Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

MAPENZI! MAPENZI! NA MAPENZI TENA

  

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

MAPENZI! MAPENZI! NA MAPENZI TENA—SEHEMU YA KWANZA


“Vipi? Mbona hivyo?” Job alimuuliza Harris ambaye alikua ameshikilia simu yake mkononi. Alionekana kuiangalia kwa hasira, huku akipandisha mkono wake juu na kuiweka simu mdomoni, aliing’atang’ata kwa hasira. Ni kama alitaka kuongea kitu lakini alisita.


JOIN US ON TELEGRAM

“Hakuna, naona ni network, nampigia wife hapokei.” Alijibu kwa mkato huku akifungua simu yake, akabonyeza namba za mke wake na kuanza kupiga tena.


“Wewe nawe, network wakati inaita?” Job alimuuliza, hakujibu chochote, alinyamaza akisikilizia simu yake sikioni, iliita mpaka kukatika lakini haikupokelewa, kwa hasira aliirudisha mfukoni, akanyanyuka na kutoka ofisini.


Alitoka nnje ya ofisi na kuanza kuzunguka zunguka, baada ya kama dakika tano hivi simu yake iliita. Alikua ni mke wake, aliipkea harakaharaka, kabla hata ya mke wake hajaongea kitu chochote alianza kulalamika.


“Kwanini napiga simu zangu hupokei, wewe ulikua wapi? Ulikua unafanya nini?” Alifoka.


“Samahani mume wangu, nilikua na kazi na simu nimeiacha kwenye chaji…” Dorris alijaribu kujitetea.


“Kazi gani  mpumbavu mkubwa, ulikua na wanaume zako shetani wewe! Na nimekuambia kuwa hiyo kazi kama ndiyo inakupa kiburi nitakuacshisha uje ukae hapa nyumbani mshenzi mkubwa wewe!” Harris aliendelea kufoka, Dorris alinyamaza kimya, hakumjibu kwa chochote zaidi ya kuitikia kila kitu alichokua akiambiwa na kumuomba msamaha mume wake.


“Nikusamehe nini sasa? Wewe si umesema ulikua una kazi, kwahiyo nikusemehe kwakua unafanya kazi?” Harris aliuliza, lakini Dorris hakujibu chochote, alibaki kimya tu.


“Pumbavu mkubwa wewe! Mwanangu anaendeleaje?”


“Anaendelea vizuri mume wangu…” 


“Nipe simu niongee naye.”


“Lakini mume wangu si nimekuambia kuwa nipo kazini, sasa nitaendaje kazini na mtoto.”


“Ndiyo maana sitaki ufanye kazi! Nampigia Fatma hapokei simu, huyu binti ameshaanza kiburi, yaani ni kama wewe si jui unamfundisha umalaya wako huko!” Harris aliongea sana mpaka akachoka, akakata simu kwa hasira.


“Whooooh!” Dorris alipumua kwa nguvu baada ya mume wake kukata simu.


 “Nini tena D?” Danis aliuliza.


“ Ni X wangu, yaani mwanaume anajua kusumbua huyu, mtu hata mtoto hahudumii lakini anavyopiga simu na kujifanya kujali, yaani mpaka nachoka kabisa!”


“Pole D, ni wanaume wengi ambao hawahudumii watoto wanakua hivyo! Sema unatakiwa kumpeleka ustawi wa jamii, wanaume washenzi kama hao wanakuaga wasumbufu sana, ipo siku atakuja kumdai mtoto.”


“Athubutu, namwagia maji ya moto, mimi ananijua, hawezi kuja kufanya ujinga wake hapa!”


Dorris aliongea kwa hasira huku akijifanya kuumia, alinyanyuka kutoka alipokua kaka na kujisogeza mpaka alipokua kasimama Dennis, alijiegemeza kifuani kwake kwa muda kidog huku akimkumbatia kwa kumshika kiunno.


“Hivi kwanini sikukutana na wewe kabla ya huyu mshenzi hajaniharibia maisha yangu?” Aliuliza huku akipumua pumua kimahaba.


“Hajakuharibia, si kakupa mtoto, tena katoto kazuri kabisa huna haja ya kulalamika, kila kitu kina sababu zake. Ukikutana na changamoto wewe iangalie kwa pande mbili, hasi na chanya, acha kuangalia mabaya ya kitu tu…”


Dennis alimpa nasaha nyingi lakini Dorris hakuonekana kusikiliza, kichwa chake kilikua kwingine kabisa, mlango ulifunguliwa, Dorris kusikia mtu anashika kitasa tu alishituka na kujitoa kwneye mikono ya Dennis. Alizuga kana kwamba kuna kitu alikua akikihitaji katika ile ofisi, aliyeingia alikua ni katibu muhtasi wa Dennis, aliingia na kuweka mafaili mezani na kuondoka.


“Hivi kuna haja gani ya kufichaficha mambo hapa ofisini?” Dennis aliuliza.


“Hapana, wewe ni mwanaume na tena ni Bosi wangu, watu wakijua mimi ndiyo nitakuja kuathirika, hapana, siwezi kuweka wazi mpaka unioe.


“Lakini sisi ni watu wazima, mimi sijaoa na wewe hujaoa, sasa unachoogopa ni nini? Mimi natamani hata kuja kwenu kujitambulisha tuishi pamoja, haya mambo ya kuficha ficha yanakera!” Dennis alilalamika.


“Najua unaongea hivyo sasa hivi kwakua hujavaa viatu vyangu. Mimi nilishaumizwa sana, nimekuambia kuhusu X wangu, namna alivyoniumiza na mambo aliyonifanyia, aliniacha na mimba ya miezi tisa na kwenda kuoa mwanamke mwingine, hapaan siwezi kurudia tena makosa.”


“Mbona unaishi kwa wasiwasi, si kila mwanaume yuko kwaajili ya kukuumiza. Nilazima ujifunze kuamini mtu!” Dannis aliongea kwa ukali kidogo..


“Nilishang’atwa na nyoka mara moja, hapana, nataka nikujue vizuri kwanza, isitoshe, wewe ndiyo umetoka kufiwa na mke wako, sitaki watu kuniona kama nilikua mchepuko wako kabla ya kifo cha mke wako, angalau umalize miaka miwili ndiyo tuwaonyeshe watu mapenzi yetu, walimwengu hawa wanaweza kusema hata nilimuua mke wako wakati dada wa watu hata nilikua simjui!” Dorris alionekana kutokutaka kabisa mapenzi yao kuwa wazi, Dennis alikua anampenda na alikua tayari kufanya chochote kile ingawa Dorris hakutaka kabisa.


****


“Mtoto amekula?” Dorris alimuuliza binti yake wa kazi.


“Ndiyo amekula, lakini Dada, nahisi mtoto anaumwa, atakua na homa, kwni anaonekana kuwa ni wa moto sana…”


“Lakini si amekula?” Dorris alikua anaongea kwa harakaharaka, hakutaka sana kumsikiliza Fatma. Ulikua ni usiku wa manane, baada ya Dennis kumchukua na kumpeleka nyumbani kwake ambapo alikua haruhusiwi kuingia kwani alimuambia bado anaishi na wazazi wake aliingia ndani na kubadilisha nguo tu. Mtoto wake Samweli ‘Sam’ ambaye alikua na miaka mitatu alikua kalala, hakutaka kumuamsha, alimbusu tu usoni na kuondoka zake.


Alikua ametoka na rafiki yake Mariam, Mariam naye alikua ni mke wa mtu, yeye alikua ni mwalimu wa sekondari katika shule ambayo ilikua karibu kabisa na ofisini kwa Doris ambaye alikua ni mhasimu katika halmashauri moja mkoani Arusha.


“Nini tena?” Mariam alimuuliza.


“Hamna kitu, Sam nahisi ana homa, hivi huyo mtu wako haji au? Maana nataka kuondoka kumuangalia mwanangu.” Alilalamika huku akiangalia simu yake.


“Abnakuja, mimi mwenyewe sikai, mume wangu nimemuacha ndani na nimemuambi anakuja kwako mwanao anaumwa…”


“Fala wewe kumbe wewe ndiyo unanichuria, mwanangu kaumwa kweli!”


“Hahhaa! Hakuna shoga, sasa mimi ningeagaje, si unajua kale kajamaa kangu kakorofi sana, unafikiri bila kumuambia niko kwako angeruhusu nitoke?”


“Lakini shoga yangu kuwa makini, hizi ndoa siku mume wako akijua basi utahadithia mimi sipo kabisa!” Dorris alimshauri.


“Bwanaeee hata sitaki kufikiria, unafikiri mimi hata najali, hawa wanaume ni nuksi tu, hivi wewe unafikiri yule mwanaume wako huko alipo hachepuki, anachepuka tena sana tu lakini mwenzangu ndiyo unajifanya mlokole kuliko Yesu mwenyewe!”


“Hata kama anachepuka shogaa lakini mimi siwezi kulipiza, wanaume ni wabaya sana, anaweza kukusaliti lakini wewe ukifanya hivyo hivyo basi anaweza kukuacha hapohapo.”


Dorris aliongea, Mariam hakuonekana kujali kabisa, alikua bize na simu yake akichat na mwanaume wake. Baada ya kama dakika kumi hivi alikuja Baba mtu mzima, aliwasalimia na kukaa.


“Huyu ni rafiki yangu, tunafanya wote kazi…” Mariam alimyambulisha, walipeana mikono kisha alitambulisha upande mwingine.


“Shemeji yako huyu…”


“Nashukuru kumfahamu.” Dorrisa lijibu kwa kifupi, waliongea mambo mengi lakini Dorris alikua kimya tu, hakutaka kuongea sana. Ilipofika kwenye saa nne hivi aliaga kuondoka. Aliwaambia hali ya mtoto wake si nzuri hivyo anataka kwenda kumpeleka hospitalini.


“Utatusindikiza?” Mariam alimuuliza mwanaume wake, yule Baba mtu mzima alibaki kaduwaa  tu, lakini Mariam hakumruhusu kukataa, alimuinamia kama vile anataka kumbusu mdomoni, alishusha mkono wake mpaka kwenye suruali yake na kushika kwenye mkanda akawa kama anamnyanyua, harufu tu ya manukato ya Mariam ilimchanganya Baba wa watu, alijikuta ananyanyuka na kuwafuata. Wakati wanatoka, Mariam alichukua simu na kumpigia mume wake.


“Unaweza kuja hospitalini?” Alimuuliza.


“Kwanini? Wani hali ya mtoto ni mbaya namna hiyo?”


“Ndiyo, hali yake ni mbaya, nahisi watamlaza, nilitaka uje kunichukua ili unipeleke nyumbani kwa Dorris, kale kabinti kanaogopa kulala peke yake, sas anitalala kule nilitaka ukaniache kule maana asubuhi natakiwa kumuandalia chakula.” Mariam alidanganya.


“Sasa kama ni hivyo kwanini usichukue Bodaboda uakenda, mpaka mimi nitoke huku, nichukue bodaboda mpaka huko na hapa nyumbani namuacha nani?” Mume wake aliuliza.


“Kwahiyo unaona sawa mimi mke wako usiku huu kupanda bodaboda, wakinibaka?” Aliuliza kwa hasira.


“Sasa… umesema uko wapi?” Mume wake aliuliza kana kwamba anataka kwenda kumchukua.


“Huna haja ya kuja, mimi mambo ya kulazimishana siyawezi kabisa, kama hutaki basi, nitatafuta namna nyingine!”


“Lakini…”


“Lakini nini? Si wewe unaona usingizi wako bora kuliko mimi mke wako, kwaheri na lala salama!” Aliongea kwa hasira na kukata simu.


“Nishamuaga mume wangu, tunaenda kulala wote. Dorris tutakudrop kwako, kama hali ya mtoto itakua mbaya basi utanipigia.” Aliongea kwa kuamrisha flani, mambo yalitokea harakaharaka. Waliingia kwenye gari, yule Baba alimuambia Dorris akamuangalie mtoto kwanza kuona anaendeleaje, alirudi na kuwaambia kalala yuko vizuri. Mariam aliondoka na mtu wake. Dorris alichukua simu yake na kuanza kumpigia mume wake, simu iliita tu bila kupokelewa, alipiga sana lakini haikupokelewa.


“Usiku mwema mimi nalala…” Alimtumia meseji na kuanza kujiandaa kwaajili ya kulala. Mume wake baada ya kuona meseji alipiga simu na kuanza kumtukana ni kwanini analala wakati huo, alitukana sana, Dorris alikua anamsikiliza tu na kuomba misamaha isiyo na kichwa wala miguu. Waliongea kwa muda wa kama nusu saa hivi, mazungumzo yao yote ilikua ni kugombana, mume wake akimtukana sana na kuongea vitu vya kukera. Dorris alinyamaza tu alipokata simu alisubiri kama dakika kumi hivi kisha akampigia Dennis.


“Umeshalala mume wangu?” Alimuuliza.


“Hapana, nilikua nakupigia simu inaonekana kama inatumika, ulikua unaongea na nani mud awote huo?” Dennis aliuliza.


“Mdogo wangu, alikua ananiomba pesa, ana amatumizi mabovu sana, yaani sijui hata nifanye nini, anachukulia maisha simple sana yule mtoto.” Dorris alianza kulalamika, waliongea sana mpaka kupitiwa na usingizi, mazungumzo yao yalikua matamu, kila wakati Dorris alikua akitabasamu tu, alikua na raha tofauti na alivyokua akiongea na mume wake.


ITAENDELEA….


MAPENZI! MAPENZI! NA MAPENZI TENA—SEHEMU YA PILI


Mvua kubwa ilikua inanyesha Dorris alikua nyumbani kwa Dennis, walishamaliza kula chakula cha usiku.


“Leo usiende nyumbani.” Dennis alimuambia huku akimvutia kitandani. Dorrisa lishanyanyuka kujiandaa kuondoka, alishamaliza kubaa nguo zake alikua akihangaika kuangalia alipokua ameitupia pochi yake. Ilikua kama saa nne hivi za usiku, waliyoka kazini pamoja, Dennis alikua hajisikii vizuri hivyo siku hiyo alienda kumpikia. Hakupanga kukaa sana kwani nyumbani alikua kamuacha Dada wa kazi na mtoto ambaye bado hali yake ilikua haijatengamaa.


“Hapana, siwezi kulala, nyumbani sijaaga, si unajua naishi na Mama.” Alijitetea huku akijartibu kujitoa kwenye mokono ya mpenzi wake.


“Ushakua mkubwa, hivi unafikiri mama yako yeye hafurahii akisikia una mtu…” Dennis aliongea huku akimvuta kitandani, hakutumia nguvu sana kumvutia kitandani kwake, alimvuta aklamkalia akawa kampakata, hakusubiri sana, alimrushia kitandani na kumlalia kwa juu.


“Unataka kufanya nini? Wewe si unaumwa?” Dorris alimuuliza huku akimlegezea macho, mikono yake alishainyanyua na kumkumbatia Dennis shingoni, walikua wakiangaliana, Dennis alikua akipumua kwa nguvu huku mapigo ya moyo yakiongezeka kwa kasi.


“Unajua ninachiotaka kuifanya, leo nataka ulele hapa, siwezi kukuachia uondoke.”


Aliongea huku akinyanyuka kidogo na kukaa kwa kuchuchumaa, alishusha mikono yake kwa nyuma na kuanza kufungua sketi.


“Mimi sitaki, asieee, siku nyingine nitalala, siwezi kilala leo, niache niende nyumbani…” Dorris aliongea kwa kulalamika, ingawa mdomo ulikua unasema hautaki lakini mwili ulikua unataka, alimuacha afanye chochote anachotaka juu ya mwili wake, ndani ya dakika tano alikua kabaki kama alivyozaliwa.


“Wewe si ulisema unaumwa?” Alimuuliza wakiwa wamekumbatiana kitandani.


“Ndiyo mimi lakini si Dennis, yeye haumwi na leo huondoki.” Dennis alimjibu huku akimparamia kwa juu.


“Basi ngoja nimpigie Mama nimuambie siwezi kurudi nyumbani.” Dorris aliongea huku akinyanyuka, alichukua simu yake na kutafuta namba ambayo iliandikwa “My lovel M” Aliipiga na ikapokelewa.


“Shiamoo.” Alisalimia kwa kifupi, hakutaja aliyekua akimsalimia lakini Dennis alijua kuwa anamsalimia Mama yake, baada tu ya salamu alianza kuulizia hali huku akitoka chumbani, alichukua khanga na kujifunga kisha akatoka mpaka sebuleni. Dennis alibaki kitandani akimsubiria hukua kifurahia na kumshukuru Mungu kuwa mpenzi wake kaamua kubaki.


“Ulikua unafanya nini? Mbona nimepiga simu mara kibao simu yako haipatikani. Kila nikipiga inakata tu kila nikipiga inakata tu.”


Hakua akiongea na Mama yake, Dorris alikua akiongea na mume wake, alijua kuwa ni lazima mume wake atamtafuta hivyo alitaka kuaga kwanza ndipo alale kwa uhuru, wakati wote alipokua kwa Dennis simu aliweka flight mode. Mimi sijui itakua ni Network maana hata mimi leo nimekupigia mara kibao simu haipatikani. Kama kawaida mume wake alianza kutukana, alimuambia Malaya, alimuambia mpumbavu na mjinga.


“Mbona nasikia kelel upo wkenye gari?” Dorris alimuuliza mume wake.


“Wewe inakuhusu nini? Hivi una akili kweli wewe mjinga, unanipigia simu unaanza kuniuliza maswali yako ya kijinga jinga. Kwanini kwanza ndiyo unanipigia simu sasa hivi?” Mume wake aliuliza, tena, alionekana kuwa na hasira sana, kulikua na kelele nyingi na alikua akipumua kwa shida kama mtu ambaye alikua kwenye maumivu.


 Kwakua alikua akitukana tu Dorris alisikiliza na kuomba misamaha, kwa hasira mume wake alikata simu kwa matusi. Dorris alishukuru Mungu, alimpigia Fatma binti wake wa kazi na kumuulizia hali ya mtoto, alipoambiwa anaendelea vizuri alimuambia azime simu, ingawa hakumuambia sababu lakini alijua kuwa mume wake anaweza kumpigia na kumuulizia hivyo alitaka ionekane kama Network ndiyo inasumbua.


“Aiseee wewe umeniponza, yaani Mama anavyoongea, mhhh!” Dorris aliongea wakati anarudi chumbani.


“Tena ngoja nizime simu kabisa kwani najua atanisumbua, haamini kuwa nimelala kwa rafiki yangu.” Aliendelea kujisemea, Dennis yeye alikua hoi kitandani akimsubiria, hakutaka kujua mengi sana, yeye alifurahia tu kuwa mpenzi wake karudi. Dorris hakua na wasiwasi tena kwania lishaongea na mume wake na kujua hali ya mtoto wake.


“Asubuhi utanipeleka nyumbani kwanza, sijawhai kulala nnje ya nyumbani kwetu, sijui najisikiaje ila nataka kumuona Mama kabla ya kwenda kazini, siwezi kuondokea huku lazima nikabadilishe nguo.” Aliongea, Dennis alimuitikia na kumuambia asiwe na wasiwasi.


****


“Mbona hupokei simu zangu?” Harris aliuliza. Alikua kasimama malngoni kafura kabisa, ilikua ni katika nyumba moja, kachumba kadogo ambako kalikua na kila kitu.


“Nilikua na mwanaume wangu, mtu mwenyewe pesa hutoi ndiyo unataka nikupokelee, kama unataka toa pesa kwanza!” Dada mmoja ambaye alikua kafunga khanga moja kiunoni aliongea. Ilikua ni Jioni, Harrison alikua katoka kazini, alikua akimpigia yule dada kwa muda mrefu bila simu yake kupokelewa.


“Pesa gani hiyo sijatoa, hivi jana si nilikupa laki mbili!” Aliongea kwa hasira, yule dada alinyanyuka kutoka katika kakitanda kadogo ka futi nne kwa sita, alimsohelea mpaka mlangoni, alikua kajifukiza Udi mwili mzima, alitembea kwa madaha mpaka alipokua kasimama Harris.


“Hivi wewe mwanaume una akili kweli? Kwahiyo unaniona mimi ni wa laki mbili! Hembu niangalie!”


Aliongea huku akichia khanga yake na kubaki kama alivyozaliwa.


“Hivi kweli umenipa laki mbili ndiyo unataka kunifanya niwe kama mke wako. Kwa taarifa yako nilikukubali kwakua ulikua unaona kuwa yaliyomo yamo, laki mbili kitu gani. Mimi hii ni biashara yangu, natembea mpaka na bosi wako nanihonga mshahara wako wa miezi sita, sas aunaponipa laki mbili, kazi yenyewe huwezi, unapumua kama bata! Pesa nisipate na starehe nisipate, laki mbili yako iliisha jana, leo kama unataka toa laki mbili nyingine tumalizane. Hembu angalia huu mwili, wakiniangalia wanachanganyikiwa, kitu kina tui la nazi! Toa laki mbili kama huna ondoka!”


Yule Dada aliongea kwadharau, Harrson hasira zilimpanda, alimshika shingo na kumkaba.


“Unaniletea ujinga mimi! Pesa zangu ule halafu uanidharau, kama ulizoea kutapeli watu wengine basi sio mimi!” Harris, alimkaba yule dada ambaye alianza kuomba msiamaha, aliongea huku akirudi nyuma mpaka alipokaa kitandani.


“Huwezi kunaicha kijinga jinga namna hii halafu unaleta dharau, akma ulizoea kuwachezea wengine basi ndiyo hao hao!” Alizidi kuongea, yule dada alitulia tuli, lakini aliirudisha mikono yake nyuma akma anatrafuta kitu chini ya blanketi kubwa alilokua ametandika.


“Mshenzi mkubwa wewe! Hivi unafikiri mimi ni mjinga kama hao uliowazoea!” Yule Dada alipiga kelele huku akitoa sime kubwa, aliiivuta kutoka kwenye blanketi na kuipitishia kwenye tumbo la Harrisi.


“Mama nakufa!” Harris alipiga kelele. Sime ilikua kali, ilikua imekata shati na kumkata kifuani, alimuachilia yule dada amabye alisimama, yule dada alichukua khanga yake na kujifunga, alirudi na mpaka mlangoni kisha akamuambia atoke.


“Mshenzi, sitaki kukuona kabisa, na ukikutana na mimi basi kimbia kabisa, Mbwa kabisa wewe, yaani unakuja kwangu unataka kunifanyia ujinga. Stori zako nishazisikia, kazi yako kuchukua mabaa medi uanenda kuwafanyia unyama wako unaishia kuwapiga, mimi si wa hivyo na kama ukileta ujinga nakuitia mwizi uone watakachokufanya mshenzi wewe!”


Harris alitoka akikimbia huku kashikilia kifua chake, damu zilikua zinamtoka ingawa hasikua nyingi sana, aliingia kwenye gari yake na kuondoka. Alirudi nyumbani kwake na kuangalia kidogo hakikua kikubwa sana, lakini alikua na hasira sana, alijiona kudhalilishwa, alichukua simu na kumpigia mke wake, simu ya mkewe ilikua haipatikani.


“Huyu Malaya kashaenda kwa wanaume wake!” Aliongea kwa sauri, aliingia bafuni, akachukua taulo na kufutafuta damu.


“Yule mwanamke ni mshenzi sana, ngoja atanitamba, amekula pesa yangu na bado anataka kuniua!” Aliongea kwa hjasira huku akibadilisha shati na kutopka nnje, alienda baa na kuanza kunywa.


Alikunywa bia mbili lakinio hazikupanda, alikua na hasira sana, alichukua simu yake na kuanza kumpigia mke wake, alipiga sana lakini simu zote zilikua hazipatikani.


“Hamna, kuna kitu, huyu atakua anachepuka smhenzi kabisa!” Aliongea kwa hasira, alienda na kulipa bili,  wakati huo ilikua kama saa moja usiku, aliingia kwenye gari yake, alielekea sheli akajaza mafura kisha akaanza safari ya kwenda Arusha. Hjakua na ruhusa, kutoka Singida alipokua akifanya kazi yeye mpaka Arusha ilikua ni zaidi ya kilometa 300 lakini hakujali, aliamua kuendesha wmenyewe, kwakua ilikua usiku na kwa namna alivyokua na hasira aliendesha kwe mwando wa kasi, hakukua na tochi hivyo hakusimamishwa popote. Aliondoka Singida saa moja kama na nusu usiku, ilipofika saa saba usiku ksaoro tayari alishafika nyumbani kwake.


Aligonga mlango kwa nguvu huku akimuita mke wake, fatma aliamka, aliuliza ni nani alikua anagonga.


“Mimi BabaSam, mke wangu yuko wapi mpaka wewe ndiyo unaniuliza mimi nani?” Aliuliza kwa hasira, binti wa watu alifungua mlango.


“Dada yako yuko wapi?” Aliuliza kwa hasira.


“Dada?” Binti alijibu kwa swali, alikua hajui chakuongea.


“Dada ndiyo, huna akili nini? Namuulizia bosi wako kaenda wapi, au kaenda kufanya umalaya wake!?” Alimtandika binti wa watu kofi ambalo lilimdondosha chini, hakuishia hapo, alimshika na kumnyanyua akitaka kujua mke wake ameenda wapi?


“Dada ahajarudi kazini…” Binti alijibu, alizidi kumpandisha hasira, alitaka kumpiga tena lakinia likatishwa na sauti ya mtoto wake.


“Daddy… Daddyy…” Mtoto wake ambaye alikua hajalala alikua akicheza na Dada chumbani waklati anaingia alikuja. Alimuona Baba yeka na kumkimbilia, Harris alibadilika na kuanza kuwa mstaarabu, pamoja na mbwembwe zake zote lakini alimpenda mtoto wake kuliko kitu kingine chochote. Mtoto alimkimbilia na kumrukia, alimkumbatia na kuanza kumpiga mabusu. Fatma kuona vile alikimbilia chumbani, aliwasha simu yake na kujaribu kumpigia Dorris lakinis imu ilikua haipatikani.


“Dada uko wapi? Baba kaja nyumbani ana hasira, kanipiga sana anakuulizia?” Alituma meseji lakini hazikujibiwa. Baada ya muda Harris alikuja chumbani, alikua bado kambeba Sam hivyo alikua mpole ingawa uso ulionyesha hasira.


“Kwahiyo unasema bado hajarudi kutoka kazini?” Alimuulizia.


“Ndiyo…”


“Ndiyo kawaida yake kila siku kuchelewa kurudi kazini mpaka mida hii?” Aliutliza kwa kutilia lakini bado alikua na hasira.


“Hapana, hata sijui nini kimemkuta, si kawaida yake, leo ndiyo mara ya kwanza.”


“Ni kawaida yenu Malaya kuteteana, lete hiyo simu hapa.” Alimuambia, binti wa watu aliichukua simu, alimpa, akaichukua, akaizima na kuiweka mfukoni kwake.


“Sitaki umuambie kuwa niko hapa, nataka nijue atakaa huko kwa muda gani!” Aliongea kwa hasira, alimchukua mtoto wake na kwenda naye chumbani kulala. Walicheza na mtoto hasira zikapungua mpaka akapitiwa na usingizi.


Asubuhi na mapema Dorris alijiandaa kuondoka, mwanzo alitaka kuondoka peke yake lakini Harris alisisitiza kumpaleka.


“Lakini hatufiki nyumbani, nimemuambia Mama nipo kwa Mariam, atashangaa nikipelekwa nyumbani na mwanaume.” Alijitetea.


“Hakuna shida, nitakuacha njiani ila nataka uwahi.” Ilikua ni kama saa kumi na moja na nusu, Dorris alitaka kwenda nyumbani kujiandaa kwanza kisha ndiyo aende kazini kwani pale kwa Dennis alikua hana hata nguo za kubadilisha.


“Mama atakua kanitafuta mpaka basi, nikisafiri tu Mama yangu anakua na wasiwasi sana.” Alijiongelesha huku akiwasha simu zake, alijua ni lazima atakutana na meseji kutoka kwa mume wake akimtukana.


Kwa kawiada mume wake akiwa amelewa alikua anaweza kupiga simu hata saa nane za usiku na akimkosa hewani basi hukuta meseji za matusi. Alitauta lakini hakukuta hata moja. Meseji ya Fatma iliingia lakini aliacha kuisoma na kuangalia meseji nyingine za watu wengine ambazo jana yake hakuzisoma. Kushangaa walishafika karibu na nyumbani.


“Mbona unanifikisha mpaka nyumbani, simama hapa Mama ataniona.” Aliongea kwa sauti kidogo, lakini Dennis hakusimamisha gari aliendelea mpaka alipofika karibu na geri ndipo akasimama.


“Niwakati Mama yako kujua kuwa una mwanaume, mimi sitaki kukuchezea, nataka kukuoa sasa mambo ya kufichaficha ni ya nini?” Dennis alimuambia.


“Mimi sitaki bwana nitakupeleka nyumbani mwenye…” Alishindwa kuendelea.


Wakati huo ndiyo alikua anafungua meseji ya Fatma, aliona ujumbe kuwa mume wake karudi na yupo nyumbani. Nguvu zilimuishia akabaki kaduwaa.


“Vipi?” Dennis alimuuliza lakini alishindwa hata kunyanyua mdomo kujibu kitu.


MAPENZI! MAPENZI! NA MAPENZI TENA—SEHEMU YA TATU


“Huwezi kwenda kwa Mama yangu namna hiyo!” Dorris hakupaniki, akili yake ilifanya kazi harakaharaka, alijua mume wake yupo ndani na kama Dennis angesogea kidogo basi mume wake angeliona gari na ingekua shida.


“Kwanini? Hivi kila siku utanidanganya mpaka lini, nataka kumuona Mama yako na kumuambia kuwa mimi ni mpenzi wako na jana uilala kwanhgu.” Dennis aliongea huku akipunguza mwenzo.


“Simama kwanza nikuambie kitu.” Alimuambia na Dennis alisimamisha gari.


“Unanipenda?”


“Ndiyo nakupenda, na hata ukiamua leo nikuoe nakuoa.”


“Wewe ni mwanaume, una dada zako si ndiyo?”


“Ndiyo ninao.”


“Hivi  utajisikiaje siku Dada yako anadanganya kuwa kaenda kusalimia mgonjwa, mtu kazidiwa kalala hospitalini, halafui asubuhi sa akumi na mbili anakuja na mwanaume, mbele ya Mama yako, anamuambia Mama yako jana nilikudanganya sikua kwa mgonjwa nilienda kugongwa na huyu mtu na ndiyo atanioa.”


Dennis alinyamaza bila kupata jibu, maneno ya mpenzi wake yalimuingia, alikua kama anavuta picha ya wadogo zake.


“Wewe ndiyo mwanaume wangu wa kwanza siriasi, nataka nikikupeleka nyumbani nakupeleka iheshima, si kama hivi kulazimishana, nakua kama nimefumaniwa, hivi unajua kuwa paoja na uzee wangu huu Mama yangu bado ananiona mtoto. Kwetu unafahamu, nikichelewa tu hata kurudi saa nne napigiwa simu mpaka basi, vipi nimelala nnje na nakuja na mwanaume namuambia kuwa huyu ndiyo mkwe wako, kuna heshima kweli?” Aliuliza, alikua katulia tuli akimuangalia Dennis namna maneno yalivyokua yakimuingia.


“Lakini mimi nataka kuja kwenu, anataka wazazi wako wanitambue.” Dennis alishanywea, alianza kujitetea taratibu.


“Najua, lakini si kihivyo, hapa ni kama mhuni flani, wewe ni mtu mkubwa unaheshimika, sasa kwanini tutambulishane kama tunabakana. Kuna utaratibu wa kutambulishana, kwanza mimi na wewe tunakaa tunaongea, tunakubaliana siku gani, naongea na Mama anakupikia kitu unakula. Sas ahivi Mama yangu hata hajui kama unakuja, hivi unafungua mlango unamkuta Mama yangu yuko na Khanga moja, ndiyo kaamka hata hajaoga, kweli kuna heshima hapo?”


Kwa manano  yale Dennis alijiona mjinga, aliona kakahakisha mambo sana, alimuomba msamaha na kumuambia wataongea.


“Nakusubiri hapa kajiandae twende kazini…” Alimuambia.


“Hapana, wewe tangulia, hata sijajua chakufanya huko nyumbani, ngoja niende kwanza nitakupigia, wewe tangulia.” Dorris aliongea huku akishuka kwenye gari, alifanikiwa kumpanga Dennis amabye hakukaa sana aliondoka. Alisubiri kama dakika tano hivi akachukua simu yake na kupiga namba flani.


“Shogaa nina matatizo…” Alikua kampigia Mariam.


“Nini tena, asubuhi asubuhi.”


“Hata sijui nini kilitokea lakini nimejichanganya. Jana nilienda kwenye sherehe moja ofisini, sikujua kuwa mume wangu atakuja, huwezi amini nilikunywa nikajisahau na kuamua kulala huko huko. Simu nilizima, narudi hapa nyumbani kabila sijaingia nakuta meseji, kumbe shemu wako kaja kawaka, tangu jana nimelala nnje na sijui chakufanya.”


“Hahahahah! Shogaa, yamekukuta, ulienda kwenye sherehe au ulikua unachepuka?” Mariam aliuliza huku akicheka kinafiki.


“Hapana, shoga yangu, wewe unanijua mimi kuwa sina mambo hayo, hata kama ni kuchepuka nisingekua mzembe kiasi hicho, hapana, najua huyu mwanaume ataniua, naomba unisaidie.”


“Sasa nifanye nini, unataka nikamuambie mume wako ulilala kwangu, kwanza mtu mwenyewe hanipendi anasema kuwa nakufundisha umalaya…”


“Hapana sio hivyo…” Dorris alimkatisha. “Si una yule jamaa yako wa TAKUKURU naomba anisaidie, nataka umpigie simu mume wangu umuambie kuwa nimekamatwa na TAKUKURU nimeshikiliwa tangu jana usiku, muambie usiku kwani jana nilionge naye, muambie kuna ishu nimeshikwa nayo na hawataki kuniachia.”


“Mbona sijakuelewa, inamaana nikupeleke kule, yule hawezi kukubali, hawezi kuchanganya kazi na mapenzi. Unataka yeye afanye nini kwani?” Mariam aliuliza.


“Si mlevi anapenda pesa?”


“Ndiyo ten asana.” Basi muambie yeye kazi yake itakua ni kunikaribisha ofisini kwake, nikae huko hata nusu saa tu, mume wangu aje, utamshawishi atoe kitu kidogo kwani nina kesi kubwa. Mimi ni mhasibu bwana, kuna mambo mengi ya kuongea, niunganishe naye tu nitajua cha kuongea.” Dorris alimuambia, rafiki yake ambaye alibaki ameduwaa.


“Unajua kuwa wewe ni sheani?”


“Najua lakini mume wangu ni Mama mkwe wa shetani, namjua, anajifranya mjanja lakini anaogopa polisi kama nini, hawezi kuniacha nipotelee kule, atatoa pesa hata kama kipigo atanipa.”


Lilikua ni wazo liliopita kichwani kwake harakaharaka, alikua hajapanga lakini kwa alivyokua anamjua mume wake hakuwa na namna. Mariam alimpigia jamaa yake na kumpa dili, Dorris alichukua Bajaji mpaka kwenye ofisi za TAKUKURU alifika na kuonana na huyo jamaa wa Mariam. Alimpanga vizuri na kumuambia.


“Nitakua na mishemishe zangu mjini, nitakuja hapa kwenye saa tisa, hapo ndipo mume wangu utamruhusu kuja kuniona mara moja. Lakini Mariam atakuja na mume wangua subuhi hii, wewe muambie kuwa nipo chini ya ulinzi na hatakiwi kunioana, jifanye kama nataka kumsaidia ili asiongee na mtu wa ofisini kwetu.


Muambie kuna watu wanaonekana wanataka kunitentenezea kesi hivyo awe makini, uytampigia, chukua namba yake kisha muambie aondoke.”


“Kwahiyo mimi Napata bei gani?” Yule jamaa aliuliza.


“Nusu kwa nusu, kiasi utakachoweza kumshawishi unachukua nusu.


“Kumbuka mimi nahatarisha kazi yangu,.”


“Baba, nina deni kikoba, sijalipa kodi, mwanaume ana pesa, hahudumii chochote. Mchune unavyoweza lakini hakikisha mimi Napata milioni na nusu!” Pamoja na kwamba yeye ndiyo alikua na shida lakini yeye ndiyo alikua akicontrol mazungumzo, yule jamaa alimualewa na kweli alifanya kama alivyoambiwa.


****


“Hutakiwi kutoka nnje ya mkoa wa Arusha mpaka hii ishu iishe. Haya mambo yamekukalia vibaya. Kuna watu wamepiga zaidi ya milioni mia mbili na wanataka kuudondoshea wewe jumba bovu.” Kaka wa takukuru alimuambia Dorris wakati wanatoka. Mume wake alikua anatetemeka  kwa uoga, alishawahi kupitia mziki wa TAKUKURU na kukaa ndani kwa miezi mitatu bila dhamana.


“Hapana, mimi siwezi kuendelea kukaa hapa, naacha kazi, sitaki kabisa.” Dorris aliongea huku akilia, alikua akitoa machozi kama mtoto, wakati wanatoka watu wengine walikua wakimshangaa.


“Usije kufanya huo ujinga ndugu yangu, una bahati tu nimelishikilia hili swala. Ukiacha kazi kila kitu kinakushukia wewe, unaona ni jambo dogo lakini ukweli nikuwa, ukiacha kazi watakusingizia wewe kuwa ndiyo umeiba ndiyo manaa ukaacha kazi. Hapa hatuzungumzii suala la kuacha kazi  bali kutoka nnje ya mkoa, cha kabisa, kama unataka kuozea jela ondoka.”


Waliagana na kutoka, Harris alimshukuru sana yule Kaka, njia nzima alikua aki mbembeleza mkewe. Kila wakati Dorris alisisitiza kuacha kazi na kusema kachoka.


“Bora kuwa Mama wa nyumbani mume wangu, jana niliogopa sana, wamekuja kunichukua kistaarabu nyumbani kwangu lakini walivyonitisha, ni bora kucha kazi, najuta sikukusikiliza.” Alilalamika,.


Mara kwa mara Harris alikua anamuambia mke wake kuacha kazi, lakini Dorris alikataa, alikua amamjua mume wake, mbali na kuwa na pesa lakini alikua ni mtu wa kumnyanyasa, kumpiga na kumdhalilisha. Hakua anamhudumia kwa chochote, pesa ya matumizi yenyewe alikua akituma kwa shida, mpaka kulalamika.


Alijua kuwa kuacha kazi tena ya serikalini ambayo ilikua inamuingizia kipato kizuri tu ilikua ni kufungua mlango wa manyanyaso. Maneno yote aliyoua anaongea yule Kaka wa TAKUKURU alikua anamuambia yeye. Alishajua kuwa mume wake alipitia hiyo hali, alijua kuwa mume wake alishahonga sana hivyo asingekua mgumu kutoa pesa.


Mume wake alikua mmgumu lakini alikua hamjali kwa chochote, lakini Harris aliposikia ishu za TAKUKURU alijua kuwa mambo yameharibika, kama mtumishi wa ume alijua kuwa hayo ni mambo ya kawaida. Alienda na kukutana na yule kaka, aliongea naye kiubwa akimuomba kumsaidia mke wake. Yule Kaka alihitaji milioni tano kwani kesi ilikua kubwa, walishushiana mpaka milioni tatu ambazo Harris alizitoa bila kinyongo ili tu kuondoka na mke wake. Alikua na wazo la kumuambia mke wake kuacha kazi lakini baada ya yale maneno ya yule mtu wa TAKUKURU alibadilisha mawazo na kuanza kazi ya kumshawishi asiache kazi.


***


“Umefanya nini kifuani?” Dorris alimuuliza mume wake baada ya kufika nyumbani na kupumzika.


“Hamna kitu, fuata ya kwako?” Harris alibaidika ghafla, alimjibu kwa mkato kama mtu ambaye hakua anataka kuongelea hilo swala.


“Mimi naondoka, sitaki kuka ahapa, utaniambia kitakachoendelea, lakini sitaki ufanya kazi!” Aliaga, ilikua ni jioni kwenye saa kumi na moja tu hivi. Harris hautaka kabisa kukaa pale.


“Sasa mume wangu nimepata matatizo, badala ya kukaa na mimi kujua kuwa unanisaidiaje wewe unataka kuondoka.” Dorris alijifanya kulalamika, ukweli nikuwa hakua akijua sababu ya mume wake kuja arusha lakini pia hakua akimtaka pale, alitamani kabisa aondoke na asirudi tena.


“Mimi nilikuja kwaajili ya mambo yangu, lakini hayawezekani tena!” Aliongea kwa kifupi, alipanda kwenye gari yake na kuondoka, hata yeye alikua hajui kaenda kwa mke wake kufanya nini.


Mume wake alipoondoka Dorris alipanda kitandani kulala, alikua kachoka sana kutonana na mishe mishe za siku ile. Alizima simu kabisa, alikuja kuamka saa mbili usiku, alimpigia simu mume wake ambaye alimuambia bado hajafika ila alikua njiani, alimtakia safari njema, baada ya kuhakikisha kuwa mume wake kaondoka alichukua simu na kumpigia Dennis.


“Nataka kuja kwako leo. Kuna mambo nataka tuongee.” Dennis ambaye alikua na hasira za kutwa nzima kwakua mpenzi wake alikua hapatikani alibadilika na kuanza kutabasamu, alimkaribisha na kumuambia kuwa anamsubiri.


***


Timbwili lile liliisha, maisha yaliendelea, Mume wake alimini kuwa siku ile mke wake alikamatwa. Upande mwingine Dorris bado alikua akimsumbua Dennis, siku hadi siku alikua akitafuta sababu ya kushindwa kumtambulisha. Alifanya siri kuwa alikua ameolewa na hatkutaka mtu ajue mahusiano yake na Dennis, alikua anamficha akimuambia muda bado. Kadri siku zilivyokua zikienda ndivyo alikua anampenda Dennis, alikua ni mtu tofauti kabisa na alivyokua mume wake, kwanza alikua ni mtu wa kujali, alikua anamhudumia kwa kila kitu kama mke wake.


Pamoja na kufanya kazi lakini alikua hagusi mshahara wake. Alimpenda kwani hata katika mapenzi alikua ni mtu wa kujali, vizawadi na kila kitu, hata katika tendo la ndoa alikua akimuandaa vizuri na alikua akiridhika tofauti na mume wake ambaye kwanza alikua hamuandai kwa chochote lakini pia alikua ni mtu wa dakika mbili kashamaliza na akitaka kuendelea anakua mkali pengine hata kipigo. Kitu kilichokua kinamsumbua kichwani ilikua ni namna ya kumuambia kuwa ameolewa tena ndoa ya kanisani na ana mtoto.


Kila siku alikua anaumiza kichwa chake kwabababu hiyo, ingawa yeye na Dennis walikua ni wakupika na kupakua lakini alijua kuwa kama akimuambia ukweli mbali na kumuumiza basi anaweza kumfanya amuache kitu ambacho hakua tayari kukiona.


“Hivi unachukuliaje kufunga ndoa ya kiserikali?” Siku moja alimuuliza. Walikua kitandani, Dorris akiwa amelaza kichwa chake kifuani kwa Dennis ambaye alikua aichezea uso wake.


“Kwanini unauliza hivyo? Hupendi ndoa ya kanisani?” Dennis alimuuliza. Aliuliza kwa mshangao kidogo ingawa hakupaniki.


“Hapana nauliza tu, kwani nawaza hivi mfano tukioana, wewe si ushafunga ndoa tayari ya kanisani, sasa itakuaje?” Alizuga.


“Haina shida, mimi nilifunga ndoa ya kanisani kweli, lakini sikumuacha mke wangu, yeye alikufa hivyo kididni hamna shida, kama hiyo ndiyo shaka yako ondoa.” Dennis alimuondoa wasiwasi huku akimuinamia na kumbusu kwenye paji la uso. Upendo aliokua anaupata ulimfanya kutoa machozi, kichwani alikua akiwaza mambo mengi, alikua akijilaumu ni kwanini hakukutana na Dennis mapema kabla ya kukutana na mume wake.


“Mbona unalia?” Dennis alimuuliza.


“Hakuna kitu, nawaza tu, hivi watoto wako hawatajisikia vibaya kuona sisi tunaoana kanisani, mimi naogopa, naona kama ndugu zako hawatanipenda, nahofia sana.” Alimuambia.


“Inamaana muda wote huo hutaki kunitambulisha ndiyo unaogopa, mimi ni mtu mzima, wanajua kuwa mke wangu amekufa hivyo nilazima maisha yaendelee, siwezi kukaa bila mke milele.” Dennis aliongea.


“Lakini hata uchukue muda, angalau tuishi pamoja kwa muda kabla ya kufunga ndoa ya kanisani, mimi naogopa kufunga ndoa ya kanisani na wewe. Kama ni kuoana tunaona a ya kiserikali labda baada ya miaka mitau ndiyo tunafunga ndoa ya kanisani, watu wakiwa washasahau kuhusu mke wako, nahofia juzijuzi ndiyo umetoka kumzika mke wako halafu mchungaji anatufungisha ndoa tena, mimi hapana.”


Dennis alimuangalia kwa mshangao bila kummaliza, kwa umri wake alipaswa kupigania na kulilia ndoa.


“Hivi mbona ni kama hunitaki, naona kama vile na kulazimisha, hembu niambie ukweli, unanipenda kwelia unanitumia tu kumsahau X wako?” Dennis aliuliza kwa wasiwasi. Alionekana kupaniki kweli, ilibidi Dorris kubadilisha mada kwani aliona kama vile anaharibu.


“Nakupenda ila nataka ukanitambulishe kwa ndugu zako kwanza, wakinikubali ndiyo twende kwetu, nakupenda mpenzi wangu ila naogopa sana, usinichukulie vibaya kabisa nakupenda…” Alijitetea sana mpaka Dennis akakubali, walipanga kwenda kujitambulisha akimuambia wote kuchukua likizo ili ampeleke kwao.


Kama kawaida ilipofika saa nne usiku aliondoka, hakutaka kulala pale kwa kisingizio kuwa bado anaishi na wazazi wake. Alifika nyumbani usiku, aliingia kwania likua na funguo zake, lakini hamadi ile anafika sebuleni anamkuta mume wake kaa anaangalia TV. Alishangaa kwani hakua na taarifa za ujio wake, alijua kuwa siku ile ni kipigo lakini mume wake alikua katulia kama vile hakuna kitu kimetokea. Alimsalimia na kumuitikia vizuri, alimuuliza kuna nini mbona alikua pale siku ile wakati kesho yake ilikua ni siku ya kazi mume wake alimpa jibu ambalo lilimchanganya zaidi.


“Nimeamua kucha kazi, nimechoka kutumikiswa, nimekuja na pesa zangu nataka kuja kufanya biashara, nimeacha kazi nimechoka kuishi mbali na familia yangu.”


MAPENZI! MAPENZI! NA MAPENZI TENA—SEHEMU YA NNE


“Umeacha kazi? Kibvipi?” dorris alimuuliza mume wake kwa wasiwasi, mume wake alionekana kuongea kwa kujiamini, hakua na waiswasi wowote na alionyesha kama ni kitu cha kawaida.


“Ndiyo nimeacha kazi, wewe si kila siku nakuambia kuwa uache kazi tuishi pamoja unakataa? Nimeona niache mimi, siwezi kuishi mbali na mke wangu, naona haina maana wote kufanya kazi wakati tupo mbalimbali, nimeamua kuacha, nataka nikae hapa nifanye biashara, hapoa arusha kuna pesa nyingi. Kuna jamaa yangu yupo Mererani amesema kuwa ataniunganisha, nimeuza kila kitu, nina kama milioni tisini.”


“Milioni tisini? Za nini? Unataka kufanya biashara gani?”


“Biashara ya mawe mke wangu, inalipa sana, yaani kuna watu ambao wameanza juzijuzi sasa hivi wako mbali. Kesho kutwa naletewa mzigo wa kwanza, utaona, nakuambia hata wewe utaacha kazi, kuna pesa sana kule.”


“Mume wangu hivi umewasikiliza hao matapeli wa Arusha, unajua biashara ya mawe weli? Ulishawahi kuona hata hiyo tanzanite mpaka unataka kufanya biashara?” Dorris aliuliza hukua kimkazia macho mume wake. Harrisa lipandwa na hasira.


“Acha kuniona mjinga, kwahiyo kwakua tu umekaa Arusha muda mrefu ndiyo ushaanza kujiona na wewe mtaalamu! Hii ndiyo shida ya kushirikisha mawazo yamaana wanawake ambao hawana hata akili. Naongea habari za pesa wewe unaongea ujinga wako, hembu niondoee huko!” Aliongea kwa hasira, Dorris alijua kuwa anakaribisha kipigo, alikaa kimya hakuonega chochote ingawa alitamani kumshauri mume wake, aliingia ndani na kumuandalia chakula.


Mume wake hakula, alijhifanya kuwa na hasira, walipanda kitandani wote wakiwa wamenuniana. Kila m,moja alikua na mawazo ya kivyake.


“Kwahiyo umeshawapa hiyo pesa yote hao marafiki zako?” Dorris alishindwa kuvumilia na kuamua kuuliza. Milioni 90 zilikua ni pes anyingi sana na alijua kabisa kuwa mume wake hawezi biashara, alijua kama akimuacha hizo pesa zikapotea basi ingekula kwake, lakini mume wake hakujibu alibaki kimya tu.


“Hata kama unataka kufanya biashara basi nenda taratibu,a nza hata na milioni kumi, uisome bioashara kwanza, bada ya muda ukishajua biashara inavyoenda basi ndiyo uongeze kidogo kidogo.” Aliendelea kuongea lakini mume wake hakujibu chochote.


Sio kwamba alikua amelalaa, hapana, Harris alikua anamsikiliza na alikua anasikilzia mawazo yake, yalikua mazuri lakinia lishachelewa, tayar alishatoa zile pesa na alichoua anakisubiria ni kuletewa mzigo tu.


“Tanzanite kuna wachimbaji na madalali, madalali si watu wa kuwaamini sana kwani nirahisi kulizwa, hata kama mtu unamjua…” Aliongea lakini hakumalizia. Harris aliasirika, alimgeukiia na kumpiga ngumi ya pua.


“Mamaaa nakufaaaa!” Dorris alipiga kelele hukua kishika pua yake, hatakaharaka alinyanyuka, alijua mume wake kashakasirika.


“Hivi unajiona kama una akili sana, wewe ndiyo nani kunishauri kitu cha kufanya kuhusu pesa zangu, siku nyingi nakuangalia unajiona wamaana sana, nimekuvumilia muda mrefu, nimekuambia kuwa nimeshaacha kazi, pesa nimeenda kufungua biashara, kama hutaki basi ondoka, tuachana mapema kabsia!”


Harris alipiga kelele, kulikua na giza lakini alipapasa na kumfikia mkewe, alimvamia na kuanza kumpiga, alimpiga sana hukua akimtukana matusi mengi ya nguoni. Walikua wakiishi nyumba ya kupanga, Dorrisa lijitahidi kunyamaza, hakutaka kupiga kelele na kuwaamsha majirani. Baada ya kumpiga sana, Harris alitoka, alichukua begi lake dogo na kuondoka.


“Kama hutaki niishi kwako basi naondoka, siwezi kuishi na mwanamke ambaye kila kitu ni kulalamika, haoni jema kwangu.” Aliondoka usiku uleule kwa hasira, ingawa Dorris alimbembeleza na kumuomba msamaha lakini hakumsikiliza, alikasirika na aliapanga kumaucha mke wake.


Hakurudi nyumbani mpaka baada ya wiki mbili, wakati wote huo hakuwahi hata kupiga simu kuulizia hali ya watoto wake. Siku moja Dorris alirudi kutoka kazini na kumkuta mume wake amekaa ndani. Walisalimiana lakini hakusema chochote, kwa uoga Dorris alishindwa kuuliza kitu. Uliopita kama mwezi tu mume wake yupo nyumbani, anaamka saa nne anasubiri chakula, anatoka kidigo anarudi tena kulala. Alikua hasemi chochote kuhusiana na biashara zake na Dorris hakumuuliza.


“Mwanamke una roho mbaya sana wewe!” Siku moja Harris alimuambia mke wake, ulikua ni usiku wamelala kitandani, Dorris alikua hajalala lakini alijifanya kutokumsikia mume wake kwani alitaka kuepusha ugomvi.


“Hutaki kuuliza hata ni nini kimeniotokea? Mume waoko Napata matatizo lakini hata hujali, wewe ni mshenzi sana, unaweza hata kuua mtu!” Aliendelea kuongea, hapo ilimlazimu Dorris kuamka kwani alijua kama akiendelea kulala basi itakua shida nyingine.


“Kwani kuna kitu gani kimetokea?” Aliuliza kwa upole.


“Kitu gani? Unajifanya hujui, una mdomo mbaya sana, yaani najuta kukushirikisha katika mambo yangu. Wewe ni mshenzi an ukiongea kitu chako kinatokea!” Aliendelea kuongea.


“KItu gani lakini?”


“Niomepoteza pesa yangu yote, mgodi nilioonyeshwa kuwa tumenunua na rafiki yangu ni wamtu, nmefika kule naleta vurugu nimekamatwa na kuwekwa ndani wiki nzima, nimeachiwa sina hata shilingi kumi.” Alianza kulalamika, Dorris alitaka kumuambia kuwa alimuambia lakini alisita, alijua kuwa atapigwa bure.


“Pole mume wangu…” Aliongea kwa upole na kunyamaza.


Mume wake naye alinyamaza wakakala. Kichwani Dorris alikua akijiuliza mambo mengi, alitamani kuuliza na kujua namna ambavyo mume wake katapeliwa lakini alikua anaogopa, alikua akimfahamu mume ake kuwa kitu kidogo tu amnakua na hasira na angeweza kumpiga. Hali ile iliendelea kwa meizi mitatu, Harris kweli alikua katapeliwa lakini hakutaka kumuambia mke wake kilichokua kimetokea. Dili la kufanya biashara ya madini alipewa na rafiki yake ambaye walisoma chuo pamoja.


Yeye alikosa kazi tangu zamani akajiingiza katika bishara ya madini, mwanzo alikua geita, lakini mambo yalivyomshinda alihamia mererani, kule alienda kama dalali wa kulangua madini ya tanzanite, alikua akidili na wafanyabiashara bwakubwa, ananunua mzigo kutoka Tanzania kisha anarusha kinyemela kwenda Kenya. Wakati mmoja akiwa anavusha mzigo dili liliyeyuka, wakiwa mpakani walikamatwa na askari, walikua na mzigo wa zaidi ya milioni mia mbili, kuna mtu aliwachomea.


Haukua ni mzogo wake, yeye alikua kama dalali, kama kawaida wlijaribu kuhonga lakini ilishindikana kwani wale askari ni kama walitumwa, kuna mfanyabiashara mwingine ambaye alicheza nao dili. Kwa maana ilibidi kuondoka na kuuacha mzigo wote ule, sasa baada ya kurudi ishu ilikua ni kulipa hela ta watu, ulianza mtafuyano, wenye mali walikua hawaelewi, katika kuzungushana yeye na jamaa yake ambaye walienda wote walianza kulipa kidogo kidogo, kwanza aliuza gari yake ambayo alinunua kama milioni 130 lakini akaiuza kwa milioni 60 kwakua alikua na shida, alihangoka mpaka kulipa zaidi ya nusu ya pesa waliyopigwa. Katika mihangaiko hiyo ndipo alikutana na Harris na kumpa hilo dili.


Kwa namna alivyomuelezea pesa inapatikana Harris alichanganyikiwa, alimuambia kuwa kuna shimo linauzwa milioni mia tatu akampoeleka mpaka kuliona, akaongea na wadau na kumtaka Harris yey kusimamia kama mkurugenzi mkuu kwakua tayari anauzoefu wa mambo ya ofisi. Harris alivyosikia stori na kuona namna ya watu wenye pesa ya mawe wanavyokula maisha alikubali, aliuza nyumba ambayo walijenga na mkewe, akauza gari yake na kujikusanya kusanya akapata milioni 90, akampa rafiki yake na kuaha kazi ili kwenda kuwa mkurugenzi mkuu katika kampuni yao.


Hakuacha harakaharaka, ulikua ni mpango wa muda mrefu kwani walienda mpaka kusajili kampuni BRELA wakakodi na ofisi na kuajiri watu, alipoona mambo yanaelekea ndipo alitoa pesa yake ili kununua shimo na wao kufanya kazi kama kampuni huku yeye akiwa bosi. Alipoacha kazi na kwenda mererani zile wiki mbili alikua akiingia ofisini kama kawaida lakini alikua haoni kitu kinachoendelea, ghafla rafiki yake yule anamuambia kuwa wameibiwa mzigo, walienda mpaka polisi, waligombana na vitu kibao lakini mwisho wa siku alitapeliwa.


Baada ya kutapeliwa alirudi nyumbani kwa aibu kwani hakumuambia mke wake chochote kwa kuona kuwa mke wake hana akili. Harris alijaribu kurudi kazini, lakini alikuta barua yake ya kucha kazi ishapitishwa, hapo hakua na namna, alirudi kwa mkewe na kazi ya kutafuta kazi ilianza tena. Lakini kwa ubabe hakumuambia mke wake chochote juu ya namna alivyotapeliwa, alijifanya mbabe huku akiwa na hasira kwani hakua na kazi, biashara wala kitu chochote cha kumuingizia kipato.


****


“Kwahiyo tunakula nini?” Harris alimuuliza mke wake, miezi sita ilikua imepita, Harris alikua bado hajapata kazi na alikua hata hahangaiki tena, baada ya kuacha kazi na kuhamia kwa mke wake kila kitui kilianza kwenda vizuri kwake. Alikua haoni tena umuhimu wa kufanya kazi, alikua ni mt wa kuamka saa nne asubuhi, anakunywa chai anarudi kulala na usiku anatoka na marafiki zake, katika muda huo alishatengeneza marafiki wengi walevi.


“Umeshaamka?” Dorris alimuuliza kwa mshangao kwani haikua kawaida yake.


Ilikua ni asubuhi saa kumi na mbili na nusu Dorris anajiandaa kwenda kazini.;


“Nimekuuliza swali tuna kula nini mchana, mimi sitaki kula ugali, samaki jana waliisha na dada anasema hujaacha pesa, nakuuliza tunakula nini?” Aliuliza kwa hasira zaidi hukua kinyanyua blanketi na kulirusha pembeni.


“Mimi jana si nilikupa elfu kumi, sasa ulitaka nikupe elfu kumi na bado niache pesa ya samaki kwa dada?” Dorris aliuliza, alikua anavaa herein huku anaongea na mume wake. Harris alinyanyuka kwa hasira, alimvamia na kumshika, alishika ile hareni ambayo ilishaingia kwenye sikio na kuanza kuivuta kwa nguvu. Dorris alianza kupiga kelele masikio ya kimuuma, alishikilia sikio huku akijipeleka upande wa mume wake ili sikio lisichanike.


“Unaongea na mimi unavaa hereni, hivi unanidharau kwakua sina kazi? Unajiona kuwa wewe ni wamaana sana, unajiona kuwa una akili sana, mimi kila siku nakuangalia, unanichia elfu kumi inatosha nini? Mimi ni mwanaume, nina matumizi mengi, unaponiachia elfu kumi kila siku unafikiri nitaifanyia nini? Hivi unajua nilikua nalipwa shilingi ngapi huko kazini? Au kwakua unaona sina kazi ndiyo uannidharau uanfikiri matumizi yamepungua!” Alifoka, Dorris alilalamika akiomba msamaha lakini mume wake hakumsikiliza, alianza kumpiga asubuhi ile na alipomaliza alimnyang’anya simua yake aina ya iphone nambayo alinunuliwa na Dennis.


“Hii hapa naenda kuiuiza, chukua vilaini vyako na ole weko uende kuifunga, nakumwagia mafuataa nakuchoma huo uso wako tuone kama utakua na kiburi tena.” Aliichukua ile simu na kurudi zake kitandani kulala, Dorris alijaribu kumsihi asiiuze atamtafutia pesa lakini alikataa, alimuambia simu ndiyo inampa kiburi hivyo anaichukua ili kumkomeisha. Alimpa ili afuite vitu vyake vyote na kumuachia simu, Dorris hakua na namna, alihamisha vitu vyeka harakaharaka, akaenda kutafuta na Box na kumpa mume wake. Mchana Harris aliamka, alienda kutafuta mteja, simu ambayo bado ilikua mpya ambayo ilinunuliwa kwa milioni moja na laki sana aliiuza laki nane tu.


“Mke wangu nilikukosea sana, sikupaswa kuuza simu yako, ulinisaidia sana…” Wiki moja ilikua imepita tangu kumnyang’anya simu mke wake. Alipenda kuiuza na kupata pesa hakurudi kabisa nyumbani na wala hakumafuta tena mke wake, alienda zake dar kwa mwanamke wake ambaye walikutana na walikua wakichat naye kwa muda mrefu facebook. Alizitumia zile pesa zilipoisha ndipo alirudi, alirudi kimya kimya na alipofika mke wake alimpokea lakini hakumesha. Dorris alikua kama kanuna akimsalimia tu na kutimiza majukumu yake kama mke lakini hakumchekea tena mke wake.


“Nimeshakusamehe, simu kwani kitu gani, maisha lazima yaendelee.” Dorris alijibu kwa mkatao, ingawa bado alikua na hasira lakini hakua na namna, alijua kabisa kuwa hata akilalamika, hata akilia na kusaga meno kwa mume wake haiwezi kusaidia chochote.


“Mona unajibu hivyo, inamaana bado hujanisamehe?” Alimuuliza.


“Hapana mume wangu, nimechoka tu na haya mambo, hata nikijibu vipi lakini kama ni kuuza ushauza, simu haiwezi kurudi tena, sitaki kubeba vinyongo katika moyo wangu, nimeona yaishe basi.” Majibu yake yalimkasirisha sana Harris, kwa mambo aliyomfanyia alitegemea hasira, lakini Dorris hakuonenaka kama ana hasira, alionekana kuchoka na kukata tamaa, alikua hajali tena kictu chochote anachofanya mume wake.


“Wewe utakua na mwanaume mwingine wewe! Hembu simu yako?” Harris alianza kutafuta kitu cha kumkasirisha,a limnyang’anya Dorris simu yake ndogo kutaka kujua kama alikua na mtu mwingine, aliangalia na hakukuta meseji yoyote ya mapenzi, alimrudishia kwa hasira. Alitoka na hakurudi mpaka asubuhi yake, ilikua ni siku ya jumamosi na Dorris hakwenda kazini, alirudi akiwa kalewa lakini mke wake hakumuuliza kama alikua wapi? Alikua bize na mambo yake, Harris alikua kanywa pombe na kulewa makusudi, alifanya hivyo ili kumkera mke wake lakini Dorris alikua hakereki alikua bize na mambo yake kitu ambacho kilizidi kumchanganya.


Baada ya kuona mke wake hakereki Harris alizidisha vituko, alianza kuongea na wanawake wengine kwa simu bila kujali kama mke wake anamsikiliza au la. Alikua akifanya hivyo usiku, anatongoza wanawake facebook anawaomba namba za simu kisha usiku wanapigiana simu kuongea na kutumiana picha za uchi, bdao Dorris hakujali, alishachoka tabia za mume wake hivyo hata hakujali kama anachepuka au la. Alipoona hiyo haisaidii, Harris alihisi kuwa mke wake ana mwanamke mwingine, alianza kumfuatilia lakini hakujua kitu chochote, baada ya kuona hagundui kitu mke wake yupo bize na kazi alianza kuwa karibu na Mariam.


Mariam na Dorris walikua ni marafiki wakubwa, walisoma pamoja na baada ya kumaliza chuo, mariam alienda kuwa mwalimu na huku Dorris akiwa mhasibu lakini wote katika halmashauri moja. Harris alikua akimfahamu Mariam na kwakua wake zao walikua marafiki basi hata yeye alimjua mume wake na wakawa marafiki. Mariam alikua mnywaji na mara nyingi alikua ni wale watu wa kukaa baa mpaka usiku, pamoja na kuwa na mume lakini alipenda Bata sana, mume wake alikua ni mtu wa kusafirisafiri kutokana na kazi yake hivyo alikua na muda mwingi wa kuzuruda.


Ukaribu wao ulianzia Baa, kila alipokua akikutana naye Baa alimnunulia Bia wakaongea na kumdodosa kuhusu mke wake. Lakini hakujua kitu chochote, Dorris alikua anamfahamu rafiki yake hivyo alikua makini sana kumuambia siri zake. Mariam alikua akimfahamu Dennis kwa kumuona tu na kujua kama mfanyakazi mwenzake lakini hakuwahi kuwa karibu naye wala kuhisi kama ni wapenzi. Harris hakupata kitu chochote, lakini katika kipindi hiki alifanya juu chini mpaka akaanzisha mahusiano na Mariam, walianza kuwa wapenzi na mapenzi yalipamba moto.


Lengo la Harris halikua ni mapenzi na Mariam bali kumuumiza mke wake, baada ya kuhangaka na wanawake wengi bila mke kuumia aliamua kwenda na rafiki yake. Alianza kupiga picha za uchi kitandani na Mariam na kumtunmia mke wake, ilikua ni mchana na Dorris alikua kazini, alikua amekaa anakula na walikua na Dennis meseji nyingi zilivyoingia. Alifungua na kumuona mume wake akiwa kitandani uchi wa mnyama na rafiki yake kipenzi ambaye alikua akimuona kama dada yake, pozi lilimuishia akashindwa hata kula. Alibadilika ghafla mpaka Dennis akashiituka.


“Vipi umeona nini?” Dennis alimuuliza.


Dorris ameona mesehi za rafiki yake na mume wake, yuko Mbele ya Dennis ambaye anataka kujua nini kimetokea? Lakini je vipi mahusiano yake na Dennis yapoje, si Dennis alikua anataka kujitambulisha nini kilitokea mpaka sasa


MAPENZI! MAPENZI! NA MAPENZI TENA—SEHEMU YA TANO


“Hakuna kitu!” Dorris alimjibu Dennis, huku akiendelea kuziangalia meseji za mume wake na rafiki yake kitandani. Alijitahidi kutulia kama vile hakuna kitu kibaya kimetokea lakini ukweli nikuwa alikua anaumia sana. Tangu mume wake kurejea Dorris alikua amebadilika sana, alianza kuwa mtu wa hasira na mara kwa mara walikua wanagombana na Dennis. Kila alipokua akikasirikiana na mume wake kupigwa au kufanyiwa kitu chochote kibaya hasira zote alizielekeza kwa Dennis ambaye alimvumilia kwakua alikua anampenda. Mara kadhaa Dennis alijaribu kuwa karibu naye lakini alimkasirikia na kumsukuma mbali kabisa.


“Sitaki kufuatwa fuatwa, kama unaona huwezi kuvumilia basi na niache ondoka, kwani kuna wanawake wengine wangapi mpaka kila siku kuning’ang’;ania mimi!” Mara kadhaa alimuambia, Dennis alimuuliza ni lini atampeleka kwao kujitambulisha kwania lishachoka kusema subiri subiri.


“Siku hizo umebadilika sana, kwanini umekua hivyo, kila nikitaka kuja kwenu unakua mkali, huniambii sababu, nakupenda lakini na mimi ipo siku nitachoka.” Denisi alimuambia kwa upole.


“Kama umechoka si uniache, kwanza kwanini unaning’ang’ania kunioa, wewe mke wako si amekufa, mimi nitajuaje kama umemuua na unataka kunitoa sadaka na mimi?”


Maneno yalimtoka Dorris bila kujipanga, alishamuambia Dennis kila kitu lakini Dennis alikua bado anamng’ng’ania, baada ya kuja mume wake alijua kuwa ni lazima atatakiwa kuchana na Dennis hivyo alijaribu kumkera ingawa alikua king’ang’anizi sana. Mara zote Dennis alimuelewa, hakuwahi kumuacha wala kuonyesha kukasirika, lakini manano ya siku hiyo yalimuuma sana. Alimkumbuka mke wake na kuanza kulia, alimuangalia Dorris na kufuta machozi, bila kusema chochote alinyanyuka na kuondoka, tangu siku hiyo hakuongea tena na Dorris kuhusu mapenzi.


Hakumkasirikia, aliendelea kumsalimia kama mfanyakazi mwenzake lakini aliamua rasmi kumuacha, aligundua kweli kuwa hatakiwi. Kitendo kile kilimuuimiza sana Dorris, aliongea yale maneno akiwa na hasira, hakua akimaanisha lakini alikua amechoka na maisha yake, alikua anampenda sana Dennis na alikua akimfanyia mema mengi sana, akimfariji kila akiwa na mawazo lakini alijua kuwa hawawezi kuwa pamoja kwani yeye tayari ni mke wa mtu. Mara kadhaa alijilaumu ni kwanini hakukutana naye mapema kabla ya kuingia kwenye ndoa na mume wake.


Maneno aliyomuambia yalimuuma, alimfuata na kumuomba msamaha akisingizia hasira, Dennis hakujua kilichokua kimemkasirisha lakini alimsamahe na kumuambia kuwa hatamsumbua tena na kweli hakumsumbua. Doris alikua anaumia kimya kimya kwani alishamzoea lakini alijua kuwa hawawezi kuwa pamoja hivyo alivumilia. Hawakuongea tena mpaka siku ile walipokutana sehemu ya chakula, alipoziona zile picha na kubadilika ndipo Dennis alishindwa kuvumilia na kuamua kumuuliza.


Dorris hakutaka kumuambia Dennis kitu chochote, alinyanyuka kwa hasira na kuondoka, lakini hakufika mbali, alidondoka chini, akaishiwa nguvu na kupoteza fahamu. Dennis na watu wengine walimnyanyua na kumpeleka hospitalini, kulefahamu zilimrejea, aliambiwa kuwa presha ilikua juu, alipumzishwa kwa muda na baadaye kuruhusiwa, wakati wote huo Dennis alikua naye akimuangalia kama rafiki yake, hakuondoka pembeni yake, ingawa alitamani kujua kilichokua kimetokea lakini hakumuuliza chochote.


Aliporuhusiwa alitaka kumpeleka mpaka nyumbani, Dorris aligoma kabisa kwani alijua kuwa wanaweza kukutana na mume wake,


“Sina hata ya kufika kwenu kuonana na Mama yako, nataka nikufikishe kwanu basi.” Alimuambia na kuonyesha kuwa hakua tayari kwa namna yoyote ile kumuacha aende peke yake. Dorris hakua na namna, alikubali kupelekwa mpaka nyumbani, walienda na walipofika Dorris kuna kitu kilimuingia, njia nzima alitamani kumuumiza mume wake, alitamani kulipa kisasi, alitamani kufanya kitu ambacho kitamkera mume wake.


“Ingia ndani…” Alimuambia.


“Una uhakika?” Dennis alimuuliza kwa wasiwasi. Hakutaka kuingia ndani lakini alitaka kujua kama kweli Dorris anamruhusu kuingia ndani kwake.


“Ndiyo nina uhakika, kwani hutaki?” Alimuuliza huku akijilegeza, alikua na hamu sana ya kufanya mapenzi hasa kwa lengo la kulipa kisasi. Lakini Dennis hakua tayrai, slishaunfunga moyo wake na mamboyote aliyomfanyia siku ile alimfanyia kama rafiki.


“Hapana, siwezi kuingia ndani kwenu, natamani sana kumuona Mama yako, kujitambulisha kwenu kama mchumba wako lakini najau kuwa hunitaki, siwezi kujilazimishia kwako, hata kama nakupenda namna gani lakini najua kuwa sitakiwi hivyo siwezi kuingia.” Alimjibu huku akifunga mlango wa gari na kuondoka, hapo ndipo Dorris aliamini kuwa kweli mapenzi yake na Dennis yaliisha, alijisikia vibaya kwani bado alikua anampenda na alijua kuwa ipo siku watakuja kuwa pamoja.


****


“Nani amekushusha hapo nnje?” Harris alimuuliza mke wake, muda wote alikua dirishani anamuangalia mke wake akishuka kwenye gari ya Dennis. Alijifanya kukasirika.


“Nimeona picha zako na rafiki yangu, yaani kati ya watu wote umeona utembee na rafiki yangu?” Dorris hakujibu swali, alimgeuzia kibao na kuzungumizia suala la picha.


“Najua umeona, si nimeona umesoma kabisa, nilikutumia ili uone kuwa kuna wanawake bado wananitaka, mimi ni kidume naweza kufanya kitu chochote, naweza kutembea na mwanamke yeyote, naweza kutembea hata na Mama yako mzazi na huwezi kunifanya chochote!” Aliongea kwa hasira huku akijilazimisha kucheka. Maneno yake yalimkera Dorris, lakini hakutaka kuendelea kuongea alinyamaza kimya na kuondoka kuelekea chumbani kwake.


Harris hakuridhika, aliona kama kadharauliwa, alimfuata na kumshika bega kisha akamuambia.


“Nina shida ya laki mbili?” Aliongea hukua kimnyang’angya pochi yake.


“Najua una pesa lakini unazificha, nataka kutoka na mpenzi wangu ila sina pesa.” Dorris hakua na pesa yoyote, alimuachia achukue ile pochi, aliigakua lakini hakukuta kituu. Kwa hasira alimpiga nayo kichwani akaondoka.


“Mshenzi mkubwa wewe, mwanamke umjinga sana, yaani kama yule rafiki yako, wote Malaya tu, unafanya umalaya huko badala hata uwe unapata pesa uajiuza bure, rafiki yako naye bia mbili tu kashatoa mzigo, Malaya nyie!” Alitukana lakini Dorris hakujibu kitu chochote, alibaki kimya na kuingia chumbani kupumzika kwani kichwa kilikua kinauma.


Aligika chumbani kwake na kukaa, lakini kabla hata hajatulia simu yakle iliita, ilikua ni namba ya Mama mkwe wake, aliipokea lakini hata kabla ya kuanza kuongea alianza na matusi.


“Msheniz kabisa wewe, mwanangua likuchukua huna kitu, kakuhangaikia umepata na kazi leo ni wa kumdharau, kama umechoka ndoa basi ondoka niachie mwanangu, mambo ya kumtukana na kumsengenya, kila siku unamtangaza kuwa hana kazi, hana pesa ya kuhudumia familia, wewe una nini masikini mkubwa wewe…”


Mama mkwe alitukana sana, wala hakumpa muda wa kujitetea. Dorris alinyamaza kimya, alijua ni lazima mume wake kashaenda kuongea maneno ya uongo, ilikua ni kawaida ya mume wake, kila akifanya kitu kibaya basi anawapigia simu ndugu zake, anawapanga kwa maneno ya uongo mpaka wanamuamini. Alinyamaza tu kwani alishazoea, lakini kabla hajafanya chochote simu iliingia, ilitoka kwa Mama yake, alimsalimia lakini alishangaa Mama yake anaanza kumlaumu.


“Mwanangu ndoa haziko hivyo, kama mume wako akikosa wewe kama mke ndiyo una kazi ya kumsitiri, kwanini kumdhalilisha mpaka kwenye mitandao kuwa hana kitu, kuna haja gani ya kutuma meseji kwa watu kuelezea kuwa wewe ndiyo unamlisha mume wako?” Mama yake aliongea kwa sauti ya chini lakini iliyojaa machungu makubwa.


Dorris alishangaa na kumuuliza Mama yake ni kitu gani kimetokea.


“Mume wangu kanitumia meseji ambazo unasambaza kwa marafiki zako, unamuita mume mwako ni mwanaume suruali? Kweli, nilikusomesha ili uwe na kipato usaidia familia lakini si kumdhalilisha mume wako. Baba wa watu kasimamishwa kazi, alikua anajitahidi kuhudumia lakini huwezi jua matatizo yanatokea, mara nyingi alikua ananisaidia, alikua ananitumia pesa bila hata kumuomba, ni mtu mzuri, mwanangu ukimpoteza huyo mwanaume huwezi kupata mwanaume mwingine kama huyo.” Mama yake alimuambia.


Dorris alishangaa ni meseji gani alikua ametuma ndiyo Mama yake alimtumia meseji ambayo katumiwa na mume wake.


“Nakuambia, mwanaume niliyenaye ni shida mimi ndiyo nahudumia kila kitu, mwanaume hana pesa ya kununulia hata kilo ya sukari, nishamchoka, nina mzee wangu ndiyo anahudumia familia, hapa natafuta sababu nimuache, na nikiipata nadai talaka ya mahakamani, siwezi kuishi na mwanaume hana pesa.” Ni meseji ambayo mume wake alimtumia Mama yake na kumuambia kuwa mke wake alikua akisambaza kwa marafiki zake akimuambia kuwa anamtafutia sababu ya kumuacha.


“Mwanangui, sikupangii maisha lakini kama tabia zako ndiyo hizi basi jua kuwa ukiondoka kwa mume wako kwangu usirudi. Baba yako sijamuambia, sitaki uje kumuua kwa presha!” Mama yak ealiongea kwa hasira, Dorris alijaribu kujitetea lakini hakumsikiliza.


“Nnamjua mume wako, ni mtu mzuri hawezi kudanganya, nimekuambia kuwa wewe ni mwanangu lakini ukimuacha huyo mwanaume kwasababu ya pesa basi kwangu usikanyage na sahau kuwa ulishawahi kuwa na Mama.” Mama yake alikata simu na kumaucha Dorris akiwa kachanganyikiwa hajui nini chakufanya, alipanda kitandani ili kulala lakini usingizi haukuja, alikua na hasira nyingi sana zilizochanganyika na kuchanganyikiwa.


MAPENZI! MAPENZI! NA MAPENZI TENA—SEHEMU YA SITA


(ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO; Harris anamtumia mke wake picha za uchi akiwa chumbani na Mariam rafiki yake na Dorris. Dorris anamleta Dennis mpaka nyumbani kwake na kutaka kumtambulisha lakini anakataa kuingia anaondoka ndiyo anaona kama vile kaachwa. Anaingia ndani mume wake anamgeuzia kibao kwa kupigia simu ndugu zake kuwa mke wake anataka kumuacha kwasababu ya mali, ndugu wanamshangaa, Mama yake anampigia simu na kumuambia kama akimuacha mume wake kwasababu ya kazi basi yeye si mwanae. Je nini kitaendelea? ENDELEA….)


Harris alikua kammaliza mke wake kila sehemu, kila mtu alikua akimchukia Dorris akijua kuwa yeye ndiyo mwenye matatizo. Kazini nako mambo hayakua mazuri, Dennis pamoja na kumpenda lakini aliacha kuhangaika, alikua mahajali tena, alipunguza mawasiliano na ikafika kipindi hata alikua hapokei tena simu zake. Baada ya muda alisikia kuwa Dennis ana mwanamke mwingine ambaye anatoka naye, ni wafanyakazi wenzake walikua wanazungumzia, aliumia sana, kwani bado alikua anampenda na alikua anatamani sana kuendelea kuwa naye ingawa hali ilikua hairuhusu.


“Nasikia anataka kumuoa, jamani mwanaume atakayempata yule Kaka anabahati, Bosi lakini haring, natamani hata angenitongoza ningekiacha kile kibwana changu, kutwa kicha mwanaume kujishaua lakini hana chochote!” Rafiki yake mmoja ofisini aliongea, mahusiano yao yalikua ya siri, ingawa walikua na ukaribu lakini hakuna mtu aliyekua anajua kuwa wanatoka pamoja.


“Nakuambia, wanaume wa namna hiyo hata hawatuoni! Shogaa sijui una balaa gani, si mlikua karibu, kwanini hata usingejilengesha akutongoze, yaani ningekua mimi wewe hata kamahasimamishi ningelazimishia poteli ya mbali, Dennis kifaa bwana!” Waliendelea kuongea manano ambayo yalizidi kumchoma.


Alitamani kuondoka lakini hakutaka kuonekana kama nayeye kaumizwa, alisikiliza na kuchangia huku akitamani kulia kabisa. Alitafuta sbabau na kuondoka, moja kwa moja bila kudhamiria alienda ofisini kwa Dennis, alitaka kumuuliza kujua kama ni kweli.


“Nilipanga kukuambia mambo ya kiwa siriasi, lakini tangu kipindi kile uliponikataa nisije kwenu niliona kama napoteza muda hunipendi. Wanangu ni wadogo wanahitaji kuwa na Mama, nahitaji mtu wa kunisaidia, najua ungekua Mama bora lakini niliona tu dalili kuwa hunipendi. Sijakasirika ndiyo maisha ni kweli naoa mwezi ujaoa, sitafanya sherehe kwaheshima ya mke wangu, ni ndoa tu y amarafiki wa karibu, kama utaweza unakaribishwa.”


Kama kawaida Dennis aliongea kwa sauti yake ya upole, Dorris aliumia sana lakini hakua na namna, alilazimika kukubaliana namatokeo. Aliondoka akiwa hajielewielewi. Alirudi nyumbani na kukuta mume wake katoka, hata hakuuliza, alipanda kitandani moja kwa moja kulala hata kucheza na mtoto alishindwa. Usiku kwenye saa tisa hivi mumewe alirudi, alikua kalewa chakari, aligonga sana mlango lakini hakufungua, alikua kalia sana, alikua kachoka, dada wa kazi alienda na kumfungulia mume wake, ambaye alikua kitandani na kuanza kumtukana lakini hakujibu chochote.


“Nikinyanyuka hapa naweza kumuua huyu mwanaume!” Alijisemea kichwani, mume wake hakukoma kuongea, aliongea mpaka alichoka, akapanda kitandani na pombe zake akalala hivyo hivyo na Dorris hakumsemesha. Aliumizwa sana na kuoa kwa Dennis, ndiyo mwanaume pekee aliyekua anampenda, alikua anampenda kuliko hata mume wake, alijisikia vibaya. Asubuhi alishindwa hata kwenda kazini, aliendelea kulala, hakupiga hata simu kazini kusema kuwa anaume, alikaa tu, hata hakuamka kumuandaa mtoto kwaajili ya kwenda shule, alimuachia dada wa kazi.


***


Harris aliacha kabisa kutafuta kazi, hakua na kitu kwani kila kitu alikua anamtegemea mke wake. Kuanzia chakula mpaka pesa za kuhonga alikua anamtegemea mke wake. Pamoja na kumtegemea mke wake kwa kila kitu lakini bado aliendelea kumnyanyasa, alikua ni mtu wa kumtukana kila siku, kubadilisha wanawake na Dorris akilalamika ilikua ni kipgo. Tatizo jingine lilikua ni katika tendo la ndoa, Harris alikua hana uwezo mkubwa katika kufanya tendo la ndoa, kwanza alikua hapendi kufanya mapenzi na mke wake na kama ikitokea akafanya basi ni kwa matusi na hawezi kufika hata dakika tano.


“Mwanamke unanuna sana, unajua najitahidi sana kuvumilia lakini nashindwa, ndiyo maana siwezi hata kumudu muda mrefu, huko kwa wengine nafanya mpaka asubuhi lakini wewe ni Mbaya, unanuka, sijui hata nikikuacha nani atakuoa!” Mara kwa mara alipenda kumuambia mke wake wakati wa kufanya mapenzi, alikua akiongea hivyo akiwa kifuani kwake. Maneno yake yalimchoma sana mkewe lakini hakua na namna, alinyamaza na kweli akiamini kuwa kama akimuacha mumewe basi hawezi kupata mwanaume mwingine.


Baada ya muda sasa Harris alianza kulalamika alikua anataka mtoto mwingine lakini mkwe hakua tayari. Jukumu la kulea lilikua kubwa na aliona kama mume wake hawezi kubadilika, alikua ashabweteka na kufurahia kuhudumiwa na mkewe hivyo aliona kama atabeba mimba yake basi itakula kwake. Wakati mmoja Mama yakee na Harris alikuja kuwatembelea, kutokana na maneno ya Harris ya kumsema alikua hawana mahusiano mazuri, mama alikua hampenzi Dorris aliona kama vile anamharibia maisha mwanae, lakini Dorris hakua na kinyongo, alijua kua chuki zote zilisababishwa na mume wake ivyo asingeweza kuziia, hakumlaumu Mama mkwe wake kwani hata Mama yake mzazi alikua aamemkasirikia na ababu kubwailikua ni mumem wake.


Mama mkwe alikuja kwakua alikua anaumwa, alikua anamatatizo ya Inni, ingawa hali yake haikua mbaya sana lakini alihiaji uangalizi wa karibu. Dorris alijitahidi sana kuwa karibu na Mama mkwe wake, alimfanyia mambo mazuri ambayo yalimshangaza Mama mkwe wake. Kwanza Mama mkwe alishangaa kuona kuwa yeye ndiyo anahudumia kila kitu tofauti na namna ambavyo alikua akiambiwa na mwanae, alishangaa namna ambavyo anavumilia tabia za mwanae za kurudi usiku tebna akiwa kalewa.


Siku moja Mama mkwe alitoka chumbani, ilikua ni usiku kwenye saa tano hivi. Dorris alikua bado hajalala amekaa sebuleni kwenye kochi ili mume wake akirudi amfungulie mlango. Ilikua ni kawaida yake klulala kwenye kochi kwani kama akilala chumbani na mume wake akaja na kugonga mlango akashindwa kufungua kwa wakati basi ilikua ni kipigo cha mbwa. Alishazoea hiyo hali, alikua anapigwa mbele ya mtoto wake na binti yake. Mume wake alikua ni mtu wa hasira za karibu. Pamoja na kuwa Mama yake alikua pale lakini alikua akichelewa na wala hakujali kabisa.


“Mwanangu unafanya nini usiku wote huu?” Alimuuliza.


“Mama, mbona umeamka, unajua unaumwa, hembu rudi kalale…” Alimuambia huku akinyanyuka na kumshika Mama mkwe wake.


“Hapana, unajua kila siku mwanangu ananiambia maneno kuhusu wewe lakini sasa hivi nimeona. Hivi mwanangu unafanya nin na huyu mwanaume, ni mwanangu kweli lakini kwanini unamlea, mtu hatoi hata pesa ya sukari lakini anakurudia nyumbani saa tisa usiku halafu unamuangalia. Nasikia anakupiga, nasikia anakutukana, nasikia ana wanawake, hivi wewe si una kazi kwanini unahangaika naye?” Mama mkwe alimuuliza, Dorris hakua na jibu, ni kweli alishachoka lakini alikua hawezi kuondoka, alitamani sana kuondoka lakini hakujua ni kwa namna gani anaweza kumuacha mume wake.


“Mama nimechoka lakini sijui hata chakufanya, huyu ni mume wangu, siwezi kumuacha, nimevumilia nimechoka, naamini atabadilika.” Alijitetea, ukweli nikuwa alishakata tamaa na alikua anajua fika kuwa mume wake hatabadilika. Mama mkwe wake alikua hajisikii vizuri, aliondoka na kurudi nyumbani. Dorris alimasubiri mume wake mpaka aliporudi akamfungulia wakalala. Siku iliyofuata Mama aishindwa kuvumilia, alimuita mwanae na kumsema sana, Harris alijifanya kumuelewa lakini alikasirishwa na kile kitendo akidhani kuwa mke waka ndiyo kaenda kumlalamikia.


Jioni ya siku hiyo Harris alimuomba mke wake msamaha, alimuomba watoke pamoja, alichukua gari la rafiki yake, akimtoa kama vile anampeleka out walienda mpaka kwenye hotali moja, akachukua chumba na kuingia naye. Dorris alishanagaa kwani ilikua kama maajabu, aliiona kama mume wake kabaidlika kweli, Harris alimuambia avue nguo nayeye alifanya hivyo, lakini ile kumaliza Harris alitoa mkanda wake na kuanza kumpiga, alimchapa sana na mkanda alimpiga mpaka Dorris akaanza kupiga kelee. Watu walikuja ndipo Harris alisema kuwa alienda pale kumfumania mke wake, alimkuta na mwanaume chumbani ndiyo akaamua kumpiga.


Alipoulizwa alipokua mwanaume aliwaambia kuwa amekimbia na kuacha nguo zake, kweli walipoangalia walikuta viatu vya kiume na shati pale chini, Dorris alikua uchi wa mnyama wakati mumewe alikua kavaa nguo. Watu walianza kumzomea, alimuambia mkewe avae nguo kisha akamchukua mpaka kwenye gari yake.


“Hii ndiyo adhabu yaw ewe kuongea na Mama yangu. hapa leo nimekuonjesha kuwa huwezi kunikwepa, ukiendelea kunichafua kwa Mama yangu kitu nitakachokufanya hutakuja kunisahau, nitakumwagia tindikali usoni na kukupeleka hospitali mwenyewe ili ukipona ukijiangalia usoni ujue mimi ni nani?” mimi ndiyo mwanaume hapa na sitaki ushenzi ushenzi wako. Tunarudi kwa Mama sasa nisikie umeongea kitu, siwezi kukupiga mbele ya Mama lakini unaweza kujikuta hata umevunjwa kiuno huko barabarani watu wakasema umegongwa na gari! Mimi si mtu wa mchezomchezo!” Alimuambia wakati wanarudi kuelekea nyumbani.


MAPENZI! MAPENZI! NA MAPENZI TENA—SEHEMU YA SABA


(ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA; Harris aliacha kabisa kutafuta kazi na kuwa mtu wa kutegemea mke wake kwa asilimia mia. Alikua mtu wa kulewa, anarudi asubuhi. Mama yake anakuja kumtembelea na kugundua hizo tabia, anamuonya mwanae kitu ambacho kinamkasirisha Harris akidhani labda mke wake kaenda kulalamika na kumchafua kwa Mama yake. Anajifanya kumuomba msamaha, anampeleka mpaka nyumba ya kulala wageni kisha anaanza kumpiga kana kwamba kamfumania, anatoka na kumtishia kuwa akiendelea kumshitaki kwa Mama yake basi atamfanyia kitu kibaya zaidi. ENDELEA… Kama hukusoma sehemu ya sita basi bonyeza hapa; https://www.instagram.com/iddimakengo/ )


Hali ya maisha ilizidi kuwa mbaya, baada ya Mama yake kuondoka Harris alikua kama kahamia Baa, kila siku alikua ni mtu wa kunywa na akirudi kazi yake kubwa ni kumpiga mke wake. Kila siku alikua anarudi usiku wa manne. Pamoja na yote hayo lakini Dorris alijitahidi sana kufanya kazi,a lkijitahidi kuficha mapungufu ya mume wake, hakuonyesha kama ana shida, alikua ni mtu wa kuvaa vizuri, akipendeza na kuvaa tabasamu, kwa watu wa nnje hakuna aliyedhani kama ana matatizo katika ndoa yake.


Kila kitu kilikua kinamuuma sana mume wake, aliona kama anamdharau kwamba pamoja na chuki zote hizo, vipogo na manyanyasa lakini bado mke wake alikua ni mtu mwenye furaha.


“Atakua na mwanaume mwingine, hakuna namna yuko vile?” Siku moja Harris alimuuliza Mariam. Walikua Baa wanakunywa, tangu kuanzisha mahusiano yao hawakuacha, mume wa Mariam alikua ni mtu wa kusafiri safari sana hivyo alikua na mda mwingi wa kula bata na Harris.


“Hata sijui, ni rafiki yangu lakini ni msiri sana, sema kule ofisini kwao kuna Kaka mmoja nasikia yuko karibu naye sana, kuna kipindi walikua na ukaribu lakini sasa hivi naona kama wamegombana kwani nasikia kaoa.” Alimuambia, pamoja na Dorris kumpuuza na kutokumuuliza chochote lakini bado alikua anamfuatilia, ilikua inamuuma sana kuona kuwa katembea na mume wa rafiki yake, rafiki yake kajua na wala hajamuuliza chochote maisha yanaendelea, hata wakikutana mjin bahati mbaya bado anamsalimia na hamnunii.


“Huyo huyo ndiyo atakua mtu wake, haiwezekani akawa na furaha namna hii, mwanamke hata nisiporudi wiki mbili haongei chochote!” Harris alifoka kwa hasira.


“Nadhani atakua, ingawa watu wanasema ni marafiki lakini sidhani, kwanza nahisi ndiyo atakua kamnunulia mke wako gari.” Alimuambia.


“Kamnunulia gari? Gari gani hilo?” Harris aliuliza kwa mshangao, alikua hana hizo habari.


“Wewe ni mwaname gani sasa, tatizo lako ni hii mipombe yako, inamaana hujui kama mke wako kaagiza gar tena jipaya kabsia, ameagiza IST mimi najua kila kitu wewe unalala naye kila siku hujui. Ana pesa gani ya kununua gari kama si kuhongwa!”


Ni kweli Dorris alikua kaagiza gari, hakutaka kumuambia mume wake kwani alijua kuwa itakuja kuleta shida mbeleeni. Zile havari zilikua ni mpya kabisa kwa Harris, zilimchanganya na kuzidi kumpa wivu, alishindwa hata kunywa pombe, alitondoka bila kuaga na kurudi nyimbani. Haikua kawaida yake kurudi mapoema namna hiyo, ilikua ni sa nne na ndiyo kwanza alikua anaanza kunywa pombe aliposikia habari za mke wake kununua gari, aliingia ndani akionekana kukasirika sana, mkewe kumuona alijua kuwa kuna kitu. Mtoto alikua kashalala na dada wa kazi alikua anangalia TV.


“Unafanya nini macho sasa hivi?” Alimuuliza binti wa kazi mara baada tu ya kuingia, binti aliogopa hata kabla ya kujibu alinyanyuka na kuingia chumbani kwake. Mkewe ambaye naye alikua akiangalia TV aliacha kuangalia na kumskiliza yeye.


“Nikuwekee chakula?” Alimuuliza baada ya kukaa, huku yeye akisimama kutaka kwenda kumtengea mume wake chakula. Harris aliamuangalia kwa hasira, alimuacha akatembea umbali kidogo kama wa hatua tatu hivi, kisha alimvuta gegani, akamvuta kwa nyuma na kumsukuia kwenye kochi. Alianza kuvua nguo na kumlazimisha kufanya mapenzi palepale sebuleni. Dorris aliona aibu na kua za kujizuia.


“Mume wangu unataka kufanya nini?” Alimuulza huku akijitahidi kutaka kumtoa katika mikono yake.


“Mimi si ni mume wako, unaniuliza ili nini? Nakutaka, nataka kufanya mapenzi na wewe, unaona shida gani, au kuna mwanaume mwingine ambaye unamtimizia haja zako?” Aliongea kwa hasira huku akimtandika makofi.


“Hapana, lakini hapa ni sebuleni mume wangu, angalau basi tuiongie chumbani.” Alijitetea huku akijitahidi kujistiri, Harris alikua na hasira sana, alimzidi nguvu na kumchania chania nguo.


“Watoto watatoka mume wangu!” Aliongea kwa kunong’oneza lakini mume wake hakujali asliendelea kumlazimisha, alikua amebaki tu na nguo ya ndani, mume wake alimshika na kuivuta, mara damu zilianza kutoka.


“Ninini hiki?” Harris aliuliza kwa hasira.


“Niko kwenye siku zangu mume wangu, inamaana hujui, nimeanza tangu jana!” Alimuambia, ni kweli alikua katika siku zake na damu zilikua zikimtoka nyingi tu.


“Mehsni mkubwa wewe, hii ndiyo michezo yenu nyie wanawake, mkishachepuka mnakuja kujimwagia mi coca cola ili sisi waume zenu tusiwaguse, hivi unaniona mimi kama mtoto wa juzi, najua kila kitu. Wewe umetoka kufanya mapenzi na huyo bwana wako aliyekununulia gari, sas angoja nikuonyeshe!” Aliongea kwa hasira huku akimvua il enguo ya ndani, aliivuta kwa nguvu mpaka ikakatika, akachukua ile Pedi ambayo ilikua imeloa na kumsukumiza mdomoni.


“Si unajifanya una bleed sasa kula madamu yako, si hutaki kunipa, kama ni soda tutajua leo!” Aliongea kwa hasira hukua akijaribu kumsukumizia kwa guvu mdomoni, Dorris alijitahidi kujitoa mikononi mwake, alijisukumiza mpaka akaweza, aliitupa ile pedi chini kisha akakimbilia chumbani kwake. Lakini kabla ya kufunga mlango mume wake aliingia, alimshika na kuanza kumpiga, alianza kumlazimisha kufanya mapenzi, alijaribu kufanya kawaida kidogo.


“Si uko kwenye siku zako, sasa ni huko mbele, huku nyuma si hamna cha siku zako!” lifoka akijaribu kumuingilia kinyume na maumbile, Dorris alijtahidi kubana miguu kwa muda wa kama dakika tano, alijua kuwa mume wake hawezi kukaa amesisimka kwa muda huo.


Kikawaida huwa hawezi kufanya mapenzi kwa zaidi ya dakika tano, angalau mwanzo alikua anaweza lakini tangu kuwa mtu wa mippombe na wanawake sanasana aliishia dakika mbili au tatu. Kweli alibana miguu mpaka mume wake nguvu zikamuishia, kwa aibu alijilaza pembeni huku akitukana.


“Mwanamke mwenyewe unanuka, yaani naishi na wewe kwa shida tu! Ndiyo nimetoka kufanya mapenzi na rrafiki yako, yaani ni mtamu balaa, najuta kabisa kwanini sikumuoa yeye!” Aliongea, Dorris alibaki kimya, alitamani kumjibu lakini alijua majibu kwake yalimaanisha kipigo. Harris alimtukana sana mpaka akapitiwa na usingizi, kuona vile Dorris alinyanyuka na kwenda kujisafisha kwani alikua anasikia kinyaa kutokana na kusokomezwa Pedi mdomoni.


****


Aubuhi Harris ndiyo alikua wakwanza kabisa kuamka, hakutoka nnje, kabla ya kunnyanyuka kitandani alimuamsha mke wake.


“NI nani kakununulia gar? Wewe kila siku unalalamika kuwa huna pesa, nikikuomba pesa nifanye Biashara hutaki umepata wapi pesa? Kama huna majibu ya maana unaondoka hapa na sitaki kukuona, unaondoka unaniachia mwanangu!” Alifoka.


Dorris aliamka na kuanza kujitetea kuwa alichukua mkopo kazini, na hakumuambia kwakua alijua kuwa atakataa lakini ameamua kununua gari kwakua amechoka na daladala.


“Kwahiyo unajifanyia mambo yako mwenyewe mwenyewe! Hapana, nahisi kuna kitu, hujachukua mkopo. Nitaongozana na wewe mpaka kazini kwako kujua kama ni mkopo au umehogwa.”


Alifoka, Dorris alihisi kama ni utani, lakini wakati anamaliza kujiandaa mume wake naye alikua tayari na alikua anataka waondoke wote. Alimsihi kuwa atamletea nyaraka zote lakini hakukubali, alimuambia ni lazima aende ofisini kwake na kuonana na bosi wake. Dorris alichanganyikiwa, alijua kuwa kama akienda ofisini kwake ni lazima atakutana na Dennis, ingawa walishaachana na kuoa mtu mwingine lakini ilikua inamuuma sana, alikua anawaza kuwa itamuumiza kama akijua kuwa alikua ni mke wa mtu muda wote alikua anamdanganya. Alimuomba mume wake asiende kazini kwakea lakini hakukubali.


Kila alivyokua akimbembeleza ndiyo kama alikua anachochea moto.


“Kuna nini unaficha, kwanini hutaki niende kazini kwako? Wewe si mke wangu? Unaogopa nini mimi kuja kazini kwako?”


“Hakuna ninachokificha lakini kuna haja gani ya wewe kwenda wakati kila kitu nakuleta hapa?” Alimuuliza, Harris hakumuelewa, alisisitiza, alienda ofisini kwao na mpaka kwa bosi wake, aliulizia kama mke wake kachukua mkopo. Mwanzo alikataa kumuambia lakini Dorris aliwaomba wamuambie kwani itakuja kuleta shida, walimuambia na kumuonyesha nyaraka zote. Kwa bahati nzuri siku hiyo Dennis alichelewa kuja kazini, alikuja mchana wakati Harris ashaondoka hivyo hawakukutana.


Dorris alishukuru Mungu kwani hofu yake kubwa ilikua ni kwa Dennis kuujua ukweli, alijua kuwa ni lazima ataumia na atyamchukia kwa kumdanganya kwani muda wote waliokua pamoja alijua kuwa Dennis anampenda tana sana na alikua tayari hata kumuoa. Alirudi nyumbani akijua labda mambo yameisha, labda mume wake kaelewa lakini haikua hivyo.


“Bado sina Imani na wewe, haiwezekani uchukue mkopo ununue gari, mimi nadhani itakua ni geresha, kumbuka na mimi nilishakua mfanyakazi, mtu anachukua mkopo ili kuficha madhambi yake.”


“Lakini mume wangu si umeshaona kila kitu, nikufiche nini tena?” Alimuuliza kwa sauti ya juu kidogo, ndiyo kwanza alikua katoka kazini, alikua kachoka na bado alikua na mawazo akiamini kuwa pamoja na Harris kutokua kazini lakini anaweza kuja kuambiwa.


“Unaona una kiburi, kwanini unanijibu kwa ukali!” Harris alikua amekaa kwenye kochi huku mke wake akiwa kasimama pembeni kidogo ya mlango kwani ndiyo alikua kaingia hata kukaa hajakaa.


“Nisamehe mume wangu nimekosea.” Alimjibu kwa unyenyekevu, ingawa hakuona kosa lake lakini hakua na namna zaidi ya kuomba msamaha.


“Mshenzi mkubwa wewe, ndiyo kawaida yenu, mkishakua na vipesa mnakua na viburi mnaanza kujibu watu kwa visauri. Mimi ndiyo mwamaume humu ndani kama ulikua hujui!” Alifoka huku akinyanyuka na kumfuata, mkononi alikua ameshikilia Galas ya maji.


Alitembea taratubu kama vile anaenda kumkumbatia mke wake, lakini alimfikia na kuchukua ile glasi ya maji, aliinyanyua kwa nguvu na kutaka kumpiga nayo kwneye jicho. Kwa bahati nzuri Dorris aliikwepa kwa kusogea pembeni kidogo, ikampiga na kumpasukia pembeni kidogo ya jicho.


“Nitakuua siku moja wewe mshenzi nifungwe!” Alipiga kelele, damu zilikua zinamtoka, Harris hakujali, alimvuta mpaka chumbani na kuanza kumpiga bila sababu yoyote. Alimpga sana huku akimtukana na kumuambia kuwa yeye ni Malaya hivyo amuambie nani kamnunulia gari.


“Wewe una majukumu mengi, kwa msahahara gani uweze kununua gari na kulipa ada ya watoto?” Aliongea huku akiendelea kumpiga, Dorris hakua na jibu jipya zaidi ya kurudiarudia kuwa alichukua mkopo.


“Gari inakuja lini?” Alimuuliza.


“”Wiki ijayo.”


“Umeandika jina la nani? Maana nataka kujua, kama ni yako kweli au unahongwa na mwanaume wako.”


“Nimeandika jinalangu mume wangu, gari ni yakwangu si ya mtu.” Aliendelea kujitetea, mume wake alishaacha kumpiga amekaa anamhoji.


“Sasa, kuanzia leo kila kitu nitafuatilia mimi, utaenda kubadilisha na kuandika majina yangu, mimi ndiyo mwanaume, huwezi kumiliki gari wakati mimi sina hata pikipikio!” Alifoka, Dorris alinyamaza kama vile hajamsikia.


“Umenisika, nataak gari iwe na jina langu!” Aliongea huku akimpiga kofi la usoni mpaka kumpa kizunguzungu.


MAPENZI! MAPENZI! NA MAPENZI TENA—SEHEMU YA NANE


(ILIPOISHIA SEHEMU YA SABA; Harris anajua kuwa mke wake aneagiza gari, anakasirika kwanini hakuambiwa mapema, anampiga mke wake wanaenda mpaka kazini kujua kama alikopa au la. Anakuta kweli alikopa lakini bado hamuamini, anaendelea kumpiga akitaka gari liandikwe jina lake, je Dorris atakubali gari iandikwe jina lake? Basi endelea, kama hukusoma sehemu ya Saba basi bonyeza hapa; https://www.instagram.com/iddimakengo/ )


Dorris hakua na namna, alikubali gari ikaandikwa jina la mume wake, kuanzia siku ile mume wake alifuatilia kila kitu yeye mwenyewe, mpaka gari inaingia hakujua kitu chochote. Alikua anajua kuendesha na alikua na leseni lakini mume wake hakumruhusu kuendesha. Asubuhi alikua akimpeleka kazini na jioni alimuambia apande daladala kwani alikua anasema yupo bize apande dalaala, hali ilikua hivyo, Harris akitumia gari kama yake na mke wake hakuwahi kuligusa, Dorris alizoea ila hali na kuanza kuona kama kawaida.


Kitu kilichokua kinamuumiza kichwa ni Dennis, alikua tayari ashajua kuwa kaolewa, mara ya kwanza mume wake alipoenda ofisini kwao hakuepo lakini alisikia maneno, alikuja kumuona tena mume wake wakati anampeleka kasini, aliulizia na kujua lakini hakumuuliza Dorris moja kwa moja kitu ambacho kilizidi kumuumiza, alitamani amuongeleshe, alitamani amuambie kitu hata kumtukana lakini haikua hivyo. Alimuacha tu kimya bila kusema chochote na kujifanya kama hakuna kitu kilichotokea.


“Kwanini huongei chochote?” Siku moja uzalendo ulimshinda, walikua kwenye gari, walikua wametoka nnje ya mji, ilikua ni safari ya kikazi lakini kutokana na uhaba wa magari ya ofisi na udharura wa lile jambo walitrumia gari binafsi la Dennis. Walikua wengi lakini baadahi wakati wa kurudi walishuka na wao kubaki wawili. Dennis alikua akimrudisha nyumbani, alikua kimya haongei chochote, walikua kama wanategeana hivi.


“Niongee nini?” Alimuuliza.


“Najua una hasiara na mimi, lakini ungeniuliza hata ni kwanini nilifanya hivyo?” Aliendelea kujiongelesha, Dennis alijua anachotaka kuongea lakini hakumpa nafasi, alikua anapotezea kwa kuchombeza vimaneno vya hapa na pale kuonyesha kama vile hajali.


“Naomba unisamehe, nipo kwenye ndoa ya mateso sana, yaani ni kama sina mume kabisa, nilipanga kumuacha mume wangu lakini sijui hata nifanye nini?” ananinyanyasa sana!” Alilalamika.


“Hayo ni mambo yako, huna haja ya kuniomba msamaha, wewe ni mke wa mtu na mimi nimepata mwanamke mwingine, nimeoa na nina furaha na maisha yangu, huna haja ya kujielezea kwangu.” Alionekana kutokujali lakini uso wake ulionyesha kabisa kuwa alikua kaumizwa na alikua analia kwa ndani.


“Hapana, najua umeumia, naomba unisamehe…” Dorris alilazimishia, alitaka kusikia anasemehewa lakini Dennis hakukubali kabisa kuwa ameumia.


“hayo ni ya kwako, mimi niko sawa na siwezi kuumizwa na mapenzi, nina maisha yangu, kama uliniumiza ilikua zamani, lakini kama ni msamaha unaotaka basi mimi niseme tu kuwa nimekusamehe, kuwa na amani.” Aliongea kwa mkato, bado alikua akimpenda Dorris na alikua anaumia, ni kweli aliumizwa alipojua kuwa alikua anatembea na mke wa mtu, aliumia zaidi kwani alimpenda sana na alishamtambulisha mpaka kwa ndugu zake, kibaya nikuwa Dorris alimuacha bila kumpa sababu,a kaumia mara mbili, kwanza kwa kuachwa na pili kwa kujua kuwa mwanamke aliyekua anampenda alikua ni mke wa mtu.


Pamoja na yote hayo hakutaka mazungumzo sana, alikua na mke na bado alikua anampenda Dorris alijua kama akimpa nafasi akaongea sana basi angemruhusu shetani akaingilia kati. Alimpeleka mpaka alipofikia karibu na nyumbani, Dorris alishuka sehemua mabyo alijua kuwa hawezi kuonenana na mume wake. Alirudi nyumbani akiwa amteua mzigo kidogo lakini si wote, alijua kabisa kuwa Dennis hajamsameha na abdo anaumia lakini angalau walikua wameongea kidogo na angalau kuna kitu kilikua imepungua moyoni.


****


Harris aliwahi kurudi nyumbani, haikua kawaida yake na wala hakua amelewa wala nini? Alirudi na kuongea na mke wake vizuri, ilikua ni saa nne usiku, mke wake alipomuona alienda kumuandalia chakula, yeye aliingia chumbani, baada ya muda alirudi kutoka na kukaa mezani kula. Dorris alishakula lakini alilazimika kula na mume wake kwani mara nyingi alikua akikataa kula nikipigo. Hakua anajua kuwa atawahi kurudi, alijua atachelewa mpaka kwenye saa tisa kama kawaida yake hivyo asingeweza kukaa njaa mpaka wakai huo.


“Mbona una dokoa dokoa? Au ulishakula kabla yangu?” Mume wake alimuuliza alipoona anakula kwa kutegeategea.


“Hapana, mbona nakula mume wangu.” Alijibu huku akichota vijiko vya harakaharaka. Ukimya kidogo ulitanda, harris hakujibu chochote ila aliendelea.


“Vipi kazini, huko kwenu mkoje? Kazi inaendelea vizuri?” Alimuuliza, lilikua ni swali ambali lilimshangaza sana kwani haikua kawaida yake kumuulizia mambo ya kazi.


“Iko vizuri tu, nashukuru Mungu.” Alijibu kwa mkato huku akila harakaharaka, mume wake hakuendelea kuuliza.


Ukimya ulitanda, harufu flani ilisikika, kuna kitu kilikua kama kinaungua na ilikua ikitokea chumbani.


“Kuna nini, mbona nasikia kama kuna kitu kinaungua?” Dorris aliuliza huku akitaka kunyanyuka, lakini mume wake alimuambia akae asiende popote, alikaa mpaka mume wake akamaliza kula, ilipita kama nusu saa hivi. Harufu ilikua kali sana, ndipo harris alimuambia anende chumbani kuangalia kama kuna tatizo gani, alinyanyuka kwenda na Harris alimfuata kwa nyuma. Ile kufungua mlango tu kuingia Harris alikuja na kumkanyaga kwa nyuma mgongoni, alidondokea kwa mbele huku akigonga kichwa sakafuni, kulikua na giza hivyo hata hakuona vizuri.


Mume wake alimkanyaga mgongoni kisha akaenda kuwasha taa, wakati alipoingia chumbani alikua amechomeka pasi kwenye umeme, iliku ishapata moto imekua nyekundu. Aliichomoa na kuishika vizuri, alimfuata mpaka alipokua pale chini kalala, alikua kalala kifudifudi, aliichukua ile pasi na kuanza kumchoma kwenye mapaja huku pembeni.


“Sitaki ushindwe kukaa! Nimekuona siku hizi una dharau sana, yaani imefikia hatua unamleta mpaka Malaya wako nyumbani kwangu? Alimchoma upande mmoja wa paja, kutokana na moto mkali nguo ilishikana na ngozi, maumivu aliyoyapata yalimfanya kupiga kelele za ajabu, watoto walishazoea kupigwa kwa Mama yao hivyo hawakunyanyuka kumsaidia pamoja na kusikia.


Alijitahidi kujinyanyua, wakati ananyanyuka pasi ilimdondokea tumboni, apamoja na kwamba haikikandamizwa sana lakini aliumia sana, nguo iligandana na tumbo. Alijitahidi kunyanyuka akafanikiwa kufungua mlango na kutoka nnje. Mwili mzima ulikua unamuuma, alikimbia mwenyewe mpaka Hospitalini kwa mguu, walikataa kumtibu kwa madai ya kuwa anahitaji PF3 kwani alionekana kupigwa. Hakua tayari kwenda hospitalini, alikua katika maumivu makali, aliazima simu na kumpigia Mama yake akimuambia kuwa kachoka naataka kurudi, alikua anaonge huku analia.


“Umemfanya nini mume wako? Mwanaume hawezi kukupiga kama hujamfanya chochote!?” Hilo ndiyo lilikua jibu la Mama yake.


“Utamleteaje mwanaume mwingine katika nyumba yake, hata kama wewe ndiyo nalipa kodi lakini yeye ndiyo mwanaume, hiyo nyumba ni yake.” Mama yake aliendelea kumsihi, alimuongelea maneno mengi mpaka akashindwa, alikata simu, alimuomba nesi mmoja kumfunga hata vile vidonda.


“Wewe ni mwanamke, mume wangu ndiyo kanifanyia hivi, lakini nikienda Polisi anaweza kuniua mimi na mtoto.” Aliongea huku akilia, yule dada alimuonea huruma, alimfunga vidonda vyote viwili.


Kidonda cha tumboni hakikua kikubwa sana bali kile cha kwenye paja, kilikua kikubwa kwani pasi ya moto ilikandamizwa kabisa tumboni. Alipewa huduma ya kwanza na kuondoka kurudi nyumbani, lakini alipofdika alimkuta tu binti wa kazi, alimuuliza alipokua mume wake na mtoto.


“Kaondoka na mtoto kasema yeye ndiyo anakutia kiburi hivyo hawezi kukuacha naye kama ni kukosa mkose wote.” Dorris nguvu zilimuishia, alijihisi kuchanganyikiwa kwani alikua hajui nini chaufanya, kwa hasira alizomuacha nazo mume wake alihisi labda anaweza kumfanyia kitu kibaya mtoto.


Najua unawaza hivi kweli haya yote yanatokea? Kuna mwanamke kweli anaweza kuvumilia vitu kama hivi? Jibu ni ndiyo. Rafiki yangu mmoja alikua anapigwa na kuchomwa na pasi mapajani, si mara moja wala mara mbili, ameshaachwa lakini bado anapenda, sasa hivi anahangika kwenye maombi kumrudisha mwanaume. Nilimuuliza kwanini akaniambia, ameshanizalisha watoto wawili siwezi kumuacha, najua sio akili zake kuna mwanamke kamloga ili asinipende mimi. Bado 


MAPENZI! MAPENZI! NA MAPENZI TENA—SEHEMU YA TISA


Dorris alichanmganyikiwa, alichukua simu ya na kumpigia mume wake lakini simu iliita tu bila kupokelewa. Harris alikua anampenda mtoto wake lakini alikua hamuamini kwani akiwa na hasira alikua akibadilika sana. Baada ya kuona kuwa hapokei simu zake aliamua kumpigia Mama mkwe wake, alimuambia kuwa mwanae kaondoka na mtoto na hapokei simu zake. Alimuuliza kuna nini kimetokea lakini hakua tayari kusema. Mama mkwe alimbana sana kumuambia lakini hakusema, aliishia tu kumuambia.


“Tumegombana Mama na sijui chakufanya, kaondoka na hasira kali…” Alimuambia, Mama mkwe alimuelewa na kukata simu.


Baada ya kama nusu saa hivi mume wake alimpigia simu, alikua kwenye sehemu yenye kelele.


“Unajiona mjanja, umetoka kuchepuka na Malaya wako unaona haitoshi na bado unaenda kunigombanisha na Mama yangu?  hukumbuki nilichokufanyia kipindi kile? Yaani unaniletea mwanaume mpaka nyumbani kwangu lakini bado unaona kama mimi ndiyo mwenye matatizo. Mwanaume mwenyewe ni mume wa mtu, kwa taarifa yako najua kila kitu, najua kuwa nafanya naye kazi na hii gari ndiyo kakuunulia!” Harris alitukana sana na kutishia kumuacha huku akisema kabisa kuwa lile gari atalichoma moto. Dorrios alimsihi kumrudisha mtoto lakini ndiyo kama alizidi kuchochea moto.


“Unaona, hata hunijali unaona mimi kama mjinga flani hivi, naongea na wewe uaanza kumtaja mtoto? Kwanza nina uhakika gani kuwa huyu mtoto si wangu? Na nakuambia, nilazima tukapime DNA na kama si wangu namwagia mafuta na kumpiga kiberiti…” Aliongea sana, kelele zilikua nyingi, alimtukana sana mke wake na kukata simu. Baada ya kuona mke wake kakimbia Harris alijua kuwa kamuumiza sana na anaweza kwenda polisi, bila kufikiria akijua kama anamkomoa alimchukua mtoto.


Lengo lake lilikua kutoroka na kuondoka naye, alikua anataka kumkomoa mke wake kwani alijua kuwa kitu pekee kilichobaki cha kumuumiza mke wake ni kumchukua mtoto. Lakini akiwa njiani kwenda kusikojulikana alipigiwa simu na Mariama ambaye alikua analia, alikua kagombana na mume wake amabye alurudi ghafla na kumfumania na mwanaume mwingine nyumbani kwake. Mume wake alikua kamfukuza nyumbani na alikua hana pakwenda. Walikubaliana kukutana baa ya jirani ili kama ni kuondoka waondoke wote.


“Mimi sitaki kukaa hapa kabisa, najua atakua kaenda polisi, natana niende sehemu ikipoapa basi nitaerudi.” Harris alimuambia Mariam baada ya kukutana.


“Naondoka na wewe, nataka kutuliza kichwa, si dhani kama mume wangu atanisamehe…” Alimuambia.


“Hakuna shida, ila sijajua naenda wapi? usiku huu siwezi kuendesha masafa, nadhani twende moro, tukalale hata chalinze…” Alimuambia na Mariam laikubaliana naye.


“Lakini huyu mtoto unampeleka wapi? huoni kama wakigudua umeondoka na mtoto ndiyo watapaniki na kuhisi umechanganyikiwa?” Mariama limuuliza, si kama alikua anajali kuhusu mtoto lakini aliona kabisa kama wataondoka na mtoto basi hawawezi kufaidi maisha.


“Najua lakini nataka kumkomoa yule mwanamke, hasikii, nimempiga sana lakini hasikii, kashakua sugu, najua kuwa nikimchukua huyu mtoto basi ataumia, tena sana!” Aliongea kwa hasira.


Walikua wamekaa Baa lakini bado walikua hawajaagiza, walipanga kuondoka bila kunywa, wakie wamekaa pale mhudumu alikuja na kuauliza kama wanakunywa nini.


“Hapana tunaondoka.” Harris alimjibu.


“Hapana, mimi lazima nipashe, nipe Mzinga mmoja wa konyagi na maji makubwa, nitabeba.” Walimpa pesa mhudumua na kwenda kuwaletea kama alivyokua kawaagiza. Alienda na kuleta, lakini Mariam aliamua kufungua na kunywa kidogo, Harris naye alichukua kidogo kuonja. Walikunywa na ndani ya dakika tatu walikua washamaliza mzinga mmoja wa konyagi, waliagiza mwingine na safari ilisimama kwa muda wakaanza kunywa na kulewa.


Wakiwa washalewa mke wake ndiyo alianza kupiga simua, alipiga sana lakini hakupokea. Ghafla aliona Mama yake anampigia, Pamoja na mambo yote lakinia likua akimpenda sana Mama yake, alikua akimheshimu na kumuogopa. Hukua kiyumbayumba alinyanyuka na kutoka nnje kabisa, aliingia kwenye gari na kufunga vioo ili sati ya mziki mkubwa na makelele ya baa isisikike. Alipokea na kumsalimia Mama yake kwa heshima, baada ya salamu Mama yake hakutaka hata kuuliza kama yuko wapi bali alimuulizia mjukuu wake.


“Niko naye Mama, nimetoka naye,” Alijitetea.


“Naomba kuongea naye.” Kalala Mama, niligombana na Mama yake, kuna mambo yalitokea, pale nyumbani si salama, mke wangui kaja na mwanaume mwingine mpaka ndani, mtoto ananisimulia hizi ni…” Alijaribu kuongea uongo lakini Mama yake alimkatisha.


“Sijazaliwa jana, mke wako namjua na wewe nakujua, namtaka mjukuu wangu kabla sijatoka ndani na kupanda gari nikaja kumtafuta, nitazungu Dar nzima kukutafuta ulipo. Mrudishe huyo mtoto kwa Mama yake, sitaki ujinga, na ukishamfikisha nipigie simu wewe!” Mama yake hakumpa nafasi ya kuongea ujingajinga, kweli Harris alikubali kumrudisha mtoto wake.


Lakini baada tu ya kumaliza kuongea alimblock Mama yake, alierudi ndani ndipo akanywa kidogo na kumpigia simu mke wake kumtukana na kumuambia kuwa hampati tena mtoto. Waliendelea kunywa mpaka wakalewa, wakati wote huo mtoto alikua kaka amelala kwenye kiti, pamoja na kelele zote lakini alikua kachoka sana. Kwenye saa nane usiku hivi ndiyo waliamua kuondoka, waliingia kwenye gari n a safari ya kwenda Morogoro ilianza huku wote wakiwa wamelewa chakari.


****


Dorris alikua kama mtu aliyechanganyikiwa, hakuweza kukaam baada ya kuongea na mume wake alimpigia tena Mama mkwe na kumuambia kila kitu. Mama mkwe alimtuliza na kumuambia kuwa mwanae alikua anamsikiliza hivyo alikua anamtania tu. Alimpa moyo na kumuambia alale yeye atamtafuta, lakini hakupata usingizi, alikaa mpaka saa tisa usiku alikua macho, alichukua simu yake na kuanza kumpigia mume wake. Aliipokea na kuanza kutukana, wakati huo walikua washaanza safari, Mariam alimnyang’anya simu na kuanza kumtukana matusi mengi lakini yeye hakujali alichotaka ni mtoto wake.


“Ongea na Mbwa wako na ndiyo humuoni tena!” Mariam alimjibu huku akinyanyuka kwenye kiti cha nyuma, alifungua mkanda na kugeka kwa nyuma, huku akitukana alimpa mtoto simu ili kuongea.


“Mamaaaa Nakufaaaa!” Ndiyo sauti ambayo Dorris aliisikia, baada ya hapo alisikia vitu vinagonga gonga na hakusikia tena kitu. Aliita na kuita lakini hakusikia kiti. Alikata simu na kupiga tena ila ilikua haipokelewi. Mariam alinyanyuka kutoka kwenye kiti, wakati anarudi kukae kwenye kiti alimgusa Harris ambaye alikua kashalewa hivyo kuguswa tu kidogo alikosa uelekeo, uskani ulimshinda na gari ilipoteza njia na kutoka barabarani, iliviriongika zaidi ya mara tano.


Mariam alifungua mkanda wakat anamgeukia mtoto hivyo alirushwa nnje na alifia palepale, mtoto naye hakufunga mkanda alirushwa mbali naye alifia palepale. Harris yeye alikua kafunga mkanda, pamoja na gari kuviringika lakini halikuharibika sana hivyo alitoka salama, lakini alivunjika kiuno hivyo hakuweza kutoka pale mpaka asubuhi wasamaria wema walivyokuja na kumchukua. Walikua hata hawajajfika mbali, ndiyo walikua wamepita Kimara wakielekea Moro.


Asubuhi simu ya Dorris iliita, ilikua ni Polisi, kupokea alishukuru Mungu kwani alijua kuwa mume wake alikua kakamatwa labda kafanya kitu flani huko ndiyo ameamua kumpigia.


“Mwanangu mko naye? Huyo mwanaume muacheni afie huko ninachotaka tu ni mwanangu, nieshamchoka na mambo yake.” Aliongea, Polisi walipojua kuwa ni mke wa Harris na mtoto waliyemuokota ni Mtoto wake walimuomba kuongea na mtu mwingine. Lakini hakukua na mtu mwingine, aliwalazimisha kumuambia ukweli lakini hawakusema, walisema wameokota simu tu walikua wanataka kuirudisha kwa mwenyewe.


Pamoja na kujaribu kumdanganya ili angalau watafute mtu mwingine wamuambie ilia kaongee naye lakini hawakuweza. Alihisi kitu na alipowabana sana ndipo kwanza walimuambia ataje anapoishi, ndipo walimuambia kuhusu ajali na kufariki kwa mwanae. Hata hawakumaliza kuongea alidondoka na kuzimia. Polisi walifuatilia mpaka kwake, wakamchukua na kumpeleka hospitalini.


Wakati wote huo Harris alikua kalazwa hospitali hajitambui kwani ile subirisubiri ya kupata msaada ilimfanya kupoteza nguvu nyingi. Kutokana napombe walishindwa kumpa dawa yoyote mpaka alipozinduka ndipo aliambiwa kilichotokea, hakuamini, alijaribu kunyanyuka ili kuenda kumuona mwanae lakini alikua hawezi. Alikua kumia nyonga, aliishia kulia tu hukua kijilaumu kwa hasira za kijinga. Mpaka mtoto wake anazikwa alikua kitandani, alikua kaumia hawezi kunyanyuka kwani kiuno kilivunjika kabisa, walitaka kumpeleka lakini mke wake ligoma kabisa.


Mpaka anatoka hospitalini Dorris hakuwenda hata kumuona, aligoma kumsamehe kabisa. Yeye mwenyewe maisha yake ni kama yalisimama, walilazimika kumpa likizo ya ugonjwa ya miezi sita pamoja na kuhamisha arusha ndipo alikua sawa na kwenda kufuatilia talaka, hakutaka kuonana na mume wake na wala hakutaka usuluhishi. Harris alilazimika kurudi kwa Mama yake ambaye alimhudumia kwani ndugu zake karibu wote walikua washamtenga hata kabla ya ajali.


Hata Mama yake alipofariki hakua na mtu wa kumsaidia, alivunija kiuno hivyo kuwa mtu wa kuzunguka na kiti cha magurudumu. Alijaribu sana kuomba kazi lakini alikosa, hakua nanamna aliamua kujiajiri kwa kufungua sehemu ya kusafisha viatu ambayo ndiyo hupatia kipato chake. Dorris maisha yaliendelea lakini alibaki na kovu, alikua anawaogopa sana wanaume, kila wakati akitaka kuanzisha mahusiano mapya alishindwa alijikuta akimkumbuka mwanae, mara mbili alijaribu kujiua lakini watu walimuokoa kibahati, alilazimika kurudi kwa Mama yake ili kuwa karibu na mtu anayemuelewa.


***MWISHO;

0 comments:

Post a Comment

BLOG