IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!
Simu yangu ilikua inaita, nilishindwa kuipokea kwani nilikua bize katika kuendesha gari, kutokana na mvua kubwa iliyokua ikinyesha paoja na giza nene niliona kuwa naweza kugonga mtu kama nikiingiza mkono mfukoni na kuchukua simu. Ndiyo kwana nilikua nimenunua gari, sikua hata na miezo miwili hivyo nilikua bado sijapata uzoefu, niliendesha taratibu huku nikichanganywa na milio ya honi ya magari yaliyokua nyuma yangu, waliniona kama vile nimesimama.
JOIN US ON TELEGRAM
Sikuwajali akili yangu ilielekea mbele tu, nilijifanya siwasikii kwani hata hivyo mvua ilikua kubwa kuwasikia vizuri. Pamoja na mikiki mikiki yote lakini nilifanikiwa kufika nyumbani, bado nilikua sijaweka Geti hivyo niliingiza gari sehemu ambayo naipaki, nikawaka alam kisha nikaingia ndani, mvua ilikua imepungua kidogo ingawa kitendo cha kushuka kwenye gari mpaka kuingia ndani tayari nilikua nimeloana. Nilijibanza pembeni ya mlango, nilitoa funguo ili kufungua mlango.
Nilijua mke wangu atakua ndani lakini sikutaka kumsumbua, alishanikatza mtindo wa kuwagongea, pamoja na kuwa na binti wa kazi lakini mke wangu alikua hataki kabisa kama nikichelewa kutoka kazini nikamgongea. Alinipa funguo hivyo kila nikichelewa basi nakua najifungulia mwenyewe, naingia ndani na kwenda jikoni kuangalia kama kuna chakula wamenibakizia, nakula na kupanda kitandani kimya kimya bila kumbughudhi.
Yeye hapendi kelele hivyo kama ikitokea nikamuamsha basi ugomvi wake ni hakuna kulala usiku mzima. Ili kuepusha shari basi naamua kujiongeza na kujifanyia mambo yangu mwenyewe. Lakini wakati naingiza ufunguo mlango ilikua haiingii, kuna kitu kilikua kinaizuia funguo, nilishika kitasa na kukishusha chini ili kuangalia ni nini ndipo mlango ulifunguka, funguo za ndani ndiyo zilikua zikizuia funguo zangu kuingia. Mlango ulikua haujafungwa ikimaanisha kuwa mke wangu alikua bado hajalala.
“Kelele nyingine hizi!” Niliwaza wakati naingia ndani, kwangu nikiwa nimechelewa kurudi ilikua ni bora kukuta mke wangu kalala kuliko kumkuta macho. Nilikua nimechoka sana kuweza kuvumilia kisirani chake. Niliingia ndani taratibu, taa ilikua imewashwa, nilimkuta binti wa kazi akiwa kasimama, amembeba mtoto huku akimbembeleza. Mtoto alionekana kama anataka kusinzia lakini nilipoingia alishtuka na kuanza kulia.
“Baba! Umemuamsha tena!” Binti wa kazi aliongea wakati naingia.
“Pole, vipi, hataki kulala?” Nilimuuliza huku nikimsogelea kutaka kumsaidia, lakini nilishtuka na kukumbuka kuwa nilikua nimeloana hivyo niliacha kumchukua na kumuulizia kuhusu mke wangu.
“Dada?” Aliniuliza na mimi.
“Ndiyo yuko wapi?” Binti aliniangalia kwa mshangao kidogo, ni kama alikua anatafuta jibu la kunipa lakini hakua nalo. Niliona kama ananichelewesha hivyo niliingia chumbani nikidhani kama nitamkuta mke wangu akiwa kalala lakini haikua hivyo. Chumba kilikua kitupu, haikua kawaida yake kutoka kwa kipindi kile.
Baada ya kujifungua mke wangu alikua ni mtu wa kutulia nyumbani, ndiyo kwanza mtoto alikua na mwezi mmoja na nusu. Nilitoka na kumuuliza vizuri binti wa kazi.
“Alitoka tangu mchana hajarudi na simu yake haipatikani.” Aliniambia, nilishangaa kwa yeye kutoka tangu mchana, bado tulikua hatujaanza kumlisha mtoto kitu chochote zaidi ya maziwa ya Mama yake, kumuacha mtoto mchanga kwa muda wote ule ilimaanisha kumshindisha njaa, ilikua ni kama saa tano za usiku hivyo nilishangaa kusikia kwamba alitoka tangu mchana.
“Ametoka tangu mchana, hivyo unakata kuniambia kuwa huyu mtoto tangu mchana hajanyonya?” Nilimuuliza binti wa kazi, hakujibu, alitingisha kichwa kukubaliana na mimi.
“Hajanyonya, nimejaribu kumpa uji lakini amekataa,a likua analia tu…” Umeniulia mwanangu wewe! uji kwa umri huu, hivu una akili za wapi wewe? Umetoka wapi wewe hujui kwamba mtoto cmhanga hatakiwi kupewa chochote?” Nilimuuliza kwa hasira huku nikimnyang’anya mtoto, alikua kachoka sana, aliionekana kulia mpaka kukaukiwa, nilichanganyikiwa sikujua hata nifanye nini.
“Hakuna maziwa ndani?” Nilimuuliza,
“hapana, niliweka kwenye uji wa mtoto lakini Akaka….” Sikutaka hata kuendelea kumsikiliza, nilitoka nnje kwa majirani kuona kama kuna mtu mwenye maziwa, ilikua usiku lakini Mama mmoja alinipa, alitaka kudadisi ili kujua kilichokua kimetokea lakini sikumpa nafasi, nilichukua maziwa na kwenda kuyachemsha kisha nikayapooza na kumpa mtoto. Lakini hakunywa, aliendelea kulia kwa sauti ya kukauka huku mwili wake ukianza kubadilika rangi na kuwa kama wa bluu.
Niliogopa na kuhisi nishamuua mtoto, akili ilifanya kazi hatakaharaka nikakumbuka kuwa nilimpa kwa kijiko, nilichukua chupa ya kumnyeshjea maziwa nikampa akawa ananyonya sema kidogo sana, alikua akijirahidi na ilionyesha kama vile anajilazimisha. Hakua na nguvu, alijitahidi sana lakini alishindwa, nilijua kama nampoteza nilichukua simu na kuanza kumpigia mke wangu ili kujua kama yuko wapil nilipiga sana lakini simu yake ilikua haipatikani.
Niliamua kuwapigia rafiki zake ili kuwauliza, kuna marafiki ambao nilijua fika ni lazima watajua alipo. Nilipiga na baadhi walipokea ila walijifanya kuwa hawajui, niliwaambia kuwa sijali kama anachepuka au la ninachoitaka kujua ni alipo kwani mtoto alikua anaumwa. Walinielekeza sehemu ya mwisho walipokua wamemuona, nilimchukua binti wa kazi, nikamuambia ampakate mtoto kisha mimi nikaanza kuzunguka Baa moja hadi nyingine kumtafuta mke wangu. kila nilipofika nikiulizia naambiwa aliondoka na mwanaume flani labda mcheki sehemu flani.
Nilizunguka baa kama tatu hivi na zote jibu lilikua ni lile lile, kila aliyenmiona alihisi kama nimechanganyikiwa lakini mimi sikujali, nilikua naangalia hali ya mwanangu hivyo wivu niliweka pembeni. Nilifika baa moja ambayo ilikua na Gest ndani yake, nilimuulizia na kweli niliambiwa alikua pale lakini alitoka, nilipouliza alipokua ameelekea hakukua na jibu la kueleweka. Nilitoka lakini wakati naondoka kuna gari ilikua imesimama sehemu ya parking, ilikua inatikisika na nilipoiangalia nilikua kama naifahamu.
Mara kadhaa nilishawahi kuiona nyumbani kwangu, kipindi hicho mke wangu akiwa mjamzito ilikua inakujaga kujaga sana. Ilikua ikija na rafiki yake mmoja wakike na mara nyingine mke wangu alikua anakuja akiiendesha yeye. Nilihisi kitu nikiamini labda mke wangu atakua ndania u huyo rafiki yake niliisogelea ile gari, niligonga kwenye kioo cha mbele lakini haikufuunguliwa, ilikua inatikisika tu, sijui kwanini lakini kuna kitu kiliniambia kuwa nifungue mlango na kweli nilifungua.
Katika siti za mbele hakukua na mtu lakini kule nyuma kuna watu walikua wamelala uchi wanafanya mapenzi, sikua, ingawa ilikua ni usiku lakini mwanga wa taa ya ile Gest ulikua ukiwapiga hivyo niliweza kumuona mke wangu akiwa na mwanaume mwingine. Walikua wamekumbatiana wakinyonyana ndimi huku huyo mwanaume akiwa bize kumvua mke wangu, naye pia nilimfahamu kwani nilishamuona mara nyingi akiwa na huyo rafiki wa mke wangu aliyekua anakuja na lile gari na nilijua kuwa ni mchumba wake.
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SEHEMU YA PILI
(ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA; Rama anatoka kazini, mkewe ambaye ana mtoto mchanga haonekani, mtoto hajanyonya na kaanza kubadilika rangi. Rama anaamua kumtrafuta mke wake, anazunguka kwenye mabaa bila mafanikio, anafanikiwa kumkuta mkewe akiwa ndani ya gari na mwanaume mwingine wamekumbatiana, je Rama atafanya nini? ENDELEA… Kama hukusoma sehemua ya Kwanza Bonyeza hapa @iddi makeng )
Hawakuniona hata nilipofungua mlango, walikua bize na mambo yao, hasira zilinipanda, nilikua nimeshika simu yangu mkononi, niliirudhsa ili kumpiga yule mwanaume lakini kwa bahati mbaya ilimpiga mke wangu kichwani, alipiga ukulele.
“Mama nakufaaaa!” Wote walishtuka walipoangalia nilikua ni mimi. Mke wangu alionekana kulewa sana, lakini yule mwanaume yeye alionekana kama hajalewa, ile kuniona alipaniki, walikua bado hawajavua nguo, mimi nilikua nimefungua mlango wa mbele.
Aliponiona alifungua mlango wa nyuma na kumvuta mke wangu kama mzigo mpaka nnje, mke wangu alipiga kelele za malalamiko kuwa anamuumiza lakini yule mwanaume hakujali, nilipoona vile nilitoka kule mbele na kumfuata kwa nyuma.
“Broo mambo gani haya tunafahamiana, inamaana hujui kama huyu ni mke wa mtu na ana mtoto mchanga?” Nilimuuliza huku nikimkunja kutaka kupigana naye, kwa kumuangalia nilikua nammudu, naye alinishika lakini kabla ya kuanza kupigana Binti wangu wa kazi alikuja, yeye ndiyo alikua kamshikilia mtoto.
Mtoto alianza kulia tena, nilikumbuka kilichokua kimenipeleka pale, nilimuachia yule Kijana na kumfuata mwanangu, pale pale alipata upenyo, akaingia kwenye gari na kuondoka zake. Nilibaki mimi, mke wangu binti wa kazi na mwanangu. Nilitamani kumpiga makofi mke wangu lakini sikua na ujasiri huo, alikua kakaa chini huku kashika kichwani anaugulia maumivu ya ile simu ambayo niliirusha kwa nguvu.
“Umeniumiza, mimi nilishasema kuwa sipigwi, kama umenichoka bora uniache, kwetu sijaua kwanini unipige. Kwanza mambo gani ya kufuatana fuatana mpaka huku sehemu za sitarehe!”
Mke wangu alilalamika, niliinama na kumshika ili kutaka kumuingiza kwenye gari lakini hakutaka. Alikataa katakata huku akilia kuwa nimempiga.
“Mimi siendi ppopote, kwanini umekuja na kunipiga, kwani siruhusiwi kutoka, tatizo lako una wivu sana, wewe umenikuta na mwanaume badala ya kuuliza kwanza kuwa ni nani na tulikua tunafanya nini unaanza mambo yako, unaanza kunipiga!” Aliongea kwa hasira huku akijilegeza na kujilaza chini kwa kugalagala, hasira zilinipanda lakini sikuweza kumpiga, nililazimika kumbembeleza ili angalau anyanyuke pale, mvua ilikua imekata lakini chini kulikua na matope, mke wangu hakujali alijilaza na kujigalagaza.
Alianza kupiga kelele, nikiona kuwa atanijazia watu nilijikaza kiume nikamshika vizuri na kuanza kumkokota mjpaka kwenye gari, nilimlazimisha kuingia na kumkalisha siti ya nyuma, niliingia kwenye gari na kumkabishi mtoto, sikujali matope, nilimvua nguop ya juu na kumlazimisha kumnyonyesha mtoto. Nilifanya hivyo mbele ya dada wa kazi, sikujali chochote, mke wangu alikua kalewa sana ni kama alikua hatambui kama ana mtoto, huwezi amini nilipomvua sidiria ilikua imeloa maziwa, sijui ni kwa namna gani alikua akinywa katika hali ile kwani maziwa yalikua yanatoka yenyewe.
Nilimsaiduia kubeba mtoto kwa kumuwekea kifuani na huwezi amini mtoto alipogusishwa tu titi la Mama yake alianza kunyonya mwenyewe, alinyonya bila kupumzika na aliposhiba alilala palepale. Nilimshukuru Mungu nikawasha gari na kumchukua mke wangu mpaka nyumbani. Kwa namna alivyokua amechafuka nisingeweza kumuingiza ndani, nilimuweka kibarazani, nikaenda kuchukua khanga, nikamvua nguo na kumfuta kidogo kisha nikaingia naye mpaka bafuni, nilimsafisha vizuri na wakati huo ndiyo kama alikua amepata fahamu kidogo.
Alishangaa kujikuta yuko nyumbani, alianza kulalamika kuwa kichwa kinamuuma, ni kama mtu ambaye fahamu zilikua zikimjia na kuondoka kwani aliniuliza kuwa alifikaje pale lakini wakati mwingine alinilaumu kwa kumpiga simu. Sikutaka kugombana naye usiku huo, baada ya kumsafisha nilimrudisha kitandani ili apumzike. Alipanda kitandani na dakika mbili tu tayari alishalala. Nilibaki namuangalia kwa hasira, nilitamani hata kumuua, kichwa kilikua kinaniuma, mishipa ya kichwa imenisimama huku kila dakika nikimuomba Mungu anijaalie nisije kumuua mke wangu kwani nilikua naumia sana.
Nilipitiwa na usingizi lakini nilikuja kushtuka kwenye saa tisa na nusu hihvi, mke wangu alikua kaamka na alikua akitapika, alitapikia kitanda kizima huku akijifuta kwa mashuka. Nilitaka kumnyanyua mpaka bafuni lakini hakutaka, alitapika sana vitu vinanuka pombe sijui alikua kanywa nini kwani haikua kawaida yake, ni mnywaji mzuri na hata siku moja nilikua sijawahi kumuona akitapika vile. Alitapika sana na abada ya kumaliza alijifuta na shuka kisha akatoka na kwenda kulala chumba kinginge akiniacha mimi pale ndani na matapishi yake, sikuweza kulala nilitoka na kulala sebuleni.
Asubuhi niliamka mapema sana, ilikua ni siku ya kazi, nilitoa mashuka na kufanya usafi ndani, yeye bado alikua kalala, niliyaloweka mashuka nikamuangalia mtoto alikua anaendelea vizuri. Kabla ya kuondoka nilimuamsha, alikua kachoka sana hangover bado inamsumbua.
“Mambo gani ya kusumbuana asubuhi?” Aliniuliza huku akijigeuzia upande mwingine.
“Hivi wewe hukumbuki ulichokifanya?” Nilimuuliza, bila kunyanyuka alinisonya na kujifunika shuka. Sikutaka kuharibu siku yangu, nilitoka nikaingia kwenye gari na kuondoka kwenda kazini, mchana kutwa nilikua napiga simu kwa dada wa kazi ili kujua kama yuko nyumbani na alikua amemnyonyesha mtoto.
Aliamka kama hakuna kitu kilichokua kimetokea na kuanza kumtukana binti wa kazi kwa kuacha mashuka yenye matapishi, binti wa watu alilazimika kufua huku yeye akitoka kunywa supu. Mchana nilirudi kumuangalia mtoto, alikua vizuri kachangamka, sikutaka kuliongelea lile swala na yeye alikaa kimya tu bila kuongea, alinichangamkia kama vile hakuna kitu kilichokua kimetokea, alikua kachangamka na nikiwa hapo rafiki yake mwingine alikuja. Wakati naondoka nilimuita ndani na kumuambia siku hiyo sitaki atoke kabisa na kama akitoka basi atanitambua.
“Utanifanya nini? Nikutambue wewe kama nani?” Alinijibu kwa dharau, nilijikuta napandwa na hasira na kumtandika makofi mawili. Yalikua ni makofi madogo lakini alianza kupiga mayowe huku akijigaragaza chini, rafiki yake bila kujali kuwa ni kwangu aliingia mpaka chumbani eti anataka kunishika kwakua nampiga rafiki yake, alinikuta nimesiomama pembeni kabisa namuangalia anavyogalagaza, alitaka kuongea lakini kwa namna nilivyomuangalia alinyamaza kimya. Sikutaka kuendelea kubaki pale nilitoka na kurudi zangu kazini kuendelea na mambo yangu.
Kama nusu saa hivi baada ya kufika kazini nilipigiwa simu, ilikua ni namba ngeni, nilipokea nikidhani ni mtu anahitaji huduma lakini nilishangaa na kutana na matusi, kelele na vitu vingine vingi vya kukera.
“Kama mwanangu huwezi kumlea, kama unaona tabia zake zimekushinda basi nirudishie. Ulimchukua kwangu mzima, hana kovu sasa unataka kuniulia mwanangu kisa nini? Si ulimkuta anakunywa pombe ndiyo nini unataka aache, mtu kanywa bia mbili unataka kumuua!” Ingawa namba haikua yake lakini ilikua ni sauti ya Mama mkwe wangu, sikutaka kumjibu kwani niliona kama nitamkosea heshima.
Nilikata simu na kuizima kabisa, niliendelea na kazi zangu mpaka jioni, nilirudi nyumbani na sikumkuta tena mke wangu. Mtoto alikua na binti wa kazi, nilimuuliza mke wangu kaenda wapi akaniambia tangu mchana nilipompiga alichukua mabegi yake na kuondoka na rafiki yake akisema kuwa hawezi kuendelea kuishi kwenye nyumba ambayo anapigwa na mwanaume. Nilichanganyikiwa kujua kuwa mtoto alikua hajanyonya tangu mchana, nilijua kabisa kuwa kwa kiburi chake mke wangu hawezi kurudi hivyo anaweza kuniulia mtoto.
Nilimpigia simu lakini hakupokea, nilihangaika sana hakupokea na hata rafiki zake nao hawakupokea. Nilipoona hazipokelewi nilimchukua binti wa kazi na mtoto mpaka kwenye gari, nilienda mpaka kwa yule rafiki yake, nilimkuta mke wangu, kaakaa katulia tena wanapika bila wasiwasi wowote, nilimsalimu na kumuomba kuongea naye.
“Hapana, kama unataka kuongea na shoga yangu utaongea mbele yangu, una mnyanyasa sana!” Rafiki yake aliongea, mimi sikutaka kupaniki, kwa maslahi ya mtoto niliamua kuwa mpole ili kumbembeleza arudi na kukubali kulea mtoto.
“Hapana shemeji haya ni mambo yetu, naomba niongee naye!” Nilijishusha pamoja na hasira nilizokua nazo.
“Kama unaongea basi ongea mbele ya Mage (Sio jina lake halisi) sitaki mambo ya siri, unataka nitoke nawewe ili uanze kunipiga!” Mke wangu alijibu kwa hasira, alijifanya kununa kavimba kama vile nimemfanyia kitu kibaya sana. Kabla sijaongea chochote mtoto alianza kulia, ilikua ni njaa, nilimuomba mke wangu kumnyonyesha lakini aligoma, aliniambia kabisa kuwa naringa na namnyanyasa hivyo nibaki na mwanangu.
Nilibembeleza sana mpaka akakubali kumnyonyesha lakinia alikataa katakata kurudi kwangu.
“Naomba basi kama unaishi hapa mimi nitalilipia kila kitu lakini ubaki na mtoto…” Nilimbembeleza baada ya kuona kuwa hakuna dalili za yeye kurudi kwangu.
“Kwani wakati anakuja kwako alikuja na mtoto, hapana, hapa kwangu hawezi kuishi na mtoto, Shogaa kama unaona una shida ya kulea rudi kwa mume wako mimi siwezi kukulea na bado nikamlea na mwanao!” Rafiki yake aliongea, nilimuangalia mke wangu kwa hasira bila kummaliza, nilitaka kumruukia na kumtandika makofi hata kummaliza lakini nilishindwa, nililazimika kuzuia hasira zangu.
Nilianza kazi ya kubembeleza mpaka mke wangu akakubali kubaki na mtoto kwa masaharti kuwa niwe nampa laki mbili kwa wiki na pia nimuachie gari yangu, kwa wakati huo sikua na namna zaidi ya kukubaliana na matakwa yake, ingawa nilikua na wasiwasi sana lakini sikua na namna, nilikua sina njia nyingine ya kumlea mwanangu. Nilimuacha mke wangu pale pamoja na binti wa kazi ili kumsaidia kulea kwani nilijua kabisa mke wangu hawezi kukaa na mtoto masaa yote.
Kila siku nilikua napiga simu kuulizia hali ya mwanangu, nilikua nikimpigia binti wa kazi kwani mara nyingi mke wangu alikua hapokei simu zangu. Lakini baada ya wiki mbili mke wangu alirudi, alikuja na kuniomba msamaha kuwa anajutia makosa yake hivyo anataka turudiane kama zamani na tulee mtoto wetu. Nilifurahi sana kumuona mke wangu na hasa yeye kuomba msamaha, aliniomba msamaha kwa vitu vingi na matendo mengi ambayo alishanifanyia nyuma.
“Baada ya kukaa mbali na wewe ndipo nimegundua kuwa nakupenda na siwezi kuishi bila wewe.”
Aliniambia huku akilia, nilifarijika sana, sikuweza kuuliza hata sababu ya yeye kurudi, nilikua na amani kiodgo kuwa mwanangu atakua mikononi mwangu na nitaweza kumlea mimi mwenyewe. Tulirudiana na maisha yaliendelea, mke wangu alianza kuwa na nidhamu, hakua akitoka toka tena, alikua kama kaacha pombe, kwa wiki mbili alitulia kabisa. Lakini siku moja rafiki nikiwa mjini nilikutana na yule rafiki yake, yule yule ambaye alimpokea. Aliponiona ingawa nilitaka kumkwepa lakini alinifuata na bila salamu aliniambia.
“Muambie huyo Malaya wako kama alifikiri nitamuacha mchumba wangu basi amebugi, nimerudiwa na pete nimevalishwa!”
Sikutaka kujua kilichoendelea lakini kama unavyojua mtu mwenye hasira, aliniambia kuwa alimfukuza mke wangu kwake baada ya kumfumania kitandani na mchumba wake.
“Wewe na wewe ni fala tu, mwanamke gani anafanya mapenzi na mwanaume mwingine tena kitandani mtoto wake akiwepo?” Aliongea na kuniambia mambo mengi sana ya mke wangu, niliumia sana lakini sikusema chochote, ilikua ni sehemu ya wazi hivyo nilihoifia kama nikihjibishana naye basi ataropoka na hata kunidhalilisha. Nilimuacha akaongea mpaka akamaliza akaondoka zake.
Nilirudi nyumbani nikiwa na hasira sana, niliumia kuwa mke wangu hakurudi kwakua kajutia makosa yake bali alirudi kwakua kafumaniwa na hakua na sehemu nyingine ya kwenda. Niliumia sana, nilijaribu kuficha hisia zangu lakini nilishindwa, niliamua kumuuliza mke wangu sababu ya kuja kwangu. bado alisisitiza kuwa alirudi kwaajili ya mapenzi, niliamua kumuambia ukweli kuwa nimekutana na rafiki yake na kaniambia kila kitu. Aliruka futi mia kisha akanigeuzia kibao kuwa mimi ndiyo natembea na rafiki yake na nina mpango wa kumfukuza ili niishi naye.
“Nilijua muda mrefu kuwa una mtaka nikanyamazia lakini sasa hivi naona mmeamua kukaa ili kunisingizia vitu!” Alijiongelesha sana lakini mimi bado niliendelea na msimamo wangu. Tuligombana sana akanuna hukua kiniambia kuwa kama nimemchoka basi nimuache salama lakini si kumsingizia mambo ya uongo, alianza kulia kama mtoto, sijui kwanini lakini nilianza kumuonea huruma na ingawa mimi nilishawahi kumfumania na yule mwanaume lakini nilianza kama kumuamini na kuhisi labda rafiki yake anamuonea wivu kweli, nilimuomba msamaha mimi lakini hakukubali, alinuna kabisa.
Siku iliyofuata ilikua ni Ijumaa, baada ya Swala niliitwa na Shehe, aliniambia kuwa anataka nibaki. Mke wangu siku hiyo hakuja Msikitini, nikijua ni mambo ya Msikitini kwani mimi ni mmoja wa viongozi Msikiti nilikubali, aliniita mpaka ofisini kwake. Lakini ile naingia nilishangaa namuona mke wangu kakaa na mtoto, alionekana kuvimba macho kama mtu aliyekua analia. Nilishtuka na kuuliza mke wangu alikua anafanya nini pale wakati hata hakuja Msikitini.
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SEHEMU YA TATU
“Mume wangu anatembea na rafiki yangu!” Mke wangu aliongea kwa sauti ya kupiga kelele mara tu baada ya mimi kuingia.
“Hapana Shemeji, hembu tulia, umeshanielezea kila kitu, hembu tulia kwanza tusikilize upande mwingine!” Mke wangu hakutaka kutulia, aliongea maneno mengi ya kunipondea, aliongea jinsi nilivyompiga, hakusema kuhusu kunywa pombe na kumucha mtoto. Kila kitu kilikua ni kunishutumu mimi. Ingawa alishamuambia Shehe kila kitu lakini nilipoingia alirudia tena, kwa hasira huku akilia.
Nilinyamaza tu nikimuangalia kwa mshangao, kwa namna alivyokua anaigiza sikua na neno la kuongea. Hasira zilinipanda na kutaka kuongea kila kitu, lakini kuna kitu kiliniambia.
“Hata ukiongea ni kujidhalilisha tu, mwanaume huwezi kuwa hivyo, hembu kuwa na kifua bwana!” Nilinyamaza kidogo kila nilopokua nikiulizwa nilishindwa cha kujibu.
“Kwahiyo unataka njni? Unataka talaka, kama ni talaka sema hapa mimi niandike, nina kalamu na karatasi!” Hasira zilinipanda, ingawa sikua nimepanga kumuacha mke wangu lakini nilijikuta tu nimachoka,a liyonifanyia ni mengi nilishindwa kuvumilia.
“Hamkuja kuchana hapa, hapa mmekuja kusuluhisha….” Shehe aliongea akininyang’anya kalamu na karatasi kwani nilishatoa na kuanza kuandika. Mke wangu kuona vile nilimuona kabisa ananywea, alianza kutetemeka kwani nilikua nimekasirika kiasi kwamba hata kuongea nilikua naongea kwa kigugumizi. Niliona kama wananizingua, nilitoka nnje kwenda nyumbani kwangu, lakini sikufika, kichwa kilikua cha moto, nilikua nimepaniki sana, nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa, sikua na gari siku hiyo, nilijikuta natembea mpaka kwenye Baa moja.
Katika maisha yangu nilikua sijawahi kunywa pombe lakini siku ile nilitamani sana kunywa pombe. Niliagiza bia mbili Safari, nilitaka kuzinwa lakini kila niliposhika chupa kujaribu kuiweka mdomoni niliona picha ya binti yangu, mtoto wangu ambaye bado alikua mchanga.
“Siwezi kuwa kama Mama yake, siwezi kunywa, nikianza kunywa yule mtoto atakufa. Picha ya siku Mke wangu alipomtelekeza na kwenda kwa mwanaume mwingine ilinijia, nilishindwa kunywa, masaa mawili nilikua naziangalia zile bia, nilishindwa kunywa nikatoa noto ya elfu kumi nikampa mhudumu nikaondoka bila hata kudai chenchi.
Nilienda nyumbani na kukuta mke wangu bado hajarudi, sikushangaa nilichukua simu na kuanza kumpigia lakini hakupokea. Nilianza kupaniki kwani nilijua kabisa atakua kaenda kwenye mambo yake, nilihangaika kutafuta marafiki zake lakini hakuna aliyejua alikua wapi? Nilimpigia rafiki yake mmoja ambaye hawakua karibu sana na kumuuliza, kusema kweli sikutegemea jibu lolote lakini nilikua nimepaniki hivyo nilitaka tu kuuliza kila mtu kwani nilikua nishaanza kuchanganyikiwa.
Sijui nini kilitokea lakini alikuta ananishauri kutafuta maziwa ya kopo, alinielekeza vizuri na mimi sikuwaza sana nilienda kununua na kumpa moto kwelia liyapenda. Mke wangu alirudi saa nne usiku na alikua kalewa, kwakua mtoto wangu alikua kashiba amelala sikuhangaika naye kabisa. Hakua amelewa sana, alikua bado anajitambua hivyo alivyoona kuwa simfuatilii alianza kujirudi na kuomba msamaha. Mimi sikusema chochote nilipanda kitandani kulala, nililala mpaka asubuhi, lakini nilipoamka sikumuona mke wangu.
Nilijua kama kawaida kaenda kwenye mambo yake lakini kuangalia pembeni mtoto naye hakuepo, nilitoka nnje nikijua labda wapo lakini Dada wa kazi aliniambia kuwa Mke wangu alimuamsha usiku ili kumuandalia nguo za mtoto. Hakujua wamewenda wapi, nilianza kupiga simu kwa kupaniki. Simu ya mke wangu iliita bila kupokelewa kwa dakika kama tatu, baadaye meseji iliingia.
“Unataka kuniua, mwanaume gani hunisamehi, nimeondoka nimerudi kwetu, nimemchukua mwanangu akikua utakuja kumchukua.”
Meseji iliishia hapo, haikua siku ya kazi hivyo sikua na sehemu ya kwenda, nilimpigia simu Mama yake akaniambia kuwa mwanae alimpigia simu kuwa na mnyanyasa hivyo akamuambia arudi kwani kwao hajaua. Mama mkwe aliongea maneno mengi ya kashfa na kejeli na kuniambia kuwa hajashindwa kumlea mtoto wake hivyo nisimnyanyasie. Nilijaribu kumuelewesha kilichotokea lakini hakuelewa, alikua mkali na alinishutumu sana kwa kumnyanyasa mwanae kisha akakata simu.
Sikua tayari kumuacha mwanangu akateseke na mke wangu, kwa tabia zake nilijua kabisa hawezi kukaa na mwanangu kwa amani. Niliwasha gari na kumchukua Dada kwenda kwa Mama mkwe wangu. Nilipanga kumchukua mwananguhata kwa nguvu, niliendesha gari kama mwehu, nilikua na hasira sana, nilishaandika talaka tatu za kumpa mke wangu nikijiambia kuwa nikifika nampa talaka zake kisha namchukua mwanangu kwa nguvu. Nilishachoka mambo yake, mke wangu alishanifanyia ushenzi mwingi lakini kumchukua mwanangu bila idhini yake kwangu kilikua ni kitu kikubwa sana.
Mke wangu kwao ni Tanga, pamoja na kuwa yeye ndiyo aliwahi kuondoka lakini mimi ndiyo niliwahi kufika. Alichelewa kupata gari kwani hakua na tiketi na gari aliyopanda ilichelewa kujaza. Nilifika na Mama mkwe alinipokea vizuri.
“Shikamoo Baba…” Mtoto wa miaka sita alinisalimia, nilikua namfahamu kwani kama mara mbili hivi nilipoenda ukweni nilimuona. Mke wangu alinitambulisha kuwa ni mtoto wa dada yake na alikua akiishi na Mama yake, sikujali sana jina la Baba kwani kwakua nimemuoa Mama yake mdogo niliona kama ni mwanangu.
Wakati huo Mama mkwe alishatoka nnje baada ya kunikaribisha, tofauti na kwenye simu ambapo aliongea kwa kisirani tulioonana alikua mchangamfu, alinikaribisha vizuri kama vile hakuna kitu kilichotokea. Nikiwa pale simu yangu iliita, alikua ni yule rafiki yake na mke wangu amabye jana yake alinielekeza kuhusu maziwa ya kopo. Aliniulizia kuhusu mwanangu na kuuliza kama mke wangu alirudi. Sikuweza kuongea sana, nilimuambia.
“Niko Tanga ukweni siwezi kuongea nikitoka nitakutafuta.”
“Tanga!?”Aliniuliza kwa mshangao.
“Ndiyo kwa Mama mkwe wangu…”
“Mhhhh!” Aliguna, ni kama alikua anataka kuniambia kitu lakini alisita, nilimuuliza alikua anataka kusema nini akanyamaza na kukata simu. Wakati huo huo Mama mkwe alikua anaingia, alituuliza tunakunywa soda gani tukamtajia kisha akatuletea.
“Baba amekuja kunichukua?” Yule mtoto aliongea, Bibi yake alimkata jicho mtoto akanyamaza kimya klwa uoga, ni kama alikua anaambiwa asiropoke kitu. Kwa namna alivyonyong’onyea nilijisikia vibaya nikalazimika kumuambia kuwa nimeenda kusalimia ila wakati mwingine wakiwa likizo shuleni basi nitaenda kumchukua. Alijibu tu kukubali lakini hakua na raha.
Masaa mawili baadaye mke wangu alikuja, tofauti na nilivyodhani kuwantutagombana mpaka kufikia kumpa talaka mke wangu alinichangamkia.
“Nilijua tu utanifuata, unanipenda sana, huwezi kuniacha, mimi nakuambia yule mbuzi ndiyo anataka tu kutuharibia lakini hawezi!” Aliongea huku akinikumbatia.
“Mambo si ndiyo haya sasa mwanangu, hakuna kugombana, mkisikiliza maneno ya wtau basi ndoa yenu haiwezi kudumu, waja ni wanafiki wanangu mambo yenu malizeni wenyewe!”
Mama mkwe aliongea, kwa namna walivyokua wamebadilika ilinishangaza sana, haikua tena mimi kumfuata mke wangu baada ya kukimbia na mtoto bali ilikua ni kama mke wangu alienda kwao kujifungua na mimi nilienda kumchukua.
“Mama inabidi tuongee, kuna mambo hayaendi sawa…” Nilimuambia Mama mkwe baada ya kukaa, sikuwalewa kabisa.
“Mwanangu haina haja ya kufufua makaburi, nimeongea na mke wako kwenye simu kanielezea kila kitu, najua wewe ni mwanaume huwezi kuomba msamaha lakini nimemuambia mwanangua kusamehe, dunia hii ni mapito tayari mna mtoto kwanini kugombana.”
Mama mkwe alinikatisha, kila nilipotaka kuongea waliibua kitu kingine na kunifanya kushindwa kuelewana nao. Walikua wananichanganya na maneno yao.
“Hatuwezi kuondoka leo, tutaondoka kesho, Mama tutakua wageni wako sema utakaa na mtoto nataka kumuonyesha mume wangu viwanja.” Mke wangu aliniambia huku akinisogelea na kunishikashika, hakujali kama Mama yake alikua pale, alinishika sehemu mbalimbali mpaka nikaona aibu, nilikua najisogeza sogeza huku nikifurahia namna alivyokua akinishika, vidoele vyake vilinichanganya sana, nilijikuta nasisimkwa na kukosa chakuongea.
Usiku mke wangu aliniambia tutoke, alimnyonyesha mtoto tukatoka kwenda kulala nyumba ya wageni. Aliniambia kuwa kuna zawadi anataka kunipa na hawezi kunipea nyumbani kwao. Mimi niliona ninafasi nzuri ya kuongea naye kuhusiana na tabia zake kwani nilijua fika siwezi kuongea na kuelewana naye mbele ya Mama yake. Kweli tulitoka lakini hatukuongea, ile tunaingia ndani tu mke wangu alinivamia na kunipa mapenzi ambayo nilikua sijawahi kuyapata, vitu ambavyoa linipa mke wangu nilishindwa kusimulia.
Alinichanganya sana kwani niliacha kufanya naye mapenzi tangu akiwa na ujauzito wa miezi mitatu, aliniambia kuwa mimba yake hainitaki na tangu kipindi hicho nilikua sijawahi kufanya mapenzi na mwanamke zaidi ya kumalizia mambo yangu bafuni. Nilisahau kila kitu na asubuhi mimi na mke wangu tulianza safari ya kurudi tena Dar tukiwa vizuri kabisa. Maisha yaliendelea, mke wangu bado aliendelea kunywa pombe lakini hakua akichelewa kama zamani. Siku moja nikiwa chumbani nimelala mke wangu alikua sebulani, alikua akiongea na simu, kuna mtu walikua kama wanagombana naye ni kama alikua anadaiwa kitu.
Nilitoka na kumuuliza lakini hakua na jibu, alirudi chumbani kulala bila kuniambia chochote. Sikutaka kujibishana naye sana, nilirudi kulala, lakinia subuhi niliamshwa na kelele, kuna watu walikua nnje walikua wakigombana na mke wangu. Nilitoka na kukuta polisi wawili na kujana mmoja, walikua wanamuambia mke wangu kuwapa funguo za gari langu, nilienda kuulizia tatizo lilikua nini ndipo waliniambia kuwa mke wangu alikua kawauzia gari lakini kila sikua anawadanganya kuwa atawapa atawapa ila hatoi.
Nilimgeukia mke wangu kumuuliza ndipo aliniambia kuwa nikweli lakini hawezi kuwapa ufunguo kama hawammalizii pesa yake.
“Umeuza gari gani wewe? Kwani una gari?” Nilimuuliza mke wangu kwani alikua hana gari, gari pekee mule ndani lilikua ni lakwangu na lilikua na jina langu. Alinyamaza bila kujibu ndipo yule kijana alinionyesha kadi ya gari yangu na mkataba wa mauziano kuwa mke wangu alikua kapewa milioni tano ilikua badi milioni mbili, ikimaanisha kuwa mke wangu aliuza gari kwa milioni saba. Sahihi ilikua ya kwangu mke wangu alifoji sahihi yangu.
Nilimgeukia tena mke wangu na kumuuliza kama ni kweli kauza gari yangu Rav 4 New model ambayo nilinunua kwa milioni 30 ilikua hata haina maika miwili aliiuza kwa milioni saba.
“Una akili kweli wewe mwanamke, gari ya milioni 30 unauza milioni 7?” nilimuuliza kwa hasira.
“Sasa mimi kama nilikua na shida ningefanya nini, wanilipe kwanza milioni mbili zangu ndiyo niwape funguo…” Aliongea kwa nyodo.
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SEHEMU YA NNE
Nilimtambua yule kijana kama John, mke wangu alikua amekuka pesa zake nyingi tu, mbali na yale makubaliano lakini mara kadhaa mke wangu alikua akienda kumkopa pesa bila kujua kuwa yuke kijana alikua akiandika na alitaka gari lake. Nilitaka kuingilia kati na kumlipa lakini alikataa na kwakua Kadi ya gari ilikua na jina langu lakini mke wangu alifoji sahihi ili kuonekana kama mimi ndiyo nilikua nimeuza ile gari. Niliangalia ule mkataba kweli ulikua na sahihi yangu, sikutaka kukubali niliikataa kabisa ile sahihi.
Kutokana na mimi kukataa basi walimkamata mke wangu na kumuweka ndani kwa kesi ya utapeli na kufoji nyaraka. Hapo ndipo nilichanganyikiwa zaidi, mke wangu alikaa kituoni kwa siku moja, nilienda kuongea na John kuona ni namna gani naweza kumlipa pesa yake aliyokua kachukua mke wangu lakini hakutaka. Aliniambia kuwa alichokua anataka ni gari, na kama siwezi kumpa basi atahakikisha kuwa anamfunga mke wangu kwakua kamtapeli pesa zake na kwakua alifoji sahihi yangu, kwamba kama mimi nikikataa kuwa ile sahihi si mimi niliyesaidi basi mke wangu anaweza kufungwa kwa kufoji.
Baada ya kuhangaika siku nzima na usiku mzima kuona namna gani naweza kulipa ile hela, asubuhi nilienda kumuona mke wangu, alikua mahabusu, nilimpelekea chai lakinia ligoma kabisa kuonana na mimi achilia mbali kula chakula nilichokua nimempelelea. Aligoma kula kwa madai kuwa nimemtelekeza kwa kitu kidogo tu, nilitaka kumuwekea dhamana lakini ilikataliwa, John alikua shatoa pesa ya kutosha hivyo nilikua napigwa chenga chenga kutwa nzima.
Mpaka wakati huo nilikua sijamuambia mtu yeyote kilichotokea, kwa kawaida nilikua sipendi kabisa kutangaza maatizo yangu. Nilihangaika sana pale lituoni lakini mke wangu hakupata dhamana, alilala tena usiku mwingine. Nyumbani sikua na amani kabisa, usiku mtoto alikua akilia, pamoja na kujitahidi sana kumpa maziwa ya dukani lakini bado alimhitaji Mama yake. Nilikaa kimya sikuwaambia ndugu zake na siku tatu nzima mke wangu alikua hataki hata kuonana na mimi.
Lakini kila siku nilikua nikienda, nilikua nikibembeleza kumuona, kuna askari mmoja wakike alikua akinisaidia mpaka kwenda kuchungulia kwenye selo alipokua, nilimuita lakini alikataa katakata kabisa kuniona mara zote akiniambia kuwa kama mimi naona kuwa Gari ni bora kuliko yeye basi nimuachea ozee jela. Alinitukana mpaka kila mtu akawa ananichangaa, nilikua kama chizi, nilijitahidi sana kutafuta pesa ya kulipa lakini John hakutaka chochote na dhamana haikupatikana na kibaya zaidi hata mahakamani hawakumpeleka.
Baada ya kuona kama hapelekwi mahakamani labda kupata dhamanai huko nilijua kuwa nimeshindwa, niliamua kutafuta wakili. Nilienda kwenye ofisi moja hivi ya uwakili, nikapaki gari langu lakini kabla ya kuingia niliona dada mmoja akitoka, nilimkumbuka, alikua ni askari ambaye mara kwa mara nilikua nikimuona kituoni, mara nyingi alikua akinisalimia vizuri na ni yeye alikua akiniingiza kinyume cha utartibu kwenda kumuona mke wangu pamoja na yeye kukataa. Yeye alikua ni askari mpelelezo, sijui alifuata nini pale lakini niliamua kumsalimia.
Niliongea naye mawili matatu, alionekana kuwa na haraka kama mtu ambaye alikua akinikwepa kuwa hataki kuongea na mimi. Ni kama kuna kitu alikua ananificha, nilimuuliza lakini hakutaka kuniambia.
“Sitakiwi hata kuongea na wewe, kuonekana na wewe hapa ni kama vile na hatarisha kazi yangu,….” Aliniambia huku akiondoka, alikuja na gari yake, aliingia kwenye gari na kutaka kuondoka, lakini kabla ya kuondoka alishusha kioo cha mbele na kuniita kwamkono.
“Acha kuhangaika, siko katika kesi ya mke wako lakini nahisi kuna mchezo wanakuchezea, mke wako si mtu wa kukosa dhamana, hujiulizi anafahamiana na mkuu wa kituo lakini analala rumande, mkeo sidhani kama analala pale, chunguza…”
Aliongea na bila kunipa majibu alikanyaga mafuta na kuondoka. Nilikaa kimya kwa muda nikajikuta sina hamu tena ya kuingia kwa wakili, wka nilivyokua namfahamu mke wangu asingekubalia kukaa mahabusu, angekua analia kila siku nihakikishe namtoa. Sidhani kama angekubali kula chakula cha mahabusu, lakini katika siku zote tano kila nikitaka kuonana naye alikua anakataa, kila nikimpelekea chakula nilikua narudishwa nacho, tena kwa ukali kabisa kuwa sitakiwi kupeleka chakula pale.
Ni kama kulikua na kitu hasa nikiuliza ni kwanini hapelekwi mahakamani na kama ni mke wangu kuwa na hasira na mimi ni kwanini alikua hata hawapigii simu ndugu zake kuja kumchukua. Niliumiza kichwa sana, niliamua kaucha mambo ya wakili na kuchunguza, nilihangaika kupata taarifa lakini sikupata, kesho yake nilimvizia yule dada wakati anaondoka nikaamua kumfuatilia nyuma mpaka kwake, nilikomaa na kumuambia kuwa siwezi kuondoka mpaka anipe majibu.
Kusema kweli yule dada alikua ananionea huruma, kuna kitu nilikiona kwake, kwa namna alivyokua ananiangalia nilihisi kama vile ananipenda hivyo niliamua kuutumia udhaifu wake huo kupata taarifa.
“Hivi kwanini unampenda yule mwanamke?” Aliniuliza, nilijisikia vibaya kidogo kumuita mke wangu mwanamke kwani niliona kama anamdhalilisha.
“Si mwanamke ni mke wangi, nina mtoto mchanga naye na nimemuoa ndiyo maana nampenda.” Nilijilazimisha kumjibu kwa ustaarabu kidogo kwani pamoja na hasira zangu lakini nilikua nahitaji sana msaada wake.
“Si kwa ubaya lakini hakustahili, anakuchezea akili tu…”
“Kivipi?” Nnilimuuliza huku nikimsogelea karibu, nilimuona kabisa kama anatetemeka, nilimshika mkono na kumvuta mpaka kwenye gari.
“Tusiongelee hapa, watu wanapita…” Nilimuambia, kweli alinifuata bila hata kuuliza, gari yake alikua kaipaki vibaya lakini hata hakujali, aliingia kwenyue gari yangu.
“Tunaelekea wapi?” Aliniuliza, ni kama alitaka twende sehemu, sijui kwanini lakini nilijisikia vibaya, gahfla nilijihisi msaliti, niliona kama vile namsaliti mke wangu kama vile natoka nnje ya ndoa yangu, nilijaribu sana kujizuia lakini aliona.
“Unampenda sana mke wako?” Aliniuliza baada ya kuona kwamba mimi ndiyo nilikua natetemeka kwa uoga, nilikua nahisi kama kuna kitu kibaya nakifanya.
“Kwanini unauliza hivyo? Kawaida tu, si mke wangu…”
“Kwanamna unavyomhangaikia, hivi unajua kila siku nakuja tu kukuangalia, unatia huruma unayofanya huku mwanamke mwenyewe daaa…”
“Mwanamke mwenyewe nini? Mke wangu kafanya nini? Niambie! Unamanisha nini….” Aliongea kwa wasiwasi kama vile kuna kitu alitaka kuniambia lakini alisita, nilimkatisha nikiwa nimepaniki kabisa.
“Unaona wewe si wakuambiwa kitu, unaweza kuniharibia hata na kazi, nimesema hivi tu umepaniki, si unaweza enda kumuambia mke wako ukaniharibia na kazi, mke wako anakula na wakubwa, nikijulikana kama nimeongea kazi sina, kila mtu anajua….daa kuna wanawake wanapendwa lakini hata hawajui kupendwa, ningekua na mwanaume kama wewe…” Alijiongelesha, nililazimika kutulia kwnai nilishapaniki, presha imepanda nahema kama nimepanda mlima, nilitulia na kumbembeleza, aliamua kuniambia hukua kinisihi sana nisimuambie mtu yeyote.
Mke wangu alikua hataki kutoka kituoni kwakua alikua anataka niitoe ile gari, kuna pesa nyingine alikua ameahidiwa na kuhusu dhamana ni mke wangu alikua hataki kwakua alikua halali pale kituoni. Mara nyingi alikua akiletwa asubuhi na jioni mimi nikiondoka nayeye huondoka kwani alikua ni mchepuko wa muda mrefu wa mkuu wa kituo.
“Mbona kila mtu anajua, kila askari anajua na mke wako alikua anakuja mara kwa mara hapa tangu kipindi akiwa mjamzito.” Yule dada aliongea akionekana kama anamjua mke wangu kwa muda mrefu.
“Hivi mwanaume unajisikiaje kuwa na mke wa namna ile, maana hata huyo mkuu mwenyewe anaibiwa, yaani wanawake wengine….”
“Wanawake wengine nini? Wanawake wengine nini?” Nilimuuliza kwa kupaniki, ingawa nilikua najua tabia za mke wangu tangu zamani lakini kuzisikia ilikua ni kama naambiwa upya. Nilishindwa kujizuia nikajikuta hasira zinanipanda, yule dada kuona vile natye alikasirika na kushika.
“Mijitu mingine inasaidiwa lakini haijiongezi!” Aliongea huku akitoka, nilishtuka na kumuomba msamaha, hakunisikiliza sana zaidi ya kuniambia kuwa anaomba nisimuambie mtu kwani nitampotezea kazi.
“Ushauri wangu rudi nyumbani, lea mtoto wako, ukikaa siku mbili tu huajaja kujiliza liza kituoni mke wako atatoka kwa dhamana na huyo anayekudai atakubali umlipe. Sasa hivi hataki pesa zako kwakua mke wakoa najua kua huwezi kumaucha akaozea jela lazima utatoa gari.” Alinishauri na kuondoka, niliondoa gari nikiwa na hasira, mwanzo nilipanga kurudi kituoni kuongea na mke wangu, nilikua na hasira sana lakini nilipofioka nnje ya kituo niliona kama nitahaeribu, niliamua kufuata ushauri wa yule dada. Nilirudi nyumbani nikakaa na kuamua kukaa mpaka mke wangu ajitoe mwenyewe kwani niliamini kuwa ananichezea.
Nilikaa siku mbili bila kwenda kituoni, jioni ya siku ya pili nilipokea simu kutoka kwa John, alitaka kuonana na mimi, nilimuambia nipo bize lakini alilazimishia. Nilikutana naye akaniambia ameona asifuatilie kesi kwani itampotezea muda anataka nimlipe pesa zake lakin kwa riba.
“Mke wako kakaa na pesa zangu muda mrefu, kama ni kufura kasi bais unipe na riba.” Nilimuangalia kwa dharau na kunyanyuka, nilishajua mchezo waao
“Wakati mnapena pesa sikuepo, una kadi ya gari yangu utanipa au nitaenda tu kutoa ripoti kuwa imepotea basi, sitahangaika nayo na kwakua nina kila kitu kingine basi hiyo itakua kama karatasi tu.
Kuhusu mke wangu mtajuana wenyewe, mimi nishamuacha hivyo kamalizane naye.” Niliongea huku nikiondoka harakaharaka,k sijui nilipata wapi ujasiri lakini nilimkazia na kuondoka, hakuamini, wakati naondoka alinitishia tishia kuwa nitafungwa lakini sikujali, niliondoka na kuendelea na mambo yangu. Nilirudi nyumbani nikiwa na mawazo sana, bado nilikua sijui hatima ya mke wangu, nilikua sijui kama atatoka au la, pamoja na yote lakini bado nilikua nampena na nilikua tayari kumsamehe kama angeomba msamaha.
Asubuhi ya siku ya tatu nilitaka sana kwenda kituoni, nilitaka hata kumpeleka mtoto kumuona Mama yake lakini nilisita, baada ya John kunitafuta jana yake nilijua fika kuwa mke wangu kashajua nimemkatia tamaa hivyo wataacha ujinga wake. Kweli ilipofika kwenye saa nne hivi za asubuhi mke wangu alikuja nyumbani, alikua kachoka sana, nilifurahi kumuona lakini sikuonekana hata kujali. Alipoongia alianza kujiongelesha kuwa kapata dhamana, nilimuitikia bila kuuliza chochote, ingawa nilitamani kujua lakini nilitaka kuwa mgumu kidogo.
Alianza kunilaumu kwa kumuacha bila kumtembelea, kuthamini gari kuliko yeye na mambo mengi lakini sikutaka kumsikiliza, nilimuacha anaongea na kuondoka zangu. Hakuaminia lipokua akipiga simu zangu hazipokelewi, hakumini nilipokua nikiacha kujibu meseji zake, ingawa nilitamani kumjibu, kumkumbatia na kumuambia nimemsamehe lakini niliona kuwa amenichezea sana hivyo kama nikimuendekeza basi atanifanyia ujinga mwingine. Nilimchunia na kuzunguka mtaani tu nikiwa sina hili wala lile.
Kwenye saa kumi hivi za jioni bado nilikua mtaani, nilikua sitaki kurudi nyumbani kuonana na mke wangu kwani nilijua kama nikifanya hivyo nitamsamehe na kuwa mdhaifu kwake. Nikiwa sina hili wala lile simu yangu iliita, ilikua ni namba ngeni na nilipopokea ilikua ni sauti ya kike.
“Samahani, nimechukua namba yako kituoni, mimi Joan ( si jina lake halisi) yule dada dada askari…” Alianza kujitambulisha.
“Nakukumbuka, habari? Za tangu siku ile, samahani nilikua sina namba yako, nilitaka kukushukuru kwa taarifa.” Nilimuambia.
“Hakuna shida, nilisafiri ila nimekuja nimesikia mke wako katoka, wamemuachia na hakuna kesi tena.” Aliniambia, nilimuambia nikweli, mbinu aliyonipa ilisaidia.
Nilimshukuru sana na tulijikuta tunaongea sana, sikupanga lakini niliongea na Joan kwa zaidi ya masaa mawili, nilijisikia raha na wala sikujisikia vibaya kuongea naye. Tuliongea mambo mengi akaniambia hajaolewa lakini ana watoto mapacha ambao alizaa na X wake, ambaye alikua akimpiga sana akaona kuachana naye na yule X wake kumkomoa akaenda kumuoa Binamu yake mtoto wa Shangazi yake ambaye pia alikua ni rafiki yake. Stori ya mahusiano yake ilikua ya kusikitisha, niliumia sana namna alivyokua akimhangaikia huyo mwanaume lakini bado akaja kumuacha tena kwa dharau na kejeli.
Baada ya kumaliza kuongea nilikaa mtaani mpaka saa nne usiku, nilirudi na kukuta mke wangu hajalala, alianza kujiongelesha na kunilaumu kuwa simjali ndiyo maana sijamuuliza hata kama kesi imeisha au anadaiwa, sijauliza makubaliano ya yeye kuachiwa kama anatakiwa kumlipa John au la.
“Wakati mnakopeshana sikuepo sasa kwanini unataka kunishirikisha sasa hivi kwenye kulipana. Mtajuana wenyewe, kama mlivyokopeshana basi mlipane hivyo hivyo bila kunishirikisha mimi, na kesho nataka kadi yangu ya gari kama si hivyo huyo mtu wako namfunga na usidhani kama kituo cha polisi kipo kimoja!”
Niliongea maneno ambayo yalimshtua sana mke wangu, tangu kujuana hakuamini kama naweza kumjibu vile, alijua kuwa mimi ni mtu tu wa kumsikiliza na kufanya kile anachokitaka yeye. Nilipanda kitandani na kulala huku mke wangu akiendelea kuongea, alilalamika sana labda mimi namsaliti lakini wapi sikujali. Asubuhi nliliandaa kwajili ya kazi, nilimuacha mke wangu nyumbani, nilimpa Shilingi elfu tano.
“Yanini?” Aliniuliza.
“Kwaajili ya mboga, au hamli leo?” Nilimuuliza huku nikitaka kuirudisha mfukoni, aliniangalia kwa mshangao.
“Elfu tano? Sasa hiyo inatisha nini?” Aliniuliza nilimuangalia kwa mshangao na kumuambia.
“Kila kitu kipo ndani, kama elfu tano huwezi kununua mboga zikatutisha basi toka katafute kazi, sina pesa ya ziada.” Niliiweka juu ya meza na kuondoka zangu nikimuacha mke wangu kaduwaa.
Alilalamika sana lakini hata sikumsikiliza, nilitoka, nikiwa kwenye gari simu yangu iliita, alikua ni Joani akinisalimia tuliongea kidogo na kuagana. Kusema kweli nilijisikia vizuri, nilipokata simu nilitamani kumpigia tena simu ili kuendelea kusikia sauri yake, lakini nilijizuia mpaka mchana, nikitaka asiwe wakwanza kunipigia nilimpigia na baada ya kuongea bila kupanga nilijikuta namuuliza.
“Vipi jioni unaweza kuwa na muda, natamani sana kuonana na wewe, last time najua nilikukwaza, nahitaji kuomba msamaha uso kwa uso…” Nilimuambia, moyo ulikua unadunda nikiwaza kama atakubali ombi langu au la?
***
Ninakua na wateja wengi hivyo kumjibu kila mtu anayenitumia SMS ni ngumu, kama unahitaji ushauri ni lazima uwe umenunua vitavu vyangu, kama unahitaji ushauri wa mahusiano ya kawaida nilazima uwe umenunua Kitabu cha “Ndoa yangu Furaha Yangu” Bei yake ni Shilingi elfu kumi tu!
Kama ushauri unahusiana na mapenzi lakini unagusa upungufu wa nguvu za kiume wa mwenza wako au wewe mwenyewe mwanaume au maumbile madogo na namna ya kumrishisha mwanamke basi Kitabu ni “MWANAUME” bei yake ni Shilingi elfu ishirini.
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SEHEMU YA TANO
Ilikua ngumu sana kwangu kupata sehemu ya kukutana na Joan, mke wangu ni mtu anayefahamika hivyo nilijua kuwa kukaa na mwanamke sehemu yoyote basi angepata taarifa na kwa nilivyokua namjua basi angekuja na kunifanyia fujo. Joan alikubali kukutana na mimi, aliponiuliza wapi nilishindwa kumjibu, nilimuambia tu nitaenda kumchukua kwake, alikubali ingawa sikujua kama nampeleka wapi lakini nilitaka tu kuonana naye na kuongea naye.
Jioni hata sikurudi nyumbani, nilikaa kazini mpaka muda wa kukutana na Joan ulipofika, nilimfuata mpaka nyumbani kwake, alikua shajiandaa kavaa kapendeza, aliingia kwenye gari na kunisalimia.
“Unananipeleka wapi?” Lilikua ni swali lake la kwanza mara baada ya salamu. Nilinyamaza kidogo nikitafakari kisha nikamjibu.
“Hata sijui, mimi naona kwakua ni siku yetu ya kwanza basi tuongelee hapa kwenye gari….” Niliongea huku nikitetemeka, sijui kwanini lakini nilikua ninaogopa, ni miaka kadhaa ilikua imepita tangu kuwa na mwanamke mwingine zaidi ya mke wangu.
Si kwamba nilikua sijui kutongoza, hapana, nilikua najua sana lakini nilikua na h0fu, nilijisikia sana kumsaliti mke wangu na kwa mimi kukaa na joan namna ile niliona kama usaliti. Jibu lile lilimshangaza sana joan lakini tofauti na nilivyotegemea hakupaniki, alitulia kidogo na ni kama alikua anasoma akili yangu.
“Unamuogopa sana mke wako, najua anajulikana kila sehemu lakini huna haja ya kuwa na wasiwasi.” Aliniambia, nilinyamaza kidogo, nikiwaza kitu cha kumjibu, niliogopa na kuna wakati hata sikujiona mwanaume.
“Mwanaume gani mimi namuogopa mwanamke namna hii?” Niliwaza, Joan ambaye alikaa kiti cha abiria alipitisha mkono wake na kunitengeneza shati, alitoa kitambaa na kunifuta jasho, pamoja na kuwasha AC mpaka mwisho lakini nilikua nikitokwa jasho kama vile nimetoka kukimbia.
“Usiogope, acha kupaniki basi, washa gari nitakupeleka sehemu ambapo mke waho hajulikani kabisa. Nilimuuliza wapi lakini hakunijibu, aliniambia atanielekeza, niliwasha gari na kweli safari ilianza, tulikua tunaelekea maeneo ya Mbagala, tulienda mpaka Chamanzi.
Alinipeleka mpaka nyumba moja kubwa tu nzuri, ilionekana mpya ni kipindi kile chamanzi haijajengeka, ndiyo ilikua inaanza kujengeka taratibu. Aliniambia nipaki gari, nikijua ni nyumba ya kulala wageni alitoa funguo zake na kufungua mlango. Aliniambia niingie, huku nikiwa na wasiwasi nilimuuliza pale ni wapi aliniambia nisiogope niingie. Ilikua nyumba nzuri ya kisasa na kule ndani kulikua na karibu kila kitu, lakini kila kitu kilionekana kama ni kipya kama hakuna mtu anakaa.
Kwa hofu nilimuuliza ndipo aliniambia kuwa pale ni kwake, ni nyumba alikua anajenga muda mrefu, ishakamilika lakinia nataka mpaka aweke fenicha zoet mpya ndipo ahamie. Nilijisikia huru kidogo kwani niliona kama ni sehemu salama. Alinikaribusha tukaongea na kuongea, nilijua kuwa alikua hajaolewa lakini alikua na mtoto mmoja wakike ambaye alizaa na mwanaume mmoja ambaye aliachana naye kwakua alikua akimpiga sana, alikua akiishi naye kama mke na mume lakini ndugu zake walipoona kuwa anamnyanyasa walienda kumchukua ingawa yeye alikua hataki.
Baada ya hapo ndipo alitafutiwa nafasi jeshi la Polisi, ambapo ana miaka kama saba na kwa wakati huo alikua hana mwanaume yeyote. Mtoto wake haishinnaye anaishi kijijini na Mama yake lakini ana mpango akishahamia katika nyumba yake kwenda kumchukua. Siku hiyo tuliongea tu bila kufanya chochote, nikiwa pale mke wangu alikua akipiga simu sana lakini sikupokea, nilikaa mpaka saa nne usiku, tukarudi nikamuacha kwake na mimi kurudi kwangu.
Nilimkuta mke wangu ameshalala, niligonga mlango na binti wa kazi ndiyo alinifungulia. Chakula kilikua mezani huku mke wangu akiwa kalala, nilikua nimeshiba lakini nilitaka kula nyumbani kidogo ili kuepuka shari, kuangalia chakula ilikua ni wali kuku. Nilishtuka kidogo kwani ndani niliacha elfu tano na hakukua na mboga, nilitaka kula nikashindwa, nikarudi ndani kulala, ile kuingia tu mke wangu alishtuka, akanyanyuka na kunisalimia, kisha akaelekea chooni.
Cha ajabu hakuniuliza kwanini nilikua nimechelewa, hakuniuliza kama nilikua na nani! Nilisubiri labda akiwa katika chooni kama mimi angelalamika lakini wapi, alipanda kitandani na kujifunika. Simu yangu iliita, alikua ni Joan, kwa makusudi nikijua kuwa mke wangu atasikia niliipokea na kuongea kidogo, mke wangu alisikia lakini hakuniuliza chochote. Nilijikuta nalala kwa shida nikiwaza ni kwanini mke wangu haniulizi chochote, labda hanipendi, labda ana mwanaume mwigine, labda anataka kuniacha na mawazo mengine mengi mengi lakini sikua na jibu.
Kwakua sikupata kabisa usingizi asubuhi nilikua wakwanza kabisa kuamka, nilijiandaa kwaajili ya kwenda kazini, mke wangu alikua bado kalala, hata nilipokua namuaga kuwa naondoka hakugeuka, nilipokua nampa pesa hakugeuka aliniambia.
“Mimi nimechoka, weka hapo kwenye meza!”
“Hutaki hata kujua nimekuachia Shilingi ngapi?” nilimuuliza huku nikiwa nimeshikilia shillingi elfu tano yangu mkononi, niliona kama vile namkomoa kumuachia pesa kidogo.
“Unafikiri hata najali, mimi hata usipoacha pesa ya kula nitakula tu. Umenikuta mtu mzima nakula, kama hukunilisha utotoni huwezi kunitisha na pesa ukubwani, hata mimi najua kutafuta.”
Alinipa jibu ambalo mpaka leo linanichoma, alinivunja nguvu kabisa, nilisi kama kuna mtu kanikatakata vipande vipande na kuvichemsha. Sikuweza kuendelea kuongea, niliacha ile eelfu tano mezani na kuondoka zangu. Nikiwa njiani Joan alinipigia simu, aliniuliza kama nimeshafika kazini nikamuambia bado. Alianza kunishukuru kwa siku ya jana alianza kuniambia namna alivyofurahia lakini sikujali.
“Niko barabarani naendesha, naomba nikutafute baadaye.” Nilimuambia nakukata simu bila hata kusubiri jibu lake, kichwani nilikua nimechanganyikiwa, nilikua na mawazo mengi sana kuhusu mke wangu hasa kwanini hajali mimi kuchelewa au kumuachia pesa kidogo.
****
Kila siku jioni nilikua nikimtafuta Joan, sikufanya siri tena, ni kama nilitaka mke wangu kujua, sikua nikifanya kama kujifurahisha bali ni kamja nilitaka kumtia wivu, nilikua na maumivu makali moyoni kiasi kwamba niliamini kwa mimi kuachepuka au kutaka kumuonyesha mke wangu kuwa nachepuka basi ingesaidia kumuumiza kama nilivyokua naumia. Nilikutana na Joan sehemu za wazi kabisa tena sehemu ambazo nilijua kabisa kuwa ni lazima mke wangu angesikia na hata kuja kutufumania.
Lakini haikutokea hivyo, pamoja na kuchelewa kurudi, wakati mwingine kurudi asubuhi lakini mke wangu hakuwahi kuniuliza kama nimetoka wapi, hakuwahi kuniyonyesha kisirani kama kile ninachomuonyesha kitu ambacho kilizidi kuniumiza.
“Mbona hauko sawa, una uhakika unataka kufanya hiki kitu?” Joan aliniuliza, ilikua ni siku ya jumamosi, nilimpeleka joan Bagamoyo, baada ya kuwa naye kwenye mahusiano kwa meizi sita na baadhi ya ndugu zake kunifahamu nilikua tayari kufanya naye mapenzi, katika kipindi chote hicho tulikua kama marafiki tu.
Ingawa alitaka sana lakini nilijikuta nakataa, nilijizuia na nilijiona kama siko tayari.
“Niko sawa, niko kwaajili yako, nimeamua wewe ndiyo mwanamke wa maisha yangu.” Nilimuambia huku nikimsogelea na kumkumbatia, alinishika na kunitomasa, alinichezea kila sehemu ya mwili wangu lakini nilikua wa baridi kama vile nimemwagiwa kwenye friji, akili zangu hazikua pale, nilikua namuwaza mke wangu mpaka uume wangu ulishindwa kusimama kabisa.
“Au una muwaza mke wako?” Aliniuliza, ingawa ilikua ni kweli lakini niliona aibu kukubalia, nilitingisha kichwa kumkatalia.
“Nadhani ni kwakua ni mara ya kwanza hatujazoeana, nina ihakika mpaka subuhi tutaweza.
Nilimsogeza karibu yangu na kumkumbatia, nilichukua simu yangu na kuanza kupiga picha.
“Unafanya nini?” Aliniuliza, nilinyamaza sikumuambia chochote, niliendelea kupiga mpaka aliponinyang’anya simu, tulikua uchi kitandani na nilikua nataka kupiga naye picha.
“Unafanya nini wewe? si unajua kuwa unha mke, akija kuziona?” aliniuliza, nilimkumbatia vizuri kwa nguvu, nilijikuta nasisimkwa, hata yeye alishangaa, alicha wazo la picha na kuanza kunikumbatia, simu ilikaa pembeni tukaanza kufanya yetu. Kwa mara ya kwanza nilimsaliti mke wangu na nilijisikia vizuri sana.
Weekend ile ilienda vizuri sana, tulifurahia na tulifanya kila kitu, nilirudi nyumbani nikiwa nimechangamka. Lakini niliporudi sikumkuta mke wangu, naye alikua katoka, nilipomuuliza Binti wa kazi alinijibu kuwa alitoka siku ile tu nilipoondoka na alikua hajarudi. Kumbuka weekend nzima sikumpigia simu mke wangu, nilifanya hivyo ili kumuumiza, lakini naye hakunitafuta, kumbe naye aliondoka, nilichukua simu na kuanza kumpigia, nilipiga mara ya kwanza simu haikupokelewa, nilipopiga mara ya pili ilipokelewa lakini hakua mke wangu, ilipokelewa na Mama mkwe wangu.
Moyo ulitulia kidogo, mwanzo nilihisi kama mke wangu kaenda kwa mwanaume mwingine tena na mtoto, alipopokea Mama yake nilimsalimia na kumuulizia mke wangu. Aliniambia kuwa yuko salama lakini hawezi kuongea na mimi kwani namfanyia vituko na kashajua kuwa nina mwanamke mwingine hivyo anahitaji nimpe talaka.
“Yessssss!” Nilijikuta napiga kelele kufurahia.
“Unasemaje?” Mama mkwe aliniuliza, nilinyamaza kwani kelele zangu hazikua sababu ya mke wangu kudai talaka bali nilifurahi kuwa hatimaye nimefanikiwa kumuumiza mpaka akaenda kwa Mama yake.
“Mimi Mama talaka siwezi kutoa, mke wangu bado nampenda, najua kuoa lakini sijui kucha!” Nilimuambia huku nikikata simu, nilijua kabisa kuwa nimewaumiza, nilijua kuwa mke wangu kakasirika na kajua kuwa mimi nachepuka ndiyo maana kaenda kunishitaki kwa Mama yake. Nilikata simu nikijua kuwa watanipigia ili kunibembeleza, lakini haikutokea hivyo, nilisubiri na kupiga tena usiku, alipokea Mama mkwe wangu na kuniambia kuwa mke wangu hawezi kupokea simu zangu kwani ameumia sana anachosubiri ni talaka yake basi.
Nilifurahi sana, sikua na mpango wa kumaucha mke wangu lakini nilijua namimi nimeweza kumuumiza. Nilimuambia Mama mke kua siwezi kutoa talaka, nilikaa kimya kwa siku tatu bila kuwatafuta lakini nao hawakunitafuta, nilianza kuwa na wasiwasi nikidhani kuwa labda mke wangu kweli alikua akimaanisha, niliamua kumpigia tena simu mke wangu ili kumuomba msamaha na kuacha yaishe. Nilipiga simu ikaita sana lakini haikupolekewa, iliita sana mpaka kukatika lakini kila ilipoita nilizidi kupiga, nilijihisi kuchanganyikiwa kwani niliona kama mke wangu ananiacha.
Mwisho mke wangu alipokea simu, alikua akilia sana huku akinilaumu mimi kuwa yeye kaamua kubadilika lakini mimi simuoni nimeamua kuwa Malaya.
“Najua unalipa kisasi lakini magonjwa ni mengi, nimechoka wewe kunirudia usiku wa manane, nataka talaka yangu sitaki tena kuishi na wewe!” Mke wangu alilalamika, nilimbembeleza sana lakini hakutaka kunisikia, alikua akidai talaka na kusema kuwa hawezi kurudi tena kwangu. Tulishindwa kuelewana na kuamua kumpigia simu Mama yake, nilimuambia nikweli nilikua na mtu lakini ni rafiki tu na nilifanya hivyo baada ya mke wangu kunisaliti. Mama mkwe naye alikua upande wa mwanae akidai nimpe talaka.
Nilikataa katakata, siku hiyo hiyo nilipanda gari kuelekea tanga, nilifika usiku hivyo sikufika moja kwa moja kwa Mama mkwe wangu. nilienda kwenye nyumba moja ya kulala wageni, lakini usiku huo huo nilimtafuta mzee mmoja ambaye alikua ni kama mshenga kwangu, yeye ndiyo ambaye mara nyingi alikua akinipokea nikienda tanga kwani kipindi Baba yangu ni Askari Tanga alikua ni rafiki yake mkubwa. Kwanza alishangaa kuniona, nilimsalimia na kumuambia swala langu, kumuambia nilipokua nimekosea na kumuomba kesho yake kuongozana mpaka kwa mke wangu ili kuomba msamaha.
“Msamaha wa nini tena, kama ulitoa talaka hakuna cha msamaha tena…” Aliniambia.
“Hapana Baba, mke wangu bado sijampa talaka, ameondoka tu bila kuniaga.” Nilimjibu, aliniangalia kwa mshangao zaidi, aliniuliza mara mbilimbili kama nilimpa talaka au la lakini nilikataa.
“Mbona sielewi sasa, maana leo tu ndiyo nimetoka kule, kuna watu walikuja kutoa mahari nikajua labda mshaachana! Hii familia vipi ndoa juu ya ndoa, hata mume wake wa kwanza sidhani kama alitoa talaka, yule mwanaume alifukuzwa tu kama mbwa baada ya wewe mwenye pesa kuja!”
“Mume wake wa kwanza?” Nilimuuliza, yule Baba aliniangalia kwa mshangao.
“Inamaan hujui kuwa mke wako alishawahi kuolewaga na ana mtoto mkubwa tu?” Aliniuliza swali ambalo liliniacha mdomo wazi.
***
Ninakua na wateja wengi hivyo kumjibu kila mtu anayenitumia SMS ni ngumu, kama unahitaji ushauri ni lazima uwe umenunua vitavu vyangu, kama unahitaji ushauri wa mahusiano ya kawaida nilazima uwe umenunua Kitabu cha “Ndoa yangu Furaha Yangu” Bei yake ni Shilingi elfu kumi tu!
Kama ushauri unahusiana na mapenzi lakini unagusa upungufu wa nguvu za kiume wa mwenza wako au wewe mwenyewe mwanaume au maumbile madogo na namna ya kumrishisha mwanamke basi Kitabu ni “MWANAUME” bei yake ni Shilingi elfu ishirini.
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SEHEMU YA SITA
Suala la mke wangu kuwa na mtoto nilishalihisi, alikua akifanana sana na yule mtoto na mara zote alikua akimuita Mama. Mke wangu alikua akiniambia nikwakua yeye ndiyo kamlea lakini namna alivyokua akimjali ilikua ni zaidi ya mtoto wa ndugu yake. Lakini suala la kuolewa kabla lilinichanganya zaidi, sikutaka kuamini lakini namna yule mzee alivyokua akiongea na matukio ya mke wangu nilijikuta naamini. Niliumia sana kwani nilikua nampenda sana mke wangu, alishanifanyia mengi lakini nilimsamehe kwasababu ya upendo wangu kwake.
“Ukitaka amani mpe tu talaka, andika tatu aendelee na maisha yake…” Yule mzee aliniambia, aliongea kana kwamba kilikua ni kitu kidogo sana, mimi tayari nilishanganganyikiwa, hata kukaa pale niliona shida, niliondoka kama mtu aliyechanganyikiwa na kwenda mpaka nyumbani Kwa kina mke wangu. kila mtu alishangaa kuniona lakini cha ajabu walinikasirisha vizuri tu, katoto ka mke wangu kalikuja kunisalimia Baba, mke wangu aliniangalia kwa aibu, Mama yake alikua kimya na ndugu zake wengine walikuja kunisalimia.
Ukimya ulitawala, kila mmoja alikua akimtegea mwenzake ili kuongea, baada ya kuona ukimya umezidi niliamua kuuvunja.
“Nimekuja kukuchukua, wewe ni mke wangu mimi siwezi kukupa talaka! Kwa kosa gani hasa mpaka mimi nikuache!” Nilianzisha mazungumzo.
“Umemsaliti mwanangu, wewe si una mwanamke wako, sasa kwanini hutaki kumuacha mwanangu!” Mama mkwe aliongea kwa hasira, mke wangu bado alikua kanyamaza, alikua anajua kuwa sijamkosea chochote, mambo yote niliyokua nayafanya yalitokana na tabia zake.
“Hapana Mama, mwanao kanifanyia mambo mengi mabaya, lakini nimesamehe, mimi kosa moja tu ndiyo anajifanya kuniacha, siwezi kumuacha mke wangu nampenda sana!” Niliwaambia, yalizuka mabishano makubwa kati ya mimi na Mama mkwe wangu, yeye alitaka mimi na mke wangu tuachane. Wakati wote huo mke wangu alikua kimya, alikua akiangalia chini, akijifanya kuwa ana aibu na kujifanya kuumizwa na yele mambo, nilijua janja yake, alitaka kuonekana kama mwema na mimi kuona kama ndiyo mwenye tatizo.
Sikutaka kuuliza kuhusu habari za yeye kuolewa tena, si kwamba kile kitu kilikua hakinikerteketi lakini nilikua sijamuamini sana yule mzee, lakini nilitaka mke wangu kuniambia yeye mwenyewe. Nilimdodosa sana ili kuniambia sababu za kutaka kuachana na mimi lakini hakutaka, hata Mama yake hakusema, walizidi kusingizia tabia zangu huku mke wangu akisema kanichoka anataka nimpe talaka.
“Una hangaika nini? Kwani talaka basi ni lazima akupe, akikutamkia tu ni kama kakuacha!” Mdogo wake wakiume aliongea, nilimuangalia kwa hasira na kumuambia.
“Mimi dada yako sijamuacha, kama ndiyo mipango yenu basi mmechina, sijamuacha mke wangu si kwa maneno wala si kwa maandishi, huyu ni mke wangu na nimakuja hapa kwa njambo moja tu ambalo ni kumchukua.”
“Nilikuambia tu kiheshima ili uniache lakini mimi nilishaachika kwako muda mrefu. Mimi sisalitiwi na kwa taarifa yako talaka ulishanipa tena tatu…” hatimaye mke wangu aliongea, wakati nabishana na ndugu zake alitoa kipande cha karatasi, kilikua na muandoka wangu na saini yangu kuonyesha kuwa mimi nimemuacha mke wangu tena kwa talaka tatu.
Kama alivyofoji sahihi yangu katika kuuza gari ndivyoa livyofanya kwenye talaka.
“Kwahiyo nikweli unataka kuachana na mimi?” Nilimuuliza, baada ya kuona kile kikaratasi ndipo niliamini kuwa mke wangu anataka kunicha. Nilikua naumia sana lakini kama alishafikia hatua ile nilijua ndiyo basi.
“Ndiyo, nimeamua nimechoka na tabia za….” Alijaribi kujitetea hukua kijifanya kulia lakini sikukubali anisingizie.
“Hapana, wewe unajua kila kitu, utadanganya kila mtu kuniumiza mimi lakini kumbuka kuwa mimi na wewe tunaujua ukweli, machozi yako hayasaidii, umeniumiza sana na kama kweli umeamua basi baki na mimi naendelea na maisha yangu.”
Niliongea huku nikinyanyuka kwa hasira, niliona aibu, nilijisikia vibaya, pamoja na kumpenda sana mke wangu lakini niliona kuwa ameshaamua, sikua na haja tena ya kumtetemekea, kumlilia wakati hanitaki. Niliingia kwenye gari nikaenda sheli na kujaza mafuta kisha nikarudi zangu dar siku ileile. Sikutaka tena kusubiri, akili ilikua haiku sawa. Nilifika bila kupumzika nilimtafuta Joan, nilimuomba kuja nyumbani, alishangaa ni kwanini lakini nilimuambia kuwa mke wangu nimemfukuza.
“Nimechoka tabia zake, nimemuacha na sasa nataka kuanza upya.
Niliumia sana lakini kama mwanaume nisingeweza kusema kuwa nimeachwa, nilijifanya kumuacha mke wangu, kila rafiki yangu, kila ndugu nilimuambia kuwa nimempa mke wangu talaka tatu. Katika kipindi hicho ndipo niligundua madudu mengi ya mke wangu, kila mtu sasa alianza kufunguka.
“Afadhali umemuacha, alikua anatembea na flani….mimi nilishamuona sehemu flani akiwa hivi na vile…nina wasiwasi hata yule mtoto si wako…nilishawahi kumfumania,….yule si mwanamke” Nilisikia madudu mengi sana ya mke wangyu, alitembea na zaidi ya nusu ya marafiki zangu, alishatembea mpaka na Baba yangu mdogo na vite nilisikia baada ya kusema kuwa nimemuacha.
Ingawa kila mtu alikua ananipongeza lakini sikua na amani, hongera zao zilikua kama dhihaka kwangu, nilijisikia vibaya walivyokua wakiniambia kuwa ni Malaya, niliumia kwakua bado nilikua nampenda, nililia, nilihuzunika lakini nilificha huzuni zangu. Sikutaka watu wajue na kwakua nilikua na joan wangu nilimfanya kama mke, nilikua nikifanya naye mapenzi kila siku, kwangu ilikua kama kazi, kilikua ni kitu cha kunifanya nimsahau mke wangu kwa muda flani, sikua na furaha pamoja na Joan kufanya kila kitu ili kunifurahisha.
Bado nilikua na hasira na mke wangu, nilitaka kulipa kisasi, nilitaka kama mimi nilivyoumia yeye naye aumie. Lakini nilimuona kama vile haumii, alikua kawaida kabisa anaendelea na maisha yake, alikua hanitafuti na kila siku alikua akipost picha facebook kuonyesha kuwa ana furaha. Niliumia hivyo na mimi nilitaka kumuonyesha kuwa nina furaha, nilianza kumtumia picha zangu nikiwa na Joan, kipindi hicho ilikua ni Facebook tu ndiyo ina nguvu, sikutaka kumpost Joan kwani sikutaka watu wengi kujua kuwa niko naye.
Lakini nilitaka mke wangu ajue hivyo nilimtumia picha zangu na joani kila safari, kila starehe, picha za kitandani, picha tukifanya mapenzi na kila kitu lengo lilikua kumuumiza lakini niliona kabisa kuwa haumii. Hakuniblock zaidi ya kunidhihaki kwa kumsifia Joan kinafiki, hali hiyo iliniumiza sana, nilikosa amani ingawa mimi ndiyo nilikua namtafuta na kumsumbua lakini nilimblock ila baada ya muda nilifungua akaunti nyingine feki na kuanza kumfuatilia tena. Hali ilikua mbaya sana kwangu mpaka joani akagundua kuwa namtumia yeye ili kumsahau mke wangu.
Alijua kabisa kuwa si mimi niliyemuacha mke wangu bali ni mimi nilikua nimeachwa, alikasirika na kuondoka, hakutaka kuja kwangu tena, alidhani nitamuomba msamaha lakini wapi, sikua tayari kwa hilo. Baada ya Joan kuondoka na kuwa kama vile kaniacha kisirani kilizidi, hasira zilizidi na nilitaka kulipa kisasi. Nilifikiria njia nyingi za kulipa kisasi nikajua ili mke wangu nayeye asiwe na amani nimharibie kwa mchumba wake mpya, ingawa alifanya siri nisimjue lakini nilihangaika mpaka nikampata, yeye alikua dar, alikua na kampuni ya maji na pia alikua na hoteli mbili kubwa tu.
Kwakifupi ni mtu ambaye alikua na pesa zake tena kijana kabisa, niliamua kumfuata ofisini kwake na kumuambia aachene na mke wangu. Alikua ni kijana mtulivu tu ambaye alionekana kutoka kwenye familia bora. Yeye na mke wangu walikua kwenye mahusiano kwa miezi na alishangaa sana kusikia kuwa mke wangu kaolewa kwani alimuambia kuwa aliachana na mpenzi wake miaka minne kabla kutokana na kumpiga mara kwa mara hivyo alihitaji mwanaume muaminifu. Alishangaa zaidi nilipomuambia kuwa mke wangu nilikua nikiishi naye kwani katika hiyo miezi sita alishaenda mara nyingi kwa mke wangu na kulala kwake.
Aliponielekeza sehemu aliyokua kapelekwa niligundua kuwa ni nyumbani kwa Mama yake mdogo na mke wangu na siku zote ambazo mke wangu alikua akimkubalia kwenda kulala au mke wangu kwenda kwake kulala zilikua ni siku ambazo nipo safari kikazi. Niliona kabisa kachanganyikiwa na hakutaka kukubaliana na ukweli.
“Kwahiyo unataka kuniambia kuwa hata mimba aliyonayo si yangu?” Aliniuliza swali ambalo mimi lilizidi kunichanganya, sikua najua kuwa mke wangu ana mimba. Lakini sikutaka yule kijana kujua kuwa mimi sijui, nilitaka kuzidi kumchanganya.
“Mimba ni yangu, sijui kwanini anataka kuniacha lakini nimeona kuwa huwezi kumuoa mke wangu.” Nilimtolea picha zetu za harusi, picha nyngine za kawaida na picha za m,toto wetu.
“Hapana, yule mwanamke hajazaa, haiwezekani!” Alijiongelesha wakati anaangalia picha za mke wangu. alionekana kuchanganyikiwa, alichukua simu kumpigia mke wangu lakini haikupokelewa, baada ya kuona haipokelewi aliniambia.
“Nashukuru kwa kunitafuta lakini mimi nitafanya uchunguzi wangu mwenyewe, haiwezekani yeye kuwa na mwanaume mwingine. Ananioenda sana na alikua tayari kubadilisha dini uili nimuoe, wewe unafikiri nitawaambia nini wazazi wangu! kwetu wote wanamjua na wanampenda sana.”
Niliona kabisa kuwa hatuwezi kuelewana, niliondoka nikijua kabisa kuwa hawezi tena kumuoa mke wangu. Nilipotoka tu katika ile ofisi nilianza kumtumia meseji mke wangu. “Si ulikua unajifanya kuwa unaweza kunikomoa sasa nishamuona mtu wako nishakuharibia…tuone kama sasa utaolewa…nakuambia lazima utaachika na hiyo mimba nataka uitoe siwezi kulea mtoto haramu….” Kwa hasira nilijua kuwa nimemkomesha mke wangu nilianza kutuma meseji nyingi za matusi nikiwa kama namshushua mke wangu.
Hapo nadhani ndipo nilipokosea kwani mke wangu alipojua nimafanikiwa kumpata mchumba wake alimpigia simu huku akilia, alijifanya kuwa hajui kinachoendelea ndipo alianza kumlalamikia akimuambia kuwa ni bora waachane. Niliajua hayo siku iliyofuata, nikiwa ofisini sijui hili wala lile walikuja watu wawili, walivbaa kiraia lakini walijitambulisha kama askari, wakanitilea vitambulisho na kuniomba tuongozane nao, hawakuniambia kosa langu lakini walinipeleka mpaka kituni.
Nilipofika nilikutana na yule mchumba wa mke wangu, yeye ndiyo alifungua kesi kuwa nimemtishia mchumba wake. Madai yake nikuwa mke wangu alimpigia simu kuwa nimetumia meseji kuwa hawezi kuolewa, atoe mimba na nimemharibia kwa mchumba wake. Alinionyesha meseji, nilijaribu kujielezea lakini nilinyang’anywa simu na kweli walipoangalia nilionekana nimezituma mimi zile meseji.
“Ni kawaida yake, alishaachwa miaka minne iliyopita lakini kila siku anamharibia binti wa watu, yeye kashaoa ana maisha yake lakini kila binti akipata mchumba anaenda kumchafulia, nampenda sana mchumba wangu siwezi kumuacha kwakua tu umesema.”
Hapo ndipo nilijua kuwa kweli nimeharibu, kutuma meseji na simu za vitisho ingeonekana kuwa mimi nina matatizo.
“Kafoji mpaka vyeti vya ndoa ili tu kumaharibia mtu.” Aliendelea kuongea, alikua na hasira na kwakua alikua na pesa niliwekwa ndani, nilikaa huko kwa siku tatu. Lakini mke wangu hakurudi Dar, hakutaka kuonekana, hakutaka kunigungulia kesi na kwakua yeye ndiyo alikua katishiwa maisha basi yule mchumba wake alinitoa lakini kwa onyo kuwa nisimsumbue tea mchumba wake, alinitishia kuwa hata kama mke wangu hataki kufungua kesi na kunifunga lakini kama nikimpigia simu au kumtishia tena maisha basi atanipoteza kwani mke wangu kabeba kiumbe chake tumboni.
Pamoja na vitisho vyote hivyo lakini sikukoma, niliendelea kumtafuta mke wangu ila hakua hewani, hata ndugu zake walikua hawapatikani ndipo nikajua tayari nimeshaachwa. Nilikaa mwenye kwa mwezi mmoja mpaka nilipokutana na Joan mjini, tulisalimiana, aliniona nilivyokua nimenyong’onyea. Aliniuliza sababu lakini sikutaka kumuambia, alishaniacha hivyo sikutaka aingilie maisha yangu tena. Lakini kumbe alikua anajua, alikua anajua kuwa nimepelekwa Polisi na mwanaume ambaye anataka kumuoa mke wangu. tuliongea kidogo, sikutaka kupoteza muda naye, niliaga na kuondoka.
Lakini jioni Joan alikuja kwangu, nilimkaribisha vizuri tu ingawa sikua katika Mood kabisa.
“Kuna kitu nilitaka kukuambia muda kidogo lakini nilisita, nilijua utarudiana na mke wako hivyo sikutaka kuumizwa.” Alianza kuongea, mimi nilimsikiliza tu, akili yangu haikua pale kabisa, nilikua na mawazo mengi kuanza kumuwaza na maneno yake.”Nina mimba yako, ina miezi mitatu, nilijua muda lakini nilikua sijapanga kama nizae au la?” Aliniambia, nilikua kama sijamsikia mpaka aliporudia tena, nilimuambia hakuna shida hata mimi nahitaji mtoto.
Kusema kweli sikua na hisia naye lakini baada ya kuniambia kuwa ana mimba yangu niliona nibora kubaki naye kuliko kuendelea kumsubiria mwanamke ambaye hanitaki. Tulirudisha tena mahusiano na wakati huu nilijitahidi sana kukata mawasiliano kabisa na mke wangu, siku mtafuta tena niliacha aendelee na mwanaume wake pamoja na uongo wake. Ilipita kama miezi mitatu hivi, muda mwingi nilikua kwa Joan, nyumba yangu ilikua na kumbukumbu nyingi za mke wangu na kwakua sikua na mfanyakazi nilikua kama nimehamia kwa Joan ingawa bado nilikua naenda enda nyumbani kwangu.
Siku moja nikiwa kazini nilipokea simu, ilikua ni namba ngeni, nilipoipokea ilikua ni sauti ya mke wangu. kitu kilinipiga Paaa! Nilitamani sana kumkatia simu lakini sikuweza, kuna kitu nilitaka kujua, kuna kitu kiliniambia kuwa msikilize huyo mtu.
“Mbona hauko nyumbani, nimekuja tangu jana lakini hujarudi nyumbani, kwanini unaiacha nyumba peke yake?” Mke wangu aliniuliza baada ya salamu ambayo hata sikuiitikia.
“Nyumbani? Unafanya nini nyumbani kwangu? wewe si ulijipa talaka mwenyewe, si ulisema kuwa hujaolewa sasa kwa taarifa yako hupati chochote, kama ni mali unataka basi tutamalizana mahakamani, sikupi kimya kimya ili huyo mwanaume wako unayemdanganya ajue ushenzi wako!” Nilimuambia kwa hasira, kwa namna nilivyokua namjua mke wangu nilijua kuwa asingeweza kuniacha kwa amani, angetaka kuchukua baadhi ya vitu hasa nyumba ambayo ilikua na jina lake.
“Nani kakuambia ana shida ya mali zako? Njoo nyumbani tuongee!” aliniambia na kunikatia simu.
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SABA
Nilirudi nyumbani nikiwa kama mtu aliyechanganyikiwa, akili yangu ilikua inawaza mambo mawili, jambo la kwanza nikifika nimfukuzie mbali na kuendelea na maisha yangu na jambo la pili nilitaka sana kujua sababu ya yeye kuja kwangu, nilitaka kumuacha palepale nyumbani ili aone namna nilivyonafuraha na Joan.
“Kwanini hukai nyumbani? Umeamua kuitelekeza nyumba?” Mke wangu aliniuliza baada tu ya kuingia ndani. Tumbo lake lilikua kubwa, ni muda nilikua sijaonana naye hivyo sikua na uhakika kama kweli ana mimba au la.
“Unafanya nini nyumbani kwangu?” Nilimuuliza huku nikikaguiakagua vitu kana kwamba naangalia kuona kama nimeibiwa au la? Hakujibu chochote, alinyanyuka na kunifuata kutaka kunikumbatia.
“Inamaana hujanimiss, hujanikumbuka, yaanui baada ya kufurahi kuwa mke wako karudi wewe unaanza kuuliza nimefuata nini? Si nimekuja kwangu jamani…” Aliniambia huku akinishika akilazimishia kunikumbatia, nilitamani kumsukuma lakini nilishindwa, bila kumgusa nilimuacha anikumbatie anavyotaka. Niliuhisi mwili wake wa moto, ghafla nilikumbuka kipindi chake cha ujauzito, namna nilivyokua napenda mimba yake, namna alivyokua amebadilika na kuwa mke mwema.
“Hapana, wewe una mume wako, nilishakupa talaka, sikutaki tena, mimi nina maisha yangu, nina mtu wangu na nampenda sana.” Nilimuambia, yeye hakujali, aliendelea kunishika, hasira zilinipanda bila kujijua nilijikuta namsukumia pembeni. Alidondoka kwenye kochi na kuanza kupiga keleel.
“Mamaaa! Uaniuaaaa! Unaniuaaaa!” Nilimsukuma kidogo lakini alipiga kelele kana kwamba nilikua nimempiga makofi na mateke. Alianza kulia na kulalamika kuwa nimemuumiza, alilia sana huku akiomba nimpeleke hospitalini. Kwanza nilidhani ananitania lakini baadaye niliona alikua siriasi, alikua kakasirika na alitaka kupelekwa hospitali.
Kwa uoga nikidhani kaumia sana nilimbeba mpaka kwenye gari na kumpeleke hospitalini. Kufika walitaka kumhudumia huku wakitaka kujua nini kilikua kimetokea.
“Mume wangu ndiyo kanipiga, ana mwanamke mwingine, mimi nimemfumania yeye ndiyo akaanza kunipiga, siowezi kutibiwa bila PF3!” Ghafla mke wangu alinigeuka na kuongea maneno ambayo yaliniumiza sana, nilibaki nikiwa nimeduwaa kama mtu aliyechanganyikiwa.
“Nikweli Baba, umemfanya nini mke wako?” Daktari aliniuliza, nikijua kama sijafanya kosa lolote nilimjibu.
“Hapana, mimi sijampiga, tulikua tunabishana nimemsukuma tu kidogo….”
“Hii si kidogo, inaonekana ana hali mbaya na hii ni ishu ya Polisi!” Daktari aliongea, nilikua nimejichanganya mwenyewe kwani nilikubali kumsukuma.
“Mke wangu acha mambo yako! Hujaumia chochote nyanyuka, kama ndiyo unataka nikusamehe namna hii basi umeharibu kabisa!” Nilimuambia mke wangu kwa hasira huku nikijaribu kumnyanyua alipokua amelala, baada ya kunisingizia kuhusu kumpiga na kumuumiza nilijua fika haumwi popote bali alikua anaigisa, sikujua sababu za yeye kufanya hivyo lakini sikutaka kufungwa kwaajili yake, nilikua najua connection aliyokua nayo Polisi hivyo niliona kama nikipelekwa basi itaniharibia sana.
“Ananipiga! Ananipiga! Nisaidieni ataniua!” mke wangu alianza tena kupiga kelele, nilitambua kosa langu na kumuachia, lakini kwakua nilikua nimemuinamia yeye ndiyo akanishika kama ananikumbatia huku akipiga kelele nimuachie. Kuona vile nilimshika kumsukuma pembeni hivyo watu kuanza kuona kama vile nilikua nampiga na kuja kunishika. Watu walijaa na kuanza kunitukana kuwa nampiga mwanamke mjamzito, maneno yalikua mengi, nikashikwa na walinzi na kufungiwa stoo mpaka Polisi walipokuja na kunichukua. Sikujua kilichoendelea mpaka jioni nilipotolewa, Joan alipata taarifa za mimi kukamatwa kwakua alikua akifahamiana na baadhi ya atu akafanya mpango nikaachiwa.
Sikurudi nyumbani siku hiyo, nilienda moja kwa moja kwa Joan na kumuambia kitu kilichotokea. Alinipa pole na kuniambia kuwa atahakikisha ile kesi inapotea, siku iliyofuata nilipigiwa simu kuwa nahitajika Polisi, nilienda na kuambiwa kuwa mke wangu kaamua kufuta kesi ila natakiwa kurudi ustawa wa jamii kuongea na kama hatutaelewana basi kesi itaendelea, mke wangu alisema kanisamehe lakini nikaonywa kuwa kama nikipiga tena basi nitaozea jela. Tulienda ustawi wa jamii nikaeleza ya kwangu na mke wangu naye akaeleza ya kwake.
Alisema nilimrudisha kwao bila sababu yoyote, nikamfukuza na mimba yake huku mimi nikiondoka na kuishi na mwanamke mwingine ambaye ana mimba yangu. Niliulizwa na kukataa nikawaambia kilichotokea kuhusu mke wangu kutaka kuolewa na mwanaume mwingine na kujipa talaka mwenyewe. Niliulizwa ushahidi sikua nao nikaulizwa kama kweli nina mwanamke mwingine nikakubali lakini nikiwaambia yeye ndiyo aliondoka kwanza. Tulibishana sana ikaamriwa kuwa turudi nyumbani na kuishi kama mke na mume, nilikataa na kuwaambia kuwa kwa mambo aliyokua kanifanyia mke wangu basi siwezi kuishi naye na nitakachotoa ni talaka tu.
“Hata ukinipa talaka mimi siwezi kuondoka kwangu, siwezi kwenda kwangu na watoto wawili, yule mwingine nimemuachia Mama kwakua hutaki kumtunza, hujui mwanao anakula nini? Analala wapi? Akiumwa wala hujali! Hapana siwezi kuondoka, kama umenichoka basi utaondoka wewe lakini sio mimi!” Mke wangu aliondoka, ulizika ubishi sana lakini mwisho mimi ndiyo nilionekana kama nina tatizo na kuambiwa kama nina mwanamke mwingine basi niondoke mimi na mke wangu akashauriwa kunichukulia RB ili nisije kumsumbua kwani nilishampiga hapo mwanzo.
Sikutaka kubishana sana, niliondoka, nikachukua vitu vyangu na kuhamia kwa Joan. Mke wangu aliendelea kunisumbua kila siku kuniomba misamaha na kutaka turudiane lakini nilikataa katakata. Mpaka alipojifungua nilikua sina mawasiliano naye, sikurudi tena nyumbani na baadaye Joan naye alijifungua. Maisha yalikua ya amani kwa Joan, alipoenda uzazi kwao nilichukua hiyo nafasi kwenda kujitambulisha na kutoa mahari, nilishafanya maamuzi ya kumuoa Joan, nilishajiandaa kumpa mke wangu talaka na nilikua tayari kumuachia hata mali zote.
Mke wangu hakurudi kwa mapenzi, baada ya mimi kumfuata mchumba wake kazini na mke wangu kumshawishi kuwa mimi ni X wake mchumba wake alikua tayari kumuoa. Lakini kumbe yule mwanaume Mama yake naye ni mtu wa Tanga, ingawa alikua hajuani na mke wangu wala kuijua familia yake lakini wakati wanaenda ukweni kila kitu kishakamilika alikutana na Shangazi yake na mke wangu ambaye alisoma naye, yeye ndiyo alimpa ubuyu wote akimshangaa kwanini mtoto wake alikubalia kuoa mwanamke ambaye tayari ana ndoa mbili na watoto wawili.
Mama yake alimuuliza mwanae ambaye hakuonekana kujali, alionekana kujua lakini hakujali. Kile kitu kilimuumiza sana yule Mama hivyo akaanza kuhangaika kivyake mpaka wakaachana kabla ya kufunga ndoa. Mwanaume alizindika na kumkataa katakata mtoto, baada ya kuona kule kakataliwa ndiyo aliamua kuja kwangu akidai kuwa mimi bado nilikua sijamuacha kwakua nilikua sijampa talaka. Niliumia zaidi niliposikia habari hizo kwani nilijua fika kuwa mke wangu hakurudi kwangu kwa mapenzi au kwakua kanikumbuka bali alirudi kwakua ameachika huko kwingine hivyo nilijua hata kama nikirudisha moyo na kumrudia basi ipo siku anaweza kunigeuka.
****
Siku zote mke angu alijua kuwa ananidhibiti, hakujua kuwa nina ubavu wa kumuacha. Hata baada ya kusikia kuwa nataka kumuoa Joan alikua akiamini kuwa ni hasira tu, alikua anaamini kuwa nataka kumuumiza hivyo akili zangu zikinirudia basi nitarudi kwake. Lakini kwakina Joan ni watu wa dini sana, walikataa kunipokea kwakua mimi nimuislamu, kwakua nilishachoka kuumizwa na Joan ndiyo mtu pakee niliona kama ananielewa basi nilikubali kubadilisha dini. Nilibadili dini na kuwa muikristo, ndugu zangu hawakua na shida sana kwani si watu wa duni.
Haikua na tatizo kwangu kwakua Baba mwenyewe alikua muikristo lakini akabadilisha dini kwasababu ya Mama. Mke wangu aliposikia nimebadilisha dini alichanganyikiwa, alijua fika nimemuacha kwani hata kama nilikua sijampa talaka lakini kwa sheria za kiislamu mtu mmoja anapobadilisha dini inamaanisha ndoa inakua imekufa. Alihaha sana, ndugu zake walianza kunipigia, kuniomba msamaha, vitisho na mambo kibao lakini sikujali, nilishaamua kumuoa Joan na hakuna mtu ambaye ningeruhusu kuingilia chochote.
Baada ya utambulisho nilirudi ili kujipanga, lakini siku moja Joan alikuja nyumbani, alikua kanyong’onyea sana, nilimuuliza kwanini akaniambia kuwa alikua anataka kuacha kazi. Nilimuuliza sababu akaniambia kachoka tu lakini anataka kaucha kazi ila anaogopa kwakua kuna watu wanataka kumfanyia fitina. Alinichanganya sana kwania subuhi yake wakati anaondoka alikua vizuri tu, nilijaribu kumpeleleza ndipo akaniambia kuwa alikua kapandishwa cheo na kahamishiwa kikazi Kigoma.
Kwanza nilifurahi kusikia kapandishwa cheo, lakini nilipokuja kutafakari na kusikia neno Kigoma basi nilichangayikiwa.
“Wananiambia nilazima niende, ni kazi maalum, natamanai kuacha kazi lakini unajua kuwa kazi za jeshi, unaweza hata kushitakiwa kwani cheo cheo chenyewe kimekaa kifigisu figisu.” Nilimuuliza ni lini anatakiwa kuondoka aliniambia kesho yake.
“Hii barua nilipewa tangu mwezi uliopita, ilitaka kupambana ili nisiende lakini kuna mzee jana kaniita akaniambia kuwa niende tu kwani hata huku kuhamishwa ni watu wamenipambania, nilishachomewa TAKUKURU hivyo nibora kuondoka.”
Nilimsikiliza kwa makini na baada ya kusikia ishu yake nilimuambia ni bora kuondoka kwani mimi nampenda na kama ni ishu ya kuoana basi ipo pale pale.
“Kigoma sio mbali, ni hapahapa Tanzania, naweza kuja kila mwezi, wewe nenda mambo yakikaa sawa basi tutajua chakufaya.” Nilimuambia huku nikimpa moyo, hata mimi nilikua nimechanganyikiwa, nilikua sijui nini chakufanya kuweza kuokoa mapenzi yetu. Nilishaanza kuwa na amani, nilishaanza kuwa na mwanamke anayenipenda na kunijali na sasa alikua anaondoka, kwa wakati huo shata sikujua sababu ilikua ni nini, nilihisi ni mambo yao ya kazini wamechomeana na sikutaka kuingilia.
Siku iliyofuata kweli Joan aliondoka, niliumia sana kwani nilikua nampenda na sikujua sababu ya yeye kuondoka. Lakini kama wiki mbili baadaye nilipigiwa simu, mke wangu alikua kalazwa hospitalini na nilitakiwa kwenda. Muda ulikua umepita tangu mimi kuwasiliana naye lakini kwakua sikua na kitu cha kufanya kutokana na upweke wa kuondoka kwa Joan niliamua kwenda, nilimkuta kweli anaumwa, alikua amedondoka na kutenguka mguu. Mama yake alikuepo kumbe baada ya kumuachia nyumba Mama yake na mdogo wake wakika walikuja kuishi pale.
Niliwasalmia vizuri tu, baada ya salamu na kuona yuko sawa niliondoka zangu. Usiku alinitumia meseji.
“Inamaana huwezi kusamehe, hata watoto wako hutaki kuwaona?” Aliniuliza, sikuijibu ile meseji mpaka kesho yake.
“Waao wanakukumbuka, unatakiwa kuja kutoa jina la mtoto wako mdogo, jina la dini tumempa ila wewe kama Baba yake unatakiwa kutoa jina la ukoo.” Meseji ilitumwa, nilikasirika kwani nilijua ni kama dhihaka, nilijua kabisa mtoto si wangu kwani kipindi anapata ujauzito nilikua sishirikini kabisa kimwili na mke wangu.
“Naomba usinichokonoe kabisa! Unajua kabisa kuwa mtoto si wangu hivyo usinichore!”
Nilimjibu, mke wangu alikaa kimya hakunijibu tena mpaka baad aya kama wiki moja tu. Alinipigia simu na kuniambia mtoto wangu anaumwa hivyo anahitaji niende kumuona, alikua nyumbani. Nikweli nilikua na muda sana sijamuona mtoto wangu, tangu nilipoondoka Tanga kipindi kile nilikua sijamuona. Pamoja na hasira za mume wangu lakini nilikua na hamu ya kumuona mwanangu na nilijua isingekua haki kumtelekeza mwanangu kwasababu ya mke wangu. Nilienda kumuona, ingawa alikua mdogo lakini alinitambua, alinikumbatia na kuniita Baba.
Nilifurahi sana, raha ambayo niliipata nilikua sijawahi kuipata kabla, tangu siku ile nilijikuta kila siku jioni naenda kumuona mtoto wangu, walinipokea vizuri na kila siku mke wangu alikia akiniomba msamaha ili tududiane lakini sikukubali. Akili yangu bado ilikua kwa Joan na kila siku tulikua tukiwasiliana ingawa yeye kazi zilikua zikimbana kuja kufunga ndoa. Siku moja nilikua nyumbani kwangu ambapo alikua akiishi mke wangu na ndugu zake, Mama yake alikua kaondoka kaenda Tanga.
Nilishazoea kwenda kila siku na kwa namna flani nilikua afurahia, nilikua nacheza na watoto, hata mtoto wake naye nilianza kumpenda kwani naye alinipenda, mara nyingi nikiwepo alikua akinililia na nikimlisha alikua anakula vizuri. Tofauti na siku nyingine ambapo mke wangu alikua akinisisitiza kulala siku ile ni kama alikua anataka niondoke. Kila dakika alikua akiniuliza kama naondoka saa gapi, mara akimuambia mdogo wake mchukue mtoto shemeji yako awahi nyumbani, mara akisema usiku umeingia nataka kulala.
Sikujua sababu lakini ile hali ilinishangaza na kwa kisi kikubwa ni kama alikua ananiambia subiri usiondoke. Nilikaa mpaka saa nne usiku, mke wangu alionekana kuwa na wasiwasi sana, alikua na mawazo sana mpaka nikamshitukia. Nilipomuuliza aliniambia hajisikiivizuri aataaka kulala, niliona hamna shida ngoja niondoke, nilinyanyuka kutoka lakini ile nafika getini nilikutana na yule mchumba wake wa zamani. Yule mwanaume ambaye alitaka kumuoa, kabla sijamuuliza chochote yule kijana alinivamia na kuanza kunipiga, alinidondosha chini na kuanza kunipiga hukua kinitukana.
“Kama mwanamke kakuacha kubali! Nasikia unamtishia mtoto wangu nitauja kukuua! Mshenzi mkubwa wewe! Nakuambia kuwa nitakuua! Mwanaume gani unapiga mwanamke!” Aliendelea kunipiga huku akitukana, alionekana mwenye hasira mtu aliyeumizwa, mke wangu alikua pembeni akilia tu huku akimsihi aniache lakini hakuniacha. Alinipiga sana, si kwamba alikua na mwili mkubwa hapana lakini kwakua alinivamia mimi sijajiandaa aliweza kunidhibiti, alinisukuma mpaka nnje na yeye kuingia ndani.
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SEHEMU YA NANE
Nikiwa pale chini nilijifanya kuchoka, nilijifanya kuumia ili kukusanya nguvu, alizubaa kidogo nikafanikiwa kunyanyuka, nilimsukuma na kuanza kulipoa kisasi, nilimpiga sana mpaka mke wangu alipoingilia na kunishika ndipo nilimuachia.
“Anafanya nini hapa huyu mpumbavu?” Yule kijana aliuliza, bado alikua chini anaugulia maumivu huku na mimi nikiwa nimesimama lakini nikiugulia maumivu yangu.
“Hapa nikwake, huyu ni mume wangu, wewe si uliamua kumsikiliza Mama yako na kuniacha, sikutaki nimemrudia mume wangu na huyu mtoto ni wakwake!”
Mke wangu aliongea huku akinikumbatia, alinishika shika ili kumpa wivu na mimi bila kujali kama nilikua natumika au la nilimkumbatia mke wangu na kuanza kumla mate.
“Hakuna, kitu kama hicho! Nimekugharamia sana huwezi kuniacha kirahisi rahisi namna hiyo! Nimekuambia kama unataka kuishi kwaamani basi utaendelea kuwa mwanamke wangu! mimi nakupenda wewe na siwezi kuruhusu mtoto wangu kupewa mwanaume mwingine hata kama nikiwa maiti Mama yangu atamlea!” Yule kijana alilalamika akiwa bado pale chini, nilimpiga vizuri na alionekana kuumia sana.
“Unaona akili zako sasa, mwanaume gani kila kitu ni Mama! Mama! Mamma! Uajiona mwanaume kweli, hivi huwezi kuwa na maamuzi yako mpaka kumshurikisha Mama yako! Unasema nimekuacha wakati Mama yako kakuozesha na mwanamke ili tu usiwe na mimi! Kwanini unahangaika na mimi, si una kimwanamke chako umepewa na Mama yako, kamfuate basi! Pesa zako lakini kutumia mpaka Mama yako. Nimekuambia uninunilie gari lakini eti mpaka Mama yako akumbie, uensema mtoto wako hujui anakula nini? Analala wapi? Wanaume wenzako wanakusaidia kulea wewe umekaa na Mama tu kupanga maujinga yenu, sikutaki! Nisharudiana na mume wangu na kwa taarifa yako hata talaka hakunipa basi!”
Mke wangu aliongea kwa kujiamini, wakati wote huo alikua kanikumbatia na ndipo niligundua kuwa kumbe bado jamaa alikua anampenda lakini tatizo lilikua ni Mama yake.
“Nimekupa vitu vingapi, nimekupa pesa kiasi gani wewe unakula na Mama yako! Mbona mimi sisemi kuhusu mambo mnayofanya na Mama yako! Yule ni Mama ana nafasi yake lakini haimaanishi kwamba kwakua kaseam tuachane ndiyo nikuache kabisa, hapana mimi bado nakupenda na una mtoto wangu, kama ni gari nimekuambia subiri mambo yapoepoe, kuna hela nakusanya nitakununulia, sitaki mwanangu ateseke lakini siwezi kukununulia kama bado utaendelea kuwa na huyu mshenzi!”
“Sio mshenzi ni mume wangu tena mheshimu sana! Mwenzako anajielewa hana umama mama kama wewe!”
“Hana Umama mama, kwahiyo mwanaume kukupiga ndiyo unaona uanaume, unataka na mimi niwe nkaupiga, nakunyima chakula, niwe malaya na kukutukana kila siku ndiyo utaniona sina umama!” Aliongea akimaanisha mimi ndiyo nilikua namfanyia mke wangu hayo mambo, nilimuangalia mke wangu mpaka akaona aibu, alionekana kunisema maneno mengi mabaya.
“Bwanaeee! Ondoka, hii ni nyumba yangu na huyu ni mke wangu, sijampa talaka na kama ni gari mimi mwenyewe nina uwezo wa kumnunulia, ondoka!”
Baada ya kuona wananizingua niliamua kumtolea uvivu, nilimfukuza yule kijana na kufunga geti, nikiwa ndani mke wangu alianza kuniomba msamaha, aliniambia ananipenda na alikua anafanya yote hayo kwakua mimi nilibadilika.
“Unakumbuka kipindi kile ulipoanza na yule mwanamke wako, mimi niliona kabisa utaniacha ndiyo maana nikaamua kutafuta mwanaume mwingine. Si unajua kuwa mimi siwezi kuwa peke yangu sasa ukawa unachelewa kurudi na mimi nikapitiwa, lakini nakupenda na siwezi kuishi bila wewe! Unaona huyu kaka kila siku ananisumbua, anasema ananitaka lakini mimi nishakuchagua wewe siwezi kukuacha.”
Mke wngu aliongea huku akilia, alilia sana hukua kinikuumbatia, aliniomba usiku ule kulala pale. Kwakua sikua na chakufanya nyumbani nilijikuta namkubalia, tulilala na kujikuta tunafanya mapenzi, nilijikuta naendelea kuja kulala nyumbani mpaka tukarudiana, nikarudisha chumba na kuhama kabisa. Nilimrudia mke wangu kimya kimya bila kumuambia mtu yeyopte, mwanzo niliona aibu kwani karibu kila mtu alikua anajua kuwa aliniacha na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine lakini baadaye sikujali, yalikua ni maisha yangu nilirudiana na mke wangu huku nikiamini kuwa atabadilika na kuwa mke bora.
Katika kipindi chote hicho mke wangu alikua ni Mama wa nyumbani, alikua si mtu wa kutaka kufanya Biashara ingawa mara nyingi nilishamtafutia Biashara na kumpa mtaji lakini aliishia kuula. Ila baada ya kurudiana ghalfa alianza kuniambia kuwa kachoka kuwa Mama wa nyumbani anataka kitu cha kufanya. Mwanzo niliona kama ni utani na kudhani kuwa kama nikimpa mtaji basi nitapoteza pesa zangu lakini kadri siku zilivyokua zinaenda ndipo nilimuona kama yupo siriasi na Biashara.
Aliniambia kuwa anataka kufanya Biashara ya Dagaa wa mwanza, alianiambia kuwa kuna rafiki yake anafanya Biashara ya namna hiyo hivyo kama nikimpa mtaji wa milioni moja basi anaweza kuifanya hiyo Biashara vizuri. Tatizo langu likawa ni kusafiri, kwa nilivyokua namfahamu mke wangu nilimuonea wivu sana kama angesafiri, tabia zake zilinitia shaaka. Nilikataa na kumuambia abadilishe Biashara kwani mtoto bado ni mdogo hivyo hawezi kusafiri na kama ni kutafuta Biashara basi atafute Biashara ambayo si ya kusafiri. Tofauti na kawaida yake ambayo anakua mbishi sana alikubali na kufungua duka la nguo.
Nilimpa mtaji wa milioni mbili pamoja na kumlipia fremu, Biashara ilianza taratibu lakini ghafla niliona inapanuka, mtaji unakua mkubwa na mke wangu anakua bize sana na kazi. Mwanzo nilifurahia lakini siku moja nilimfuata dukani, ilikua ni jioni na nilienda kumchukua ili kurudi naye. Sikumkuta dukani, duka lilikua limefungwa, nilimpigia simu ili kujua yuko wapi lakini simu ilikua haipokelewi, ilikua inaita tu. Nikiwa nimesimama pale nimeshikilia simu kuna dada mmoja wa duka la jirani, nilimsogelea na kumuuliza alipokua mke wangu.
“Mbona huyo muda wake wa kufungua bado…” Yule dada aliniambia, kwanza nilishangaa kwani ilikua kama saa kumi na moja na nusu za jioni, mara nyingi dukani mke wangu hufungua saa mbili za asubuhi na karibu kila siku saa moja jioni naenda kumchukua kasoro siku ile ndiyo nilikua nimewahi kwenda.
“Unasemaje?” Nilimuuliza kwa mshangao.
“Namuulizia mke wangu unasema sio muda wake wa kufungua, unamaanisha kufungua au kufunga.” Dada kwanza alicheka kwa dharau, alikaa kimbeambea na nilijua kuna kitu alitaka kuniambia ni kama alikua anasira, nilimkazia macho kumuonyesha kuwa nilikua siriasi.
“Huyo Dada hafungui duka mpaka saa moja kasoro na saa moja ukija kumchukua anafunga, hata hakai nusu saa dukani lakini kila siku ni mzigo mpya.” Aliongea, nikiwa hata sijajua cha kumjibu kuna gari flani VX ilisimama pembeni, ilikua na Vioo vyeusi sikuweza kuona waliokua ndani.
“Ndiyo huyo analetwa kufungua duka…” Yule dada aliongea lakini ile gari haikusimama muda mrefu, iliondoka kwa mwendo wa kasi. Nilibaki namuangalia yule dada ambaye naye hakua na chakuseama, nilimuona mmbea tu nikarudi upande wa dukani kwa mke wangu kumsubiri nikijua kabisa atakua katoka mara moja.
“Niko nyumbani mume wangu, sijisikii vizuri kabisa leo nimefunga mapema.” Ujumbe mfupi kwenye simu yangu uliingia. Nililazimika kunyanyuka taratibu nikaingia kwenye gari na kwenda nyumbani. Nilimkuta mke wangu kalala na nilipojaribu kumsemesha alijifanya kuchoka, sikuongea chochote, niliamua kunyamaza huku nikijipanga kumchunguza. Kama wiki moja hivi nilikua nikivizia nyakati za mchana nakuja kumuangalia dukani, nilikuta amefungua na kuona kuwa labda yule jirani alikua kanidanganya, lakini kumbe ni kama alishtukia kwani baada ya hapo kila nikienda dukani kwake nilikuta kumefungwa.
Nilienda kwa zaidi ya mwezi kila siku mchana kumefungwa lakini jioni nakuta kumefunguliwa, roho iliniuma nikiwaza mke wangu alikua akienda wapi? Sikua na jibu, siku moja asubuhi nilimuaga kuwa naenda kazini, niliondoka lakini baadaye nilirudi nyumbani kwa mguu, nilivizia mpaka ule muda mke wangu anaondoka kwenda dukani na kuanza kumfuata nyuma. Kutoka nyumbani mpaka dukani ulikua ni mwendo wa kama dakika kumi kwa Gari, alichukua Bajaji na mimi nikachukua, nikamfuatilia, hakwenda dukani kweake bali alishika njia nyingine.
Aliondoka mpaka mtaa kama wa tatu hivi, alifika na kushuka, nikidhani labda anaenda nyumbani kwa mwanaume niliona anafungua duka jingine. Lilikua duka la nguo pia lakini kubwa kuliko duka nililokua nimemfungulia yeye. Lilikua kubwa zaidi ya kama mara tatu hivi, aliingia na kuanza kuuza, nilijikuta nakaa pale mpaka mchana nikimuangalia, nilikua nimejibanza katika baa flani jirani nakunywa soda, mchana lile gari ambalo lilipita siku ile na kusimama kisha kuondoka lilifika pale, lilisimama na akashuka baba mmoja mtu mzima, aliingia dukani kwa mke wangu.
Alisimama kwa muda upande wa wateja kisha akaingia kwa ndani sikumuona tena. Nilishikwa na hasira, wivu ulinijaa, kichwani nilikua na maswali mengi, nilitamani sana kwenda kufanya vurugu lakini nilijua kuwa haiwezi kusaidia. Nilijikuta naondoka bila kufanya chochote, jioni kama kawaida mke wangu alikuja dukani, akafungua na mimi nilipoenda nilimchukua. Nilimuuliza kuhusu siku yake alishukuru kuwa Biashara nzuri tukaenda nyumbani, kwake kila kitu kilikua kama kawaida, kama vile hakuna kitu kimetokea, wakati mimi nikichanganyikiwa kwa mawazo yeye alijaribu kuchangamka kama vile hakuna kitu kimetokea.
Siku iliyofauata nilienda kazini, lakini mchana nilishindwa kuvumilia, nilimfuata mke wangu mpaka kwenye duka lake jipya. Alishangaa sana kuniona sehemu ile, alikua peke yake.
“Unafanya nini hapa? Inamaana unanifuatilia?” Aliniuliza kwa wasiwasi, alikua akiangalia saa mara kwa mara, mwanzo nilihisi kuwa ule wasiwasi ulikua ni kutokana na mimi kugundua anayoyafanya lakini mwisho nilikuja kujua kuwa kumbe hata alikua hajali kama mimi niko pale au la, alikua akiwaza mtu wake.
“Ondoka, nitakuelezea kila kitu nikifika nyumbani, naomba usipaniki kwani utaniharibia! Sio kama unavyofikiria, sikusaliti, naapa nitakuambia ukweli!”
Aliongea kwa wasiwasi, nilimuangalia kwa hasira bila kusema chochote, niliomuona anatetemaka kabisa kwa uoga.
“Rama ondoka Pleassseee! Utaniharibia kwakweli, kuna ishu ya maana nafuatilia, naomba ondoka….” Aliongea huku bado akiangalia saa, nilijua ule ulikua ni muda wa jamaa yake kuja, sikutaka kuondoka, nilitaka aje anikute pale nimuone tuonane nione mke wangu atafanya nini. Nliingia ndani na kuanza kuchagua chagua nguo, kweli haukupita muda yule Baba alikuja, nilimuona kwa karibu alikua ni mtu ambaye namfahamu, mtu mkubwa tu na cheo chake, nilimfahamu kutokanja na umaarufu wake.
Alinisalimia vizuri lakini kwakua ni mtu na familia yake alijifanya kuchagua nguo na kuondoka, mwanzo nilihisi labda kaniheshimu anajua kuwa mimi ni mume wa mchepuko wake lakini baadaye ndipo nilipojua kuwa kilichomuondoa nikwakua alikua ni mume wa mtu na ana cheo kikubwa serikalini hivyo hakutaka kuonekana kama anacheuka na hakua akinijua.
“Umeona sasa, ungeniharibia? Hivi unajua kuwa huyo ni nani?” Mke wangu aliniuliza baada ya kuondoka.
“Namjua sana, lakini sijui ni kwanini unamuogopa na wewe unafanya nini hapa wakati duka lako liko kule?” Nilimuuliza na kumfuata kutaka kumpiga.
“Nilishakuambia kuwa mimi sipigwi na mwanaume, nitakufunga na kama umenichoka unanirudisha kwetu, hii ni Biashara ya watu ukileta vurugu siwezi kukutetea!” Mke wangu aliongea kwa hasira.
“Biashara ya nani?” Nilimuuliza, bado nilikua na kimuhemuhe cha hasira.
“Nitakuambia lakini utulie, wewe najua una wivu na una haki ya kuwa na wivu, ila sasa hivi nikuambie kuwa sifanyi kitu kibaya kabisa, mimi hii ni Biashara tu lakini hakuna kitu kibaya.” Aliniambia, nilimuomba aniambie pale lakini aligoma, aliniambia kuwa niondoke mpaka jioni atakuja kuniambia kila kitu, nilitamani kujua kila kitu kwa wakati huo lakini aligoma kabisa kabisa kuniambia, sikua na namna zaidi ya kuondoka na mawazo yangu.
“Yule Baba alikua ni X wangu wa zamani, nimekutana naye nikamuambia kuwa nina shida ndiyoa kanifungulia lile duka, sasa unafikiri mimi ningekataa, alinipa mtaji wa milioni 15, kaninunulia kiwanja na wala sitembei naye!” Mke wangu aliniambia, ulikua ni usiku ndiyo kwanza karudi, kwa namna alivyokua anaongea ni kama kilikua kitu cha kawaida sana kwake. Nilimuangalia huku nikitetemeka kwa hasira, nilikasirika kiasi kwamba machozi yalianza kunitoka.
“Unakasirika nini? Mwanaume mwenyewe ana sukari, tangu zamani hata kipindi niko naye alikua hawezi fanya chochote, nilimuacha mimi sasa hivi ananisaidia tu…”
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SEHEMU YA TISA
“Sitaki urudi katika lile duka?” Nilimuambia mke wangu, aliniangalia kwa dharau hukua kicheka.
“Una akili kweli wewe? kwakipi unachonipa hasa? Huwezi kunipangia maisha yangu kama ambavyo mimi siwezi kukupangia maisha yako! Wewe sib ado uaendelea kuwasiliana na kile ki mwanamke chako? Au unafikiri mimi sijui?” Nilinyamaza kimya kwa muda nikiwaza nini chakumuambia, nilikua nimekasirika sana lakini nilijizuia nisimpige.
“Kimwanamke gani? Mimi yule ni Mama wa mtoto wangu, siwezi kuacha kuwasiliana naye?”
“Una uhakika gani kuwa na mimi yule si Baba wa mtoto wangu? au kwakua unaona ana sukari ukadhani kuwa hana uanaume?”
Aliniuliza kwa dharau, hapo nilipata kanafasi ka kumuuliza mke wangu kuhusu yule mtoto wake wa kwanza, yule ambaye alinidanganya kuwa ni mtoto wa mdogo wake. Nilikua bado sijapata jibu la uhakika, mke wangu alikua hajamkataa wala kumkubali ingawa alishamleta pale nyumbani na alikua akimuita Mama ila kila nilipotaka kuongea naye alikwepa, siku nyingine aliniambia kuwa ni mwanae lakini nikimbana sana anasema amemlea hivyo anamuona kama mtoto wake. Hakukubali kuwa alishaolewa zaidi ya kusema “Nilikua nikiishi na Malaya mmoja akahisi kanioa ila mimi sikumchukulia kama mume.”
“Umeshaanza ujinga wako, mimi awe ni mwanangu au si mwanangu wewe inakuhusu nini? Nimepungukiwa nini kama nilizaa kabla, mbona wewe una mtoto na mwanamke mwingine lakini silalamiki, au unataka mpaka tuwekeane masharti ya kulea watoto wetu?”
“Hapana lakini nataka kujua, wewe ndiyo umeianzisha hii mada, unasema yule Baba anaweza kuwa ni Baba wa mtoto wako, mtoto gani huyo?” Nilimuuliza.
“Sasa kwani kusema ndiyo lazima awe yeye, si nina watoto wawili kwanini usisieme hao au unajihakikishiaje kuwa kuna wakwako hapa?” Aliongea tena kwa dharau, maneno yake yaliniumiza kwani alionyesha kama kusema kuwa mtoto wangu wa kwanza hakua mtoto wangu.
Nilijua hivyo kwakua mtoto wapili nilijua kabisa si wangu, pamoja na kutumia jina langu lakini nilijua kuwa ni wa yule kijana ambaye alitaka kumuoa.
“Unamaanisha nini kusema hivyo?” Nilimuuliza, alionekana kushtuka kidogo, maeno aliyoyaongea hakuyategemea ni kama aliongea kwa hasira.
“Yaishe na wewe, kama ni suala la huyo Baba mimi nuitaachana naye tataribu lakini usinilazimishe kumuacha ghalfa, kanipa vitu vingi sana akininyang’anya unafikiri mimi nitaishije. Tusiwaingize watoto kwenye mambo yetu ya kiutu uzima itakuja kuwa na athari huko baadaye.” Aliongea na kuimaliza kabisa hiyo mada, hata nilipojaribu kuileta alibaki kimya, alijifanya kununa na hakunijibu tena.
Baada ya siku ile mke wangu alibadilika sana, alianza kutoka kwa uhuru kwenda kwa yule mwanaume, aliacha kabisa kwenda kwenye duka nililokua nimemfungulia, mwanzo alilifanya stoo lakini baadaye aliliacha kabisa, alihamishia vitu vyote katika duka alilofunguliwa na yule Baba na kuwa anashinda huko. Alinipiga marufuku kwenda kumuona kule akihofia kuwa yule Baba atajua kuwa bado anaishi na mimi. Alimuambia kuwa nimemuacha na kumptelekezea watoto.
“Akijua hujaniacha atakasirika sana, nibora ajue kuwa nimetelekezwa na watoto, ananisaidia sana kuna kiwanja kaninunulia na anataka kunijengea. Huna haja ya kuwa na wasiwasi, ana Kisukari yule mashine haifanyi kazi!”
Mke wangu aliniambia, pamoja na kuambiwa yote hayo lakini kama mwanaume niliumia sana, nilikua nalia kila siku nikitamani aachane naye lakini wapi. Mke wangu hakua tayari kumuacha yule mwanaume na kila nilipokua nikimuambia kama hivyo ni bora tuachane alikataa, alishuka chini kidogo akiniambia kuwa nimpe muda wa kujipanga amuache taratibu. Alichepuka naye kwa uhuru na baada ya kama miezi sita hivi yule mwanaume alimnunulia gari, ingawa mke wangu alinidanganya kuwa ilitokana na pesa zake za Biashara lakini sikumuamini, nilijua kanunuliwa na mwanaume mwingine na mimi sikua na chakufanya zaidi ya kuvumilia.
Mtu pekee ambaye alikua akinifariji alikua ni Joan, bado tulikua tunawasiliana naye, nilikua sijamuambia kuwa nimesharudiana na mke wangu ingawa alishasikia kwa watu. Hasira zangu zote nilikua nikipeleka kwake, kila nikikorofishana na mke wangu nilikua nikimpigia ili kunifariji na kama akileta mdomo basi naishia kumtukana, tulikua tunagombana sana na kwakua mwishoni aliishia kuomba msamaha yeye basi nilikua naona fahari kidogo na kujihisi mwanaume.
“Nimeshakuambia huyu mwanaume itamuacha, lakini tuna watoto wawili, siwezi kumuacha ghafla namna hiyo, kuna mambo nakamilisha ili nikiachana naye niwachukue wanangu.” Kila siku nilikua nikimuambia hivyo Joan na yeye alikua akikubali.
Pamoja na kupenda kumpigia simu mara kwa mara lakini nilikua nikifanya hivyo kisiri, sikutaka mke wangu kusikia, si kwamba nilikua nikimuogopa sana mke wangu, hapana nilikua nakwepa kelele zake, nilijua kabisa kama akijua nawasiliana kila siku na Joan angekasirika na hata kuniacha. Siku moja Joan alinipigia simu kuwa mtoto wetu anaumwa, alikua kalazwa hospitalini, alikua na hali mbaya na hakua na pesa. Miaka miwili ilikua imepita tangu kutengana na Joan, nilikua sijawahi kwenda kumuona wala kumuona mtoto.
Kuna pesa flani nilikua nayo kama laki nane nilimtumia yote, ilikua ni pes aya ada kwaajli ya mtoto wangu wa kwanza ambaye alikua anakaribia kuanza darasa la kwanza. Niliitoa nikiamini kuwa kuna pesa nyingine nitapata, niliituma yote kwaajili ya matibabu na mambo mengine, ingawa mtoto alikua na Bima lakini kama unavyojua hospitali zetu kama huna pesa kuhudumiwa ni shida, sikutaka mwanangu ateseke. Lakini katika kuituma nilisahau kufuta meseji ya M-Pesa, mke wangu wakati anakagua simu yangu aliiona, usiku aliniuliza ni kwanini nilikua nimemtumia Joan pesa nyingi kiasi kile.
“Si aa mtoto wangu ulitaka nimtelekeze mwanangu!” Nilimjibu kwa hasira, nilikua na mawazo ya mtoto wangu kuumwa hivyo niliona kama ananichulia tu na mikelele yake.
“Nimekuvumilia sana lakini naona unataka kunipanda kichwani, kila siku nakuangalia tu, najua unawasiliana na yule Malaya wako lakini nimekaa kimya kwakua huniathiri chochote, ni ujinga wako kuwasiliana naye lakini sijali. Ila sasa umevuka mipaka, pesa zote unamtumia yeye, mimi nahangaika kutafuta ili kuwekeza kwaajili ya familia yetu wewe unapeleka pesa zote hizo kwa huyo mwanamke, uafikiri mimi siumii, au unaona kama nafurahia?”
“Siko hapa kwaajili ya kukufurahisha, mambo mangapi unafanya mimi siyafurahii lakini navumilia, hatupo hapa kufurahishana, pesa nimetuma na hunifanyi chochote?” Nilimjibu kwa hasira kwani niliona kama ananipanda kichwani.
“Nikuambie kitu naona huyo Joan kakuchanganya sasa kwa taarifa yako naweza kumfanya chochote kile, kama niliweza kumpeleka kigoma hata jela naweza kumpeleka!” Mke wangu aliongea, mwanzo nilikua kama sijamsikia vizuri lakini alirudia tena.
“Kigoma, umanaanisha nini kusema umempeleka Kigoma?” Nilimuuliza kwa mshangao.
“Mimi nikitaka kitu kiwe kinakua, ukitembea na wakubwa hakuna kitu kinashindikana, unafikiri huyo Malaya wako Kigoma nani alimpeleka, sasa ukizidisha ujinga wako na kazi itamshinda huko uone kama huyo mtoto wako atamlea akiwa jela au akiwa hana kazi?”
Nilianza kuunganisha matukio na kujua ni kwanini mke wangu alikua anasema vile, kipindi anataka kunirudia ndicho kipindi Joan ali[pata matatizo na kuhamishwa, nilikua sijawahi kuwaza kama alikua anahusika mpaka siku ile. Kile kitendo kilinikasirisha sana, nilijikuta napata hasira na kumtandika makofi, sikujali chochote, kwa namna nilivyokasirika mke wangu alinywea, alijifanya kutania.
“Hakuna kitu nilikua nakutania, mimi nina nguvu gani ya kumhamisha mtu!” Aliniambia lakini nilikua simuamini tena, nilijikuta napata na hasira mpaka yeye kuniogopa, sijui hata zilitoka wapi lakini niliumia sana kwani angalau nikiwa na Joan nilikua na furaha na nilikua najiona mwanaume kidogo.
***
Kila kitu kilifanyika kimya kimya, mke wangu alikua hanisemeshi, zilikua zimapita wiki mbili tangu kumpiga makofi mke wangu baada ya kuniambia kuwa yeye ndiyo alikua sababu ya kuhamishwa kwa Joan. Alikasirika sana, akawa haongei na mimi, kila kitu alikua anaongea na binti wa kazi, hata pesa za matumizi alikua haniambii, anamuambia binti wa kazi muambie Baba nahitaji kitu flani, muambie mchele umeisha, muambie mtoto anaumwa na mambo mengine. Shughuli nyingine kama mume alikua akinidfanyia lakini kimya kimya, alikua akifua, kupika na kufanya kila kitu kasoro kuongea na mimi
Hali ile ilinichanganya sana, nyumba ilikua haina amani, kulikua hakuna furaha, kuna wakati nilitamani hata kuondoka na kumuacha na ukimya wake lakini nilishindwa, isingekua na maana. Nilitaka kumpigia simu Mama yake kumuambia aongee na mwanae lakini niliona ni kama kujidhalilisha kuwa nimeshindwa kuwa mwanaume na kuitawala nyumba yangu. Nilijitahidi sana kuwahi nyumbani, kutimiza majukumu yangu kama mume, kumnunulia zawadi, kumpa lesa lakini hakujali, alikua kakasirika ana kisirani chake. Muda mwingi aliutumia kuangalia TV na kucheza na watoto, nilijiona mpweke ndani kwangu nilijiona kama mgeni vile.
“Hali hii itaendelea mpaka lini?” Nilimuuliza, ulikua ni usiku tumepanda kitandani nilipojaribu kumshika ili kufanya mapenzi alijiachia aliniruhusu nifanye kila kitu lakini alilala kama Gogo, hakuonyesha ushirikiano wowote.
“Wewe ni mke wangu, utaendelea kuninunia mpaka lini?” Nilimuuliza huku nikimnyanyua kwa nguvu kukalisha.
“Ungekua unatambua thamani ya mke ungenifanyia uliyonifanyia?” aliniuliza, kwa mara ya kwanza baada ya wiki kama tatu hivi alinijibu, nilijua huo ndiyo mwanzo.
“Nimekufanyia nini? Kama ni kukupiga si niemshakuomba msamaha. Kwanini bado uaendeleza vitu…”
“Msamaha wako una maana gani? Hivi ungeniua ungekuja kuomba msamaha kaburi langu?” Aliniuliza, nilinyamaza kimya na kuona kweli alikua na mantiki.
“Lakini uliniudhi,ulinikasirisha sana kumhamisha Joan….” Nilihjaribu kujitetetea lakini ndiyo kama nilipalia mkaa.
“Hicho ndiyo kilichonikera zaidi, kwamba huyo mwanamke wako ni wa muhimu kuliko mimi. Hivi kama unaweza kunipiga kwasababu tu kahamishwa akifa si unaweza kuniua!”
“Uamaanisha nini kusema akifa?” Niliuliza kwa kupaniki zaidi kwani kwa namna alivyokua anaongea ni kama alikua anapanga kumfanyia kitu kibaya, nilikua simuamini sana mke wangu hivyo niliogopa.
“Unaona sasa unavyopaniki? Kwani huyo mwanamke wako hatakufa, unafikiri ataishi milelea? Atakufa kaka sisi wengine lakini nina wasiwasi kama utakuja kumsahau kama hapo Kigoma tu unataka kuniua!” Aliona mshangao wangu na kujaribu kujielezea, bado sikumuamini, nilimuambia nampenda lakini sikufurahishwa na mambo yake, nilimuomba msamaha na kumuambia sitampiga tena.
“Mimi sijali kupigwa bali sababu ya kupigwa! Katika maisha yangu niliapa kuwa siwezi kupigwa nikigombania mwanaume na mwanamke mwenzangu…”
“Kwani nani unamgombania sasa?” Nilimuuliza kwa mshangao.
“Si ni wewe, uko na mimi lakini unahangaika na huyo mwanamke, sasa uchague kati ya mimi na yeye, kama ukiendelea kuwasiliana naye basi mimi naondoka, sitaku umpigie simu, sitaki uwasiliane naye!”
“Lakini ana mtoto wangu, siwezi kumtelekeza mtoto wangu…” Nilijaribu kujitetea, sikuona sawa kabisa kuacha kuwasiliana na Joan.
“Sitaki kusikia, wakati anatembea na wewe alijua kabisa kuwa wewe ni mume wa mtu lakinia kajilegeza mpaka kupata mimba, hiyo mimba ni yake si yako, haituhusu na kama ni mtoto basi si lazima kumpigia simu, unaweza kutuma pesa kwenye M-Pesa na mtoto akalelewa huna hjaja ya kumuona Mama yake au kuongea naye. Ni uchague kayi yangu na huyo mwanamke, mimi siwezi kuchanganywa kama hunipendi uniambie kabisa nijiondokee zangu.” Aliongea kwa hasira, nilimkubalia kuwa nitaacha kuongea na Joan na nitakua nikutuma pesa bila hata kumpigia simu.
Niijua yameiha alitoa simu yake alipiga namba ya simu na kunipa simu.
“Nini? Nani huyo?” Nilimuuliza.
“Huyo mwanamke wako, nataka uongee naye muambie kabisa kuwa humtaki, asikutafute tena uko na mke wako na kama ni matumizi nitakua nikituma mimi na si yeye.” Sijui alipata wapi namba yake lakinia likua tayari ahsampigia Joan, nilisikia Halloo ya upande mwingine. Nilikua sijapanga cha kuongea, nilitaka kukata simu lakinia aliniambia kabisa nichague kati ya yeye na Joan, kama nikikata ndiyo basi mapenzi mimi nayeye. Nilikua nampenda sana mke wangu, nilishindwa kukata simu,niliichukua na kumuambia Joan kila kitu nilichokubaliana na mke wangu, nikaongea naye mbele ya mke wangu kisha niakakata simu.
Joan alinipigia katika simu yangu, mke wangu aliipokea na kuanza kumtukana, alimtukana sana matusi ya nguoni mpaka nikawa nakasirika lakini sina chakufanya. Joan aye alikua akitukana hivyo walianza kutukaana mpaka nikaona aibu nikaondoka nikatoka kwenda kulala sebuleni. Sikurudi ndani mpaka asubuhi yake ambapo mke wangu alitoka kwa hasira, alianza kulalamika kuwa Joan kamtukana sana na ni kosa langu hivyo natakiwa kuchagua kati yake na Joan, nilimuambia nimemchagua yeye ndipo aliniambia kuwa kwa namna alivyotukanwa siku akiniona na wasiliana na Joan basi ndiyo mwisho wa ndoa yetu kwani nitakua nimemdhalilisha sana.
Nililazimika kukubaliana na mke wangu kwani hata nilipomtafuta Joan hakutaka kuongea na mimi, sliishia kuniambia kuwa wewe tunza mwanao sitaki mawasiliano nawe huyo mwanamke wako ni mshenzi sitaki kujihusisha naye. Baada ya hapo hakutaka mawasiliano na mimi, lakini hata mimi nilijitenga naye, sikutaka kumuudhi mke wangu, mwanzo nilikua nikituma pesa nampigia simu kumuuliza kama amezipata au la ila baada ya muda niliacha kumuuliza. Nilimblock kila sehemu na kuwa natuma pesa kwa wakala tu, wakala akinithibitrishia kuwa zimefika basi naridhika maisha yaliendelea.
Mwaka mzima ulipita bila kuwasiliana na Joan, nilianza kuona kama kitu cha kawaida, ndugu zangu walipokua wakiniuliza kuhusiana na mwanangu niliishia kuwaambia kua anaendelea vizuri ingawa nilikua sijui chochote kuhusu yeye. Maisha yalikua ya amani kidogo kitu pekee ambacho kilinitesa ni mke wangu kukataa katakata kuachana na yule Baba akisema hawafanyi kitu kibaya chochote. Niliumia lakini angalau alikua hachepuko na watu wengine, baada ya kuwa na yule Baba mke wangu alikua na heshima debe, alikua si mtu wa kunywa pombe sana kama zamani ingawa bado hakutaka kabisa niende dukani akisema ni sehemu yake ya kazi mbona yeye haji kwangu.
Mwanangu alipofika Darasa la pili mke wangu alilazimishia kumpeleka Bweni, alisema shule aliyokua anasoma si nzuri na anataka kumhamisha. Ingawa sikupenda lakini alilazimishia sana ili kukwepa kelele niliamua kukubali. Alifuatilia uhamishio wa kila kitu na kumpeleka shule nyingine, kila kitu alifanya mwenyewe mimi alinipa tu taarifa. Aliniambia tu kwamba mtoto kampeleka shule flani lakini hakuniambia chochote kingine. Wiki mbili tu baada ya kumpeleka mtoto wetu shule nilienda shuleni kwao, sikupanga lakini kuna mfanyakazi mwenzangu ambaye naye mtoto wake alikua akisoma katika ile shule, alianguka darasani ghafla hivyo alipigiwa simu na mimi ndiyo nilimpeleka.
Kwangu niliona kama fursa ya kumtembelea mwanangu, nilifika na kweli nilimuona mwanangu, aliponiona tu alinikimbilia kunisalimia. Mtoto aliyedondoka alikua anaendelea vizuri lakini Baba yake aliombva kumchukua ili kwenda kumpeleka hospitali kubwa kuchekiwa vizuri. Wakati tunaondoka mtoto wangu alining’ang’ania na kutaka tuondoke wote, niliwafuata walimu kumuombea na kutaka kwenda naye ntamrudisha jioni.
“Hapana huruhusiwi kumchukua, hata kama ni ndugu lakini mtu aliyeandikwa hapa ndiyo anaruhusiwa, Baba yake au Mama yake.” Mwalimu aliniambia, kwakua nilikua sijawhai kufika pale niliwaelewesha kuwa mimi ndiyo Baba yake.
Aliniomba kitambulisho changu ili kuangalia jina, nilikitoa bila wasiwasi wowote.
“Hapana, mbona jina la Baba na hata picha sio wewe. Anahtajika Baba mzazi si Baba mdogo au Baba mkubwa.” Mwalimu aliniambia, niliwaka kidogo mpaka akanionyesha kwenye Mfumo wao jina la Mama lilikua la mke wangu pamoja na Picha yake. Lakini jina la baba na picha havikua vyangu kabisa.
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SEHEMU YA KUMI
Walinigomea kabisa kumchukua mtoto, mwanangu alikua akinililia na kutaka kuondoka na mimi, ili kuepusha aibu niliamua kumuacha mtoto. Hata rafiki yangu aliponiuliza nilimuambi hamna kitu. nilimchukua rafiki yangu na mwanaeo tukaondoka pale shuleni. Akili haikua pale kabisa, nilikua na mawazo mengi, nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa hata njia nilikua siioni vizuri.
“Vipi mbona hivyo?” Rafiki y angu aliniuliza.
“Hapana, hamna kitu nipo sawa sema kichwa naona kama kinaniuma, ghafla tu nasikia kizunguzungu. Hembu endesha gtari ni drop nyumbani, sijisikii vizuri kabisa.” Nilimuambia huku nikipaki gari pembeni, kwa namna nilivyokua ikijisikia nilijua naweza kudondosha gari, sikua sawa kabisa.
Alichukua gari na kuniacha nyumbani, kwakua yeye gari yake aliacha ofisini aliondoka na gari yangu. niliingia ndani mpaka chumbani, nikaingia kwenye kabati la mke wangu na kwenda kwenye briefcase yake moja ambayo alikua ameifunga, ni zile za kufunga na namba na kila siku nilikua nikiiheshimu, alikua hapendi niguse vitu vyake hivyo nilimheshimu kwani nilijua kama nikigusa inakua ni kelele na mimi huwa sipendi kugombana naye sana. Sikuhiyo sikujali chochote, nilishachoka na nilitaka kujua ukweli, nilijua kabisa kuwa kama nikifungua pakle nitakutana na kila kitu.
Nilitafuta kisu na kufungua huku nikiharibu kabisa ile sehemu ya kufungulia. Kulikua na document nyingi tu, nilianza kutafuta vyeti vya watoto. Kulikua na vyeti vya watoto vyakuzaliwa vitatu, vilikua original kabisa. Cha kwaza kilikua ni cha yule mtoto wake wakwanza ambaye mimi aliniambia kua ni mtoto wa mdogo wake. Cha pili kilikua ni cha mwanangu wa kwanza na chatatu kilikua ni cha mtoto wake ambaye alizaa kipindi aataka kuniacha. Cha ajabu vyote vilikua na majina ya yule Baba, hakuna hata kimoja kilikua na jina langu wala la yule kijana na vyote yeye ndiyo alikua Mama.
Nilishangaa kwakua cheti cha kuzaliwa cha mwanangu ambacho nacho kilikua ni original nilikua nacho mimi na cha yule mtoto wa pili nacho nilikua nacho na aliniandika mimi ingawa nilijua kabisa kuwa si mwanangu. Nilitafuta tafuta na kukuta tena cheti kingine cha mtoto wake wa tatu ambacho kilikua na jina la Baba la yule ambaye alitaka kuoana naye ikimaanisha kuwa huyo mtoto alikua na vyeti vtatu, vyote original ila kila kimoja na Baba yake. Nilikutana na hati mbili za nyumba ambazo zina jina lake, ni nyumba ambazo mimi nilikua sizijui na pia nilikuta cheti cha ndoa ambapo jina lilikua la yule mtu ambaye nilitajiwa mwanzo kuwa alishawahi kumuoa.
Niliishiwa pozi kabisa, kulikua na vitu vingine vingine lakini sikuvijali sana. Nilitaka kukaa kumsubiri mpaka arudi lakini nilishindwa, niliamua kwenda kumfuata dukani. Aliponiona alishangaa, alishanikataza kwenda dukani hivyo aliwaka sana na kuanza kuniambia niondoke.
“Leo nimeenda kumuangalia mtoto shuleni…” Nilimuambia.
“Mtoto? Mtotop gani?” Aliuliza huku bado akinisukuma ili niondoke. Sikuondoka, niliingia ndani na kukaa.
“Mtoto gani? Kwani una watoto wangapi wanasoma, nimeenda shuleni kwa mtoto wetu lakini cha ajabu nilitaka kumchukua nikaambiwa mimi si Baba yake?” Nilimuambia lakini hakuonekana kabisa kushtuka.
“Hayo ni mambo ya kuzugumzia nyumbai!” Aliongea huku bado akinisukuma, nilishangaa ni kwanini alikua hata hashituki.
“Mbona unaongea kirahisi namna hiyo, unajua kuwa nimeumia sana, nimeenda mpaka nyumbani kwenye begi lako nakuta vitu vya ajabu.”
“Begi langu? Hivi wewe una akili kweli, kwanii unaenda kupekua vitu vyangu? Umechukua nini? Hivi mimi nakaguaga vitu vyako, kwanini hukuja kuuliza kwanza kabla ya kuingilia mambo yangu! umenikara sana, ushaniharibia siku yangu!” Aliongea kwa hasira, sasa alionekana kupaniki kabisa aliposikia kuwa nimekagua vitu vyake. Alitoa simu yake na kupiga namba flani.
“Naomba usije leo, sisikiii vizuri naenda nyumbani.” Aliongea na mtu kwenye simu.
“Hapana siumwi! Sijisikii tu vizuri!” Aliendelea kuongea kwa asauti ya juu, walikua kama wanabishana.,
“Hapana, nsihakuambia huwezi kuja nyumbani kwangu, naishi na Mama yangu unafikiri Mama yangu akijua kuwa natembea na mume wa mtu! Nilishaambiwa nikuache mimi ndiyo king’anganizi, sitaki kumuua Mama yangu kwa mapresha yeye ni mtu wa dini! Nishasema usije, si umwi sana naenda tu kulala basi!” Aliongea kwa hasira na kukata simu, bila kujali kama nimesikia au la alianza kufuga duka, alikua akifunga huku akinilalamikia kwa kuingilia mambo yake, alitoka na kuingia kwenye gari, aliondoka na kuniacha pale.
Kwakuwa sikua na gari nilichukua bodaboda na kumfuata, tulifika pamoja, aliingia ndani moja kwa moja mpaka chumbani. Ile Briefcase niliyoipasua ilikua kitandani kila kitu nimemwaga chini, lakini hakuijali, aliingia kwenya kabati, akatoa nguo zaote, akatoa mbao flani kisha akatoa kabegi kadogo. Hako nilikua sijakaona, alikafungua na kuangalia vitu vilivyopo ndani na hapoa lipumua kidogo. Alirudisha ilipokua na kurudi kitandani, akaagalia vile vyeti na kuniuliza.
“Kwahiyo hivi ndiyo vimekupanikisha?” Aliongea hukua kicheka, ilikua ni kama kitu cha kawaida kwake, ni kama aliniona mpuuzi mimi kupaniki kwaajili ya kitu kama kile.
“Kwahiyo wewe unaona kama haya mambo ni mdogo? Kwanza una watoto wangapi? Lakini wakwangu ni yupi?”
“Maswali gani hayo sasa, wewe mwenyewe unajua nina watoto wawili, na unajua kuwa kitanda hakizai haramu, huyu mdogo si wako kweli lakini ulishanismahee kwakua hata wewe ulichepuka na una mtoto.” Aliniambia, nilimuuliza kuhusu vyeti na yule mtoto wa mdogo wake kutumia jina lake kama Mama.
“Hivi ni feki tu, hivi ni vyeti natumia kudanganyia wakati nikitaka pesa, unafikiri yule mzee angenijengea kama angejua sina mtoto wake. Hapa anajua nina watoto watatu wote wake lakini ukweli nikuwa hana hata mmoja, huyo mtoto wa mdogo wangu nilimuingiza tu ili apate mali zake, mzee ana pesa yule akifa tunatajirika.”
Aliendelea kuongea maneno ambayo sikumuelewa kabisa, mke wangu alikua anaongea kana kwamba kitu alichokifanya kilikua ni chakupongezwa, alijiona mjanja flani, nilimuangalia bila kummaliza.
“Watoto niwako na wewe ndiyo nakupenda, lakini siwezi kumaucha yule Baba kirahisi namna hiyo, nimetoka naye mbali, ameshanitumia sana hivyo na mimi lazima kumtumia, wewe unafikiri nikimuacha sasa hivi na akijua watoto si wake si ataniua. Mimi nimebadilika, kweli nakiri zamani nilikua sina akili nimefanya maujinga mengi lakini sasa hivi najielewa, najua nafanya nini, nakupenda wewe mume wangu lakini yule mzee nikimuacha ananiua, lazima niendelee kukaa naye kumdanganya danganya mpaka sukari imchukue basi!”
Mke wangu hakujali hisia zangu, aliongea kama kitu cha kawaida sana, nikiwa pale bado natakafakari sijui nini chakufanya alikusnaya vitu vyake, aliangalia nyaraka zake kama ziko sawa na kuondoka navyo. Alirudi jioni, mimi bado nilikua nyumbani, bado nilikua sijisikii vizuri na nilitamani kuongea naye ingawa hakuwa tayari kwa hilo.
“Mimi kesho naenda nyumbani, naenda kumuona Mama anaumwa.” Aliniambia, nilimuitikia tu sawa kwani nilikua na hasira sana, aliingia jikoni kuandaa chakula cha usiku lakini sikuweza hata kula, nilimuambia najisikia vibaya, aliishia kuniambia sawa kisha akaendelea na mambo yake, alikula na kurudi kupanga nguo, asubuhi aliondoka na kuniacha.
Mke wangu aliondoka na kuniacha na watoto wake wawili, mtoto wake wa kwanza ambaye alinidanganya ni wamdogo wake na yule wa tatu ambaye alizaa na mtu mwingine baada ya sisi kuoana. Mtoto ambaye wakati huo hata sikujua kama ni wangu au la alikua bweni anasoma. Nilikua na hasira sana hata kazini nilishindwa kwenda, nilikua najisikia vibaya kwani kila nilipokua nikimpigia mke wangu simu ilikua haipokelewi. Nilikua sijielewielewi, mpaka jioni nilikua sijatoka ndani na simu ya mke wangu ilikua haipokelewi, hasira zilinipanda. Nilimpigia simu Mama yake, baada ya salamu nilipotaka kuongea na mke wangu alijifanya network inasumbua na kukata simu.
Hapo hasira zilinipanda zaidi, nilijikuta naingia jikoni, nikachemsha maji mengi ya moto. Binti wa kazi alikua ashalala, ulikua ni usiku wa manane nilikua macho peke yangu. niliyaepua maji yale baada ya kuchemka sana nikayaweka kwenye ndooo, kisha ilitoka kuelekea chumbani kwa watoto.
“Hawa ndiyo wanampa kiburi ngoja niwaonyeshe!” Nilifungua mlango wa chumba cha watoto, bila kuwasha taa niliingia ndani, nikanyanyua ile ndoo huku nikielekezea kilipokua kitanda cha watoto niliyamwaga maji nusu kwenye kitanda kimoja nikageuka upande wapili na kumwaga maji ya moto nusu kwenye kitanda kingine ambacho kilikua na mtoto mwingine.
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SEHEMU YA KUMI NA MOJA
“Nimefanya nini…” niliwaza huku nikikaa chini, nilikua nikisubiria kelele za watoto kutokana na kuwamwagia maji ya moto. Lakini kimya kidogo kilipita, sikusikia kelele, nilinyanyuka na kuwasha taa. Vitanda vilikua tupu, hakukua na mtoto. Kama mtu aliyechanganyikiwa nilienda kukagua vitanda, nilitoa mpapa magodoro lakini hakukua na kitu. nilitoka mpaka sebulani, nikaenda mpaka jikoni kuona kama walikua kule. Hawakuakule, nilipata wazo kwenda chumbani kwa binti wa kazi kuona kama walilala huko. Mlango ulikua umefungwa nikaanza kugonga kwa nguvu.
“Watoto wako wapi? Mbona hawajalala chumbani kwao?” Nilimuuliza binti wa kazi baada ya kuniitikia.
“Mama akisafiri huwa wanaogopa kulala wenyewe, wanakuja kulala kwangu, sijui kwanini….” Binti wa kazi aliniambia huku akitaka kufungua mlango.
“Basi nilikua nawaangalia tu.” Nilimjibu huku nikitoka, moyoni kuna kitu kilikua kinaniambia warudie uwamaliza si damu yako, ukiwamaliza ndiyo utamuumiza yule mwanamke. Lakini kuna kitu kilikua kikiniambia kuwa hapana hawanakosa lolote, shukuru Mungu umeiepuka dhambi hii. Nilirudi chumbani na kutoa magodoro yote mawili, maji hayakua mengi sana hivyo ilikausha chini kidogo, niakchukua magodoro na kuyapeleka chumbani kwetu. Nilijua asubuhi kama wangeona kuwa yemeloa wangejiuliza maswa, ilikua ni bora kuona kama hayapo nikawaambia nimeamua kuyabadilisha.
Asubuhi niliamka mapema na kuondoka nayo, nilienda kuyatupa nikanunua mengine na kurudisha kama zawadi nikiwaambia kuwa nimeamua kubadilisha magodoro kwani yalikua yamechakaa. Nilishinda kutwa nzima nikiwa na mawazo sana, kila daikika nilikua nikiangalia siomu yangu kuona kama mke wangu atanipigia lakini hakunipiga. Nilikua na hasira sana lakini cha ajabu sikua na hasira na mke wangu, nilikua na hasira na watoto wake, niliona kama wao ndiyo walikua wamenikosea na si mke wangu.
Mpaka jioni mke wangu alikua hajanipigia simu na nikipiga simu yake ilikua haipokelewi. Nikiwa chumbani mtoto wake mkubwa alikuja, aligonga chumbani kwangu nikamruhusu aingie, lakini nilipomuona tu sura ya yule mbaba ilinijia. Ilipandwa na hasira na kujikuta naanza kumtukana, nilimtukana sana nikimuambia ni kwanini alikua akiingia chumbani kwangu bila hodi. Kumbuka aligonga na mimi ndiyo nilimuambia aingie, aliniomba msamaha huku akilia lakini sikujali, nilimuambia anitokee.
“Mama anapiga anasema simu yako haipatikani…” Aliongea huku akilia, alikua kashikilia simu ya Dada yake mkononi. Nilinyanyuka harakaharaka na kumkimbilia, nilimnyang’anya ile simu na kuanza kusema.
“Haloo! Haloo!”
“We mshenzi nini, kwanini unawatukana watoto wangu, kama una hasira na mimi malizia kwangu!” Mke wangu alianza kwa kunitukana.
“Hapana, sijafanya hivyo, nilikua namuonya ameingia chumbani bila kugonga.” Sijui kwanini lakini baada tau ya kusikia sauti ya mke wangu nilinywea kabisa, nilijikuta naomba msamaha huku nikidanganya ili tu kumridhisha mke wangu. Mke wangu hakukubaliana na majibu yangu, alitukana sana mpaka kunikatia simu, hakuniambia chochote kilichomfanya kunmipigia.
Nilijaribu kumpigia tena lakini simu yake haikupokelewa. Nilijikuta napandwa na hasira, nilitaoka nnje na kuanza kutukana, sijui nilikua natukana nini, lakini nilitukana, nikaenda mezani na kumwaga chakula, watoto walibaki kimya hata yule mdogo. Dada wa kazi alishangaa kuniona katika hali ile, nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa. Baada ya kutukana sana tena matusi ambayo hawayahusu nilirudi chumbani nakuanza kulia. Nilikua na hasira sana, baada ya kama nusu saa hivi simu yangu ilianza kuita, alikua ni mke wangu, nilijua lazima watoto wamemuambia kila kitu hivyo sikupokea.
Nilipoona anazidi kunisumbua ilizima simu na kulala mpaka asubuhi. Siku iliyofuata sikutoaka kabisa, hata kazini sikwenda, nilijifungia ndani huku nimezima simu. Mara kadhaa binti wa kazi alikuja kugonga lakini sikufungua mlango. Nilikua na hasira sana na niliogopa kutoka nnje kwani nilihisi kabisa kuwa naweza kufanya kitu kibaya. Jioni mke wangu alirudi. Alikua ashaambiwa kilichotokea hivyoa liahirisha safari zake na kurudi, alijaribu kuongea na mimi kuniuliza tatizo nini lakini sikua na majibu, nilimuambia kuwa niko sawa.
Kwa mara ya kwanza aliniomba msamaha akiniambia kuwa mtoto mmoja ni wangu na wale wawili kweli si wangu, aliniambia kuhusu mtoto wake wakwanza akaniambia kuwa ni mtoto wake kweli na alishawahi kuolewa. Nilimsamehe tukaendelea kuishi, ingawa nilijaribu kusahau na kulazimisha furaha lakini bado nilijikuta nina hasira. Nilikua nimewakasirikia watoto wa mke wangu, niliwaona wao kama sababu ya mimi kukosana na mke wangu.
Siku moja nilikua nimetoka kazini, mke wangua liniambia nimpitie mtoto wake mkubwa shuleni, nilimpitia nikarudi naye nyumbani. Lakini baadaye kulikuja wageni, nikawa nimwasindikiza na Gari, wakawa wamembeba mtoto mdogo wa mke wangu na yule mkubwa naye akaingia kwenye gari.
Niliwafikisha wageni lakini wakati narudi mke wangu alinipigia simu, kuna kitu alikua ananiulizia baada ya kumaliza akidhani kuwa kakata simu aliendelea kuongea, nilimsikia akiongea na simu.
“Hawezi kuondoka pale ananisaidia nyumbani yule ni binamu yangu, unaona sasa sipo kaenda kumchukua mtoto shule…” mke wangu aliongea.
“Mimi hata siwaelewagi, mtu mzima kama yule hana familia anaishi kwako tu….” Ilikua ni sauiti ambayo nilikua naifaham, aliokua ni yule Baba. Waliendelea kuongea mara nikasikia mabusu. Hasira zilinipanda, nilianza kuendesha gari pembeni, nilikua nikilielekeza kwenye nguzo ya taa ya barabarani, mtoto mkubwa wa mke wangu alikua kakaa mbele huku kampakata mdogo wake.
“watu watajua ni ajali!” Nilijisemea huku nikitaka kugongesha gari kwenye mlingoti wa taa za barabarani. Nilikua nataka kutengeneza ajali, nilikanyaga mafuta kwa nguvu lakini kabla ya kufikia ule mlingoti kuna gari nyingine ilikua inakuja kwa kasi mbele yangu, ilikua inakuja upande wangu hivyo nililazimika kuikwepa, nikajikuta narudi kulia na kuparamia gari nyingine ndogo. Niliikwaruza ile gari ndogo upande wangu na ile nyingine uiliyokuja kwa kasi ikapita. Nililazimika kusimama, tukaanza kutukanana kila mtu akimlaumu mwenzake, kwakua aliyekua anakuja mbele yangu ndiyo alionekana ana makosa na alishakimbia tuligombana na kila mtua kaondoka zake.
Hapo akili zilinirudia kidogo. “Hivi nataka kuwafanya nini hawa watoto?” Niliwaza, nilikua nikitetemeaka, watoto nao walikua wakitetemeka. Nilirudi nyumbani nakuingia ndani, mke wangu hakurudi mpaka saa mbili usiku. Alirudi na kukuta nishamuandikia talaka tatu nakumkabidhi.
“Hii ni nini?” Aliuliza kwa mshangao, hakuamini kilichokua kimetokea, hata mimi sikuamini kuwa nilikua namuacha mke wangu.
“Talaka, nimekupa talaka tatu si mke wangu, kesho uondoke.” Nilimuambia, mke wangu alidhani ni utani, aliaza kutukana kama kawaida yake huku akiniambia kuwa ile nyumba ni yake, ina jina lake hivyo kama nikuondoka basi niondoke mimi.
“Hii ni mara ya pili na nusurika kuwaua watoto wako, mara ya kwanza niliwamwagia maji ya moto lakini hwakuepo kitandani, kama unakumbuka nilibadilisha magodoro. Leo nilitaka kuwagongesha kwenye gari wafilie mbali lakini Mungu kawaoko, kaangalie gari imekwaruza. Naamini mara ya tatu nitafanikiwa, sitaki kufanya hivyo lakini siwezi kuishi na watoto wako, sikutaki na utaondoka. Hii nyumba nimejenga kwa jasho langu utaondoka au kama uking’ang’ania inaweza kuwa ni kaburi la wanao, sikutaki wewe na wanao.”
Nilimuambia taratibu kabisa na kutoka kuondoka, sikurudi tena mpaka kesho yake, nilikuta mke wangu anafungasha vitu vyake anaondoka. Alijaribu kuniomba msamaha lakini sikua tayari kwa hilo.
“Naweza kukusamehe lakini siwezi kuishi na wanao, sina mtoto na wewe, hata yule niliyekua nadhani ni wangu sidhani kama ni wangu tena. Nitapima DNA ila kwa sasa ondoka, sikutaki, najua siwezi kukufanya chochote ila hawa watoto nitawaua.” Mke wangu aliniangalia na kujua kuwa nilikua namaanisha, aliondoka na talaka zake kurudi kwao. Sikukaa hata miezi miwili niliiuza ile nyumba, niliancha kazi na kwenda Kigoma.
Lengo langu lilikua ni kumshitukiza Joan lakini nilipofika nilikuta kashapata mwanaume mwingine, wamefunga ndoa ya kiserikali na ana mimba yake. Miezi sita nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa, nilimaliza pesa yote, sikurudi hata kupima DNA ya mtoto wangu, nilikua naogopa. Mwaka jana nilibahatika kupata kazi sehemu nyingine maisha yangu sasa hivi kidogo nimazuri lakini bado sijapata ujasiri wa kumtafuta aliyekua mke wangu na kupima DNA. Joan naye hataki kabisa mawasiliano na mimi, matumizi ya mtoto natuma lakini nikipiga simu hazipokelewi hivyo sijui hata mwanangu anaendeleaje.
Baada ya kumpa talaka mke wangu hata hakurudi kwao, kuna nyumba alikua amejengewa na yule mwanaume, alihamia na sasa hivi ni kama kawekwa kinyumba. Mara kadhaa nakutana naye mjini akiwa na wanaume tofauti lakini hatusalimiani, naona kinyaa na kuna wakati najiuliza hivi alinipa nini mpaka kuvumilia utumbo wake wote. Anaonekana kabisa hajabadilika na hata tukikutana hajali chochote. Naumia sana kumuona na sasa hivi nafuatilia kazi nyingine Dodoma kwani nataka kuanza maisha yangu upya, hii ni mara ya kwanza kutoa yaliyonikuta katika maisha yangu kwani hata ndugu zangu hawajui ni sababu gani hasa zilinifanya kuachana na mke wangu.
***MWISHO
0 comments:
Post a Comment