Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

MIMI, MAMA NA BABA PEMBENI

  

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

 

SAFARI; MIMI, MAMA NA BABA PEMBENI!—SEHEMU YA KWANZA.


Mvua kubwa ilikua inanyesha, mimi nilikua ndani chumbani nimejifungia, Baba alijua kuwa nimelala kwakua nilikua nishazima taa tayari. Lakini bado nilikua macho, niliweza kuchungulia katika kona ya dirisha na kama unavyojua mtu ukiwa kwenye giza basi ni rahisi kuona nnje kwani taa ilikua inawaka. Ingawa mvua ilikua inanyesha lakini niliweza kuona kila kitu kilichokua kikiendelea nnje.


JOIN US ON TELEGRAM

Gari ya Baba ilikua imesimama nnje, Mama alikua yuko bize kufunga geti kwani ndiyo alikua katoka kumfungulia. Baada ya kufungua geti Mama alitaka kurudi ndani lakini Baba alidfungua mlango kidogo na kuonekana kama kamuita, Mama alisogelea gari ya Baba, sikusikia walichokua wameongea kwani nilikua mbali na mvua ilikua inanyesha. Lakini nilimuona Baba akimpiga Mama mateke.


Kwanza alimpiga teke la tumbo, mam alipepesuka na kudondoka chini, hakukua na matope kwani nyumba yetu ilikua na nyasi nzuri na sehemu lilipokua gari kulikua na zege. Bila kujali mvua Baba alishuka kwenye gari, alionekana kupepesuka pepesuka, alimfuata Mama pale chini na kuanza kumpoiga mateke, alionekana kuongea kwa hasira, nilimuona namna alivyokua kabadilika kama mnyama, alikua akintyanyua mdomo kwa nguvu ingawa sikusikia chochote.


Mama alikaa chini na kujikunyata huku akizuia tumbao lake, alijikunja sana kuzuia tumbo, sikujua kwanini mpaka baadaye nilipokua mkubwa ndiyo nilikuja kugundua alikua akizuia kupigwa tumboni kwani kipindi hicho ndiyo alikua na ujauzito wa mdogo wangu Rajabu (Sio jina lake halisi). Sikujua walikua wanagombania nini lakini niliogopa sana, Baba alionyesha hasira na alikua akimpiga Mama bila huruma, katika maisha yangu nilikua sijawahi kumuona Baba katika hali ile.


Baba yangu alikua mtu mstaarabu, mswali hina, kipindi hicho nikiwa mtoto wake wa pekee alikua akinipenda sana, hakuwahi kunipiga wala kunifokea na mara nyingi nilikua namuona yeye ni mtu poa kuliko Mama. Mpaka siku hiyo nilikua nampenda Baba yangu kuliko Mama yangu, sikuwahi kumuona akiwa kakasirika, sikuwahi kumuona akimpiga mtu na wala sikuwahi kufikiria kama anaweza kunyanyua mkono na kumpiga mtu yeyote achilia mbali kumpiga Mama.


Alimpiga sana Mama, Mama hakulia wala kupiga kelele, alikua kakaa chini tu kajikunyata, wakati akiendelea kumpiga alishuka Rahma (sio jina lake halisi) huyu nilitambulishwa kama Shangazi. Alikua ni mgeni ambaye alikua kakaa pale nyumbani kwetu kwa kama wiki moja hivi, ingawa ilikua ni mara yangu ya kwanza kumuona lakini Baba aliniambia kuwa ni Shangazi yangu na alikua masomoni simjui. Nilimpenda sana Ant Rahma kwani alikua akiniletea zawadi, alikua akinipenda na mara nyingi alikua akinitembeza sehemu mbalimbali.


Aliposhuka niliona kama anamuinamia Mama na kumuongelesha maneno ambayo pia sikuyasikia. Baada ya kumuongelesha alimsukuma Mama na viatu vyake virefu. Kwanza nilishangaa kwa namna alivyokua amevaa, alikua kavaa kisketi kifupi ambcho kama angeinama basi ungeweza kuona nguo yake ya nadni, alikua kavaa viatu virefu na minywele inaonekana. Nilishangaa kwani kwa kawaida ni mtu wa kuvaa mahijabu na kujitanda.


Sikuelewa kwakweli, usiku ule kila kitu kilikua kigeni kwangu, wakati nikiwa nawaza ni kitu gani kilikua kinaendelea nilimuona Shangazi Rahma akimvamia Baba, walimkumbatia na kuanza kunyonyana ndimi, ingawa nilikua bado binti mdogo nina miaka nane tu lakini nilikua najua wanafanya nini. Nilishaona hayo mambo katika michezo ya kuigiza ya wanaigeria na wazungu hivyo nilijua ni kufanya mapenzi, nilishangaa sana kwani kama yule alikua shangazi inamaanisha ni ndugu wa Baba yangu.


Nilishangaa ni kwanini Baba anapeana mate na Shangazi tena mbele ya Mama. Walishikana kimapenzi na bila aibu Baba alinyanyua kigauni cha Rahma na kutaka kumvua nguo, walitaka kufanyia mapenzi palepale. Wakati huo mvua ilishakata na kulikua na manyunyumanyunyu. Mama kuona vile alinyanyuka na kuwavamia.


“Mume wangu kuna watoto ndani mnataka kufanya nini?” Mama alipiga kelele ambazo nilizisikia, Baba aliacha kufanya alichokua akikifanya na kumvamia Mama.


Alianza tena kumpiga hukua kimuambia asimpangie maisha ile ni nyumba yake na kama hataki kuona kinachoendelea basio aondoke.


“Kwanini unaning’ng’ania, si uondoke!” Baba alipiga kelele. Mama alikua anamuambia amuogope Mungu na kuacha kufanya ushenzi wake mbele yake.


“Si uondoke! Mwanamke umeletewa mwanamke mwingine mpaka ndani lakini hutaki kuondoka! Ondoka tuachie nyumba yetu tufanye mambo yetu kwa uhuru!” Rahma aliongea huku akiwa kama anamsuta Mama.


Mama hakusema chochote, alinyamaza kimya, alianza kutembea kwa shida kuingia ndani lakini Baba alimfuata na kuanza kumpiga tena. Kule ndani nilikua nimechanganyikiwa, kwangu ile ilikua kama sinema, kuna wakati nilijihisi kama vile naota nikaanza kujifinya finya mimi mwenyewe kuona kama niko macho. Sikuwahi kumuona  baba namna ile wala sikuwahi kufikiria kuwa anaweza kumpiga Mama, nilitamani kutoka na kuuliza lakini niliogopa sana.


Baba alikua tofauti na kawaida yake, alimpga Mama kama mbwa na baada ya kumaliza kumpiga aliingia ndani na Rahma, walifunga mlango kwa ndani na kumuacha Mama pale nnje. Niliumia sana, mama alitembea mpaka kwenye kibaraza na kujibanza ukutani, kwa sehemu niliyokua sikuweza kumuona tena kwani aliegemea ukuta, nilikaa pale dirishani mpaka nilipopitiwa na usingizi nikalala.


***


Kutokana na kukesha usiku asubuhi nililala sana, ulikua ni wakati wa likizo hivyo hakukua na shule, siku hiyo Mama hakutaka hata kuniamsha mapema. Nilikuja kuamshwa asubuhi kwenye saa tatu hivi na Dada (Mfanyakazi wetu wa ndani).


“Njoo umuage Shangazi aonaondoka, Baba anakuita!” Aliniambia, nilijikuta nanyanyuka harakaharaka kwenda kumuona Shangazi, alinichangamkia sana na kuniahidi kurudi tena, ingawa ilikua ni siku ya kazi lakini Baba alikuepo.


Alionekana kuja kumsindikiza Shangazi.


“Mama yuko wapi?” Nilijikuta nauliza, bado nilijihisi kama niko ndotoni, mambo ya jana yake sikuyaona kama mambo halisia, nilijihisi nimeota kitu kibaya. Wakatiwanaongeana Rahma kujiongelesha kama mtu mwema mimi kichwa changu kilikua kikizunguka mambo ya jana.


“Bado ana usingizi huyu, kwanini umemuacha akalala mpaka sasa hivi?” Baba aliongea bila kujibu swali langu, nilikua kimya sana kama nimeshikwa na bumbuwazi.


Rahma alijiongelesha ongelesha na kuondoka na Baba, sikujua ameenda wapi na wala sikujali.


“Jana usiku mvua ilinyesha?” Nilimuuliza dada, bado nilikua na wenge la usingizi, akili yangu ilikua haijakubali kama Baba anaweza kumpiga Mama.


“Mimi sijui nilikua nimelala lakini nnje majani yameloa, itakua ilinyesha. Kwanini unauliza?” Dada alinijibu, sikua na jibu kamili hivyo nilinyamaza tu kimya.


Nilirudi chumbani kwangu nikiwa sina raha kabisa, kuna mambo mawili yalikua yananichanganya, moja ni kwa Baba kumpiga Mama na jingine ni kwa Baba kukumbatiana na kulana mate mwanamke mwingine ambaye nilimjua kama Shangazi. Siku ile ilikua ndefu sana, sikua na amani mpaka jioni, Mama ndiyo alitangulia kurudi kutoka kazini, nilimsalimia kwa kumkumbatia huku nikimkagua kagua kuona kama vile kaumia.


Alijitahidi kucheka ingawa nilimuona kabisa hayuko sawa.


“Una nini wewe mbona unaniangalia hivyo? Nimebadilika?” Aliniuliza, sikua na jibu, bado nilikua sina uhakika na kitu nilichokiona jana yake hivyo sikuongea chochote. Baadaye Baba alikuja, walisalimiana vizuri tena kwa kukumbatiana, kama kawaida Baba aliniletea zawadi, nilizipokea lakini sikua na Bashasha, akili yangu bado ilikua inawaza mambo ya jana yake, ingawa sikutaka kuamini lakini nilimuogopa sana Baba.


Niliingia ndani nikiwa na mawazo sana, kwa kawaida Baba si mtu wa kutoka sana, mara nyingi anakua nyumbani akinisaidia homework na kunibembeleza mapaka kulala, mara nyingi anakuja chumbani kwangu kunisomea hadithi na huwa tunacheza pamoja. Kama kawaida siku hiyo alikuja, lakini sikutaka kuongea naye hivyo niolivyomsikia tu anafungua mlango nilipenda kitandani, nikafunga macho na kujifanya kulala.


Alisimama kwa muda wa kama dakika mbili kisha akatoka na kufunga mlango, nilipoona katoka nilitembea mpaka mlangoni kumchungulia.


“Asha (si jina lake halisi)  atakua anaumwa, leo kutwa naizma hana raha kabisa, sijui ana nini ila namuona kaingia kalala.” Baba alimuambia Mama ambaye alikua kakaa kwenye kochi anaangalia TV.


“Sijui, ngoja nitamuangalia ana nini?” Mama aliongea lakini Baba alimkataza akimuambia hataki nisumbuliwe kwani nishalala.


Nilimuona Mama akinyong’onyea, ukimya ulitawala kidogo, nilirudi ndani kulala, kichwani nilikua na mawazo mengi tu, nilikua na maswali mengi kuliko majibu. Niliwaza mpaka kupitiwa na usingizi. Nyumba ilikua na amani kwa muda mrefu, furaha ilirejea, sikuwahi kumuona Baba akimpiga au kumkasirikia tena Mama, kuna wakati niliamini kabisa labda nilikua naota kwani kila mtu alikua na amanai na sikuona kitu chochote kibaya.


Siku moja nakumbuka nilikua kwenye gari, ilikua ni wiki moja kabla ya kufungua shule, zilishapita zaidi ya wiki tatu tyangu kile kitendo kutokea. Nilikua nimekaa siti ya nyuma nimelala, tulikua tunatokea kijijini kwa bibi ambapo nilipelekwa kusalimia.


“Unajua tunatakiwa kutoa ada angalau nusu?” Nilimsikia Mama akisema. Usingizi ulikua unakuja na kurudi lakini wao alijua kuwa nimelala.


“Kwahiyo? Si utoe unaniambia nini?” Baba alijibu kwa hasira, aliongea kwa sauti ya juu kiasi cha kunishtua, lakini sijui kwanini, sikushtuka, niliendelea kufunga macho ili kusikiliza, nadhani umbea ulikua unanisumbua.


“Sina pesa mume wangu, mwaka jana uliniambia hivyo hivyo nitoe, nikachukua mkopo lakini hukulipa, hapa nadaiwa, mshahara wangu nakatwa deni la nyumba na sasa hivi natakiwa tena kumtumia mdogo wangu kaosa mkopo chuo, nisaidie mume wangu…” Mama aliongea kwa kulalamika.


“Kwahiyo ndugu zako unaona ni wamhuhumu sana kuliko mwanao! Mimi sina pesa na kama hutaki asome muache abaki nyumbani, wewe si unasomesha ndugu zako, waache wasome wakati wakwako anabaki nyumbani!”


Bbaa aliongea kwa hasira, Mama alikaa kimya kwa muda wa kama dakika tano, kule ndani ya gari kila kitu kilikua kimya kimetulia mpaka Mama alipoongea tena.


“Lakini wewe mshahara wako unaenda wapi? Hutoi pesa ya chakula, nyumba nimejenga mimi, mavazi mimi na hata ada ya…” Mama aliongea lakini kabla ya kumalizia Baba ambaye alikua ndiyo anaendesha gari alichukua simu yake ambayo ilikua kwenye dashboard na kuirusha, ilimpiga Mama kwenye pua.


“Mshenzi mkubwa wewe! Mimi ni nani kwako unaanza kunihesabia vitu unavyovifanya ndani ya nyumba yangu! pumbavu Malaya mkubwa wewe!” Baba aliongea kwa hasira, simu ilimpiga Mama puani, alipiga kelele moja tu “Nakufaaaa!” Baba alikua kama kachanganyikiwa, aliacha usukani na kumrushia ngumi Mama, ya uso, alionekana kukasirika zaidi. wakati anafanya hivyo gari ilianza kuyumba, kwakua tulikua kwenye mwendo kasi, ilipoteza uelekeo na kuacha barabara. “Nakufaaaa! Nilipiga kelele nilipoona mti mkubwa uliokua mbele yetu na gari ilikua ikiufuata!”


MTAG rafiki yako muambie hii si ya kukosa na kwa muendelezo hakikisha unafuatilia ukurasa wangu wa Instagram @iddimakengo


ITAENDELEA….


SAFARI; MIMI, MAMA NA BABA YANGU PEMBENI!—SEHEMU YA PILI.


Kila kitu kilikua kinatokea haraka lakini nilikiona, pamoja na umri wangu mdogo lakini ile picha iliendelea kubaki kichwani kwangu mpaka sasa. Baba aliuona ule mti, alijaribu kuukwepa gari ikawa inaenda kama kuugonga kwa upende wake, lakini ghfla nilimuona akigeuza usukani na kuligeuza na kuugonga ule mtu kwa uapende wa Mama. Nilisikia kishindo kikubwa na baada ya hapo sikuelewa ni kitu gani kingine kilikua kimetokea.


“Hajaumia popote, naona kama ni mshituko tu, hajazindika lakini viungo vyake viko salaama, atazinduka, havuji damu kwa ndani….” Nilisikia sauti nzito ambayo sikuielewa, nilikua katika usingizi mzito, mwili ulikua umechoka na nilijaribu sana kugumbua amcho lakini hayakufunguka. Mara nilisikia mtu ananishika mkono, hakusema chohote lakini alionekana kukaa pembeni yangu, nilijitahidi sana kufungua macho yangu, alikua ni Baba, alikua mzima kabisa kakaa pembeni yangu.


Kulikua na watu wengine wengine pale chumbani lakini kwa sasa siwakumbuki, walikuja kunisalimia. Nilipepesa macho nikijaribu kuwaza kilichokua kimetokea. Nilijitahidi kunyanyuka lakiniBaba alinishika, alinirudisha kulala.


“Pumzika kwanza…” Aliniambia kwa kunibembeleza, mikono yake ilikua usoni kwangu aliniuliza maswali maswali namna nilivyokua nikijisikia, mimi nilibaki kimya nikishangaa, bado nilikua sijazinduka vizuri, lakini taratibu picha ya lile tukio ilianza kuja kichwani kwangu.


Niliiona ile ajali kama ndiyo kwanza ilikua inatokea, niliona namna ambavyo Baba alimpiga Mama na kisha kuanza kugombana  mpaka alipoligongeshea gari kwenye mti.


“Muache Mama! Muache Mama! Usimuue!” Nilijikuta napiga kelele huku nikimpiga makofi Baba, nilijitoa katika mikono yake na kujirusharusha, nilipoga kelele nyinyi lakini yeye hakupaniki, alinishikilia chini na kuniambia nipumzike ni mshituko wa ajali lakini nitakua salama.


Nilijaribu kujitoa mikononi mwake lakini nilishindwa, nilipiga kelele sana mpaka nikachoka, baadaye nilituliamwenyewe, aliwaomba watu waliokua mule ndani kutoka na kunaicha nipumzike. Alitoka na kuniacha mwenyewe, alikaa nnje kwa muda kidogo kisha akarudi, alikua na chakula na alitaka kunilisha, tayari akili yangu ilishaanza kukaa sawa na nilijua nini kilikua kimetokea.


“Mama yuko wapi?” nilimuuliza baada ya kuingia, alijaribu kubadilisha mada lakini sikumruhuhusu, bado nilikazania kujua alipokua Mama yangu.


“Yuko chumba kingine, anaendelea vizuri.” Aliniambia hukua kikaa pembeni yangu na uji mkononi.


“Nataka kumuona…” nilimuambia, alikataa na kuniambia kuwa nile kwanza kama natataka kuonana na Mama yangu. nilijaribu kubisha lakini huo ndiyo ulikua ni msimamo wake, aliniambia kama nataka kumuona Mama basi nile chakula kwanza, alijaribu kunibembeleza, kunichekea lakini kila nikimuangalia sikuona tena picha ya Baba wa zamani, nilimuona Baba mpya ambaye alikua anampiga Mama na kugongesha gari upande wa Mama.


Nilikula harakaharaka, nilikua najisikia vizuri na baada ya kumaliza kula niliweza kunyanyuka, alinisaidia kunishika akidhani labda nilikua nimeumia lakini sikua nimeumia popote, sikupata hata mchubuko, kama alivyokua Baba mimi nilitoka salama kwani nilikua katika siti yangu nimefunga mkanda lakini pia nilikua ule upande wa Baba hivyo sikuumia popote. Nilitaka kwenda kumuona Mama lakini alinikatalia.


Kwa namna alivyokua anakataa nilijua lazima kuna kitu kibaya kimetokea, moja kwa moja nilihisi Mama amekufa, nilianza kupiga kelele na kumlaumu yeye kwa kumuua Mama yangu, alijaribu kunisihi kwa kuniambia kuwa Mama yuko salama na hajafa lakini sikumuamini, nilihisi ananidanganya na kumuambia kama kweli yuko salama basi anipeleke kumuona. Kwa namna nilivyokua nikisumbua hakua na namna, aliniambia twende kumuona Mama.


Alinipeleka mpaka kwenye chumba kimoja, hapo niliona watu wamekaa nnje, wengi nilikua nawafahamu, kulikua na Shangazi zangu, Mama zangu wadogo na ndugu wengine wengi wengi.


“Kaaa hapa, Mama yako yuko huko ndani kwenye chumba cha upasuaaji,a lipata ajali na wote tunasubiria.” Aliniambia, sikua naelewa kitu nilitaka tu kumuona Mama, nilipiga kelele mpaka kulazimika kuondolewa pale, nilirudishwa chumbani na kuchomwa sindano moja nikalala.


***


Nilikua nimetoka likizo kwa Bibi, pamoja na kwamba nilikua nasoma day lakini baada ya ile ajali nilihamishiwa bweni. Siku ile nilipozinduka nilikua nimetulia kidogo, mama alishatoka katika chumba cha upasuaji na niliruhusiwa kumuona, alikua kalala kitandani haongei chochote zaidi ya kupepesa macho kuniangalia, hapo ndipo nilijua kuwa Mama yangu yupo hai. Hakuonekana kuumia sehemu yoyote, usuo ulikua hauna michubuko mingi, alivimba kidogo  na bandeji kidogo.


“Mama yako huyo hapo, anaendelea vizuri hivyo kama unataka apone basi usimsumbue, muacha apumzike.” Baba aliniambia kwa upole, sijui ni nini lakini nilimuelewa, siku hiyo ndiyo akili zangu zilianza kuwa za mtu mzima. Lakini pia siku hiyo ndiyo ilikua mara yangu ya mwisho kumuona Mama hospitalini, nilirudi nyumbani na huko Baba aliniambia natakiwa kwenda bweni. Nililia sana na kugoma lakini alikataa, nakumbuka nilikua naingia darasa la nne na Baba alitumia kisingizio cha mtihani wa taifa kwa mimi kwenda kukaa bweni.


Nilitaka kwenda kumuona Mama lakini alikataa, aliniambia Mama ni mgonjwa na haruhusiwi kuoanana na watu. Nakumbuka nilisoma kwa bidii nikisubiria likizo ili kwenda kumuona Mama, lakini ilipofika nilipelekwa kijijini, wakati huo Mama alikua kashapona na niliweza kuongea naye kwenye simu, alikua anaongea vizuri tu na niliambiwa kuwa nina mdogo wangu wa kiume. Nilikua na hamu sana ya kumuona na kumjua lakini nilipigwa tarehe mpaka likizo ya mwezi wa kumi na mbili, kipindi naingia darasa la tano.


Walitaka kunipeleka kijijini kwa bibi lakini nilikataa, nililia sana mpaka nikaruhusiwa kwenda kumuona Mama.nilichokiona kilinishangaza sana, Mama alikua kakaa kwenye kiti, kapooza kuanzia kiunoni kushika chini, mikono yake nayo ilikua haifanyi kazi vizuri, ilikua inanyanyuka kwa shida hivyo kila kitu alikua ni  mtu wa kufanyiwa. Alikua anaongea vizuri lakini alionekana kuwa katika maumivu makali, alijitahidi sana kutokunionyesha kuwa anaumia au anaumwa lakini ukweli nikuwa alikua katika hali mbaya.


Mdogo wangu ambaye wakati huo alikua na kama miezi sita kama sijakosea alikua haishi na Mama, alishachukuliwa na Shangazi na yeye ndiyo alienda kumlea, nilienda kumuona na nilifurahi sana kua na mimi nilikua na mdogo wangu. kitu kilichoniumiza sana ni hali ya Mama, si hali ya ugonjwa bali hali yake ya kiafya, alikua kakonda sana, alionekana kama mtu  mwenye mawazo, kulikua na dada wa kazi pale nyumbani kwaajili ya kumhudumia lakini ni kama vile hakuepio.


Mama alikua mchafu, nguo zinanuka, alikua hawezi kufanya chochote hivyo mara nyingi alikua anajisaidia hapohapo kwenye kiti chake na kuja kusafishwa baadaye, lakini hakukua na mtu wa kumsafisha na huyo dada wa kazi naye aliku akimntukana na kumlalamikia kwani alikua halipwi vizuri. Baba alikua si mtu wa kukaa nyumbani na hata akikaa alikua hakai chumba kimoja na Mama, kipindi nipo alijitahidi kuigiza ili mimi kumuona kama Baba bora lakini alishindwa.


Niliumia sana kumuona Mama katika hali ile, alikua ni  mtu wa mawazo, mtu wa kufungiwa ndani, dada wa kazi akiwa na mizunguko yake angeweza kumfungia Mama ndani kwa kutwa nzima bila hata kumpa chakula, kwakua Baba naye alikua hajali anaweza kukaa hata wiki bila kurudi nyumbani basi dada alifanya kile anachojisikia bila kujali kama kuna mtu atajua au atapoteza kazi. Hakua anapika kwa wakati na suala la kumbadilisha nguo ilikua mtihani.


“Nani wakufua kila saa mtu mwenyewe atakuja kujinyea tu, bora ayakusanye nikija nafua jumla.” Alikua anapenda kuongea mara kwa mara. Hali ile iliniumiza sana, Mama alikua hajiwezi hata kulishwa alihitaji kulishwa lakini angeweza kukaa kutwa nzima na njaa bila kupata mtu wa kumhudumia. nililazimika kubeba jukumu la kumhudumia Mama, kitu ambacho nilikua siwezi ilikua ni kumsafisha kwania likua ni mzito sana, lakini kwa hali yake ileile alijitahidi kujinyanyua  na kujigeuza na wakati mwingine nililazimika kutoka kwenda kuomba watu nnje wanisaidie kumnyanyua.


Wakati wa kurudi shule ulipowadia nilikataa kabisa kwenda bweni, nilimuambia Baba nataka kubaki na Mama ili kumsaidia, Baba alaijaribu kunibembeleza lakini sikukubali. Nilimuambia kama hanirudishi nyumbani basi sitasoma kabisa, alikasirika sana na kunitukana, Baba yangu ananipenda na katika maisha yake alikua hajawahi kunikaripia wala kunipiga lakini siku hiyo alikasirika na kuniambia kuwa nitaenda shule na kunipiga makofi, nilikataa na kumuambia kuwa sitaenda nitakaa na Mama! Tena nilizidisha zaidi kwa kumuambia kuwa yeye ndiyo kasababisha Mama kuwa vile.


Nilimuona Baba akikiasirika zaidi, alivimba na kutaka kunipiga lakini alijizuia, alikua akikaa na kusimama ara kwa mara, kwa namna alivyokua niliogopa, lakini na mimi hasira zilishanipanda, sikua tayari kumsikiliza, nilimuambia kabisa siwezi kwenda shule kwani Mama anateseka. Baada ya kuona kuwa hawezi kunishawishi na kunibadilisha msimamo wangu aliamua kunywea, akakubalia na kuniambia kuwa nitakaa nyumbani atanitafutia uhamisho.


Aliniomba msamaha kwa kunikaripia na kunipiga akiniambia kuwa haitakuja kutokea tena, nilimuelewa. Mimi nina chumba changu lakini kutokana na hali ya Mama nilikua nalala naye chumbani kwake alipokua katelekezwa kwa Baba, kwakua mara nyingi Baba alikua halali nyumbani na siku akiwepo basi nalala chumbani kwangu hakua akilijua hilo. Usiku ule nilikua chumbani kwangu, nikijua kuwa Baba hajarudi kwani sikuiona gari yake niliamua kwenda chumbani kwa Mama kumpa kampani,.


Nilitembea mpaka chumbani kwa Mama, lakini ile nafika mlangoni nilisikia sauti ya Baba ikiongea taratibu.


“Nitakuua! Yaani nimekuweka hapa sijataka kukuacha kwakua watu wataniona mnyama lakini leo unataka kumgeuza mwanangu ili anichukie, umemuambia nini mwanangu!” Baba alikua akiuliza, nilimsikia Mama akikohoa kama vile anataka kuongea kitu lakini hawezi, ilikua kama vile anakabwa, sijui nilipata wapi ujasiri lakini niliusukuma mlango kwa nguvu nikigonga na kupiga kelele ili Baba aufungue kwani ulikua umefungwa kwa ndani.


Baba ambaye alikua anajua kuwa nimelala alikurupuka na kufungua mlango, taa ilikua imezimwa, alinipiga kikumbo pale mlangoni na kutoka kukimbia, sikumjali, niliingia ndani na kuwasha taa ili kumuangalia Mama. Nilimsogelea alikua hatingishiki wala nini, nilichanganyikiwa nikafanya kama watu wa kwenye TV kumuangalia mapigo yake ya moyo, hakukua na kitu, Mama alikua katulia tuli kitandani.


Kama hukusoma sehemu ya kwanza ya simulizi hii basi fuatilia katika ukursa wangu wa Instagram @iddimakengo ambapo utapata sehemu ya kwanza pamoja na muendelezo wa sehemu ya tatu.


ITAENDELEA….


SAFARI; MIMI, MAMA NA BABA PEMBENI!—SEHEMU YA TATU


Nilianza kumsukuma Mama ili atingishike lakini hakutingishika, sijui wazo lilikuja wapi nilimnyanyua kichwa kwa juu kidogo na kuanza kumtingisha huku nikimbonyeza kifuani, ghafla alianza kukohoa, alikohoa sana kama anatafuta pumzi.


“Baba alikua anataka kukuua kama kwenye gari!” Niliongea kwa hasira baada ya kuona kuwa kashaakaa sawa, aliniangalia kwa uchungu, macho yalikua mekundu sana kama vile alikua analia kutwa nzima ingawa alikua halii. Nilirudia tena maneno yangu nakumalizia kuwa namchukia Baba.


“Hapana mwanangu, hakua anataka kuniua, Baba yako ananipenda sana na anakupenda, sana, ile ilikua ni ajali na hapa tulikua tunacheza tu, hakua anataka kuniua….” Mama alijaribu kumtetee, nilipendwa na hasira na kutaka hata kumukuma au kumpiga makofi, lakini nikiangalia macho yaek nilimuonea huruma, hakua akilia lakini machozi yalikua yakimtoka, alijaribu kunyanyua mukono yake isiyokua na nguvu ili kunifuta machozo lakini alishindwa.


Nililazimika kumfuta mimi machozi, sikuongea chochote kwani nilikua na hasira na niliona kabisa kuwa Mama anaumia.


“Mwanangu usije kumchukia Baba yako hata siku moja, mimi nayeye tunaweza kugombana lakini bado ataendelea kubaki kuwa Baba yako, kamwe usije kumchukia wala kumkosea heshima…”


“Lakini mama…”


“Hakuna cha lakini, yule ni Baba yako, anakupenda sana na anakujali, ni lazima kumsikiliza kwa kila kitu, mambonyote anayofanya ni kwaajili yako, wewe na mdogo wako, anafanya kwakua anakupenda ndiyo maana nataka uende shule…”


Aliongea kwa kujilazimisha lakini alishindwa kumalizia, machozi yalianza kumtoka tena nikalazimika kumfuta.


“Mama nikienda wewe utabaki na nani hapa?” Nilimuuliza, alikaa kimya kwa muda kisha akaniambia.


“Kuna mfanyakazi, si kazi yako kunihudumia, wewe bado mtoto mdogo, hutakiwi kubeba haya majukumu, nenda kasome kapate elimu, utakuja kuisaidia familia yako, una mdogo wako wa kumuangalia, sitakua na amani nikijua kuwa husomi kwaajili yangu. nataka ubaki shuleni, msikilize Baba yako rudi ukasome.”


Alikua katika maumivu makali, si maumivu tu ya matendo aliyokua akifanyiwa lakini pia alikua katika maumivu ya kimwili.


“Mama una nini, mbona unakua hivyo….” Nilimuuliza baada ya kuona kama anapumua kwa shida, kabla ya kunijibu niliona pua zake zinatoa damu. Hazikua damu nyingi lakini ilionekana kama kuna kitu kimepasuka kwa ndani.


“Mbona pua zinatoa damu, vipi zinauma?” Nilimuuliza, alitingisha kichwa kusema hapana lakini nilijua kabisa anaumia, akili yangu ilitaka kumpeleka hospitalini lakini ningempelekaje.


Nilitoka kule chumbani na kumfuata Dada wa kazi, nilimuambia kuhusu Mama na kumuambia kuwa ntunatakiw akumpeleka hospitalini.


“Una hela wewe?” Aliniuliza. Nilimjibu sina, aliniambia hata yeye hana na hawezi kuhangaika na Mama, alianza kulalamika mambo mengi akisema kuwa hawezi kujihangaisha kwakua hata kumlipa hawamlipi hivyo anakaa pale kwakua ana mipango yake na ikikamlika anaondoka.


“Ningekua na pakuishi ningekua nishaondoka muda mrefu!” Aliongea hukua kiwasha TV kuangalia, hakujali chochote. Nilitoka na kurudi nyumbani kwa Mama, alikua kafunga macho kama vile kalal, niligopa sana, tangu ile ajali huwa naogopa sana, nikiona mtu kalala hata kipindi niko shuleni nilikua namuangalia mara mbili kuona kama yuko hai au la. Nilimkimbilia Mama na kumuamsha kumuangalia kama yuko hai, alinyanyuka na kuniambia kuwa anajisikia vizuri nisihangaike nimuache alale.


Pamoja na kusema hivyo lakini hakua akiendelea vizuri, nilimuambia niende kumahs amajirani alikataa katakata na kuniambia yeye yuko vizuri. Sikua na namna zaidi ya kulala pembeni yake, nilipitiwa na usingizi mpaka asubuhi, Mama ndiyo alikua mtu wa kwanza kuamka, niliamka na kwenda kumfuata dada ili kuandaa chai lakini hakuepo, nilikagua chumba chake na kukuta kuwa ameshachukua kila kitu chake, nilikuja kumuambia Mama, hakuonekana kushtuka.


“Mwanangtu hata kama ni mimi nisingekaa, ana ziadi ya miezi sita hajalipwa pesa yake…” Mama aliongea kwa uchungu, nilimuangalia na kumuambia kuwa siwezi kwenda shule tena. Alinisihi na kunibembeleza lakini nilimuambia hapana. “Nikiondoka hapa Mama utakufa, Najua Baba hatoi chakula nikiwa sipo, lakimi mimi ananipenda hawezi kuniacha nife njaa, namjua, nikiondoka ukabaki peke yako basi atakuacha ufe humu ndani lakini mimi nikiwa nipo hawezi kukufanya chochote, najua ananipenda na anaogopa nikimchukia, nitabaki kukulinda.”


****


Baba yangu alikua ananipenda kuliko kitu kingine chochote kile, kila wakati alikua akijaribu kunifanyia mambo ili kuniridhisha, alitaka nimuone Baba mwema, hakutaka nijue namna alivyokua akimnyanaysa Mama. Nilikuja kugundua mateso aliyokua akipitria Mama baada ya kuanza kumhudumia. Alikua na makovu mengi sana mgongoni na kwenye mapaja, alikua kachanywa na viwembe mgongoni na alikua kachomwa na pasi kwenye mapaja.


Ingawa Mama hakuwahi kunielezea wala kuniambia kilichokua kimetokea lakini nilikua na akili zangu, nilikua naona na nilijua kuwa yale yalikua ni mateso aliyokua akiyapata kutoka kwa Baba. Kila siku mama alinisisitiza kumpenda Baba, alikua akisingizia ajali kuwa kapata yale makovu kwa ajali lakini wapi! Nilishajua sababu na sikudanganyika, mara kadhaa nilijifanya mjinga kumuamini ili ajisikie vizuri lakini moyoni nilijua kabisa kuwa Baba yangu ni mshenzi wa kutupwa.


Nilimuambia Baba sitaenda bweni na kama akilazimisha basi aje kuchukua maiti shuleni, nilikua namaanisha na kweli alikubali nibaki kutwa kumhudumia Mama. Ingawa nilijaribu sana kumpenda lakini baada ya kugundua ushenzi wake kila kitu kilibadilika, tulianza kuwa kama paka na panya, sikua nikimheshimu tena kama Baba na hata alipokua akiniletea zawadi nililazimisha tu kuzipokea na kucheka lakini sikua na furaha kabisa.


Maisha yaliendelea hivyo hivyo, Baba liatafuta  mfanyakazi mwingine lakini nilijua kabisa hakutafuta kwaajili ya Mama bali kwaajili yangu. Alitafuta mtoto mdogo kabisa, ingawa kiumri alikua mkubwa kwangu lakini kiumbo nilimzidi na alionekana dhaifu, singeweza klumsogeza Mama. Pale nyumbani Baba alikua anakuja mara moja moja, sijui alikua anaishi wapi kwani hata Anti Rahma aliyekua akiishi kwake mwanzoni walishaachana na alishaolewa.


Alikua anaweza kuja kukaa siku mbili na kuondoka wiki bila kurudi nyumbani, hakua akileta tena marafiki zake na hakukua na ndugu aliyekua anakuja kumuangalia Mama. Kwakifupi ni kama tulikua tumetegwa na nilijua fika Baba anatamani kumfukuza Mama ila anaogopa nitaondoka naye kitu ambacho alikua hakipendi. Niliendelea na masomo mpaka nilipofika darasa la saba, nilijitahidi sana kufanya bizuri darasani ili kupata zawadi kutoka kwa Baba na kuziweka kwaajili ya Mama.


Kama kawaida yangu sikuwahi hata kushika namba mbili darasani, pamoja na hali ngumu ya pale nyumbani lakini nilijitahidi sana katika masomo. Kila siku Mama alinisisitiza kusoma na kusoma ili nije kuwa na maisha yangu. Hali ya Mama ilikua inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, mwanzoni ilikua rahisi kumsogeza kwani alikua anaweza kujinyanyua kidogo  lakini kutokana na kulala sana, kutokana na kuacha kuafnya mazoezi mwili ulilemaa na ikafikia wakati hawezi kujinyanyua tena.


Alikua mzito sana hivyo ikawa shida sana kwa mimi na binti wa kazi kumnyanyua, alibakia kulala tu hivyo kila kitu akawa anafanyia pale chumbani kitandani. Tulichokua tunafanya ni kumtandikia mpira kama mtoto mdogo anayekojoa kitandani,asubuhi tukiamka kazi ya kwanza ni kumuangalia kama kajisaidia, tunamgeuza taratibu palepale kitandani na kubadilisha mpira pamoja na mashuka. Kwakua hatukua tunaweza kumnyanyua tulikua tunamsukuma kama kumviringisha.


Wakati mmoja anamsukuma na kumshikilia mwingine analazimika kuweka shuka chini yake au mpira. Ilikua ni kazi ngumu sana ambayo tulilazimika kuifanya. Wakati huo nilikua na miaka 13 tu na dada yetu wa kazi alikua na miaka 17 ingawa alionekana mdogo kwangu. lilikua ni zoezi la kila siku, mama alikua kakakata tamaa kabisa, nilimuona katika maumivu makali lakinia lijitahidi nisimuone kuwa anaumia.


Kutokana na ugumu wa kumsogeza hata kumvalisha nguo ilikua shida, mara nyingi ili kurahisisha kazi tulilazimika kumfunika tu na vitenge au shuka. Mara nyingi Mama alikua akiniulizia kuhusu Sudi (sio jina lake halisi), mdogo wangu ambaye wakati huo alishakua mkubwa ana miaka minne lakini alikua hajawahi kuletwa pale nyumbani kumuona Mama. Kile kitu kilikua kikimuumiza, aliishia kuona picha zake katika simu kwani Baba alikua hataki kabisa amuone.


Alikua akisema ni bado mdogo asubiri mpaka apone ndiyo atamleta pale. Nilikua naumia sana kwani sikuona dalili zozote za Mama kupona, hakua akipatiwa matibabu ya aina yoyote zaidi ya Panado ambazo ni mimi nilikua nikienda kumnunulia na hazikua zikimsiadia. Katika wiki mbili za mwisho kumaliza darasa la saba nilitakiwa kwenda kukaa shuleni, zilikua ni taratibu za shule yetu, tulitakiwa kuandaliwa miezi miwili kabla lakini nilikataa.


Babaa linibembeleza sana nikakataa, lakini zilipobakia wiki mbili alinilazimisha na kuniambia kuwa atamleta Shangazi kumhudumia Mama, kweli Shangazi alikuja ndipo nilikubali kuondoka kwa shingo upande. Nilienda kujiandaa na mitihani na nilipomaliza nilirudi nyumbani, lakini nilimkuta tu binti wa kazi na nilipomuuliza kuhusu Shangazi aliniambia kuwa aliondoka siku ileile na mimi nilipoondoka hivyo katika wiki mbili zote alibaki peke yake.


Nilimkuta Mama katika hali yake ileile, alilazimisha tabasamu na kujifanya yuko sawa, nilimuangalia na kumkagua kama yuko sawa, nilimuona yuko sawa. Lakini kwa kukaa kwenye kile chumba kwa nusu saa nilihisi kitu tofauti, kuna harufu ilikua inatoka. Kulikua na harifu ya kitu kama kimeoza. Pamoja na ugonjwa wa mmaa, pamoja na kwamba alikua anajisiadia pale kitandani lakini kwenye kitu ambaho nilikua makini nacho ni usafi.


Nilihakikisha kila siku namsafisha Mama vizuri na kusafisha chumba kwani nilijua kuwa yeye analazimika kulala pale kila siku, kila saa na kila daika. Kama kukiwa na harufu mbaya basi anaumia mara mbili, kuumia kwa harufu na maumivu ya ugonjwa. Nilimuita dada wa kazi na kumuuliza kama amesikia harufu, alinijibu hapana, ni kama alishaizoea flani hivi, sikukubali nilianza kukagua chumba kizima kuangalia kama kuna mdogu kafa lakini hakukua na kitu.


Pamoja na uchafu wa kawaida lakini sikusikia kitu kingine, nilikosa na kuamua kutulia. Jioni mama alijisaidia, nilimuita dada ili kunisaidia kumsafisha. Nilimuambia anisaidie kumnyanyua ili nitoe mpira aliokua kalalia, ile kumnyanyua tu ndiyo harufu ilijaa chumba kizima. Nilijajaribu kutoa ule mpira aliokua amelalia Mama na kuana kukutana na wadudu, wale wadudu ambao hukaa kwenye nyama iliyooza, walikua ni wengi na kulikua na harufu kali, nilimuangalia Mama mgongoni nikajikuta naanza kulia bila kujijua…


Asha anarudi nyumbani na kukuta wadudu katika kitanda cha Mama yake, unafikiri wanatoka wapi? Nikwanini imekua hivyo? Usikose sehemu ya nne, hakikisha unanifuatilia Instagram @iddimakengo na Facebook ni Iddi Makengo


ITAENDELEA…


SAFARI; MIMI, MAMA NA BABA PEMBENI!—SEHEMU YA NNE!


Mama alikua kalazwa chini hajasogezwa hasa sehemu ya mgongo, kutokana na uzito wake Dada wa kazi alikua hawezi kumnyanyua mzimamzima, alichokua akifanya kama akijisidia ni kupanua miguu yake na kusafisha kidogo kwa chini, katika kumuosha upande wa juu alikua akimfuta kwa maji bila kumsogeza. Kwa sbabau hiyo maji yalikua yakiingia chini ya mgongo, kwakua tulikua tukimlaza kwenye mpira ilimaanisha maji yalikua hayawezi kupenye chini kwenye godoro na kutoka.


Alichokua anafanya nikuwa kama maji ya kitokea pembeni anafuta basi, kwa sbabu hiyo kukaa wiki mbili bila kusafishwa na ile hali ya uchafu wa maji na wakati mwingine hata mkojo na kinyesi alikua hasafishwi vizuri kulianza kuleta wadudu na mgongo ulianza kuoza.  Mgongo ulikua unatoa harufu mbaya sana.


“Inamaana hujawahi kusikia hii harufu?” Nilimuuliza Dada kwa hasira, alikua mkubwa kwangu lakini niliona kama hafikirii vizuri.


“Nasikia mara moja moja lakini sikuwahi kuona wadudu…” Aliongea kwa suti ya kudanganya danganya alikua akiniogopa sana kwani  nilikua nimekasirika kupita maelezo. Mgonngo ulikua umeoza kuanzia kiunoni yanapoanza makalio mpaka mabegani, kwa kumuona nilijua kuwa Mama alikua katika maumivu makali, nilijaribu kumsafisha lakini hakuonekana kusikia chochote, hakuonekana hata kujua kuwa huko nyuma ya mgongo wake kuna kidonda kikubwa namna ile.


“Mama husikii maumivu?” Nililazimika kumuuliza kwani wakati naondoka alikua kapooza tu sehemu ya kiuno kwenda chini na ingawa alikua hawezi kujisogeza kwa kukosa nguvu lakini kama ukimshika sehemu ya juu alikua akihisi, lakini siku ile hakuhisi kitu. “Maumivu gani mwanangu, nawewe una wasiwasi wa bure, hembu kapumzike mimi niko sawa kabisa…” Aliongea kwa kunitania, nilishtuka zaidi kwani mule ndani kulikua na harufu kali nilishangaa ni kwanini Mama alikua haisikii au kuilalamikia.


“Mama unanisikia ninavyokugusa?” Nilimuuliza, alionekana kunishangaa, aligeuza shingo kwa shida kuangalia mikono yangu ikimguisa lakini hakuhisi chochote.


“Mama unanisiki?” Nilimuuliza tena na tena lakini hakuonekana kupata hisia zozote.


Nilipaniki na kujua kuwa Mama kapooza mwili mzima, nilimuuliza kuhusu harufu akaniambia hasikii harufu yoyote. Bila kujijua nilijikuta naanza kutokwa na machozi, mnama alianza kunibembeleza, alitaka kunishika lakini mikono yake ilikua hata haitingishiki tena, nilishangaa kwani wiki mbili kabla wakati naondoka hali yake haikua mbaya kiasi kile.  Nilikasirika na kumuita dada nnje, nilimuuliza nini kilikua kimetokea na ni  nani alikua amekuja, alimuacha Mama na nani lakini hakunijibu.


Majibu yake yalionekana kama alikua na ugoa, kuna kitu alikua ananificha.


“Baba alikuja lini?”Nilimuuliza, alikaa kimya kama kuna kitu alikua anaficha.


“Alikuja kumuona Mama?” Nilimuuliza, hakuongea lakini alitingisha kichwa kama kukubali kuwa wakati naondoka Baba alikuja kumuona Mama. Sijui kwanini lakini nilipata wasiwasi kidogo, nilikua simuamini Baba na nilihisi labda kuna kitu alikua kamfanyia Mama ndiyo maana hali yake ilibadilika ghafla kiasi kile.


Niliachana na dada na kurudi nyumbani, nilimfuata Mama na kumuuliza kama Baba alikua kaja pale na ni kitu gani alikua kamfanyia, alinyamaza kimya hakusema chochote, nilijikuta naanza kukasirika, machozi yananitoka kama maji.


“Baba yako hawezi kunifanyia kitu, ni mume wangu ana haki ya kuja, mwanangu mpende Baba yako yehe ndiyo utabaki naye, mimi sitakua nawe kila siku, Baba yako anakupenda sana…”


Mama aliongea, machozi yalikua yananitoka, kwa jibu lake hilo sikua na haja ya kujiuliza wala kutaka kujua Baba alikuja na alifanya kitu kibaya. Mara nyingi tangu Mama kuanza kuumwa na mimi kujua unyanyasaji wa Baba kila mara walipokuwa wanagombana au Mama kuniona nimemkasirikia Baba alikua akinikumbusha kuwa ni baba yangu na ananipenda. Niliumia sana kwani kwa hali aliyokua nayo Mama ulikua ni unyama wa hali ya juu kumtukana achilia mbali kumpiga.


Kwa hali aliyokua nayo Mama nilijua kabisa anahitajika kwenda hospitalini, nilichukau simu ya Mama ambayo mara nyingio ndiyo tunaitumia kuongea na wetu na kupiga namba ya mjomba. Kaka yake na Mama. Nilimuambia kuwa Mama anaumwa na hali yake ni  mbaya sana hivyo anahitajika kwenda hospitalini. Nilimualezea kila kitu lakini jibu lake lilinifanya kutamani kutapika.


“Baba yako yuko wapi?” Aliniuliza, nilishikwa na kigugumizi kuweza kuongea, nilitamani kumuambia kuwa nahisi Baba ndiyo kamfanyia haya yote lakini nilijua kuwa Mama atakasirika.


Nilimuambia kuwa hayupo kasafiri kikazi na sijui kama anarudi lini. Nililazimika kudanganya ingawa nilikua naumia.


“Basi nitampigia shemeji kujua kuwa tufanye nini kama humpati kwenye simu basi nitamtafuta mimi, ngoja niongee naye halafu nakuja kumchukua.” Aliongea na kukata simu, nilibaki na hasira tu, nilirudi chumbani na kumuangalia Mama kwa hasira zaidi.


“Kwanini hutaki kuwaambia akina mjomba kuwa Baba anataka kukuua? Unataka ufe ndiyo useme?” Nilimuuliza Mama kwa hasira.


Kitu cha ajabu nikuwa, badala ya kujibu swali langu alianza kunifokea na kuniambia kuwa mimi bado ni mtoto sijui maisha ni nini, akaanza kunipa risala kuhusu Baba kunipenda, nilikasirika na kutoka nnje. Sikukaa nusu saa Baba alikuja, kwanza alishangaa kuniona pale, alishangaa kuona nimerudi kutoka shule bila kuniambia, alinichangamkia na kuingia ndani,a lijifanya kumuuliza Mama hali yake na kutaka kujua ni kwanini hakumuambia kuwa anaumwa.


“Wewe mshenzi kabisa, unataka kunigombanisha na watu! Ni kiherehere gani cha kumuambia mtoto awapigie ndugu zako kuwa mimi sipo?  Kaka yako tumekutana asubuhi nikamuambia unaendelea vizuri sasa unamtuma mtoto adanganye nimesafiri, unataka watu wanione vipi? Unatka mimi kuonekana kama mshenzi, umenigombanisha na mwanangu sasa unataka kunigombanisha na kila mtu hapa mtaani? Una nini lakini wewe mwanamke, mimi nakusaidia lakini hata huonyeshi shukurani? Unataka nikufanyie nini?”


Nilikua malngoni nikisikiliaza namna ambavyo Baba alikua akimgombeza Mama, nilihisi kitu kibaya hivyo sikusubiri aanze kumpiga. Nilifungua mlango harakaharaka na kuingia, Baba alishtuka, aliniambia nitoke kwani anamuandaa Mama kumpeleka hospitalini.


“Siku nyingine kama Mama yako kazidiwa unakuja na kuniambia mimi sio kutangaza tangaza matatizo yetu kwa watu! Hao unaowambia kila siku kama wangekua wanampenda si wangekuja na kumchukua wakamhudumia wao! Kwanini wamemuacha, kwanini hawamtaki!”


Aliongea kwa hasira, alijifanya kumsagisha Mama kumtrafutia nguo na kumpa pole, alijishaua na maneno mengi lakini nilijua kuwa yote hayo alikua anajikosha kwangu. Baada ya kumaliza kumuandaa, alimnyanyua, alimnyanyua na kumuweka katika kiti chake, ulikua ni mdua mrefu umepita tangu Mama kukalishwa pale kwani mimi na Dada tulikua hatuwezi kumnyanyua, alikua hawezi hata kukaa mwenyewe tena tofauti na zamani tulilazimika kumshikilia mkapa kwenye gari tukampeleka hospitalini.


****


Hospitalini kulikua na watu wengi, kulikua na idadi kubwa ya ndugu na marafiki ambao zaidi ya nusu hata nilikua sijawahi kuwaona, walikuja kumuona Mama baada ya kusikia kuwa hali yake ni mbaya amelazwa. Karibu wote walikua wakimpa pole Baba, walikua wakimuonea huruma kwa namna alivyokua kahangaika na Mama. Hakuna aliyejali hali ya Mama, kila mmoja alihakikisha kuwa Baba kamuona na kampa pole yake. Hali ya Mama ilikua inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, ilifikia hatua akashindwa hata kuongea.


“Ameteseka sana muache tu akapumzike!” Watu wawili walikua wanaongea, nilikua nimekaa pembeni kabisa, nimetoka katika chumba alichokua Mama kwani kulikua na watu wengi wanakuja na kuondoka na kujifanya kama vile wanajali. Katika kipindi chote Mama anaumwa nyumbani, katika kipindi ambacho mimi na dad andiyo tulikua tunahangaika sikuwahi kuona hata mtu mmoja akija hata kumsalimia.


Mara chache sana baadahi ya ndugu hara dada zake mama walikua waki9piga simu kumsalimia. Hata wale ambao niliona kabisa Mama anawasaidia, wale nilikua nikiwaita Mama wadogo, Shangazi sijui nani hawakuja kumuona Mama. Mara chache ukikutana na mtu njiani alikua akikuuliza kuhusu Mama na wengine walijua ni kama kashapona, kila mtu alikua bize na maisha yake, lakini sasa baada ya kusikia tu hali yake imekua mbaya kapooza mwili mzima basi nawaona wanakimbilia hospitalini na kujifanya wanajali.


Baba alionekana shujaa, nilichogundua na kitu kilichoniuma kuliko vyoye nikuwa hakuna mtu aliyekua akimjua Baba, mbele za watu Baba alionekana kama malaika, mtu aliyemchukua mwanamke ambaye alikua anaumwa, hana mbele wala nyuma na kuamua kuishi naye.


“Huyu Baba kateseka sana, wangekua ni wanaume wengine angemuacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine! Mwanamke sijui mwaka wa ngapi yuko kitandani lakinia navumilia, Baba wawatu hata kuoa mwanamke mwingine kashindwa…”


“Labda anajisikianvibaya, wakati anapata ajali yeye ndiyo alikua akiendesha gari….”


“Hapana unawajua wanaume wa siku hizi, kwanza kabisa angemrudisha kwao aende kuhudumiwa na ndugu zak, wanaume unawajua wewe…”


“Masikini huyu dada ndugu zake ndiyo walikua wanamtegemea. Nimefanya naye kazi, alikua na roho nzuri sana, hata pale ofisini kuna watu alikua anawasaidia, ndugu zake kawasomesha wote lakini ukiangalia hapa mwanaume pekee ndiyo anahangaika naye. Nimemuona tu Kaka yake mmoja hapa sijui na mdogo wake tana kaja nakuondoka eti kaolewa yuko bize na familia.”


Baadhi ya watu walikua hawanifahamu, wengi waliniona nikiwa mdogo sana, walikua wakiongea kuhusu Mama kana kwamba vile wanaishi ketu. Hawakujua kilichokua kikiendelea, walikua wakimsifia Baba na kumuona kama malaika. Kwa kupenda kusifiwa na kuonekana kama malaika Baba alikua anajali sana, muda mwingi alikua hospitalini,a likua akiongea na masaktari na alitaka kuonekana kuwa anamjali sana Mama  na  ndoa yake iko vizuri, alimlete mdogo wangu Sudi kumuona Mama, alikua hamfahamu vizuri zaidi ya kuambiwa kuwa huyu ndiyo Mama yako.


Lakini Mama hata hakumuona, siku mbili tu baada ya Mama kufikishwa hospitalini hali yake ilizidi kuwa mbaya. Alisafishwa kidonda lakini aliambiwa kuwa kimeleta kitu kama sumu kwenye mwili, alitundikiwa drip nyingi lakini hali yake ilizidi kuwambaya, alipoteza fahamu na kuwa anapumulia kwa mashine. Hali ilikua mbaya, kila mtua liogopa na kila mtu alijua kuwa anakufa, karibu kila mtu niliyekutana naye ambaye alikua akinifahamu aliniambia kuwa atapona nisiwe na wasiwasi.


Lakini kila niliokutana nao waliokua hawanifahamu, hawajui kama mimi ni mtoto wake walikua wakisema ni bora Mama kupumzika kwani kateseka sana. Walikua wakimuonea huruma Baba na kumpa moyo. Sijui kwanini lakini mimi sikuwaza kuhusu kufa kabisa, nilikua kama nawashangaa, nilikataa kuondoka hospitalini na hata nilipopelekwa nyumbani kinguvu basi nilitoroka na kurudi, sikuwahi kutoa hata chozi moja, moyoni nilikua najua kabisa Mama atapona na kunyanyuka kabisa, sikua na wasiwasi wowote na nilishangaa kila mtu aliyekua akiongea kama vile Mama hatapona.


Wiki mbili zilipita Mama akiwa hospitalini, hali yake bado ilikua tete kwani mara kwa mara ilikua inabadilika na kuwa mbaya na wakati mwingine inakua nzuri ingawa bado alikua akipumulia mashine. Kila siku Baba alikuja hospitalini, nilijua kabisa hakuwa na upendo bali alijua kuwa Mama anakufa na alitaka watu kumuona kuwa alikua mume bora, ndugu zake nao walikua wanakuja, sanasana walikuja kumuona Baba, kutokana na uwezo mkubwa wa kifedha aliokua nao Baba kila mtu alikua akijipendekeza kwake hata ndugu wa Mama.


Alikua wakimuonea huruma kama vile yeye ndiyo alikua anaumwa. Mimi sikusema chochote, nilikua na hasira nyingi lakini kamwe sikuwahi kunyanyua mdomo kuwaambia watu ukweli kuhusu Baba. Siku moja nilikua nimesimama nnje ya chumba alichokua kalazwa Mama, bado nilimuona Nesi akimfungua mipira ya Oxygen, nilifurahi kwani nilijua kuwa hali yake inaendelea vizuri labda kaweza kupumua mwenyewe. Harakaharaka niliingia ndani, ingawa watu walikua hawaruhusiwi kuingia lakini nililazimishia, nilianza kumuita Mama! Mama! Huku nikimsukuma lakini hakuitikia, nilimgeukia nesi na kumuuliza mbona anatoa mipira ya kupumulia wakati hapumui alishindwa kunijibu, alinyamaza kimya hukua kiniangalia kwa huruma, machozi yakikua yakimlenga lenga.


Unataka kujua ni kitu gani kimemtokea Mama yake, basi hembu hakikisha unaFollow ukursa wangu wa Instagram @iddimakengo utakutana na kila kitu huko.


ITAENDELEA…..


SAFARI; MIMI, MAMA NA BABA PEMBENI! —SEHEMU YA TANO


“Mama kafanya nini? Mbona mnamuondoa hiyo mipira, Baba si alisema inamsaidia kupumua? Mbona mnamuondoa?” Niliuliza maswali mfululizo baada ya kuona macho ya Nesi, yale matumaini kuwa Mama alikua anapata nafuu yaliondoka kabisa na nilihisi kama vile kuna kitu kibaya. Lakini kabla nesi hajanijibu chochote Baba aliingia, aliniita na kuniambia nitoke. Nilikayaa na kumuambia kuwa nataka kujua kama Mama kafariki au la? Hakunisikiliza alianza kunilazimishia na alipoona sitaki kutoka alinishika na kunivuta nnje.


Nilianza kulia kwa nguvu nikisema namhitaji mama namhitaji Mama, watu waliokua pale walianza kunipa pole, wote walijua kuwa nalia kwakua Mama ameshafariki dunia na walijaribu kunituliza. Mmoja wa watu waliokua pale nnje alikua ni Mama mdogop, mdogo wake kabisa na Mama, baada ya kuona nalia vile alianza kupiga kelele.


“Dada yangu umeniacha! Dada umeniacha! Nitamuita nani dada! Ulinisomesha mpaka chuo leo hii umeniacha…”


Aliendelea kupiga kelele, Baba alinibabe mpaka kwenye gari, njia nzima nilikua nalia nataka kujua kwanini mama alikua anatolewa ile mipitra na kwanini watu wanalia kuwa mama kafariki.


“Acha ujinga, acha kuwapanikisha watu Mama yako hajafa lakini wewe unalia mpka kila mtu anajua amekufa! Atakufa lakini hajafa bado!” Baba aliniambia mameno ambayo mpaka mleo sijui ni kwanini alisema hivyo. Kwanza alinipa habari nzuri kuwa Mama yangu bado yupo hai, lakinia limalizia kwakuniambia kuwa atakufa.


Sikumuelewa kabisa Baba alichokua akikiongea, hata yeye alikua haelewi, alinifokeafokea sana na kuniambia naiche utoto kwani nawaumiza watu wengine.


“Au unafikiri wewe peke yako ndiyo unampenda Mama yako? Alikua na ndugu yule unafikiri wanajisikiajae, nimekudekeza sana ndiyo maana hutaki kukua wewe!” Aliongea tena kwa hasira, bado sikumuelewa, nililazimika kumuuliza kama Mama bado yupo hai na ni kwanini alikua anasema kuwa atakufa.


“Mama yako hajafa lakini tumeona kuwa hawezi kupona, tumeamua kumrudisha nyumbani akapumzike, ile mipira kila siku inazidi kumuumiza tu na ni gharama watu kuja kila siku kumuona hapa…” Aliongea na kunielezea maneno mengi ambayo hata siyakumbuki, mimi nilishikilia tu kuwa Mama yuko hai, sikujali hilo alilokua akilisema kuwa sijui akapumzike wala nini. Kwa wakati huo sikuelewa kwanini walikua wakimtoa hospitalini na kusema akapumzike nyumbani, hata mimi niliona kama ni vizuri akitolewa ile mipira kwani niliona kama vile inamuumiza.


Nilifurahia sana kuwa Mama anatoka hospitalini nikiamini kuwa mtu akiruhusiwa kutoka hospitalini basi hali yake ni nzuri. Sikujua kuwa wameona kuwa hawezi kupona na walikua wakimleta nyumbani ilia kafie nyumbani. Nilinyamaza na kurudi ndani, nilikuta Mama mdogo na ndugu wengine bado wakilia, hakuna aliyekua kawaambia kuwa Mama bado yuko hai, mimi sikuwajali kwani niliona kama wanafiki tu.


Mama mdogo aliyekua akigalagala chini na kumsifia Mama baada ya kuhisi ashakufa alikua hajawahi kuja kumuangalia hata mara moja kipindi anaumwa, kila siku alikua bize tu na ndoa yake na sasa hivi anajifanya kumpenda.


“Mama yangu hajafa na hawezi kufa!” Nilijikuta nawaambia huku nikiwazomea kama vile nawasuta, Baba aliona kile kitendo na kunikemea lakini sikujali, niliwaona wakinyamaza kwa aibu. Wakati huo Mama alikua akitolewa hospitalini, alikua akitolewa na kitanda kikisukumwa mpaka kwenye gari.


Alikua kalala kimya kama mtu aliyekua kwenye usingizi mkali, ingawa kila mtu alimuangalia kwa jicho la kukata tamaa lakini mimi nilimuangalia kama mtu ambaye alikua amelala na wakati wopwote ule atanyanyuka. Aliingizwa kwenye gari na kulazwa vizuri kisha wote tukaanza safari ya kurudi nyumbani. Ndugu wengine walikuja na magari yao, nyumba ilijaa watu na walikua wanapika kama vile kuna sherehe au tayari kuna msiba. Mama aliingizwa ndani, mimi bado nilimuona kama kalala na nilijua wakati wowote atanyanyuka na kuniongelesha.


Kwakumuangalia ni kama alikua ameoata nafuu kwani kwa nnje alionekana msafi, wakati anachukuliwa na kupelekwa hospitalini kwa alikua kaoza, anatoa na wadudu lakini sasa vidonda vilikua vimekauka ingawa alikua haongei wala kujitingisha, lakini ukimuangalia alikua bado anapumua. Nilikaa naye chumbani kwake mpaka na mimi nikapitiwa na usingizi. Nilikuja kuzinduka usiku giza lilishaingia, watu walishaondoka isipokua baadhi ya ndugu wa Baba, Shangazi, Baba mdogo na Bibi mdogo ambaye alikua anazaliwa tumbo moja na Bibi yangu.


Walikua wamekaa sebuleni wakiongea, nilipotoka walinyamaza na kuniambia nikae nao. Waliniongelesha mambo mengi kutaka kujua kuhusu shule, Shangazi akinitania kwanini sitaki kwenda kwake, waliongea mambo mengi sana lakini mimi wala sikuwasikiliza. Akili yangu ilikua bado kwa Mama na niliwaona wote kama wanafiki tu, nilikua na hasira sana na nilitamani hata kuwafukuza.


“Huyu niende naye akakae na mdogo wake…” Shangazi alijiongelesha, sijui kwanini lakini nilijikuta natetemeka kwa hasira nilimuangalia kwa hasira mpaka mwenywe akajishtukia.


“Ngoja akae kae na Mama yake hapa labda atapata nafuu,…”Baba aliniona namna nilivyokua nikimuangalia Shangazi na kwakua alikua anajua naweza kuropoka basi alizuga. Nilinyanyuka bila kusema kitu chochote na kwenda jikoni, lakini wakati naondoka hata sijafika ndani nilimsikia Bibi akisema.


“Utafute mwanamke mwingine, umekaa peke yako kwa muda mrefu, mke wako hata nyanyuka tena, umri unaenda watoto wawili hawatoshi, tunajua unampenda mke wako lakini alishakufa muda mrefu hivyo hutakiwi kuomboleza sana…”


Nilitamani kugeuka na kuwaambia kuwa Mama yangu bado yupo hao, kuwaambia kila kitu alichokua akikifanya Baba kwani walikua wanamuona kama malaika lakini nilishindwa, nilitembea harakaharaka mpaka jikoni. Huko nilikuta dada wa kazi akiwa na Mama mdogo, mke wa baba yangu mdogo, sikutaka kukaa kwani naye nilikua nikimchukia, nilirudi chumbani kwa Mama kumuangalia. Taa ilikua imezimwa hivyo nilivyoingia niliiwasha na mwanga mkali ukamulika.


“Zima hiyo taa unaniumiza macho…” Ilikua ni sauti ya Mama, aliongea kama vile ndiyo ametoka usingizini, nilijikuta nashikwa na butwaa, sikujua hata nini cha kusema, nilisimama tu nikimuangalia sijui nizime taa au niache ikiwaka nimuangalie tu.


“Njoo basi unikumbatia, au ulijua kuwa nimekufa? Bado una kazi mwanangu hata sifi leo wala kesho…” Aliongea safari hii nilimuona akitabasamua, alikua akijaribu kunyanyua mikono lakini ilikua hainyanyuki sana, ilikua ikinyanyuka kidogo kama kipindi kile nilipomuacha wakati naenda shule. Nilimsogelea Mama na kumkumbatia, nilitamani kupiga kelele lakini sikutaka mtu yeyote kingia kwani nilijua fika hawatafurahia, nilikaa pale kitandani mpaka nilipopitiwa na usingizi na kweli hakuna mtu hata mmoja ambaye aliingia.


***


Asubuhi nilikua ndiyo mtu wa kwanza kuamka, hakuna mtu aliyekua ameingia katika kile chumba hata kuja kuuliza kama Mama amekula au la, kwa bahati mbaya hata mimi nilikua sijala hivyo niliamka nikiwa na njaa sana. Lakini kabla ya kufanya chochote nilimgeukia Mama ambaye bado alikua kalala, niliangalia mapigo yake ya moyo nakuona kama bado anapumua. Ilikua ni alfajiri sana ingawa mwanga ulishaanza kuingia, nilienda kwenye friji kuangalia kama kulikua na chakula lakini hakukua na kitu.


Nilitoka lakini nilipofika sebulani niligundua kuwa mlango wakutoka nnje ulikua umefunguliwa, nilitoka ili kuangalia ni mtu gani alikua ameufungua asubuhi yote ile. Nilitembea taratibu mpaka kwenye gari ndipo nilisikia mazungumzo kati ya Baba na Shangazi.


“Nawahi kazini nitakuja kwenye saa nne kuwaangalia?”


“Si ungemuangalia kwanza wifi kama kaamka?” Shangazi alimuuliza.


“Nimewachungulia walikua bado wamelala, hawezi kuamka na sikutaka kumuamsha binti yangu, anampenda sana Mama yake, muache afurahie kipindi hiki cha mwisho mwisho.” Baba aliongea hukua kiingia kwenye gari.


“Kwahiyo mimi nitakaa hapa mpaka lini?” Shangazi alimuuliza.


“Sijui, huyo ni wifi yako, haitaeleweka vizuri kama tumemchukua hospitalini katika hali ile halafu akakosa mtu wa kumhudumia. nataka ukae hapa mpaka Mungu atakapomchukua, najua ni kazi nzito lakini Asha ashakua mkubwa, anaelewa kila kitu, anajua kuwa kipindi kile uliahidi kumhudumia Mama yake lakini hukufanya hivyo. Nataka kabla Mama yake haajfariki basi abaki na picha nzuri, sitaki wanangu kuja kunichukia kwa mtu ambaye ahsakua maiti tayari, kaa siku mbili tatu tutaona hali yake inaendeleaje?”


Walikua wanaongea bila wasiwasi wowote, kwa namna walivyokua wakimuongelea Mama ni kama walikua wakiomba afe wakati wowote. Nilijua kuwa Mama hakurudishwa nyumbani kwakua hali yake ni nzuri bali alirudishwa kwakua walikua wanajua kua hawezi kupona, walimrudisha ili kuja kufia nyumbani. Baba aliingia kwenye gari na kuondoka, kuona vile nilijua fika Shangazi ataingia ndani, sikutaka anione hivyo nilikimbia harakaharaka na kuingia chumbani, nilirudi kitandani na kujifanya kulala mpaka kulivyopambazuka.


Baada ya kupambazuka nilitoka na kumkuta Shangazi akiandaa chai, nilimsalimia akaitikia vizuri tu huku akinichangamkia.


“Halafu jana wewe hukula?” Aliniuliza huku akinishika mavega kama Mama anaye jali mwanae.


“Nilikua nimeshiba Shangazi…”


“Ulishiba wapi acha uongo, hembu kanawe uso kisha uje unywa chai mwanangu, umechoka sana, acha kumuwaza Mama yako atapona tu kwa nguvu za Mungu…” Aliongea, sikumjibu chochote, nilienda kunawa uso kisha nikachukua maji kwaajili ya Mama, nilishazoea kumsafisha, nilifika chumbani kwake, alishaamka hivyo nilichukua maji na kuanza kumnawisha.


Alionekana kuwa na nguvu na aliongea vizuri tu, alikua kama mwanzoni kipindi namuacha.


“Vidonda haviumi?” Nilimuuliza alikua na maumivu lakini hakukiri, baada ya kumaliza kumnawisha uso nilirudi na kuchukua chai, nililaribu kumpa lakini alishindwa kunywa, nilienda kumpikia uji lakini nilikuta tayari dada ashampikia, niliuchukua na kuja kumlisha. Mpaka wakati huo Shangazi alikua hajaingia chumbani wala kuulizia hali yake, alikua sebuleni yuko bize kuangalia TV. Kwenye saa nne hivi watu walianza kuja, walewale waliokua hospitalini jana yake ndiyo walikuja.


Walionyesha nyuso za huzuni, ni kama wote walitaka Mama afe au walijua atakufa hivyo walijifanya kujiweka karibu na sisi. Mpaka wakati huo nilikua sijamuambia mtu yeyote kuwa Mama kanyanyuka na sikutaka kumuambia, niliona kama wachawi. Lakini dada aliingia chumbani na kumuona Mama kaamka na yuko vizuri, aliniita mimi kutaka kuniambia kabla ya kumuambia mtu yeyote, hakujua kama ninajua, nilimuaambia kuwa najua, wakati huo huo Mama aliniambia kuwa anataka kutoka nnje.


Alionekana kuwa na nguvu kidogo, aliweza kujisogeza mwenyewe, alikua na nguvu kuliko mwanzoni, tulimsogezea kiti chake cha magurudumu ambacho kilikua pembeni yake, alikua hakitumii muda mrefu lakini kilikua kinafanya kazi. Tulimsaidia kunyanyuka tena bila kutumia nguvu nyingi, akakaa katika kiti chake na tukaanza kumsukuma kutoka naye. Ile tunatoka tu nnje kila mtu alishanaga, hakuna aliyetegemea kumuona Mama katika hali ile, Mama pia alishangaa kuwaona pale kwani ni kama alikua hajui chochote kilichokua kikiendelea kipindi anaumwa.


Walijishaua kumsalimia nayeye aliwasalimia vizuri tu, walijiongelesha na kumpogeza lakini mpaka kufika saa sita kila mtu alikua ashaondoka, ni kama walikosa kilichokua kimewapeleka, hata Shangazi aliondoka. Baba alirudi kwa mshangao, alishangaa sana kumuona Mama kapona kwa haraka namna ile, alikua kapaniki sana, alijitahidi sana kuzuia mshangao wake lakini ulionekana na alionekana kabisa kuchanganyikiwa kwa kumuona Mama akiwa katika hali ile.


Alilazimisha kumpa pole na kumshukuru Mungu lakini nilimuona kama vile analia. Hakukaa sana alitoka nnje na kuingia kwenye gari yake, hakwenda popote nilimuona akiongea na simu kwa masaa zaidi ya matatu. Baada ya hapo alirudi ndani na kuingia chumbani kwake mpaka usiku wakati wa chakula ambapo alikula kidogo na kurudu chumbani kulala. Mama alikua chumbani tayari kalala, baada ya kumaliza kula na mimi niliingua chumbani kulala.


Lakini kabla ya kushikwa hata na usingizi Baba alikuja chumbani, alikua akihema kwa nguvu, aliniamsha na kuchukua mabegi ya nguo zangu na kukusnaya baaadhi ya nguo zangu, alininyanyua na kuniambia tunaondoka. Nilimuuliza wapi lakini alikua mkali na kuniambia kuwa yeye ni Baba yangu na ndiyo huamua kila kitu kaamua kuwa hataki nikae pale hataki, alinibeba kwa nguvu na kuniingiza kwenye gari, alionekana kuwa na hasira sana akiongea mwenyewe maneno ambayo sikumuelewa, nilimuuliza kuhusu Mama akanipa jibu ambalo liliniacha njiapanda. “Ushakua mtu mzima nilazima ujifunze kuishi bila Mama…” aliongea huku akiwasha gari na kuondoka kwa nguvu nyuma akilibamiza geti ambalo lilikua halijafunguliwa vizuri.


Unashani ni kwanini anamuambia Asha kuwa ajifunze kuishi bila Mama, kwanini anamuondoa usiku ule tena kw aharaka manana ile, je anampeleka wapi na ni kitu gani kimetokea wakati akiwa chumbani na Mama asha? Usikose kupata sehemu ya sita kupitia ukurasa wangu wa instagram @iddimakengo.


ITAENDELEA


SAFARI; MIMI, MAMA NA BABA PEMBENI!—SEHEMU YA SITA


Akili yangu yote ilikua ikijua na kuamini kuwa Baba kamuua Mama, alikua kapaniki sana. Niliwaza sana ni kwanini alikua akiniambia natakiwa kuishi bila Mama yangu wakati Mama yangu alikua hai, sikumuelewa kabisa lakini pamoja na maswali yangu mengi Baba hakunjibu, aliendesha gari mpaka kwenye nyumba moja, aliponishusha ndipo niligundua kuwa kulikuwa ni kwa Shangazi. Aligonga mlango tukafunguliwa, hakufungua Shangazi bali mjomba, walisalimiana akamuulizia Shangazi ambaye alikuja.


“Vipi?” Mjomba aliuliza kwani baada tu ya kuingia Baba alianza kuongea na dada yake kimya kimya vitu ambavyo Mjomba hakuvielewa. Walimsikia lakini walinyamaza, ni kama walikua wanamdharau flani, mjomba kuona vile aliwafuata na kumgusa Baba.


“Vipi mbona usiku usiku kama huu, kuna nini kimetokea…” Aliujiza, kabla ya kujibiwa  Baba alinigeukia na kuniambia niingie ndani.


“Hapana shemeji, hapa ni kwangu, nataka kujua kwanza kuna nini usiku huu unakuja na mtoto, upo katika hali hiyo na unamuambia kuingia ndani?”


Mjomba aliuliza, Baba alionekana kutokutaka kumjibu na ni kama alikua anamdharau bado, Shangazi alijaribu kumshika mume wake na kutaka kumuingiza ndani.


“Kaka sasa hivi hayuko sawa, ingia ndani nitakuambia baadaye…” Aliongea lakini mjomba aliamua kuwa mkali, alimsukuma Shangazi na kumuambia ile nyumba ni yake na anahitaji kuheshimiwa.


“Nataka kujua nini kinaendelea, huwezi kuniambia kuwa utaongea na mimi baadaye wakati mko kwangu, kama ni suala la kifamilia mngeongelea huko, hapa ni kwangu hivyo natakiwa kujua kila kitu kinachoendelea humu.”


Mjomba aliongea kwa hasira, pamoja na kuambiwa kuingia ndani lakini sikua tayari kwa hilo, nilitaka kusikia, akili yangu bado ilikua ikimuwaza Mama. Kwa namna Baba alivyokua nilihisi kuna kitu kibaya kakifanya na alikua ameniondoa ili kutokiona. Niliingia kwa ndani na kusimama pembeni ya mlango ili kusikia wanaongea nini. Shangazi aliingia kuchungulia kuona kama nilikua nimeingia ndani, kwa bahati nzuri hakuniona kwani nilikua nimejibanza kwa pembeni na kufunikwa na mlango.


“Mtoto hatakiwai kusikia mume wangu. Mama yake kamkimbia kaondoka kamuacha Kaka!” Shangazi aliongea, kwanza kidogo nicheke kwani ilikua haiingii akilini kabisa kwa Mama kukimbia, kusema kweli sijui kwanini, labda nikwakua niliona kama wamekamatwa na kukosa uongo mwingine lakini nilijikuta nacheka chini chini nikiamini kuwa Mjomba hawezi kukubali ujinga alioambiwa.


“Unasema nini? Kakimbia? Nani huyo mnamzungumzia, mimi nilidhani utasema hapa unasema kakimbia? Kwa miguu gani hiyo aliyonayo yakuweza kukimbia? Si katoka hospitali yuko mahututi wakupumua na mipira?”


Mjomba aliuliza, ingwa neno kufa lilinikera lakini nilifurahishwa na maswali yake.


“Sio hivyo shemeji, mke wangu kapona…”


“Kapona? Kivipi na kama kapona kwanini akuache, kwanini atelekeze watoto?”


“Hajapona kihivyo, lakini ndugu zake ndiyo wamekuja kumchukua, alipotoka hospitalini alirudi kwangu, mimi na watu wengine tulijua kuwa hawezi kunyanyuka, tulimrudisha nyumbani ili likitokea la kutokea basi awe nyumbani kwake na familia yake. Lakini Mungu mkubwa mchana huu mke wangu alinyanyuka na kuwapigia simu ndugu zake.


Nimerudi kutoka kazini nakuta ndugu zake wapo nyumbani, wanasema wanataka kumchukua ndugu yao na wanasingizia mambo ya kishirikina. Kwa namna flani wanamaini mimi ndiyo nimemsababishia yale mambo. Nimeshindwa kuwaelewa lakini walikuja na gari kabisa wamemchukua mke wangu na kuondoka naye. Nimemleta mtoto hapa kwakua mimi nataka kuondoka, nataka kufuatilia hili swala kwa undani, siwezi kuruhusu mke wangu ambaye nimehangaika naye kuchukuliwa kirahisi namna hii.


Nataka kufuatilia na sitaki wakati haya yakitokea Asha kuona,a shakua mkubwa hatakiwi kuona kama mimi na Mama yake hatuko viziuri, nibora akae hukua na mdogo wake, baada ya wiki mbili nikishaweka mambo sawa nitakuja kumchukua.” Baba aliongea kwa suti ya taratibu, kwa namna alivyokua anaongea hata mimi kama nisingejua kilichokua kinaendelea ningeweza nikamuamini, alikua anatia huruma na alionekana kulalamika kana kwamba amedhulumiwa mke.


Nilitamani kujitokeza nilipokua nimejibanza na  kumsuta kusema si kweli lakini nilijua kuwa haiwezi kusaidia. Bado nilitaka kujua ni kitu gani kilikua kimemtokea  Mama, nilitaka kujua mipango ya Baba na ni kwanini alikua anasema ndugu wa Mama walikuja na kumchukua Mama wakatio haikua kweli, kwanza hata pale nyumbani walishaondoka na hawakua watu wa kufikafika mara kwa mara, tangu mama kuanza kuumwa zaidi miaka mitano walimtelekeza, niliwaza ni kwanini kuja kumchukua wakati huo.


Mjomba alionekana kumuelewa, alieleweshwa kuwa mimi nitakaa hapo kwa muda na mambo yakitulia nyumbani basi nitaenda. Baaba alimuambia anahofia kama nikijua kuwa Mama yangu kaondoka kwakua anadhani kuwa yeye ni mchawi basi italeta chuki kati yao hivyo nibora kuniambia kuwa Mama kapelekwa nnje ya nchi na mimi kukaa nao mpaka atakaporudi. Waliongea maneno mengi wakimpanga mpaka akakubali, ilikua ni stori nzuri sana kuiamini.


Nikiwa bado nimejibanza pale mjomba aliingia, kwa bahati nzuri hakufunga mlango, alienda moja kwa moja mpaka chumbani kwake na hakuniona pale. Kule nnje walinyamaza kwa muda kuhakikisha kuwa ameenda mbali ndipo walianza kuongea.


“Unafanya nini sasa?” Shangazi alimuuliza Baba.


“Sijajua chakufanya lakini siwezi kuendelea kuishi haya maisha, nitampa talaka yake na kumuachilia mbali, kaumwa sana na mimi nimechoka kugombana na binti yangu, ananiona mimi shetani kwa kumtelekeza Mama yake, nataka kumrudisha kwao.”


Baba aliongea kwa kujiamini, kwa maneno yake yale niliamini kuwa Mama bado yuko hao hivyo nilifurahia kidogo.


“Atakubali, vipi mtoto unafikieri Asha atakubali kukaa mbali na Mama yake?”


“Hapana, najua hawezi kukubali, hii ndiyo maana nataka kumuambia kuwa Mama yake yuko hospitali Nairobi, naamini atafurahi mimi kumjali Mama yake, nimemleta hapa kwakua kesho ndiyo nataka kumuondoa, nampeleka kijijini kwao kabisa, sitaki mambo ya kuja kumuona na kuniletea shida.


Siwezi kumpa talaka kwa sasa kwakua kila mtu atanishangaa, lakini dini inaruhusu wake wawili, nikishaoa mke mwingine basi ndiyo nitamuelewesha mtoto. Nataka nifanye mpango akasome bweni ili asione yanayoendelea. Haya mambo yamemuathiri sana na nina wasiwasi kuwa huko mbeleni itamsumbua, nataka ajue nampenda Mama yake lakini siwezi kuendelea kuishi naye tena.” Baba aliongea kwa sauti ya chini kidogo, alionekana kuwa na mawazo flani, niliwasikia wakitaka kuingia ndani hivyo nilitoka na kukimbia kwenye chumba ambacho nilijua Sudi analala na kujifanya nimelala.


***


Kama alivyokua amepanga Baba aliniambia kuwa Mama amezidiwa na kalazimika kumpeleka Nairobi kwa matibabu. Kwakua nilishasikia kila kitu niliamua kuigisa, nilimkubalia na kumshukuru kwa kumjali Mama yangu, nilijua hata kama nikikasirika au kuonyesha kuwa ninajua isingesaidia chochote. Nilimshukuru sana nikiangalia ni kitu gani kitakuja kutokea mbeleni, wakati huo hata matokeo yalikua hayajatoka hivyo nilijua kuwa itachukua muda mrefu kwenda shule na nitajua ukweli karibuni.


Baba alikua mjanja, alikua anataka kumaucha Mama lakini alikua akijua kuwa kama wakiachana na Mamaa kaamua kufuatilia basi wangegawana mali, baada ya kumuondoa Mama pale nyumbani alianza kutafuta mteja wa ile nyumba. Alimrudisha Mama kijini lakini alirudi naye na kumpeleka kwa mdogo wake, alifika kule Bibi anaumwa ana hali mbaya hivyo alizuga kana kwamba Mama alienda kumuona Mama yake na sikua alimpeleka kumuacha.


Alimrudisha na kumuacha kwa Mama mdogo ili kumhudumia, hata huko hakusema kama kamuacha au anataka kumuacha bali alisingizia kuwa anasafiri na aliataka akae pale kwa muda kidogo. Nilisikia yote hayo kwakupitia mazungumzo yake na Shangazi, kila jioni walikua na tabia ya kutoka nnje kuongea mambo yao kimya kimya, walikua hawajui kama nawafuatilia, wao waliamini kua nimedanganyika na stori zao. Babaa lihangaika sana kutafuta mnunuzi wa nyumba lakini hakupata, kila aliyekua akimpata alikua anashindwa kupanda dau.


Kule kwa kina Mama mdogo nako walikua wakimsumbua, ndugu walimuita kikao na kumuambia aseme kuwa kama kamuacha mke wake au la. Kwa bahati nikuwa Baba yangu ni wale watu ambao wanapenda kuonekana wema mbele za watu,a napokua na wati hataki kuonekana kama mtu mbaya, pamoja na kutaka kumuacha Mama lakini alihofia sana kumuacha katika hali ile, alibanwa sana mpaka kufikia hatua ya kumrudisha tu nyumbani.


Nakumbuka ilikua ni usiku, mwezi mmoja ulishapita tangu mimi kuanza kuishi kwa Shangazi, kama kawaida walitoka na kuanza kuongea mambo yao ndipo nilipata zile habari kuwa Baba kalazimika kumrudisha Mama.


“Lakini nitaoa mwanamke mwingine, yule atakaa paleopale na mimi nitatafuta nyumba nyingine na kuoa mwanamke mwingine, dini inaruhusu kabisa.”  Baba aliongea, alionekana kuchanganyikiwa, alionekana kuwa na mawazo mengi, Shangazi alimshutumu na kumuambia awe mwanaume, nilazima ajue kufanya maamuzi na si kuogopa watu.


“Hata hivyo yule ni Mama wa wanangu, siwezi kumaucha akawa ombaomba barabarani, nilazima kusaidia, atakaa pale mpaka mungua takapomchukua, sitaki wanangu kuja kunichukia kuwa nilimuacha Mama yao akafa barabarani wakati nyumba ninayo…”


“Huna lolote, yule mwanamke kakuloga, siku ile wakati unaongea ulikua na akili zako, lakini sasa baada ya kumrudisha kwao naona akili zimekuruka tena, tangu zamani unakua hivi hivi, tunapanga mambo lakini ukishaonana na huyo mwanamke wako basi unakuja kutugeuka!”


Shangazi alionekana dhahiri kukerwa na kile kitendo,a limsema Baba kama mtoto mdogo, alimchamba sana na kumtolea maneno mengi ya kashfa. Baba alinyamaza na kuopokea kila kitu, pamoja na kukosewa heshima lakini hakujibu, mwisho alimuambia tu kuwa ataoa mwanamke mwingine na yule ataendelea kubaki naye kama Mama wa watoto wake.


“Hakuna kitu hapo, hizo si akili zako na kesho kitu cha kwanza namuambia Mama, huwezi kuishi na mwanamke anakusumbua kiasi hiki. Hata kabla ya kuumwa alikua kakutawala mpaka sasa hata kutembea hawezi bado kakutawala.


Baba aishikilia msimamo wake, alimrudisha kweli Mama na mimi kunirusisha nyumbani, alinidanganya kuwa Mama alikua katoka hospitalini na hali yake ilikua bado haijabadilika. Mama pia aliniambia hivyo hivyo, nilijua kabisa alilazimishwa kusema hivyo lakini nilijifanya kuwaamini. Maisha yaliendelea, matokeo yalipotoka nilikua nimefaulu vizuri, nilipangiwa Ashira Girls Morogoro. Nishule ambayo niliipenda na nilitamani kwenda lakini sikutaka kwani nilitaka kukaa karibu na Mama.


Bado nilikua simuamini Baba na nilijua fika kama nikiondoka hata chakula pale nyumbani itakua shida. Ingawa hali ya Mama ilianza kuimarika lakini badoa likua hawezi kunyanyuka, alikua ni mtu wa kulala sana na mara chache tulijitahidi kumlaza kwenye kiti cha magurudumu na kumtoa nnje. Baba alikua anakuja mara moja moja nyumbani, hakua amesema lakini nilihisi atakua kaoa mwanamke mwingine kimya kimya.


Maisha yaliendelea baba akirudi nyumbani mara moja moja, nilisoma shule ya kutwa ili kumhudumia Mama, hali ya Mama iliendelea kuwa vile na wote tulishakubaliana na ile hali kuwa hatasimamama tena. Lakini kuna kitu nilikiona kama kinabadilika, tumbo la Mama lilikua linakua kubwa siku hadi siku, sikujua ni kwanini, nilihisi ni sababu ya kulala sana. Ila siku moja nikiwa chumbani nilimsikia Baba akipiga kelele chumbani kwa Mama, alikua kaja mara moja tu kusalimia.


“Hiyo mimba si ya kwangu na sitaki mtoto na wewe kabsisaa! Utaniambia ni yanani! Utajua mwenyewe lakini mimba si yangu na nitakuacha ufe nayo!” Nilishtuka kusikia vile nikiwaza hivi Mama ana mimba na ni ya nani mbona Baba alikua anamchukia namna ile hata kula ndani ilikua shida.


Inaonekana kama Mama Asha ana mimba, hakuna anayejua ni ya nani?


SAFARI; MIMI, MAMA NA BABA YANGU PEMBENI—SEHEMU YA SABA!


“Wewe ndiyo umenibaka, mimi nilikua hata sijui siku zangu, hata mimba sijui nimepataje! Lakini ulitegemea nini kama kila siku unakuja na kuniingilia!” Nilimsikia Mama akipiga kelele, nilitoka chumbani kwangu nakusogea mlangoni kabisa kwa Mama.


“Nimekubaka! Nimekubaka? Wewe si ni mke wangu? kuna siku nilishawahi kukupa talaka wewe mbwa, nilikubaka wakati nimekuoa aunakula na kunya kwangu, hivi ulitegemea nitakuhudumi kila siku halafu nisikuto*** mshenzi mkubwa wewe mwanahizaya…”


Baba alitukana sana matusi ambayo ahata hayasimuliki, wakati wote huo Mama alikua akijaribu kujitetea lakini hakumpa nafasi.


“Hii mimba utaitoa, siwezi kuzaa mtoto mwingine nawewe! Mimi nina maisha yangu, nina mke wangu, nimekusubiri sana ili ufe lakini naona kama Mungu anakuchelewesha, sasa ukiibeba hii mimba nitakuua mwenyewe na mikono yangu!”


“Kama nikunioa niue, nimeshachoka haya maisha, nimechoka manyanyaso ya kila siku. Sikuwahi kuwa na furaha na wewe, kila siku ilikua ni vipigo umenitia ulemavu lakini hata hunionei huruma!”


Mama alilalamika, aliongea mambo mengi ya kabla ya kupata ulemavu, namna ambavyo Baba alikua akimpiga, alikua akimfungua ndani na kumchoma na pasi, namna alivyokua akimlazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile na mambo mengi mengi.


“Mshenzi wewe, si ulikua unapenda, kama ungekua hupendi si ungeondoka, umenipotezea maisha yangu mbwa kabisa na sasa hivi nakuua sikuachi, najua unafanya yote haya ili nikikuacha mimi nionekena mkatili, sasa sikuachi nakuua, hiyo mimba lazima itoke.”


“Njoo tu uitoe, hata leo ukitaka toa, sitaki kuzaa tena na mwanaume kama wewe, huyo mtoto simtaki, mwanaume gani kila siku ni kumbaka mwanamke amabye hata kunyanyuka hawezi, unajifanya mwema mbele za watu lakini kumbe ni shetani, leta hivyo vidonge nitakunywa hata vyote nife tu nikuache nione kama utakua na amani!” Mama aliongea lakini ghafla nilisikia vitu vikirushwa rushwa, nilisikia kitu kama kikisukumwa na mama alipiga kele huku nikisikia Puuu kama mtu aliyedondoka chini.


Sikuweza kuvumilia tena, nilisukuma mlango na kuingia, taa ilikua inawaka, mama alikua kalala chini huku Baba kashikilia mguu wake mmoja kwa juu, ni kama aliushika na kumvuta kutoka kitandai akadondokea chini, alikua akimpiga mateke ya makalioni ambayo hayakua na idadi, nilipoingia ghafla Baba wote walishtuka.


“Muache Mama yangu!” Nilipiga kelele, baba alinitishia akiniambia nitoke hayanihusu lakini nilikataa, nilimuambia yule ni Mama yangu na kama anataka kumuua basi ataniua mimi kwanza.


“Mwanangu toka huu ugomvi haukuhusu!” Mama alipiga kelele kuniomba nitoke, nilikataa katakata.


“Sasa si unataka kuona ngoja nikuonyeshe kazi yangu! ngoja nikuonyeshe namna ambavyo waawake wasiokua na heshima wanaadhibiwa. Alizidi kumpiga Mama mateke akiwa pale chini, kuona haitoshi alivua mkanda wake na kuanza kumtandika, cha ajabu Mama hakupiga kelele sikujua ni kama alikua hasikii maumivu au alikua anavumilia. Lakini sikutaka kuona hilo likiendelea, nilimvamia Baba na kumshika kiuono huku nikimvuta kwa nyuma.


“Umeshakua sasa, huyu Malaya kakufundisha kutokuniheshimu, yaani unaniingilia wakati nampiga Mama yako? Nimekudekeza sana sasa utanijua!” baba aliongea huku akimuachia Mama na kunigeuka mimi, aliishika mikono yangu na kuitanua kuiondoa kiunoni kwake, baada ya hapo alinisukuma nikaangukia kwenye kochi doge, alikuja na kunirukia na teke kama anataka kunikanyaga tumboni, kwabahati nzuri nilimuona na kumkwepa, nilinyanyuka hatakahataka na kumkimbilia Mama.


Yeye abdo alikua kalala chinia napiga kelele akiniambia nitoke Baba atanioa. Mimi sikujali kuhusu kupigwa na Baba, nilikua simuogopi, niliinama chini nakuanza kumuangalia Mama, nilikua naangalia kamakaumia, lakini kabla ya kufanya chochote Baba alinikanyaga mgongoni, nilidondoka kwa mbele na kujikuta namlalia Mama. Nilijitahidi kunyanyuka lakini babaa linikanyagia kwa juu, nikawa nimemlalia Mama tumboni niko kwa juu yake, aliendelea kunisukumiza kwa mguu wake wakulia.


Alichukua mkanda wake ambao ulikua umedondokea kitandai na kuanz akunichapa nao, alinichapa sana lakini sikutoka juu ya Mama, nilimlalia mama kumkinga na kipigo cha Baba.


“mwanangu toka, mauche anipige mimi siumii!” Mama alipiga kelel, alijaribu kunyanyua mikono yake ili kunisukuma lakini hakuweza na mimi sikuitoka.


“Kama anataka kukuua basi ataanza kuniua mimi! Wewe si mtoto wake, ni mtoto wa watu muache aniue mimi kwanza!” nilimuambia mama huku nikizidi kumkumbatia, Baba linichapa sana mpaka yeye mwenyewe akachoka na kuanza kulia kama mtoto.


Sikujali, mama alilia sana lakini sikutoka juu yake, nilijua kama nikiondoka basi zile fimbo zitamdondokea yeye. Baba alichoka na kukaa kitandani, alikua anatukana sana, alikua ananiambia kuwa mimi si mwanae tena, aliniita mshenzi na kuniambia kuwa nitaondoka mule ndani na hataki kuniona tena, aliniachaia laana zote lakini bado sikutoka juu ya Mama yangu. baad aya kuona kama sitetereki baba alinyanyuka na kutoka nnje, niliendelea kukaa pale juu ya Mama kwa kama dakika kumi hivi ndipo nilikua na uhakika kuwa kaondoka na mimi nikanyanyuka.


Nilitoka nnje na kumuita binti wa kazi, kumbe alizisikia zile kelele lakini aliogopa, aliingia ndani na kujifungia. Nilimgonge ana kumuambia kuwa Baba kaondoka hivyo afungue, alifungua kwa uoga, nikamuambia aje kunisaidia kumnyanyua Mama, ilikua ni kazi ngumu sana kwani alikua ni mzito. Alionekana kuumia sana, nilimuambia nilazima nimpeleke hospitalini lakini alikataa.


“Hawatanitibu hivi hivi, watataka PF3 Baba yako anaweza kufungwa…” Aliongea maneno ambayo yalinikasirisha.


Nilishangaa nikwanini pamoja na mambo yote yale lakini bado alikua akimfikiria Baba na kumuonea huruma.


“Afungwe tu! Hata akifilia mbali huko mimi sijali, simta…”


“Nyamaza tena tema mate chini, yule ni baba yako hata kama binadamu anakosea lakini bado ni Baba, ni mzazi wako na anakupenda sana….” Alitaka kuongea maneno yake yale lakini sikumsikiliza, nilimkatisha na kuanza kumtukana Baba, nilimuambia ni mshenzi na sitaki kabisa kumuita Baba. Sikutaka kuongelea hiyo ishi kabisa, tulimfikisha kitandani na kutokana na maneno yake nilikasirika na kutoka nnje kabisa.


****


Mwili mzima ulikua unauma, nilianza kuyasikia maumivu baada ya kutoka chumbani kwa Mama na kuingia chumbani kwangu, nilijiangalia na kuona nimevimba miguuni, kwenye mapaja kuna michubuko na mgongo ulikua unauuma, nilipojaribu kunyanyuka nilipata maumivu makubwa kiunoni. Nilijikuta nakaa nikishindwa nini cha kufanya, wakati nikiwa nawaza nifanye nini, nikiwa bado siamini kama Baba yangu mzazi anaweza kufanya vitendo vile dada aliingia.


“Mimi kesho naondoka, nadai mshaara wa mwezi huu lakini siutaki, nina nauli yangu nataka kurudi kwetu…” Aliongea kwa wasiwasi flani, niliacha kuwaza tena kuhusu maumivu na kumuomba akae ili kuniambia ni kwanini alikua anaondoka.


“Najua mengi sana, Baba yako anaweza kuniua, kama wewe kakupiga hivyo mimi ni nani mpaka kuniacha.” Aliongea maneno ambayo yalinishangaza.


“Mengi gani hayo unazungumzia?” Nilimuuliza, alikua mzito sana kuniambia lakini nilimsihi kwa kumuomba aniambie.


Nilimuambia nimekubali aondoke lakini kama ananiacha peke yangu ni lazima mimi kujua kilichokua kinaendelea.


“Baba yako si mtu, anajifanya mtu mbele za watu lakini ni sheteni…” Alianza kuongea, ingawa nilishajua hilo lakini kwa namna alivyokua akionekana nilijua lazima kuna kitu kingine cha ziada ambacho alikua hataki kuniambia.


Kila mara alikua anakuja, ananifungia chumbani kwangu halafu anaingia chumbani kwa Mama,a naka huko muda mrefu na akimaliza mambo yake ananiambia nitoke niende kumsafisha Mama ili wewe ukirudi kutoka shuleni usimuone.”


“Anafanya mambo gani hayo?” Nilimuuliza ingawa nilikua nishapata jibu lakini nilitaka kusikia kutoka kwake.


“Inamaana hujui? Unafikiri Mama kaipataje hiyo mimba, alikua anakuja na kumbaka Mama yako, anamfanyia kwa nguvu na wakati mwingine Mama anapiga kelele lakini hajali, aliishia kumpiga tu. Baada ya kumaliza hunaimbia nimsafishe shahawa na kuhakikisha hazionekani, ananiambia nimsugue kabisa, mimi nimechoka, ni unyanyasaji lakini alikua ananitishia kuniua, baada ya kuona alivyokupiga hata mimi nimemuogopa naondoka.”


Kwa mtu ambaye alikua hajawahi kuishia na Baba asingeweza kuyaamini hayo maneno, lakini kwa mimi ambaye nilianza kumuona akimfanyia Mama unyama tangu nikiwa na miaka nane nilijua yana ukweli.


“Sasa ukiondoka mimi nitabaki na nani? nitawezaje kumhudumia Mama…”


“Hapana, mimi hilo halinihusu, hata mimi nina maisha yangu, kwetu masikini sana lakini siwezi kuishi katika nyumba kama hii, unyama anaofanyiwa Mama unafikiri naweza kuuvumilia. Baba yako ni shetani, muuaji kabisa, kuna vitu vingine hata siwezi kukuambia kwakua utaishia kumuua bure.”


Aliongea, ingawa nilikua naumia lakini nilitamani kuvisikia, nilimbembeleza sana ilia niambie lakini alikataa, nilimuomba nakulia ndipo aliniambia.


“Kuna kipindi nilikua natoa shahawa mpaka kwenye makalio ya Mama yako, Baba yako ni mshenzi, Mama yake angekua ashapona mud amrefu lakini kwa mabo anayomfanyia kwa namna alivyokua anmpiga na kumbaka kila siku sidhani kama angeweza kupata hata nafuu achili mbali kupona.”


“Kwanini hukuniambia sasa, kwanini ulicha yote hayo kutokea unaishi na Mama lakini humuonei hata huruma?”


Nilikua nataka tu mtu wa kumlaumu, nilitaka kumfanya ajisikia vibaya ingawa nilijua kabisa si kosa lake.


“Ungeanza kwa kumuuliza kwanza Mama yako hilo swali, kwanini yeye anayenyanyaswa na kufanyiwa unyama wote huo hakusema?” Alinipa jibu ambalo lilinifanya kunyamaza, baad aya kumaliza kuongea alinyanyuka na kuondoka, nilimbembeleza sana asiondoke lakini aliingia chumbani kwake na kuanza kupanga nguo zake, aliniamba anatuonea huruma lakini hawezi kuendelea kukaa na sisi.


“Kama una ndugu yeyote basi mchukue Mama yako na mpeleke, Baba yako ni mshenzi atakuja kuwaueni wote.” Alinipa ushauri lakini sikumjibu chochote, nilikua na hasira kwanini alikua anaondoka, pamoja na maumivu makali amayo nilikua nayo lakini akili yangu ilikua sehemu nyingine kabisa, nilikua nikiwaza ni kwa namna gani nitaweza kuishi na Mama akiwa katika hali ile. Roho iliniuma sana, nilirudi ndani na kuanza kulia, nililia sana nikimuonea Mama huruma kwani alikua kabaki peke yake, ndugu zake wala hata hawajali kama ana matatizo.


Asubuhi Dada aliondoka, sikumlaumu sana kwani hali ya mule ndani ilikua ni ya kukimbia, lakini alikua ni Mama yangu na nisingeweza kumkimbia, ilikua ni siku ya shule lakini si kwenda na wala sikujali, nilipofika chumbani kumsalimia Mama aliniuliza kwanini nilikua sijaenda shule, alifikiri labda nikutokana na kipigo naumwa nilimuambia hapana, dada ameondoka na tutabaki wawili. Macho yake yalionekana kunyong’onyea na kukata tamaa.


“Ungeenda tu, elimu ni muhimu mimi naweza kukaa mwenyewe hapa mpaka ukirudi.”


Aliongea lakini nilijua kabisa alikua hamaanishi, alikua anajua kuwa anahitaji msaada na mimi pekee ndiyo wa kumsaidia.


“Shule itasubiri Mama, hata nikienda sitasoma nikijua kuwa haupo salama.” Nilimuambia, alinyamaza kimya bila kusema chochote.


“Mimi ndiyo nilitakiwa niwe Mama yako, nimechukua utoto wako wote na sasa nachukua na elimu yako…” Alianza kuongea lakini nilimkatisha, nilimuambia yeye hakuamua kuwa mgonjwa na kama ni ishu ya kuwa Mama basi alishakua kwa kunizaa.


Nilitoka na kuendelea na maandalizi ya chai. Mchana ulipita lakini usiku nilipokea simu, ilikua ni ya Bibi mzaa Baba, kabla hata ya salamu alitaka kuongea na Mama, niliweka loud speaker na kuiweka pembeni ya kitanda, ile Mama anasema haloo tu alianza kutukana. “Mshenzi mkubwa wewe, yaani mwanangu kakulea hivyo kakuvumilia mtu ushakufa tayari lakini ukaona haitoshi umeenda kubeba mimba ya wanaume wengine! Hivi mwanamke una akili kweli wewe? Wewe ndiyo wa kuingiza wanaume ndani tena unamtumia binti yako kabisa kukutafutia wanaume?


Siju umemlogea nini mwanangu! Nilishamuambia kipindi sana akuache lakini hataki, eti anakupenda anaogopa watu watamuelewaje, sasa unaona aibu, unabeba mimba ya mwanaume mwingine tena unafanyia mapenzi nyumbani kwake mbele ya mwanao! Wewe ni shetani kabisa na nakuhakikishia kabla sijaingia kaburini kwenye hiyo nyumba utatoka na talaka utapewa, kama unajua kuloga mimi najua kuwanga!” Bibi aliongea kwa hasira na kabla Mama hajajibu alikata simu, wote tulibaki na butwaa tunashangaana tu.


SAFARI; MIMI, MAMA NA BABA YANGU PEMBENI—SEHEMU YA NANE!


Nilimuuliza Mama ni kwanini alikua hawaambii watu ukweli lakini hakua na jibu. Nilizidi kumdodosa kuhusu mimba yake, aliniambia kweli ana mimba lakini hataki kulizungumzia hilo.


“Mwanangu unatakiwa kuniacha, nenda kaishi na Baba yako.” Aliniambia, nilimuangalia kwa mshaangao, nilimuona kama mtu aliyechanganyikiwa, yaani pamoja na mambo yote yale aliyokua kafanyiwa na Baba bado alitamani mimi nikaishi naye.


“Mama kwanini unafanya hivyo? Kwanini unamlea Baba namna hiyo, tangu nikiwa mdogo nilikua nampenda Baba nikijua kuwa ni baba mwema, kumbe ni shetani anakupiga kila siku?”


Nilimuuliza kwa mshangao nikiwa na hasira kidogo, uso wangu ulichaa chuko.


“Hapana, Baba yako si kama unavyodhani, kuna wakati anakua na hasira tu, kuna wakati hata mimi nakua namkasirisha…..” Alianza kuongea maneno yake ambayo yaliniboa, nilitoka kabisa kwani nilikua nimekasirika sana, nilitamani hata kumpiga Mama kwani nilikua namuona kama mjinga, nilijikuta nina hasira, nilijikuta nalia na kuanza kutukana.


“Kama wanaume wenyewe ndiyo hawa basi mimi sitaki kabisa wanaume, sitakuja kuolewa kamwe!” Nilijiambia kwa hasira, Mama yangu alikua kateseka sana na nilijua kuwa ataendelea kuteseka kama sitafanya chochote. Nilirudi chumbani na kuchukua simu yake, nilimpigia simu, kwanza alianza kutuikana akidhani kuwa ni Mama alikua anampigia, lakinia liposikia ni mimi alinywea na kuanza kuongea maneno mabaya kuhusu Mama.


“UNa uhakika na hayo unayoyaongea Bivi?” Nilimuuliza, alinijibu majibu marefu ya vitu ambavyo havieleweki.


“Mimi ndiyo nakaa na Mama kila siku, najua kila kitu kinachoendelea, Baba ni mshenzi, Baba alikua anambaka Mama kila siku, hivi kwa akili yako unadhani Mama anaweza kuingiza mwanaume ndani?” Nilimuuliza kwa hasira, pamoja na kumuambia mambo mabaya ambayo Baba alikua akiyafanya lakini hakujali, alinigeuka na kunitukana hata mimi, aliniambia maneno mengi kuwa mama kashaniharibu na atanifanya Malaya.


Nilimjibu mbovu na mwisho nilikata simu kwa hasira, nilianza kutafuta namba nyingine za kupiga kutafuta msaada lakini kila namba ya ndugu niliyepiga hakuna aliyekubali kupokea. Walipona namba ya simu ya Mama waliona kama vile anahitaji msaada. Akili ilishindwa kufanya kazi kabisa, nilikua natamani kuondoka pale, kwa mambo ambayo Baba alikua akimfanyia Mama nilijua kabisa ipo siku atakuja kumuua.


Kabla sijajua ni kitu gani cha kufanya nikiwa nnje na simu yangu Baba alikuja, alikua kawaida hakua na hasira tena, nilimsalimia kishongo upande nayeye aliniitikia vizuri. Aliniuliza kama Mama yupo ndani nikamuambia ndiyo, lilikua ni swali la kijinga kudhani kama Mama angeweza kutoka na hali yake. Aliingia ndani na mimi nikamfuata nyuma, aliingia mpaka chumbani wakati akitaka kufunga mlango nilikimbilia mpaka ndani na kukaa kitandai.


“Toka nataka kuongea na Mama yako mambo ya kikubwa…” Aliongea kwa sauti ya chini lakini yenye kuonyesha msisitizo.


“Hapana, siwezi kuondoka, huyu ni Mama yangu na nitamlinda, chochote unachotaka kuongea utaongea mbele yangu!” Nilimjibu kwa hasira, nilikua nimefura balaa. Baba naye alipandisha hasira na kuanza kunitukana akinilazimishia kutoka, Mama alinisihi sana nitoke lakini sikutoka, nilibaki palepale.


“Unataka niondoke ili umbake tena?” Bila kupanga nilijikuta naropoka.


“Unasema nini wewe?” Baba aliniuliza kwa hasira hukua kinifuata, alinishika na kuninyanyua juujuua na kuanza kunitandika makofi.


“Ili umbake, unafiokiri mimi sijui, unawaambia watu kuwa mimba si yako wakati kila siku nikienda shule ulikua unakuja kumbaka Mamama, wewe ni shetani mbwa kabisa, sikuogopi, wewe si Baba yangu kama Mama anakuogopa basi mimi sikuo…” sikuweza kumalizia maneno yangu baba alinitupa chini, alichukua chupa ya chai iliyokua mezani ambayo nilimpelekea Mama na kunirushia, alikua ananipiga kichwani lakini niligeuka na ikanipiga mgongoni.


Ni kama alichanganyikiwa, alinifuata na kuanza kunipiga kama vile anapiga mwizi,a linipiga mateke, ngumi na kila kitu,. alikua akinipiga hukua kinitukana,a kiniachia laana kuwa mimi si mwanae na hanitaki tena. Alinipiga mpaka nikapoteza fahamu, wakati ananipiga Mama laikua akipiga kelele kuomba msaada na kumsihi kuwa ataniua lakini alisema niachwe nife. Sikujua kilichoendelea mpaka kesho yake siku ya pili.


Baba alipoona nimezimia alidhani kuwa nimekufa, aliondoka kwa uoga na kunaicha pale chini, kwakua Mama hakuweza kufanya chochote aliishia kuniangalia. Mama yangu hakulala usiku mzima akisubiria ninyanyuke. Nilinyanyuka mwili ukiwa unauma kila sehemu, nilikua nimeumia sana, nimevimbia damu karibu kila sehemu ya mwili wangu, niliponyanyuka tu Mama alikua amcho, aliniomba nisogee karibu yake na kunisihi nikamuombe Baba yangu msamaha kwani nilimtukana na kumpandisha hasira.


Nilimuangalia Mama badala ya kukasirika nilimuonea huruma, sikumsogelea wala kutaka kumgusa.


“Naenda kumuomba  msamaha…” Niliongea huku nikitoka nnje, nilikua nakumbuka kila kitu, pamopja na kuumia sana lakini nilikua na nguvu ya ajabu, ilikua ni asubuhi. Niliongoza moja kwa moja mpaka kituop cha polisi, nilienda kuomba PF3, kwanza polisi wenyewe walishangaa ni kwa namna gani nilitembea mpaka pale kwa namna nilivyokua nimeumizwa.


Niliwaelezea kila kitu kuanzia mwanzo, sikuficha kitu niliendelea namna ambavyo Baba alikua akimpiga Mama, namna alivyomgongesha mpaka kumpa ulemavu pamoja na namna alivyokua anambaka akiwa kitandani mpaka kumpa ujauzito kisha nikamuambia suala langu, namna ambavyo alinipiga na kunitishai kuniua. Walitaka kunipeleka hospitalini lakini niliwaambia kuwa nataka Baba yangu akamatwe kwanza kwani nina wasiwasi kumaucha Mama peke yake.


“Alishajaribu kumuua Mama yangu mara kibao naingilia, najua pamoja na hasira zote lakini hawezi kumuua Mama mbele yangu hivyo kama hamumkamati absi siendi hospitalini narudi nyumbani nikafe na Mama yangu!” Nilimuambia askari Mama mtu mzima amabye  ndiyo alikua mkuu wa  kituo. Alinisihi sana na kunitishia kipolisi lakini nilimpa jibu amablo lilimhangaza.


“Mama nishakufa  tayari sina chakuogopa, najua haki zangu huwezi kuniweka ndani kwani sijafanya kosa lolote na kama hutaki kumkamata Baba basi naondoka!”


Niliongea huku nikinyanyuka kuondoka, alipoona niko siriasi na namna alivyokua akiniangalia nikitembea kama naenda kudondoka aliniita na kuniambia Baba atakamatwa, aliita askari wawili na kuwaambia wakamkamete Baba, baada ya hapo alimuita mwingine na kumuambia anipeleke hospitalini.


“Mama hivi hunielewi nataka Baba akamatwe au niondoke mimi, kuwatuma hao askari haimaanishi kukamatwa, najua mnamuogopa Baba yangu, nilipo taja tu jina lake niliona ulivyobadilika,a napes ana kila mtu anamheshimu kuwa ni mtu wa maana, hana maana yoyote, nitatoka  hapa nikiona Baba anaingizwa mahabusu!”


SAFARI; MIMI, MAMA NA BABA PEMBENI!—SEHEMU YA TISA


Nilikaa kituoni kwa muda wa kama masaa mawili hivi, waliachana na mimi na kuendelea na mambo yao, bado nilikua katika maumivu makali lakini nilitaka kuona haki inatendeka, nilijua kabisa kuwa Mama hawezi kujipigania na ni wajibu wangu kupigana kwaajili yake. Nilitamani kuondoka nikiwa na wasiwasi kuwa labda Baba alikua kaenda nyumbani na kufanya vurugu, lakini kabla ya kuondoka nililiona Gari la Baba likiingia, yeye ndiyo alikua akiliendesha na askari mmoja alikua siti ya mbele.


Alishuka akiwa kaongozana na askari wawili, walikuja na kunipta, sikumsalimia na yeye hakuonekana hata kujali, hakuniangalia kabisa, aliingia moja kwa moja mpaka kwenye ofisi ya mkuu wa kituo. Walikaa huko kwa muda wa kama dakika mbili hivi kisha wakatoka.


“Umeona mwanangu, Baba yako huyu tushamkamata, sasa nenda katibiwe…” Aliniambia huku akijichekesha, nilimuangalia kwa dharau bila kumjibu, nilijua kabisa hakuna kitu ambacho polisi wangenisaidia, nilinyanyuka na kutaka kuondoka.


Askari mmoja alinifuata na kutaka kunisaidia lakini sikutaka, nilitoka pale kituoni na kwenda moja kwa moja mpaka hospitalini, niliwaambia kilichotokea na walipodai PF3 niliwaambia pia kuhusu Baba yangu na kuwaambia nimemuacha kituoni labda atakuja nayo. Walikua wakimjua Baba yangu na walijua kuwa hawezi kufanywa chochote, walinitibia na kutaka kunilaza lakini nilikataa.


“Nikilala hapa Mama yangu atakufa nyumbani hana mtu wa kumsaidia angalau mimi naweza kusimama.


Pamoja na hali yangu mbaya lakini walinipa dawa ya maumivu na kuniruhusu kuondoka. Nilifika nyumbani na kumkuta Mama kapaniki,a liniuliza nilipokua nikamuambia, alianza kunipigia kelel kwanini nimesmhitaki Baba na kuniambia habari za laaana  na mambo mengine kibao, nilimsikiliza na kumuambia haijasaidia chochote kwani Baba amemnunua kila mtu, hakuna mtu wa kumgusa.


“Mwanangu unafikiri sijawahi kujaribu huko, alishanipiga nikampeleka polisi akaitwa na kuja kunipiga palepale kituoni na hakukua hata na mtu wa kunigombelezea…” Mama aliongea kwa uchungu, niliona machozi yakimtoka, nilitaka kumfuta lakini nilishangaa kanyanyua mkono wake na kujifuta. Mwanzoni sikushtuka, hata yeye Mama hakushtuka kuwa amenyanyua mkono, nilimuangalia kwa huruma, kwa mara ya kwanza Mama alikua kazungumzia kuhusu mateso ya Baba, kila sikua likua ni mtu wa kubisha na kumtetea Baba lakini siku hiyo aliongea.


“Nyamaza mwanangu, sisi wanawake ni watu wa kuvumilia, ndoa ndiyo zilivyo mwanangu ukikua utayaona.” Aliongea huku akinyanyua mkono wake wakulia na kunishika mashavyuni, hapo ndipo nilishtuka kuwa Mama alikua kaweza kunyanyua mkono wake.


“Mama umenyanyua mkono?” Nilimuuliza kwa mshangao, aliniangalia kwa huzuni hukua kipepesa macho yake kama alikua anautafuta mkono wake kuwa uko wapi. Hata yeye alishangaa kuwa mkono umenyanyuka, lakini baada ya kama sekunde tano hivi uliishiwa nguvu akashindwa tena kuunyanyua na kuushusha chini.


Nilimuambia ajaribu kuunyanyua lakini ilishindikana, kafuraha kadogo kalikokuja baada ya kuunyanyua kalipotea. Jioni ilishaingia, nilitoka kwenda kuandaa chakula cha usiku, bado kulikua na vitu ndani ingawa sikua nikifahamu ni kitu gani kitaendelea baad aya hapo kwani nilijua fika kuwa Baba hawezi kutuhudumia tena. Nilipika chakula harakaharaka, pamoja na kuwa katika maumivu makali lakini nilijua fika kuwa ulikua ni wajibu wangu kufanya hivyo.


Nilimaliza kupika chakula, lakini kabla ya kukitenga mezani nilisikia mlango wa geti unagongwa, ulikua ukigongwa kistaarabu tu, nilienda kufungua alikua ni Mama Abdul, yeye alikua ni mjumbe wa mtaa na alikua kaongozana na watu wengine watatu waliokua wamevaa kiraia na askari wawili.


“Baba yako yupo?” Mama abdul aliniuliza, nilitingisha kichwa kuashiria hapana. Lakini kabla ya kuwaruhusu kuingia ndani waliingia wenyewe.


“Hayupo na wala hawezi kurudi leo, Baba haishi hapa!” Niliongea kwa hasira kwani sikuwakaribisha ila waliingia tu.


“Hakuna shida, hata kama yeye hayupo lakini nyumba ipo, tunachohitaji sisi ni hii nyumba.” Kaka mmoja ambaye aliambatana na Mama Abdul aliongea.


“Ni nani mwingine yuko humu ndani?” Yule Kaka aliuliza.


“Hakuna ni mama tu.”


“Muambie atoke nnje!” Alifoka, mjumbe alimshika mkono, akamsogeza pembeni na kumnong’oneza kitu. lakini hakuonekan akuelewa aliwageukia vijana wake na kuwaambia.


“Hawezi kutembea, mtoeni mumu weke hapo nnje kisha toeni kila kitu, nyumba hii ishauzwa na Benki, Mzee wanu kashindwa kulipa deni na sasa hivi ina mmiliki mpya.”


Aliongea kwa kujiamini, nilijikuta natetemeka kwa hasira, nilimuuliza kuhusu mkopo na kumuambia nyumba ni yetu na Baba hajaiuza.


“Unajua kusoma?” Aliniuliza huku akinionyesha makaratasi kibao amabyo hata sikuyasoma. Hakukajali, wale askari waliingia na kumtoa Mama nnje, walimkalisha kwenye kiti cha magurudumu, walitoa kila kitu chetu nnje na kuviacha hapo kisha wakafunga mlango na kutondoka.


“Mume wako ndiyo alichukua mkopo na kashindwa kurejesha, document zao zote ni halali, mimi sina chakufanya ni mjumbe tu kuhakikisha kuwa hakunakitu kinaibiwa.” MamaAbdul aliongea kwa huruma, alimgeukia Mama na kumuuliza kama ana mtu wa kumpigia ili kuja kumchukua lakini alikua hana, aliulizia kuhusu vitu atavipeleka wapi lakini hakua na jibu.


“Hapa vitaibiwa, ngoja nitafute mtu akaviweke pale kwangu uwani kuna sehemu kubwa, sema tatizo mvua kama itanyesha ingawa si msimu wake ila vikikaa hapa ni hatari zaidi.”


Alitafuta vijana wa pale mtaani na kuwaomba kumsaidia kuvipeleka vile vitu ndani, alifanya hivyo na kumpeleka Mama ndani, mimi nilikua sikuingia ndani, nilikaa nnje nikiiangalia nyumba yetu kwa uchungu, sikujua ni kwanini Baba alikua akiyafanya mambo yote yale. Wakati nikiwa nimekaa pale nnje niliona magari mawili makubwa yakiingia, walishusha vitu usiku uleule na kuviingiza ndani, sikujua ni akina nani, lakini nikiwa nimekaa pale nnje mtu alinishika begani.


Sikugeuka, nilikua katikati ya  mawazo mpaka niliposikia sauti ya Mama.


“Asha nini kimetokea mbona watu wanaingia katika nyumba yetu?” Nilishtuka kidogo, nikiwaza kama kuna mtu alikua kamtoa tena Mama nnje niligeuka harakaharaka. Lakini haikua hivyo, nilimuona Mama kasimama mwenyewe pembeni yangu anaonekana mzima wa afya kabisa. Nilishangaa kuona hali ile kabla sijasema chochote simu ya Mama iliita, niliikata kwani bado nilikua na mshituko kuhusu Mama, ilipiga tena na kupiga tena.


“Kwanini usipokee nani anakupigia?” Nilishangaa kidogo kwa swali lake kwani ilikua ni simu yake, lakini sikutaka kumuuliza kama yuko sawa au la na kwanini alikua hajui ni kitu gani kilikua kinaendelea.


“Pokea anaweza kuwa ni rafiki yako!” Namba ilikua ni ngeni nilipokea na kumpa Mama lakini hakutaka kuongea niliisogeza sikioni kwangu. Haikua ni sauti ngeni, ilikua ni sauti ya Bibi, lakini tofauti na kawaida yake ambapo mara nyingi akipiga simu anakua anatukana na kuonyesha kiburi sasa hivi alikua mpole, alionekana kulia.


“Rudini nyumbani, mchukue Mama yako umrudishe nyumbani, sikua namaanisha kuwa aondoke, mrudishe nyumbani, mrudishe, utamuua Baba yako, mrudishe, nakuomba mjukuu wangu kama unampenda Baba yako basi mrudishe Mama yako katika kule ndani Baba yako anakufa.” Bibi aliongea kwa sauti ya kubembeleza.


SAFARI; MIMI, MAMA NA BABA PEMBENI!—SEHEMU YA KUMI


 Bado nilikua katika mshangao, sikutaka kujua Bibi anamaanisha nini, nilipoona anaongea maneno ambayo yanaonekana hayaeleweki nilimkatia simu, aliendelea kupiga simu mara kwa mara lakini nilikata na kuzima kabisa. Nilimgeukia Mama na kuanza kumshikashika, nilikua nikimkagua kila sehemu ya mwili wake. Nilikua simini kama Mama kaweza kuamka, nilikua simini kilichokua kimetokea ni muda mchache tu alikua hawezi hata kunyanyuka ni mtu wa kubwabwa.


“Mama umepona?” Nilimuuliza huku nikimkumbatia kwa bnguvu, bado nilikua siamini kilichokua kimetokea, nilimuomba kukaa chini nikiamini kuwa anaweza kudondoka lakini alionekana kuwa imara sana.


“Wale watu wanafanya nini nyumbani kwangu?” Mama aliongea kwa hasira huku akitembea kuelekea nyumbani, sijui kwanini lakini nilihisi kama kuna kitu kibaya kinaweza kumtokea Mama kama akiingia katika ile nyumba, nilimvamia na kumshika huku nikimlazimisha kusimama.


“Kuna nini? Mbona unanishika, hembu niache, huoni kama kuna watu wanataka kuingia nyumbani kwetu?”


“Hapana Mama usiingie katika ile nyumba, nimekuambia usiingie, ile nyumba si yetu tena, imeshauzwa na kama ukiingia utakamatwa!” Nilimuambia lakini Mama hakujali, alitaka kulazimishia kuingia, nikiwaza simu aliyonipigi Bibi na  mabadiliko niliyoyaona kwa Mama kwa muda mfupi nilijua ni lazima kuna kitu, nilimshuka Mama huku nikianza kupiga kelele.


“Mama kachanganyikiwa! Mama kachanganyikiwa! Nisaidieni kumshika! Nisaidieni kumshika kachanganyikiwa huyu!”


Nilimpiga kelele, Mama Abdul ambaye alikua ndani alitoka na mume wake, kwanza walishangaa kumuona katika hali ile, ni muda mufti tu alikua ndani kalala hajiwezi lakini ghafla alikua kanyanyuka na alikua anatembea kama hakuna kitu kilichokua kimetokea.


“Kuna niini kimetokea mbona Mama yako yuko nnje? Haumwi tena?” Mama Abdul aliuliza.


“Mama anaumwa, kachanganyikiwa, anataka kwenda kuwapiga wale watu wanaoingia nyumbani kwetu, kawatukana, naomba tumrudishe ndani nahisi anaweza kukamatwa kwani haturuhusiwi kuingia kule.


Niliongea harakaharaka huku nikiwa bado nimshikilia Mama, Mama Abdul alikuja na kumsihi Mama kuingia ndani, ili kukwepa aibu alirudi na kuingia ndani kwa Mama Abdul. Baada ya muda Mama Abdul alitoka na kuniuliza nini kilikua kimetokea.


“Bibi yangu ni mchawi!” Nilimuangalia, aliniangalia kwa mshangao mpaka nilipomuambia kitu kilichotokea, nilimuelezea kusimama kwa Mama na namna ambavyo Bibi alinipigia simu na kuniambia turudi katika nyumba yetu kwani tunamua Baba yetu.


Alinisikiliza kwa makini, niliona kabisa maneno yangu yakimuingia, alionekana kuwaza kitu flani na bila kujijua aliniongea.


“Inawezekana  ndiyo maana alikua akinipa pesa kipindi kile ili hii nyumba isiuzwe!”


“Pesa gani? Nani alikua anakupa?” Nilimuuliza lakini baada ya kuona kama nimemsikia alitaka kubadilisha mada, lakini sikumruhusu, nilitaka kujua alikua anamaanisha nini, nilimbana sana mpaka aliponiambia. Kipindi ambacho Baba alimfukuza na kumtelekeza Mama alitaka nyumba yetu kuuzwa.


Lakini kila alipokua akipata mteja basi mambo yalihaeribika, alikua hafiki bei au anaahirisha kununua mwishoni.


“Alikua akiniambia kuwa wateja wakija basi niwaambie kuwa nyumba hii inamgogoro mahakamani! Kuna kipindi ilifikia Baba yako akataka kuipangisha akamuambia lakini kila mpangaji akitaka kuhamia alikua akinituma kumtishia kuwa kuna vitu vya kishirikina wapangaji wana ahirisha.


“Alikua anamchukia sana Mama yako lakini hakutaka ahame katika hii nyumba, nilijua ni huruma zake lakini sasa nimeelewa, kuna kitu humo ndani.”


Aliongea maneno ambayo hata mimi yalinifungua akili, nilikumbuka siku moja nilisikia Bibi akimgombeza baba.


“Hivi wewe ungejua ninavyohangaika juu yako usingesema, hivi kwani kuoa wake wawili unaona shida gani, si unapesa ishi katika nyumba nyingine, kwanini tusumbuane, muache yule mwanamke aishi pale, tatizo lenu vijana wasasa hivi mkishafanikiwa mnaanza kupiga mateke vyungu vilivyowapikia wakati hmna kitu na kuhangaika na masufuria mapya!” Nilikua mdogo na kwa wkatai huo niliona kama ni Bibi anampenda Mama sikujua sababu zake.


Nilikumbuka pia kuna wakati Shangazi alikua anahangaika sana kutaka kuhamia katika ile nyumba  baada ya kukosa mnunuzi kwakua aliipenda lakini Bibi aliikataa akimuambia kama wakimfukuza Mama basi hata kuja kutembelea kaburi lake kipindi akifa wasifike. Kwa kipindi hicho niliishia tu kushangaa kwani pamoja na Bibi kumtetea Mama lakini yeye ndiyo alikua haishi kumtukana, ni mara nyingi tu alikua akimuambia Mama atamfukuza na kumuacha kuishi mitaani, ni mara nyingi alimfanyia vituko vingi vingi na kumtishia kumgukuza mwenyewe.


“Una ndugu yeyote ambaye Mama yako anaweza kwenda? Hii sehemu si salama kwake, Mama yako bado hajawa sawa, sidhani hata kama anakumuka kitu kilicokua kimemtokea.” Mama Abdul aliniuliza, niliwaza sana bila majibu, ni kweli Mama alikua na ndugu wengi lakini karibu wote walishamtengea, kutokana na hali yake walimuona kama takataka na hakuna hata mmoja ambaye alikua tayari kumsaidia. Nilimuambia Mama Abdul, alifikiria sana kisha akiniambia kuwa hata kama walimsusa lakini wakimuona katika hali mpya watampokea.


“Hii sehemu si ya kuamini amini, anatakiwa kwenda mbali, shemeu ambayo hawezi kukutana na Bibi yako kwani najua lazima ataanza kumtafuta aki…”


Kabla ya Mama Abdul kumaliza kuongea simu yake iliita, sikujua ni nani alikua anapiga simu, lakini waliongea kama dakika tano hivi, katika maongezi yake niliyashuku, ingawa hakuondoka kwenda kuongelea pembeni lakini ni kama alikua haongei anasikiliza tu, mara kadhaa alikua akiishia kusema “Mhhh… sawa… naelewa… nitajitahidi” na maneno mengine kibao ambayo kiuhalisia ilikua ngumu mtu kuelewa.


“Ni nani huyu?” Nilimuuliza kwa shauku ya kujua, alinyamaza kimya kidogo kama mtu aliyekua akitafuta jibu la kunipa kisha akaniambia.


“Ni rafiki yangu tu alikua ananiambia umbea wake, sikutaka kuongea lakini ndiyo hivyo, ningemkatia simu angekasirika.” Aliongea huku akinishika mkono kuniingiza ndani, nilitamani kuingia kweli lakini akili yangu haikukaa sawa. Nilihisi aliyempgia simu ni Bibi.


“Kama alikua akipokea pesa ili kuzuia nyumba isiuzwe ni kitu gani kitamzuia asipokee sasa hivi!” Nilihisi kitu kibaya, nilitamani kumuambia lakini nilisita, nilijua kuwa haitasaidia, nilijua hata nikiongea namna gani asingekubali kama alikua anaongea na Bibi.


Niliingia ndani kama alivyosema, Mama alikua kakaa, alikua yuko vizuri kabisa na ilionekana kama Baba Abdul kuna mambo alimuelewesha na alikua kaelewa kwani tulipoingia hakutaka tena kwenda nyumbani. Tulikaa tukiangaliana Mama Abdul alikua na wasiwasi flani, ni kama niliuelewa.


“Nimpigie Mama mdogo?” Nilimuuliza, lilikua ni swali la mtego kutaka kujua alikua akiongea na nani na kama alikua kabadilisha mawazo ya mimi na Mama kuondoka.


“Atapokea kweli? Si umesema hapatani, mimi naona umuache tu usiku huu.” Nikweli usiku ulishaingia lakini nilijua hiyo si sababu, nilinyamaza nikitafakari nini chakufanya. Kabla ya kupata jibu, simu yake iliita, safari hii hakupokelea mbele yetu, alitoka nnje, nilijua lazima alikua anaenda kuongea na mtu ambaye hataki sisi wengine kusikia na nilijua ni lazima alikua ni Bibi.


Sikua mgeni katika ile nyumba hivyo nilivyomuona katoka tu nilinyanyuka na kuchukua kikombe, nilijifanya natoka kwenda jikoni kuchota maji ya kunywa lakini niliyokea huko huko kwenye mlango wa jiko, nikasogea kwenda kumsikiliza.


“Mwanao ile nyumba kauza kimya kimya, aliichukulia mkopo ikauzwa na Binki, tena kinyemela kwani mimi mjumbe sikushirikishwa, alishirikishwa mtendaji wa mtaa, ningejua inauzwa ningekuambia, mimi leo wamenikurupusha na polisi kuniambia kuwa anatakiwa kutoka sikujua chochote.”


Alikua anongea, sikuweza kusikia upande wapili lakini nilijua lazima atakua ni Bibi na kwa namna alivyokua akimjibu basi nilikua na uhakika wanamzungumzia Mama.


“Anatembea kweli, kama miujiza kila mtu anashangaa, akili zake hazionekani kuwa sawa lakini ni mzima kabisaaa!” Alijibu na kufuatiwa na ukimya kidogo.


“Nitamrudishaje kwenye ile nyumba, nashindwa cha kumuambia, halafu huyu mjukuu wako ana akili sana, mimi sijamuambia chochote lakini naona kashtukia na hataki Mama yake kurudi…” Ukimya ulitawala kisha nilisikia 


“Nitajitahidi…”


Nilijua kabisa alichokua anataka kufanya yule Mama, harakaharaka nilirudi ndani wakati yeye akiwa anaongea na simu, nilimshika Mama mkono na kumnyanyua, kwa bahati nzuri alinyanyuka na kunifuata, nilienda kama naenda kumuonyesha kitu jikoni, nikatoka naye mpaka nnje kisha nikamvuta paka barabarani, wakati nikifanya hivyo Mama alikua akilalamika na kukataa kwenda lakini nilimsihi na kumuomba anifuate kwani kuna kitu kibaya kinataka kutokea. 


Nilifika Barabarani, kabla ya Mama kuwaza vizuri nilisimamisha Tax na kumumuambia Mama apande, hakujua tunaenda wapi lakini alinifuata, niliona kabisa kuwa ana kama kauoga flani kalikokua kakimsumbua, aliingia, ingawa sikua na pesa yoyote lakini nilimuelekeza derava Tax mpaka kwa Mama mdogo, mdogo wake na Mama, sikujua watampokeaje lakini kwao nilijua kuna afadhali kidogo kuliko kule nyumbani, njia nzima Mama alikua akiniuliza ni kitu gani kilikua kimetokea lakini sikumpa majibu ya kueleweka.


Nilifika kwa Mama mdogo na kugonga mlango, alifungua yeye mwenyewe,


“Mlipe derava Tax kwanza…” Nilimuambia huku nikiigia ndani, nilikua nimesmahika Mama mkono namvuta kama Mtoto mdogo. Mama mdogo kumuona Mama akiwa katika hali ile kwanza alishangaa, alisimama kaganda kama sanamu, mdomo umefunga hawezi hata kuunyanyua. Nilimsukuma na kumuambia aingie ndani na kwenda kuchukua pesa ya kumlipa dereva, alitoka nnje n akuongea naye, wakaelewana bei kisha akarudi ndani.


Alichukuapochi na kwenda kumlipa, alirudindani na kutukuta tushakaa, mume wake naye alikua sebuleni, alishangaa kumuona Mama katika hali ile. Kwao hawakujua kama ni miujiza sana, hawakujua kama mabadiliko yale yalitokea ndani ya siku moja, walikua wakijua kuwa labda Mama alikua kaanza ku[pona muda mrefu kwani muda ulikua umepita bila wao kujishughulisha chochote na Mama.


Mama mdogo alianza kujisemesha semesha mambo mengi, nilijua fika ilitokana na aibu, kwa namna ambavyo Mama alikua kamsaidia hawakuamini kama angeweza kupona.


“Tunataka sehemu ya kulala…” Nilimuambia, kwa namna alivyokua akijishauashaua kuita dada, kutoa pole na mambo mengine mengine ya kinafiki nilijua kabisa kuwa hawezi kukataa. Alitaka kujua mambo mengi lakini nilimuambia kuwa tuna njaa hivyo kama kuna chakula atupe lakini pia tunaomba sehemu ya kulala.


Huwezi amini kulikua hakuna chakula chochote mule ndani lakini aliingia jikoni na kutupikia. Sikuwaambia chochote kwani hata wao nilikua siwaamini, kwa mambo waliyokua wamemfanyia Mama na jinsi walivyomtelekeza sikuona sababu ya kuwaambia chochote, nilijua wataanza kujipendekeza kwani wanajua kuwa Mama sasa hivi yuko vizuri, nilikula chakula na kuingia kwenye chumba walichotuonyesha ili kulala. Mama yeye akili yake bado ilikua haiku sawa, alikua kama mtu ambaye katoka katika usingizi mkali hivyo niliweza kumuamrisha na kumlazimishia kufanya kila kitu ninachotaka mimi.


Tuliingia ndani na kulala, nilikua nimechoka sana hivyo ile kupanda tu kitandani na baada ya kuhakikisha kuwa Mama yuko pembeni yangu na mlango nimefunga basi nililala fofofo, nilikuja kuzinduka asubuhi yake. Jua lilishawaka, niliangalia pembeni na kuona Mama kashaamka, nilitoka nnje, sikumkuta mtu yeyote zaidi ya binti wa kazi, nilishtuka na kumuuliza Mama  Mdogo yuko wapi?


“Kaenda kazini…” Aliniambia.


“Na Mama?” Nilimuuliza lakini alionekana kama vile haelewi chochote.


“Mama yangu? Hujamuona Mama mrefu amevaa….”


“Kaondoka asubuhi ile ile na Mama mdogo, kapigiwa simu sijui Baba yako anaumwa Mama mdogo kamsindikiza nyumbani….”


“Nyumbani????” Niliuliza kwa mshangao huku nikitoka mbio kumkimbia kuelekea nnje…”


SAFARI; MIMI, MAMA NA BABA PEMBENI!—SEHEMU YA KUMI NA MOJA


Nilichukua simu ya Dada na kumpigia Mama mdogo, nilijua Mama hana simu, alipokea na nilipoongea naye aliniambia tayari alishamuacha mama nyumbani kwetu na alikua anaenda kazini.


“Rudi kamchukue, Mama hatakiwi kuingia ndani!” nilimuambia kama kumuamrisha, aliniuliza kwanini nikamuambia kuna mambo ya kishirikina na kama Mama akiingia basi atarudia kuumwa. Sikujua sababu ya Mama kuumwa lakini nilishahisi hivyo na nilijua moyoni mwangu kuwa kama Mama akiingia nyumbani basi atarudia hali yake ya zamani.


Mama mdogo alinisikiliza na kuonyesha kunipuuzia, aliniambia kuwa Mama alipigiwa simu kuwa Baba anaumwa na anatakiwa kurudi nyumbani.


“Baba yako ana hali mbaya, nimefika kuna watu wamejazana, acha hayo mambo yako, Bibi yako hawezi kumfanyia hivyo Mama yako!” aliongea kwa hasira na kukata simu, sikukubali, niliendelea kumpigia mara nyingi lakini hakupokea na alipoona kama namsumbua basi alizima simu kabisa.


Kuona vile niliamua kutoka, kama kawaida yangu nilichukua Tax, ingwa sikua na pese ya kulipa lakini nilitaka kufika nyumbani na kumtoa Mama kwani nilijua kwakuingia tu ndani basi angerudi kuwa mlemavu. Nilifika nyumbani na kukuta watu wamejazana nnje, nilihisi labda kuna msiba na akili zangu nilijua kuwa ni Mama, lakini kwa namna walivyokua wamesimama ilionyesha kama wanshangaa kitu kwani kuna wakati walikua wakipiga makelele ambayo hayakueleweka.


Nilimuambia Dereva Tax kusimama nimefika, aliniomba pesa nikamuambia ziko ndani, alianza kubiahsa bisha lakini kabla ya kufunga milango nilishashuka na kujichomeka katikati ya watu, nilimsikia akipiga kelele kuniita lakini sikugeuka nyuma. Nilijipenyeza katikati harahakaharaka kama mshale, ghafla nilijikuta nimesimama katikati ya kundi la watu.


Kama umeshawahi kuangalia wale wachekeshaji wa mitaani ambao hukaa katikati na kuchekesha au kupiga sarakasi huku wakizungukwa na watu waliosimama kwenye duara basi ndiyo ilikua hivyo kwangu. Nilikua katikati ya watu, mbele yangu kulikua na mwanamke kavua nguo yuko uchi wa mnyama, nguo zake ziko pembeni, watu walikua wakimuangalia jinsi alivyokua akijiviringisha kwenye mchanga na kupiga kelele mchewi huyo mchawi! Wengine wakiongea chizi huyo chizi!


Nilimuangalia hakua mwingine bali ni Bibi yangu mzaa Baba, alikua peke yake katikati, nguo zake ziko pembeni yake. Watu walikua wanshangilia tu, hakuna aliyekua anajali kuwa ni mtu mzima, ingawa nilijua kuwa ni cmhawi na sikujua ni kitu gani kilikua kimetokea lakini bado alikua ni Bibi yangu. sikutaka kuendelea kumuona akiadhirika kiasi kile, nilikimbilia harakaharaka zile nguo na kumfunika nazo, ile kumgusa tu ni kama nilikua nimemshtua kutoka usingizini.


Alijiangalia na kukuta yuko uchi, alizipokea zile nguo na kujisitiri, kulikua na kitenge alijifunga harakaharaka  na kuvaa gauni.


“Niko wapi?” Aliniuliza.


“Nyumbani Bibi, sijui ni nini kimekupata lakini tuondoke hapa. Nilimuambia huku nikimshika mkono kumtoa kwenye kundi la watu. Watu kuona nimemvalisha nguo nataka kumuondoa pale walianza kupiga kelele za kuashiria kuwa ni mchawi na asiachwa aondoke, walimzuia kupita na kuanza kumpiga. Nilijua kuwa watamuua hivyo nilijipenyeza harakaharaka na kumvuta mpaka mlangoni.


Geti lilikua wazi, nilimsukumizia Bibi ndani harakaharaka kisha nikaingia na kulifunga kwa ndani, kwa bahati nzuri watu waliishia kupiga kelele tu hakuna aliyejaribu kuingia. Bnililifunga na kumkimbiza bibi kuingia ndani kwenye nyumba kubwa. Lakini ile alipokanyaga tu mlangoni, mlango wa nyumba kubwa ili kuingia ndani alipiga ukulele.


“Nakufaaa! Nakufaaa!” Kuna kitu kilimrusha juu na kumdondosha chini kama shoti ya umeme, kufika chini alianza kujigalagaza na kupiga kelel kuwa anaungua hivyo akaanza kuvua nguo tena.


Nilimfuata kumvalisha na nilipomgusa tena alirudi katika hali yake ya kawaida akaanza kushangaa ni kitu gani kilikua kimetokea. Nilishangaa na kumuuliza inamaana alikua hakumbuki chochote akasema hapana, nilimuuliza mambo mengi na hakua na majibu yoyote alikua akinishangaa tu. Nikiwa niko pale chini namuangalia alitoka bibi mmoja hivi, alikua ni wamakamo ya Bibi yangu, nilisimama na kumsalimia.


“Wewe ndiyo Asha?” Yule bibi aliniuliza, nilishangaa kwani ilikua ndiyo mara yangu ya kwanza kumuona.


“Mama yako anakutaja sana, akushukuru sana kama si wewe angekua shakufa, una nguvu za ajabu mjukuu wangu, una akili sana.” Aliniambia huku akininyooshea mkono kutaka kunishika, nilisita kwani nilikua simfahamu lakini yeye alionyesha kunifahamu sana.


“Mama yangu yuko wapi?” Nilimuuliza, badala ya kunijibu aliendelea kuninyooshea mkono, kwa uoga nilijikuta nampa mkono wangu, alininyanyua hivyo kunifanya kumuachia bibi pale chini amabye alikua kalala kwa aibu.


“Mama yako yuko ndani, kalala, hali yake si nzuri lakini atapona, atatembea tena.” Aliniambia, nilianza kuwa na wasiwasi kwa yeye kusema kuwa Mama atapona na kutembea tena wakati aliondoka nyumbani kwa Mama mdogo akiwa anatembea. Alinivuta mpaka ndani, niliingia kwa wasiwasi, ingawa nilikua nikiifahamu ile nyumba mpaka uvungu wake lakini siku ile nilikua mgeni kidogo, kila kitu kilikua kikpya mule ndani na watu waliohamia walionekana kuwa na uwezo mkubwa kifedha kwani fenicha zilikua zinaonyesha za gharama sana.


“Mwanangu ndiyo kanunua hii nyumba, tumehamia jana lakini mambo yake ni makubwa,!” Aliongea wakati anaenda kunionyesha alipokua Mama.


“Tangu jana usiku Bibi yako alikua akizunguka humu kutaka kutoa vitu vyake, lakini nilishamuwahi, hawezi kuvitoa na hivyo ndiyo vinamsumbua, bado vipo lakini havifanyi kazi, Mama yako ndiyo vinamuumiza!” Aliendelea kuongea, akili yangu yote ilikua kwa Mama, nilitaka kujua ni kitu gani kilikua kimemtokea. Niliingia kwenye chumba alichokua Mama, alikua kalala kitandani, picha ya kwanza kipindi nimekuja kutoka shule na kumuona kwa mara ya kwanza kapooza ilinijia.


Mama alikua kalala hajiwezi, nilijikuta natetemeka, miguu ikashindwa kabisa kunyanyuka, uoga ulinishika mpaka yule bibi aliponisikuma na kuniambia nimshike Mama yangu mkono, nilimshika na nilishangaa Mama anasimama na kurudi kama kawaida.


“Nilikuambia una nguvu kubwa sana, Bibi yako hawezi kupenya nguvu uliyonayo,. Jina lako linatoka mbali upande wa Babu yako, uchawi wao si wa kununua kama wa bibi yako.” Yule bibi aliongea mambo mengi sana, ni kama alikua akinijua nilishangaa aliponiambia.


“Ile ajali ilikua ni Mama yako afe lakini kwakua ulikua ndani ya lile gari alishindwa…” Nilizidi kutetemeka kwa uoga aliponiambia mambo ambayo yalitokea zamani.


“Mama umemuambia kitu?” Nilimuuliza Mama ambaye alitingisha kichwa kuacha.


“Hajaniambia mtu, mimi si mganga lakini kama nimechanjwa, Mama yako alikua kama msukule, tena si wa mali hapana, Bibi yako ana maagano yake na sadaka yake ilikua ni Mama yako. Hakupona kwasababu alihama hii nyumba, hpana….


Ingawa vitu aliwekewa humu lakini nilipoingia humu na mwanangu vitu vyangu vikagongana na vya Bibi yako ndiyo maana alichanganyikiwa.” Aliongea maneno mengi na yote ya kishirikina, tukiwa pale aliingia Kaka mmoja, nilikumbuka nilimuona jana yake, alikua ni mmoja wa wale waliokua wakihamisha vitu. Alitusalimia na yule Bibi alituambia kuwa ni mtoto wake kisha akabadilisha mada. Alionekana kutokutaka mwanae kujua kilichokua kikiendelea alizuga na mambo mengine.


“Kumbwa hawa ndiyo walikua wakiishi humu, walikuja hapa kuangalia kama kuna vitu vyao humu. Kuna vyeti vya masomo vya huyu binti, hujamuonea?” Alibadilisha mada kabisa, mwanae hakuonekana kama ni muongeaji sana, alisema hapana kisha akauliza kuhusiana na kundi la watu huko nnje.


“Hata sijui lakini labda ni tamaduni za huku, Mama Nancy yuko wapi?” Alijibu na kubadilisha mada hapohapo.


“Kazini, kuna Mtu kakaa hapo nnje, anaonekana kama ombaomba, si nilishakuambia Mama hapa ni mjini acha kuwafungulia watu hovyo hovyo, najaribu kuongea naye lakini hata hanielewi!” Yule Baba alifoka kidogo.


“Mjukuu wangu mwenye nyumba ndiyo huyo, kashakuja na kaseam hakuna kitu walichokiona, wewe ondoka tu kama tukiona nitakuambia, ilimradi namba zenu ninazo basi kama vipo humu ndani tutaviona na tutawapigia simu.” Aliongea huku akitunyanyua, wakati huo mwanae alishaenda zake chumbani kwani tulishatoka kwenye chumba alichokua Mama na baada ya kunyanyuka tulirudi sebuleni.


Nilijua kabisa anazuga hivyo nilimshika Mama mkono tukatoka,a litundikiza mpaka nnje. Tulimkuta Bibi kakaa hajielewi elewi, alipotuona alinyanyuka, yule bibi alimsogelea na kumpiga makofi mawili kulia na kushoto usoni. Alizindika na kunyanyuka, akili zake zilionyesha kurudi.


“Usikanyage tena kwenye hii nyumba na hata siku moja nikisikia umemsumbua huyu binti nitadili na wewe mimi mwenyewe, hutaishia tena kuvua nguo kama kichaa, kama sasa hivi ulikua ukiungua mwili basi nitayaunguza maini.”


Bibi alitoka mbio mule ndani, alionekana kumuogopa yule Bibi mwingine, mimi na Mama tulitoka taratibui na kumkuta Bibi kakaa chini analia, watu walishatawanyika tawanyika lakini walipomuona  pale nnje walianza kurejea, Bibi alikua akilia huku akipiga magoti kuomba msamaha, alikua akimlilia Mama na kumuomba msamaha kwa yote aliyokua kayafanya. Kwakua watu walikua wakizidi kuongezeka niliona itakua ni msala, nilimshika Bibi na kuingia kwenye Tax iliyokua pembeni yangu, sikuangalia lakini ilikua ni ya yule yule niliyemkimbia.


“Nataka pesa yangu!” Alianza kuongea baada ya sisi kuingia. Watu walsihaanza kutuzingira na kupigapiga gari lake kumtaka amshushe Bibi, kuona vile aliacha kulumbana na kuondoa gari kwa kasi, alienda mpaka sehemu salama ndipo alisimamisha gari na kusema hakuna mtu kushuka mpaka alipwe. Sijui alitoa wapi lakini Mama alikua na pesa zake, alitoa na kumlipa. Alitaka kuwahsa gari lakini nilimkataza.


“Huyu anashuka.” Niliongea huku nikimuangalia Bibi, aliniangalia kwa mshangao hata Mama alinishangaa.


“Kwanini uansema hivyo, kwani Bibi yako kafika, tunampeleka nyumbani, kwake kwanza.”


“Mama huyu mwanamke ni mchawi siwezi kukaa naye gari moja!” Niliongea kwa hasira, nilikua nimekaa katikati wote watatu tukiwa siti ya nyuma, niliinama kwenye ule mlango aliokua kakaa bibi kisha nikafungua na kuanza kumsukuma atoke.


“Nimekuambia kuwa huyu ni Bibi yako ni lazima umheshimu, hata kama kakosea lakini huna haki ya kumjibu hivyo, nitabia mbaya!” Mama alianza kunifokea huku akinishika nisimshushe Bibi, tulizozana sana nikiamini kuwa labda Mama akili zake zishamruka na kasahau mambo yote aliyofanyiwa na Bibi.


“Nafahamu kila kitu mwanangu, mimi ndiyo niliteseka, najua Bibi yako kakosea lakini kashakuomba msamaha, huyu ni Bibi yako, Mama wa Baba yako, ni lazima kumheshimu kama unavyoniheshimu mimi! Hivi unafikiria Baba yako atajisikiaje akisikia unamuita Mama yake mchawi na kumsukuma kumfukuza kwenye gari?”  Aliniuliza, sikutaka kumchelewesha nlimjibu palepale.


“Hata akijisikia vibaya sijali, wote wachawi tu tena wang…” Kabla sijamaliza Mama alinipiga kofi zito usoni, niliona nyotanyota na kushikwa na kizunguzungu.


Niliksairika kuwa Mama bado anawatetea, nilijaribu kulia lakini machozi hayakutoka, Mama alikua akiongea maneno yake ya kila siku kuhusu kuwa na adabu, kuwaheshimu wakubwa na mambo mengine mengi. Mimi sikumsikiliza, kwa hasira nilijikuta najirusha kwenye mlango ambapo nilishaufungua, nikamruka bibi kisha nikatoka nnje. Mama alitoka kunisihi niingie kwenye gari lakini sikukubali, nilitoka na kuanza kutembea kwa miguu huku nikiapa kuwa siwezi kukaa gari moja na  Bibi yangu.


Mama alinibembeleza sana lakini nilikataa, nilimuambia ni bora kuishi mitaani kuliko kuishi na Bibi, nilimuambia kwa namna nilivyoteseka kumhudumia siko tayari kusamehe.


“Basi baki hapa, ngoja nikamkabidhi Bibi yako kwa Baba yako nitakurudia, au chukua pesa hii panda gari nenda kwa Mama yako mdogo nitakukuta huko, ngoja nimgikishe kwanza Bibi yako.” Aliongea hukua kitoa notion ya Shilingi elfu tano mfukoni, sijui kwanini lakini nilijikuta naipokea tu.


Mkono wangu na wa Mama uligusana, kitendo kile kilinipa huzuni ya ajabu, nilipatwa na msisimoko ambao hata hauelezeki. Niliushika mkono wa Mama kama vile ilikua ndiyo mara yangu ya mwisho kuushika. Mama alinikabidhi harakaharaka na kuingia kwenye gari, wakati wote alikua akinisisitiza nirudi kwa Mama mdogoa tanikuta kwani anampeleka Bibi nyumbani kwake. Aliingia kwenya gari na gari ikaondoka, lakini iliposhika kasi tu nilijisikia vibaya, nilihisi kitu kibaya.


Nilishindwa kuvumilia, nilianza kuikimbilia nikimuomba dereva kuimamisha gari ili na mimi niingie, sijui kwanini lakini nilihisi kuna kitu kibaya kinaenda kutokea. Gari iliondoka kwa kasi kidogo, nilipoanza kuita Derevaa alisikia akachungulia dirishani na kuninyooshea mkono kama vile ananiuliza vipi. Lakini kabla ya kumjibu niliona lori ambalo lilikua limebeba Mchanga likiipitia ile gari waliyokua Mama, Dereva alikua anaingia kwenye barabara kuu bila kuangalia pembeni ndipo lile lori lilimvaa na gari kurushwa juu kama takataka.


“Mamaaaaaaaaaaaaaa!” Nilijikuta napiga kelele huku nikilikimbilia lile gari.


Unadhani nini kimemkuta Mama Asha, je ndiyo Bibi kaamua kummaliza au nini kimetokea. Hamtasubiri sana ni kesho au endelea kufuatilia ukurasa wangu wa Instagram @iddimakengo kuwa wakwanza kujua kitakachoendelea.


ITAENDELEA….


SAFARI; MIMI, MAMA NA BABA PEMBENI!—SEHEMU YA KUMI NA MBILI


Baada ya kuviringiswa mara kadhaa ile gari ilitulia, iligeukia juu chini na ilikua imepondeka sana. Nilikimbilia mpaka pale, kwa bahati nzuri kulikua na watu wengi hivyo walikimbilia ile sehemu na kuanza kuokoa. Walifanikiwa kuvunja milango na kuwatoa watu, Derava alifia palepale, mama alitoka akiwa kaumia kidogo na Bibi alikua anapumua lakini hajitambui, alikua kavunjika mguu na kupasuka kichwani, kuna chuma kilimchoma kwenye paji la uso, damu nyingi zilikua zinamtoka, alikua akirusharusha mikono ingawa hali yake ilikua mbaya sana.


Gari ya pilisi ilikuja ndani ya muda mfupi, waliondolewa pale lakini Bibi alifia njiani, Mama alifika hospitalini, hakuumia sana hivyo siku iliyofuata aliruhusiwa. Wakati wote huo mimi nilikua hospitalini na Mama, hakukua na ndugu yeyote upende wa baba ambaye alikuja kumuona Mama, hata Baba hakuja, kila mara nilipomuuliza Mama aliniambia.


“Baba yako ana mambo mengi, wewe hujui kuwa Bibi yako kafariki, ulitaka aje hapa kufanya nini?” Nilinyamaza, sikutaka kuongea kitu kibaya lakini nilijua kabisa kuwa Baba hakua akimpenda Mama na niliamini kuwa alitamani Mama ndiyo angekufa.


Baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Mama alirudi kwa Mama mdogo, lakini hakukaa, alianza kujiandaa kwenda msibani. Nilimsihi kupumzika lakini hakukubali, nilimuambia kuwa wale watu hawampendi lakini hakujali,a lisema yule ni Mama mkwe na ni lazima kwenda kumzika.


“Lakini ni mchawi!” Nilimpa jibvu ambalo lilimkasirisha, alinishika na kunifinya sikio kwa nguvu.


“Kua na heshima na Bibi yako, Marehemu hawasemwi vibaya!”


“Lakini ni kweli Mama, kama mtu ni mchawi unataka tusemeje, kama asingetaka kusemwa vibaya asingekua mchawi!”


Nilimuambia kitu ambacho kilizidi kumkasirisha, alinishika kutaka kunipiga lakini Mama mdogo alikuja na kuingilia kati.


“Usiseme hivyo wewe bado mtoto!” Mama mdogo alinifokea, nilimuangalia kwa hasira kwani nilijua nayeye pia ni mnafiki tu, lakini sikua na chakusema hivyo nilinyamaza. Mama alijiandaa kwenda msibani.


“Twende ukamzike Bibi yako!” Aliniambia wakati anataka kutoka, nilimuangalia kwa hasira bila kusema chochote, sikutaka kujihusisha chochote na familia ya Baba, lakini Mama alinibembeleza na maneno yake ya kukasirisha.


“Baba yako kafiwa na Mama yake, anahitaji mtu wa kumfariji, hivi unafikiri ningekufa mimi wewe usingetaka mtu wa kukufariji?” Aliniuliza, sikumjibu chochote, nilibaki kimya. Wakati anatoka nilimfuata, nilimuambia naenda, ingawa yeye alifurahia kuwa nimemsikiliza naenda kumfariji Baba lakini moyoni nilienda kumlinda, sikua na imani  yeye kwenda peke yake. Kwa muda niliokaa kumhudumia Mama nilishaanza kumuona kama mtoto wangu hivyo kuna wakati nilijisikia vibaya sana kumuacha peke yake, niliongozana naye mpaka wkenye Gari la Mama  mdogo ambaye alitupeleka.


Kule msibani hakukua na watu wengi sana, wengi walikua ni ndugu wa karibu, tuliingia ndani walipokua akina Shangazi, baada ya sisi kuingia tu, Baba alinyanyuka na kumfuata Mama, alimshika mkono kama mtu anamminya vile na kumvuta kwa nnje, waliongea maneno ambayo mimi sikuyasikia, walikua wakinong’onezana lakini kwa namna ambayo ilikua ni kama kufokeana. Waliongea kwa kama dakika tatu hivi kisha Mama akarudi, alikua kabadilika, alikua na hasira sana.


Alinishika mkono na kuniambia kua tuondoke, sikumuelewa, nilitaka kubaki ili kujua nini kimetokea lakini alinilazimisha, nikatoka na wote kama tulivyoingia tukaondoka. Kwenya gari Mama mdogo alimuuliza sababu ya kufanya vile lakini hakujibu, Mama alikua akilia tu, kuna maneno Baba alimuambia na naamini kuwa yalimchoma sana lakini hakua tayari kutuambia. Msiba ulikua ukisafirishwa kijijini, hatukuenda na nilipomuuliza Mama hakua na jibu, moyoni nilijua kuwa hakua akitakiwa kwenye msiba na nilijua kabisa kuna maneno mambaya ambayo baba kamuambia.


****


Hali ilikua nzuri sana, baada ya mazishi akina Baba walirudi lakini hawakuwahi kututafuta. Ulipita mwezi mmoja, Mama alikua na afya nzuri na alianza kutafuta kazi, mimi nilishaacha shule zamani kipindi namhudumia Mama, ingawa Mama alitaka nirudi shule lakini niliona shida kwenda kurudia, nilitaka kufanya Biashara nikiamini kuwa mafanikio ni popote. Lakini Mama hakutaka, alitaka nirudi shule na siku moja alimpigia simu Baba ili aongee na mimi kuhusu kurudi shule.


Bado tulikua tukiishi kwa Mama mdogo, siku hiyo nikiwa nimetoka mjini kuonana na marafiki zangu nilirudi nyumbani na kumkuta Baba kakaa, alinichangamkia lakini mimi niliingia bila hata kumsalimia. Nilipofika Mama alianza kujishaua kuwa Baba yako anataka kukusomesha, unatakiwa kurudi shule.


“Hapana, sijasema hivyo, uliponipigia simu nimeamua kuja kumchukua mwanangu! Umemharibia maisha yake na unaweza hata kumuua kama ulivyomuua Mama yangu, wewe ni shetani, na makafara yako yote tunayajua…” Baba alitukana sana, alionekana kubadilika ndani ya dakika moja.


Alimtukana Mama matusi ya nguoni, alikua akimshutumu kwa uchawi huku akimuambia kuwa Mammbo yake hayaendi kwakua alimloga.


“Nimesimamishwa kazi! Biashara zangu haziendi, kila kitu kimebadilika, Umemuua Mama yangu sasa unataka na kunifilizi mimi!” Alitukana sana akimaanisha kuwa tangu Bibi kufariki kila kitu kilikua kinamuendea kombo na alikua akimlaumu Mama kwa hilo.


“Siondoki na wewe! mama yako ndiyo alikua mchawi, alimfanya Mama yangu msukule, nyie wote niw achawi na nibora kufa kuliko kuishi na wewe!”


Niliongea kwa hasira, nikijua kabisa kuwa Mama atakua upande wa Baba nilityoka nnjke na kukimbia, nilishakua mkubwa na akili zangu sikutaka kupelekwa pelekwa tu! Mama alianza kunikimbizaa kiniambia niende kumuomba msamaha Baba kwa kumtukana lakini sikujali, niliondoka kabisa, sikurudi nyumbani siku ile, nilichofanya ni kwenda kwa rafiki yangu, nilimpigia simu Mama na kumuambia kuwa siwezi tena kurudi nyumbani na kama ni kuhusu Baba basi mimi ni yatima sina Baba nina Mama tu kama yeye atavumilia basia vumilie kunyanyasika lakini si mimi.


Mama alinisihi sana lakini sikukubali, niliamua kuendelea na maisha yangu. Rafiki yangu huyo alikua ni mtu mzima kidogo, ni dada ambaye alikua akiuza mihogo nnje ya shule yetu, alikua na katoto kake kadogo ambako alikua akija nako, kalikua kakinipenda sana na mimi nikikapenda, kwakua kipindi nasom Baba alikua akinipa pesa nyingi basi nilikua namsaidia sana hivyo alikua kama dada yangu. bado alikua akiuza mihogo na mwanae alishakua mkubwa kidogo, nilimuambia nataka kuishi kwake na nataka kufanya Biashara, alijaribu kunishawishi kurudi nyumbani lakini nilikataa, nilitaka kuwa na maisha yangu.


Kwakua alikua akiuza mihogo katika shule niliyokua ninasoma niliona shid akuongozana naye, nilijua kama nikienda basi kuna watu wataniona na watamuambia Baba nilipo. Niliamua kuachana na Biashara ya mihogo na kuanza kuuza matunda, nilianza na mtaji wa elfu kumi na nilikua nikiuza machungwa. Nilikua nikiyaweka kwenye beseni kisha naenda kwenye kijiwe ambapo kuna wakaka wengi naanza kuwauzia, nilikua na malengo makubwa hivyo kila Shilingi niliyokua nikiipata nilikua nikiweka.


Mama yeye alifanikiwa kupata kazi, ingawa iskumuambia nilipokua lakini nilikua naongea naye kila siku na namuambia anendeleaje. Kwa upande wa Baba kila kitu kilikua kimeharibika, kumbe alishaoa wanawake wawili na waote walimuacha, waliondoka na watoto, Sudi alikua akisoma bweni akilipiwa na Shangazi yangu mmoja,  baba alikua hanapesa tena mtu wa kutangatanga. Aliuza vitu vingi walivyochuma na Mama, na baada ya kuona kuwa Mama mambo yake yanamnyookea basi alianza kumtafuita na kumuomba msamaha.


Kila siku nikiongea na Mama alikua akiniambia namna ambavyo Baba kabadilika, namna ambavyo kajutia na mambo mengine mengi. Mimi sikumuelewa nilimuambia kuwa Baba ni shetani na sitaki kusikia mambo yake. Pamoja na kumuambia lakini bado alikua akisisitiza kubadilika, Mama yangu ananipenda na alitaka baraka zangu. Ingawa nilijua kuwa watarudiana lakini sikutaka kumuambia Mama arudiane naye, nilikua namchukia sana Baba yangu na mpaka sasa bado namchukia, nilijua Baba ni shetani na pamoja na mambo ya kishirikina ya Marehemu Bibi lakini Baba naye alikua na matatizo.


Biashara yangu ilikua inaenda vizuri, Mama alitaka kunipa mtaji lakini nilimuambia hapana, yeye mwenyewe maisha yake yalikua hayajasimama vizuri. Baada ya kama mwaka hivi niliacha kuuza mchungwa ya rejareja na kupanuka mpaka kwenda shambani kununua na kuuza machungwa ya jumla. Mama alirudiana na Baba kimya kimya bila kuniambia mpaka siku moja nilipoenda kumtembelea na kumkuta Baba pale nyumbani. Walimchukua mdogo wangu na kuanza kuishi naye, waliniomba sana kurudi nyumbani lakini nilikataa mpaka sasa bado sijamsamhee Baba na najua yuko na Mama kwakua hana kazi.


Baba hana kazi, Mama alishampa mitaji mingi ya Biashara lakini zinaishia kwa wanawake zake, mimi najua, Mama anajua lakini hawezi kuongea. Nikimuambia kitu ananiambia kuwa “Wewe bado mtoto hujajua ndoa ni nini?” Baba anaishi kwa Mama na anamtegemea kwa kila kitu, mimi nina maisha yangu na namsaidia Mama kumsomesha mdogo wangu. Ndugu wa Mama nao wanajipendekeza kwakua Mama mambo ni mazuri, kwa upande wa ndugu wa Baba ni kwamba washamtenga na hakuna hata mmoja ambaye anahangaika naye kwakua hana  pesa analishwa na kuvishwa na Mama.


****MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG