Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

NILIACHANA NA MALAIKA SASA NAZUNGUKA KUMTAFUTA SHETANI!

  

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

 

MY STORY; NILIACHANA NA MALAIKA SASA NAZUNGUKA KUMTAFUTA SHETANI!


“Kama unafanya kazi ni lazima mshahara wako uonekane, kuna haja gani ye wewe kwenda kazini kama kila kitu nakuhudumia mimi? Yaani unafanya kazi, mshaara wako ni kama wangu lakini mpaka nauli ya kazini nakupa?” Mume wangu alipenda sana kuniambia, lakini mimi niliona kama vile ananionea, niliona kuwa hakikua sawa mimi kujihudumia wakati nimeolewa.


JOIN US ON TELEGRAM

“Wanaume wenzako wanafanya hivyo, mimi siwezi kujihudumia kama wewe upo, mimi ni mwanamke nahitaji matunzo!” niliongea kwa hasira huku nikinuna, mara nyingi mume wangu alipokua akiniambia kuhusu suala la pesa basi mimi nilikasirika na kununa hata mwezi mzima.


Kwakua mume wangu ni mtu mkimya, hapendi maneno basi huniomba msamaha yanaisha. Mume wangu alikua ananipenda sana, ingawa kipato hakunizidi sana lakini alikua ananihudumia kwa kila kitu, kuanzia mimi mpaka wazazi wangu, na akikosa huwa nilikua na tabia ya kununa. Mbali na kunihudumia lakini alipenda sana kunishirikisha kwenye mambo yake ya maendeleo, alikua akinunua kiwanja ananishirikisha, hata kama aliandika majina yake lakini alinishirikisha na kuhakikisha kuwa najua kila kitu.


Kusema kweli mimi sikujali kabisa kuhusiana na mali zake kwani nilikua naamini kuwa ni zake, niliona kama vile ana kiherehere cha kunishirikisha. Nilinunua kiwanja na kuanza kujenga kimya kimya bila kumshirikisha mume wangu, hata alipojua na kuniuliza wala sikumuambia, nilikataa na kama kawaida yangu nilinuna hivyo akaacha kufuatilia. Rafiki yangu mmoja alinishaauri nikasome, kweli niliomba nafasi ya kwenda masomoni kimya kimya, sikumuambia mume wangu mpaka napata nafasi ya masomo.


Kila kitu kilikua kimekamilika, lakini wiki mbili kabla ya mimi kwenda kusoma mume wangu alipata ajali ya gari, alivunjika mbavu mbili na alikua hawezi kufanya chochote. Wakaqti anapata ajali nilikua bado sijamuambia kuwa nimeomba kwenda chuo ingawa kila kitu kilishakamilika, nilisubiri mpaka alipoanza kupata nafuu lakini akiwa bado hospitalini ndipo nilimuambia kuwa nimepata nafasi ya kusoma. Alinisihi sana nisiondoke niahirishe mwaka kwani kwa hali yake alihitaji msaidizi, lakini mimi sikujali, nilishapanga kuondoka na tayari nilishapata ruhusa.


Tuligombana sana mpaka kufikia kupelekana kwa wazazi ila sikujali, alipokua ananiambia kuwa nibaki niliona kama ni mtu aananikwamisha hivyo niliamua kwenda hata baada ya ndugu zangu kuniambia nimsikilize mume wangu.


“Kama hubaki kwaajili yangu hembu basi baki kwaajili ya watoto. Mtoto mkubwa ana miaka mitatu, mdogo ana mwaka, unaenda kusoma na unawaacha hapa, hali yangu unaiona hii, hivi kweli mimi naweza kuwalea?” Mume wangu aliniuliza, nawapenda wanangu lakini niliona kama mume wangu anataka kuwatumia watoto kunibakisha.


Niliongea na rafiki yangu kuhusu kuah8irisha mwaka lakini hakukubali, aliniambia kua wanaume ni washenzi na kuna uwezekanao mkubwa mume wangu anatumia watoto ili nisisome.


“Hiyo ajali mbona ya kawaida, kwani ukibaki kuna kikubwa kipi utafanya, yeye si ana ndugu zake, Mama yake hana kazi, kwanini asiende kulelewa na Mama yake, kwanini watoto msipeleke kwa Mama?” Aliniuliza, niliona sawa, nikamuambia mume wangu kuwa mimi naondoka na kutokana na hali ya kule basi siwezi kwenda na mtoto, kweli niliondoka pamoja na mume wangu kuongea sana, nilimuacha mume wangu na mtoto wa mwaka mmoja na yule mkubwa.


Mume wangu alinikasirikia kwa kama miezi miwili tu lakini kama kawaida yake ni mtu ambaye hapendi ugomvi basi alinitafuta, akataka tuyamalize, nilijifanya kukasirika nikimuambia anapaswa kuniomba msamaha kwani hakuniruhusu kwa mouyo mmoja, kweli aliomba msamaha yakaisha. Lakini nikiwa chuoni nilikutana na Kaka mmoja, yeye alikua ni mfanya kazi jirani na chuo kwenye benki moja hivi, naye alikua ni mume wa mtu ila kama mimi mke wake alikua mbali, kwa maana hiyo tulianzisha mahusiano na yalipopamba moto basi tukawa kama tunaishi pamoja kupika na kupakua.


Ingawa nilikua nafanya kazi, nalipwa msahara na nilikua nasomeshwa kazini lakini nilimdanagnya mume wangu kuwa silipiwi kazini, akawa ananihudumia kwa kila kitu ikiwa pamoja na kulipia ada. Pesa niliyokua nikipata nilinunua kiwanja na kuanza kujenga kulekule kimya kimya bila kumuambia mume wangu, huyo Kaka niliyekua naye kwenye mahusiano ndiyo alikua anajua kila kitu na kunisaidia kusimamia. Maisha yaliendelea, mume wangu alikua naajali, anapiga simu asubuhi, mchana na jioni kujua hali.


Hali ile ilinikera kwani wakati mwingine akipiga simu nakua nipo na mpenzi wangu, anakua kama ananichosha, lakini pia yule Kaka alikua ananionea wivu hivyo alinikataza kuongea na mume wangu mbele yake. Kweli nilianza kumkatia simu mume wangu, nikawa namjibu vibaya tena kwa kifupi mara nyingi nikimuambia kuwa mimi nimechoka siwezi kuongea naye. Pamoja na yote hayo mume wangu alijitahidi, kuna kipindi hasira zilinipanda tu, labda nimeuziwa na mchepuko wangu kwakua ulikua unanichunga sana.


Unashika simu yangu na kunipangia namna ya kuongea na mume wangu lakini yeye alikua anamheshimu mke wake, akiongea na mke wake mimi nakaambali kabisa ili nisikohoe au kuonekana kwani mara nyingi mke wake alipenda kumpigia video call. Hali hiyo ilinikera najikuta namblock mume wangu, nampigia na kukasirika kitu cha kijinga namtukana lakini mume wangu anakua mtu wa kujishusha. Hali hiyo iliendelea mpaka nikamaliza chuo, nilikua nachukua Master na wakati huohuo nafanya mitihani na bodi hivyo nilifaulu vyote na kupata na CPA yangu.


Kumbuka katika kipindi cha miaka miwili ambacho nilikua chuoni nilirudi nyumbani mara mbili tu, tena sikukaa sana kwakua mchepuko wangu ulikua unanihitaji, niliporudi nyumbani nilikuta mume wangu kafungua kampuni ya mikopo. Alikua anakopesha watu na ilikua inaenda vizuri, aliniomba kuwa kwakua nimerudi, kuliko kuajiri watu basi niwe nafanya na Part Time pale kwani yeye anakua bize sana na ile Biashara ni ya familia, mimi nilikataa na kumuambia kuwa Biashara ni yake na mimi nikitaka kufanya Biashara basi nitafanya kivyangu. Mume wangu alikasirika sana kwani alijua kuwa elimu yangu itasaidia, kampuni alisajili kwa majina ya ngu, yake na ya watoto lakini sikuona kama ni yangu, nilikasirika kuwa alianzisha kampuni yeye mwenyewe bila kuniambia.


Ukweli nikuwa aliniambia, tena kwa kunipigia simu, wakati aanisajili aliniambia kuwa anaandika jina langu lakini sikujali, nilimjibu kwa mkato, alinitumia mpaka meseji lakini sikujibu. Wakati ananiambia sikuona kama ina umuhimu, niliona kuwa ni kampuni ya kipuuzi tu na itakufa hivyo sikutaka kujishughulisha. Lakini mume wangu ni wale watu ambao wana kismat, kila kitua nachokianzisha kinasimama, alinza kukopesha na mtaji wa milioni mbili tu, tena alizokua anacheza mchezo kwani hakua na pesa, pesa yote aliitumai kunisomesha mimi.


Lakini wakati naenda biashara ilikua na mtaji wa kama milioni 40, alichokua anafanya ni kuchukua pesa kwa watu, anakopesha kisha anawarejeshea kwa riba kidogo, aliniambia kila kitu lakini niligoma. Ilikua shida kwania litegemea baada ya kunisomesha ningerudi na kufanya naye kazi ila niligoma. Kusema kweli nilitamani sana ile Biashara lakini nilihofia kuwa mume wangu atafanikiwa sana, niliamua kuchukua mkopo ili kufungua Biashara yangu, namimi nilifungua kitu kile kile Biashara ya kukopesha tena karibu na mume wangu.


Lakini sikufanya wazi wazi, nilichukua watu wakajifanya ni kampuni yao kumbe ni yangu, lengo lilikua ni kushndana na mume wangu. Pamoja na kwamba niligoma kushiriki lakini mume wangu aliniambia kuwa mimi ni mke wake hivyo anataka nijue mali zake na Biashara zake kwani akifa hataki watoto wateseke. Alikua ananiambia kila kitu kuhusu Biashara na wateja, nilitumia huo mwanya kuharibia kwa wateja, kuchukua wateja wake na kushusha riba ili kuvuta wateja, mwanzo ilisaidia lakini kutokana na usimamizi mbaya biahsara ilikufa.


Nikawa kwenye mshahara sina kitu, nikaanza kukopa mtaani, nilikopa sana ikiwa ni pamoja na kuchukua hati ya nyumba ambayo alijenga mume wangu na kuiweka dhamana. Lakini mwisho wa siku nilishindwa kulipa, nilipoona hali imekua mbaya nyumba inataka kuuzwa niliamua kumuambia mume wangu, nilimuomba sana msamaha na kumuambia kila kitu. Alikasirika sana na siku hiyo alinipiga kofi, sikuumia lakini ile kupigwa tu nilikasirika na kuondoka, nilirudi nyumbani nikimuambia kila mtu kuwa mume wangu anataka kuniua, kiliitishwa kikao, tuliongea mengi lakini mume wangu hakuongea chochote kuhusu mkopo, mimi ndiyo nilikua naongea, mara kusema alinikataza kusoma, mara amenipiga na maneno kibao.


Mume wangu alikiri kunipiga lakini hakusema sababu, aliwaambia kuwa ametambua kosa mimi ni mke wake hata kama nimemkosea alipaswa kuzuia hasira zake, basi baada ya hapo aliomba msamaha tukarudi. Alitafuta watu waliokua wananidai akaandikishana nao na kuahidi kulipa, nakumbuka nilikua na deni la milioni 16. Mume wangua lililipa kwa awamu mpaka akalimaliza. Maisha yaliendelea, kweli nilibadilika lakini baad atu ya yeye kumaliza deni nilianza kujihisi kama vile nanyanyasika, nilihisi kukosa uhuru, nilitaka kuondoka nyumbani ingawa sikutaka kumuacha mume wangu.


Nilianza kufuatilia uhamisho kimya kimya, nilitaka kazini ionekane kama vile nimehamishwa bila mimi kuomba. Lakini wakati nahangaika na uhamisho niligundua kuwa nina ujauzito, nilitaka kutoa mimba lakini iligoma, niliamua kuibeba hivyo hivyo kishongo upande. Wakati wote huo nilikua bado nawasiliana na ule mchepuko wangu, mara moja moja naenda kwani kazini ruhusa ilikua shida. Nilimuambia kuhusu kuhamia kule lakini alikataa, aliniambia kuwa mke wake anakatibia kuja hivyo nibaki na mume wangu kama nataka kuendelea naye.


Kusema kweli niliumia lakini nilishamchoka mume wangu, nilitaka sana kukaa mbali na mume wangu hivyo niliendelea na shughuli za uhamisho ambazo nazo zilikwama. Baada ya uhamisho kugoma, wakati mimba ikiwa kubwa nakaribia kujifungua ofisini kwetu ilitokea nafasi ya kusoma, ilikua ni kozi fupi ya miezi sita, niliihangaikia mpaka nikaipata mimi, kwakua nilikua najua mume wangu hawezi kukubali kutokana na hali yangu, nilijiandaa kimya kimya, nikakamilisha kila kitu, nilimuaga mume wangu kuwa naenda safari ya kawaida ya kikazi lakini nilipofika ndiyo nikamuambia kuwa nimeenda kusoma na sitarudi baada ya miezi sita.


Mume wangu alikasirika sana, aligoma kunitafuta mpaka baada ya mwezi mmoja nilipokaribia kujifungua, akamtuma Mama yake ili kuja kunihudumia uzazi kwani niligoma kabisa kuacha kusoma hiyo kozi, nilitaka kuishi mbali na mume wangu. Nilikaa na Mama mkwe kwa wiki mbili tu, ingawa alitaka kuendelea kukaa lakini nilipata rafiki mmoja, tukawa tunaishi naye ananisaidia hivyo nikamuambia Mama mkwe kuondoka, ingawa hakuonyesha kukasirika ila ilimuuma mpaka kumuambia mume wangu ambaye alinitafuta na kunisema sana mpaka nikaamua kumblock.


Nilikaa mapaka kozi ikaisha lakini bado sikurudi kwa mume wangu, nilimtafuta yule mwanaume wangu tukaombana msamaha na kurudiana, nilikaa kwa mwezi mmoja ndipo nikarudi kwangu na kwa mara ya kwanza mume wangu alimuona mtoto.


“Unavyofanya sio vizuri mke wangu, kuna wakati nitachoka, nakuheshimu lakini umenipanda kichwani sana, mimi ndiyo nakua kama mwanamke, si kama siwezi kuwa mbabe naweza lakini kwa faida ya nani?” Siku moja mume wangu aliniambia, nilijikuta napandwa na hasira na kuanza kumuambia kuwa ananitishia na kama kanichoka basi tuachane.


Ghfla kisirani cha kuachana kilianza, mume wangu hakua na tatizo lolote lakini nilihisi tu kuwa natakiwa kuachana naye, nilianza kama utani lakini kadri nilivyokua naongea na marafiki zangu ambao kila siku nilikua nawaambia mambo mabaya ya mume wangu kichwa kilivimba nikajikuta nadai talaka kweli kweli. Mume wangu hakua tayari kuniacha, alihanagika na mimi kanisani, akahangaika na mimi kila mahali lakini niligoma na kumuambia kuwa mimi nataka kuachana naye simtaki. Nakumbuka kila mtu alinishangaa kwani watu wa nnje waliniona kama nipo kwenye ndoa nzuri, Mama alikua ananiuliza kila siku kama mume wangu ananipiga, ananinyanyasa lakini sikua na majibu zaidi ya kuwa simtaki na kuna mambo ananifanyia ambayo siwezi kuwaambia.


Tulihangaishana suala la talaka kwa zaidi ya miezi sita, mume wangu aligoma kabisa kuniacha, mimi kila sikui zilivyokua zinaenda ndivyo hasira zilizidi kunipanda. Kuna siku nilikua naongea na rafiki yangu, aliniambia kuwa kuna njia nzuri na rahisi ya mume wangu kuniacha.


“Tena kama ukiwa makini basi jua kuwa mali zote zitabaki kwako kwani anaweza kufungwa kabisa!” Aliniambia, nilimuuliza ni kitu gani akaniambia kuwa nimsingizie mume wangu kuwa alitaka kumbaka binti wa kazi, kwangu ilikua ngumu sana, kwanza nilijua kuwa Binti yangu wa kazi asingeweza kukubali kwakua ananichukia sana, amekaa na mume wangu kwa zaidi ya miaka kumi wakati mimi nahangaika na maisha na pia alikua ashamsomesha yaani alikua kama ndugu.


M2aSp3onrhche4 28,1 2020h  · 


MY STORY; NILIACHANA NA MALAIKA SASA NAZUNGUKA KUMTAFUTA SHETANI!—SEHEMU YA PILI


Rafiki yangu alinishauri nibadilishe mfanyakazi wa ndani, nikishabadilisha atanipelekea mfanyakazi wake ambaye ataweza kusema kuwa mume wangu anamtaka kimapenzi ili tu tuachane.


“Lakini mimi sitaki kumfunga mume wangu?” Nilimuambia kwani pamoja na yote mume wangu anajali sana satoto na mimi siwezi kuwahudumia peke yangu.” nilimuambia, aliniambia kuwa haitakua na shida, tulikubaliana mimi nifanye visa na kumfukuza binti wa kazi ambaye mume wangu alikua anamuamini ili kutafuta mwingine.


Nilianza kushurumu kuwa nahisi mume wangu anatembea na binti wa kazi, hivyo simtyaki, kama anataka ndoa irudi basi amgukuze binti wa kazi na mimi nilete mwingine. Mume wangu alishangaa sana, kila mtu alishangaa lakini mimi nilienda mpaka kuongea na wazazi wangu kuwa simtaki huyo  binti wa kazi kwakua anatembea na mume wangu ndiyo sababu hata ya mume wangu kumsomesha. Ilikua shida sana, lakini mwisho wa siku mume wangu alikubaliana na mimi, akamuondoa yule binti na kumpeleka kwao. Baada ya kama wiki moja hivi shoga yuangu aliniletea mfanyakazi wake.


Lengo lilikua ni yule binti kuanza kulalamika kwa watu kuwa mume wangu anamtaka kimapenzi na usiku kupiga kelele kuwa mume wangu kambaka. Lakini nakumbuka siku mbili baada tu ya kumleta huyo binti Baba alikuja nyumbani kwangu, siku zote Baba yangu alikua ni mkimya, mtu wa kusikiliza, mara nyingi alikua upande wa mume wangu lakini hakuniambia moja kwa moja.


Haikua kawaida ya Baba yangu kuja nyumbani kwangu na kukaa, mara nyingi alikua ni mtu wa kupita tu, lakini siku hiyo alikuja, nakumbuka ilikua jinoni, kwenyue saa kumi hivi,a likuja nyumbani, wakati huo mimi na mume wangu tulikua kazini, hivyo alimkuta binti wa kazi tu. Nilirudi kwenye saa 12, mimi ndiyo nilianza kufika, baadaye mume wangu alikuja.


“Nilitaka kuondoka lakini kuna kitu kikaniambia hapana, ngoja niwasubiri wopte…” Baba aliongea, Kaka kawaida yake aliongea kwa utulivu.


“Mpe mke wako hicho anachokitaka kabla hajaharibu maisha yako.” Baba alianza kuongea, nilishtuka na mume wangu alishtuka.


“Unamaanisha nini Baba?” Mume wangu alimuuliza.


“Mke wako si anataka talaka?”


“Ndiyo…” Mume wangu alimjibu.


“Basi mpe talaka aondoke zake, mimi huyu ni mwanangu lakini ni takataka, kitu alichotaka kukufanyia angekua mimi ningemkeketa kwa meno, nataka kesho nenda baraza la kata, saini hiyo barua, nenda mahakamani kama atataka mali muachie zote utaanza upya!” Baba aliiongea kwa hasira na uchungu mkubwa, kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilimuona Baba yangu akitokwa na machozi. Nilishtuka lakini nilishindwa kuongea, sikuhisi kama Baba kajua mpango wangu, mume wangu aliuliza kama kuna nini ndipo Baba alimuita mfanyakazi wa ndani.


“Mimi ni mwanaume najua haya mambo, shida yangu mwanangu umeoa halafu badala ya kuwa mwanaume umekua Bibi harusi, umemuacha mwanamke kuendesha nyumba yako, kila kitu anachoongea unamkubalia, ndiyo hivyo wanawake hawa hawapaswi kuwa vichwa vya familia bali wanapaswa kuwa moyo wa familia, wewe umemuacha amekua kichwa, kichwa kinafanya maamuzi lakini moyo unapenda, sasa nilipoona binti yangu ghafla kabadilisha binti wa kazi nilishtuka, lakini sbabau zake zilinishtua zaidi.


Niliwaza, siku zote anadai ntalaka hajawahi kusema kuwa wewe ni Malaya, kakufumania au unatembea na binti wa kazi, lakini ghafla anasema hivyo tena anatak kubadilisha binti wa kazi. Nilihisi kuna mtego, nilijua kuwa kuna kitu, nilijua anatengeneza ushahidi, lakini nilipomuuliza Mama yako kuhusu wewe kupata mfanyakazi, kwa maana wewe una watoto na tulipanga mfanyakazi wetu kuja kukusaidia, lakini ghafla unamuambia Mama yako kuwa una mfanyakazi, namuuliza Mama yakoa annimbia umepewa na rafiki yako huyo mfanyakazi, nikajua kuwa kuna kitu, kuna mchezo, nawafahamu wanawake, vichwa viwili vilivyojaa upumbavu vikikaa pamoja vinaleta mauti, basi nikaona mauti ndiyo maana nikaamua kusema hapana, hembu nifanye kitu.


Nimekuja hapa, nikamuona binti mwenyewe, nimeongea naye maneno matatu nikajua kunakitu. Nimembana kaniambia kila kitu, sasa Mama hembu waambiwa ulikuja hapa kufanya nini?” wakati Baba anaongea nilihisi kuchanganyikiwa, nilikua natetemeka kwani Baba yangu ni mkali Balaa, sikujua kama anaweza kushtukiza mchezo. Yule mfanyakazi alieleza kila kitu kuwa aliletwa ili kusema kuwa mume wangu kambaka ili tu tuachane, mume wangu aliniangalia nilitingisha kichwa kukataa lakini baba alinipiga jicho moja tu nikajikojolea na kusema kila kitu.


Niliwaambia kila kitu na kuomba msamaha, Mume wangu alimshukuru Baba, hakuongea sana, Baba alipoondoka aliniambia tu nashukuru, alichukua nguo zake na kuondoka, kama kawaida yake nilijua kua hawezi kuniacha, lakinia subuhi ya siku iliyofuata mume wangu alienda ustawi wa jamii, akasaidi barua kuwa yupo tayari mambo yaende mahakamani, mimi nilishasaidi yeye ndiyo alikua anazungusha. Nilipigiwa na Dada wa ustawi kuwa niende kuchukua barua ya mahakamani ili kwenda kudai talaka, ingawa nilikua nipo tayari kuachana na mume wangu na nilishajiapnga lakini nilihisi kutetemeke, yaani mwili ulikufa ganzi wote.


Siku iliyofuata nilianza kutafuta wakili, nilitaka kumkomesha mume wangu kuwa kama anataka talaka basi nitachukua kila kitu na kumuacha hana kitu kabisa. Nilianza kwa kuorodhesha mali zote za mume wangu ambazo nilikua nazijua, Biashara zake nyingi nilikua nazijua na nilijua kuwa moja kwa moja tutagawana kama ikitokea tukaachana. Lakini haikua hivyo, mume wangu alikua mjanja, kila kitu ni kama alishajiandaa kuwa ataniacha, mimi nilikua najua kuwa mume wangu ana mali lakini nilikua sijui ameandika majina ya nani.


Mwanzo alikua ananionyesha kaandika majina yake, lakini baada ya kuona kuwa sieleweki mume wangu alisajili kampuni, aliweka umiliki wa mali zote katika kampuni na hakuandika jina lake hata mali moja zaidi aliandika majina ya watoto na baadhi ya ndugu zake. Kwa maana hiyo hata kama tukiachana tusingeweza kugawana mali ambazo zina majina ya watoto tena ambazo zipo chini ya kampuni ambayo mimi hata si mmoja wa wakurugenzi. Mpaka napata talaka niliondoka sina kitu kabisa. Mpaka napokea talaka nilikua siamini kuwa mume wangu ana ubavu wa kuniacha, nilijua kabisa kuwa atakuja na kuniomba msamaha kwani ananipenda sana.


Maisha yalianza kuwa magumu baada ya kuachana na mume wangu, mwanzo niliwang’ang’ania watoto, ingawa waligoma kuja kwangu lakini mume wangu aliniacha nao. Ila sikuweza kukaa nao hata kwa miezi sita, kwanza waliku aananisumbua kurudi kwa Baba yao, pioli gaharama zilikua kubwa kwani mume wangu alikua hahudumii kwa chochote, zaidi ya chakula na alikua akitoa laki moja tu kwa mwezi, lakini pia walininyima uhuru wa kufanya mambo yangu, niliwarudisha kwa Baba yao. Mara kwa mara nilikua nikisafiri kwenda kwa mchepuko wangu, tulifikia hotelini kwani kwake aliniambia kuwa alikua akiishi na mke wake na hakua tayari kumuacha.


Lakini pia hakutaka niende mara kwa mara kwenye nyumba yangu ambayo nilijenga na yeye kubaki kuisimamia kwani aliniambia ina mpangaji kachukua nyumba nzima. Maisha yaliendelea mpaka siku nilipokuja kugundua kuwa kumbe nyumba haikua na mpangaji bali alihamia yeye na mke wake kwenye nyumba yake, na alishabadilisha jina nyumba ilikua na hati yenye jina lake. Nilipomuuliza basi niliishia matusi tu, alinitukana sana na kuniambia nisimjue. Nilirudi numbani nikiwa sina hili wala lile, nyumbani kwetu kila mtu alikua ananichukia kutokana na ujinga niliouifanya.


Nilirudi kumuomba mume wangu msamaha, alinisamehe na kuwa ananihudumia lakini aligoma kabisa kurudiana na mimi. Ingaw awatu wengi walimuambia kuwa asihangaike na mimi lakini mume wangu alinisamahe, aliniambia kuwa hawezi kurudiana kimapenzi na mimi lakini mwisho wa siku nitaendelea kuwa Mama wa watoto wake hivyo hawezi kunitenga. Alianza tena kunishirikisha katika Biashara, nilijua ni jinsi gani Biashara zinaenda, hakunipa hisa lakini nilishiriki katika kuendesha Biashara, aliniruhusu kuonana na watoto lakini watoto wenyewe hwakutaka kukaa na mimi.


Mwaka huu mwanzoni miaka kama miwili baada ya mume wangu kunisamehe nilikutana na dada mmoja kwenye mitandao, alikua anashauri namna ya kumtengeneza mwanau, limbwata la kumuwekea mwanaume ili arudi, kulikua na shuhuda nyingi namna ambavyo watu wamefanikiwa, kwakua nilikua bado nampenda mume wangu na najua ananipenda basi niliamua kumtafuta, akanipa dawa ya kumuwekea mume wangu kwenye chakula. Kweli nilifanya hivyo.


Kwakua mume wangu mara moja moja alikua anakuja kwangu, anakuta chakula anakula basi nilimuwekea hiyo dawa, lakini mambo hayakuenda vizuri, baada ya kumpa ile dawa kwa w2iki kama mbili hivi mume wangu miguu ilianza kuvimba, alipelekwa hospitalini na kuambiwa kuwa figo zake zimefeli, walisema kuwa kuana sumu nyingi mwilini kwake alianza kusafishwa damu lakini haikuchukau muda mume wangu alifariki dunia mwezi wa pili mwaka huu. Nilimpigia yule dada aliyenipa ile dawa kumuuliza ni kwanini imekua hivyo akaniambia kuwa nimezidisha dozi, akakata simu haupetikana tena na wala ukurasa wake mpaka leo sijawahi kuuona na wala namba zake hazipatikani tena.


Baada ya mazishi ya mume wangu kila kitu kilizidi kuparanganyika, mume wangu aliacha wosia kuhusiana na mtu wa kusimamia mali za wanangu mpaka watakapotimiza miaka 18, sikua mmoja wao, sikupata chochote kwakua tayari tulishagawana kila kitu wakati wa talaka. ingawa bado napata huduma kutoka kwenye kampuni na Biashara ambazo aliacha mume wangu lakini kila siku namkumbuka, nilikua na ndoa nzuri sana lakini nikaja kuiharibu kwasababu ya tamaa na imani kuwa mume wangu nimemshikilia hawezi kuniacha, kila nikikumbuka nilivyoharibua maisha yangu sioni tena hata haja ya kuishi ila nalazimika kuendelea kujikaza kwaajili ya wanangu.


MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG