Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

DADA USIMPIGIE MAMA AKIJUA ATANIPIGA

 

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

DADA WA KAZI; DADA USIMPIGIE MAMA AKIJUA ATANIPIGA!—SEHEMU YA KWANZA


Nina umri wa miaka 18, nimeanza kufanya kazi za ndani tangu nikiwa na umri wa miaka 15, nilifanya kwenye nyumba moja kwa miaka mitatu mpaka mwaka huu mwezi wa nane ndipo niliondoka, hii ni baada ya Baba mwenye nyumba kuanza kunitaka kimapenzi, alikua ni mtu wa kunisifia, kunitamani tamani lakini sikuwahi kuhisi kama anaweza kunitaka kimapenzi.


JOIN US ON TELEGRAM

Nakumbuka ilikua siku ya jumamosi, kulikua na sherehe usiku huo, wao walikua wanaenda na mimi nilibaki tu nyumbani. Bosi wangu hasa Mama alikua ni mtu mzuri, tena sana, alikua ananipenda na kikubwa nilikua napenda sana watoto wake. Ana watoto wawili, wote wadogo, nakumbuka wakati naajiriwa mtoto wa kwanza alikua na mwaka mmoja, hivyo nilibaki naye nikamlea kama mwanangu.


Napenda watoto kwakweli nao wananipenda, unajua mimi nimezaliwa peke yangu hivyo sikua na mtu wa kucheza naye na wale watoto pamoja na kuwa ni wadogo tulikua tunacheza nao, walinizoea kuliko hata Mama yao. Simu ninayotumia sasa ni yule Mama kaninunulia na kubwa zaidi alikua akinichukulia kama mdogo wake.


Mwanzo nilikua Napata vihela natumia hovyo, lakini baada ya kuanza kukusoma Kaka Iddi, nilianza kubadilika, nikaanza kujikusanya mpaka nikanunua kiwanja changu kwani kweli mbali na msahaha kwakua kila kitu cha ndani nilikua nanunua mimi vihela nilikua Napata. Sasa siku hiyo waliondoka na kuniacha na watoto. Nilihangaika nao mpaka wakalala, nakumbuka nilikua naangalia Tamthilia.


Nilisikia geti linagongwa, nilitoka kufungua lakini nikiwaza inakuaje wamewahi, nilisikia honi nikajua tu ni Baba, nikafika mlangoni, nikachungulia na kuiona gari ya Baba, nilimfungulia akaingiza gari kisha nikafunga geti. Baada ya kufunga geti niliingia ndani, lakini nilishangaa anashuka Baba peke yake, aliniita karibu na gari na kuniuliza kama watoto wamelala nikamuambia ndiyo.


“Basi nnjoo, hatuwezi kufanyia ndani, njoo kwenye gari.” Aliniambia huku akinishika na kunivuta kwenye gari, mapaka wakati huo nilikua sijajua ni kitu gani alikua anataka kufanya, lakini kwa namna alivyonishika mkono niliumia, nilijivuta ndipo akanishika na kuninyanyua, akafungua mlango wa nyuma wa gari akanirushia huko, aliniinamia na kunichania suruali yangu niliyokua nimevaa kisha naye akaanza kuvua suruali yake.


Alikua akiongea manenoi ya kunibembeleza lakini sikumsikia, hapo ndipo nilija kuwa anataka kunibaka, sikua tayari kwa hilo, katika maisha yangu nilikua bado sijawahi kufanya mapenzi, sikutaka siku yangu ya kwanza iwe vile. Kwa namna nilivyomuona nilijua kabisa kuwa siwezi kumshinda nguvu, nilimuacha akamaliza kuvua suruali, lakini sikubisha, na mimi nilijiweka tayari kama vile nampokea.


Suruali yangu alikua ameichana kwa juu na kuivuta chini, lakini bado nilikua nimebaki na nguo ya ndani, nnje kulikua na mwanga wa taa hivyo tulikua tunaonana vizuri. Wakati anahangaika kuvua suruali nilijinyanyua kwenye gari na kumalizia kuivua suruali, alishangaa ninavua na chupi huku nikitabasamu, ni kama nilimkata stimu kwani lengo lake lilikua ni kunibaka hakujua kama nitakubali.


“Nawewe unataka?” Aliniuliza.


“Baba mimi nakupenda muda mrefu ni wewe tu!” Nilimuambia huku nikimsogelea kama vile namkumbatia, alikua ndiyo naamalizia kuvua suriali hivyo ilikua haijatoka vizuri, alisimama suruali ikiwa ameiachia miguuni. Nilijikaza sana na kukusanya nguvu, nikiwa nimemsogelea nilikunja mguu wangu wa kulia, kwa nguvu niliurudisha nyuma na kumpiga katikati ya miguu yake kwenye mashine yake.


“Mamaaaa !” Alipiga kelele huku akiinama kushikilia vifaa vyake, kwa namna nilivyokua nimempiga kwa nguvu hakuweza kunyanyuka, alilala chini akipiga kelele hivyo na mimi nilipata upenyo, nikiwa uchi vilevile nilikimbia nakutoka mpaka nnje ya geti. Nikajibanza kwa pembeni sehemu ambayo haikua na mwanga, sijui nilipata wapi huo ujasiri kwani baada ya kutoka nilikua natetemeka kwa uoga nikijua kuwa Baba atakuja kunivamia.


Hakutoka mpaka baada ya nusu saa hivi, alitoka na gari ndipo mimi nilipata nafasi ya kuingia ndani, nilienda mpaka kwenye chumba cha watoto na sikutoka mpaka Mama aliporudi na kunipigia simu kuniambia nimfungulie mlango. Walirudi na Baba ambaye alionekana kama vile anachechemea, sikumsemesha chochote lakini siku iliyofuata nikijua kabisa kuwa siwezi kuendelea kufanya kazi pale nilimuambia Dada kuwa nyumbani wameniita.


Nilimuambia naenda na kurudi lakini alipona nakusanya kila kilichochangu alijia surudi, aliuliza sana sababu lakini sikumuambia, sikutaka kuvunja ndoa yake. Alinibembeleza sana lakini baba alimuambia aniache, aliongea maneno mengi lakini sikumjibu, niliondoka, nikarudi nyumbani kwetu iringa, sikukaa sana ndipo nilipata kazi kwenye hii nyumba ambayo nipo hapa.


Nina kama mwezi hivi tangu kuja hapa, mwezi kasoro naweza kusema, hii nafasi nilitafutiwa na Dada mmoja hivi ambaye nilikutana naye Facebook. Sababu ya kuja kufanya hii kazi nilitaka tu kuwa dar, kwakua nilishanunua kiwanja changu nilitaka kuja kujipanga ili nifanye Biashara kwani nilishanunua kitabu chako cha Biashara.


Kwa pesa niliyokua nayo nilijua kabisa kama nikija na kuanza kupanga itaishia kwenye kodi, hivyo niliona nianze taratibu kama ulivyosema kwenye kitabu chako cha Biashara 50. Hii nyumba ni tofauti na ile ya mwanzo, hapa Mama mwenye nyumba hafanyi kazi, ni Mama wa nyumbani lakini hatulii kabisa nyumbani, ana kisirani cha hali ya juu.


Kwanza nilipokuja tu alianza kuhusu mavazi, hataki nivae suruali, hataki nivae nguo fupi, nywele ni kunyoa yaani ni masharti mengi mengi ambayo kusema kweli yanaboa, lakini kwakua mimi nina akili zangu na ninajua hajiamini nilifanya kila kitu nikijua kuwa mwisho wa siku natafuta nini. Kazi zote za humu ndani nafanya mimi, Mama hafanyi kazi lakini hagusi chochote, hata nguo za ndani namfumia mimi.


Ana watoto wawili wadogo na ni mjamzito hivyo tumatuma yake ni balaa, mtoto mmoja ana miaka mitano na anasoma Bweni chekechea na mdogo ana miaka mitatu. Ni katoto kakike kadogo na kazuri, lakini ile siku nakabidhiwa tu mtoto nikahisi kwamba kuna kitu hakiko sawa, kwanza katoto kadogo lakini kana nidhamu ya ajabu, mfano ukiwa jikoni, kwa kawaida watoto wanakua wasumbufu, mara kamwaga hiki mara kamwaga kile.


Lakini kenyewe ukikaambia kaa hapo hakatanyanyuka mpaka kanapata usingizi, lakini si kachangamfu, kamenyamaza nyamaza tu. Lakini kwenye chakula, kuna watoto wa aina mbili, aina ya kwanza ni wale ambao hawapendi kula, hawa kwenye kula mtakabana, mtasumbuana, mtabembelezana na kula inakua ni kwa kilio.


Aina ya pili ni watoto ambao wanapenda kula, hawa wao kwenye kula wanakua wachangamfu, anakula lakini atajimwagia, atachezea chakula, atacheka, yaani katoto kanakopenda kula kanakua kamechangamka flani hivi. Sasa kuna aina ya tatu ya watoto ambao ndiyo huyu, yeye kula anakula, lakini anakula kama adhabu.


Ukimpa chakula hata kabla ya kumeza kama ukinyanyua kijiko basi anafungua mdomo kula, anakauoiga flani kana kwamba utampiga, unakuta anakula, anatamani kulia lakini hawezi amefungua mdomo, lakini kitu kingine kama anakula, usipoacha kumlisha atakula mpaka apasuke kwani hawezi kusema nimeshiba, ni kama mtoto ambaye anapigwa sana hivyo anajua asipofungua mdomo basi atapigwa.


Lakini kuna kitu kingine, ni kaoga, yaani kapo mbali na mimi na nikaoga, ana miaka mitatu, anajisaidia kwenye Poti akimaliza anapeleka chooni mwenyewe, unaweza kudhani kamefunzwa vizuri lakini kanafanya kwa uoga yaani kana kwamba kujisaidia ni kosa. Siku ya kwanza sikumuogesha mimi wala siku ya pili, ya tatu Mama yake aliondoka.


Hafanyi kazi lakini anatokaga na kurudi jioni kuna suka flani anaenda kukaa sijui anauzaga madera mimi hata sijui. Sasa wakati namuogesha maji ya kimuingia tu kidogo basi anapiga kelele, mimi nilikua nashangaa, anapiga kelele kama anapata maumivu lakini anaogopa kulia. Labda niwafafanulie, kuna wale watoto ambao hawapendi kuoga.


Hawa ukiwaogesha ni kulia mpaka mnashikana, lakini huyu anakuacha umuogeshe ila maji ya kimuingia anapiga kelele, nilimuuliza ana tatizo gani akanijibu kwa uoga.


“Inaumaaa!” Aliongea kwa uoga.


“Nini inauma?”


“Huku, inauma…” Aliongea huku akinionyesha makalio, kwa kumuangalia kwa nnje alikua kawaida, lakini ukichanua makalio yake, ukiangalia hapa katikati huwezi amini, kuna makovu na vidovindonda kama mtu alikua anafinywa.


Yaani ni kama ukucha umekata, aisee, nilishtuka, nilimpanua vizuri kumuangalia nyuma, alikua kama kaoza, mpaka nikawaza hivi mama yake jana yake si kamuogesha inamaana hakuona hiki kitu. Nilimnyanyua na kumkalisha mapajani kwangu, kisha nikamkagua vizuri sehemu ya mapaja hapa katikati ya uke na makalio, kuna vidonda vidonda vidogo vidogo, lakini sasa kwa sisi ambao tumezoea watoto tunajua kuwa mtoto anatakiwa kuwaje.


Kwenye uke wake, ni katoto kadogo lakini  ukikagua ni kama kamefanya mapenzi jana yake, mtoto wa miaka mitano amepanuka yaani sijui nikuambieje.


“Umefanya nini?” Nilikauliza, kalianza kulia, nilihisi kitu ni kama alikua anafabakwa, mwanzo nilihisi labda ni mwanaume, niliwaza unajua inawezekana labda Baba yake anamfanyia hivi.


Maana nakusoma sana Kaka najua mambo yanayotokea, niliogopa, moja kwa moja nilijua kuwa huyu mtoto hayuko salama. Nililimkausha vizuri kisha nikarudi naye chumbani, nikakaa naye kitandani, uzuri kanaongea na uzuri najua watoto, nikaenda dukani, nikamnunulia pipi za vijiti, nikampa alikua anaogopa hata kupokea lakinia lipokea akala nikaanza kumuuliza.


Kabla yangu kulikua na mfanyakazi mwingine, sikuhisi kama labda anamfanyia kitu kibaya lakini niliamua kukauliza kijanja janja.


“Huku umefanya nini?” Nilikauliza.


DADA WA KAZI; DADA USIMPIGIE MAMA AKIJUA ATANIPIGA! —SEHEMU YA PILI


“Dadaaa, dadaa ananiingiziaga vitu humu, ananifinya…” Nilishtuka kidogo lakini sikumuonyesha, mwanzo nilijua kama kale katoto hakaongei lakini baada ya kum,teka na kumdanganya, alivyoanza kuongea ndipo alifumuka kila kitu, yaani kama charahani katoto kadogo ila kaliongea mambo makubwa.


Nilichokuja kugundua nikuwa dada wa kazi alikua anampiga sana, yaani Mama yake akioka tu, ni kupigwa, kulishwa vyakula vya moto na huwezi amini alikua akimfinya sehemu za siri. Niliongea sana na kale katoto, nikampigia simu Mama yake kumuambia kuwa kuna kitu anatakiwa kuja nyumbani. Lakini wakati naongea na Mama yake kalisikia, kakaanza kulia na kuniambia kuwa nisimuambie Mama yake.


“Mama atanipiga! Mama atanipiga!” Kalikua kanaongea huku kakininyang’anya simu, alionekana kumuogopa Mama yake kuliko kitu kingine chochote kile. “Ni Mama wa aina gani huyu?” Niliwaza, kama kila siku alikua anaishi na mtoto wake bila kugundua kuwa anafanyiwa unyama lakini mimi nimekuja siku moja tu nimegundua huyu ni Mama kweli. Nilikata simu na kumuahidi kuwa sitamuambia Mama yake.


Nilisubiri mpaka jioni, Mama yake alirudi kwenye saa mbili usiku, aliporudi alikuta mtoto kashalala, kwanza alianza kufoka kwani mbali na kupika chakula cha mtoto nilikua sijafanya kitu kingine chochote kile.


“Hivi wewe una akili kweli? Unataka mume wangu akija ale nini?” aliongea kwa hasira huku akitaka kunipiga, sikufanya zile kazi makusudi, nilitaka kujua tu yule mwanamke ni mwanamke wa namna gani kwani nilikua sijamsoma vizuri.


Nilimuacha akanipiga makofi kama matano hivi na kuanza kunifinya, alitukana sana kuonyesha kuwa mimi ni mvivu alipomaliza aliniambia niingie jikoni kupika. Mimi nilirudi kukaa na kumuuliza “Hivi unaongea na wanao kweli?” Alishtuka kuona namna ambavyo nilikua nimetulia hata sijali mambo yake.


“Kwanini, wewe ni nani unanifundisha kuhusu watoto…” Alibwabwa sana na mimi nilimuacha akabwabwaja.


“Kwanini mfanyakazi wako aliondoka?” Nilimuuliza.


“Umeshaanza kusikiliza manenio ya watu, hivi kwanini watoto mnakua washenzi namna hii….” Alitukana tena mpaka basi, lakini mimi wala sikujali, nilimuangalia kama chizi flani akaongea maneno yake akamaliza.


“Kuna kitu nataka kukuambia, lakini siwezi kukuamba hapa, mtoto anaweza kuamka na kusikia naongea na wewe na sitaki asikie kwa sasa…” Nilimuambia, alitaka kufoka lakini alipoona jinsi nilivyokua nimetulia alinyamaza.


Nilimshika mkono kama mtoto na kumtoa nnje kisha nikamuambia inaonekana msichana aliyeondoka alikua akimnyanyasia watoto. Alishangaa na kuniambia kuwa mimi ni muongo.


“Hako katoto kaongo, ni mtundu sana, mimi angekua anafanya huo ujinga ningejua, afanye ujinga mbele yangu si ningemua! Unanijua unanisikia!” Aliongea maneno mengi, alijikuta anaropoka namna alivyokua anampiga na kumnyanyasa yule mfanyakazi, aliongea sana na hapohapo nilijua sababu ni kwanini huyo msichana kabla yangu alikua akimnyanyasia watoto.


“Ukimuogesha mtoto si unaona namna anavyolia?” Nilimuuliza.


“Anaona lakini yule hapendi kabisa kuoga!” Alifoka, nilimtuliza na kumuuliza.


“Ulishawahi kumuangalia katikati ya matako ukaona makovu, ulishawahi kumchunguza uke wake ulivyopanuka au unamwagia maji tu?” Alinyamaza kwa muda kisha akaniambia.


“Wewe umetumwaee? Utakua umekuja kuniharibia ndoa!” Alifoka, nilitamani kumzaba kofi lakini nilisita.


“Ndoa gani wakati mwanaume mpaka sasa hivi hajarudi, nimekaa siku mbili tu lakini ushapigwa na mume wako nikikaa mwezi si ndiyo nitaona ushetani wote?” Niliwaza lakini sikumuambia.


“Mwanao kuna vitu anafanyiwa, nimeongea naye anasema kuwa mfanyakazi aliyeondoka ndiyo alikua anamfanyia hayo mambo!” Nilimuambia kwa upole, alikaa na kuanza kunisikiliza, nilimuambia kila kitu alichokua kaniambia mtoto wake, alishangaa kusikia vile vitu.


“Kwahiyo unaniona mimi mjinga? Unaona kama mimi simjali mwanangu naweza kumuacha akfanyiwa ushenzi huo bila kusema?” Aliniuliza, nilimuangalia yule mwanamke bila kumpatia jibu, niliwaza hivi huyu ni Mama wa mtoto au ni Mama wa kamb, mbona anajali sana kuhusu yeye kuonekana mzuri kuliko afya ya mtoto.


“Kuna mtu yeyote umamuambia?” Aliniuliza.


“Hapana, mimi sijamuambia mtu yeyote, nimeamua kukuambia wewe kwanza.” Nilimuambia, alionekana kupumua kwa nguvu kama amepata ahueni kidogo.


“Basi usimuambie mtu, acha mimi nitadili na hiki kitu mimi mwenyewe!” Aliniambia kwa sauti ya ukali, sikuwa na mpango wa kumuambia mtu yeyote lakini nilitegemea kama labda atamuambia Baba.


“Hata baba nisimuambie?” Nilimuuliza.


“Umuambie kama nani? Wewe ni nani hasa mpaka umuambie mume wangu? Kwanza nakuaminije kama unayoongea ni kweli?” Alifoka sana bila sababu, kuepusha shari nilimuomba msamaha, alinilazimisha kuingia jikoni kupika, nilifanya hivyo, chakula kilichelewa kuiva na wakati wa kula hatukuongea chochote.


Asubuhi ya siku iliyofuata niliwahi kuamka kama kawaida yangu, nilifanya kazi zangu vizuri za asubuhi, mtoto alikua bado hajaamka, aliamka kwenye saa mbili hivi. Alipoamka tu Mama yake ni kama alikua anamsubiri, hata kabla ya kunawa uso, au kunywa maziwa alianza kumvua nguo ili kumuangalia. Mimi nilikua sebuleni, nilisikia sauti za mototo akilia chumbani.


“Umefanya nini huku? Nani kakufinya? Ni dada kakupiga? Alikua anakufanyia nini?”


Mama alikua anamuuliza mtoto maswali, mtoto hakua anajibu zaidi ya kulia tu, nilijikuta napandwa na hasira, nilikimbia harakaharaka mpaka chumbani kuwafuata.


“Unamuumiza mtoto!” Nilimuambia huku nikimshika Maka aliyekua amekaa kitandani kamuinamia mtoto anamkagua kama anatafuta kitu katika mwili wake.


“Wewe muongo, mbona hakuna kitu, haya si makovu tu ya kawaida! Muongo! Unataka tu nionekane mbaya! Muongo!” Mama aliongea kwa hasira, alikua kama anataka kulia, unajua nilimshangaa, sasa mimi nidanganye nini wakati kila kitu kinaonekana.


“Unamtisha mtoto! Hivi unavyomfanyia hivi unafikiri anaweza kukuambia kitu! Yaani mtoto ataona kabisa kuwa humuamini! Hembu muache! Hata kama mimi ni muongo lakini ongea na mimi si mtoto, unaona unavyomshika hata wewe mwenyewe unamuumiza!” Niliongea kwa hasira, sijui nilipata wapi nguvu kwani yule Mama alikua na mwili mkubwa, alikua kakaa, nilimnyanyua na kumsukuma nnje kisha nikafunga mlango kwa ndani, nilianza kumbembeleza mtoto.


“Kwanini umemuambia Mama? Kwanini umemuambia Mama? Mama atanipiga! Nilikuambia usimuambie Mama!” Mtoto aliongea, kwa namn alivyokua anaongea alikua kama mtoto mtu mzima anaumia, ukizingatia ndiyo kwanza ana miaka mitatu labda na nusu sasa hivi lakini alikua na hisia za mtu mzima. Nilimbembeleza na kumuambia asiogope Mama yake hatampiga, alikua anaonekana kumuogopa sana Mama yake, alinikumbatia sana huku akinisihi nisimuache kwani Mama atampiga sana.


Kila nilipokua nataka kutoka pale chumbani alikua akinishika na kuniambia nisitoke, nililazimika kutoka naye mpaka jikoni, nikampa maziwa akanywa kwanza kisha nikaanza kumpikia uji. Mama yake alikuja na kuanza kujichekesha chekesha, akimuomba msamaha na kumuambia kuwa asimuogope kwani yeye ni Mama yake. Nilimuomba aondoke kwani mtoto anaumia na kuna kitu. Aliondoka na kwenda kukaa chumbani kwake, baada ya kumaliza kupika uji nilimpa mtoto akatoka nnje kucheza na watoto wenzake kisha nikarudi chumbani kwa Mama.


“Kwanini umefanya vile? Unajua mwanao anakuogopa, kuna mambo mengi mabaya anafanyiwa lakini anaogopa kukuambia?” Nilimuuliza kistaarabu kwani nilimuona kama ni mtu ambaye yupo kwenye mawazo mengi, alionekana kuwa mbali sana.


“Baba yake akijua ananiacha, unajua kuwa mume wangu yupo na mimi kwasababu ya watoto tu, akijua hata nimeshindwa kuelea ataniacha na sijui nitakua mgeni wa nani?” Alianza kulalamika, nilimuangalia kwa mshanagao lakini sikusema chochote.


“Hivi unafikiri ndiyo sababu Zack aling’ang’ania kukaa boarding, labda nayeye ananiogopa?” Aliniuliza Zack (Sio jina lake halisi) ni mtoto wake wa kwanza wakiume ambaye naye alikua anasoma bweni.


“Mimi sijui kwanini Baba akuache wakati wewe ni mke ake?” Nilimuuliza.


“Wewe hujui ndoa hizi mdogo wangu, hivi umekuja juzi, umeshawahi kumuona anarudi mapema humu nyumbani? Basi ukikaa hapa ndiyo utaona, anaweza kuondoka hata mwezi harudi nyumbani, anatuma tu matumizi kwakua anajua nina mtoto wake, kila siku tunagombana, nimeshamfumania mapaka nimechoka, anatembea na kila kiumbe kilichopo mbele yake, hivi unafikiri akiniacha mimi hapa nitakua mgeni wa nani?”


Alianza kunielezea matatizo yake ya ndoa, alianza kunielezea namna ambavyo mume wake anachepuka na jinsi ambavyo anabadilisha wanawake. Ingawa nilimuonea huruma lakini sikuona ni kwa namna gani kuchepuka kwa mume wake kunamfanya kutokujali watoto wake. Hakua na jibu la kueleweka, nilimuambia pamoja na yote lakini mtoto anahitaji msaada anahitaji kupelekwa hospitali. Aligoma katakata kuhusu hilo, aliniahidi tu kuwa atakua makini lakini hawezi kumpeleka hospitalini kwakua Baba wa mtoto atajua.


Nilitoka na kumuacha chumbani nikiwa sielewi kabisa ni kwa namna gani mwanamke anaweza kuacha mtoto wake akateseka kwa namna ile kisa tu analinda ndoa. Niliendelea na mambo yangu, mchana Mama alitoka na kuniambia nisimuambie mtu yeyote kilichotokea.


“Lakini watu wanatakiwa wajue, huyo binti inawezekana akaenda kufanya kazi sehemu nyingine sasa huoni kama anaweza kuharibu mtoto mwingine.”


“Akiharibu ni wakwako? Wewe naona kazi itakushinda, umekuja kufanya kazi na si kuharibu ndoa za watu mshenzi wewe! Unajifanya una uchungu sana, huyo ni mwanangu nimemzaa mimi najua chakufanya!” Nilimuambia kistaarabu lakini alinijibu kwa hasira, alionekana kupaniki sana hivyo nilinyamaza nikiwa sielewi kwanini anakua hivyo.


Sijui ni kama nina kiherehere lakini kwa kawaida si mtu wa kuacha mambo yapite, pamoja na kuambiwa kuwa hayanihusu lakini nilitaka kujua zaidi. baada ya kumaliza kazi zangu nilitoka nnje kupiga umbea, nilikua na mtoto nimempakata, nnje ya nyumba kulikua na kama kakijiwe flani hivi, ni ka wamama watu wazima na wengine wamakamu tu. Nilitoka na kuwasalimia, baada ya kuniona nimetokea kwenye ile nyumba wala sikua na hata tabu ya kupata umbea.


“Wewe ndiyo umekuja kwa huyo Mama?” Waliniuliza, niliwaitikia na baada ya maswalimaswali mmoja aaliropoka.


“Nawewe utaondoka tu!” Nilitulia sikutaka hata kuuliza kwanini, raha ya mbea usimuonyeshe kuwa una shauku ya kujua mambo, muache atawashwa na kuongea mwenyewe.


“Kale katoto kengine alikua anakatumikisha sana, kamekaa mwaka mmoja kakafukuza, kalikua kakimya sana. Huyu Mama sijui kwani hakaagi na mfanyakazi?” Mwingine aliongea.


“Yaani kapata mume mzuri lakini anayomfanyia! Unajua alikua anaingiza wanaume mpaka ndani, kuna Mbaba mtu mzima alikua anamuingiza humu ndani, mume wake akisairi analeta wanaume ndani!” Aliongea, waliongea maneno mengi mimi nawasikiliza tu, nilikua nashindwa kuelewa, Mama alikua anamlaumu Baba kwa umalaya, wambea mtaani wanasema kuwa naye ni Malaya analetwa wanaume ndani, nilishindwa hata kujua lipi la kushika.


“Sma kela katoto nako kalikua kakimya lakini kababe! Unakumbuka siku ile kanaondoka walipigana hapa nnje, alikua hataki kumpa pesa zake!” Aliongea.


“Alikua anakanyanyasa sana, hivi unajua yule binti alikua anapigwa sana, kuna siku nilienda kwao kuchota maji, aisee kalikua kanafua, eti nguo haikutakata, yule Mama akawa anakapiga akachukua nguo nakumbuka ilikua suruali na kuanza kuisokomiza mdomoni, yaani yule Mama ni mshenzi, na mwili wake mkubwa alikua kakashika katoto kawatu kakakaba na suruali ameisokomeza mdomoni!” Waliendelea kuongea.


“Kua makini, aisee hii si familia, kuwa makini sana kwani huyo Mama sio mtu. Mume wake hakai sana, halafu unajua kuwa yule Baba ni mkimya sana?” Mmoja aliuliza.


“Mkimya lakini nasikia anampigaga.”


“Hata mimi, kukaa na mwaamke kama yule kazi sana, ningekua namdunda kila siku, hana kazi lakini hata kukaa na sisi humu hataki, anatuona wambea wakati anatoka anenda kushinda huko mtaani! Mimi nahisi anaenda kwa mabwana zake! Mwanamke huna kazi mama wa nyumbani mfanyakazi wa nini?”


“Wanini, kuna watu wavivu, hivi unajua yule binti mpaka chupi zake alikua anamfulia, aisee, dniyo maana hata kalimuibia bwana!”


“Kalimuibia bwana?” Mwingine aliuliza, alionekana kama hajui chochote, nilitega masikio kujua zaidi.


“Ndiyo, si unamkumbuka Fred (sio jina lake halisi) yule dereva wa bajaji, alikua anakuja analala na yule Mama usiku mume wake aisafiri asubuhi Mama akiondoka anarudi analala na binti. Wewe unafikiri alifukuza kwanini, kuna siku alikuja kawahi kurudi nyumbani mtoto kafungiwa nnje analia, Bajaji imepaki nnje wao wapo ndani wanafanya mapenzi!


Mama kuona hivyo akakasirika, wakagombana na kupigana hapo nnje, Mama mtu mzima anagombani mwanaume ambaye hata si mume wake, tena katoto kadogo kama kale?”


“Aisee, haka katoto kameona mengi, kuna kale kakubwa kakiume ndiyo kalikua kakorofi kalikua kanamtukana mpaka Mama yake, yaani, siku hiyo nimesikia kanasimulia wenzake, kalikua kanaongea na mwanangu kanasema Mama yake Malaya, katoto kadogo kanasema Mama Malaya, aisee!”


“Sasa kwanini kasiseme, Mama anabadilisha wanaume kama nguo, wanaume wenyewe basi hata hawna akitu anawaleta mpaka nyumbani watoto wanaona.” Waliongea mambo mengi sana, mimi nilikua kimya na wao walikua wanatiririka, walionekana kuwa na taarifa nyingi, familia ilianza kunichosha, hata wiki nilikua sijamaliza nilishaanza kuchanganyikiwa kwa kusikia vituko. Mwisho waliongea kitu ambacho kilinivuta.


“Sema hasara kwake, yule binti kaondoka, wala hajaenda sehemu nyingine, kahamia kwa mwanaume, huyo huyo waliyekua wanamgombania, nasikia ana mimba yake!”


Nilikua na hamu sana ya kujua alipokua kahamia, nilitaka kujua nini kilikua kinatokea kwanini alikua anamfanyia unyama wote huo mtoto mdogo kama yule. Waliongea mambo mengi lakini niliopoona kuwa hawataki kutaja alipohamia niilazimika kuuliza.


“Kahamia wapi? Awapi na huyo mwanaume?” Niliuliza, walinigeukia wote kunishangaa kwani wakati wote walipokua wanapiga umbea nilikua kimya, ghafla wanasikia ninaongea, lakini kabla ya kupata jibu nilisikia sauti ya Mama.


“Naona unanichimba, wahiyo ndiyo umeamua kuja kwaambia kila kitu hawa wambea wanzako, sasa kwa taarifa yako ondoka, sikutaki tena, mtoto umekuja juzi unataka kunikaa kichwani!” Mama alikua karudi kanikosa nyumbani ndipo akaja na kunikuta pale, alikasirika sana kwani alikua hapatani kabisa na hao wanawake.


DADA WA KAZI; Anaambiwa kuwa kazi imemshinda, kuna mambo mengi yanaendelea, je ataondoka kimya kimya? Je atamuambia Baba kilichotokea, basi endelea kufuatilia hapa, stori bado mbichi, ni ya wiki moja tu iliyopita hivyo bado mbichi kabisa, hembu kama unajifunza kitu #SHARE kuna Baba hafuatilii familia yake, anarudi usiku na anadhani wanae wapo salama.


DADA WA KAZI; DADA USIMPIGIE MAMA AKIJUA ATANIPIGA!—SEHEMU YA TATU


Nilishaamua baada ya ile nyumba sitafanya tena kazi za ndani, taayri nilishajikusanya na kamtaji kangu kadogo. Nakumbuka siku naenda kwenye ile nyumba nilikupigia simu Kaka iddi kukuomba wazo la Biashara kwakua nilishanunua kitabu chako, ulinishauri vizuri na kikubwa kilichonifanya kufanya kazi za ndani ni kukosa sehemu ya kuishi, sikutaka kupangisha nyumba kabla ya Biashara yangu kusimama.


Lakini nilikua na uwezo wa kupangisha nyumba na nikakaa, akili yangu ilikua inafanya kazi harakaharaka, “Kama ananifukuza naenda kutafuta fremu na nalala hapohapo kwenye fremu yangu, naigawa kwa nyuma naweka kasehemu kagodoro na mbele ndiyo nauza, nitapata hewa kweli?” nilikua nawaza wakati natembea kuingia ndani, Mama yeye alikua anabwbwaja bwabwaja, hata sikumsikia anongea maneno gani, nilijua nitafukuzwa na sikutaka kukaa mule, nilitaka kuondoka.


“Hata hapa mshahara sidai maana siku mbili hawawezi kunilipa!” Niliwaza, tulifika ndani, Mama alikua ananisemesha simsikii, niliingia mpaka chumbani kwangu na kuanza kukusanya nguo zangu, kumbe Mama alikua ananifuata.


“Unafanya nini?” aliniuliza.


“Napanga nguo zangu.” Nilimjibu kwa mkato huku nikiendelea kupanga nguo.


“UNapanga nguo unaenda wapi?” Aliniuliza.


“Si umesema niondoke,naondoka naenda kutafuta maisha kwingine, mambo ya kulea watoto wa watu yamenichosha, ngoja nikatafute changu na mimi!” Kusema kweli sikujua kama alikua anatania lakini sikujali.


“Hakuna kuondoka, yaani umenza kazi juzi unataka kuondoka, isitoshe mtoto ameanza kukupenda, baki hapahapa! Huendi popote!” Aliongea kwa hasira huku akinifuata na kuanza kupangua nguo, alizotoa kwenye begi na kuzirudisha kwenye kabati. Alikaa chini na kuanza kulia.


“Hivi unajua kuwa watoto wangu mimi hawanipendi? Sijui mimi nina balaa gani, yaani mwanangu mkubwa aliniita Malaya kabisa!” Alianza kulalamika huku akilia, nilitaka kuondoka kweli lakini kuna kitu kama kiliniingia, si jui ni kaumbea au huruma lakini nilikaa na kuanza kumsikiliza.


“Hivi unajua nilikua nafanya kazi? Mimi nina digrii yangu lakini mwanaume aliniachisha, yaani mwanaume wangu ni Malaya, kila mtu anamuona mkimya lakini ni Malaya sana, alishatembea mpaka na mdogo wangu wa damu!” Alianza kunielezea, nilishindwa kuelewa umalaya wa mume wake na yeye kushindwa kuhudumia watoto wake vizuiri vinakujakujaje?


“Watoto wanahusika nini na matatizo ya mume wako?” Nilimuuliza.


“Wewe hujui tu, lakini mimi nina hasira sana, na yote haya kasababisha mume wangu, ni mtu wa kunipiga kila siku, yuko na mimi kwaajili ya watoto, nahisi kama anawapenda watoto zaidi yangu, yaani mpaka kuna wkaati nawaonea wivu wanangu kwa jinsi anavyowapenda.”


Nilimuangalia yule Mama bila kummaliza, kila dakika mbili akiongea ya tatu atyajizungumzia yeye,a tazungumzia namna anavyonyanyasika, namna anavyoumia.


“Nimeamua kuwa Malaya ila mume wangu hata hajali, mwanzo nilikua nachepuka kwa starehe, lakini sasa hivi nachepuka kwakua nataka mume wangu aumie kama aninavyiumia, lakini haumii, yaani huwezi amini, mume wangu anaweza kuja hapa nyumbani, akaniona na mwanaume lakini hata hajali, anaingia ndani kulala bila kunigeukia, yaani akishatoka na Malaya wake basi ndiyo hivyo, hajali chochote kuhusu mimi!


Malaya wake wananipigia simu, wananitukana mpaka matusi ya nguoni, lakini mume wangu wala hajali. Hembu angalia, unaona hizi picha….” Aliongea huku akitoa simu yake, alifungua sehemu ya picha na kuanza kunionyesha. Kulikua na picha nyingi za wanawake wamekaa uchi uchi, nyingine wakifanya mapenzi na mume wake, zilikua zinatia kichefucgefu.


“Yaani mume wangu anafanya yote haya, anajirikodi na Malaya wake nao wananipigia na kunitukana, wananitumia picha zake, yaani nashindwa hata kusema nifanye nini?” Aliongea kwa uchungu sana, nilimshangaa nikijiuliza, saasa kama anaona yote haya kwanini anavumilia.


“Kwanini sasa unavumilia, wewe si umesema ni msomi, una elimu yako kwanini usitafute kazi na kuondoka?” Nilimuuliza, aliniangalia kama vile ananionea mimi huruma.


“Mdogo wangu maisha hayako hivyo, nina watoto wawili, sina kazi unafikiri nikiondoka hapa nitakuja kuolewa na nani? Unajua nina miaka mingapi? Nani ataoa mwanamke kama mimi?” Aliongea kama vile anafoka.


“Unafikiri sitaki kuondoka, lakini niende wapi na wanangu wawili, kuna kipindi nilitaka kuondoka akasema nimuachie watoto, sasa mimi niache wanangu wakalelewe na Malaya wake hata siwezi.” Aliongea maneno mengi na kuniacha tu nashangaa, watoto anaosema hataki walelewe na Mama wa kambo yeye mwenyewe hawalei.


“Usoje kumuambia Baba yao ataniahca…” Aliniambia, nilinyamaza bila kusema chochote, nilimuona kama vile hana akili kwani kitu kikubwa alichokua anakifanya ni kuogopa kuachwa.  Niliwaza sana, kama mwanaume anamuona anachepuka, kamaa naingiza mpaka wanaume ndani na mwanaume anajua, ni kosa gani jingine anaweza kulifanya mpaka kumkasirisha mwanaume. Niliwaza sana lakini sikupata jibu, niliona kama mazingaombwe flani.


Niliacha kupanga nguo na kutoka chumbani, nilienda nnje kuendelea na kazi zangu. Yeye pia alitoka na kurudi jioni kabisa, alirudi akiwa kalewa tena sana, alilingia ndani na baada ya kama nusu saa hivi Baba naye alirudi. Tangu kuja pale ilikua ni kama mara ya pili kumuona, kumbuka wakati huo hata sijamaliza wiki kwenye ile nyumba, aliingia chumbani na mke wake, baada ya kama dakika tano hivi nilisikia kelele, walikua wanagombana, wanapigana kabisa, walikua wanatukanana tena matusi ya nguoni.


Mtoto alikua sebulani, baada ya kusikia alianza kulia, ilibidi nimtoe na kumpeleka chumbani kwake. Walitukanana huko baada ya kama dakika 45 hivi Baba alitoka, alikuja mpaka chumbani kwa mtoto. Alikuja na kuniona nimelala na mtoto kanikumbatia kwani alikua anaogopa analia.


“Kwanini unalala na mwanangu? Umekuja kufanya kazi au kulala na mwanangu, nyie ndiyo mnaowafanyia watoto mambo mabaya! Si una chumba chako wewe!” Baba alifoka huku akinishika na kunivuta pembeni kwa nguvu, alinivuta kwa nguvu kiasi kwamba nilidondoka chini ya kitanda na kuumia.


“Dadaaaa!” mtoto alipiga kelele huku akinyanyuka na kutaka kunifuata pale chini. Lakini baba yake alimuwahi, akamshika na kumpakata. Alimpakata na kukaa naye chini kisha akaanza kumbemebelza.


“Mwanangu nisamehe, najua umesikia nagombana na Mama yako, Mama yako ni mbaya sana, lakini mimi nakupenda!” Aliongea maneno mengi yote ya kumponda mke wake na kujisifia yeye, alitoa pili na biscuit na kumpa mtoto, nilishangaa kwani ilikua usiku na mtoto alishakula nilikua nambembeleza tu alale.


“Unafanya ni nini hapop?” Aliniuliza kwa hasira baada ya kuniona kama nimekaa chini namuangaia. Nilinyanyuka kutaka kuondoka, lakini mtoto alianza kunililia akitaka nisiondoke. Aliona aibu na kuniabia nikae, alimuacha mtoto akaniambia kuwa nimbembeleze mpaka alale. Kweli nilifanya hivyo, nilitumia kama masaa mawili kumbembeleza mtototo, alipolala nilitoka zangu nnje. Kumbe alikua ananisubiri mlangoni,. Ile natoka tu niliambulia kofi.


“Umemfanya nini mtoto wangu? Mbona anakupenda wewe kuliko anavyonipenda mimi? Wewe utakua ni mchawi mshenzi mkubwa wewe!” Alifoka na kunipiga sana, nilishangaa kwani sikufanya kitu chochote, kibaya zaidi nilikua hata sijuani naye vizuri na kibaya zaidi nikuwa nilikua namuona Baba ni mpole kushinda maelezo, lakini alikua kama mtu aliyechanganyikiwa.


“Kesho utaondoka hapa! Sitaki kukuona!” Alianza kufoka, mimi niliitikia tu sawa, nilikubaiana na kila kitu anachosema ili nisipigwe.


Baada ya kunipiga sana Baba alitoka nnje, hakurudi ndani, aliondoka kabis ahuku akiniambia kuwa akirudi hataki kuniona katika ile nyumba. Baada ya kuondoka Mama alikuja, alikua bado kalewa na usoni alikua na alama alama za kipigo.


“Unaona, nimekuambia huyu si mwanaume, yaani anahisi watoto wanakupenda kulkiko wanavyo mpenda yeye, hana akili kabisa, nakuambia kuwa huyu akijua watoto siwalei vizuri ataniacha na mimi sina pakwenda, lakini mimi simuamini hata kidogo kumuachia watoto.”


Mama aliongea kwa masikitoko, alikua ananikandkanda usoni kwani nilikua nimepigwa sana.


“Sasa mimi nimefanya nini?” nilimuuliza..


“Unafikiri wanaume hawa ni lazima ufanye kitu, akitaka kukupiga anakupiga tu, huna kosa lolote lakini atakufanyia vituko tu, ana hasira zake, mimi nakumbia anawapenda wanae mpaka anaboa, kibaya chochote anaweza kuua. Ndiyo maana nakuambia kuwa usimuambie chochote, huyo binti mimi nitadili naye, alichomfanyia mwanangu ni unyama lakini mimi ninajua cha kumfanya, wewe niachie mimi.” Aliniambia.


Nilimuitikia nikiwa nawaza kuondoka, nyumba ile ilikua na vituko vingi sana, sikuwa hata na hamu ya kuendelea kuishi pale. Niliingia moja kwa moja chumbani kwangu, nikapanga nguo zangu ili kuondoka, nilipomaliza nilipanda kitandani ili kulala. Lakini asubuhi naamka nakuta mtoto kalala pembeni yangu kanikumbatia, nilishangaa sana kwani usiku nilimuacha chumbani kwake.


“Dada usiondoke, mimi sitaki uondoke.” Aliniambia, niliposhtuka alishtuka pia, hicho ndiyo kilikua kitu cha kwanza kuniambia, nilishangaa kwani alikuja na mabegi yake, alikua na kabegi kadogo ambako alikua kaweka vitu kana kwamba alikua ashajipanga kuondoka na mimi.


“Mimi siondoki, bado nipo?” Nilimdanganya.


“Hapana, unaondoka, mbona una mabegi? Nilimsikia Baba akikupiga na kukuambia uondoke, mimi sitaki kukaa hapa, naondoka, sitaki, naondoka!”


Alikua anaongea na kasauti kake ka kitoto, nataka niwakumbushe tu kuwa huyu mtoto ana miaka mitatu na nusu lakini alikua anaongea vizuri na alikua anaongea kama mtu mzima. Kusema kweli niliumia, nilikua nimekaa pale kama siku tano tu, hata wiki sijamaliza lakini alishanipenda, alishakua rafiki yangu na alikua hataki kuishi na wazazi wake.


“Baba kila siku anampiga Mama, mama ananipiga mimi, mimi sikai hapa, kaka aliondoka na mimi naondoka!” aliniambia, nilimuagalia kwa huruma sana kwani nilijua kabisa siwezi kuondoka naye.


Kusema kweli iliniuma kwamba mimi nilikua na uwezo wa kuondoka katika ile nyumba wakati yeye alikua hawezi kwakua tu ni wazazei wake. Baba yake alikua anadai anampenda, na kweli kwa namna nyingine ukimsikiliza alionekana kumpenda, mtoto alikua na kila aina ya zawadi, chumba kizuri, alikua na kila kitu lakini alikua hana furaha, alikua hana amani, alikua ni mpweke, mwanzo wakati nafika alikua mkimya, alikua ni muoga, alikua hawezi hata kuongea vizuri.


Lakini ilinichukua kama siku mbili tu hivi mtoto kunizoea, ilinichukua kama siku mbili mtoto kuanza kuongea kama chiriku na kuniambia kila kitu, siku nne tu alinipenda na siku ya tano alikua tayari kuondoka na mimi mtu ambaye hajui hata jina lake zaidi ya kuniita dada, alitaka kuwaacha wazazi wake. Sikua na namna zaidi ya kumuambia kuwa nitaenda naye, lakini nilikua sijui kama nitaendaje naye, machale yalimcheza, alichukua mdoli wake anaoupenda na hakulala siku ile paka usiku.


Kila sehemu niliyokua naenda alikua ananifuata, alikua anahisi labda akilala nitaondoka na kumuacha. Niliambiwa niondoke lakini sikuweza kuondoka siku hiyo, kwa bahati nzuri Baba yake naye hakuja mchana kutwa. Lakini usiku alikuja, alishangaa bado nipo pale, nilikua nimelala chumbani kwa mtoto, mtoto alikua kanishikilia mguu, alipokuja aliniamsha lakini ile nashituka tu mtoto aliamka na kuanza kulia.


“Baba usimpige dada! Baba usimpige dada! Mimi naondoka na Dada, naondoka na Dada!” Mtoto alilia sana, Baba aiobu ilimshika akaniacha akaondoka kwa hasira. Nilirudi kitandani kulala lakini usingizi haukuja, hata mimi nilitaka kuondoka, kwakua mtoto alikua kachoka sana haikuchukua muda kulala. Baada ya kulala niliiondoa mikono yake kwenye miguu yangu na kumuacha kalala, nilienda chumbani kwangu na kuchukua mabegi yangu mawili ili kuondoka.


Nilitaka kuondoka kimya kimya usiku uleule lakini ilihofia naweza kuambiwa nimeiba, niliamua kwenda kumgongea Mama kwani nilijua Baba atakua kaondoka, nilienda kumuaga Mama, nilifika mpaka mlangoni lakini wakati nagonga nilisikia Mama anamuambia.


Jana nilikuambia ukashindwa kumfukuza, huyu binti ni mchawi, kuna vitu kamfanyia mtoto, mimi nahisi ni msagaji!” Mama aliongea.


“Nyamaza, kwanini wewe ulimfukuza?”


“Nimfukuze ili useme kuwa nina mdomo, si wewe ndiyo ulimleta, sasa kwanini mimi nihangaike, unaona, kamjaza mtoto maneno mpaka hata wewe Baba yake hakutaki, siku ngapi kaja, hata wiki hana mtoto kashakua hivyo!”


“Najua, lazima aondoke na sitaki mfanyakazi tena, wewe unafanya nini? Kazi huna, kila siku kuhangaika na wanaume tu!”


“Eeehh! Sasa hivi ndiyo umeona kuwa nina wanaume, kila siku wanakuja hapa huiongei, umeona mtoto wako kaharibiwa ndiyo unaongea!” Mama alilalamika.


“Ulitaka nifanye nini na umalaya wako! Wewe si umeamua kuwa Malaya!”


“Acha kuniita Malaya, unafikiri mimi sina akili nifanye umalaya ndani ya nyumba yangu? wale ni marafiki zangu, nawaleta kukuonyesha kuwa na mimi na pendwa ili unioneee wivu lakini mwanaume hata kushtuka hushtuki! Najua ulishaacha kunipenda muda mrefu ila wameguswa wanao ndiyo unakasirika.” Mama alilalamika kwa namna walivyokua wanaongea niliona kabisa wanaelekea kupatana.


“Najua, lakini nafanya yote haya kwakua una kiburi, unanidharau sana, niliamua kukuacha tu na maisha yako lakini sasa hivi lazima ujitambue, haya maiisha sio, sitaki tena wafanyakazi ndani ya nyumba yangu, kama ni msagaji basi ataniharibia mtoto, na kweli naona, kwanini mtoto anamng’ang’ania?”


“Ndiyo umfukuze sasa, maana nimemchunguza mtoto sijui, nahisi kashamfanyia vitu vibaya!” Mama aliongea, nilioka kabisa msala unanigeukia, Mama alikua anataka kunigeuzia kibao ili mimi kuonekana kama ndiyo nimemfanyia mtoto ule ushenzi.


Nilitamani kugonga na kumuambia Baba ukweli lakini niliogopa, nikaona hapana, bora kuondoka kimya kimya.


“Kesho anaondoka lakini kabla ya chochote ni lazima mwanangu akapimwe, kama kamfanyia kitu kibaya nitamuua kwanza kabla ya kuondoka!” Baba aliongea kwa hasira.


“Kweli kabisa, wewe unachukua mtu huko hujui katoka wapi unamleta akulele mwanangu, mimi nakuangalia tu, kila siku si unaniona mimi Malaya siwezi kulewa, ndiyo maana nikasema nikuangalie tu, yakikukuta ni wewe mwenyewe!”


“Haondoki hapa, tena kamuangalie kabisa asije kuroroka. Kesho mguu wangu mguu wake, kama ni msagaji nitajua, namalizana naye mwenyewe, mshenzi mkubwa, kaangalie asije kurodtoka.


DADA WA KAZI; DADA USIMPIGIE MAMA AKIJUA ATANIPIGA!—SEHEMU YA NNE


Nilitaka kuondoka na kukimbia, nilihisi labda nitashushiwa msala wote, ningeweza kufungua geti na kundoka, nilitembea taratibu mpaka getini, nikafungua kabisa. Lakini wakati nataka kutoka kuna kittu kiliniambia.


“Unajua wewe ni fala, sas aunawaogopa nini hawa wapumbavu, huyo mtoto ukimuacha na hao watu atakufa, hawafai kabisa kuwa wazazi!” Sijui nilipata wapi ujasiri lakini nilifuinga geti, nilitupa mabegi yangu na kurudi ndani kama vile nakimbia, nilienda mpaka kwenye mlango wa chumba chao na kugonga.


Bado walikua wanaongea, waliuliza ni nani anagonga nikawaambia kuwa ni mimi. Walifungua mlango, Baba alitaka kunifguata na kunipiga.


“Achana na mimi, utampiga huyo huyo mkeo ambaye hana akili, mimi ukinigusa hakikisha unaniua kabisa  kama si hivyo wala sikupeleki polisi na kukeketa mimi mwenyewe!” niliongea kwa hasira, nilikua nauoga wa hali ya juu lakini uso wangu ulikua unaonyesha kujiamimini.


“Mnakaa hapa ndani mnadanganyana ujinga kuona kama mimi ndiyo tatizo, hivi nyie ni wazazi kweli, yaani hata hamjiulizi kwanini mtoto ananipenda mimi na si Mama yake, kweli wewe Baba unaacha kuwa Baba unaanza kuleta mazawadi tu! Chumba cha mtoto kimekua kama duka la midoli, sasa si mnaona kama mimi ndiyo namnyanyasa mtoto wenu, njoo! Njoo uone ushenzi anaofanyiwa mtoto wako!”


Niliongea ka hasira, wasingenifanya chochote, nilishapanga kuondoka na kusema kweli nilikua sijali. Nilimshika Baba mkono kumvuta ili kuingia kwenye chumba cha mtoto, Mama alimshika kumvuta ili asiende kula, lakini sikuruhusu, nilimshika kwa nguvu na kumvuta, tulienda mpaka chumbani kwa mtoto, wakati tunafungua mlango mtoto aliamka.


Huwezi amini, mtoto alikua katikati ya usingizi lakini alinyanyuka harakaharaka na kunifuata.


“Dada usiniache, naondoka na wewe! Mimi sikai tena hapa!” Alipiga kelle kwa nguvu huku akinishika miguu. Alining’ang’ania sana bila kuniachia, Baba yake kila wakati alijifanya kuwa ni Baba bora, alijifanya kama yeye ni tofauti na Mama yake hivyo aliinama na kumchekea akitaka kumbeba lakini mtoto alikataa katakata.


“Unasema nimemloga mtoto, sasa hembu angalia kama nimemloga, huyo mke wako sio kakuambia kuwa mimi ndiyo namfanyia unyama, sasa angalia!” Nilimuambia huku nikimnyanyua mtoto na kumkalisha kitandani, alikua kavaa nguo za kawaida kwani aligoma kabisa kuvaa nguo za kulalia kwa madai kuwa hatalala kwakua akillala nitamuacha usingizini!” nilikua na hasira, nimepaniki na sijui nini chakufanya.


Harakaharaka nilimvua mtoto nguo, nilimlaza chini na kumpanua miguu, nilianza kulazimisha Baba yake kumuangalia.


“Wewe ni mtu mzima, una akili, angalia hii michubuko, angalia kama ni ya lini? Angalia kama kweli huyu mtoto kafanyiwa hivi vitu na mimi, muangalie mwanao, huu I uchi wa mtoto wa miaka mitatu, mtoto wako ananyanyaswa! Unajua kweli mtoto wako anaishia na nani, unajua kweli mtoto wako anafanyiw anini? Lini ulikaa na mwanao ukemuuliza chochote, wewe ni baba kuna mambo yanaendelea huku honi?


Mimi nimekuja siku ngapi? Angalia mtoto alivyooza? Angalia hizi alama, kweli ni zasiku mbvili, hata kama huna akili kiasi hicho hata kama umeolegwa kweli hivi ni vitu vya kuamini! Halafu nikuambie tu, mtoto wako mkubwa sijawhai kumuona, lakini hembu kaongee naye utaona kama nadanganya au la?” niliongea kwa hasira, Baba alibaki kaduwaa, macho yamemtoka kwa mshangao, akarudi na kuwa mdogo kama mtoto, nilimfunika mtoto kwani alikua analia, nilisimama mbele yake kumuangalia kama atafanya nini?


Kwa dakika kama mbili hivi aliua kama kashikwa na bumbuwazi, ghafla alimgeukia mke wake, alianza kumpiga na kumlaumu kuwa hawezi kulea watoto, kaishia umalaya na kushindana na yeye wakati yeye ni mwanaume. Niliingilia kati na kuwaambia kuwa wanawaharibu watoto.


Watoto wenu hawawapendi kwasababu ya mambo yenu, kila siku mnagombana, unafikiri watoto hawaoni?” Niliwauliza, Baba alijifanya kukasirika, alitoka nnnje bila kusema chochote, Mama alimfuata, mimi nilibaki na mtoto, sikutaka kuhangaika nao.


Mtoto alikua analia, anaogopa ananiambia tu nissiondoke.


“Mimi sitaki kubaki nao, wanapigana kila siku, sitaki kabisa kubaki nao!” Aliongea, nilimkumbatia na kumuambia sitamuacha, nilijua nadanganya kwani nilijua kabisa baada ya nilichokifanya siwezi kuendelea kuishi pale.


“Angalau wanajua labda watajirekebisha!” Niliwaza wakati nimemkumbatia mtoto. Lakini kama dakika kumi hivi Mama alirudi, alikua kafura, amenuna, akaanza kunitukana kwanini nimemuambia mume wake, alidai nimemharibia ndoa kwani lawama zitakuja kwake.


“Wewe ni shetani, heri hata mwenzako aliniibia bwana nikajua ni Malaya lakini wewe unajifanya malaika, unataka kuniharibia ndoa!” Alianza kufoka, nilijaribu kujielezea lakini akunisikia, alinifuata na kuanza kunipiga, tulivurugana sana lakini hakujali, aliniambia nikusanye vitu vyangu niondoke. Mtoto alilia lakini hakumjali, alimchukua mtoto na kwenda kumfungia chumbani kwake, mimi alinisimamia mpaka nikamaliza kukusanya vitu vyangu, baada ya hapo alinitoa nnje usiku uleule na kuniambia niondoke.


Ilikua kama saa sita usiku hivi, hakujali, alikua anatukana sana na kunilaumu kwa kuongea vile. Nilikua nnje, peke yangu sijui hata pakwenda, nilikua siogopi chochote lakini nilikua na hofu, nilihofia kumuacha yule mtoto na wale watu, kuna kitu kiliniambia hapana, niliogopa sana kwani nilijua yale matukio yamemuathiri. Nilitamani kuondoka lakini kweli sikuweza, nililala pale nnje mpaka asubuhi, Baba hakurudi na wala Mama hakutoka kuniangalia kama nimeondoka au la.


Asubuhi nilichukua mabegi yangu, pale jirani kuna Kaka mmoja ana duka la mangi, tulikua hatijazoeana lakini kama unavyojua najiamini, nilimfuata na kumuambia naomba kuweka mabegi yangu. Nadhaini ilikua ndiyo mara yangu ya kwanza kufika dukani kwake, nilikua namuona tu kwa mbali nayeye alikua ananiona.


“Unafanya kazi kwenye hiyo nyumba?” aliniuliza, nilimuona mbea  na kutaka kumuambia anyamaze yeye ni mwanaume atasutwa lakini kwakua nilikua na shida nilimuitikia ndiyo.


“Wamekufukuza?” aliuliza.


“Hapana!” nilijibu kwa mkato nikijua labda atajiongeza atanyamaza, lakini hakufanya hivyo.


“Sasa mbona na mabegi? Huyo Mama ndiyo kawaida yake, juzi kamfukza mwenzako kama mbwa, walikua wanagombania mwanaume, mwanaume mwenyewe mshenzi tu bodaboda! Hivi unajua huyo Mama analeta wanaume ndani, mwanaume anatembea naye, anatembea na mfanyakazi na huwezi amini alikua anakabaka na kale katoto kake! Yaani, mimi simuamini mtu na mwanangu, mimi na hisi na kale kakiume nako wameshakafir* yaani kuna watu washenzi, halafu anakuja kijiwenia naringishia kabisa. Heri uondoke, hata wewe watakufanyia mambo mabaya, yaani hawa matajiri sijui wakoje?”


Aliongea huku akicheka kana kwamba ni kitu cha kawaida, nilimkata jicho mpaka pozi likamuishia akanyamaza.


“Kwahiyo na wewe umeona yote hayo lakini hukusema, kwanini hukuenda hata polisi kama mwanaume mtu mzima anajisifia kumbaka mtoto wa miaka mitat?” Nilimuuliza kwa hasira.


“Niende kwani ananihusu, unataka mimi kuonekana mnafiki? Mimi ni mwanaume sio snichi, sasa kama Baba wa mtoto yupo, Mama yupo tena yeye ndiyo anaingiza wanaume ndani, unataka mimi nifanye nini? Niwaonee huruma kwani wanangu?”


“Bure kabisa, huna lolote, mwanaume gani unaona kitu kama hicho na unanyamaza! Hovyo!” nilimjibu kwa hasira.


“Bwanae kwanza ondoa takataka zako, sitaki kesi!” Alifoka akitaka kunirudishia mabegi yangu.


“Ushapokea mbwa wewe, nayaacha hapo mabegi yangu, sasa ole wako kipungue kitu, yaani hata ukifungua zip utu nitajua, na nitakachokufanya hutaamini utajuta kuzaliwa mwanaume mbwa wewe!”


Alishanitibua mizimu yangu, nilimtukana na kuondoka nikimuachia mabegi yangu, sikuweka pesa huko hivyo sikujali. Niliondoka na kwenda kukaa pembeni kidogo, si mbali na pale bali nilitaka kwenda kukaa sehemua ambayo nitaiona nyumba, baada ya kuambiwa mtoto alikua anabwakwa nilikua na hasira zaidi, nilipaniki zaidi na nilitaka kufanya kitu, akili yangu haikua sawa kabisa. Unjua pamoja na kuongea na mtoto lakini hakuniambia kuhusu kubakwa, aliniambia tu kuhusu dada wa kazi kumuingizia vitu sehemu za siri na kumpiga lakini hakuniambia kuhusu kubakwa.


Nilikaa na hasira zangu nikiangalia, nilikua naangalia kuona Mama kama atatoka ili niende kumchukua mtoto, sikua najua nitampeleka wapi lakini sikutaka kae pale, niliwaza kumpeleka polisi, niliwaza kumpeleka kwa mtendaji, nilikua nawaza mambo mengi lakini sikua na majibu. Nilikaa pale kama masaa mawili, baadaye ndiyo Mama alitoka, alifunga mlango kwa nnje, hakutoka na mtoto ikimaanisha kuwa alikua amemfungia mtoto ndani.


Nilisubiri kama nusu saa hivi, nilipoona harudi nilienda mpaka kwenye ukuta, kwa namna ile nymba ilivyojengwa ni kwamba kuna geti sehemu ya mbele tu, lakini huku nyuma kwingine ni ule ukuta wa nyumba ndiyo unakua umezunguka, kwa maana unaweza kugonga dirishani. Nilienda mpaka kwenye dirisha la chumba cha mtoto, nikaanza kuita, alinisikia, alikua ndani akilia, aliposikia sauri yangu alinyamaza.


“Mama kafunga mlango?” Nilimuuliza, alikua katulia kabisa, akapanda kitandani, akafungua dirisha kisha akaja tukawa tunaonana.


“Sijui, katoka tu kaniacha humu.” Nilimuambia akaangalie  malango wa ndani ulikua wazi, nilimuambia atoke mpaka nnje, alitoka, shida ikawa ni kutoka getini. Niliirudi na kumfuata yule kaka, nilimuambia nataka anisaidie kuruka ukuta na kumtoa mtoto.


“Kwanini uruke ukuta wakati geti lao halifungi kwa nnje.” Aliniambia, ingawa kulikua na kufuli lakini kuna namna alilifyatua komeo na kuniruhusu kuinga.


“Umejuaje kufungua?” nilimuuliza.


“INakuhusu nini wewe ingia.” Niliingia na kumchukua mtoto, alitaka kuchukua nguo zake lakini sikumruhusu, tuondoke Mama atarudi, tulitoka lakini ile tu tunatoka getini. Baba yake huyo hapo kasimama mlangoni ananiangalia.


“Unampeleka wapi mwanangu?” Aliniuliza, nilinyanyua uso kumuangalia, alikua kakasirika kafura hacheki wala nini?


DADA WA KAZI; DADA USIMPIGIE MAMA AKIJUA ATANIPIGA!—SEHEMU YA TANO


“Nondoka, naye, nitampeleka hata polisi lakini siwezi kukuchia huyu mtoto!” Nilisimama na kumuangalia usoni, nilikua najiamini sana na nilijisemea moyoni ama zangu ama zake.


“Nitakuvuruga wewe binti! Yaani nitakuvuruga!” Alipiga kelele na kutaka kunishika.


“Hunifanyi chochote mwanaizaya wewe! Mbwa mkubwa, yaani kama unataka nipige kelele hapa ndiyo ujue mimi ni nani? Watu wote hapa mtaani wanakuchukia, nikipiga kelel hapa watakuja kukupiga kama mwizi, kama huamini jaribu kuniguza. Hivi wewe ni Mama gani, mtoto wako anabakwa na mwanaume wako lakini bado unaendelea kutembea naye, yaani una akili kweli?”


Nilifoka, hapo niliona kama kashtuka, aiishiwa nguvu na kukaa chini, kwa kumuangalia ni kama alikua hajui chochote. Alimuita mtoto kutaka kumpakata lakini mtoto alikataa, alikua amenishikilia miguuni hataki kuniachia.


“Hpana, unaongea uongo! Hapana! Unaongea uongo, hawezi kumbaka mtoto wangu!” Aliongea kama chizi flani hivi.


“Majirani wote wanajua wanakuchora tu! Wewe si huongei na watu, nimekuambia hapana! Huwezi kubaki na huyu mtoto!” Niliongea kwa hasira sana, nilijua kuwa naondoka lakini ilikua ni lazima kufanya kitu.


Nilimchukua mtoto na kuondoka naye, nilienda mpaka kwa yule Kaka nikakaa nikiwaza nini chakufanya.


“Twende kwa Bibi…” Mtoto aliniambia.


“Unajua Bibi yako anakaa wapi?” Nilimuuliza.


“Anakaa Morogoro, mimi napajua nilishawahi kuendaga.” Alisema, nilimuitikia nikijua kuwa haiwezekani kwenda naye, nilibaki tu nimekaaa sijui chakufanya, nisingeweza kuondoka naye, nisingeweza kufanya chochote kile.


Mwiso nilirudi kwa Mama yake, nilikuta katulia, alikua halii tena, aliniangalia kwa dharau na kuanza kuniambia mimi ni muongo nataka kumharibia mtoto wake maisha yake.


“Nimempigia simu anasema kuwa hajawahi kufanya kitu kama hicho!” Aliongea, nilimuangalia yule Mama na kuzidi kumdharau.


“Una akili kweli lakini? Hivi unafikiri kuna mtu unaweza kumuambia kuwa kabaka akasema nimebaka?” nilimuuliza, alinyamaza kimya.


“Usije ukamuambia Baba yake! Atakuja kuniua!” Aliongea, lakini kabla hata sijamkjibu ilikuja Bajaji na kusimama kwa nnje, ilipiga honi sana tukalazimika kutoka.


Dereva bajaji alishuka na kufungua mlango wa sehemu ya abiria, akamtoa Baba wa mtoto, alikua kalewa chakari hajitambi.


“Nimemleta mzee…” Aliongea, walisalimiana na Mama kama ni watu wanafahamiana. Nilijua kama wanajuana, walimuingiza ndani kisha yule Dereava akaondoka. Nilimuangalia Mama alivyokua anamuangalia nlihisi kitu, kwanza nilihisi kuwa labda ni yule ambaye alikua kabaka, nilitoka nnje na kujaribu kumuita lakini alikua kashaondoka. Mama alijua hisia zangu, niliporudi tu aliniambia kuwa sio huyo.


“Yeye alishaacha kuendesha bajaji.” Aliongea kwa mkato.


Baba alikua kalewa hajitambui, nilikua nimechanganyikiwa sijui nini chakufanya. Nilitoka nnje ndiyo nikakumbuka nina namba yako Kaka, Iddi, nilikupigia simu kukuuliza nini chakufanya. Baaada ya kukuelezea mkasa mzima ukaniambia kuwa hao watu hawatakiwi kukaa na watoto kwani wana migogoro yao ya ndani na inawaathiri watoto. Uliniambia kabla ya kuwaza kwenda polisi au kushitaji kwanza nitafute ndugu hata mmoja ambaye anaweza kusaidia.


Uliniambia niongee na mtoto kumuuliza kama angetaka wote tuende na kuishi wapi? uliniambia jibu atakalonipa ndiyo  ndugu ambaye watakua salama  ukaniambia hata kama hapajui basi nitafute namba ya simu ya mhusika na kama sitaweza kuongea naye nikupe uongee naye. Uliniambia kama ikishindikana basi niende pilisi au hata kwa mwenyekiti wa mtaa kuongea naye ili mtoto alindwe na huyo mwanaume ambaye alikua anamfanyia unyama akamatwe.


Niliongea na mtotop akaniambia anataka kwenda kwa Bibi yake Morogoro, lakini nisingeweza kumpigia, nikamuuliza kuhusu Babu na ndugu wengine wa Baba yake akamtaja Baba yake mdogo. Nilitafuta namba yake kwenye simu ndogo ya Baba ambayo niliichukua kwenye suruali yake, nikampigia na kumuambia kila kitu lakini kwa kifupi.


Kilichoonekana ni kuwa walikua hawalewani sana na Kaka yao, lakini baada ya kumpigia alikuja kumchukua mtoto. Mama alishangaa kuona anakuja, waligombana, alimtukana lakini yule Kaka hakujali, alimchukua mtoto na kwenda naye polisi moja kwa moja, aichukua PF3 tukaenda hospitalini, mtoto alipimwa na kukutwa kweli kashaingiliwa kimwili.


Alichukua RB, Baba na Mama wote walikamatwa, Mama aliwapeleka mpaka kwa yle kijana, lakini kumbe baada ya kupigiwa simu na Mama kuulizwa ni kama alishtuka, tayari siku ileile yeye na yule binti mwingine wa kazi walichukua vitu vyao na kuondoka, ni kama walijua watatafutwa kwani walichukua vitu vyote.


Baba mdogo alituchukua mpaka kwake, yeye ni msela hajaoa, kesho yake Baba yao alikuja, Baba walitolewa mahabusu wakaamua kumaliza mambo kifamilia lakini yule Kaka aliyefanya huo unyama alikua bado akitafutwa.  Mimi na mtoto tuliondoka na kwenda Morogoro kwa Bibi yake ndiyo tunaishi hapa. Bbi yake ni mtu mzuri kwani ni watu wadini sana, tangu nimeondoka sijawahi kuwasiliana na akina Mama.


Ninachosikia nikuwa Baba kamrudisha Mama kwao na yeye kahamia kwenye pombe. Kusema kweli nimechoka kufanya kazi kwenye nyumba za watu, nina miezi miwili tu nakusanya mtaji wangu nitakuja kwako Kaka kwaajili ya Biashara. Ugomvi wa Baba na Mama unawaathiri watoto sana, wazazi wanakua wabinafsi na kufanya mambo bila kujua kuwa watoto ndiyo wanaumia. Nimekusimulia kaka kwakua naamini kuna watu watajifunza na kuacha kuhusisha watoto katika maugomvi yao


***MWISHO; 

0 comments:

Post a Comment

BLOG