Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

KWAHERI MKE WANGU

  

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

SIMULIZI; KWAHERI MKE WANGU — SEHEMU YA KWANZA.


JOIN US ON TELEGRAM

Sikua najua kama mke wangu alitoka siku ile, nilirudi nyumbani na kufunguliwa mlango na dada wakazi, nilikua nimechoka na moja kwa moja nikaingia chumbani. Nilivua nguo nikikua kuwa mke wangu alikua jikoni kwani ulikua ni usiku na mara nyingi ndiyo mida yake ya kumalizia kupika. Lakini wakati natoka chumbani kuwasalimia watu ndipo niliposikia akigombana na Mama yake.


“Hivi kweli wewe unajua kabisa kuwa mume wako kasafiri, anarudi leo lakini hukao nyumbani hata kumpokea?” Mama yake alikua akilalamika.


“Wiki nzima mume wako hayupo unarudi asubuhi, leo Baba wa watu kapiga simu kabisa kuwa anarudi lakini hata hujali?” Mama yake alikua anafoka, mke wangu aliishia tu kukjitetea na kumuambia kuwa anyamaze kwani nitasikia. Mama mkwe wangu ambaye alikuja kwenye sherehe ya shemeji yangu mdogo wake na mke wangu alikua anaondoka kesho yake.


Nilikua sijaonana naye kwani wakati wa sherehe mimi nilienda Kigoma kikazi, kutokana na ratiba zangu nisingeweza kuhudhuria sherehe ingawa kwa kiasi kikubwa mimi ndiyo nilisimamia.


“Shikamoo Baba.” Binti yangu wa kazi alinisalimia, nilimuitikia hivyo huko chumbani kwa Mama mkwe wangu walisikia kuwa nimetoka, mke wangu alitoka chumbani kwa Mama yake akiwa kajifunga kifuani lakini kwa kumuangalia tub ado alikua na Makeup usoni lakini hata nguo ambazo zilikua ndani ya ile Khanga zilionyesha kuwa alikua katoka sehemu.


Nilijifanya sijasikia chochote, Mama mkwe alitoka na kunisalimia, nilijikaza sana, nikatoa zawazi nilizokua nimeleta, nikaongea na kufanya kama niko kawaida. Kichwani nilikua na mawazo mengi sana, mke wangu ni mtu niliyekua nikimuamini sana, nilikua nampenda sana, kutoka sawa lakini kurudi asubuhi? Hicho ni kitu ambacho kilinichanganya sana, usiku nilitaka kumgusa, sikua na hamu naye kabisa, nilikua nimechoka lakini nilitaka kumpima.


“Nimechoka mume wangu sijisikii?” Aliniambia wakati namshika nataka kufanya naye mapenzi.


“Umefanya nini mchana kutwa mpaka kuchoka hivi? Inamaana hujanimiss?” Nilimuuliza.


“Wewe nawe, si nimekuambia nimechoka, kwani ni lazima kila siku kufanya!” Alinijibu kwa ukali kidogo, akageuka pembeni, hakutaka tena nimguse,a lijifanya kukasirika na hatukuongeleshana tena mpaka asubuhi. Usiku mzima zikulala, akili yangu ilikua inawaza mambo yake, nilikua nawaza ni kwanini anasema kachoka wakati hana kazi, ni Mama wa nyumbani na tunamfanyakazi, tunaishi na mdogo wake, Mama yake alikuepo! Kuna kazi gani hapa za kumchosha.


Niliwaza sana, niliwaza alikua anaenda wapi lakini sikupata jibu. Ingawa sikua na tabia ya kumfuatilia mke wangu lakini baada ya ile siku nilianza kumfuatilia, kwanza aktika simu ambapo sikugundua chochote lakini pili katika maisha yake ya kawaida. Mimi ni mfanyakazi, lakini pia nafanya bishara, kutokana na kazi zangu mara nyingi nakua bize sana pia nakua ni mtu wa kusafiri sana, kwa maana hiyo nakua na muda mchache sana wa kuwa na familia yangu.


Pamoja na yote hayo lakini najitahidi sana kila nafasi ninayopata ya kuwa na mke wangu basi naitumia vizuri. Napenda kumtoa out, namhudumia kwa kila kitu, namjali na najali wanangu. Ingawa wanasoma bweni lakini kila nikipata muda nawatembelea, najitahidi kumridhisha mke wangu na ni mtu wa kumsikiliza sana. Sikupenda mke wangu kukaa nyumbani na kuwa Mama wa nyumbani, ndiyo sababu ya kufungua bishara.


Lakini tatizo likawa ni usimamizi, ikawa ukimuacha kwenye bisahara basi haichukui miezi ita inakua ishakufa, baada ya kuona si kitu ambacho anapenda basi niliamua kumuacha ili awe Mama wa nyumbani. Nilimfuatilia kwa muda bila kugundua chochote, siku moja niliaga kusafiri, sikua na safari lakini nilitaka kujua kama mke wangu nikisafiri huwa anatioka au la. Niliaga naenda Mwanza lakini sikuenda, nilitafuta chumba na kupumzika sehemu.


Niklikaa siku ya kwanza, kesho yake nilirudi nyumbani, mke wangu sikumkuta, sikumuulizia, nilijiafanya kama najua alipokua, nilichokua nafanya ni kuongea naye kwenye simu wakati Mdogo wake na binti wa kazi yupo. Nilijua kama kaondoka kuna uwezekano kaaga uongo kuwa anaenda wapo au hajaaga, hivyo kama ningeulizia basi wangempigia simu na kumuambia kuwa baba kaja anakuulizia.


Lakini kwa kuka akimya na kuongea naye kwenye simu wakati watoto wapo basi wangeaamini kuwa mimi najua alipo hivyo wasingehangaika kumuambia. Kweli mbinu hiyo ilifanya kazi, nilikaa kwa wiki moja pale nyumbani na mke wangu hakurudi mpaka ile siku ambayo nilisema kuwa nitarudi ndiyo alirudi. Niliumia sana lakini sikumuuliza kitu chochote, nilikaa kimya, aljishaua shaua sana mimi nikabaki tu kimya.


Nilianza kufuatilia kwa rafiki zake, ndipo niligundua kuwa kuna mwanaume ambaye alikua anatembea naye, si mtu mzima sana, lakini kanizidi umri na ni mume wa mtu. Anaishi na mke wake na katika kipindi chote ambacho nakua sipo basi wanakua wanakaa hotelini na mke wangu. Baada ya kuchunguza na kuwa na ushahidi wote niliamua kuongea na mke wangu, nilijua kabisa kuwa anaharibu maisha yake, nilidhani ni tamaa za kimwili au kutokana na ubize wangu hivyo sikutaka kuharibu ndoa yangu.


Siku moja usiku nilimuambia kuwa ninajua anachokifanya, mwanzo alikataa na kudai kuwa ni maneno ya watui lakini nilimuambia mimi si mjinga. Nilimuambia kila kitu nilichokua nakijua, kuanzia nilipogundua siku ya kwanza mpaka safari yangu ya Mwanza, nilimuambia sehemu ambazo wanakutania mpaka na chumba ambacho wanakutania, nilikua najua kila kitu kuhusu wao, nilikua nimekasirika sana.


Baada ya kuona kuwa najua kila kitu aliniomba msamaha na kuniambia hatarudia tena. Kwangu ilikua ngumu lakini nilimuambia kabisa kuwa nipotayari kumsamehe, kesho yake tukaenda kupima UKIMWI na kukutwa tuko sawa. Nilimuambia nimemsamehe, pamoja na uchungu niliokua nao lakini nilijua fika haiwezi kusaidia kama nikimtangaza mke wangu kuwa ni Malaya. Ni mke wangu, tena wa ndoa ya kanisani, ni kwanini nimtangaze wakati sikua tayari kumuacha? Niliwaza, ingawa mambo hayakua kama awali lakini kama mwanaume nilivumilia na kukubali kuwa nimesalitiwa na yaishe.


Tulikaaa kama wiki hivi, nilikua bado simfuatilii, lakini siku moja nikamsikia akiongea na simu, nilikua chumbani na yeye alikua nnje, alikua hajui kama nimerudi kutoka kazini na nilikua nimelala ndani. Alikua akuongea na huyo huyo mwanaume, ni kama mwanaume alikua analalamika kuwa amemuacha ghafla lakini yeye alikua anamuambia kuwa mimi nimejua hivyo hana namna ni bora kuachana kuliko kuendelea kupotezeana muda.


Mwanaume alikua anambembeleza sana, kwa namna mke wangu alivyokua anaongea ingawa alikua anakataa kataa lakini niliona kabisa kuwa hajamuacha huyo mwanaume. Niliona kama anataka kuonana naye, nilibaki ndani kimya bila kusema chochote, alipomaliza kuongea akaingia ndani aliniona nimelala, kwa sehemu ambayo alikua alijua kabisa kuwa mimi nimesikia kila kitu lakini sikumsemesha wala kumuuliza kitu, sikionyesha kama nimekasirika ingawa muda mwingi alikua anajishtukizia sana.


Sikutaka kukaa. niliona kabisa ni ujinga, mwanaume anatembea na mke wangu, anajua kuwa nimefahamu lakini anaendelea kumsumbua. Niliondoka jioni ya siku ile, kwakua nilikua namfahamu yule mwanaume nilijikuta naenda mpaka nyumbani kwake, niligonga mlango na kufunguliwa na mke wake, nilijitambulisha kama rafiki wa mume wake. Alinikaribisha vizuri, yule jamaa alikua ndani, kwa namna nilivyomuona ni kama alikua hanifahamu.


Alikua antembea na mke wangu na alikua anijui, nilisalimiana naye baada ya salamu nilimuomba tuongee nnje kidogo, nilitoka mpaka nnje nilipoua nimepaki gari yangu. Hapo ndipo nilijitambulisha vizuri na kumuambia kuwa mimi ni nani? Alishangaa kuniona, alijua kuwa nimekuja kishari, kwa nilivyomuona nilihidsi tu mke wangu alikua kaniponda sana, kana kwamba kaongea kuwa mume wake ni mtu mjinga mjinga, alishangaa kuniona kama bado ni kijana, nina nguvu na najielewa.


Alijiongelesha maneno mengi sana lakini nilimuambia kuwa sikuenda kwa ugomvi, nimeenda kumuambia aachane na mke wangu kwakua ni familia yangu na siwezi kuona ndoa yangu inaharibika.


“Wewe ni mwanaume, umeoa na unaonekana una familia nzuri, sidhani kama utafurahi kama mtu akija kukuvunjia familia yako. Una watoto, unafikiri mtu akiharibu familia yako watoto wataishije?” Nilimuuliza, alibaki kimya, aliishia kuniomba msamaha na kuniambia kuwa ataachana na mke wangu na hatamsumbua.


Alidanganya kuwa mke wangu eti kamuambia tumeachana, sijui mimi nina wanawake wengine na mambo kibao. Nilikua na hasira sana, sikutaka kuongea sana nilimuonya tu kuachana na mke wangu. Baada ya hapo niliingia kwenye gari na kuondoka. Ile nafika tu nyumbani nakuta mke wangu kakasirika, anaanza kulalamika kuwa mimi namdhalilisha, namtangaza kwa watu kuwa ana wanaume wengi, nimemdhalilisha kwenda kwa huyio mwanaume na mambo kibao.


Nilijua kabisa wanawasiliana na huyo mwanaume, nilimnyang’anya simu yake na kukuta kweli walikua wanachate naye.


“Yule fala wako kaja kunitishia, anasema kuwa nikuache, nakuonea huruma, hivi utaishije na mwanaume kama huyo?” ndiyo meseji ambayo yule jamaa yake alimtumia, walijibishana mara mbili tatu meseji nyingi zote za kunitukana mimi lakini sikujali, nilimumbia nataka aachane naye kama nataka ndoa yetu iendelee. Aliniitikia ataachana naye lakini bado alikua ananilaumu mimi kuwa nimemdhalilisha kwenda kuonana na mchepuko wake.


Mimi sikujali ilimradi nilshamuambia basi nilijua atanielewa. Kesho yake niliendelea na mambo yangu kama kawaida, lakini nikiwa ofisini nikiwa sina hili wala lile, mke wangu alinitumia meseji kuwa anataka tuongee. Kabla hata sijajibu iliingia meseji nyingine.


“Nimechoka, siwezi kuishi tena na wewe, mimi naona kila mtu achukue ustaarabu wake, nataka tuachane tugawane mali, nilikukuta huna kitu, hizi mali tumechuma wote, watoto nakaa nao mimi ila sitaki tena kuendelea kuishi na wewe, nimepoteza muda wangu mwingi sana na wewe, sitaki tena, nahitaji uhuru wangu….”


Wakati mzuri wa kufua nguo ni wakati ukiwa umepumzika nyumbani, mwisho wa wiki, wakati ambao huhitaji kuzivaa, ukifua nguo wakati unatoka unataka kwenda kazini basi utaishia kuvaa mbichi. Hivyo hivyo kwa kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” wakati mzuri kabisa wakukisoma ni ule ambao haujaingia kwenye ndoa, upo kwenye mahusiao ya kawaida au hata hujaingia kwenye mahusiano.


SIMULIZI; KWAHERI MKE WANGU — SEHEMU YA PILI


“Mimi najua kuoa tu sijui kuacha!” Nilimjibu mke wangu kwa kifupi, alinitumia magazeti ya meseji lakini sikusopma na wala sikujibu. Niliona kama vile kachanganyikiwa, kwanza sikuona kosa lolote la yeye kusema kuwa ananiacha, lakini poili hata kama kungekua na hilo kosa lakini tuna watoto, hivi ni kwa namna gani mwanamke anaweza kuamua tu kuivunja ndoa yake kwa namna ile.


Kama ni hasira, kama ni kumuacha nilipaswa kumuacha mimi kwani mimi ndiyo nilimfumania na kujua kuwa ana mwanaume mwingine. Nilitaka kufanya kazi lakini kichwa hakikua sawa kabisa, kila kitu nilichokua nikikigusa niliona hakiendi. Niliwasha gari na kurudi nyumbani, nilimkuta mke wangu kajaa tele, sikutaka kiuongea naye niliingia chumbani kujipumzisha lakini hata sikukaa sana, alikuija na kunifuata.


“Inamaana unanidharayu?” Aalianza kuongea, nilikua nimejilaza kitandani, nilinyanyuka na kukaa, nilimuambia akae ili tuongee.


“Hakuna cha kuongea hapa, mimi ninachotaka ni talaka yangu, kama huwezi kunipa basi ninajia pakuzipata, si kila siku unaniona mkjinga, nimekuchoka mimi sikutaki!” Asliongea kwa hasira, pamoja na hasira zote nilizokua nazo lakini niliona haitasaidia, nilijishusha na kumuuliza kiutaratibu tatizo ni nini? Mbona kama ni mambo madogo na ni vitu ambavyo tunaweza kuviongea na kuvimaliza.


“Kama ni kuchepuka mimi nimekusamehe, wewe ni binadamu, najua ulipitiwa, lakini tuna watoto, hivi tunatengeneza picha gani na umri huu kuanza kukimbizana kwenye talaka.” Nilimuambia kwa upole kabisa lakini hakunisikiliza, alifoka na kutioshia kufanya chochote, aliniambia kuwa kama ni talaka nitampa na mali tutagawana nusu kwa nusu kwani nayeye kasirikiki kuchuma.


“Usione nilikua nyumbani, kwakati unasafiri huko nani alikua anahangaika na watoto wako, nani alikua anahangaika na mafundi, nakuambia tutagawana upende usipende!” Aliniambia.


Kwa namna alivyokua anaongea niliona kama kikwazo ni mali, labda anaona kwakua vitu vingi vina majina yangu basi ndiyo nayeye anataka. Kusema kweli labda ndiyo kosa nililifanya, si kufanya kwa makusudi kuandika kila kitu kwa jina langu, hapana, niliandika tu na haa sikuwahi kufgikiria kuwa hiki ni changu hiki ni cha mke wangu au kudhulumiana. Mimi  nililelewa katika familia ambayo Baba alikua nio mtu wa kuchepuka, ni mtu wa wanawake wengi.


Nilikua naijua michepuko ya Baba yangu, nilikua naona jinsi ambavyo Mama yangu anateseka, pamoja na kwamba Mama alikua anaficha lakini kama mtoto wa kwanza wakiume nilikua naona. Tangu nikiwa mdogo niliapa kuwa mke wangu hatakuja ateseke, sitataka wanangu kupitia mateso ambayo nilipitia mimi. Kufikiria kwamba mke wangu anaweza kudhani labda nimeandika majina nyumba zote na Biashara kwakua nataka tukiachana nimddhulumu basi nili0na kama matusi na iliniumiza sana.


Nilinyanyuka na kwenda kwenye kabati, niltoa document zote za nyumba zangu na kumkabidhi.


“Chagua unataka nyumba ipi niandike jina laki, chagua hata mbili naandika, hizi mali zote natafuta kwaajili ya wanangu, si kwaajili ya Mama yangu wala ndugu zangu, nilishafanya majukumu yangu kuwasomesha, nilishamjengea Mama yangu na sina deni tena kwao. Deni pekee nililonalo ni kwako wewe mke wangu na wanangu, kama unaona unahitaji kubaki na mali zangu basi chukua, lakini siwezi kukupa talaka na kuacha wanagu kwenda kulelewa na mwanaume mwingine. Hapana, ni bora nife lakini sipo tayari kwa hilo!”


Nilimuambia, nilikua namaanisha, kwa namna mke wangu alivyokua pamoja na kunikosea lakini nililazimika kuwa mtu mzima na kujishusha. Si kwamba sikua na hasira, hapana, nilikua nazo tena nyuingi sana lakini nilijua hata ni kivimba na kupasuka isingesaidia kitu.


“Hivi tutagawana mahakamani nikisha kuacha, nimeshakuambia kuwa mimi sikutaki basi! Nakuambia talaka yangu utanipa, ni uamue mwenyewe, sikutaki, sikutaki kwanini huelewi?” Aliongea kwa hasira, alinirushia zile document za nyumba na kuondoka kwa dharau, sikutaka kumfuata, nilimuacha atulie kwanza.


Hatukuliongelea lile swala kwa wiki mbili hivi, nilijua mambo yamepita, lakini siku moja nilipigiwa simu na Mama mkwe wangu. Muda kidogo ulikua umepita tangu kuongea naye, kiukweli sikua na mazoea ya karibu sana na Mama mkwe wangu, mara nyingio maongezi yetu yalikua pale ambapo ananipigia, ananiomba pesa namtumia basi, hatukugombana lakini hatukua karibu kihivyo. Tangu kukor0fishana na mke wangu nilikua sijaongea naye, kwakua nilikua sijamuambia chochote nilijua ni salamu kama kawaida na mimi kumtumia pesa kama kawaida yake.


“Kama umemchoka mwanangu unamleta! Umemkuta mwanangu akiwa mzima kabisa, nimemtunza kwa shida, vihelahela vyako visikufanye kutudharau, au kwakua nakupigia simu nakuomba pesa ndiyo ukadnani sisi ni masikini kihivyo…” Mama mkwe wangu alianza kwa matusi, hakuitikia hata salamu ambvayo nilimpa, alitukana sana akinilaumu kwa kumpiga mtoto wake na kumuita Malaya.


“Ni kweli ni Malaya, hata mimi Mama yake ni Malaya kama ulivyosema, ila ninmachotaka ni unirudishie mwanangu akiwa mzima, kama umemchoka Baba si unasema!


Kila siku unasafiri, mwanangu anabaki nyumbani analia, anahangaika, nimekuja kwako nimekaa wiki nzima unarudi siku moja, eti unamtukana mwanangu unamuambia Malaya! Haya ni Malaya na mimi nimekukosea nini, unamuambia Malaya kama Mama yako kweli!” Mama mkwe alikua anaongea bila breki, maneno yake yalinichoma kwani ilikua ni uongo mtupu, ilionekana kuwa kuna mambo ambayo mke wangu alimpigia simu na kumuambia.


Alimpigia simu na kumuambia kuwa nimempiga, nimemuita Malaya na kikubwa zaidi kilichomuumiza Mama mkwe wangu ni mimi kumtukana yeye kwa kumuambia mke wangu kuwa ni Malaya kama Mama yake. Ni kitu ambacho hata mimi kiliniumiza kwani yule Mama alikua ni sawa na Mama yangu mzazi, hakuna kitu ambacho angekifanya ningeweza kumuita vile, mke wangu mwenyewe alikua kachepuka, kanisaliti lakini sikuthubutu kumtukana achilia mbali kumuita mapaya.


Pamoja na yote hayo lakini alikua bado ni Mama wa watoto wangu, hakuna namna ambbayo ningeweza kumdaliiisha wanamke na kumuita Malaya achilia mbali Mama wa watoto wangu. Nadhani kilichomuumiiza Mama mkwe wangu ni ile hali kuwa alikua na watoto watano ambao watatu alizaa na wababa tofauti na wawili ndiyo alizaa na baba mmoja ambaye ndiyo alikuja kumuoa.


Kuwa na Baba wa nne kwa watoto watano ni kitu ambacho nadhani kilimuumiza na kumfanya kumuamini mwanae kwa urahisi. Nilijaribu kumuelezea sana lakini haikusaidia, ni kama nilikua natwanga maji kwenye kinu.


“Siku zote nilikuona mtoto mwenye heshima, nilikua namuona mwanangu labda ndiyo mwenye matatizo, nilikua naona kama mimi ndiyo nimekosea kuoa lakini kwa mambo uliyomfanyia basi nataka umpe talaka yake, tuache sisi na umalaya wetu. Tena nimemuambia kabisa na watoto akuachie kwakua sisi hatiwezi kulea basi tusije kuwafanya na wanao kuwa Malaya.”


Aliongea sana, wakati anaongea nilijikuta natokwa na machozi, mke wangu alikua amenisaliti, kuna mambo mengi nilikua navumilia kwenye ndoa lakini lile liliniuma. Nilijaribu kumuomba msamaha lakini hakunisikiliza, aliongea mpaka akalia, uchungu aliokua anaupata niliizidi kuomba msamaha ingawa hata sikujua kosa langu lilikua nini? Mwisho nilishindwa kuvumilia, nilikaa simu, nakumbuka ilikua mchana, nilikua nakaribia kuingia kwenye kikao.


Baada ya kuongea na Mama mkwe wangu nilikua siwezi kufanya chochote. Nilimpigia simu secretary wangu na kumuambia kuwa siwezi kwenda tena kwanye kikao, nilimuambia atafute mtu mwingine wa kuniwakilisha na mgeni yoyote akija basi amuambie sipo. Nilifunga mlango na kuingia ndani, kusema kweli sikuwahi kulia hivyo katika maisha yangu, nilikaa na kulia kama masaa mawili, kila nikijaribu kutulia sauti ya Mama mkwe wangu ilinijia na kuaza tena kulia.


Baad aya kama masaa mawili nilijifuta nakutoaka, sikuongea na mtu nilitoka na kuelekea nyumbani, sikumkuta mke wangu, nilimkuta tu binti wa kazi na mdogo wake, sikuuliza chochote, walinisal;mia nikawaitikia kisha nikaingia zangu chumbani, nilikaa mpaka jioni sikuoak, mke wangu alitudi kwenye saa tatu usiku, alikuta nimshakula chakula cha usiku na nimeoga, aliingia ndani na kulala kana kwamba hakuna kitu kilichotokea.


“Umenifanyia mambo mengi sana mke wangu lakini hili sidhani kama naweza kukusamehe…” Nilianza kumuambia, hakujibu chochote, ingawa nilijua kabisa yupo macho lakini hakunijibu, nilijiongelesha sana, niliongea kwa uchungu namna ambavyo nimeumia kutokana na maneno yake, mambo aliyokua kamuambia Mama yake na jinsi yalivyonichoma lakini hakujali. Alilala usingizi, mpaka asubuhi niliondoka kwenda kazini na mke wangu hakunisemesha.


Ile nafika tu kazini meseji yake iliingia “Kama yamekuchoma basi nipe talaka yangu, kwa taarifa yako nitafanya makubwa zaidi ya hayo, nipe talaka yangu kabia sijakuaibisha, sikutakai, sikutaki!” sikujibu mseji zake, nilikaa kimya, nilikua na kazi nyingi sana siku hiyo ambazo nisingeweza kuziahirisha. Nilifanya kazi na nilipomaliza niliamua kutafuta safari, kulikua na semina ya kwenda Dodoma ambapo nilishamuambia msaidizi wangu kwenda lakini nilitaka kuwa mbali kidogo na mke wangu.


Nilimuambia ataenda semina nyingine, niliichukua ile, nilirudi nyumbani na kujiandaa, niliondoka siku hiyo hiyo. Mpaka wakati huo nilikua sijamuambia mtu yeyote kuhusiana na matatizo yangu na mke wangu kwakua nilijua ni upepo tu na utapita.


“Kwanini nimdhalilishe wakati sina mpango wa kumuacha!” Niliwaza, nilienda Dodoma na kukaa wiki nzima, bado mke wangu alikua akinisumbua kuhusu talaka lakini mimi nilimpuuzia.


“Nitakchokufanyia usijekunilaumu, mimi nimekuambia sikutaki, nataka tuachane na mali tugawane, labla sijaenda mahakamani nakupa nafasi ya mwisho!” Mke wangu alinitumia mseji, kama kawaida yake nilijua kuwa ni meseji ya vituko, nilifanya yangu Dodoma na kurudi Dar. Wakati nikiwa njiani niliwaza ni kitu gani kinamfanya mke wangu kufanya yote hayo.


“Labda ni upweke, unajua muda mwingi nipo safarini, tuahitaji muda wa kupumzika mimi na yeye tu. Nalazimika kuchukua likizo hata kama ni ya wiki mbili.” Niliwaza, niliporudi nilimuomba mke wangu kuongea naye, nilimuambia hata kama ni kweli anataka talaka lakini naomba kitu kimoja, achague nchi oyote ambayo tunaweza kwenda kupumzika na kama tukirudi na bado atadai talaka basi nitampa.


Ingawa ilikua ni ngumu lakini alikubali baada ya kama siku tatu hivi, aliniambia kuwa anataka kwenda Dubai, kwangu kusikia hivyo ilikua ni hatua kubwa, ingawa sikua na pesa kwa wkaati huo lakini nilijibana, nikasimamisha baadhi ya vitu nikasema hembu ngoja nikamuonyeshe mke wangu maisha. Mimi kila siku nakua ni mtu wa kusafiri nnje ya nchi na mikonai labda kaboreka kukaa nyumbani ndiyo kinampelekea kutamani watu wengine.


Nilifanya mipango na tulienda kweli, katika safauri nzima ya wiki moja mke wangu alikua na furaha sana na hatukuzungumzia mambo ya talaka tena. Kwa mtu yoyote aliyetuona asingedhani kama tuna matatizo, ilikua ni raha na kwa namna flani nilijihisi vibaya kuwa labda kutonana na mimi kumtelekeza mke wangu, kaucha kutoka naye mara kwa mara ndiyo maana amekua hivyo, anatamani maisha mengine ambayo sikumpa.


Baada ya kurudi mambo yalitulia kwa mwezi mmoja tu, mke wangu alibadlika, hakuzungumzia talaka na tulikua na amani. Lakini siku moja usiku tumelala mara mke wangu akaniamsha.


“Unajua sikuelewi?” Aliniuliza. Nilikua na usingizi sana hata sikujua alikua anazungumzia nini. Nilimuambia aache tulale lakini hakua tayari, alizidisha maswali.


“Uliniambia tukirudi utanipa talaka, lakini sasa hivi ni mwezi, umejifanya kusahau, au unafikiri nakutaka tena kisa umenipeleka dubai,kwa taarifa yako tukiachana nachukua mali na nitaenda mwneyewe si safari za kulazimisha lazimisha.”


Nilimsihi basi hata aache tulele mpaka kesho yake lakini aligoma, alikua siriasi kuwa anataka talaka. Mimi niligoma kutoa na kumuambia kuwa kama anataka talaka basi aanze yeye mchakato. Aliniambia kuwa hana shida lakini hataki mambo ya kudhalilishana.


“Mimi nilitaka tuniandikie kuwa umeniacha na unipe mali zangu, sitaki mambo ya kudhalilishana kwa watu!” Aliniambia, nilihisi labda anaogopa kuwa, kama akidai talaka basi nitamdhalilisha kwa kufumua mabaya yake, nilichukulia huo kama mwanya na kumuambia kuwa kama anataka talaka basi aanze yeye.


Alinyamaza na zilipita kama wiki mbili nyingine mambo yakiwa kimya. Lakini siku moja niliitwa na mchungaji wa kanisa letu, Baba mtu mzima ambaye ndiyo alitufungidha ndoa. Ni mzee amabye tunaheshimiana na kwakua mimi ni mchangiaji mkubwa wa ujenzi wa kanisa basi nilijua kuwa naitwa kwa mambo ya kanisa. Nilienda na kumsalimia, alinikaribisha ofisini kwake, baada ya kuongea ongea mambo ya jingo mwisho aliniambia kuwa mke wangu alikuja kulalamika kuwa anataka talaka.


Nilishtuka lakini sikumuonyesha, mpaka wakati huo ndiyo nilikua nashtuka na kuona kumbe kweli mke wangu alikua siriasi. Kijasho chembamba kilinitoka, nilikua nashindwa chakuonga, mchungaji aliongea mambo mengi kuhusiana na ndoa, maadili namambo kama hayo. Baad aya kumaliza kunielezea nilimuuliza.


“Kakuambia sababu ya kutaka kuchana na mimi?” Aliniangalia kwa wasiwasi na aibu, aliinama chini na kuniambia.


“Mwanangu hizo sababu za mke wako ndiyo zimenichanganya, sikuhukumu lakini hata mimi kama usipobadilika naweza hata kukubaliana na mke wako. Kanisa halitoi talaka lakini kwa unayoyafanya hata Mungu aliangamiza dunia kwasababu hiyo!”


Aliongea kwa sauti ya juu kidogo, nilishtuka kwani ilionekana kama mke wangu kaenda kwa Mchungaji na kanigeuzia kibao. Nilimuuliza alichokiona akawa kama ananishangaa kuwa sijui kitu.


“Mke wako kaja na picha, wewe unamtumia mwanaume mwingine picha zako za uchi, unafanya ushoga na mwanaume halafu unamsingizia yeye kuwa anakusaliti.” Kwanza nilishtuka, ni kitu ambacho sikukitegemea, lakini Mchungaji aliniambia wazo kuwa ni aibu, mke wangu alikuja ofisini kwake na picha ambazo mimi nimemtumia mwanaume mwingine nikiwa uchi wa mnyama na tukawa tunachat mamboa ya mapenzi.


Nilishangaa sana, lakini aliniambia kuwa mke wangu alihack simu yangu bila mimi kujijua na akaona picha na meseji nachata na mwanaume. Sikuamini nilijua kuwa ni mchezo tu, Mchungaji aliniomba simu yangu, nilimpa, akaingia Whatsapp, akaweka namba ambayo mke wangu alimpa, akaingia, ile namba nilikua sijaisave, lakini alipoiweka tu niliona kama kuna mtu nilichat naye.


Kilichotokea ni kama kuna mtu alichat na hiyo namba, kulikua na meseji nyingi za mapenzi, na ilionekana kama ni mimi nachat na mwanaume mwingine, namtumia picha, naongea namna ambavyo nafurahia kufanya naye mapenzi na yeye ananitumia picha za uume wake. Ilikua ni simu yangu, meseji zipo wala hazijafutwa na ilionenana ni za muda mrefu tangu kipindi tupo Dubai, kusema kweli nilishindwa hata cha kumuambia mchungaji kwani si mimi niliyechat na huyo mtu ila kila kitu kilikua katika simu yangu.


Kama ndiyo unataka kuanza Biashara unatakiwa kujua kuwa kuna tofauti ya pesa na mtaji. Unaweza kuwa na milioni 10 lakini isiwe ni mtaji wa Biashara na mwingine akawa na milioni 10 hiyo hiyo ikawa ni mtaji. Pesa inakua mtaji pale ambapo unaweza kufanya kitu ambacho kinaweza kuleta wateja ambao wanaendana na uwekezaji wako.


SIMULIZI; KWAHERI MKE WANGU — SEHEMU YA TATU!


Kuna mwanaume ambaye alikua anamsumbua mke wangu, alikua akimuaminisha kuwa kama akiachana na mimi basi atakua na furaha zaidi, alimuaminisha kuwa mimi ndiyo kikwazo cha kumpa yeye furaha. Alikua akimshauri mambo mengi, alikua anajua sharia kidogo hivyo alimuambia kuwa ili kupata talaka kirahisi basi ni kunitangaza kuwa mimi ni shoga na siwezi kufanya naye mapenzi, alijua kwa njia hiyo hata kanisa litakubali sisi kutengana.


Nilimsikiliza mchungaji kwa makini, kwa kuzingalia zile charting na kusoma meseji ambazo zilikua katika simu yangu nilijua kabisa kuwa mke wangu alikua kajipanga vizuri. Mke wangu hakutumia simu yake, alituia simu yangu kunipiga picha nikiwa nimelala na kuzituma kwa mwanaume wake kisha kuonekana kama mimi nachat na huyo mwanaume. Tayari alishanidhalilisha, nilijua kabisa kuwa yupo tayari kufanya makubwa zaidi ya yale.


Pamoja na kundihalilisha kote huko lakini bado alikua ni mke wangu lakini kubwa kabisa alikua ni Mama wa watoto wangu, kwangu hilo lilikua kubwa zaidi. nilijua ni shetani kamuingilia, nilikua na mambaya yake mengi na nilikua na ushahidi wa kila kitu, lakini isingesaidia chochote mimi kumuambia mchungaji, ningekua tu najitetea na katika kujitetea huko basi ningemdhalilisha na mke wangu. Sikuona sababu ya kuongea mabaya ya mke wangu na kumchafua mbele  za watu.


“Kwahiyo amesema anatka talaka?” Nilimuuliza mchungaji, niliongea huku nikilengwalengwa na machozi, nilijikaza sana kulia mpaka mchungaji aliona.


“Kuna nini mwanangu, mbona kama sio wewe kabisa, siamini kabisa kama unaweza kufanya kitu kama hiki?” Aliniuliza, nilijitahidi kunyanyua uso kumuangalia, nilitamani kumuambia kila kitu lakini mdoo uligoma kabisa.


“Naamini ni wakati wasisi kutengana, kwa hatua tuliyofikia sihdani kama kuna cha kuongea, kusema ni mimi au sio mimi hakutabadilisha chochote, nampenda sana mke wangu lakini ni wakati sasa wa kumuacha kuwa huru na kutokumfanya mateeka.”


Nilimuambia mchungaji huku nikinyanyuka, nilimuambia kama ni talaka basi nitampa mke wangu, nilimuambia kama alikua anataka ruhusa ya kwanda mahakamani basi ampe kwani sioni tena haja ya kuendelea na ile ndoa. Mchungaji alijaribu kunisihi sana lakini sikumsikiliza. Kikubwa alikua anataka nimuelezee upande wangu, niligoma kabisa kumuambia.


“Hakuna cha upande Baba Mchungaji, nadhani ni ndoa imefika mwisho, upendo ukishapotea hakuna tena cha nani kafanya hiki nani kafanya kile.”


Niliongea taratibu na kuondoka, nilirudi mpaka kwenye gari, niliwasha gari na kuondoka. Sikuweza kwenda mmbali nilifika sehemu nikapaki gari yangu kisha nikaanza kulia kama dakika 45 hivi, nilikua na hasira sana na sikutaka kwenda nyumbani nikiwa katika hali ile. Nilijua kuwa mke wangu anataka kuachana na mimi lakini sikujua kama anaweza kufanya kitu kama kile ili tu nimpe talaka. Nilirudi nyumbani nikiwa nimechoka sana, mtu wa kwanza kuonana naye alikua ni shemeji yangu, mdogo wake na mke wangu ambaye tulikua tunaishi naye.


“Semu unaumwa?” Aliniuliza, nilishtuka kwani mimi nilikua najiona kama niko sawa.


“Hapana, niko sawa.” Nilijibu kwa mkato, niliona kama kuna swali jingine anataka kuniuliza lakini sikumpa nafasi. Niliingia chumbani kwangu na kuanza kukusanya vitu vyangu, nilikusanya kila kitu ambacho niliona ni cha muhimu kwa wakati huo, nilivitoa na kuweka kwenye gari. Mke wangu alikua katoka, sikutaka kuondoka paka arudi, aliporuidi alijifanya kunisalimia vizuri, nililazimisha tabasamu ingawa halikutoka kabisa.


“Mbona uko hivyo? Unaumwa?” Aliniuliza, nilijikaza sana kumkasirikia, nilijikaza sana kutoa machozi lakini nilishindwa.


“Nimepata ujumbe wako kutoka kwa mchungaji, naona ni kweli umenichoka, nilitamani sana hii ndoa iendelee lakini naona kama ni kitu ambacho hakiwezekani. Mimi nadhani nibora nikikuacha uendelee na maisha yako, kwa sasa siwezi kuendelea kuishi na wewe hapa. Wakati tukifuatilia suala la talaka basi mimi naona niondoke. Nitakuachia nyumba na kila kitu.


Najua labda ni wewe ungependa kuondoka ila sidhani kama italeta picha nzuri hasa kwa watoto, nikiondoka mimi haitakua shida sana kwani wamezoea nasafiri safari. Hakuna haja ya kudhalilishana, najua ulichokifanya, kama umefikia hatua hiyo basi nitakua mjinga kulazimisha kuwa wewe bado ni mke wangu. Tuna watoto, tufichiane aibu zetu, haitakua na maana mimi kuanza kukutangaza au wewe kuanza kunitangaza, ukweli tunaujua sisi hivyo ni muhimu kila mtu abaki na ukweli wake.”


Niliongea huku nikibubujikwa na machozi, ingawa alijikaza kuonyesha kuwa hajali lakini niliona kabisa maneno yangu yakimuingia.


“Unaondokaje sasa, hii nyumba unaniachia tu nikae au ndiyo tunagawana? Vipi kuhusu Biashara, nataka unikabidhi Biashara yangu, tuachane kwa maandishi na si kwa mdomo, kama  vii tukagawane kabisa vitu kwa mwanasheria!” Aliongea kwa hasira, nilimuangalia mke wangu bila kummaliza, mpaka wakati huo nilikua sielewi kabisa sababu ya yeye kuniacha, yaani ishu ni mali au ni nini? Nilishindwa kuelewa ni kwa namna gani mtu unaweza kuvunja ndoa yako kwasabau ya mali!


“Kama ishu ni mali mke wangu naweza kukuachia kila kitu, sikuzaliwa na hizi mali, angalia kwenye droo kila kitu nimekiacha, kama ni suala la kugawana wala hakuna shida, hata ukitaka kesho nakuachia kila kitu! Wewe tafuta tu mwanasheria nikuandikishie kuwa nimekupa kila kitu, mbona rahisi sana, kama ni nyumba hata nikifa leo sitakufa nazo!” Nilimuambia nakutoka mule ndani, hasira zilinizidi nikaona kama nikiendelea kukaa mule ndani ningeweza kufanya kitu kibaya.


Niliingia kwenye gari na kuondoka, sikumuambia tu yoyote kuwa nimegombana na mke wangu. Kwa wakati huo nilienda kukaa gest na huo ndiyo ulikua mwanzo mpya wa maisha mengine. Nilishukuru Mungu sana wanangu walikua shuleni, bado walikua wadogo sana kuona mimi na Mama yao tuinagombana na kupitia yale maisha. Pamoja na kwamba bado nilikua nampenda mke wangu lakini nilijua kabisa imefikia mwisho, nilijua kuwa hakuna namna ningeweza kurudiana na mke wangu na tukaishi kama zamani.


****


Sikumuambia mtu yoyote kuhusiana na kutengana na mke wangu, hata ndugu zangu sikuwaambia. Mke wangu alikua na haraka sana, baada tu ya kumuambia nimemuacha alitafuta wakili, alianza mchakato wa talaka akitaka tugawane mali, kwakua sikua na pingamizi mchakato ulianza, kikwazo kilikua ni kanisani, ilihitajika barua kutoka kanisani kuwa wameshindwa kutusuluhisha, Mchungaji aligoma kabisa lakini tulivyorudishwa ustawi wa jamii wote tulisaini kuwa tunataka kutengena.


Alienda kufungua kesi ya talaka mahakamani huku akitaka tugawane mali nusu kwa nusu. Sikua na pingamizi na hilo, ingawa nilijua kuwa sio akili yake lakini na mimi nilishachoka, sikutaka kugombania mali. Tulikua na nyumba nne, mbili zilikua na majina yangu na mbili zilikua na majina ya watoto, hizo za watoto zilibaki hivyo hivyo na hizo mbili tukakubaliana kugawana, pia tulikua na maduka mawili yeye akachagua moja na mimi nikabaki na moja.


Mahakamani hatukupewa talaka, tulipewa Separation Oder ya mwaka mmoja wakituambia tukae tofauti kwa mwaka mmoja kisha ndiyo turudi kama bado tunahitaji talaka au la? Mambo yalienda harakaharaka sana, mke wangu alipewa nyumba tuliyokua tunaishi na mimi kubaki na nyumba nyingine, sikuhamia, kwani ilikua na wapangaji. Katika kipindi chocte hicho siokuongea chochote, nilikua nishaamua kuachana na mke wangu lakini sikuona sababu ya kutangaza matatizo yetu.


Nilimuachia Biashara moja akawa anaendesha yeye, pamoja na yote hayo lakini bado niliendelea kumpa matumizi, ingawa watoto walikua bweni lakini alikua anaishi na mfanyakazi na mdogo wake, nilijua kama nikiacha kumhudumia na yeye akawa anachukua pesa za dukani basi duka lingeweza kufa. Watoto waliporudi likizo walirudia kwake, mimi nilikua nimepangisha chumba na sebule.


Nilimuomba niende kuwasalimia watoto ili wajue tu kuwa Baba labda kasafiri kikazi tusiwaambie kama tumetengana lakini alikataa. Aliniambia ameshaniacha hivyo nilazima watoto wajue kuwa tumeachana kwani yeye hana mpango wa kunirudia ana mwanaume wake mwingine ambaye anasubiri talaka tu ili waoane. Nilimbembeleza sana lakini aligoma, niliumia sana kwani niliona watoto bado niwadogo sana kujua hayo mambo.


Hakuna siku ambayo niliumia kama siku ambayo mtoto wangu mdogo wakike alinipigia simu na kuniambia.


“Baba sikupendi, kwanini umemkimbia Mama, humtaki Mama Mpaka amepata Baba mwingine!” Kuna maneno ambayo mke wangu aliwajaza wanangu kuwa mimi ndiyo nimeondoka na kumuacha, mke wangu alikua analeta mwanaume wake ndani na analala hapo hapo kwenye nyumba yetu, kwakua watoto walikuepo basi walikua na maswali mengi hivyo ili kujisafisha aliwaambia maneno mengi mabaya kuhusu mimi kuwa ndiyo nimemtelekeza, siwataki hata wao ndiyo maana yeye akaaua kutafuta Baba mwingine ambaye anawapenda.


Sikua na jibu la kumpa mwanangu zaidi ya kumuambia nampenda, sikutaka kumponda Mama yake wala kuonyesha kwa namna yoyote kuwa Mama yake ndiyo mwenye makosa, nilijua kabisa kuwa nitazidi kuwachanganya wanangu hivyo nililazimika kukaa kimya. Likizo nzima hakutaka niwaone watoto, visa vilikua vingi, pamoja na kwamba nilikua ha hamu kubwa ya kuwaona watoto lakini nilikubali matokeo, nikaa kimya na kuacha mpaka wakarudi shule.


Huku nyuma maneno yalianza, alianza kusema nimeondoka nimetelekeza watoto, aliongea maneno mengi kwa ndugu zake na ndugu zangu. Mama yangu alinipigia simu kiniuliza kilichotokea lakini mimi nilimuambia kuwa hiyo ni ndoa yangu najua namna ya kudili nayo, ikutaka mtu kuingilia, rafiki zangu waliokua wananijua vizuri walikua upande wangu, wapo waliokua wanajua tabia za mke wangu, waliniambia niongee lakini nilikaa kimya.


Pamoja na watoto walikua shuleni, alikua akiishi na mdogo wake pamoja na mfanyakazi lakini matumizi yalikua makubwa sana tena kuliko kipindi ambapo tulikua pamoja, kila wakati alikua ni mtu wa kuniombaomba pesa, mwanzo nilikua natuma lakini baadaye niliona ujinga, kama nimemuachia Biashara ninampa pesa ya kununulia vitu vya ndani, ana mfanyakazi wa ndani ambaye hata hamhitaji, anaishi na mdogo wake kwanini mimi nihangaike kumhudumia.


Nilianza kupunguza matumizi, nikawa nampa laki tatu kwa mwezi, alikua akilalamika lakini sikujali sana. Ilikua imepita kama miezi sita hivi tangu kutengana na mke wangu, tulikua hatuijawahi kuonana zaidi ya kuwasiliana kwa simu tu. Siku moja nilipigiwa simu na jamaa mmoja hivi, ni rafiki yangu ambaye anafanya kazi Benki. Baada ya kunisalimiana aliniuliza kama kuna tatizo lolote, nilimuambia hakuna, aliniuliza sasa kama hakuna tatizo mbona imepita miezi miwili bila mimi kupeleka rejesho.


Kwanza nilishanga, katika maisha yangu ya Biashara nilikua sijawhai kuchukua mkopo, rafiki yangu huyo kila siku alikua ananishawishi lakini sikua tayari kwa hilo, nilikua najiweza na sikutaka usumbufu wa mikopo. Baada ya kumuuliza sana niligundua kuwa mke wangu alikua kafoji saini yangu, akachukulia mkopo nyumba aliyokua anaishi kwaajili ya Biashara.


Nilimpigia simu mke wangu kuongea naye akaniambia nikweli amechukua kwakua niyake na siwezi kumpangia. Nilimuuliza sababu akaniambia nikwakua Biashara ilikua ngumu akaamua kuchukua mkopo. Nilikata simu, jioni niliamua kwenda kuangalia duka la mke wangu, kuona kama biashara ilikuaje. Kwanza nililikuta lipo tupu kabisa.


Hakuna kitu kabisa ni jeupe, kilichonuiuma zaidi, nilimkuta mwanaume wake, yuleyule mume wa mtu ambaye nilimuambia achana na mke wangu kakaa ndiyo anauza, kusema kweli hasira zilinipanda kwani alikua akiniangalia kwa dharau, ananiona kama mjinga flani hivi. Watu waliokua wananifahamu waliponiona walianza kujisogeza, wote walikaaa kimbeambea, ni kama walijua nimekuja kufanya fujo wakawa wanasubiri nitafanya nini?


Kujichua ni moja ya sababu kubwa ya wanaume kupoteza nguvu za kiume, kwanza kunaathiri ubongo wa mwanaume kiasi kwamba hasisimkwi akimuona mwanamke wa kawaida lakini pili kunaathiri misuli ya uume kuweza kupitisha damu kwa urahisi na uume kusimama. Kuna stage 4 za kujichua, ni muhumu kuzijua kwani ukishafikisha stage ya 3 ni ngumu sana kurudia hali ya kawaida.


SIMULIZI; KWAHERI MKE WANGU — SEHEMU YA NNE!


Katika ule mtaa nilikua nafahjamika kama able ya pili, kila mtu alikua ananijua na kwakua nilikua naishi na watu vizuri wengi walikua wananionea huruma. Ni muda mrefu sana watu walikua wakinipigia simu na kuniambia mambo anayofanya mke wangu. Kwakua mimi ni mtu wa kusafiri safari walidhani labda sijui, hakuna aliyekua anajua kuwa mimi na mke wangu tushatengana, wengi walidhani anachepuka hivyo walikua wanaumia kumuona anakuja na mwanaume mwingine, wanafanya uchafu wao, wanakumbatiana na mambo mengine vilikua vinawauma.


Ile kuniona tu walijua kuwa kitawaka, nilijitahidi kuzuia hasira zangu, niijua kabisa kuwa wengi pale ni wanafiki hivyo hawatasiadia chochote. Nilisogea mpaka kaunta, duka lilikua tupu, kidogo nitokwe na machozi.


“Za saa hizi mheshimiwa?” Nilimsalimia, yeye alionekana kuwa na wasiwasi, alihisi kama nitafanya vurugu hivyo alijisogeza sogeza kutafuta kitu cha kuokota ili anipige nacho. Ingawa alikua mtu mzima kama mimi lakini kwa kumuangalia tu ukiangalia umbo langu nilimuona kama bwana mdogo tu hivyo hakuna kitu ambacho angeokota kingeweza kikanitisha.


“Salama, una shida gani, kama umekuja kwa shari utaipata….” Alianza kuwaka, aliongea maneno mengi, nilimuona kabisa anatetemeaka, mimi nilitulia na kumuambia si kwenda pale kishari, nilienda kuulizia kuhusiana na duka pamoja na mkopo waliochukua kwanini hawataki kupeleka rejesho nyumba inataka kuuzwa.


“Wewe inakuhusu nini? Hivi vitu ni vya mimi na mke wangu, wewe havikuhusi, nyumba si mmegawana, ikiuzwa wewe inakuhusu nini?” Aliongea kwa dharau kama Baba mwenye nyumba, nikikumbuka namna nilivyoijenga ile nyumba kwa shida nilitamani kummeza.


Nyumba waliyokua wamechukulia mkopo ni nyumba ambayo nilikua naishi mimi na mke wangu. Ndiyo nyumba yangu ya kwanza kuijenga, nakumbuka kipindi hicho hata sijaanza Biashara niliijenga kwa kudunduliza mshaara, nakumbuka wakati nanunua kiwanja hata kuoa nilikua sijaioa.


“Mlichukua shilingi ngapi na zimebaki shilingi ngapi?”  Nilimuuliza, alikaa kimya kwa muda lakini niliendelea kumkodolea macho, watu walikua wanaanza kuondoka taratibu baaada ya kuona kuwa hakuna vurugu yoyote.


“Unajua unatembea na mke wangu, najua unajiona mwanaume sana lakini mimi na wewe tunajua kuwa wewe si mwanaume, tunajua kuwa wewe humpendi mke wangu ila unapenda pesa zake ambazo ni zangu. Ninakuangalia tu kwakua namheshimu mke wangu, pamoja na ujinga wake wote lakini ni Mama wa watoto wangu, siwezi kumkosea heshima. Sitaki siku moja wanangu wamuangalie Mama yao na kusema Mama alikua Malaya, kwa namna ninavyompenda Mama yangu sitaki mtu amuone Malaya.


Nimejitolea kwaajili ya wanangu, ndiyo maana nimekuja kistaarabu. Mimi si mjinga, nyumba uliyomdanganya mkachukulia mkopo ni yangu, niliijenga kwa jasho la damu, siwezi kuiacha kuona ikiuza, nataka kujua kuwa mlichukua mkopo kiasi gani, sitarudia tena niambie kiwang0 cha mkopo mlichochukua na kwanini hamlipi?” Niliongea kwa utaratibu sana lakini kwa sauti yangu tu na namna nilivyokua nimepangilia maneno nilimuona kabisa anataka na kujikojolea, sikuonyesha hasira, alinijibu.


“Brooo mimi sihusiki, mke wako ndiyo alichukua, alichukua milioni sitini.” Alinijibu kwa kutetemeka.


“Mmeshalipa shilingi ngapi?”


“Mimi sijui, mke wako ndiyo analipa, sijui kalipa milioni kumi sijui kumi na tano.” Kwa eneo ambalo hiyo nyumba ilikua kiwanja tu huwezi kupata chini ya milioni 50. Wamechukua mk0po wa milioni 60, nyumba yangu ilikua kubwa sana, kwanza nyumba ya kawaida ya chini ambayo ndiyo nilianza nayo lakini katika kiwanja hicho hicho niliunganisha na kaghorofa. Ilinua na thamani ya zaidi ya milioni mia mbili na washenzi wanachukua mkopo wa milioni 60.


Sikutaka hata kuongea naye, nilikasirika na kuondoka, baada ya kuondoka nilimpigia simu rafiki yangu wa benki. Niliomba kuonana naye, mawazo yangu ilikua ni kumuambia kuwa, niache nyumba iuzwe lakini nije kuinunua mimi, ingawa sikua na hiyo pesa kwa wakati huo lakini nilikua tayari kukopa au kuuza kiwanja seemu nyingine au hata nyumba nyingine lakini nisiipoteze ile nyumba. Nilimuita na kuongea naye lakini aliniambia kuwa hilo si wazo zuri.


“Mke wako anachezewa akili, yule mwanaume si mjinga, ile sehemu wakubwa wengi wanaitaka, na tunavyoongea wameshatoa notsi ya mwisho, kama wasipopeleka rejesho absi nyumba inauzwa, na fununu nikuwa, yule mwanaume ndiyo kapanga kuinunua ile nyumba, alimdanganya mke wako ili wachukue mkopo akijua kabisa kuwa hawezi kuulipa, baada ya hapo ikitangazwa kuuzwa basi yeye anainunua. Hana hiyo pesa lakini kuna dada yake yuko NSSF ndiyo anaitaka watanunua shea.


Nillipoongea na wewe ukaniambia huhusiki niliamua kuchunguza, ndiyo hata nikajua kuwa kumbe hata umechana na mke wako hujaniambia. Huu ni mchongo wa muda mrefu, wanasubiri akosee tu nyumba iuzwe. Ubaya nikuwa kuna watu washaweka dau zaidi, yaani hata huyo mjinga hii nyumba haipati.”


“Sasa nifanye nini maana siwezi kuicha nyumba iuzwe?” Nilimuuliza.


“una machaguo mawili, ingawa mlitengana na mke wako lakini bado nyumba ina hati yako, kisheria wewe ndiyo ulitakiwa kusaini, lakini wamefoji sahihi yako yaani kila kitu kimefojiwa ili tu nyumba ichukuliwe. Unaweza kukataa kulipa ukaenda mahakamani tatizo nikuwa mke wako atahusika na kufoji ni kesi ya jinai.


Benki itapambana na hujui yataishaje, njia ya pili ni wewe kulipia marejesho yote, uzuri si lazima yule awepo, ukijua akaunti namba waliyokopea wewe unadumbukiza pesa tu wanakatwa juu kwa juu, huna hata haja ya kuwaambia.” Alinielezea vizuri, ningeweza kwenda mahakamani kweli lakini nilijua kuwa nitamuumiza mke wangu, sikua tayari kwa hilo, siku iliyofuata nilipeleka marejesho benki ya mpaka siku waliyotakiwa kulipa, niliamua kulilipa lile deni kidogo kidogo ili liishe.


Nilikua tayari kupoteza ile pesa lakini si kupoteza ile nyumba wala kumuacha Mama wa watoto wangu kuozea jela. Sikuogopa kuwa labda nikimaliza kulipia watampa mke wangu hati tena hapana, kwakua ilikua na majina yangu, walifoji mpaka sahihi kuonekana kuwa ni mimi nilikopa nilipanga siku naweka rejesho la mwisho basi naenda kuchukua na hati yangu. Niliendelea kulipa, sikumuambia mke wangu wala mchepuko wake, nilifanya mambo yangu kimya kimya.


***


Mke wangua likua ndiyo kila kitu kwangu, mimi nimfanyakazi, shirika moja la umma kubwa tu, kama unavyojua huko kazini madili yanakua mengi tu. Kwakua nilikua nampenda na kumuamini mke wangu basi wakati wote wa ndoa yangu nilikua nikimuambia kila kitu, namna ninavyopiga madili, namna pesa flani ilivyopatikana na kila kitu. Alikua ananisikiliza na alikua anajua kila kitu changu, lengo lang kubwa ilikua ni kumfanya kuniamini lakini wakati mwingine nilijitaji tu mtu wa kuongea naye.


Siku moja nikiwa kazini walikuja vijana wawili, waliomba kuongea na mimi. Mimi ni mtu mkubwa kidogo, si sana lakini ni mtu mkubwa flani hivi. Niliwakaribisha ofisini, waliingia lakini hawakutaka kukaa. Waliniambia wameamua kuja na kutoka na mimi kwa heshima kutokana na cheo changu na kwakua nilikua nafahamiana na bosi wao hivyo aliwaambia wanichukue kiheshima.


Walikua ni maofisa wa TAKUKURU, walijitambulisha na kuniomba niongozane nao, nilishangaa kwanini kwani kila kitu changu kilikua sawa wao walisema kuwa nahitajika nitajua mbeleni,. Nilitoka na kumuaga msaidizi wangu, tukaingia kwenye gari yao tukaondoka. Walinipeleka mpaka ofisini kwao, huko hawakunipokea kiheshima tena bali kama mtuhumiwa. Nilihojiwa TAKUKURU kwa masaa nane, nilipotoka pale nilipelekwa mahabusu.


Kwa mwenendo wa mahojiano yao nilijua kuwa tayari mke wangu ashaongea, mambo waliyokua wanahoji kuhusiana na mali zangu yote yalitokana na mambo ambayo nilishamuambiaga mke wangu. Nilikaa mahabusu kwa siku tano nimeshikiliwa bila dhamana, niliomba kuwa na wakili lakini waliniambia bado si mtuhumiwa, wananihoji tu, waliongea mambo mengi mengi nikaona kuwa ni bora kwangu kutokua na wakili kwani niligundua kuwa pamoja na mambo mengi waliyoambiwa bado walikua hawana ushahidi wakunipeleka mahakamani.


Baada ya siku tano waliniachia kwadhamana, lakini nilipotoka tayatri nilikua nimesimamishwa kazi mpaka uchunguzi utakapo kamilika. Kibaya zaidi walifungia akaunti zangu zote, nikawa sina pesa, Biashara zangu zote zilifungwa, kwababu ya kufungwa kwa Biashara zangu basi nilsihindwa kupata pesa kwaajili ya kulipia rejesho. Hapo ndipo nilielewa mchezo mzima, baada ya kuona nalipa rejesho inamaana kuwa isingewezekana wao kuninyang’anya nyumba yangu, walikasirika na kutaka kunikamata ili tu nishindwe kulipa rejesho na nyumba yangu kuuzwa.


Niliumia sana lakini sikukata tamaa, kilka wakati nilikua najiambia kuwa Mungu ataleta njia. Muda wa separation ulikua umeisha, mke wangu alienda mahakamani kudai talaka. Sikua na pesa na niliona kabisa nyumba yangu inaondoka, hapo ndipo niliamua kufunguka, mtu pekee ambaye ningeweza kumuambia akanielewa alikua ni Dada yangu wa Baba mkubwa, yeye alikua anafanya Biashara na ni mtu pekee ambaye nilijua kuwa anaweza kunishauri na kunisaidia hata kama atakua hana pesa.


Nilimpigia simu na kuomba kuonana naye, ni mtu ambaye tunaongea kila siku, ananiuliza familia namuambia iko sawa, naenda kwake ila mara nyingi anapotaka kuja kwangu namuambia sipo nyumbani hivyo kwa zaidi ya mwaka wa kutengana na mke wangu si yeye wala ndugu zangu walikua wanajua. Alikuja tukaonana na kumuelezea kila kitu, yeye ni mtu mzima kwangu kidogo na ana mwili wake umepanda vizuri.


Wakati namuambia alikua ananiangalia tu, ile namaliza kuongea alintandika makofi kama matano ya nguvu ya harakaharaka. Nikiwa nashangaa shangaa bado sijajua nini aliniambia.


“Nilsihakuambia tangu zamani mke wako umemdekeza sana mpaka amekua mpumbavu, huo si upendo ni ujinga! Haya sasa tushamalizana na mambo ya ndoa yako, nimetoa hasira zangu, sasa niambie unataka shilingi ngapi? Ukitaka kuachana na hao watu wewe maliza deni, niambie unataka ngapi? Sina pesa lakini Dada yako najuana na watu, nimedanga sana, nitaweka hata nyumba yangu dhamana kukusaidia, na ujinga wako wote lakini nitakusaidia, umenitoa mbali.


Kwenye familia yetu nzima sisi ndiyo wenye akili, ukifa wewe utaniachia mzigo mkubwa, hii ngoma tunaimaliza kesho kimya kimya, tunalipa deni lote kisha tunaanza na hao TAKUKURU!” Nilichokua nampendea dada yangu ni kitu kimoja, akiwa na hasira hata kama kashika chupa ya chai basi atakupiga nayo kichwani, atakutandika kisha hasira zake zinakua zimeisha hapo hapo. 


Alinisaidia mpaka kupata ile pesa, baada ya kuipata niliipeleka Benki ili kulipia deni langu lote na kulimaliza, mwanzo walinza kuleta mizengwe lakini nilimuambia meneja kuwa achague moja tumalizane au niende mahakamani kwani kila kitu kilifojiwa na yeye anajua kwani mimi kama mchukua mkopo nilikua sijawahi kufika kabisa ofsisini kwake. Hakua na namana, tulivutana sana lakini baada ya kama wiki mbili kila kitu kilimilika wakanirudishia hati ya nyumba yangu.


Kazi ikawa kwa TAKUKURU, walinisumbua sana, hawakua na ushahidi wowote, nilikaa miezi sita nazungushwa ni kuitwa kuhojiwa lakini mwisho waliniachia. Pamoja na kwamba nilikua namuambia mke wangu kila kitu lakini sikua mjinga kiasi hicho, nilikua nafanya mambo yangu kisomi na kubwa zaidi makaratasi yangu yalikua vizuri. Hakukua na ushahidi wowote, mali zangu zote zilikua zinaelezeka kwani nilikua na Biashara mbili, nalipa kodi na kila kitu kilikua kinaonekana.


Mpaka namaliza yote hayo ndugu zangu wote walishajua kuwa nimeachana na mke wangu, hawkaujua sababu lakini walijua hatuko pamoja, kama kawaida ndugu wakishajua kuwa ndiyo umeachana na mtu basi wanaanza kumponda na kukulazimisha kuwa umuache. Mimi sikuwajali, pamoja na yote lakini bado nilikua sipo tayari kumuacha mke wangu, yeye alikua anang’ang’ania sana talaka.


Baada ya ule mchongo wa nyumba kushindikana waligombana na mwanaume wake, waliachana na mwanaume akarudi kwa mke wake, mke wangu alikua hana Biashara, nyumba zina majina yangu hivyo akawa hawezi tena kuziuza au kuchukulia mkopo. Maisha yake yalikua hayaeleweki, mara kwa mara nilienda kuongea naye kumuomba ili tuudiane, nikidhani labda kajifunza kuwa maisha si rahisi kiasi hicho lakini hakukubali, aliishia kuniutukana akisema hanitaki.


Kikubwa yeye alichokua akikiongea nikuwa anataka talaka yake ili tugawane mali awe na maisha yake mwenyewe. Mke wangu alikua kachoka sana mpaka namuonea huruma, kibaya zaidi alianza kunywa pombe akawa ni mtu wa kukesha club usiku, hali hiyo ilikua inaniumiza sana kwani bado nilikua nampenda na kikubwa zaidi wakati wa likizo alikua akikaa na wanangu hivyo kuharibikiwa kwake ilimaanisha kuwa na wanangu wanaharibikiwa kitu ambacho kwakweli sikua tayari kukiona.


Ndugu zangu walikua wananishawishi sana kumuacha, ilifikia kipindi hata Mama yangu tukawa hatuongei, kila mtu alidhani nimelogwa lakini nilifanyakila kitu kwaajili ya Mama. Sikutaka wanangu kuteseka kwakua tu nimeshindwa kusamehe, lakini baada ya kuona kuwa haiwezekani nilikubali kutoa talaka ili kila mmoja awe na amani. Mimi nikawa nipo tayari ishu ikaja ni kwa mahakamana, bado wakawa wanatuzungusha kutokana na kushindwa kuelewana kwenye mgawanyo wa mali.


Baada ya mimi kukubali tulisumbuana kwa zaidi ya mwaka mmoja, ishu ilikua ni mke wangu na ndugu zake, mwanzo walikua wanataka mgawanyo sawa, kila nyumba na Biashara, mimi sikua na shida, ila walitaka mke wangu ndiyo abaki na watoto, niligomakaakata. Lakini baadaye niliona watoto wanateseka kwani tulikua tunasumbuana hapa na pale. Nikasema sawa, tutagawana na kwakua ni Mama yao basi atabaki nao.


Lakini tunafika mahakamani mke wangu kabadilika, akaanza kusema anachotaka kila kitu kiuzwe tugawane pesa. Niliona ujinga, siwezi kuuza nyumba zangu kisha nichukue pesa, tukasumbuana mpaka nikasema hapana, tulisumbuana mpaka ikafikia hatua nikachoka, nikamuambia kama unachotaka ni mali ziuzwe basi ziuzwe tugawane pesa. Hapo napo alikataa, akaanza kusema mimi na ndugu zangu tumepanga kuwa wakiuza vitu basi ninunue mimi, tumepanga kumzunguka.


Hali ile ilikua inanitesa sana, niliamua kukaa kimya, baada ya sisi kushindwa kuelewana mahakama ilipanga siku ya kutoa hukumu na kuamua mgawanyo wa mali uweje. Zikiwa zimebaki kama wiki mbili hivi kupewa hukumu mke wangu alikuja nyumbani nilipokua naishi. Bado nilikua nimepanga tu chumba na sebule, alikuja na kugonga mlango, nilimfungulia na kumkaribisha.


Tangu kutengana mara ya kwanza kabisa tulikua hatujawahi kukaa sehemu moja na kusema tunaongea, mara nyingi ilikua tunagombana, matusi na vitu kibao. Lakini siku hiyo alikua msataarabu kabisa, alikaa na kuanza kuniomba msamaha. Mimi nilimsikiliza tu,a kaongea sana kisha akamalizia na kitu ambacho kilinishangaza sana.


“Sitaki kuchukua hata shilingi, hata kama hutanisamehe utaniacha nataka mali zote zimbaki kwa jina lako. Mimi siwezi kutunza mali, zitapotea, au tuandike majina ya watoto wetu illi usimamie wewe, nimechezea maisha sana, siwezi kuishi bila wewe, siwezi kuishi na hizo mali.”


Hakua akilia, alikua anaomba msamaha na alionekana kumaanisha, aliongea mambo mengi sana, mambo aliyopitia, jinsi ambavyo marafiki wamemdanganya na mambo kibao. Nilimsikiliza sana lakini sikutaka kufanya maamuzi, nilimuambia aondoke anipe muda wa kufikiria. Aliondoka na kuniaga huku akiniambia kuwa, hahitaji tena mali zangu ananihitaji mimi hivyo hata kama akipata talaka basi hatachukua chochote.


Kusema kweli bado nilikua nampenda mke wangu, pamoja na mvutano mwingi lakini nilikua nampenda na siku zote niliamini kuwa atarudi. Lakini bado sikutaka kumuamini, nilihisi labda kuna mchezo anaucheza, sikumuambia mtu yoyote nilitaka kumchunguza kwanza, baada ya kama siku mbili hivi nilimuita nyumbani kwangu,a kaja tukaongea nikimuuliza kuhusiana na uamuzi wake, nilikua na mdodosa kutaka kujua kama ni kweli kabadilika au la?


Alikua mchangamfu sana, nilifurahia kampani yake kwa maana hiyo wiki mbli zile zote alikua anakuja kwangu na bila kujijua wala kupanga tulijikuta tunaanza kukutana kimwili, sikuwa nimemsamehe lakini nilitaka kumchunguza kwanza. Tuliendelea hivyo mpaka zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya hukumu. Alikua ananiomba saha tuiondoe kesi mahakamani, mwanzo sikutaka lakini niliongea na wakili wangu kuhusu kuomba kuahirishwa kwa hukumu kwani kuna mambo ambayo tunaweza kuweka sawa.


Kweli iliwezekana, ingawa kesi ilishasumbua sana lakini alikua anafahamiana na hakimu, ikasogezwa mbele kidogo. Nilipopata hizo habari niliamua kuenda kumuambia mke wangu, nilikua naenda nyumbani kwangu alipokua akiishi, yeye na Mdogo wake, Dada wa kazi na ndugu zake wengine wawili. Kufika alikua hayupo, kila mtu alinishangaa kwani ni muda sana nilikua sijakanyaga kwenye ile nyumba, binti wa kazi alikua ni mpya nilikua simjui.


Ndugu zake wengine nao nilikua siwajui zaidi ya kuniona, mtu pekee niliyekua nafahamiana naye alikua ni mdogo wake wakike, wakati huo yeye alikua chuo, kipindi natengana na Dada yake tulikua tunaishi naye na alikua sekondari. Alifurahi sana kuniona, unajua ile kama ya kuchanganyikiwa kabisa, alinikumbatia muda mrefu, akanikaribisha, akawa kama alikua na mambo mengi anataka kuniambia lakini hawezi.


“Umerudiana na Dada? Mbona umekuja hapa?” Aliniuliza, sikutaka kumjibu lakini yeye aliendelea.


“Nimemsikia Mama akisema akurudie, lakini usirudiane naye, usirudiane naye, acha kuwasikiliza!” ilinibidi kumkatiza kwani niliona kabisa anataka kuingilia mambo yangu, lakini kuna kitu ni kama alikua anajua ila sikutaka mtu aingilie mahusiano yangu. nilimuambia sijarudiana naye nilikuja tu pale kuongea.


“Shem wewe ni mjinga, dada anakupeleka paleka, usirudiane naye!”


Aliongea kwa hasira, ni kama alikua ananifokea kama mtoto, ilibidi nikasirika na kumuambia awe na adabu.


“Adabu ninayo kweli, hivi wewe hujiulizi kwanini anataka kukurudia, dada ni Malaya, naishi naye tu lakini ni Malaya, usirudiane naye!” Aliendelea kuongea, kidogo nimtandike makofi kwa kumkosea heshima dada yake, nilimkanya sana lakini hakuacha, aliendelea kuongea, mara akaanza kulia na kumzungumzia dada yake kuwa ni mshenzi.


“Kila mtu anamsikiliza, kila mtu anamuona malaika lakini ni mshenzi, Malaya mkubwa, ondoka muache ili aipate nawatoto wako chukua Shem!” Niliopoona viloe nilijua kabisa kuwa dada yake hayupo, nilinyanyuka na kutoka zangu lakini alinifuata.


“Shem wewe ni mjinga ndiyo Maana dada anakuendesha, mimi namvumilia kwakua tu ananilipia ada, ananiona mjinga lakini nitakachomfanyia kila mtu atanishangaa. Dada ni mshenzi, kaninyang’anya boyfiend wangu kwaajili ya vipesa vyake, kamuambukiza UKIMWI kaka wa watu na bado anajifanya ni ndugu yangu ananipenda, dada ni mshenzi shem mueche! Muache ateseke Mbwa mkubwa yule!”


SIMULIZI; KWAHERI MKE WANGU — SEHEMU YA TANO


Nilijikuta kama naishiwa nguvu vile, miguu iligoma kabisa kunyanyuka, nilisimama kama dakika tano hivi bila kunyanyua mguu, nilikua kama nimeganda. Shemeji yangu alikua anaendelea kuongea lakini sikua nikimsikia, kicwa kilikua mbali sana. Zaidi ya miaka mitatu ambayo nilikua nimetengana na mke wangu nilikua sijawahi kufanya mapenzi na mwanamke mwingine, tena si miaka mitatu tu, tangu nimuoe mke wangu nilikua sijawahi kumsaliti, pamoja na yote aliyokua ananifanyia lakini nilikua najisikia kinyaa kabisa kuwa na mwanamke mwingine.


Wakati wote tuliotengana na mke wangu nilijua ipo siku tutarudiana, sikutaka kuchepuka kwani niliona kuwa, nikichepuka kwa lengo tu la kulipa kisasi nitakua najidhalilisha mimi. Lakini nilikua na waza huyo mwanamke ambaye nitachepuka naye nitamdanganyaje, si nitakua nimemharibia maisha na yeye? Sasa ni kwa namna gani nimdanganye kuwa labda nampenda wakati upendo upo kwa mke wangu.


Sio kwmba nilikua sikutani na watu, sio kwamba nilikua sipati vishawishi, kwa pesa nilizokua nazo, kwa safari nilizokua nazo ilikua ni kawaida sana kutongozwa na wanawkae, tena mabinti wadogo na wengine wangi wazuri kuliko mke wangu. Lakini nilijizuia nikiamini kuwa ipo siku nitaruidiana na mke wangu na sitakua na kitu cha kuomba msamaha. Nilijitahidi nikatembea taratibu mpaka kwenye gari, niliingia na kukaa, nikafunga mlango lakini sikuondoka.


“Wanangu watalelewa na nani?” Ndiyo swali nililokua najiuliza nikiwa kwenye gari huku nikiwa nimelalia usukani.


“Wanampeda saana Mama yao, hivi kwelia natumia dawa, anafahamu kweli kuwa kaambukizwa, siku hizi ukitumia dawa haina shida sana, lakini namfahamu mke wangu, atakua na hasira, atakua anataka kulipa kisasi….” Nilikaa pale kwa masaa mawili, nilikua siwezi kuondoka, mke wangu alikuja na kuniona nipo kwenye gari, alifungua mlango wa upande wa abiria na kuingia, alinisalimia, nilikua nimepitiwa na kausingizi, nilinyanyuka na kumuangalia.


“Umekuja muda mrefu?” Aliniuliza, nilimuangalia nkitafuta hasira zangu lakini hazikuja, ilikuja huruma. Nilijikuta namuuliza.


“Umeanza kutumia dawa?”


“Dawa gani? Nani kakuambia kuwa naumwa?” Sliniuliza kwa ukali, sikumjibu chochote, nilimkata jicho flani mpaka akajua kuwa ninajua kila kitu. Niliona uso wake ulibadilika, alianza kuona aibu, alijaribu kulia lakini machozi hayakutoka, alitamani kuomba msamaha lakini sauti haikutoka, mimi niliendelea tu kumuangalia.


Kama unavyojua, ukimuangalia kwa nguvu mtu ambaye anamkosa basi anajiongelesha mwenyewe. Aliongea mambo mengi, aliomba msamaha huku akiniambia kuwa alikua hajui, mara alijua lakini alikua na hasira sana kwani alitaka kuniambukiza kwani ananipenda sana na hakutaka tuachane. Niliendelea kumuangalia aliongea maneno mengi lakini mimi kwangu bado swali lilikua ni lilelile.


“Umeshaanza kumeza dawa?”Alilizunguka hilo swali bila majibu, moja kwa moja nilijua kuwa hajaanza kumeza dawa, nilikasirika sana, si kwasababu nilihisi kaniambukiza bali kwakua nilijua anahatarisha maisha yake.


“Toka kwenye gari yangu!” Nilimuambia kwa hasira, alianza kuomba msamaha akijua kuwa nitamsikiliza. Nilirudia kumuambia atoke, alipuuza tena, nilishuka mpaka chini, nikaenda upande wake, nikafungua mlango na kumtoa nnje. Niliingia kwenye gari na kuwasha, nikaondoka mpaka kwa wakili wangu, kwa kawaida mimi si mtu wa kuongea mambo yangu lakini siku hiyo nilikua na hasira sana, ilikua ni lazima kuongea na mtu la sivyo ningeweza hata kuua kwa namna nilivyokua na hasira.


Nilimuambia wakili wangu kila kitu, sababu za mimi kutaka kuahirisha hukumu, na namna ambavyo mke wangu alikua kaniambukiza UKIMWI kwa makusudi. Kwa wiki mbili, kwa namna tulivyofanya mapenzi nilijua kuwa ni lazima nilikua nimeambukizwa, nilikua na hamu sana na mimi shughuli yangu si ya dakika tano. Alinionea huruma, akaongea, akatukana na kumuongelea maneno mabaya mke wangu, ingawa karibu yote yalikua ya kweli lakini nilijisikia vibaya, niliona kama anamdhalilisha mke wangu, nilijuta hata kumuambia kwani yeye alionekana kuwa na hasira kuliko hata mimi.


“Usimalaumu sana, mimi ndiyo nilishindwa kujizuia, hajaniambukiza makusudi bali mimi ndiyo nilikua mzembe, kwanini nisingelazimishia kupima!” Nilimuambia lakini hakuonekana kuelewa, alinishangaa na kuuliza hivi nina roho ya namna gani? Kwa namna alivyokua na hasira niliona kuwa hawezi kuwa msaada kwangu, sanasana ananiongezea hasira nizidi kumchukia mke wangu, nilitoka na kuingia kwenye gari, njiani mke wangu alikua anapiga simu sana na kutuma meseji nyingi lakini sikupokea hata moja wala kuzijibu. Mwisho niliona usumbufu unazidi nikaamua kuizima simu yangu na kurudi nyumbani.


Sikutaka kuwasiliana na mtu tena, nilipiga simu kazini na kupanga safari amabyo haikuepo, niliondoka na kuzima simu kwa wiki nzima, nilienda sehemu kupumzika nikijaribu kuwaza kuhusu maisha yangu. Nikiwa kule nilikutana dada mmoja, nakumbuka ilikua ni Baa usiku, walikua ni wale akina dada wa kujiuza, nilimnunulia pombe, tukaongea sana kiasi tukawa kama marafiki. Wakati wakuondoka niliondoka naye, kwa mara ya kwanza nilidhamiria kufanya mapenzi na mwanamke ambaye si mke wangu.


Kwangu kilikua kama kitu kipya sana, tulifika, tukapatana bei, nakumbuka aliniambia kuwa nitampa elfu hamsini, nilimpa hata kabla ya kufanya chochote. Alivua nguo lakini wakati wa kufanya tendo la ndoa nilishindwa, nilikua na mawazo mengi sana, hakunilazimishia, alivaa nguo zake na kutaka kuondoka kwakua nilishampa pesa yake, lakini nilimuomba asiondoke kwani nipo katika hali mbaya na nahitaji mtu wa kuongea naye.


Kwangu niliona kama yeye ndiyo mtu sahihi wa kuongea naye wkakua hatukua tukijuana. Nilianza kumuambia kila kitu kuhusu maisha yangu, mambo ambayo yalikua yananiumiza, jinsi nilivyokua nikiishi na mke wangu na jinsi ambavyo mke wangu alivyoniumiza mpaka kupelekea kuambukizwa ukimwi.


“Una bahati sana.” Aliniambia huku akitabasamu, kwa niliyomuelezea nilidhani kuwa atanionea huruma lakini aliona kama ni kitu cha kawaida.


“Kwanini unasema hivyo?” nilimuuliza.


“Kwakua wewe umeambukizwa UKIMWI lakini una watoto, unafamilia, una pesa na una maisha, mimi sina vyote hivyo, sina UKIMWI kama wewe lakini nimepitia mambo mengi sana kuliko wewe, unavyoniona hapa sina kizazi.


Nina mtoto mmoja ambaye nilizaa na mwanaume mtu mzima ambaye nilianza naye mahusiano baada ya kutoroka nyumbani. Baba yangu alikua akinibaka tangu nikiwa na miaka 12 mpaka nilipofikisha miaka 19 ndiyo nilikimbia nyumbani, nikaja mjini na kutafuta kazi, nikawa na Biashara yangu, nikajenga nyumba yangu na kufanikiwa. Lakini nikaja kukutana na mwanaume, Baba mtu mzima, akaniambia kafiwa na mke wake, tukaanzisha mahusiano.


Baada ya miaka miwili alinipa ujauzito, alinirubuni akachukua nyumba yangu akauza, alinipiga wakati nikiwa na ujauzito wa miezi sita mpaka mimba ikatoka na ikatoka na kiazi baada ya hapo alininyang’anya mtoto na kila kitu changu. Niliondoka kuanza upya, nilichanganyikiwa mpaka nikaanza kutumia dawa za kulevia, nimekua teja, mpaka sasa siwezi kufanya kazi nyingine, ni umalaya kwaajili ya pesa ili ni nunue dawa, nimejaribu kuacha nimeshindwa.


Sasa hivi unaniona nipo sawa, lakini mpaka asubuhi bila unga nitatetemeka hapa mpaka utanionea huruma. Kila siku nawaza kuacha lakini siwezi, nimejaribu imeshindikana. Wewe umetembea na mwanamke mwenye UKIMWI lakini haimaanishi kuwa una UKIMWI, ingekua unaambukizwa kirahisi namna hiyo na mimi ningekua mgonjwa. Unafikiri ni mara ngapi nimetembea na wanaume wakagoma kutumia kinga.


Wengine wakanibaka na asubuhi wakaniambia wameniambukiza, ninajirahidi kujilinda lakinikuna wakati inashindikana, lakini yote hayo sina, niko sawa, hembu kapime kwanza, jua hali yako na kama uko sawa basi ishi na wanao, acha kuharibu maisha yao kwakua yako yashaharibika.” Yule Binti alikua anaonge kwa uchungu sana, nilimsikiliza kwa makini na kusikiliza maisha yake mpaka nikajona kweli mimi nina bahari. Hakuongea sana aliondoka, nilijaribu kutaka kumsadia lakini alikataa.


“Siwezi kurudi huko Kaka yangu, unaonekana una nia nzuri, roho nzuri lakini haya ndiyo maisha niliyochagua kuyaishi, nimechoka kila mtu kutaka kunisaidia, wewe si wakwanza, kama unataka kusaidia nenda kamsaidie mkeo na wanao.” Aliondoka na kuniacha, usiku ule nilitafakari sana, asubuhi yake nilienda kupima, nilikutwa ni mzima, sikuamini, nikaenda kupima sehemu nyingine kama nne hivi, nako nilionekana kuwa ni mzima.


Niliambiwa kurudi kupima baada ya miezi mitatu, lakini kidogo nilikua na amani, nilirudi nyumbani kwangu, nikawasha simu zangu, kulikia na meseji nyingi sana lakini sikujibu hata moja. Baadaye wakili wangu alinipigia simu, aliniambia kuwa hukumu imetoka, mahakama imetoa talaka, tumegawana vitu nusu kwa nusu. Nilimuuliza kwanini wakati nilimuambia asuburi aliniambia alifanya mchakato huo harakaharaka kwakua anajua mke wangu kaniloga naweza kumrudia.


Kuna wakati nilidhani kama nitakua na furaha kwa kuachana kabisa na mke wangu lakini kusikia talaka imetoka niliumia sana. Ndugu zangu ambao walikua hawnaipati walinipigia simu, walinipongeza kwa kuachana na mke wangu lakini niliishia tu kuwakatia simu kwani sikuona raha yoyote. Siku ile sikua na amani kabisa, nilienda mpaka nyumbani kwangu ili kuonana na mke wangu, nilikuta tu binti wa kazi, mke angu alikua hayupo nyumbani.


Mdogo wake alishamfukuza baada ya kujua kuwa yeye ndiyo kaniambia kuhusu kuambukizwa. Nilianza kazi ya kumtafuta kwani niliambiwa kuwa ana wiki hajarudi nyumbani, nilimpigia simu zangu lakini hakupokea, niligangaika kumtafuta mpaka kumpata. Alikua yupo kwa rafiki yake, baada ya kupewa talaka ni kama alikua amechanganyikiwa, katika kipindi chote hicho alikua haamini kama nitamuacha, alikua bado ana matumaini kuwa nitamrudia hivyo kupata talaka kwake ilikua ni ngumu sana kukubali.


Niliomba kuongea naye lakini aligoma, aliniambia mimi si mke wake hivyo nisijue chochote. Aliniambia kuwa nimemnyang’anya na watoto hivyo hataki kunisikia. Hapo ndipo nilishtuka kuwa, kumbe katika hukumu mimi ndiyo nimeambiwa nitakaa na watoto na yeye ataruhusiwa kuwatembelea tena kwa ruhusa yangu. Nilikua na wakili mzuri na wanangu walipelekwa mpaka kwa Mwanasaikolojia na ilionekana mimi ni mtu sahihi kubaki na watoto.


Hicho kilikua kitu kilichokua kinaniumiza sana, wanangu kukaa na Mama yao niliona kama wataharibikiwa, alikua ni mtu wa kuwaambia maneno mabaya na kuwajaza chuki. Niliposikia hivyo na ukizingatia kuwa alikua hajali kuhusu mimi nilisema poteli ya mbali. Ngoja nimuache aendelee na maisha yake, mtu mwenyewe ndiyo alikua amenikosea lakini hataki hata msaada wangu, niliondoka pale kwa rafiki yake, nikarudi nyumbani kwangu, sikua na furaha lakini nilikua na amani kuwa angalau sasa hivi wanangu watakua sehemu salama.


*****


Nilijua kama ananikomoa, mke wangu aligoma kabisa kuwaona watyoto, baada ya talaka niliacha kufuatilia maisha yake isipokua wakati wa likizo ambapo watoto walikua nyumbani, nilikua nampigia simu ili kuonana na watoto lakini aligoma. Alikua analalamika kuwa nimemtenga hiovyo kama hana thamani kwangu basi nisubiri akifa ndiyo niwaambie wanangu kwanini nilimuua Mama yao. Nilikua naumia sana kwani mara kwa mara watoto walikua wakimuulizia Mama yao.


Hawakujua ni kwanini tumetengana ingawa walikua wakihisi kwani mara kwa mara walikua wakiniuliza kama nimekasirika kwakua Mama ana Baba mwingine. Niliwaambia hapana, nilijaribu kuwaambia kuwa Mama yao anawapenda na sio kama hataki kuwaona, lakini kama unvyojua watoto wa siku hizo, wanajua kila kitu, wakiona mambo hayaendi sawa basi wanajua. Nilichofanya ni kuwazungusha kwa Bibi zao ingawa nako ilikua shida, ilifikia kipindi nikaona nilazima nibaki na wanangu tu.


Ndugu zake nao walikua hawanitaki mimi na wanangu, walikua wakinilaumu kuwa nimemloga mtoto wao, nyumba tulizogawana alichukulia mikopo zikauzwa, Biashara zilikua zimekufa na hakuna aliyekua anajua kuwa anaishi wapi? mimi ndiyo nilionekana mbaya, ingawa nilikua naumia lakini kulikua hamna namna, ilikua ni lazima maisha yaendelee. Nilianzisha mahusiano mengi na kama mara tatu hivi lakini hayakudumu, sikuwa sawa kimahusiano, bado nilikua nampenda sana mke wangu.


Siku moja nikiwa kazini nilipigiwa simu na Mama mkwe wangu, nakumbuka ilikua siku ya jumapili lakini kwakua nilikua na kazi nyingi nilienda kufanya kazi. Kwanza nilishangaa, kwani haikua kawaida yake, kwanza alishaniblock, alishanitukana sana na kuniambia kuwa mimi ni mchawi na mambo kama hayo. Lakini nilijua kuwa ni hasiraza mzazi pale anapoona mtoto wake akiharibikiwa. Sikua na hasira naye, nilimsalimia vizuri lakini hata hakujibu, alianza kulia.


Moja ya vitu ambavyo naviogopa sana ni mwanamke kulia, huwa nasikiliza lakini nakua na huruma sana, kila wakati ninapoona mwanamke akilia namkumbuka Mama yangu, wakati akiwa mdogo, akipigwa na Baba yangu, alikua akilia sana lakinia kiniona ananyamaza, nikimuuliza sababu basi anaishia kuniambia. “Mwanangu macho yanauma, nikipata pesa nitanunua miwani.” Mwanzo nilikua namuamini lakini baada ya kujitambua niligundua kuwa tatizo si macho bali ni Baba.


Hivyo kila nikisikia mwanamke akilia naona kama nimekosea mimi, najikuta naomba msamaha bila hata kosa.


“Nisamehe Mama…. Huna haja ya kulia kwani kuna nini?” Nilianza kwa kuomba msamaha.


“Mwanangu, mimi ndiyo napaswa kukuomba msamaha…” Alishindwa kuongea na kuanza kulia tena, nilishindwa kuvumilia, niliweka simu pemebeni kidogo ili nisimsikie akilia, kisha nilirudisha sikioni.


“Najua amekukose, alakini mwenzakoa nakufa, usimuache, hawezi kuishi bila wewe, rudiana na mke wako. Ni mwanangu, naumia sana nikimuona katika hali hii, njoo hata uongee naye, mwenzako anakufa.”


Alianza kunielezea kuhusiana na hali ya mke wangu, alikua kazidiwa, virusi vishaanza kumtafuna kwani alikua kagoma kabisa kumeza dawa, alikua kakata tamaa amekua ni mtu wa kunywa pombe na kushinda Baa, kila siku Mama yake alikua ni mtu wa kupigiwa simu kwenda kumchukua kwenye baa mbalimbali. Mama yake alimshauiri sana kuja kuniomba msamaha angalau nimsaidie kimaisha lakini aligoma, alisema ni bora kufa kuliko kurudiana na mimi.


“Sasa Mama kama mtu hataki mimi nihangaike naye wanini?” Nilimuambia.


“Sio kwamba hataki, anaona aibu, yule ni Mama wa watoto wako, anaona aibu kwa aliyoyafanya, dunia ishamfundisha.” Aliniambia na kuanza kulia tena, niliweka tena simu pembeni kisha nikamuambia anipe muda nifikirie, nilikata simu kwani sikutaka kumsikiliza. Baada ya kukata simu, tofauti na siku nyingine ambapo ningejisikia vibaya na kumuonea huruma sijui ni kitu gani kilinitokea, siku hiyo sikusikia huruma kabisa, nilikata simu na kuendelea na mambo yangu.


Nahisi nilishaacha kumpenda mke wangu kwani baada ya hapo sikujali tena, nilishachoka na mambo yake na niliamua kuendelea na maisha yangu. lakini baada ya kama siku mbili hivi nilipigiwa simu. Alikua ni shemeji yangu, yule yule ambaye aliniambia nimuache Dada yake kwakua alimuambukiza UKIMWI mpenzi wake. Baada ya salamu naye alianza kulia, kidogo nikate simu lakini aliniambia.


“Shem njoo hata useme kwa heri. Dada kalazwa hospitalini, hali yake mbaya, ni mgonjwa na kapigwa huko Baa, najua aliyokufanyia lakini usiache afe kabla hujamsamehe, anahitaji msamaha wako.”


Katika Biashara, sehemu ya kufanyia Biashara inaweza kuwa ni ya muhimu kuliko mtaji wenyewe. Unaweza kuwa na wazo kuwa la kuleta kitu kizuri namtaji ukawa nao, lakini ukikosa sehemu sahihi wzo lako lisiwe na maana. Kwa mfano, unataka kufungua mgahawa wa kisasa lakini ukauweka sehemu ambayo idadi kubwa ya wateja ni watu wa hali ya chini.


SIMULIZI; KWAHERI MKE WANGU — SEHEMU YA SITA!


Sikuenda siku ile kumuona mke wangu, nilikua na hasira flani kutokana na namna ambayo ameamua maisha yake kuwa ya pombe. Lakini usiku sikulala kabisa, kichwani nilikua nawaza mambo mengi hasa wanangu, namna ambavyo watajisikia kama Mama yao akifariki wakati sijafanya chochote, asubuhi na mapema nilikua mtu wa kwanza kwenda hospitalini. Hali ya mke wangu ilikua ishatengamaa ingawa afya yake ilikua imechoka sana.


Nilikaa naye hospitalini mpaka kwenye saa tano hivi, alikua na majeraha kichwani, kisogoni pamoja na kwenye mkono, kipigo cha kichwani ndiyo kilimfanya kuzimia. Nikiwa pale ghafla niliwaona watoto wangu, walinikimbilia na kunikumbatia, lakini hawakunikumbatia sana, walimuona Mama yao akiwa kitandani kalala, walimkimbilia na kumkumbatia, wakaanza kulia, wakimpa pole na kumuonea huruma.


Muda mrefu ulikua umepita tangu wanangu kumuona Mama yao, tangu kuachana na mimi kupewa watoto ni kama alinisusia waoto, lakini walisahau kila kitu, wakasahau hata kama nilikua pale, wakaka akitandani, wakaanza kumsimulia mambo ya shule, zaidi ya nusu saa walikia na Mama yao, walisahau hata kama anaumwa, mke wangu alijitahidi sana kujizuia kulia lakini kila wakti nilimuona machozi yanamtoka.


Nilishindwa kuvumilia kwani hata mimi nilianza kulia, nilitoka nnje na kumkuta shemeji yangu.


“Kwanini umewaleta watoto, nani kawaruhusu shuleni?” Nilimuuliza kwa hasira kidogo, ingawa nilifurahi kuwaona namna walivyomfurahia Mama yao lakini sikufurahishwa na kile kitendo cha kuwachukua shuleni bila kunishirikisha.


“Mama yao angeweza kufa leo, unafikiri wasingetaka kumuona. Isitoshe dada hataki kuwaona watoto hivyo niliona ndiyo njia nzuri, hawezi kukataa kuwaona hapa hospitalini.”  Sikuendelea kumuuliza kwani nilijua anawapenda sana wanangu.


Tangu kutengana na Dada yake yeye ndiyo alikua kama Mama kwao, alikua anakaa nao mara nyingi wakati wa likizo mimi nikiwa nimesafiri, kwakua aliwalea tangu wakiwa wadogo nilikua namuamini. Niliondoka nikijifanya nimekasirika, nikaingia kwenye gari na kuanza kulia. Nilikaa pale kama nusu saa hivi, bila kujijua niliwasha gari mpaka nyumbani, nikaingia kabatini, nikachukua makaratyasi ya talaka, nikaenda jikoni, nikachukua kiberiti na kuyachoma moto. “Watoto wangu wanamhitaji Mama yao, siwezi kuendelea hivi, nahitaji kuwa na familia.” Niliwaza.


Baada ya kumaliza nilirudi hospitalini, niliwachukua wanangu na kuanza kuzunguka nao mjini. Niliwaambia kuwa hjawatarudi tena shuleni, watakaa nyumbani.


“Na Mama?” Ndiyo kitu ambacho waliniuliza, niliwajibu ndiyo na Mama, niliwaona jinsi walivyokua wamefurahi, walianza kuponda shule, namna walivyokua wanachukia kukaa bweni, waliongea sana, tulizunguka sana, nikaenda  mpaka shuleni kwao, nikaongea na walimu kuwa wanangu watakua wakisoma hule ya kutwa, sikuwa na haja ya kuwapa sababu, ulikua ni uamuzi wangu.


Aliniambia sawa lakini nisiwabadilishe ghafla niwape muda kwani walikua wamebakiza miezi miwili kumaliza mwaka. Nilielewa na niliona utakua ni wakati mzuri wa mimi na mke wangu kujipanga. Niliwarudisha shule na kuwaahidi hawatakaa bweni tena. Mke wangu alikaa hospitalini kwa siku nne, baada ya hapo aliruhusiwa, nilimchukua na kumpeleka mpaka kwenye kilinini ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWi, nilimuambia ni lazima kutumia dawa na nitamsimamia mimi mwenyewe.


Kwakua alikua hajaanza kunywa pombe akili yake ilikua sawa, alinielewa na kukubaliana na mimi. Baada ya kuondoka hapo nilimpeleka nyumbani kwangu, alishangaa na kumuambia kuwa ndoa yetu ilikua ni ya kanisani, imeunganishwa na Mungu hivyo hakuna binadamu wa kuitenganisha. Alishangaa sana na nilimuambia kuwa nitaishi naye kama mke wangu na nitahudumia mpaka arudie hali yake ya kawaida.


Sula la kumeza dawa lilikua gumu sana, ni kama alikua hataki, mke wangu alishakata tamaa na muda mwingi alikua akijutia mambo aliyokua amenifanyia. Kazi yangu kubwa ilikua ni kumpa moyo na kumhudumia, baada ya watoto wetu kurudi nyumba ilikua na amani, lakini bado hali ya mke wangu ilikua haijatengamaa, alichelewa sana kutumia dawa na aina ya maisha yake ya pombe tu bila chakula vilichangia.


Siku moja nikiwa kazini mke wangu alinipigia simu, wakati naondoka nyumbani alikua sawa kabisa, alikua yuko vizuri. Ainiambia niende kuwachukua watoto shule kwani anataka tutoke, nilimuambia kwanini asisubiri mpaka jioni ila yeye alisisitiza kuwa ni lazima tutoke mchana huo. bila kuwaza mara mbili nilienda shuleni, nikawachukua watoto na kurudi nao nyumbani, aliniomba nimpeleke Mlimani City.


Hali yake haikua mbaya kihivyo lakini alionekana kama ana kitu moyoni, nilifanya kama alivyotaka, tukaenda, tukala, watoto wakacheza na kufurahi. Kama saa kumi hivi aliniomba turdi nyumbani kwani anahitaji kupumzika. Niliwashagari na safari ya kurudi nyumbani ilianza, akiwa njiani alishusha siti kidogo na kulala. Nilimuacha alale mpaka nilipofika nyumbani, nikaingiza gari ndani, nikaenda upende wake ili kumuamsha.


Lakini mke wangu ndiyo alikua amelala moja kwa moja, alishakua wa baridi muda mrefu, niliangalia mapigo yake ya moyo yalikua hayapigisikutaka kupaniki mbele ya watoto, niliwashusha watoto na kuwaingiza ndani, walimuulizia Mama yao nikawaambia anakuja kapumzika. Waliingia ndani, nikatoka mpaka nyumba ya jirani, nikamuita jirani yangu ili anisiadie kuendesha gari kuelekea hospitalini.


Sijui kwanini, nilishajua kuwa mke wangu amefariki lakini nilitaka tu kumpeleka, jirani alikuja na kumuangalia, alikua kashafariki, aliniambia hakuna haja ya kumpeleka hospitalini lakini niligoma. Tulimpeleka na wao walithibitisha kuwa mke wangu alikua amefariki. Hapo ndipo chozi la kwanza lilianza kunitoka, niliumizwa sana na kifo cha mke wangu, alikua katika hali nzuri wakati anafariki, sijui ni nini kilimuua kwani hakuugua sana.


Pamoj na yote niliyopitia na mke wangu lakini nashukuru san Mungu alitupa nafasi ya pili, kwa takribani miezi nane ya kumuuguza mke wangu mimi na wanangu kama familia nimejifunza mengi. Mke wangu alihangaika sana lakini hakupata furaha ya kweli huko alipoenda lakini miezi nane ya kumuuguza naweza kusema kuwa mke wangu alikufa akiwa na furaha, lakini pia kaniachia mimi na wanangu kumbukumbu iliyobora, Pumzika kwa amani Mke wangu, Kwaheri mke wangu.


***MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG