Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

VUMILIA KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA!

  

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

YAMENIKUTA; VUMILIA KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA!


“Mke wangu hawezi kunizalia tena mtoto, mimi nataka mtoto wakiume lakini yeye kanizalia mtoto mmoja tena wakike, hospitalini wanasema alikua na yai moja tu hivyo suala la kupata mtoto haliwezekani tena.” Aliniambia wakati ananishawishi nimzalie mtoto, bado nilikua na wasiwasi, nilishaumizwa sana, kipindi hicho nilikua na watoto wawili ambao nilizaa na wanaume tofauti, pamoja na kuwa na kazi nzuri lakini nilishajiapia kuwa mwanaume mwingine atakayenizalisha atakua ni mume wangu.


JOIN US ON TELEGRAM

Sikupanga kabisa kuzaa bila ndoa, hata wakati nakutana na Robert (Si jina lake halisi) nilimuambia, aliniambia ana mke wake hivyo hahitaji watoto. Lakini kadri siku zilivyokua zikienda ndivyo alianza kunipenda na kunifanyia  mambo ambayo hata mimi yalinishangaza. Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu wa mahusiano yetu alikua tayari ahsaninunulia nyumba tena kubwa tu kwa jina langu, alishaninunulia Gari na wanangu alikua akiwasomesha katika shule nzuri.


Alikua ananipenda sana na naweza kusema kama alichanganyikiwa juu yangu, hapo ndipo alianza kuongelea kuhusu kuzaa na mimi huku akiniambia kuwa ananipenda. “Siwezi kumuacha mke wangu kwakua tumetoka mbali na kama unvayojua ndoa ya kanisani kwangu ni ngumu sana, lakini wewe kwangu ni kama mke na nitakupa chochote kile ilimradi tu unizalie mtoto wa kiume. Nilifikiria sana nikashindwa, nilishindwa kabisa kufanya maamuzi, niliamua kwenda kuongea na Mama yangu ambaye ndiyo alikua mshauri mkuu.


“Wanaume wenyewe wako wapi siku hizi mwanangu, kama umepata mwanaume anataka kuzaa na wewe na kakupa kila kitu wewe zaa, muhimu amheshimu mke wake asijue kwani ndoa inauma.” Mama liniambia, kweli nilimbebea mimba na mungu alijaalia mtoto wa kiume, alifurahi sana na kuzidi kunipenda, baada aliniandika katika mali zake nyingi bila mkewe kujua, kipindi hicho penzi letu lilikua la siri, alikua anamheshimu sana mke wake na mimi nilimheshimu, sikua nikimpigia simu usiku wala kuonyesha dharau yeyote kwake.


Haukupita muda nilibeba mimba ya pili na kumzalia mtoto mwingine wakiume, alichanganyikiwa zaidi juu yangu na mimi nilianza kujiona kama mke. Nilijisikia vibaya kufichwa na nilitaka haki zangu, nilitaka anitambulishe kwa watu na mimi kuheshimika kama mke wake. Nilianza kumfuata ofisini na watoto, kwa namna walivyokua wamefanana kila mtu alijua, sikutaka kuwa tena wakificho, nilitaka kuwa mke, sikumoja bila kupanga nilimpigia simu mke wake, nadhani alishanijua, nilijitambulisha nikiamini kuwa atatukana sana.


Lakini hakufanya hivyo, aliongea na mimi kistaarabu, hakuniambia hata niachane na mume wake. Kuona vile nilipaniki zaidi na kuona kama vile anaigiza, nilimtukana na kumuambia yeye ni shetani, hana akili anakaa tu kusubiriwa kupewa, nilimtukana yule Mama matusi  mengi lakini hakujibu, nilizidi kupata hasira na kutukana zaidi, mwisho aliniambia nashukuru kisha akakata simu. Nilijua lazima atamuambia mume wake na kuja kuniuliza, nilijiopanga sana kuwaka na kumsingizia kuwa ndiyo kanianza.


Lakini hakumuambia chochote, wiki ailipita bila kuulizwa, hapo ndiyo kisirani kilizidi, nilianza kumuambia mwanaume awe analala kwangu, nilianza kumuambia anipeleke kwao na kuwatambulisha watoto kwa Mama yake. Alifuata kila kitu nilichomuambia, alinipeleka kwao na cha ajabu kila ndugu alinipenda, yeye ndiyo alikua na pesa kwao hivyo alikua na kauli ya mwisho, ndugu walimnyenyekea kama Mungu. Mama mkwe alifurahi kuletewa mtoto wakiume.


Baada ya kupelekwa kwao nilijiona mke kabisa, nilikua huru kwa kila kitu, nilianza kumpangia vitu vya kufanya, siku za kukaa na mke wake na pesa za kumhudumia mke wake. Mkewe alikua ni mama tu wa nyumbani hivyo nilijua hawezi kufanya kitu hata akifanyiwa nini? Mwanaume alihamia kwangu na nyumbani kwake alikua akirudi mara moja moja, nilifurahi sana kwani kwa mara ya kwanza nilijihisi kama nimeolewa, nina mwanaume wangu amabye ananipenda na kunijali kama mke wake.


Kitunpekee ambacho kilikua kikiniudhi kuhusu yeye nikuwa alikua hataki kumuacha mke wake. Kila nilipozungumzia suala la sisi kufunga ndoa hata ya serikali alikua akizugazuga na kusema nisubiri mambo yatakua mazuri. Kitendo kile kiliniumiza sana kwani niliona ni kama anampenda huyo mwanamke mwingine kuliko mimi, niliumia sana na kunifanya kukosa raha, pamoja na kupewa kila kitu nilichotaka lakini sikuwahi kuwa na amani, niliona bado yule mwanamke mwingine kama vile ni tatizo kwangu.


Wakati mmoja kipindi cha likizo mwamake alienda kwao, alienda kusalimia naa alienda na mtoto. Sijui kwanini, pamoja na kupewa nyumba yangu nzuri tu kuliko ile aliyokua akiishi yule mwanamke nilitaka anipeleke kule, alikataa nikawa nimenuna, akaamua kunipelaka ingawa sikulala, nilitaka tu wafanyakazi kuona na kumuambia ili kuzidi kumuumiza. Akiwa kule alikaa mpaka likizo ikaisha, alianza kumuomba mwanaume nauli ili kurudi kwani gari aliyokua akiitumia tulishamnyang’anya nikampa wifi yangu mmoja.


Kwakua nilikua nikisikia akiongea na simu pamoja na kusoma meseji zake nilimkataza kumpa nauli, nilimuambia anatakiwa kukaa kwanza kijijini ili sisi kufurahia maisha. Sikujua hata sababu ya kufanya hivyo, nilitaka tu aumie. Aliomba nauli sana, lakini mwanaume hakutuma alimiambia abaki ataenda kumchukua. Alikaa wiki akaanza kusema kuwa mtoto anaumwa na anahitaji pesa za hospitali, nilimuambia mwanaume kuwa hiyo ni janja janja anamtumia mtoto ili kumuendesha.


“Wanawake nawafahamu, hapo hakuna kitu cha kuumwa wala nini, mtoto mzima kabisa, anataka kukuendesha tu kwa kumtumia mtoto, ukiingia kwenye huo mtego shauri yako!” Nilimuambia, kwangu mimi niliona fursa ya yeye kubaki kwao kama fursa ya mimi kuolewa na yeye kuachika kabisa hivyo sikutaka arudi tena. Mwanaume hakutuma pesa, alikaa kwa siku tatu ndipo alikuja mjini, ndugu zake walimchangia nauli kwani kweli mtoto alikua anaumwa hali yake ilikua mbaya na hawakujua tatizo ni nini.


Aliletwa na kwenda moja kwa moja Muhimbili, kule waliambiwa anahitajika upasuaji kwani alikua na matatizo tumboni. Mwanaume alipigiwa simu na alipoambiwa yupo Muhimbili hata mimi niliogopa na kumuambia aende. Alipelekwa katika chumba cha upasuaji lakini hakutoka, alifariki dunia. Nilijilaumu sana kwnai nilijihisi kama nimehusika, lakini mwanaume alinipooza na kuniambia kuwa ni mipango ya Mungu hata sikuhusika. Siku ya msiba wifi yangu mmoja alikuja, aliniambia twende wote.


“Hakuna tena kipingamizi wewe ndiyo unaolewa, yule hana tena mtoto na hawezi tena kuzaa.” Aliniambia, sijui ni ujinga au ni shetani gani lakini nilivaa na kwenda kwenye msiba, tena nilikaa mbelembele, nilijisukuma mpaka kwenda kumpa pole. Aliniitikia tu vizuri kama watu wengine, hapo ndiyo nilijisikia vibaya na kujiona kama shetani, sikujua kwanini afanya yote hayo wakati dada wawatu hakunikosea chochote. Sikua na chakumuambia zaidi ya “Pole sana Kazi ya Mungu haina makosa.” Alinijibu kweli kisha akaendelea kusalimiana na watu wengine.


Baada ya msiba maisha yaliendelea, lakini mke wake aliamua kuondoka pale nyumbani, alitaka kurudi kwao kwanihakua na kazi, hakua na mtoto, alimuambia mume wake kuwa anataka kukaa mbali ili kumsahau mtoto wake. Kwakua alikua na mimi hakua na kipigamizi, aliponiambia nilijua kuwa ndiyo nimepata fursa ya kuolewa mimi, niliona ni nafasi yangu ya kumlazimisha mwanaume kutoa talaka. Sikua na haraka sana nilitaka nimpe angalau miezi sita ya kuomboleza ndiyo nianze kusumbua ili aachike.


Lakini haikufika, miezi minne tu baada ya kifo cha yule mtoto mwanangu wa kwanza alianza kuumwa, alikua shuleni amekaa darasani akaanza kutapika, akalalamika tumbotuombo, alipopelekwa hospitalini hata hakukaa alifariki dunia. Ilikua ni huzuni sana kwangu, nililia na kulia, nilichanganyikiwa. Nilizimia kila mara hata siku ya mazishi sikuweza kumzika mwanangu. Baada ya kama mwezi mmoja hivi ndiyo nilipata nafuu na kukubaliana na ukweli kuwa mwanangu hakua tena duniani.


Nikiwa nimeanza kukubaliana na ile hali siku moja nilipokea simu kutoka kwa namba amabyo sikuijua, nilipokea ilikua ni sauti ya kike, mhusika alinisalimia, sikuitambua vizuri lakinia lijitambulisha alikua ni mke wa Robert. Hasira zilinipanda na kutamani kuikata simu lakini niliona kumsikiliza kwania likuja kistaarabu.


“Pole sana, nimesikia umefiwa na mwanao, sikukupigia kukukudhihaki, najua mimi na wewe tunatofauti ztu lakini kama Mama ambaye nimepitia unayopitia basi najua kuwa nilazima kuziwe pembeni na kukupa pole…”


Alionge amaneno mengi kistaarabu sana, pamoja na ustaarbu wake lakini bado alinikasirisha, nilitamani kumjibu vibaya lakini sikua na nguvu hizo, nilichoshwa na msiba kuweza kumtukana. Aliongea sana lakini maneno aliyomalizia ndiyo yalinichanganya kichwa mpaka leo hii.


“Pole sana kazi ya Mungu haina makosa…” Aliongea akirudia kauli ambayo mimi nilimuambia kipindi alipofiwa na mwanae, hapo ndiyo nilitaka kukata simu kabisa kwani nilijua kabisa ananisanifu ila aliendelea.


“Najua unayopitia ni kitu ambacho sitamani kukipitia tena, najua siwezi kupitia tena kwakua sina mtoto mwingine na siwezi kuzaa, pole sana kwani wewe umebakiza watatu wakuzika na bado una kizazi…pole sana ni safari ngumu sana…”


Nilitaka kumuuliza alikua anamanisha nini lakini alikata simu na nilipojaribu kumpigia namba ilikua haipatikani tena. Niliwaza sana yale maneno hasa aliposema kuwa nina watatu wengine wakuzika, niliongea na mwanaume na kumuambia kila kitu lakini aliniambia nimpuuzie ana hasira tu. Kweli nilimpuuzia, nilinyamaza na maisha yaliendelea. Lakini baada ya kama miezi sita hivi nilipigiwa simu tena shuleni, mtoto wangu wa pili naye alianza kutapika kama yule mwingine.


Nilienda na kumwahi, alikua katika hali mbaya alikalamika tumbo, hakua amezidiwa sana hivyo nilimpakata kumpeleka hospitalini, lakini kabla ya kufika alianza kutapika na alifia mikononi mwangu. Sikuamini kilichokua kimetokea, wakati watu wakinishika kwani nguvu ziliniishia simu nyingine iliingia, sikuipokea mimi, alipokea mtu mwingine lakini nilisikia maneno mengine ambayo nayo yalinichanganya.


“Kadondoka? Tumbo?”


Unadhani ni nini tena kimetokea; Hiki kisa nilitaka kukiandika sehemu moja tu sema kimekua kirefu sana kitakua na sehemu mbili.  Mnaowaza kuhusu safari itaendelea kesho, nilishindwa kuiandika leo. Kutaka kujua nini kimetokea kwanini simu ya pili basi fuatilia Instagram @iddimakengo itaendelea jioni kwa watu wa Facebook ni kesho asubuhi.


YAMENIKUTA; VUMILIA KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA—SEHEMU YA PILI


Sikujua ni nini, tulienda hospitalini nikiwa sitaki kuamini kuwa mwanangu alishanitoka, niliwashinikiza madaktari kumpima tena kuwa kama yuko hai au la. Nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa hata sikulia tena nilitaka tu kumuona mwanangu akiwa hai. Nilikua namuamrisha kila mtu aliyekua karibu yangu, nilikua natukana na kutukana kila mtu nikiona kama hawafanyi vyakutosha kumhudumia mwanangu, suala la kumpoteza mwanangu sikuliruhusu kabisa.


Watu walinishika, nilichikuliwa na kulazimika kupigwa sindano ya usingizi, nilizindika baadaye na kumuona Robert kakaa pemebeni yangu, alikua kachoka, alionekana kutoka kulia na alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa.


“Alikuambiaje yule mwanamke?” Robert aliniuliza, alionekana kupaniki sana. Sikumuelwa swali lake, alirudia na kumtaja mke wake akiniambia nirudie maneno ambayo alimuambia.


“Huyu mwanamke ni mchawi kamuua na mwanangu!” Aliongea kwa hasira, hapo nilishruka kidogo kwani watoto wote wawili waliokua wamefariki hawkaua wa Robert, ni wale ambao niliza na wanaume wengine kabla ya kukutana naye.


“Unasema nini? Mbona sikuelewi!” Nilimuuliza huku nikinyanyuka kitandani, nilikua nimepaniki sana na nilitaka jibu. Hapo ndipo aligundua kuwa nilikua sijui chochote, alisita kuniambia lakini nilimshika na kumkaba nikimlazimisha kuniambia.


“Aron kadondoka kwenye meza, alikua anacheza tumbo likaanza kumuuma akawa anatapika akadondoka kwenye meza na kufariki dunia.” Aliniambia Aron (sio jina lake halisi) alikua ndiyo mtoto wetu wa kwanza mimi na Robert.


Pamoja na kupewa zile habari lakini sikuzimia, nilimshurumu mke wake kwa kila kitu, nililalamika na kumuambia kuwa kaniulia wanangu.


“Nilishakuambia kuwa huyu mwanamke ni mchewi, yeye ndyo kawaua wanangu, unamuangalia tu! Nasema ni cmhawi huyu mwanamke!” Nilipiga kelele huku nikimpiga Robert, alinishika na kunisihi kuwa ninyamaze, aliniambia anajua ni mchawi kweli lakini atamfundisha adabu. Niliumia sana kwa vifo vya wanangu, lakini tofauti na kifo cha kwanangu wakwanza hivi nilikua na nguvu. Kuna kitu ni kama kilikua kikiniambia kuwa wanangu bado wapo hai.


Nilishiriki mazishi yao, wakatio tunatoka makaburini nilimuona mke wwa Robert, bila aibu alihudhuria mazishi ya wanangu, nilitamani kupoga kelele na kumuambia mchawi lakini Robert aliniona, alinisogelea na kunikumbatia, aliniomba nisipige kelele, aliwaita watu wawili na kumuomba waende kumchukua mke wake na kumuondoa pale. Walimfuata na kutaka kumchukua, alitii na kuondoka, lakini sijui alirudi namna gani lakini usiku nikiwa chumbani tena katikati ya watu wakiwa wamenizunguka kunipa pole alikuja.


Alikua kajifunga mtandio vizuri na kujifunika, kwakua kulikua na giza watu hawkaumtambua. Alikuja mpaka nilipokua nimekaa na kunipa mkono, alinipa pole, kichwa changu kilikua katika mawazo mengi, hata mimi sikumtambua mpaka aliponiambia.


“Kazi ya Mungu haina makosa, najua uchungu unaoupata, lakini angalau hawa wamekufa kwa pamoja hutaumia mara mbili…” Niliisikia sauti yake ikipenya masikioni mwangu, nilitamani kupiga kelele lakini nilishindwa, mdomo haukunyanyuka.


Nilikaa kimya mpaka aliponyanyuka mwenyewe na kuondoka, hakurudi nyumbani kwao alirudi katika nyumba yake na aliwaambia watu kuwa karudi kwa mume wake kwani kashamaliza kuomboleza. Baada ya kama siku tatu hivi nilimuambia Robert kilichotokea, alikasirika sana na kwenda nyumbani kwake ili kumtoa yule mwanamke, alimpiga na kumuambia aondoke hamtaki katika nyumba yake. Alimtolea vitu vyake nnje na kutaka kumfukuza, lakini hakuondoka, alienda Polisi kumshitaki, alichukua RB na aliposhauriwa kuondoka alikataa katakata.


Robert alikatamwa na Polisi kwani mke wake alifungua kesi ya jinai kwa kumpiga, alishauriwa kwenda dawati la jinsia lakini alikataa na kusema hakuna kitu cha kusuluhisha alikua anataka kufungua kesi ya jinai. Alikaa ndani usiku mmoja, kwakua alikua na pesa basi alitoka, wakati huo mke wake bado alikua katika ile nyumba yake ya zamani, kipindi amefiwa na kuondoka an kuondoka kurudi kwao kuna wifi yangu alikua anakaa pale ila baada ya kurudi tena kila mtu alimkimbia na kubaki mwenyewe.


Robert ambaye alikua kama mume wangu alirudi nyumbani, sikulia kabisa, nilikua mkimya tu, watu wakinisemesha nawaangalia bila kuwajibu chochote, ingawa nilikua najua kila kitu kilichokua kinaendelea lakini nilikua kama zuzu. Nilikua na kila kitu katika maisha yangu lakini nilikua naogopa, kichwani nilikua natamani kupoteza kila kitu ili tu nirudishiwe watoto wangu.


“Rudi kwa mke wako?” Nilimuambia mume wangu baada ya kuingia chumbani, kulikua na watu wengi, alikuepo Mama yangu, Shangazi zangu na ndugu wengine.


Aliponiona kama nimepaniki mume wangu aliwaomba wale watu kutoka na kutaka kuongea na mimi, walitoka na kutuacha wawili.


“Mke wangu nani zaidi yako?” Alijiongelesha huku akitaka kunishika.


“Hapana, ushaniulia wanangu watatu, siwezi kuruhusu kuniulia na huyu mwingine, najuta kuingia kwenye mahusianao na wewe, najuata kukujua, najuta kujua mali zako!” Nililalamika sana nikipiga kelele, alijaribu kunishika na kunikumbatia lakini sikumruhusu,  nilikua katika maumivu makali sana.


Ghafla machozi yalianza kutoka, nililia kama mtoto, nilipoga kelele na kuwataja wanangu, alinikumbatia na kunishika kwanguvu, mimi nilimsukuma na kumuambia kuwa simtaki, sitaki kuwa naye, sitaki chochote kuhusi yeye. Alinisihi sana kutulia lakini sikujali, nilijua sababu ya yote hayo kutokea ilikua ni yeye. Nililia mpaka kuishiwa nguvu, nilipitiwa na usingizi, asubuhi na mapema niliamka nikiwa vizuri kabisa, nilikua niko sawa kiasi cha kushangaza watu.


Nilikunywa chai vizuri na kumuogesha mwanangu, nilimvalisha vizuri kisha na kumchukua nikambeba mpaka nnje, watu walikua wakinifuata kwani walihisi kitu kibaya, niliingia kwenye Bajaji na kuondoka, mume wangu aliwasha gari na kunifuata nyuma. Nilikua naelekea nyumbani kwake kwa zamani, alinifuata taratibu bila kunisimamisha mpaka nilipofika, niligonga mlango na nilifunmguliwa na mlinzi, nilimuuliza kama Mama yupo akanijibu ndiyo, nilimuomba aniitie.


Hakusita alienda kumuita, wakati huo mume wangu alishuka kwenye gari na kutaka kunishika, aliniambia nisijidhalilishe lakini sikumsikiliza, nilimuomba aniache nifanye yangu. aliniacha na wakati huo mke wake alikuja, kama kawaida yake kujifanya kuwa mwana sana alinikaribisha vizuri lakini sikutaka kukaa.


“Naomba unisamehe, najua nilikukosea sana kukuchukulia mume wako, naomba unisamehe, nimejifunza, mtoto aliyebaki ni huyu tu, naomba unionee huruma, mwanaume nimekuachia, simtaki tena, niachie mwanangu, wewe ni Mama unajua uchungu wa mwana, nisamehe….”


Nilipiga magoto huku nikimuomba msamaha, nililia sana na kuongea sana, watu walijaa nnje kwani si mume wangu pekee ambaye alinifuata nyuma, ndugu wengine walinifuata na walikua wakiangalia. Yule mwanamke hakuonekana kupaniki, alinishika mkono na kuninyanyua.


“Acha kumkufuru Mungu, mimi ni binadamu kama wewe, hutakiwi kunipigia magoti, kampigie Mungu wako na kama kuna kosa umemfanyia basia atakusamehe. Mimi hujawahi kunikosea, ulitembea na mume wangu lakini hukumbaka.


Si wewe uliyesaliti ndoa yangu ni mume wangu ndiyo maana hata siku moja sijawhai hata kukutukana kwakua wewe kama mwanamke binti mdogo kabisa ulitongozwa na kama mimi nilivyokubali basi na wewe ulikubali sasa kwanini niwe na chuko na wewe…”


Aliongea kistaarabu huku akinifuta machozi, kwa sekunde chache kidogo nilijihisi amani na kudhani kuwa labda kanisamehe lakini alimalizia.


“Huwezi kumrudisha mume wangu kwani hukuwahi kumchukua, wewe ulikua chombo chake cha starehe lakini si mke wake, kwenye mbingu takatifu mimi ndiyo nilikua mke wake hivyo huwezi kututenganisha.


Lakini sikuwahi kukuambia kuwa nina shida ya mwanaume, ndiyo maana hata ulipokua ukinipigia simu kunitukana sikuwahi kumdai, sihitaji mwanaume ili kuishi wala kuwa na furaha. Najua unaniomba msamaha kwakua unaamini mimi ndiyo nimewaua wanao, labda nikuulize kwani wewe ndiyo ulimuua mwanangu?”


“Hapana, mimi sikuhusika kwa chochote, ilikua ni kazi ya Mungu.” Nilijibu harakaharaka, aliniangalia na kunifuta tena machoazi yaliyokua yakinitiririka.


“Sasa kama unakubali kuwa kifo cha mwanangu ni kazi ya Mungu kwanini hutaki kukubali kazi hiyo hiyo ya Mungu kwa wanao. Kwanini unakuja kuniomba mimi msamaha kana kwamba mimi nahusika, au mimi ndiyo Mungu?” Aliniuliza kwa upole kabisa,a likua akiongea vizuri mpaka niliona kama kila mtu aliyekua akisikiliaza aligeuka upande wake.


“Hapana lakini….” Alinikatisha.


“Kama mimi sio Mungu basi sidhani kama nina chakukusaidia, sikuchukua wanao na wala siwezi kuzuia huyu kuchukuliwa.


Najua unaumia, nimepoteza mwanangu wa pekee, najua uchungu wa kuzika mtoto. Lakini nikuambie kitu mdogo wangu, bado hujaupata uchungu bado, ni uchungu sana kuzika mtoto lakini unapata uchungu zaidi pale unapozika mtoto huku ukijua kuwa huwezi kupata mwingine utaishi peke yako mpaka unakufa. Hapo hupati uchungu tena bali unakufa kabisa, mimi nishakufa hapa unaponiona hakuna kitu kingine cha kuniumiza tena, mwanangu katangulia na wewe bado umebakiza mmoja, siku ukipoteza hicho kizazi na kuzika huyu wa mwisho ndiyo utauona uchungu wenyewe.”


Alimaliza kuongea na kuingia ndani akafunga mlango, mume wangu alitamani kuingia kumvamia lakini watu walimshika. Niliondoka pale nikimuambia mume wangu kuwa narudi kwetu na siwezi kurudi tena kwake. Aliniomba msamaha na kunibembeleza lakini niliingia kwenye Bajaji na kurudi nyumbani ketu. Sikutaka kusikia chochote kuhusu yule mwanaume. Niliondoka na kurudi nyumbani, Mama alinibembeleza sana lakini sikua tayari kurudi kwa yule mwanaume, nilikua naogopa hata kupokea simu yake.


Baada ya kuona msimamo wangu mwanaume ambaye alikua akipiga simu kila siku ghafla alikata mawasiliano na kuacha kunitafuta, ndugu zangu nao walirudi nyumbani kasoro mdogo wangu wakike ambaye alikua chuo. Nilikua naishi naye kwenye nyumba ambayo nilijengewa na Robert,  alikaa huko akisingizia mambo ya chuo lakini mimi sikujali sana, akili yangu haikua pale kabisa, nilikua sina kazi namtegemea Mama ambaye naye hakua na kazi, akiba aliyokua nayo ni ile ya Robert pesa ambazo sikua nikizihitaji.


Hali ilikua ngumu kidogo kwani ndugu zangu wote ni kama walikua wananitegemea mimi. Miezi mitatu ilipita bila Robert kunitafuta, hali ya mwanangu ilikua nzuri na mimi nilikua naendelea vizuri. Siku moja mdogo wangu aliyekua akiishi na Robert alikuja nyumbani, alinisalimia vizuri na tuliongea mambo mengi, alitaka kuniambia mambo ya Robert lakini nilimuambia kuwa sitaki kwani nina amani.


“Wako kwenye talaaka, anataka kumpa mwanamke wake talakaa eti anataka kumuachia kila kitu!” Mdogo Lydia (si jina lake halisi) aliongea, alionekana kuwa na hasira sana akilazimishia mimi kimsikiliza.


“Amuachie, yule si mwanamke, hata mimi nimeacha kila kitu sitaki!”


“Mjinga kabisa, yaani mwanamke hakua na kazi anakaa tu nyumbani anataka kila kitu, haaa hapana! Hawezi kuchukua chochote, hivi unajua yule Baba ana pesa. Lakini kachanganyikiwa eti anataka kumpa na nyumba uliyokua ukiishi lakini mwanamke kakataa anasema hataki chochote, anataka talaka na nyumba waliyojenga wote basi!”


Mdogo wangu aliongea kwa hasira sana, ingawa niligoma kabisa kusikiliza lakini alinisimulia, alionekana kuumia kuliko hata huyo Robert, wakati anaongea kaka yangu wa Baba mkubwa aliingia, alinyamaza na wote tukamsalimia, tuliongea kidogo akituaga na wote tukamsindikiza. Nilijifanya kuchoka ili nisiongee na Lydia na kuchukua simu yangu, nikaingia chumbani ili kulala. Lydia kuona kuwa hakuna mtu wa kumsikiliza aliondoka.


Baada ya kama nusu saa hivi simu iliita, nilikua kitandani nimelala ndiyo natafuta usingizi, nilipokea bila kuangalia aliyekua anapiga, lakini nilisikia sauti ya mume wangu, niliganda kidogo bila kusema chochote, nikiwa nimeshikwa na butwaa nilisikia maneno ambayo yalinichanganya kichwa.


“Kwanini unakua na hasira hivyo, mimi pesa naweza kutafuta lakini ninachotaka ni kumuacha huyu mwanamke ili kuwa na amani, unaona alichomfanyia dada yako, sitaki kitutokee, nataka kuwa na watoto sasa kama atakua anawaua kila siku hata nikikuoa kutakua na haja gani ya ndoa…”


Mume wangu alijielezea mambo mengi lakini sikujibu chochote, nilikua kama nimepigwa ganzi, alijiongelesha sana akidhania anongea na mdogo wangu, alimbembeleza na kumuita maneno mengi ya kimapenzi lakini mwisho alizidi kuniumiza.


“Nataka mpaka unajifungua niwe nishampa talaka, sitaki  mambo ya dada yako kujirudia…”


Aisee unajua nilidhani nitamaliza hiki kisa leo, tukimalizieni kesho, lakini hivi unadhani kuna nini kati ya Lydia na Robert, mapenzi yao yalianza lini? Vipi unadhani ni nani anahusika na vifo vya watoto wa Robert, lakini kwanini mke wa Robert alikua ansherehekea? Mimi sijui endelea tuimalizie kesho maana. Ile kama una haraka sana basi hembu ingia kwenye ukurasa wangu wa INstagram @iddimakengo muendelezo ni le oleo weka na notification kabisa.


ITAENDELEA…


YAMENIKUTA; VUMILIA KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA—-SEHEMU YA TATU


Nilishindwa kuongea chochote, mwili ulikua ukitetemeka kwa hasira, nilikua nimepewa habari mbili kwa wakati mmoja, habari ya kwanza nikuwa mwanaume ambaye nilimuona kama mume wangu alikua akitembea na mdogo wangu wa damu, lakini pili nikuwa mwanaume huyo huyo alikua amempa ujauzito mwanaume niliyekua nikimuona kama mdogo wangu.


“Robert unatembea na mdogo wangu?” Nilijikuta nauliza bila kutarajia.


Ulitanda ukimya kidogo kama wa dakika mbili hivi kisha akanijibu.


“Ndiyo ukome kushikashika simu za watu pumbavu mkubwa wewe! si uliondoka ukajifanya una uchungu kwa kufiwa basi kajifungue!” Aliongea kwa hasira na kukata simu, nilizidi kuumia, mwili ulikua unanitetemeak, nilitoka nnje nikitembea kama mwenda wazimu, sikujua naenda wapi lakini nilikua nikiongea mwenyewe mwenyewe. Nilikutana na Mama ambaye alinisimamisha na kunikalisha chini.


Aliniuliza kilichokua kimetokea lakini nilishindwa kumuambia, nililazimika kumuambia kuwa nimekumbuka wanangu, bado nilikua sijawa na uhakika kuwa mdogo wangu anatembea na mwanaume wangu, sikutaka kumuingiza Mama kwenye hayo mambo. Nilinyamaza na kumuambia kuwa nimekumbuka wanangu basi, Mama alinituliza na kuniambia nikawaida, alinisomea risala ndefu, nilijifanya kumuelewa ili tu aniruhusu kuingia ndani kulala kwani sikutaka kuongea na mtu kwa wakati huo.


Nilitoka kuingia ndani, nilifika chumbani na kukaa kidogo, wazo lilinijia kuingia katika simu ya mdogo wangu na kuangalia kilichokua kikiendelea kati yao. Ilikua na passwed hivyo nilianza kubuni ikashindikana. Wakati nikihangaika pale kuifungua mdogo wangu alikuja, aliniona nimeshika simua yake.


“Samahani nimechanganya simu, zinafanana sana…” Alijisemesha huku akinikabidhi simu yangu na kunipa ya kwake. Nilimuangalia kwa hasira nikitamani hata kummeza. Hakujali alionekana kuwa na mawazo mengi kichwa chake kilikua mbali kabisa.


“Mwanaume wako amepiga!” Nilimuambia baada ya kuona kuwa anataka kuondoka kabla ya kuzungumza, ilionekana alikua bado hajaongea na Robert na kujua kuwa najua kila kitu.


“Mwanaume gani?” Aliniuliza kwa mshanagao, alionekana kama anataak kudadisi na kujua nilikua najua nini.


“Najua kila kitu, yaani wewe ndiyo wa kutembea na mume wangu…” nilianza kumsomea risala ndefu, alinisikiliza kwa maniki, alionekana kama vile ananielewa na maneno yangu yanamuingia lakini baadaye ndiyo nilichoka kabisa.


“Wewe ni mshenzi kabisa, unajua wewe ni mjinga? Hivi kila siku unasema mume wangu mume wangu alikuoa lini? Wewe ni Malaya kama mimi umechukua mume wa mtu umeshindiwa katikati mimi nakusaidia kumalizia!”


Aliongea hukua kinyanyuka, nilimshika na kumrudisha nikaanza kumtukana kuwa hana adabu hajiheshimu na mambo kibao.


“Acha kunitia shombo, hivi mimi na wewe nani hajiheshimu, angalau mimi nimemchukua tayari kahaharibu ndoa yake, wewe umemchukua  Baba wawatu ndoa yake inaamani, ukamtukana Mama wawatu na kumuulia mtoto wake leo unajifanya malaika, wote sisi ni wezi lakini wewe ni mwizi mjinga, umefiwa kidogo unakimbia hutaki mali, sasa kwa taarifa yako mimi naolewa, mali nachukua na mwanaume namuacha, nikishamzalia nina uhakika kila kitu cha kwangu.


Mke wake hana kizazi wewe ndiyo hivyo hata hujielewi angalau ushukuru hata nimekusaidia mali zimerudi kwa gamilia unakalia kupiga piga kelele hapa!” Alinisukuma chini akachukua simu yake na kuondoka, alipofika mlangoni wakati anatoka aliniambia.


“Unajishaua hutaki mali zake lakini kila kitu unachokula na huyo mwanao ni chakwake, au unafiiri Mama ana kazi gani ya maana kuweza kukuhudumia, pesa zote natoa mimi! Nahenyeka najiuza kwajaili ya familia halafu unajifanya mwema na mawaidha yako haya ya kijinga, nenda kwahubirie watu wako wa motoni mtakaochomwa nao!”


Aliondoka na kuniacha peke yangu, kisirani kilinipanda nikamfuata na kumkimbiza, kabla hajatoka sebuleni nilimshika na kumvuta kwa nyuma, alinigeukia na kunipiga kofi. Sikumshika kwa nia ya kumpiga lakini aliponipiga nililazimika kumrudishia, hapo ndiyo ulianza mkikimkiki, tulianza kumpigana huku kila mmoja akimtukana mwenzake, pale nyumbani alikuepo Mama tu, alitokea na kuanza kututenganisha, lakini hatukuachana, tulikua tukipigana huku kila mmoja akimtukana mwenzake.


Nilimtukana na kumuambia Malaya kaniibia mume wangu huku yeye akiniambia kuwa yule si mume wangu ni mwanaume tu nimezaa naye.


“Na kwataarifa yako hao watoito wako wote watakufa utabaki mwenyewe kama mchawi!” Aliongea kwa hasira, nilizidi kuumia na kuzidi kupandwa na hasira, akiwa hatarajii nilichukua kistuli kidogo cha kioo nikakiokota na kukinyanyua,  nilikirusha kutaka kumpiga lakini mama aliingilia kati, alijisogeza kumkingia nikajikuta nampiga Mama kichwani.


“Nakufa!” mama alipiga ukulele mmoja na kudondoka chini, damu vioo vilimpasukia usoni, damu zilikua zinamtoka, alikua akijirusharusha na ghafla alitulia.


“Umeaua! Umemuua Mama mshenzi mkubwa wewe!” Lydia alianza kupiga tena kelele, badala ya kumshughulika Mama alinigeukia na kunishika nywele na kuanza kunivuta, tulianza tena kupigana huku Mama akiwa kalala pale chini, tulipigaka kama dakika mbili hivi, nilimuona Mama akijisogeza nikajua kuwa bado yuko hai, nilimuambia Mama kajisogeza akaniachia tukamnyanyua na kumuingiza kwenye gari kwaajili ya kumpeleka hospitalini.


Tuliondoka bila hata kufunga milango, pale nyumbani hakukua na mtu, binti wa kazi alikua katoka na mtoto wangu. Hospitalini tuliwaambia kadondoka kwenye ngazi akadondokea meza ya kioo, walimuangalia mapigo ya moyo yalikua vizuri,. Alipatiwa huduma ya kwanza na kupumzishwa. Tuliamiwa kusubiri kwania likua kapotezafahamu ili kujua kuwa nini kinaendelea. Mdogo wangu alishatulia lakini alikua kapaniki sana, yeye na Mama walikua katibu sana,a likua analia, tulisahau yote na wote kuwa pamoja, alikuja na kunikumbatia akiniomba msamaha.


Bado nilikua na hasira lakini haikua mahali pake, Mama likua katika hali mabya nilipaswa kuwa dada mkubwa, niliwaza kupiga simu lakini nilikumbuka kuwa simu yangu niliacha chumbani.


“Wapigie akina Kaka simu…” Nilimuambia, alichukua simu yake kwenye begi na kutoa, aliifungua na kuanza kupiga, alikua akitetemeka naalishindwa hata kuongea, ilinibidi kumnyang’anya simu ili kuongea na Kaka, lakini simu ilishakata na nilipotaka kupiga tena ilishajifunga, nilimpa na kumuambia fungue.


Asijui kwanini lakini wakati anafungua kw amara ya pili nilijikuta nikichungulia na kupata passwed yake, alifungua bila kujua kama naangalia akanipa nikampigia simu kaka na ndugu wengine. Mama alikaa bila fahamu kwa zaidi ya masaa matatu, ndugu walikuja na kuuliza kilichotokea, jibu lilikua ni kadondoka, hakuna  aliyeamini, maswali yalikua mengi lakini si mimi wala mdogo wangu aliyeongea ukweli. Mara tuliitwa, Mama alizinduka na alikua vizuri kabisa tulimshukuru Mungu, wakati wakikumbatiana na kulialia nilichukua simu ya mdogo wangu nakutoka nayo nnje.


Nilitaka kujua kilichokua mule ndani, nilitaka kujua ni siku gani alikutana na kuanza mapenzi na mwanaume wangu. Nilifungua na kuja kugundua kuwa alianza mapenzi na Robert kipindi nina mtoto wangu wa kwanza, nakumbuka kipindi hicho alikua kamaliza kidato cha nne na alikuja nyumbani kunisaidia uzazi, kuna mambo mengi walikua wanakumbushiana kuhusu zamani.


“Wewe ndiyo mwanaume wangu wa kwanza, lakini naona bado unampenda dada, pamoja na yote ninayokufanyia hata nusu dada hakufanyii lakini bado unamkumbuka…”


Zilisomeka baadhi ya meseji. “Kwani kuzaa ni nini, kwanini uhangaike na mtu ambaye hakutaki, mbona na mimi naweza kubeba miba kila siku unasingizia huwezi kumuacha kwaajili ya watoto, watoto si wanakufa na kuzaliwa, wanaweza kufa wote na mimi nikakuzalia tukaanza familia…” Hii meseji ilinichanganya, haikua hii tu kuna messeji nyingi ambazo mzigo wangu alikua akizungumzia kufa tu na kuzungumzia waoto kana kwamba ni kitu cha kawaida.


“Nataka umuachje mke wako, mtoto ameshakufa ndoa ya kanisani inavunjwa mahakamani, hata kama dada hataki umuoe mimi nataka unioe…”


Ni meseji ambayo ilitumwa wiki mbili tu baada ya mtoto wa kwanza wa Robert aliyekua kazaa na mke wake kufariki. Robert alionekana kukasirishwa na meseji za namna hiyo na mara kadhaa alikua akimuonya kuhusu kauli zake.


“Mdomo unaumba, hao ni wanangu unaowazungumzia, nakupenda lakini unavyotaka sivyo, acha utoto ushakua mtu mzima, utanitibua…” zilikua ni meseji nyingi sana na zilichosha kusoma, Lydia alionekana kuwa na chuko sana na mimi pamoja na mke wa Robert, alionekana kuumia sana kuona sisi hasa mimi ninapendwa zaidi yake.


Hasira zilikua zinanipanda lakini nilijizuia, sijui kwanini lakini niliamua kuangalia na meseji nyingine. Zilikua za watu tifauti tofauti lakini kuna meseji mbili zilinishtua. Zilikua moja ilikua imeandikwa siku niliyofiwa na mtoto wangu wakwanza ambayo ilisema.


“Mbona hatukuelewana, mimi hao siwataki sio watoto wake hata wakifa haisaidii chochote, mbona unaniangusha nilichokua nataka ni watoto wake, wao ndiyo wanamfanya aendelee kuwa na dada, wakfa atamuacha tu!” Ilitumwa hiyo meseji lakini ilijibiwa kwa kifupi.


“Acha kuwa na pupa, usiwe na papara mambo hayaendi hivyo.”


Meseji ya pili amayo aliandika mdogo wangu, hii haikujibiwa iliandikwa.


“Ameondoka lakini bado mwanaume hanitaki, anaweweseka kuhusu mtoto wake, mimi nataka nimzalie lakini sitaki kugawana mali na mbwa wengine, huyo mtoto wake unamuacha wanini?” haikujibiwa, nilipitia meseji nyingine lakini hazikua na maana sana. Sijui nilipata wapi ujasiri lakini baada ya kumaliza nilitoka pale nilipokua nimejificha, niliizima ile simu na kuificha katikati ya nguo zangu za ndani, nilirudi na kumuaga Mama, nilimuambia kuwa nilikua sijisikii vizuri.


Mdogo wangu yeye bado alikua bize kuongea na Mama, kaka zangu walishatoka nnje, alikua bado hajashtuka kama nimechukua simu yake, niliondoka harakaharaka ili asinishtukizie, nilichukua bajaji na kuiwasha tena ile simu, nilipoiwahsa haikukaa dakika hata tano, iliita na alikua ni Robert, niliipokea na kumuambia ni mimi naomba kuonana naye kwani kuna kitu nataka kumuambia kuhusu watoto wetu, aliniulizia alipo Lydia nilimuambia kuwa yuko na Mama hospitalini kalazwa.


Alikata akuniona lakini nilimsisitizia na kumuambia kuwa mtoto wetu anaweza kufa kama tusipoonana, niliokena kupaniki akaniambia kama nataka kumuona nimfuate nyumbani kwake. Ingawa sikutaka kwenda lakini nilikua na hamu sana ya kumuona,. Nilitaka aone meseji za mdogo wangu na kujua mwanamke aliyakua akiishi naye. Nilifika na kumkuta ananisubri, yeye pia alikua kapaniki, alionekana kuwa na mawazo mengi, aliniuliza kuhusu Lydia, bila kumjibu nilijikuta napandwa na hasira na kuanza kumpiga makofi nikimtukana kwa kutembea na mdogo wangu.


Wakati nasimuliwa sikujua kama itakua ndefu namna hii, sehemu ya mwisho tukutane jioni katika ukurasa wangu wa Istagram @iddimakengo na  wala wa Facebook ni kesho saa tatu asubuhi @iddi makeng


ITAENDELEA…


YAMENIKUTA; VUMILIA KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA—-SEHEMU YA NNE


“Mnatumiana mameseji ya ajabu ajabu, mapicha ya ajabu ajabu, yaani watoto wako wanakufa lakini wewe hujali unahangaika na mwanamke ambaye amakuulia watoto!” Niliongea huku nikitoa simu ya Lydia, alianza kunishutumu kwanini niemshika simu yake na kwanini nasoma meseji zake.


“Nimekuambia kuwa huyu mwanamke wako ni mshenzi, kuna mesji ukiziona hapa utamuua! Nimechanganyikiwa, simu yake ina vitu vya ajabu hata siamini…”


Niliongea huku nikijaribu kuifungua ili kumuonyesha, sijui alikua anawaza nini lakini aliopoona nimeishikilia, labda akijua kuwa ina ushahidi wa meseji za yeye kutembea na mdogo wangu alinipokonya.


“Acha simu ya watu, ushahidi gani unataka wewe, mimi nishakuacha kwanini kutudhalilisha kwa watu, ndugu zako wananihesimu kuwa nawasaidia sitaki ujinga wako, wewe si mke wangu hivyo naweza kutembea na mwanamke yeyote yule.” Alinipokonya ile simu, nilimshika kutaka kumnyang’anya lakini tulianza kuigombania, hakutaka niishike tena.


Kuona nakaribia kumnyang’anya aliichukua ile simu na kuirusha kwa nnje, nnje ya geti kabisa, niligeuka na kutaka kutoka kwend akuiokota lakini alinishika kwa nguvu.


“Hizo meseji hazikuhusu, wewe hukuwa mke wangu huwezi kunipangia mwanamke wa kutembea naye, sitaki uitangaze!” Aliongea huku akinipiga makofi, ilikua ndiyo mara yake ya kwanza Robert kunipiga, alikua ananipenda sana. Nilijaribu kumuelezea sababu ya mimi kwenda pale kuwa sijali kuhusiana na meseji za mapenzi bali nawaza meseji nyingine.


“Lydia ndiyo kawaua watoto wetu na kuna meseji anachat anataka kuwaua wote, nimekuja kukuonyesha ili uone ushetani wake lakini wewe unakaa kuwaza mapenzi, sina shida na wewe nilikuacha mimi sikutaki na wala siwezi kuwa tena na mwanauem mshanzi kama wewe ulikua unatembea na mdogo wangu tangu mtoto mpaka sasa umemharibu kawa shetani!” Niliongea kwa hasira lakini hakuonekana kuelewa, aliacha kunipiga na kunisikiliza, nilimuelezea kuhusiana na meseji nilizoziona lakini hakuamini.


Alitoka nnje harakaharaka kuangalia simu ya mdogo wangu lakini hakuikuta, tuliitafuta sana na tulipoipiga ilikua inaita bila kupokelewa na baada ya muda ilizimwa. Hakukua tena na ushahidi hivyo hata nilivyombuambia hakuniamini, aliniambia niondoke kwani hataki maneno na mdogo wangu.


“Huo ni wivu tu unakusumbua, kubali kuwa umeshaachika basi, aliinga ndani wkake,a kafunga geti nakuniacha pale nnje, nilirudi hospitalini nilimkuta msogo wangu akihaha kutafuta simu yake, aliniuliza kama nimeiona nilimuambia hapana.


Alikua na wasiwawasi sana, sikutaka kuongea chochote kwani Mama alikua na hali mbaya na yote ni kwasababu ya sisi kugombana. Niliingia ndani kumsalimia Mama lakini nilimuona kama kanuna.


“Wewe una roho mbaya sana.” Mama aliniambia baada ya kuniona. Nilishindwa kuelewa anazungumzia nini, nilimuomba kupumzika kwanza lakini hakutaka.


“Ulitaka kumuua mdogo wako kwa mambo ya kijinga, kisa mwanaume unataka kumuua mdogo wako, hata kama unayoseam ni kweli yeye pia ni mwanamke katakwa, kwani huyo mwanaume alikua wako mpaka ukasirike?”


Mama alikua na jazba sana, alinishutumu kwa kila kitu na kuniambia kuwa natakiwa kumuomba msmaaha mdogo wangu kwa kumsingizia mambo kama hayo. Mama alijifanya hata hajui kilichokua kinaendelea.


“Mdogo wako  kabaki kukulindia mwanaume lakini unamdharau, hivi tungekula nini na huyo mwanao angekula wapi kama nayeye angekua mjinga kama wewe na kuondoka.” Alizidi kuongea, niliwaza kumuambia kila kitu lakini niliona kama haitasaidia, nilikua na hasira na kunyanyuka kuondoka.


“Unaondoka, unanicha naongea unaondoka, mimi ndiyo nakupa kila kitu unaondoka, sasa kama umeshakua unaweza kuondoka ondoka kabisa sitaki nikirudi kwangu nikuone.” Sukutaka hata kumjibu, nilinyanyuka zangu na kuondoka,pale nnje nilimuona mdogo wangu.


“Umechukua simu yangu, umapata ulichokua ukikitaka?” Aliniuliza kwa dharau.


“Najua ulichokifanya kwa wanangu lakini huyu wa mwisho hata akiumwa mafua tu nitasahau kuwa wewe ni ndugu yangu, nitakuchoma kama mishikaki!” Niliongea kwa hasira, alikua akijichekeshachekesha lakini nilimuangalia kwa hasira mpakakanyamaza.


“Mimi sijui unamaanisha nini?” Alijifanya kujitetea.


“Unajua, nimeona meseji ulizokua ukimtumia mtu wako, najua kila kitu ulichonifanyia mimi na mke wa Robert.” Nilimuona kabisa anaishiwa nguvu kidogo adondoke, nilimuacha pale na kuondoka zangu, nilirudi nyumbani na kumchukua mwanangu, nilichukua na vitu kidogo kisha nikaondoka, nilienda kwenye nyumba ya wageni kulala, sikutaka kuongea na mtu, sikua na ushahidi wowote hivyo hata kama ningeongea hakuna mtu ambaye angenielewa.


Siku iliyofuata nilienda Iringa kwa rafiki yangu, nilikaa huko nikijipanga na kuamua kuanzisha Biashara ya kuuza nguo za mtumba, nilitaka kuanza maisha yangu mimi kama mimi bila kuhusisha ndugu zangu wala kumhusisha Robert, sikutaka mawasiliano na mtu yeyote. Nilikaa mwaka mmoja bila kuwasiliana na mtu yeyote mpaka nilipopewa taarifa kuwa Mama yangu mzazi kafariki dunia, sikua na namna zaidi ya kwenda kumzika.


Hapo ndipo niligundua kuwa Lydia alikuja kuachana na Robert, baada ya kupata mimba na mimba kuwa kubwa ndugu zake Robert waliingilia, walikasirishwa na kile kitendo has abaada ya kuona kwamba alikua anataka kuchana na mke wake ili kumuoa mdogo wangu na kumpa mali zake zote, alishaanza kubadilisha majina ya mali hata kabla ya kumuoa hivyo kwakua nao walikua wakizitaka walianza kupambana naye kwa waganga mpaka kufanikiwa kumtoa, mdogo wangu alipoachika aliitoa ile mimba ikiwa tayari ishafikisha miezi nane na mtoto alishakua mkubwa kabisa.


Nilikutana naye kwenye mazishi ingawa hatukuongea, Robert alikua bado anasumbuana na mke wake mahakamani, baada ya kuachana na mdogo wangu hakutaka kumuacha mke wake, alimuomba sana msamaa lakini mwanamke hakua tayari, alikataa katakata kubaki naye na hakutaka chochote kutoka kwake zaidi ya talaka. Nilitamani kumtafuta ili kumuomba msamaha kwa kudhani kuwa yeye ndiyo kasbaabisha yote hayo lakini niliona haitasaidia.


Watoto walishafariki na mimi ndiyo nilikua sababu, niliamua kuendelea na maisha yangu lakini mpaka sasa bado maneno “Kazi ya Mungu haina makosa…” yananiumiza sana kichwa kila nikiyakumbuka maumivu yote yananirudia kichwani kwangu. bado ninaishi na mwanangu, Baba yake anajitahidi kutaka kuhudumia lakini situmii pesa yake, nimemfungulia tu akaunti namuwekea, maisha kwangu yamebadilika na moyo umekufa, nikisoma visa vyako hapa Kaka naona namna ambavyo kuna watu wanateseka nimeona niandike na mimi kisa changu labda na mimi maumivu yatapungua, nashukuru sana kwa muda wako Kaka Iddi.


****MWISHO


0 comments:

Post a Comment

BLOG