IMEANDIKWA NA IDDI MAKENGO
MAMA MAGGIE; NAKUPENDA SANA ILA SHETANI AMEKUPENDA ZAIDI!—SEHEMU YA KWANZA
Nilikua nimelala kitandani, ulikua ni usiku wa manane, kama saa tisa hivi, ghafla nilisikia kama shuka linaondolewa nikasikia ubaridi flani. Nilinyanyuka kutoka kitandani na kuangalia ilikua ni nini? Nilimuona mke wangu kasimama katikati ya kitanda huku kashuikilia shuka, kawa kama kajifunika flani hivi.
JOIN US ON TELEGRAM
Kwa kawaida huw atunalala na taa, hatuzimagi, ni mazoea ambayo tumekua nayo kwa muda mrefu.
“Vipi, unafanya nini mbona hivyo?” Nilimuuliza mke wangu huku nikifikichafikisha macho kutokana na usingizi.
“Nimechoka, mimi nataka alaka yangu, huwezi kuwa unanisaliti kila siku!” Mke wangu aliongea kwa hasira, kwanza nilianza kwa kucheka, nilikua najijua na nilikua najua kabisa katika maisha yangu siwezi kumsaliti mke wangu.
Hata yeye nilijua hawezi kunisaliti, katika miaka kumi ya ndoa yangu nilishaona wanawake wengi lakini hata siku moja nilikua sijawahi kufikiria kumsaliti mke wangu.
“Unamaanisha nini kusema kuwa ninakusaliti?” Nilimuuliza baada ya kuacha kucheka kwani nilimuona kama yuko siriasi flani hivi! Alifunga lile shuka na kutaka kutoka nnje, loakini nilinyanyuka harakaharaka na kiumkimbilia mke wangu, nilimshika na kumrudisha ndani.
“Unataka kutoka hivyo wakati kuna watu huko nnje, hivi unafikiri Baba yako akitoka na kukuta umejifunika shuka atajisikiaje!” Nilimuambia kwa hasira.
Pale nyumbani nilikua nikiishi na wazazi wa mke wangu. Mama mkwe wangu alikua ana matatizo ya Figo hivyo alikua anahitaji kusafishwa mkojo kila wiki kwa maana hiyo ilimlazimu yeye na Baba mkwe wangu kuja kuishi pale nyumbani, kwani mimi na mke wangu wote ni wafanya kazi hivyo Mama alihitaji mtu wa kumpeleka hospitalini. Kwakua Baba mke wangu bado alikua na nguvu, Nilimuachia gari yangu kwaajili ya matumizi yake na mara nyingi mimi nilikua natumia gari ya kazini.
“Waaache waone, kwani wakati unafanya ujinga wako mimi nilikutuma, waache waone na kama ni kuachana tuachane!” Mke wangu aliongea, ilinishangaza sana kwani sikua najua anazungumzia nini kwani mimi sikua nimemsaliti.
“MBona umeshikilia sana hilo suala la mimi kukusaliti, lini nilifanya hivyo na kwanini usiku huu?” Nilimuuliza huku nikimlazimisha kusogea mpaka kitandani. Nilimkalisha na mimi kukaa huku nikimuangalia, alinikodolea macho kwa kama dakika mbili hivi kimya, mimi nilikua namkodolea lile jicho la niambie, sema nimefanya nini?
“Halima ni nani?” Mke wangu aliniuliza.
“Halima! Halima gani huyo mbona sikuelewi?” Nilimuuliza kwani alityaja tu jina moja, na kama ni Halima wapo wengi tu niliokua nikiwafahamu sasa sikujua anamzungumzia yupi na ni kwa maana ipi?
“Unaniuliza mimi sasa, wewe si ndiyo ulikua unamtaja usingizini?” Aliniambia.
“Usingizini?”
“Ndiyo! Nimekusikia wakati umelala unamtaja Halima, unamuambia kuwa unampenda na hunitaki tena, upo tayari kuniacha kwaajili yake!” Nilijikuta napandwa na hasira mpaka kutamani kumtandika makofi, lakini kwakua sipigi wanawake basi nililazimika kumsikiliza.
Kwa madai yake mke wangu alikasirika kwakua alinisikia naota kuhusu mwanamke mwingine. Alinieloezea mambo mengi amabyo niliyaongea usingizini huku akiniambia kuwa ndotyo hazidanganyi hivyo anataka kuniacha. Kusema kweli nilihisi kama ni utani, nikacheka na kumuambia kuwa hakuna kitu kama hicho ila yeye hakukubali, aliniambia kuwa hanitaki na anataka kuondoka.
“Inamaana unataka kuondoka kwasababu ya ndotyo?” Nilimuuliza.
“Ndiyo, wewe si unaona kitu kidogo kwakua wewe ndiyo umefanya, ninachokuambia nikuwa, mimi sikutaki, nilishakuambia tangu mwanzoni kuwa mimi huwezi kunisaliti, narudia huwezi kunislaiti, Mungu ana namna yake ya kuniambia mambo na ameniambia kupitia wewe, yaani unaongelea kuhusu mwanamke mwingine mbel yengu!” Aliniambia mwanzo nilijisi kama utani lakini baadaye nilijua kuwa mke wangu yuko siriasi baada ya kuvaa nguo akatoka na kwenda kulala chumba cha wageni.
Nilijaribu sana kumsihi kurudi chumbani tuyaongee kwani isingeleta picha nzuri kwa wazazi wake lakini hakukubali, alienda kulala. Asubuhi na mapema nilikua mtu wa kwanza kuamka, kitu cha kwanza nilienda mpaka chumba cha wageni kumuangalia mke wangu. Lakini sikumkuta, alikua hayupo, nilitoka nnje na kukuta milango imefungwa lakini si kwa vitasa bali kwa funguo, nilijaribu kumuangalia mke wangu sikumuona.
Nilijaribu kumpigia simu yake lakini ilikua inaita tu haipokelewi. Kuona hivyo niliingia ndani na kujiandaa kwaajili ya kwenda kazini. Njia nzima nilikua na mawazo, Gari ya mke wangu ambayo mara nyingi tunaitumia kwa yeye kunipeleka mpaka kazini kwangu kisha kuendelea na mambo yake akiniacha mimi kutumia gari ya kazini ilikua pale ila yeye hakuepo.
Nililazimika kupanda daladala mpaka kazini, njia nzima nilikua najaribu kumpigia simu mke wangu lakini alikua hapokei. Kusema kweli nilichanganyikiwa kwani sikujua ni kitu gani kilikua kimempata mke wangu, mpaka wakati huo nilikua naamini tu alikua na hasira na mimi kutokana na hiyo ndoto.
“Wanawake lakini wana mambo yaani ananikasirikia wkasababu ya ndoto.” Nilijikuta naongea, mwanzo nilihisi kama naongea peke yangu kcihwani lakini kumbe nilikua nawaza.
“Ndugu yangu mimi mke wangu aliwahi kwenda kwao kwakua aliota nimezaa nnje ya ndoa, yaani mpaka leo nadaiwa mtoto, hawa viuombe ni kuishi nao tu kwa akili.” Baba mmoja ambaye alikaa pembeni yangua linisikia na kuniambia. Nilijikuta nacheka tu nikiamini yataisha.
“Unaona, yaani hata nilikua sijui kama naota ila kanihama kitanda kaenda kulala chumba cha wageni na huwezi aminia subuhi kaondoka bila kuniaga, sijui ana hasira gani, yaani simu zangu hapokei kabisa!” nilimuambia, yule Baba alinipa moyo na kunipa stori nyingi za wanawake huku akiniambia kila kitu kitakua sawa nisiwe na wasiwasi.
Mpaka nafika kazini mke wangu alikua hapokei simu zangu, nilimtumia meseji kutaka kujua anaendeleaje lakini hakunijibu. Mpaka kwenye sa atano hivi za mchana ndipo alinitumia meseji.
“Tunatakiwa kuongea, mimi siwezi kuendelea kuishi hivi!” Aliniambia, nilimkubalia kuwa tunahitaji kuongea kwani nilikua sijamuelewa na nilikua sitaki kilichotokea jana yake usiku kitokee tena.
“Uchague kati ya mimi na huyo Halima wako, siwezi kushea mwanaume!” Alinijibu, nilijaribu kumpigia lakini hakupokea, basi nilisubiri mpaka jioni tulipoudi nyumbani.
Mke wangu hakunisemesha, nilitaka kuongea naye kujua tatizo lilikua ni nini lakini alionekana kuwa na hasira sana, alikua na kisirani mpaka Baba yake aligundua, ingawa hakuniuliza ila nahisi alimuuliza mke wangu. Usiku wakati wa kulala nilimuambia kuwa tunahitaji kuongea kwani kilikua ni kitu cha ajabu sana, ilikua ni mara yangu ya kwanza kugombana na mke wangu kiasi kile.
“Mimi sina chakuongea na wewe, ninachotaka kwasasa labda unipe tu talaka yangu!” Aliongea kwa hasira, mimi niliishia kucheka.
“Una akili kweli wewe, hivi unataka kuachana na mimi kwasababu ya ndoto?” Nilimuuliza.
“Kwahiyo unaona unayoyafanya ni mazuri, yaani umetembea na wanawake zako huko halafu unakuja kunisimulia kwneye ndoto nakuambia uancheka, hapana, mimi nataka talaka yangu na nitachunguza kujua huyo Halima ni nani?” Mke wangu aliniambia, tulibishana sana mwisho aliondoka na kwenda kulala chumba cha wageni, aliniambia kuwa hawezi kulala na mimi kitanda kimoja wakati akijua kuwa nina wanawake wengine.
Nilikua na hasira sana hivyo hata sikuhangaika kumbembeleza, nililala na nilipoamka asubuhi sikumuona mke wangu, nilijua labda siku hiyo atajisikia vibaya na kuja twende wote kazini lakini hakufanya hivyo na gari aliiacha. Nilijiandaa na kwenda kazini, wakati nikiwa kazini meseji zilianza kuingia, zilikua ni meseji nyingi za whastaapp, nilifungua na kukuta picha nyingi za mwanamke ambaye nilikua hata simjui.
Niliziangalia, zilikua ni picha za kawaida, zilitoka kwa mke wangu, mwisho niliona screenshot ya akaunt ya Facebook. Mwisho nilikutana na meseji, “Huyu ndiyo malaya wako, nimeshamjua Halima anayekupa kiburi!” nilzifuta zile picha zote kisha nikampigia simu mke wangu, nilimuuliza huyu ni nani akaanza kunitukana huku akiniuliza inamaana najifanya simjui?
“Najua mnajuana, yaani binti mnafanya naye kazi halafu unajifanya humjui, huyu si mnaongea kila siku kwenye simu yako, kwa taaraifa yako najua kila kitu!” Nilikua nishafuta zile picha alizonitumia, lakini aliponiambia kuwa ninafanya naye kazi nililazimika kuandika jina lake Facebook kuona kama nitamuona, kweli jina lilikuja na kuona zile picha, mke wangu alionekana kuzichukulia huko. Nilimuita msaidizi wangu na kumuuliza kama anamfahamu huyo mtu akawa kama hamjui, yaani alipomuangalia kwa mara ya kwanza hakumgundua lakini alipoangalia vizuri alimgundua.
“Namjua, huyu si Halima, yuko masijala, amehamia hivi karibuni kutoke Singida.” Aliniambia, nilimuangalia vizuri kuona kama nilishawahi kukutana naye hata kwa bahati mbaya lakini wapi, picha haikuja kabisa.
“Vipi bosi?” Aliniuliza.
“Hakuna kitu, ondoka kaendelee na mambo yako.” Nilimuambia, sikutaka kuendeleza mjadala, sikutaka mambo ya kuchunguzana sana. Alipoondoka akili ilianza kuwaza ni kwa namna gani nilikutana na huyo binti mpaka kufikia hatua ya kumuota tena kimapenzina mke wangu kusikia, niliwaza sana lakini sikupata majibu, kila nilipokua nikifikiria kama namjua akili ilikataa kabisa.
Mpaka narudi nyumbani nilikua sijapata majibu kuhusu Halima, nilienda mpaka kumuangalia anapofanya kazi nikagundua kuwa nilikua sijawahi hata kukutana naye kwa bahati mbaya, hata yeye aliponiona hakuonekana kunikumbuka. Nilimsalimia naye akanisalimia kama Bosi wake lakini hakuonyesha kabisa kunifahamu. Niliporudi nyumbani mke wangu alikua kakasirika zaidi.
“Nimechunguza na nimempata mwanamke wako, kumbe mnafanya naye kazi?” mke wangu aliniambia.
“Hembu kaaa sikiiliza mke wangu, sijui ni kwanini nimemuota huyo binti lakini mimi simfamu, sijui umemjuaje ila ndiyo mgeni na leo ndiyo mara yangu ya kwanza kumuona baada ya wewe kunitumia picha zake!” Nilijaribu kumuambia mke wangu lakini hakunielewa. Wakati huo tulikua chumbani, alitoka nnje kabisa, nilimfuata kwa nyuma lakini nilipofika sebuleni nilikutana na Baba mkwe akiangalia TV, nilizuga kuwa tuko sawa na kukaa kuangala Tv na Baba mkwe wangu.
“Kila kitu kipo sawa mwanangu?” Baba aliniuliza.
“Kipo sawa Baba, hakuna tatizo lolote.” Nilimjibu kwa mkato, aliniangalia kwa wasiwasi lakini hakusema kitu, wakati huo mke wangua likua kasharudi, alikua kakasirika na aliingia chumbani, bila kujali kuwa Baba yake alikua pale alitoa nguo zake na kuhamishia cbumba cha wageni. Baba mkwe aliniangalia kutaka niongee kitu lakini sikua na kitu cha kuongea, nilinyamaza kimya na kuendelea kuangalia TV.
Nilirudi chumbani, nikakaa kumsubiria mke wangu kuona kama atakuja kulala lakini wapi, nilijaribu kumpigia simu kuona kama atapokea lakini simu yake ilikua inatumika, kwa muda wa kama lisaa lizima hivi ilikua inatumika. Nikiwa kitandani nilipitiwa na usingizi. Kwa kawaida mimi na mke wangu huwa tunaamka saa nane za usiku kwaajili ya kusali, hivyo ulipofika muda huo niliamka, lakini kabla ya kusali nilisema hapana, kwanini nimuombe Mungu wakati mimi na mke wangu bado hatuko sawa.
Nilinyanyuka mpaka chumba cha wageni, niligonga mlango lakini haukufunguliwa, niliusukuma mwenyewe, nikawasha taa, nilimuona mke wangu kalala kitandani, nilimsogeloea na kumgusa.
“Mama Maggie! Mama Maggie!” Niliongea huku nikimshika lakini haukua ni mwili wa mke wangu, nilikuta kapanga mityo na kuifunika shuka huku yeye hayupo.
“Huyu kaenda wapi? inamaana kalala chumba kingine?” Nilijiuliza lakini sikupata jibu, nilihisi labda kaenda chooni lakini nilisubiri zaidi ya masaa mawili hakutokea. Nilijaribu kumpigia simu lakini simu yake ilikua haipatikani, nilikagua kagua na kukuta kuwa nguo alizokua amezivaa usiku ule wakati anaingia chumba cha wageni zilikua pale.
Niliendela kukagua kuangalia nguo za kazini ambazo aliingia nazo kwenye kile chumba hazikua pale.
“Huyu atakua kalala wapi?” nilijiuliza lakini sikupata jibu, usiku huo sikulala, nilitamani kugonga kila chumba ili kumtafyta mke wangu nikiamini kuwa yupo tu mule ndani lakini ulikua ni usiku, naishi na wazazi wake, sikutaka wajue kuwa tuna matatizo. Nilitoka mpaka sebuleni, kufika nikakaa mpaka subuhi nikiwa macho, niliamini kwakua kila siku tukigombana anawahi kuenda kazini basi siku hiyo akitoka atanikuta pale.
Nilisubiri mpaka asubuhi saa moja za ausbuhi mke wangu hakutoka, malengo ulikua umefungwa kwa funguo tu, vile vitasa vya ndania mambavyo vinafunga kwa ndani tu vilikua vimefunguliwa ikimaanisha kuwa aliyefunga mlangoa lifunga kwa nnje hakuweza kufunga vitasa vya ndani.
“Mke wangu kaenda wapi? Mbona tangu saa nane usiku niko hapa, hata kama ni kuwahi kazini si kwa namna hiii? Nilijiuliza bila kupata majibu na simu yake ilikua haipatikani kabisa.
Mambo ndiyo yanaanza, kama una rafiki yako muambie tu kuwa sasa hivi tumeanza simulizi nyingine na hii inasimuliwana Baba Maggie na nikuhusu Mama Maggie, naomba usipitwe kujua Mama Maggie yuko wapi? je kaamua kuondoka na kumuacha mume wake kwakua tu alisikia ndotoni akimtaja mwanamke mwingine, Je, Halima ni nani na ni kwanini anatajwatajwa hapa, nisikuchoshe wewe endelea kufuatilia hapahapa!
MAMA MAGGIE; NAKUPENDA SANA ILA SHETANI AMEKUPENDA ZAIDI!—SEHEMU YA PILI
Mpaka saa nne asubuhi nilikua bado sijaenda kazini, nilikua namsubiria mke wangu na kila nilipokua nikimpigia simu yake ilikua haipokelewi, inaita tu haipokelewi.
“Baba mzima, mbona uko hivi unaumwa?” Mama mkwe angu ambaye alikua anaumwa kalala kitandani hawezi hatakunyanyuka aliniuliza. Nilikua nimeingia chumbani kwake kumsalimia na kumuoga kuwa ninaenda kazini kwani nilishachoka kusubiri.
“Hapana Mama niko vizuri…” nilimjibu kwa makato, kusema kweli nilikua naumia kwani nilikua nikiona kabisa ndoa yangu inakufa kwa vitu vya kijinga tu.
“Njoo mwanangu….” Aliniambia, huku akionionyesha ishaa nimsogelee, nilimsogelea mpaka karibu na uso wake, alinyanyua mikono yake kwa shida na kunishika mashavu yangu, alinivuta kwake na kunibusu kisogoni.
“Mama Maggie amepata mume, mwanangu kapata mume lakini naona kama anataka kufa kifo kibaya.” Aliniambia, ghafla nilimuona Mama mkwe wangu akianza kutoa machozi, hakua akilia bali machozi yalikua yanatoka yenyewe.
“Kuna nini Mama mbona unalia?” Nilimuuliza.
Alifuta machozi yake kwa shida kisha akaniangalia na kuniambia.
“Hakuna kitu mwanangu lakini naona mwanaume anayeumia, naimbie, una tatizo gani na mke wako?” Mama mkwe aliniuliza, alikua akiongea kwa shidashida lakini alijitahidi nisikie. Ingawa nilikua na matatizo na mke wangu na nilitamani kupata mtu wa kumuambia lakini sikua tayari kumuambia Mama mkwe wangu.
Kwanza kutokana na hali yake niliona kama namchosha tu, lakini pia alikua ni Mama mkwe wangu, Mama wa mke wangu sikutaka kumuambia mambo yangu, niliona ni kama kumdahalilisha mke wangu mbeye ya Mama yake na mimi kujidhalilisha kuwa sina uanaume wa kutosha kudili na matatizo yangu.
“Mwanangu, wewe ni Baba bora, wewe ni mwanaume, sijui ni kitu gani lakini sura yako inaonyesha unaumia, usiumia sana mwanangu kuhusu mapenzi, yapo, tumeyakuta sisi na bado tutayaacha….”
Alinipa wosia mwingi, nilikua sijamuambia Mama mke wangu kitu chochote lakini ni kama alihisi kitu, alihisi kuwa mimi na mtoto wake hatuko sawa.
“Agness ameenda kazini bila hata kuja kuniona Mama yake.” Aliniambia, alionyesha huzuni sana, nilijisikia vibaya kwani ni kitu ambacho huko nyuma kilikua hakiwezekani. Mke wangu alikua akimpenda sana Mama yake, walikua karibu sana na mara zote kabla ya kwenda kazini alikua na utaratibu wa kwenda kumsalimia Mama yake.
Hata kama anapoingia chumbani Mama yake anakua amelala mke wangu alikua anambusu Mama yake na kuangalia mapigo ya moyo kisha kuondoka bila kusalimia. Alikua anampenda sana kiasi kwamba hata akiwa amesafiri asubuhi lazima aniambie nimsalimie Mama yake.
“Mama yangu anaumwa sana, sitaki kwenda kazini na kumuacha bila kujua kaamka au la?” Mke wangu alipenda kuniambia, kitendo cha Mama mkwe kuniambia kuwa mwanae hakwenda kumsalimia asubuhi kilinishtua na nikiunganisha na ile ya kumsubiri usiku kucha bila kumuona nilihisi kama mke wangu hajalala nyumbani.
“Hapana Mama, Mama Maggie hawezi kufanya hivyo, aliwahi kuondoka ausbuhi lakini ulikua umelala, alikuja kukuaga nadhani ulikua usingizini!” Nilijaribu kumuambia Mama mke wangu, nilitaka kumdanganya ili ajisikie vizuri, sikutaka ajue kuwa mwanae kalala nnje.
“Nashukuru mwanangu, nashukuru kwa kujaribu kunifanya nijisikie vizuri ila mwanangu akinigusa najua, nina kansa mwanangu, sina usingizi wa hivyo kila dakika niko kwenye maumivu, kila sikua asubuhi nakua nimeamka, wakati mwingine naamka kumsubiria aje aniguse nakusikilizia mapigo yangu ya moyo, napata faraja sana…”
Nilijikuta naumbuka, sikutaka kuendelea kumchosha Mama mkwe wangu, nilimuambia apumzike mimi nikatoka, nnje nilikutana na Baba mkwe wangu, nilimsalimia lakini naye aligundua kuwa siko sawa, aliniuliza ila mimi nilimuambia niko sawa na hakuna shida, nikatoka, nikachukua Bajaji na kwenda kazini, Gari ya mke wangu ilikua pale nnje ikimaanisha kuwa hakwenda nayo, sikutaka kuichukua kwani nilijua naenda kutumia gari ya kazini.
***
“Nimekumiss” Ni meseji ambayo nilitumiwa na mke wangu, ilikua ni jioni wakati nakaribia kutoka kazini. Nilishamtafuta mara nyingi hapokei simu zangu. Nilishangaa ghafla tu ananitumia meseji.
“Missing you too mke wangu…” nilimjibu, ingawa sikuelewa ni wkanini kanitumia wala sikujua mabadiliko ya haraka ya mke wangu lakii sikutaka kumjibu vibaya, bado nilikua nampenda, ingawa kichwa changu kilikua na maswali mengi lakini nilidhani kuwa nikikutana naye basi ndiyo nitaongea naye.
“Nimewaza sana kuhusu mambo uliyonifanyia nimeona tu nikusamehe, isitoshe wewe ni Baba bora, nimekusamehe mume wangu ila usirudie tena.” Alinitumia meseji nyingine, kusema lweli nilikua sijui kosa langu lakini kwakua sikutaka kuendeleza ugomvi, nikikumbuka sura ya Mama mkwe wangu, namna alivyokua akiumia asubuhi niliamua kaucha yapite.
“Nashukuru kwa kunielewa mke wangu, sitarudia tena, nitakua makini sana kwenye kuota.” Nilimuambia.
“Hahahahahah!” Alinijibu, sikumjibu kitu kwani niolikua na hasira, kichwa kilikua kina mawazo kuhusiana na mambo yaliyotokea siki mbili hizo.
“Mbona ndoa yangu ilikua haina shida kabisa, nini kimetokea, yaani mke wangu ananisamehe kwa kitu cha kijinga na mimi nakubali kama nimekosa! Hivi kuna nini kinaendelea!” nilijiuliza maswali yote hayo bila majibu, mwisho nilijikuta nalia mwenyewe kama mtoto, machozi yalinitoka na nilishindwa kabisa kujizua. Sikua na hamu tena ya kufanya kazi, nilitoka na kumuambia Derava naondoka, nilimuambia anopeleke ofiosini kwa mke wangu.
“Sijui alipolala na sitaki kujua, kama kajitambua na kuamua kubadilika absi nimemsamehe, siwezi kuweka vinyongo, sitaki kujua alichokifanya jana naondoka zangu naenda kumchukua mke wangu hata tutoke kidogo!” Niliwaza huku nikiwa kwenye gari, akili yangu ilikua inaniambia kuwa mke wangu alikua na mwanaume mwingine, alikua kalala kwake ndiyo maana hakulala nyumbani, nilijua hivyo na niliamini hivyo, lakini kiuhalisia sikutaka kujua hayo mambo, nilijua itaniumiza hivyo sikupanga hata kumuuliza chochote.
“Nikimuona namuongiza kwenye Gari tunaenda sehemu kupumzika mpaka usiku!” niliwaza, tulifika ofisini kwake, nilimpigia simu kwua nipo nnje nataka tutoke lakini siku yake haikupokelewa, nilimtumia meseji mbili zaote hazikupokelewa. Mke wangu ni mfanyakazi wa serikali, kwa sehemua lipokua alikua hayuko bize kabisa hivyo nilijua nikifika na kumuambia tuondoke basi isingekua shida kwake.
Baada ya kuona hapokei simu nilienda mpaka ofisini kwake, no ofisi ambayo inatumiwa na watu wengi, yaani si kama ana ofisi yake mwenyewe. Nilienda na kumuulizia.
“Agg mbona hayupo, leo hajaingia kabisa, kwani jana mlirudi saa ngapi maana alinipigia usiku amelewa…” Rafiki yake mmoja alianza kuniambia, kusema kweli nilijihisi kcuhanganyikiwa, kwanza kujua kuwa hajaenda kazini na pili kuambiw akuwa mke wangu alikua kalewa, yaani kalewa, mke wangu anywe pombe? Hapana, ni kitu ambacho sijawahi kukiwazia kabisa! Yule rafiki yake nilikua namuona tu, sikua na mazoea naye lakini yeye ni kama alitaka kuongea na mimi.
Kiuhalisia hakua na haja ya kuniambia kuwa mke wangu hajaenda kazini, kwamba kama mimi mume wake naenda kumtafuta nilikua najua kuwa yuko kazini, hata kama alikua kandanganya yeye kama rafiki alitakiwa ajiongeze hata kusema kuwa ametoka kidogo lakini aliamua kuniambia kabisa kuwa hajaenda kazini. Kuhusu kulewa nadhani aliniambia makusudi kwani hata kama kweli nilikua nimelewa na mke wangu yalikua hayamhusu, alitaka kuendelea kuongea lakini nilimkatisha.
“Ohhhh! Nimesahau, alikua hajisikii vizuri, sema aliniambia akiwa poa atakuja jioni kuna kazi anataka kumalizia ndiyo maana nikaja.” Nilimuambia, nikamshukuru kisha nikaondoka, sikutaka kuendelea kumsikiliza, hata kama ningekua namatatizo gani na mke wangu lakini mimi si mtu wa kuyatangaza tena sehemu ambayo anafanyia kazi, nilijua anaumbea mwingi lakini niliwaza kuwa hauwezi kunisaidia.
Niliondoka na kuanza safari ya kurudi nyumbani, nikiwa njiani mke wangu alinipigia.
“Bado uko hapo ofisii?” Aliniuliza.
“Hapana, nimetoka, nimefika ofisini nikakukosa nikaamua kuondoka.””Jamani Baby, yaani sasa mimi nitarudi na nani, unajua niliitwa na Mkurugenzi na simu niliahca ofisini, sasa itakuaje na mimi leo sijaja na gari, si unaninjua nikiwa na hasira sipendi kuendesha, asubihi nilikua na hasira sana lakini sasa hivi nimekusamehe niko sawa, kama hujafika mbali nipitie basi?” Mke wangua liniambia, nilikua kweli sijafika mbali hivyo nililuiambia Dereva kugeuza gari kwenda kumchukua mke wangu.
Nilifika ofisini kwao na kumpigia simu lakini alikua hapokei, nilisubiri kama dakika kumi hivi ndipo nilimuona anashuka kwenye gari, aliingia ofisini kwake harakaharaka ndipo alinipigia simu.
“Niko huku ndani, njoo tutoke wote.” Sikutaka kubishana, nilipanda mpaka juu nikamkuta, akajifanyakama anachukua mikoba yake kisha akanifuata na kunikumbatia.
“Nimekumisss sana mume wangu, yaani nimejua kuwa siwezi kukukasirikia muda mrefu, msamaha kidogo tu nimenywea!” Aliongea huku akijichekesha, nilijikaza sana nisifanye kitu kibaya kwani nilishikwa na hasira nikajua kama nisipojizuia naweza hata kumpiga makofi.
Sikuongea sana, sikutaka kutibua mambo, niliingia kwenye gari mpaka nyumbani. Tulivyofika na kusalimiana na wazazi wake mimi niliingia chumbani, lakini mke wangu alienda kumsalimia Mama yake moja kwa moja. Alikaa huko kwa muda wa kama nusu saa, aliporudi alikua amebadilika.
“Umemuambia nini Mama?” Alianza kuniuliza kabla hata sijajibu aliwaka.
“Unajua kabisa kuwa yule ni Mama yangu, anaumwa halafu unamuambia upupu wako, kwanini usingemuambia kuwa unafanya na umalaya mpaka inafikia hatua unawaota wanawake zako!” Hkunipa hata muda wa kujibu mke wangu aliamua kuwaka.
“Unamuambia Mama nimelela nnje, wkanini hukumuambia kuwa nimekuhama chumba, hukumuambia kuwa unataka kuniletea magonjwa, yaani wewe mwanaume ni mpumbavu, hivi unafikiriu unaweza kuninyanyasa katika maisha yangu! Uninyanyase kwa kipi hasa! Kama ni kazi ninayo, mimi ni mzuri na ninaweza kupata wanaume wengine tena wamaana kuliko wewe!”
Mke wangu aliongea bila kituo, alinitukana bila kujua sababu ya kutukanwa.
“Unaongea nini wewe? Hivi unaniona mimi mjinga kuongea mambo hayo na Mama yako, unafikiri nitapata nini nikimuambia tabia zako, mimi ni mwanaume na siwezi kusolve matatizo yangu kwa kumtangaza mke wangu. Nakupenda na tuna watoto, siwezi kukudhalilisha mbele yao!”
“Watoto unawajua wewe, watoto gani? Una uhakika gani hata kama ni wakwako, kujitia mwanaume wakati huna kitu chochote, nimekuambia achana na Mama yangu, kama una mambo yako malizana na mimi lakini si kumshirikisha Mama yangu!”
“Nitajifanya sijasikia kuhusu hiyo ishu ya watoto, ila naomba uniheshimu, mimi ni mume wako, lazima iwe na ndiahamu!” Nilimuambia kwa hasiraq kidogo, aliniangalia kwa dharau kishaakacheka.
“Utajua mwenyewe, usikie au ujifanye umesikia mimi hayanihusu, nimekuambia kuwa achana na Mama yangu, kama una kitu cha kuongea na mimi ongea na malizana na mimi, kama umenichoka njiache, njia nyeupe, sitaki maujingaujinga yako!” Mke wangu aliniambia, nilikua nimechika nikaona isiwe shida, yeye alitaka kuendelea kubishana lakini mimi sikutaka.
“Basi yaishe mke wangu.” Nilimuambia huku nikikaa kitandani, nilichukua simu yangu kuanza kuangalia vitu. Alinisogelea wka hasira kisha akanisukuma kwa kidole kichwani kama vile ananisuta.
“Yaise sawa ila ukome kujipendekeza kwa Mama yangu, kama unaona Mama nidili kamfufue Mama yako kaburini kisha jipendekeze kwake!” Aliniambia, mimi nimvumilivu lakini nilipandwa na hasira, nilinyanyuka harakaharaka nakutaka kumkunja mke wangu kumpiga makofi lakini nilijizuia.
“Hivi kwanini umtaje Mama Yasngu lakini?” Nilimuuliza huku machozi yakinitoka. Sijui kwanini Mke wangu aliamu kumtaja Mama yangu wakati anajua maisha niliyopitia. Baba yangu alifariki nikiwa darasa la saba, wakati huo nina wadogo zangu wanne na Mama alikua Mama wa nyumbani, ndugu wa Baba wlaimnyang’anya kila kitu. Mama kalazimika kuishi kwa kuuza nguo za mitumba zile za kuzungusha, tulikua hatuna sehemu ya kulala, tukawa tumepata chumba kimoja ambacho tulipewa na jirani yetu.
Hakikua chumba kama chumba lilikua ni Banda la mkaa ambalo aliacha kutumia akatupa nikawa naishi na wadogo zangu. Tuliishi kwa shida, kutokana na matatizo sikuweza kufaulu ila Mama alihanagiaka mpaka nikasoma private, tukiishi pale nilishuhudia Mama yangu akibakwa na vijana wawili mbele yangu nakumbuka ilikua usiku tumetoka kuuza matunda, wakatuvamia, wakanipiga sna na kumbaka Mama yangu mbele yangu.
Yote hayo mke wangu alikua anayajua, nilimuambia kwakua nilikua nampenda na namuamini, haiishii hapo, Mama alihangaika mpaka nikamaliza chuo, chuoni nilipata nafuu ya kusomeshwa na serikali na hapo ndipo nilimhamisha Mama na wadogo zangu kwenye lile banda la mkaa. Nilipomaliza chuo, ile napata kazi tu, siku naenda kuripoti kazini Mama yangu nalikua amelala tu akafariki dunia, hakula hata shilingi kumi yangu, hakugusa hata jasho langu, mke wangu alikua anajua na bado anamtaja Mama yangu.
“Mama yangu amekuja kujaje hapa, inamaana mimi kumpenda Mama yako imekua tatizo?” Nilimuuliza huku nikimsogalkea, nilijikuta namshika nguo kama nataka kumpiga lakini nilisita, kusema kweli ile nataka kumpiga tu niliona sura ya Mama yangu mbele yangu.
“Mwanangu, mwanamke hapigwi, kama mwanamke akikuudhi basi nanyuka ondoka tembea hasira zikiisha rudi.” Nilimuachia harakahartaka kama nimepigwa na shoti ya umeme. Niliondoka kama nakimbia na kutoka kabisa pale ndani, kwa hasira nilizokua nazo najua ningemuua.
Nilitoka na kuanza kutembea kwa masaa zaidi ya matatu, kurudi ilikua ni usiku, watu walikua wameshakula chakula cha usiku hakukua na mtu sebuleni, niliingia chumbani kuelekea bafuni, nilioa ile namaliza nataka kutoka mke wangu naye aliingia. Alikua anaongea na simu, kama anagombana na mtu wkenye simu.
“Kwahiyo huyo Malaya wako amekuambia hawezi kusafiri ndiyo unaniambia, kwanini usingeniambia tangu jana, mimi si nilikuomba sana twende wote ukakaataa….” Alikua anabishana na mtu upande wa pili.
“Hata kama ni mke wako, kwani kinakuuma nini mimi nikimuita Malaya, si umesema humpendi, wewe si ndiyo ulikua unaniambia niachane na mume wangu utanioa, nimemuita mke wako malaya unakasirika….”
“Nakuja lakini iwe mwisho, mimi nitamuagaje mume wangu, nakuja wkasasa kwakua mimi na mume wangu tumegombana ila mambo ya kusafiri kesho siwezi. Mimi ni mtu na heshima zangu, nina watoto natakiwa kuheshimiwa, sio unagombana na mke wako unakuja tu kunichukua kama katakataka flani hivi!”
Mke wangu aliongea kwa hasira, kabla sijajua nini chakufanya alikata simu, nilimsikia kama anatafuta kitu, mara baada ya muda kidogo nikasikia mlango ukifungwa kwa nguvu. Nilikaa bafuni kwa dakika kama kumi na tano hivi, kisha nikatoka, mke wangu hakua chumbani, nilivaa harakaharaka na kutoka mpaka chumba cha wageni, hakua huko pia nilitoka nnje na kukuta gari yake haipo. Nilirudi ndani kwa hasira ile naingia tu nikakutana na Baba mkwe.
“Ameondoka tena?” Baba aliniuliza, nilimuangalia bila majibu, nilimuacha na kuingia zangu chumbani, nikaanza kumpigia simu mke wangu kila nikipiga simu inaita mpaka inakata hapokei, simu ilikua imejaa chaji nilipiga simu mpaka chaji ikakaribia kuisha lakini mke wangu hakupokea wala kuzima simu.
Kwa ushauri wa mija kwa moja hakikisha unanunua kitabu changu. Kwasasa nina vitabu vinne, cha mahusiano ya kawaida hasa kwa wanawake, cha wanaume wenye changamoto ya kumfikisha mwanamke kileleni, cha Biashara na cha Interview na Ajira , chagua kinachoendana na tatizo lako.
MAMA MAGGIE; NAKUPENDA SANA ILA SHETANI AMEKUPENDA ZAIDI!—SEHEMU YA TATU
Mpaka wakati huo nilijua najua mke wangu anachepuka, sikua na sababu ya kuuliza lakini kilichokua kikiniumiza nikuwa nilikua sijui sababu yake ya kuchepuka. Kama kitandani nilikua vizuri, tena yeye ndiyo alikua hapendi kabisa kufanya mapenzi, mara nyingi alikua anafika hoi ananiacha njiani, nilikua namhudumia kwa kila kitu, hata pesa yake nilikua sijui inaenda wapi, lakini bado anachepuka, nilishindwa kujua nini chakufanya.
Nikiwa pale chumbani nikiwa sina hili wala lile, nilikua nazunguka tu chumba changu nikiwa sijui nimemkosea nini Mungu mpaka mke wangu kufikia hatua ya kunifanyia vile mlango uligongwa. Nilijua kuwa hakua mke wangu kwani huwa hatuna tabia hiyo ya kugongeana milango. Nilienda kufungua huku nikilazimisha tabasamu, nilikua nikiogopa kuwa mtu niliyekua naenda kumfungulia mlango labda angeniona na machozi na kutaka kujua nina tatizo gani.
Nilienda kufungua mlango, alikua ni Baba mkwe wangu, kwanza nilishtuka kwani mwanzo nilidhani ni binti wa kazi, haikua kawaida ya Baba mkwe wangu kunigongea, mara nyingi akihitaji kitu humpigia simu mke wangu na kumuambia hata kama ni kuongea na mimi anaweza kumtuma binti wakazi kuniita lakini sikuja kunigongea chumbani kwangu.
“Mwanangu naomba kuingia ndani…” Aliniambia kwa unyenyekevu, nilishangaa kwani hiyo haiokua tabia yake, nilikaa nimeganda kidogo, aliniangalia na kujua wasiwasi wangu.
“Nimekuja kwakua najua binti yangu hayupo humu ndani na nichaokuambia hata sebuleni naogopa kukuambia, nataka tuongee mwanaume kwa mwanaume!” Baba aliniambia, kusema kweli nilijua anachotaka kuniambia ni kuhusu mke wangu, sikutaka kumpa hiyo nafasi, sikutaka wazazi wake kuingilia kuhusu ndoa yangu.
“Baba kama ni kuhusu ndoa yangu mimi na mke wangu tuko sawa, kabisa, kama unaona kuna changamoto jua ni ndogo ndogo!” Nilimuambia kwa sauti ya juu kidogo.
“Mke wako yuko wapi?” Aliniuliza, nilitamani kudanganya lakini kwa alivokua ananiangalia ilinibidi kuzuga.
“Baba mimi na mke wangu tuko vizuri, sihitaji kuongea mambo yangu, nikihitaji nitakuja kwako.” Nilimuambia huku nikitoka nnje, nilitoka ili naye ajiongeze atokea na wkeli alitoka.
“Mwanangu, mizigo mingine ikikushinda unaitua chini hata kupumzika kidogo. Huyu mtoto akikuchezea mrudishe kwao hata miezi miwili ajue thamani ya ndoa!” aliniambia hukua akiondoka. Nilibaki nawaza hivi huyu mzee vipi anataka nimfukuze mwanae aende wapi wakati yeye na mke wake yuko hapa.
“Baba, huna haja hata ya kukaa na mimi, najua unawaza nimfukuze aende wapi wakati wazazi wake wako hjapa! Haana mwanangu kama hana nidhamu ya kukuheshimu wakati unaishi na na wazazi wakie unatakiwa kutufukuza wote humu ndani ilia one thamani ya mume. Unamfanyia yote haya unaishi na wazazi wako bado aanondoka na kukuacha humu ndani, hapana, fukuza wote! Mimi na Mama yako hatutakulaumu!”
Baba mke waliongea kwa uchungu sana, nikama alikua anasikia mawazo yangu, pamoja na kuniruhusu lakini bado nilimuambia kuwa mimi sina tatizo kabisa mke wangu bali kuna changamoto za kawaida.
“Nitaongea naye akija, unaonekana umeshakaliwa kichwani, mwanamke hapaswi kukufanyia hivyo!” Aliniambia.
“Baba hapana, nakuheshimu lakini naona kama unavuka miipaka kuingilia ndoa yangu, hayo ni mambo yangu mimi na mke wangu, nikihitaji ushauri nitakuja kwako kama Baba ila kwasa niache mimi na mke wangu na hili swala sitaki kulizungumzia tena!” Nilimuambia kwa hasira kabisa, aliondoka huku akisikitika lakini sikujali kabisa.
Baada ya hapo nilirudi chumbani na kuanza kumtafuta mke wangu kw aismu, simu yake iliita bila kipokelewa kwa muda mrefu sana, mwisho niliamua kupanda kitandani kulala. Nilikua nimechoka sana lakini huwezi amini asubuihi ilifika bila kupata hata lepe la usingizi wala mke wangu kurudi. Kusema kweli ilikua kama ni ndoto hivi, mke wangu kulala nnje kwa mara ya pili iliniumiza sana. Ausbuhi nilimpigia simu kutaka kuongea naye lakini aliikata, ila baada ya hapo alinitumia meseji.
Nilienda kazini, sikua na kazi ya kufanya lakini nilitaka tu kuondoka nyumbani, mchana wote mke wangu hakupokea simu zangu, hakujibu meseji zangu. Mpaka jioni mke wangu alikua hapokei simu zangu, nilitamani kwenda kazini kwao lakini niliona kuwa itakua kujidhalilisha tu, nilitamani kurudi nyumbani hata kulala lakini nikikumbuka Baba mke wangu nilijisikia vibaya jinsi nilivyomjibu saubuhi yake.
Mpaka muda wa kutoka kazini unafika nilikua sijajua niende wapi, mimi si mnywaji wa pombe lakini huko nyuma wakati wa ujana wangu nilishawahi kunywa pombe. Niliondoka na kwenda Baa, sikua na lengo la kunywa, nilitaka kutuliza tu mawazo, lakini kutokana na mawazo hasa nikipiga simu na kukuta inaita tu bila kupokelewa nilijikuta nakasirika na kuanza kunywa pombe.
Kama kawaida mwanzo ilikua chungu, lakini kila nilivyokua nikiongeza bia ya pili ilianza kuingia kichwani mwisho nililewa kabisa. Kwakua nilikua na muda mrefu sana sijawahi kunywa pombe nilijikuta nalewa tena sana, nilimpigia Rafiki yangu mmoja ambaye alikuja kunichukua na kunirudisha nyumbani. Nilifunguliwa mlango na Binti wa kazi, kwa bahati nzuri wakwe zangu walikua wameshalala.
“Mama amerudi?” Nilimuuliza binti wa kazi, aliniangalia kwa huruma kisha akatingisha kichwa kuwa mke wangu alikua baod hajarudi.
Nilihisi kama pombe inakata kichwani, lakini nilikua nimechoka sana hivyo moja kwa moja nilipanda kitandani, ilikua ni usiku sana, hata sikumbuki ilikua ni saa ngapi. Lakini nikiwa nimelala nimepitiwa na usingizi mke wangu aliingia chumbani, yeye alikua mzima kabisa, alikuja kama anchukua kitu na kutoka, kwani nilishtuka tu kutoka usingizini na kumkuta ameshikilia pochi yake, kuna kitu kingine anakitoa kabatini na aliponiona nimeamka alitoka kama vile anakimbia.
Pamoja na kulewa kwangu lakini nilipata nguvu, nilinyanyuka harakaharaka na kumzuia, nilimshika na kumuambia.
“Unaenda wapi usioku huu?” Nilimuuliza.
“Unaniuliza wewe kama Nani? Una mamlaka gani ya kuniuliza kwani nimekua mtumwa wako, mimi ni mke wako lakini nina kazi yasngu, umenisaliti….” Kabla ya kumaliza nilijikuta namtandika kofi la nguvu, sijui kwanini nilifanya hivyo lakini nilijisikia vizuri sana.
“Unaniuliza mimi ni nani? Inamaana wewe mwanamke ndiyo wakunijibu hivyo!” Nilimuuliza huku nikimtandika kofi jingine, lakini baada ya kumpiga kofi la pili akili yangu ilikua kama imeruidi.
“Nimefanya nini?” Nilijiuliza, “Hivi mimi ni mtu wa kupiga mwanamke kweli? Hapana?” Nilijisikia vibaya na kujikuta nasamehe kila kitu alichonifanyia mke wangu, nilipiga magoti na kuanza kuomba smamaha.
“Nimsamehe mke wangu, sijui ni kitu gani kimenitokea mpaka kukupiga, umenikosea lakini si sawa mimi kukupiga….” Mke wangu ni kama alipata nguvu flani, alinisukuma kwa mguu yaani kama ananipiga teke nikadondoka chini.
“Mshenzi mkubwa wewe, yaani wewe ndiyo wakunipiga mimi? Unanipiga mimi? Hunijui, umefanya umalaya wako huko mimi nimekaa kimya, nimetoka tu kidogo nimeamua kuwa na maisha yangu unajifanya kunipiga, aisee nitakuonyesha. Au ulifikiri kuwa mimi ndiyo wale wanawake wakupigwa pig3wa na kujiliza kama wajinga, hapana Baba nitakuharibia maisha mpaka utanijua mimi nani?” Aliongea kwa hasira, hakuonekana kuumia kihivyuo lakini kitendo cha mimi kuomba msamaha kilimpa nguvu.
“Naondoka, sitaki kuishi na wewe, kama ni ndoa nataka ife, Baba yangu hajawahi kunipiga lakini wwe unanipiga, hapana! Mamamamamma! Mamamamam! Nakufaaaa! Mume wangua naniua!” yaani ghafla alianza kupiga kelele hukua kilia, alifungua mlango na kutoka kuelekea chumbani kwa wazazi wake. Ingawa bado nilikua ninanuka pombe lakini pombe iliisha kcihwani kabisa, nilikua nimempiga mke wangu kweli lakini sikutaka wazazi wake wajue has aMama yake.
Niliwaza hali yake na kuona kuwa hahitaji kushirikishwa kwenye mambo hyo, nilimkimbilia mke wangu na kumshika ili asiende chumbani kwa wazazi wake lakini ndiyo kama nilimchochea,a lipiga kelele nyingia kilia kupigwa na kusema kuwa anataka kuondoka. Baba yake alitoka na kutukuta tuko sebuleni tunashikana.
“Kuna nini hapa? Hivi unajua kuwa Mama yako ndiyo ameanza kupata usingizi halafu wewe unaanza kupiga kelele?” Baba mkwe alimuuliza mke wangu kwa hasira.
“Hapana Baba, sikia, huyu mwanaume ni mzinzi, juzi nilimfumania, alikua anaota mchepuko wake, mimi nikakasirika na kuondoka, basi yeye akaanza kunitangza vibaya mpaka kwa Mama, anasema mimi ni malaya, sasa leo kaja kalewa anatka kunipiga!” Mke wangu alipiga kelele.
“Kwahiyo ndiyo unataka kumuamsha Mama yako, hivi una akili wewe, umepigwa wapi? unajua shida anayopata Mama yako kupata usingizi halafu unampigia makelele.” Baba mkwe alimuangalia mtoto wake na kumuona kama mjinga flani hivi, hakutaka kumsikiliza, mke wangu hakuridhika.
“Naona nyie ni wanaume mnateteana, sasa ngoja nikaongee na Mama yangu, nateseka mimi napigwa halafu unamtetea! Mama alishaniambia nisikubali kupigwa na Mwanaume!” Mke wangua liongea huku akiniachia na kuanza kukiambia kuelekea chumbani. Baba mkwe wangu mara nyingi hata kama ni usiku anatembea na fimbo yake, hawezi kutembea bila fimbo ingaw ana nguvu tu vizuri. Ile tu mke wangu ananyanyua mguu kutaka kuingia ndani alinyanyua fimbo yake na kuiingiza katikati ya miguu ya mke wangu.
Mke wangu aliyekua akikimbia, alidondoka, aklajigonga kidevu kwenye stuli.
“Mamamaaa! Nakufa!” Alipiga kelele. Nilijua labda ni bahari mbaya yule Baba alikua ananyoosha fimbo yake lakini nilishangaa anamfuata mke wangu pale chini.
“Mchezeee mume wako huko lakini si mke wangu. Nimehangaika tangu asubuhi hajapata usingizi halafu uje kulialia kijinga hapa! Nyamaza mbwa wewe! Sijawahi kumpiga Mama yako, sijawahi kukupiga wewe kama mwanangu lakini huyu mume wako alitakiwa kukucharanza viboko, mwanamke unaondoka unalala nnje, unamuacha mume wako ndani unaenda kulala nnje?”
Alifoka hukua kimfuata na kuanza kumtandika bakora tena kwa hasira, Mke wangu alikua akilai na kila akilia Baba yake ndiyo alikua anazidi kumtandika, nilimfuata Baba mkwe wangu na kumshika.
“Baba huyu ni mke wangu, huwezi kumpiga ukiwa kwangu?” Nilimuambai.
“Usijali mwanangu, sitampigia tena kwako, kesho naondoka na mke wangu!” Baba aliongea, mke wangua liyekua akipiga kelele za maumivu aliposikia vile alinyanyuka hakaraharaka na kupiga magoti, alimuomba Baba yake msamaha na kumuomba asiondoke.
“Mwanangu, Mama yako amebakiza siku chache kufa, hawezi kupona lakini nitafurahi mke wangu akifa kwa kansa, nilishajiandaa kuhusu hilo ila siwezi kuruhusu mke wangu kufa kwa presha.” Baba mkwe aliongea, wote tulikua tunajua hali ya Mama, mke wangua likua anampenda sana Mama yake, ingawa alikua na ndugu wengine wenye uwezo ila hawakua kama sisi na kwa mazingira ya kwetu yalikua mazuri na rafiki zaidi. Tulimbembeleza sana lakini alishaamua, aliingia ndani na kutuacha mimi na mke wangu tukiwa tunaangaliana.
“Inabidi tuyamalize haya mambo, siwezi kumuacha Mama yangu kuondoka atakufa!” Mke wangu aliniambia.
“Mimi niko sawa, sihitaji aondoke, nadhani ni muda tukae tuongee kuhusu ndoa yetu. Niambie ni kitu gani kimetokea, kwanini umebadilika na usinidanganye kuwa ni mambo ya ndoto?” Nilimuambia mke wangu.
“Hakuna ndoto mume wangu, ni shetani alinipitia….” Mke wangu aliniambia. Nilimuangalia bila kusema chochote kutaka ajiongeze mwenyewe na kuongea.
“Kuna Baba mmoja alikua ananitongoza, sijawhai kufanya naye chochote lakini nilikaribia kufanya, siku ile niliyokuambia kuhusu wewe kuchepuka nilitaka kwenda kuonana naye. Alinitumia meseji usiku kuwa anataka kuniona, basi mimi nikawa natafuta sbaabu ya kugombana na wewe ili niondoke kulala chumba cha wageni niondoke niende kwake.” Aliniambia, nilishikwa na hasira lakini nilijua kama nikipaniki basi itakua ngumu sana kwangu kuujua ukweli.
“Kwahiyo ulienda kulala na huyu mwanaume?” Nilimuuliza, alikaa kimya kidogo kama mtu aliyekua anajisikia vibaya, anawaza kitu.
“Hapana, siwezi kukusaliti mume wangu, nimejaribu sana lakini nimeshindwa. Nimejaribu, siku hizi mbili tatu nilitaka kukuchukia uili nichepuke lakini wapi….” Alianza kujielezea.
“Nilikutana na huyu baba kazini kwetu, yeye anafanya kampuni ya kusafrisha mizigo nnje, ni meneja, alikuja pale kuna vitua likua anatafuta, basi akaniomba namba za simu kwaajili ya mambo ya kikazi.
Kwakua ni kawaida kuwapa wateja namba nilimpa, lakini siku iliyofuata alinipigia simu na kuniambia kuwa anataka kuonana na mimi nnje ya ofisi. Mume wangu mimi unanijua, hata kutoka ni shida, lakini kwa namna alivy0ongea sijui nini kilitoke anilisema ngoja nikamsikilize kwani alionekana kama anataka kunipa dili flani. Basi nilitoka naye, kama unakumbuka kipindi kile uko safarini, nilitoka naye nikarudi saa mbili usiku.
Nilijsikia vibaya sana kwani kwanza alinitongoza na mimi badala ya kumuambia kuwa ni mke wa mtu nilimuambia kuwa niliwahi kuolewa ila sina mume kwasasa kwakua tuligombana. Nisamehe mume wangu, sijui kwanini nilidanganya ila nakumbuka kuna rafiki yangu mmoja aliniambiaga si kila mwanaume unapaswa kumuambia kuwa umeolewa kwani kuna watu wanaweza kukuletea madili ya maana ila wakisikia umeolewa basi wanaacha.
Baada ya hapo tuliendelea kuwasiliana, kila siku akianiambia kuwa tuoke lakini mimi namzungusha wkakua wewe upo. Basi kuna siku naongea na shoga yangu ndiyo akanipa hilo wazo la ndoto, nisingizie unachepuka ili nikasirike na kuhama chumba niende kuonana na huyo mwanaume. Nikafuatilia ofisini kwenu kuna kabinti kazuri kamekuja, nilikaona siku moja nimekuja kukuchukua basi nikafuatilia jina lake, nikaenda kwenye mitandao yake ya kijamii nikachukua picha zake bila yeye kujua ili kukusingizia vizuri.”
“Kwahiyo ukaenda kulala na huyo mwanaume?” Nilimuuliza.
“Hapana mume wangu, sikulala naye, siku ile nimeondoka nilienda kuonana naye, lengo lilikua ni chakula cha usiku kisha naondoka. Lakini yeye alinipeleka Baa, alinilazimisha mpaka nikanywa pombe, ila cha ajabu wakati mimi niko naye tunakunywa aliondoka na mwanamke mwingine na kuniacha hapo. Nisingeweza kurudi nyumbani kwakua nilikua nimelewa sana hivyo sikutaka Mama yangu kujua kuwa nakunywa pombe.”
“Vipi siku ya pili na yatatu.” Nilimuuliza.
“Najua huwezi kuniamini mume wangu lakini ndiyo ukweli, sijalala na huyo mwanaume ila najutia sana kwani nimekusaliti na nikokaribu kuvunja ndoa yangu kwaajili ya maujinga. Siku ya pili nilitoka naye, lakini sasa mke wake akampigia simu, wakati tuko kwenye gari basi akapokea bila kujijua, mke wake akakata simu,a lipopiga tena ndipo akamuambia kuwa amejua kila kitu, basi mwanaume akaniacha ila sikufanya kitu chochote, na siku nyingine hata sikua naye kwani alinidanganya akaondoka na mwanamke mwingine sema kwakua nilishaanza kuona raha ya pombe nikaamua kwenda kunywa pombe peke yangu!”
Nilimuangalia mke wangu na kuwaza hivi huyu ananiona mjinga kiasi gani? Nilijua kila alichokua ananiambia niuongo lakini kwakua nilikua nampenda niliona ni bora uongo wa namna hiyo kuliko ukweli ambao utaniumiza. Nilijifanya kukasirika, nikamuambia sitaki tena huo ujinga, nilimpa nasaha nyingi sana akanisikia na kuniomba msamaha, nilijua ni wauongo lakini nilijikuta nakubali huku nikiamini labda atabadilika.
Tulirudi chumbani, usiku mzima nilikua nimelala nikijaribu kuiaminisha akili yangu kuwa mke wangu hajachepuka, nikajaimbia mambo mengi kuwa mke wangu angechepuka ningeshagundua, mbona tabia hizi hazikuanza zamani, mbona ni sasa hivi tu, nilijiambia mambo mengi ili tu kuilazimisha akili yangu kuamini kuwa mke wangu hakuchepuka lakini bado sikupata usingizi. Nikiwa sina usingizi najaribu kujiaminisha kuwa mke wangu hawezi kuchepuka labda nishetani alimpitia nilijikuta nashika simu ya mke wangu.
Niliingia sehemu ya meseji na sikukuta meseji ya mwanaume yoyote, niliamua kupitia meseji za marafiki zake nikakutana na meseji moja ambayo kidogo nichanganyikiwa.
“Nahii mimba nayo unamsingizia mume wako au unampa Kelvin, Mamaa yule mshenzi hawezi kulea, unajipa moyo kabadilika ila hatahudumia, bora mume wako anajali watoto.” Nilijikuta naishiwa pozi, haikua ishu tena ya kuchepuka bali ya kusingiziwa mtoto, nguvu ni kama ziliiniishia na kubaki nimeganda tu.
Haya sasa, Baba Maggie ana watoto wawili ambao anaamini kuwa ni wakwake, unadhani ni wake wote, je ni yupi ambaye kasingiziwa. Vipi je atasamehe na kumvumilia mke wake, je ataikubali hiyo mimba nyingine, vipi watoto ataendelea kuwa Baba yao? Nisikuchoshe, subiria sehemu ya nne.
MAMA MAGGIE; NAKUPENDA SANA ILA SHETANI AMEKUPENDA ZAIDI!—SEHEMU YA NNE
(ILIPOISHIA SEHEMU UA TATU; Mama Maggie anaanza kumshutumu mume wake kuwa anachepuka, anatafuta ugomvi ili kutoka ndani kumbe yeye niyo anachepuka, analala nnje kwa kama siku tatu hivi. Anamfokea mume wake na kumtukana lakini mume wake anavumilia.
Mwisho anapigwa na Baba yake ila mumewe anemtete, anakiri kwa mume wake kuwa ametongozwa ila hajachepuka. Mume anamsamehe lakini anagundua kuwa ana mimba ambayo si yake na hata huko nyuma alimsingizia mtoto, je Baba Maggie ataendelea kumsamehe au? ENDELEA….)
Kusema kweli nilikua nampenda sana mke wangu, lakini suala la kuwa watoto si wangu liliniumiza sana, nilijaribu kulala lakini sikupata usingizi. Nilitamani kuuliza ili kujua majibu lakini kila nilipofikiria majibu nitakayopewa, kuambiwa kuwa Maggie au Jacobo mmoja wapo si mtoto wangu basi nguvu ziliniishia na nilijikuta nashindwa chakuongea. Nilijikuta nanyamaza nikifugulia maumivu.
Niliiirudisha simu ya mke wangu kama nilivyoikuta kisha nikajifunika shuika ili kulala, usingizi haukuja, nilikua najisikia vibaya sana, nilikua na hasira nyingi sana zilizokua zimechanganyika na uoga, nilikua naogopa sana kujua kuwa mwanamke niliyekua nampoenda, ambaye nilikua nikiamini kuwa ananipenda, ananijali na kunithamini alikua anachepuka ena kwa muda mrefu kiasi cha kufikia kunisingizia mtoto.
Nilikua na hasira sana, usiku mke wangu alinyanyuka, akanisoghelea na kunikumbatia. Nilimsikia lakini nilijifanya nimelala, nikajisogeza pembeni kana kwamba nimegeuka usingizini kumbe nilikua namkwepa. Mpakaasubuhi sikulala, nilikua mtu wa kwanza kuamka, lakini wakati najiandaa naenda kumgongea Mama mkwe wangu kuona wanaendeleaje nilikuta tayari wameshajiandaa wanataka kuondoka.
“Baba kwanini mnataka kuondoka?” Niliuliza tu kinafiki, kusema kweli nilikua nawapenda sana wakwe zangu, walikua watu wazuri wananipenda na ikizingatiwa nilikua sina wazazi basi wao walikua kama Baba na Mama yangu lakini kwasiku hiyo akili yangu ilikua mbali kabisa. Yaani nilikua nina mawazo kiasi cha kushindwa kuwabembeleza, niliuliza tu huku rohoni nikitamani kila mtu kuondoka na kuniacha mwenyewe.
“Hapana Baba, unahitaji kukaa na mke wako, ndoa yako ina matatizo hatutakiwi kuwa sehemu ya matatizo!” Baba mkwe aliniambia, sikutaka kuendeleza mjadala, nilimuambia sawa, nikamsalimia Mama, bila hata kujiuliza kama wanaenda wapi nilitoka ili kwenda zangu kazini. Mke wangu alikua bado hajaamka, sikujua kama anaenda kazini au la lakini sikumuamsha, wakati narudi chumbani kuchukua viytu vyangu mke wangu aliamka.
“Baby, inamaanaumeacha kuniamsha, unaona mpaka nimechelewa kazini….” Alijiongelesha kimapenzi, nilimuangalia kwa hasira bila kummaliza, nilijikuta nahisi kumchukuia, nilitamani kumpiga, nilitaka kumuuliza lakini kwa hasira nilizokua nazo nilijua kuwa kama nikinyanyua mkono kutaka kumpiga mke wangu basi ningemuua. Nilichukua kile nilcihokua nikikichukua kisha nikaondoka zangu, sikutaka kuongea naye na wala sikujali kama atalichukuliaje hilo swala.
Haikua mara ya kwanza kulisikia hilo jina la Kelvin, nakumbuka mke wangu alishawahi kunitambulisha kwa mtu mwenye jina hilo. Mara nyingi nilishawahi kumsikia akimtaja huyo mtu na alikua akiniambia kuwa ni rafiki yake na kwakua nilikua nikimuamini sana mke wangu hata sikutilia mashaka. Nilipofika ofisini kazi ya kwanza ilikua ni kumtafuta huyo Kelvin, wala haikua shida kabisa kwani niliingia tu facebook na kumtafuta nikakuta ni mmoja kati ya marafiki wa mke wangu.
Kwa kuangalia tu picha zake nilijua kua ni mume wa mtu, anafamilia yake na watoto ambao walionekana kuwa na furaha sana. Nilianza kuwaangalia wanae kuona kama kuna hata mtoto mmoja kafanana na mwanangu yoyote yule lakini haikua hivyo, nilichunmguza kila kitu ila sikuona, lakini baada ya kukosa nilijikuta nalazimishia vitu. Wanangu wamefanana na Mama yao, na mtoto wangu wa kwanza Maggie kwakua ni mweupe basi nilikua najiambia kuwa kafanana na mimi na baadhi ya watu waliniambia hivyo, ila kwakua mshikaji alikua ni mweupe kama mimi basi kuna wakati nilijisikia vibaya na kudhani ni mtoto wake.
Nilimfuatilia sana lakini sikufanikiwa kuona kitu, siku hiyo sikufanya kazi yoyote mke wangu alijaribu kunipigia simu lakini sikupokea. Alituma meseji nyingi, mwanzo akiniuliza kama kuna tatizo llolote kwani wazazi wake wameondoka lakini niliishia kumjibu kimkato tu.
“Kwani ulitaka waishi kwangu milele, si wana watoto wengine waende huko!” Nilimjibu, hakunitafuta tena bali alibaki kimya na mimi nikabaki kimya nikiendelea kumchunguza kelvin. Sikua na namba yake ya simu kwani hata nuilipokuta meseji kwenye simu ya mke wangu nilitafuta jina lake kama kuna namba yake lakini sikumuona.
Ili kupata namba yake bila kumuuliza chochote niliiteneneza akaunti fake facebook, nikatafuta picha nyingi za wanawake kwenye mitandao kisha nikaziweka na kumuomba urafiki. Wala hakuchukua muda aliukubali, basi baada ya kukubali nilianza kulike picha zake zote na kucomment kusifia familia yake, nilijua tu kama mwanaume ni lazima angenifuata inbox na kweli alifanya hivyo, alinisalimia na kuniuliza kama tunafahamiana.
“Hapana, Kaka, mimi ni mgeni huku, nilikua naadd tu marafiki hivyo facebook wakaniletea jina lako nikaona mkaka mzuri nikasema basi nilike picha zake.” Nilimjibu, hakuchukua muda, alianza kwa kunitongoza mwisho kama kawaida ya wanaume wengi aliomba namba ya simu.
Hapo ndipo nilimuambia anipe yeye nitamtafuta, kwelia litoa namba zake mbili, nikachukua na kumuambia nikipata muda nitamtafuta. Nilitoka online na kurudi kuendelea na mambo yangu, sikumtafuta tena kwenye Facebook kwani sikua na sababu ya kufanya hivyo, hata kwenye Facebook mimi kama mimi sikuingia.
****
Sikumuuliza mke wangu chochote wala sikuwahi kumpigia yule Kaka, niliporudi wakwe zangu walishaondoka na kwenda kuishi kwa Baba mdogo wa mke wangu. Sikuulizia sana, mke wangu alilalamika sana lakini sikumjali. Nilikua na hasira sikua naongea naye, kwa kipindi cha kama wiki mbili hivi mke wangu alijishusha sana, akajitahidi kuniomba msamaha kwa kila kitu lakini nilimjibu tu kuwa nishamasamehe ila sikua sawa, nilishindwa kuongea naye na akili yangu kila siku ilikua katika tumbo lake.
Kila wakati nilikua nikiangalia tumbo lake ili kuona kama linakua au la, nilitaka kuthibitisha kama ana mimba au la lakini sikuona mabadiliko yoyote. Siku moja nilichelewa kurudi nyumbani, ilishakua kama kawaida yangu baada ya wakwe zangu kuondoka nilianza vituko vya kuchelewa kurudi nyumbani, si kama nilikua na kitu cha maana nakifanya huko nnje, hapana, huko nilikua nakaa tu, sikutaka kunywa tena pombe kwani nilijua zitaniharibu hivyo mara nyingi nilikua nikitoka nakaa hata baa mpaka saa nne ndioyo narudi nyumbani.
Mwanzo mke wangu alikua haongei lakini baadaye alianza kulalamika ila hata sikumjali, bado nilikua na hasira naye. siku hiyo nilichelewa kurudi kama kawaida yangu, nafika nyumbani moja kwa moja nikaingia chumbani, kufika sikumkuta mke wangu, nilirudi sebuleni na kumuuliza binti wa kazi ambaye aliniambia kuwa mke wangu alikua bado hajaraudi.
Nilimuambia aniandalie chakula ili nile, nilitaka kumpuuza mke wangu, nilitaka sijue kuwa najali hivyo nilikula chakula na moja kwa moja nikapanda kitandani ili kulala. Nilijitahidi kutafuta usingizi lakini sikuupata, mpaka saa sita usiku mke wangu alikua hajarudi nyumbani. Hapo uzalendo ulinishinda, niliamua kumtafuta kwenye simu lakini simu yake ilikua haipatikani, nilipiga sna anikakuta haipatikani, baada ya kuona kimya nilimpigia simu Baba mkwe wangu nikiamini kuwa labda kwakua kila siku hupitia kwa Baba mdogo wake kumuangalia Mama yake basi kaenda huko na hali ni mbaya.
“Kuna shida gani mwanangu, mbona usiku, mkeo hajakuambia kuwa Mama anaendelea vizuri?” Baba mkwe aliniuliza, nilipompigia sikumuulizia kuhusu mke wangu, kwa nilivyokua namjua Baba mkwe wangu kama ningemuulizia mke wangu basi ingekua shida, angejua kuwa hajarudi na angekasirika, sikutaka kumuudhi hivyo niliulizia tu hali ya Mama, pamoja na kutokuulizia lakini alishtuka.
“Ameniambia ila nilitaka tu kujua kuwa anaendeleaje, muwe na usiku mwema.” Nilimjibu kw amkato kisha nikakata simu, wakati nakata simu mke wangu naye aliingia, kwa kumuangalia tu ni kama alikua analia, mwili ulikua umevurugwavuirugwa, kama mtu kapigwa nilimuangalia usoni na kukuta alikua anaalama za vidole, ni kama mtu aliyekua amepigwa makofi tena ya nguvu. Jicho lake la kulia lilikua limevimba tena sana.
“Una nini? Nini kimetokea? Mbona uko hivi?” Nilimuliza, lakini badala ya kunijibu alinisukuma pembeni.
“Nawewe usinisumbue, kama huna cha kufanya lala kama huna usingizi kaangalie Tv, nina mawazo yangu halafu unakuja na maswali yako ya kijinga jinga!”
Alinijibu kwa hasira huku akinisukuma pembeni, aliingia moja kwa moja bafuni na kuoga, baada ya kumaliza alirudi chumbani, bila kunisemesha alipanda kitandani kulala. Nilikaa pembeni yake kumuangalia lakini nilishindwa kumuuliza kitu, ingawa huko nyuma mimi ndiyo nilikua namchunia lakini kwa wakati huo yeye ndiyo alinichunia. Sijui kwanini lakini kuna kitu kiliniambia ingia bafuni, niliingia kweli kuangalia kulikua na nini. Huko nilikutana na nguo zake kazitundika, nikaanza kuzichukua kuzikagua.
Nguo yake ya ndani ilikua na shahawa sehemu ya mbele, silikua nyingi tu kuashiria kuwa mke wangu alikua katoka kufanya mapenzi.
“Lakini mbona yuko hivi, mbona kaumia, au amebakwa?” nilijiuliza maswali mengi bila majibu. Mwisho nilirudi kitandani lakini nilishindwa kulala, nilivumilia mpaka asubuhi, siku hiyo haikua siku ya kazi. Aubuhi niliamka mapema na kumuanalia mke wangu supu, nilijisikia vibaya nikiamini labda mke wangu alkua kavamiwa na vibaka wakambaka hivyo amekua na hasira ameshindwa kuongea.
“Amka unywe supu…” Nilimuambia, aliamka kweli alionekana kuchoka na alikua na njaa kali, nilimuacha akanywa supu na kumaliza, baada ya hapo nilimuomba kuongea naye.
“Naona hauko sawa, nahisi kuna kitu kibaya kimekutokea, kama umebakwa….” Nilimuambia lakini alinikatisha.
“Achana na maisha yangu wewe Baba, hayo mambo ya kubwakwa unamletea nani? Kama unapenda sana watu kubakwa basi kabakwe na wewe kwani si unashimo, mjinga mkubwa, kama umenichoka niache na maisha yangu ila mambo ya kufuatana fuatana sitaki!”
Aliniambia, majibu yake yalinifanya nihisi kuwa mke wangu hayuko sawa, najua tulikua tumegombana lakini alikua si mtu wa kunijibu hivyo. Nilitoka nnje bila kumuambia kitu nilimtafuta rafiki yake ambaye mara nyingi huwa wanapenda kutoka pamoja na kumuuliza nini kimetokea.
“Kwani hajakuambia? Atakua hawezi kuongea, anaona aibu, siunajua mke wako jinsi alivyo….” Alianza kunielezea.
“Nini kimetokea, naona kabadilika, na ameumia, sijui kafanya nini?”
“Shem nakuambia lakini naomba usijekunitaja, si unajua Mama Maggie hapendi mambo yake kutangazwa, anaona aibu, jana wakati anatoka kwa Mama alikua hana usafiri, basi alichukua Bodaboda ila walichomfanyia…” Aliongea huku akilia, alinyamaza kidogo.
“Wamemfanyia nini? Mbona sikuelewi?” Nilimuuliza kwani alikua akiongea kwa kutuliatulia kama vile nayeya alikua katika maumivu makali.
“Niambie shemu, siwezi kumuambia kitu….” Nilimuambia, lakini kabla ya kuniambia alichokua kafanyiwa mke wangu na bodaboda mke wangu alijitokeza.
“Akuambie nini? Mshenzi mkubwa wewe unaongea nini na mume wangu? Unamtaka mume wangu, mambo yako yamekushinda unafuata ya kwangu, si nilikuambia kuwa sitaki mume wangu kujua mambo yangu!” Mke wangu alininyang’anya simu na kuanza kumtukana shoga yake, alimtukana sana na kumuambia kuwa hataki kabisa kuingilia mambo yake kwani ni mambo yake binafsi.
“Kama nikibakwa wewe inakuhusu nini? Unamuambia mume wangu ili nini?” Mke wangu alizidi kutukana, nilisikia yale maneno, nilijisikia vibaya kwani mwanzo nilimhisi mke wangu kuwa katoka kuchepuka lakini kwa maneno yake ni kama alikua kabakwa, alimkatia shoga yake simu na kunitupia kisha akaondoka zake, hakutaka kuongea na mimi hata nilipomuomba msamaha bado hakutak kunisikiliza aliondoka na kuniacha nikiwa na maswali mengi.
Ilikua ni asubuhi lakini mke wangu hakurudi mpaka usiku wa saa nne hivi, simu zake zilikua hazipokelewi, nilimpigia rafiki yake ambaye aliniambia kuwa hataki kungilia mambo ya familia yangu kwani hata yeye ana mambo yake. Nilipigia ndugu zake lakini hakuna mtu hata mmoja ambaye alikua anajua kilichotokea. Kusema kweli nilijihisi kuchanganyikiwa, pamoja na yule mke wangu aliyokua amenifanyia lakini bado nilikua nampenda na nilihisi kuna kitu kibaya kitakua kimemtokea. Nikikumbuka maneno yake akimuambia rafiki yake kuhusu kubakwa nilijisikia vibaya sana nikiamini kuwa labda ameenda hata kujiua kwa hasira.
Ingawa alikua na tabia ya kutoweka bila taarifa lakini kwa niliyoyasikia asubuhi na namna alivyokua na hasira nilijua moja kwa moja labda kaamua kujidhuru. Sikutaka kusubiri tena usiku huo huo nilienda Polisi kutoa taarifa kuhusiana na mke wangu, nilibeba na picha yake. Kituo cha kwanza nilienda na kuwaambia kila kitu lakini walionekana kutokujali sana, ni kama walichukulia mzaha na kuniambia hii ni weekenda hivyo nisubiri mpaka Jumatatu kama hajarudi ndiyo niseme kapotea.
Niliona kama hawajali hivyo nilihamia kituo kingine, lakini nako sikupata msaada mpaka nilipofika kituo cha tatu.
“Unasema unahisi kajiua?” Dada mmoja aliyekua kaunta alinijibu kwa dharau.
“Ndiyo, nahisi kuna kitu kibaya kinaweza kuwa kimemtokea kwani jana alirudi saas sita usiku ila alikua kaumia hivyo nina wasiwasi kwani kuna mambo rafiki yake kaniambia nina wasiwasi.”
“Hivi kwanini wakaka wazuri kama wewe mnakua wajinga namna hii, mwanamke anarudi saa sita usiku kapigwa unahisi kafanyiwa kitu kibaya, wanaofanyiwa vitu vibaya hawarudi wanaokotwa na polisi. Wakwako tumemkamata tangu asubuhi na leo hatoki subiri mpaka jumatatu uje kuchukua mzigo wako!”
Aliniambia kwa dharau, mimi nilikua simuelewi, aliniambia nimfuate, tukasogea mbele kidogo tu kulikua na giza akawasha tochi kisha akasema.
“Wewe! Njoo mume wako kaja kukuona, njoo akuone umuambie umefanya nini mpaka ukakamatwa maana anaamini umefanyiwa kitu kibaya!” Yule askari aliongea huku akimpiga tochi mke wangu ambaye alisimama na kusogea, macho yetu yaligongana, alikua kachoka, uso umevurugika, jicho lilisharudi kawaida ila alionekana kavurugikiwa sana. Nilimuangalia kwa uchungu yaani hakua tena yule mwanamke mwezi mmoja tu kabla tulikua na furaha sana pamoja.
Mama Maggie aliondoka nyumbani kapigwa lakini haklurudi, mume wake baada ya kumtafuta anamkuta mahabusu. Unadhani ni kitu gani kimetokea basi usiokose sehemu inayofuata, Tumrudi upya kama kawaida.
MAMA MAGGIE; NAKUPENDA SANA ILA SHETANI AMEKUPENDA ZAIDI! —SEHEMU YA TANO
(ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE; Mama Maggie anarudi nyumbani akiwa amechoka, jicho lake limevimba kama mtu aliyekua amepigwa sana, moja kwa moja anaelekea Bafuni. Mume wake anajaribu kuhijii hamuambii kitu, anaongea na rafiki yake ila wanaishia kutukanana anakuta kuna shahawa kwenye nguo yake ya ndani, anahisi mke wake amebakwa. Mke anaondoka Baba Maggie anaenda kumtafuta anafanikiwa kumuona akiwa Mahabusu kituo cha Polisi, je unajua ni kitu gani kimetokea? ENDELEA….)
“Wewe mbwa unafanya nini hapa? Kwanini huondoki, ondoka acha kunifuatilia na maisha yangu!” mke wangu alipiga kelele baada ya kuniona. Nilijaribu kumsihi anyamaze na kuniambia ni kitu gani kilikua kimetokea lakini hakuniambia, aliishia kunitukana.
“Wewe Kaka, kwanini unahangaika na huyu mwanamke, ni mke wako wa ndoa kweli?” Askari mmoja aliniuliza.
“Ndiyo, ni mke wangu wa ndoa, Mama wa watoto wangu, sijui ni kitu gani kimem,pata lakini ninahitaji kumchukulia dhamana, siwezi kukubali mke wangu kulala ndani!” nilimuambia kwa sauti ya uchungu, yule Askari aliniangalia kwa huruma kisha akaniuliza tena.
“Ni mkwe wako kweli?” Safari hii alikua ananikodolea macho kama vile haamini kuwa mimi ndiyo nilikua mume wake.
“Ndiyo dada kwani kuna tatizo gani? Au kwakua ana matatizo ndiyo nimkane?”
“Baba aondoka, mimi si mke ako na mambo yangu niachie mwenyewe, sitaki kusikia kuhusu wewe na kama nikuniacha basi nikitoka hapa nipe talaka yangu, nimechoka kuishi na mwanaume kama kinyago, hapana nahitaji maisha yangu, nahitaji uhuru nwangu, nimechoka kuwa mfungwa wako!” Mke wangu alifoka baada ya kuona naongea na yule askari.
“Hakutaki ondoka, hivi mbona kaka unaonekana mtu mzuri kabisa, yaani mwanamke anakuambia hivyo na bado unamng’ang’aniua? Mwanamke mwenye kapigana nusu kuuana na malaya mwenzake wakigombania mume wa mtu halafu unamuita mke wako?” Askari aliongea, ingawa sikumuuliza nini kimetokea lakini alikua na hamu ya kuniambia.
“Wewe mbwa na wewe hayakuhusu? Unamuambia mume wangu nimepigana kwani kakuuliza!” Mke wangu alifoka, lakini yule askari ni kama alikua anamsikilizia aongee kitu. Alifungua mlango akaingia kisha akaanza kumtandika mke wangu virungu!
Mke wangu naye hakukubali, walishikana na kuanza kupigana, kuona vile askari mwingine aliingia na kumtoa askari mwenzake kisha akaniambia niondoke mpaka jumatatu ndiyo anaweza kupewa dhamana.
“Hapana, siwezi kumuacha mke wangu hapa, naomba kuongea na mkuu wa kituo!” Nilimuambia lakini waligoma kabisa mimi kuongea na mkuu wa kituo. Kutokana na kazi yangu nilikua nafahamiana na watu wengi, askari wengi wenye vyeo vikubwa walikua ni rafiki zangu na nilishawasaidia sana.
Niliomba kukutana na mkuu wa kituo lakini walinikatalia, nilipoona haiwezekani nilichukua simu yangu na kumpigia rafiki yangu mmoja ambaye ni askari, alikua na cheo kikubwa sana, katika maisha yangu nilikua sijawahi kumuomba msaada wowote, sikuwa mtu wa namna hiyo isitoshe nilikua sijawahi kujiingiza kwenye mazingira ambayo yatanifanya nilazimike kuomba msada lakini kwa upande wake nilishamsaidia sana hivyo nilipompigia simu haikuchukua muda mkuu wa kituo alikuja mwenyewe, akaongea na askari wa pale kisha nikaambiwa nimchukue mke wangu.
“Una mume mtu mkubwa hivi lakini unahangaika na waume za watu, nakuambia kuwa umetoka tu kwa dhamana ila ukiendelea kugombania wanaume baa basi jua kuwa utaishia kupigwa au kuozea jela?” Dada mmoja askari aliyekua akipigana na mke wangu aliongea wakati tunatoka. Sikumjibu kitu chochote, nilitoka na mke wangu mpaka kwenye Gari nilimuambia aingie kwenye gari lakinia ligoma.
“Umenitoa mahabusu, sikukuomba nilitaka kupambana na kesi yanu mwenyewe, nani kakuambia kuwa nataka kurudi nyumbani kwako? Sikutaki, hivi wewe mwanaume unataka nikufanyie nini mpaka ujue kuwa sikutaki!” Mke wangu aliongea kwa hasira, nilimbembeleza sana ili niondoke naye lakinia ligoma, aliniambia kuwa nimueche yeye anajua pakwenda, ulikua ni usiku, bado tulikua nnje ya kituo cha polisi, wakati tunabishana askari mmoja ambaye alikua pale nnje alitokea na kutuuliza nini kinaendelea.
“Huyu ni X wangu, ananilazimisha kuingia naye kwenye gari na mimi sitaki!” mke wangu alimuambia, nilijisikia vibaya, hata yule askari aliponiuliza kama mimi ni nani sikumjibu. Niliingia kwneye gari yangu na kuondoka. Nilienda mbele kidogo na kusimamisha gari, akili yangu ilikua haifanyi mkazi sawasawa, kumuacha mke wangu usiku ule iliniumiza sana, nilisimama kwa muda na kumuona mke wangu akipita, anatemeba peke yake baridi linampiga. Alikua hana kitu chochote mkononi, hata simu zake sijui alipotezea wapi.
“Hata kama hutaki kuondoka na mimi, kama una mambo amabyo unataka kufikiria kabla ya kunirudia basi naomba uchukue hata nauli na hii hela ya Gest ukalale ausbuhi tutaongea.” Niliongea huku nikimkabishi shilingi elfu kumi, alizichukua na kuondoka, niliendelea kumfuatilia nyuma kwa gari ili kuhakikisha kama yuko salama mpaka pale alipopanda Bodaboda na kuondoka, nilitamani kumfuatilia nyuma ili kujua kama anaenda wapi lakini mke wangu ni kama alijua kuwa nitamfuatilia, waliingia vichochoroni, sehemu ambayo siwezi kumfuata hivyo nikalazimika kurudi nyumbani.
Nilirudi nikiwa na mawazo sana, sikujua ni kitu gani nilikua nimemfanyia mke wangu mpaka kubadilika vile.
“Hivi alikua hivi tangu zamani au kuna kitu kimebadilika sasa hivi?” Nilijiuliza, qwakati nikiwa katikati ya mawazo niipigiwa simu, haikua namba ngeni, ilikua ni namba ya Mama mdogo wa mke wangu. Ingawa alikua ni Mama yake mdogo lakini kiumri alikua sawa na mke wangu, tulisalimiana ndipo akaniambia kuwa mke wangu yuko kwake.
“Nashukuru sana amefika sehemu salama, nilikua na mawazo mengi snaa!” Nilimuambia huku nikishukuru Mungu kuwa mke wangu hajaenda kwa mwanaume, kwa matukio ambayop yalikua yametokea nilihisi labda anaenda kwa mwanaume mwingine lakini nilipoambiwa kuwa kaenda kwa Mama yake mdogo basi nilikua na amani kidogo.
“Ulidhani kuwa atakosa pekwenda, ulidhani kuwa kila mtu atamtenga, ulipokua unampiga ulidhani kuwa hana kwao?” Mama mdogo alinijibu kwa hasira, nilishangaa mambo ya kumpiga yamekuja kujaje?
“Unamaanisha nini? Mbona sikuelewi?” Nilimuuliza lakini hakunijibu, alinikaia simu, nilijaribu kumpiogia simu lakini hakupokea ila baadaye alinitumia meseji.
“Kaa mbali na Mama Maggie, tunaenda kuchukua RB na kila kitu kitajulikana, si unapenda kujifanya malaika mpaka umewateka wazazi wake umewafanya wako, sasa hivi nitapambana mpaka mwisho, nahakikisha kuwa unafundishwa adabu, wanaume kama wewe mnajifanyaga watu waheshima sana, nilikua nakuheshimu sana ila si kwa ulivyompiga shoga yangu!”
Sikuijibu ile meseji wkani niliona kabisa haiwezi kusaidia kitu chochote, nilinyamaza huku nikiwaza ni kitu gani nilikua nimemkosea mke wangu mpaka kaumua kuwa vile. Mpaka kunisingizia kuwa nilikua nimempiga, sikuelewa mke wangu anataka nini? Sikujua sababu zake za kunisingizia kwa Mama yake mdogo wakati anajua kabisa sijafanya kitu chochote.
“Anataka nini huyu mwanamke?” niliwaza, siki mbili tu nyuma nilikua vizuri na mke wangu, tunaishi kama Malaika ananipenda nampenda halafu ghafla mambo yanabadilika! Nilijaribu kulala, kufunga macho lakini usingizi haukuja mpaka asubuhi.
***
Mke wangu aligoma kabisa kurudi nyumbani, sikutaka kuwashirikisha wazazi wake kutokana na hali ya Mama mkwe wangu hivyo kila wakati nikienda kuwasalimia nilikua naongea vizuri tu kama vile hakuna kitu kimetokea. Hali hiyo ilikua inaniumiza sana kwani bado nilikua nampenda mke wangu na nilikua sijui ni kitu gani kibaya nilikua nimemfanyia. Kila siku nilikua nampigia simu asubuhi kumuulizia hali yake, ingawa alikua akinijibu kwa ukali lakini niliona ni wajibu wangu kujua alipo.
Nilimuomba arudi nyumbani lakini aligoma kabisa na kuniambia anachotaka yeye ni talaka. sikua tayari kuachana na mke wangu kwa talaka hivyo niliendelea kupigania ndoa yangu. kwa kawaida kila watoto wakifunga shule mimi na mke wangu huwa tunaenda kuwachukua shuleni, hii ilikua ni kawaida yetu na ni mara chache sana ambapo huwa sisi ambapo mimi huenda peke yangu au mke wangu kwenda peke yake.
Wanangu walifunga shule, nilimkumbusha mke wangu kuhusiana na likizo ya watoto huku nikimuomba kuwa katika kipindi cha likizo basi aje nyumbani ili watoto wasijue ni kitu gani kilikua kimetokea lakini aligoma.
“Kama ni kukuacha nitakuacha sasa kwanini kuhangaika kuwadanganya?” Aliniuliza kwa hasira, ulikua umepita mwezi na nusu bila kuonana na mke wangu, nilimbembeleza sana lakini aligoma.
“Basi kama ni hivyo ngoja mimi niondoke nyumbani, si hutaki kuishi na mimi, basi ngoja niondoke nyumbani ili wewe ubaki na watoto. Ni rahisi mimi kuwaambia watoto nimesagiri kikazi kuliko wewe, watoto wanamhitaji Mama yao, naomba basi njoo nyumbani na mimi nitaondoka?” Nilimuambia mke wangu lakini hjata hilo nalo alilikataa.
“Wewe baki na watot0 mimi nitakuja kuwaona! Kwani wewe ukibaki nao na mimi kuonekana kama nimesafiri ndiyo haitawezekana, au unadhani wanaume wtu ndiyo wanaweza kusafiri?” Sikua na jibu, sikua najua nifanye nini, kusema kweli nilichanganyikiwa.
Siku ya kwenda kuwachukua watoto shule nilijua kama atakuja, lakini hakuja, niliwachukua watoto na kurudi nao nyumbani. Waliniuliza alipokua Mama lakini sikua na jibu, nililazimika tu kuwaambia kuwa kasafari ingawa sikua najibu walipouliza atarudi lini. Nilirudi na wanangu nyumbani lakini hawakua na furaha, nilimpigia simu mke wangu ili kuongea nao lakini hakupokea simu zangu wala kujibu meseji.
“Baba Mama yuko wapi? mbona hata hutaki tuongee naye kwenye simu?” Magge aliniuliza, nakumbuka ilikua ni usiku, kama saa nne hivi, aliniamsha kutoka chumbani kwangu na kuniuliza.
“Mama yako kasafiri kikazi….” Kabla ya kuendelea kumdanganya alianza kulia na kuniambia anataka kumuona Mama yake.
“Mama amekufa ndiyo maana Baba hataki kutuambia….” Jacob mtoto wangu mdogo aliongea, sikujua kama alikua kafuatana na Dada yake mpaka chumbani kwangu.
“Kwanini unaongea hivyo, nani kakufundisha huo ujinga? Mama yako yupo!!” Nilijikuta nafoka, lakini kadri nilivyozidi kuwa mkali ndiyo nilikua nawaumiza, walianza kulia kama vile wamefiwa. Nililazimika kuwafokea na kuwaambia kuwa Mama yao yuko hai hajafa ila hawakukubali mpaka kuongea naye, nilimpigia simu mke wangu lakini hakupokea, nilijikuta nazidi kuchanganyikiwa.
“Baba kama Mama kafa tuambia, sisi tushakua wakubwa…” Maggie aliniambia.
“Anna (sio jina lake) Baba yake alikufa, aliorudi nyumbani walimficha wakisema kuwa ni mdogo, lakini walikataa asiongee na Baba yake, kama wewe unavyofanya, mpaka watoto wengine walipomuambia kuwa Baba yake amekufa, baba kama Mama amekufa basi tuambie, mimi ni mkubwa nitambembeleza mdogo wangu!” Maneno ya mwanangu yaliniumiza sana mpaka nikajikuta nalia, nilipiga magoti kumuomba Mungu ili angalau amfungue mke wangu ajue jinsi ninavyoumia na namna anavyowatesa watoto ili angalau apokee simu yangu lakini haikua hivyo.
“Mama yenu ni mzima, nendeni kulala nawaahidi kesho nitaenda kumchukua ili aje kuwaona, atatoka safari ili kuja kuwaona nyie tu.” Niliwabembeleza sana mpaka wakakubali kulala, sikupata usingizi, asubuhi yake nilimtafuta mke wangu na kumuambia kila kitu, alionekana kusikitika na kuniahidi kuwa atakuja nyumbani kuwaona watoto. Nilimuomba sana kuja kuishi nyumbani kwaajili ya watoto mpaka pale watakaporudi shuleni lakini alikataa, aliniambia atakuja tu kuwaona basi.
Sikua na namna zaidi ya kumkubalia, basi nilikaa mpaka jioni na kumpigia simu tena, sikutaka kurudi nyumbani bila mke wangu, nilitaka kumpitia kazini kumchukua lakini aligoma.
“Kama unataka nije niache nije mwenyewe ila si kwa kunipanmgia pangia huko!” aliongea kwa hasira, nilijisikia vibaya lakini sikua na namna, kwakua nilijua lazima atakuja basi moja kwa moja nilienda mpaka kwa Mama yake mdogo, sehemu ambayo nilikua najua kuwa anaishi. Sikugonga mlango ila nilipaki tu nnje ili akiniambia kuwa niko tayari basi nimchukue na kuondoka naye.
Wakati huohuo nilikua nikimpigia simu Binti wa kazi kumuuliza kama ameshafika, lakini mpaka saa nne usiku mke wangu alikua hapokei simu zangu wala alikua hajafika nyumbani kwetu. Nilichoka kusubiri na kuamua kuenda kugonga mlango. Marida, Mama yake mdogo nalinifungulia mlango. Toafauti na siku ambayo niliongea naye kwenye simu akanitukana siku ile alikua mchangamfu kabisa. Mara nyingi hupenda kuniita ‘Mkwe’ na ingawa sikua na utani sana naye ila alikua ni mchangamfu.
“Mkwe ndiyo nini kuja kwangu usiku huu, si unajua naishi mwenyewe watu wasijekudhani kuwa ni danga langu na ulivyo Hansome natamani ungekuja hata mchana niwarushe roho….” Aliongea kwa utani lakini nilishangaa sana na niliona aibu flani kwani sikua na utani wa namna hiyo na Mama yake mdogo. Lakini kwakua nilikua nashida na nilikua kwake sikua na namna zaidi ya kujichekesha chekesha kama chizi flani hivi.
“Hahahahahah! Una maneno wewe!” nilimuambia huku nikicheka, alizidisha utani lakini sikumpa muda, nilimuambia sababu za mimi kwenda pale.
“Hivi wewe ni mwanaume wa namna gani?” Aliniuliza, nilihisi kama anataka kunitukana na kunifukuza kwa maneno aliyoambiwa na mke wangu.
“Sikiliza mkwe, najua umesikia vitu vingi vibaya kuhusu mimi lakini nakuambia kuwa, sikuja kwaajili ya hayo, nimekuja kwaajili ya wanangu, kama nilivyokuambia kuwa wanahisi Mama yao amekufa….” Nilimuambia lakini ni kama nilikua naongea peke yangu, yaani hakunisikia kabisa nilichokua naongea.
“Una pesa, umzuri na kwajinsi mwanangu anavyokuzungumzia yaliyomo yamo, sasa kwanini unahangaika na mtu ambaye hakupendi! Aisee kuna wanawake wana bahati! Yaani sijui nikuambie nini? Ningepata mwanaume nusu ya wewe ningemuabudu kabisa!” Alianza kuongea, ingawa sikua na mazoea naye lakini nilikua najua tabia zake, alikua ni mwingi ambaye akimtaka mwanaume havungi, alikua na watoto wawili ambao walikua na Baba tofauti na wote alizaa na waume za watu.
“Najua nina changamoto na mke wangu lakini naomba kujua kama yupo ilia kawaone watoto?” nilimuambia, kuashiria kuwa sikua nikihitaji kuendelea na mazungumzo aliyokua anayataka.
“Yuko wapi? nani alikuambia anaishi hapa?” Aliniuliza, nilibaki na mshangao kwani sikujua kama mke wangu kashaondoka kwa Mama yake mdogo, mara zote alikua ananiambia kuwa anaishi kwa Mama yake mdogo na haondoki kwani huko ndiyo kuna amani.
“Inamaana kaondoka? Mbona hajaniambia? Ameenda kupangisha wapi?”
“Kweli wewe huna akili, hivi yule mwanamke ni wakwenda kuishi nyumba ya kupanga, mtu ameshahamia kwa mwanaume mingine wewe unaendelea kumng’ang’ania?” Aliniambia, ni kitu ambacho nilikua nakiwaza kila siku, aliponiambia nilihisi kuchanganyikiwa, nilijifanya kutokujali lakini niliumia sana.
“Sawa lakini ninachotaka kujua niwapi anaishi kwani nataka aje kuwaona watoto?’
“Hawezi kuja, sidhani kama yule mwanaume atamruhusu, na sasa hivi mimba imeshakua kubwa…”
Nilimuangalia kwa hasira, sikutaka aniambie mambo kuhusu mke wangu kwani niliku najua anachepuka na ilikua inaniumiza sana. Kabla sijaonge kitu chochote alichukua simu yake na kuanza kupiga.
“Ngoja niongee naye tuone….” Aliniambia huku kashikilia simu inaita, nilijua anaongea na mke wangu lakini simu ilipopokelewa ilikua ni sauti ya kiume na alimuweka loud speaker ili nimsikie.
“Shem nimeona nikupigie simu wewe kwani Mama kijacho hapokei, ni hivi, mume wake kaja kumtafuta kwangu, anaomba ruhusa ili akawaone watoto mara moja! Yuko hapa ngoja nikupe uongee naye!” Aliongea huku akinikabishi simu, niliipokea lakini sikuweza kuongea, nilisikia haloo! Haloo! Halooo! Sauti ya kiume kisha akakata simu! Nilipandwa na hasira na kujikuta natetemeaka kama nimemwagiw amaji ya barafu, nilinyanyuka ili kuondoka lakini simu yangu iliita na alikua ni mke wangu, nilijikuta naipokea kabla sijasema chochote nilisikia.
“Mbona nakuja nyumbani kuwaona watoto halafu sikukuti, kama umeenda kufanya umalaya wako huko halafu unaniita ili iweje, mimi naondoka!” mke wangu alifoka akimaanisha kuwa yuko nyumbani, kwa alivyokua anaongea hakuonekana kujua kua Mama yake mdogo alimpigia mchepuko wake na kunipa simu niongee nao.
Mambo ndiyo hayo. Unadhani Baba Maggie atafanya nini? Je atarudi nyumbani kuonana na mke wake? Vipi akifika atafanya nini? Naomba nisikuchoshe, subiria sehemu ya sita ili kujua nini kitaendelea.
MAMA MAGGIE; NAKUPENDA SANA ILA SHETANI AMEKUPENDA ZAIDI! —SEHEMU YA SITA
Nilikua na hasira sana lakini kitendo cha mke wangu kuniambia kuwa yuko nyumbani kilinifurahisha kidogo. Angalau niliona wanangu wanaenda kuwa na furaha. Nilimuomba mke wangu msamaha na kumuambia ku3wa kuna vitu nilitaka kwenda kununua kwaajili ya watoto ndiyo maana nikatoka.
“Uje harakaharaka kwani mimi nataka kuondoka!” Aliniambia, nilimbembeleza sana ili asiondoke bila kuonana na mimi kwani pamoja na yoe nilitaka kumuona. Nilikua na mambo mengi sana ya kuongea na mke wangu kikubwa nilitaka kujua ni kwanini aliondoka na kuniacha. Nilirudi nyumbani na kumkuta mke wangu amekaa na watoto, walikua sebuleni wanaangalia TV.
“Suprizeeee!” Maggie alipiga kelele baada tu ya kuniona, alinikimbilia na kunikumbatia, kisha akanichukua mpaka kwa Mama yake, akanilazimisha kukumbatiana naye.siku ana namna zaidi ya kumkumbatia mke wangu, naye alisimama na kunikumbatia, watoto nao walitukumbatia huku wakilia.
“Baba sitaki Mama asafiri tena!” Jacob aliongea, nilikua natamani kitu hicho, ingawa nilikua najua kuwa mke wangu alikua akiishi na mwanaume mwingine lakini nilikua nampenda sana na kusema kweli sikutaka asafiri tena.
“Hatutaki kurudi Bweni Baba, mimi sirudi, siaki kurudi na kukuta kuwa mmekufa!” Maggie aliniambia.
“Wewe uliwaambia nini watoto kuhusu kufa?” mke wangu aliniuliza, sikua na jibu, niliwaza nimuambie nini, hata mimi sikutaka kukaa tena mbali na wanangu, kuna wakati nnilihisi labda tabia za mke wangu nikwakua yuko mbali na watoto, niliamini watoto kusoma bweni labda kunamfanya asahau kuwa yeye ni Mama hivyo anafanya mambo ya ajabu ajabu.
“Hatukuambia kitu, lakini rafiki zetu wakienda shule wazazi waop wanakufa, mimi sitaki kwenda Mama tumekuja likizo lakini haupo, tukajua umekufa, hapana, sisi hatuendi tena shule, kama hamtaki kuaa na sisi mseme, kama mmetuchoka mseme lakini sisi hatuondoki!” Jacob alimjibu Mama yake, ilionekana ni kitu ambcho walikipanga, mke wangu alinyamaza kimya hakujibu, aliwakubalia kwa kichwa lakini alionekanma kununa, ni kama alikua na hasira flani ambazo hakutaka watoto wazione.
Tulikaa na kwenda mezani kwaajili ya chakula, wanangu waligoma kula ili kunisubiri na wote kula kama familia. Wakari tunafika mezani tunaanza kula simu ya mke wangu ilianza kuita, alikua ameiacha kwenye kochi, alitaka kunyanyuka kwenda kuichukua lakini Maggie alimuwahi.
“Mama ngoja nikakuchukulie!” Alienda na kuichukua, wakati anarudi aliuliza.
“Baba mbona unampigia Mama wakati uko hapa?” Alimuuliza Mama yake huku akimpa simu. Nilikua nimekaa karibu na mke wangu hivyo nilichungulia na kuona ni nani alikua anapiga. “My Hubby” Alikua amesave namba yake hivyo ndiyo maana Maggie alipoiona akajua kuwa mimi ndiyo nilikua nikimpigia simu Mama yake.
Mama yake alibaki anababaika hajui cha kufanya, sikutaka wanangu kujua kuwa Mama yao alikua anachepuka, basi nilitoa simu yangu harakaharaka na kumuambia.
“Simu imejipiga, ikate tu mke wangu.” Nilimuambia mke wangu ambaye ndiyo kama alikua kazinduka na kuikata simu yake. Basi aliiweka mezani lakini dakika mbili tena ikapiga, mtu yuleyule.
“Baba!” Maggie aliniambia tena.
“Hii simu yangu ina matatizo, ngoja niizime hatutakula chakula kwa raha kabisa!”Niliwaambia huku nikizima simu yangu, lengo langu lilikua ni mke wangu kushtuka naye kuzima simu yake. Lakini hakufanya hivyo, wakati nazima yangu yake iliita tena, nililazimika kuichikua na kuizimia mfukoni kwangu.
Mke wangu alionyesha kukasirika lakini hakuongea kitu chochote, alikula harakaharaka, hakua mchangamfu tena na alipomaliza bila kujali kama watoto wanataka kuendelea kuwa naye aliniambia nimpe simu yake akaingia chumbani kuongea, nilijua anaongea na mwanaume wake lakini sikua na namna, nililazimika kuwachekeshachekeasha watoto ili wasijue kama mimi na Mama yao hatuko sawa.
Tuliendelea kula mpaka kumaliza, niliingia chumbani na kumkuta mke wangu anapiga simu, alikua anapiga simu haipokelewi ila anapiga tena, haipokelewi, alikua kakasirika.
“Unakata simu yangu ya nini? Unajua kabisa tumeshaachana lakini unahangaika na mimi, umewapanga hawa watoto lakini nikuambie ukweli kuwa sikutaki, mimi nina mtu wangu na nina mimba yake, kama ulidhani utawatumia wanangu kunirudisha basi jua kuwa umechina, sikutaki niache na maisha yangu!’ Mke wangu aliniambia kwa hasira, nilitamani kumbembeleza ili abaki kwaajili ya watoto lakini nilikua na hasira sana nikikaaa kimya na kumuacha afanye anachotaka.
Aliendelea kupiga simu yake huku mimi nikiwa nimekaa kitandani, alikua akijiongelesha maneno ya hasira, wakati wote huo nilikua nikiliangalia tumbo lake ambalo lilishakua kubwa.
“Mamaaaa! Tunataka kulala huku!” Wanangu waliingia wakikimbia, walimkumbatia Mama yao na kumpeleka mpaka kitandani, mke wangu alilazimisha kuchjeka huku akiwaambia wakalale chumbani kwoa lakini waligoma kabisa. Wakati yuko kitandani na watoto simu ilianza kuita na ilikua ni namba ileile, mimi niliona ila watoto hawakuona, mke wangu hakua na namna zaidi ya kuizima simu.
Nililala pembeni yao, wanangu walikua na maswali mengi hasa kuhusu tumbo la Mama yao, walishakua wakubwa hivyo walijua kabisa kuwa Mma yao ni mjamzito na wanakaribia kuletewa mjukuu wao, walikua na furaha sana kwasababu hiyo. Asubuhi mke wangu aliwahi kuamka, akajiandaa, watoto aliwarudisha chumbani kwao, mimi pia nilijiandaa na kumuomba tuondoke wote kwaajili ya kwenda kazini kwani sikutaka wanangu kujua kama kuna tatizo.
“Ulichonifanyia sio sawa, kuwatumia watoto sijapenda kabisa, nakuambia sijapenda!” Alianza kulalamika kana kwamba mimi ndiyo niliwatuima waoto kuwa vile.
“Nimechoka na mambop yako, kudhani kuwa labda nawe4za kukung’ang’ania, naona ushanifanya mjinga, sijawatuma watoto nilikutafuta kwakua watoto walikua na huzuni wakiamini kuwa umekufa, lakini sasa washaakuona, hawatanisumbua tena hivyo uamuzi ni wako, kama unaondoka ondoka na kama unabaki baki, nenda kawaambie kuwa unaondoka hutaki kuishi nao ten!” Nilimjibu kwa hasira nikiamini kuwa mke wangu atatumia busara kuona kuwa tuna watoto na kubaki kwenye ndoa lakini haikua hivyo.
Aliniambia nimshushe, niligoma lakini alilazimishia, nilimshusha na kuendelea na safari yangu ya kazini. Lakini mchana nikiwa ofisini simu yangu iliita, ilikua ni simu ya nyumbani na aliyekua anaongea ni Maggie, binti yangu, alikua akilia akilalamika kuwa Mama yake kaondoka amewaambia hatarudi tena kwakua ana safari ya kikazi. Nililazimika kurudi nyumbani ndipo niliambiwa kuwa mke wangu alikua kaaga kuwa anasfari ya kikazi hivyo hawezi kukaa nao, akachukua baadhi ya nguo ambazo zilibaki nyumbani na kuondoka.
Niliwatuliza wanangu na kuwaambia kuwa ni safari ya muda tu na mwisho Mama yao atarudi. Ingawa nilijua kuwa si kweli lakini walinyong’onyea sana. Sikujua ni kwanini mke wangu alikua anafanya vile, akili yangu iliwaza mara mia nikifikiria ni wapi nilikua nimemkosea mke wangu lakini sikua na jibu. Nilimpigia simu zangu lakini hakupoke, nilihangaika sana hakupokea simu zangu wala kujibu meseji zangu, mwisho niliamua kukaa kimya.
****
Fuaha yote ambayo ilikua jana yake ilitoweka, wanangu walikua na huzuni kwani mbali ya Mama yao kuondoka lakini hata kwenye simu alikua hapatikani tena. Usiku mzima tulikua na kazi ya kumpigia simu mke wangu lakini simu yake ilikua haipatikani, ni kama alikua ameizima. Tuliwahi kulala kwani kila mtu alikua na mawazo yake. Lakini ilipofika saa nne hivi za usiku mlango uligongwa, mara simu yangu ikaiuta, alikua ni mke wangu, mwanzo sikutaka kuipokea lakini nilihisi labda anataka kuongea na watoto hivyo nikaamua kupokea.
“Fungua mlango au unataka nikabwe na vibaka!” Mke wanhgua liongea kwa hasira kisha akakata simu. Nilinyanyuka mpaka getini, nikaenda kufungua mlango, mke wangu alikua kasimama peke yake, hana kitu chochote mkononi. Pembeni yake kulikua na dereva bodaboda ambaye alikua kama anasubiria pesa yake, kwa bahatti nilikua nimevaa nguo ya mchana hivyo nilikua na hela, nilimlipa akaondoka. Mke wangu aliiingia ndani na kuniacha nikifunga geti.
Moja kwa moja aliingia bafuni, nilimsubiri mpaka akatoka wakati anajifuta ndipo niliona mwili wake ukiwa umevimbavimba, mbali na kuvimba na kuvilia damu kuonyesha kuwa alikua ametoka kupigwa lakini alikua na makovu mengi sana mgongoni, kama vile alikua akitandikwa viboko.
“Una nini, mbona uko hivi?” nilimuuliza, aliniangalia kwa hasira kisha akapanda kitandani kulala, nilijaribu kumuuliza lakini hakunijibu, alikaa kimya. Kwa kumuangalia nilijua kabisa alikua anapigwa, wakati akiwa amelala nilichukua simu yake, ilikua inatumia alama za vidole hivyo nilichukua kidole chake na kuifungua.
Kule nilikuta meseji nyingi akiomba msamaha kwa mwanaume wake lakini zote hazikujibiwa isipokua moja tu.
“Nimekuacha sikutaki tena, nakuambia hiyo mimba toa, nataka kurudiana na mke wangu, wewe si umerudiana na mume wako, toa hiyo mimba la sivyo nitakuua wewe na mwanao!” Alimjibu hivyo lakini mke wangu alizidi kutuma mseji nyingi za kuomba msamaha huku akisisitiza kuwa alishindwa kupokea simu kwakua alikua na watoto. Ilionyesha kuwa huyo mwanaume wake alikasirika kwa kitendo cha mke wangu kulala kwangu na kumkatia simu.
Niliiruddisha simu yangu na kulala, asubuhi haikua siku ya kazi hivyo watoto walipoamka walitukuta.
“Nimeamua nisisafiri ili nikae na nyinyi wanangu.” Mke wangu aliwaambia watoto, nilijua ni uongo lakini kuwapa wanangu siku moja mbili kwangu ilikua na ahueni, sikutaka kuwoana wanangu katika hali ile. Muda mwingi mke wangu alitumia na watoto, hakutaka kuongea na mimi, alikua anakwepa sana sisi kukaa wawili, hata ikitokea nimemkuta kakaa peke yake basi alinyanyuka na kuondoka au aliwaita watoto ili tu tusiwe wawili.
Mke wangu hakuondoka nyumbani lakini alikua hana amani kabisa, kila wakati alikua ni mtu wa kulia na mara nyingi nilikua nikimfumania anaongea na simu kama vile anaomba msamaha.
“Nataka uniambia huyo mwanaume ni nani na mbona anakutesa namna hiyo, niambie ni kitu gani ambacho anakupa mimi sikupi?” Nililazimika kumuuliza, kusema kweli nilikua naumia sana na nilishachoka kuishi na mwanamke ambaye naona kabisa anampenda mwanaume mwingine na yupo na mimi hata si kwasababu ya watoto bali kwakua tu amekataliwa.
“Mambo yangu hayakuhusu, kama hunitaki niambie, wewe si umewadanganya wanao kuacha kwenda shule ukidhani kuwa nitabki nao, mimi nina mwanaume mwingine, nina mwanaume wangu, kama unataka niendelee kubaki yhapa kuwafurahisha wanao basi nyamaza, ukitaka niondoke basi endelea kuongwa!” Aliniambia, ingawa sikutaka aondoke lakini nilishindwa kuvumilia, nilizidi kumbana ili aniambie huyo mwanaume ni nani lakini hakuniambia, nakumbuka ilikua ni jioni, alitoka ndani na kuondoka bila kuaga, hakurudi mpaka saa nne usiku nilipopigiwa simu na Mama yake mdogo.
“Mke wako yuko hospitalini, kaenda kufumania huko kapigwa mpaka kalazwa!” Aliniambia, nilijisikia vibaya lakini kwa namna alivyoniambia nilijua kuwa mke wangu ana hali mbaya, nilimuoba anielekeze hospitali aliyokua mke wangu, nilienda na kumkuta kwelia kwia kwenye hali mabya. Nilimuuliza kilichotokea lakini hakuniambia, aliniambia nimuache tu na maisha yake, Mama yake mdopgo ndiyo aliniambia kuwa, mke wangu alienda kwenye nyumba ambayo alikua akiishi mwanzoni na huyo mwanaume wake, lakini akakuta mwanaume wake anaishi na mfanyakazi mwenzake.
Akaanza kuzua vurugu na kutaka kumpiga huyo mwanamke mwingine lakini wote walimvamia na kumpiga sana. Alipotoka huko ndipo akampigia yeye simu ndiyo akampeleka hospitalini.
“Kwanini hakwenda Polisi?” Nilimuuliza.
“Angeenda yule wmanaume angemuua, mbona anampiga sana, hii si mara yake ya kwanza kulazwa hospitalini kwasababu yake, yaani tangu aondoke kwako kila siku ni vipigo, pamoja na mimba yake lakini anapigwa ila hakomi!” Ujauzito ulishakua mkubwa unakaribia miezi sita, niliumia sana, nilitamani kumuacha mke wangu pale na kuondoka kuendelea na maisha yangu lakini kila nikiondoka nilikua nashindwa, nilikua nampenda sana mke wangu hivyo nilijisikia vibaya kuona kuwa anateseka.
“Hivi mkwe naomba nikuulize kitu?” Mama yake mdogo aliniuliza. Tulikua tumekaa kwenye kiti nnje ya chumba alichokua kalazwa mke wangu, alikua amepumzika kwani presha ilikua imeshuka na walimtundikia Dripu. Tofauti na kawaida yake ambapo huongea kwa utani utani wakati huo Mama yake mdogo alikua siriasi kuna kitu anataka kujua.
“Niambie, uliza tu mkwe?”
“Kwanini unampenda Mama Maggie, unapata nini kwa huyu mwanamke, mbona umzuri na mambo yako kitandani si haba, anakusifia kuwa wewe ni bora kuliko huyo mbwa wake, una kila kitu lakini bado unamng’angania, amekupa nini, maana kama ni Mganga ningejue, mimi ndiyo shoga yake ila kama ni kuloga anahangaika kumloga yule ngedere lakini sio wewe!” Swali lake lilijaa maelezo ambayo kwa namna flani yalinifariji, kuna wakati nilikua najisikia vibaya nawaza labda mke wangu anchepuka kakua simridhishi kitandani.
Ingawa nilikua najiamini niko vizuri lakini nilikua na wasiwasi kwani kusema ukweli nilikua nampa mke wangu kila kitu, tulikua tuna watoto lakini bado alikua haniheshimu,a nachepuka na kunidhalilisha.
“Ni mke wangu, tumeapa kanisani mpaka kifo kitutenganishe.” Nilimjibu kwa kifupi kwani sikutaka kabisa kuzungumzia mambo yangu ya ndoa. Aliniangalia kwa huruma kana kwamba alikua anataka kuniambia kitu lakini akanyamaza.
“Unajua nimemzoea sana mke wangu, miaka yote hii ya ndoa tulikua vizuri ila sijui ni shetani gani kampata mwaka huu ndiyo mambo yakabadilika, naamini ni kipindi cha mpito, yatakuja kuisha tu.” Nilimjibu baada ya kuona kakaa kimya ananiangalia kwa huruma.
“Hivi unajua kuwa tangu unaoana naye alikua na huyo mwanaume na mpaka leo hawajachana, hivi unajua mamboa mabyo wanafanya, unajua kuwa alikua anamhonga, amemjengea mpaka nyumba, mwanaume anamnyanyasa, anamdhalilisha, anampiga kama mbwa, yaani hata kipindi mko vizuri alikua anampiga lakini mke wako alihangaika mpaka kuhakikisha anamzalia….” Aliongea maneno ambayo yalinichefua, ni kweli nilishajua kuwa mke wangu alikua amemzalia lakini sikutaka kujua ni mtoto yupi ambaye hakua wangu.
Nilishawakubali wanangu wote wawili kama wangu hivyo nilijua kama nitamuacha aendelee kuongea basi anaweza kunitajia mtoto ambaye si wangu.
“Naomba tuyaache haya mambo, ni mambo ya mimi na mke wangu, sasa hivi mke wangu yuko hospitalini kalala, sitaki kumhukumu, haya si mambo ya kuongea!” nilimjibu kwa hasira kidogo.
“Lakini….” Alijaribu kujielezea ila niligoma kabisa kumsikiliza.
“Hakuna cha lakini, niache na mke wangu, niache na maisha yang….” Nilimuambia lakini kabla ya kumalizia niliona mtu anaingia kwenye chumba cha mke wangu. Nalifika mlangoni ksiha akageuka, alikua kama kashtuka vile alipotuona.
Sikua nikimfahamu lakini sura haikua ngeni kabisa, nilimuangalia kwa kumkodolea macho huku nikivuta kumbukumbu kutaka kujua kuwa ni nani lakini sikuzipata. Alikuja mpaka tulipokua tumekaa, akanisalimia mimi kistaarabu kisha akamgeukia Mama mdogoa mabye nilimuona kama anatetemeak flani, ni kama alitaka kuongea kitu lakini alishindwa, ni kama alikua anaogopa flani hivi.
“Agness kalazwa chumba gani?” Aliuliza huku akimuangalia Mama mdogo, ahata hakumsalimia,a likua anamuangalia kwa ukali, ni kama alikuja kishari. Mama mdogo alinyamaza kimya, hakusema kitu chochote.
“Wewe mjinga si nimekuuliza kuwa mjinga mwenzako kalala chumba gani? Amenipigia simu kuwa yuko hospitalini nimekuja kukuona anshangaa nakukuta huku, kaniambia kuwa yuko peke yake, sasa wewe unafanya nini hapa? Nataka kujua kalazwa wapi?”
Aliuliza tena kwa dharau.
“Kelvin hapa si mahali pake kabisa, naomba uondoke, Mwanangua naumwa, hembu ondoka!” Mama mdogo aliongea, alitaja jina ambalo lilinifanya kukumbuka kila kitu. Kelvin alikua ni X wa mke wangu, sikua nikimfahamu bali nilsihawahi kuona picha yake kwenye simu ya mke wangu, tena zamani kabisa hata kabla hatujaanza ugomvi na sikuwahi kuuliza kwani nilijua ni picha tu, ilikua picha ya kawaida kama Pasport ya zamani na kwakua nilikua nikimuamini mke wangu basi niliacha kuuliza na sikuona shida.
Hasirfa zilinipanda, nilimuangalia kakitu kwenyewe kusema kweli hata kiganjani alikua hajai, sikujua alikua na kitu gani cha maana mpaka kumchanganya mke wangu kiasi hicho, alikua akiongea kwa dharau na alionyesha kuwa hajali kitu chochote.
“Si mahali pake, yeye ndioyo kaniita sasa unataka nini, nianchotaka nikujua kuwa yuko wapi na kujua kama hiyo mimba kaitoa au la, sitaki tena mawasiliano naye kwani ananiharibia ndoa yangu, akakea na huyo mpuuzi wake!” aliongea.
Nilijikuta napandwa na hasira, nilinyanyuka na kusimama mbele yake kwani alishaanza kumsogelea Mama mdogo kama vile anataka kumpiga.
“Broo hembu kuwa na heshima, mbona huwi mstaarabu lakini!” Nilimuambia huku nikimuangalia kichwani kwani alikua ni mfupi sana kwangu, aliniangalia kwa juu kama vile anatyaka kunipiga lakini mimi sikua kishari nilikua nahitaji tu aondoke. Lakini kabla sijafanya kitu chochote alinisikuma, nilikua sijajiandaa kwa chochote hivyo nilipepesuka na kudondoka.
“Acha kuingilia mambo ya watu hayakuhusu!” Aliongea kwa hasira hukua kimfuata Mama mdogo na kumkunja kama anataka kumpiga.
Baba Maggie ndiyo kwanza anakutana na mwanaume ambaye anatembea na mke wake. Anajaribu kuwa mstaarabu lakini mwenzake hata hataki ustaarabu, unafikiri ni nini kitatokea?
MAMA MAGGIE; NAKUPENDA SANA ILA SHETANI AMEKUPENDA ZAIDI! —SEHEMU YA SABA
Nioliona huu ni ujinga, hivi huyu anataka kunipadna kichwani, mbona anataka kufanya mambo kama haya! Yaani anatembea na mke wangu halafu anakuja kunidhalilisha. Alikua kamshika Mama mdogo na kurusha kofi kumpiga, lakini nililiona, bnilikaklamata kamkono kake kembamba na kuanza kumkunja mkono. Kwa kuniangalia mimi nayeye ni kama alikua mtoto kwangu, sikutaka kumpiga lakini nilitaka kumfundisha adabu.
“Mamaaaaaaa!” Alipiga kelele wakati na mkunja mkono, nilimbana sana mpaka akwa anainama ili nisiendelee kumkunja lakini sikumuacha.
“Wewe mshenzi naichie! Niache haya mambo hayakuhusu!” Alipiga kelele lakini sikumuachia, nilikua na hasira kuona kuwa mbali na kutembea na mke wangu kumbe pia alikua anampiga na mabya zaidi hana hata nidhamu kampiga halafu amekuja kumuona hospitalinji.
Sikurusha hata ngumi lakini nilimkunja mpaka akajikojolea, alipiga kelele walinzi wakaja na kunishika.
“Kuna nini hapa?” Mlinzi aliuliza baada ya kunishika na kunifanya kumuachia, mimi sikuongea kitu, yeye alikua analalamika kama mtoto akipiga kelele tu!
“Nimekuja kumuona mke wangu huyu Kaka kanivamia, hata simjui anhaingilia mambo yangu! Nakuambia utanitambua! Unataka kujua mimi nani basi nitakuonyesha, umenidhalilisha sana ila nitakuonyesha!” Alipiga kelele, kwa kawaida mimi ni mpole lakini siku hiyo nilishindwa kuzuia hasira zangu.
Nilibadilika kwa hasira nikawa mwekundu, mwili umenivimba yaani mpaka watu waliniogopa. Mlinzi aliyekua amenishika mwenyewe nilimuona akitetemeaka kwani alikua hajui kama nitafanya nini kutokana na hasira nilizokua nazo.
“Sio mke wake, ni hawara tu na huyu ndiyo mume wake wa ndoa, kampiga mke wa mtu halafu anakuja haopa kuleta fujo!” Mama mdogo ambaye naye alikua ananiangalia anatetemeka aliongea, Kelvin kusikia hivyo aliniangalia kwa uoga zaidi, aliniangalia juu mpaka chini hakunimaliza, alikua akifurukuta na kuongea vitisho lakini baada ya kusikia kuwa mimi ndiyo mume wa mchepuko wake basi alinyamaza kimya, alinywea.
“Broo wewe ondoka tu hapa maana utatuletea shida!” mlinzi aliongea huku akimshika kumuondoa. Lakini ni kama aligoma flani, aliona kama andhalilika.
“Nawewe uisinishike kwani siwezi kuondoka mwenyewe?” Aliongea kwa hasira, nilijikuta namimi napandwa na hasira na kutaka kumrukia, lakini mlinzi aliniwahi, huku suruali yake ikiwa imeloa alikimbia na kuingia kwenye gari. Nililiangalia vizuri lilikua bni gari la mke wangu, ambalo nakumbuka nilimnunulia muda mrefu wakati anajifungua mtoto wetu wa kwanza, nilimnunulia kama zawadi lakinibaada ya muda aliniambia linasumbua akaliuza.
Lilikua ni gari la muda lakini bado nilikua nalikumbuka, namba zilikua zilezile, aliulza nikamuongezea pesa kanunua jingine, sikujua kama alinidanganya hakuuza alimpa hawala yake. Roho iliniuma sana.
“Inamaana huyu mwanamke hakuwahi kunipenda kabisa, mbona hili gari ni lazimani sana. Kumbuka wakati huo mwanangu wa kwanza alikua na miaka tisa. Ila nilimnunilia wakati anajifungua, kipindi hciho ndoa yetu ina kama mwaka na nusu, alikuja kuliuza baada ya miaka miwili tu, akidai linamsumbua.
“Inamaana ameanza kuchepuka wakatio ndoa haijafikisha hata miaka minne!” ingawa sikusema chochote lakini niliumia sana.
“Sijui hata kwanini Agness anahangaika na huyu mwanaume, yaani hana kitu, ana mke kila siku anagombana na mke wake anaondoka. Anapigwa kila siku lakini hasikii, hata sijui ni kwanini anamng’ang’ania, yaani hata pesa hampi lakini amechanganyikiwa!” Mama mdogo aliongea, maneno yake yalikua yananikera na kuniumiza kiasi kwamba nilishindwa kuvumilia, kwa hasira nilizokua nazo niliona kama nikiendelea kukaa pale basi nitachanganyikiwa.
Niliondoka pale na kwenda Bar, nilikaa Baa kwa zaidi ya masaa kumi, nimekaa tu nakunywa maji. Sikutaka kunywa pombe kwani nilishaapa sinywi tena pombe ingawa nilitamani kuinywa kwaajili ya kunipotezea mawazo lakini nikikumbuka wanangu niliacha nilikunywa maji mpaka mhudumu akagoma kuniletea. Aliniona kama nina mawazao, hakua ni mtu mzima, akalikua ni kabinti kama ka miaka 22 hivi, kalikuja kukaa pembeni yangu na kuanza kuniongelesha.
“Kaka kama una mawazo sana kunywa bia, haya maji yatakuchanganya, unajazia mikojo tu!” Aliniambia, wakati huo nilikua nimeshakunywa kama maji chupa kumi za lita moja na nusu, nilikaa muda mrefu pale, nilikua na safari za kwenda chooni kila dakika. Nilikaangalia kale katoto kisha nikacheka kwani niliona kama hakawezi kunisaidia kitu chochote.
“Baba yangu alipokufa nilikua na mawazo sana, tena kipindi hicho ndiyo nilitoka kuachwa na mchumba wangu, nakuambia, aisee niliumia, yaani….”
Kalianza kuongea mambo yake, sijui kwanini lakini nilikasikiliza, kalikua ni kabinti kazuri, kanaonekana bado kadogo, nilipokauliza umri kalinimbia miaka 22, muonekano wake ulikua ni wa kitoto, kana shape nzuri, ukisikia ile namba nane ilikua namba nane haswa. Ingwakua ni kipindi changu, sijaoa na kuapa kuwa siwezi kumsaliti mke wangu kwa kumuangalia yule binti tu basi msisimko wake ungekua ni wa haja kwani kusema kweli kalikua kazuri na kialikua kanaongea mpaka basi.
“Yaani kaka yangu wanaume wanaumiza, unajua siku hiyo ilikuaje. Ben alikuja nyumbani wakati Baba anaumwa, basis hi kuna rafuiki zangu walikuja kumuona Baba yangu ambaye alikua na hali mbaya, kumbe wakati mimi niko ndani wakaonana huku nnje, wakabadilishana namba. Basi wakaanza mahusiano mimi sijui, huwezi amini siku nampigia simu Ben ili kumuambia kuwa Baba yangu amekufa, yaani hembu fikiria Kaka. Mimi ndiyo nilikua namuuguza Baba yangu, mimi na Mama yangu, wakati huo nilikua chuo na mama yangu alikua ni Mama wa nyumbani.
Baba alikua anaumwa sanaa, lakini alikua na Biashara zake ila alikua hataki Mama afanye kiazi, basi lipopata kansa si akatumia hela yote kumtibu, tukauza na nyumba, wadogo zangu wakalazimika kurudi shule za serikali na mimi chuo ni kaacha. Mama wakati namuuguza Baba si ndiyo ikabidi auze nguo, Bai kaka si akawa anazungusha mitumba, kwa wtau, mimi niko nyumbani na Baba basi Baba akafariki.
Ni mwaka jana unajua Kaka….” Kale kabinti kaliendelea kuongea, sikutaka kuongea naye lakini kwa alivyokua anaongea nilijua kuwa huyu mtoto anasumu nyingi anatakiwa kuitema.
“G, unafanya nini na mteja, njoo uhudumie watu wengine huku?” Meneja wa ile Baa alimuita kabla ya kumalizia, binti alinyanyuka na kwenda kuhudumia meza nyingine kisha akarudi tena, hata sikumuambia kama nataka kuendelea kusikiliza au la ila aliendelea kuongea.
“Basi Kaka samahani kwa kukukatisha, Baba alifia mikononi mwangu, nilipaniki kaka. Unajua nini, kwakua nampebda Boy wangu kabla hata ya kumpigia simu Mama kuwa Bbaa amefaiki nikampigia Ben, huwezi amini kaka kilichotokea…” alinyamaza kidogo kuniangalia kama nilikua namsikiliza, kweli nilikua namsikiliza lakini sikujua kama natakiwa kumjibu, nilimuona kama kakasirika kidogo hivyo nikalazimika kuongea ili afurehi nayeye.
“Nini kilitokea?” nilimuuliza, kusema kweli nilikua sihitaji kusikia matatizo yake lakini sikua na namna.
“Basi Kaka, nilipiga Ben hakupoke, alipoke arafiki yangu akanitukana na kuniambia nisimtafute mwanaume wake. Yaani kaka iliniumiza sana, nililia sana mpaka nikasema siwei kupenda tena!” Aliniambia, nilimuangalia alivyokua, umri wake na vitu anavyoongea mpaka nikatamani kucheka, hata penda tena wakati bado mdogo.
“Kaka huwezi amini, Ben alikuja na rafiki yangu kwenye msiba wa Baba yangu na walikua wanshikanashikana nililia vingi sana lakini nilipona. Basi nikasema maisha laima yaendelee, nilikua sijwahahi kunwa pombe Kaka lakini nilikunywa mpaka niksahau, kama unataka nikuletee bia unywe utasahau kila kitu!” Yule mtoto aliniambia, nilimuonea huruma na kuona kama alishaharibikiwa kwani alikua ananishawishi ninywe kana kwamba mimi ni mtoto.
“Kama hunywi ninunulie basi Bia?” Aliniambia nilimuambia aagize pombe, nilishanga analeta Konyagi kubwa na kuiweka mezani, nilimuangalia bila kummaliza lakini yeye wala hakujali.
“Unasema ulikua uansoma chuo?” Nilimuuiliza.
“NdiyoKaka, nilikua nasomea Sheria Mzumbe, wakati Baba anafariki mwaka jana nilikua mwaka wa kwanza, si nikekuambia nina miaka 22. Sikua na mkopo nilikua Private, yaani Kaka, so kila kitu kiliharibika. Unajua Baba yangu alikua na pesa na alikua anatujali sana, lakini alipougua ndugu wote walimtenga, ubaya nikuwa, Biashara zake wote alikua anafanya kwa kificho na ndugu zake, Maama alikua ni Mama wa nyumbanitu. Nikuambie Kaka, mimi nikiolewa siwezi kukaa ndani, mwanaume hanikalishi ndani.
Mama yangu sasa hivi anauza chupi na sididia za mtumba anazungusha wakati Baba alikua ni tajiri ana maduka na nyumba!” aliniambia maneno ambayo yalinichoma sana.
“Inamaana mali za Baba yako ziko wapi, hakuwaachia?” Nilimuuliza.
“Mali ziliisha wakati Baba anaumwa, na kwakua Mama alikua anakaa tu absi marafiki zake walimdhulumu vitu vingi, ndugu waliuza nyumba kipindi Baba yuko hai kwa madai ya matibabu lakini walimdhulumu, Baba hakumuamini Mama hata kusimamia uuzwaji wa nyumba, aliuza nyumba mbili kwaajili ya kwenda India ila alifia nyumbani hata Muhimbili hakua na pesa ya kulipa!”
Nilijiona nina matatizo lakini huyu binti nilihisi kapitia mengi kuliko mimi. Alikua akinywa konyagi tena kavu kama vile chizi, yaani kuna wakati nilimzuia na kumuambia nataka kumsikiliza zaidi.
“Wewe ni mzuri na unaonekana una pesa, hakuna mwanamke wa kukusumbua! Aisee ningekua wewe ningekula kila mwanamke, hivi kuna mwanamke gani atakusumbua wewe! Mimi hata ukinitaka ni pesa yako tu, nafanya kila kitu ila nyuma hapana, najiheshimu, lakini nikikaa na wewe nakusahaulisha kila kitu!” Aliongea huku akipitisha mikono yake kwenye suruali yangu, niliona pombe ishamkolea alipoona simtongozi absi yeye alianza kunitonngoza.
“Kwahiyo chuo ndiyo umeacha, huna mpango wa kurudi tena?” Nilimuuliza huku nikiuondoa mkono wake kwenye mapaja yangu na kuuweka pembeni. Sikutaka afike huko.
“Kaka nina waodogo zangu wanne nawatafutia hata pesa ya kula, mama yangu anauza chupi mtaani, pesa yake haitoshi hata kulipia kodi, inabidi kuhangaika wadogo zangu wale. Hapa nilipo nalipwa elfu sitini, nikidangadanga na viti ndiyo unakuta naweza kununua chakula na vinguo vya waodgo zangu. Kusoma tena sijui, labda huko mbeleni nikijipanga vizuri ila kwasasa hapana!”
Wakati tunaongea simu yangu iliita, ilikua ni simu ya Mama modgo, niliiangalia bila kuipokea, alianza kunishikashika.
“Huyo ndiyo mwanamke aliyekuumiza?” G, ambaye nilikuga kujua kuwa anaitywa Grace aliniuliza.
“Najua, unavyoonekana umechanganyikiwa juu ya mwanamke, nauza hapa huu mwaka najua wanaume walivyo!” Aliniambia, sikumjibu kwani simu yangu iliiita, ilikua ni simu ya nyumbani. Niliipokea aliyekua akiongea ni Mage.
“Baba uko wapi Mamka anaumwa, Mama kapata ajali huko safarini, njooo….” Mwanaqngu alikua analalamika, mpaka wakati huo nilikua hata sijawaambia kitu kuhusu Mama yao na wala nilikua sijui ni kitu gani cha kuwaambia, simu yake ni kama ilinishtua kuwa kumbe nina watoto ambao wananingojea nyumbani.
“Naomba niondoke, nyumbani kwangu hakuko vizuri.” Nilimuambia huku nikinyanyuka, nilitoa pesa na kulipa kisha nikamuachia shilingi laki moja.
“Kamuongezee Mama yako mtaji.” Nilimuambia nakuondoka, hakuniomba namba ya simu wala nini niliondoka na kurudi nyumbani. Kichwani nilikua na mawazo mengi pamoja na hasira lakini nilijitahidi sana kujizuia kwaajili ya wanangu.
Ulikua ni usiku, sikujua kilichokua kikiendelea hospitalini ila nilipofika nyumbani nilikuta mke wangu yupo nyumbani na Mama yake mdogo. Wanangu wamemzunguka na stori nikuwa alikua kapata ajali ya gari. Nilisalimiana nao na kujifanya nilikua sijui chochote, sikumuonyesha mke wangu hasira, ingawa nilikua naumia lakini nililazimisha furaha. Sikukaa sebuleni sana, pamoja na wanangu kutaka nikae, kutaka niwe na Mama yao lakini sikutaka kukaa.
“Mama yenu anaumwa muacheni apumzike.” Niliwambia wanangu nikamchukua mke wangu m[paka chumbani, tukaingia ndani.
“Mkwe utalala chumba ha wageni huwezi kuondoka usiku huu!” Nilimuambia Mama mdogo wake lakini aligoma, aliniambia ameshaita bodaboda wake kumchukua na mimi sikua na muda wa kubishana naye, nilimuacha akaondoka na mimi kuingia chumbani na mke wangu.
Kuingia tu chumbani nilifunga mlango, kwajinisi nilivyokua nwafahamu wanangu nilijua lazima watakuja chumbani kutaka kulala na Mama yao kwakua anaumwa kitu ambacho nilikua sitaki kuona kikitokea. Nilimlaza mke wangu kitandani kisha nikaenda bafuni kuoga, nikiwa huko nilimsikia mke wangu akilalamika lakini hata sikumjibu.
“Sio kama nimerudi, nimekuja tu kwakua wanangu wanatakiw akuniona…” Aliongea, mimi sikumjibu kabisa, nilibaki kimya tu. Nilitoka bafuni na kumkutabado analalamika.
“Kwahiyo ndiyo ukaona kuwa uniharibie, Kelvin hapokei simu zangu, si ulikua unamuulizia, basi ushamuona, yule ndiyo mwanaume wa maisha yangu, ananijulia, ananipenda na mimi nampenda!” Sijui kwanini mke wangu alikua ananichopkonoa namna ile, nilishamvumilia sana lakini niliona kama anataka kunipenda kichwani, kama mtu anayetaka kupigwa tu.
“Ukaamua kumdhalilisha, najua sasa hivi ana hasira hataki kuongea na mimi, ila nikuambie, sasa hivi nikipona nadai talaka mwenyewe. Sijali kuhusu watoto!” Aliniambia, nilipandwa na hasira kiasi nikaona siwezi kuka atena mule ndani nilitaka kutoka lakini kabla ya kutoka simu yangu iliita. Namba ilisaviiwa G, nilishangaa kwani sikua na namba kama hiyo, kwakua nilikua na hasira nataka mke wangu anyamaze basi niliiokea tu ambapo nilikutana na sauti ya kike.
“Hahhahahaha! Najua uanshangaa namba yangu imekujakujaje kwako, niliisave katika simu yako na mimi kuchukua yako. G, Grace, vipi umefika nyumbani?” Aliniuliza, nilimjibu vizuri na kukaa kitandani.
“Mimi nimeshafunga, kama vipi unaweza kunipitia, nimekupenda, umstaarabu sana!” Kale kabinti kalianza kuongea mambo ya kimapenzi na kuniambia kuwa anataka kuonana na mimi.
Nilimsikiliza na kuongea naye viziri tu ila nilimuambia kuwa mimis iwezi kutoka usiku huo. Baadaye nilikata simu.
“Inamana umeamua kuongea na Malaya wako mbele yangu! kwahiyo huniheshimu, unaniomba msamaha lakini bado unachepuka!” mke wangu aliwaka sana, lakini cha ajabu sikujisikia vibaya, jinsi alivyokua akikasirika ndivyo nilikua nikijisikia raha, niliona kama nayeye anaumia.
Mke wangu aliacha kabisa kujitapa kuwa anaondoka na kuanza kulalamika kuwa nachepuka, namsaliti na kulalamika sana, mimi ndiyo nilijisikia raha. Nilijikuta nachukua ufunguo wa gari, kisha nikampigia G, nakumuuliza.
“Uko wapi? Nielekeze ulipo nataka kuja kukuchukua, kama ulivyosema sitakiwi kuumizwa tena na mapenzi!” nilimuambia huku nikitoka na kumuacha mke wangu chumbani akilalamika, nilijisikia vizuri sana na kweli nilikua na hamu ya kuonana na G, kitendo cha kumuacha mke wangu namna ile kiilinipa raha, ni kama nilikua nimepata uhuru flani hivi!
INTERVIEW NA AJIRA; Hiki ni Kitabu changu kipya ambacho kinazungumzia mambo ya AJIRA. Kina maelezo kuanzia namna ya kuandika Barua ya kuomba kazi, kuandika CV kujiandaa na usahili. Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kwenye Usahili na namna ya kuyajibu, namna ya kutengeneza Connection za kiajira na namna ya kutumia mitandao kupata ajira.
Kisome kutokana na mahitaji yako ya wakati huo, iwe unajiandaa kwa usahili au ndiyo unaandika Barua au kuandaa Cv. Bei yake ni shilingi elfu kumi. Kupata kitabu unalipia kwa M-pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222 Jina linakuja Iddi Makengo, sina namba nyingine zaidi ya hizo baada ya hapo kitabu utatumiwa kwa njia ya Whatsapp/Email/Facebook.
Je, huu ndiyo mwanzo wa Baba Maggie kuchepuka na kuanza kumnyanyasa mke wake? Vipi Mama Maggie atafanya nini? Je ataondoka na kumuacha mume wake kurudi kwa Kelvin, vipi je Kelvin atampokea. Nisikuchoshe aendelea kufuatilia hapahapa!
MAMA MAGGIE; NAKUPENDA SANA ILA SHETANI AMEKUPENDA ZAIDI! —SEHEMU YA NANE
Niliondoka na kumuacha mke wangu akilalamika, G, alikua ndiyo anafunga Baa anataka kuondoka, nilimpitia kwenye ile Baa na kuondoka naye. kusema kweli sikujua naenda naye wapi wala sikua nimepanga ni kitu gani cha kufanya naye ila kwa kuondoka tu pale nyumbani na kumuacha mke wangu akilalamika basi ilinipa uhuru wa ajabu, nilikua kama nimetua mzigo flani ambao huko nyuma nilikua sijawahi kuutua.
“Tunaenda wapi?” G aliniuliza, nilikua nazunguka tu kwenye gari, kusema kweli nilikua sijapanga kufanya kitu chochote ingawa nilikua na furaha ya kuondoka nyumbani.
“Kwani unaonatakaje? Mimi naona tubaki tu kwenye gari?” Nilimuuliza kisha akacheka.
“Aisee, wewe ni mshamba kweli, inamaana hujawahi kucheuka kabisa?” Aliniuliza.
“Kuchepuka nini, mimi nilijua kuwa umenitafuta ili tuongee.” Nilijiongelesha, ingawa nilijua anataka tufanye mapenzi lakini sikutaka kuingia kichwa kichwa.
“Uongee na nani? Hivi kweli mimi mtoto mzuri hivi nikuite ili tuongee, ningetaka mtu wa kuongea naye si ningeenda kwa mashoga zangu amabo wamekosa mtu wa kudanga!” Aliongea kwa hasira kidogo hukua kiingiza mikono yake kwenye suruali yangu, kabla sijakaa vizuri aliniinamia sehemu zangu za siri na kutaka kunifungua zipu. Binti alikua harakaharaka, hakujali kama nilikua barabarani naendesha gari.
“Acha bwana, unajua nitagonga, naendesha gari, hembu acha nisije kugonga.” Niliongea kwa haisra huku nikimuondoa mapajani mwangu kwani nliona kama anataka kuniua.
“Kama unaendesha gari basi simamsiha, mimi siwezi kukuacha uondoke hivi hivi!” Aliniambia, nilinisi kama ni utani lakini haikua hivyo, alikua anamaanisha, aliendelea kuhusika na sehemu zangu za siri mpaka nilipoona kuwa kuna jali inakuja nikasimaisha ghari pembeni.
“Ushawahi kufanya mapenzi ndani ya gari?” Aliniuliza, nilimuambia hapana alicheka tena kisha akanifungua zipu ya suruali, kweli nilikua simesisimkwa na nilitaka kufanya naye mapenzi pale. Lakini kabala sijafanya kitu chochote simu yangu iliita, alikua ni mke wangu, niliacha kuipokea kwani sikua katika hali nzuri ya kuongea na sikutaka mke wangu kusikia mambo yaliyokua yanaendelea.
“Ni mke wako, pokea, ndiyoa nakusumbua?” Aliniuliza huku akiacha alichokua akikifanya na kukaa kuniangalia, kulikua na kagizagiza hivyo hatukuonana vizuri.
“Umejuaje kama mke wangu ananisumbua?”
Nilimuuliza, aliniangalia na kucheka.
“Unaonekana umechanganyikiwa, nimeshatembea na waume za watu wengi tu, mwanaume malaya unamjua na mwenye stress unamjua, una mawazo na haya si ya kazi ni ya mke.” Aliniambia, niliona kama ananijua, ananisoma kwa kuniangalia, sikutaka kuongea mambo yangu lakini nilijikuta kwa yule binti nafunguka.
“Nampenda sana mke wangu, lakini ananisumbua sijui hata shida ni nini? Yaani, anhisi kuchanganyikiwa kabisa!” Nilijikuta namuambia. Alichukua tena mkono wake na kuuingiza tena sehemu zangu za siri, alinisuguasugua kisha akaniambia.
“Unaona, hakuna kitu, yaani, sijui kwanini unahangaika hivi na huyo mwanamke. Uko na mtoto mzuri namna hii lakini unahangaika na yule mjinga!” Aliongea kana kwamba anamfahamu mke wangu, nilishtuka na kuhisi kama ni mtego.
“Unamfahamu mke wangu?” Nilimuuliza kwa uoga kidogo kwani yule binti nilianza kutokumuelewa.
“Hapana, ila nimeona picha zake, hata sio mzuri kihivyo, ni mzuri ila kazeeka sio mtu wa kunitishia maisha.”
“Picha zake, uliziona wapi?” Alikua ameniinamia kisha akarudi kwenye siti yake, alifunga mkanda na kuniambia tuondoke.
“Unaona jinsi ulivyo na mawazo, hata hujui kuwa nilishika simu yako, nikaweka namba yangu na kujibeep na wewe picha uliyoweka hapo kwenye sgreensaver ni ya mke wako na watoto!” Aliniambia, nilipimua kidogo kujua kuwa alikua hamfahamu mke wangu.
Aliniambia tuondoke, sikujua kama nianenda wapi ila alinielekeza mpaka kwake. Alikua akiishi katika kachumba kamoja, hakua na kitanda bali godoro tu ambalo lilitandikwa chini, ndoo ya maji na ya vyombo pamoja na kajiko kadogo kagesi. Sijui ni kwasababu ya mawazo lakini nilijikuta naingia bila shida yoyote na kukaa pale kwenye godoro.
“Unataka nikupikie nini?” aliniuliza kama utani, nilimuambia niko sawa naye hakuuliza tena. Alivua nguo nikiwa namuangalia, akaingia kuoga kisha akarudi akiwa uchi wa mnyama alikaa kitandani.
Nilikua namuangalia lakini ni kama nilikua simuoni, alikua ananiongelesha ila ni kama alikua anaongea peke yake kwani mimi nilikua na mawazo yangu mengi tu. Sikumtilia maanani mpaka aliponivamia, akanikumbatia na kuanza kunivua nguo.
“Mke wangu kila siku ananisaliti, huu ndiyo wakati wangu wa kulipa kisasi!” Nilijikuta naongea kwa hasira. Nilihisi kama nawaza kwamba ni maneno yanazunguka kichwani kwangu lakini kumbe nilikua naongea kwa sauti na alikua anasikia.
Maneno yangu yalimuongezea nguvu ya kuhangaika na mimi ili nisisimkwe lakini kusema ukweli pamoja na uzuri wake, pamoja na juhudi zake za kuuchezea mwili wangu sikujisikia kitu chochote. Nilishindwa kabisa kufanya mapenzi na yule binti, aliniangalia kwa huruma na kunipa moyo ila mimi sikujisikia vizuri kabisa.
“Ni kawaida, hii ni mara yako ya kwanza kuchepuka, una mawazo sana, nakuambia baada ya muda utakua vizuri tu!” Aliniambia, nilimsikiliza lakini kichwa changu hakikua sawa.
Sikua nimepanga kufanya mapenzi na yule binti siku hiyo, lakini kitendo cha kujaribu kufanya mapenzi na kushindwa kiliniumiza sana. Nilianza kujisikia vibaya, niliogopa na kuhisi labda atanitangaza. Nilishindwa kukaa naye, nikavaa nguo zake na kumpa laki moja.
“Unanipa ya nini?” unaniona kama mimi ni malaya?” aliniuliza kwa hasira, nilishindwa kumuelewa kwani tangu kukutana naye, stori zake na matendo yake yalionyesha kuwa alichokua akikihitaji yeye ni pesa tu, sasa nashangaa kwanini nampa hizo pes anaaikataa.
“Mimi ni malaya kweli lakini sikutaka kufanya mapenzi na wewe kwaajili ya pesa. Ningekua na pesa ningeondoka ne yule mheshimiwa, tena nikitembea naye ananipa pesa ya maana lakini nikaamua kukuitafuta kwakua una mawazo! Nimekutafuta kama rafiki kukufariji halafu leo unanipa pesa kama malaya!”
Aliongea kwa hasira na hisia nyingi, kusema kweli nilijisikia vibaya tena, niliiacha ile pesa pale chini na kutoka kama mwizi kwani niliona kabisa kuwa anazidi kunichanganya. Nilirudi nyumbani na kwenda moja wka moja kuoga, mke wangu alijaribu kunisemesha na kulalamika lakini sikumjibu kitu chochote, nilikua na mawazo mengi kiasi cha kushindwa kuongea. Kesho yake niliamka nikiwa katika mawazo mengi, nilitamani kumtafuta G ili kujaribu kufanya naye mapenzi lakini niliogopa, mchana mzima sikufanya kitu chochote, nilikua na mawazo mengi sana.
Usiku nilitoka tena, safari hii niliamua kwenda kutafuta mwanamke wale wa kujiuza, nilitaka kuangalia kama nikifanya mapenzi nitaweza au la. Nilichukua mwanamke na kwenda naye nyumba ya kulala wageni, sikujali kuhusu hadhi yangu wala kitu chochote kile, akili yangu nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa.
“Kaka una matatizo au ndiyo mara yako ya kwanza?” Yuile binti aliniuliza baada ya kujaribu kufanya mapenzi na mimi ila uume haukusimama, nililazimika kumuambia kuwa ndiyo siku yangu ya kwanza akanielewa lakini hata baada ya kujaribu haukusimama hivyo nilimlipa pes ayake na kuondoka.
Lakini sikuishia na huyo mwanamke, nilienda sehemu nyingine na siku hiyo nilijaribu kufanya mapenzi na wanawake kama watano bila mafanikio, uume ulikua hausimami. Hali hiyo iliendelea kwa wiki mbili, nilibadilika sana, nikawa na mawazo mengi, nyumbani sikai mpaka sasa mke wangu ndiyo akaanza kunionea wivu, bado alikua anaumwa, bado alikua na ujauzito wa mwanaume mwingine lakini sikujasli, kila nikirudi ndani ni kama vile mke wangua likua hayupo, aliniona nabadilika, mwili umepungua sana kiasi cha kushindwa kufanya kitu chochote.
****
Baada ya mimi kubadilika kutokana na mawazo ya kushindwa kufanya tendo la ndoa mke wangu naye alibadilia. Hali yangu ya afya ilikua mbaya na nilikua mtu wa hasira sana, sikuwahi kuwapiga wanangu lakini nilikua nahasira kiasi kwamba mtoto akinisemesha kidogo nakasirika nusu kumpiga.
“”Mume wangu unachofanya sio sawa!” siku moja mke wangua liniambia, nakumbuka ilikua ni siku ya jumapili, tulikua tumetoka kanisani. Kwa kawaioda kila tukitoka kanisani na wanangu tunapend kuongea kuhusu mambo ambayo wanangu wamejifunza, sikuhiyo nilipotoka tu kanisani niliingia chumbani na sikutaka kuongea na mtu mwingine yoyote.
Mage alikuja chumbani na kuanza kunisomea Bibilia, mwanzo niliona kawaida ila jinsi alivyokua anauliza maswali nilikasirika na kumfukuza.
“Ondoka! Mungu! Mungu! Mungu gani huyo? Kama angekuepo nngeteseka namna hii.. watoto wakikae hasara kabisa, wewe si ni kama Mama yako, utakuja kuolewa umsumbue na mume wako, mshenzi kabisa, nakuambia kitu husikii! Ndiyo Mama yako kakufundisha kwua usisikie! Mimi ndiyo mwanaume humu ndani kama huwezi kunizikiliza mimi huyo Mungu wako utamsikiliza, nimekuambisitaki kusomewa Bibilia lakini hutaki kunisikia! Kwanza sina hata imani kuwa wewe ni moto wangu!”
Niliongea maneno mengi nikimlaumu Mungu kutokana na maisha yaangu. Wakati namfokea mtoto Mama yake ndiyoa likua anaingia, Mage alibaki kasimamama, haongei, hapigi kelele lakini machozi yanamtoka, niliongea sana na kumfokea nikimuambia mpaka mambo amayo hayamhusu. Hakuondoka mpaka Mama yake alipokuja na kumchukua akamtoa nnje na kumbembeleza ndipo alikuja kwangu kuongea na mimi.
“Najua nimekukosea lakini nimeamua kujirekebisha na hawa watoto hawahusiki na chochote!” Mke wangu aliniambia, nilimuangalia kwa hasira bila kusema chochote nilinyanyuka na kuondoka zangu. Nilipoondoka tu alianza kunitumia meseji za kuniomba masamaha na kutaka tuongee lakini sikua tayari, nilikua kama vile nimechanganyikiwa sisikii chochote. Aliniomba sana msamaha lakini hata sikujali, nilishapanga sinywi pombe lakini siku hiyo nilikunywa. Nilirudi nyumbani usiku na kwenda moja kwa moja kulala.
Nilifika na kumkuta mke wang bado hajalala, alikua kakaa kitandani na mimba yake kubwa ananiangalia.
“Unajau watoto wanakuogopa?” Aliniambia, nilimuangalia kwa dharau kisha nilihisi kupandwa kwa hasira.
“Wananiogopa eeehh! Hivyo ndiyo ninavyotaka, wewe si ndiyo Mama yao, unawafundisha ujinga hawaniheshimu! Kwanza nawewe unatakiwa kuniogopa, si unaniona mimi kuwa si mwanaume! Sasa ngoja nikuonyeshe uanaume wangu!” Niliongea kwa hasira lakini kadri nilivyokua nikiongea nilishangaa kuona kuwa uume wangu unasimama, nasisimkw akupita kiasi.
Nilimvamia mke wangu nakufanya naye mapenzi, hakunizuuia, alinipokea na nilifanya naye mapenzi bila kuchoka kwa karibu lisaa lizima, alifikia hatua mpaka akaniomba nimauche apumzike! Nilimuacha akapumzika tukakumbatiana tukalala, siku hiyo nilijisikia vizuri sana, nilikua na amani na nilipoamka niliwaomba wanangu msamaha wka kuwa na hasira. Nilimsingizia shetani mkama kawaida, ilikua ni siku ya kazi lakini nilitaka kutoka na wanangu, niliwaambia hakuna kwenda shule na mimi na mke wangu tulitoka.
Nilikua na amani sana, baada ya kutoka huko mke wangu aliniomba smamaha sana lakini nilimuambia kuwa sitaki kuzungumzia hayo mambo. Mimi si mtu wa kuweka vinyongo na mara nyingi nikiwa na kitu nakimaliza kwa kuongea kisha sipendi kuzungumza zungumza tena. Nilimsamehe mke wangu na kutaka kusahau kabisa.
Nyumba ilikua na amani kwa miezi miwili, kila kitu kilirudi sawa. Mke wangu alikua anakaribia kujifungua hivyo nililazimika kumkaribisha Mama yake mdogo ili kuja kwangu kumhudumia. Hakua na ndugu mwingine mjini wa kumsaidia kwani alishagombana na karibu kila ndugu. Nilikua najua kabisa kwua ujauzito si wangu lakini kwakua kitanda hakizai haramu niliamua kupotezea na kukubali kumlea mwanae kama wangu.
Siku ya kujifungua nilimpeleka mimi hospitalini na alifanikiwa kujifungua salaama. Hakusumbuka kabisa kwani nilimpeleka hospitalini kwenye saa nne asubuhi na ilipofika saa nane alijifungua. Yaani hakua na matatizo yoyote. Aliyeniambia kuhusu mmke wangu kujifungua alikua ni Mama yake mdogo, alinipigia simu nikiwa kazini kwenye saa nane na kuniambia kwua mke wangu kajifungua yeye na mtoto wapo salama.
Kusema kweli hakua ni mtoto wangu lakini nilijisikia vizuri, nilisikia raha hasa nikiona namna ambavyo mambo ya uzazi yanasumbua basi nilifurahi. Sikutaka hata kukaa ofisini muda huohuo niliwasha gari mpaka hospitalini kwani niliambiwa kutokana na hali yake basi anaruhusiwa siku hiyo hiyo. Kutokana na foleni nilifika pale hospitalini kwenye saa kumi hivi.
Nilimkuta Mama yake mdogo lakini nilipotaka kuingia kumuona mtoto aliniambia nisubiri kwanza.
“Kuna nini? Mbona uliniambia kuwa hali yake ni nzuri?” Nilimuuliza, aliniangalia kwa kucheka kisha akaniambia.
“Baba yake anamuangalia mtoto, subiri kwanza atoke, sitaki ije kuwashida hapa!” Nilijisikia kama kitu kinakata tumboni, kama mtu kachukua wembe na kunicha tumboni.
“Unasema nini?” Nilimuuliza kwa hasira.
“Baba yake yupo ndani anamuona mtoto wake!” Aliniambia na kuanza kucjeka, nilihisi kama vile ananikebehi, nilijisikia vibaya, nilitaka kuingia ili kuhakikisha lakini nilipogeuka kidogo nikaiona gari ambayo nilimnunulia mke wangu akaihonga ilikua pale. Nilishindwa kuvumilia na kuondoka, sikutaka kurudi nyumbani, nilikua na hasira zangu, bila kujijua nilijikuta nikienda kwenye ile Baa amabyo nilikunywa maji, nikafika na kuagiza Bia.
Wakati mhudumu ananiletea G, alikuja.
“Huyo hanywi pombe anakunywa maji?” aliichukua ile bia na kuirudisha,a kaniletea maji kisha kukaa pemebni yangu. Kutokana na jinsi tulivyoachana siku ile nilijua kama kanikasirikia lakini wapi.
“Mbona siku ile ulinikiambia na hujanitafuta tena?” Aliniuliza swai ambalo sikua na jibu lake. Nilimuomba tu msamaha na kumuambia kuwa sikufanya vizuri kumlipa kwakua yeye alikua kama rafiki uyangu na si Malaya!
“Bado unakumbuka tu hayo mambo, mimi nishasahau, vipi leo una jipya lipi jingine?”
Aliniuliza, lakini kabla ya kumjibu simu yangu iliita, alikua ni mke wangu, nilitaka nisipokee lakini nilijikuta tu napokea. Alianza kulalamika kuwa sijaenda kumchukua na kumuona mtoto wangu.
“Unaniacha hospitalini mimi mwenyewe, njoo unichukue basi!” Aliniambia, nilitamani kumuuliza kuhusu mwanaume wake lakini nilisita nikajikuta namuuliza kuhusu Mama yake mdogo.
“Tumegombana, kuna mambo kanifanyia sijayapenda, anaingilia sana maisha yangu.” Aliniambia.
“Mambo gani?” Nilimuuliza.
“Unajua, kuna vitu kavifanya, ni kama anataka tugombane kwani amesababisha umkute X wangu hapa na mimi sikutaka itokee hivyo. Najua umekasirika ndiyo maana umeondoka lakini msimi sikumuita ni Mama mdogo. Siku nyingi sana ananionea wivu, najua anakupenda na anataka tuachane ila nakuambia siwezi kumpa nafasi. Kwanini amuambie kuwa nimejifungua wakati anajua moja kwa moja kuwa wewe ndiyo umenileta!”
Aliongea kwa hasira, nilikua na hasira sala lakini baada ya kuniambia hivyo nilijisikia tofauti kabisa. Nilijisikia raha kuona kuwa kumbe mke wangu siye aliyemuite yule mwanaume. Niliacha kunyw amaji na kuondoka zangu, hata kulipa nilishaau nikaondoka mpaka hospitalini, nilimchukau mke wangu nakurudi nyumbani kwangu, njia nzima alikua analamika akimlalamikia Mama yake mdogo, nilimuambia asiwaze kwani mimi siwezi kumuacha kwakusikiliza maneno ya watu.
Tulifika nyumbani, mke wangu alikua analalamika sana kiasi niakereka na kuamua kumpigia Mama mdogo wangu. Nilianza kwa kuongeanikimlaumu kwa kumuita x wa mke wangi ili nimuone. Nilimlaumu na kumtukana sana nikamuambia aachane na familia yangu kwani maisha yatu hayamhusu. Hakuongea chochote mpaka nakata simu ndipo alinitumia meseji.
“Angalia kwenye pochi yake kubwa, kwa ndani kuna kazipu kadogo angalia hapo ksiha rudi nitukane tena.” Akiniambia, sikumjibu kitu lakini nilipata hamu ya kuangalia, wakati mke wangu kalala nilichukua pochi yake na kuangalia.
Mwanzo sikuona kitu, lakini niliposhika vizuri nilikuta kakaratasi kamefungwa, nilikafungua na kukutana na laini ya simu. Hapo nilishtuka kidogo, nikaichukua na kuiweka kwenye simu yangu kisha niakaiwasha. Hakukua na meseji mpya ila niliona meseji za zamani, ambazo mke wangu alituma kwenye namba moja tu, moja ambayo iliniumiza sana iliandikwa.
“Nimejifungua salama mpenzi, mwanao kazaliwa salama, Hope huyu utamkubali uje hata umuone, naumia sana ukiwa hujamuona mwanao mpaka amekua mkubwa, naomba uje umuone, hata kama hutaki kumlea, nitampa mume wangu yule atalea hana shida ila natamani umuone labda utanipenda kwa kukuzali mtoto wakiume ambaye mmefanana naye, labda yule mwingine hukumpenda kwakua ni wakike!”
MAMA MAGGIE; NAKUPENDA SANA ILA SHETANI AMEKUPENDA ZAIDI! —SEHEMU YA TISA
Niliumia mara mbili, maumivu ya kwanza ilikua ni kujua kuwa mke wangu alikua amemtaarifu X wake kuwa kajifungua. Alikua akinidanganya kuwa ni Mama yake mdogo alitaka kututenganisha kumbe ni yeye mwenywewe alifanya hivyo. Maumivu ya pili nikujua kuwa kuambe Maggie wangu ndiyo alikua si mwanangu. Nilikua nawapenda wanangu wote lakini kama unavyojua wanaume tunapenda zaidi watoto wakike na hivyo ndiyo ilikua kwangu.
“Nimekuzalia tena kwakua nakupenda, najua una hamu sana ya mtotyo wakiume kwakua mkeo naye huzaa wakike, hivyo nimekuletea dume. Naomba uje hata umuone, natamani tuishi pamoja lakini sijui kama kwa aliyokufanyia mume wangu utapata nafasi katika moyo wangu mpaka kunisamehe, nakupenda sana Kelvin wangu, nakupenda, sijui kwanini lakini maisha bila wewe si maisha, naomba uje kumuona mwanao, uje utoe jina.”
Nilitamani kuitoa hiyo laini katika simu yangu, nisisome tena meseji zake lakini sikuweza. Nilikua naumia sana lakini nililazimika kusoma meseji zake. Nyingi zilikua ni za mke wangu, kelvin hakujibu chochote zaidi ya matusi, usinisumbue na endelea na mbwa wako! mwisho niliitoa ile laini katika simu yangu, niliirudisha nilipokua nimeitoa na kupanda kitandani kulala.
“Acha kuingilia ndoa yangu, nimejua michezo yako na mambo unayotaka kunifanyia, sikuamini tena!” Nilimtumia meseji Mama mdogo, ingawa maelezo yake yalikua ni ya kweli lakini sikutaka mke wangu kujua kuwa nimesoma na kuujua ukweli. Bado nilikua sijaamua nifanye nini kutokana na zile taarifa hivyo sikutaka kukurupuka.
“Wakati napanda kitandani ili nilale mtoto alimka na kuanza kulia. Nilimsikia lakini sikutaka kufanya kitu chochote, nilijifanya nimelala mke wangu akaamka na kumnyonyesha, wakati anamnyonyesha aliniamsha.
“Hutaki kumuona mwanao akiamka, kidume chako hiki, hembu muangalie….” Aliongea hukua kijichekesha chekesha, nilijifanya nina usingizi sana na kulala, sikumjibu kitu chochote. Asubuhi niliamka sawa kabisa, ingawa nilikua na mambo mengi sana kcihwani kwangu lakini sikutaka yaharibu siku yangu, bado nilikua sijafanya maamuzi. Nilidhani nitasikia kitu chochote, labda nitajisikia vibaya nikiamka na kumuona Magge, mtoto ambaye nilipojua kuwa mtoto mmoja si wangu nilikua nikimuangalia Maggie kama tumefanana huku Jacob nikijaribu kumtafutia kasoro hata ya masikio ili yeye ndiyo asiwe wangu eti leo ndiyo si wangu.
“Maggie mwanangu, chochote kitakachotokea jua kuwa nakupenda!” Nilimuambia wakati namkumbatia, nilimkumbatia kwa nguvu huku nikimkagua kagua, nikimuangalia mwili mzima, masikio na kila kitu. Nilikua naangalia kama kile nilichokisoma ni kweli au ni maneno tu.
“Baba unakufa?” Aliniuliza, nilimuangalia kwa huzuni huku machozi yakinittoka na kumuambia hapana.
“Sasa mbona unaongea kama unakufa, unaumwa nini Baba, kama ni Figo mimi nitakupa yangu…” Aliniambia, Magggie alikua mjanja sana,a likua na akili na anajua mambo makubwa kuliko hata umri wake.
“Figo? Yanini, nani kakuambia hayo mambo?” Nilimuuliza huku nikilazimisha kucheka, sikutaka mwanangu kuhisi kitu chochote kibaya.
“Unaniangalia, unaonekana ulikua unalia, ni kama unaniaga Baba. Kwanini unaniambia kitu chochote kikitokea? Kwani kuna kitu gani kitatokea kibaya. Niliangalia kwenye TV wanasema mtoto anaweza kumpa Baba yake Figo, mimi Baba nitakupa yangu, nakupenda sana!”
Aliongea huku akitabasamu, uzalendo ulinishinda, machozi yalinitoka kama mtoto, aliniuliza nina tatizo gani lakini sikumuambia.
“Wewe ni mwanangu, hata itokee nini wewe ni mwanangu, nakupenda, siumwi Fiigo wala sitakufa karibuni ila jua wewe ni mwanangu na nakupenda.” Nilimuambia huku nikimkumbatia tena, nilinyanyua na kumuweka mavegani kisha niakaanza kuzunguka naye, nilijisikia vizuri sana nilijisikia raha ya ajabu kwani nilikua nampenda mwanangu kuliko maelezo.
****
Sikumuambia kitu chochote mke wangu, nilibaki kimya na kuamua kuwa kawaida. Lakini baada ya kama siki mbili hivi mke wangu alibadilika, alianza kuwa mtu wa hasira, visirani na kibaya zaidi akazishushia kwa mtoto. Kwanza kabisa aligoma kumnyonyesha, ingawa maziwa yalikua yanatoka kiasi kwamba yanamwagioka lakini mke wangu aligoma kabisa kumnyonyesha mtoto.
Kila nikimuuliza ananiambia kuwa yuko sawa na mtoto hatakiwi kunyonya sana, ananidanganya mtoto hapendi maziwa huku wakati mwingine akiniambia kuwa amechoka kunyonyesha anataka kupumzika. Pamoja na kuacha kumyonyesha lakini aligoma kabisa kumjali na kumhudumia, hata maziwa ya kopo aligoma kununua, nikawa nanunua mimi ila hata kumpa ikawa ni shida.
Wiki ya tatu alianza kwenda kazini, nilikasirika sana na sikumuelewa kwani alikua na miezi mitatu ya kupumzika lakini yeye aligoma kabisa na kusema kachoka kulea mtoto.
“Kwanza huyu mtoto nilikua simtaki niwewe ulikua umenilazimishia!” Alilalamika.
“Unamaanisha nini? Mbona unataka kunifanya mjinga naman hii?” Nilimuuliza, nahisi alishtuka akanyamaza.
“Nachoka tu kukaa nyumbani, nimechoka tu na haya maisha, sioni hata sababu ya kuishi. Namuonea huruma mwanangu ni mdogo sana, kuna wakati natamani hata afe kabisa ili asiteseke, siko tayari kuwa Mama kwasasa!” aliniambia baada ya kuona namuuliza uliza sana, kusema kweli maneno yake yaliniumiza lakini nilijikuta namuonea huruma mtoto ambaye nilijua kabisa kuwa si wangu.
Siku moja wakati amelala nilijikuta natamani kushika tena ile laini yake, niliangalia kwenye pochi yake na kuikuta. Nikagundua kuwa alikua akitembea nayo kila mahali, kila akbadilisha pochi basi anaichukua. Nilitaka kujua kama bado wanawasiliana na X wake na kweli nilikuata meseji za yule X wake.
“Ulizaa kwa mpango wako, nani alikuambia kuwa anataka mtoto wakiume, mimi sitaki kabisa kujihushsiha nawewe, uliniomba kuja kumuona mtoto nilikuja. Bianafsi nilidhani nitampenda, lakini nimeona kuwa mmeafanana sana, hata sijui kama ni wanmgu.
Mwanangu sitaki kuifanana na wewe kwani anaweza kuchukua mpaka akili za kijinga kama zako. Hii ni meseji ya mwisho, nimechoka na vitisho vyako, huyo si mwanangu, mbona huyo mjinga mjinga wako kamkubali. Mpe na sitaki ume jina langu! Achana na mimi mbona hunisikii!” Alimumia meseji moja ndefu.
Mke wangu yeye meseji zake ni nyingi.
“Kama humtaki na mimi simtaki, sijui kwanini lakini naona namchukia mtoto wetu, naona kama ni yeye ndiyo amechangia mimi kuwa hivi. Juzi nilikuja kwako, nikataka tufanye mapenzi, lakini ulinitukana vibaya, ukanidhalilisha, yaani kukupa zawadi ya mtoto ndiyo unenitukana hivi.
Najua mtoto kaniharibu lakini nitakua sawa kipenzi! Acha kunifanya kumchukia mtoto, utanifanya nitende dhambi, nahisi naweza hata kumuua!” Alimtumia, kumbe mke wangu baada ya kujifungua hata kabla ya kumaliza wiki mbili alimtafuta mwanaume, akaenda mpaka kwake na kutaka kufanya naye mapenzi.
“Kama unamuua muue, mimi simtaki na wewe si kutaki, niache na maisha yangu! huna akili kabisa, hivi unajiona jinsi ulivyochoka, hapana, utanitia dhambi bure lakini mimi sikutaki kabisa!” alimjibu, baada ya hapo hakumjibu tena lakini mke wangua lituma meseji nyingi sana zote akubembelezea mapenzi.
“Najua ni mchoka, ningejua kuwa hatutakua pamoja basi nisingezaa. Nimejitunza muda mrefu kwaajili yako lakini bado hunipendi. Najua uliumia nilipomzalia mume wangu, lakini kipindi kile nilikua na hasira, ulitembea na rafiki yangu, ukatembea na mtoto wa Baba mdogo, nilikasirika ndiyo nikaamua kubeba mimba nyake.
Najua mpaka leo hujanisamehe lakini nifanye nini, mbona nimekusikiliza, nimetoa mimba ngapi za mume wangu baada ya hapo ili tu kukuridhisha wewe. Mimi umri unaenda, nilitaka mtoto mwingine ndiyo maana nilibeba mimba na nilipokuambia ulikubali, sasa kwakua nimeza andiyo unabadilika. Nakuhakikishia nitarudi kawaida hivi karibuni, simnyonyeshi tena huyu mtoto, najau inauma ila nakuhitaji sana wewe nionee huruma, nakupenda sana.”
Hiyo ndiyo ilikua meseji ya mwishoa mbayo niliiona katika ile laini, niliitoa na kuirudisha. Nilijisikia hasira kuwa kumbe mambo yote hayo alikuasa nafanya kwaajili ya huyo mwanaume.
“Hivi kampa nini huyu mwanaume, mbona nampa kila kitu. Yaani mke wangu yuko tayari kuona mwanae anakufa kisa mwanaume?” nilijiuliza lakini sikupata majibu. Baada ya kuzisoma zile meseji nilijikuta nabadiliaka kabisa, nakua mtu mpya, nilianza kuelewa ni kwanini mke wangu anakua hivyo, niliona kuwa kama nikimuendekeza basi anaweza kuua watoto.
Kwasababu hiyo nilichukua jukumu la kumlea Sam, Samweli ndiyo jina ambalo mke wangu alimpa mtoto wake na nilipokuja kuchunguza hilo jina ni jina la Baba yake na Kelvin, ingawa nilikasirika lakini sikua na namna, niliona kabisa kuwa watoto hawatakiwi kuteseka kutokana na dhambi za wazazi wao. Nilianza kumnunulia maziwa ya kopo, Mama yake aligoma kabisa kumnyonyesha. Ingawa nilikua na mabinti wawili wa kazi mmoja kwaajilia ya mtoto tu na mwingine kwaajili ya kazi nyingine lakini bado sikua na amani.
Bado nilikua narudi kila siku mchana kuja kumuangalia mtoto, nilifanya hivyo huku mke wangu akibadilika mara kwa mara, kuna wakati anakua mkarimu, anawapenda na kuwahudumia watoto na kuna wakati anabadilika kabisa. Mama yake alishafariki hivyo Baba yake aligoma kabisa kubaki mjini na kurudi kijijini. Nilikua naongea na Baba yake mara kwa mara akiniuliza kuhusu wajukuu na mimi nilikua nikimjibu vizuri.
Mara k3wa mara nilikua naangalia laini ya mke wangu, mwisho niliona kama kakata tamaa kwani alikua akilalamika tu lakini hajibiwi kitu chochote. Mtoto alipofikisha miezi sita niliona mke wangu akirudi na kujaribu kumnyonyesha tena mtoto lakini maziwa hayakutoka na wala mtoto hakutaka kunynonya. Mtoto alinipenda mimi, yaani kama angekua mtu mzima basi ungesema kuwa kafundishwa lakini haikua hivyo, akibebwa na Mama yake analia, nikimpa maziwa mimi basi hunywa mpaka kushiba lakini si akifanya hivyo mke wangu.
Niliona mke wangu kabadilika, akawa ananishiriksiha katika mambo yake, kilakitu tukawa tunafanya pamoja, hakuniomba msamaha lakini nilijisikia vizuri. Pamoja na kuona mabadiliko lakini sikua na amani, nilikua namjua mke wangu, anaweza kuwa na furaha leo lakini kesho akawa na huzuni ya ajabu, sikutaka kukubali kirahisi kuwa mke wangu kabadilika tu. Nilianza kuchunguza sababu ya yeye kubadilika, nilikuja kugundua kuwa Kelvin alikua kaachana na mke wake lakini badala ya kumtafute yeye basia likua anaishi na mwanamke mwingine.
Tena si mwanamke tu alikua ni binti mdogo hivyo nilidhani mke wangua likubali matokeo kuwa ameachika. Ingawa haikua sababu nzuri ya mimi kurudiana na mke wangu lakini angalau ilikua ni sababu, sijui kwanini lakini nilijikuta nafurahia na kuona kuwa angalau sasa hivi mke wangu alikua kajitambua. Nilijaribu kuiangalia ile laini lakini sikuiona tena, hapo nilihisi kama mke wangu kakasirika na kuitupa na kweli kuna siku naangalia kwenye gari lake nakuta amekng’atang’ata ile laini hivyo nikawa na amani kuwa mke wangu kabadilika kabisasa.
Nilikua na furaha isiyo nakifani mpaka siku moja nilipokua nimekaa sebuleni nikaona meseji imeingia kwenye simu ya mke wangu.
“Nataka kuwachukua wanangu wote!”
MAMA MAGGIE; NAKUPENDA SANA ILA SHETANI AMEKUPENDA ZAIDI!—SEHEMU YA KUMI
Mke wangu aliiona ile meseji ila hakujua kama na mimi nimeiona, tulikua tumekaa sebuleni tunaangalia TV. Baada ya kuiona ile meseji nilimuona kama kachangayikiwa vile, alikua hakai na kutulia, baada ya muda aliaga anaenda jikoni, nilijua kabisa anaenda kuongea na mwanaume wake. Ingawa sikutaka kujua kilichokua kinaendelea lakini nilishindwa kuvumilia, nilimfuata mke wangu mpaka jikoni bila yeye kujua.
“Unamaanisha nini kusema unataka kuchukua watoto? Wewe si una mke wako, inamaana unataka kunichukua na mimi?” Mke wangua liuliza, sikusikia alichokuasa najibiwa upande wa pili lakini ilionyesh ani kama akakataliwa kwani alilalamika.
“Huwezi kuchukua watoto na kuniaha mimi, hivi unajua mume wangu hajui kiama Maggie si wake, anampenda sana, ukimchukua atachanganyikiwa, ataniacha, nakuambia hivii kama unataka kuchukua watoto basi jua mimi sitaki wanangu kulelewa na mama wa kambo!” Waligombana sana kwenye simu lakini mchepuko wake ulionekana kuwa umedhamiria kuchukua watoto.
Mke wangu alikasirika na kukata simu, mimi nilirudi sebuleni harakaharaka bila kusema kitu chochote. Alirudi akiwa hana amani, hataki kuongea na mtu, hata mtoto alipolia hakujali, nikalazimika mimi kumbembeleza.
“Una tatizo gani mke wangu, mbona uko hivyo, unaumwa?” Nilimuuliza baada ya kuamka usiku wa manane, m toto alikua analia lakini mke wangu alikua hata hajali. Nilinyanyuka mimi na kumbembeleza.
“Kwahiyo unataka niwe na matatizo, hivi wewe mwanaume una shida gani, kila ukiniona unaniwazia mambaya tu!” Alijibu kwa hasira.
“Basi yaache!” Nilimjibu huku nikinyanyuka na kuzunguka zunguka na mtoto.
“Kwanza nipe mwanangu, naona umekua na kiherehere sana, kama hunitaki hapa kwangu basi mimi naondoka, safari hii sitaki tena mambo ya kuondoka na kurudi nataka talaka. naona huwapendi wanangu si unatangaza huko mtaani kuwa si watotop wako, ushamuambia kila mtu kuwa nimekusaliti, sasa naondoka nao kama huwataki!”
Aliniambia, nisingekua najua kilichotokea ningeshangaa, lakini nilijua kabisa kwanini anafanya hivyo, nilijua anatafuta sababu ya sisi kutokua na maani. Nilipa mwane ili ambembeleze lakini hazikupita hata dakika tano, alishindwa, akamuacha kitandanio na kutoka zake, alienda kulala chumba cha wageni na kuniacha mimi na mtoto. Nilimbeleza mpaka akalala, nilijaribu kutafuta usingizi lakini sikuupata, bila kujijua nilijikuta nachukua simu yangu, nikamtafuta G, na kuanza kuchart naye, nilijikuta nachart mambo ya kawaida mpaka nikapatwa na usingizi.
Asubuhi mke wangu alikuja chumbani, aliniomba msamaha kwa kunijibu vibaya lakini mimi hata sikujali. Baada ya kuchart na G, nilikua na amani sana, nilikua najisikia vizuri hivyo kisirani chake hakikunisumbua kabisa.
“Leo nitachelewa kurudi, kuna sehemu napitia.” Aliniambia, nilimjibu tu sawa kwani nilishaanza kuchoka mambo yake, mke wangu hakua mtu wa kuniaga, alikua ni mtu wa amri na kunipangia maisha. Kweli siku hiyo alichelewa kurudi, si kidogo bali alirudi usiku wa manane, kwenye saa tisa hivi. Alikua kalewa sana na kwa kumuangalia alikua ana maalama mengi usoni kama vile katoka kupigana, nilipandwa na hasira na kujaribu kumfokea lakini nilimuona analia.
Alikua akilia si kilio cha kawaida bali kilio cha uchungu, ni kama kuna vitu vilikua vinamuumiza, nilimuuliza nini kimetokea aligoma kuniambia akwa analia tu. Hali ile iliniumiza sana, nilijikuta namuonea huruma, sikumuambia kitu lakini nilitamani kumsiadia.
“Hivi mtu utampendaje mwanaume namna hii, anakufanyia vituko lakini bado unampenda!?” Nilijiuliza lakini sikupata jibu, mke wangu alikua kalewa sana hivyo alipopanda kitandani hakuchukua muda kulala. Nilichukua simu yake kuangalia, ingawa namba haikua imeseviwa ila moja kwa moja nilijua kuwa ni Kelvin alikua anchart naye.
“Hivi kwanini hunipendi, nimekukosea nini? Huyo mwanamke wako ana kitu gani cha ziada!?” mke wangu aliuliza lakini hakujibiwa. Mwanzo nilidhani labda mke wangu alikua na Kelvin na yeye ndiyo alimpiga. Lakini kwa kusoma zile SMS niliona kuwa mke wangu alitoka mwenyewe kwa malengo kuwa Kelvin atamfuata lakini haikua hivyo. Aliendelea kutuma meseji kuomba aje lakini hakuja.
“Nimekuambia nataka wanangu sijakuambia nakutaka wewe, kama unataka nisiwachukue basi fanya kitu.” Baada ya meseji nyingi Kelvin naye alimtumia meseji.
“Unamaanisha nini?” Mke wangu alimuuliza.
“Namaanisha kuwa, yule boya wako anakupenda sana, lakini najua anawapenda watoto wake sana hasa Maggie ambaye anahdani kuwa ni wake kumbe ni wangu. Sasa ninachotaka ni hiki, mimi nataka kubadilisha gari, ninunulie Crown mpya nitakuacha wewe na mume wako muwe salama.” Alimuambia.
“Lakini mimi sitaki kuachana na wewe Kelvin, nakupenda na nipo tayari kuachana na mume wangu kwaajili yako, wewe niambie tu, mbona hutaki kunielewa!”
Meseji hiyo haikujibi3wa pamoja na mke wangu kutuma meseji nyingi sana kwake. Niliumia sana lakini sikufanya chochote, nilichofanya nikuchukua namba ya Kelvin na kusave kwenye simu yangu.
“Lazima niyamalize haya mambo, siwezi kuvunja familia yangu na kudhalilika kwaajili ya huyu mtu! Hapana! Hapana!” niliwaza, susiku huo sikufanya kitu chochote, lakini kesho yake nilimpigia simu Kelvin, nilijitambulisha kama nimteja nilikua nahitaji kununua gari, nilimuambia nimepewa namba na dalali wake. Nilifanya hivyo kwakua kwenye moja ye meseji zake kuna sehemu alisema kabisa kuwa anauza gari yangu ambayo alipewa na mke wangu.
Alikubali kuonana na mimi, hakua akijua sauti yangu vizuri, nilipanga kuonana naye sehemu na nilimuacha akatangulia kufika, niligika na kumkuta amekaa anamsubiria mteja, nilienda na kukaa kiti cha pembeni. Baada ya kuniona alishtuka.
“Broo, mimi nilishamalizana na wewe, naomba uondoke, nipo kibiashara, sihitaji ugomvi!” Aliniambia.
“Sikuja kwaajili ya ugomvi bali nimekuja ili kuyajena, nampenda sana mke wangu ila naona unataka kuniharibia ndoa yangu.”
Alianza kujitetea akiniambia kuwa alishaachana na mke wangu hivyo nisimsumbue kwani hahitaji tena kugombana na mimi.
“Najua hujaachana naye, jana tu umemtumia meseji, nahisi pia umempiga tena, hivi wewe ni mwanaume wa namna gani?”
“Hapana, yeye ndiyo alikua ananitumia meseji, mimi nilimjibu vile ili aniache, nikuambie ukweli mimi simhitaji kabisa mke wako. kuhusu kumpiga sio mimi, alipigana na mhudumu wa baa amabye alihisi anatembea na mimi, niliyasikia haya mambo lakini mimi sikuhusika. Broo, sasa hivi nina maisha yangu, nina mke wangu na nina familia yangu, mke wako ndiyo ananisumbua, mimi si mtaki.
“Vipi kuhusu kuwachukua wanangu na kutaka kununuliwa gari?” Nilimuuliza, alionekana kushtuka,s mi kitu ambacho alikitegemea, lakini alionekana kuniogopa zaidi.
“Mimi sina mtoto na mke wako, mimi nilikua namtania, tu, nilijua nikimuomba gari hawezi kukubali na tunaachana moja kwa moja, niamini nikikuambia kuwa mimi na mke wako tumeshamalizana, naomba niamini, mimi sina mpango tena na mke wako.”
Alijitetea sana lakini nilijua kuwa ni uongo, nilimuambia kuwa sitaki aendelee kuwasiliana na mke wangu.
“Niambie unataka nini ili usiwasiliane na mke wangu, niambie maana nimechoka hii hali ki8la siku. Najua wale watoto ni wako, lakini Maggie nimemlea mimi kama mwanangu, nampenda, siwezi kumuacha aondoke, siwezi kumuacha akateseke, najua humpendi na unachotaka ni kumtumia mke wangu ili kupata mali. Sasa unamchanganya sana mke wangu, hivyo naomba niambie unataka nini na mimi nitakupa.
Niambie unataka shilingi ngapi ili kuwa mbali kabisa na mke wangu. Nakuahidi nitakupa lakini uniachie wanangu na uniachie familia yangu!” baada ya kumuambia vile niliona kama anabadilika, mwanzo alionekana muoga flani, ila nilipotaja mambo ya pesa niliona anacheka na kujitingisha tingisha kwa dharau.
“Unataka unipa pesa? Unadhani mimi nanunulika?” ASliniuliza kwa dharau.
“Najua unanunulika, niambie unataka kiasi gani?”
“Kweli niuze damu nyangu kwaajili ya pesa….” Alijifanya anafikiria sana kisha akanyanyuka na kutaka kuondoka, nilimfuata lakini alinisukuma pembeni.
“Nawataka wanangu, kumbe na wewe unawahitaji, umenidharau kutaka kununua wanangu, nakuambia nataka wanangu na nitahakikisha kuwa nitawapata!”
Aliongea kwa hasira na kuondoka, nilijisikia vibaya kwani nilihisi nimetibua mambo, mwanzo alishakubali kuachana kabisa na mke wangu, lakini nilipomtajia pesa alionekana kama anawahitaji watoto.
“Najua anataka kunisumbua lakini nitampata tu, nitachukua wanangu nayeye atabaki na pesa hawa watu nawajua!” niliondoka na kurudi nyumbani, nilimkuta mke wangu kakasirika, kafura, hakuniambia chochote lakini nilihisi labda tayari kashaongea na mchepuko wake.
Hakuniongelesha kwa hasira na mimi sikutaka kuongea naye, saa nne usiku nilitoka nyumbani na kwenda Baa kwa G, nilimkuta nikaagiza bia tukaanza kunywa naye na kuanza kuongea. Mpaka nafika bia ya sita nikawa nimeshamuelezea kila kitu katika maisha yangu, ilikua ni mara yangu ya kwanza kufunguka kwake namna hiyo. Mara nyingi nilikua namuambia kuhusu mambo yangu lakini si kila kitu.
“Unajua ni kwanini wanakuchezea?” Aliniuliza.
“Hapana, labda nikwakua nampenda mke wangu sana, nampenda nashindwa kumuacha, yaani kila nikifikiria kuhusu familia yangu naona siwezi kuishi bila mke wangu.” Nilimuambia.
“Nipe simu yako.” Aliniambia, siokujua anataka kuifanya nini lakini aliichukua na kuandika meseji.
“Si unasema anaitwa Kelvin?” Aliniuliza.
“Ndiyo uanataka kufanya nini?” niliuliza kwa wasiwasi huku nikitaka kumnyang’anya simu lakini alishatuma ile meseji. Niliichukua na kuisoma.
“Nimekaa nimefikiria nimeona siwezi kulea Ngedere wa watu, naomba kesho uje kuchukua mbwa wako kwangu, la sivyo nitavichoma moto vile vitakataka vyako!” Niliisoma ile meseji.
“Umefanya nini? Hivi unajua kuwa wale ni wanangu!” Nilimuuliza kwa hasira huku nikitaka kumpiga. Lakini yeye hakujali, alicheka na kuniambia.
“Nilikua nakufanya mwanaume, huyo mbwa hamtaki mtoto lakini kwakua unamgombania basi anatumia udhaifu wako kukunyanyasa. Hivyo hivyo kwa mke wako, anakusumbua kwakua unampenda, anajua kuwa huwezi kumuacha, ninachokuambia nikuwa, sasa hivi badilika, ukitaka mke wako kubadilika basi badilika wewe na kuwa mwanaume ndani ya nyumba!”
Aliniambia, nilishindwa kumuelewa, lakini baada ya kama dakika kumi hivi nilipokea meseji kutoka kwa mke wangu. Alikua kanifowardia meseji niliyokua nimemtumia Kelvin kisha akamalizia.
“Naona unaniutafuta, unawaita watoto wangu ndedere, nakuambia ukirudi basi hakikisha kuwa unakuja na talaka yangu!” Mke wangu alionekana kuwa na hasira sana, kusema kweli niliogopa na kuanza kutetemeka, sijui kwanini ila nilikua namuogopa mke wangu kupita maelezo, nilikua kama nimetishiwa kitu.
“Umefanya nini lakini wewe?” Nilimuuliza G, ambaye alicheka na kuninyang’amya simu kisha kajibu meseji.
“Malaya mkubwa wewe, nikirudi uwe umeshakusanya hao mbuzi wako na kuondoka nao. Hao wawili nina uhakika si wangu, huyo Jacob tutapima DNA na kama si wangu simtaki!” Aliituma ile meseji, niliogopa sana lakini aliniambia nimuache atamalizana na mke wangu. Kama dakika mbili tu baada ya ile mseji mke wangu alipiga simu, niliipokea lakini kabla ya kuongea G, alininyang’anya simu na kuongea naye.
“Wewe ni nani unampigai mume wangu simu usiku namna hii?” Alimuuliza, mke wangu alikata simu kwa hasira lakini baada ya kamda kika tano tu alipiga simu.
“Dada ushaambiwa kuwa hutakiwi, kusanya vitu vyako na mbwa wako kisha ondoka, nakuja mimi Mama mwenye nyumba, wewe si ulishaichezea nafasi….” Walitukanana sana, G, alikua anatukana kupita maelezo, mke wangu yalimshinda, akakata simu. Nilikua na hofu sana ya kutaka kurudi nyumbani.
“Wewe ulivyo mjinga ukienda utaenda kuomba msamaha, huyo mke wako unatakiwa kumfundisha adabu, kama unataka abadilika basi niachie mimi hii kazi. Mwanaume mzuri namna hii unasumbuliwa na mwanamke! Kibiriti ngoma hicho, leo unaenda kulala kwangu!” Aliniambia kama ananiamrisha.
“Vipi kuhusu wanangu watasemaje?” Nilimuuliza, aliniangalia na kucheka.
“Wanao watasemaje kuhusu nini? Mbona unanishangaza, hivi unafikiri wanao wanaweza kusema kitu. Wale ni watoto tu, kazi yao kula, kunya na kusoma, suala la Babamkarudi au hajaudi haliwahusu, wakipiga kelele sana tandika makofi mawili watakaa kimya!”
Nilibaki kimya na kumsikiliza kama mtoto mdogo, siku hiyo sikurudi kwangu, usiku mzima mke wangu hakunitafuta kitu ambacho kilizidi kuniumiza. Asubuhi aliniambia niende nyumbani, lakini nisikae bali nichukue nguo zangu na kuondoka, nilifanya hivyo, aliniambia nirudi wakati mke wangu yuko kazini ili tusionane kwani nitanywea. Aliniambia mke wangu anatakiwa kupata taarifa tu kwa binti wa kazi kuwa Baba alikuja.
Nilifanya hivyo na kweli mke wangu alijua kuwa nimerudi kuchukua nguo na baadhi ya vitu vya kazini na kuondoka. Jioni mke wangu alinitafua na kuniambia kuwa anataka kuongea na mimi, nilimuambia hapana, nimeshafanya maamuazi kuwa simhitaji yeye na watoto wake hivyo awapeleke kwa Baba yao.
“Nina mtoto mmoja hapo mabaye nahisi ni wangu hivyo ukiwaondoa hao wengine mimi nitakuja, nimechoka na ujinga wako, si ulitaka kuniacha basi niache!” Nilimuambia, hayakua maneno yangu bali ni maneno ambayo nilifundishwa na G, alikua mtoto mdogo lakini alijua kila kitu.
Siku ya tatu nilienda nyumbani, watoto walinikimbilia lakini sikuwahali, nilikua bize zaidi na Jacob na sikujali kuhusu Maggie wala Sam ambaye naye alinililia. Mke wangu aliona na ilimuumiza sana, hata mimi iliniumiza, nilijisikia vibaya kwakua nilijua watoto hawajakosa kitu ila kwa maelezo ya G, ambaye alikua ndiyo Mwalimu wangu ilikua ni lazima kufanya hivyo.
“Mbona umekua hivyo mume wangu, kwanini unanifanyia hivyo, hawa watoto wana kosa gani?” Aliniuliza.
“Unakumbuka ile gari ambayo nilikupa kipindi kile ukaniambia umeiuza?” Badala ya kumjibu kuhusiana na watoto nilimuuliza kuhusu gari yangu. ule gari nilimpa mke wangu na ilikua na jina lake tayari, nilimuambia kuwa naihitaji.
“Mbona nilishaiuza, si ulinipa mimi lakini?” aliniambia.
“Hapana, hukuiuza, ulimpa hawara yako, nimesharipoti POlisi kuwa gari ya mke wangu imeibiwa, najua hukubadilisha kadi baso inasoma jina lako. Sasa ninachotaka ni hivi, jamaa yako akikamatwa basi utasema kweli imeibiwa, umenisikia?” Nilimuuliza kwa hasira.
“Sasa ufanye ujinga na useme kuwa ni yako ulitoa zawadi ndiyo utanijua mimi ni nani?” Mke wangu aliniangalia kwa mshangao sana. Hakuamini kuwa huyu alikua ni yule mwanaume aliyekua akimsumbua kila siku.
Mke wangu alikua na kadi zangu zote za Benki, alikua akitumia anavyotaka na nilikua nikimsikiliza kwa kila kitu. Nilichukua mikoba yake na kuzichukua, kisha nikafungua kabati na kutoa nyaraka zote za mali zangi, alishangaa na kuniuliza kwanini?
“Wakati natauta mali zangu wewe ulikua bize kuhonga pesa zako, sasa nakuambia kuwa, tunapeana talaka na hutachukua hata kijiko amabcho nimenunua kwa pesa yangu, ulichonunua wewe utachukua lakini si nilichonunua mimi!” nilimuambia kwa hasira.
MAMA MAGGIE; NAKUPENDA SANA ILA SHETANI AMEKUPENDA ZAIDI!—SEHEMU YA KUMI NA MOJA
Sijui nini kilitokea lakini nilianza kujihisi raha kuchepuka, G, alikua mdogo sana kwangu lakini alikua na akili ya mapenzi kuliko hata mke wangu. Sikutaka tena kurudi nyumbani, muda mwingi nilikua nautumia kwake.
“Nataka uhame hapa, haka kachumba kadogo sana, naaka nikutafutie nyumba kubwa na ile kazi nataka uache.” Nilimuambia G usiku mmoja. Nilikua na siki mbili sijarudi nyumbani, mke wangu alikua ananipigia simu kuniulizia lakini nilikua namjibu hovyo.
“Kuhama kwenda kupanga hapana, kama unataka nihame unisaidie kumalizia nyumba yangu, nina kiwanja changu kiko Goba, nimejitahidi nyumba ipo kwenye lenta, kama utakua tayari poa lakini mambo ya kunihamisha halafu naenda tena kupanga siwezi.” Aliniambia na alionyesha kumaanisha, kwangu hilo halikua tatizo, nilikua na pesa shida ilikua ni mtu wa kutumia naye. nilienda kuona kiwanja chake, kiwanja kilikua kikubwa tena sana lakini yeye alijenga vyumba viwili tu.
Nilimuambia ile ramani si nzuri, nikatafuta mafundi wakabomoa na kuanza upya nyumba kubwa.
“Nataka unizalie, mtoto ambaye nina uhakika kuwa ni wangu ili aishi hapa kwangu!” Nilimuambia, kusema kweli nilishaqanza kuchanganyikiwa kwake, nilishakinahi kabisa mambo ya mke wangu hivyo hata watoto sikuwaona wangu, ingawa Jacob nilikua namuona kama mwanangu lakini naye upendo ulipungua kwakua tu alizaliwa na mke wangu.
“Hakuna shida, kama ni mambo ya kuzaa nitakuzalia, lakini niwe na uhakika wa maisha, mimi niliacha shule, lakini nilikua na akili sana, nahitaji kurudi chuo, nahitaji kuwa na maisha yangu. kazi nimekubali kuacha lakini siwezi kuwa mama wa nyumbani, kuna leo na kesho, sasa hivi unanipenda, upo, siku ukiniacha na kurudi kwa mke wako unafikiri itakuaje?” Aliniuliza, nilimuahidi kuwa siwezi kumuacha lakini yeye alisisitiza kuwa anahitaji kusoma, tayari nilishabeba jukumu la kuhudumia familia yake na kusomesha waodgo zangu, nyumbani kwangu nilisahau kabisa.
Niliacha kutoa matumizi kwakua nilikua sikai sana nyumbani, sikua nailipa bili ya umeme wala maji, niliacha kutoa hela ya chakula, mke wangu alikua akilalamika lakini sikujali, nijiona mjinga kuhudumia watoto wa mwanaume mwingine huku mke wangu akiwa hana shukurani.
“Unajua mshahara wangu nilikopea, sina pesa, hutoi chochote hapa nyumbani, Maggie umegoma kumlipia ada, umelipa ada ya mtoto wako, tu, pesa ya chakula hutoi hivi mume wangu unafikiri tutaishije, watoto unajua wanakula nini?”
Siku moja mke wangu alinilalamikia, nilikua nimerudi nyumbani kubadilisha nguo. Nilimuangalia kwa dharau kisha nikatema mate chini.
“Una akili kweli wewe mwanamke? Hivi unataka nihudumie watoto ambao najua kabisa sio wangu, au unadhani mimi ni mjinga kiasi hicho? Ulivyokua unambembeleza mwanaume wakoa kuchukue wewe na wtaoto uliona kama mimi nitavumilai siku zote, ninaujua ukweli, Maggie na sam si wangu, mwanangu pekee hapa ni Jacob naye sina uhakika sana ila nitamhudumia mpaka tutakapopima DNA!” Nilimuambia, alikosa pozi hata la kuendelea kuniulizia.
Tangu kumuoa mke wangu alikua hajui majukumu ni nini? Alikua hajui kununua chakula, kulipa bili ya maji wala umeme, alikua hajui cha nguop za watoto wala ada, kila kitu nilikua nafanya mwenyewe na pesa yake iliishia kuhudumia ndugu zake na mambo madogo maodgo basi. Ilikua ni mara yake ya kwanza kubeba majukumu yote ndani ya nyumba, ingawa mwanzo alikua anasaidiasaidia lakini sikumlazimisha na wala nilikua simuulizi kitu chochote.
Najua nilikosea lakini kwanini unawaadhibu watoto, unasema unahudumia Jacob kwakua ni mwanao, lakini hulipi umeme, hununui chakula, hufanyi chcochote, hivi kweli….” Niliona kama ananipigia kelele, nilishamaliza kcuhukua nguo zangu hivyo nilitoka na kumuacha akiongea, alilalamika sana na kupiga kelele ila sikujali.
“Kama unaona sawa basi njoo umchukue huyo mtoto unayesema ni wako! si umeamua kuniacha, niache basi na maisha yangu kwanini unarudi kubadilisha nguo hapa!” Aliongea, sikumsikiliza, sikujali akili yangu haikua hapo kabisa.
Nilirudi nyumbani nilipokua nikiishi na G, nilikua na hasra pamoja na mawazo, kidogo nilijisikia vibaya kwani wakati natoka Maggie alinisalimia na kuniomba nikae aniambie mambo ya shule lakini sikutaka kukaa. Ingawa nilikua na hasira sana na Mama yake lakini bado nilikua nampenda nikimuona kama mwanangu hivyo nilijisikia vibaya. G aliniuliza kama nina tatizo gani nikaamua kumuambia.
“Najisikia vibaya kuhusu wanangu?” Nilimuambia.
“Wanao akina nani? Una mtoto mmoja na mwingine wapili naenda kukuzalia, sasa kwanini kuwaza….” Aliniambia, nilishtuka kwani aliniambia kuwa kuna mtoto wapili anakuja.
“Unamaanisha nini? Inamaana unasema unaujauzito?” Nilimuuliza huku nikishika tumbo lake, alijibu kwa kichwa kuonyesha kuwa alikua anakubaliana na mimi, nilijisikia vizuri sana, nilimnyanyua juujuu na kumkumbatia kwa nguvu sana, furaha niliyokua nayo haikua na kifani.
Nilihisi huo ndiyo ulikua wakati wangu wa kuwa na furaha, siku iliyofuata nilienda shuleni kwakina Jacob na kumhamishia bweni, hakutaka lakini niliamua kujiweka mbali kabisa na mke wangu.
“Kama ishu ni matumizi absi namtoa mtoto wangu, atakaa bweni na akitoka nitaishi naye mimi!” nilijiambia, mke wangu hakukubali lakini hakua na namna. Nilishaamua kila kitu sikutaka ushauri wa mtu yoyote yule.
Hali ya mke wangu kiuchumi ilikua mbaya, kuna aina flani ya maisha ambayo aliyazoea yaliyeyuka kabisa, alianza kuwa mtu wa madani, kila wakati kusumbua marafiki zangu kulalamika kuwa mimi simhudumii lakini mimi sikujali, sikumuambia mtu yoyote kuhusiana na sababu za mimi kumuacha ila sikurudi pia.
Nilimaliza kumjengea G, tukahamia, mimba ilikua kubwa, sikuficha tena kuhusiana na mahusiano yangu, kila mtu alijua, watu wengi walikua hawafahamu manyanyaso aliyokua ananipa mke wangu hivyo walimuonea huruma na kunishurumu mimi ila sikujali.
“Baba unakuja lini?” Siku moja Maggie alinipigia simu, ilikua ni siku ya shule lakini hakwenda,a litumia simu ya binti wa kazi ambaye naye sikua nikimfahamu. Sauti ya Maggie ilinichanganya sana, ni mara nyingi nilikua namkumbuka lakini kila nikifikiria kuwa si Mwanangu basi nilijisikia vibaya na sikumtafuta.
Baada ya kumchukua Jachob nilishakata mguu kabisa kwenda nyumbani kwangu, sikutaka kwenda kwakua nilihofia kumuonea huruma, namna alivyokua ananipenda nilijisikia vibaya ingawa kila siku nilikua nikijiambia kuwa sio kosa langu ni kos ala Mama yake.
“Nitakuja mwanangu, niko safarini…” Nilimjibu kwa mkato na kutaka kukata simu lakini aliniwahi.
“Hapana Baba, najuas haupo safarini, upo hapa mjini, najua kila kitu Baba, najua mimi si mtoto wako lakini mimi nakupenda, wewe ndiyo Baba yangu sio yule mwingine.” Aliniambia huku akilia, nilishikwa na uchungu kiasi nikashindwa hata kukata simu.
“Baba kwani nilishawahi kukukosa kitu? Kwani mimi ni mtoto mbaya?” Aliniuliza, nmachozi yalianza kunitoka, nilishindwa kujizuia kabisa.
“Hapana!” nilimujibu.
“Basi Baba kwanini umeniacha, hata kama mimi si mwanao, mimi nina kosa gani Bbaa. Mama hanipendi, amenipelejka kwa huyo Baba mwingine, ananiambia ndiyo Baba yangu, Baba mimi nimeteseka sana, nimetoroka kule, naomba uje kunichukua la sivyo nitakufa!”
Aliniambia, ingawa kuna wakati mke wangua likua akinitishia kuwa kama nisipomhudumia atampeleka Maggie kwa Baba yake lakini sikutilia maanani. Nilijua ananitishia kwakua anajau nampenda sana Maggie hivyo nikisikia anampeleka kwa Kelvin basi nitamuonea huruma. Niliongea na G, akaniambia kuwa huyo ni mtoto wake ana maamuzi naye, nimpe nafasi ampeleke kwa Baba yake. Ingawa sikutaka lakini nilimjibu kuwa utajua mwenyewe ni mwanao sikukusaidia kuzaa. Sikujua kama mke wangu ni mjinga kiasi hicho kiasi cha kumpeleka mtoto kwa huyo mwanaume.
“Baba kule tunakula mara moja tu kw3 aiskju, halafu Baba mimi ni mtoto wakike, lakini nalala na watoto wengine wakubwa wkaiume, wananifanya kila mmoja, nikimuambia huyo Baba mwingine basi anaishia kunipiga. Nikimuambia Mama ananipiga na kunikasirikia, Mama anasema mimi ndiyo nimemharibia maisha yake. Baba mimi nimeharibuje, siendi shule, sipewi chakula lakini nafanyishwa kazi nyingi, naomba nisaidie baba. Hata kama wewe si Baba yangu lakini nisiadie nipeleke hata nikakae shule nikwia mkubwa nitakulipa.”
Alikua bado mtoto lakini alikua amejipanga, aliongea kwa uchungu sana, nilijisikia vibaya na kujiona kama mnyama.
“Hivi mimi ni mtu wa namna gani? Yaani kweli ujinga wa mke wangu ndiyo unanifanya kumtelekeza mtoto!?” Nilijiuliza bila kupata majibu, sikuweza tena kuendelea na kazi, niliingia kwenye gari mpaka nyumbani. Kufika tu nikakutana na Maggie getini, ni kama laikua anajua kuwa nitaenda alikua ananisubiria, kwa kumuangalia alikua kachoka sana, alikua kama ombaomba.
Alinikimbilia na kunikumbatia, alilia kifuani kwangu mpaka akazimia. Nilijaribu kumpepepea lakini hakunyanyuka hivyo nikalazimika kumpeleka hospitalini. Alitundikiwa maji na baada ya vipimo iligundukulika kuwa alikua akibakwa. Nilishawahi kusalitiwa, nilishawahi kuingia kwye maumivu lakini katika maisha yangu hakuna maumivu ambayo niluiyapata kama siku ile, nilitoka nnje ya hospitali nikaingia kwenye gari, nililia kwa zaidi ya nusu saa kama mtoto. Nilijisikia vibaya, nilijiona muuaji, yaani kila kitu cha kujisikia vibaya kilikuja.
Picha ya Mama yangu ilikua haiondoki kichwani kwangu.
“Umefanya nini? Umefanya nini? Unamuua mwanao? Unamuua mwanao?” Nilimuona Mama ananiuliza bila majibu. Nilirudi wodini na kumkuta Maggie kashaamka, aliniomba nikae pembeni yake na kumshika mkono, nilikaa nikajikuta nalia, bila kutaka.
“Baba kama kuna kitu nimekukosea nismaehe. Nimechoka kuteseka, Mama ananipiga kila siku ananiambia kuwa mimi ndiyo nilimharibia usichana wake, nilimharibia ndoa nyake, nisingezaliwa yeye angekua na mani….” Alianza kujielezea lakini nilimkatisha.
“Hapana, hujanikosea kitu, nisamehe mimi mwanangu, hutateseka tena, nakuambia hutateseka tena….” Nilimuambia lakini niliona kama aitaka kuongea, alikua na mambo mengi ya kuongea. Mke wangu baada ya mimi kuondoka alihamia kwenye pombe, akawa yeye ni mtu wa kunywa kila siku. Akirudi nyumbani yeye ni hasira, anatukana na kuwapiga, mwanzo walikua wakifarijiana kwakua alikuepo Jacob lakini baada ya mimi kumchukua basi alibaki peke yake, hivyo kila kitu akawa anafanyiwa yeye na hakua na mtu wakulia naye.
“Dada naye aliondoka, kuna siku Mama alikuja na mwanaume nyumbani, basi alipokujja huyo mwanaume akamtaka Dada, mama akakasirika akamgukuza, ndipo akaleta dada mwingine naye akaondoka, na mwingine naye akaondoka. Mwisho akasema mimi ndiyo namnyima raha, akaniambia ananipeleka kwa Bbaa yangu, basi mimi nikafurahi nikajua kuwa ananileta kwako, lakiki haikua hivyo. Akanipeleka kwa huyo Baba mwingine na kuniambia kuwa ndiyo Baba yangu, kwanza alikua hanitaki, wakagombana sana lakini Mama aliniacha hapo nnje na kuondoka zake.
Huyo Baba ana mke wake, anaishi na wadogo zake pia, nyumba n indigo tena sana hivyo tunaishia kubanana banana, mimji nikawa nalala na wadogo zake wawili wakiume na mkaka mwingine rafiki yao hao wadogo zake, yeye ndiyo alianza kunifanyia kisha akawaambia na wenzake wakawa wananifanyia huku wakinitishia kuniua. Nikamuambia huyo Baba lakini hakujali, alimpigia simu Mama kuwa mimi nimuongo nataka kuwafunga ndugu zake aje kunichukua.
Mama alikuja, badala ya kunisikiliza alinipiga sana na kuniambia kuwa nivumilie la sivyo nitakua mtoto wa mtaani. Nikakaa nikchoka na kuamua kutoroka kurudi nyumbani, niliporudi ndiyo nikamuomba dada mwinginesimu na kuamua kukutafuta, Mama aliniambia nisikutafute lakini nimechoka. Baba nisamehe, naomba unichukue, najua mimi si mwanao lakini nikiwa mkubwa nitafanya kazi, mimi nina akili. Nitasoma sana nitapoata kazi nzuri nikipata kazi Baba nitakulipa pesa yako yote, nisaidie maama Mama yangu hajali.”
“Utakua salama kwangu mwanangu, huna haja ya kunilipa, nilikutelekeza, nisamehe wewe, haitajirudia tena!” Nilimuambia, alitingisha kichwa kuonyesha kafurahia ingawa niliona kabisa kuwa hana furaha, alikua na wasiwasi kidogo. Nilitoka nnje na kumpigia simu Mama yake, nilimuambia kuwa nataka kuonana naye kwani kuna mambo ya kuongea sisi wawili ambayo hayatafaa kama yakiongelewa kwenye simu.
“Nimeshachukua RB yako, umemtorosha mtoto na nakuambia huyo mtoito si wako, si ulishamkataa sasa ndiyo nini kuja kumchukua bila idhini yangu. Baba yake anamtaka!” mke wangu alinijibu kwa hasira, jkwani alisharudi nyumbani na kuambiwa nimemchukua mtoto akaongea na Baba yake na wote walikua wanamtaka.
Kuna matapeli wengi wanatumia jina la Iddi makengo. Kua makini sana nao, hakikisha unaponunua Kitabu basi jina linakuja IDDI MAKENGO na nina namba mbili tu za kulipia. M-Pesa 0742-381-155 na Tigo Pesa 0657-552-222 hakuna jina lingine sijui wakala au nani.
Unadhani Mama Maggie amechukua RB kweli? Unadhani Jamaa ataruhusu Maggie kuchukuliwa? Nisikuchoshe, nikuambie tu kaa kwa kusubiri kujua Hatma ya Maggie na mimba ya G.
MAMA MAGGIE; NAKUPENDA SANA ILA SHETANI AMEKUPENDA ZAIDI! —SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Nilimsikiliza mke wangu kwa makini akibwabwaja, kuna sauri flani huwa nikiongea na mke wangu anahisi kama vile namuomba msamaha hivyo hutaka kuniendesha na kunikalia kichwani.
“Una akili wewe mbwa!?” Nilimuuliza mke wangu kwa hasira, ghafla alinyamaza na kuacha kuongea.
“Hivi nakuambia kuhusu mambo aliyofanyiwa mtoto wako halafu unaongea upuuzi wa kumtorosha mtoto? Unaongelea mambo ya RB? Nadhani ulikua huniujui! Maggie anaweza asiwe mwanangu lakini nilimlea mimi? Nilimuogesha mimi, nilikua naamka usiku kumbembeleza, nilifanya ujinga sana kumuacha Maggie kwako nikijua kuwa wewe si mwanamke ni mpumbavu, sasa nakuambia si umechukua RB, unataka kuniitia polisi?
Basi nikupe taarifa wewe na huyo mpimbavu wako, nitawafunga wote, hao ndugu zake na kila mtu aliyehusika katika ujinga huu nitamfunga! Siulikua unaniona mpole, ulikua unaniona mjinga sasa kaa kwakutulia kwakua nitatumia kila shilingi yangu kuhakikisha kuwa wewe na huyo mjinga mwenzako mnaozea jela!” Mama Maggie alikata simu na kila nilipokua nikimpigia hakupokea, alinikasirisha kweli, ingawa nilijua kuwa itakua ngumu kupata ushahidi lakini nilishaamua kuwa hawa watu nitawafunga, hawawezi kumfanyia mwanangu ujinga wa namna hii halafu nikawaangalia.
Nilirudi nyumbani nikiwa na Maggie, nilikua na wasiwasi sana kwani pamoja na kuishi naye nilikua simuamini sana G. kwanza nilimuona kama mtoto na pili nilikua najua kuwa ananisanga hivyo hawezi kuishi na mtoto. Kazi yake ya ubaamedi ilinichanganya zaidi nikiamini kuwa hana maadili. Lakini nilipofika tu nyumbani akakutana na Maggie nilishangaa wanakuamarafiki ndani ya siku moja tu, alimpokea vizuri kama mtoto wake na kumhudumua vizuri kuliko hata Mama yake.
“Hutakiwi kumpeleka bweni, huyu mtoto hayuko sawa….” Aliniambia, ilikua ni sikui ya tatu tu tangu kuja na Maggie pale nyumbani, nilishapanga kumpeleka shule bweni ili asikae na G kwani nilikua simuamini sana, nilikua nikiamini kuwa akiwa huko shuleni atakua salama zaidi kuliko nyumbani.
“Kwanini? Unataka ukae naye? Wewe unaweza kukaa na mtoto?” Niliongea kwa hasira flani hivi. Aliniangalia na kutabasamu, ingawa niliona kabisa kuwa maswali yangu yamemuumiza kwa namna falani lakini hakutaka kuonyesha, alitabasamu na kuniambia.
“Najua huniamini, najua kwasehemu uliyonikuta unaamini kuwa mimi ni malaya, ni kweli ni malaya, lakini kumbuka kuwa mbali na umalaya wangu mimi ni mtoto wa kike, nibinti, ni dada nina ndugu. Kikubwa zaidi kuwa malaya kumenifanya kutembea na waume wengi za watu hivyo nimekutana na familia nyingi ambazo zimeharibika, aisee huyu mtoto mmeshamharibu, wewe na Mama yake, ameathirika sana kisaikolojia huyu mtoto amebakwa mara nyingi, anahitaji mtu wa kuwa rafiki yake, mtu wa kumsikiliza na kumuelewa hahitaji Mwalimu wa kumfundisha bali rafiki wa kuongea naye?” Aliniambia kwa upole, ingawa niliona ana mantiki lakini kitendo cha kuniambia kuwa namimi nimehusika katika kumharibu mtoto kilinikasirisha kidogo.
“Inamaana wewe niyo huyo mtu? Wewe ndiyo unaweza kuwa rafiki yake? Weweee!” niliongea kwa dharau kidogo.
“Ndiyo mimi!” Alinijibu kwa mkato.
“Hapana, mtoto wangu hawezi kukaa na we3we, bora niishi naye mwenyewe au nimpeleke shuleni?”
“Ulishawahi kubakwa?” Aliniuliza, sikua na jibu nilishikwa na butwaa nikimuangalia kwa mshangao.
“Huko shuleni walimu wake walishawahi kubakwa?” Aliniuliza tena huku akinikodolea macho.
“Sijui, ila mimi sijawahi kubakwa!”
“Basi nyamaza, mimi nilishawahi kubakwa, najua namna ambavyo mtu aliyebakwa anakua, najua maumivu yake na najua jinsi ambavyo akili yake inafanya kazi. Kama unataka kumharibu huyu mtoto mpleke shuleni, sehemu ambayo hata mtu wa kuongea naye, huyu mtoto anahitaji matibabu, anahitaji mwanasaikolojia ila nikuambie tu ananihitaji mimi kuliko hata huyo mwana saikolojia, kama huamini nenda muulize anataka kwenda kwa Mama yake, shuleni au kubaki na mimi, asiponichagua mimi basi niache na mimba yangu niondoke humu kabisa nifukuze kabisa!”
Aliongea kwa kujiamini, sijui alimuambia nini Maggie lakini nilipoenda kuongea naye kuhudu kuondoka aligoma kabisa.
“Baba mimi nataka kubaki na Dada G…” Aliniambia, nilimuuliza kwanini anataka kubaki naye hakua najibu ila alionekana kujisikia furaha zaidi akiwa naye kuliko akienda shuleni au kurudi kwa Mama yake. Sikua na namna zaidi ya kukubalia na kile alichokua antaka mtoto, nilimruhusu kubaki pale na kweli mambo yalikua mazuri, alirudi shule, alikua anasoma vizuri na G alikua anamfundisha kila siku, ufaulu wake darasani ulirudi kama kawaida na kweli tulikua na amani.
*****
Miezi miwili ilikua imeita, tangu kumuambia mke wangu kuhusu kuwafunga yeye na mwanaume wake alikua hajanitafuta. Ni kweli nilipanga kuwafunga, kuwatafutia kesi yoyote ile lakini G alinikataza, aliniambia kuwa Maggie alishaanza kusahau maumivu, kisheria ingekua ngumu sana kuthibitisha kuwa alibakwa na wale vijana kwani muda ulishapita, hakukua na ushahidi wa maana na kwa namna alivyoongea Maggie ni kama alishasahau kilichokua kimetokea, aliniambia kesi inaweza kumharibu zaidi na hakuna uhakika kama watafungwa, aliniambia niachane nao.
Sikuwasiliana tena na mke wangu wala yeye hakunitafuta, mwanangu Jacob alikua shule, nilitamani kumleta lakini abdo nilikua sijapata mfanyakazi wa kueleweka na kwa hali ya G, ilikua ngumu kwake kuhudumia watoto wawili wakati naye alikua na ujauzito. Nikiwa naamini kuwa kila kitu kimeisha siku moja Maggie alirudi nyumbani akiwa analia, alikua anatetemeka huku akinipigia magoti akiniomba nisimpeleke kwa Baba yake.
Nilishangaa kwani nilishamuambia kuwa kitu kama hicho hakiwezi kabisa kutokea, nampenda kama mwanangu na kamwe siwezi kuwa mbali naye.
“Mama alikuja shuleni kunislaimia, hakuniambia chochote lakini kaniambia kanimiss na ipo siku atanichukua.” Aliniambia, kusema ukweli nilikasirika, mieziwi miwili ilikua imepita bila kuongea na mkew angu, sikujua hali yake sikujua chochote lakini siku hiyo nilimpigia na kumuuliza kwanini alienda kumuona mtoto wakati siku zote anakua hamtaki.
“Nina shida ya milioni mbili, mimi kazi nimesimamishwa hivyo sina pesa, nahitaji unisaidie milioni mbili.” Badala ya kunijjbu swali langu kuhusu mtoto aliongea mambo ya pesa.
“Una akili kweli, mimi nakuuliza kuhusu mtoto wewe unaongea kuhusu pesa!? Nilimuuliza kwa hasira.
“Ndiyo mimi nina shida na milioni mbili, sina kazi, sina pesa, unafikiri ninaishije, umeniacha na mtoto mdogo, humhudumii….” Nilimkatisha.
“Mtoto kwani wangu, si ana Baba yake?”
“Abnaye ila wewe si imeniharibia kwa baba yake, Baba yake alikua akihudumia mwanae lakini baada ya kumuiba Maggie amegoma kuhudumia kabisa.” Aliniambia kama analalamika lakini kwa kiburi.
“Kumuiba kivipi, hivi ana akili kweli, amekaa na moto muda oe huo mtoto anabakwa na dnugu zake lakini anakaa kimya, sasa hivi anasema mtoto nimemuiba, hivi nimemuiba au katoroka?”
“Mimi sijui, ninachojua umemchukua mtoto na Baba yake kanikasirikia! Usivyo na hyaya umeenda kuongea na huyo mtoto ili kumsingizia Baba wa watu kuwa amembaka, hivi unafikiri yeye atajisikiaje, mtoto wake wakike! Magge ni muongo! Huyo mtoto ana akili sana, alikua hataki kukaa kwa Baba yake kwakua akiwa na wewe unamdekeza hivyo akaanza kulalamika kuwa anabakwa! Hivi unafikiri mimi sina akili, mimi ni Mama ningejua mwanangu anabakwa kweli ningemuacha.
Kelvin ndiyo Baba wa huyo mtoto, ana uchungu sana na mwanae, sasa unafikiri angeruhusu mwanae abakwe nayeye kuchekelea.” Aliniambia kama ananisuta, kwa maelezo yake alikua akimini kabisa kuwa mtoto wake alikua anadanganya, nilimuona Maggie na daktaria limpima na kugundua kuwa alikua akiingiliwa kimapenzi.
“Nilikuacha kimya kwakua kipindi kile ulikua una hasira, ungeweza kutumia pesa kutufunga, lakini sasa hivi namimi nina mwanasheria wangu, najua huna ushahidi wowote hivyo namataka mwanangu! Kama unataka kubaki naye basi nipe milioni mbili, nitakuachia huyo mtoto!”
Nilishindwa kuamini kama mke wangu alikua kafikia hatua ile niliomba kuonana naye ili kuongea kuhusu hiyo ishu ila aligoma, aliniambia kama nikuonanana naye basi nimpe milioni mbili.
“Milioni mbili? Hivi kweli mke wangu ndiyo kafikia hatua hii ya kudai milioni mbili kwasababu ya mtoto! Sijui maisha yake yakoje?” Niliwaza bila majibu, sikutaka kumpa hiyo hela kwani nilikua najua, mtu kama huyo hata ukimpa leo basi na kesho atataka nyingine. Nilikaa kimya nikiwaza nini cha kufanya, usiku nilikua bilabia, niliamua kwenda nyumbani ili kuonana na mke wangu na kuongea kwani sikuwa tayari kumuachia mtoto.
“Kama ana matatizo nimsadie kumpa hata mtaji afanye Biashara lakini si kumlipa kwaajili ya kuniachia mtoto, hii haitaisha.” Nilienda mpaka nyumbani lakini sikumkuta mke wangu, nilichokikuta kilikua tofauti kabisa, mke wangu alikua katafuta mpangaji ambaye alikua amepanga nyumba kubwa, yeye alikua akikaa mabanda ya uani, hakua na mfanyakazi na nilipoulizia niliambiwa kuwa anakuja pale mara moja moja ila hawajui anaishi wapi?
Nilimtafuta kwenye simu lakini hakupokea, nilihangaika sana ndipo Mama yake mdogo alinipa namba yake nyingine ambayo aliipokea. Niliomba kuonana naye na kumuambia kuwa nina pesa yake, kweli baada ya kusikia hivyo aliniambia sehemu ambayo alikuepo. Alinielekeza, ilikua ni nyumba ya kawaida nzuri tu kwa nnje, niliofika hakutaka niingie kwani ilikua na geti kubwa tu alitoka lakini namna alivyokua amevaa nilishtuka kidogo.
“Unaishi humu?” nilimuuliza lakini hakunijibu, alitaka tu pesa zake.
“Hayakuhusu, ninachoteka mimi ni pesa zangu, la sivyo namchukua Maggie nampeleka waka Baba yake. Nipo tayari kupima mpaka DNA!” Aliongea kwa hasira.
“Sam yuko wapi? Mbona nyumba umepangisha? Ndiyo uansihi humu….” Nilimuuliza lakini kabla ya kunijibu alitoka Mama mtu mzima ambaye alikua amevaa kinguo kama yuko uchi. Aliniangalia kwa tamaa, ingawa ilikua usiku lakini kulikua na taa kali hivyo niliweza kumuona vizuri tu.
“Huyu ndiyo alikua mume wako? mbona mboga namna hii? Shemu usitusahau, sisi ndiyo tunamuweka mjini mke wako!” Aliongea huku akinifuata akanishika sehemu zangu za siri.
“Shemu umebarikiwa!” Aliongea hukua kitaka kunikumbatia, kitendo kile kilimkera sana mke wangu, ghafla nilimuona anamrukia yule Mama wakaanza kupigana.
“Mshenzi mkubwa, yaani umesikia tu nina mwanaume unatyaka kuninyang’anya, nimekuambia nitakuua!” mke wangu alianza kutukana, walishikana, wakavurugana wakapigana na kutukanana. Mwanzo nilishikwa na butwaa na kuwa kama nimeganda tu sijui nini chakufanya, lakini niakshtuka na kuwaamua.
“Unafanya nini Mama Maggie?” Nilimuuliza, alishtuka kama niko pale na kuona aibu.
“Wew ni mshenzi tu, ndiyo nini unakuja kwangu unaruhusu mwanamke mwingine kukushikashika. Wewe ni mume wangu tena wa ndoa, hata kama nilikukosea lakini hutakiwi kunifanyia hivi!” Alinigeuzia kibao na kuanza kunilaumu mimi, nilijisikia vibaya kwakweli, nikamuambia yule Mama aondoke, aliondoka na kuniacha pale huku akitukana.
“Nakuambia humu utaondoka, mimi ndiyo Don, hapa, kila siku huna kitu tunakusaidia, unakua arosto tunakuokoa leo umekuja na kijimwanaume chako hapa unajifanya nini? Siku ile unapigwa na kile kimwanaume chako kingine tunakutetea leo unajifanya una wivu, wewe si ndiyo ulikua unasema uliolewa tu ile basi kwakua sijui nani wako alikuacha akaoa mtu mwingine sasa ndiyo nini kujifanya unampenda!” Aliongea maneno ambayo yalinichoma lakini nilishindwa kufanya chochote.
“Mke wangu tuondoke humu, siwezi kuongea nawewe kitu cha maana humu.” Nilimuambia, mwanzo aligoma lakini nilipomuambia kuwa kama ni kumpa pesa basi nitampa tukiwa sehemu nyingine ila si hapa alikubali.
“Subiri basi niingie ndani.” Aliniambia, nilimuacha akaingia ndani, lakini wakati mke wanu anatoka nilimuona kama anachechemea hukua kikunja uso kuonyesha kuwa ana maumivu makali.
“Unaumwa, mbona uko hivyo?” Nilimuuliza kwani nilianza kupatwa na wasiwasi, ni kweli alikua kakonda tena sana, mwanzo nilijua labda nikwakua ana mawazo lakini jinsi alivyokua akiongea kwa kujikaza nilihisi bado anaumwa.
“Nikupeleke hospitalini?” Nilimuuliza, lakinia ligoma, aliniambia kuwa yeye anachohitaji ni pesa tu au mtoto wake.n nilimuambia aingie kwenye gari lakini aligoma kabisa kukaa siti ya mbele, aliniambia anahitaji kukaa nyuma kwani kuna mambo yake anataka kuyafanya. Ikua na namna nilimruhusua Akaka nyuma lengo langu lilikua ni kuondoka naye mpaka nyumbani ili aniambie ni kwaninia likua kapangisha nyumba na kuniambia alipokua mtoto wake mdogo.
Tukiwa njiani nilikua nageukageuka kumuangalia, mwanga ulikua hafifu lakini nilimsikia akifungua pochi yake na baada ya muda nilimsikia akiguna kama vile ana mjaumivu flani. Lakini kila nikigeuka nikimuuliza nini tatizo alikua akijificha na kuniambia kuwa yuko sawa. Nilimpeleka mpaka nyumbani kwetu, nyumba ambayo nilikua nimemuachia, tukaingia kweye mabanda ya uani alipokua akikaa yeye.
“Ndiyo unanipa pesa yangu?” Nilimuuliza.
“Mbona unaongea sana kuhusu pesa, vipi mtoto yuko wapi?” Nilimuuliza lakini hakujibu, alichokua anataka yeye ni pesa. Nilimuambia sina na hapo ndipo alikasirika, aliwaka na kuanza kunitukana.
“Hivi unafikiri mimi nitaishije? Umenitoa huko mpaka huku kuja kuniuliza kuhusu watoto, kwanza ni wanao wale, nataka pes ayangu la sivyo nakuja kumchukua Maggie mimi mwenyewe!” Aliwaka sana na kutukana sana, sikua na ile pesa ila nilitaka kumsaidioa.
“Hembu tulia kwanza, ishu ya pesa si tatizo, mimi si wa kukosa milioni mbili, lakini ninachotaka nikukusaidia, nikikupa milioni mbili leo vipi kesho utataka ngapi, najua huna kazi ndiyo nataka kukupa mtaji ili ufungue Biashara!” Niliongea huku nikijaribu kumtuliza lakini hakutulia, alifoka na kupiga kelele sana, alitukana sana mpaka majirani ambao ni wapangaji wake wapya walisikia na kuja.
Kuepusha mzozo niliondoka huku nikimuambia kuwa nipo tayari kumpa hata milioni kumi kama mtaji lakini si kumlipa ili aniachie Maggie.
“Sina shida ya msaada wako, sitaki kabisa kusaidiwa na wewe, nakuambia nitakuja kumchukua mwanangu na hakuna Mbuzi yoyote wakunizuia!” Sikumjibu niliondoka zangu kimya kimya, nilirudi nyumbani, G aliniuliza kilichotokea lakini sikumuambia, nilimuambia kuwa mambo yamekua sawa basi.
Keshjo yake ilikua ni jumamosi, kwa kawiada mimi naenda kazini. Kwenye saa mbili hivi nikiwa kazini G, alinipigia simu na kuniambia kuwa Mama Maggie alikua nyumbani na alikua anafanya vurrugu. Sijui alijuaje nilipokua nikiishi lakini nilimsikia kwenye simu akitukana kuwa anataka pesa au mtoto. Niliingia kwenye gari kama mwehu mpaka nyumbani, kufika nilikuta watu washakuja na kumkamata. Nilimchukua mpaka ndani nikaingia na G, nikajaribu kuongea naye ila hakusikia kitua lichokua anataka yeye ni milioni mbili, hata nilipomuambia nitampa milioni kumi aligoma kabisa.
“Baba Maggie hembu naomba tukaongee chumbani kidogo” G aliniambia, tuliingia chumbani ndipo aliniambia.
“Huyu hahitaji msaada bali anataka kwenda kulipa madani, watu wanaomdai ni watu wabaya wanaweza hata kumuua hivyo mtaji wako hauna maana.” Alianza kuniambia.
“Unamaaanisha nini mbona sikuelewi, kwani kakuambia kuwa kuna watu wanamdai?” Nilimuuliza.
“Hapana, hana haja ya kuniambia lakini kwa namana anavyodai na jinsi alivyo najua kuwa anadaiwa na mapisha hukohuko anakonunulia unga!” Aliniambia.
“Unamaanisha nini? Yaani mke wangu anakula unga?” Nilimuuliza kwa mshangao.
“Sio anakula unga bali ni teja, hivi wewe mwanaume ni wa namna gani, huyo mtu kaanza kula unga muda, angalia anavyotetemeka, hapo hajapata unga. Nina uhakika anadaiwa, kashakua teja humuoni alivyo…”
MATAPELI: Kuna matapeli wengi ambao wanatumia jina la Iddi Makengo, kuna huyu anakuambia tumakwa jina la wakala anaitwa ukituma anaitwa ALLY SAYE, mwingine ni namba ya wakala anaitwa SADIKI ZAKARIA na nyingine SADIKI TWEVE. Wote hao ni MATAPELI jamani ukilipia pesa hakikisha jina linakuja IDDI MAKENGO sina namba ya wakala wala nini!
Kwa ushauri wa moja kwa moja hakikisha unanunua kitabu changu. Kwasasa nina vitabu vinne, cha mahusiano ya kawaida hasa kwa wanawake, cha wanaume wenye changamoto ya kumfikisha mwanamke kileleni, cha Biashara na cha Interview na Ajira, chagua kinachoendana na tatizo lako.
MAMA MAGGIE; NAKUPENDA SANA ILA SHETANI AMEKUPENDA ZAIDI! —SEHEMU YA KUMI N TATU
!
Nilirudi kumuangalia vizuri mke wangu. Kwelia likua anateemeka, alikua na uoga flani ambao ulinifanya kujua kuwa kuna kitu anakihofia.
“Unamtaka mtoto mchukue, kwanza si mwanangu hivyo siwezi kukuzuia, kama unamtaka mchukue lakini milioni mbili siwezi kukupa!” Nilimuambia mke wangu ambaye alishtuka, ni kama hakutegemea hivyo, alijua nampenda Maggie na ni kama alikua anamuuza. Alibaki ameduwaaa ananiangalia hajui cha kuongea.
“Nakuambia kamchukue Maggie, nimechoka na usumbufu wako, mchukue, ni mwanao kama hutaki asome basi utajua mwenyewe!” Nilirudia kumuambia baada ya kuona kabaki kaduwaa tu hana chakuongea.
“Una uhakika? Mimi sitanii? Najua unampenda sana hivi unajua kama nikimchukua hutamuona tena!?” Aliniuliza, nilimuangalia kwa dharau na kumuambia utajua mwenyewe, mchukue sitaki tena kumuona.
Wakati akikaa anatafakari nini cha kiufanya, alionekana kama kakwama, alianza kung’ata vidole, alikua kasimama lakini alikaa chini kabisa. Nilitaka kumjaribu ili kuthibitisha maneno ya G, sikua tayari kumpeleka Maggie kwake hata kwa dakika mbili. Nilipoona kasimama ananishangaa huku ananitishia kuwa atamchukua kweli mwanangu niliingia ndani chumbani kwa Maggie ambaye alikua kajifungia ndani baada ya kumuona Mama yake.
“Unanipenda?” nilimuuliza.
“Nidyo Baba.” Alijibu huku akianza kulia, nilimfuata na kumukumbatia.
“Mbona unalia.” Hakunijibu, aliishia tu kunikumbatioa huku akiniomba nisimpeleke kwa Mama yake.
“Bbaa najua Mama kaja kunichukua, lakini usiache akanichukua, mimi sitaki kwenda.” Hata nilipomhakikishia kuwa siwezi kumpeleka kwa Mama yake bado alilia na kunibembeleza.
“Mama yako hataki kukuchukua, anacheza na akili zangu, sasa mimi nataka nimuambie akuchukue tuone kama atakuchukua” Nilimuambia lakini hakuamini, alinishika na kuning’ang’ania huku akiniambia hataki kabisa kuondoka na kurudi kwa Mama yake.
Ingawa nilitaka kumtishia Mama yake kuwa nipo tayari kumpa mtoto lakini nilimuonea huruma, nilijua kuwa atateseka na kuumia kama akihisi nilikua tayari kumrudisha kwa Mama yake hata kama ni kwa utani. Nilimuambia abaki ndani kisha mimi nikachukua begi lake na kutoka.
“Shika, mizigi ya mwanao, tokeni kwangu sitaki kuwaona, kamsubirie mwanao huko nnje anajiandaa ili muondoke!” Nilimuambia mke wangu huku nikimsukuma kumtoa nnje, alijua kabisa kuwa nipo siriasi kwani nilikua nimekasirika.
“Nakaribia kupata mtoto mwingine, sitaki kulea watoto wa watu, hata Jachob sina uhakika kama ni wangu hivyo unaweza kumchukua muondoke wote, simhitaji!” nilimsukuma mke wangu mpaka getini na kumkabidhi begi la Maggie, sikua na mpango wa kumpa mtoto ilia nilitaka kupima upepo. Kweli baada ya kuona kuwa nipo siriasi sitaki kubaki na mtoto mke wangu alipiga magoti na kuanza kuomba msamaha.
“Sihitaji watoto mume wangu, nina shida ya pesa, nisaidia hata milioni moja, nisipotoa hizo pesa wataniua, nimeshauza kila kitu, nisaidie, naomba unisaidie….” Alianza kulia huku akiomba msamaha, alikua kapiga magoti hivyo nilimshika na kumnyanyua, sikutaka kuingia naye ndani, hapo nnje kwangu kulikua na kakitu kama kagogo flani hivi, nilienda naye na kukaa.
“Watu gani hao watakuua, niambie uwkeli kama si hivyo nakuacha uondoke na wanao na sitaki tena suumbufu.” Alikua mgumu sana kuniambia mwisho ndipo aliniambia kuwa yeye anatumia unga muda mrefu na ameshindwa kuacha hivyo anatoa pesa nyingi kuwalipa wanaomletea na sasa hivi ana madeni mengi sana.
“Unamaanisha nini? Ulianza lini?” Nilimuuliza ndipo aliniambia jinsi alivyoanza.
U”unga sikuanza zamani, nilianza mwishoni mwishoni hivi kabla ya kuachana na wewe, kipindi hicho nilikua karibu sana na Kelvin, alinifundisha vitu vingi sana. Wakati naanza mahusiano na Kelvin nilikua sinywi pombe, sivuti sigara wala nini, lakini baada ya kuwa naye kwenye mahusiano akawa ni mtu wa kutoka usiku hivyo alitaka nitoke naye, basi akawa anavuta sigara pombe basi mimi nakunywa naye akanifundisha mpaka kuvuta bangi.
Aliponiacha na kukutana na wewe pombe niliweza kuacha ila sikuweza kuacha kuvuta bangi, nilikua navuta kimyua kimya nikaendelea mpaka tuliporudiana naye, alikua ananisumbua sana, ananipiga ananitesa kipindi hata niko nawe na ili kuwa vizuri ilikua ni lazima kuvuta bangi ndiyo niweze kuongea na wewe la sivyo nilikua najihisi kuchanganyikiwa. Kipindi kile tunagombana nikaondoka nilikua nakesha naye baa, kwenye makasino nakua naenda naye, yeye anakua kila siku hana pesa hivyo anataka mimi nimpe pesa.
Kwakua nilikua na wivi kuwa nikimpa pesa ataenda kutumia na wanawake wengine bais nilikua naenda naye kila kitu nalipa. Lakini hata nikitoka naye, alikua ni mtu wa kuniacha, anaenda kukaa na wanawake wengine hivyo nikawa navuta shisha na mabinti wadogo. Sikujua kuwa katika shisha hiyo sehemu walikua wanachanganya na dawa za kulevia, basi hali ilizidi kuwa baya mpaka nikawa nisipoenda pale kwenye shusha basi siwezi kufanya chochote.
Nikawa nikivuta shisha ya sehemu nyingine sisikii kitu, basi nikaja kumbiwa na dada mmoja kuwa wanachanganya na dawa nayeye ndiyo akawa ananiunganisha unakumbuka yule Mama wa juzi, yeye ndiyo alikua ananiletea unga, tukagja kugombana nikawa natafuta mwenyewe, ndiyo nikauza kila kitu, nina madeni na sasa hivi nadaiwa milioni moja, hao watu wanaonida ni washenzi wanaweza hata kuniua. Nimekua nikifanya mpenzi na wanaume mbalimbali ili tu nipate pes aya kuendeshea maisha yangu lakini inaishia kwneye unga, hali imekua ngumu ndiyo maana nikaja kwako.” Aliniambia huku akilia, kusema ukweli nilimuonea huruma kwani alionekana kuumia.
Alinieleza jinsi Kelvin alivyokua anamtesa tangu kipindi wanaanza mahusiano, namna alivyokua anampiga na kumlazimsiha vitu vya ajabu ikiwa ni pamoja na kufanya mapenzi kinyume na maumbile kwa vitishi kuwa kama akigoma atamuacha na kuoa mwanamke mwingine.
“PPamoja na kukubali yote hayo lakini aliniacha na kwenda kuoa. Hakuniacha tu kimya kimya, aliniacha kwa dharau akiniambia kuwa mimi si mwanamke wa hadhi yake, akanitukana sana na kuniambia kuwa kwakunisaidia atakua akifanya mapenzi na mimi mara moja moja kujituliza kwani siwezi kupata mwanaume mwingine mwenye akili wa kufanya mapenzi na mimi.
Nilikua naumia sana lakini sikuweza kumuacha, hata kipindi anaenda kuoa, alinilazimisha mimi kumsindikiza. Sijawahi kumuambia hiki kitu lakini wakati anaenda kwenye sendoff alinilazimisha niende, mimi ndiyo nilillipia safari yake na nilipofika alifanya mapenzi na mimi kabla na baaada!” nilihisi kama ni simulizi lakini nikikumbuka namna ambavyo Mama yake mdogo aliniambia jinsi alivyokua akinyanyaswa na kupigwa niliamini.
“Kwanini hukumuacha? Mimi nilikua nakupenda, nakujali, nakufanyia kila kitu?” Nilimuuliza lakini hakua na jibu, aliishia tu kuomba msamaha na kuniomba hiyo pesa. Nilimuambia kuwa siwezi kumpa pesa kwaajili ya kununua dawa za kulevia nataka ache.
“Unafikiri ni rahisi hivyo, nimeshakua teja, sina tofauti na wale wapiga debe wa mjini, nalewa, nazima nalala, watu wananibaka na kunifanyia mambo ya ajabu! Nimechoka lakini nashindwa ni namna gani nitaacha, hembu angalia….” Aliongea huku akivua suruali yake aliyokua ameivaa ili kunionyesha mapaja yake jinsi alivyoharibika. Mke wangu alikua kama mtu aliyechanganyikiwa.
Nilimshika harakaharaka ili aisjidhalilishe kwani kuna watu walikua wanapita, nilimrudisha ndani, nilimuambia kuwa nipo tayari kumlipia madeni yake yote kwa masharti kuwa anipe watoto wote nikae nao mimi na awe tayati kukubali msaada wa kwenda sober house. Hakufikiria hara mara mbili, alikubali kila kitu nilichomuambia, alishukuru sana, nikampa hiyo pesa nikamuambia akailipe na kwelia lilipa kwani niliongozana naye mimi. Akanielekeza sehemua lipokua Samweli, nikaenda kumchukua ili kuishi naye kisha nikamtafutia sehemu ambayo alikua anaenda kutibiwa.
Alikaa huko kwa miezi sita, aliporudi alikua vizuri, nilifanya mpango akarudishwa kazini. Alitaka sana turudiane lakini kwa wakati huo nilikua na G, nilikua nampenda na kusema kweli nilikua najisikia vizuri, nakua na amani nikiwa nayeye. Alinibembeleza sana lakini sikukubali, tuliendelea kuwa kama marafiki lakini bado kidini aliendelea kubaki kuwa mke wangu. Siku moja niliitwa kanisani, mke wangu alienda huko, hii ilikua ni miaka miwili baada ya yeye kuwa sawa.
Alikua anataka kurudiana na mimi, nilipigwa neno mpaka nikahisi kuchanganyikiw,a nikajiona kama nakosea, wakati huo mimi na G, tulikua tukiishi tu, alikua chuoni kwani nilimrudisha chuo na alishaniambia kuwa hawezi kupata mtoto mwingine na mimi mpaka pale nitakapompa mke wangu talaka ya mahakamani. Kweli nilikua sina mpango wa kurudiana naye lakini kila likija suala la talaka nilijikuta nanywea na kuacha.
Basi baada ya kuitwa kanisani nilijikuta narudisha mapenzi kimya kimya. Kwakua G alikua chuoni na muda mwingi alikua bize basi Mama Maggie alikua akija nyumbani mara kwa mara kuwaona watopto kwani wote nilikua nikiishi nao mimi. Tulijikuta tunarudiana, shida ilikua ni kuwaambia watoto na kumuambia G kuwa mimi na mke wangu tumerudiana, ilikua ngumu sana lakini siku moja nilipokea simu kutoka kwa G, aliniuliza nini kilikua kinaendelea, nahsii alishajua, nilimumbia hakuna kitu il hakukubali.
“Najua bado unampenda mke wako ila kuwa makini. Wewe si mume wangu, tangu siku ya kwanza nakutana na wewe nilijua kabisa kuwa nakudanga basi, lakini nakupenda ila shida najua kuwa unampenda Mama Maggie ndiyo maana siku zote pamoja na yote aliyokufanyia lakini nikikuambia kuhusu mambo ya talaka unazungukazunguka. Aliyeniambia kuhusu kurudiana kwenu ni Maggie, anaumia sana kwani ananipenda na anamjua Mama yake, kua makini sana na hiyo hali, kumbuka kuna wtaoto wakuumia kwani mimi siwezi kuachana na wewe na kuendelea kuishi na watoto wako. Nilishaachwa mara moja nikaumia nikaja kuapa kuwa siwezi kuumizwa tena na mapenzi, nimekupigia kukuambia kuwa nimekuacha endelea na mke wako!”
Aliniambia, niliumia kidogo lakini si sana, bado nilikua nampenda mke wangu na yeye kuniambia vile ni kama alikua kanirahisishia namna ya kumuacha. Shida ilikua ni kuongea na watoto ambao walikua wanampenda sana G hasa Maggie ambaye alimuona kama Dada yake. Wakati huo alikua kidato cha kwanza, alikua mkubwa hivyo alikua anaelewa nilipomuambia hata hakulalamika sana, alikua ameshajua kuwa mimi na Mama yake tumerudiana.
“Baba kuwa makini sana, sitaki uje kuumizwa…” Aliniambia maneno ambayo yalinichoma sana, wakati mimi nilikua nikimuwazia yeye, nikiwaza ni namna gani nitaongea naye yeye alikua akiniwazia mimi akihisi kuwa ninaweza kuumia.
“Usijali, mimi ni mtu mzima, najua ninachofanya?” Nilimuambia, aliniangalia na amchozi yakaanza kumtoka, nilimuuliza tatizo nini lakini hakuniambia.
“Nitakua sawa Mwanangu, Mama yako amejifunza….” Nilimuambia lakini alionekana kama vile haamini.
“Baba kuwa makini, usimuamini Mama, atakuja kukuumiza, una roho nzuri sana unaamini wema kwa kila mtu. Mama si mtu mzuri kama wewe!” Aliniambia, nilijikuta nakasirika na kumfokea namna alivyokua anamuongelea Mama yake.
“Acha kumuongelea Mama yako hivyo! Huna adabu, Mama yako alikosea kweli lakini unatakiwa kumsamehe, ameshabadilika, kipindi kile Mama yako alikua mgonjwa ndiyo maana tulimpeleka hosspitalini, kajifunza, amebadilika!”
Nilimuambia kwa hasira lakini yeye aliniangalia kwa huruma ni kama kuna kitu alitaka kuniambia lakini anashindwa mwisho aliniambia.
“Baba najua unampenda sana Mama lakini uwe uanshika simu yake, na angalia kwenye M-Pesa yake!” aliniambia kama kuna kitu anakijua, nilimuuliza sana kwanini anasema mambo ya M-Pesa lakini hakua tayari kuniambia aliniambia niwe naangalia huko.
“Baba watu wanafuta meseji za kawaida lakini wanasahau kufuta meseji za M-Pesa.” Aliniambia na kuondoka akaniacha na mawazo, tangu kurudiana na mke wangu nilikua makini sana nafuatilia simu yake kuona kama bado anawasiliana na X wake lakini sikuona hata dalili. Maggie aliponiambia na namna alivyosema ni kama alikua anajua kuna kitu, jioni nilikutana na Mama yake, nilikua huru sana na simu yake, hivyo hata nilipoichukua kuiangalia hakujali aliniacha nayo nikawa naikagua.
Moja kwa moja nilienda kwenye M-pesa yake kuangalia kama nitaona kitu. Sikuchukua hata sekunde tano, nilikuta meseji nyingi za miamala, kwa ndugu zake Baba yake lakini kulikua na meseji nyingi akituma pesa kwa X wake Kelvin. Alikua akimtumia si pesa nyingi mara elfu kumi, kumi na tano, elfu mbili, mara katuma laki zilikua za namna hiyo na ilikua ni karibu kila siku. Hii ikimaanisha kuwa walikua wanawasiliana kial siku.
Sikuongea kitu, niliichukua ile simu na kumuonyesha mke wangu, alishtuka sana kwani ni kitu ambcho hakikutegemea.
“Nisamehe mume wangu, sijui nikuambie nini, ni shetani tu alinipitia, sina mahusiano na Kelvin, simpendi lakini sasa hivi ana wakati mgumu. Amefiwa na wazazi wake, amefukuzwa kazi, yaani namsaidia saidia tu kwakua ana matatizo, mtoto wake kalazwa hospitalini amepooza mwili mzima…..”
Alijielezea sana lakini sikumuuliza chochote, niliumia sana kuona kuwa bado anamkumuka huyo mtu, bado wanawasiliana kujua kuwa anauguliwa na mtoto. Iliniuma sana kiasi nikashindwa hata kuongea, nilinyanyuka na kuondoka. Nilienda kukaa Baa ili kunywa lakini niliishia kunya maji, nilishaacha pombe. Niliishia kumtumia meseji na kumuambia “Nilikupenda sana lakini shetani amekupenda zaidi, sikuhitaji tena mke wangu.”
Mke wangu alijua kama utani lakini kesho yake aliitwa baraza la usuluhishi nikidai talaka. Alitaka kukataa ila nilimuambia kuwa akigoma talaka namuachia watoto wake na hatakuja kuniona nikiwa Baba kwao. Aliomba sana msamaha lakini sikua tayari kumsamehe, nilihangaika mpaka nikapata Barua na kwenda mahakamani na mwisho tuliachana. Tuligawana kila kitu cha kugawana na kila mmoja akaenda njia yake. Watoto wote naishi nao mimi kwani waligoma kabisa kwenda kwa Mama yao.
Bado sijaoa, sijapata mwanamke mwingine kwani G aliniambia kuwa hayupo tayari kuendelea na mimi. Alimaliza chuo Digrii yake ya Sheria, akaenda na shule ya sharia na sasa hivi ni mwanasheria, ameolewa na ana maisha yake mazuri. Watoto nilibaki nao mimi. Maggie amemaliza yuko kidato cha tano, mke wangu Mama Maggie tunaonana tu lakini sijui maisha yake yakoje, anakuja kuwaona watoto kila akitaka ila sijui mambo ya mahusiano na kuhusu Kelvin hata sijui yuko wapi na sitaki kujua.
MWISHO;
0 comments:
Post a Comment