Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

MWANANGU SITAKI UWE KAMA MIMI MAMA YAKO

  

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

AMINA; MWANANGU SITAKI UWE KAMA MIMI MAMA YAKO—SEHEMU YA KWANZA


Nilinyanyuka Kitandani nikiwa sijitambui vizuri, nilikua nikiwaangalia watu kama wagani wageni hivi. Mama yangu alikua kaaa pembeni yangu. “Wewe si utoke nnje, kwanini unalia mbele ta mtoto?” Baba yangu alifoka. “Wewe ndiyo umemfanya hivi mtoto mpaka hamsikilizi mume wake, wanawake ni wajinga sana, unaona sasa umemsababishia Baba wa watu matatizo mpaka sasa yuko jela!” Baba alifoka, bado nilikua sijajua ni kitu gani kilikua kimetokea, bado nilikua na mshituko mkubwa.


JOIN US ON TELEGRAM

“Akafie mbeli, unaona kitu alichomfanya mwanetu, hivi wewe Baba Amina (Sio jina Lake Halisi) inamaana huna uchungu kabisa na mwanao?” Mama aliongea kwa uchungu sana, nilimuona Baba akimsogelea, alichukua mkono wake wakulia, akaupeleka shingoni kwa Mama, hapa kwa nyuma chini kidogo ya kisogo. Ni kama mtu alikua anamshikashika tu lakini alimbonyeza kwa nguvu mpaka Mama akaanza kupiga kelele. “Nakufaaaa!” Mama alipiga ukulele huku akinyanyuka kutoka kitandani, wagonjwa wengine walishtuka na kugeuka kuangalia.


“Unanikosea adabu, nimeshakuambia kuwa usiwe unanijibu jibu, au unafikiri kuwa siwezi kukupiga kwakua tuko mbele za watu. Nitakuua na kama ni kufungwa nikafungwe mshenzi mkubwa wewe!” Baba alifoka huku akimuachia Mama, alitoka pale hospitalini na sikumuona mpaka niliporuhusiwa kutoka hospitalini wiki mbili baadaye. Nilirudi nyumbani nikiongozana na Mama, nilipofika tu, ile kutaka kuingia Baba alikua mlangoni.


“Unaenda wapi?” Aliniuliza, nilinyamaza kimya nikimuangalia Mama anisaidie kujibu, lakini hata yeye alionekana kuogopa, akanyamaza kimya.


“Wewe si ulishatolewa mahari? Unataka nini hapa? Mume wako alikuja kukuchukua kwangu, kama hajakuchoka, kama hajakurudisha basi siwezi kukupokea!” Aliendelea kufoka, Mama aliniangalia, macho yake ni kama yalikua yananimbia “Ondoka mwanangu, sina chakukusidia.” Bado nilikua sijapona vizuri, nilriruhusiwa kutoka hospitalini kwakua nilipata nafuu kidogo na Mama hakua na pesa nyingine ya kulipia kuendelea kulazwa hospitalini. Mume wangu ndiyo kabisa alikua hataki kabisa kunisikia.


Bado alikua ananilaumu kwa kumsababishia kuwekwa mahabusu kwa wiki mbili baada ya kunipiga. Ingawa si mimi nilienda kumshitaki lakini alikua akilalamika kuwa kama nisingepiga kelele wakati ananipiga basi asingekamatwa na kuwekwa ndani. Haikua mara yake ya kwanza kunipiga, mara zote wakati akinipiga nilikua nanyamaza kimya, alikua akikasirika sana kama nikipiga kelele akisema kuwa ninachonganisha na watoto hivyo hataki kabisa nipige kelele.


Lakini siku hiyo ilikua tofauti, nakumbuka nilikua sebuleni, mume wangu alikua anaangalia mpira. Wakati anaangalia umeme ulikatika, alianza kuwalaumu TANESCO kwani mume wangu anapenda sana mpira. Lakini mtoto wangu mdogo aliropoka.


“Luku itakua imesha, mbona kwakina Kelvin (sio jina halisi) unawake…” Mume wangu alinyanyuka taratibu, aliwasha simu yake ya tochi na kuniita chumbani, nilienda nikikimbia, mpaka wakati naingia sikujua kama ninakosa na wala sikujua kama naenda kupigwa kwani mume wangu siku hiyo alikua katika mood nzuri.


Lakini ile naingia mlangoni nilisikia “Paaa!” umeshawahi kufungua mlango nusu, halafu ukaufunga kwa nguvu, basi ndiyo kilichotokea, mume wangu alikua kasimama nyuma ya mlango, aliufungua nusu na nilipoingia aliubamiza kama vile anaufunga, haukufungika bali mlango ulinipiga usoni, pua mdomo vilianza kutoa damu.


“Nakufaaa!” Nilipiga kelele.


“Unakufa! Hivi wewe ni mwanamke wa namna gani? Una kazi gani nyingine unanya hapa nyumbani! Yaani mimi narudi nyumbani, nataka nikae na familia yangu, lakini nawasha TV, umeme umekatika, najua ni TANESCO nalaumu serikali kumbe ni wewe mshenzi umeshindwa kuniambia kuwa umeme umeisha nikanunua umeme!” Alifoka kwa nguvu, mpaka wakati huo ndiyo nilikua nimetambua kosa langu, sikua na kitu kingine zaidi ya kuomba msamaha.


Nililazimika kunyamaza kimya bila kuseama chochote, maumivu niliyokua nayo yalikua hayaelezeki, lakini nilijua kuwa, kama nikiongea, kama nikilia, kama nikipiga kelele basi mume wangu angeniua. Mume wangu ni mtu wa hasira sana na nilijua kabisa kuwa hawezi kuniacha kama nikipiga kelele.


“Nisamehe mume wangu nilipitiwa…” NIlijitahidi kuongea huku nikizuia sauti yangu isilete mikwaruzo ya maumivu.


“Ulipitiwa? Ulikua unafanya nini tangu asubuhi ukashindwa hata kuangalia kuwa umeme umeisha?” Aliniuliza, nilikua na mengi ambayo nilikua nayafanya na ningeweza kumjibu lakini nilijua fika kuwa mume wangu hahitaji hayo majibu, alichokua anataka yeye ni mimi kumuambia umeme umeisha, anunue basi, hayo mengine hayamhudu.


“Hapana mume wangu, nisamehe, sitarudia tena…” NIlijitetea, alinyanyua kitocho chake cha simu na kunipiga usoni.


“Kwahiyo umepasuka pua ili nionekane nakupiga? Unataka watu kuniona mimi mbaya eeeh! Unataka utoke hivyo watoto waone nakupiga wanichukie mimi Baba yao?” Alifoka.


“Hapana mume wangu, nisamehe…”


“Kila siku wewe ni kuomba msamaha, hivi kwanini huna akili, hivi kwanini nimeoa mwanamke mpumbavu namna hii? Hivi unafikiri ningeoa mwanamke ana akili si ningekua mbali, wafanyakazi wenzangu waliooa wanawake wa maana sasa hivi wana maisha mazuri lakini wewe ni sifuri kabisa!”


Aliendelea kufoka, nilinyamaza kimya nikimsikiliza, kwakawaida akiongea huwa hataki kukatishwa.


“Unaombaomba misamaha kila siku, mimi naona bora tuachane, nikurudishe kwenu ukaendelee na umasikini wenu, maana nimechoka, kubeba mwanamke ambaye hana akili ni upumbavu!” Aliendelea kuongea, pamoja na kwamba hasira zilinipanda, pamoja na kuwa katika maumivu makali lakini sikuweza kuongea chochote.


“Nimekusamehe kwakua ni kosa langu mimi kuoa mpumbavu, wakati wenzangu wanaoa wake mimi nikaoa taahira.” Nilishukuru Mungu, niliendelea kubaki pale nikisubiri maelekezo mengine,


“Unaweza kununua umeme kwenye M-Pesa?” Aliniuliza.


“Ndiiyo naweza, nilijibu harakaharaka, alinipa simu yake na kuniambia ninunue umeme, niliichukua na kununua umeme. Yeye alitoka na kurudi sebuleni, kama dakika kumi baadaye alirudi.


“Ushanunua?” Aliniuliza.


“Ndiyo lakini bado hawajanirudishia meseji.” NIlimjibu huku nikimkabidhi simu yake, aliichukua na kuangalia salio.


“Wamekata lakini…”


“Ndiyo labda itakua ni network.” Nilimjibu, alirudi sebuleni, alikaa tena kwa kama dakika ishirini na kurudi tena kuniulizia.


“Simu si uko nayo wewe mume wangu, mimi sijui kama wamesha tu….” Sikuweza kumalizia, nilikua nimekaa kitandani nilishangaa mtu amenikanyaga tumboni. Kabla hata sijajipanga kuwaza naumia vipi nilisikia ngumi ya sikiko la kushoto. Nilikua nimekaa lakini nilipatwa na kizunguzungu, kilichofuata hapo ni kipigo cha Mbwa Koko! Wakati wote huo mume wangu alikua akinipiga huku akilalamika kuwa nimenunua umeme vibaya mimi halafu nampiga hovyo. Sikujua ni wakati gani nilipiga kelele, sikujua nini kilitokea, lakini nilikuja kuzindika wiki moja baadaye nikiwa hospitalini.


Mume wangu alikua kakamatwa na Polisi, sijui ni nani aliita watu lakini Polisi walijua kuwa nitakufa ndiyo maana hawakutaka kumuachia, pamoja na kuhonga, pamoja na mume wangu kujuana sana na Polisi kwani yeye ni mwanajeshi na ana cheo kikubwa tu lakini waligoma kumuachia wakijua kuwa ni kesi ya mauaji. Baada ya mimi kuzinduka ndipo walimtoa kwani ilikua si kesi ya mauaji tena bali ikabadilika na kuwa kesi ya kumpiga mke. Pamoja na Baba kujua yote hayo lakini bado alitaka nirudi kwa mume wangu.


“Baba Amina, mruhusu basi mtoto angalau alale kwa leo, hali yake bado haijatengamaa…” Mama alijitahidi kuongea, nilimuona jinsi alivyokua anaumia, namna alivyokua akilengwalengwa na machozi. Nilijihisi vibaya kwani nilijua lazima Baba atakataa na angeweza kumpiga Mama kwa hilo.


“Hapana, Mama, niko sawa, hali yangu ni nzuri, niache nirudi kwa mume wangu, nimewamiss wanangu.” Niliongea kwa shida sana, bado mwili wangu ulikua katika maumivu makali, hata kupumua ilikua shida sana achilia mbali kuongea.


“Unaona, mtoto mwenyewe anasema kapona lakini wewe kiherehere chako ndiyo unaingilia ndoa za watu wakati yakwako imekushinda, muache arudi kwake, kama mume wake kamchoka atamrudisha!” Baba aliongea, safari ya kurudi nyumbani ilianza. Mama alitaka kunisindikiza lakini Baba alikataa, alimuambia ana njaa.


“Yaani wiki ngapi hizi uko hospitalini unamuuguza mwanao, namimi nataka kuhudumiwa au unafikiri nilikuoa ili nije kujipikia mwenyewe. Huyo anapajua kwake, muache aende, hatakiwi kupelekwa.” Mama aliingia ndani, mimi nilijikusanya kusanya na kuondoka kurudi nyumbani kwangu.


Ilikua ni siku ya kazi hivyo nilijua kuwa wanangu watakua shuleni na mume wangu naye atakua kazini. Nilifika na kukuta milango iko wazi, nilijua kuwa nitakunana na binti wa kazi, niliingia getini, nikaenda mpaka ndani, niligonga kwa uoga nikijua kuwa kama kwa bahati mbaya mume wangu akiwa njiani nikiingia bila kugonga ningekutana na kipigo.


“Unataka nini wewe Mwanamke, hivi kwanini hukubali kuwa hupendwi, mwanaume anakupiga kutaka kukuua lakini bado upo tu?” Mlango ulifungulia, hakuja binti wa kazi au mume wangu bali alikua ni Sakina (sio jina lake halisi).


Ni mchepuka wa mume wangu wa muda mrefu, mara nyingi nilikua nikimfumania na mume wangu naishia kupigwa, nilishakuta mesji nyingi akimtumia mume wangu, picha zake nyingi za uchi na nikiuliza naishia kupigwa. Nilishangaa anafanya nini pale, tena akiwa kava shati la mume wangu na chini hamna kitu, yaani ni kama alikua uchi tu. Alionekana kama anaishi pale, nilishangaa kwakua Sakina alikua ni mke wa mtu, tena mke wa mmoja wa marafiki wa mume wangu, nilishangaa nikiwaza kama ndiyo kaachika na mume wangu kamuoa au?


Amina anarudi kwake baada ya kipigo cha nguvu kutoka kwa mume wake, bado hajapona vizuri anakutana na mwanamke mwingine nyumbani kweke. Mimi sisemi, ila muambie kuwa kuna 


JctuS6l6pfyl 1a3n7,s83or 20ud14f91  · 


AMINA; MWANANGU SITAKI UWE KAMA MIMI MAMA YAKO—SEHEMU YA PILI


(ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA; Amina anapigwa na mume wake mpaka kupelekea kulazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki mbili akiwa hajitambui, kosa lake kubwa ni kutokumuambia mume wake kuwa umeme umeisha. Anakaa hospitalini huku mume wake akikamatwa na polisi na kuachiwa, anatoka na kurudi nyumbani kwao akiwa na Mama yake, lakini Baba yake anamfukuza na kumuambia arudi kwa mume wake, anarudi na kukutana na Sakina ambaye ni mchepuko wa mume wake akiwa nyumbani kwake na Khanga moja tu! Je nini kitatokea? Basi endelea….)


Nilikua nikitetemeka kwa hasira, sijui kwanini lakini ghafla nilianza kujisikia vibaya, nilishikwa na kizunguzungu na kabla ya chochote nilidondoka chini tena. Sikupoteza fahamu lakini niliishiwa na nguvu kabisa, Sakina kuona vile aliogopa, aliingia ndani na kuvaa nguo, alitoka nnje akiwa na begi lake.


“Njoo, mtu wako yoko hapa sitaki kesi ya kuua mimi!” Nilijua anaongea na mume wangu, aliniruka na kuondoka zake. Nilikaa pale chini kwa nusu saa bila kunyanyuka, nilikua na fahamu naweza kusikia kila kitu lakini sikuweza hata kusogeza kidole.


Mume wangu alikuja na kunikuta katika hali ile.


“Umekuja kufanya nini hapa? Hivi unajua kuwa utaniletea majanga, wewe si ulisema kuwa nimekupiga, kwahiyo umekuja kujidondosha hapa ili nionekane kuwa nimekuua kabisa?” Aliniuliza, kusema kweli sikuweza kujibu, nilibaki tu napepesa macho. Mume wangu hakunigusa, alitoka nnje na kuita watu, baada ya dakika mbili hivi watu walikuja, mmoja wapo alikua ni mjumbe.


“Mnaona, kadondoka mwenyewe, mimi sikumgusa, hata akifa mimi sihusiki, sijui hata amefuata nini kwangu?” Mume wangu aliongea, sauti yake ilionyesha kuwa kuna kitu alikua akikiogopa.


Mjumbe aliniinamia na kuanza kuniuliza kama kuna kitu gani kimenipata, sikuweza kuongea.


“Mimi sijamgusa, nimemkuta hapa kadondoka mwenyewe! Nimeingia hata sikumgusa nikaona kuwaita, sitaki mambo ya kusumbuana na polisi!” Mume wangu aliendelea kulalamika, walinichukua na kunipakia kwenye gari langu ambalo mume wangu alikua akilitumia kisha kunipeleka hospitalini, kule walisema ni mshiruko nitakua vizuri tu.


Kweli baada kama ya masaa mawili hali yangu ilirudi na kuwa sawa. Niliruhusiwa kuondoka huku nikishauriwa kupunguza stress na kujiweka mbali kabisa na mambo ambayo yanaweza kuniletea mawazo. Nilikua na wa Mama wawili ambao wote walikua ni majirani zangu. Wal;inichukua mpaka nyumbani kwani mume wangu alishaondoka hakuja hata hospitalini akilalamika kuwa nilimshiataki Polisi hivyo simhusu. Tulirudi mpaka nyumbani, lakini kufika mume wangu alinikataa, alisema kuwa hawezi kuishi na mimi kwani kama kitu kibaya kikinitokea basi hataki kuhusishwa.


Alimpigia Mama yangu simu kuwa haniaki, akampigia na Baba yangu simu kuwa hanitaki. Baba alikua mkali sana na nilihisi kama waligomba na kwenye simu.


“Muje kumchukua motto wenu mimi simtaki, kama hamji mimi namleta!” Nilimsikia mume wangu akifoka, nilishangaa ni kwanamna gania ligombana na Baba wakati yeye ndiyo alikua kipenzi chake, mume wangu na Baba yangu walikua marafiki sana, Baba alikua anampenda na siku zote nikillaamikia tatizo lolote mimi ndiyo nilikua nikionekana kama nina matatizo.


Usiku Baba alikuja, nilijua kama atakuja na Mama lakini hakufanya hivyo, alikuja peke yake, baada ya salamu alitoka na mume wangu, walikaa kama masaa matatu, waliporudi wote walikua wamelewa.


“Muombe msamaha mume wako, mimi nimekuombea lakini kiheshima kwa yote uliyomfanyia unatakiwa kumpigia magoti na kumuomba msamaha!” Baba aliongea, nilikua nimekaa kwenye kochi, kw amacho, bila hata kuongea chochote Baba alikua kama ananilazimisha, nililazimika kupiga magoti na kuomba msamaha.


Sikujua naomba msamaha kuhusu nini lakini Baba alisisitiza.


“Tusamehe mwanangu, unajua hawa mabinti wanaolelewa na Mama zao hawajui hata ndoa ni nini!” Baba aliongea, mwili bado ulikua unauma, kichwa nilikua na mawenge mawenge. Kusema kweli nilikua sijielewi, nilimuomba msamaha mume wangu, mwanzo alijifanya kukaaa akionyesha kuumizwa sijui na kitu gani, lakini baada ya mdua alininyanyua na kuniambia kuwa kanisamehe.


“Leta chakula sasa…” Aliniambia, nilibaki nimeduwaa kwani nilikua bado sijapika.


“Sijisikii vizuri mume wangu, mimi bado sijapika…” Nilisema, lakini kabla sijamaliza Baba alinizaba makofi.


“Hayo si majibu ya kumpa mume wako, hujapika unataka mume wako akale wapi? Hivi akiwa na mwanamke mwingine bado utalalamika?” Baba alifoka, alijifanya kuwa na hasira kuliko hata mume wangu, kwa kuchelewa kupika nilijua ni lazima mume wangu angenipiga sana nusu kifo, kwa kuacha kupika kabisa niliamini kuwa ataniua. Lakini siku hiyo alikua tofauti, alijifanya kuwa ana upendo, akamtuliza Baba na kumuambia kuwa asijali kwani tutaenda kula mtaani. Baba ni kama hakukubali, hakutaka kula mtaani, alinilazimisha kuwa niende kumpikia mume wangu ndiyo adabu.


Sikua na namna zaidi ya kuingia jikoni, lakini jikoni hakukua na kitu chochote, vyombo vilikua vichafu nusu kuoza, nyumba ilikua na vumbi, hakukua na kitu chochote cha kupika, kwenye friji nako kulikua hakuna kitu. Giza lilishaingia ilikua ni kama saa nne hivi za usiku nisingeweza kutoka na kwenda sehemu yoyote kununua kitu chakupika. Nilikaa jikoni kwa zaidi ya nusu saa, nilikua nimekaa tu, mimi mwenyewe nilikua najaa sana, mwili umechoka, nilikua nalia lakini hata machozi yalikua hayatoki.


“Balaa gani hili jamani, nikirudi wale wanaume wataniua.” Niliwaza, bado walikua sebuleni, mume wangu alikua akiongea kwa suti, akimsifia Baba yangu kwa ujasiri wake wakutokutaka ujinga, alikua akitoa pombe kwenye friji wanakunywa, nilipata wazo la kumpigia simu Mama, simu yake ilikua haipatikani, sikujua sababu za kumpigia simu lakini nilitaka tu kuongea na mtu kwani nilijua kuwa kama ningetoka pale jikoni bila chakula basi wale wanaume wangeniua.


Wakati namtafuta Mama nilipata wazo la kumpigia dereva mmja wa Tax na kumuomba aniletee chakula, nilimuambia aniletee sahani tatu za wali, alishangaa usiku ule lakini nilimuambia ahakikishe ananiletea na akifika nyumbani anipigie simu asipige honi. Kweli alifanya hivyo, nilitokea mlango wa nyuma kwenda kuchukua chakula. Lakini wakati natoka sijui nini kilitokea, kumbe na mume wangu alitoka nnje, sijui alienda kufanya nini ila aliniona, hakunisemesha,a linituatilia mpaka napewa chakula na dereva Tax.


Aliponiona alianza kupiga makelele.


“Kila siku unaniona mimi Malaya! Kila siku uansema mimi nina wanwake wengi lakini leo umediriki hata kuniletea mwanaume wako hapa nyumbani kwangu! Yaani unamlata manaleteana na chakula, wewe mwanamke ni smhenzi, mbwa mbuzi kabisa!” Alitukana sana, Baba alitoka na kuona, nilimuambia dereva aondoke lakini hakuondoka, alisimama kama anamuelewesha mume wangu kwani alishasogea na pombe zake, lakini mume wangu hakutaka kuelewa, alipaniki na kuendelea kutukana, alimvamia Yule dereva na kutaka kumpiga.


Dereva alimuona, alimkwepa kutokana na pombe mume wangu alidondoka chini kama kiroba. Alijitahidi kunyanyuka na kumrukia tena dereva ambaye alifanya kazi ya kumkwepa tu mume wangu anadondoka, hakumpiga wala kumgusa lakini namna mume wangu alivyokua akidondoka basi alikua akiumia sana. Baba yangu alisikia zile kelele na kutoka, Dereva kuona kuwa watu wanajaa basi aliingia kwenye gari yake na kuondoka. Mume wangu alikua kalewa nyang’anyang’a hata kunyanyuka ilikua shida, Baba naye alikua kalewa chakari.


Hata hawakuingia ndani, waliendelea kuongea mpaka wakalala palepale nnje, walikuja kuzindika asubuhi, wakati wote huo mimi sikulala, nilikua macho nikihofia kwamba labda wanaweza kuamka na kukuta sipo ikawa msala mwingine. Asubuhi Baba alikua mzima, aliondoka bila kusema chochote, nilibaki na mume wangu, alijiandaa kwaajili ya kwenda kazini huku akiniacha nyumbani. Bado kazini walijua nipo hospitalini, nilianza kwenda kazini baada ya wiki moja ambapo nilipata nafuu kidogo.


Baada ya kile kipigo na yale matukio mume wangu ni kama alijifunza, bado kesi i.likua mahakamani, pamoja na kuhonga sana lakini kwakua ilishafika mahakamani basi ilikua ngumu kuifuta. Njiapekee ilikua ni kwa mimi ambaye nilikua kama shahidi mkuu kuacha kwenda kutoa ushahidi, baada ya kesi kusoma mara tatu bila mimi kutokea basi hakimu aliifuta na maisha yaliendelea. Watoto wangu walikua wanasoma bweni, hivyo muda mwingi walikua shuleni kasoro kipindi cha likizo ambapo walikua nyumbani.


Nulipita kama mwaka hivi bila mume wangu kunigusa, ingawa bado alikua ni mtu wa wanawake, mtu wa kunitukana lakini nilishamjulia, nilikua simjibu wala kumfuatilia. Siku moja nakumbuka ilikua siku ya pasaka, watoto walikua wamefunga shule na walikua nyumbani. Mume wangu alikua katoka, kama kawaida yake nilijua kuwa atachelewa kurudi. Motto wangu mkubwa alikua anaumwa sana, alikua na malaria, mume wangu aliondoka na gari yangu.


Labda nifafanue kidogo, mume wangu kipindi hicho alikua akifanya kazi nzuri, tu, alikua na cheo kikubwa ambacho ilimaanisha kuwa kazini kwake alikua anapewa gari wakati wa machana na siku za kazi. Lakini usiku katika mizunguko yake na mwisho wa wiki alikua akitumia usaifiri binafsi, mwanzo alikua na gari yeke tu lakini alimpa mwanamke mwingine Eliza (sio jina lake halisi) huyu alikua ni kama mke wake mwingine na nilishajua, mbali na kumpa lile gari lakini alishamjengea na kumfungulia biashara.


Baada ya kuhonga gari lake alianza kutumia gari langu, alikua akilitumia na kulifanya kuwa kama lake. Mooto alikua anaumwa sana, alikua anatetemeka, nilimpigia simu mumue wangu kuwa mtoto hali yake ni mbaya, aliniambia kuwa anakuja, tulisubiri kwa nusu saa nikampigia simu nikamuambia kuwa ana hali mbaya akasema kuwa tusitoke nyumbani tumsubiri. Kwa uoga nilisubiri, huwezi amini nilimpigia simu mume wangu kwenye saa tatu usiku lakini alikuja saa tisa usiku.


“Huyo mgonjwa yuko wapi?” Mume wangu aliniuliza.


“Kalala, nimemapa panadol homa imetuilia” Nilijibu kwa hofu kwani nilihisi kama kakasirika.


“Umempa Panadol, wewe mwanamke mshenzi kabisa, hivi kwanini hunisikilizi! Nimekuambia subiri nimechelewa kidogo unaanza kumpa mwanangu midawa yake!” Alianza kufoka, alifoka sana huku akinitukana wakati akiongea ndipo nilihisi kuwa hakua akinifokea mimi badi alikua na hasira zake nyingine.


“Nimekupa kila kitu, nyumbe nimekujengea lakini unaondoka na kwenda kutembea na dereva wa bodaboda! Hivi mimi kweli ni wakunichanganya na dereva wa bodaboda!”


Mume wangu aliongea, nilihisi lazima anamzungumzia Eliza kwani nilikua nafahamu tangu zamani kuwa, walikua akitembea na vijana wengi na mume wangu alikua akimchuna tu, sikuweza kumuambia mume wangu kwakua nilijua hataniamini nitaishia kupigwa tu. Siku hiyo mume wangu alionekana kuwa na hasira sana, alikua kalewa sana, mkononi alikua kashikilia chupa ya Konyagi kubwa na alikua akiinywakama maji. Sikusema chochote nilibaki namsikiliza, nilimuacha atukane mpaka basi kwani sikutaka maneno naye.


“Huyo Mbwa yuko wapi anayesema anaumwa, nimemuacha mwanamke wangu kwaajili yake nafika hapa kalala!” Mume wangu alifoka, nilijua kuwa kaumizwa sana kwani alikua akiwapenda sana watoto wake kwake kuwaita mbwa. Pamoja na kwamba mimi alikua akinitukana na kunipiga lakini ni mara chache alikua akifanya hivyo mbele ya watoto, mara zote alikua akinipigia ndani na hakutaka nipige kelele, nilikua nikivumilia na watoto walikua wakimpenda.


“Baba Juma jamani, watoto wamelala usiku huu…” Nilimsihi nikijaribu kumshika, alikua akitembea kwa kupepesuka kuelekea chumba cha watoto. Alikua akiwaita kwa nguvu huku akiwatukana kana kwamba kuna kitu kibaya walikua wamemfanyia. Namna nilivyokua ninamshika na kumsihi awaache ndiyo nilivyokua namtibua na kumfanya azidishe hasira. Aliingia chumbani kwa watoto, aliwanyanyua kutoka kitandani na kuwaambia watoke nnje, alianza kwenye chumba cha watoto wakiume, akawaambia watoke kisha akaenda kwenye chumba cha binti yetu, alimshika na kuanza kumvuta kulete sebuleni.


“Baba sisi tumelala wewe uatuamsha! Halafu umelewa! Kwanini unakunywa pombe na kutusumbua usiku wote huu…” Juma mtoto wangu wa kwanza alimuambia Baba yake, bado alikua na wenge la usingizi. Lakini kabla ya kumalizia kauli yake  nilisikia akiongea maneno.


“Mama Nakufaaaa!” Kisha alidondoka chini na kunyamaza kabisa. Nilimuangalia chini na kukuta vipande vipande vya chupa ya Konyagi aliyokua kaishikilia mume wangu, alikua amempiga nayo kichwani. Damu zilianza kumtoka kichwani, mume wangu yeye bado alikua akitukana na kulalamika kuwa kasalitiwa halafu watoto wanamsumbua.


Wanawake wengi wanaopigwa na kunyanyasika katika ndoa zao ndiyo wanaoongoza kwa uvumilivu, wengi wanajitengenezea uteja wa manyanyaso na huishi kwa imani kuwa labda kesho atabadilika ila si hivyo, 


AMINA; MWANANGU SITAKI UWE KAMA MIMI MAMA YAKO—SEHEMU YA TATU


Mume wangu hakua amejua kitu alichokifanya, bado alikua kalewa lewa, alimunamia mtoto na kutaka kumnyanyua akidhani kuwa alikua anaigiza, lakini haikua hivyo, ila kumgusa alikutana na damu.


“Juma! Juma! Juma mwanangu!” Aliita hukua kimnyanyua nyanyua mtoto lakini hakunyanyuka.


“NImefanya nini jamani? Juma! Juma!” Niliona kabisa kuwa pombe zopte ilikua zimemuishia ghafla, mtoto alikua hapumui kabisa. Alianza kupiga kelele kuomba msaada, mara kaite watu, mara usiite, maneno yalikua mengi sana, mume wangu alianza kuwa kama kachanganyikiwa.


Aliniambia mimi kubaki nyumbani na yeye alimchukua mtoto kumpeleka hospitalini, nilitamani sana kwenda lakini alinikataza katakata. Sikujua kampeleka wapi na wala hakuwasiliana na mimi mpaka asubuhi, usiku ulikua mrefu, nilijihisi kama nachanganyikiwa kwani kwa hali aliyokua nayo mwanangu nilijua kabisa kuwa hawezi kupona. Nilimpifia Mama na kumuambia kila kitu, aliishia tu kulia na kuniambia nisali sana kumuombea mwanangu. Sijui nini kilitokea lakini mwanangu alipona, asubuhi yake tu mume wangu alirudi na mtoto.


Alikua na bandeji kichwani lakini alikua anatembea mwenyewe.


“Hakikua kitu kikubwa, wamemshona nyuzi sita tu!” Mume wangu aliongea kamna kwamba hakikua kitu cha ajabu sana. Nilimuangalia mwanangu alikua na kidonda kichwani.


“Muache apumzike, nasitaki kabisa kusikia umemuambia kitu mtu yeyeyote, haya ni mambo ya kifamilia, mambo ya kutangaza tangaza changamoto zetu nitakuja kukuua siku!” nilimuitikia kukubaliana naye, akili yangu haikua inawaza kama anajisikiaje, mimi mwanangu kupona ilikua ni kama miujiza, nilipiga tena magoti kumshukuru Mungu kwa hilo.


Jioni Mama alinipigia simu, alitaka kujua hali ya mtoto, mume wangu alikua katoka, sikujua kama alirudi saa ngapi, lakini wakati namuambia Mama kuwa mtoto anaendelea vizuri mume wangu aliingia.


“Unaongea na Nani?” mume wangu aliuliza. Nilishtuka na kuweka simu pemebni, nilikua naogopa na kuwa kama mtu aliyefumaniwa.


“Naongea na… naongea na…” nilijiongelesha, lakini kabla ya kumalizia kumuambia naongea na nani nilishitukia teke la uso, mume wangu alikua kama kanikangaga hivbi usoni.


“Nilikuambia usimuambie mtu, lakini naona ushaanza kunitangaza! Yaani naona unamuambia kila mtu kuwa nimempiga mwanangu, sasa nimekuchoka, nataka uondoke!” Mume wangu alipiga kelele huku akiendelea kunipiga sehemu mbalimbali.


Bado nilikua sijakata simu hivyo Mama alikua akisikia kila kitu, namna nilivyokua nikipigwa. Alinipiga mpaka hasira zake zikaisha, aliondoka nayumbani na hakurudi mpaka baada ya siku tano, wakati wote huo michepuko yake ilikua ikinitumia picha zao wakila bata, wakifurahia maisha. Mimi nilinyamaza, Mama aliniuliza kilichotokea lakini nilikana, aliniambia.


“Mwanangu nimesikia kila kitu, huyo mwanaume ipo siku atakuua!” Nilinyamaza bila kumjibu kwani nilijua kuwa haitasiadia chochote, nilishachoka na maneno vumilia, nilitamani kuondoka lakini sikujua niende wapi.


Maisha yaliendelea, mume wangu hakubadilika, suala la kunipiga lilikua kama la kawaida. Baaada ya kunipiga mbele ya watoto mara moja na watoto kuanza kumuogopa nadhani hasita zilimzidia. Alikua hajali tena kama watoto wanaona, alianza kunipiga mbele za watoto na kuwapgiga watoto. Mwanzoni alikua angalau anatoa ada za watoto, lakini baada ya muda aliacha kabisa kutoa ada. Alikua hahudumii familia kwa chochote na kama nikilalamika basi nikipigo, akija nyumbani na kukuta hakuna chakula basi ni kipigo. Nilishazoea hiyo hali na nilikua sijui nini cha kufanya.


Siku moja mume wangu alikuja na mtoto mkubwa, alikua na kama miaka sita hivi, aliniambia ni mtoto wake na anataka nikae naye, nilikubali tu kwani sikutaka kumjibu, kwa hasira zake nilijua kama nikimjibu anaweza kuniua. Nilianza kuishi na yule mtoto kama mwanangu. Sikua nikimnyanyasa kwani pamoja na kujua kuwa ni mtoto wa nnje ya ndoa nilikua nafahamu fika si kos alake, hakuapanga kuzaliwa na mume wangu nnje ya ndoa. Alikua ni mtoto wakike na alionekana huko alikokua alikua hahudumiwi vizuri.


“Kwani wewe ndiyo Mama yangu wa kweli?” Siku moja Angel (si jina lake halisi) aliniuliza.


“Hapana kwanini?”


“Nimeuliza tu, sasa kama wewe ni Mama yangu wa kambo, mbona unanipenda kuliko Mama yangu mzazi, mimi nilikua mtu wa kupigwa kila siku. Baba alikua akija nyumbani naambiwa niende jikoni, nafungiwa jikoni Baba na Mama wanabaki sebuleni, wanakumbatiana na kufanya mapenzi, nilikua nasikia kelele nachungulia kwenye tundu la funguo naona kila kitu!”


Alianza kuongea, kwa namna alllivyokua anaongea alionekana kuathirtika tayari, alikua anajua kila kitu na walikua wanamnyanyasa.


“Kuna siku Mama alijua nawachungulia akawa ananipiga sana, baadaye wakawa hawanifungii tena jikoni bali wanafanya mambo yao wakati mimi nimelala!”


“Kwanini walikua wanafanyia sebuleni, inamaana hawakua na chumba?” Kipo lakini wanafanyia kila sheemu, hata kwenye gari wanafanyia na kila siku Mama alikua ananitukana kuwa mimi ndiyo nimemharibia maisha yake sina furaha. Nilipelekwa kwa Bibi alipokufa ndipo nilikuja kuishi na Mama yangu.


Sikutaka kumdodosa sana kwani alikua mdogo, lakini nilijua kuwa sababu za yeye kuletwa kwangu ilikua ni kwaajili ya kuwapa uhuru wa kufanya mapenzi. Nilikaa naye kwa mwaka mmoja bila Mama yake kuja kumuona wala kupiga simu. Lakini siku moja nakumbuka ilikua jumamosi, nilienda kazini na niliwahi kutoka kwani tunafanya nusu siku. Nilirudi nyumbani na kumkuta Agel analia, alikua chumbani kwake akikusanga nguo, nilimuuliza tatizo ni nini akaniambia kuwa Mama yake alikua kaja na anataka kumchukua.


“Naomba unisaidie Mama, mimi sitaki kuondoka! Wala hata hanitaki, ameona nina furaha hapa anataka kunichukua.” Aliniambia kwa namna alivyokua anaongea nilimuonea huruma, lakini nilijua kama mume wangu kashaamua basi nisingeweza kufanya chochote. Nilimdanganya tu kuwa nitaongea na Mama yake.


“Kwani mama yako yuko wapi?” nilimuuliza, aliniambia katoka na Baba na kamuambie akusanye kila kitu ili aondoke. Nilirudi chumbani nikiwa na mawazao, kweli hakua mwanangu lakini kwa mambo aliyokua amenielezea nilijua kabisa kuwa mtoto anaenda kutelekezwa. Ni mara nyingi walikua wanatoka usiku na kurudi asubuhi wakimuacha nyumbani bila hata binti wa kazi.


Kuna kipindi Mama yake alishawahi kusafiri akakaa siku tatu bila kujulikana yuko wapi majirani ndiyo walijitolea kumpa chakula. Mume wangu alirudi usiku, alikua na Mama Angel, mimi nilimsalimia vizuri tu lakini yeye alikua kanuna.


“Unataka kunichukulia mwanangu! Mwanamke mshenzi sana wewe na kwa taarifa yako huyu ni mtoto wangu, kama ulikua unaamini kuwa atakupenda kuliko anavyonipenda mimi basi umenoa!” Alianza kunitukana, mimi nilishangaa lakini nilikuja kugundua kuwa alikua analalamika kwakua alikuta mtoto wake kanawiri na alipotaka kuondoka naye basi alikataa na kusema anabaki.


Kitendo hicho kilimkera sana Mama Angel na kuamua kuondoka na mtoto wake. Mimi nilijitetea lakini haikusaidia, kalizuka kaugomvi flani, tukashikana, lakini kama kawaida mume wangu alikua upande wa mchepuko, alianza kunipiga, alinipiga sana mpaka nikapoteza fahamu, baada ya kuona sina fahamu, alinichukua na kwenda kunifungia stoo. Aliondoka akimchukua Angle, wanangu ndiyo walienda kuita majirani, wakaja wakavunja mlango nika[pelekwa hospitalini.


Nilikaa kw aisku tatu, mume wangu hakuja hospitalini, mtu pekee aliyekuja kunihudumia alikua ni mama yangu.


“Ukitoka hapa hurudi kwa mume wako!” Maama aliniambia kwa hasira, alikua anaonekana kuuumia sana.


“Nitaenda wapi Mama yangu, Baba hataki nirudi nyumbani…” Nilikua nimechoka, natamani kuondoka na kumuacha mume wangu lakini nilijua sijui ni kwa namna gani naweza kuondoka.


“Mwanangu unakumbuka nilivyokusomesha kwa shida, Baba yako alikua hataki usome kwakua ni mtoto wa kike, lakini kila siku nilikua napigwa, kila siku nilikua nalia, nilikopa mpaka ukasoma.”


“Nakumbuka Mama.”


“Basi mwanangu, sikukusomesha ili uje kuwa kama Mimi, mimi nilikua sina pekwenda, sikua na kazi, sikua na chochote, nilikua na watoto wadogo ambao nisingeweza kuwahudumia mwenyewe. Lakini wewe mwanangu una kila kitu, una kazi nzuri, una elimu, unaweza kuhudumia watoto kwanini uteseke kama mimi?”


Mama aliniuliza maswali ambayo sikua na majibu yake, alinisihi sana, sikua tayari kuondoka, mmbali na mateso yote lakini bado nilikua naamini kuwa siku moja mume wangu atakuja kubadilika. Nilikua najua kuwa labda ipo siku mume wanvgu shetani la chuki litamtoka na kurudi kwangu. Lakini Mama yangu hakukubali, aling’ang’ania akisema kuwa kuondoka ni lazima nipende nisi[pende.


“Lakini Mama siwezi kuwaacha wanangu, mimi nikiondoka mume wangu atawataka, hatakubali kuniachia watoto wangu!”


“Atakuachia mwanangu, ninapokuambia kuwa unaondoka basi jua ni unaondoka, huyo mwanaume atakuacha wewe! Niamini mimi ni mama yako, niliteseka kwaajili yako sitaruhusu uteseke tena.”


Mama aliongea, nilimkubalia kishongo upande nikijua kuwa mume wangu hawezi kuniacha na kunipa talaka. Nilipotoka hospityalini Mama alinisindikiza mpaka nyumbani, mume wangu hakuepo lakini alimsubiri mpaka kurudi.


“Mwanangu nimekusubiri kwakua nataka umuache mke wako! Najkua yeye anakupenda na hawezi kukuacha, na kwa sheria ya dini mwanamke hatoi talaka, ila nataka umuandikie mwanangu talaka tatu.” Mama aliongea kwa kujiamini, mume wangu alimuangalia kwa dharau.


“Umechanganyikiwa wewe, mimi najua kuoa tu sijui kuacha!”


Mume wangu alionge kwa dharau, mama alinyanyuka alimuangalia mume wangu usoni kwa muda wa kama dakika mbili bila kupepesa jicho kisha akanigeukia.


“Mwanangu kesho kutwa nitakuja kukusaidia kuchukua vitu vyako, mume wako atakua ashakupa talaka.” Mama alimaliza kwa tabasmau, aliondoka na kutuacha wote tunashangaa.


“Huyu Mama yako kichaa nini? Anafikiri kama nitakuacha, sikuachi na kama ukitaka kuondoka ondoka lakini watoto wangu niachie na utaondoka na nguo zako tu!”


Mume wangu alifoka, lakini mama hakua amefika mbali, alisikia na kugeuka akarudi, akamuangalia mume wangu kisha akamuambia.


“Mwanangu ataondoka na watoto wake, talaka utampa na ataondoka na kila kitu alichochuma kwa jasho lake.” Alinigeukia.


“Mwanangu anza kuorodhesha vitu vyako vyote katika hii nyumba, usiache chochote hata kama ni nyanya ulinunua zimeoza utaondoka nazo.” Aliongea na kuondoka, mume wangu alianza kufoka, alinifuata na kutaka kunipiga, lakini kabla ya kufanya chochote alianza kupiga kelel.


“Mamaaa nakufaaa!” alipiga kelele huku akivua nguo. Alikua anapiga kelel hukua kishika sehemu zake za siri, alivua nguo na kubaki kama alivyozaliwa, uume wake ulikua umesimama. Nilijua ni mambo ya mapenzi nikamuambia hawezi kunigusa kwani naumwa lakini alikua anapiga kelele analia kama mtoto. Kwa namna ulivyokua umesimama nilikua sijawahi kumuona, aulikua umesimama, umekua mkubwa kuliko kawaida yaake, mishipa ya damu mirefu tena vmyekundu ilikua inaonekana.


Alionekana kuwa katika maumivu makali,a lipiga kelele akilalamika kuwa uume wake ulikua unawake moto. Aliniambia nimletee maji tabaridi, nilileta akamwagia lakini wapi, alikimbia mpaka kwenye friji na kuchukua mabarafu lakini wapi, alikua kama mtu aliyechanganyikiwa. Hata watoto walipokuja ilibidi kuwatoa nnje kwani Baba yao alikua uchi. Alianza kulia akiniomba nimpeleke hospitali, nilimfunika na kumuingiza kwenye gari, huko alipelekwa walimhangaikia lakini hakulala. Alikaa hivyo hivyo mpaka asubuhi, uume umesimama, unauma mpaka umekua mweusi.


“Mama yako ndiyo kanifanyia haya, mpigie nimuombe msmaaha.” Nilimpigia Mama lakini hakupokea, nilimpigia Baba ambaye alipokea huku akiongea kwa shida, alionekana kama anaumwa, aliniambia kuwa Mama ametoka na hajui kaenda wapi. Kabla sijampigia tena Mama meseji yake iliingia, muambie akupe talaka zako tatu. Nilimuonyesha ile mseji mume wangu, alianza kulia kuniomba msamaha aking’ang’ania kuwa hawezi kuniacha. Hospitalini walisema hawana cha kumsaidia, tulirudi nyumbani akiwa katika maumivu makali.


Mpaka usiku mume wangu aliniandikia talaka zangu tatu bila kuambiwa na mtu yeyote. Cha ajabu aliponikabidhi ile talaka uume wake ulilala na kuwa kama kawaida na hapohapo Mama yangu alipiga simu.


“Hiyo nyumba najua ni ya mwanangu, kesho nitakuja na mwanasheria, mtaandikishana kugawa vitu na wewe utaondoka.” Mume wangu alikubali kama zoba, sijui Mama alifanya nini lakini alitafuta mwanasharia, tukaandikishiana na mume wangu, tukaenda mpaka mahakamani na kila kitu kikawa sawa.


Mume wangu hata hakuomba msamaha, alinikinahi na hakurudi tena kwangu, Mama yangu aliniangalia na kuniambia mwanangu kama ni kutubu nitatubu baadaye ila jua nilikusomesha ili usiteseke kama mimi. Tangu kuachana na mume wangu nimekua mtu wa furaha sana, Mama yangu alishafariki (Mungu muweke mahali pema) Baba anaishi mwenyewe, tunamhudumia lakini watoto wote hatumpendi, kwa namna alivyokua akimnyanyasa Mama hakuna mtoto hata mmoja ambaye anataka kuishi ney.


Tumemuwekea mfanyakazi wa kuishi naye, mume wangu alioa tena lakini mwanamke akashindwa kuvumilia wakaachana, kazini alishafukuzwa muda mtrefu kwani alikua na kesi ya kumpa mimba mtoto wa sekondari. Kidogo imfunge lakinia lihonga sana, sasa hivi nasikia yupo mwanza na sijui hata anafanya nini. Mimi nina maisha yangu, mambo ya wanaume kwa sasa sitaki nalea wanangu kwanza. Nimeteseka sana kiasi kwamba kila mwanaume ninayekutana naye nahisi kama anataka kuniumiza kama mume wangu.


***MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG