendeleo inakuuma sana, hivi una nini na ndugu zangu? Mbona huwezi kuwapenda kama wanavyokupenda, wanajitahidi kujionyesha kuwa wanakupenda lakini wewe wapi?” Baba aliongea kwa hasira.
“Sio hivyo mume wangu lakini wewe unawaamini sana wale. Juzi umechukua pesa niliyokopa kwaajili ya ujenzi umempa Dada yako, unafikiri mimi najisikiaje nahangaika nakatwa mshahara mimi pesa unaenda kugawa.”
“Kwahiyo ulitaka ndugu yangu kufukuzwa na kuuziwa nyumba yeka kwakua wewe bado hujajenga?”
“Sio hivyo, tatizo wewe unawamaini sana ndugu zako, wakikuambia kitu unafanya tu bila hata kuchunguza, hivi unajua kua Dada yako hata kukopa hajakopa achilia mbali kutaka kuuziwa nyumba na kwa taraifa yako kuna nyumba nyingine anajenga Kimara.”
Mama aliongea lakini Baba hakuonekana kumsikia, kila wakati alikua akisema kua hawapendi ndugu zake na anawaonea wivu. Alikasirika mpaka ikafikia hatua hawaongei kabisa. Kila mtu alimkasirikia mwenzake, mimi nilibaki kimya tu, nilitamani kunyanyua mdomo wangu kumuambia Baba kua ni kweli anaibiwa lakini niliona si nafasi yangu kufanya vile nilinyamaza na kuwaacha waendelee na maisha yao.
Nakumbuka ilikua ni siku ya ijumaa jioni, tulirudi nyumbani na kumkuta Mama Aziza, alikua amekuja na mume wake, walisalimiana na kuingia ndani.
“Tumekuja kuwachukua watoto, nilikuambia kesho ni Birthday ya Aziza, ningependa ndugu zake waje wakalale kesho kwakua si shule watarudi kesho kutwa.” Aliongea hukua kijichekesha, si kwamba alikua anaomba ruhusa bali alikua anatoa taarifa kwani tulikuta watoto washaandaliwa.
“Wifi kwani kuna tatizo nikiwachukua, au hutaki waende kulala kwangu?” Aliuliza kinafiki, Mama alimuangalia na kumsoma.
“Kwanini nisitake, si kwa Shangazi yao kuna kibaya gani kitaokea kwa Shangazi yao?” Alimjibu vilevile alivyouliza, watoto waliambiwa kuingia kwenye gari ili kuondoka.
“Kaka mafuta yameniishia kidogo, na Anko wako keki bado hatuja nunua.” Bila aibu aliongea, alikua anaomba pesa, hakuona aibu, alikua na mume wake lakini wala hakujali, Baba aliingia ndani na kutoka na noti kadhaa za Shilingi elfu kumi kumi na kumkabishi, alishukuru, nilitaka kuingia ndani lakini alinizuia.
“Unaenda wapi? Wewe tunaenda wote, twende tukasiadiane kazi si unajua shughuli.” Kidogo nitapike, nilikua sitakia kabisa kwenda katika ile nyumba, nilishawahi kufanya kazi kwake na nawajua watoto wake ni maudhi balaa, amewadekeza sana na wanadharau kwa mabinti wa kazi.
“Au wifi huwezi kumhudumia Mama peke yeko mpaka mfanyakazi?” Alimuuliza tena wifi yake, hapo nilitamani hata asema ndiyo, hata aseme ana kazi nyingi ili tu nisiondoke lakini haikua hivyo.
“Hamna shida, unaweza tu kuondoka naye, siwezi kushindwa kumhudumia Mama yangu.” Alitoa jibu ambalo lilinifanya nitamani kulia, niliingia ndani na kuchukua nguo kidogo nikatoka na kuingia kwenye gari kwaajili ya safari.
Hakusubirio hata tufike nyumbani, manyanyaso kwa watoto wa Kaka yake yalinzia palepale namna ya kukaa, namna ya kuongea na kila kitu, walijikuta wanakosa raha na kubaki kimya tu. Tulifika na moja kwa moja nilitakiwa kwenda jikoni, kumbe mfanyakazi wake wa ndani aliondoka jana yake, alikua kamfumania na mume wake ndiyo maana mumewe alikua kimya tu haongei chochote, walishatibuana. Nilijua kwani ile nimefika tu alianza kunitukana kana kwamba mimi ndiyo nilikua na mume wake.
“Nawajua nyie watu, sio nakukaribisha kwangu uananza kummendea mume wangu nitakuua, yule mjinga mwenzako nimemfukuza sasa nawewe ukijaribu kumuangalia tu mume wangu basi unaondoka kabisa mjini…” Alibwabwaja sana mimi nilimsikiliza tu, nilijua ni hasira za kuibiwa mume, niliingia jikoni kupika chakula cha usiku. Baada ya kupika nilipeleka mezani na kuwakaribisha.
Kwenye kula ilikua ni kimya kimya, yeye ana watoto watatu, Aziza ambaye ndiyo mkubwa alikua anatimzia miaka saba, wa pili ni Hassan miaka minne na watatu alikua mdogo Jabir ambaye alikua na mwaka mmoja. Wakati wa kulala Shangazi aliwapeleka watoto wa Kaka yake stoo. Nilishangaa kwani nyumba ilikua na vyumba vingi tu lakini ni kama alikua anataka kuwakomoa, alitandika kagodoro kadogo stoo na kuwaambia kua walale pamoja.
“Kwanini wasije kulala chumbani kwetu?” Aziza mtoto wake alimuuliza.
“Hawa si ndugu zenu, hawa ni watoto wa mjomba yenu lakini si ndugu zenu, ni watoto wa Mama yao. Unaona jinsi Mjomba wenu anavyowaletea zawadi, jinsi Mjomba wenu anavyowapenda, unajua kama asingekua na watoto si angekua anawapa zawadi nyinyi zaidi. Hamtakiwi kuwapenda mnatakiwa kuwachukia kwani mjomba wenu akifa wao ndiyo watachukua mali zake zote na nyie hamtapata kitu.”
Kusema kweli hata mimi nilishangaa, alikua anawaelezea watoto wake kama anawalezea watu wazima, aliongea tena bila kificho, watoto wa Kaka yake walikua wakisikia. Kwa watu waliokua wakisaidiwa kiasi kile alitakiwa kuwapenda sana watoto wake, alifungua stoo na kuwaambia kuingia, hawakua na namna zaidi ya kuingia, ilikua ni stoo ndogo tu, tena iliyokua imejaa vitu, vitunguu vilikua vimemwagwa chini ilili kukauka, kulikua na mkaa, vumbi jingi na makorokoro kibao.
“Shangazi si nipasafishe kwanza kabla hatujalala?” Nilimuuliza.
“Kwani na wewe unataka kulala huko stoo? Chumba chako si kipo kule, waache hao Mbuzi walale hivyo hivyo! Mama yao si ndiyo anawadekeza!” Aliongea kwa hasira, sijui hata zilitoka wapi kwani wale walikua ni watoto wa Kaka yake, kwa mtu mwingine ungedhani labda ni watoto wa mke mwenza, chuki aliyokua nayo haikuelezeka.
“Basi ngoja niwasafishie.” Nilimuambia.
“Wewe na wewe! utajipendekeza mpaka lini? Unawaonea uchungu hawa ni ndugu zako!” Aliongea kwa hasira huku akiwaukumiza wote wa nne mpaka ndani. Alifunga mlango kwa nnje na kuniamrisha niende kulala.
Nilipanda kitandani lakini usiku sikulala, ile famiilia ilinishangaza sana, sijui hata zile chuki zilitoka wapi, angalau basi kumchukia wifi yao kwakua wanaona labda atachukua mali za Kaka yao lakini mtoto wa Kaka yao, hiyo ilinishangaza zaidi. Mpaka saa nane usiku nilikua bado sijapitiwa na usingizi, nilikua nawawaza wale watoto katika kale kachumba. “Hata angalau basi angewafungulia mlango, wanapata hewa kweli?” Nilijiuliza bila majibu, nilitaka kulala lakini nilishindwa.
Sijui ni nini lakini roho yangu iliktaa. Nilijikuta nanyanyuka na kwenda kufungua mlango wa stoo. Lengo langu lilikua ni kuufungua na kuuacha wazi ili wapate hewa. Lakini nilipoufungua nilijikuta nataka kuwasha taa niliwasha na kukuta wote wamelala, nilitaka kuondoka lakini nilishindwa, walikua katika hali mbaya, nilimuangalia Aziza (mtoto mdogo wa Kaka yake) alivyokua amelala nikamuonea huruma.
Niliwaza kumchukua kwenda kulala naye ilia subuhi nimruidishe bila Shangazi yake kujua. Lakini nilipoinama na kumshika nilimuona mzito sana, mwanzo nilijua kua ni sababu ya usingizi lakini niligundua kua alikua hapumui. Mule ndani hewa ilikua nzito sana, nadhani alishindwa kupumua na kuwa kama kapoteza fahamu. Nilimtingisha na kumtingisha wapi hakunyanyuka, wale wangine walinyanyuka Mod alimshika mdogo wake na kumtingisha kama mimi hakunyanyuka, alianza kupiga kelele za kumuita lakini wapi.
Kelele za Modi zilimuamsha Shangazi na mumewe, walishangaa kuniona pale, nilimtoa sebuleni kwenye hewa lakini alikua bado hapumui.
“Kuna nini?” Shangazi aliuliza.
“Nimemkuta hivi hapumui, nimejaribu kumuamsha lakini hapumui.” Nilimjibu hukunikiendelea kumuamsha, nilimuona kapaniki na kuinama, alimuita na kujaribu kumuamsha lakini wapi.’
“Umemuua mdogo wangu! Umemuua mdogo wangu, kule ndani hewa ilikua ni nzito umetufungia kashindwa kupumia!” Mod alipiga kelele. Nilimuona kabisa Shangazi kashtuka anatetemeka kama mtoto.
“Wewe umemfanya nini mtoto wa Kaka yangu, kwanini uliwafata chumbani kwao usiku huu, wewe ndiyo umemfanyia hivi!” Alipaniki na kunigeuzia kibao.
(ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI; watoto wanaenda nyumbani kwa Shangazi yao, huko wanalazwa stoo, mtoto mdogo anakosa pumzi na kukosa fahamu baada ya Mary kumfuata chumbani, lakinia anageuziwa kibao kuonekana yeye ndiyo kamsababishia yale matatizo je nini kitatokea. ENDELEA… Kama hukusoma sehemu ya Pili bonyeza hapa; https://www.instagram.com/iddimakengo/
“Mtoeni nnje apate hewa!” Modi alipiga kelele, Mjomba alimnyanyua na kumtoa nnje, sijui alipata wapi ujasiri lakini Mod alipiga magoti na kuanza kumpulizia hewa mdogo wake mdomoni, sijui alijifunzia wapi lakini ghafla Aziza alianza kukohoa. Mod alikaa chini na kumpakata mapajani mwake, sisi wengine tulibaki tunashangaa, alikaa vile kwa dakika kama tano na Aziza alinyanyuka na kuomba maji, nilitoka na kwenda kumletea.
Baadaye alinyanyuka vizuri na kutaka kurudi ndani.
“Tumpeleke hospitali…” Mjomba aliongea akitaka kumgusa Aziza.
“Hapana tupeleke nyumbani!” Mod aliongea kwa hasira, Shangazi alijaribu kumsihi kubaki lakini alikataa. Shangazi alikua anatetmeka na kuomba msamaha, Mod aliwashika wadogo zake na kutoka nao nnje.
“Sisi tunaondoka, hata kama ni kutembea kwa miguu tutatembea tu!” Aliongea kwa hasira na hapo ndiyo Shangazi alijua kua amanaanisha. Aliwaambia wasubiri atawapeleka, alianza kutafuta ufunguo wa gari na kuupata. Alimuambia mumewe waongozane kuwarudisha watoto nyumbani.
Mumewe aliingia na kuendesha gari, kwakua nilikuja kwaajili yao na mimi niliingia ili kurudi nyumbani. Pamoja na kuumizwa na kila kitendo lakini kwa namna falani nilifurahia kidogo, nilijua kua Baba atajua ukweli kuhusu ndugu zake kama akisikia kitu kilichomkuta mwanae. Lakini wakati nikiwaza nilimsikia Shangazi akiongea kwenye simu.
“Mke wako sijui kawaambia nini hawa watoto, wamakataa kabisa kulala kwangu…” Alikua akiongea kwa kulalamika, kila mtua alishangaa, hata mume wake mwenyewe alishangaa.
“Mod ndiyo anatukana kabisa anasema hawezi kulala kwenye kinyumba kama changu, eti sisi tunalala stoo! Kaka hata kama ni dharau lakini zimezidi tena na watoto wadogo, wamegoma kabisa kulala nimesema nikuletee wanao!”
Aliongea hukua kitoa machozi, nilishindwa kumuelewa, Mod alikasirika na kuanza kutukana, alishagezuziwa kibao. Tulifika nyumbani na kukuta Baba anatusubiri, kabla hata ya kuuliza kilichotokea alimshika Mod na kuanza kumchapa. Alimchapa sana mpaka Shangazi mwenyewea akaingilia kati.
“Pumbavu mkubwa, hivi hujui kama nikifa leo hawa ndiyo ndugu zako, hujui hawa ndiyo utaishia nao! Hizi mali zinakudanganya, unajiona ushakua wewe!” Baba aliongea sana, hakumpa ruhusa ya kujitetea, alimuambia hawezi kuingia ndani kwake na atarudi kwa Shangazi yake.
“Kama huwezi kuishi na Shangazi yako nikiwa hai unafikiri nikifa itakuaje! Hawa ni ndugu zako! Acha kumsikiliza Mama yako!” Nilitamani kuongea na kusema ukweli lakini kwa namna Baba alivyokua amekasirika nilijua kua haitasiadia kitu, asingeweza kuniamini kwani Shangazi alishaamjaza maneno. Mama alikua akiangalia tu, muda mwingi alimsihi Baba ampe mtoto nafsi ya kuongea lakini anye aliishia kutukanwa.
“Najua huwapendi ndugu zangu lakini hawa ni wanangu, kama nikifa hapa hawa ndiyo watawasimamia, lini ndugu yako alikuja hapa hata kusalimia!” Aliongea sana na mwisho wa siku alimchukua Mod na kumuingiza kwenye gari, alimuambia anarudi kwa Shangazi yake na atakaa huko mwezi mzima.
“Kama ni kufa kwa kuishi kwenye kanyumba kadogo ufe lakini sitaki kabisa dharau zako! Na nikisikia umeleta tena dharau utabaki huko huko usikanyage kwangu!” Alituamuru wengine kuingia ndani, niliingia huku nikitetemeka, ilikua ni mara yangu ya kwanza kumuona Baba katika akiwa nmana ile, mara nyingi ni mtu mpole ambaye hawezi hata kumuadhibu mtoto.
Asubuhi yake niliamka na kuendelea na shuguli zangu kama kawaida, Baba alienda kazini hivyo nilibaki mimi na Mama, tulikua jikoni na Mama aliniuliza.
“Nini kilitokea jana? Ni kweli Mod kamtukana Shangazi yake?” Ni swalia ambalo sikulitegemea, lakini kwa namna ambavyo Mama aliuliza nilishidwa hata cha kumjibu.
“Mama, haya mambo sijui hata nisemeje, naogopa kibarua changu, wale ndiyo wameniajiri.” Nilijibu kwa upole.
“Kwahiyo hakumtukana, ni nini kilitokea?” Aliniuliza tena, kwa jibu langu alijua kua Mod hakutukana, nilitamani kumuambia lakini niliogopa lakini pia nilikua na hofu kua Mod akiendelea kukaa kule watamfanyia kitu kibaya.
“Siwezi sema Mama, hayo ni mambo ya kifamilia ila baadaye tukienda kwenye Birthday muulize Mod vizuri atakuambia ukweli. Lakini mama usikubali mwanao kukaa kwenye ile nyumba, usikubali kabisa watamuua!”
Niliongea kwa kifupi, kwa bahati nzuri alinielewa, lakini nikiwa pale simu yangu iliita. Alikua ni Mama Aziza, ni kama alijua kua nataka kutoa siri zake, alianza kwa kunichimba biti kua nisiongee chochote kama bado naitaka kazi yangu. Ili kumjibu ilinibidi kunyanyuka na kutoka nnje. Nilimhakikishai kua siwezi kuongea, aliniuliza kama Mama kaniuliza kitu nikamuambia hapana.
“Shangazi mkubwa aliniambia nisiwe naongea naye, mimi sitaki kupoteza kazi yangu siwezi kuongea naye.” Nilimdanganya, alifurahia na kuniambia nimsaidie kuchunguza kama watoto wameongea kitu, aliniambia ataninunulia gauni jipya nilimshukuru na kumuambia kua sitaongea chochote.
***
Baada ya ile shughuli Mama alimchukua Mod, waligombana sana na Baba lakini alishikilia msimamo wake, maisha yaliendelea Bibi bado aliendelea kubaki pale na kila siku walikuepo nyumbani ni kama walikua hawana kwao. Siku moja Mama na Baba walikua wanazozana, mimi nilikua nafanya usafi nnje ilikua kwa mbali kidogo lakini dirisha lao lilikua wazi hivyo nilikua nawaisikia.
“Ile ni biashara yangu hawezi kwenda tu na kuchukua pesa bila mimi kujua, wewe mwenyewe mume wangu huwezi kuchukua!” Mama alikua akilalamika.
“Kwani ni Shilingi ngapi? Sema nikulipie, kwanini kuwanyanyasa ndugu zangu na vihela vidogo namna hiyo!”
“Hivi mume wangu huoni? Tatizo si pesa wala nini, tatizo nikua ndugu zako wanakuchora tu, hivi huoni mambo wanayofanya, kila siku wanalia shida lakini wanafanya mambo yao ya maendeleo na kibaya zaidi wanamtumia Mama kukuumiza!”
“Kwahiyo hutaki ndugu zangu wafanikiwe?” Baba alimjibu kwa hasira, alionekana kukerwa na namna ambavyo Mama anawazungumzia ndugu zake.
“Hilo si tatizo ila shida nikuwa wao wanafanya mambo ya maendeleo lakini kila siku awanalia shida, hivi unajua hata watoto wetu hawawapendi? Hivi ushakaa kuwasikiliza wanao mambo wanayofanyiwa?”
“Hakuna kitu, wewe ndiyo unawajaza watoto maneno, nani hakujui kua unataka wawe na chuki kama zako lakini hilo haliwezi kutokea!”
Ulitawala ukimya kidogo, Mlango ulifunguliwa na ilionekana mtu kutoka, lakini baada ya sekunde kadhaa ulifunguliwa tena.
“Mimi nishakuambia, ndugu zako wanakufanyia hila, najua mimi hawanipendi na sijali lakini hili la kuninyanyasia wanangu siwezi kulikubali.” Mama aliongea na mlango ulifunguliwa tena na kufungwa. Nilirudi kuendelea na usafi wangu, kichwani nilikua nawaza ni kwa namna gani Baba alikua haoni mambo yote yanayotokea.
Nilimaliza usafi na kurudi ndani, mara nyingi huwa napenda kukaa chumbani kwa Bibi, mbali nakua ndiyo kazi yangu lakini pia Bibi ni mcheshi, hua ananipenda sana na mara nyingi kwakua tunakua pamoja basi huniambia mambo yake mengi. Kuna nguo zake nilifua jana yake hivyo nilikua nazikunja na kuziweka kwenye kabati.
“Mjomba wako amekuja?” Aliniuliza.
“Baba Mod?” Nilimuuliza.
“Hapana, Karim.”
“Sijamuona, tangu jana alipoondoka sijamuona, kwani alisema atakuja?”
“Ndiyo kuna hayo makaratasi hapo nilitaka ayachukue, yule ndiyo mwenye akili, huyu mkubwa anaendeshwa na mwanamke mpaka basi.” Bibi aliongea kwa sauti ya chini, ni sauti ambayo huitumia akitaka kunipa umbea, kwa kawaida hawezi kukaa na kitu.
“Makaratasi gani?” Niliuliza, kwa namna nilivyokua namfahamu nilijua ni lazima ataniambia.
“Lakini usije kumuambia mtu, naona siku hizi ushaanza ushoga na huyo mwanamke!” Aliongea huku akininyooshea mkono kunionyesha chini ya kabati.
“Niletee huo mkoba.” Aliniambia, niliinama na kutoa Begi mmoja, ulikua kama umechakaa flani hivi.
“Mimi tena Bibi, wewe ndiyo shoga yangu pekee, siwezi kuwa na shoga mwingine!” Niliongea huku nikicheka, nilimkabidhi lile begi akaufungua na kutoa kabrifkesi na kukafungua kalikua na mafaili mengi.
“Wewe mwanamke unafanya nini na vitu vyote hivi! Hata kusoma unajua kweli wewe?” Nilimtania, alicheka na kuniambia.
“Sijui lakini wanangu wote niliwasomesha na haya ni matunda yake, hizi ni hati za nyumba. Mwanangua najenga na mke wake hajui, kila kitu kanipa mimi, sitaki kuviweka humu ndani kwani huyu shetani anaweza kuvuiona siku moja. Nikifa hapa akasafisha chumba, bora nimpe Karim, yeye bado hajaoa anaishi mwenyewe alinde mali za Kaka yake.”
Nilishindwa hara chakuongea, kulikua na hati za viwanja tano, kulikua na kadi za magari tatu na makatarasi makaratasi menghi ya TRA, vyote alikua navyo Bibi.
“Baba anajua?”
“Anajua nini?”
“Kuhusu wewe kumpa Karibu hati zake.”
“Hajui, alinipa mimi Mama yake nimtunzie, lakini naona hali yangu nayo si nzuri nikifa hapa huyu atadhulumiwa na mke wake. Hizi mali ni zakwetu, mkewe hata hazijui lakini bado simuamini, nimekuambia wewe tu, hata dada zake sijawaambia, wale wameolewa na sijui wanaishije na waume zao!” Nilitamani kuongea kitu lakini nilisita, nilishindwa kabisa kumuelewa Bibi, alionekana kujali kuhusu watoto wake ila hakua akiwajua vizuri.
Kweli Karim alikuja siku hiyo hakutaka kukaa sana, baada ya kuingia kumsalimia Mama yake aliaga kuondoka, ili kuzuga niliambiwa mimi kutoka na lile Begi nililiweka kwenye mfuko kama nguo chafu na kuupeleka katika Gari la Karim, hakutaka mtu ajue. Lakini wakati natoka nilikutana na Shangazi Mama Abdul yeye ndiyo alikua anaingia, aliniuliza nimebeba nini sikua na jibu, nilimuambia ni mizigo tu ya Anko, alishangaa ni kwanini nibebe mimi na si yeye mwenyewe, baada ya kuniona nina wasiwasi wasiwasi alininyang’anya na kuangalia ndani.
“Nani kakupa, kavipata wapi hivi?” Aliuliza kwa hasira, nilinyamaza bila majibu.
“Si nimekuuliza, mbona unanyamaza, umeshakua na kiburi siku hizi?” Aliuliza tena kwa sauti ya juu. Nilimuambia Anko ndiyo kanipa na sijui kavipata wapi. Aliniambia nirudi ndani atapeleka mwenyewe. Kabla ya kurudi ndani Karim alitokea, alimuonyesha vile vitu na kuanza kuzozana. Alikua anamuuliza anavipelekwa wapi na kwanini yeye alikua hajasihirikishwa.
“Hayakuhusu, mimi ndiyo mwanaume humu ndani, unataka kujua kwani vyako hivyo!” Aliongea huku akitaka kumnyang’anya. Shangazi hakukubali, alivizuia na wakawa kama wanagombania flani.
“Hivi ni vitu vya Kaka, vina majina yake wewe unapeleka wapi? Nataka kujua, unaenda wapi na hati za nyumba za Kaka?”
“Nimekuambia havikuhusu, kanipa yeye mwenyewe, haya ni mambo ya wanaume, wewe umeolewa na ndoa yako hayakuhusu kabisa!”
“Kama kakupa basi tuingie ndani tukamuulize?” Shangazi aliendelea kung’ang’ania lakini kabla ya kujibu chochote Baba alitokea.
“Mkamuulize nani? Mnafanya nini mbona mnagombana, mnagombania nini na hilo si Begi la Mama?” Baba aliuliza huku akimsogelea Shangazi, alionekana kulitambua lile Begi kwani yeye ndiyo alimpa Bibi. Alilikimbilia na kulifungua kuangalia vilivyomo ndani.
“Mnapeleka wapi mizigo ya Mama? Mbona mnagombania?” Aliwauliza kwa wasiwasi. Nilinyamaza kimya nikiwaangalia watajibu nini, moyoni nilikua nashangilia kwani niliamini Baba sasa taujua ukweli kuhusu ndugu zake.
(ILIPOISHIA SEHEMU YA TATU; Bibi anataka kumpa Karim hati za viwanja na naaraka nyingine za mali za Baba kwani hamuamini Mama wala akina Shangazi, wananipa mimi ili nipeleke kwanye gari ambapo nakutana na Shangazi, ananisimamisha na Karim anatokea, wakati wanagombana Baba anatoka na kuliona lile Begi anawanyang’anya na kuanza kuangalia akiwauliza wanalipeleka wapi? Unajua nini kitatokea? ENDELEA… Kama hukusoma sehemuzilizopita ingia Instagram @aziranimagazine )
“Kachukue mizigo mingine!” Karim aliongea kwa kunifoke, nilishangaa kwani hakukua na mizigo mingine, lakini sikusema kitu nilinyamaza tu nikiwa nimesimama nawangalia, bado nilikua nasubiria kuumbuka kwao.
“Mizigo gani hiyo akachukue?” Baba aliuza kwa hasira, bado alikua kashikilia lile begi akiangalia vilvyomo ndani.
“Mizigo ya Mama, Mama anataka kuondoka, nilikua nagombana na Dada hapa anatakaa Mama aende kwake lakini Mama ashasema haendi popote, huyu kaolewa anasema hawezi kwenda kuvunja tena ndoa za watu kama alivyovunja yako.” Karim aliongea, kila mtu alishangaa, hata Shangazi mwenyewe alishangaa hakujua anamaanisha nini!
“Unamaanisha nini? Mama anaenda wapi?” Baba aliuliza, sasa alinyanyuka na kusimama vizuri.
“Kamuulize mke wako? Mama amesema hawezi kuendelea kukaa sehemu ambayo hahitajike, ninaondoka naye. Wewe si nimekuambia nenda kachukue mizigo mingine ya Mama, mbona unasimama tu, jua pia tunaenda wote kwani wewe ndiyo mfanyakazi wa Mama!” Aliongea kwa hasira, sikua nikielewa chochote lakini nililazimika kuondoka ili kwenda ndani. Lakini Baba alinizuia na kuniambia nisubiri kwanza.
“Hakuna mtu anayeondoka hapa! Mama aondoke kwa sababu gani?” Sijui Shangazi aliondoka wakati gani na sijui alipata hilo wazo saa ngapi lakini baada ya kama dakika mbili wakati Baba na Karim wanagombana pale nnje Shangazi alitoka kamshika Mama mkono mmoja na mkono mwingine kashikilia Begi.
“Hii familia ni washenzi sana!” Niliwaza, kwa sekunde chache walishabadilisha kila kitu hata Bibi alishaungana nao na alikua analazimisha kuondoka. Halikua tena sula la Begi bali suala la Bibi kuondoka. Baba alimzuia na kusema hondoki mtu, alimchukua Bibi na kuingia naye ndani kisha kuanza kumhoji.
“Mke wako hataki niwe hapa na mimi nishakua mtu mzima, karibuni nitakufa sitaki ugombane na mke wako kwaajili yangu!” Bibi aliongea hukua kijilazimishia kulia, sijui hata ni wakati gani walimuandaa kusema hivyo lakini nilijua ilikua ni kazi ya Shangazi na kwa mtu asiyewajua angeweza kuwaamini.
“Mke wangu kafanya nini? Mke wangu kakuambia nini Mama?” Baba aliuliza, Bibi alinyamaza bila kusema chochote.
“Anakasirika namna tunavyokuja hapa, amemuambia Mama kama anakaa hapa basi kuwe na ratiba ya kumtembelea na si kujazana jazana hapa! Anasema anashindwa kuja na marafiki zake, ndugu zake au wafanyakazi wenzake kwakua nyumba imejaa kama vile hospitali!” Karimu aliongea, kwa kumuangalia usingedhani kijana kama yule msomi namna ile anaweza kuwa mnafiki namna ile.
“Amesema hivyo Mama?” Baba aliuliza kwa hasira.
“Sitaki kuongea mwanangu, mimi sitaki kuwa sababu ya kuvunjika kwa ndoa yako.” Mama aliongea kwa ufupi lakini Baba alionekana kumuelewa. Nilimuona Baba akitoka kwa hasira, Mama alikua jikoni akipika, nilisikia vyomvo tu na kelele kadhaa kisha nilimsikia Mama akipiga kelele. Baba alimtukana sana huku akimpiga, ilikua ni mara yangu ya kwanza kumuona akifanya vile, alimpiga sana tena mbele ya watoto na kumuambia kua ataondoka yeye kabla ya Mama yake kuondoka.
Nilimuona Shangazi na Karim wakicheka, walikua wanafurahia, Mama hakujibu chochote, alivumilia kupigwa mpaka Baba hasira zilipoisha akaondoka na kuwasha gari, alikua na hasira sana, hakuna aliyejua usiku ule alikua anaenda wapi.
“Ndiyo uondoke sasa, unataka kupambana na sisi? Huyu ni Kaka yetu ndugu yetu wa damu unafikiri atakusikiliza wewe kuliko anavyotusikiliza sisi!” Shangazi alimuambia Mama kwa dharau.
“Na kwa taarifa yako ukiondoka hapa unaondoka kama ulivyokuja, mali zote ni za Kaka, usidhani utaondoka na kitu.”
Aliendelea kuongea, alitukana sana lakini Mama hakujibu chochote. Walichoka na kuondoka, walirudi chumbani ambapo walianza kugombana kuhusiana na zile hati. Lile Begi Baba alilisahau chumbani kwa Bibi, Shangazi alikua analalamika kua wao wanatengwa na Bibi anampenda zaidi Karim kuliko wao, anamuambia mambo mengi. Walilumbana sana, sikutaka hata kuwasikiliza, kwa kuwaangalia namna walivyokua wakigombea mali za Kaka yao ambaye alikua bado hajafa nilijisikia vibaya.
“Mama kwanini tusiondoke, hivi Mama kwani wewe huwezi kutuhudumia sisi wanne, mimi nitafanya kazi, nitaenda hata kuomba lakini sitaki kukuona unateseka namna hii.” Mod alimuambia Mama yake, baada ya kile kipigo bado Mama aliendelea kumalizia kupika, alitenga chakula mezani na kuwaita waje kula chakula.
“Mwanangu haya ni mambo ya mimi na Baba yako, achana nayo, huwezi kuondoka utaendelea kubaki na Baba yako hapa ni kwenu.” Aliongea kwa huzuni huku akilazimishia tabasamu, Mod hakuendelea kuuliza tena, alikaa mezani na kuchota chakula, alijaribu kula lakini hakikupanda, hata mimi nilishindwa kula, nilikua najisikia vibaya kwakua nilikua najua ukweli wote lakini nilishindwa kufanya chochote.
Baada ya kama dakika kumi hivi tangu waitwe kwenye chakula walikuja na kukaa mezani, bila aibu walikula na kujiongelesha wakicheka kama vile hakuna chochote kilichotokea. Nilishindwa kuwalewa kabisa, walijiona kawaida kabisa, walijichekesha chekesha mbele za watoto. Nilichukua chakula changu na kwenda nacho chumbani kwa Bibi, huko ndiyo nilikua nalala kwaajilia ya kumhudumia, aliniongelesha lakini nilishindwa hata kumjibu, nilikua na hasira sana, hata chakula sikuweza kula nilikiweka mezani nikapanda kwenye kitanda changua ambacho kilikua pembeni ya kitanda cha Bibi na kulala.
***
Waliendelea kufanya vituko vyao na Mama aliendelea kuvumilia, alijifanya kuona mambo kama kawaida na kila siku alijipa moyo kua yataisha, watoto walikua hawana raha na ikitokea siku watoto wa kina Shangazi wanakuja basi walitawala nyumba na walikua wakiwachukia watoto wa pale ndani kana kwamba wao ndiyo wageni wamekuja kumbe wenyewe ndiyo sio kwao.
Mama alinyamaza kimya hata walipomtukana na kumtafutia sababu ili aongee hakuongea, kile kitu kilizidi kuwaumiza na kuona kama kuna kitu anafanya.
“Wewe ndiyo shoga yake, hembu tuambie anafanya nini, mbona kanyamaza sana?” Siku moja Shangazi Mama Abdul aliniuliza.
“Mimi sijui chochote, si mliniambia nisiwe karibu naye?” Kweli sikua najua chochote kwani Mama hakua akiniambini, aliniona kama ni mtu wao, pamoja na kujitahidi kujiweka karibu naye lakini alikua akifanya mambo yake yeye kama yeye.
“Hata kama lakini ndiyo usijue, si unaishi naye hapa?” Aliendelea kunidodosa.
“Anti kweli mimi sijui kwakweli, Mama ni msiri sana.”
“Basi chunguza, hakikisha unajua kila kitu, huyu mwanamke kawa kimya sana, inawezekana anapanga kitu juu ya Kaka yetu.”
Nilimuitikia kukubali lakini kusema kweli sikupanga kufanya chochote, kwanza nilikua nawachukia lakini sikua na namna ya kumchunguza Mama na kujua chochote, hatukua na ukaribu sana kihivyo kuweza kujua kua anafanya nini. Hakua yeye tu aliyeniuliza hata Shangazi Mama Aziza nayeye aliniuliza na kitu kilichonishangaza zaidi hata Karim naye aliniuliza, walionekana kupaniki sana kwani mbinu zao zote za kumuumiza hazikuzaa matunda.
Baba naye alikua mkimya sana, mara nyingi aliporudi nyumbani alikua ni mtu wakujifungia ndani. Tangu kumpiga Mama yao mbele yao watoto walikua wakimuogopa, hawakua wakimkimbilia na kumchezea kama zamani, nilimuona mtu wa mawazo, alijitahidi kucheka kidogo pale ndugu zake wakiwepo au mbele ya Bibi lakini kwakumuangalia tu hakua na furaha. Yeye na Mama walikua wakiangaliana kama mwanafunzi na Mwalimu mkuu, hakukua na uchangamfu ule wa zamani.
Lile Begi lilibaki kwa Bibi kwa muda kidogo lakini siku moja Baba alienda kulichukua hali ile ilizidi kuwapa wasiwasi sana kwani Baba alionekana kama ana msongo wa mawazo, ule uchangamfu kwao nao ulipungua ingawa angalau kidogo alikua akiongea nao tofauti ana navyokua na Mama.
“Kwahiyo wewe huoni tatizo hapo?” Mama Abdul aliongea, tulikua kwenye gari tunaenda nyumbani kwake, mule ndani alikua na ndugu zake Karim na Mama Aziza. Mara zote ninapokua nao wanaongea mambo yao bila kujali kama nipo, walishanizoea na kuniona kama mmoja wao.
“Tatizo gani sasa, huoni kama hata wakiachana hachukui kitu!” Karim aliongea.
“Hivi wewe ni mwanasheria wawapi? Unajua wanaume mna matatizo, inawezekana hata wewe ukija kuoa utakua kama Kaka!” Mama azioza aliongea.
“Atakua au ashakua, ana kidemu chake kinamsumbua balaa, hivi hukijui, anataka kukioa lakini eti hakitaki!” Mama Aziza alidakia.
“Sio kidemu Mchumba!” Karim alijibu kwa hasira.
“Unaona walewale, sasa hapo unamtetea nini! Nakuambia wanaume wakishaoa wanakua wapuuzi kabisa, yaani hapo hata huoni kua kama kashaanza kundika viwanja watoto wake inamaana kua hatupati kitu!” Mama Abdul alimkumbusha.
“Kwani nyie mlichokua mnataka ni nini? Unajua mimi bado sijawaelewa, hivi mnachotaka ni Kaka asidhulumiwe au kuchukua malizake, maana mimi sijui, kwani kuna ubaya gani watoto wake wakichukua, mfano likitokea lakumtokea si watoto wake!?”
Walibishana sana kuhusu mali za Kaka yao, hiyo ilikua ni baada ya Karim kuwaambia kua Kaka yake alimuita kuwa kama shahidi katika kiwanja alichokua ananunua, kilikua ni kiwanja kikubwa na alindika jina la mtoto wake wa mwisho. Walikua na wasiwasi kwamba Kaka yao kashaanza kujitambua na mali zote ataandika kwa majina ya watoto wake.
“Kaka akifa watoto wanabaki kwa Mama, yule mwanamke anafanya kazi, ni msomi na watoto wenyewe ndiyo hao hawatupendi, unafikiri kuna mahakama itaamua wabaki na sisi, watabaki na Mama yao na mali zote zitakua zake!” Mama Abdul aliongea, nilishangaa sana kwa namna wakimuwazia Kaka yao mabaya, walimjadili kama mjinga flani hivi ambaye hajielewi na walikua wakiongea kana kwamba wao wataishi milele ili kuridhi maliza Kaka yao.
Tulifika kwake, wao walienda kwa Mambo yao lakini mimi nilienda kufanya kazi yangu ya ‘ukiraka’, binti yake wa kazi aliondoka kwa muda hivyo niliambiwa nikakae pale mpaka atakapopata mfanyakazi mwingine. Kilikua ni kama kichekesho kwani niliambiwa yeye ndiyo ataenda kumhudumia Bibi. Kwa ufafanuzi kidogo tu nikuwa mimi niliyeajiriwa kwaajili ya Bibi nilikua naondoka kwenda kwake ili yeye aende kufanya kazi yangu.
Nilikaa pale kwa mwezi mmoja mpaka alipopata binti wa kazi mwingine. Niliondoka na kurudi katika kituo changu cha kazi, nilifurahi kwani pamoja na kwamba kule nako kulikua hakuna amani lakini watoto walikua wananipenda tofauti na kwa Mama Abduli watoto wake walikua na kiburi na walikua wakiniona kama takataka. Nilirudi kazini na kuendelea na kazi, lakini kuna vitu vingi vilikua vimebadilika kila kitu pale nyumbani kilikua kimepangwa tofauti, lakini hivyo havikunishangaza sana, Aziza mtoto mdogo wa bosi wangu ndiyo alinishangaza.
“Mama Aziza ana tatizo gani?” Siku moja niliamua kumuuliza Mama yake. Ilikua ni jioni na ndiyo alikua ametoka kazini.
“Kwanini unasema hivyo? Mbona naona kama yuko kawaida, kwani anaumwa?” Mama aliniuliza kwa wasiwasi.
“Sijui lakini simuoni kama yuko sawa.”
“Yuko wapi?”
“Yuko chumbani kwake na kalala na hicho ndicho ambacho kinanipa shaka analala sana.” Mama alitaka kupuuzia lakini aliamua kuingia chumbani kumamsha, alijaribu kumuamsha lakini hakuamka.
“Kalala saa ngapi?” Aliniuliza.
“Tangu saa saba alipotoka shule.” Ndiyo kwanza alikua na maiaka minne hivyo alikua chekechea na wao hutoka shule mapema. Wakati huo ilikua ni saa kumi na mbili na nusu, Mama alijitahidi kumuamsha akaamka kweli lakini alikua kachoka kalegea hata kukaa hawezi.
“Imeanza lini?” Mama aliniuliza.
“Sijui, sina uhakika lakini mimi tangu juzi niliporudi alikua katika hali hiyo hiyo.” Nilimjibu, Mama alipaniki, alijilaumu kwa kutokufuatilia ingawa sikuona kosa lake, mara nyingi anaporudi jioni Aziza anakua tayari ashaamka au inawezekana hakuna mtu anayemuambia kua kalala muda mrefu.
Kitu kingine ambacho kilikua kinashangaza ni jasho, alikua anatoka jasho jingi sana na kwakuangalia ungedhani hata kajikojolea, shuka lilikua linaloa. Mama hakutaka hata kusubiri Baba arudi, alimpakia kwenye gari na kumpeleka hospitali, alikua akiendesha gari yeye hivyo aliniambia nimpigie Baba simu kumuambia mtoto anaumwa.
Nilimpigia na Baba alitufuata hospitalini, alipimwa vipimo vyote lakini hakua na ugonjwa wowote. Lakini pia alianza kuchangamka, alikua kama kawaida tu. Hawakukua na chakumpa na Mama aliona labda ni kupaniki tu, tuliruhusiwa na kuondoka, lakini kesho yake hali ilikua ni ile ile na iliendelea hivyo kwa wiki nzima. Kila akitoka shule na kula chakula basi alikua akilala kuanzia saa saba mpaka saa kumi na mbili na wakati mwingine hata mpaka saa mbili usiku.
Kibaya zaidi ni jasho alilokua akitoa. Walimrudisha tena hospitalini, sikuenda nao lakini walionekana kupima kila kitu. Siku moja walirudi wakiwa wamekata tamaa, hawakusema kilichotokea lakini walionekana kama wamechoka na kukata tamaa. Tangu lile tukio la kumpiga kutokea walikua kama paka na panya lakini siku hiyo walionekana kama mke na mume. Hawakutaka kuongea na mtu, nilishangaa Baba hakutaka hata kuongea na Bibi kitu ambaho si kawaida.
Ndugu zake walipokuja alikataa katakata kutoka chumbani, sikuwaelewa niliogopa hata kuwauliza. Walikaa chumbani kwa muda mrefu, chakula kilipoiva nilienda kuwagongea, lakini kabla sijagonga mlango nilisikia kama wanaongea, nilijikuta tu nasikiliza kwani nilikua na hamu sana ya kujua kilichotokea hospitalini mpaka woa kuwa katika hali ile.
“Itabidi twende tukapime hospitali nyingine, haiwezekani ni mtoto mdogo sana, miaka minne!” Baba alikua anaongea.
“Lakini tumepima Hospitali tano.”
“Hata kama! Hata ikiwa nnje ya nchi nitampeleka mwanangu, haiwezekani mtoto mdogo kama huyuaonekane kama kaathirika wakati sisi wazazi tuko sawa, tungekua hata tumeambukizwa hapo sawa tungesema tumemuambukiza lakini miaka minne atakua kapata wapi UKIMWI!?”
“Mimi nimechanganyikiwa mume wangu, au shuleni watakua wamembaka?” Mama alikua akiongea huku akilia, pale nilipokua nimesimama niliona nguvu zikiniishia nikaondoka na kurudi kukaa sebuleni bila kuwaita.
Kama unataka kuwa wakwanza katika muendelezo wa simulizi hii hakikisha unafollow ukurasa wangu wa instagram @iddimakengo @aziranimagazine na kama hukusoma tangu mwanzo ingia katika ukurasa huo huo na angalia utaona namna ilivyopangiliwa kuanzia sehemu ya kwanza na kama huko instagram basi like ukurasa wangu hapa facebook @aziranimagazine
(ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE; Aziza anaanza kuumwa ugonjwa ambao hauelezeki, wazazi wake wanahangaika hospitalini bila kupata majibu, hawakujua sababu ya kuwa hivyo. Siku moja wanarudi wakiwa wamekata tamaa, wanaingia na kujifungia ndani, wakati nikienda kuwaita wkaajili ya chakula nasikia wanaongea wanasema Aziza ana UKIMWI na hawajui nani kamuambukiza. Endelea….)
Baada ya kusikia vile nilishindwa hata kuwagongea, nilika pale kwenye kochi mapaka walipotoka wenyewe. Walijaribu kuonyesha nyuso za furaha lakini kwa kuwaangalia tu ilionyesha walikua na mawazo sana. Aziza alikua macho na kwakumuangalia wala usingedhani kua anaumwa. Mara zote ugonjwa wake huanza pale anapotoka shule, anapokula chakula cha mchana basi hulala mpaka usiku na kutoa jasho jingi.
Siku iliyofuata Mama alienda kazini, lakini aliniambia kumuangalia Aziza kwani hakua akienda shule siku hiyo. Sikuuliza sana kwani nilijua kilichokua kinaendelea, walikua hawajamuambia mtu yeyote na ilionyesha kua hawakutaka kumuambia mtu. Ingawa nilibaki mwenyewe lakini nilimuangalia sana, nilikua namuonea huruma, kwa udogo ule hakujua kilichokua kinaendelea. Hali ile iliendelea vilevile, kila akila chakula analala mpaka usiku lakini wakati mwingine alikua vizuri.
Baada ya kama wiki mbili hivi kuna kitu kilibadilika, Aziza bado alikua nyumbani na pale nyumbani tulibaki watatu, mimi, yeye na Bibi, mimi nilikua jikoni napika na yeye alikua chumbani kwa Bibi, walikua wakicheza pamoja na kutaniana. Mimi nilikua jikoni lakini nikiwa pale Aziza alikuja, wakatti anaingia tu nilisikia harufu mbaya sana, ilikua ni harufu ya kinyesi.
“Wewe uemjinyea?” Nilimuuliza kwa mshanagao, alishakua mkubwa kushindwa kujisaidia mwenyewe.
“Hapana Dada, mimi sijajinyea!” Alinijibu, kweli nilimuangalia alikua hajajisaidia lakini ile harufu bado nilikua naisikia, nilitoka jikoni kuangalia ilipokua inatoke alakini sikuiona.
“Kuna harufu gani kwani?” Aliniuliza kwa sauti yake ya kitoto.
“Inmaana huisikii?”
“Hapana Dada.” Nilishindwa kuelewa, ilikua ni harufu kali na nilizunguka nyumba nzima sikusikia chochote. Wakati nikitembea alikua akinifuata kuangalia nilichokua nikikitafuta.
Ile harufu nayo nilikua nikiisikia, nilitembea mpaka kwenye chumba cha Bibi.
“Huku nako kuna harufu?” Nilimuuliza Bibi wakati naingia.
“Harufu gani mbona mimi sija…” Bibi alinijibu lakini kabla ya kumalizia kuongea aliziba pua.
“Nani kajinyea?” Aliniuliza, Aziza ndiyo alikua anaingia na alipoingia tu chumba kilikua kama kimejaa kinyesi. Nilimuambia hakuna, aliniambia nimkague Aziza, nilimvua nguo kabisa ili kuhakikisha. Ile namvua tu nguo ya juu kidogo ni dondoke.
Kulikua na kidonda kikubwa kwenye kwapa lake, kilikua kama vile kimeoza, kilikua kikubwa kimetengeneza kama kasahani kadogo hivi kwapani huku kikisogea mpaka wkenye mkono. Nilishangaa sana, hata Bibi naye alishangaa, Aziza alikua akitushangaa namna tulivyokua tunamshangaa.
“Husikii maumivu?” Nilimuuliza.
“Hapana, maumivu gani mbona mimi niko kawaida.” Aliongea kwa kuiamini, nilimnyooshe mkono kumuonyesha kilipokua kidonda chake.
Ile kukiona tu alianza kupiga kelele, alikua akipiga kelele za maumivu akisena anahisi mwili kuapta moto, mwanzo nilihisi kama ni mshituko wakujiona vile lakini baada tu ya kuona kidonda chke alianza kupiga kelele za maumivu. Alianza kulia, huwezi amini Bibi na ugonjw awake hawezi tembea vizuri lakinia lipata nguvu tukamkamata na kumshikilia kitandani kwani alikua akijirusha rusha na kujipiga kwenye viti kutokana na maumivu.
Nilichukua simu yangu na kumpigia Mama, nilimuambia arudi nyumbani haraka kwani mtoto anaumwa sana. Katika simu alizidikia zile kelele aliniambia nakuja. Nilimpigia Bba asimu kumuambia nayeye alisikia kelele za mwanae na kuanza safari ya kuja nyumbani kumuona. Lakini kabla ya wao kufika alikuja Shangazi, Mama Abdul, sijui alitokea wapi lakini ghafla nilimuona kashafikia mlangoni.
“Kuna nini mbona kelele?” Aliuliza bvila wasiwasi, Bibi bado ndiyo alikua kamshikilia Aziza wakari mimi nikiwa bize kuwapigia wazazi wake simu.
“Afadhali umekuja, anatakiwa kupelekwa hospitali huyu!” Bibi alimuambia Mama Abdul ambaye hakuonyesha kushtuka, alimuangalia Aziza bvila kumgusa, alikiangalia kidonda na namna alivyokua akipiga kelele. Baada ya hapoa linyanyuka, nilijua kua anaenda kuwasha gari na kuandaa ili tumpeleke hospitali lakini zilipita kama dakika tanohivi vila yeye kurudi. Kwa hali aliyokua nayo mtoto zilikua ni nyingi sana hivyo niliamua kutoka ili kumuangalia.
Hakua mbali alikua kakaa sebuleni kwenye sofa anaongea na simu.
“Shangazi mtoto anatakiwa kupelekwa hospitali huyu atakufa!” Nilijikuta nafoka kama vile mimi ndiyo nilikua bosi pale. Kunisikia ni kama nilikua nimstua na kumnyanyua kutoka kwenye usingizi. Alinyanyuka harakaharaka na kutoka nnje, sikumuelewa, niliendelea kumpigia kelele na kumuambia arudi tumpeleke mtoto hospitalini.
“Mume wangu kanipigia simu, amesahau funguo zake, ngoja nikampe.” Alitoka harakaharaka kama vile anakimbizwa, aliingia kwenye gari yajke na kuondoka mbio kama vile alikua anawahi kitu kikuubwa cha maana.
Aliondoka bila hata kumgusa mtoto wala kufanya kitu chochote, kwa bahati zuri ile anatoka tu Baba naye alikuja na kumchukua mtoto na kumpeleka hospitalini. Huko nako hawakupata majibu, walishanga akile kidonda kilitoka wapi, alisafishwa lakini maumivu hayakupoa, walilazimika kumpa dawa za usingizi kwani alikua akilia sana, wote walikua kama wamechanganyikiwa kwani asubuhi mtoto alikua vizuri ila ghala ana kidonda tena kikubwa ambacho hakielezeki.
Aziza alikaa Hospitalini kwa wiki moja, kidonda kilikauka na maumivu yalipotea kabisa,a liruhusiwa kuruidi nyumbani wakiwa hawaelewi kua ana tatizo gani. Bado walikua hawajamuambia mtu yeyote kluhusu yeye kuambukizwa, hata akina Shangazi nilikua na uhakika hawajui kwani hawakuwahi kuliongelea, mara kadhaa walikua wakijiongelesha mambo mengine mengine lakini si la ugonjwa hivyo nilijua kabisa kua hawana taarifa.
***
Wiki moja baada tu ya kutoka hospitalini Aziza alianz akuumwa tena, sasa alikua akionyesha dalili zote za mtu mwenye ukimwi, alikua akikohoa, bidonda vilianz amwili mzima, alikosa hamu ya kula na hali yake ilianza kuwa mbaya, walimpeleka hospityalinia mbako alilazwa. Kutokana na hali yake ilibidi Mama kuomba likizo kwaajili ya kumhudumia, hakua na ndugu wengine Dar hivyo kila kitu ni kama alikua anakifanya mwenewe.
Ingawa akina Shangazi walikua wakishinda hapo nyumbani lakini walikua hawasidii chochote.
“Unafanya nini?” Siku moja Shangazi aliniuliza.
“Naandaa chakula cha Mtoto, Baba ameseme atakipitia kwaajili ya kupeleka Hospitalini.” Nilimuambia, nilishapika chakula cha mtoto, Mama ndiyo alikua Hospitalini mwenyewe, ilikua ni kama wiki nzima kalala hospitalini na mtoto.
“Hivi bado hujajua nafasi yako, si nilishakuambia kua kazi yako ni kumhudumia Mama yangu, au unataka kufukuzwa kazi?” Aliniuliza kwa hasira hukua kininyang’anya Hotpot.
“Hpana lakini Baba ndiyo kaniambia kua niandae chakula.”
Kila siku nilikua naandaa chakula mimi lakini mara nyingi wlaikua hawapo kwani baada ya mtoto kuanza kuumwa wlaikua hawaji tena mara kwa mara.
“Kwahiyo inamaana kila siku wewe ndiyo unawapikia?”
“Ndiyo!” Nilimuona Mama Abdul anakua kama vile amepaniki, alichukua kile chakula na kwenda kwenye sink la vyombo vichafu akakiweka na kisha kufungulia maji. Nilijaribu kumzuia l;akini alinipiga kofi.
“Huna akili mjinga wewe! leo ndityo mwisho wako wa kunyenyekea unaondoka humu ndani!” Aliongea kwa hasira, kusema kweli abdo nilikua sijamuelewa kwani hakuna kitu kibaya nilichokua nimekifanya.
“Ninaye kulipa mshara ni mimi halafu unaenda kufanya akzi za watu wengine, ondoka hapa nenda kakusanye vitu vyako sitai tena uendelee kukaa kwenye hii nyumba naona unataka kunipdna kichwani!| Aliongea kwa hasira, nilijua kama anatania lakini nilimuona yuko siriasi, alikuja mpaka chumbani na kunisaidia kukusanya ngu. Bibi alikua kalala lakini baad aya sisi kuingia na kumsikia alivyokua akibwabwaja aliamka.
“Nini tena?” Bibi aliuliza.
“Tuinaondoka humu ndani, unaenda wkangu, hapa hutakiwi nilazima tuwaachie nyumba yao.” Shangazi alingea kwa hasira, Bibi alishangaa, aliulizia kuhusu mtoto na shangazi akasema kua hajui.
“Mama yake ahataki hata tuende kumuona mtoto!” Aliongea lakini Bibi hakuonyesha kumuamini.
“Una kichaa wewe, hujui kua yule ni mtoto wa Kaka yenu?” Bibi alionega kwa hasira, aliulzia kwanini napanga nguo nikamuambia kua nimefukuzwa kazi.
“Huyu binti haondoki hapa!” Bibi alifoka.
“Anaondoka nawewe pia unaondoka, siwezi kukaucha ndnai ya nyumba hii, Mary akiondooka unafikiri ni nani atakuhudumia?”
Mama alikua anampangia Bibi nguo lakini bibi alisema kua hawezi kuondoka, alimuambia kua ile nyumba ni ya mtoto wake wa wkanza wa kiume na labda mtoto mwenyewe afe ndiyo ataondoka kulelewa na mtoto mwingine. Shanagzi alilazimishia lakini hakukubali, ilimbidi kuacha, akaniambia niache kupanga vitu vyangu. Wakati huo huo Bbaa alikuja, aliniuliza kuhusu chakula sikua na jibvu nilijikuta nimenyamaza tu mdomo umjejifunga.
“Kamuuliza mke wako.” Shangazi alimjibu.
“Mke wangu kivipi, si yuko hospitalini, mbona mnanichanganya!” Baba alionekana kupaniki na alikua na haraka sana kuendele akusikiliza maneno maneno ya Shangazi.
“Binti wa watu kapika lakini mke wako kapiga simu kasema sisi ndiyo tunamloga mwanao hivyo hataki chakula kutoka kwetu…” Baba hakumsikiliz ampaka kumaliza, hakutaka hata kujua kama ni kwelia u la, alionekana kuchoshwa na maneno yao, hakuingia hata ndani alimuacha wkaati anaongea na kutoka zake, aliingia kwenye gari na kuondoka.
“Atakua amekasirikeee? Mbona kaondoka bila kunisikiliza?” Shanazai aliniuliza, hata mimi sikutaka kumsikiliza, alishaniboa hivyo niliondoka na kumaucha akiendelea kuongea. Aliendelea kujiongelesha mwenyewe palle lakini sikujali nilishakasirika na nilikua tayari kwa chochote.
Tangu siku hiyo Baba ni kama alikua hajali tena, hakua akila nyumbani wala hakua akichukua chakula nyumbani wkaajili ya mwanae. Nilikua nikiwapikia chakula watoto wengine, Shangazi na Karim nao walikua si watu wa kuja kujja tena kama zamani. Mtoto alikaa hospitalini mwezi mmoja,a liruhusiwa kutoka, si kwamba alikua amepina hapana, walimruhusu ilia kauguziwe nyumbani. Alirudi kakonda kachoka sana, alionekana kuwa katika maumivu makali, chakula kilikua kikipita kwa shida.
Kwa namna alivyokua anateseka nilijikuta nalia kila siku kwani nilikua nikikumbuka namna alivyokua mchangamfu. Siku moja Baba aliamua kutuita wote na kutuambia alichokua akiumwa, hakuwaambia watoto wake, alituambia sisi watu wazima.
“Sijui kama kafanyiwa na nani hiki kitendo, labda alijichoma masindano huko wkenye majalala lakini hii ndiyo hali ya mtoto.” Aliongea huku machozi yakimtoka, alijitahidi sana kujizuia lakini alishindwa, niliyaona maumivu yake.
Walikua wakimpa pole lakini ilionekana dhahiri ilikua ni ya kinafiki, baada ya hapo kila mmoja aliondoka zake. Alitafutwa Mama mmoja mtu mzima kidogo, yeye alikua ni nesi na alikua maalum kwaajili ya kumhudumia Aziza kwani alikua katika hali mbaya. Maisha yaliendelea na hali ya mtoto haikubailika, kila siku kilikua kikibuka kitu kipya. Pamoja na kuwa katika maumivu makali lakini Aziza bado alijaribu kuwa mtoto mwema, alikua akijirahidi kuongea na mara nyingi alihitaji mtu wa kucheza naye hapohapo kitandani.
Mimi mwenyewe nilipenda wkenda kucheza naye, tulishazoeana na alikua kama mdogo wangu, kwakua wenzake walikua wakienda shule muda mwingi nilibaki naye.
“Dada hivi mimi nikifa nitaenda peponi kweli?” Siku moja aliniuliza. Nilishangaa lile swali limetoka wapi, nilijua kabisa kakata tamaa, nilijkaribu kulipotezea lakini hakuacha.
“Mwalimu alisema mtu kama haswali basi akifa anaenda Motoni, eti Dada mimi si nitaenda Motoni?” Aliniuliza tena, nilijaribu kuzuia machozi lakini ilishindikana.
“Kwanini uansema hivyo, wewe ni mtoto huwezi kwenda motoni, isitoshe bado una muda mwingi wakuishi.”
“Hapana Dada, dada mimi sitaishi, niliwasikia Baba wakisema mimi nina UKIMWI watu wenye UKIMWI si wanakufa?”
Nilinyamaza kimya sikua hata na chakumjibu, sijui hata aliyajula wpai yale mambo.
“Dada tangu nianze kuumwa sijaenda tena Madrasa, sijaswali wala sijasoma tena Quran, nikifa nitachomwa moto. Mimi sitaki kuchomwa moto dada, ninaumwa sana nikichomwa tena moto dada si nitakufa?” Nilimsogelea kitandani na kumkumbatia, nilijaribu kumuongelesha na kumpa moyo ili anyamaze lakini wapi, wakati wote alikua anazungumzia mambo yakufa. Nilijikuta nalia kama mtoto, nilitaka kutoka kumuita Nesi wake lakini alinizuia.
“Dada usiondoke, nataka tukae wote, mimi naogopa sitaki nife nikwia peke yangu.” maumivu niliyoyapata siwezi hata kuyasimulia, mpaka leo nikikumbuka najikuta nalia. Wakati huo alikua ndiyo wkanza ametimiza miaka mitano, alishaumwa zaidi ya miezi sita, kwa umri ule aliongea kama vile mtu mzima.
“Siondoki naenda kumuita Nesi.” Nilimuambia.
“Hapana Dada, sitapona tena, njoo tulale pamoja usilie, nikifika nitamuambia Mungu nilikua naumwa ndiyo maana sikuswali wala kwenda Madrasa.”
Nilirudi na kulala naye lakini bado nilidhani nahitaji msaada. Nilitoa simu na kujaribu kumpigia Mama yake. Aliniuliza nampigia nani nikamuambia Mama.
“Hapana Dada, sitaki Mama anione wakati nakufa, atalia sana, Mama nanipenda sana, Baba hanipendi tena kama zamani ndiyo maana anampiga Mama kwakua anatupenda. Mama yangu ameteseka sana sitaki alie tena, usimpigie.” Nilitamani aliondoe hilo neno mdomoni mwake lakini halikuondoka, kila baada ya dakika mbilia litaja kuhusu kufa mpaka niliogopa.
Aliongea mpaka kupitiwa na usingizi, kusema kweli niliogopa kwani nilikua nakumbuka kuwa watu wakitaka kufa huykiona kifo, nilihisi hivyo kwani kwa hali yake na maneno yake sikua na amani. Nilipomuona tu kalala nilijua ni wakati wangu wakutoka, nilinnyanyuka na kumfunika vizuri lakini ila nataka kutoka tu nilimuona akiwa anatetemeka. Kulikua kuna kitu kama kinamkaba kooni, kohoa kwa nguvu na kutusha rusha miguu, nilienda na kujaribu kumshika lakini bado aleinelea, ilinibidi kuanza kupiga kelele kumuita Nesi anisaidie.
Unatake kuwa wakwanza kujua ni nini kitaendelea hakikisha unafuatilia ukurasa wangu
(ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO; Nilikua nyumbani mimi na Aziza, anaanza kuongea kuhusu mambo ya kufa kufa na baada ya muda hali yake inabadilika, anaakza kujirusharusha, naenda kumuangalia huku nikimuita nesi. ENDELEA….)
Nilipiga kelele kumuita Nesi lakini kabla ya kuingia Mama Abdul aliingia, sijui alitokea wapi, alisimama mlangoni na kuniangalia jinsi nilivyokua nikihangaika na mtoto. Hakujali alivyokua akiumia wala hakufanya chochote, aliniangalia tu kisha akaanza kufoka.
“Nilishakuambia kuhusu kazi zako humu ndani naona bado hunielewi!” Aliongea kwa dharau. Sikunyanyuka wala kugeuka, niliendelea kumuita Nesi.
“Nimemtuma mjini haweza kuja leo huyo!” Aliongea huku akinisogelea, niliendelea kumshikilia Aziza kwani alikua akijirusha rusha sana, lakini chakushangaza baada tu ya Mama Abdul kusogea na kufika karibu naye alituilia, kuna kitu kiliniambia huyu mtoto amekufa.
Nikikumbuka kwenye Movie namna wanavyoangalia mapigo ya moyo niliangalia nakukuta bado alikua anaupumua.
“Whooooh!” Nilipumua kwa nguvu na wakati huo huo Aziza alifungua macho.
“Shangazi nisamehe… Shangazi nisamehe… Shangazi nisamehe…” Aziza aliongea, nilishindwa kuelewa alikua anamaanisha nini lakini aliyarudia yale maneno kwa zaidi ya mara kumi, alikua hasemi chochote zaidi ya.
“Shangazi nisamehe… Shangazi nisamehe!” Aliongea mpaka Mama Abdul akaona kama aibu flani nakutoka. Alipotoka nilimfuata na kumuuliza ni kwanini mtoto anaomba msamaha kwake.
“Unajiona ushakua sasa hivi unahnihoji, dawa yako ni wewe kuondoka humu ndani naona ushaanza kujiona sehemu ya familia!” Aliongea kwa hasira na kubadilisha mada, sikutaka kumsisitizia sana kwani nilijua fika hawezi kuniambia chochote.
Nilirudi chumbani kwa mtoto, alikua ameamka vizuri, lakini jasho lilikua jingi, nilimfuta jasho ingawa halikukauka, ilinibidui kubadilisha mashuka tena.
“Unasikia kiu?” Nilimuuliza kwani niliona kapoteza maji mengi sana.
“Hapana Dada, niko vizuri.” Nilisubiri ametulia ndiyo nikaamua kumuuliza ni kwanini alikua anamuomba Shangazi yake msamaha.
“Mimi Dada?” Aliniuliza.
“Ndiyo, wakati Shangazi yako ameingia hapa ulikua unalalamika na kusema shangazi nisamehe, kwani umemkosea nini?” alionekana kutokuelewa chochote, aliniangalia na kuniambia kua hakumbuki kitu wala hata hakumbuki kama Shangazi yake alikua mule ndani.
Nilinyamaza lakini nilihisi kitu, niliamini kua inawezekana kweli hakumbuki kwani wakati anaongea alikua akiongea kama mtu aliyekua anaweweseka. Akili yangu ilirudi tangu mwanzo, kwa mambo yaliyokua yekiendelea mule ndani nilihisi lazima kuna mambo ya kishirikina. Haikua sawa mtoto mdogo kuumwa namna ile, niliwaza nini chakufanya nikaamua kuongea na Mama. Jioni aliporejea nilimuomba kuongea naye, sikutaka kuongea naye hapo nyumbani. Alinichukua kama vile ananipeleka dukani tukaenda kuongea.
“Baba yake hataki hayo mambo, haamini hivyo vitu, hata mimi nilishajaribu kumuambia lakini hakutaka kunisikiliza. Nimeamua kunyamaza na kumauchia Mungu.” Alinijibu baada ya kumuambia kua nahisi kuna mambo ya kishirikina. Nilimuambia wakati niko naye alikua akiweweseka na kuongea vitu ambavyo havieleweki. Nilisita kumuambia namna alivyokua anamtaja Shangazi lakini baada ya kuona kama haelekei niliamua kumuambia.
Hakuonekana kushtuka lakini hakuonekana kutaka kufuata ushauri wangu.
“Kuna wataalamu wengi sana.” Nilimuambia lakini hakuonekana kujali.
“Baba yake hataki hayo mambo!” Alizidi kuniambia vile, nilijikuta nakasirika, alikua mkubwa wangu, Bosi wangu lakini kila nikikumbuka namna Aziza alivyokua anaongea nilijikuta napadwa na hasira.
“Hivi wewe ni mwanamke wa namna gani! Mbona unavumilia upumbavu wa namna hii, unanyanyaswa katika nyumba yako, unafantiwa kila kitu cha kijinga, una kazi yako, umesoma lakini unaendeshwa endeshwa na wapuuzi wa darasa la saba kisa ndoa! Mimi mwenyewe darasa la saba, mimi mwenyewe darasa la saba masikini mbwa kunuka lakini siwezi kuvumilia ujinga kama wako!” Nilimchamba sana kama mtoto mdogo, nilipandwa na hasira mpaka kulia.
Nilijua ndiyo napoteza ajira yangu hivyo ilinibidi kufunguka sana, niliongea mpaka basi kisha nikaondoka na kurudi zangu ndani. Alinifuata mpaka chumbani kwa Aziza ambapo ndiyo nilikua natumia muda mwingi huko, alikaa pembeni yangu na kunishika mkono. Bado nilikua na hasira nimevimba, nilikua namuangalia Aziza kwa mara ya mwisho kwani nilijua mule ndani naondoka na sitakua na mtu wa kunitetea. Nilishatibua kwa Shangazi na sasa nilikua nimetibua kwa Mama.
“Mdogo wangu mimi ni Mama, usidhani nimekaa hivi hivi kijinga jinga nahangaika sana.” Aliniambia kwa upole, niligeuka kumuangalia machoni, kulikua na mwanga hafifu wa taa kwani giza lilishaingia lakini nilimuona namna alivyokua akihangaika kuzuia machozi yasiotoke.
“Si uende kwenye maombi Dada?” Nilimuambia kwa upole.
“Nilishampeleka kila sehemu, lakini wapi, unafikiri kila ninapomtoa hapa nampeleka hospitalini, Baba yake ahataki lakini nitakula hata mavi ili mwanangu apone, nimehangaika sana.”
Kwa namana alivyokua anaongea nilijisikia vibaya kwa jinsi nilivyokua nimemchamba, nilimgeukia na kumuomba msamaha.
“Hapana, umedhihirisha ni namna gani unampenda mdogo wako, Mungu akubariki na ninaimani kwa dua zetu atapona.” Aliondoka na kunaicha pale, nilipanda kitandani na kulala, Aziza alikua amelala na kwa kawaida yake nilijua kabisa itachukua muda mrefu mpaka yeye kuamka.
Nilikaa kwa muda nakukumbuka nilikua sijaenda kumuona Bibi kwa muda mrefu, nilinyanyuka na kwenda chumbani kwake, alikua amekaa, nilimuomba samahani kwa kuchelewa kuingia kwake.
“Mjukuu wangu anaendeleaje?” Aliniuliza, nilimuambia alivyokua anaendelea, alionyesha kusikitika sana, alionekana kabisa kuumizwa namna alivyokua anaumwa. Ni muda mrefu ulikua umepita tangu kukaa na Bibi kuongea na kupiga umbea, tangu Aziza kuanza kuumwa muda mwingi nilikua nikiutumia chumbani kwake.
“Mtoto mdogo kama yule kupata UKIMWI inawezekana kweli?” Alianza kuongea, nilimuacha aendelea kuongea na kwa maneno yake nilijua kua anaamini mjukuu wake kalogwa, hakikua kitu cha kawaida.
“UKIMWI gani mtu anatoa jasho namna ile?” Aliendelea kuongea, nilitaka kumuambia nilichokua nikiwaza lakini nilihofia, mimi kuongea ilimaanisha kuwashutumu watoto wake, kwa namna alivyokua anawapenda sidhani kama angeniamini.
“Tatizo mwanangu mbishi kama nini? Anajifanya kashika dini lakini huyo mtoto watamuua, unafikiri wanafurahia namna anavyowapenda na namna alivyokaribu na ndugu zake!” Sikuchangia neno zaidi ya kusema kweli, kila lipokua akiongea nilikua namkubalia.
“Hao watu wabaya sana. Kuna makabila si ya kuoa, nilishamuambia. Hivi unajua wanaua waume zao!” Aliongea, sikumuelewa alikua anamaanisha kabila gani.
“Nani hao?” Niliuliza kwa wasiwasi, Bibi alikua anaongea mambo ambayo hayaeleweki.
“Si huyo mke wake, wanaua wanaume kwasababu ya mali, mwangu asipokua makini basi watoto wote watapuputika na atafuata yeye….”
“Unamaanisha nini Bibi?” Niliuliza, nilishajua mtu aliyekua akimlenga lakini sikutaka kuamini kua alikua anawaza hivyo, nilitaka kusikia maneno yanamtoka mdomoni mwake.
“Huyo mke wake, unafikiri mtoto anaumwa tu hivi hivi? Huyo mwanamke ni shetani, anataka kuwatesa watoto ili tu kumteka mtoto wangu, tumeshamuita kikao na kumuambia lakini hasikii. Hivi wewe huoni siku hizo walivyo karibu, huoni namna ambavyo kila kitu wanafanya pamoja. Ndugu zake hawataki teana, kila kitu ni yeye na mke, kujifungia chumbani kila siku, hata mimi Mama yake kuja kuniona inakua shida!” Bibi alikua analalamika kidogo kutoa machozi, nilimuona anaumia lakini sikuelewa kile kilichokua kikimuumiza.
Kwa namna alivyokua anaongea ni kama alikua anaamini kua Mama alimloga mwanae ili kumteka Baba. Ule ukaribu wa Baba na Mama baada ya Aziza kuanza kuumwa ulionekana kuichanganya ile familia, walionekana kuhisi labda Mama alifanya vile baada ya kuona anataka kuachwa na Baba anawasikiliza zaidi ndugu zake. Kwa namna alivyokua akiongea kama usingekua uanwajua ungeweza kudhani kua ni kweli, mimi sikutaka kuamini, nilijisikia vibaya hata kumsikiliza na kuamua kutoka zangu. Nilijifanya naenda kuandaa chakula na kutoka, nilimaucha Bibi bado akilalamika na kuongea peke yake.
***
Mwanzo wa ugonjwa akina Shangazi walikua hawapendi kuja pale nyumbani, walijiweka mbali sana na Baba, lakini ghafla niliona wanaanza kuja, walikua wanakuja na wakati mwingine hata kulala. Lakini cha cha ajabu nikua hawakua wakienda hata kumuona mgonjwa, ingawa hali ya Bibi haikua mbaya lakini muda mwingi walikua wakitumia chumbani kwa Bibi na mara kadhaa walikua wakimuita Baba na kukaa naye huko kwa muda mrefu.
Sikua najua wanafanya nini kwani sisi wengine ni kama tulitegwa flani. Niliona undugu wao unarudi vizuri na kuanza kushikana kama zamani, hapo ndipo nilijua nguvu ya Bibi kwani niliona wanaanza kumtenga Mama. Ingawa yeye ndiyo alikua anahudumia mtoto lakini maamuzi mengi alikua anafanya Baba na ndugu zake, kuna wakati Baba alitaka kumtoa mtoto pale nyumbani na kumpeleka kwa Mama Abdul lakini Mama alikataa, ilileta ugomvi mkubwa lakini Mama alishikilia kidedea na kusema mwanae haondoki. Baba alinywea na kuacha mambo yaendelee kama kawaida.
“Si nilikuambia, mwangu kapikwa na kapikika, mtoto wakwke lakinia napangiwa na mwanamke! Huyu mwanamke anajua kua huyo mtoto akipona ndoa hana, lakini anajidanganya, ngoja wamuue mjukuu wangu ndiyo atajua!” Bibi aliniambia.
“Na sasa unaondoka, nataka ukaishi kwa Shangazi yako, si anaona anaweza kumlea yeye mwenyewe basi tutaona!” Bibi aliniambia, nilijaribu kumbishia lakini aliniambia ni kitu cha muda.
“Amekataa kusaidiwa hivyo kama wewe ni mfanyakazi wangu sitaki umsaidie, nialazima atusikilize sisi na hata huyo Nesi wake hawezi kuendelea kukaa hapa!”
Nilishindwa kumuelewa Bibi, kichwani naamini alikua anaona kama anasiadia, alikua anataka niondoke pale nyumbani ili Aziza kukosa mtu wa kumhudumia na Mama yake kukubali akina Shangazi wamchukue. Sijui lilikua ni wazo la nani lakini Baba alilikubali na kweli siku iliyofuata nilifungasha virago vyangu na kuondoka, wakati naondoka Nesi ambaye alikua akija asubuhi na kuondoka jioni naye alikua anakuja. Alirudishiwa getini na kuambwia hahitajiki tena, yote hayo alifanya Baba.
“Kwahiyo unataka mtoto abaki na nani? Vipi Mama nani atamhudumia?” Mama alimuuliza.
“Mama yangu niachie mwenyewe, hakuhusu ila mtoto ni yaako, wewe si ulisema ndiyo Mama yake unaweza kumhudumia basi mhudumie.” Baba aliongea na kuingia kwenye gari yake na kuondoka, ilikua ni asubuhi lakini kina Shangazi walishakuja, walijifanya kwenda kumhudumia Mama yao. Mama hakubisha chochote, nilimuona anarudi ndani, hakuenda tena kazini na mimi niliambiwa kuondoka pale.
Kazi yangu ya kuwa kiraka ilienda kwa Mama Abdul, kwangu ile ilikua ni adhabu kubwa, kuna wakati nilikua natamani kuondoka lakini nilisita, mbali na ukweli kuwa sikua na pesa ya kuanzia maisha lakini pia nilikua nishashikana na ile familia, nilijiona sehemu ya familia na niliona kuondoka ni kama kuwasaliti hasa Mama ambaye nilitokea kumpenda kwa namna alivyokua ananichukulia kama mdogo wake, lakini niliamini kua kwa hali yake ananihitaji.
Nilifanya kazi pale kwa miezi miwili, hali ya mtoto ilikua inazidi kuwa mbaya siku hadi siku. Mama yake ndiyo alikuaa kimhudumia na kila siku walikua wakigombana kwani Baba na ndugu zake walitaka kumchukua lakini yeye alikataa. Alilazimika kuomba likizo ya muda mrefu ili kumhudumia mwanae kwani kila mfanyakazi aliyekua akimtafuta walikua wakimfukuza. Nilikua naongea naye kila siku ili kuniambia hali ya mtoto na mara nyingi tu nilikua natoroka na kwenda kumuona nyakati za mchana sikujali kupoteza kazi.
Katika kipindi chote ambacho Aziza alikua anaumwa alikua bado hajaanza kutumia ARV, pamoja na kua katika hali mbaya lakini CD4 zake zilikua juu sana kiasi kwamba ilikua inshangaza, hata madaktari walikua hawalewi ni kwanini mtu aliyezidiwa namna ile bado kua na CD4 nyingi vile. Lakini ghafla zilianza kupunguana walipendekeza aanze kutumia ARV. Nakumbuka ilikua siku ya Jumamosi, nilikua tu nyumbani na kwakua siku hiyo kila mtu yuko nyumani sikuweza kutoroka kumuona Aziza.
Mama Abdul alikuepo, wanae nao walikuepo, lakini mume wake alitoka kwenda kwenye biashara zake. Alianza kuja Baba na kisha akafuatiwa na Karim aliyekua ameongozana na Shangazi, Mama Aziza. Ungeweza kudhani wana kikao au wamepanga. Niliwakaribisha na kwenda kuwaletea juice. Baada ya kuwapa walianza kuongea kwa kumuuliza Baba hali ya mtoto.
“Hali si nzuri, leo tumempeleka hospitali lakini hamna kitu anazidi kuzidiwa.” Baba alijibu, alionekana kuchanganyikiwa sana.
“Haya mambo si ya hospitali, kuna mchezo unachezewa Kaka, hivi huoni ni kwanini anang’ang’ania kubaki na mtoto utafikiri alikuja naye. Ugonjwa wake ndiyo pona yake, alishajua hakuna ndoa kaamua kumtumia mtoto. Sisi wanawake tuna mbinu zetu!” Mama Aziza aliongea, kusema kweli nilishangaa, kwa namna alivyokua anaongea ni kama alikua anaamini kile alichokua akikizungumza. Sijui lakini familia nzima ilikua kama inaamini kua Aziza kalogwa na aliyemloga ni Mama yake.
“Mimi hata sijui ndugu zangu, nimeshindwa hata chakuamini, kila mtu ananichanganya. Namuachia Mungu kwa sasa, tumetoka hospitalini wamesema anze kutumia ARV….” Baba aliongea kwa majozni.
“ARV? Kivipi, mmesha mpa?” Mama Abdul aliulizia kwa mshituko, kwake ni kama alikua amesikia kitu cha ajabu. Alishtuka mpaka wengine walibaki wanamshangaa.
“Nini? vipi?” Karim alimuuliza kwani baada ya kusikia lile neno ni kama alikosa raha, alishindwa kukaa na kua anageuka geuka.
“Sijisikii vizuri nakuja.” Aliongea na kunyanyuka akatoka nnje, nilitaka kutoka kumfuata lakini nilisita, kwa nilipokua nimesimama nilimuona akitoka na kusimama, alitoa simu na kupiga kisha akaweka sikioni. Alikua usawa jiko hivyo nilienda jikoni na kusogea dirishani ili kumsikiliza. Kuna kitu kiliniambia msikilize hasa kutokana na namna alivyostuka nilijua tu kuna kitu anaficha.
“Mimi sijui, Kaka ndiyo kasema wamepewa ARV, sijui kama washampa au la? Wewe si ulisema CD4 zake hazitashuka ni dalili tu?” Sikujua alikua anaongea na nani kwani sikuweza kumsikia mtu wa upande wapili lakini moja kwa moja nilijua kua anamzungumzia Aziza na zile taarifa za Baba.
“Sikusema nataka afe, nilisema nataka kumtesa tu ili kumkomesha yule mwanamke!” Aliongea, nilijisogeza karibu ili kusikia zaidi.
“Siwezi kumuambia, ndugu zangu wakijua si watanitenga, huwezi kufanya chochote?” Aliendelea kuuliza kwa hasira, kila alipokua akiongea alikua akizidi kupunguza sauti hivyo mimi kupata shida kumsikia. Alikata simu nikiwa sijaelewa nini kinatokea, alirudi ndani lakini hakukaa, alikuja pale jikoni na kukaa kwenye kiti, hakuniona kwani nilikua kwa upande wa pembeni kidogo, sikujificha lakini kwa namna ile nyumba ilivyokua asingeweza kuniona.
Alikaa kwa sekunde kadhaa na kunyanyuka, alitoka lakini hakukaa tena, alirudi tena na kukaa, alitoka na kurudi tena. Alikua kama mtu aliyechanganyikiwa anatoka na kuingia anatoka na kuingia, ilinifanya hata mimi kushindwa kutoka pale nilipokua nimesimama kwani sikutaka ajue kua nimemsikia. Kuna wakati alitoka na kukaa kwa muda, nikajua kua harudi tena, lakini sikutaka kutoka mlango wa mbele, nilifungua mlango wa nyuma ili kutoka.
Lakini kabla ya kutoka nnje nilisikia mlio wa meseji, niliangalia simu yake alikua ameisahau juu ya meza ya jiko, sijui kwanini lakini nilienda kuiangalia. Kwa bahati nzuri ilikua bado haijajifunga na meseji ilikua inaonekana kwa juu, sijui ilitoka wapi lakini iliandikwa. “Hakikisha hamywi hizo dawa akinywa tu anakufa na mimi sitahusika uliyataka mwenyewe.” Namba ilikua imeseviwa jina la “Babu Chamanzi.”
Halikua jina geni kwangu, nilikua namfahamu ni Babu mmoja hivi ambaye hata pale nyumbani alishakuja na mara nyingi wakati akija walikua wanajifungia chumbani kwake. Mwanzo nilihisi anatembea naye lakini haikuingia akilini mpaka siku ile nilianza kuhisi kua ni Mganga wa kienyeji. Kichwa kilianza kuchanganya nifenye nini, nilitamani kwenda kumuambia Baba lakini nilijua hataniamini na itanichelewesha, nilichukua simu yangu ili kumpigia Mama kumuambia kua asimpe mtoto dawa.
Sikujua hizo dawa zina madhara gani lakini niliamini ni mambo ya kishirikina, nilimpigia Mama simu lakini alikua hapatikani, laini laini moja ilikua haipatikani na nyingine iko bize, nilipiga simu ya Bibi nayo ilikua imezimwa. Hapo nilianza kuchanganyikiwa, nilishapaniki, simu ya watu nimeishika mkononi, niliwaza kwenda kumuambia Baba na kumuonyesha ile meseji au nifanye nini? Akili ilifanya kazi haraka nikajisemea hata akiiona kama Mama akimpa dawa Aziza haitakua na maana tena, nilipiga tena sasa hivi simu ikaanza kuita.
(ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA; Hli ya Aziza ilizidi kuwa mbaya, mimi nilihamishiwa kwa Mama Abdul, nikiwa pale Baba anasema Aziza kashepewa ARV ili aanze kutumia, Mama Abdul anashtuka na kwenda kuongea na simu, nasikia anaongea na Mganga wanasema akinywa tu ARV anakufa. Nampigia Mama ili kumuambia. Je nini kitatokea…ENDELEA)
Simu ilipokelewa, lakini kabla sijaongea chochote wala hata kujua ni nani alipokea, Mama Abdul aliingia, aliniona nimesimama nimeshikilia simu yake. Nilishtuka sana akumuona kidogo nidondoke.
“Simu yako ilikua inaita, sijui ni nani?”Nilijiongelesha huku nikimnyooshea simu yake. Nilikua natetemeka kama vile nimemwagiawa maji ya barafu. Lakini hata yeye alikua na kimuhemuhe chake, kwa kumuangalia ni kama vile hakuniona ingawa alinyoosha mkono na kuichukua simu yake.
Nilimkabidhi harakaharaka akatoka, nilirudi katika simu yangu ili kuongea na Mama lakini simu ilishakata, nilijaribu kumpigia tena lakini namba ilikua bize. Nilijikuta napaniki na kuona njia bora ni kumuambia Baba ili yeye kuamua anachokifanya.
“Poteli yambali hata nikifukuzwa kazi!” Niliwaza huku nikitoka, nilifika sebuleni na kuona bado wanaongea.
“Unasema nini? Unamaanisha nini mbona sikuelewi?” Baba alikua akimuuliza Mama Abdul ambaye bado alikua amesimama.
“Nilikua naongea na simu hapo nnje, kama mwanao UKIMWI ni wakutumiwa akinywa hizo dawa anakufa! Kaka ongea na mke wako, haya mambo ni yakweli yapo, nina rafiki yangu yalishamkuta!” Aliongea kwa wasiwasi, ingawa nilitamani kuongea ukweli lakini kwa namnaalivyokua anaongea ni kama alikua anataka kusaidia. Nilijua kama nitawakatisha na kuwaambia kua yeye ndiyo alihusika basi kungezuka mjadala na pengine wasingemuwahi mtoto.
“Nikweli Baba, hata mimi nilishawahi kuona, kule kijijini kwetu ilishatokea.” Nilijikuta nasema ili kuonyesha msisitizo kwani Baba alionekana hataki kuamini.
Baada ya kumuambia alipaniki kidogo, alichukua simu lakini kabla ya kuipiga iliita.
“Mama anapiga…” Aliongea huku akiiangalia simu. Ni kama alikua anauliza kama apokee au aache kwanza ampigie mkewe ili asimpe mtoto dawa.
“Si yuko nyumbani, mpigie aongee na wifi.” Mama Aziza aliongea, naye alionekana kupaniki, kwa namna flani walionyesha nyuso za kujali. Baba aliipokea ile simu, Bibi alionekana kumuambia aende nyumbani kuna kitu lakini yeye alisisitiza kuambiwa ni kitu gani, kwanza alitaka kuongea na mkewe lakini aliambiwa hapana.
Walikaa kama wanabishana kitu kisha akanyamaza, sekunde kadhaa Baba alikaa chini, alionekana kuishiwa nguvu. Walimzunguka na kumuuliza ni kitu gani?
“Aziza hatunaye.” Baba aliongea kwa kifupi, nilikua kama vile sikumuelewa, nilitaka arudie lakini hakikua nafasi yangu kuongea, nilisubiri wamuulize tena lakini niliona kama vile wameridhika na majibu yake.
“Mama alitaka niende nyumbani, kama nusu saa iliyopita hivi.” Baba alijiongelesha mwenyewe, nilijikuta naishiwa nguvu na kukaa chini, akili yangu ilikua inapiga mahesabu ni muda gani wamempa hizo dawa.
Nilikua nawaza labda ningewahi, labda simu ingepokelewa! Niliwaza sana lakini kila mahesabu niliyokua nikipiga niliona kua mpaka mimi najua basi angekua tayari ashakunywa zile dawa. Nilitamani kunyanyuka na kuwaambia ukweli, nilitamani kumnyang’anya Mama Abdul simu ili kila mtu aone unyama wake lakini nilijua isingesaidia, kwa matukio ambayo nilikua nimeyashudhuia katika ile familia niliamini watageuza mambo na mimi kuonekana mnafiki.
Nilikaa chini kabisa, sikuweza kunyanyuka mpaka nilipoambiwa nibaki na watoto kwani wao wanaondoka, Baba alikua halii lakini alionekana kama kachanganyikiwa flani, alikua anajisemea semea mambo mengi, walikua wakimpa moyo na kumfariji lakini hakuonekana kupata kanafuu kokote. Waliondoka na kuniacha pale, nilijua nisingeweza kuondoka kwani nilitakiwa kubaki na watoto, roho iliniuma sana kwani wakati huo nilitamani kuwa katika ile nyumba, nilitamani kuwa karibu na Mama kwani nilijua kila mtu atamtenga.
Lakini mimi nilikua mafanyakazi tu, sikua na maamuzi yoyote na hakuona hata kama na mimi nina uchungu. Kutokana na taratibu za kiislamu mazishi yalikua ni siku inayofuata, hakukua na kucheleweshwa. Nilongea na Shangazi kumuomba kama naweza kwenda alinijibu tu kwakifupi.
“Tutaangalia kama kutapatikana mtu wa kukaa nyumbani, hatuwezi kuiacha nyumba peke yake.” Sikua na chakusema zaidi ya kunyamaza tu, hiyo ilikua ni moja ya adha ya kuzaliwa masikini na kufanya kazi kwa watu, kila mtu anakuangalia kama vile huna hisia.
Siku ya mazishi kila mtu aliondoka, mimi pekee ndiyo nilibaki nyumani, nilikua nalia tu mpaka ilipofika kwenye saa tano hivi. Karim alikuja na Gari na kuniambia nipande twende, sikua hata na muda wa kujianadaa nilipanda kwenye gari na kwenda kwenye mazishi, kumbe Bibi aliniulizia na alipoambiwa sipo akaanza kulalamika mpaka nikalazimika kuchukuliwa. Nilifika na kwenda kukaa na Bibi ndani, hakutaka kukaa na mtu mwingine zaidi yangu.
Alikua ananiambia mambo mengi lakini yote yalikua ni kumshutumu Mama, bado alikua akiamini kua Mama alihusika katika kifo cha mwanae. Mama yeye hakua na hali nzuri, presha ilipanda na alilazwa hospitali, hakuweza hata kumzika mwanae. Baada ya mazishi niliendelea kubaki pale na Bibi, Mama bado alikua hospitalini, usiku wakati wengine wakiwa kwenye kuomboleza Baba, Mama Abdul, Mama Aziza na Karim walikua chumbani kwa Bibi.
Waliniambia nitoke kwani wanataka kuongea, nilitoka lakini sikuenda mbali, nilijua wanamsengenya Mama hivyo nilikaa nnje kidogo pembeni ya mlango. Nilikua nawasikia kwa mbali sana lakini ni kama walitaka Mama aondoke.
“Kuna kitu chako chochote anakijua?” Mama Abdul alimuuliza Baba.
“Hapana, hajui vilipo lakini kuna siku aliona lile begi la nyaraka zangu. Ila sijali, mimi sitaki kumuacha mke wangu, bado nampenda na sitaki kuamini kua hii ni kazi yake, mwanangu kafa kwa mipango ya Mungu.” Baba aliongea waliendelea kumuambia kuhusu uchawi wakatoa mifano mingi mingi lakini Baba hakuamini.
“Ninaweza kuwa na tofauti nyingi na mke wangu lakini kitu ninachojua nikua anawapenda watoto, siwezi kumuacha kwasababu hiyo, isitoshe nimepoteza mtoto mmoja lakini bado nina watoto watatu wakulea. Bado wanamhitaji sana Mama yao, sijui ni kwa namna gani wanaweza kupita katika hili tukio, namna wanaweza kupona kutokana na kifo cha mdogo wao bila Mama yao!” Baba aliongea kwa suti ya juu kidogo, wote walinyamaza kasoro Bibi ambaye alikua analalamika kua hamsikilizi.
Baba alionekana kukasirika na kuwaambia kua anawapenda lakini hawezi kuendelea kukaa pale na kumshutumu mke wake wakati yuko hospitalini.
“Najua nyie mnaona anaigiza lakini naamini katika mipango ya Mungu. Mimi sina UKIMWI, mwanangu hakubakwa lakini yule ni mtoto, vipi kama alikanyaga kitu cha chuma, vipi kama aliwahi kujikata, yuko na watoto shuleni vipi kama alichangia kitu na mtoto muathirika, vipi kama alikua shuleni akaumia na mwenzake muathirika akamgusa na damu zikachanganyika? Kuna maelezo mengi lakini mwisho Mungu kamchukua mwanangu, siwezi kukaa hapa kumshutumu mke wangu wakati najua anavyoumia.
Nilikua naye hospitalini, nilikua naye wakati namuuguza, nyie mlikua wapi? Hapana nampenda mke wangu na kamwe sitamfukuza kwasababu yoyote ile. Mama nakupenda sana na nazihitaji radhi zako sana, una pepo yangu miguuni kwako lakini siwezi kuendelea kumnyanyasa mke wangu namna hii, yeye si Mungu kuamua mtoto aumwenini!”
Hapo kila mtu alinyamaza, kwa namna Baba alivyoongea nilijikuta nasisimkwa kwa furaha, katika wiki mbili tatu kabla ya kifo cha Aziza Baba alikua upande wa ndugu zake, ni kama walimteka flani lakini nilishangaa ghafla amebadilika na kuwa upande wa mkewe. Ilikua ndiyo mara yangu ya kwanza kumsikia akimtetea mkewe namna ile mbele ya Mama yake.
“Isitoshe mke wangu ni mjamzito, Mungu akijaalia tutapata mtoto mwingine, Mungu kamchukua Aziza lakini naamini atatupa mwingine hivyo siwezi kushindana na Mungu na wala siwezi kumpa mke wangu mawaza na kumfanya apoteze mtoto mwingine.”
Hapo ndiyo nilihisi sababu ya Baba kuwa vile, kulikua na habari nzuri za Mama kuwa mjamzito. Kwa namana livyokua akiongea nilijua nilazima kamaliza hivyo anakaribia kutoka, sikutaka kuonekana mbea niliondoka pale mlangoni nakurudi sebuleni kakaa na watu wengine. Kweli alitoka, sikurudi tena mlangoni kumsikiliza. Nilikaa mpaka walipotoka wengine na kwenda na kukaa na Bibi, nilimuona kapaniki, kawa kama kachanganyikiwa, sikutaka kumuuliza sababu nilipanda kitandani kutafuta usingizi ambao hata haukuja.
****
Sikurudi tena kwa Mama Abdul, Baba aliniambia kubaki pale, alileta mfanyakazi mwingine hivyo tukawa wawili, kwaajili ya kumhudumia Bibi na Mama ambaye ingawa mimba yake ilikua bado changa lakini ilibadilisha kila kitu. Baba alibaidlika sana, alianza kumjali na alitumia muda mchache sana na ndugu zake, alianza kumshirikisha Mama kwenye mambo yake na mara kwa mara alikua akitoka naye, furaha iliongezeka katika ile nyumba.
Kuna nyumba ambayo Baba alikua akiijenga kisirisiri, ilikua kubwa sana ya ghrofa, aliikamilisha harakaharaka na kuhamia, kila mtu alishangaa kwani hata ndugu zake hawakua wakiifahamu. Kidogo ilikua mbali na mji mbali na walipokua wakiishi ndugu zake hivyo kule kuja kuja kwa kila siku kulipungua. Pamoja na watu kuwa na furaha lakini niliumia sana nilipomuona Mama Abdul, alikua akijifanya mwema kumbe ni shetani, hakua hata na aibu kwani alikuja pale na kujichekesha chekesha bila kukumbuka mambo aliyokua ameyafanya.
Karim alipata mchumba na alishajitambulisha, walishapanga mpaka tarehe ya harusi. Ndugu zake walionekana kufurahia na mara nyingi walipenda kumsifia mchumba wake mbele ya Mama ili yeye ajisikie vibaya, walikua wakiongea maneno ya shombo lakini Mama hakujali, alikua akiwaangalia tu. Hawakuongea kitu mbele ya Baba, tofauti na zamani ambapo wangeweza kumtukana Mama mbele ya Baba sasa hivi walikua na adabu kwani Baba alikua haeleweki, hawasikilizi sana kama zamani.
Siku moja nilitoka kanisani, mara zote siku za jumapili kwakua mimi ni mukiristo wananirhuusu kwenda kanisani, kuna kanisa nililokua nikisalia kipindi hatujahama, likukua karibu na nyumbani ambapo hakukua mbali na Mama Abdul, wakati natoka kanisani nilikutana na Abdul, yeye kipindi hicho alikua kidato cha pili, alishakua mkubwa. Alinisalimia, ingawa sikua nampenda kihivyo kutokana na dharau zake na maneno yake ya shombo kila ninapoenda kufanya kazi kwao lakini kama binadamu nilimuuliza kinafiki tu.
“Lini mnakuja kwetu kututembelea?” Nilimuuliza kwani tangu kuhamia kwenye nyumba mpya kama miezi mitatu hivi walikua hawajafika, Mama yake ndiyo alikua akija mara moja moja.
“Unajishaua unafikiri kwenu, wewe ni mfanyakazi tu unasema niwatembelee! Ile ni nyumba ya Anko wetu na akifa tunachukua sisi!” Aliongea maneno ambayo yalinishangaza, nilimuangalia na kumuonea huruma kwani alikua bado mdogo sana kuingia kwenye chuki za namna ile.
“Yametoka wapi hayo, mimi najua mfanyakazi kweli lakini hata wewe si kwenu, ile ni nyumba ya Anko wenu kweli lakini si ya Baba yenu, hata akifa leo ana watoto na sidhani kama nyie mna nafasi kwake!” Niliamua kumchana tu makusudi kwani nilikerwa na kile kitu.
“Utajua mwenyewe lakini yule ni Anko wetu, Shangazi asingemloga sisi ndiyo tungekua tunaishi pale na kwaataarifa yako pale hawatadumu tutahamia sisi na utafukuzwa kazi masikini mkubwa wewe!” Nilijikuta nacheka kwani nilimuona kama yuko keenye ndoto, aliongea maneno mengi ambayo yalionyesha kua anachuki na Shangazi yake pamoja na watoto wa Mjomba wake. Nilijua sababu ni Mama yao ambaye kila siku alikua akiwaambia kua wanashindwa kupata vitu vingi kutoka kwa Mjomba wao kwakua tu ana watoto na wao ndiyo wanachukua zawadi ambazo wangetakiwa kuchukua wao.
“Kwataarifa yako Mama kasafiri na akirudi mtakiona cha moto, nyie si majifanya mnajua kumloga Mjomba lakini Mama ndiyo kiiboko yenu!” Aliongea kwa hasira huku akiondoka, nikweli nilikua sijamuona Mama yake kwa muda kidogo lakini kwangu niliona kama kitu cha kawaida tena nilifurahi kwani sikupenda hata kuwaona. Lakini kwa namna alivyoongea nilihisi kitu, nikikumbuka na matukio ya nyuma nilijua kuna kitu Abdul kasikia Mama yake akikiongea, akili yangu niliipeleka kwa Mganga tu na nilijua lazima ameenda kufanya mambo yake tena.
Lakini sikua na ushahidi, niliamua kupuuzia, siku zilienda na mambo yalikua bado yamepoa. Siku moja Baba likua amesafiri alikua ameenda Marekani kikazi, ilikua ni safari ya miezi miwili, pale nyumbani nilibaki mimi, Mama na Bibi pamoja na mfanyakazi mwingine. Watoto wote walikua shuleni kwani walihamishiwa bweni. Ilikua ni usiku nakumbuka nilikua sebuleni naangalia tamthilia, ilikua siku ya Jumapili hivyo kulikua na marudio ya tamthilia ya wiki nzima na mara nyingi kwakua siku nyingine nakosa muda wakuangalia Jumapili nakesha kuangalia.
Nilisikia kelele kutoka chumbani kwa Mama, nilinyanyuka na kwenda, alikua akipiga kelele sana. Damu zilikua zinamtoka sehemu za siri, nilihisi kabda kapata uchungu au nini kwani nilikua sielewi elewi. Muda wa kujifungua ulikua bado haujafika nilimsogelea kumuangalia aliniambia nimpigie simu Dereva wa Baba ambaye mara nyingi Baba akiwa hayupo hutusaidia, nilimpigia na kumuambia kua Mama anamwa sana.
Wakati tunamsubiri Dereva nilimsafisha Mama, damu zilikata lakini alianza kutokwa na maji sehemu za siri, yalikua ni maji mengi ambayo yaliloanisha mpaka godoro. Bado alikua akipiga kelele za maumivu, nilijirahidi kumsafisha lakini maji yalikua hayakauki. Dereva alikuja na kutusiadia kumnyanyua vilevile bado akitokwa na maji, nililazimika kuchukua blanketi kubwa na kulitandika kwenye gari ndipo tukamlaza.
“Kuna nini kwenye gari mbona kuna harufu hivi? Nilimuuliza Dereva, alikua hajashtuka lakini baada ya kumuuliza alishika pua.” Kabla ya kunijibu nilishtuka na kukumbuka ile harufu, akili ilinijia siku ya kwanza Aziza alipoanza kuumwa, siku niliyogundua kua anaumwa nilisikia ile harufu ambayo ilikua ni kama ya kinyesi. Mama naye aliisikia na wote tulijikuta tunaangaliana na kusema.
“Azizaaa!” Harakaharaka nilinyanyua nguo aliyokua mevaa na kumnyanyua mkono kuangalia kuona kama alikua na kidogo kama cha marehemu.
(ILIPOISHIA SEHEMU YA SABA; Mama ni mjamzito, anaanza kuumwa na anapata dalili zote alizokua Aziza kipindi anaumwa. Wote tunakumbuka na kuangaliana, je nini kitatokea?” ENDELEA…)
“Mama usiende hospitali utakufa!” Nilimuambia wakati nikimsaidai kukaa, dereva alishakaa kwenye usukani na kuwasha gari. Mama alinisikia lakini alinyamaza na kana kwamba vile hajanisikia. Nilijua ni kutokana na maumivu hivyo nilirudia tena kumuambia asiende hospitalini na kama anataka kupona basi aende kwa mganga yeyote anayemfahamu. Alionyesha akukataa, nilijikuta nakasirika na kutamani kumuambia nilichokua nikikijua.
Lakini niliona haukua wakati muafaka, dereva alikua pale na sikua nikimuamini sana.
“Basi twende kwenye maombi, utakufa Mama?” Nilimuambia lakini bado alibisha, alimuambia Dereva ampeleke hospitalini, nilikua nimepaniki sana kwani alikua hanielewi na kwa mambo niliyokua nikiyajua nilijua lazima ile ni kazi ya Shangazi.
“Mama kwa imani yako, twende hata kwa Shehe yeyote yule lakini si hospitali.”
Hapo alikubali ingawa kwa shingo upande, alikua akimuangalia Dereva kwa wasiwasi ingawa mimi sikuona chochote cha yeye kuhofia.
“Kuna Ustadhi mmoja yuko Mtoni mtongani, alikua anamsomeaga Aziza kinapoapoa.” Aliniambia, nilimuambi Dereva kutupeleka, nilichukua simu yake na kuchukua namba ya yule Ustadhi nikampigia, kwa bahati nzuri alikua nyumbani hivyo alimuelekeza Dereva kwake kwani mama alikua katika maumivu makali sana kuweza kumuelekeza.
Tulifika akatupokea vizuri, alimsomea kwa zaidi ya masaa mawili maumivu yalikata na maji kuacha kutoka ingawa bado harufu ilikua inasikika. Aliendelea kusoma na kusoma, mimi nilikua nnje na kila baada ya lisaa limoja alikua akipumzika na kurudi kumsomea. Nikiwa pale nnje simu yangu iliita, alikua ni Baba mdogo, Karim.
“Mko hospitali gani?” Aliniuliza, nilishtuka kwani nilikua sijamuambia mtu yeyote kua Mama anaumwa, hata ndugu zake sikuwaambia.
“Sisi…” nilijikuta na aanza kubabaika babaika.
“Ndiyo nyinyi kwani wewe si ndiyo umeondoka na shemeji anaumwa!” Niliwaza mara mbili kuhusu kumuambia nikasema hapana, nikimuambia nilazima ataenda kusema kwa ndugu wengine na Mama Abdul ambaye ndiyo nilikua na uhakika kua amemfanyia vile Mama angejua.
“Mimi hapa sipajui, ngoja nimtafute Dereva nakupigia.” Nilimuambia na kabla hata hajanijibu chochote nilikata simu na kuizima kabisa. Niliwaza sana nikifikiria ni kwa namna gani alikua amejua kua Mama anumwa.
“Bibi!” Nilijisemea, nilikumbuka kua wakati tunaondoka tulimuacha nyumbani. Nilimfuata dereva na kumuambia kua pale tumekuja kisiri hivyo azime simu yake kwani anaweza kuulizwa.
“Unamjua Baba, akijua umemleta mke wake kwa waganga basi itakula kwako!” Nilimuambia kwa kumtisha, sikutaka aongee na kwa hali ya Mama nilijua kua angeweza kupona na hilo ndiyo lilikua muhimu kwangu.
Nilijua watampigia simu na kweli kabla hata sijamaliza kuongea naye simu yake iliita, alikua ni Mama Abdul.
“Washaa mbiana!” Niliwaza, dereva alikua anikiangalia kama vile ananiuliza apokee au afanye nini?
“Usipokee, iache iite mpaka ikatike, wakija kukuuliza utawaambia uliisahau simu kwenye gari wakati unasaidia kumbeba Mama.” Alinielewa na kuiweka vibration kisha akawa ameishikilia tu, hakupokea tena ingawa ilipigwa kwa zaidi ya mara ishirini na meseji nyingi kutumwa.
Tulikaa pale nnje kusubiri muda ulikua unaenda na hali ya Mama ilikua haijatengamaa kabisa lakini alikua hayuko kwenye maumivu tena. Mimi na dereva tulikua nnje kwani nyumba ya yule ustadhi haikua kubwa sana na hatukushiriki kwenye maombi yao. Tukiwa pale nilishangaa Mama akitoka, alikua anatembea mwenyewe hakuwa na maumivu ingawa bado harufu ilikua inasikika.
“Tuondoke, nipelekeni tu hospitali.” Aliongea kwa huzuni, alionekana kabisa hakupenda kile kitu ni kama vile alilazimishwa, nilijaribu kumuambia bado anahitaji kuombewa na kile kitu si cha hospitalini lakini hakujali, alinilazimishia kua tuondoke. Sikumuelewa kabisa na sikua tayari kumuona akipoteza maisha yake. Nilimshika mkono na kumvuita kwa nyuma na tukiwa tumesimama pale nilimuambia.
“Ni Mama Abdul kakufanya yote haya, nina ushahidi, yeye ndiyo kamuua mwanao na anataka kukua wewe kwa sababu ya mali.” Nilimuambia, hakuonekana kabisa kushtuka, ni kama ni kitu alikua anakijua, lakini pamoja na kumuambia hivyo aliendelea kusisitiza kuondoka.
“Siku ile nilikupigia.” Nilimuambia.
“Siku gani?” Aliniuliza.
“Siku Aziza alipofariki, nilkikupigia simu ili kukuambia usimpe hizo ARV, nilimsikia Mama Abdul akiongea na Mganga wa kienyeji na niliona meseji ikisema kama mtoto akinywa ARV basi ndiyo mwisho wake.” Aliniangalia kwa kuduwaa kidogo, nilijua lazima atakasirika kwani labda ningeweza kumuambia mapema ningeokoa maisha ya mwanae.
“Sikua nikijua, mimi nilisikia wakati huohuo na kukupigia na wakati huo Baba ndiyo akapokea simu kua tayari ashafariki, nilichelewa tu kidogo nisamehe.”
Nilimuelezea kila kitu kilichotokea, nilijaribu kujitetea kutokuhusika kwangu na nilimuambia kuhusu maneno niliyoyasikia wiki moja nyuma wakati natoka kanisani na kukutana na Abdul.
Kumbe ndiyo Maana alikua anaomba msamaha.” Alijiongelesha mwenyewe, sikumuelewa alikua anamzungumzia nani lakini niliogopa pia kuuliza.
“Alikua anasema Shangazi nisamehe, Shangazi nisamehe! Nilijua tu ni wao wameniuliza mwanangu.” Alijisemesha, kwakusikia hivyo nilijua alikua anamzungumzia nani, sikutaka kumdododa dodosa kwani nilijua yuko kwenye maumivu makali ya yeye kuumwa na kumbukumbu za mwanae.
“Tuondoke!” Aliongea tena, sikumulewa, hata baada ya yote yale lakini bado alitaka kuondoka pale, kuondoka sehemu pekee ambayo nilikua namuona kama anapata nafuu. Nilimzuia na kumuuliza kwanini anafanya hivyo. Alitoa simu yake na kunionyesha namba ya mwisho kumpigia simu, ilikua ni namba ngeni ya nnje ya nchi.
“Mume wangu kanipigia, Baba Mod kaniuliza niko wapi nikashindwa kumdanganya nimemuambia nasomewa ameniambia niondoke kwani hii ni shiriki na hataki niifanye.”
Nilijikuta napadwa na hasira na kutaka hata kumtandika makofi, yeye ndiyo anaumwa, mwili wake lakini aruhusu kupangiwa na mtu ambaye yuko Marekani.
“Mdogo wangu siku ukiolewa ukiwa na mume wako utakuja kunielewa, mume wako akisema kitu hataki inamaansiha kua hataki, tuondoke.” Aliongea kama kilikua ni kitu rahisi sana kwake kukifanya, nilimuangalia bila kumuelewa lakini sikua na namna zaidi ya kufuata maelekezo ya bosi wangu. Kusema kweli sikumuelewa kabisa kwani bado alikua hayuko sawa.
“Nipeleke hospitali, mume wangu kasema niende huko.” Aliongea kwa kifupi, dereva hata yeye alishanaga lakini hakua na cha kusema, alikua mfanyakazi kama mimi na kazi yake kubwa ilikua ni kufuata maelekezo ya bosi wake. Tulimpeleka hospitalini ambako nako hawakua na hata cha kumtibu, walimpima vipimo vyote na kumuambia kua yeye yuko salama lakini inaonekana tatizo liko kwa mtoto ambaye bado alikua tumboni, waliamua kumlaza kwa uchunguzi zaidi.
Hapo ndipo nililazimika kuwapigia simu, nilimpigia Baba mdogo na kumuambia tulipo. Alinigombeza sana, akanitukana sana lakini sikujali, akili yangu ilishachoka, nilishaichoka ile familia na kwa wakati huo nilikua tayari kwa lolote. Wote walikua pamoja kwani wakati naongea Mama Abdul alimnyang’anya simu na kuniambia niende nyumbani kumhudumia Mama yake kwani haikua kazi yangu kupeleka wagonjwa hospitalini, sikua na namna zaidi ya kuondoka.
***
Mtoto alikua anapumua vizuri tumboni lakini ile harufu walihisi labda kuna tatizo ndani, kwakua muda wa kujifungua ulikua umebaki kidogo na mapigo yalikua vizuri, mtoto alikua anacheza vizuri na baada ya kumpima walimuambia yuko vizuri aliambiwa kuvumilia mpaka kujifungua ili wajue tatizo ni nini. Mama hakua na tatizo jingine lakini kutokana na hali yake walikubaliana abaki hospitalini. Baba alikua amebakiza kama wiki mbili kurudi nyumbani.
Pamoja na kwamba Mama alinikataza na kuniambia kua Baba hataki mambo ya kishrikirina lakini sikutaka kutulia, alionyesha matokeo makubwa kwa yule Ustadhi hivyo mara kwa mara nilikua nikienda kumuomba amuombee Mama hata kwa mbali. Kusema kweli nilikua naogopa sana na mara nyingi nilikua nikijilaumu kwakua sikufanya chochote wakati wa Aziza.
Mama Abdul na ndugu wengine walikua wakija hospitali, walijifanya kujali kabisa na wao ndiyo walikua wakimpa Baba ripoti zote, sikujua malengo yao lakini mimi nilikatazwa kwenda hospitalini kwa kisingizio kua nibaki na Bibi. Kwakua ndiyo ilikua sababu ya mimi kuajiriwa na sikutaka kuipoteza kazi yangu nililazimika kufuata mashariti yao kwani ningekua mkaidi ingekua rahisi kunifukuza kwakua hakukua na mtu wa kunitetea.
“Siku ile mlienda wapi? Mama Abdul aliniuliza.
“Siku gani?” Nilijifanya kutokuelewa ingawa nilishajua aliua anamaanisha siku ambayo Mama aliumwa na kwenda kwa ustadhi.
“Siku wifi yangu alipoumwa, kuna sehemu mlienda, ni mtaalamu gani mlienda kwake. Dereva kaniambia lakini yeye hakuingia ndani nakuuliza wewe kwakua uko karibu sana na yeye, mlienda wapi?”
Sijui kwanini lakini alionekana kuwa na wasiwasi sana, niliona na kuhisi kabisa kua kuna kitu hakikua sawa kwake. Nilinyamaza kujifanya kama sielewi hayo mambo, hakuongea kwa ukali kama kawaida yake ya kutishia kunifukuza kazi, aliongea kama vile anabembeleza, ilionekana kama kuna kitu muhimu kinamsumbua.
“Mimi sijui ni wapi, Mama alimuambia Dereva kutupeleka lakini mimi sijui, nilikaa nnje na Dereva Mama akaingia ndani.” Ilinibidi kudanganya.
“Aliingiaje ndani wakati alikua anumwa?”
“Mimi sijui, yeye si walimbeba, tulimbea mpaka ndani ndiyo tukatoka.” Nilijichanganya changanya kwani sikua na majibu ya uhakika, ni kitu ambacho nilikua sijakiwaza kwani sikudhani kama anaweza kuwa na ujasiri wa kuniuliza.
“Wewe kaa tu upande wake, akiondoka hapa nawewe utaondoka!” Aliongea baada ya kuona kua sitaki kumuambia kitu, mpaka wakati huo sikujali kama nitafukuzwa kazi au la.
“Kwanini unauliza, kwani alifanya vibaya kwenda huko?” Nilimuuliza huku nikimkazia macho, aliona aibu na kujifanya kunichimba biti kua niwe na adabu, alijiongelesha ongelesha na alipoona sijali aliondoka.
Nilishtuka kidogo kwani muda wa Mama kujifungua ulikua umefika na nilijua labda kuna kitu kilikua kimetokea. Sijui ni nini kiliniingia lakini niliingia chumbani kwa Mama na kuchukua nguo yake, kwakua nilikua na imani tofauti na niliamini kua Mungu ni yule yule nilichukua simu na kumpigia yule Ustadhi, nilimuambia kabisa kua Mama anakaribia kujifungua hivyo naomba amuweke kwenye maombi.
Baada ya hapo nilienda kwa mchungaji wangu, nilimuelezea kila kitu na kumuuliza kama ni vibaya nikimuombea Mama ili ajifungue salama kwa imani yangu wakati yeye akiombewa kwa imani yake. Aliniambia hakuna shida kwani Mungu tuneyemuomba ni yuleyule na Mungu huangalia nafsi ya mtu. Nilimpa nguo ya Mama ili aiombee akaniambia hakuaa shida Mungu anaweza kufika popote, hahitaji nguo wala chochote anachoangalia ni imani yako.
Tulipiga magoti na kuanza kuomba, tuliomba kwa lisaa lizima na mchungaji akaniambia kua inatosha Mungu atajibu kwa wakati wake na atampa kile anachoona kinastahili. Nilitoka na kuanza safari ya kwenda nyumbani, lakini wakati natoka nnje tu simu yangu iliita, niliangalia na kuona alikua ni Mama, nilijikuta natetemeka na kupata hofu ya kuipokea simu yake. Niliogopa sana kwani sikudhani kama hata ni yeye ananipigia. Lakini nilijipa moyo na kuipokea.
“Nashukuru Mungu katupa Aziza mwingine.” Ilikua ni sauti ya Mama, aliniambia kua mimi ndiyo mtu wa kwanza kumuambia,
“Hata Baba yake sijamuambia, sijui kwanini lakini nimeona nikuambie wewe.” Mtoto alizaliwa tena akiwa salama na afya tele, tofauti na madaktari walivyodhani kutokana na hali yake kwamba labda atazaliwa na matatizo alikua yuko salama kabisa.
“Umejifungua saa ngapi?” Nilimuuliza.
“Kama nusu saa iliyopita, sijui niko vizuri siumwi chochote na harufu hakuna tena.” Aliniambia, alionekana kuwa na mshangao, pale pale nilijikuta napiga magoti na kumshukuru Mungu. Nilipomaliza nilirudi ndani na kumuambia Mchungaji habari njema.
Baada ya hapo nilichukua simu yangu na kumpigia yule Ustadhi na kumshukuru, nilimuambia kilichotokea naye alimshukuru Mungu. Nilirudi nyumbani kuendelea na kazi zangu, lakini nilipoingia tu sikujisikia vizuri, sikujiona sawa kabisa, sikuhisi kama ile nyumba ina amani, nilikua mzito sana kukaa pale na nilihisi kama kitu kibaya kinakaribia kutokea.
Baba bado alikua hajarudi hivyo akina shangazi walikua pale na nikama walitawala nyumba, walijihisi kama vile wako kwao na wao ndiyo walikua wakifanya maamuzi ya kila kitu. Niliwaona wakijiandaa, kuchangamka kumsubiri mtoto, kuandaa chumba, kununua vinguo na vitu vingine vingine vingi. Mimi sikua na amani, roho ilikua nzito kabisa. Mama alilala hospitalini siku moja kwaajili ya uangalizi, kutokana na hali yake wakati anapelekwa walitaka kumuangalia kwanza kabla ya kumruhusu ingawa hakua na tatizo lolote wakati wa kujifungua.
Usiku mzima sikulala, ilipofika saa kumi na moja asubuhi niliamka na kujiandaa, sikua na ratiba ya kwenda hospitalini lakini nilitaka kwenda, kwa namna nilivyokua najisikia niliona kama kuna kitu kibaya kinakaribia kutokea. Niliondoka kimya kimya bila kumuoga mtu yeyote, nilienda mpaka hospitalini na mlango ulipofunguliwa nilikua ni mtu wa wakwanza kuingia, Mama alishangaa kuniona pale.
“Huna ndugu yeyote hapa Dar wakuishi naye?” Lilikua ni swali langu la kwanza tu baada ya kumuona, sikutaka hata kumuona mtoto, nilikua kama vile niemchanganyikiwa flani.
“Mtoto kalala, unataka kukaona?” Aliniuliza bila kujibu sawali langu.
“Sitaki!” Nilimjibu kwa hasira kwani niliona kama vile ananipotezea muda.
“Wanakuja kukuchukua, lakini sitaki uingie katika ile nyumba nakuuliza je huna ndugu yeyote hapa Dar wa kwenda, mtu ambaye anaweza kukuhudumia kwa muda?” Nilimuuliza kwani kusema kweli walikua wanakuja rafiki zake na abadhi ya ndugu zake lakini sikua nikiwafahamu vizuri.
“Ninaye, kwanini unauliza?” Alionekana kuwa na wasiwasi kidogo.
“Watakufanyia vitu vibaya, wale watu siwaamini, nenda huko kakae mpaka mwanao akue.” Nilimuambia lakini alionekana kutolipenda wazo langu, nilimshawishi sana mpaka akawa kama amekubali kisha akasema.
“Mume wangu sidhani kama atakubali, sijui kama atataka kuona naondoka naiacha nyumba, kwamba nitamuambiaje, Dada yake mchawi?”
Nilimuambia nikijaribu kumshawishi lakini hakukubali kuondoka bila ruhusa ya mume wake, aliniboa ikanilazimu kumtafutia sababu.
“Muambie Mama kakuita hata uende kijijini kwenu?” Nilimuambia lakini hakukubali, niliishiwa nguvu na kumuambia.
“Mimi naondoka, hawa watakuja karibuni na sitaki kupoteza kazi yangu lakini nakuambia usirudi, kama una akili utaondoka na kwenda kwa ndugu zako kwani watakuua na Baba naye ni mdhaifu kwao hawezi kuwa na maamuzi.” Nilimuambia nakuondoka, kwa alivyokua anaongea alionekana kumuogopa Baba na kuogopa kupoteza ndoa kuliko kitu kingine chochote.
“Labda na mimi nitakua mjinga namnna hii nikiolewa!” Niliwaza wakati natoka kwani sikumuelewa, kwa mambo yote aliyokua amepitia alipaswa hata kuchukia na kuondoka.
Nilirudi nyumani nikiomba Mungu asirudi tena pale, kila wakati nilikua nikiangalia simu yangu nikitamani kusikia akinipigia na kuniambia kua nimpelekee nguo zake sehemu flani lakini hakufanya hivyo. Nilichoona ni gari ya Karibu ikija imempakia yeye na Mama Abdul kambeba mtoto, nilijikuta namuangalia kwa hasira kama vile alikua mtoto wangu. Nilitamani kumtukana lakini niliona si nafasi yangu, baadaye jioni aliniambia kua Baba kamkataza kuondoka na kamuambia kama akiondoka basi asirudi tena.
Sikumjibu chohote kwani niliona isingesaidia kitu. Lakini haikupita siku mbili, ulikua ni usiku nilikua nambadilisha mtoto nguo kwakua alikua kajikololea, lakini wakati nafanya hivyo nilishangaa naloa, mwanzo nilidhani kakojoa tena lakini lilikua ni jasho, jasho jingi kama maji kabla hata sijamuita Mama nilianza kusikia harufu ileile niliyokua nikiisikia awali, lakini kabla ya kufanya kitu chochote mtoto alianza kujirusharusha, nilimuona analegea na kukosa nguvu na nilipomuangalia makwapani kulikua na kidonda kikubwa ambacho kilizunguka mkono, dalili zotezlizopitia Aziza alipitia yeye sasa kwa haraka zaidi.
Napiga kelele kumuita Mama ambaye alikua sebuleni, aliniacha chumbani wakati nambadilisha. Alikuja lakini kabla ya kumuambia chochote namuona akilia, ameshikilia simu na anaonekana kuchanganyikiwa, namuuliza nini ananiambia.
“Mod kadondoka shuleni, nimepigiwa na walimu wake sasa hivi…” Anashindwa kuongea namuona akipoteza nguvu na kudondoka.
(ILIPOISHIA SEHEMU YA NANE; Pamoja na matatizo aliyoyapata Mama alikataa kuondoka mule ndani, alirudi nyumbani mtoto akiwa salama. Lakini siku mbili tu naanza kuona dalili mbaya kwa mtoto, namuita Mama namuambia aje lakini ile kufika ananiambia Mod kadondoka shuleni. ENDELEA….)
Nilishindwa kunyanyuka kumfuata Mama, lakini ilionekana kama mtu kwenye simu bado anaongea, nilisikua tu “Halooo! Haloo!” nakisha baada ya muda simu ikakata. Bado nilikua nimembeba mtoto na nilimuona namna alivyokua akipigania pumzi yake mpaka akanyamaza kimya. Kuna kitu kiliniambia tayari lakini Mama alikua pale chini, nisingeweza kumuambia chochote, niliaangalia mapogo ya moyo ya mtoto tayari alishafariki tena mikononi mwangu.
Sijui nilipata wapi ujasiri lakini nilijihisi kuwa mtu mzima na kumlaza mtoto kitandani, nilimfunika kama vile amelala na kumrudia Mama, pale chini alikua hana fahamu, alipata mshtuko mkubwa. Nilishindwa kumnyanyua kabisa, nilitoka nnje na kupiga kelele. Pale ndani nilikua mimi na Bibi pamoja na mafanyakazi mwingine, nilimuita na kwenda kumnyanyua Mama, bado alikua mzito, nilihisi kama nayeye ameshatutoka lakini kuangalia mapigo ya moyo alikua anapumua kwa mbali.
Nilinyanyua simu na kumpigia Dereva ambaye alimchukua Mama na kumpeleka hospitalini, bado nilikua sijamuambia mtu yeyote kuwa mtoto alikua kashafariki, kwa muda nilikua nahangaikia. Nilikua nahangaikia waliopo hai kwanza na sikutaka kuwachanganya wote, akili ilikua inafanya kazi harakaharaka, nilichukua simu ya Mama ambayo niliiokota pale chini na kupiga namba ya mwisho.
Ilikua ni namba ya mwalinu na nilitaka kupata taarifa zote kuhusu Mod kabla ya kuongea na mtu mwingine. Aliniuliza mimi ni nani na kumuambia Dada yake.
“Kuna kitu umemuambia Mama, amedonoka na kupoteza fahamu, ameshapelekwa hospitalini hivyo nilitaka kujua kua kuna nini kimemtokea mtoto.” Niliongea kwa utaratibu kabisa, nilijaribu sana kuzizuia hisia zangu kwani nilikua na mengi na sikutaka kupaniki yakanikuta kama Mama.
“Hakuna mtu mzima hapo nyumbani?” Aliniuliza, nilishangaa kiodgo nimtukane kwani sijui alinionaje, lakini kwakua nilikua nahitaji msaada wake niliamua kuvumilia, nilimjibu vizuri kua hakuna.
“Mod alidondoka darasani, hakuguswa na mtu alikua amekaa kwenye kiti chake, akaanza kutoa mapovu mdomoni na kudondoka chini, amepelekwa hospitali na hali yake bado haijulikani ikoje, bado kalazwa na hawajui kua ni nini?” Aliniambia kwa utaratibu.
“Yuko hospitali gani?” Nilimuuliza huku nikitoka na kufunga mlango wa kile chumba. Alinielekeza na moja kwa moja nilimtafuta Ustadhi, tuliondoka mapka hospitali aliyokua amenielekeza. Alikua katika chumba cha wagonjwa mahututi. Nilitaka kumuona lakini walitukatalia na kutuambia kua haruhusiwi kuonwa na mtu yeyote, hata wazazi wake wasingeweza kumuona.
Nilimuomba amsaidie kumuombea palepale nnje, lakini kabla hajafanya chochote Daktari alitoka katika kile chumba.
“Nyie ni ndugu zake?” Aliuliza kwani muda merefu tulikua tumesimama kuangalia kama atatoka au la.
“Ndiyo mimi ni Dada yake.” Nilidanganya.
Alimuita ustadhi pembeni na kumuambia kitu, ni kama walikua wanajaribu kunificha lakini kwa kuwaangalia tu nilijua wanamaanisha nini, Daktari aliondoka na Ustadhi akarudi.
“Tayari?” Nilimuuliza, ingwa hakutaka kuniambia kitu lakini nilijua kabisa Mod ameshaondoka, cha ajabu pamoja na kumpenda sana lakini sikutoa hata chozi moja, kuna kitu kilikua kinaniambia kua jikaze kwani mambo bado. Kuniona nikiwa katika hali ile nimesimama imara Ustadhi aliamua kuniambia kweli kuwa Mod alikua amefariki dunia na madaktari walikua hawajui ni nini kilikua kimemuu.
“Kuna vipimo vinafanyika kuona kama alikula kitu chenye sumu au la?” Aliongea kunipa moyo lakini kwangu ilikua haina maana tena.
Nilimpigia simu Dereva ili kujua ni wapi alipokua amempeleka Mama na hali yake. Alinitajia, kumbe walikua katika hospitali ileile, nilimuomba Ustadhi twende kwenye wodi alipokua kalazwa, nilimkuta kashapata fahamu lakini alikua hawezi kunyanyuka wala kuongea chochote, nilijua kua ni mshituko hivyo nilitoka na kumuacha, sikutaka kumuambia chochote, sikutaka kumuambia kua watoto wake wawili wote washafariki dunia.
Nilitoka nikiwaza nini chakufanya, nilitaka kumpigia simu Baba lakini nilijua si kazi yangu, nilifikiria sana na kuamua kumpigia Baba mdogo, Karibu, yeye kidogo alionekana kujielewa, pamoja na mambo yake lakini nilijua angalau labda anaweza kunsikiliza. Alikua kazini na kutaka kuniambia kusubiri, ili kumfanya asikate simu nilimropokea.
“Mod kafariki dunia!” Nilimuambia bila kumung’unya maneno.
“Unasema! Wewe una kichaa nini? Mod gani huyo?” Alionekana kabisa kupaniki, nilirudia na kumuelewesha, nilimuona kakosa nguvu na kuanza kuongea kwa kutetemeka tetemeka.
“Asna naye kafariki dunia!” Nilimuambia tena, Asna lilikua ni jina la mtoto mchanga. Alikaa kimya kwa kama dakika moja hivi akitafakari.
“Shemaji anajua kuhusu Mod?” Aliniuliza akiamini kua atakua anajua kuhusu Asna kwakua alikua naye.
“Hajui chochote, hata kuhusu Asna hajui.” Nilimuelezea jinsi matukio yote yalivyokua yematokea na kumuambia kua Mama alikua hospitalini kalazwa na hawezi hata kuongea kutokana na mshituko baada ya kujua kua Mod kadondoka shuleni.
“Usimuambie kitu kwa sasa, subiri nije, Vipi Bibi anajua?”
“Hapana, hajui, mtoto nimemuacha ndani na nimefunga mlango kabisa. Wewe ndiyo mtu wa kwanza kukuambia.
Aliniambia nisimuambie mtu mwingine yeyote yeye atafanya ile kazi, nilkitaka kurudi nyumbani akaniambia nibaki pale kuangalia hali ya Mama.
“Wewe uko sawa lakini?” Aliniuliza, nilijisikia nafuu kidogo kuona angalau kuna mtu ananijali na anaona kama na mimi ni mtu.
“Niko vizuri, najitahidi.” Nilimuambia na kukatasimu, nilirudi kumsubiria Mama kama ataweza kuongea, nililazimika kukaa kwa nnje kwani sikutaka kukaa ndani, nilijua kama nikikaa ndani na akanyanyuka atataka kuniulizia kuhusu watoto wake na kwa wakati huo sikua na jibu la kumpa.
Karimu alifuatilia kila kitu, aliwaambia ndugu wengine pamoja na kumuambia Baba. Baba alizuia mazishi ya watoto wake kufanyika mpaka pale atakaporejea nchini, ilichukua wiki moja, Mama bado alikua kalazwa hospitalini, alishaambiwa kuhusu vifo vya watoto wake na alikua ni kulia kutwa nzima. Alipata stroke na kupooza upande mmoja wa mwili wake hivyo hata kuongea yake ilikua ni ya shida, siku ya mazishi ya wanae alibebwa na kitanda kisha kurudishwa hospitali.
Hali ya ile nyumba ilikua ya huzuni sana, Baba alikua mtu wa kujifungia ndani, Bibi kazi yake kubwa ilikua ni kulalamika na ndugu wengine baada tu ya mazishi walikua wakija mara moja moja. Kulikua hakuna raha tena hata mimi sikutamani kuishi tena pale ndani, nilitamani kuondoka ingawa sikutaka kurudi kijijini. Tayari nilishajikusanyia vihela hela vyangu na nilishajifunza kushona nilinunua charehani yangu na wakati huo nilikua natafu tu fremu ili niondoke.
“Ameua watoto sasa yamemrudia!” Bibi aliniambia, Bibi alikua kama shoga yangu na kwakua alikua hana mtu mwingine wakuongea naye basi kila kitu alikua akiniambia mimi.
“Hapana Bibi, hajamuua, kwa hilo namteteea. Mama anawapenda sana watoto wake.” Niliwaka kwani nilishachoshwa na namna ambavyo walikua wakimkandia Mama.
“Wewe ni kama mwanangu, sijui huyo mwanamke kawapa nini, hivi huoni mambo yanayotokea, unampendea nini lakini?” Bibi aliuliza. Nilijaribu kumuelewasha lakini hakunisikiliza, niliona haina haja kubishana kwani alikua ananiudhi na kidogo tu ningelipoka na kumuambia kuhusu mwanae.
“Anahitaji mwanamke mwingine, mtu ambaye atanisaidia kulea hawa watoto waliobaki kabla hajawamaliza kwasababu ya mali!” Bibi alizidi kunikera, asingekua ni Bosi wangu ningemtandika makofi lakini sikua na namna nililazimika kumsikiliza stu.
“Lakini Mama bado yuko hospitalini, na sidhani kama Baba atakubali.” Nilisema kwa wasiwasi lakini Bibi alionekana kuwa na uhakika na alichokua anakiongea.
“Nataka aoe mtu ambaye tunamjua, mtu ambaye namtaka mimi, mtu ambaye atawalea wajukuu zangu kama wake. Wewe naona kabisa unaweza, naona uanvyoishi nao utaweza kuwatunza.” Bibi aliongea, sikumualewa lakini pia sikua tayari kuendelea kubaki pale, nilishaamua kuondoka na kitu pekee kilichokua kinanizuia ni hali ya Mama, nilipanga kama ikitengamaa kidogo niondoke.
“Mimi Bibi nishakua mtu mzima, natakiwa kuwa na maisha yangu, siwezi kufanya kazi za ndani kila siku, lazima nitafute maisha mengine.” Nilimuambia.
“Kweli kabisa, hata mimi nakubaliana na wewe, hutakiwi kufanya kazi tena. Unatakiwa kuwa na mji wako, uwe na maisha yako na uwe na familia yako.” Nilifurahi namna alivyokua akiniunga mkono na kumuambia mipango yangu.
“Nashukuru, nimeshanunua charahani, sasa natafuta fremu ili nikatafute chumba nianze biashara yangu.” Nilimuambia lakini alionekana kushtuka.
“Simaanishi hivyo, sitaki uondoke humu ndani, mtoto wangu anahitaji kua mke mwingine na ninataka akuoe wewe.”
Bibi aliongea maneno ambayo sikuyategemea, nilishikwa na butwaa na kushindwa hata chakujibu.
“Mali zote hizi zinatakiwa kuwa zako, ukikubali tu mimi najua namna ya kumbana huyu mtoto, nataka uolewa humu ndani.” Bibi aliongea kwa kujiamini, ni kitu ambacho sikukitegemea, kilikua hakijawahi haa kupita kichwani kwangu, kwa umri wa Baba nilimuona kama Baba yangu, ingawa nilishafikia utu uzima lakini bado nilikua najiona kama mtoto, ndiyo kwanza nilikua na miaka 19 na Baba alikua na miaka zaidi ya 45.
Bibi alikua akiniangalia, alikua akitabasamua akiniona kama vile nakubali, akili yangu kidogo ilikua inahama kuna kuwaza maisha ya mule ndani, niliwaza ile nyumba, magari na kila kitu niliwaza namna watoto walivyokua wakinipenda.
“Usiogope dini yetu inaruhusu wake wawili? Ila kama hutaki kuolewa mke mwenza mimi nawezakumuondoa huyu mwanamke, atanimalizia wajukuu.” Bibi aliongea, nilishikwa na kigugumizi sikua hata na chakusema.
(ILIPOISHIA SEHEMU YA TISA; Baaada ya kupoteza watoto wake watatu Mama anapooza, anakua hawezi kufanya chochote. Bibi anasema Baba anhitaji mke mwingine na kuniambia kua anataka mimi ndiyo niolewe na Baba je nini kitaendelea. Kama hukusoma sehemu ilizopita pitia ukurasa wangu wa Instagram; @iddimakengo @iddimakengo)
Nilijikuta najichekea tu kichwani na kuwaza hivi huyu mwanamke kanionaje, yaani pamoja na matatizo yote ya hii familia mimi niwe mpuuzi tu wa kuingia. Hata kama ni shida lakini si kwa kiwango hiki. Sikutaka kumuambia sababu za kweli.
“Siwezi, nimeshamzoea Baba, namuona kama Baba yangu, siwezi kabisa kuwa mke, hapana, nasubiri Mungu akinipa riziki yangu sawa.” Niliongea huku anikijichekesha chekesha, sikutaka aone kama naichukia ile familia yake. Alijaribu sana kunishawishi lakini sikukubali, sikutaka kujihusisha kwa namna yoyote ile na ile familia.
“Nahangaika tu kwa kua niko ndani, ningekua naweza kutoka ningemtafutia mwanangu mwali mzuri.” Bibi alijisemesha, alionekana kukasirika kidogo lakini sikumjali, kwawakati huo nilikua nampa heshima tu ya uzee lakini nilikua sijali kama ni Bosi wangu, tayari nilishaamua kuondoka hivyo sikujali kama wangenielewa vibaya au la. Nilimuacha ndani na kutoka zangu nnje, nilienda kuangalia TV, Baba alikua sebuleni lakini baada ya kuniona alirudi chumbani ambapo Mama alikua kalala.
Siku iliyokua inafuata Karim alikuja nyumbani, waliogea kidogo na Baba na kuondoka naye, sikujua wameenda wapi mpaka jioni yake, nilikua chumbani kwa Mama nikimsafisha kwani alikua hawezi kujifanyia mambo mengi, mara nyingi mimi ndiyo nilikua namsafisha hasa kwa kumfuta kumuogesha nilisaidiana na mfanyakazi mwingine. Lakini siku hiyo nilikua namfuta tu, alikua bado anaweza kuongea lakini kwa shida, lilikua likimtoka neno moja moja.
“Ataoa mke mwingine…” Aliniambia, kidogo nilishtuka nikidhani kua labda kasikia kuhusu mambo yangu na Bibi. Nilinyamaza bila kumjibu.
“Ndiyo Mama yake anavyomuambia, anasema hawezi kuoa lakini namjua, hawezi kumkatalia Mama yake kwa chochote. Zamani niliweza kupambana ila kwa hali yangu hii siwezi tena, ataoa na sasa hivi sitamlaumu.” Aliendelea kuongea kwa taabu sana, nilimuangalia na kumuonea huruma kwani alikua mpweke sana.
“Hawezi, Baba anakupenda sana, kama ni kuoa angekua ameshaoa tangu zamani, kwa namna ninavyowafahamu ndugu zake kwanza angekua ameshakuacha.
Nilijaribu kumpa moyo lakini aliendelea kusisitiza, nilimaliza kumsafisha na kutoka sebuleni, wakati naelekea jikoni kupika nilisikia sauti zinatoka chumbani kwa Bibi, kuna watu walikua wanabishana. Nilisikia sauti ya Mama Abdul akiongea, usiku ulishaingia sikujua nimekaa na Mama muda mrefu kiasi kile.
“Hawezi kuoa mke mwingine, ataoaje wakati mke wake anaumwa, hivi jamii itatuelewaje kwamba sisi ni watu wa kukimbia wengine katika matatizo?” Mama Abdul aliongea kwa hasira.
“Halafu Mama, Kaka ni mtu mzima, haiwezekani wewe kumpangia, ameshasema anahudumia mke wake, wewe cha kuingilia ni nini?” Mama Aziza aliongea.
“Najua walipoenda, najua wewe ndiyo umemlazimisha Karim kwenda kujitambulisha kwa sijui mwanamke gani, lakini nasema hapa ndani haingii.”
“Ataingi kwani ni kwako hapa, hivi mwenzanu hamumuonei huruma kafiwa na watoto watatu kwa mpigo na bado anaenda kupoteza mke halafu mnasema asioe, unafikiri ataishi vipi?” Bibi aliongea kwa hasira, nilishindwa kuelewa kwani kwa namna walivyokua wanamchukia wifi yao nilidhani wangechekelea lile wazo la Kaka yao kuoa mke mwingine.
Walilumbana sana, nilisikiliza lakini mlango ulikua unafunguliwa hivyo nikakimbia kurudi jikoni. Alikua ni Baba na Karim, waliingia, Baba alielekea chumbani na Karim alikaa tu pale sabuleni, nadhani chumbani waliwasikia wakati wanaingia hivyo walitoka, Mama Abdul walipomuona mdogo wao kakaa sebuleni walimchukua na kwenda naye nnje kabisa,
“Huo ujinga unaofanya na Mama ninaujua na utakuja kukutokea puani?” Alimuambia hata kabla hawajafika mbali, mimi nilikua kwanyuma nikiwafuatilia, nilikua natembea bila kujali kama wataniona au la, kuna kitu katika kichwa changu kilikua kinaniambia fukuzwa kazi, fukuzwa kazi.
“Ujinga gani, mbona sikuelewi?” Karim aliuliza huku akirusha mkono wake, alikua anausogeza kwani shangazi alimshika kwanguvu.
“Sio huo wa kumtafurta Kaka mke!” Alimjibu kwa hasira.
“Sasa huo ni ujinga, ina maana wewe bado unataka aendelee kuishi na yule kilema?” Aliongea maneno ambayo yalinichoma sana ingawa hayakunishangaza kwani nilijua anawachukia.
“Hivi mdogo wangu huna akili kabisa, yaani hujui hata tangu mwanzo tulikua tunahangikia nini? Nitakua nimewaua watoto wa Kaka Bure kama ataoa mwanamke mwingine na kuja kuzaa tena akachukua ma…” Mama Abdul aliongea lakini kabla ya kumalizia Karim alimkatisha.
“Umewaua watoto wa Kaka? Kivipi mbona sikuelewi, unahusika nini na vifo vyao?” Sikua nimesimama mbali nao na kwakua walikua wakipigwa na mwanga wa taa nilimuona Karim akikasirika, alikunya uso na kumshika Dada yake mikono yote miwili kama vile anataka kumpiga, alikua akimtingisha tingisa kumuuliza anamaanisha nini anaposema kuua.
“Sijamaanisha kitu lakini nilikua nakuambia kua kama akioa mwanamke mwingine inamaana kugawana mali upya. Heri huyu kilema tunajua kua hata Kaka akifa hawezi kuchukua chochote na hawa watoto tutabaki nao.” Alijaribu kujitetea lakini Karim hakuonekana kumuelewa, aliendelea kumsukuma sukuma na kumlazimishia aongee.
“Unaniumiza!” Mama Abdul aliongea huku akijajribu kujitoa katika mikono ya mdogo wake ambaye alimshika kwanguvu, hakutaka kumuachia.
“Nataka uniambie umewafanya nini watoto wakaka? Kila siku tuansema ni Shemeji na kumuita mchawi, lakini umevuka mipaka, ulihusika namna gani?” Aliendelea kumsukuma, hasira zilizidi kumpanda na kutaka kumpiga kabisa.
Shanagzi alipaniki, alionekana kuishiwa pozi kabisa, kwa namna alivyokua amekasirika nilipata picha kuwa Karim hakua akijua chochote kuhusu mambo aliyokua akifanya Dada yake.
“Hivi unajua ile ni damu yetu, una roho mbaya kiasi gani, hizi mali huu ujinga mtupu ndiyo unakufanya kuwa na roho mbaya namna hii!” Aliendelea kuongea huku akimuachia na kumsuma kwa dharau, nilisogea pembeni na kujificha kwani sikutaka tena kufukuzwa kazi.
“Humu siondoki mpaka nijue mwisho wao!” Nilijisemea, ni bahati tu niliposogea na mlango ulifunguliwa, alitoka Shangazi, Mama Aziza na kuwafuta kwani walikua wanaendelea kugombana.
“Nawewe uko pamoja na huyu mpumbavu?” Karim amuuliliza.
“Kivipi, mbona unamshushia heshima, huyu ni Dada yako!” Mama Aziza aliongea.
“Hakuna cha Dada Shetani mkubwa huyu, Mbwa kabisa muuaji mkubwa!”
“Basi yaishe huna haja ya kutangaza dunia nzima.” Mama Abdul aliingilia kati, pamoja na kuwa yeye ndiyo alikua ametukanwa lakini alioneka kama anataka yaishe.
“Kuna nini kwani?” Mama Aziza aliuliza, aliwageukia wote kila mmoja kwa wakati wake lakini hakuna aliyekua na jibu. Wote walikua wanaangaliana Karim akimuangalia kama vile anasema muuliza huyo na Mama Abdul akimuangalia kama vile anasema hakuna kitu.
“Hakuna kitu, si unamjua mdogo wako akikasirika, sijui leo ana nini, hakuna kitu Mama anaendeleaje? Umemuona wifi? ushakula? Unataka kwenda nyumbani?” Mama Abdul liuliza maswalia ambayo hayaeleweki, nilipata picha kua alikua hataki Mama Aziza kujua na ilimaanisha kua mambo yale alifanya mwenyewe.
“Sitaki kuendelea kuwasikiliza, lenu moja!” Karim aliongea, hata bila kuingia ndani kuaga aliingia kwenye gari yake na kuondoka.
Kimya kilitanda wakiangaliana kila mmoja akitaka mwenzake kuongea.
“Kuna mambo wanapanga na Mama na ninavyoona watakuja kutugeuka.” Mama Abdul aliongea kumuambia mdogo wake.
“Kivipi?”
“Sijajua bado ila naona kama vile hili suala la kuoa ni siriasi na ninavyomsikiliza Karim anataka kutafuta mtu wake, nimejaribu kuonega naye naona anatugeuzia kibao, naona kuna mambo wanaongea na Kaka, ni kama anamuambia sisi ni wabaya na ndiyo tumevunja ndoa yake.
“Sisi wabaya, kivipi mbona sikuelewi!” Mama Aziza aliuliza kama vile kahcanganyikia.
“Ushawahi kwenda kwa Mganga?” Alimuuliza, Mama Aziza alibaki kushangaa.
“Mganga kwa namna gani? Mbona sikuelewi, mimi kwa mganga nifanye nini, unajua kabisa mimi mtu wa dini mambo ya kishirikina siamini?” Mama Aziza aliongea kama vile anajitetea.
“Basi wanadhani sisi ndiyo tumemloga wifi kwakua hatumpendi na kibaya zaidi eti watoto wa Kaka sisi ndiyo tumewaua, ndiyo tulikua tunagombana sana, sijui kuna rafiki yake nani kamletea Karim umbeya sijui ulishaonekana wapi, mimi nikawa nakutetea lakini haamini anasema letu moja mimi na wewe ndiyo tumewaloga na kuwaua watoto wa Kaka ndiyo maana nakutetea. Wewe unaongea nini na mchumba wake, maana mko karibu sana siku hizi kuna vitu unamuambia, labda ulienda kwa mtaalamu kwaajili ya mambo yako na mume wako ukamuambia?”
Hapo ndiyo niliamini kua Mama Abdul ni shetani wa mashetani, alikua anamgeuzia mdogo wake kibao. Suala la Mganga lilikua lao. Mama Aziza alijitetea aliapa na kuapa kua hajawaghi na wala hawaongei mambo hayo.
“Mbona makubwa, hawa mawifi tunaoletewa mbona mitihani, mtu usiwe shoga yake tu anaanza kukuharibia.” Mama Aziza alilalamika, ni kama alikua naamini kua mchumba wa Karim alishaanza kumsema vibaya.
“Usiwaze sana ndiyo dunia ilivyo yakiwa mazuri ni yakwao lakini yakiharibika ni ya mawifi.” Mama Aziza aliongea hukua kimshika mkono ndugu yake aliyeonekana kama kuchanganyikiwa falani. Waliondoka na kuingia kwenye magari yao, hawakurudi tena ndani na wote walikua wamechanganyikiwa flani hivi mawazo tele, mimi kidogo nilifurahi kwamba anaglau hata hawapatani wenyewe kwa wenyewe.
Nilirudi ndani kuendelea na shunguli zangu, lakini usiku wakati nakaribia kulala nilisikia geti likifunguliwa na mlinzi gari iliingia na kusimama kwa nnje, nilitoka dirishani na kuchungulia. Ilikua ni kama saa tano usiku hivi, ilikua ni gari ya Mama Abdul, nilishangaa anafanya nini usiku wote huo, kwakua nilikua nahitaji kujua kilichokua kikiendelea nilitaka kutoka nikisubiri agonge mlango na mimi kumfungulia. Lakini hakugonga, alikaa kama dakika kumi pale nnje na kwenye mwanga nilimuona Baba akitoka.
Alitoka na kusimama pembeni ya mlango wa gari, upande wa dereva mlango ulifunguliwa Baba akawa kasimama pembeni kawa kama kaegemea mlango huku Shangazi akiwa kakaa ndani lakini unaona miguu kaitoa nnje. Waliongea kama dakika tano, kwa namna walivyokua wakiongea ni kama walikua hawakubaliani wanzozana kitu flani. Uzalendo ulinishinda, nyumba ile ina milango mitatu, wa sebuleni, mlango wa nyuma na wajikoni, yote hutoka nnje, nilitaka kusikiliza hivyo niliangalia na kuona kama nikitokea mlango wa nyuma basi ningeweza kuwafikia bila wao kujua.
Nilitoka harakaharaka na kwenda kujibanza sehemu, niliwasikia vizuri kwa namnawa livyokua wakiongea, tayari walishamaliza mazungumzo yao ni kama walikua hawakubaliani kitu.
“Siwezi kwenda kwa mganaga maisha yangu yote!” Baba alikua akiongea.
“Kaka, mali zako zinawausumbua wengi, hivi unafikiri, mke wako akifa, wewe ukafa hapo ni nani atachukua kila kitu, angalia mwenyewe nani? Wanaume mko wawili unategemea nini? Ni nani anakua msimamizi wa familia! Najua una imani zako lakini yule mtoto wa watu anateseka, hivi unafikiri vifo vya wanao ni vya kawaida. Wote wamekufa kwa magonjwa ya ajabu ajabu amabyo hata madaktari mpaka leo hawajui ni nini? Unataka kumzika na mke wako?” Shangazi aliendelea kubemebeleza.
“Siwezi kuamini kua Mama yangu anaweza kujua haya mambo na akanyamaza!”
“Mama hajui chochote anatumiwa tu, mimi nimeyasikia, Mama anatumiwa ili kukucontrol wewe, hivi unafikiri kwanini Mama analazimisha uoe na huyo uanyemuona ndugu yako anahangaika sana kukutafutia mchumba, unajua hao wanawake anaokutafutia! Hiivi wewe hujifikirii, katika kipindi hiki ndiyo wakati wa kumuolewa mkeo mke wa pili, hivi hata kama dini inaruhusu kwa hali yake si mtu mweye busara angesema hapana tumuache Shemeji apone lakinia kasikikila kidedea mpaka basi!”
Baba alinyamaza kimya bila kusema chochote, ulibaki ukimya wa muda kama dakika mbili hivi.
“Mimi sitaenda huko, sitahusika chochote. Kama ni kuenda muende nyinyi kwani wewe huwezi kumpeleka?” Baba aliongea alionekana kuchanganyikiwa, ni kama alikua anamuamini flani..
“Ingakua vyema ungehusuka ili mkeo kujua kua uko pamoja naye, mke wako mimi hanipendi kwani kusema kweli kwa mambo ambayo mdogo wetu alikua anamjaza Mama na Mama kutuaambia nilikua namchukia, lakini baada ya kuyasikia leo nimeona sikua sawa, nitamuomba msamaha baadaye lakini inabidi apone kwanza, mimi nitakuelekeza, mpeleka muache hapo apewe dawa basi, ni vizuri ungeenda naye.”
Aliongea Baba alionekana kumsikiliza na kumualewa ingawa alionekana kuwa mgumu kuamini. Kila mara alikua akisema “Mbona nampa kila kitu, biashara zangu zote ndiyo anajua, yeye ndiyo namuamini!”
“Hata mimi sijui, labda mwanamke kambadilisha, maana tangu kupata huyo mchumba wake kawa tofauti kabisa.” Mama Aziza alionbgea kwa kusikitika, alimuambia Baba kumuandaa Mama ili waondoke saa kumi usiku kabla watu hawajaamka kwani ikigundulika basi anaweza kuharibu mambo. Aliaga na kuondoka hukua kimsisitizia kumuandaa Mama ili kumpeleka kwa mtaalam kumpona.
***
Mambo yanaanza kuwa ya moto, baada ya Karim kugundua kuhusika kwake katika vifo vya watoto wakaka yao, Mama Abdul anaamua kumbadilishia kibao na kashaanza kumgeuza kila mtu, unadhani nini kitafuta, je Mama Mod atapona, vipi hatima ya Karim na mchumba wake.
(ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI; Mambo yanaanza kubumburuka Mama Abdul anaanza kugombana na Karim na anawageuka wenzake kwa Kaka yake. Anamuambia wao ndiyo wanamloga na anaweza kumsaidia wifi yake, anataka kumpeleka kwa mganga ili apone je ataweza? ENDELEA…)
Usiku sikulala, nilijua ni lazima Baba ataingia katika mtego wa Mama Abdul na kwa nilivyokua namjua niliamini kua ile ilikua ni njia ya kummaliza kabisa Mama. Nilitamani kwenad kumuambia Baba kila kitu lakini nilikua naogopa, nilitamani kwenda kumuambia Mama asikubali kwenda kwa mganga lakini nilijua hana uwezo wa kukataa, kwa hali yake alikua anapelekwa pelekwa tu. Nilikaa macho mpaka saa kumi na moja asubuhi, nilimuona Mama Abdul akija na Gari yake na wote watatu kuondoka katika Gari ya Mama Abdul.
Sikuweza kufanya chochote, walimchukua Mama na kuondoka naye, Baba alirejea siku iliyofuata lakini alikua peke yake, sikumuona Mama na sikuweza hata kuulizia kama yuko wapi. Kwa wasiwasi nilienda nyumbani kwa Mama Abdul, nilijifanya nina ujumbe wake kutoka kwa Bibi lakini niliambwiwa kasafri, hapo ndipo nilijua kua alikua amebaki na Mama ingawa hata sikujua walikua wameenda wapi?
Lakini baada ya wiki moja nilirudi nyumbani na kumkuta Mama na Mama Abdul wamekaa sebuleni, walikua wakiongea na kucheka, nilishangaa mambo mawili, jambo la kwanza ni namna ambavyo Mama alikua akionekana, alikua kama kawaida, kapona kabsia, anaongea na kucheka, tena aliponiona alinyanyuka kabisa na kuniambia.
“Mungu anatenda miujiza, nimenyanyuka, nimepona kabisa, ashukuriwe wifi yangu mpenzi, mashatani wameshindwa!” Aliongea kwa furaha huku akinikimbilia na kunikumbatia, nilishangaa sana.
Kitu cha pili kilichonishangaza ni namna alivyokua akicheka na Mama Abdul, kusema kweli ilikua ni kama mtu na rafiki yake, kama mashoga wa muda mrefu. Sikujua ni nini kilikua kimetokea katika hizo wiki mbili. Sikujua ni miujiza gani ilitokea lakini kwa namna nilivyokua nikimfahamu yule Mama nilijua kua hana jema na ushoga wao usingeishia pazuri. Mama Abdul naye alinichangamkia ingawa si sana, niliwasalimia na kulazimishia furaha, sikutaka kukaa nao ingawa Mama alisisitiza, niliondoka na kwenda chumbani kwa Bibi.
“Wamerudi!” Bibi aliniambia hata kabla ya kumsalimia. Alionekana kuwa katika lindi kubwa la mawazo.
“Kweli Mama kapona…” Nilisema huku nikitabasmu.
“Kapona kwani alikua anaumwa, si alikua anaigiza tu ili watu kumuonea huruma wasijue kaua watoto wake. Huyu mwanamke, kanichukulia mwanangu wakiume na sasa huyu naye kamchukua, dakika mbili wamekua mashoga, yaani alikua anajifanya kuumwa ili tu kuteka akili za wanangu!” Bibi aliongea, kusema kweli nilishaichoka ile familia, yaani kwao kila kitu kilikua ni kulaumu wengine, walikua wakijiona kama Malaika kumbe walijaa ushetani.
“Watajua wenyewe ni watu wazima.” Niliongea huku nikitaka kutoka, sikua na chakufanya huko nnje lakini Bibi naye alishaniboa na sikutaka kuendelea kumsikiliza.
“Naraka unisaidie.” Bibi aliniongelesha huku akininyooshe mkono kuniita, alinionyesha kukaa pembeni yake, sikua na namna zaidi ya kutii maagizo yake.
“Nataka umfuatilie huyo mwanamke, nataka kujua ni kitu gani kawapa wangu, wewe wanakuamini hivyo nataka ufuatilie kila kitu.”
Aliongea kwa sauti ya chini kama vile kulikua na watu wengine mule ndani lakinia anninong’oneza yeye. Nilishachoka na sikujali tena kufukuzwa mule ndani, istoshe kwa hali niliyokua naiona nilishapanga kuondoka mwenyewe kabla ya kufukuzwa.
“Hapana Bibi, hayo ni mambo ya familia yenu, hivi unafikiri Baba akijua kua nina wachunguza itakuaje, si nitaonekana kama mchochezi, hawa ni watu wazima siwezi kuchunguza.”
Niliongea kwa hasira kidogo na kunyanyuka kutaka kuondoka, Bibi aliniita tena. Safari hii aliniambia kua nifungue kwenye kabati lake, aliniambia nitoe nyaraka flani na kumkabidhi.
Alizipokea na kutoa kisha kunikabidhi mimi.
“Chukua.” Aliniambia, sikujua ni nini lakini baada ya kufungua ilikua ni hati ya kiwanja ilikua na jina langu.
“Kipo Sinza, tahmani yake ni kama milioni sihirini na ushee, hicho ni chakwako.” Aliniambia, kusema kweli sikuamini macho yangu, nilisoma mara mbilimbili nikidhani imekosewa lakini kila kitu kilikua sawa.
“Sijakupa ili umchunguze Mama yako, nimekupa kwakua wewe ni kama mwanangu, umenihudumia sana, umenilea sana, umeshika mavi yangu, hata wanangu walikua wanakuachia kila kitu kunihudumia. Nilishakuandikisha muda mrefu na nilisubiri wakati muafaka.”
Aliongea na kunyamaza, hapa alionyesha uchungu kidogo.
“Najua ninachokuomba hustahili lakini hawa ni wanangu, najua wanaongea kwakua mimi niko hai, nikifa leo hapa hata salamu watakua hawasalimiani. Hivi unajua Bakari (Baba, sio jina lake halisi) anamuambia mdogo wake mchawi, mwanamke kaua watoto wake wote kisa kutaka mali na tamaa za dunia lakini bado anaivuruga na familia yangu. Siwezi kufa kwa amani kama nitakufa nikijua wanangu hata kuongea hawaongei.” Alionekana kuumia sana na kumaanisha kile alichokua akikiongea.
Nilitaka sana kumuambia ukweli lakini nilijua haitasiadia, alikua anaamini Mama ni mchawi na anaumizwa na ukaribu weka na Mama Abdul, nilitaka kumkatalia lakini kila nikiangalia ile hati ya kiwanja nilishindwa.
“Poteli ya mbali kwani bei gani, kuna ndugu yangu hapa, isitoshe si lazima kumuambia ukweli nitachunguza, huyu ana vitu vingi vya kunipa!” Nilijiwazia, lakini sikutaka kukubali wakati uleule, nilimkabidhi hati yake na kumuambia nitafikiria.
“Hapana, hicho ni chakwako, hata ukiondoka leo kitabaki kuwa chako, sikukupa ili unichunguzie, nataka unichunguzie kama rafiki lakini si kukununua.” Aliniambia na kuniambia nitoke kwani anataka kupumzika.
“Fikiria, ukifanya maamuzi niambie, nataka kujua namna ambavyo huyu mwanamke ameweza kuwateka na kuwagombanisha wanangu mpaka wanaitana wachawi.” Alimaliza kuongea na kujilaza kitandani, mimi nilitoka na kwenda kuweka ile hati sehemu nzuri, bado nilikua siamini amini kama na mimi nina kiwanja kwangu ilikua kama ndoto flani.
***
Baada ya ile hati wala haikunichukua muda kumuambia Bibi kua nabaki na nitamsaidia kuchunguza. Hakukua na kitu cha kuchunguza kila mtu alikua anendelea na maisha yake, Mama alikua ameacha kazi sehemu aliyokua anafanya mwanzo na alikua akisimamia biashara za Baba. Ukaribu wa Baba na Mama Abdul uliongezeka, yeye ndiyo alikua kila kitu mule ndani, walikua wakimuamini na alikua akiitumia hiyo nafasi vizuri.
Kwa upande wa Karim na Mama Aziza mambo yalikua tofauti, Karim alikua haji kabisa, alishaoa na harusi yake Baba alienda kwakua tu Bibi alitaka kumauchia laana kama asingeenda, alikua akimchukia balaa na walikua hawongei vizuri. Mama Aziza yeye alikua kama anajipendekeza pendekeza lakini hakuna mtu aliyekua akimjali, alikua kama mgeni flani ingawa bado alikua anakuja, kila kitu mule ndani ilikua ni Mama Abdul.
“Nataka kujua vitu vyao wanaweka wapi?” Mama Abdul liniambia, sikuelewa kua alikua amanaanisha nini.
“Hii nyumba ina jina la nani?” Aliniuliza, tulikua jikoni tunapika, alishageuza pale kama kwake na aliweza kuingia na kutoka wakatio wowote ule. Nilinyamaza kama vile sijamsikia mpaka aliporudia.
“Nimekuuliza hii nyumba ina jina la nani, Kaka yangu bado kuna vitu ananificha, ila nataka kujua, huyu mwanamke ukimuachia kila kitu anaweza kutugeuka mwishoni.”
“Wewe si ni rafiki yako, naona siku hizi mko karibu.”Nilimuambia huku nikicheka kwa utani.
“Hivi ni lini mdogo wangu utajua kuhusu maisha, hakuna cha rafiki katika hii dunia, kila kitu kwenye maisha ni kujipambania wewe mwenyewe. Hivi wewe hutaki siku moja kuondoka na kauchana na hii kazi ya ndani, ushakua mtu mzima tafuta chako.”
Aliniambia maneno ambayo yalinichoma kweli kwani nilishachoka kazi za nndai, kila siku kusikiliza matatizo ya watu na kuwafanyia kazi watu ambao hata walikua hawana shukurani.
“Nimechoka na nataka kuwa na chakwangu.” Nilijisemesha.
“Unajua Bei ya hii nyumba?” Aliniuliza, nilitingisha kichwa kumuambia kua sijui.
“Kiwanja tu hiki si chini ya milioni mia, fikiria mpaka kujenga si milioni hata mia tano zinafika, kuna watu wa Benki nimeongea nao wananiambia kua naweza kuchukulia mkopo hata wa milioni mia nne, muhimu niwe na biashara tu, sema sijajua hati yake ina jina la nani?”
Aliongea kwa kujiamini, nilishangaa ni kwanini alikua akiniambia yale maneno.
“Inabidi tushirikiane kuipata na nina uhakika mgao wako utakua mkubwa tu.” Aliendelea kuongea, nilimuangalia kidogo nicheke, kweke ni kama nilishakubaliana na kile kitu.
“Au hutaki?” Aliniuliza, nilibaki kimya kwani sikua na jibu la moja kwa moja la kumpa.
“Najua una akili hutamuambia mtu, unataka pesa na nina uhakika hakuna atakaye kuamini hivyo ninachotaka ni wewe kuchunguza. Kesho mimi na mabosi wako tutasafiri, nataka usiku uingie na kuchambua kila kitu humo ndani, nataka uhakikisha unaipata hiyo hati, sitaki uibe chochote nataka unipigie picha na simu. Nipigie jina lake na sahihi yake, piga picha na namba ya hati.”
Aliongea kwa kujiamini, nilikua sijakuabaliana na kila kitu alichosema lakini kweke yaye alikua kama anaamini kua nimekubaliana naye. Alionekana kuwa na haraka nayo, alionekana kulazimishia sana, ilionyesha ni kitu alichokua kakiwaza kwa muda mrefu lakini alikua hana namna.
“Nataka iwe siri, sitaki maneno maneno haya kuvuja, wewe ni mtu mzima naamini unaweza kutumza siri au huwezi?” Aliniuliza huku akinikazia macho, nililazimika kumjibu kumuonyesha kuwa imemuelewa.
“Wewe ni kama mwanangu, sitaki kitu kibaya kikutokee. Nadhani hutaki kupoteza kile kiwanja ambacho Mama kakupatia.” Aliongea kwa kunitega flani, nilishtuka alikua amejuaje.
“Mimi ndiyo naiendesha hii familia, kila kitu kinachoendelea nakijua na sidhani kama kuna mtu wa kunizunguka. Eti kwani wewe unaweza kunizunguka?”
Nilijikuta naitikia kwa kichwa tu kumuambia hapana, kusema kweli kwa wakati ule nilikua naogopa. Nilishajua mambo yake aliyokua ameyafanya huko nyuma na niliogopa kama nisipofuata mashariti yake basi anaweza kunifanyia kitu kibaya. Tuliandaa chakula cha usiku na wote kukaa mezani.
“Kaka kesho itabidi tuende wote, utatuendesha wewe na Babu anataka kukuona.” Aliongea kwa kifupi na Baba hakubisha kabisa alionekana kukubali tu.
“Mary atabaki hapa, anaweza kuitunza familia, eti mwanangu si unajua chakufanya?” Aliniuliza, nililazimika kuitikia tu kwa kichwa kumuambia najua lakini ukweli nikua nilikua naogopa sana.
Waliendelea kuongea na kukubaliana kila kitu, safari ilikua imekamilika na nilijua kua Mama Abdul alikua namaanisha. pamoja na kutaka pesa lakini sikua tayari kumsaidia kufanya wizi ule, niliwaza nini chakufanya lakini sikua na jibu. Nilikua na wasiwasi mpaka kushindwa kula.
“Naomba unisindikize mpaka nnje.” Mama Abdul aliniambia, sijui ni muda gani lakini alishamaliza kula na kuaga, nilijifanya nakula akanisisitiza.
“Dadkika mbili tu utakuja kumalizia chakula chako.” Alisisiziza.
“Msindikize Shangazi yako usitake atoke mwenyewe.”
Mama aliniambia, sikua na namna zaidi ya kunyanyuka na kutoka naye. Sjui kwanini lakini nilikua natetemeka kama vile namuogopa flani, tulitembea mpaka kwenye gari.
“Unajua chakufanya lakini, nataka picha ya kila kitu utakachokiona naamini utaweza kufungua kabati, umekaa muda mrefu hapa kushindwa kujuua funguo zinawekwa wapi najua wewe ni mtu wa kuchunguza chunguza vitu una akili sana.” Nilinyamaza bila kusema kitu, aliingia kwenye gari lake lakini kabla ya kufunga mlango aliniambia.
“Usijekufanya kose tena la kumuambia Mama yako, unakumbuka ulivyomuambia kuhusu maneno ya mwanangu Abdul, ulivyomuambia kuhusu meseji zangu ulizosoma na ulivyonisikia nikiongea kuhusu ARV. Ukijaribu tena jua kua nitajua, mimi ndiyo shoga yake sasa, nimekusamehe mara moja sitakusamehe mara ya pili kama unataka kutembea unanuka mavi niharibie mipango yangu uone.” Aliongea kwa sauti ya kumaanisha lakini alimalizia kwa kicheko cha dharau, kidogo nidondoke kwani vitu vile nilikua nimemuambia Mama tu!
(ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MOJA; Mama Abdul anataka kujua kuhusu hati ya nyumba ya Baba, anataka mimi ndiyo nimsaidie kuitafuta, nasita lakini ananiambia kuhusu mambo ambayo nilimuambia Mama na kuniambia kua anayajua. Naogopa kwani ananitishia vitu vingine. ENDELEA…)
Nguvu aliyokua nayo Mama Abdul ilikua nikubwa, ingawa nilikua siamini sana mambo ya kishirikina lakini niliona kwa macho yangu vitu alivyokua akifanya hivyo sikumpuuzia. Kama alivyoniambia siku iliyofuata waliondoka, pale nyumbani nilibaki mimi, Bibi na mfanyakazi mwingine. Mama Aziza alikuja lakini hakukaa sana, usiku ulipoingia Mama Abdul alinipigia simu na kunikumbushia kazi niliyokua natakiwa kuifanya, aliniambia nihakikishe napiga picha kila kitu namtumia na nisionekane na mtu yeyote yule.
Niliitikia na kumkubalia huku nikitetemeka kwa uoga. “Baada ya hii naondoka katika hii nyumba ipo siku watakuja kuniua!” Niliwaza kwa hasira, mlango wa chumba cha Baba ulifungwa lakini Mama Abdul alishanipa ufunguo wa ziada, naamini alizitengeneza, ulikua ni mpango alioupanga kwa muda mrefu. Niliingia chumbani na kuanza kupekua, nilipekua kila kitu lakini sikuona chochote, kulikua na nyaraka nyingi za Baba lakini hakukua na hati yoyote ya kiwanja.
Nilipiga picha kile nilichokiona na kumtumia, nilimuambia nimekosa lakini hakuamini, aliniambia niendelee kutafuta, nilitafuta mpaka kunapambazuka sikuona chochote. Nilichoka na kutoka kwenda kulala, asubuhi alinipigia nikamuambia sikupata kitu. Tofauti na nilivyodhani kua labda atakasirika alijichekesha chekesha na kuniambia nisijali.
“Vile vilikua vitisho tu wala usijali, siwezi kukufanya chochote, najua huwezi kunidanganya.” Aliongea akijichekesha, nililazimisha kicheko lakini ukweli nikua nilikua naogopa.
Hawakukaa sana, nilipomuambia tu kuwa nimekosa ile hati siku ileile walirejea, alikua kachoka wakati Baba na Mama wameingia chumbani kulala yeye alilala sebuleni. Alikua kakaa akapitiwa na usingizi, nilitamani kumuamsha na kumuelezea vizuri kua nilihangaika kuitafuta ila sikupata chochote lakini niliogopa pia. Nilimuacha pale sebuleni ambapo alilala mpaka asubuhi, wengine walipoamka walishangaa kumkuta pale.
“Umelala hapa, si ungeingia ndani?” Baba alimuuliza, ilikua ni alfajiri sana, kama kawaida mimi ndiyo nilikua mtu wa kwanza kuamka, nilimuona pale lakini sikumsemsha mpaka Baba alipoamka na kumkuta ndiyo akamuamsha.
“Daaaah! Jana nilichoka sana, nimepitiwa. Wifi yuko wapi nimuage?” Alijiongelesha huku akinyanyuka na kujitengeneza tengeneza nguo.
“Hapana, kaa kwanza unywe chai, Mary, muandalie Shangazi yako chai. Wifi yako hajisikii vizuri, nadhani nayeye ni uchovu wa jana, hakulala vizuri.” Baba alimjibu.
“Kuna nini, yale mambo yameibuka tena?”
“Hapana, ni uchovu tu.”
“Aaaaah!” Mama alionyesha kujali sana, nilimuangalia namna alivyokua akiigiza mpaka nikatamani kutapika.
Nilimuandalia chai akanywa, Baba aliondoka kwenda kazini, kutokana na ugonjwa Mama alishaacha kazi na alikua akisimamia biashara za Baba hivyo hakua na sababu za kuwahi kuamka. Nilikaa kumuangalia Mama Abdul kama ataondoka lakini alionekana kama vile hana haraka.
“Nikamuamshe Mama?” Nilimuuliza baada ya kuona hata haondoki, baada ya kumaliza kunywa chai alikaa kwenye kochi anaangalia TV, ingawa alionekana kuwa mbali kimawazo lakini hakuonekana kabisa kama ni mtu wa kuondoka.
“Hapana usimuamshe. Hivi unaweza kuendesha gari? Aliniuliza.
“Ndiyo lakini sina leseni…” Nilimjibu, sikujua sababu za yeye kuniuliza vile.
“Una hela ya Tax, kuna sehemu nataka nikutume.” Nilishangaa kidogo kwanini alikua ananiuliza vile, kama ni pesa nilijua kabisa alikua nazo nyingi sasa kwanini aniulize mimi.
“Ndiyo, unataka kunituma wapi?” Nilimuuliza kwa mshangao, alionekana kuwa na wasiwasi na uso wake haukua ule wa kuamrisha, ilikua ni kama anataka kuniomba kitu flani.
“Si unajua kuficha siri lakini?” Aliniuliza hukua kiniyooshea mkono na kunitaka nikae kwenye kiti pembeni yake.
“Ndiyo, nina siri nyingi sana naficha.” Nilijibu huku nikikaa, bado nilikua simuelewi bado nilikua sijajua alikua akimaanisha nini.
“Nataka uende nyumbani kwangu, mume wangu sasa hivi atakua kazini, nataka ukanichukulie baadhi ya nguo zangu uniletee.” Aliongea kwa upole, nilimuangalia kwa mshangao, nayeye aliniangalia kuona kama nimeelwa.
“Kwanini, si unaweza kwenda kuzichukua?” Nilimuuliza kwani nilitaka kujua ni kwanini hataki kwenda kwake.
“Hapana, nataka wewe uende kuzichukua, niletee nguo nyingi uwezavyo, hakikisha mume wangu hayupo nyumbani ndiyo uingie, kama yupo jifanye ulienda kunisalimia, niulizie mimi na jifanye hujui kabisa niko wapi.”
Aliongea kwa kusisitiza, kusema kweli sikumuelewa lakini sikua na sababu ya kuuliza maswali mengi. Nilihisi kuna kitu ambacho hataki mtu yeyote kukijua.
“Ukikutana na mtu yeyote usijekumuambia niko wapi!” Aliongea kwa suti ya juu kama vile ananifokea. Nilinyanyuka na kuinga ndani, nilichukua pesa kidogo nilizokua nazo na kuanza safari ya kwenda kwake. Wakati natoka alinielekeza nguo za kuchukua pamoja na baadhi ya vitu vyake vingine na sehemu vilipo.
Nyumbani sikumkuta mume wake, nilimkuta binti wa kazi, nilimpigia simu na kumuambia kua kuna binti wa kazi, akaniambia nimpe simu aongee naye, nilimpa na baada ya wao kuongea binti wakazi bila kuniambia chochote alinielekeza mpaka ndani, nikachukua nguo kama nilivyoagizwa na kuondoka. Wakati tunapanga nguo nilijaribu kumdodosa lakini hakuniambia, aliniambia hakuna kitu kama nataka kujua nimuulize Mama Abdul mwenywe, kwa kumuangalia alionekana kuogopa kusema kitu chochote cha Bosi wake, sikumlaumu hata kama ni mimi ningeogopa.
Nilirudi nyumbani na kumkabidhi zile nguo, Mama alishaamka lakini alikua jikoni, aliziingiza katika chumba cha wageni na kukaa huko.
“Usijekumuambia mtu!” Alinitishia.
“Kumuambia nini?” Niliuliza kwa mshangao kwani kusema kweli sikua nikijua ni kitu gani kilikua kinaendelea.
“Acha kunifanya mjinga najua Agness (Binti wake wa kazi/sio jina lake halisi) kashakuambia kua nimegombana na Baba Abdul ni jambo la muda tu sitaki uanze kupiga piga umbea.”
“Hapana shangazi, hakuniambia chochote na mimi sikumuuliza.|” Alishtuka kidogo kusikia vile lakini aliniambia.
“Ndiyo nishakuambia sasa, mimi na Mjomba wako hatuko vizuri. Watu wanajua niko hapa kumhudumia Mama lakini huo ndiyo ukweli, sasa sitaki maneno maenno kusambaa.
Nilimhakikishia kua siwezi kuongea chochote.
“Isitoshe mimi nataka kuondoka, sitaki kuendelea kufanya tena kazi, kuna sehemu nataka nikashone naondoka wiki hii.” Nilimuambia, alionekana kushtuka.
“Unaenda wapi? Huwezi kuondoka, kuna mambo yangu mengi sijayakamilisha, unafikiri ukiondoka kazi za hapa nani atafanya.” Alionekana kupaniki sana, ni kitu ambacho hakukitegemea.
“Si kuna mfanyakazi mwingine na wewe si umesema utakaa hapa kumhudumia Bibi?”
“Hakuna mfanyakazi mwingine! Lazima ubaki mpaka apatikane.”
“Si yupo jamani, mbona hapa tuko wawili…” Nilimuambia kujaribu kumuelewesha lakini aligoma.
“Huyo nishamfukuza.”
“Tangu lini mbona nimemuacha sebuleni.”
“Tangu uliposema unaondoka, simtaki tena, huwezi kuondoka mpaka unikamilishe mambo yangu, unajua siri zangu nyingi sana hivyo kama nikikuacha ukaondoka sitapata mtu mwingine wa kunisaidia.
Sikujua anataka msaada gani lakini alikua anamaanisha, alitoka na kumuambia yule mfanyakazi mwingine kuchukua kilichochake na kuondoka.
“Ni mwizi, nimemuona akipekua pochi yangu!” Alimuambia Mama, kusema kweli nilijisikia vibaya kwani hakufanya chochote, niliona kama ni mimi ndiyo nimemfukuza, nilitamani kumteteea lakini nilijua kua siwezi kusikilizwa, kwa wakati ule yeye ndiyo alikua Bosi mpya, binti wa watu aliondoka na mimi kuendelea kubaki pale kama mfanyakazi. Hakuna aliyejua kua kagombana na mume wake zaidi yangu, wengine wote aliwaambia kua kaenda pale kumsiadia Mama yake kwani hana mfanyakazi.
***
Pamoja na kusema kua alikua pale ili kumhudumia Bibi lakini hata siku moja hakuwahi kumhudumia, muda mwingi alikua bize na Mama, wakienda na kuzunguko wote dukani, walikua mashoga haswa kitu ambcho kilizidi kunikera. Shangazi alisusa nyumba yake kabisa, hata katika biashara zake alikua haendi kitu ambacho kilinifanya kuchunguza. Niliyoyasikia sikuyaamini kwani haikuingia akilini mtu mwenye roho kama ya Mama Abdul kufanyiwa vile.
Alikua amemfumania mume wake na mwanamke mwingine na pale alipojaribu kuongea basi aliambulia kupigwa na kufukuzwa. Nilishangaa kwani nyumba waliyokua wakiishi kwa kiasi kikubwa ni yeye alijenga kwa kutumia pesa za Kaka yake, lakini baada ya uchunguzi wangu nilikuja kugugundua kua kumbe mwanaume aliandika kila kitu jina lake. Wala haikua mara ya kwanza kumfumania, mume wake alikua akionekana mpole kwa nnje.
Kwa kumuangalia ungesema labda Shangazi alikua akimtawala lakini kumbe si kweli, alikua ni mtu wa kubadilisha wanawake na mara nyingi akifumaniwa Shangazi huishia kupigwa. Kwangu ilikua ni kama maajabu lakini kwa kukaa na Shangazi muda mrefu na kumchunguza niligundua kulikua na ukweli flani. Mara nyingi anapokua peke yake anakua mpweke, anaweza kujifungia chumbani na kulia.
Kuna mara kibao nilishamsikia akiongea na simu na mume wake kumuomba msamaha na kumuomba hata awatembelee watoto wake shuleni lakini ilionekana kama mume wake alimkatalia. Biashara zote alizokua akimiliki zilikua na majina ya mume wake hivyo alikuja pale nyumbani akiwa hana kitu kabisa. Kwa mambo aliyokua akiyafanya usingeweza kuamini kua alikua akinyanyasika na kuumizwa na mume wake.
Siku moja nilikua nimekaa zangu chumbani, Mama Abdul aliingia na kunipa noti mbili za Shilingi elfu kumi.
“Ile pesa yako ya Tax siku ile.” Aliniambia, nilijaribu kumkatalia lakini alisisitiza, pamoja na shida zangu za pesa lakini nilikua naogopa pesa zake, sikua na pesa nyingi lakini niliziona pesa zake kama za kichawai flani.
“Chukua, hazina shida.” Ni kama alisoma akili yangu, kwa aibu flani iliyochanganyika na uoga nilizipokea.
“Ulisema unataka kuondoka hapa?” Aliniuliza, nilijikuta nadakia kwa furaha.
“Ndiyo nataka kuondoka, si kwasababu sitaki kumhudumia Bibi lakini nataka kuanza maisha yangu.” Nilijaribu kujielezea, hakuonekana kujali sana maneno yangu, alikua na mambo yake kichwani.
“Kuna kazi moja nataka unifanyie, ukishaimaliza hiyo nitakuacha uondoke na kama ni pesa nitakupa pia.” Aliongea kwa sauti ya chini, alikua mpole kidogo.
“Kazi gani?” Nilimuuliza kwa shauku.
“Utajua tu huko mbeleni, lakini unapaswa kunikubalia hapa, sitaki mambo ya kuja kugeukana huko mbeleni.” Aliniambia, nilitafakari na kumuuliza tena kama ni kazi gani, nilimuambia itakua vizuri kama nikijua ni kazi gani kabla ya kuikubali lakini alikataa kuniambia.
“Si kazi mbaya ni kazi halali lakini nitakuambia mwishoni, ninachotaka niwewe kunikubalia na ikifanikiwa basi wewe utaondoka kwenda kuanza maisha yako, Mama tutamuondoa hapa.”
Kwa namna alivyokua akiongea hata sikua na namna, nikubali nikatae nilijua kabisa nilazima nitaifanya ile kazi yake, nilikua kama mateka flani hivi na sikua na maamuzi ya chochote kile. Aliondoka na kunaicha akiwa kashajijibu kua nimekubaliana na kile alichoniambia. Siku ile niliwaza sana lakini sikupata jibu, ukaribu wake na Mama ulizidi kuongezeka, walikua wakizunguka kila sehemu pamoja kitu ambacho kilikua kikimuuma hata Bibi.
“Umeona, kashamharibia mwanangu ndoa yake, katelekeza mume kazi ni kuzunguka na wifi yake, hivi kwanini wanawake tunakua hivi, mtu ndoa yako inakushinda ndiyo unaanza kuhanagika na ndoa ya mwingine!” Bibi aliongea, nilimuangalia kwa kumshangaa, nilitamani kumuambia kila kitu lakini nilijua haitasiadia.
“Mshenzi kabisa, na mwanangu ni lazima aoe mwanamke mwingine, labda nife lakini huyu shetani hapa ataondoka, wanagu hawaongei kwaajili yake, hapana lazima aondoke!”
Nilishazoea huo wimbo, nilijua hawezi kufanya chochote kwani aliyekua akiendesha show nzima ni Mama Abdul ambaye naye alikua na matatizo yake. Hakuhangaika hata na Mama yake, katika miezi miwili ambayo alikua pale sikumuona hata siku moja hata akifua nguo za mgonjwa aliyekua ameenda kumsalimia. Yeye alikua akihangaika tu na biashara za Baba ambazo Mama ndiyo alikua akizisimamia.
Siku moja aliniita chumbani kwake, nilienda kama kawaida lakini ile naingia nikakutana na Mama, alikua amekaa kitandani akilia. Nilimsogelea na kumuuliza tatizo ni nini.
“Muambie ukweli, ashajua kila kitu, ni Kaka yangu lakini siwezi kuona mwanamke mwennzagua anteseka na mimi nikamuangalia. Muambie kilichonikuta kwa mume wangu!” Mama Abdul aliniambia, nilisita kusema lakini alinisisitiza. Ilibidi kumuambia kua ni kweli Shangazi alikua kagombana na mume wake na ndiyo maana akaja pale.
“Mimi ndiyo nilienda kumchukulia nguo zake.” Nilimuambia Mama.
“Unaona, hata nyumba yangu niliyojenga mwenyewe hataki nirudi, unaona wanaume walivyo washenzi, wewe ni mwanamke mwenzangu. Nimeumia sana kuona kua Kaka yangu anataka kukufanyia kitu kile kile ambacho mume wangu kanifanyia…” Aliongea kwa kusikitika, alikaa na kumkumbatia Shangazi, kusema kweli sikumuelewa alikua anamaanisha nini.
“Muambie, muambie mipango ambayo Mama anapanga na wengine ili kukuondoa hapa, utafukuzwa kama mbwa nakuambia.”
Aliongea kweli kulikua na mipango hiyo hivyo nilimuambia kila kitu nilchokua nimesikia.
“Nahuyo mwanamke kashaletwa mpaka kwenye nyumba hii, muuliza Mary hapo kua ukiwa dukani si huyo mchumba alochaguliwa huja kulala humu ndani! Imeniuma sana kuona unayofanyiwa, binti wa watu ndiyo kaamua kuniambia kwakua anaogopa, kumbe sisi tukitoka tunahangaika kutafuta pesa ili wale wao yeye analeta mwanamke mwingine ndani, muulize usije kusema mimi namuwekea maneno!”
Pamoja na kwamba nilishasikia mipango ya Bibi kumtafutia Baba wanamke lakini hata siku moja sikuwahi kumsikia Baba akisema anataka hivyo vitu, mara nyingi alikua akigombana na Bibi kwa sababu hiyo. Lakini kilichonishangaza zaidi ni ile kusema kua Baba analeta wanawake wengine ndani, ilikua ni mara ya kwanza kusikia lakini Shangazi aliniangalia kiasi kwamba nikashindwa kuongea, nilitingisha kichwa kukubliana naye moyoni nikijua kua ni uongo.
“Umemsikia mwenyewe, binti wa watu kaja kuniambia kwakua anajua kua kinachofanyika si kitu kizuri, nani anahangaika na baishara? Nani anahangaika na watoto? Kila kitu unafanya wewe lakini wanataka kukudhulumu uondoke bila hata sumuni, wanataka kukunyang’anya na watoto, imeniuma sana kwani hata mimi nimefanyiwa unyama huo huo!” Alikua anatoa machozi kabisa, sikuelewa sababu zake lakini niliamini kua ana sababu zake ingawa bado nilikua sijui ni nini?
Mama Abdul naonekana kuwageuka wenzake na kumuambia wifi yake siri kua anatakiwa kuondolewa mule ndani. Je ni kwamba kaokoka na anamtakia mema au kuna kitu chake kakipanga basi hembu fuatilia sehemu ya kumi
(ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI MBILI; Mama Abdul anafukuzwa na mume wake na kuja kuishi kwa Kaka yake, anaanza kuwa rafiki na wifi yake na kumteka akili kabisa. Baada ya kushindwa kupata hati ya nyumba anaamua kumuambia wifi yake kua anakaribia kuachwa hivyo kuwa makini je ana sababu gani za kumuambia vile wifi yake? Kama hukusoma sehemu zilizopita pitia iukurasa wangu wa Instagram @iddimakengo @iddimakengo…ENDELEA.)
Sikua nikijua mpango wa Mama Abdul mpaka baada ya wiki mbili baadaye, kuna wakaka wlaikuja pale nyumbani na walionekana kama wanatoka Benki, walikua wakikagua nyumba, waliongozana na Mama Abdul na Mama. Niliwaangalia nikijifanya kua sifuatilii, lakini ni kama walikua kama wanafanya tathimini, hawakutaka kunishirikisha kwani hata siku ile wakati wanaongea Shangazi aliniambia nitoke nnje hivyo sikujua waliongea nini.
Nilisubiri mpaka jioni, nakumbuka siku hiyo Baba alikua kachelewa kurudi, sijui alipitia wapi kwani haikua kawaida yake. Mama alikuja chumbani kwangu, ni kama alitaka kuniambia kitu, alikua amenyong’onyea, anaonekana kutokwa na machozi. Nilimuuliza kama kuna nini kimetokea lakini hakua na jibu sahihi, aliniangalia tu kwa huruma kana kwamba kulikua na kitu kibaya. Baadaye alijikaza na kuniambia kua anataka niondoke pale, hataki niendelee tena kufanya kazi kwake.
“Sikutaka kukufukuza lakini nataka kesho uondoke.” Mama aliongea huku akinikumbatia, ni kama mtu ambaye hakutaka niondoke pale. Nilishindwa kumuelewa lakini nilijua kua dawa za Mama Abdul zinafanya kazi.
“Hakuna dhida Mama, nimeishi vizuri hapa kwenu hivyo huna haja ya kulia, utakua sawa tu, mimi kuna sehemu nimepata nataka kufungua sehemu ya kushona nataka kuanza maisha yangu.”
Niliongea kumpa moyo, nilishachoka maisha ya ile nyumba na nilipanga kweli kuondoka.
Aliondoka na baada ya kama dakika tano hivi alikuja tena.
“Chukua hii hapa, ni laki moja, najua sikubwa lakini nina uhakika tukishapata mkopo basi nitakupa zaidi.” Aliongea huku akinikabidhi ile pesa, niliipokea lakini maneno yake yalinichanganya kidogo, aliogelea suala la kuchukua mkopo.
“Mnataka mchukue mkopo?” Nilimuuliza, nilijifanya kama sitaki kujua sana, kama vile sikutaka kuwaingilia lakini nilishapata wasiwasi.
“Ndiyo wifi kasema tunaweza kupata hata milioni mia tano, amesema mimi nimpe tu hati yeye atafuatilia kila kitu.”
“Unamuamini Mama Abdul lakini?” Niliuliza swali la kimtego ambalo mwisho nilijuta kuliuliza alianza kunisimulia namna alivyomsaidia kipindi anaumwa, namna alivyokua karibu, namna alivyowageuka ndugu zake na kuwa upande wake kwani walitaka kumuua na namna anavyomsaidia katika biashara.
“Walitaka kunifukuza lakini sitaondoka bila kitu, nitachukua watoto wangu na nyumba hii itakuja kuwa yangu tu.” Aliongea kwa kujiamini, kwamimi nilimuoka kama vile kachanganyikiwa, hakua yeye kabisa.
Lakini kwa namna alivyokua akiongea nilijua hakuna kitu ambacho ningeweza kusema kikambadilisha. Nilimshukuru kwa pesa yake na kumuambia kua nitashukuru zaidi kipindi akipata pesa ya mkopo na kunipa zaidi. Alitoka na kuniacha chumbani huku akiniambia natakiwa kuondoka siku ileile. Nilijua hazikua akili zake, zilikua ni akili za Mama Abdul. Sikutaka kuingilia mambo yao, nilikusanya vilivyo vyangu na kuita Tax, nilishapata sehemu ya kwenda, kuna rafiki yangu nilimuambia kua nitaenda kwake kukaa wakati nikitafuta chumba changu.
Nilitaka kwenda chumbani kwa Bibi kumuaga lakini Mama Abdul alikua kasimama mlangoni, alitaka niondoke kimya kimya. Kichwani nilijua lazima kuna mchezo anaucheza, nilijua tayari kashamteka Mama hivyo mimi pekee ndiyo nilikua kikwazo cha yeye kumdhulumu kila kitu Kaka yake. Lakini wakati natoka pale niliona gari la Baba likiingia, hawakutaka anione wakati naondoka hivyo waliniambia kurudi ndani harakaharaka.
Baba alishuka lakini hakuonekana kama yuko sawa kabisa, alionekana kama mtu mwenye mawazo, alimchukua Mama na kuingia naye chumbani. Mama Abdul aliondoka mara tu baada ya kumuona Baba, lakini alinitumia meseji na kuniambia “Ukipata upenyo ondoka, sitaki kukuona tena hapo.” Sikumjibu chochote kwani nilishaamua kuondoka. Baba hakukaa sana ndani, alitoka na kuniita, alioneka na kuwa na wasiwasi, aliniambia nimfuate mpaka kwenye gari.
“Mama yako ana matatizo gani?” Aliniuliza, nilijifanya sikulielewa swali lake, nilinyamaza tu lakini alirudia.
“Mama yako ana matatizo gani? Wewe si ndiyo unakaa naye, humuoni kama vile kabaidlika?”
“Mbona mimi naona kama yuko sawa, sijui lakini muulize mwenyewe.” Nilikua nimejibana sana kuongea, nilitamani kumuambia kila kitu lakini nilisita, ile familia ilikua haieleweki hivyo niliogopa kama nikiongea basi mambo yanaweza kunigeukia. “Ninachotaka hapa ni kuondoka tu kwa amani mambo yao watayalamiza wenyewe.”
Nilijisemea kichwani huku nikitamani aniache na kuondoka ili na mimi niondoke zangu.
“Hembu muangalie, kama akifanya kitu amcho hakieleweki basi niambie.” Aliniambia huku akitaka kuondoka, niliwaza na kuamua kumuambia ukweli kua mimi sifanyi kazi tena pale.
“Mama kaniambia niondoke hanihitaji tena.” Nilimuambia, aligeuka na kunaingalia.
“Mama kakuambia au wewe unataka kuondoka?”
“Hata mimi nataka kuondoka lakini Mama naye kasema niondoke.”
Alifikiria kidogo kisha akarudi ndani. Alimuita Mama, nikijua kua atanichongea kwake kua nimemuambia nafukuzwa alisema.
“Huyu binti kesho kutwa nataka nimfungulie biashara, tumekaa naye sana hapa kama binti yetu, hembu zunguka zunguka naye mjini kuangalia fremu, mkipata mtaniambia.” Baba aliongea, hakutaka kubishana wala hakutaka majibu, aliondoka na kuniacha pale. Mama hakusema chochote, alichukua simu yake na kumpigia Mama Abdul ambaye alionekana kama ndiyo ana control kichwa chake.
Baada ya kuongea naye Mama Abdul alinipigia simu kunitukana na kuniambia kama nimelogwa nikaongea mambo yake ataniua. Alinitishia sana, lakini cha ajabu sikuogopa. Baada ya kukata simu nilipatwa na hasira, nilijikuta nachukua simu na kupiga Namba ya Baba, aliipokea lakini mdomo ulishindwa kuongea, nilishindwa kumuambia kitu chochote. Nilikata simu na kumtumia meseji. “Nenda kaongee na Baba Mdogo, msikilize sana Karim, nenda kamuulize na kila atakachokuambia ndiyo ukweli.” Nilibonyeza kitufe cha kutuma meseji kisha nikazima na simu kabisa.
Sijui kwanini lakini nilikua naogopa kabisa, mwili ulikua unanitetemeka na nilitamani kuondoka kabisa pale. Sikuwasha simu yangu mpaka usiku wakati wa chakula, Baba alichelewa kurudi siku hiyo, alirudi sisi tushakula. Mama Abdul ambaye alikua anaishi pale alikua kwenye chumba cha wageni ambacho kilikua ni kama chumba chake. Baba alikuja na kula chakula vizuri, baada ya chakula alienda kumgongea Mama Abdul, ni kama walikua wanataka kuongea.
Lakini ghafla mlango ulifungwa, tulianza kusikia Kelele za Baba akifoka, alikua akimuulizia kuhusu watoto wake, akamuulizia kuhusu hati ya nyumba yake na vitu vingine vingi. Sijui hata alijulia wapi kwani mimi sikumuambia lakini aliongea kwa uhakika. Tulianza kusikia kelele, Baba alikua akimpiga Dada yake, alikua akimpiga huku akimtukana akilalamika kwa kuharibu maisha yake. Alimkumbushia kuhuu Mod, Aziza, alimkumbushia namna alivyokua anamjali, namana livyowapa kila kitu lakini walimgeuka.
Hakikua ni kipigo cha muda mrefu lakini kilionekana kipigo cha nguvu. Mama Abdul alipiga kelele sana, aliomba msaada lakini Baba hakuacha kumpiga, alimpiga sana, tulienda mpaka mlangoni kujaribu kuuvunja lakini ulikua mlango imara. Bibi alisikia akatoka chumbani kwake na kwenda kugonga, alipika kelele na kumuambia atamuachia laana lakini Baba hakujibu chochote, aliendelea kumpiga mpaka hatukusikia kelele tena. Baada ya muda kidogo alifungua mlango na kutoka.
Alikua kama anchungulia na kusema “Mama njoo uchukue Maiti ya mwanao.” Alitoka na kuingia zake chumbani kulala, wala hakwenda popote alikua kama yuko sawa kabisa. Pale chini Mama Abdul alikua amepoteza fahamu, mimi Mama na mdada mwingine wakazi tulimnyanyua na kumbeba mpaka kwenye gari. Alikua bado anapumua, tulimpeleka mpaka hospitalini. Ilibidi kudanganya kua alivamiwa usiku na vibaka wakampiga na kumnyang’anya kila kitu.
Mama Abdul alikaa hospitalini kwa wiki mbili ndipo aliruhusiwa kutoka, alikutana na talakakutoka kwa mume wake na kwenda kuanza maisha ya peke yake kwenye chumba kimoja cha kupanga. Baba likataa kabisa mawasiliano na ndugu zake hata Karim na Mama Aziza hakutaka kuwasikia, Mama yake alichukuliwa na Karim na mkewe kwani alimuambia kabisa yeye ndiyo kamharibia maisha yake na hawezi kuishi naye. Alibaki na Mama, mimi pia nilifukuzwa kwani nilionekana kama nilikua nawasaidia kwa kutokusema chochote.
Angalau nilikua na mtaji wangu na niliondoka na hati ya kiwanja changu ambayo nilipewa na Bibi. Bado mpaka leo najilaumu kwa mambo mengi lakini kila nikiwaza sijui hata ningefanya vipi tofauti na nilivyofanya. Sina mawasiliano tena na ile familia kwani baada ya kuona maisha ni magumu niliuza kile kiwanja milioni arubaini, nikaenda Dodoma na kununua kiwanja kingine nikapandisha nyumba na kuweka fremu za maduka, sasa hivi nina maisha yangu nina biashara yangu mwenyewe kubwa tu lakini kila nikikumbuka ile familia bado siamini ndugu kwenye kitu changu chochote kile.
MWISHO;
0 comments:
Post a Comment