Search This Blog

Wednesday, June 22, 2022

KAMA HUTAKI MWENYE MAMBO YA KIKE OA MWANAUME!

 


IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO


KAMA HUTAKI MWENYE MAMBO YA KIKE OA MWANAUME!

HUYU MAMA YAKO NAYEYE TUMPELEKE WAPI?

MWANANGU MWANAUME NI KAMA GARI!



Hiki ni kitu kikubwa, wanaume ni tofauti sana na wanawake, mwanaume ni mtu wa kutatua matatizo hivyo unapomuambia matatizo yako basi anakupa jibu moja kwa moja, wakati wanawake wao wanapenda kuongea, wakati mwingine hata hawataki majibu. Sasa unapoongea na mume wako ukamuambia shida yako usimfanye kama shoga yako kwamba akusikilize tu unalalamika kutwa nzima bila kukuambia suluhu.


Hapana, utamuambia kuwa labda kazini kuna shoga yangu ananiwekea vijembe whatsapp status, wanaume wengi haawatataka kujua hata sababu, utasikia anakuambia, wewe mblock basi, hapo ashamaliza. Ila wewe ulitaka mu0ngee, umchambe huyo shoga yako


“Baba mimi huyu mwanamke namuacha, yaani hataki kunisikiliza kabisa, ana kisiorani balaa, kila siku tunagombana, nikimuambia kitu hafanyi, yaani nimechoka na hii ndoa!” Hamisi alimuambia Baba yake.

“Kwani kuna tatizo gani?” Baba yake alimuuliza, walikua wamekaa sebuleni wanaongea.

“Hata sijui, simuelewi kabisa, kila siku anarudi kanuna, anagombana na majirani akirudi anataka na mimi nigombane nao….”


Hamisi alionmgea kwa hasira, lakini kabla Baba yake kumjibu Mama yake aliingia. “Nilishakumbia kuwa usiongee naye lakini hunisikii, mbona kaniambia kuwa ulimsalimia, hivi nyumba hii mbona mimi naonekana kama kituko, ni nini lakini….” Mama yake bila hata salamu alianza kulalamika, aliweka pochi yake chini na kukaa kwenye kocho huku akijiinamia.


Baba Hamisi alinyanyuka na kwenda kukaa karibu na mke wake kisha akamuuliza.

“Nini tena, yule mshenzi amefanya nini tena?” Hamisi alishangaa Baba yake kuongea vile lakini alibaki kimya, mara Mama yake akaanza kulalamika.

“Yaani nakuambia, nimetoka zangu sokoni nimepita pale kwake ananirushia jicho la dharau mimi nikasema hapana, ana nini huyu, mara ooo husalimii ila mume wako akipita hapa anasalimia…..” Mama yake alilalamika vitu vingi. Kazi ya Baba yake ilikua ni kumuambia “Achana naye… sikusumbue… kuanzia kesho hata mimi sitaongea naye… aisee… mhhh hapana….”


Alikua hatoi ushauri wowote, alimsikiliza mke wake kwa zaidi ya nusu saa ndipo akawa sawa. Mama Hamisi ndiyo alinyanyuka na kusalimiana na mtoto wake kisha akaingia chumbani kubadilisha nguo.

“Baba inamaana na Mama anye analalamika kiasi hicho, halafu mbona kakuuliza mambo mengi na kila kitu unakubaliana naye… mbona wagombana vitu vya kijinhga anakuja kukuambia…. Inamaana yeye kukorofishana na shoga yake anakuja kukuambia wewe?”


“Mwanangu, Mama yako ni Mke wangu, unataka umbea wake aende kumuambia nani?”

“Sasa Baba wewe hayo mambo ya kike yanakuhusu nini?” Hamisi alimuuliza, Baba yake alinza kwa kucheka kisha akamuambia.

“Yananihusu kwakua nimeoa mwanamke, ningetaka mtu wa kuongea naye mambo ya kiume ningeoa mwanaume. Mwanangu, si kila wakati mke wako anapokuja kwako anahitaji mawazo yako, hapana, mara nyingi wanawake wanahitaji watu wa kuonge nao.


Wao ni tofauti na sisi, sisi tukiwa na visirani vyetu tunakaa navyo, ila wake zetu wakiwa na visirani vayo wanaongea na wanahitaji mtu tu wa kusikiliza. Mfano nimeongea na Mama yako zaidi ya nusu saa ananielezea ugomvi wake ambao hata haunihusu ila, nimemsikiliza na sielewi chochote na yeye kaondoka na furaha. Hivyo mwanangu, nenda kaongee na mke wako, mpe angalau nusu sa kila siku ya kusikiliza malalamiko yake.


Mwanangu, mwanamke anaweza kutoka sokoni na kuanza kulalamika jinsi alivyouziwa vitunguu vibovu au jinsi Dada wa M-Pesa alivyomuangalia kwa dharau, msikilize, mponde huyo dada wa Mpesa ambaye hata humujui basi utakua na amani. Lakini kama kila ukirudi upo bize na mambo yako, anakuelezakuhusu mfanyakazi wa jirani ambaye anatembea na mume wa mtu unajifanya hayakuhusu analalamikia mtu wa saluni alivyoiba mabunda yake ya rasta unajifanya hujali basi kia siku utakua mtu wa kisirani mwanangu, kama hutaki mwenye mambo ya kike oa mwanaume au kaa mwenyewe!”


MWISHO


HUYU MAMA YAKO NAYEYE TUMPELEKE WAPI?




“Baba, mimi nakuambia kuwa, kwa yule mwanaume sirudi kama hajamfukuza Mama yake! Hapana, siwezi kukaa na yule mwanamek, yaani anajifanya kuwa kila kitu anakijua, kila saa nikuongea, nyumba yangu lakini nakua kama mgeni! Amuondoe Mama yake au niondoke mimi, ndoa haina hata mwaka naanzas kupangiwa maisha tena na Mama mkwe!” Halima alimuambia Baba yake, alirudi nyumbani kwa hasira ili kuongea na Mama yake lakini alikua katoka hivyo alilazimika kumuambia Bbaa yake.


“Kwani huyo Mama mkwe aanakupiga?” Baba Hamisi alimuuliza.

“Hapana Baba, lakini kwa anavyoongea na kutukana ni bora kupigwa, sitaki, simtaki yule mwanamke.”

“Unataka aende wapi, ndiyo kafiwa na mume wake, kijijini hakuna mtu na anaumwa, si umesema ana Presha na dawa zake anachukulai Muhimbili sasa atakaa wapi?”

“Sijui lakini siwezi kukaaa naye, sina amani, siawezi kumvumilia.” Halima aliendelea kuongea, Baba yake alimuambai atulie na asiwe na wasiwasi.


“Mwanangu hapa ni kwako, utakaa mpaka uchoke.” Baada ya kumuambia hivyo alitoka nnje na kuchukua viatu vya Halima nakuviingza ndani, akaviweka sebuleni katikati sehemua mabyo vi8naonekana. Halima alimuuliza ni kwanini anafanya hivyo ila alimuambia subiri utaona, Mama yako akija utaona. Baada ya kama nusu saa hivi Mama yake alikuja, Halima alimsalimia, lakini hakuitikia, aliona viatu chini na hasira zilimpanda.


“Hivi wewe una akili wewe? Unajua nainamisha mgongo mara ngapi hapa? Hivi nilizaa mtoto au jiwe ambalo haliosikii, unaingia na viatu unaweka ndani, nilikufundisha nini? Umekuja kwangu unajikalisha, Baba yako yuko hapo hata kuona aibu kuwa umeolewa uwwe msafi, hivi kama hapa kwangu unaacha viatu hivi kwako si utaacha chupi mezanio!”


Mama yake aliona viatu tu lakini alionga na kutukana sana, hata salamu hakuitikia,a kachukua viatu akavitupa nnje kisha akaingia chumbani.

“Mama yako nayeye unataka tumfukuze, sema neno mimi kesho namtimua.” Baba Hamisi alimuuliza.

“Kwanini umfukuze Mama?” Halima aliuliza kwa mshanagao, wakati Mama yake anaongea alikua anasikiliza tu, wala hakukasirika.

“Huoni mdomo wake, unaona jinsi anavyotukana, hembu fikiria hivyo ni viatu tu anapiga kelele hivyo, vingekua vingine na mimi nimemchoka Mama yako mwanangu….” Alimuambia kwa kumaanisha.


“Inamaana Baba hujamzoea Mama, ndiyo kawaida yake, kitu kidogoa taongea, unatakiwa tu umzoeem huwezi kumfukuza kwakua tu anaongea sana, Mama ndivyo alivyo.” Baba yake alimuangalia kisha akacheka.

“Mwanangu, umetoka kuniambia kuwa unataka mume wako kumfukuza Mama yake kwakua ana mdomo, lakini mimi nataka kumfukuza Mama yako unaniambia nimzoee kwanini wewe usimzoee Mama mkwe wako?”

“Lakini Baba huyu ni tofauti, huyu ni Mama yangu nimemzoea!”

“Ni tofauti kwamba wewe Mama yako mimba yako aliibebea tumboni lakini mumeo kwa Mama yake mimba ilibebewa wkenye makalio ndiiyo hazoeleki!


Mwanangu, unapoolewa unaingia kwenye familai mpya, unaweza kukutana na ndugu wa mume wazuri wakakupenda au ukakutana na wenye visirani kama Mama yako! Kama mtu hakupigi unamzoea unapuuzia, lakini si kutaka afukuzwe. Hata kama ni mbaya vipi lakini ni Mama yake, hakuna mwanaume mwenye akili atamfukuza Mama yake kwakua tu mkewe hajisikii vizuri kukaa naye.


Huyo Mama ni Bibi tu, mpe muda, atazeeka badala ya kupiga kelele atacheza na wajukuu. Lakini ukishaanza kumuonyesha mume wako kuwa humpendi Mama yake hata akifa kifo cha Mungu basi utaonekana umemuua wewe. Hapa si kuna mawifi zako, unafikiri nao hawamchukii Mama yako, wanamchukia kwani ana mdomo lakini wamenyamaza wanampuuzia wanamuona mzee maisha yanaenda. Kama hakupigi muache aongee mzomo ni wake.”


“Inamaana bado umekalisha makalio chini unataka mimi ndiyo nije kuviondoa hivyo viatu vyako. Huoni hata aibu mtoto wa kike umerudi nyumbani unajua naishi mimi na Baba yako tu, badala hata usaidie usafi umejikalia tu hapo na Baba yako. Au kwakua Baba yako mpole hawezi kuongea hivi kweli una ndoa kweli……” Mama Hamisi alitoka na kuanza kuongea, bila kuambiwa kitu Halima alinyanyuka akachukua viatu vyake na kuudi kwa mume wake.


MWISHO 



MWANANGU MWANAUME NI KAMA GARI!


Baada ya kutolewa Mahari Hamisa alitaka kuondoka, lakini Baba yake alimuambia asubiri kwanza, alimuambia kuwa anataka abaki Mwanza ili amfunde. Kwanza Hamisa alicheka kuwa Baba yake anataka kumfunda. Lakini Baba yake alisisitiza kuwa anataka kukaa naye mwezi mzima. Hamisa alimuambia kuwa ampe muda akachukue likizo kazini, kweli alienda kuchukua likizo na kurudi nyumbani.


Baba Hamisi ndiyo alikua kastaafu na ndiyo kwanza alikua amenunua gari, alikua anamuozesha Binti yake wa kwanza Hamisa. Hamisa alikaa wiki kwa Baba yake bila mafunzo yoyote, siku moja Baba yake alimuambia aamke, ilikua subuhi sana. Alimpeleka mpaka lilipokua Gari lake na kumuambia alisukume mpaka mjini. Hamisa alijua utani lakini Baba yake alikua anamaanisha.


Gari halikuwashwa alitaka tu asukume, Hamisa alisukuma mpaka basi ila halikusogea, Baba yake hakumuacha aliingia ndani na kuliwasha, bila kukanyaga mafuta bado alimuambia alisukume, alisukuma kutwa nzima kachoka lakini gari halikufika mjini. Jioni alimuambia aoge akalale, asubuhi alimchukua na kumpeleka VETA, alifundishwa Udereba kwa wiki mbili akaweza kuendesha.


Siku nyingine akamuamsaha asubuhi, akampa funguo na kumuambia aliwashe, alikua anajua kuendesha, gari lilikua linawaka lakini lilitembea kidogo likazima,a lihangaika sana lakini halikutembea kutwa nzima halikutembea ikafikia hatua hata kuwaka haliwaki tena. Baba yake alienda na kuchukua Mafuta, akaweka na kumuambia aliwashe, alipowasha gari iliwaka ikatembea wakaenda mpaka mjini na kurudi.


Waliporudi Baba yake alimuambia sasa hivi umeshakua unaweza kuingia kwenye ndoa, kesho nenda kajiandae na harusi yako. Hamisa aliitikia lakini hakumuelewa Baba yake, usiku alimua kumfuata na kumuuliza.

“Inamaana Baba kunifunda kwenyewe ni kunifundisha kuendesha gari? Mbona sijaelewa, kuendesha gari kutanisaidia nini kwenye ndoa, mbona nina rafiki zangu wanajua kuendesha mafari lakini wanaachika?” Alimuuliza, Baba yake alitabasamu na kumuambia.


“Mwanangu, mwanuame ni kama Grari, hasukumwi bali anaendeshwa. Ukiingia kwenye ndoa najua kuna mambo utataka mume wako kukufanyia, kuna namna utataka mume wako awe, akupende, awahi kurudi nyumbani, aache pombe, asiwe malaya, akuhudumie, akupe kila kitu. Kuna wanawake wanapata bahati wanakuta waume zao wanajua majukumu yao ila kuna ambao hawapati hiyo bahati.


Kama hutaipata hiyo bahati basi ni lazima ujifunze namna ya kumuendesha mume wako, na si kutaka kumsukuma. Kama utaingia kwenye ndoa na kuanza kulalamika mume wangu anachelewa kurudi, mume wangu anapenda ndugu zake, mume wangu na unataka abadilike basi jua ni kama unamsukuma, uliposukuma gari mara ya kwanza halikuwaka, lilibaki limesimama.


Hivyo hivyo kwa mwanaume, ukimpigia kelele sana, ukalazimishia kuwa awe kama unavyotaka wewe basi hatabadilika, utakua kama unamsukuma mwisho utaishia kuchoka na kulalamika tu. Ndiyo maana mara ya kwanza kabla ya kuliwasha gari halikuondoka kwakua ulikua unasukuma tu.”


“Mara ya pili niliwasha lakini halikutembea wakati nilishajua kuendesha?” Hamisa alimuuliza Baba yake.

“Nikweli, mwanaume kama gari anahitaji mafuta, anahitaji kujaliwa, anahitaji matengenezo. Kujua tu kuendesha bila kujua majukumu yako kama mwanamke ni kazi bure, gari itawaka lakini haitatembea. Unalalamika awahi kurudi nyumbani lakini akirudi ni kelele, akirudi unamnyima unyumba, akirudi anakuta chakula hakuna, nyumba chafu!


Unataka mume wako asiwe karibu na ndugu zake wakati wewe kila siku uko na Mama yako, ndugu zako unawajali hutaki wake awajali, anakupa matumizi ya nyama unapika dagaa na mchicha mwingi. Mwanangu mwanaume ni kama Gari, ili liwake linahitaji kwanza Petroli au Dizeli, pili oili ibadilishwe, tatu lifanyiwe service mara kwa mara, kama humjali mume wako hata kama unajua kumuendesha hatakujali.


Ndiyo maana mara ya tatu tulipoweka mafuta Gari liliwaka tukaenda safari yetu na tukarudi salama. Hivyo mwanangu unaenda kuolewa, mwanaume ni gari, hata gari liwe zuri namna gani lakini kama kila siku unaligongesha basi litakufa, kama kila siku mume wako wewe ni kelele umenuna basi ni kama unaligongesha gari, hata kama unajua kuliendesha basi jua litakushinda!”


MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG