Search This Blog

Tuesday, June 21, 2022

BABA WA KAMBO!

  

IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO

 

SIMULIZI; BABA WA KAMBO!—SEHEMU YA KWANZA


Katika maisha yangu ya kumfahamu mume wangu nilikua sijawahi kumuona akiwa na hasira kiasi kile. Alirudi nyumbani mchana kitu ambacho hakikua kawaida yake, mimi nilikua chumbani nimepumzika kwani tumbo lilikua linanisumbua. Aliingia chumbani bila kunisalimia, alitembea kama vile anelekea bafuni lakinialijigonga katika mlango, ni kama vile alikua haoni ingawa alikua kavaa miwani yake na hata kama asingevaa macho yake hayakua mabovu kiasi hicho.


JOIN US ON TELEGRAM

Alirudi na kukaa kitandani pembeni yangu, pamojja na mwanga hafifu wa mule ndani lakini nilimuona kavimba, anapumua kwa shida, anajaribu kuongea lakini hawezi, alikua aanajaribu kufungua vifungo vya shati anashindwa. Kusema kweli niliogopa, nilinyanyuka harakaharaka na kwenda kuchukua maji, nilimsaidia kufungua vifungo vya shati na kuanza kumkanda na maji ya baridi kwani alikua na joto sana.


Nilimpa maji mengine kunywa, alikunywa maji mengi mpaka nikayachukua, bado alikua akitaka kunyanyuka lakini hawezi. Sikutaka kumuuliza kilichokua kimetokea, nilitaka apumzike kwanza kwani nilijua kuwa kwa kumuuliza basi ningemkasirisha zaidi na labda kumfanya hali yake kuwa mbaya zaidi.


“Hawezi kuolewa! Mimi nampa kila kitu kwanini aolewe! Nasema hawezi kuolewa! Wanangu nitawachukua na hatawaona milele!” Aliongea kwa hasira, sauti yake ilikua kama inakwama kwama, sikuelewa alikua akimaanisha nini na ni watoto gani alikua akiwazungumzia.


Nilipaniki kidogo kwani nilijua kuwa alikua akizungumzia mwanamke mwingine.


“Unamaanisha nini? Nanni huyo hawezi kuolewa?” Nilimuuliza, alinigeukia na kuniangalia kwa mshangao, ni kama alishtuka flani hivi.


“Unazungumzia nini na wewe? sina muda wa kusikiliaza upumbavu wako, ondoka huko!” Aliongea huku akinisukuma pembeni, nilikua nimekaa pembeni yake bado nimshikilia Jagi la maji, nilipepesuka mpaka lile Jagi likadondoka na kupasuka. Hakujali, alinyanyuka kwa shida na kuondoka zake. Aliniacha nikiwa na wasiwasi, kwanza ni kutokana na hali yake aliyorudi nayo lakini pili ni kutokana na kutaja mwanamke mwingine na mtoto, sikujua alikua anamaanisha nini lakini nilihisi kitu kibaya.


***


Simu yake ilikua inatia tu lakini haipokelewi, nilimpigia sana lakini haikupokelewa, nilichoka na kuamua kumpigia rafiki yake. Iddi (Sio jina lake halisi) alikua ni kama ndugu yake, nilimpigia kumuuliza kama alikua kamuona mume wangu akaniambia hapana, alikua safari kikazi na walikua hawajaonana siku kama nne hivi, hata kuongea walikua hawajaongea. Nilizidi kupatwa na wasiwasi, nilitaka kuwapigia ndugu zake lakini nilisita, bado nilikua sijui kuna nini hivyo sikutaka kuwapanikisha niliamua kusubiri.


Nilisubiri sana mpaka ilipofika kwenye saa nane usiku bado mume wangu alikua hajarudi na simu yake sasa ilikua haipatikani. Nilipatwa na wasiwasi na kuamua kumpigia simu wifi yangu, nikiwa nimeshika simu ili kumpigia wifi yangu simu yangu iliita, ilikua ni namba ya mume wangu. Nilipokea harakaraka na kuanza kuongea, hakuwa mume wangu, ilikua ni sauti ya kike, mhusika alinisalimia vizuri na kuniomba samahani kisha akaniambia.


“Nina uhakika wewe utakua ndiyo mke wako, hembu njoo umchukue mume wako, kalewa sana hapa, watamfanyia kitu kibaya.”


Aliongea yule Dada, alionekana kutokutaka maneno mengi hivyo pamoja na maswali mengi kichwani niliyokua nayo nililazimika kuuliza kama alikua sehemu gani na nilipoambiwa hata hakusubiri niseme chochote alikata simu. Nilitoka na kuchukua gari, nikaelekea hiyo sehemu, haikua mbali, ilikua ni mwendo wa kama dakika tano hivi kwa gari. Ilikua ni Baa flani hivi ya uchochoroni, nilimkuta mume wangu kakaa wahudumu wamemzunguka pamoja na mlinzi, alikua kama kazimia.;


“Mmemfanya nini mume wangu?” Niliuliza, waliniangalia kwa mshangao na kadharau flani, nadhani wangenijibu vibaya ila walinionea huruma kutokana na hali yangu.


“Dada huyu kalewa, kaanza kunyw atangu saa kumi jioni mpaka sasa, kazima!” Kaka mmoja aliniambia, nilichanganyikiwa sijui hata cha kufanya, mume wangu alikua hanywi pombe, sio kunywa tu hata harufu yakke alikua haipendi sasa nilishangaa ni kwa namna gani kafika kule na kunywa mpaka kuwa kiasi kile.


“Nisaidieni tumpeleke hospitalini, huyu si mzima.” Niliongea huku nikijaribu kumshika, mume wangu alikua mzitro sana, mrefu, mnene na kwa namna alivyokua nilihitaji watu watatu ili kumnyanyua, Akaka mmoja alikuja kunisaidia, dada mwingine akaniambia nikae pembeni ili wamnyanyue na kumuingiza kwenye gari.


Lakini kabla ya kufanya hivyo mume wangu alishtuka. “Mnanipeleka wapi? Mnataka kuniibia? Nishasema haondoki, siwezi kuruhusu chochote! Mage haolewi na kama akiondoka watoto wangu ataniachia, ni Mama gani atakubali kuolewa akale stareghe na kuacha watoto wake kuteseka na Mama wa kambo? Nimesema haolewi na mimi wanangu hawatalelewa na Mama wa kambo, nimeshasema haolewi na kama anabisha anijaribu…” 


Aliendelea kuongea maneno amayo sikuyaelewa kwakweli, sikutilia maanani, alinyanyuka mwenyewe kwa shidashida mpaka kwenye gari, aliingia tukaondoka mpaka nyumbani ambapo alipofika alilala sebuleni, sikuweza kumuingiza chumbani. Bado alika anaonge vitu ambavyo nilikua sivielewi, alikua akimtaja Mage na watoto wake, hali hiyo ilinichanganya kwani kwa nilivyokua nikifahamu mume wangu hakua na mtoto ziadi ya huyu ambaye alikua na miezi sita tumboni kwangu.


***


Usiku ule nilishindwa kabisa kulala, niliingia chumbani na kutoka zaidi ya mara kumi, kichwa cahangu kilikua hakitakai kukaa sawa kabisa, mume wangu yeye alikua kalala fofofo anakoroma. Nilianza kumpapasa mifukoni na kuchukua simu yake, niliitoa na kwakua ilikua ikitumia finger print kufunguka nilichukua kidole chake na kuifungua. Niliangalia lakini hakukua na kitu, hakukua na simu wala nini aliyokua kapiga, miss call nyingi zilikua za kwangu, za rafiki yake Iddi na Mama yake.


Niliirudisha na kuingia mifukoni mwake, nikatoa wallet yake, sijui kwanini lakini nilianza kuikagua kutaka kuona kilichondani, nilikuta katikati ya vitambulisho vyake kuna laini ya simu, niliitoa  na kuweka kwenye simu yangu. ile kuweka tu mesejiz ilianza kuongia, ziliingia meseji kama tano hivi zote kutoka kwenye namba moja, ndiyo namba pekee ambayo iliseviwa kwenye ile laini.


“Baki na mke wako, nimechoka kuwa kinyago chako! Nina maisha yangu sasa, nilikuambia umuache mkeo unioe ukaringa sasa niemshaamua, naondoka na watoto wangu naondoka nao!” Meseji moja ilisema hivyo.


“Ndiyo nini kunificha ficha, wewe si ulikua unamuogopa Mama yake, nimeshakuambia watoto ni wangu na kama ukinisumbua nabadilisha mpaka majina ya Baba zao!” Ilisomeka meseji nyingine.


“Ulishaniacha na nilishakubaliana na hilo, mwanaume gani unakua na kisirani namna hiyo, nilikusaliti kweli lakini hata wewe si ulinisaliti, kwanini mimi nilikusamehe lakini wewe hukutaka kunisamehe! Kwanza nimechoka na huyo Mama yako, unamuona Mungu sana, ninaendelea na maisha yangu na kamwe sitaki kusumbuliwa!” Ilisomeka meseji nyingine, nilichanganyikiwa kabisa kwani sikujua ni nani huyo alikua anamtumia mume wangu meseji za namna hiyo.


Mwili ulikua unanitetemeka, nilitamani kwenda kumuamsha mume wangu ili anipe maelezo, nilitamani kujua ninui kilikua kimetokea huko nyuma lakini nilishindwa hata nifanye nini.


“Watoto unawaficha kama Bangi halafu leo unajifanya kuwataka kisa umeona na move ona na maisha yangu! Baba mimi ni yuleyule msaliti ambaye uliniacha kipindi kile kwa dharaau! Mambo aliyonifanyia Mama yako siwezi kusahau, hakujua mimi ni mwanamke mwenzake eti kisa tu nimepitiwa mara moja, tena wewe si mwanaume, sikutaki, utaendaje kumuambia Mama yako eti mchumba wako anagongwa na mwanaume mwenzako? Wewe mshanzi tu unikome!”


Niliacha kusoma, nilijiona nachanganyikiwa zaidi, nilichukua simu yangu na kuandika ile namba ksiaha nikairudisha ile laini kwenye simu. Nilirudi chumbani nikiwa na hasira sana, sikua na mtu wa kumuambia chochote, mume wangu alikua kalala chini hajielewi. Nilikaa macho mpaka saa kumi na mbili asubuhi, mume wangu bado alikua hajazinduka, ulikua ni muda wake wa kujiandaa kwenda kazini na kwa nilivyokua najua kazini kwao alikua na wageni, kulikua na wakaguzi hivyo niliona kama nisipomuamsha basi itakua shida kwake.


Huku nikiwa nimechanganyikiwa nilimfuata pale chini, nilimtingisha na kumuita, kwa bahati nzuri alinyanyuka, alikua bado na wenge la pombe, alijishangaa yuko pale chini. Aliniuliza nini kilikua kimetokea nikamuambia alikua kalewa, slishangaa lakini kabla hata ya kusema chochote alianza kutapika, nilikimbia hakarakahara na kumletea ndoo, alitapika sana. Baada ya kumaliza alienda bafuni kuoga huku nikimuandalia supu, nilimpa akanywa akaanza kujisikia vizuri.


Alijiandaa kwenda kazini ingawa alionekana kabisa kuwa hayuko sawa, wakati wopte huo nilikua nikivumilia nisiongee chochote kwani hasira zilikua zimenikaba. Alijiandaa na wakati natoka aliniona kama siko sawa, aliniuliza na hapo uzalendo yulinishinda nikaamua kumuuliza Mage ni nani na kwanini alikua anamtajataja kila mara.hapo ndiyo niliona zile hasira za jana yake, alianza kunitukana ananiambia kwanini namuuliza maswali ya kijinga jinga, wewe ni nani, umefanya nini, umejuaje, umeongea naye, umempigia na mambo mengine mengi.


Alikua amepaniki, anajikaguakagua. “Kama umempigia nakuua,a kiondoka nakuua! Kwanini unafuatilia mambo yangu! wewe umemjuaje!?” Aliuliza huku akinishika kwa nguvu, alikua akinitingisha tingisha na kunisukuma, mimi ni mdogo sana kwake na yeye kapanda juu  mwili mkubwa hivyo mikonmo yake kunishika mabegani alikua akiniminya sana, nilishindwa kuvumilia na kuwa kama namsukuma.


“Unataka kunipiga! Unataka kunipiga? Nakuuliza unataka kunipiga?” Aliuliza kwa hasira, nilimuambia hapana lakini hakunisikia, alianza kunitandika makofi ya nguvu. Alinipiga sana, hakujali hata kama nina ujauzito wake alikua ananipiga kila sehemu. “Kama ni kuondoka nawewe ondoka! Si mnataka kuondoka wote! Ondokeni niacheni mwenyewe na hao watoto siwataki tena! Si mnaona watoto dili sana!” Aliongea huku kwa makusudi kabisa akinipiga tumboni, alinipiga mateke mengi ya tumbo bila kujali nina ujauzito wake.


Nilijikunja na kukunjia kichwa changu na miguu kwenye tumbo langu lakini hakukubali, aliitoa na kunipiga tumboni, alikua akiongea maneno kuwa hataki tena mtoto, ataniua mimi na hao watoto wengine, anasema ni bora kubaki mwenyewe hahitaji tena mwanamke katika maisha yake! Alinipiga sana, nilianza kutoa damu mdomoni na puani, bado hakujali aliendelea kunipiga, niliona giza na macho kufunga na bado aliendelea kunipiga na niliendelea kusikia sauti yake akitukana kuwa hataki mtoto mpaka nilipopoteza fahamu kabisa.


SIMULIZI; BABA WA KAMBO!—SEHEMU YA PILI


Alinipiga mpaka nikapoteza fahamu, sikujua kilichoendelea mpaka mchana, kwakua aliacha mlango wazi jua liliingia ndani na hapo ndipo nilishtuka, nilikua nimeumia sana sikuweza hata kunaynyuka, macho yakikua hayafunguki vizuri. Nilijiburuza kwa kutamba ampaka chumbani na kuchukua simu yangu, nilitaka kumpigia mtu ili aweze kunisaidia, sikutaka kumpigia simu mume wangu kwani nilijua kingekua kipigo zaidi, kwa wakati huo mtu pekee niliyekua namuwaza ni Mama mkwe wangu.


Ilikua ni siku ya kazi, ndugu zangu sikutaka kuwaambia kwani niliona kama ni mambo ya kifamilia na Mama mkwe wangu ndiyo mtu pekee niliyekua nikimfahamu ambaye alikua tu nyumbani. Nilimpigia na kumuambia niko kwenye hali mbaya mwanae kanipiga, kwanza alipaniki hasa kusikia sauti yangu na kusikia neno kupigwa. Aliniambia nisifanye chochote anakuja, kutoka kwake mpaka kwangu ilikua nikama mwendo wa masaa mawili kama kuna foleni na nusu saa ukipanda bodaboda bila foleni, kweli alipanda bodaboda na baada ya kama dakika arubaini hivi alikua kwangu.


Nilishajinyanyua na kupanda kitandani, aliniangalia nilivyokua nimeharibika, damu zilinivimbiana mwili mzima, aliniuliza kilichotokea na kumuambia.


“Yule mshenzi hataki kumuacha mwanangu! Sijui kamlogea nini Mungu wangu!” Alilalamika, nilimuuliza ni mshenzi gani lakini alizuga na kujifanya kama hajui alichokua ameongea. Sikutaka kubishana naye sana kwa wakti huo, nilikua katika maumivu makali na kitu pekee nilichokitaka ni kwenda hospitalini hasa kuangalia hali ya mwanangu aliyekua tumboni.


“Hapana, hawawezi kukutibu mpaka PF3, kaaa hapahapa mimi nitakuhudumia.” Mama mkwe aliongea, nilitamani kumtukana kwamba anamuwaza mwanae mpaka wakati huo. Nilimuambia hapana, yeye anawaza mwanae lakini mimi namuwaza mwanangu, nilimuambia kamwe siwezi kubaki ndnai kwani mwanae kanipiga sana na nina wasiwasi kamuathiri mwanangu tumboni. Tulibishana sana akinibembeleza nisiende hospitalini lakini nilimuambia kama yeye ana uchungu sana na mwanae basi mimi nitampigia Mama yangu na naamini kabisa atakua na uchungu sana na mimi.


Alinywea na kukubali kunipeleka hospitali, alinikokota mpaka kwenye gari, aliingia na kuanza kuendesha. Mtaa wapili kulikua na hospitali lakini nilishangaa ananipeleka sehemu amabyo hata siijui, nilimuuliza akaniambia nisimsumbue ananipeleka kutibiwa na kama sitaki basi niruke kwenye gari lakini yeye hatasimamsiha gari. Alionekana kuwa na hasira sana na sijui zilitoka wapi wakati mimi sikumfanyia chochote, wakati akiendesha gari alikua bize sana na simu, alikua akimpigia mume wangu lakini hakupokea, aliishia kutukana tu.


Alinipeleka maeneo ya Mwananyamala, katika kituo kimoja cha afya, ilikua kama nyumba ya mtu lakini ilionekana inatoa huduma za afya, alinishusha na kunipeleka mpaka mapokezi, alionekana kufahamika, nilipokelewa na daktari na waliponiuliza kilichotokea alimshika daktari mkono akamsogeza pembeni wakaongea na aliporudi nilichukuliwa na kwenda kutibiwa. Walinipima vipimo vingi lakini mimi bado nilikua nawaza kuhusu mwanangu, nilikua naulizia kila saa na daktari aliniambia yuko sawa nisiwe na wasiwasi.


Pamkoja na maneno yake mazuri lakini kwa kumuangalia niliona kama kuna kitu hakiko sawa, alitoka na kuniacha pale, aliingia nesi na kuanza kunisafisha vidonda na kunichua. Walinitundikia Dripu mpaka sasa sijui hata ilikua ni ya nini, baada ya kunisafisha walinipa dawa za usingizi kwani nilishaanza kupiga kelele kutaka kupelekwa hospitali nyingine. Nilikuja kuzinduka usiku, Mama mkwe alikua pembeni yangu, aliniambia niko salama na kuniambia kuwa madaktari wamesema nitapona na mwanangu yuko vizuri hivyo nitulie.


Nilikubali kwa wasiwasi ingawa bado nilikua na maswali mengi, nilikaa pale hospitalini kwa siku tatu, vidonda vilikauka, sehemu nilizokua nimevimba zilikaa sawa nikaruhusiwa kuondoka. Mpaka wakati huo mume wangu alikua hajaja kuniangalia, Mama mkwe aliniambia nibora nirudi kwake. Nilirudi nikiwa na wasiwasi, aliniambia nisimuambie mtu kitu chochote kilichokua kimetokea, lakini hata nilipomuuliza ni kitu gani na huyo Mage ni nani Mama mkwe hakuniambia aliniambia niyaache hayo mambo atakuja kuniambia baadaye.


Nilinyamaza lakini katika kipindi hicho nilishangaa kuwa mwanangu alikua hachezi tumboni, nilimuuliza Mama mkwe akaniambia kuwa ni kawaida, lakini sikukubali kwani nilianza kuapta maumivu ya kwenye tumbo. Kila nilipomuuliza Mama mkwe aliniambia ni kawaida na kuniambia kama nataka basia nirudishe hospitalini, sikutaka kwani nilijua alipokua anataka kunipeleka, nilimuambia niko sawa lakini baadaye niliyoka mwenyewe nikachukua bajaji na kwenda mwenyewe hospitalini.


Kule waliniangalia na kuniambia kuwa mtoto alishakufa tumboni muda mrefu tu. Nilichanganyikiwa, nguvu ziliniishia nikapoteza fahamu. Nikiwa sina fahamu kwakua sikua na ndugu pale walichukua simua yangu na kuangalia, waliona namba ya mume wangu na kumpigia, wakamuambia kilichokua kimetokea na mpaka nazinduka alikua pembeni yangu. Alikua kaakaa anlia ananiomba msamaha. Hapo alikua mtu mwingine kabisa, akilia na kujutia huku bado akimlaumu Mage kuwa ndiyo kamsababishia yeye kuwa vile.


Nilikasirika zaidi kwani alikua anamtaja mtu ambaye nilikua simfahamu, alikua hataki kukubali makosa, kukubali kuwa ameniumiza yeye alikua anamlaumu Mage tu.


“Huyo Mage ni nani?” Nilimuuliza kwa hasira kwani alionekana kama kachanganyikiwa. Alikataa kuniambia akiniambia tuyaache hayo mambo yapitte, mimi pia nilikasirika na kumuambia kama hataki kuniambia kuhusu huyo Mage basi aondoke na sitaki tena kumsikia. Alitulia kidogo na kuamua kuniambia kila kitu kuhusu huyo Mage.


***


Walikutana na Mage kipindi wanasoma chuo SUA, walikua wakisoma kozi moja na walianza kuishi pamoja kama mke na mume ili kubana matumizi. Wakiwa mwaka wapili Mage alipata ujauzito wake wa mtoto wa kwanza, alijifungua mtoto wakike. Lakini alipoenda kujitambulisha kwao wazazi wa Mage walimkataa, walikua na sababu mbili, kwanza alimpa binti yao ujauzito kipindi bado yuko chuo, hiyo haikua kubwa lakini kubwa ilikua ni kabila.


Wazazi wake hawakutaka binti yao kuolewa na mtu wa lile kabila, mabli na hilo ilikua ni kuhusu uwezo wa kifedha, mume wangu kwao walikua ni watu wa maisha ya kawaida wakati kwakina Mage walikua ni watu wenye uwezo. Eric (Mume wangu/si jina lake halisi) aliumia sana kwani alikua akimpenda sana Mage, walirudi chuo na wazazi wake Mage walihakikisha kuwa hawaishi pamoja, hapo ndipo migogoro ilianza kwani pamoja na kwambaMage hakuacha kumpenda lakini Eric alianza kuwa na wivu, akawa hajiamini na kuanza kuwa kero.


Alianza kumchunga na kumkataza kuwa na marafiki, alikua akimbana kama mke wake na kumpangia kila kitu, Mage alikasirika na kuamua kumuacha, ukichanganya na presha kutoka kwa wazazi na tabia za mume wangu za wivu aliona hakuna tena raha kwenye mahusianao. Mwaka watatu akapata kijana mwingine, hakua akimpenda lakini kwakua aalitaka kumsamahau mume wangu na alitaka kumuonyesha kuwa hamtaki tena aliingia naye kwenye mahusiano na alifanya wazi wazi ili kuonekana.


Kuona vile mume wangu naye alitembea na rafiki yake makusudi tu ili kumuumiza, waliishi kwa kugombana hivyo lakini mwisho wa siku baada ya kumaliza chuo walikuja kurudiana, wakaombana mismaaha na kuwa pamoja. Huku wazazi wa pande zote wakiwa hawataki walianza kuishi pamoja na kupata mtoto wapili wakiume. Wakati huo Eric pekee ndiyo alikua anafanya kazi, ila baada ya kujifungua mtoto wapili Mage alipata kazi, sasa hapo likaja tatizo jingine.


Mume wangu alimuambia kuwa hataki afanye kazi kwani atamdharau, mume wangu ni ile aina ya wanaume ambao hawajiamini hivyo baada ya kuona Mage kapata kazi tena nzuri yenye kipato kikubwa kuliko yeye alianza maneno, Mage hakukubali, alianza kazi lakini mume wangu alizidisha wivu, ilifikia mpaka kipindi akawa anampiga wakapelekana polisi na wazazi wa Mage walienda kumchukua mtoto wao. Walisimamia kidete kesi mahakamani ya kumpiga na ilibaki kidogo mume wangu afungwe ndipo Mage aliamua kufuta kesi.


Waliachana lakini familia zote zikiwa hazipendani, hawakusalimiana na familia ya mume wangu iliwasusa mpaka watoto. Mume wangu alikaa miaka saba bila kuwa kwenye mahusiano ya maana mpaka tulipokutana. Hakuniambia chochote kuhusu kuwa na watoto na hata ndugu zake hawakutaka nijue, alikua msiri sana na sikujua hata ni lini walianzisha mahusiano. Alisema alikua hawasiliani kabisa na Mage, sio kwamba yeye alikua hataki lakini Mage alikua hataki, alishamtafuta na kumuomba msamaha mara nyingi lakini hakukubali.


Kuna kipindi alikua kama chizi na ndugu zake walidhani kuwa kalogwa lakini Mage hakutaka hata kumuona kitu ambcho kiliwakasirisha ndugu zake na kumuona Mage kama shetani. Baaada ya Mage kuona kama kaoa na ka move on na maisha yake ndipo alianza kumtafuta, alianza kwa kduai matumizi ya mtoto na kutaka awe na mahusiano na wanae.


“Nilishindwa kujizuia kwani nawapenda sana wanangu, nilimtafuta kwajaili ya watoto lakini nilijikuta naingia kwenye mahusiano naye, nisamehe sana mke wangu alikua ni shetani tu, haliwezi kujirudia tena.” Erick alimuambia mke wake ambaye muda wote alikua akilia kwa chungu.


Je atamsamehe mume wake, nini kimetokea mpaka Eric kufikia kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa. Kwanini Baba wa kambo? Hakikisha unafuatilia katika ukurasa wangu wa Instagram @iddimakengo ili kuwa wakwanza kujua na Facebook @iddi makeng


ITAENDELEA…


SIMULIZI; BABA WA KAMBO—SEHEMU YA TATU


Mume wangu aliniomba sana msamaha na kwa namna alivyokua anaongea na kujutia nilijua fika kuwa hawezi kurudia tena kunipiga kwani alishajifunza kwa kumpoteza mtoto. Nilimuambia ni lazima kukubali kuachana na Mage na kujua kuwa kama yeye ameoa na kaamua kuendelea na maisha yake basi ni lazima kukubali na kumuacha Mage kuendelea na maisha yake.


Tuliongea sana na alinikubalia kila kitu, lakini aliniomba kitu kimoja ambacho hata mimi nilimuelewa. Aliniambia kuwa pamoja na kuwa amekubaliana na Mage kuolewa lakini hawezi kukubali wanae kulelewa na mwanaume mwingine, aliniomba mimi kukaa na wanae kwani itakua rahisi kwake kuwahudumia. Sikua na kipingamizi, nilikubali harakaharaka nikiamini kuwa kama nikibaki nao itanisaidia mimi.


Nilijua kwa mimi kukaa na watoto basi itakua rahisi kwake kuwahudumia na hatakua na sababu za kuwasiliana na Mage mara kwa mara, kwangu ilikua ni kama kitu kizuri kwani kingenipunguzia wivu. Alienda kuonge na Mage, hata yeye hakua na kipingamizi kwani ni kama alikua anatafuta sehemu ya kuwapeleka watoto, ilionekana kama mchumba wake alikua hataki yeye kukaa na watoto na hivyo alitaka kuwapeleka kwao kukaa na wazazi wake.


Niliwachukua watoto na mambo yalikua mazuri, mume wangu alibadilika na kuwa mtu wa upendo, alianza kujali na muda mwingi alikua nyumbani, hatukugombana tena mara kwa mara kama zamani na baada ya kama miazi sita hivi Mungu alinijaalia nikapata ujauzito wa pili. Upendo uliongezeka na kila mara alikua akiniambia kuwa atakua makini kunitunza na kumtunza mtoto wetu mtarajiwa hatanigusa tena.


Ujauzito wangu ulipofikisha miezi minne nilianza kuona mabadilika, mume wangu alikua anawahi kurudi kazini kama kawaida yake lakini kila mara alikua bize na simu yake, ilikua ni kwa kuongea au kuchat na sikujua anachat na nani. siku ana yutaratibu wa kushika simu yake ingawa yeye alikua anashika simu yangu lakini hakua na passwed ila mara kaweka mapasswed kitu ambacho kilinishangaza. Niliamua kumuuliza lakini aliishia kuwa mkali, kwakua nyumba ilishakua na amani niliamua kunyamaza sikutaka kumkera tena.


Hali ile iliendelea mpaka nikaizoea, baada ya hilo likaibuka jambo  jingine la kutokuacha matumizi nyumbani, mara nyingi huwa tunanunua vitu vya mwezi mzima hivyo kunakua  na pesa ya mboga tu ambayo huniachia kila siku, alianza kupunguza kidogo kidogo mpaka akawa haachi, kumbuka nilikua naishi na watoto wake ambao tulikua tunaishi nao vizuri tu. Nilalamika alikua akikasirika na kusema pesa ni ngumu na mimi sijui kwakua ni kulakulala tu.


Kuna kipindi aliacha kutoa pesa kwa wiki nzima na mimi akiba yangu ilikua kama imeisha, nililazimika kupika maharage wiki nzima. Kwakua watoto hawakuzoea basi walilalamika, niliwaambia wamuambie Baba yao nikijua kuwa labda kwa namna ambavyo anawapenda basi wakimuambia wao atabadilika. Lakini mtoto alipoongea tu ghafla alianza kutukana.


“Pumbavu mkubwa! Mimi nahangaika kuwahudumia lakini hamna shukurani kama Mama yenu! Ananyanyaswa huko namsaidia lakini bado anaenda kuto*** mwanaume mwingine! Amekosa nini hapa mpaka kuniacha!” aliongea akitukana matusi makubwa makubwa, nilishangaa kwani aliulizwa kuhusu mboga lakini alijibu vitu vingine kabisa. Watoto walinyamaza na kukimbilia chumbani kwao, mimi nilimsihi kuwa sio vizuri alivyowajibu lakini hakunisikia, aliingia kitandani na kuniacha peke yangu sebuleni.


Niliondoa kila kitu nakurudi chumbani, ingawa alikua kitandani lakini alikua bado hajalala. Alionekana kama ana mawazo sana, nilimuuliza ni kitu gani kilikua kinamsumbua lakini alinijibu kwa hasira.


“Wewe lala na usitake kunitibua kabisa, fuata mambo yako, siaki kabisa kusumbuana, nilishakuambia sitaki kumuua mwanangu tena na unajua hasira zangu!” aliongea huku akinyanyuka, alitoka nnje, mimi nilibaki kitandani nikijaribu kupata usingizi lakini haukuja. Yalipita masaa mawili bado hajarudi nilipata wasiwasi na kuamua kutoka nnje kwend akumuangalia.


“Nimekuambia wewe ni mshenzi, yaani unamsaliti mume wako na mwanaume mwingine! Hivi hutosheki, unajua kuwa na mimi ni kama umenisaliti, kila siku unanipigia kuniambia shida zako, mimi ndiyo nahangaika kuchat na wewe lakini wewe upo bize na wanaume wengine! Hata kama mume wako hakutimizii mahitaji kwanini unahangaika na hao wengine….” Alikua akiongea kwenye simu, kwa namna alivyokua anaongea nilijua fika alikua anaongea na Mage.


Hasira zilinipanda na bila kujijua nilitoka nnje, aliponiona alishtuka na kuniambia niruidi ndani, sikua tayari kwa hilo nilimfuata na kumnyang’anya simu yake nikakimbia na kuingia ndani, ilikua bado haijajifunga, nilikimbia mpaka chumbani na kujifungia mlango kisha niakanza kuipekua. Niliona namba ya mwisho aliyokua anawasiliana nayo ilikua ni ya Mage, nilijua ni yeye kwani nilikua na namba yake, mara kwa mara alikua akinipigia simu kutaka kuongea na watoto wake.


Alikua akijifanya mwema na kujifanya kuwa hataki kuwasiliana na mume wangu kwani wameshaachana. Ingawa meseji zilikua zimefutwa lakini kwenya simu ilionekana kama wanapigiana simu kila siku. Nikiwa kule ndani alianza kugonga mlango kwa hasira akinitaka nifungue lakini sikufanya hivyo, nilikua na hasira sana, kwakua sikua na kitu cha kukiona katika simu yake, niliiruisha chini ya mlango ikatoka na kumuambia kuwa sitaki kulala naye chumba kimoja, nilipanda kitandani kulala.


Alilala sebuleni akijua kuwa nitafungua mlango lakini sikufungua mpaka asubuhi nilimkuta kalala kwenye makochi, nilienda kuwaamsha watoto ili kujiandaa kwaajili ya kwenda shule. Aliamka na kujifanya kukasirika, nilimuambia hata akikasirika mimi sijali kwani nimechoka, nilimkumbusha kuwa kashaachwa akubali kwanini anahangaika na mwanamke ambaye hamtaki.


“Kama angekua anakupenda asingekuacha! Kubali matokeo umeshaachwa achika!” Nilimuambia kwa haisra, alitaka kunipiga lakini nilimuambia kuwa hatanipiga tena katika maisha yake.


“Siku ukinigusa nahakikisha kuwa hutakuja kupiga mwanamke mwingine, ukinipiga jua nitaondoka lakini nitakua nishakuvunja uti wa mgongo!” nilimuambia, sikuwa lakini niliongea kwa ujasiri wa hali ya juu kiasi kwamba aliniamini. Alitukana sana lakini sikujali maneneo yake, mimi pia nilitukana tukawa kama tunatukanana, watoto walitoka na kutuona katika hali ile. Alipoona haniwezi aliwageukia wao na kuanza kuwatukana, walitoka na kukimbia kwenda shule kwani muda wote tulivyokua tunazozana walikua wakijiandaa.


****


“Wanangu wanaendeleaje?” ilikua ni sauti ya Mage, nilinyamaza kimya bila kusema chochote, kuna donge lilinikaba kooni na kutamani kumtukana, nilijua kabisa ananidhihaki kwani nilijua kama ni habari za wanae basi anazipata kutoka kwa Baba yao.


“Wanaendelea vizuri!”Nilimjibu kwa kifupi, sikusema maneno mengi, alijisemesha semesha sana lakini sikusema chochote, nilikua nikimjibu kwa kifupi sana, nilijibu swali kama alivyouliza bila mbwembwe zozote.


Alipona simchangamkii aliniaga na kukata simu. Jioni ya siku hiyo mume wangu alirudi akiwa amenuna, sikumuuliza kwani ilishaanza kuwa kama kawaida yake kujinunisha vitu mabavyo havieleweki. Lakini baada ya kuona simuulizi aliniuliza mimi.


“Hivi kwanini unapenda tusiwe na amani humu ndani? Unafurahia sana ukiniona nimekasirika?” Aliniuliza, sikujua alikua akimaanisha nini kwani nilikua sijafanya kitu chochote. Nilimuuliza alichokua anamaanisha lakini hakunijibu, nilijua anataka kubembelezwa sikufanya hivyo.


“Wewe ndiyo wa kumpa Mage majibu machafu namna hiyo?” Aliniuliza, nilishangaa ni majibu gani nilimpa,. Nilimuambia kilichotokea lakini hakukubali, alihisi kama namdanganya.


“Sasa usije ukalalamika ukisikia naongea naye, amesema hataki kuongea na wewe kuhusu mimi! Alitaka kuwachukua wanae, nisingembembeleza angewachukua na unajua sheria iko upande wake, yule ndiyo Mama yao!” Aliongea kwa hasira, mimi nilinyamaza huku moyoni nikijisemea wachukue tu, sikuona sababu ya kuendelea kukaa nao wakati bado walikua wanawasiliana.


Aliingia chumbani na kuanza kuongea na simu, sikutaka kumsikiliza nilirudi jikoni na kuendelea na shughuli zangu. Lakini kama masaa mawili baadaye alitoka chumbani, watoto walikua mezani wakijisomea, aliwaambia kutoka mezani na kwenda chumbani kulala, nilishindwa kumuelewa, alionekana kuwa na hasira zisizo na msingi hasa kwa watoto, ni kitu ambacho kilikua kimeanza ghafala nilishindwa kuelewa sababu ilikua ni nini?


Kunikasirikia mimi sawa, sikuona shida kwani nilijua labda Mage anamjaza maneno, lakini nilishangaa ni kwanini anawakasirikia wanae bila sbabau yoyote ile. Watoto waliingia chumbani lakini bado aliwafuata.


“Nitawafukuza mkamfuate Mama yenu hukohuko! Mna tabia mbaya sana na mimi siwezi kuvumilia kabisa!” Akllifoka, mimi sikumualewa kabisa kwani kusema kweli sikuona ni kwa namna gani walikua na tabia mbaya, sikua Mama yao lakini walijaa heshima, walikua wakinisaidia kazi na kila mara walionyesha kunipenda na nidhamu ya hali ya juu.


Nikiwa bado katika mawazo sijui nini kimetokea simu yangu iliita, alikua ni Mage, kwanza nilitaka kutokupokea lakini niliamua tu kupokea, nilipokea bila kuongea chochote, alianza kuita haloo…haloo… sikujibu nilimsikiliza tu.


“Najua unanisikia, lakini hutai kuongea, sina shida na wewe ila muambie huyo mume wako kuwa mimi si mke wake hivyo hawezi kunichunga, kama ni wivu basi akuonee wewe na si mimi. Nimemuambia nasafiri anafikiri kama naenda kwa mwanaume mwingine muambie anikome mimi si mke wake wa kumchunga chunga!”


Aliongea kwa hasira na kukata simu, sasa nilijua ni kwanini alikua kakasirika, nilishamuangalia muda mrefu, mara nyingi akichata kwenye simu muda mrefu na kukwaruzana na Mage ndiyo huja kwangu kwa hasirana kuwatolea hasira watoto wake. Nilikasirika na kumfuata, alisharudi chumbani, nilimpa ujumbe wake kutoka kwa Mage.


“Hata kama tumeachana lakini yule ni Mama wa watoto wangu, lazima nimlinde, hivi unafikiri anavyomsaliti mume wake akipata magonjwa unafikiri wanangu hawataathirika!” Alijiongelesha, mimi bado nilikua simuelewi kwani mimi hakua akinionea wivu kiasi kile.


“Mume wake kweli hamjali na wala hafanyi mapenzi nayeye lakini anachukua vijana waodgo tena wa bodaboda, nimefuatilia najua kuwa anatembea na watu wengine wawili, kuna magonjwa mengi siku hizi! Yeye ni mtu gani hashauriki, mimi namshauri kwa faida yake…” aliendelea kuongea kama chizi flani hivi, nilishindwa kumualewa ni kwanini bado alikua anahangaika na yule mwanamke.


“Wewe inakuhusu nini? Mume wake kutokumjali inakuhusu nini? Hjalafu umeyejulia wapi hayo mambo? Mtu mzima unakaa kutwa nzima unachata na mke wa mtu, hivi mimi nikichat na mwanaume mwingine utafurahi?” Nilimuuliza kwa hasira.


“Unaweza kuchat si unasimu kwani nimekukataza? Lini ulishaona nakufuatilia watu unaochat nao!” Aliongea maneno ambayo yalinikera sana, nilitamani hata kutapika, hakuonyesha kunionea wivu kabisa, niliumia sana kwa namna alivyokua akimpenda Mage, alishindwa kujizuia, kila mara alipokua akimzungumzia alikua akikasirika na kupata  uchungu mkubwa sana.


Nilishindwa kuvumilia ile hali na kutoka nikamuacha chumbani, nilienda kulala chumba cha wageni mpaka asubuhi. Siku iliyofuata ilikua ni Jumamosi, Mage huwa anakuja kuwachukua watoto na kukaa nao. Lakini siku ile hakuja kuwachukua na nilipomtrafuta wkenye simu kwani watoto walishajiandaa kwenda naye hakua akipatikana. Watoto walilazimika kubaki, mume wangu alienda kazini, aliporudi aliwakuta watoto na kuwauliza kwanini hawakuenda kwa Mama yao, nilimuambia alikua hajaja kuwachukua na alikua hapatikani kwenye simu.


“Atakua kasafri kweli! Huyu mwanamke ni mshenzi kabisa! Anawaacha watoto hapa halafu yeye anaenda kutom*** na wanaume wengine! Hivi ana akili kweli! Sasa hawa mbuzi wake anamuachia nani?” Aliongea maneno machafu tena mbele ya watoto, mimi nilijaribu kumsihi kupunguza ukali wa manano lakini hakujali, alianza kuwatukana watoto na kusema kuwa hawataki tenapale!


“Ondokeni na nyinyi, mnanikumbusha tu Mama yenu washenzi wakubwa nyie!” Alitukana hukua kiingia chumbani, hakuka asana litoka na kuanza kutembeatembea huku akishika simu yake kuanza kupiga na kutokana pale alipoambiwa kuwa simu haipatikani.


“Nampigia mume wake, ni lazima ajue mambo ambayo mke wake anayafanya, mimi nimechoka kumfichia siri zake!” Aliongea kwa hasira, lakini kabla hajafanya hivyo nilisikia honi, kuna gari ilikua inakuja, nilienda kufungua na ilikua ni gari ya Mage, mara nyingi anapokuja kuwachukua watoto haingii ndani, anapiga honi na watoto wanatoka. Watoto walikua ndani, mume wangu aliposikia honi naye alitoka, alimkuta Mage kakaa kwenye gari anaendeshwa na Makaka mmoja hivi ambaye alikua ni mrefu, mtanashat na wakuvutia flani hivi.


Nilimuona mume wangu akiwaangalia kwa hasira, Mage alishuka na kudai watoto lakini mume wangu alikataa kumpa. Alianza kutukana na kusema kuwa Mage kamdharau kwa kumjia na hawara yake pale, Mage alishangaa na kumuambia kuwa yule ni rafiki yake lakini hakujali, alianza kutukana hovyohovyo huku akimuambia yule kijana kushuka kwenye gari kwani lilikua ni gari lake kamnunulia Mage, nilishangaa kwani lilikua ni jipya na namba zilikua mpya kabisa, kwa kuziangalia zile namba nilijua kuwa limenunuliwa baada ya Mage kuolewa kipindi amenipiga na mimba yangu kutoka.


“Kwahiyo kumbe bado mnawasiliana mpaka kumnunulia gari?” Nilimuuliza lakini wala hata hakunisikiliza, akili yake yote ilikua ni kwa mage, alikua na hasira sana na yule kijana. Alitembea mpaka kwenye mlango wa dereva akaufungua na kutaka kumtoa yule kijana, lakini yule kijana hakutaka kutoka, aliusukumiza mlango kwa nnje na kumpiga nao mume wangu kisha akaufunga. Aliwasha gari na kutaka kuondoka lakini ile anarudisha nyuma kumbe Mage naye alikua mlangoni, upande wa abiria mlango umefunguliwa.


Alikua ni kama anataka kuingia lakini kwakua alikua hajaingia vizuri na yule kijana aliufungua mlango kwa nguvu, alidondoka chini. Kichwa kilishuka chini na miguu ikabaki kwenye gari hivyo akawa kama kavurutwa flani. Alipiga kelele “Nakufaaa!”….


Unataka kujua nini kimempata Mage? Kwanini Baba wa Kambo na si Mama wa Kambo? Usijali hakikisha unaendelea kufuatilia ukurasa wangu wa Instagram @iddimakengo kwa sehemu inayofuata.


ITAENDELEA…


SIMULIZI; BABA WA KAMBO!—SEHEMU YA  NNE


Mage hakua ameumia sana, alikua amevutwa tu kidogo na kuchubuka mkono huku mguu ukiwa kama umetenguka, lakini baada ya kudondoka chinia lipiga kelele nyingi, mume wangu alimkimbilia, akainama pale chini na kuanza kumbembeleza, alimnyanyua na kumkalisha chini huku akimuegemeza kwenye mapaja yake, alikua akimbembeleza akimuuliza kama alikua kaumia na kumuomba misamaha ambayo hata sikuilewa ilikua ya nini.


Wakati huo yule kijana aliyekua naye alishageuza gari na kuondoka.


“Nimekuambi huyo ni mtoto wa Shangazi yangu lakini una wivu wa kijinga, unaona sasa ulikua unataka kuniua!” Mage alifoka, alikua akijaribu kunyanyuka huku akijifanya kama vile kashindwa kunyanyuka.


“Mimi sikuamini, mume wako akisafiri unakua hupokei simu zangu, sas aunafikiri mimi nitajua unaendeleaje? Haiwezekani mume wako akiwpao unakua unanitumia mimi, kwakua anakuchunga unakua unachat na mimi lakini akiondoka hata simu zangu hupokei@”


Mume wangu alilalamika kama mtoto mdogo, hakujali hata kama nilikua pale, aliongea kama mwehu, nilishangaa kwani kwa namnaalivyokua akiongea alionekana kumpenda sana Mage, nilipata wivu nilitamani kuondoka nisione kilichokua kikiendelea lakini miguu hata haikunyanyuka.


“Nakuwa nimeenda kupumzika, nataka kupata upepo, mume wangu ananichunga sana, ni Malaya lakini mimi hataki hata nitoke, nikitoka kazini ni nyumbani na sasa anataka kuniachisha kazi kabisa!” Mage alilalmika, alikua kashanyanyuka.


Alitaka kuondoka lakini mume wangua limzuia, alimuambia kwa hali yake hawezi kuondoka na kumuambia aingie ndani.


“Kufanya nini? Ndani kwangu hawezi kuingia!” Nilijikuta naropoka, muda wote nilikua kimya ni kama hawakuniona, nilivyoongea hivyo ndiyo mume wangu alikua kama kashtuka, akajiumauma kujielezea lakini sikujali, niliingia ndani bila kusema chochote, baada ya kama dakika tatu hivi mume wangu aliingia, akachukua funguo za gari na kuondoka.


Hakurudi mpaka siku iliyofuata, alirudi asubuhi, nilikua nimechoka na sikutaka kumsemesha.


“Unajua jana aliumia sana na pale mume wake kasafiri ilibidi mimi kubaki naye mpaka ajisikie vizuri.” Mume wangu alijiongelesha, mimi sikusemesha kwa chochote, nilirudi zangu chumbani kulala, wka haisra nilizokua nazo nilijua naweza kumtukana na kuzua ugomvi tu. Mume wangu kuona vile alitoka bila kusema alikua anaenda wapi?


Alirudi jioni akiwa na furaha, alkua kachangamka na sijui hata ilikua ni sababu gani, nilimuuliza lakini hakujibu, alijichekesha chekesha tu na kuniambia nisiwe na wasiwasi kuanzia sasa mambo yatakua mazuri. Aliwaletea watoto zawadi na kuwalazimisha kufurahi, kwa kipindi kifupi walichoishi pale tayari wlaishaanza kumuogopa Baba yao, dakila moja alikua vizuri na dakika nyingine alikua anabadilika na kuwa kama mnyama hivyo walikua wana wasiwasi kila wakati.


Hakukaa sana alitoka na hakurudi mpaka siku iliyofuata, ilikua ni siku ya kazi lakini alikuja mchana.


“Kuna ile pesa nilikupa wiki iliyopita kwaajili ya kujifungulia umeweka wapi?” Aliniuliza, nilimuambia ipo ndani kwenye droo. Mara nyingi huwa akipata pesa hunipa kidogo akiniambia hiyo ni kwaajili ya maandalizi ya vitu vidogo vidogo pindi nikijifungua. Nilishakusanya kama milioni tatu hivi kama akiba, alienda wkenye droo kimyakimya na kuzihesabu zile pesa.


Alizichukua na kutaka kuondoka, nilishtuka na kumuuliza ni zanini na anapeleka wapi mbona alishanipa wkaajili ya maandalizi.


“Mimi si ndiyo nilikupa?” Aliniuliza, alionekana kama kukasirika mkidogo. Nilimjibu ndiyo basia katoka.


“Kama mimi ndiyo nilikupa basi ni zangu nazichukua na nikitaka nitazirudisha nisipotaka sirudishi!” Aliongea, nilitaka kuendeleza mazungumzo lakini hata hakujali, aliondoka zake na hakurudi tena mpaka baada ya siku mbili mbele.


Nilikua na wasiwasi sana, nilimpigia simu nyingi sana lakini hakupokea, ilifikia wakati akaniblock na akawa hapatikani. Aliondoka bila kuacha chochote nyumbani, pes ayote ya akiba alishaichukua hivyo sikua na namna zaidi ya kupika wali mkavu na wakati mwingine na maziwa, nilitamani kumuambia mtu lakini nilisita, nilijua kama nikimuambia Mama yake basi utazuka ugoomvi.


Alirudi nyumbani na kunipa elfu hamsini kisha akachukua begi, akachagua nguo zake nyingi nyingi na kuziweka, aliondoka bila kuniambia anaenda wapi? Nilimuuliza lakini aliniambia nimuache nisimuingilie maisha yake. Sikua nikimuelewa kabisa kwani ni kama alikua ananiacha.


“Unanitelekeza, kama umenichoka kwanini usiniambie nirudi kwetu?” Nilimuuliza, aliniangalia kwa hasira na kuniambia kuwa namtafuta.


“Unataka kuondoka na hawa watoto nani atawalea?kaa hapa na kama ukiondoka basi jua siji kukutafuta na ndiyo ndoa itakua imefia hapohapo!” Alinisukuma na kutoka, aliingia kwenye gari na kuondoka bila kuniambia chochote.


***


Tabia ya mume wangu kuondoka bila kusema anaenda wapi, mambo aliyokua akiyafanya kwa wakati ule vilinipa shida kidogo, sikumuelewa kabisa na nilitaka kujua nini kinaendelea. Kila akiondoka hakua akipokea simu zake, lakini nilikua lazima alikua ni Mage, tyangu Mage kuolewa alikua kama mtu aliyechanganyikiwa, alikua akifanya mambo ambayo hayaeleweki, kuchanganyikiwa kwake nilijua kuwa ni lazima Mage alikua anahusika.


Hizo lala lala zake nnje nilijua ni lazima anakua na Mage na kwakua anilishamsikia akisema kuwa mume wake kasafiri basi nilijua kuwa ndiyo sababu. Kwakua nilijua alipokua akiishi Mage sikupata shida kuchunguza, nilianza kufuatilia na kuja kugundua kuwa kumbe siku ambayo alikuja nyumbani na kutaka kugongwa na gari Mage alifumaniwa na mume wake. Wakati mume wangu anamchukua na kumpeleka nyumbani akijua kuwa mume wake hayupo kumbea alisharudi.


Alipoona gari ya mume wangu inampeleka na kwakua walikua wakijuana na mara nyingi alishamkanya kuwasiliana na mume wangu basi alimpiga Mage na kumukuza. Mage alipofukuzwa aliishia kumtafuta mume wangu na ndipo niligundua ni sababu gani siku ile mume wangu alirudi na furaha kwania lijua kabisa kuwa Mage kaachika. Niliumia sana kujua vile, nilimpigia simu mume wangua likua hapokei nikaamua kumpigia simu Mage, alijishaua kunisalimia vizuri.


“Najua unachokifanya ila kama umeamua kumchukua mume wangu basi njoo uchukue na wanao, sitaki kulea matatiozo ya mtu!” Nilimuambia lakini alinigeuzia kibao kuwa nawaita wanae matatizo, siwapendi nawanyanyasa na mambo kibao. Mimi sikumjali nilimuambia anatakiwa kuja kuwachukua watoto wake na kama hataki nitampelekea. Alinitukana na kuniambia nisimtishe kama ni watoto nimpelekee, nilimuambia ni wakwake basi aje kuwachukua kwani nimechoka nataka kuwa na amani na maisha yangu.


Nilikata simu kwa hasira lakini jioni yake Mage alikuja na kuniambia nimpe kila kitu cha watoto wake akawachukua, huwezi amini watoto walikua hawataki kuondoka, walikua wakinililia na kuniomba nibaki nao. Hali ile ilimkasirisha, alianza kuwatukana na kuwapiga, akawaingiza kwenye gari kwa lazima na kuondoka nao. Nilijisikia vibaya kwa watoto kuondoka, namna walivyokua wakiniangalia kuomba kubaki na mimi iliniumiza sana lakini sikua na namna ni Mama yao ni bora yeye kubaki nao na mimi kbaki na msalaba wangu.


Muda wote huo mume wangu alikua hayupo na sijui hata alikua wapi kwani alikua na zaidi ya sikutatu hajaruidi nyumbani, tangu alipochukua nguo zake hakurudi tena. Usik sikupika kwani hakukua na kitu cha kupika, nilikaanga tru viazi vya chips na kula, sikujua kama mume wangu atarudi, lakini kwenye saa nne hivi nilisiia honi ya hgari lake getini, nilitoka kwenda kufungua geti, nilifungua lakini kabla sijafungua vizuri mume wangu aalikanyaga mafuta kw anguvu gari likamalizia kufungua geti, nilikua nimeshikilia upande mmoja wa geti nilirudshwa juu juu na kudondokea pembeni.


Nikiwa bado pale chini sijajua nini kimetoke amume wangu alisimamisha gari, akaashuka na kunifuata pale chini, alianz akunipika makofi usoni na miguuni.


“Hivi unafikiri kwakua una mimba ndiyo siwezi kukupiga? Hivi unataka kunipanda kichwani, kwanini unafuatilia maisha yangu? wewe si unakaa kula na kunya bure hapa? Sasa kwanini uwafukuze watoto wangu? Nyumba yako hii mpaka unajifanya kuwa hutaki kukaa na wanangu? Umechangia chochote hapa mpumbavu wewe!”


Alinipiga sana hukua kinisomea risala, alikasirishwa na Mage kuja kuwachukua watoto wake! Alikua akinilaumu mimi kuwa nimewafukuza, aliongea mambo mengi sana, nilijaribu kujitetea lakini ndiyo kwanza nilikua napalia mkaa,a lizidisha kunipiga. Lakini hakua akinipiga kama mwanzo, safari hii alikua akinipiga sehemu ambazo anajua kabisa hawezi kumdhuru mtoto tumboni. Alinipiga sana kisha akaninyanyua na kunirudisha ndani.


Baada ya hapo alitoka nnje, kumbe watoto walikua kwenye gari, aliwatoa na kuwasukumiza ndani.


“Na nyie wajinga wajinga sio kila kitu mkiambiwa mnakubalia, mtakaa hapa! Hivi mnataka kumuua Mama yenu, ndiyo katoka kwenye matatizo lakini badala mumuache apumzike basi mnamng’ng’ania kama nini. Mtakaa na huyu mbwa mwenzenu hapa na nisikie mnaita Mama! Nitawaulia mbali, mambo gani haya kunyimana uhuru, nimesema mtakaa hapa na sitaki mtu kutoka!”


Aliongea maneno mengi sana lakini hata sikumuelewa, alikua na hasira mpaka anachemka, sijui hata kosa lilikua nini, alikua anapumua kwa nguvu mpaka nikaanza kumuonea huruma, likua akitetemeaka anashindwa hata kukaa, nilihisi presha imempanda, nilinyanyuka hakarakaharaka, nikamvua shati ksiha nikamkalisha chini, nilimpa maji na kuanza kumpepea kwani alionekana kutoa jasho kama vile alikua anakimbia muda mrefu.


Alitulia kwa muda ksiha akaanza tena kunilaumu.


“Utakuja kuniua wewe mwanamke, hivi kwanini huridhiki, kwani ni lazima kila siku kuhangaika na maisha ya watu, unakosa nini humu ndani, unakosa nini?” Alianza kuonge, ilinibidi kumuomba msamaha ingawa hata sikujua kosa langu, aliongea maneno mengi sana mimi niliishia tu kumsikiliza bila kusema chochote zaidi ya kuomba msamaha kwani nilijua kama sitaishia kupigwa basi anaweza hata kuzimia.


Baada ya kuona sisemi chochote alinyanyuka na kuingia chumbani, alichukua nguo zake nyingine na kutoka bila kusema kuwa anaenda wapi! Nilipandwa na hasira lakini nilijizuia, sikutaka kufanya chochote kwa wakati ule kwani nilishchoka na sikutaka kupigwa tena. Nilisimama mpaka niliposikia anawasha gari akaondoka, nilienda kufunga geti, bahati nzuri halikua limeharibika, nilirudi na kukaa kwenye makochi.


Muda wote watoto walikua ndani na waliposikia gari ya Baba yao ikiondoka walitokanna kunikuta nimekaa peke yangu kwenye kochi. Walikuja na kukaa na mimi kimya bila kusema chochote, niliwaona kabisa wana mawazo mengi, nilitamani kuwaambia kitu lakini nilishindwa, niliwaonea huruma kwani kwa namna Baba yao alikua akiwafanyia usingedhani ni baba yao mzazi.


“Ile nyumba ya kule ni kubwa kuliko hii…” Walianza kuongea.


“Mama anasema atatuchukua lakini Baba hataki waishi na mtu…” Waliendelea kuongea, mimi nilikua kama vile sipo mwili umekufa ganzi niliwaza kuondoka na kuwaacha pale kila mtu apambane na hali yake nilishachoka yale maisha!


Unadhani kama ataondoka? Vipi akiondoka watoto watabaki na nani? je mume wake atakubali aondoke? Endelea kufuatilia simulizi hii ya Baba wa kambo katika ukursa wangu wa Instagram @iddimakengo


ITAENDELEA…


SIMULIZI; BABA WA KAMBO!—SEHEMU YA  NNE


Mage hakua ameumia sana, alikua amevutwa tu kidogo na kuchubuka mkono huku mguu ukiwa kama umetenguka, lakini baada ya kudondoka chinia lipiga kelele nyingi, mume wangu alimkimbilia, akainama pale chini na kuanza kumbembeleza, alimnyanyua na kumkalisha chini huku akimuegemeza kwenye mapaja yake, alikua akimbembeleza akimuuliza kama alikua kaumia na kumuomba misamaha ambayo hata sikuilewa ilikua ya nini.


Wakati huo yule kijana aliyekua naye alishageuza gari na kuondoka.


“Nimekuambi huyo ni mtoto wa Shangazi yangu lakini una wivu wa kijinga, unaona sasa ulikua unataka kuniua!” Mage alifoka, alikua akijaribu kunyanyuka huku akijifanya kama vile kashindwa kunyanyuka.


“Mimi sikuamini, mume wako akisafiri unakua hupokei simu zangu, sas aunafikiri mimi nitajua unaendeleaje? Haiwezekani mume wako akiwpao unakua unanitumia mimi, kwakua anakuchunga unakua unachat na mimi lakini akiondoka hata simu zangu hupokei@”


Mume wangu alilalamika kama mtoto mdogo, hakujali hata kama nilikua pale, aliongea kama mwehu, nilishangaa kwani kwa namnaalivyokua akiongea alionekana kumpenda sana Mage, nilipata wivu nilitamani kuondoka nisione kilichokua kikiendelea lakini miguu hata haikunyanyuka.


“Nakuwa nimeenda kupumzika, nataka kupata upepo, mume wangu ananichunga sana, ni Malaya lakini mimi hataki hata nitoke, nikitoka kazini ni nyumbani na sasa anataka kuniachisha kazi kabisa!” Mage alilalmika, alikua kashanyanyuka.


Alitaka kuondoka lakini mume wangua limzuia, alimuambia kwa hali yake hawezi kuondoka na kumuambia aingie ndani.


“Kufanya nini? Ndani kwangu hawezi kuingia!” Nilijikuta naropoka, muda wote nilikua kimya ni kama hawakuniona, nilivyoongea hivyo ndiyo mume wangu alikua kama kashtuka, akajiumauma kujielezea lakini sikujali, niliingia ndani bila kusema chochote, baada ya kama dakika tatu hivi mume wangu aliingia, akachukua funguo za gari na kuondoka.


Hakurudi mpaka siku iliyofuata, alirudi asubuhi, nilikua nimechoka na sikutaka kumsemesha.


“Unajua jana aliumia sana na pale mume wake kasafiri ilibidi mimi kubaki naye mpaka ajisikie vizuri.” Mume wangu alijiongelesha, mimi sikusemesha kwa chochote, nilirudi zangu chumbani kulala, wka haisra nilizokua nazo nilijua naweza kumtukana na kuzua ugomvi tu. Mume wangu kuona vile alitoka bila kusema alikua anaenda wapi?


Alirudi jioni akiwa na furaha, alkua kachangamka na sijui hata ilikua ni sababu gani, nilimuuliza lakini hakujibu, alijichekesha chekesha tu na kuniambia nisiwe na wasiwasi kuanzia sasa mambo yatakua mazuri. Aliwaletea watoto zawadi na kuwalazimisha kufurahi, kwa kipindi kifupi walichoishi pale tayari wlaishaanza kumuogopa Baba yao, dakila moja alikua vizuri na dakika nyingine alikua anabadilika na kuwa kama mnyama hivyo walikua wana wasiwasi kila wakati.


Hakukaa sana alitoka na hakurudi mpaka siku iliyofuata, ilikua ni siku ya kazi lakini alikuja mchana.


“Kuna ile pesa nilikupa wiki iliyopita kwaajili ya kujifungulia umeweka wapi?” Aliniuliza, nilimuambia ipo ndani kwenye droo. Mara nyingi huwa akipata pesa hunipa kidogo akiniambia hiyo ni kwaajili ya maandalizi ya vitu vidogo vidogo pindi nikijifungua. Nilishakusanya kama milioni tatu hivi kama akiba, alienda wkenye droo kimyakimya na kuzihesabu zile pesa.


Alizichukua na kutaka kuondoka, nilishtuka na kumuuliza ni zanini na anapeleka wapi mbona alishanipa wkaajili ya maandalizi.


“Mimi si ndiyo nilikupa?” Aliniuliza, alionekana kama kukasirika mkidogo. Nilimjibu ndiyo basia katoka.


“Kama mimi ndiyo nilikupa basi ni zangu nazichukua na nikitaka nitazirudisha nisipotaka sirudishi!” Aliongea, nilitaka kuendeleza mazungumzo lakini hata hakujali, aliondoka zake na hakurudi tena mpaka baada ya siku mbili mbele.


Nilikua na wasiwasi sana, nilimpigia simu nyingi sana lakini hakupokea, ilifikia wakati akaniblock na akawa hapatikani. Aliondoka bila kuacha chochote nyumbani, pes ayote ya akiba alishaichukua hivyo sikua na namna zaidi ya kupika wali mkavu na wakati mwingine na maziwa, nilitamani kumuambia mtu lakini nilisita, nilijua kama nikimuambia Mama yake basi utazuka ugoomvi.


Alirudi nyumbani na kunipa elfu hamsini kisha akachukua begi, akachagua nguo zake nyingi nyingi na kuziweka, aliondoka bila kuniambia anaenda wapi? Nilimuuliza lakini aliniambia nimuache nisimuingilie maisha yake. Sikua nikimuelewa kabisa kwani ni kama alikua ananiacha.


“Unanitelekeza, kama umenichoka kwanini usiniambie nirudi kwetu?” Nilimuuliza, aliniangalia kwa hasira na kuniambia kuwa namtafuta.


“Unataka kuondoka na hawa watoto nani atawalea?kaa hapa na kama ukiondoka basi jua siji kukutafuta na ndiyo ndoa itakua imefia hapohapo!” Alinisukuma na kutoka, aliingia kwenye gari na kuondoka bila kuniambia chochote.


***


Tabia ya mume wangu kuondoka bila kusema anaenda wapi, mambo aliyokua akiyafanya kwa wakati ule vilinipa shida kidogo, sikumuelewa kabisa na nilitaka kujua nini kinaendelea. Kila akiondoka hakua akipokea simu zake, lakini nilikua lazima alikua ni Mage, tyangu Mage kuolewa alikua kama mtu aliyechanganyikiwa, alikua akifanya mambo ambayo hayaeleweki, kuchanganyikiwa kwake nilijua kuwa ni lazima Mage alikua anahusika.


Hizo lala lala zake nnje nilijua ni lazima anakua na Mage na kwakua anilishamsikia akisema kuwa mume wake kasafiri basi nilijua kuwa ndiyo sababu. Kwakua nilijua alipokua akiishi Mage sikupata shida kuchunguza, nilianza kufuatilia na kuja kugundua kuwa kumbe siku ambayo alikuja nyumbani na kutaka kugongwa na gari Mage alifumaniwa na mume wake. Wakati mume wangu anamchukua na kumpeleka nyumbani akijua kuwa mume wake hayupo kumbea alisharudi.


Alipoona gari ya mume wangu inampeleka na kwakua walikua wakijuana na mara nyingi alishamkanya kuwasiliana na mume wangu basi alimpiga Mage na kumukuza. Mage alipofukuzwa aliishia kumtafuta mume wangu na ndipo niligundua ni sababu gani siku ile mume wangu alirudi na furaha kwania lijua kabisa kuwa Mage kaachika. Niliumia sana kujua vile, nilimpigia simu mume wangua likua hapokei nikaamua kumpigia simu Mage, alijishaua kunisalimia vizuri.


“Najua unachokifanya ila kama umeamua kumchukua mume wangu basi njoo uchukue na wanao, sitaki kulea matatiozo ya mtu!” Nilimuambia lakini alinigeuzia kibao kuwa nawaita wanae matatizo, siwapendi nawanyanyasa na mambo kibao. Mimi sikumjali nilimuambia anatakiwa kuja kuwachukua watoto wake na kama hataki nitampelekea. Alinitukana na kuniambia nisimtishe kama ni watoto nimpelekee, nilimuambia ni wakwake basi aje kuwachukua kwani nimechoka nataka kuwa na amani na maisha yangu.


Nilikata simu kwa hasira lakini jioni yake Mage alikuja na kuniambia nimpe kila kitu cha watoto wake akawachukua, huwezi amini watoto walikua hawataki kuondoka, walikua wakinililia na kuniomba nibaki nao. Hali ile ilimkasirisha, alianza kuwatukana na kuwapiga, akawaingiza kwenye gari kwa lazima na kuondoka nao. Nilijisikia vibaya kwa watoto kuondoka, namna walivyokua wakiniangalia kuomba kubaki na mimi iliniumiza sana lakini sikua na namna ni Mama yao ni bora yeye kubaki nao na mimi kbaki na msalaba wangu.


Muda wote huo mume wangu alikua hayupo na sijui hata alikua wapi kwani alikua na zaidi ya sikutatu hajaruidi nyumbani, tangu alipochukua nguo zake hakurudi tena. Usik sikupika kwani hakukua na kitu cha kupika, nilikaanga tru viazi vya chips na kula, sikujua kama mume wangu atarudi, lakini kwenye saa nne hivi nilisiia honi ya hgari lake getini, nilitoka kwenda kufungua geti, nilifungua lakini kabla sijafungua vizuri mume wangu aalikanyaga mafuta kw anguvu gari likamalizia kufungua geti, nilikua nimeshikilia upande mmoja wa geti nilirudshwa juu juu na kudondokea pembeni.


Nikiwa bado pale chini sijajua nini kimetoke amume wangu alisimamisha gari, akaashuka na kunifuata pale chini, alianz akunipika makofi usoni na miguuni.


“Hivi unafikiri kwakua una mimba ndiyo siwezi kukupiga? Hivi unataka kunipanda kichwani, kwanini unafuatilia maisha yangu? wewe si unakaa kula na kunya bure hapa? Sasa kwanini uwafukuze watoto wangu? Nyumba yako hii mpaka unajifanya kuwa hutaki kukaa na wanangu? Umechangia chochote hapa mpumbavu wewe!”


Alinipiga sana hukua kinisomea risala, alikasirishwa na Mage kuja kuwachukua watoto wake! Alikua akinilaumu mimi kuwa nimewafukuza, aliongea mambo mengi sana, nilijaribu kujitetea lakini ndiyo kwanza nilikua napalia mkaa,a lizidisha kunipiga. Lakini hakua akinipiga kama mwanzo, safari hii alikua akinipiga sehemu ambazo anajua kabisa hawezi kumdhuru mtoto tumboni. Alinipiga sana kisha akaninyanyua na kunirudisha ndani.


Baada ya hapo alitoka nnje, kumbe watoto walikua kwenye gari, aliwatoa na kuwasukumiza ndani.


“Na nyie wajinga wajinga sio kila kitu mkiambiwa mnakubalia, mtakaa hapa! Hivi mnataka kumuua Mama yenu, ndiyo katoka kwenye matatizo lakini badala mumuache apumzike basi mnamng’ng’ania kama nini. Mtakaa na huyu mbwa mwenzenu hapa na nisikie mnaita Mama! Nitawaulia mbali, mambo gani haya kunyimana uhuru, nimesema mtakaa hapa na sitaki mtu kutoka!”


Aliongea maneno mengi sana lakini hata sikumuelewa, alikua na hasira mpaka anachemka, sijui hata kosa lilikua nini, alikua anapumua kwa nguvu mpaka nikaanza kumuonea huruma, likua akitetemeaka anashindwa hata kukaa, nilihisi presha imempanda, nilinyanyuka hakarakaharaka, nikamvua shati ksiha nikamkalisha chini, nilimpa maji na kuanza kumpepea kwani alionekana kutoa jasho kama vile alikua anakimbia muda mrefu.


Alitulia kwa muda ksiha akaanza tena kunilaumu.


“Utakuja kuniua wewe mwanamke, hivi kwanini huridhiki, kwani ni lazima kila siku kuhangaika na maisha ya watu, unakosa nini humu ndani, unakosa nini?” Alianza kuonge, ilinibidi kumuomba msamaha ingawa hata sikujua kosa langu, aliongea maneno mengi sana mimi niliishia tu kumsikiliza bila kusema chochote zaidi ya kuomba msamaha kwani nilijua kama sitaishia kupigwa basi anaweza hata kuzimia.


Baada ya kuona sisemi chochote alinyanyuka na kuingia chumbani, alichukua nguo zake nyingine na kutoka bila kusema kuwa anaenda wapi! Nilipandwa na hasira lakini nilijizuia, sikutaka kufanya chochote kwa wakati ule kwani nilishchoka na sikutaka kupigwa tena. Nilisimama mpaka niliposikia anawasha gari akaondoka, nilienda kufunga geti, bahati nzuri halikua limeharibika, nilirudi na kukaa kwenye makochi.


Muda wote watoto walikua ndani na waliposikia gari ya Baba yao ikiondoka walitokanna kunikuta nimekaa peke yangu kwenye kochi. Walikuja na kukaa na mimi kimya bila kusema chochote, niliwaona kabisa wana mawazo mengi, nilitamani kuwaambia kitu lakini nilishindwa, niliwaonea huruma kwani kwa namna Baba yao alikua akiwafanyia usingedhani ni baba yao mzazi.


“Ile nyumba ya kule ni kubwa kuliko hii…” Walianza kuongea.


“Mama anasema atatuchukua lakini Baba hataki waishi na mtu…” Waliendelea kuongea, mimi nilikua kama vile sipo mwili umekufa ganzi niliwaza kuondoka na kuwaacha pale kila mtu apambane na hali yake nilishachoka yale maisha!


Unadhani kama ataondoka? Vipi akiondoka watoto watabaki na nani? je mume wake atakubali aondoke? Endelea kufuatilia simulizi hii ya Baba wa kambo katika ukursa wangu wa Instagram @iddimakengo


ITAENDELEA…


Nilipandwa na hasira kwa mambo aliyokua akinifanyia mume wangu, nilikasirika kwamba pamoja na kuwa na ujauzito wake lakini aliniacha ndani na kwenda kuishi na mwanamke mwingine tena ambaye bado ni mke wamtu huku akiniachia wanae nimlele.


“Lakini bora kukaa hapa, Mama ana hasira sana anatupiga kila siku anasema sisi ndiyo tulimharibia usichana wake! Weti kwani sisi tulifanya nini Mama Mdogo, mbona mimi sijamfanyia chochote anasema nimemharibia usichana wake?” Joackim mtoto wa kiume wa mume wangu aliniuliza.


Pamoja na hasira zangu lakini nilijikutwa napatwa na huruma, wale watoto walikua na huzuni sana, walikua kama watoto yatima ingawa wazazi wao waote walikua hapo.


“Hakuna kitu, hujafanya chochote, usichana wake kaharibu mwenyewe.” Nilimpa moyo huku nikimsogelea na kumkumbatia, walinyamaza kwa mdua kisha Nancy, mtoto wa kike wa mume wangu aliongea.


“Anasema asingezaa angeolewa na mwanaume tajiri lakini Baba akampa mimba ndiyo maana hampendi Baba kwani nayeye kamharibia maisha pia.” Aliongea, nililazimika kubadilisha ile mada kwani ilionekana kuwaumiza watoto.


Walikua na mawazo mengi kutokana na mahusiano ya wazazi wao, ilionekana shida haikua kwa Baba yao tu hata Mama yao alikua akiwanyanyasa.


“Mama mdogo wewe si ni Mama wa kambo?” Joackim aliniuliza.


“Hapana mimi ni Mama, hakuna Mama wa kambo, Mama ni Mama. Kwanini unauliza hivyo?” Nilimjibu vizuri ingawa bado nilitaka kujua sababu za yeye kuniuliza vile.


“Mama kila siku anatuambia tusikuheshimu kwakua wewe ni Mama wa kambo, na shuleni kila siku wanasema Mama wa kambo ni wabaya lakini wewe mbona hutupigi kama Mama?” Alionyesha kuchanganyikiwa kabisa na mambo yaliyokua yakiendelea, bado alikua mdogo sana lakini maisha yalimlazimisha kukomaa haraka kiakili.


“Hakuna kitu kama hicho, Mama ni Mama na mimi ni Mama yenu, hata kama sikuwazaa lakini bado ni Mama yenu, mimi ndiyo nawalea hivyo manatakiwa kuniheshimu.”


“Mimi nakuheshimu, tena kuliko hata Mama, Mama yeye kila siku anatupiga simheshimu…” Nancy alidakia.


“Hapana, yule ni Mama yenu, wakati mwingine anawapiga kuwafundisha lazima mumheshimu, hata kama akikosea lakini bado ni Mama na watoto wazuri wanawaheshimu Mama zao kila siku. Nyie si ni watoto wazuri?” Niliwauliza, waliitikia kwa vichwa nikawaambia basi kama ni watoto wazuri basi ni lazima kuwaheshimu wazazi wao wote hata kama wakati mwingine wanakua wakali.


Niliwauliza watoto kama walikua wamekula wakaniambia hapana, nilienda kuwaandalia chakula na walipokula walilala. Kila wakati  wakati wanakula walikua wakiniomba nibaki nao na wasirudi kwa Mama yao, walionekana kuchukia kwenda kule kwani Mama yao ana hasira sana na hata mume wangu alipoenda na kuwakuta pale alikasirika na waligombana sana na Mage, mume wangu hakua akitaka watoto kwa Mage.


Hapo ndipo nilijua kuwa kumbe zile pesa alikua kanipa kwaajili ya kujifungulia alizichukua na kwenda kumpangishia nyumba Mage baada ya kufukuzwa na mume wake. Watoto walikua wakiniambia namna ambavyo mume wangu alikua akimlalamikia Mage kwa kuchukua watoto wakati yeye aliikodi ile nyumba kwajili yao wawili akiwaambia mimi nipo kwaajili ya kuwalea na ni kazi yangu kwani sina kazi nyingine yoyote. Nilikasirika lakini kwa namna flani niliona bora kubaki na watoto kuliku kuwaacha waende kuteseka kwa Mama yao.


***


Mume wangu alikuaakirudi nyumbani mara moja moja, pesa ya matumizi alikua anaacha lakini kidogo sana, sikua nikilalamika na watoto nao waliizoea ile hali hawakua wakilalamika, walikua wakila chochote kile ambacho ningepika, ni kama walielewa hali halisi. Nyumba ilikua na amani kwa muda na kwakua mume wangu akirudi ni kununiana na kelele kuna wakati nilikua nikitamania sirudi kabisa, ningekua nina kazi wala hata simu nisingempigia kwani akiwa hayupo huwa nakua na amani sana.


Siku moja mume wangu alienda Arusha kikazi, aliniaga juu juu kwani alionekana kuwa na hasira sana, waligombana na Mage, alimumbia Mage anataka waende wote akakataa, sijui kwanini lakini ni dhahiri alikua hampendi kabisa mume wangu na yeye ndiyo alikua akijipendekeza kwa kumfanyia kila kitu ili kumridhisha lakini Mage wala hakujali, kila siku ilikua ni vituko. Baada ya mume wangu kuondoka Mage alienda kuwachukua watoto shuleni, hakunipa hata taarifa.


Aliwafuata mwenyewe shuleni na kuwachukua, nilisubiri sana siku hiyo nyumbani lakini watoto hawakutokea, kwakua nilikua na namba ya mwalimu wao nilimpigia na aliniambia kuwa walienda shuleni kama kawaida na kutoka sawa na watoto wengine. Niliamua kumuambia mume wangu ambaye alionekana kupaniki.


“Umekua mzembe sana, nimesafri siku moja tu umewapoteza watoto, hivi unafikiri nitamuambia nini Mama yao, mwanamke mjinga sana wewe…” Alinitukana sana lakini katika mazungumzo yake hofu yake kubwa ilikua ni Mage na namna ambavyo atalichukulia hilo swala, aliniambia nisimuambie atamuambia mwenyewe. Alikata simu lakini baada ya kama dakika mbili alinitumia meseji “Wako kwa Mama yao.” Hakutoa maelezo mengine na hata nilipomtafuta ili kuongea naye hakuwa akipatikana, alizima simu mara tu baada ya kunitumia meseji.


Ingawa niliumia ni kwanini awachukue watoto bila kuniambia lakini nilikua na amani kuwa angalau wapo salama. Nilikua nishapika kwajaili ya watoto hivyo nilikiweka chakula kwenye friji na kupanda kitandani kulala. Lakini kabla ya kupatwa na usingizi simu yangu iliita, alikua ni Mage, nilipokea nikitegemea kwamba labda angeweza kuomba msamaha kwa kuwachukua watoto bila kuniambia akijua kuwa bado walikua mikononi mwangu, lakini ile kupokea tu nilikutana na matusi.


“Mshenzi mkubwa wewe! hivi unafikiri kuwajaza chuki wanangu ndiyo utapendwa na huyo mwanaume! Mpumbavu mkubwa mwanamke gani hukubali kuwa hutakiwi! Mwanaume hakutaki lakini kutwa kucha kuwajaza wanangu maneno ili tu wanichukie mimi Mama yao!


Kwa taarifa yako mimi hii ni damu yangu, nimeenda leba mwenyewe na mshono bado ninao, wewe mpuuzi ndiyo unakuja na kujifanya unajua kulea wakati hata mtoto huna, mtu hujazaa unajifanya unajua kulea, kwa taarifa yako wanangu hutakuja kuwaona tena, nabaki nao na kama unafikiri kwamba utapendwa kwa kujipendekeza kwa wanangu basi umenoa. Mwanaume hapa hachomoki na nilikua simtaki ila kwa ulichokifanya kwa wanangu basi jua sitakusamehe narudiana naye na wewe utaachika tu! Utaumia kama nilivyoumia mimi shetani mkubwa wewe!”


Alitukana sana, mimi nilibaki kimya, nilikua nikitetemeka kwa hasira kiasi cha kushindwa kuongea, sikujua anamaanisha nini na ni kitu gani watoto walikua wamekuambia mpaka kukasirika kiasi kile. Nilimuacha akaongea mpaka akakata simu, nilishindwa kulala nikakaa kitandani nikitafakari, kabla sijawaza na kujua nini cha kufanya simu yangu iliita, alikua ni Mume wangu, alianza kuongea naye kwa hasira.


Alikua akinishutumu kwamba nataka kuwagombanisha watoto na Mama yao, hakunaimbia ni kwa namna gani lakini alionekana kukasirika sana.


“Unataka kuniua! Hivi unataka nini wewe mwanamke? Kwa taraifa yako safari hii nakurudisha kwenu, sitajali kuhusu Mama yangu, siwezi kufa kwa presha wkwaajili yako, nasema kuwa nikirudi nisikuone mshenzi mkubwa wewe! kwanini usisubiri mpaka ukazaa mtoto wako ndiyo ukamlea unavyotaka unajifanya unajua kulea tu wa wenzako, nimekuambia sas ahivi nimefikia mwisho…”


Aliendelea kunishutumu bila kuniambia kuwa nimefanya nini! Nilijaribu kujitetea lakini nilimuona anazidi kupandisha hasira, kwa ninavyomjua mume wangu nilijua fika kuwa presha ishapanda hivyo nilipaswa kumtuliza. Nilianza kuomba msamaha na kumuambia nimekosa haitajirudia tena, nililalamika na kulia kabisa, kidogo mume wangu alitulia, nilimuambia anywe hata maji ajitulize lakini ni kama nilimpampu zaidi, alianza kutukana upya mpaka akakata simu na nilipojaribu kumpigia ili kujua hali yake alikua hapokei tena simu zangu.


Nilipiga sana simu lakini mume wangu alikua hapokei, nilijikuta napatwa na wasiwasi, kwa hasira alizokua nazo nilihisi kitu kibaya na kwakua sikujua alikua na nani kule nilizidi kuumia. Nilitamani kumpigia simu Mama yake ili kumuambia aongee na mwanae kujua anaendeleaje lakini nilisita, sikutaka kumshirikisha Mama mkwe wangu kwani angejua mambo yaliyokua yanaendelea angepaniki na  kusababisha matatizo mengine, ingezua ugomvi  mwingine usio kua na maana kwani alikua hampendi Mage na mimi nilijua mume wangu hawezi kukubali kumuacha, nililazimika kukaa tu nikisubiria kama atapiga lakini hakupiga mpaka asubuhi nilikua macho nasubiria simu ya mume wangu lakini haikupigwa.


***


Sakumi na moja za asubuhi nilisikia geti likigongwa, nilitoka harakaharaka kwani nilikua bado sijalala, nilifungua na kukutana na gari ya Mage, hakushuka lakini alifungua milango na watoto wakashuka, bila kusema chochote aliwasha gari na kuondoka. Niliwachukua watoto mpaka ndani na kuanza kuwauliza ni nini kimetokea na ni kwanini Mama yao alikua na hasira na kwanini kawarudisha asubuhi yote ile.


“Mimi sijui tangu jana alipotuchukua kutoka shule Mama alikua anatukana tu, mimi nilimuuliza kama tunarudi kwako ndiyo akaanza kulalamika kwanini hatukufurahia kumuona wakati yeye ni Mama yetu, alitukana sena akisema wewe ndiyo unatufundisha tumchukie ndiyo maana hatukufurahia kurudi nyumbani!” Joackim aliniambia, lakini hakua akijua ni kwanini aliwarudisha tena asubuhi asubuhi, hata hakuwapeleka shule, aliwaamsha usikuusiku na kuwaondoa kama vile anawafukuza.


Walionekana kuchoka sana, niliwaambia walale na siku hiyo wasiende shule, niliongea na mwalimu wao na kumuambia kuwa wanaumwa hawawezi kwenda shule, alinielewa. Usiku Mage alianza kunitumia meseji, alikua akiniambia najifanya kuwa ni mama bora lakini atanikomesha!


“Utakaa na hao watoto lakini mimi ndiyo nitakuonyesha kuwa ni mwanamke zaidi yako, si unajifanya wewe ni mama bora sasa tutaona kama mimi na wewe nani ni Mama nani anajua kuzaa!” Alituma meseji nyingi sana za vitisho lakini mimi sikujibu chochote, nilimchukulia kama kichaa.


Baada ya kuona katuma meseji nyingi za kawaida simjibu alinitumia meseji na kuniambia “Ingia Whatsapp? Uone sasa kuwa mimi ni mwanamke wa namna gani?” Nilijikuta naingia Whatsapp harakaharaka, sijui kwanini lakini nilikua na hofu na sikujua sababu ya kuniambia vile,ile kuwarudisha watotoa subuhi asubuhi ilinifanya kuamini kuwa kuna kitu kibaya ambaco amekipanga kunifanyia kwani alikua na hasira. Niliingia Whatsapp, ilikua ni video niliibonyeza ili kuifungua lakini ilikua inachelewa kufunguka.


Unadhani Mage kamtumia nini? Mimi sitaki nikuambie sana kuendelea na sehemu ya sita hakikisha unafollow ukurasa wangu wa Instagram @iddimakengo huko  mambo ni moto!


ITAENDELEA….


SIMULIZI; BABA WA KAMBO!—SEHEMU YA SITA


Ilikua ni video akifanya mapenzi na mume wangu, walikua kitandani na ulikua ni uchafu mtupu, nilikasirika na kuifuta, sikutaka hata iwe katika simu yangu kwani niliona kama ni uchafu, nilishangaa ni kwa namna gani mwanamke unaweza kujidhalilisha namna ile. Nilimshangaa zaidi mume wangu kwa kukubali kufanya kitendo cha kipumbavu namna ile.


Baada ya kuifuta haukupita muda zilianza kuingia meseji mfululizo akiniambia kama mimi nimechukua watoto wake basi yeye atamchukua mume wangu. Nilinyamaza kimya bila kumjibu chochote, alipoona sijibu meseji zake alianza kupiga simu lakini sikupokea,a lipoona sipikei simu yake alitumia simu ya mume wangu kunipigia, nilipokea na aliongea yeye akinitukana sana. Alinitukana matusi mengi ya nguoni.


“Wewe si unajifanya Mama tutaona sasakama hao watoto utaweza kuwalea na kuaa kwako nyumbani, na nina uhakika utajifungulia hapo nyumbani mshenzi mkubwa wewe!” Aliongea lakini sikujibu chochote na wala sikukata simu, nilijua kama nikikata mume wangu atakasirika kwakua katumia simu yake. Nilibaki kumsikiliza mpaka alipochoka na kukata simu yeye mwenyewe. Mimi nilinyamaza tu, sikumtafuta mume wangu kwa siku tatu nayeye hakunitafuta, nilikua na hasira kujua kuwa alikua na mwanamke mwingine.


Siku ya nne mume wangu alirudi kutoka safari yake, alikua peke yake, alinikuta nyumbani niko sawa tu, nilimkaribisha kawaida na yeye alinisalimia kwa kunichangankia. Aliingia ndani na kuoga, nilimuandalia chakula lakini alisema kashiba. Sikumuuliza chochote hata jioni alipotaka kutoka nilimuambia hamna shida, aliondoka kwenye saa kumi na mbili hivi kisha akarudi kwenye saa nne usiku, nilimuandalia chakula cha usiku na kukaa naye mezani wakati anakula.


“Mbona huulizi chochote?” Alianda, nilimuona kama anajishtukia shtukia na nilimuacha ahangaike mwenyewe kwani nilijua hata kama nikiuliza kitu gani haiwezi kusaidia, nilijua kuwa hawezi kumuacha Mage, nilikubali nafasi yangu na sikutaka kuumiza kichwa tena, nilishachoka.


“Mbona nimekuuliza mume wangu kuhusiana na safari ukaniambia uko vizuri, nashukuru Mungu umerudi salama.” Niliongea kwa utaratibu, alinyamaza kama anawaza kitu cha kuniambia lakini aliaacha, mimi pia sikusema chochote.


Alikula chakula na kumaliza, aliingia chumbani huku akiniacha sebuleni nikiondoa vyombo. Baada ya kumaliza nilirudi chumbani,a likua bado hajalala na alikua bize na simu, lakini alikua hachat ni kama alikua napiga simu namba flani naambiwa haipatikani ila anairudia tena. Kama ziadi ya nusu saa hivi anapiga na kuambiwa hapatikani, mimi sikujali wala sikumuuliza kama huyo aliyekua akimpigia ni nani.


Nilipanda kitandani kulala, roho ilikua inaniuma sana lakini sikutaka kumuuliza na kuleta ugomvi usiku ule.


“Wanawake ni mashetani kabisa hamridhiki! Mtu hata umpende vipi lakinia tatrafuta namna ya kukuumiza tu!” nAliongea kwa suti, nilijifanya kama nimelala sijamsikia, aliendelea kupiga ile namba hukua kitukana mambo mengi, nilijua tu lazima atakua ni Mage kampigia na hajampata ndiyo anapaniki.


“Kwanini hata huniulizi kuwa ni kitu gani kimetokea, mimi sijarudiana na Mama watoto wangu lakini yeye alikuja tu kunifuata sas amimi ningemfukuza.”


Alianza kujiongelesha, nilimsikia vizuri na kutamani kuonge naye kumuambia yangu ya moyoni lakini nilijizuia, nilimuomba mungua nisaidie nisinyanyue mdomo.


“Nimeshaachana naye na najua ana wanaume wengine, hivi kwanini hatulii, anakua ni mtu wa wanaume tu, kila sikua nalalamika kuwa mume wake anamnyanyasa lakini nayeye ni mtu wa wanaume, unaona usiku huu hapatikani kwenye simu. Najua unaweza kudhani kama nampenda lakini yule ni Mama wa watoto wangu, siwezi kulala bila kujua anaendeleaje, kutwa nzima tangu turudi hapokei simu zangu, nyumbani hayupo na sijui kaenda wapi?”


Aliendelea kujiongelesha, mimi bado sikusema chochote, nilinyamaza, hasira zilishanipanda na machozi yalikua yakinitoka, nilimuomba Mungu sana kunipa ujasiri wa kuvumilia kwani nilijihisi kufa. Alijiongelesha sana mambo mengi lakini mimi sikumjibu kabisa, nilijifanya kulala nikanyamaza mpaka alipoona sijibu basi alilala nayeye, huwezi kuami sikupatwa na usingizi mpaka alfajiri.


Siku iliyokua inafuata ilikua ni siku ya kazi, niliamka mapema kama kawaida yangu na kumuandalia kila kitu, nilimtengea chai yake mezani lakini aliniambi hajisikii anawahi. Aliniuliza vipi najisikiaje, akauliza kama vile naumwa, akauliza kam akuna tatizo, nilimjibu hakuna kitu mimi niko sawa. Aliondoka ingawa alikua na wasiwasi sana, nilijitahidi kutabasamu ingawa moyoni nilikua nalia. Aliondoka akaniacha mimi nikiendelea na kazi zangu, nilikua nimechoka na sikutamani kumuona tena.


****


“Wewe ni shetani kabisa unaweza hata kuniua, sikuamini tena, nakaa mbali sana na wewe!” Mume wangu alinitumia meseji, ilikua ni mchana, tangu kuondoka asubuhi yake nilikua sijawasiliana naye chochote.


“Nashukuru mume wangu…” Nilimjibu, sikuongeza maneno mengi lakini yeye alinitumia mesesji nyingi za matusi hukua kiniambia hanitaki. Alikua akinitukana matusi mengi ya nguoni ambayo hata hayatamkiki lakini sikumjibu chochote. Baada ya kumaliza alikata simu, sikujishughulisha niliendelea na mambo yangu.


Kichwani nilikua kama nimechanganyikiwa kila saa nikimuuliza Mungu ni kwanini haya yote yananitokea, sikuwa mkosefu kiasi hicho, niliwaza kama ni adhabu Mungu ananidhibu kuhusu nini? Niliwaza sana lakini sikupata jibu. Nikiwa katikati ya mawazo simu yangu iliita, ilikua ni simu ya Mama yangu mzazi.


“Hivi wewe ni mwanamke wa namna gani? Hata kama umegombana na mume wako ndiyo uwakatae na watoto! Hivi mwanaume kuongea na mwanamke aliyezaa naye ndiyo inafikia hatua ya kutaka kuondoka, hivi kwanini unataka kuniua mwanangu!”


Mama alilalamika sana sikumuelewa kabisa kwani sikujua hata anazungumzia nini? Kwa madai yake nikuwa mume wangu alikua kampigia simu akimuambia kuwa tumegombana kwakua nimekuta meseji akisalimiana na Mage nikakasirika na kumuambia kuwa sitaki kumsaidia kulea watoto tena kwani hana shukurani. Mume wangu alimuambia maneno mengi tena ya ajabu hukua kijiosha na kuonyesha kama mimi nina matatizo. Nilishiwa pumzi, nilijaribu kumuelewesha Mama lakini hakusikia, alimuamini zaidi mume wangu.


“Wewe ni mnafiki mshenzi mkubwa, kama kungekua na matatizo si ungesema, umekaa kimya mpaka Baba wawatu kaongea ndiyo unajifanya kunyanyaswa. Nana sema, ukiondoka hapo jua kuwa mimi si mama yako, hata ukijifungua sitakuja kumuona huyo mwanao, kama watoto wa mume wako unawaona kama takataka unafikiri wakwako yeye atakua na maana, sitaki kukuona na kwangu usirudi, mwanamke unapewa kila kitu mpaka gari umenunuliwa lakini huridhiki!”


Mama aliongea na kukata simu, nilirudi chumbani na kuanza kulia kwa uchungu, ni mambo mengi sana alikua akinifanyia mume wangu lakini nilikua sijamuambia mtu yeyote, alishanipiga na kunifanyia vituko vingi lakini sikumuambia Mama wala ndugu yangu yeyote. Nilishangaa ni kwanini mume wangu kuamua kuniharibia kwa ndugu zangu.  Nililia sana na katika kipindi hicho ndiyo nilitamani kabisa kuondoka kwenda hata kujifungulia jalalani na si kukaa katika ile nyumba tena.


Baada ya kuongea na Mama yangu hazikupita hata dakika ishirini, simu yangu iliita, alikua ni Mama mkwe wangu, niliipokea lakini hata kabla ya salamu naye alianza kutukana.


“Hivi una akili kweli, wajukuu zangu wanakuhusu nini? Kwanini lakini, kama huwezi kuwalea basi niletee mimi niwalee lakini ukiondoka basi jua kuwa huna chako hapo. Kwanini mwanamke huwezi kusamehe, makosa ya miaka 70 leo unaona makubwa, hivi kama wote tungekua kama wewe kungekua na ndoa.”


Mama mkwe aliongea sana na alizidi kunichanganya kwani ilionekana kabisa mume wangu alimuambia stori nyingine kabisa tofauti na ile ambayo alimuambia Mama yangu.


“Yule mwanamke kashaolewa na sasa hivi ana familia yake, anafuraha na ndoa yake, sasa mume wako akisafiri kikazi unakua na wivu wa nini? Hivi kama akikaa hapo nyumbani mtakula nini? Unamuambia achague kati ya wewe na watoto kwa kipi hasa ulicho nacho, hiyo mimba ndiyo inakupa kiburi mshanzi kabisa wewe!”


Mama mkwe aliongea sana mpaka salio likamuishia, alienda kuongeza na kunipigia, alishusha hasira na kaunza kunipa wosia, alinihusia weee mpaka basi, mimi nilichoka hata kumsikiliza nikawa namkubalia tu kila kitu. Kila akiongea nilimuambia sawa, hakuna shida sijui hivi sijui vile. Nilimuambia hakuna shida nitaishi na watoto ilikua ni kutokuelewana kidogo. Alinywea na kuniambia wanaume ni wakubembeleza na nisiwe na hasira, nilikua namuitikia kila kitu na kukubaliana na yeye ili tu akate simu kwani nilishachoka kumsikiliza.


Aliniaga vizuri na kukata simu, kusema kweli nilichanganyikiwa kwani sikujua ni mambo gani ambayo mume wangu aliwaambia. Nililia mpaka machozi yakakauka, ukishanganya na uchovu nilijikuta nalala palepale kitandani. Nilikuja kushtuliwa na watoto wambao walikua ndiyo wametoka shule. Waliniona siko sawa na kuniuliza lakini niliwaambia sina tatizo lolote.


“Ni Mama tu huyo kampigia simu!” Nancy aliongea, alionekana kabisa kukasirika na kuumizwa na mambo aliyokua akifanya Mama yake.


Mimi nilimtuliza na kumuambia hakuna kitu kama hicho, nilimuambia Mama yake hajafanya chochote bali ni mimi tu ambaye sijisikii vizuri, hakuamini lakini hakua na namna. Nilipika harakaharaka chakula cha usiku, baada ya watoto kula niliingia chumbani kulala, kwa namna mume wangu alivyoongea mchana wake nilijua fika hawezi kurudi siku hiyo. Nilipanda kitandao kutafuta usingizi, lakini kabla ya kulala mume wangu alirudi mapema tu kwenye saa tatu, nilimkatibisha na kumtengea chakula, hakula alikua kakasirika zake.


Nilijua ni mambo ya mchana lakini hapana, walikua wamekorofishana na Mage. Alikua na hasira na alikua akiongea ongea peke yake.


“Hivi kwanini wanawake mnakua wapumbavu kiasi hicho, hivi kwanini hamkubali kuachika! Mwanaume amekufumania kakuacha lakini bado unahangaika kutafuta wazee ili kusuluhishya unataka nini? Unafikiri mwanaume atakusamehe, sisi wanaume si watu wa kusamehe, hata wewe mke wangu nakupenda lakini nikikufumania basi jua nakuacha hapohapo!”


Aliongea maneno mengi lakini mwisho nilikuja kujua kuwa Mage katafuta wazee na mshenga ili kwenda kumuombea msamaha kwa mume wake na hicho ndiyo kilikua kikimuumiza. Nilimsikiliza huku nikicheka moyoni kwani angalau niliona nayeye anaumia kama alivyokua ananiumiza. Alikua akipiga simu mara kwa mara hazipokelewi, lakini ghafla simu moja ilipokelewa, alienda kuipokea kwa nnje lakini aliporudi nilimuona kama kanywea, anapumua kwa shida hata kutembea hawezi vizuri, alikua anapepesuka pepesuka mpaka kumuonea huruma.


Unadhani Eric kapewa ujumbe gani katika simu? Je unahisi kama mke wake ataweza kumsaidia au atamuacha. Kama hukusoma sehemu za nyuma ingia Instagram katika ukurasa wangu @iddimakengo na kwa muendelezo wa kisa hiki ni huko huko @iddimakengo.


ITAENDELEA…


SIMULIZI; BABA WA KAMBO!—SEHEMU YA SABA


Hali ile ilinichosha, nilijua kabisa mimi ndiyo namuendekeza, sikujua ni kitu gani ambacho Mage alikua nacho mimi sikna ila kwa uhakika sikutaka kuwa na hicho kitu, hata kama ni kupendwa ule haukua upendo bali laana. Nilimuacha mume wangu akiendelea kuhangaika hangaika na kupanda kitandani kulala. Nilikua nimechoka na nilijilazimisha kufunga macho kabisa. Alijaribu kuniongelesha sana lakini sikunyanyua mdomo wangu.


Hasira zilimzidi, nilimsikia namna alivyokua akipumua, alika akipata shida, nilitamani kunyanyuka kumsaidia lakini nilisita.


“Kama ni kufa afe tu tutazika, nimechoka kuwa kama takataka yake!”Niliwaza, kwa hasira nilizokua nazo sikujali kitu chochote kile, nilitaka kujilalia zangu na kuacha maisha yaendelee. Kaukimya kadogo kalitawala ka kama dakika tano hivi, hapo nilishtuka na kudhani labda kuna kitu kibaya tayari kimesha mtokea.


Bila kujijua nilinyanyuka harakaharaka kuangalia kama alikua amezidiwa hawezi hata kunyanyuka, lakini sikumuona, nilipepesa macho pale chumbani lakini sikumuona, wakati nikijirudisha zangu kitandani nikujua labda kaamua kutoka nnje na kuendelea na mambo yake baada ya mimi kumpuuza nilianza kusikia kelele zikitokea sebuleni.


“Nasema mtaondola hapa mumfuate huyop Mama yenu, yeye si anajifanya anajua kuolewa, si anajifanya anawajua wanaume sasa nampelekea mbuzi wake! Hamuwezi kumsumbua mke wangu ni mjamzito anahangaika kulea mbuzi wa watu!”


Mume wangu alikua akiongea kwa nguvu. Nilinyanyuka harakaharaka na kukibilia sebuleni.


“Mama! Mama! Nakufaaa!” Nancy alikua akipiga kelele, mume wangu alikua amevua mkanda wake wa sukari na alikua akiwaadhibu watoto. Aliwapiga sana na nilipotaka kuingilia alinisukuma akiniambia kuwa nimuache wale ni wanae atawafunza adabu.


“Hawa washenzi kuna vitu wanamuamia Mama yao, nasema kuwa ni lazima waondoke usiku huu huu, kwanini yeye akupe wanae umlele.


“Lakini mimi sina shida mume wangu, mbona mimi nawapenda na tunaishi nao vizuri?’ Nilijaribu kumsihi lakini nikiwa nimesimama kwa mbali, sikutaka kufanya kitu chochote ambacho kingehatarisha mimba yangu na kwa namna alivyokua na hasira nilijua kama nikifanya chochote labda kumgusa basi angeweza kunisukuma na mimba ikaharibika.


Aliwapiga sana watoto akiwachapa na mikanda, walilia na kuniomba niingilie kati lakini kila nilipomsogelea alikua akinisukuma na kuanza upya.


“Mtaondoka tu humu ndani, nataka kukaa na mke wangu kwa amani, yaani tangu kuoa sihjawahi kufurahia ndoa yangu hata siku moja, kwanini nihangaike na nyie wakati Mama yenu yupo.” Aliendelea kuongea kama vile kachanganyikiwa, nilishindwa kuelewa sababau ya kuwapiga wanae, tena watoto wake wa damu.


“Tena nyie si wanangu, mtoto wangu ni mmoja tu, nyie mna damu ya kishetani ya Mama yenu, siwataki kabisa kwangu!” Aliwashika na kuwavuta watoto mmoja mmoja mpaka nnje, alifungua mpango wa gari na kuwasukumiza huko. Aliingia chumbani kwao na kukusanga mabegi yao kisha akayapeleka wkenye gari na kuwafungia huko. Alirudi mpaka sebuleni na kuanza kuniomba msamaha, aliniambia kanikosea sana kwa namna alivyokua akihangaika na Mage.


“Naishi na wmanamke mzuri lakini simuoni kwakua tu nahangaika na shetani, subiri mke wangu baada ya hili utakua na furaha, sitaki tena kitu chochote cha kunikumbusha yule mwanamke. Kaniloga mpaka nimechanganyikiwa, shizi si akili zangu, mimi si mtu wa kufanya hivi, mimi ni mtu mkubwa, nina kazi yangu nzuri, nina pesa zangu na familia yangu inaniheshimu! Hivi mke wangu wewe huoni kama ni melogwa, hizi si akili zangu na ndiyo maana nawaondoa hawa watoto.


Hivi mimi ni mtu wa kuhangaika namna hii, kutwa kucha nahangaika kumsumbukia mwanammke ambaye anatembea na kila mwanaume anayekuja mbele yake, mume wake mwenyewe kamshindwa mimi ndiyo nitamuweza! Dawa zake zimeisha na nakuahidi mke wangu ukiona hata naongea naye kwenye simu, chukua kisu ni chome, nakuamua kuwa mimi nimeamua kubadilika mwenyewe na hakuna mtu wa kunirudisha nyumba.” Alionge sana hukua kisisitiza mimi kumsamehe.


Alikua akiongea mfululizo mpaka wakati mwingine anaishiwa pumzi,a likua anatia huruma, ili kuepusha sahari nilimuambia nimemsamahe.


“Lakini watoto hawana kosa, mbona ni wanao, hembu waache mimi nitaishi nao hawana shida wananiheshimu.” Niliongea kumuomba kuhusu watoto lakini hapo ndiyo kama nilikua nimepalia mkaa, alianza kuwaka na kaunza risala nyingine ambayo ilichosha, kila kitu kilikua ni Mage na namna ambavyo kama tukiwaacha watoto pale basia atatumia mbinu kuingia.


“Mimi najua, kwani mwanzo ilikuaje, sisi si tulikua na amani kabla ya hawa mbwa wake kuja, lakini akajifanya mumewe hataki watoto9 ili tu mimi niwachukue anirudie, najua anaumia mimi kuoa mke mzuri kama wewe, nakuambua kuwa amenoa, simtaki na kama andhani anaweza kuwatumia watoto basi kanoa, mchezo wake nimeugundua, anataka watoto wabaki hapa ili apate sababu ya kunipigia simu na kuvuruga ndoa yetu, thubutu, mimi ni ng’ang’ari, nilishang’atwa na hyoka mara moja nimejifunza!”


Aliongea kwa hasira, alinisihi nirudi chumbani nikapumzike kwani yeye usiku uleule alikua anawarudisha watoto na asubuhi atakusanya kila kitu na hataruhusu tena Mage kuingilia ndoa yetu. Sikua na cha kufanya, nilimuacha akaondoka, aliingia kwenye gari na kukaa kwa muda kama wa nusu saa bila kuondoka, wakati nikidhani kama labda kabadilisha mawazo na kuona watoto hawahusikia u kuwaonea huruma usiku ule aliwasha gari na kuondoka hukua kiniacha peke yangu nikiwa na uoga hata wa kufunga macho.


***


Masaa yalipita bila mume angu kurejea, nilikua na wasiwasi sana, kwa hasira alizokua nazo nilihisi anaweza kufanya kitu kibaya. Nilitamani kumpigia simu Mama mkwe wangu ili kumuambia kilichotokea lakini nilijua kabisa kuwa hawezi kuniamini kwani walishajazwa chuki dhidi yangu. Niliwaza sana ni mtu gani mbaye naweza kumpigia ili amtulize mume wangu kwani nilihisi kama akiachwa vilevile angeweza hata kuwadhuru watoto. Niliwaza sana mwisho nikaamua kumpigia simu mshanga wetu.


Nilipiga simu sana lakini ilikua haipatikani, nilipiga weee mpaka nikachoka nikaamua kupanda kitandani ili kutafuta usingizi lakini haukuja. Nilikua na mawazo mengi sana nikijirafakari nikifikiria ni kwanini nilikua nahangaika na yule mwanaume. Mpaka subuhi saaa mbili mume wangua likua hajarudi, ilipofika saaa tatu hivi ndiyo niliona gari yake, alishuka akiwa kama vile yuko sawa flani, kama mtu ambaye ametoka kuamka na kuanza kujitambuatambua kama vile dunia ni kmpya.


“Watoto wakow api?” Hilo ndiyo lilikua swali langu la kwanza kumuuliza baada ya yeye kushuka.


“Hapo kwenye gari!” Aliongea hukua kitembea kuingia ndani, nilikimbia harakaharaka kuwaangalia kwani nilihisi labda amewafanyia kitu kibaya. Nilifungua mlango na kuwakuta wamelala wkenye gari, walionekana kuchoka, sikujua kilichotokea usiku wote lakini sikutaka kuwaamsha, nilishusha vioovya gari, nikafunga milango na kurudi kwa mume wangu.


“Nimeshindwa kuwapeleka, nimegundua hata mimi ni wanangu, nawadhibu tu kwa maksoa ya Mama yao, nimezunguka sana kwenye gari na wanangu. Naomba unisaidie kuwalea, naamini wewe utakua Mama bora kuliko hata Mama yao, najua na wewe una mambo yako ilahawa ni wanangu, siwezi kuwapeleka kwenda kulelewa na mwanaume mwingine, kila nikifikiria namna dunia ilivyojaribika naona kabisa nibora kubakia nao mimi, wewe nakuaminia huwezi kuwafanyia kitu kibaya.”


Aliongea maneno mengi sana na mimi nilimuitikia kukubaliana naye, sikujua ni kitu gani kilikua kimembadilisha lakini nilishukuru, kwa namna walivyokua wakimzungumzia Mama yao namna anayowanyanyasa sikutaka warudi, hawakua wanangu ila kila siku nikiwaona na kuwafanyia jambo jema nilifanya huku nikimuambia Mungu kuwa hiki ninachokinya ni kileamabcho natamani siku moja kama nisipokuepo basi mtu mwinginea awafanyie wanangu hivi hivi.


Tuliongea vizuri tu, aliniamba anaenda kazini mara moja, nilienda kuwaamsha watoto, waliponiona kwanza walishangaa lakini pili walinitukia na kunikumbatia. Walikua kama wanashanaga, hawakujua kama wako wapi. Mume wangu aliingia ndani kujiandaa na kutoka, alipotoka aliwachangamkia wanae mpaka basi, aliwauliza awapelekee zawazi gani. Walinyamaza tu kwani walionekana dhahiri kuogopa, lakini aliwatoa wasiwasi na kuwaomba msamaha akiwaambia zilikua ni hasirana ile hali haitakuja kujirudia tena.


Watoto walishia kusema pipi nakaranga, aliondoka na  kuniacha na watoto.


“Amesema tunakuja kukaa hapa au anarududisha kwa Mama?” Joackim aliniuliza, lakini kabla sijamjibu Nancy naye alidakia.


“Mama kaa na sisi, Baba hatupendi, mama yetu hatupendi, usikubali wakatuchukua, hata wewe unateswa kwanini tusitoroke…”


“Hawezi kuondoka hana kazi…” Joackim alieleza.


“Hata kama si tunaenda kuwa ombaomba. Maam ukiondoka na kukaa barabarani sisi ni watoto tutaomba kwa watu na tukipata pesa tunakula wote.


Walikua wakiongea nakubishana mpaka nilipowakatiza, ingawa sikua na uhakika kwani mume wangu ni kigeugeu sana niliwaambia kuwa hawataondoka na mimi ndiyo nitawalea kama Mama yao. Walinekana kufurahi lakini kama mimi niliona kabisa kuwa wana wasi, ni kama hawakua na uhakika na majibu yangu.


“Sema Baba kigeugeu, hata kama kasema sisi tutabaki hapa anaweza kubadilika na akatufukuza. Niliwahakikishia kuwa hapana siwezi kuliruhusu hilo.


Maisha yaliendelea vizuri tu, kila kitu kilikua sawa, mume wangu alibadilika kabisa, alikua akiwahi kurudi nyumbani, alianza kunihudumia vizuri na watoto alikua akiwahudumia, hakua akiwapiga wala kuwatukana kama awali. Sikumuona wala kuhisi kama bado anawasiliana na Mage ingawa nilichunguza sana kwa kuhangaika na simu yake lakini sikuona kitu chochote, sanasana alikua akimzungumzia vibaya na kila siku kunikumbusha kuwa ananipenda sana.


Nikiwa nimebakiza wiki moja kujifungua bado nilikua sijapata binti wa kazi, tulishahangaika sana lakini wapi? Nilimuambia mume wangu nahitaji mtu mzima, nilimuambia hiyo ni mimba ya kwanza hivyo niende nyumbani kwetu kujifungulia lakini alikataa, nilimuambia Mama yangu kuja au ndugu yangu yeyote lakini alikataa, aliniambia kuwa ataeleweka vibaya kama akiniruhusu kwenda kwetu, nilimuomba basi hata angalau niende kwao lakini alikataa, Mama yake mwenyewe alikua hataki, tangu kuambiwa na mwanae kuwa siwataki wajukuu zake alibadilika sana alikua hataki hata kuongea na mimi.


Sikumuelewa mume wangu ni kwanini alikua anasema hivyo, nilijaribu kumbembeleza aila aliniamia kuwa yeye ni mwanaume hivyo hapangiwi, ameshaamua kuwa siendi popote hivyo siendi. Nilimuuliza ana mipango gani kuhusu mimi kujifungua akawa yuko kimya, hakua akitoa majibu ya kueleweka. Nilienda hivyo mpaka nilipojifungua, hakumuambia ndugu yeyote hata kama niko hospitalini, alinipiga marufu kabisa akiniambia yeye ndiyo mwanaume anajua nini cha kufanya.


Nilijifungua salama lakini tukiwa njiani alianza kuniambia maneno ambayo sikuyaelewa.


“Kuna kitu nimekifanya ila naomba usikasirike, nimekifanya kwa manufaa yetu sisi wawili na familia yetu…” Alianza kuongea, nilimuuliza kitu gani lakini hakujibu, aliniambia nitajua yu nisiwe na hararaka. Nilinyamaza tukaenda mpaka nyumbani, ile naingia tu ndani namkuta Mage huyu hapa kavaa kama katoka jikoni kupiga, yaani hakuonekana hata kuwa ni mgeni kaja kusalimia mara moja, alionekana kama ni mtu anaishi pale.


Unadhani ni kitu gani kimempeleka Mage pale? Unadhani nini kitatokea? Nisikuchoshe endelea kufuatilia kurasa zangu Instagram @iddimakengo na Facebook @iddi makeng


ITAENDELEA…


SIMULIZI; BABA WA KAMBO!—SEHEMU YA NANE


Mume wa Magea likua ni mtu mzima kidogo, kabla ya kukutana na Mage tayari alsihaoa mwanamke mwingine, walizaa naye watoto wanne lakini walikuja kushindwana na mwanamke akaondoka na watoto wote. Pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha lakini alikua hahudumii familia yake na mkewe alishakata tamaa kumuomba huduma za mtoto. Alikua ni mtu mkubwa tu sherikalini mwenye pesa n cheo kikubwa lakini ni wale wanaume ambao huwa hawajali kabisa.


Wakati anakutana na mage alimuambia kuwa hajawahi kuoa na wala hana mtoto, alimuambia kuwa ametumia muda mwingi katika masomo na kufanya kazi kiasi cha kushindwa kuanzisha familia na alikua tayari kumchukua Mage pamoja na watoto wake. Walipanga kufunga ndoa muda mrefu, lakini alikua akisogeza mbele kila wakati na miwsho waliamua kufunga ndoa ya serikali kwani mwanaume alikua bize sana na kazi, alikua ni mtu wa kusafiri safari na Mage alikua na haraka ya kuolewa.


Baada ya kupata mtu anayeeleweka ndipo Mage alimua kauchana na mume wangu, kumbvuka kipindi mimi naingia kwenye ndoa wakati simfahamu wala sifahamu kama wana mahusianao wao walikua wakiendelea na mambo yao kimya kimya, kila kitu kilikua vizuri kwakua mume wangu alikua akimhudumia Mage kwa kila kitu na kwakua Mage hakua akimpenda mume wangu sana hakutaka kuolewa naye ingawa mara nyingi tu mume wangu alimuomba wafunge ndoa ya serikali lakini alikataa akisingizia mume wangu tayuari ana ndo ya kanisani na Mama mkwe wangu hampendi.


Hapo ndiyo mambo yalianza kubadilika kwani ile kusikia kyuwa Mage anaolewa mume wangu ni kama aliachwa tena kwa mara ya pili, mume wangu aliumia zaidi aliposikia kuwa anafunga ndoa ya kiserikali, aliona mkama kadharaulika kwakua yeye alishamuambia wafunge ndoa ya namna hiyo lakini Mage alikua akikataa.  Akiamini kuwa labda akimtishia kuhusu waototo Mage atarudi nyuma na kuahirisha kuhusu ndoa, mume wangu alimtishia na kumuambia kuwa kama akiolewa atawahukua watoto na hataruhusu awaone.


Mage hakuonekana kujali hata kidogo, alimuambia kuwa ni watoto wake anaweza kuwachukua na hajali. Alimuambia “Hata mimi nimchoka kukulelea mitoto yako, unafikiri ni kazi rahisi kuhangaika na watoto wakati wewe unafurahia ndoa na mke wako! Wahcukue tena siwataki kabisa niache nikale maisha na mume wangu!” mume wangu aliumizwa sana na maneno yake mpaka kufikia kuwachukua watoto na kuniletea, mwanzo wa ndoa Mage hata hakujali, mume wangu ndiyo alikua anahangaika, kisirani kilongezeka.


Kila siku alikua ni mtu wa kukasirika, kutukana na kufanya mambo ya ajabu, kufanya vituko na kwa bahati maya alaijaribu kuwaumiza watoto ili angalau walalamike kwa Mama yao na kutaka kaucha ndoa lakini haikusaidia. Mara nyingi nilikua nashangaa namna ambavyo mume wangu alikua akimtumia meseji Mage kuhusu kulalamika kwa watoto, namna ninavyowatesa na kila wakati alikua akiwapiga na kuwanyanaysa ili mradi tu wakalalamike kwa Mama yao, mume wangu aligeuka na kuwa ndiyo Baba wa kambo wa wanae huku mimi nikiwa ni mtetezi wao.


Pamoja na kufanya yote hayo lakini Mage hakurudi, kikubwa ni kwamba walizidi kugombana na kuwaumiza watoto. Watoto walipokua wakilalamika kwa Mama yao waliishia vipigo na hivyo kuwa wananyanyaswa pande zote. Mara nyingi walikuja kwangu kulalamika, walikua wakimlalamikia Baba yao pamoja na Mama yao, kuna kipindi walikua hata hawatamani kwenda kwa Mama yao kwakua tu walikua hawana amani huko. Niliongea na mume wangu lakini alikua anakua mbogo na alikua akinipiga mara kwa mara.


Badala ya mume wangu kufurahia namna nilivyokua nikiishi vizuri na wanae kama wanangu, namna watoto wake walivyokua wakinipenda yeye alikua akikasirika, mara nyingi sana alika akinitukana kuwa najipendekeza kwa watoto, nawadekeza kama mayai na nataka wanipende mimi zaidi kuliko wanavyompenda yeye lakini sitafanikiwa. Nilishindwa kumuelewa, alitaka niwe wale Mama wa kambo amabo kila siku ni kupiga na kunyanaysa watoto, lengo lake kubwa ilikua ni mimi kuwanyanyasa watoto ili tu walalamike kwa Mama yao na yeye kuchagua watoto zaidi ya mume.


Mwanzoni Mage alikua akimpigia mume wangu simu kujua hali za watoto, lakini waliishia kugombana ikafikia hatua hampigii tena yeye simu na anipigia simu. Alishangaa naongea naye vizuri, namjibu vizuri na nampa watoto kuongea nao, alishangaa kuona sina kisirani kama anavyoambiwa na mume wangu na namna watoto wanavyochangamka wakiwa na mimi. Mwanzo alifurahia ile hali, lakini ghafl;a niliona nayeye anaanza kisirani, sikujua kimetoka wapi lakini alianza kuniksirikia.


Akipiga simu hakuna salamu, hakuna tena kuongea kidogo kidogo, hakuna chochote kikubwa kwake ni kutaka kuongea na watoto wake na baada ya hapo anakata simu kwa hasira. Siku moja niliamua kumuuliza ni kwanini anafanya vile lakini aliishia kunitukana, alikua akiniambia kuwa najipendekeza na kuwajaza wanae maneno ili tu wanipende mimi zaidi yao. Kila siku maneno “Hao ni wanangu tu na wewe ni mama wa kambo, hawawezi kukupenda zaidi yangu!” yalikua hayatoki  mdomoni, kila mara alikua akituma meseji za ajabu ajabu.


Matusi na kuniambia nizae wangu na kwamba kama ni rahisi basi na mimi niingie leba. Niliumia sana kwani bado sikua na mtoto na nilikua nahangaika, mume wangu tulikua tukigombana kila siku kwaajili yake, niliumia kwakua nilikua najitahidi kuwa Mama wa wanae lakini hakuna mtu aliyekua akiona. Kuna kipindi nilimkasirikia na kumuambia kuwa kama anaona mimi sifai kuwa Mama basi aje kuwachukua wanae, aliishia kunitikana na kuniambia ni mipango ya mimi na mume wangu.


Nilimshangaa kwani niliona kama ana akili ndogo sana, kwa akili yake eti alifikiri kuwa mimi na mume wangu tumekaa na kupanga eti kunyanyasa watoto ili yeye akasirika na kuondoka kwa mume wake na kuja kuishi na mume wangu. Sikumualewa na sikujua kama ana akili za namna gani kudhani kuwa labda kuna mwanamke ambaye atapenda mume wake kuchepuka na mwanamke mwingine, nilishangaa, lakini sikutaka kuumiza kichwa changu, nilifanya yangu kama Mama kuwalea wanae na kuacha wapambane wenyewe yeye na mume wangu kwa namna ambavyo wanajua kivyao.


***


Pamoja na kufunga ndoa lakini Mage hakuwahi kupelekwa ukweni, ndugu pekee wa mume wake aliokua akiwafahamu ni wale aliokua akitambulishwa na mume wake, kila wakati alikua ni mtu wa kudanganywa kuambiwa kesheo keshiokutwa na sijui lini nitakupeleka. Hali ile ilimpa shida kidogo, alikosa amani na kuwa mpweke, kwakua mume wake alikua ni mtu wa kusafiri safari alijikuta anabvoreka. Bado  mume wangu alikua akimsumbua kumtafuta, kumtumia meseji na vitu vingine vingi.


Mwanzo aliacha kujibu lakini baada ya kuwa mwpeke sana alianza kujibu, walianza kuchat mara moja moja. Hali ya ndoa ya Mage haikua nzuri sana, alikuja kumfumania mume wake kumbe alikua na wanawake wengine wawili ambao alishawatolea mahari na kila sikisafiri basu husafiri na mwanamke. Walikua wakigombana mara kwa mara na kila wakati wakigombana Mage alikua akimpigia simu mume wangu kumuambia matatizo yake.


Mume wangu alipenda, ile hali ya Mgae kumhitaji ilimgaya kujisikia vizuri na wakati akifanya hivyo basi alikua akiua ndoa yangu kwani nyumbani alikua si mtru wa kujali, alikua ni mtu wa hasira. Pamoja na Mage kumtumia kipindi akiwa mpweke lakini hakumtumia kama mpenzi wake, alimtumia kama shoga yake, Mage alianza kuchepuka lakini hakuchepuka na mume wangu bali alikua na wanaume wengine, mume wangu alijua na alizidi kukasirika. Alikua akichepuka na vijana wengine na alipoulizwa na mume wangu alimuambia kuwa hatembei na mume wa mtu.


Kwa mume wangu alikua hataki chochote, alijifanya rafiki tu, mume wangu alikua akikasirika lakini alikua hawezi kuacha kuwasiliana na Mage. Hasira zote za kauchwa na kutokufanywa hata mchepukoa linishushia mimi na watoto wake. Hakujali hisia za mtu mwingine ziadi ya hisia zake, alikua anaweza kufanya kitu chochote kibaya bila kujali kama kinaniumiza mimi au wanae. Kila alipokua akikorofishana na Mage kwasababu ya umalaya wake alikua akiwatukana wanae na kuwaambia hata hana uhakika kama ni wake atawarudisha kwa Mama yao.


Lakini baada ya siku mbili tatu basi Mage akituma meseji hata bila ya mume wangu kuomba msamaha ananywea na kurudisha mapenzi akiamini wakati huo kabadilika ingawa haikua hivyo. Siku ya Mage kufumania kwa mume wake mume wangu ndiyo aliafanya huo mpango, mume wa magea liakua si mtu wa kufuatilia, alikua na mambo yake na wala hakua na muda huo au hakua akimpenda kihivyo. Lakini mume wangu alikua akifuatilia kila kitu mpaka kufikia hatua ya kuhack simu ya Mage.


Alijua kila kitu na Mage alipokuja na yule kijana nyumbani kwetu alijua fika ni bwana wake na alitaka kumharibia. Alimpigia simu mume wake na kumuambia sehemu alipo na mwanaume, mumewe alienda kumfumania na kumfukuza. Alipofukuzwa na mume wakwa ndiyo walianza kuishi pamoja, alikua hana pesa lakini alikuja kuchukua pesa alizokua kanipa kwaajili ya kwenda kumfungulia, akampangia nyumba nzima na kuanza kuishi kama mke na mume. Alifurahia sana kwani Mage hakua na pakukimbilia na kuamua kumkubali yeye.


Tatizo lilikuja pale ambapo Mage alimchoka na kuamua kwenda kuomba msaamaha kwa mume wake, mume wangu aliumia sana na kuapa kabisa kuwa hawezi kumtafuta tena. Kweli alibadilika lakini ilikua ni kwa muda, alikuja kugundua kuwa kumbe mume wa mage hakumsamehe Mage na alitaka kumpa talaka, siku hiyo hiyo aliposikia alienda kumuomba Mage waishi pamoja tena lakini Mage alikataa, alimuamia kuwa hawezi kuishi na nwanaume mwingine kwani bado alikua anampenda mume wake.


Aliondoka katika nyumba aliyokua kapangiwa na mume wangu na kwenda kuishi kwao. Lengo ni kumuonyesha mume wake kuwa kabadilila, alijua kuwa kama akiishi na mume wangu na mumewe kujua basi asingeweza kusamehewa kwani moja  ya vitu ambavyo mumewe alilalamikia nikuwa wametengana kwa muda na yeye akaamua kwenda kuishi na mwanaume mwingine hivyo hamtaki kwani hana heshima.


Mage aliishi kwao kwa muda kwa matumaini kuwa mumewe atamrudia lakini alishanagaa mchakato wa talaka umeenda harakaharaka na mumewe kamuacha kwa talaka kisha kaenda kumchukua mke wake wa zamani na kuanza kuishi naye. Hapo ndipo alijua na kukubali kuwa kaachika, hali yake ilianza kuwa mbaya, alianza kuwa mtu wa mawazo, hasira zake alikua akizipeleka kwa watoto wake, akiwafuata shule na kuwapeleka kwake anakaa nao hata siku mbili lakinia nawanyanyasa na kuwafanyia vitu vya ajabu.


Kitendo hicho cha kuwachukua watoto kinguvu nguvu kilimfanya mume wangu kumkasirikia, walikua wakigombana wanatukanana lakini hakujali, alikua akiwachukua anaenda nao wkake yeye anatoka na kwenda kunywa pombe. Kwao alishaondoka na kuamua kuishi kivyake, kila alipowachukua watoto mume wangu alienda kuwachukua, walikua wakionana, kutukanana na kununiana lakini siku iliyofauata alienda kuwachukua tena shuleni na mume wangu alienda kuwachukua, aliufanya kama mchezo flani, mimi sikuingilia chochote kwani kipindi hicho nilikua nakaribia kujifungua.


Sikutaka kitu chochote kuingilia kwenye mimba yangu, ingawa niliumia lakini nilisema ni watoto wao wanaweza kuwafanya chochote kile na si kazi yangu mimi kuwaingilia. Nilitaka kujifungua salama, mume wangu alijaribu kuigiza sana mbele yangu, alikua anajifanya kabadilika na mimi nilikua mjinga kuamini labda alikua kabadilika kwani wakati huo nilikua sifahamu chochote kilichokua kikiendelea katika ndoa ya Mage, sikujua kama kaachika na talaka kashapewa.


Nilianza kuwa na wasiwasi pale alipogoma mimi kwenda kwetu au kutafura mtu wa kunihudumia, sikujua mipango yake na wala sikujua sababu zake. Alionekana kujiamini sana na kila wakati alikua akinipa moyo kuwa kila kitu kitakua sawa ingawa mimi sikumuamini kwani sikua hata na binti wa kazi.


“Anafanya nini hapa? Hiki ni kitu gani unanifanyia mume wangu, hata kama umenichoka si kwa kiwango hiki, huyu mwanamke anafanya nini nyumbani kwangu?”


NIlimuuliza mume wangu baada ya kuingia ndani na kumuona Mage sebuleni kavaa kama anaishi kwangu.


Lakini Mage anafanya nini hapo? Ndoa yake ishavunjika na sasa yuko huru hvi ni kwamba Eric kaamua kumuoa na kumchukua kuishi naye? Vipi mke wake atakubali kuishi na Mage? Endelea kufuatilia ukurasa wangu wa Instagram @iddimakengo na Facebook Iddi Makengo


SIMULIZI; BABA WA KAMBO!—SEHEMU YA TISA


“Hembu tulia kwanza, huyu kaja kukusaidia, acha kupaniki, badala ya kufurahia kua umepata msaidizi unakasirika, nyie wote ni watu wangu wa karibu hakuna haja  ya kukasirikiana.”  Mume wangu aliongea hukua kijicheksah chekesha, alinishika ili kunikalisha chini lakini sikukubali, pamoja na yote niliyokua nimevumilia lakini sikua tayari kuishi nyumba moja na yule wmanamke achilia mbali yeye kunihudumia uzazi.


“Kwahiyo ndiyo maana ulikua hutaki niende kwetu kwasababu ya huyu mwanamke?” Niliuliza lakini mume wangu hakua na jibu, nilimuona kama akipaniki na kuanza kukasirika, alikua anafura na kutaka nianze kumbembeleza yeye, lakini sikujali.


“Presha ipende itakavyompanda lakini mimi nataka kujua, huyu mwanamke anafanya nini kwangu?” niliendelea kumuuliza kwa hasira, aliongea maneno mengi ya kunichanganya changanya, sikumuelewa kabisa.


Nilimuambia nipe mwanangu niondoke, sikua tayari kudhalilishwa kiasi kile.


“Unaenda wapi sasa?” Aliniuliza.


“kwetu, kwani wewe ulinikuta wapi, si ulikuta ninaishi nakula na kulala, naondoka narudi kwetu.” Niliongea kwa hasira huku nikimnyang’anya mtoto, mume wangu alijua natania, alijaribu kunielezea kuwa hakua na nia mbaya bali yeye ndiyo alimuomba Mage kuja kunisaidia uzazi eti kwakua yeye tayari alsiahazaa na anajua hayo mambo, alijiongelesha sana lakini sikujali.


“Wewe hujajielewa, umpumbavu kabisa! Ungejua ninayopitia, ungekua na utu ukajua namna unavyoniumiza usingefanya huu ujinga, naondoka na sitaki tena kurudi katika nyumba hii! Mwanaume gani hukubali kauchika, huyu mwanamke hakutakia, kila sikua ankuacha na kukurudia, kwanza ni mke wa mtu ana ndoa yake lakini hata hujali!” Niliongea kwa hasira.


“Hapana huyu kashapewa talaka, hata si mke wa mtu….” Aliongea akidhani kama itasaidia lakini ndiyo kwanza likua anazidi kunichefua.


Nilimchukua mwanangu kinguvu na bila kuchukua kitu chochote nilitoka nnje kuondoka, aliponiona kama nikoa siriasi alininyang’anya mtoto tena, alianza kuniambia kuwa sikwenda na mtoto na kama naona kuwa siwezi kuishi kwake na kufuata masharti yake basi nimuachie mwanangu. Aliongea kwa kujiamini hata Mage mwenyewe alishangaa, wakati wote huo tukigombana Mage alikua kimya akituangalia, lakini baada ya kusikia yale maneno aliingilia kati.


“Mimi naona sihirajiki hapa, sikuja kwa nia ambaya nilikuja tu kukusaidia lakini kama hutaki basi mimi naondoka. Sitaki kuvuja ndoa yenu najua unayopitia mimi ni mwanamke hivyo sitaki kuona mwanamke mwenzangu akiteseka.” Aliongea kwa utaratibu sana hukua kijishusha, nilizidi kukasirika kwani nilijua kabisa kuwa anaigiza na anataka kuonekana kuwa yeye ni mwema, mume wangu alivyokua mpuuzi alimuamini.


“Unaona mwenzako kaja kwa nia nzuri, hivi kwanini hutaki kusikiliza, kaa tuongee iliangalau ujue nini kinaendele, kuwa na hasira namna hii hakusaidii!” Nilimuangalia mume wangu na kutamani kutapika kabisa, nilishindwa kuelewa kama kalogwa au ana matatizo gani, kwetu kuna shid alakini nilijua kabisa siwezi kuendelea kuishi na mwanaume wa namna ile, nilitaka kuwa na amani katika maisha yangu na nilijua kabisa mume wangu hawezi kunipa hiyo amani.


“Kama ni mtoto tu mchukue, ni mwanao, simhitaji, maziwa yapo dukani mwengi utanyonyesha.” Niliongea huku nikimkabishi mume wangu mtoto, hakuamini macho yake kujua kuwa kumbe nilikua siriasi na nilikua tayari kumuachia mtoto, alimpokea kwani nilishamuachia mikononi mwake, nilitopka nnje getini na kuita Bajaji kuondoka, sikujua ninaenda wapi lakini nilikua kama nimechanganyikiwa, nilsiavumilia mengi lakini sikua tayari kulivumilia lile.


Mume wangu kuona vile aliingia kwenye gari hararakaharaka mtoto mkononi na kuanza kunifuatilia, dereva wa bajaji alipomuona aliniambia ankuja nikamuambia asisimame, nilishachoka na nilitaka kukaa mbali na mimi, aliniuliza unaenda wapi nikamuambia sijui yeye aendehse tu kwena mbele mpaka hapo nitakapomuambia asimamishe gari.


Aliendesha lakini hakufika mbali sana, mafuta yalimuishia na alialzimika kupaki pembeni, mume wangu alikuja na mtoto na kunikabidhi,. Alipiga magoti kuniomba msamaha na kuniomba nirudi nyumbani. Nilimchukua mwanangu ambaye kipindi hicho alikua na siku mbili tu na kuanza kumnyonyesha kwania likua analia sana,. Mume wangu alianza kujielezea mambo mengi, alimlaumu  Mage na kusema kamloga na mambo mengi mengi sana, nilimsikiliza sana lakini sikumuelewa.


Nilimuambia kuwa mimi siwezi kuishi tane na yeye, nataka kuondoka na kuwa na maisha yangu kwani nilishachoka mambo yake, alinisihi sana lakini nilimuambia kuwa sasa hivi nina mtoto na tabia zake zinaweza kumuathiri mtoto. Aliniomba sana lakini sikukubali, aliniambia atabdilika lakinsi ikukubali, nilimuambia kabisa kuwa hawezi kubadilika na hata yeye analijua hilo kuwa hawezi kuabdilika ni kujidanganya tu kwa mimi kudhani kama atabadilika.


Tuliongea sana lakini mwisho alikubali kuwa kakosea, aliniambia kuwa mimi siwezi kuondoka.


“Kila mtu atanishangaa, mtotyo basoa ana siku mbili nikufukuze urudi kwenu au uende ukapange nyumba! Hapana , nitaondoka mimi, mimi ni mwanaume naweza panga hata chumba kimoja, watu wakija kusalimia watajua niko kazini lakini ndoa yetu iko salama, hata kama ni kuachana basi mtoto akuekue hata umalize uzazi, kwa hali yako hutakiwi kuhangaika na mtoto mitaani.”


Aliongea maneno ambayo nilikubaliana nayo, tulikuabliana aondoke na mimi nitabaki nyumbani, Mama yangu kuja kunihudumia na kunitafutia binti wa kazi ila kwa wakati huo tusiseme chochote kwa watu kuwa tumeachana.


****


Mume wangu aliondoka na kuniachia nyumba, Mama yangu alikuja kunihudumia mpaka nilipomaliza uzazi, sikumuambia chochote na kwa hali aliyokua akiiona pale nyumbani alihisi kuwa mambo ni mazuri. Alikaa kwa mwezi mmoja na katika kipindi chote hicho alifahamu kuwa mume wangu kasafri mkoani kikazi hivyo hata suala la kutokuja pale halikumshangaza. Mume wangu kweli alitii alichokiongea, hakuja nyumbani na hakua akinisumbua, alipiga simu kuulizia kuhusu watoto kwani bado nilikua nikiishi na wanae.


Mage hakunisumbua tena, nilijua tu bado wapo na mume wangu lakini sikujali, nilishaanza kujibana kidogo kidogo pes aaliyokua akituima mume wangu kwaajili ya kuondoka na kutafuta Biashara. Ilikua inaniuma sana kumuona mume wangu akimpenda na kumthamini mwanamke mwingine ziadi yangu, nilijua fika kuwa pamoja na kuniachia nyumba lakini kamwe asingeweza kunipenda kama alivyokua akimpenda Mage.


Nilijua kabisa kuwa mimi ni chaguo lake la pili na kujua hata kama tukirudiana lakini Mage ndiyo ataendelea kuyaendesha maisha yake. Mume wangu hakua na kauli juu yake na mimi nililijua hilo, nilijua kabisa kuwa mimi ni namba mbili hivyo nilipanga kuondoka pindi nikiwa nimemaliza uzazi na kujipanga kufanya Biashara. Kila alipokua akinipigia simu mume wangu alikua akiniambia namna alivyobadiolika, naman ambavyo kajitambua na sasa hivi masuala ya Mage hataki kuyasikia, nilimuambia tu hongera.


Ingawa alitaka ufafanuzi kujua kama mimi nitarudiana nayeye lakini sikumuambia chochote, nilimuambia anipe muda na kusubiri mpaka mtoto akuekue. Sikutaka kumuudhi, nilitaka kumpeleka peleke na kumchuna chuna kidogo mpaka pale ambapo nitaona kabisa kuwa nina mtaji wakutosha ndiyo niweze kumuacha. Sikutaka kumuacha ghafla kwani nilijua kabisa kuwa ningeteseka na mtoto na sikua na namna nyingine yakuishi, nilijua fika ndugu zangu ahwawezi kunipokea wala kunisaidia.


Baada ya kumaliza uzazi na Mama yangu kuondoka mume wangualiniomba awe anakuja kuwaona watoto, sikuona kama nitatizo kwani ni wkake na ana watoto, nilimruhusu akawa anajuka mara moja kwa wiki kuja kuwaona watoto. Kila alipokuja hakusita kuniomba msamaha lakini mimi sikua tayari kumsamehe. Katika kipindi hicho kipindi ndiyo tu nimetoka uzazi mama yake alianza kuumwa, kwakua yeye ndiyo mtoto wa kiume kwao mkubwa na ana nafasi nzuri alilazimika kumchukua Mama yake.


Hatukua na namna hapo mume wangu alilazimika kurudi nyumbani, hakutaka Mama yake kujua kama mimi nayeye hatuishi pamoja, alirudi na tukawa tunalala chumba kimoja kwani tusingeweza kutengana vitanda wakati Mama amkwe yuko pale. Ile mume angu kukaa mbali nilikuja kugundua kuwa ndiyo ilikua sababu ya sisi kuwa na amani, kuja kwake karibu na kuanza kushi pamoja nilikuja kugundua kuwa kumbe walikua wakiishi pamoja na Mage kwenye nyumba moja na walikua hawajaachana.


Mume wangu alikua akimpigia simu mara kwa mara, usiku mmoja alikua akimpigia simu Mage kujua kuwa yuko na nani, ni kama alikua hamuamini. Hali ile ilinikera na kuanza kulalamika, kila siku tulikua tuinagombana na yeye alikua akishikilia msimamo kuwa mimi ni kama nimemuacha hivyo yeye kama mwanaume hawezi kukaa bila mwanamke. Nilikasirika na niliumia sana, nilikua najua hawezi kukaa bila mwanamke lakini iliniuma sana kuona kuwa mwanamke mwenyewe ni Mage.


Pamoja na kuumia kote lakini nilijipa moyo kuwa kile kilikua ni kipindi cha mpito tu, nilikua najiambia kuwa nikipata chakwangu naondoka na kwenda kuanza maisha yangu bila yeye. Nilimchoka na nilichoka tabia yake, mbaya zaidi ni pale alipokua akipiga simu na kumkosa Mage hewani au simu yake kuacha kupokelewa, alinikasirikia mimi na alitafuta sababu ya kugombana na mtu hata watoto wake alikua akigombana nao. Mama yake alikua mgonjwa sana hivyo hakuweza kuiona ile hali na sikuona sababu ya kumuambia.


Nilijua nitazidi kumchanganya tu kwani alikua hampendi Mage kabisa. Siku moja niliamka usiku, mtoto alikua analia, nilimuona mume wangu kakaa kitandani kashikilia simu yake, nilishangaa ni kwanini alikua kashaamka na mtoto analia yeye anamuangalia tu. Nilimuuliza kwa utaratibu kuwa tatizo ni nin? Nikamuuliza kwanini hamchukui hata mtoto na kumbemeleza. Hakunijibu chochote, nilinyanyuka ili kwenda kumchukua mtoto nimbembeleze, lakini kabla sijapigahjatua mbili mume wangu alinivamia.


“Siwezi kuendeshwa endeshwa na wanawake, mimi ni mwanaume na huwezi kunipangia kitu chochote, nitafanya kile ninachotaka na wala huwezi kunipangia chochote.” Alinishika na kunilaza chini, alinivua nguo kwani nilikua nikilala na nguo na kuanza kufanya mapenzi na mimi. Nilimtishia kupiga kelelee akaniambia nipige kwani hkuna atakaye nisikiliza, yeye ni mume wangu na anaweza kunifanya chochote kile. Alifanya mapenzi kwa nguvu, alikua na hasira na kwakua hakuniandaa basi nilikua napata maumivu makali.


Nilijirusharusha sana lakini kutokana na umbvo lake alinizidi nguvu, alifanya mapenzi hukua kinipiga makofi. Nililazimika kuvumilia, lakin hakuishia kupafanya mapenzi na mimi kwa njia ya kawaida, baada ya kumaliza kawaida alinigeuza na kuanza kunilazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile, alinishikilia chini na kunilazimisha, nilipata maumivu makali. Kilichoniuma zaidi nikuwa alikua akinifanyia vile mbele ya mtoto aliyekua kalala kitanda kilekile tulichokua tumelala sisi kwa upande mwingine.


Ingawa alikua ni mtoto wa miezi mitano lakini niliona aibu kama vile kanifanyia mbele ya mtu mzima.


“Tuone sasa kama huyo Mage atanisumbua tena, sasa hivi hata wewe tutakua tukifanya hivyo hivyo kinyume na maumbile, wewe ni mke wangu siwezi kwenda kuhanagika huko kwa wanawake wengine wakati uko hapo na una kila kitu!” Aliongea kwa suti ya juu baada ya kumaliza, nilikua nimelala kitandani, damu zinanitoka sehemu za nyuma, mume wangu alikua kakaa tu ananiangalia,taa niliyokua nimeiwahs awakati nataka kumuangalia mtoto ilikua inatumulika naona aibu kabisa.


Eric anamfanyia unyama mke wake mbele ya mtoto wake? Je hiyo ndiyo ilikua sababu ya kumganda Mage? Vipi ataweza kumuacha mage moja kwa moja? Lakini vipi mke wake atakubali kuendelea kufanyiwa hivyo? Vipi ataondoka? Hakikisha unakua wa kwanza kusoma simulizi hii katika ukurasa wangu wa Instagram @iddimakengo


SIMULIZI; BABA WA KAMBO!—SEHEMU YA  KUMI


Asubuhi mume wangu alikua mchangamfu kupita kiasi, alikua akiniongelesha na kujichekesha hata bila sababu ya msingi, mimi bado nilikua na hasira na nilikua na maumivu makali.


“Shika hii hapa…” Mume wangu aliongea huku akinikabidhi bulungutu la pesa, sikumuuliza ni za nini, nilizipokea kwa hasira na kuingia zangu chumbani, yeye alikua sebuleni na alikua anajiandaa kwenda kazini. Nilirudi chumbani na kuziweka kabatini, bado akili yangu ilikua haifanyi kazi sawasawa, nilikua baso sijajua nifanye nini.


“Hiyo ni zawadi yako, kama wewe ulivyonipa zawadi jana na mimi nimeona nikutunuku, nunua chochote kile unachokitaka, hayo ndiyo matunda ya kazi yako.” Meseji ya simu iliingia, niliisoma nikaishia kusonya, nilirudi kwenye ile droo na kuzitoa zile pesa, nilizihesabu na kukuta zipo milioni mbili kamili. Kimoyomoyo nilifurahia ingawa bado nilikua na maumivu ya mwili, wakati huo mtoto naye alianza kulia, nilimchukua kwa aibu, nilijisikia vibaya sana kwa kile kitendo alichonifanyia mume wangu tena mbele za mtoto.


Kuna wakati niliwaza kuondoka lakini niliwaza naenda wapi. “Lakini nina milioni mbili tayari…” Nilijisemea. “Ila kama hiki ndiyo ambacho kilikua kinamfanya kumpenda Mage naamini na mimi atanipenda!” Nilijiambia wakati nawaza kama niondoke au la? Siku ile iliisha vizuri, kesho yake mume wangu alikua anasafiri kikazi hivyo hatukufanya chochote, lakini aliporudi alinitaka tena kimapenzi, nilimkubalia nikijua kua itakua kawaida lakini alilazimishia tena kinyume na maumbile.


Sijui kwanini lakini nilijikuta namkubalia na wakati huu nilimuonyesha ushirikiano, nilikua naogopa, alitoa mafuta flani na kunipaka tukafanya vizuri, mchezo huo uliendelea nikaanza kuufurahia. Nyumba ilianza kuwa na amani tena, bado mtoto alikua mchanga hivyo sikutaka kufanya mapenzi kila siku, kila nilipokataa mume wangu alikasirika, alibadilika na kunilazimishia, kwa kuogopa nililazimika kukubaliana na kila kitu kwani niliona kwa kukubali nitamfurahisha na nyumbna itakua na amani.


Hali ya Mama yake ilikua inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, nilitumia muda mwingi kumhudumia, kila wakati Mama mkwe wangu alikua akiniomba msamaha kwa namna ambavyo zamani aliniudhi lakini alimalizia kwa kuniambia niwa makini na mwanae, nimtunze vizuri na nisiruhusu mtu yeyote kuingilia ndoa yangu. mimi nilimkubalia nikijua kuwa alikua ni mgonjwa na anampenda mwanae, sikujua sababu ya kusisitizia kuwa nimpende mwanae na kulinda ndoa yangu.


“Mwanangu kwani kuna kitu unakikosa kwa mume wako?” Sikumoma Mama mkwe angu aliniuliza.


“Hakuna Mama, kila kitu nakipata, mtoto wako amekua mwema kwangu. Nikweli kabisa, nafurahi umemzalia, alikua anahangaika sana na watoto…” Mama mkwe alisema, mimi nilishangaa ni kwa namna gani alikua akihangaika na watoto wakati tayari alikua na watoto aliozaa kabla yangu.


“Usije ukamtenda, wewe najua kuwa si mtu wa wanaume kama yule mwingine…”


Aliniambia, yalikua ni mambo ya ndani sana ambayo sikuona sababu ya kuyajibu, nilikua namuitikia tu nikitaka anyamaze lakini sikumuelewa alikua anamaanisha nini?


“Kuna wakati nilidhani mwanangu hawezi kuoa kabisa…” Aliniambia, nilimdodosa kujua alikua anamaanisha nini lakini hakunijibu, alinishukuru na kuniambia tu nisije kumuacha mwanae.


“Atakufa, unajua ana presha,a naa magonjwa mengi yanamsumbua, hembu hakikisha humuumizi, mimi ndiyo Mama yake namjua, Magreth alimtesa sana hembu wewe usiwe kama yeye!”


Aliendelea kunisisitiza na mimi niliishia kumkubalia, kila mara mazungumzo yake yalikua ni kuhusu mtoto wake, sikua nikimuelewa kabisa kwani alikua na maswali mengine ambayo yalikua ya ndnai lakini kila alipouliza alitaka nimjibu tena kwa ufasaha, nilishangaa sana na wakati mwingine niliona mpaka aibu na kuwaza inakuaje Mama mkwe anauliza maswali ya namna ile, yalikua ni mambo ya ndani, mambo ambayo hata mimi na Mashoga zangu siwezi kujadiliana naye.


“Si anafanya mapenzi vizuri lakini?” Siku moja aliniuliza, nilishtuka sana kwani si swali nililolitegemea kutoka kwake. Nilizuga ka kumuuliza kama alikua na njaa lakini ile hali ya kutokumjibu ilimchanganya zaidi, alizidi kuuliza na kutaka nimpe majibu. Nilimhakikishia kuwa mwanae yuko vizuri na hana tatizo lolote ni mwanaume kamili. Alionekana kufurahia, kwahiyo hata mtoto ni wake, maana huyu kafanana naye kabisa? Aliniuliza, ni swali ambalo lilinikera sana lakini kwakua ni  Mama tena mgonjwa sana sikua na namna zaidi ya kumjibu vizuri tu kuwa ni wake.


Maswali yeke yalinipa wasiwasi. Mume wangu hakua na tatizo lolote, alikua ni mwanaume barubaru na akiamua shughuli yake kitandani si mchezo, ingawa mara nyingi anapokua na mawazo anakua hafanyi chochote lakini sikuwahi kutilia shaka uanaume wake. “Kuwa makini na mali zake, wewe ndiyo mke wake hakikisha kila kitu kinakua na majina ya watoto wako, wanaume hawa si watu wa kuaminika, umeshamzalia sasa aachane na yule mwanamke wake ambaye alimloga, sitakia hata kumsikia!”


Aliniambia, hata mimi nilikua sitaki kumsikia na huo niliuona kama ni ushauri mzuri. Lakini kuna kitu kimoja nilikigundua, Mama mkwe wangu alikua akionyesha kuwapenda wajukuu zake wote, ingawa alipenda sana mwanangu lakini nilijua kuwa labda nikwakua ni bado mdogo, kwa upande wa Nancy na Joackim kuna kitu cha tofauti amabcho nilikihisi, mara kwa mara alikua akijilazimisha kuwa nao karibu, alikua akijichekesha na alipenda kulala kila wanapoingia chumbani kwake, niliona hicho kitu lakini sikusema chochote.


Kuna wakati alikua anapandwa na hasira anawafokea na kuwatukana matusi makubwa makubwa lakini akikaa vizuri anawaomba msamaha na kujifanya ulikua ni ugonjwa. Nilikua na wasiwasi nikihisi kuwa labda wale watoto si wa mume wangu, nikilinganisha na namna ambavyo mara nyingi mume wangu huwa mkali kwao nilihisi lazima kuna kitu, niliamua kuchunguza kivyangu vyangu ili kujua ni kitu gani kililikua kinamfanya Mama mkwe wangu kuwa vile analazimisha kuwapenda wajukuu zake.


***


Sikuwahi kupata jibu mpaka Mama mkwe wangu anafariki dunia, tulienda mpaka kwake kwa mazishi, siku ya msiba nilichefukwa sana kwani Mage alikuja tena bila aibu. Nilijizuia kukasirika lakini nilishindwa, nilijikuta napandwa na hasira natamani hata kumpiga hasa pale alipokuja kunisalimia. Nilishamuondoa katika maisha yangu na nilijua kama mume wangu akimuona basi ni lazima atataka kurudiana naye kitu ambcho kiliniuma zaidi, lakini mume wangu alimuona na hakuonekana kama kujali kabisa.


Wakati wa msiba alikua bize na watoto wake, alijifanya kama Mama anaye jali, nilimuangalia kwa hasira kwani wanae walikua wakiomboleza kikweli kweli wakati yeye alikuja kama kikejeli.


“Kuna watu hawana aibu? Marehemu anaweza kufufuka upya ampige makofi akija kujua kama huyu mwanamke kaja kumzika.”


“Nakuambia, huyu dada ni mshenzi sana, alimsumbua sana Mama wawatu na kijana wake leo kafa ndiyo anakuja.”


“Kaachwa ndiyo maana yule mwanaume kaoa mwanamke mwingine na Mama yake ndiyo kasimamia!”


Wamama flani aliokua wamekaa karibu na mimi waliongea, hawakua wakinifahamu lakini kwa walivyokua wakiongea walionyesha dhahiri kumfahamu Mage.


“Anaringa na hao watoto, Marehemu alilazimishia DNA hakua akiamini kua ni wajukuu wake!” Aliongea mmoja wapo, lakini kabla ya kumalizia na hata kutoa majibu nini kilitokea maombi yalianza na walilazimika kunyamaza, nilijikuta napandwa tu na hasira ya kutaka kujua majibu yake lakini mpaka msiba unaisha sikujua chochote.


Baada ya mazishi ya Mama mkwe wangu nilirudi nyumbani, nilidhani labda mume wangu ataamua kuondoka kwakua alikuja kwaajili ya Mama yake lakini hakuondoka, maisha yalirudi kama awali na mapenzi yalianza upya. Nilimruhusu mume wangu kuutumia mwili wangu atakavyo nikiamini kuwa labda hicho ndiyo kitu ambacho kitamtuliza, nilijipa moyo kumuambia kuwa ndiyo kitu ambacho roho yake inapenda na ndoa itakua na amani kama nikimfurahisha.


Maisha yaliendelea, mume wangu alibadilika kidogo na kuwa mtu mwema kwangu lakini si kwa watoto. Mara kadhaa alikua akiwatukana na kuwaambia wawe wanakaa ndani kipindi anapokua nyumbani, mabadiliko yale yalinishtua kwani kila mara akiwa anabadilika basi kulikua na kitu. Sikutaka kumuuliza chochote kwani nilijua kuwa nitazidi kumchanganya na akichanganyikiwa anakua mkali inakua shida kwangu. Siku moja alirudi nyumbani kalewa, ni muda sana nilikua sijamuona katika hali ile, alikua kakasirika sana.


Nilimuuliza tatizo lilikua ni nini aliishia kunitukana na kuniambia kuwa anataka tuachane, hataki kuishi na mwanamke kwani wanawake wanamchanganya maisha yake.  Mimi nilijua kuwa ni pombe na labda zikiisha asubuhi yake ataacha, lakini haikua hivyo, asubuhi yake alibadilika sana, alikua akimka na kujifanyia mwenyewe kila kitu, hakutaka hata niguse nguo zake kumnyooshea, ingawa nilikua naumia kwakua sikua nikijua sababu ya yeye kufanya hivyo lakini sikufanya chochote, nilinyamaza tu na kumuacha na mambo yake.


Hali ile iliendelea kwa wiki mbili hivi, ikafikia hatua hataki kurudi nyumbani, alikua akiondoka na kukaa hata mwezi bila kurudi nyumbani, nikimpigia simu zangu hapokei na hata nikienda kazini kwake anakaataa kuonana na mimi. Nyumbani alikua haachi tena pesa za matumizi, kumbuka hapo kaniachia wanae alozaa na Mage na mwingine niliyezaa naye. Hali ilikua ngumu sana, nilitumia akiba yangu yote mpaka ikaisha, hakukua na sehemu nyingine ya kwenda kuongea kila ndugu alikua na maisha yake.


Nilivumilia nikashindwa siku mojka nilimtumia meseji kuwa nawarudisha watoto kwa Mama yao kwani mimi siwezi kuwalea tena, alinijibu kuwa kama nikiwaondoa watoto wake basi niondoke nyumbani kwake hanitaki tena. Nilifikiria mara mbili na kusema poteli ya mbali, niliamua kuwarudisha watoto kwa Mama yao, ingawa ilikua ngumu sana kwangu lakini sikua na namna.


“Mama tutakua hata ombaomba lakini si kurudi kwa Mama…” Nancy aliniambia wakati nawaambia kuwa nataka wakakae na Mama yao kwa muda.


Nilijaribu kuwaelewesha kuwa lilikua ni tukio la muda lakini hawakukubali, walilia sana, walikua hawataki kabisa kwenda kuishi na Mama yao mzazi. Sijui mume wangu alipata wapi taarifa kuwa nuimedhamiria kuwarudisha watoto wake kwa Mama yao, siku ileile alikuja nyumbani, alikuja kuomba msamaha na kutaka kurudisha familia. Nilikataa katakata na kumuambia kuwa nimeshampigia simu Mama yao anasubiri kuwapokea na mimi niko tayari kuondoka katika ile nyumba kwani sioni tena thamani yangu pale.


Aliniomba sana msamaha, alikua akilia kama mtoto mdogo, mimi sikua tayuari kumsamehe, alinipa Shilingi milioni moja za kuanzia maisha, aliniambia kama kweli nataka kuondoka basi nihakikishe kuwa wmanangu hateseki, aliniambia kuwa yeye atatafuta binti wa kazi kwaajili ya kukaa na watoto lakini hawezi kuwapeleka kwa Mage. Aliongea maneno mengi sana na kusingizia msiba wa Mama yake kuwa ndiyo umemfanya kubadilika,a likua anaogopa kuishi katika ile nyumba kwakua alikua akimkumbuka Mama yeke.


Sijui ni kwanini lakini nilijikuta namuamini na kumsamahe, nilimpa nafasi nyingine na kumuambia kama ana tatizi basi ni bora kuongea na mimi kuliko kupotea kimya kimya. Alishukuru Mungu na kuniahisi kuwa atabadilika, hataondoka tena, nilimuuliza alikua wapi akaniambia alikua akiishi kwa rafiki yake. Jioni aliondoka akiniaga kuwa anaenda kuchukua vitu vyake, nilimruhusu, aliondoka lakini mpaka kufika saa sita usiku alikua hajarudi. 


Nilibaki ndani na wasiwasi nikiwa sijui atarudi saa ngapi, pale ndani kulikua na begi lake dogo alionekana kama kulisahau. Niliamua kulifungua tu kwakua nilikua sina chakufanya,  lilikua begi  la saizi, lilikua na nguonguo nyingi, nilikagfua kuangalia kama nitakuta nguo za mwanamke mwingine, lakini hakukua na nguo za mwanamke ila nilikutaka na vitu ambavyo vilinishangaza sana, sikuamini macho yangu niliona midoli mingi ya maumbile ya mwanaume, nilishaangaa mume wangu alikua anafanya nini na nyeti za kiume katika begi lake, nikiwa bado nashangaa sijui mume wangu aliingia saa ngapi lakinia likuja nakunikuta nakagua begi lake nimeshikilia vile vitu mkononi!


SIMULIZI; BABA WA KAMBO!—SEHEMU YA KUMI NA MOJA


Kuniona na vile vitu mkononi mume wangu alinivamia, hakuruhusu nimuulize vilikua ni vitu gani, alianza kunipiga mangumi na mateke huku akinitukana kwa kukagua vitu vyake, aliniambia kuwa hanitaki tena na anataka niondoke. Alinipiga sana, katika maisha yangu nilikua sijawahi kupigwa vile, mume wangu alionekana kuwa na hasira za ajabu, hazikua hasira za kawaida na wakati huu alivimba zaidi na haikua ile ya kupandwa na presha, hapana, ilikua ni hasira nyingine kabisa.


Nilipiga kelele lakini hakukua na mtu wa kunisaidia, mtoto alilia sana lakini hakujali, alinipiga mpaka nikapoteza fahamu. sikujua chochote zaidi ya kuamka asubuhi na kukuta niko hospitalini, kumbe majirani walisikia kelele usiku na kuja, mume wangu aliwasikia wakati wanakuja na kukimbia. Nililazwa hospitalini kwa wiki nzima, mume wangu alikamatwa na polisi na kufunguliwa kesi ya shambulio, alitoka kwa dhamana na kuambiwa asiniisohelee kabisa, nilirudi nyumbani baada ya wiki moja na kukuta tayari Mage kashawachukua watoto wake.


Sikua na amani tena katika ile nyumba, niliamua kuondoka kwenda kutafuta maisha yangu kwingine, sikua na pesa yoyote lakini niliondoka na kurudi kwetu. Wakati huu Mama yangua linipokea na kwa namna alivyoniona nilivyokua nimeharibika nikiwa hospitalini aliamini kuwa nina teseka. Nilirudi nyumbani kujiuguza, nilikua nimevunjika mbavu na mkono, ilinichukua muda kupona. Katika kipndi hicho mume wangu alikua akihangaika sana kunitafuta, ndugu zangu walikataa na mimi pia sikutaka kumuona.


Alituma ndugu zake, kule Polisi kesi ilikua unamuelemea na alijua kua atafungwa kwani aliniumiza sana, walishamlia pesa zake nyingi ili kesi ifutwe lakini wapi! Alianza kuhangaika na mimi kuniomba msamaha, alikua akiwatumia ndugu zake, marafiki zake na marafiki zangu. Aliniambia kuwa yuko tayari kufanya chochote kwaajili yangu ili tu nimsamehe na kufuta ile kesi. Alihangaika sana, lakini nilikua na hasira sana kumsamehe.


Pamoja na kupata dhamana akawa uraiani lakini hali yake ilikua mbaya, alikua mtu wa mawazo, hakuweza kufanya kazi vizuri mpaka ikafiia hatua ya kusimamishwa kazi. Hapo ndiyo nilishtuka kwani pamoja na kutamani kuachana naye lakini bado nilikua namtegemea sikua na kazi yoyote, niliwaonea huruma Nancy na Joackim nikaamua kufuta ile kesi ingawa niligoma kabisa kurudi kwake pamoja na kunibembeleza sana.


Maisha yaliendelea, kuna mjomba wangu mmoja ambaye alikua hajui kilichokua kikiendelea katika ndoa yangu, baada ya kuniona nimepigwa vile alinitafutia kazi na kuniambia nianzishe mchakato wa talaka, kusema kweli baada ya kupata kazi sikutamani tena kurudi kwa mume wangu, niliamua kuendelea na maisha yangu ingawa suala la talaka lilikua gumu sana. Nilikata mawasiliano na mume wangu na wala sikutaka kumuomba matumizi tena, alijaribu sana kunitafuta lakini sikua tayari kurudi.


Siku moja nilipigiwa simu, ilikua ni usiku, ilikua ni namba mpya amabyo siifahamu, nilipopokea nilisikia “Baba kanywa sumu, Mama njoo anakufa!” Simu ilikata, sauti likua ni ya Nancy, mwazo nilitaka kupuuzia lakini kuna kitu kiliniambia hapana, yule ni mume wako tena mna mtoto hutajisamehe kama kwelia kiwa kanya sumu. Nilitoka nyumbani usiku uleule, nilikua tayari naishi peke yangu na binti wa kazi, nilitafuta bodaboda na kwenda, kufika kweli nilimkuta mume wangu kalala chumbani anatoa mapovu tu.


Hakukua hata na maziwa mule ndani, nilifanya mpango nikampeleka hospitalini usiku uleule, hali yake ilikua ni mbaya lakini kwa bahati nzuri alipona,  hatukushirikisha polisi hivyo siku ya pilia liruhusiwa kutoka, bado alikua katika hali mbaya, sikutaka kujua sababu ya yeye kutaka kujiua lakini aliniomba kuongea na mimi. Tulirudi mpaka nyumbani, aliniomba msamaha kwa yote na kuomba turudiane, lakini bado nilimkatalia. Aliniambia twenda chumbani kuna kitu anataka kunionyesha, nilionyesha kuogopa lakini alinihakikishia kuwa hawezi kufanya chochote kwani kashajifunza.


*****


Sijui kwanini lakini nilimuamini, nilienda naye mpaka chumbani, alitoa  begi lilelile ambalo niliona vile vitu mpaka ikafikia hatua ya kunipiga. Alivitoa vile vitu, nilishtuka kidogo lakini aliniambia kuwa anayaka kuniambia ukweli kwani amechoka kunificha. Alinitolea vile vitu kisha akanitolea picha zake kipindi akiwa mdogo, picha moja alikua na Baba mmoja ambaye mimi nilikua simfahamu, nilimuuliza ni nani na ni kwanini alikua akinionyesha ndipo aliniambia kuwa yule alikua ni Baba yake wa kambo.


“Wakati nakua nilikua najua kuwa ndiyo Baba yangu, alinilea kama mwanae, sikujua kuwa ni Baba yangu wa kambo na wala sikujua kama Baba yangu alinitelekeza nikiwa na mwezi mmoja, alimuacha Mama yangu na kwenda kuoa mwanamke mwingine. Nilikua nikitumia jina lake na alikua akinipenda kupita kiasi, mama yangu alikua akinipenda pia na sikuwahi kujihisi tofauti na ndugu zangu wengine. Hakuna mtu mwingine zaidi ya Mama yangu aliyekua akijua kuwa mimi si mtoto wake.


Nikiwa darasa la pili wakati huo nikiwa na mika nane Mama alisafiri, alienda kijijini kujifungua mdogo wangu wa pili, kwakua nilikua nasoma aliondoka na mdogo wangu mwingine ambaye alikua na miaka minne mimi nilibaki nyumbani na Baba pamoja na mfanyakazi wa ndani. Usiku baba aliniambia niende kulala chumbani kwake, sikua nikiogopa lakini aliniambia kwakua Mama hayupo basi mimi niende kulala nyumbani kwake.


Nilienda lakini usiku wa manene nilishangaa Baba ananishika shika sehemu za makalio, nilishtuka, kipindi hicho nilikua mshamba sijui hata anafanya nini, aliniambia nisipige kelele kwani ananifundisha namna ya kuwa mwanaume. Mimi nilikubali akanipaka mafuta sehemu za haja kubwa na kuanza kuniingilia kinyume na maumbile. Niliumia sana lakini Baba hakujali, nilitoka mpaka damu, nilipiga kelele lakini sikupata msaada, mlango ulikua unafungwa na dada wa kazi alikua akimuogpa sana Mama.


Asubuhi Baba aliniambia nisiende shule, alinipa vidonge flani kumeza na kuniambia kua nitajisikia vizuri. Alinitishia kuwa nisimuambie mtu yeyote kwani nikimuambia tu atamuua Mama yangu, mimi nilishangaa kwani alisema ananifundisha unaume nilwaza kama ni hivyo ni kwanini sasa nisiseme na kwanini amtishie Mama yangu? sikua na jibu lakini ile hali iliendelea mpaka Mama aliporudi kutoka kijijini kama miezi miwili baadaye nilishazoea ile hali na mimi mwenyewe nilianza kupenda.


Sikumuambia mtu yeyote lakini Dada wa kazi alikuja kujua ila Baba alikua akimpa pesa nyingi tu ili asiseme. Siku moja wakati natoka shule nilienda chumbani kwa Dada, Mama alikua kasafiri kaenda kwenye msiba, kipindi hicho nilikua darasa la tano, nilimkuta Baba akiafanya mapenzi na dada wa kazi, sijui kwanini lakini nilipata wivu sana, nilishaanza kumpenda baba na niliumia kuchangia, nililia sana siku hiyo, baba bado alinitisha nisimuambie mtu kwani ataniua.


Lakini sikujali, kwa hasira Mama livyokuja nilimuambia kila kitu kuhusu dada wa kazi, mama alimuita na baada ya kumbana alikubali, Mama alimfukuza ila wakati anaondoka alimuambia Mama kuwa anahangaika nayeye wakati mimi ndiyo mke wa Baba. Mama alishtuka, mimi sikuwepo wakati anafukuzwa lakini usiku Mama alikuja chumbani kwangu,a kakagua nguo zangu na kukuta zina mabaki ya shahawa,a linikagua na kukuta nishaharibiwa, aliniuliza na kunibana sana nikaamua kumuambia.


Nilimuomba asimuambie Baba kwani amesema kama nikisema atamuua yeye na wadogo zangu. Mama alilia sana lakini alinituliza na kuniambia kuwa Baba hatakuja kunigusa tena, sikujua kwanini na wala sikujua kama Mama alifanya nini ila tangu siku hiyo Baba hakunigusa tena, afya yake ilianza kuzorota taratibu taratibu na haikuchukua miezi sita Baba alifariki dunia, sijui Mama alifanya nini lakini nilihisi kuna kitu, baada ya hapo Mama alisimamia biashatra za Baba na kutulea yeye mwenywe mimi na wadogo zangu.


Tangu siku hiyo Mama alikua na wasiwasi na mimi, alikua ni mtu wa kunikagua,a likua ajkinitafutia wanawake na kuhakikisha nakua nao, nilipokua mkubwa ndipo aliniambia ukweli kuhusu Baba kuwa hakua Baba yangu mzazi. Mama alizidi kunichunga ndiyo maana nilipokutana na Mage akawa ananisumbua aliumnia sana na kumchukia. Mage nilimpenda sana na ndiyo alikua mwanamke wa kwanza kumuambia ukweli wangu, hivi vifaa unavyoviona hapa ndiyo ambavyo mimi na Mage hutumia.


Kwa muda mrefu nimekua siwezi kufanya mapenzi bila kubostiwa, ili na mimi kufanya mapenzi inabidi hivi vitumika, hapo ndiyo nasisimkwa nakua na akili yangu, ndiyo maana nilishindwa na mpaka sasa nashindwa kumuacha Mage kwani yeye ndiyo ananifanyia huu mchezo na nisipofanyiwa nachanganyikiwa kabisa. Najua ni vibaya lakini nimeshindwa kuacha na yote haya ni kwasababu ya Baba yangu wa Kambo, alinifanyia hivi na sasa siwezi tena kuishi kwa amani, naomba unisamehe kwa yote.


Sikuambii ili kuhalalisha unyama wangu ila nakuambia kwakua nakupenda na naumia ninavyokufanyia, natamani ungekua kama Mage, nilikubaka kinyuma na maumbile si kwakua napenda bali nilikua nha hasiara na niliona labda kama ningefanya hivyo ningapata nafuu lakini haikuwezekana.” Alimaliza kuongea huku machozi yakimtoka, nilimuangalia na kumuonea huruma, nilitamani sana kumsaidia lakini hakuniruhusu aliniambia nimuache kwanza atafakari maisha yake.


Aliniambia niondoke na kunikabidhi ka briefcase flani, akaniambia nikifika nyumbani nikafungue, niliondoka na kwenda kukafungua. Kulikua na hati za viwanja, kadi za magari na kila kitu chake, pia kulikua na kabarua kalikoandikwa ka kifupi. “Nimeshindwa kuendelea na maisha, naomba uendelee kuwa Mama Bora kwa wanangu, Mage hawezi kuwalea, nashukuru kwa yote.” Kaliishia hapo, nilihisi kitu kibaya, nikachukua simu kumpigia lakini hakupokea, niliwapigia ndugu zake na kuwaambia waende kumuangalia.


Walifika chumbani na kukuta tayari ameshaaga dunia. Kumbe mule ndani kulikua na sumu nyingine na alikunywa pale nilipoondoka tu. Ni miaka sasa imepita lakini bado namkubuka, pamoja na mabaya yote aliyonifanyia lakini bado najaribu kuyakumbuka mazuri yake hata kama ni machache, naomba uandikie kisa changu na jaribu kukibadilisha kidogo kwani kuna ndugu zake wangi humu wanakusoma na nilitaka iwe siri ila nimeona ni vyema kuandika na wengine wakajifunza, nashukuru sana Kaka iddi kwa muda wako.


****MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG